Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

BENKI YA KCB YATOA MSAADA WA VIFAA VYA WATOTO NJITI ZANZIBAR

$
0
0
  Meneja wa KCB  Bank Tawi la Stone Town mjini Zanzibar, Cosmas Mwankemwa akizungumza  kwenye sherehe ya kukabidhi msaada wa vifaa vya kuhifadhia watoto wachanga ambao hawakutimia umri wa kuzaliwa "njiti" kwaajili ya hospitali ya Kivunge Zanzibar jana vikiwa na thamani ya sh.12 milioni.
  Mgeni Rasmi katika hafla hiyo, Dk.Fadhil Mohamed akizungumza kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kuhifadhia watoto wachanga ambao hawakutimia umri wa kuzaliwa "njiti" kwa dhamana ya hospitali ya Kivunge Zanzibar vilivyotolewa na Benki ya KCB Tawi la Stone Town mjini Zanzibar jana vikiwa na thamani ya sh.12 milioni.
Meneja wa Benki ya KCB Tawi la stone Town Zanzibar, Cosmas Mwankemwa (kulia) akikabidhi vifaa vya kuhifadhia watoto wachanga ambao hawakutimia umri "njiti" kwa  Dk.Yussuf Haji,ikiwa ni dhamana ya hospitali ya Kivunge Zanzibar jana vikiwa na thamani ya sh.12 milioni.
  Baada ya kukabidhiana vifaa hivyo.

RAIS KIKWETE AMPONGEZA KIJANA HAMIS KWA KUTWAA UBINGWA WA DUNIA WA MCHEZO WA KURUKA KAMBA

$
0
0
Rais Jakaya  Kikwete akimpongeza kijana wa Kitanzania Hamisi Mohamed mwenye umri wa miaka 14 aliyeipatia sifa Tanzania kwa  kunyakua ubingwa wa Dunia wa mchezo wa kuruka kamba kwenye michuano iliyofanyika huko Orlando, Marekani, mwezi uliopita. Kijana huyo, ambaye  awali alilelewa katika kituo cha watoto yatima cha Dogo Dogo  Dar es Salaam, alianza kupata mafunzo ya mchezo huo ambapo alishiriki mashindano ya Afrika Mashiriki yaliyofanyika Mombasa na kunyakua Medali ya Dhahabu. Kulia ni mfadhili wa kijana huyo, Amy Canady, na kushoto kwa Rais Kikwete ni Sister Jean Pruitt, mwanzilishi wa kituo cha kule yatima cha Dogodogo Centre

 Rais Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya dunia 
 Bingwa wa dunia wa kuruka kamba akionesha medali na kombe alivyonyakua Marekani
 Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
 Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
 Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote katika michezo ya kimataifa.

Mwenyekiti wa Sport  Training Centre (TSTF), Dennis Makoi amesema  kuwa walipotambua kuwa kijana huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. Alisema kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili huyo  alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480 kutoka  timu 44 kutoka nchi 14 ambapo jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.

Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania ili kuukuza  ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini kwao  na kuitangaza Tanzania.


Hamisi Mohamed alisema anashukuru kwa malezi aliyoyapata katika kituo hicho cha watoto yatima cha Dogodgo Centre na kwa msaada waliojitolea katika kukiendeleza kipaji chake.

Waraka wa Michael Wambura kuhusiana na sakata la Ukiukwaji Wa Utaratibu Na Sheria Za Marekebisho Ya Katiba Ya Tff 2013.

MAMA ASHA BILAL AFUTURU PAMOJA NA WANAFUNZI WENZAKE WA CHUO CHA DIPROMASIA

$
0
0
  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akizungumza na wananfunzi wenzake wa Chuo cha Dipromasia, baada ya kufuturu wakati alipowaalika katika futari ya pamoja kwenye Makazi yake Oystabay jijini Dar es Salaam, jana Agosti 3.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Dipromasia, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, kwa wanafunzi hao.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Dipromasia, wakipata futari wakati wa hafla hiyo ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, kwa wanafunzi hao
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kike wa Chuo cha Dipromasia, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja aliyoiandaa jana Agosti 3, 2013 kwenye Makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kiume wa Chuo cha Dipromasia, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja aliyoiandaa jana Agosti 3, 2013 kwenye Makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha za upendeleo na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Dipromasia, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja aliyoiandaa jana Agosti 3, 2013 kwenye Makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. 
  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha za upendeleo na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Dipromasia, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja aliyoiandaa jana Agosti 3, 2013 kwenye Makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. 
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa katika picha za upendeleo na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Dipromasia, baada ya kushiriki nao katika futari ya pamoja aliyoiandaa jana Agosti 3, 2013 kwenye Makazi yake Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

BANDA LA NSSF LATIA FORA MAONESHO YA 8 8 KANDA YA MASHARIKI,VIWANJA VYA Mwalimu Julius Nyerere.

$
0
0
 Afisa Biashara mkoa wa Morogoro Lucas Mwaisaka akipata maelezo ya mfuko huo kutoaka kwa Afisa matekelezo wa NSSF mkoa wa Morogoro Christopher Msagati nyuma yake ni Afisa mwandamizi wa Mafao mkoa Morogoro Adolfide Mulokozi baada ya kuvutiwa na huduma zinazotolewa na mfuko huo uwanajani hapo.(picha na Joseph Malembeka)

Twanga Pepeta kutambulisha wapya, Ige Moyaba Iddi Pili

$
0
0
Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” itatambulisha wanamuziki wapya pamoja na warembo watakaoshiriki Miss Ilala siku ya Iddi Pili Katika ukumbi wao wa Mango Garden, Kinondoni.


Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka alisema jana kuwa onyesho hilo limeandaliwa na Bob Entertainment na kudhaminiwa na Konyagi, Freddito Entertainment, Saluti5 na Twitter Pub.


Alisema wanamuziki watakaotambulishwa siku hiyo maalum ni wanenguaji wapya, muimbaji Ige Moyaba ambaye alikuwa mwanamuziki wa bendi hiyo kabla kwenda Ufaransa kuendeleza kipaji chake.


 “Tumeamua kuleta wanenguaji wapya kabisa, wenye damu changa ili kuleta mapinduzi kwenye muziki wa dansi. Madansa wetu ni mabinti warembo, pia tuna  wanenguaji watanashati,” alisema Asha na kuongeza kuwa awameamua kubadilisha wanenguaji ili kuenda na wakati pamoja na soko la muziki.


Kwa upande wa Ige Moyaba aliyetamba kwenye albamu ya ‘Mtu Pesa’ katika mwaka wa 2004,  Asha alisema ameanda vitu vipya kuwapa mashabiki wa bendi hiyo inayotamba kwa staili ya Kisigino.


“Kwa kweli hi siyo onyesho la kukosa kwani itakuwa ni zawadi yetu ya Idd kwa mashabiki wetu,” mkurugenzi huyo alisema.


Mwezi uliyopita Twanga Pepeta walizindua albamu yao ya 10 lijulikanayo kana “Nyumbani ni Nyumbani”. Albamu zingine ambazo zitapigiwa siku hiyo ni Jirani, Fainali Uzeeni, Chuki Binafsi, Ukubwa Jiwe, Mtu Pesa, Safari, Password, Mtaa Wa Kwanza, Mwana Dar es Salaam na Dunia Daraja.


Naye mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga alisema kuwa warembo watakoshiriki kwenye shindano la kumtafuta Redds Miss Ilala pia watatambulishwa siku hiyo.


CATHERINE FOUNDATION YATOA MKONO WA IDD EL FITIRI KWA YATIMA ARUSHA

$
0
0
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha na Mkurugenzi wa Taasisi ya Catherine Foundation, Catherine Magige akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto yatima wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya zawadi za Mkono wa Idd El Fitiri kwa yatima na wasio jiweza.
 Catherine (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi na wasimamizi pamoja na watoto wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha.


 Watoto wa kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha walipata zawadi mbalimbali kwaajili ya siku Kuu ya Iddi.

 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Arusha na Mkurugenzi wa Taasisi ya Catherine Foundation, Catherine Magige akiwa katika picha na watoto mara baada ya kutoa msaada wa vyakula na vitu vingine mbalimbali kituo cha Help for the Maasai kilichopo kwa Mrefu mkoani Arusha leo.
Catherine Magige akiwa na Mwandishi wa Channel 10 mjini Arusha, Jamilah Omar.

Bill clinton atinga Ikulu na 'Daladala

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton baada ya mazungumzo na kisha kushuhudia utiwaji saini mkataba wa maelewano kati ya serikali ya Tanzania na taasisi ya Clinton Foundation kusaidia maendeleo ya kilimo na afya nchini Ikulu jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma
 Gari aina la HIACE likisogea kumchukua Mhe Bill Clinto
Mhe Bill Clinton akiingia kwenye gari baada ya kuhitimisha shughuli zake Ikulu huku mwenyeji wake akimwangalia. Hilo lilikuwa tukio la nadra kwa kiongozi kama huyo kutumia usafiri wa kawaida kama huo.

TAARIFA YA KUMBU KUMBU YA KIFO CHA MAREHEMU DORCAS ANDESO MBUSI

Endapo itatokea Mhe. Edward Lowassa akagombea Urais kweli sintompa kura yangu-Kigwangalla-

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla-Jana nilialikwa na dada yangu Fina wa Mango kwenye show yake adhimu ya Makutano na Fina Mango. Nianze kwa kumshukuru dada Fina na timu yake kwa kazi nzuri wanayofanya. 

Nimshukuru pia Ndg. Uswege Mwaipyana (my Twitter friend) kwa kupendekeza nialikwe na Fina kwenye show, baada ya yeye (Uswege) kufuatilia ile iliyopita Jumamosi iliyotangulia na kuona ingependeza kama nami ningealikwa. 

Niliongelea mambo mengi ikiwemo historia yangu ya utoto na nilivyougua kwashiakor na marasmus na kuponea chupuchupu kufariki dunia kijijini Goweko, Mlimani kwa babu yangu, elimu yangu na uzoefu wangu kwenye uongozi kwenye taasisi mbalimbali nilizopitia. Niliongelea mapinduzi ya kilimo cha Pamba na Alizeti Nzega ambayo ninayaongoza na pia ndoto zangu za Urais, utendaji wa Rais Kikwete na pia hatma ya Taifa letu kwenye mchakato wa kumpata Rais mpya 2015.

 Dada Fina Mango aliniuliza swali moja lililohusisha Urais 2015 na Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb.) ambaye anatajwa tajwa kuwa huenda akawemo among presidential contenders watarajiwa. Majibu yangu yote yalijikita, kama ilivyo kawaida yangu, kwenye ukweli na kwenye tafsiri sahihi ya kimantiki inayotokana na uelewa na utashi wangu. 

Ni kweli nilisema kuwa endapo itatokea Mhe. Edward Lowassa akagombea Urais kweli sintompa kura yangu, sikutafuna maneno, na wala sina chuki ama uadui naye, na nilisema ametenda mengi mazuri na nilisifia ujasiri na umahiri wake kabla ya suala la Richmond, naam kabla ya Richmond saga, niligusia dedication yake, lakini nilihitimisha kwa kusema kuwa kwa zama hizi siwezi kumuunga mkono. Alipofikia panatosha. Naam, panatosha. Kwa kuwa kuna script ya nilichokiongea, acha nikiweke wazi hapa ili wenye kupenda kufuatilia suala hili wajisikilizie wenyewe.  http://www.wavuti.com/4/post/2013/08/sitampa-kura-yangu-edward-lowassa-dk-hamis-kigwangalla.html#axzz2ajMNY4xU

Hongera mdau Shauku kihombo kwa kuendelea na shahada ya uzamili (MBA)

$
0
0

Its a honour to the family of Mr. & Mrs Starford Kihombo that their son SHAUKU KIHOMBOhas been enrolled to continue with Master's Degree at BEIJING INSTITUTE OF TECHOLOGYon 10th september 2013.Shauku is going to major on Masters of Business Administration specifically on Technological Business and Innovation. 
The efforts that he has made during his undergraduate programmes has resulted to this important post.
MR AND MRS STANFORD KIHOMBO -
Shauku Sharing crucial Ideas with Vice President of Beijing institute of Technology,China University.Prof. Zhao Shanglu.

regards

KRANTZ 
CTO & AUTHOR 
MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG

CLOUDS MEDIA GROUP YAPATA IFTAR YA PAMOJA NA WADAU WAKE.

$
0
0
 
 Kampuni ya Clouds Media Group mwishoni mwa wiki iliandaa Ftari ya  pamoja kwa wafanyakazi wake na baadhi ya wadau mbalimbali,maeneo ya  Sinza-jijini Dar Salaam.Pichani kushoto ni  Mkurugenzi wa vipindi na utafiti,Ruge Mutahaba pamoja na Meneja Vipi wa Clouds FM Sebastian Maganga wakiongoza wageni waalikwa mbalimbali kupata ftari.Pichani chini ni baadhi ya wafanyakazi wa  kampuni hiyo na wadau wengine waalikwa wakijipakulia ftari safi kabisa.
Sehemu ya Wadau wakiendelea kupata ftari.

Uchochoro wa kuvusha dawa za kulevya Dar huu hapa.!

$
0
0
MFUMO wa ukaguzi wa wasafiri na mizigo yao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) umetekwa na sasa uko mikononi mwa matajiri na wanasiasa wanaofanya biashara ya dawa za kulevya hapa nchini, MTANZANIA Jumapili linaandika kwa uhakika.
Vyanzo vya habari vya kuaminika vilivyo ndani ya serikali vinavyofanya kazi bega kwa bega na dawati la habari za siasa na uchunguzi la MTANZANIA Jumapili vimedokeza kuwa, baadhi ya watoto wa viongozi wakuu wa nchi, wafanyabiashara wenye ukwasi wa kutisha na wanasiasa wenye utajiri ambao umekuwa ukitiliwa shaka kwa muda mrefu, wamebainika kuingilia mfumo wa kiitelejensia wa JNIA kwa kuupandikizia watu ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa maelekezo yao.
Ripoti ya uchunguzi wa kikachero iliyo mikononi mwa maofisa wa juu serikalini na ambayo waliinukuu katika mazunguzo yao na gazeti hili, inaeleza kuwa mtandao wa matajiri wauza dawa za kulevya umewaondoa wafanyakazi kadhaa watiifu waliokuwa katika kitengo cha ukaguzi wa abiria na mizigo cha JNIA na kupachika watu wao walio kwenye mfumo wa malipo wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya.
Sambamba na hilo, walieleza kuwa kitengo cha kupambana na biashara ya dawa za kulevya nchini kimedhoofishwa na hata mbwa wa polisi waliokuwa wakitumika kukagua mizigo ya wasafiri wanaotumia uwanja wa JNIA wameondolewa katika mfumo wa ukaguzi na sasa watumika kwa nadra, hasa zinapovujishwa taarifa za usafirishaji wa dawa za kulevya ambazo hutolewa aghalabu wafanyabiashara hao wanapohitilafiana kibiashara na kuamua kuumbuana.
Taarifa hizi zimethibitishwa na kauli ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Nzowa, ambaye katika mahojiano yake na MTANZANIA Jumapili, alieleza kuwa mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya hapa nchini una pesa nyingi zinazouwezesha kufanya jambo lolote ili kufanikisha biashara hiyo.
Kamishina Nzowa, ambaye alitakiwa na gazeti hili kutoa taarifa ya uchunguzi kuhusiana na matukio hayo ya dawa za kulevya, likiwemo lile la Watanzania wawili waliokamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na kiasi kikubwa cha dawa za kulevya pamoja na uwezo wa kitengo chake wa kupambana na wauza dawa za kulevya, alisema kazi hiyo ina changamoto kubwa katika kufanikiwa kwake, kwa sababu inawahusisha watu wenye fedha nyingi hapa nchini.
Alisema, Watanzania wawili, Agnes Gerald (25) na Melisa Edward (24), waliokamatwa na kilo 150 za dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini, Julai 5, mwaka huu, walifanikiwa kupita JNIA bila kugundulika kutokana na watu waliokuwa kwenye mashine za ukaguzi wa abiria na mizigo.
“Hawa Watanzania waliopita kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere na kukamatwa Afrika Kusini, waliweza kupita kwa sababu inategemea na watu waliokuwepo kwenye mashine za ukaguzi siku hiyo. Unajua hakuna ushirikiano wa karibu baina ya watendaji wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya. Hilo ni tatizo kubwa linalosababisha vikwazo katika kupambana na mtandao wa dawa hizo.
“Sisi tunategemea kupata taarifa za wauza dawa za kulevya kutoka kwa watu, wakiwemo wakaguzi wa mizigo na abiria, hapo ndipo tunakwenda kumpekua mtu anayeshukiwa kubeba dawa hizo. Tunapopewa taarifa tunafanya ukaguzi, mbwa tunawanusisha, lakini mara chache kwa sababu wakati mwingine wanashindwa kugundua mizigo yenye dawa hizo iliyopuliziwa manukato au kunyunyiziwa kahawa,” alisema Nzowa.
Kamishina Nzowa pia alilalamika kukithiri kwa rushwa kwa watendaji ndani ya kikosi cha kupambana na dawa za kulevya pamoja na jamii kuwa ni jambo ambalo linasababisha kushamiri kwa biashara hiyo.
Mbinu mpya za kusifirisha dawa za kulevya
Duru za uchunguzi za MTANZANIA Jumapili, zimebaini kuwepo kwa mbinu mpya inayotumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kusafirisha mizigo yao tofauti na ile iliyozoeleka.

Wafanyabiashara, wanasiasa na watoto wa viongozi wa serikali wanaojihusisha na biashara hiyo sasa wameligeukia kundi la wasanii wa filamu na wanamuziki wa kizazi kipya wanaotajwa kuwa na tamaa ya utajiri wa haraka haraka na kulifanya wasafirishaji wakuu wa dawa hizo.
Uchunguzi unaonyesha kuwa, wasanii hususan vijana, ndio wanaotumiwa zaidi kubeba dawa za kulevya huku wakihakikishiwa usalama wao na matajiri na wanasiasa wanaotajwa kuwa karibu na baadhi ya viongozi wa serikali wanaowatumia kama kinga yao, kwa makubaliano ya kugawana kipato kinachotokana na biashara hiyo au kuwa katika orodha ya malipo maalumu.
Mbinu zinazotajwa kutumika kusafirisha dawa za kulevya ni pamoja na mzigo baada ya kufungwa hunyunyiziwa pilipili, manukato au kahawa ambazo huondoa uwezo wa mbwa wenye mafunzo maalumu ya kutambua dawa za kulevya kubaini.
Imebainika kuwa dawa za kulevya zilizofungwa vizuri na kunyunyiziwa unga wa pilipili au kahawa juu yake huondoa uwezo wa mbwa kunusa harufu kwa usahihi na badala yake humfanya apige chafya.
Njia nyingine inayotajwa ni kufunga dawa za kulevya ndani ya karatasi ya kaboni ambayo mashine za ukaguzi zilizo katika uwanja wa ndege hazina uwezo wa kubaini kilichofungwa ndani pamoja na uvaaji wa nguo maalumu za ndani za wanawake zinazofahamika zaidi kwa jina la ‘tight’ zilizoshonewa dawa za kulevya ndani ambazo hazitambuliwi kirahisi na maofisa wa ukaguzi, bali humuonyesha mwanamke akiwa amejazia.
TAA wagwaya
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman, alipoulizwa na MTANZANIA Jumapili namna mamlaka yake inavyokabiliana na tishio la ongezeko la upitishaji dawa za kulevya JNIA, alikataa kuzungumza lolote kwa kile alichoeleza kuwa kufanya hivyo ni kuathiri mwenendo wa uchunguzi unaoendelea.

Malipo ya punda wa ‘unga’ 
Taarifa zaidi za uchunguzi zinaonyesha kuwa punda wa dawa za kulevya hulipwa Dola za Marekani 450, ambazo ni sawa na Sh 702,000 kwa kusafirisha mzigo kutoka Dar es Salaam hadi Afrika Kusini. Malipo hayo hufanyika mzigo unapofika salama kwa mnunuzi.

Bei ya sasa ya dawa za kulevya sokoni 
Gazeti hili limedokezwa kuwa bei ya dawa za kulevya inapanda kila wakati kutokana na kamata kamata inayoendelea kwa kudhibiti na kuzuia usafirishaji wake. Imeeleza kuwa cocaine kilo moja inauzwa kwa zaidi ya Sh milioni 50, huku heroine ikiuzwa Sh milioni 45 kwa kilo.HABARI HII KWA HISANI YA GAZETI LA MTANZANIA JUMAPILI.

nani mwehu hapa ?

$
0
0
Ni eneo la Tabata  Relini .

Hotwire PRC brings the Lilac Media Perception Survey to Tanzania

$
0
0
 Kabelo Binns and Davis Seema Sunday Standard Advertisng manager Lilac Awards 2012.
Kabelo Binns and Owen Rampha YaronaFm station manager Lilac Awards 2012
=========   ========  ========= 
Hotwire PRC brings the Lilac Media Perception Survey to Tanzania-


The Lilac Media perception survey is an independently conducted media survey offered by Hotwire Public Relations Consultancy -Tanzania. The Lilac Media Survey focuses on the public’s perception of local media as voted by the respondents over a specific given period of time.


 “We have used The Lilac Media Survey in other African markets such as Botswana and Mozambique, where it was a huge success. This unique tool provides information on the general perception of the public on local media. These perceptions help give valuable feedback to media houses,” Said Mr Kabelo Binns, the Group Managing Director of Hotwire Africa who was in Dar es Salaam last week.


The Lilac Survey targets the entire Tanzanian public at large, addressing the various demographics which include gender, age and basic income. The Lilac Media Survey is an innovative idea fully owned by Hotwire PRC. The Survey is all about what the public actually feels and thinks about the local media on which they depend on to get their daily information. Hotwire PRC prides itself in bringing to the forefront a professional platform for media houses to be able to do their work better.



Hotwire is a Pan African PR Consultancy that has opened its doors in Tanzania under the Roots255 stable of brands. “We are very excited to be able to offer our clients great value adds from the Hotwire suite of services. The Lilacs are just the beginning,” promised the MD of Roots255, Denise Rosiello.


Exim Bank hosts Iftar for Zanzibar clients.

$
0
0
 The Zanzibar Acting Secretary to the Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo (centre) addresses Muslims in Zanzibar during an Iftar event organized by Exim Bank at the weekend in line with the Holy month of Ramadan. Looking on is the Zanzibar Minister without portfolio Machano Othman Said (left) and Exim Bank Zanzibar Branch Sales Manager Mohamed Ally
 The Zanzibar Acting Secretary to the Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo (centre) addresses Muslims in Zanzibar during an Iftar event organized by Exim Bank at the weekend in line with the Holy month of Ramadan. Looking on is the Zanzibar Minister without portfolio Machano Othman Said (left) and Exim Bank Zanzibar Branch Sales Manager Mohamed Ally.
 The Zanzibar Acting Secretary to the Mufti, Sheikh Thabit Noman Jongo (left) addresses Muslims in Zanzibar during an Iftar event organized by Exim Bank at the weekend in line with the Holy month of Ramadan. Looking on at the right is the Mjini Maghrib Regional Police Commander (RPC) Mkadam Khamis. 
The Zanzibar Minister without portfolio Machano Othman Said (second left) addresses Exim Bank clients during an Iftar event organized by Exim Bank at the weekend in line with the Holy month of Ramadan.Looking on at  the left is the Exim Bank Tanzania Retail Banking Head Ramakrishna Rao and the Exim Bank-Zanzibar Branch Sales Manager Mohamed Ally (right). 
=======     ========   =======
Exim Bank hosts Iftar for Zanzibar clients.

IN keeping with the spirit of sharing during the Holy Month of Ramadan that ends this week, Exim Bank Tanzania held an Iftar event for its Muslim clients in Zanzibar during the weekend.

The event was officiated by the Zanzibar Minister without portfolio Machano Othman Said who called upon Muslims to live in line with the principals of the Islamic faith. Speaking during the function, the Exim Bank Tanzania Retail Banking Head Ramakrishna Rao said his bank is committed to providing tailor-made products to the people of Zanzibar in a bid to reduce the unbanked gap.

 “Exim Bank understands the importance of the holy month of Ramadan .This Iftar event is yet another opportunity to interact with our muslim clients.
“We are committed to providing tailor-made products to our Zanzibar clients in a bid to reduce the unbanked gap,” he said.

The event was among other dignitaries attended by Mjini Maghrib Regional Police Commander (RPC)Mkadam Khamis .

MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA KUMUAPISHA RAIS WA IRAN.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya IRAN Mhe. Al-Akbar Hashemi Rafsanjani wakati Makamu wa Rais alipofika kwenye Makazi ya Rais huyo mjini Teheran Iran leo Ogast 05-2013, Makamu wa Rais yupo Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo alieapishwa jana jioni. (Picha na OMR Teheran)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya IRAN Mhe. Al-Akbar Hashemi Rafsanjani wakati Makamu wa Rais alipofika kwenye Makazi ya Rais huyo mjini Teheran Iran leo Ogast 05-2013, Makamu wa Rais yupo Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo alieapishwa jana jioni. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, kipata maelezo kutoka kwa maafisa wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya kiislam ya Iran alipotembelea makazi ya Rais Al-Akbar Hashemi Rafsanjani mjini Teherani Iran leo Ogast 05-2013.

==========  ========   ========
MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA KUMUAPISHA RAIS WA IRAN, AGOSTI 05, 2013

Makamu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana alikuwa mmojawapo wa wageni mashuhuri katika sherehe za kumuapisha Rais wa mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran  Mheshimiwa  Hassan Rouhani, sherehe iliyofanyika katika makao makuu ya nchi hiyo yaliyopo jijini Tehran. Kabla ya sherehe hiyo ya kuapishwa, Jumamosi Agosti 4, 2013, Mkuu wa Kidini wa nchi hiyo Ayatollah Ali Khamenei alimthibitisha Rais Rouhani na akatumia nafasi hiyo kufafanua kuhusu aina ya mahusianio ambayo Iran inataka kuyaona baina yake na nchi zingine duniani.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alikuwa miongoni mwa viongozi wapatao 55 kutoka nchi mbalimbali walioshiriki sherehe hizi huku vyombo vya habari kutokana nchini Iran vikielezea kuwa tukio la jana kwamba ni la kihistoria kwani Iran haikuwahi kuwa na wageni mashuhuri wengi kiasi hicho katika sherehe zake za kuapisha viongozi wa nchi hiyo. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais aliyemaliza muda wake, Rais Mahmoud Ahmadinejad.

Akihutubia wananchi wa Iran sambamba na wafutiliaji wa siasa za Iran mara tu baada ya kuapishwa, Rais Rouhani alisema Iran inategemea kuwa nchi za ulimwengu wa kwanza zitatafuta suluhu nayo kwa mazungumzo na siyo kwa kutumia vikwazo. Kauli hii alikuwa anaitoa siku moja baada ya seneti ya Marekani kupitisha kwa azimio moja vikwazo zaidi kwa Iran saa chache kabla ya Rais Rouhani kuthibitishwa na Ayatollah Khamenei, Kiongozi mkubwa kabisa na mwenye heshima ya juu katika Iran.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kimashirikiano wanaamini kuwa serikali ya Rais Rouhani ambayo aliitangaza mara tu baada ya kuapishwa, itaanza kazi kwa wakati huku ikibadili uelekeo kutoka katika siasa za mrengo wa kushoto na kuwa siasa za kawaida ambazo zitafungua mahusiano zaidi na nchi za Mashariki.

Tanzania ina uhusiano wa siku nyingi na Iran na siku kadhaa za mwisho wa utawala wa Rais Ahmadinajad, Iran ilikubali kuifutia Tanzania deni lake lililokuwepo kwa miaka mingi kwa lengo la kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Pia, Iran imekuwa ikisisitiza ukuzaji wa biashara hasa ya nyama kati yake na Tanzania huku kukiwa tayari na makampuni kadhaa ktoka Iran yanayowekeza katika eneo la Ujenzi.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alipata fursa ya kukutana na Rais wa tatu wa Iran Akbar Hashem Rafsanjeni na kufanya naye mazungumzo kuhusu mashirikiano baina ya nchi zetu mbili. Rais Rafsanjeni aliyepata kufika Tanzania mwaka 1996 alisisitiza kuwa kuna mengi ambayo Iran ilipanga kufanya na Tanzania mbayo yalizorota baada ya utawala wake lakini ni imani yake kuwa yataendelea kufanyiwa kazi sasa. Baadhi ya maeneo aliyoyajadili ni katika elimu ambapo katika kipindi chake alianzisha kozi za Kiswahili katika vyuo vya Iran na eneo lingine likiwa la kuwezesha upatikanaji wa viwanda vya Korosho.

Kwa upande wa Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Rais Mstaafu Rafsanjeni kuwa, Tanzania inatambua uhusiano wa kihistoria iliyonao na Iran na kwamba ina nia ya dhati kuona uhusiano huo unaimarika zaidi na hasa katika maeneo ya uwekezaji na biashara za pamoja. Rais Mstaafu Rafsanjeni alisema kuwa Iran kwa sasa inakabiliwa na vikwazo kadhaa ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimekwamisha baadhi ya mambo ambayo wao kama nchi waliyapanga kuyafanya lakini akafafanua kuwa anaona tuendako kuna nuru hivyo mafanikio ya kutimiza makubaliano baina ya nchi zetu yanaweza kufikiwa.

Msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais ambao pia uliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Maalim umeondoka leo hapa Tehran kurejea nyumbani. “Tuna mengi ya kujifunza kutoka Iran na uhusiano wetu wetu una kila sababu ya kudumishwa,” alimalizia Mheshimiwa Makamu wa Rais baada ya kuagana na Rais Mstaafu Rafsanjeni na saa chache kabla ya kurejea nyumbani.

Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Tehran, Iran
Jumatatu Agosti 05, 2013

MSAJIRI WA VYAMA VYA SIASA JOHN TENDWA ASTAAFU,RAIS KIKWETE AMTEUA JAJI FRANCIS MUTUNGI KUSHIKA NAFASI YAKE.

$
0
0
Jaji Francis S.K.Mutungi.Picha kwa hisani ya Robert Okanda.
========   =========  =========
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
             press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.


5 Agosti, 2013

Chimwemwe atamba kumchapa Cheka

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Best Man Promotion, Zumo Makame (katikati) akiwatambulisha mabondia wawili kutoka Malawi,  Chiotcha Chimwemwe (kulia) na Bgright Mdoka (kushoto) kwa waandishi wa habari tayari kwa mapambano yao ya Agosti 10. Cimwemwe  atapambana na Cheka wakati Mdoka atazipiga na Jitu Samia. Mwingine katika picha ni promota wa Chimwemwe, Steven Msiska. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Best Man Promotion, Zumo Makame (kulia) akimtambulisha bondia Chiotcha Chimwemwe  kwa waandishi wa habari tayari kwa mapambano yao ya Agosti 10 dhidi ya mtanzania, Francis “SMG” Cheka lililopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro
 Bondia Chiotcha Chimwemwe akitoa tambo zake kwa Cheka  kwa waandishi wa habari. Chimwemwe atapambana na Cheka Agosti 10 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika pambano lililoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Best Man Promotion, Zumo Makame.
=========   ==========   ==========
Chimwemwe atamba kumchapa Cheka

BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa wa Malawi, Chimwemwe Chiotcha amewasili nchini na kutamba atamtwanga bondia alisyekuwa na mpinzani Tanzania, Francis “SMG” Cheka katika pambano lao la uzito wa super-middle lililopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Chimwemwe ambaye hajawahi kupoteza pambano nchini Malawi zaidi ya kupigwa kwa pointi na Cheka Desemba 27 mwaka jana, alisema kuwa amekuja kulipiza kisasi huku akiponda matokeo ya awali kuwa Cheka alibebwa sana.
Alisema kuwa hajui ni ushindi wa aina gani atakaoupata kwa bondia huyo, kwani Knock Out (KO) au Technical Knock Out (TKO) utokea ulingoni tu na wala si ushindi wa kupangilia. “Nimekuja hapa kushinda na wala si vinginevyo, nakuja Cheka amejiandaa sana, sikuridhika na matokeo ya awali na ndiyo maana nimeamua kuja kurudiana naye, najua nitaibuka na ushindi,” alisema Chimwemwe.
Alifafanua kuwa si kweli kuwa kila bondia aliyepigana na Cheka na kushindwa kuwa hajui ngumi za kulipwa zaidi ya hofu tu kutoka kwa mabondia hao. Mimi nimedhamilia kufanya kweli na ninajua nitashinda, hii ni fursa yangu,” alisema Chimwemwe ambaye ni mwanajeshi wa Jeshi la Malawi.
Mkurugenzi wa kampuni ya Best Man Promotion inayoaandaa pambano hilo, Zumo Makame alisema kuwa maandalizi ya pambano yamekamilika na siku hiyo kutakuwa na mapambano makali nay a kusisimua.
Makame aliyataja mapambano hayo kuwa, Deo Njiku atawania ubingwa wa Taifa wa Shirikisho la Masumbwi la PST dhidi ya Cosmas Cheka, Rashid “Snake Man” Matumla atazichana na Maneno “Mtambo wa gongo “ Oswald na bondia mwingine kutoka Malawi, Bright Mdoka atazipiga na Jitu Samia.
Mapambano mwngine kwa mujibu wa Makame ni Nasibu Mkude atapigana na Juma Kihiyo katika uzito wa super welter bout, Juma Afande v Epson (featherweight) na  Karim Mandonga dhidi ya Ramadhan Agogo katika uzito wa superwelter

Event Planners & Consultants yawavutia wadau wake maonesho ya nane jijini Arusha.

$
0
0
SAM_1063
Mmoja wa Wahudumu  ndani ya banda la Konyagi,Bi.Matha Charles pichani kushoto akimuonesha mmoja wa wateja aliyetembelea banda hilo,kinywaji kipya cha kampuni hiyoo kiitwacho Zanzi kwenye maonesho ya Nane jijini Arusha,ambapo watu mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kuyashuhudia maonseho hayo.SAM_1057Katika msimu huu wa sherehe za nane nane ,kampuni ya Event Planners &Consultants inawakaribisha katika banda la Tanzania Distilleries Limited linalojulikana kama JUMBA LA KONYAGI lililopo katika maonyesho ya nane nane Njiro,jijini Arusha.
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images