Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia akiongea na mshindi wa nyumba mara baada ya kupatikana katika draw ya mwenzi iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel morocco ambapo bwana Silvanus Juma kutoka mkoa wa iringa aliibuka mshindi wa nyumba hiyo wakishuhudia Msimamzi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao katikati akifatiwa na Meneja Uhusiano wa Airtel Bw,
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akiongea wakati wa kuchezesha droo ya kwanza ya kumsaka mshindi wa nyumba ya kwanza kupitia promosheni ya Airtel yatosha , kushoto Msimamzi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao kulia Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel yatosha ilimpata mshindi wa nyumba bwana Silvanus Juma kutoka mkoa wa iringa.
========= ======== =======
Airtel Tanzania imetangaza mshindi wa kwanza wa nyumba kupitia
promosheni ya Airtel yatosha Shinda nyumba inayoendelea na
kuwazawadia wateja wake kila siku.
Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa mwenye umri wa miaka 33 ambaye ni
mhasibu katika shirila la Tanzania Rural women and children
development foundation - TARWOC ameibuka mshindi na kuzawadiwa nyumba kisasa iliyojengwa na shirika na nyumba la taifa NHC iliyopo kigamboni jijini Dar es saalam.
Akiongea wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel
bwana Jackson Mmbando alisema" kama tulivyowangazia awali leo ndio ile
siku muhimu na maalumu ya kumpata mshindi wetu wa kwanza wa nyumba na tumeshuhudia bwana Silvanus Juma akiibuka mshindi kupitia droo ya kwanza tuliyoichezesha hapa.
Sambaba na hilo leo tunao washindi 7 wa wiki kutoka katika mikoa
mbalimbali ambao hawa wataondoka na pesa taslimu shilingi milioni
moja kila moja, washindi hawa ni pamoja na Peter Ignasho kutoka
Muheza Tanga, Edita Rweyabura kutoka Bukoba, Steven Maguro , Rakesh
Ali Mauji, Mwajuma Hassani kutoka Dar es Saalam, Siasa Yahaya Songo
kutoka Manyoni Singida and Vero Mispela Kiwango kutoka Bihalamulo.
Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kuendelea kutumia huduma ya
Airtel yatosha na kujiunga na vifurushi mbalimbali na kupata nafasi ya
kujishindia zawadi mbalimbali , kujiunga nirahisi piga *149*99#
kisha nunua kifurushi chacko cha siku, wiki au mwezi na kisha
kuingizwa moja kwamoja kweny droo ya kuweza kushinda milioni moja kila
siku au zawadi kubwa ya Nyumba.
Akiongea mara baada ya kutangazwa mshindi Bwan Silvanus Juma
alisema"Ninayofuraha sana kupata zawadi hii kubwa kutoka Airtel
napenda kutoa wito kwa watanzania na wateja wa Airtel waendelee
kutumia huduma ya Airtel yatosha na waamini kuwa hakuna upendeleo.
Binafsi sijawahi kushinda Bahati nasibu yoyote na nilikuwa siamini
kama hakuna ubaguzi kwenye kushinda, lakini leo nashuhudia kwamba
ushindi ni wa uhakika usio na upendeleo wala ubaguzi hivyo wajaribu
nao wanaweza kuwa washindi.
Kwa upande wake moja ya wafanyakazi wenzake Bwana Beatus Magoti ambaye ni Mshauri wa fedha na utawala TARWOC alisema" tumefurahi sana kuona kijana mgodo mwenzetu ambaye ni mchapa kazi ameweza kushinda nyumba kupitia promosheni ya Airtel yatosha. Hii imetupa hamasa na sisi
kushiriki na kueneza habari kwa wengine kushiriki na kushinda kama
laivyoshinda Silvano.
Airtel inaendelea na promosheni ya Airtel yatosha shinda nyumba tatu
ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wake na kutoa huduma bora zenye
gharama nafuu kupitia huduma ya Airtel yatosha. Sambamba na hilo
Airtel pia imewawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa
bure bila makato yoyote.