Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1337 | 1338 | (Page 1339) | 1340 | 1341 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akisikiliza maelezo kutoka kwa Inspekta Ibrahim Samwix, wakati alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (aliyevaa suti), akisikiliza maelezo jinsi uvunjaji wa sheria za usalama barabarani unavyoweza kusababisha ajali, wakati alipotembelea banda la Maaskari wa usalama barabarani, kwenye Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akimkabidhi tuzo Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa kutambua mchango wake katika suala nzima la Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Balozi wa Usalama Barabarani, Samira Abuu (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kupokea cheti cha kutambua mchango wake katika masuala ya Usalama Barabarani wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani lililofanyika jana, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Mgeni Rasmi,Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akizungumza wakati wa Tamasha la Usalama Barabarani ambapo aliwaasa watumiaji wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazosababisha ulemavu na vifo.Tamasha hilo limefanyika jana, Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0


  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwakabidhi bendera ya taifa askari kumi (10) waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa kwenye picha ya pamoja na askari waliopata uteuzi wa kwenda kuiwakilisha nchi ya Tanzania kwenye kazi ya Ulinzi wa Amani nchini Sudani ya Kusini (UNMISS) IGP Sirro, amewataka askari hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya sheria na taratibu. Picha na Jeshi la Polisi.

  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Bi Zuhura Sinare Muro akikabidhi vifaa vya malazi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku. Makabidhiano hayo yalifanyika katika kituo hicho, Zanzibar.

  Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Bi Zuhura Sinare Muro akikabidhi vyakula na vifaa vya malazi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku. Makabidhiano hayo yalifanyika katika kituo hicho, Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Bi Zuhura Sinare Muro akikabidhi vyakula na vifaa vya malazi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku. Makabidhiano hayo yalifanyika katika kituo hicho, Zanzibar.

  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania Bw. Cosmas Kimario (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyakula na vifaa vya malazi vyenye thamani ya shilling 2,963,000 katika kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage, Zanzibar. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro, Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku (wapili Kushoto), Mkuu wa masoko na mahusiano Bi, Christine Manyenye (wakwanza kulia) na Mkuu wa huduma za kibenki za Kiislamu Bw. Rashid Rashid (wakwanza kushoto)

  Uongozi na wafanyakazi wa Benki ya KCB kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku (waliokaa, watatu kushoto) na watoto wa kituo hicho.

  Baadhi ya watoto wa Montessori School and Orphanage wakitoa burudani kwa uongozi wa benki ya KCB.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Montessori School and Orphanage Bi. Susana H. Maziku (wapili Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuishukuru Benki ya KCB kwa mchango wao katika kituo hicho.

  Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vyakula na vifaa vya malazi vyenye thamani ya shilling 2,963,000 katika kituo cha watoto yatima, Montessori School and Orphanage, jana Zanzibar.


  Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya KCB Bi Zuhura Sinare Muro na Wafanyakazi wa Benki ya KCB wakifanya ziara katika kituo cha Montessori School and Orphanage.
  ……………………………………………………………


  Benki ya KCB Tanzania imekabidhi misaada mbalimbali kwa kituo cha watoto yatima Montessori School Orphans Organization kisiwani Unguja.

  Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Bw, Cosmas Kimario alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

  “Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu”, Bw. Kimario alisema na kubainisha kwamba tangu benki hiyo ilipofunguliwa hapa Tanzania mwaka 1997, benki hiyo imekuwa ikijikita katika kuisadia jamii.

  Alisema ni vyema jamii ikatambua uwepo wa watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo, kwa kuwapatia mahitaji mabalimbali kama wanavyopata watoto wa majumbani kwani ni haki yao ya msingi. “Tukiwajali hawa watoto hata kwa Mungu tunapata dhawabu kwani wengi wao hawajapenda kuwa katika mazingira haya” alisema Kimario.

  Bw. Kimario, Alielezea kuhusiana na programu endelevu inayoitwa KCB 2jiajiri, na kusema; “KCB 2jiajiri ni programu inayowapa elimu ya nadharia na vitendo wanawake wajasiriamali nchini. Zanzibar, KCB 2jiajiri imefundisha wanawake 32 darasani na maafisa wetu watatu ambao ni wa masoko, fedha na sheria wanazitembelea biashara za wakinamama hao ili kuwapa elimu kwa vitendo.”

  Benki ya KCB ilikabidhi misaada mbalimbali ikiwemo magodoro, mashuka, neti na vyakula.vyenye thamani ya shilling 2,963,000. Mwenyekiti wa bodi ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro alielezea kuhusiana na mchango wa benki hiyo Zanzibar na kusema “Benki ya KCB mbali na kufanya biashara imekuwa ikijihusisha katika miradi mbalimbali yenye manufaa kwa wazanzibari wahitaji.”

  Bi. Muro alizitaja baadhi ya michango iliyotolewa na benki hiyo ili kuinua hali ya maisha ya wananchi wenye shida kuwa ni; ujenzi wa kisima cha maji Mazizini Orphanage Centre, utoaji wa vyakula mbalimbali kwa Zanzibar Hayunani Association, vifaa vya kusomea na kuandikia katika shule ya Bwefum na vifaa tiba katika hospitali za Kivunge Cottage, Mwembeladu na Kombeni. Kwa misaada hii yote Benki imetumia zaidi ya milioni 100.

  Mkurugenzi wa kituo cha Montessori School Orphans Organization Susan H. Maziku aliishukuru benki ya KCB kwa mchango wake katika kituo hicho na kuwataka makampuni na jamii kuiga mfano huo wa kuwakumbuka watoto yatima wenye uhitaji mkubwa sana.

  0 0

  Makamu wa Rais mhe. Samia Saluhu akimkabidhi Meneja wa kanda ya Kusini wa Kampuni ya Tigo  Uthmaan Madati tuzo ya  ushindi wa pili kipengele cha mawasiliano kwenye maonesho ya nanenane yaliyomalizika hivi karibuni kitaifa mkoani Lindi


  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mke wake Mary wakimjulia hali  leo August 13.2017 ,Mbunge wa Viti maalumu CCM Mkoa wa Kigoma  Mheshimiwa Josephine Ngezabuka .ambaye amelazwa kwa matibabu katika Hosptali ya Muhimbili (MOI) Baada yakupata ajali hivi karibuni Mkoani Kigoma. katikati mwenye miwani ni Naibu spika Dkt. Tulia Akson.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
  Naibu Spika Dr Tulia Akson mwenye miwani  akiwa na Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako (c) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Catherine Magige wakimjulia hali  leo August 13.2017 ,Mbunge wa Viti maalumu CCM Mkoa wa Kigoma  Mheshimiwa Josephine Ngezabuka ,ambaye amelazwa  kwa matibabu katika Hosptali ya Muhimbili (MOI) Baada yakupata ajali hivi karibuni Mkoani Kigoma.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheir (kushoto) mara alipowasili katika Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo.  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili Shehia ya Kinyasini katika Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Viongozi mbali mbali mara alipowasili Shehia ya Kinyasini katika Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini”A” Unguja Hassan Ali mara alipowasili Shehia ya Kinyasini katika Uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo akiwa katika ziara ya kutembelea Miradi mbali mbali ya maendeleo


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia Ujenzi wa Mradi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini”A” Unguja wakati alipofanya ziara maalum ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Mkoa wa Kaskazini Unguja
  Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika sherehe ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza na Wananchi hao alipofanya ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mkandarasi wa Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini”A” Unguja Nd,Ali Mbarouk na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ZECCON CO LTD,wakati alipoweka jiwe la msingi Ujenzi huo leo alipofanya ziara maalum ya kutembelea Miradi ya Maendeleo,(kushoto) Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamadi Rashid Mohamed
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mbyu maji alipofika kuangalia maendeleo na kupata maelezo mafupi juu ya huduma za jamii,karika Wilaya ya Kaskazini “A:” Unguja leo alipofanya ziara ,maalum Wilayani humo, [Picha na Ikulu.] 13/08/2017.

  0 0

   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano ambazo kati ya nyumba 10 zilizojengwa na NHC, nyumba saba zimeishanunuliwa.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikabidhi hati kwa wamiliki wa awali wa eneo la Safari City wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano na makabiadhiano ya Hati Miliki za Viwanja 100 kwa ajili ya Uendelezaji.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikabidhi hati kwa wamiliki wa awali wa eneo la Safari City wakati wa uzinduzi wa nyumba za mfano na makabiadhiano ya Hati Miliki za Viwanja 100 kwa ajili ya Uendelezaji.

   Baadhi ya Nyumba zilizokamilika ujenzi wake katika Eneo la Safari City mkoani Arusha.
   Waziri Lukuvi akipokea taarifa ya ufutwaji wa mashamba kumi na mbili (12) yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
   Waziri Lukuvi pamoja na viongozi wa mkoa wa Arusha wakifanya ukaguzi wa eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.

   Waziri Lukuvi pamoja na viongozi wa mkoa wa Arusha wakifanya ukaguzi wa eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.
   Eneo la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya Arusha Gabriel Fabian wakiteta jambo wakati wa Uzinduzi wa Safari City.

  0 0


  0 0

  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole (wa pili kushoto) akiongoza nyimbo ya hamasa mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana kuwasili kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

  Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani (kulia) ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo(kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi .

  Katibu Mkuu wa CCM ndg:Abdulrahman Kinana akifunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

  Katibu wa NEC Uchumi na fedha Dkt.Frank George Haule hawassi akiwasilisha mada wakati wa mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Mikoa CCM
  tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.

  baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini Mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  maofisa wa chama wakifuatilia kwa umakini Mafunzo elekezi kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Mafunzo yakiendelea

  washiriki Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani wakiwa katika mijadala kwa makundi mbalimbali kuchambua yale walio jifunza katika mafunzo elekezi yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Katibu wa NEC Oganaizesheni ndg: pelela Ame Silima,akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ndg:Humphrey Polepole akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela  ubinga,akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa
  Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makao makuu ya CCM mjini Dodoma.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM- Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Mabodi, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo elekezi ya siku mbili kwa
  Makatibu wa Mikoa CCM tanzania bara na Visiwani yaliofanyika katika Ukumbi wa sekretariet katika jengo la ofisi ya makaomakuu ya CCM mjini Dodoma.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

  0 0
  · Yasajili wateja wapya 132,826 kwa kipindi cha miezi mitatu
  · Wateja wapya 1.038 milioni wa Airtel Money wasajiliwa

  Airtel Tanzania ndio kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania ambayo imefanikiwa kuongeza wateja wengi kwenye robo ya pili ya mwaka huu huku makampuni ya simu za mkononi wakishindania kuongeza wateja wapya na watumiaji wa huduma za kifedha kulingana na ripoti ya Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA).

  Kulingana na ripoti ya robo ya pili ya 2017 (TRCA’s Quarterly Communication Statistics Report), makampuni ya simu za mkononi Tanzania yaliongeza watumiaji wapya wa huduma za kifedha 1,059,163 milioni kwa kipindi cha April mpaka Juni.

  Kutokana na idadi hiyo, Airtel Tanzania ilisajili wateja wapya 1,038,193. Hii inamaanisha ya kwamba kwa kipindi hicho asilimia 98 ya wateja wa huduma za kifedha za simu za mkononi wapya waliojiunga na Airtel Tanzania.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema ‘Hii ni ishara nzuri kuwa Airtel inatoa suluhisho sahihi kwa huduma za kifedha kwa makampuni ya simu za mkononi hapa Tanzania. Kwa mfano tuangalie huduma ya mikopo rahisi ya Timiza inayotolewa kupitia Airtel Money, hatimaye imeanza kuzaa matunda’.

  Huduma ya mikopo ya Timiza inadhihirisha juhudi zetu za kutoa suluhisho inapokuja suala ya huduma za kifedha kwa kutumia simu za mkononi. Pia inaenda samba samba na juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wafanya biashara wadogowadogo na wakati wanapata huduma ya mikopo yenye marshati nafuu, alisema Singano.

  Ikiwa na ongezeko la 1.038 milioni, Airtel Tanzania kwa sasa ina jumla ya wateja milioni 5.9 wa Airtel Money kwenye soko ambalo jumla ya makampuni matano ya simu za mkononi yanashindania wateja milioni 20. Airtel Tanzania pia imefanikiwa kusajili laini mpya 132,826 kwenye robo ya pili ya mwaka na hivyo kufikisha jumla ya watejakuwa milioni 10.3. Kwa ujumla, jumla ya wateja wapya wa simu za mkononi waliongeza na kufikia 40.358 milioni mwishoni mwa mwezi Juni kutoka 39.856 mwishoni mwa Machi mwaka huu.

  Kwa kuendeleza uwekezaji zaidi nchini kwa mujibu wa Singano anathibitisha kuwa Airtel Tanzania inazidi kukua vizuri huku kampuni hiyo ikiendelea kuwekeza zaidi kwenye miradi mbali mbali ili kufuta wateja wengi wapya.

  Moja ya mradi mkubwa wa uwekezaji ni mradi wa U900. Kulingana na Singano, Mradi wa U900 unatafuta kuboresha miundombinu ya kiufundi kwa nia ya kuongeza kiasi cha data na kuboresha kasi ya data

  "Hii mikakati yetu ya kuimarisha maisha ya Tanzania kupitia huduma za kidigitali. Katika jiji la Dar es Salaam zaidi ya maeneo 300 tayari yamebadilishwa, mpango wetu ni kueneza mradi wetu wa U900 kwa mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dodoma, Arusha na kisha katika masoko mengine yenye uwezo mkubwa hapa nchini Tanzania, "aliongeza Singano.

  0 0

   Mkuruegenzi  Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza  na Wanafunzi  wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya  nje ya nchi  wakiwa na  wazazi wakipata taarifa juu taarifa mbalimbali kabla ya safari ya kwenda katika vyuo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Zamani wa Elimu, Mbunge wa Bagamoyo, Mhandisi Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje katika Mkutano ulioandaliwa na Global Education Link (GEL) 
   Afisa wa Habari Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU),Edward Mkaku akizungumza juu ya Global inavyofanya  kazi kwa ukaribu  na TCU kwa wanafuzi wanaokwenda  kuwa  taarifa za  tuume hiyo.
   Mwanasaikolojia ,Chris Mauki akizungumza juu ya masuala ya Saikolojia katika kuwajenga wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje ya nchi.
   Baadhi ya wazazi wakichangia maada zinazohusiana na wanafunzi wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya Nje ya Nchi.  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi akishuka kwenye ndege yake baada ya kuwasili nchini mchana huu, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais Dkt. John Pombe Magufuli. 
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake,  Rais wa Jamhuri ya Misri, Mhe. Abdel Fattah El-Sisi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa J.K Nyerere, Jijini Dar es salaam mchana huu, ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili Agosti 14-15, 2017. 
  Rais wa Jamhuri ya Misri Mhe. Abdel Fattah el-Sisi akisalimiana na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili nchini hivi punde kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe  akizungumza  na  ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco waliofika  Mkoani  Dodoma kwa ajili ya kuanza shughuli za awali za ujenzi  wa  eneo  changamani  la Michezo .Kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na  Michezo  Mhe.Dk.Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu kutoka Morocco waliofika Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuanza shughuli za awali za ujenzi wa eneo changamani la Michezo.Wengine pichani  ni  Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw.Petro Lyatuu.Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.


  0 0

  Mamia ya watu wenye Ulemavu wa Miguu wamejitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, kuchukuwa vipimo kwanajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.

  Mwitikio huo ni kufuatia Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.Paul Makonda kuwatangazia wenye uhitaji ya Miguu Bandia kufika ofisini kwake kwa ajili kuchukuliwa vipimo ili wapatiwe miguu hiyo bila malipo, ambapo hadi saa nne asubuhi walemavu waliokuwa wamefika ni zaidi ya 500.

  Makonda amesema licha ya idadi hiyo kuzidi ile ya watu 200 iliyokusudiwa atahakikisha wote wanapimwa na wataalamu na kupatiwa huduma bila ubaguzi wa Mikoa wanayotoka sababu wananchi wote wapo chini ya Rais Dkt.Magufuli.

  Amesema wote watakaopimwa watatengenezewa Miguu yao kulingana na vipimo vilivyochukuliwa.Hata hivyo Makonda amesema kutokana na wingi wa watu wenye uhitaji ataongeza siku za upimaji na kuongeza idadi ya wataalamu ili wote watakaofika wahudumiwe.

  Aidha amesema awamu hii ya kwanza walemavu 200 watapatiwa miguu ya bandia wakati akiendelea kufanya jitiada za kuwasiliana na wadau ili waweze kuchangia na kuhakikisha wananchi wote wanahudumiwa.

  Mbali na miguu bandia pia Makonda amefanikiwa kupata Magongo ya kisasa 17 kutoka Nchini Marekani ambayo pia atayatoa bila malipo kwa wale wenye uhitaji.
   Baadhi ya watu wenye Ulemavu wa Miguu wakiwa wamejitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, kuchukuwa vipimo kwa ajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.
  Mkuu wa Mkoa  Mh.Paul Makonda akizungumza na baadhi ya watu wenye Ulemavu wa Miguu waliojitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi yake , kuchukuwa vipimo kwa ajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.
  Mkuu wa Mkoa  Mh.Paul Makonda akizungumza na mmoja wa  watu wenye Ulemavu wa Miguu waliojitokeza kwa wingi leo kwenye Ofisi yake , kuchukuwa vipimo kwa ajili ya kupatiwa Miguu bandia ambapo idadi imekuwa kubwa tofauti na ilivyo tarajiwa, huku wengine wakitokea Mikoani.

  0 0

   Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na mgeni wake wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Misri zikipigwa uwanjani hapo.
   Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akikagua gwaride la Heshima mara baada ya nyimbo za Taifa kupigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi akiangalia vikundi vya ngoma za asili mara baada ya kuwasili nchini. PICHA NA IKULU

  0 0

  Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) limejipanga kuanza kutekeleza kwa vitendo fursa zitakazotokana na ujenzi wa mradi mkubwa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleni Tanga kwa kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi watakaotaka  kuzitumia fursa hizo.

  Mradi huo mkubwa uliosainiwa mwezi mei mwaka huu na kuwekwa jiwe la msingi hivi karibu na Rais John Magufuli na Yoweri Museveni wa Uganda unalenga kutoa fursa za kiuchumi kwa watanzania.

   Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi Beng’i Issa alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwisho mwa juma, kwamba wamejipanga kuwaelimisha, kuwaonesha na kuwawezesha wananchi kuzitumia fursa za ujenzi wa maradi huo kuanzisha shughuli za kiuchumi.

  “Tuejipanga vizuri katika kuwaelimisha, kuwaonesha fursa zitakazo kuwepo na kuwapa uwezesha kupitia mifukoa ya uwezeshaji 19,” serikai imeweka fedha katia mifuko hii hivyo waahitajika kuchagamikia,aliongeza kusema Bi. Issa.

  Alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kutoa fursa za ajira 10,000 na baada ya hapo kutakuwa na ajira 1,000 kwa watanzania,  na pia amezitaka Taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi stadi ikiwemo VETA kuendelea kuandaa vijana watakao endana na fursa za ujenzi huo.

  Bi. Issa  alizitaja shughuli za kiuchumi zinatarajiwa kuwepo katika mradi huo ni biashara za usafirishaji wa bidhaa na watu, ujenzi wa miundombinu mbalimbali, huduma za chakula, uuzaji wa bidhaa za chakula, ulinzi, uuzaji wa vifaa vya ujenzi.

  Zingine ni huduma zingine ni kama vile  afya, sheria, fedha, bima, huduma za taka, huduma ukarabati na vifaa vya usalama kazini.  

  Alifafanua kwamba baraza litashirikiana na mikoa ambayo bomba hili linapita kama vile Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga na wilaya 24 na vijiji 184 ili kuhakikisha kwamba wananchi wana shiriki kikamilifu katika mradi huo.

  “Sisi tumejipanga na tutakuwa karibu na ujenzi huu na fursa zote kadiri zitakavyo zinajitoeza tutazitangaza katika tovuti yetu “ na pia watazipata katika halmashauri zao,” alisema

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC, Bw. James Washima alisema kwamba taasisi yake imejipanga kuwawezesha watanzania kupata uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali na wafanya biashara ili kuweza kuzitumia fursa katika mradi huo mkubwa.

  “Tunatoa mikopo ya aia mbalimbali tunawakaribisha kuja kuomba mikopo ili wazitumie fursa za mradi huu wa bomba la mafuta,” alisema Bw. Washima.

  Aliogeza kusema wanaotaka ni vyema kuwa katika vikundi, watapata mikopo wanayotaka ikiwemo ya vitendea kazi na mikopo ya kutekeleza zabuni walizoshida na afuzo ya ujasiriamali.

  Naye Msajili Msaidizi wa Maendeleo na Tafiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB),Bw. David Jere alisema kwamba wakandarasi wanahitajika kujiunga katika ubia ili kuwa na sifa ya kuingia katika mradi huo mkubwa wa ujenzi wa bomba hilo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dkt. John Jingu wa pili kushoto akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumzia namna baraza litakavyo waelimisha wananchi kutumia fursa za mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta toka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga Tanzania, wa pili kulia Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa, kushoto Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hudua za Kifedha na Mikopo-UTT Microfinance PLC. (Picha na Mpigapicha Wetu).

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa kilichokuwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Chabanga Hassan Dyamwale (76).

  Mbali wa wadhifa huo katika eneo la mpira wa miguu, pia Dyamwale atakumbukwa zaidi akiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na kwa miaka ya hivi karibu alikuwa Mjumbe wa Kamati huru ya uchaguzi TFF tangu 2004 mpaka 2012.

  Hayati Dyamwale aliyezaliwa Juni 01, 1941, aliondoka FAT mwaka 1978, lakini pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo nchini miaka ya mwanzo ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Handeni mkoani Tanga kuwa Ofisa Utamaduni, lakini Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere akamrudisha Dar es Salaam.

  “Nimeguswa na kifo cha Mzee Chabanga Hassan Dyamwale. Inna Lillah wainaillah Rajauun. Natuma salamu zangu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, majirani na marafiki wa hayati Mzee Dyamwale ambaye nimetaarifiwa kuwa amefariki dunia Agosti 13, mwaka huu kwenye Hospitali ya Muhimbili,” amesema Karia.

  “Ni msiba mkubwa kwa wanafamilia ya michezo hususani soka,” amesisitiza Rais Karia na kuomba familia, ndugu, jamaa, marafiki kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu baada ya kumpoteza mpendwa Dyamwale.

  Rais Karia amesema: “Namfahamu Mzee wetu huyu tangu miaka mingi akiwa mteuliwa kutoka serikalini kushika wadhifa wa utendaji ndani ya FAT wakati ule (Kwa sasa ni TFF), alifanya kazi kwa uhodari mkubwa na uadilifu,” amesema Rais Karia.

  Rais Karia amesema kwamba mbali ya kuwa mtendaji ambaye alifanya mabadiliko makubwa katika soka la Tanzania kutoka ligi ya kituo kimoja hadi ligi ya mikondo miwili (nyumbani na ugenini). Taarifa zinasema kwamba alifanya kazi hiyo akiwa kwenye hema.

  Pia Rais Karia alimfahamu Mzee Dyamwale alipokuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Uhuru) aliyekuwa mtaalamu wa masuala ya ujenzi wa viwanja.

  Rais Karia amesema kwamba atambukuka zaidi hayati Dyamwale kwa uhodari wake wa kazi na msimamo kwenye jambo aliloliamini lilileta mafanikio makubwa katika soka la Tanzania.Kumbukumbu nyingine zinaonesha kuwa Dyamwale ndiye aliyebuni mpango wa watoto kuingia bure uwanjani miaka ya 1980 maarufu yosso.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

  0 0

  *Ahimiza elimu kwa mtoto wa kike, akemea mimba za utotoni  

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa mkoa wa Tabora wawapeleke watoto wao shule na waache kuwatumia kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku. 

  Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumapili, Agosti 13, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa idara za kilimo na ushirika na viongozi wa wilaya ya mkoa huo kwenye kikao alichokiitisha ili awape maagizo maalum. 

  “Ninasisitiza kuanzia sasa jamii iwapeleke watoto shule kuanzia elimu ya awali hadi sekondari na tuache kuwatumia watoto wadogo kama vibarua kwenye mashamba ya tumbaku. Wakuu wa wilaya simamieni eneo hili la kuondoa watoto kwenye ajira,” alisema.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo pia kusisitiza viongozi wa mkoa huo wasimamie elimu ya mtoto wa kike na kuhakikisha kuwa wanahitimu elimu ya sekondari.

  “Kuna tatizo la mimba kwa watoto wa shule. Eneo hili pia linahitaji usimamizi ili kuwalinda watoto wa kike wamalize elimu yao. Tuwalinde wanaposoma elimu ya msingi na sekondari, wakishafika vyuo vikuu watakuwa wamepevuka na kuweza kufanya maamuzi ya kujilinda,” alisema.

  Akihutubia kwenye mikutano ya hadhara wakati wa ziara yake ya siku nne moani Tabora, Waziri Mkuu aliwaasa vijana wa kiume wasithubutu kuwaoa mabinti wanaosoma, kwani kwa kufanya hivyo, wataishia kufungwa jela miaka 30.

  Pia aliwaasa wazazi wanaoamua kuwaoza mabinti zao ili wapate mahari, nao pia wana hatari kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 endapo watabainika kushirikiana na waoaji.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, AGOSTI 14, 2017.

  0 0

  Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akiondoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka jijini Dar es Salaam leo.
  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
  RAIA wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kujibu mashtaka ya kutishia kwa mtandao, kuishi nchini kwa muda wa miaka minne bila kibali na kutumia paspoti yenye visa ya kugushi.

  Mshtakiwa huyo ambaye kabla ya kuanza kusomewa mashitaka yake alitishia kuwapiga wandishi waliokuwa wakimpiga picha kwa kujaribu kurusha mateke na ngumi. Amesomewa mashtaka yake hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo amekana mashtaka yote na amerudishwa rumande hadi hapo upande wa mashtaka utakapothibitisha uhalali wa Visa yake na makazi yake ya kudumu.

  Akisoma hati ya Mashtaka wakili wa serikali, Nassoro Katuga amedai, Juni 22, mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa kwa kutumia mfumo wa kompyuta, alimuandia barua pepe Costa Gianna Koulos, yenye maneno ya vitisho kwa nia ya kumsababishia Koulos hisia za uoga.

  Pia imedaiwa kuwa, Julai 20 Mshtakiwa Tsampos, alimuandikia barua pepe nyingine Koulos yenye maneno hayo ya kadhaaa ya vitisho na kumpa masaa 48 kumtaka wakae na kumaliza tofauti zao kinyume na hapo atamfanyia kitu kibaya. Wakili Katuga ameendelea kudai kuwa mshtakiwa huyo mwenye pasi ya kusafiria namba 246184272,  raia wa Afrika Kusini, Julai 6, mwaka huu alikamatwa akiishi nchini bila ya kuwa na kibali maalumu.

  Aidha Agosti 7, mwaka huu katika kituo cha polisi cha Kati, Tsampos, alikutwa akiwa na pasi ya kusafiria yenye namba M00101612 ikiwa na Visa ya kughushi.

  Mshtakiwa amekanusha kutenda makosa hayo na amerudishwa rumande baada ya mahakama kuutaka upande wa utetezi kufanya uchunguzi na kuhakikisha kama kweli mshtakiwa anaishi mbezi kama ana visa yake.
  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 16, mwaka huu.
   Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akipelekwa mahakamani wakati amejifunika sura kwa nguo ya rangi ya bluu bahari leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.
   Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akipandisha katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya kusomewa mashtaka yanayomkabili katika mahakama hiyo.
  Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akisubiri kusomewa kesi yake inayomkabili katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
  Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61) akitishia kuwapiga waandishi waliokuwa wakimpiga picha.
  Raia wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61)  akiwafokea waandishi waliokuwa wakimpiga picha wakati akisubiri kusomewa mashtaka katika Mahaka ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaama  leo na Polisi wakimzuia kutimiza adhima yake. 
     Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi katikati na Ujumbe aliofuatana nao wakiwa katika mazungumzo na Viongozi was Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiongozwa na Rais Dkt.John Pombe magufuli leo alipokuwa katika ziara ya siku mbili mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Ikulu ya Jijini Dar es Salaam
  Mazungumzo ya Viongozi baina ya Ujumbe wa Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi (kulia) na Viongozi wa Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam,Rais Abdel Sisi na Ujumbe wake wakiwa nchini kwa ziara ya siku mbili, [Picha na Ikulu).14/08/2017.

older | 1 | .... | 1337 | 1338 | (Page 1339) | 1340 | 1341 | .... | 1897 | newer