Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

WANANCHI KATA YA MABILIONI WILAYANI SAME WATUMIA MAJI YENYE CHEMBECHEMBE ZA KINYESI CHA BINADAMU

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki akizungumza katika mkutano na wananchi katika kata ya Mabilioni wilayani Same.
Baadhi ya wananchi katika kata ya Mabilioni wilayani Same wakimsikiliza mkuu wa wilaya alipozunumza nao katika mkutano uliofanyika katika ofisi ya kata.
Afisa Elimu wa Kata ya Mabilioni wilayani Same,Richard Sekibojo akimkabidhi taarifa ya kata hiyo Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mabilioni waliohudhuria mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Same ,Rosemarry Sitaki akifuatilia maelezo ya kero mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi katika mkutano huo.kushoto kwake ni Diwani wa kata ya Mabilioni,

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini..

WANANCHI katika Kata ya Mabilioni wilayani Same wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kutumia maji ya mto Ruvu yaliyopimwa na kugundulika kuwa na chembe chembe za Kinyesi cha Binadamu.
Wakazi 5109 wanaounda kaya 1158 wamekuwa wakitumia maji ya Mto Ruvu unaopita katika vijiji vitatu viliyoko kaika kaa hiyo vya Chekereni,Mabilioni na Ruvu Mbuyuni  kwa ajili ya Kunywa,Kupikia ,Kufulia ,kuogea pamoja na Kilimo .
Afisa Elimu wa kata ya Mabilioni ,Richard Sekibojo aliyasema hayo wakati akitoa taarifa ya kata hiyo kwa Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemarry Sitaki alipofanya ziara katika kata hiyo na kufanya mkutano na wananchi wa kata ya Mabilioni.
“Mh Mkuu wa wilaya kata ya Mabilioni haina maji safi ya kunywa,kwani wananchi wanatumia maji ya Mto Ruvu kwa matumizi yote ya nyumbani pamoja na Kilimo  na maji hayo yalipimwa yakaonekana kuwa yana chembechembe za kinyesi cha binadamu zinazosababiha ugonjwa wa kipindupindu”alisema Sekibojo.
Akijibu malalamiko hayo Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki alisema uko mradi mkubwa sana wa maji wa serikali toka wizara ya Maji ,ambao unatoa maji Bwawa la Nyumba ya Mungu  kupitia wilaya ya Mwanga,Same hadi Korogwe mkoani Tanga .
“Kuhusu suala la maji ,nilikuwa naambiwa hapa kuwa kila visima vikichimbwa maji yanakuwa na chumvi nyingi sana na kwamba hayawezi kutumika kama maji ya kunywa na yale ya mtoni ndio kama tulivyosikia kuwa hayana sifa za kiafya na kutumika na binadamu.”alisema Sitaki.
Mradi huu mkubwa ndio utakuwa suluhu ya haya matatizo ,mradi tayari umeanza kujengwa kwenye chanzo ukiwa katika hatua za mwisho kukamilika na katika wilaya ya Same mkandarasi amekwisha patikana na ameanza kuchimba matenki .
Alisema kulingana na ukubwa wake,mradi huo utachukua hadi miaka mitatu kukamilika kwake na kwamba utagharimu zaidi ya Sh. Bilioni 142 ukifadhiliwa na serikali kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa na mashirika ya misaada ya kimataifa kutoka nchi za Falme za Kiarabu.
Kwa mujibu wa serikali mkoa wa Kilimanjaro,mradi huo utawaepusha idadi kubwa ya wananchi kwenye Wilaya hizo kuondokana na hatarini kuugua magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu na Kuhara kutokana na kunywa maji yasiyo safi na salama.
Hadi kukamilika kwake mradi huo utanufaisha zaidi ya wananchi 247,500 wa vijiji 28 vya Wilaya za Mwanga na Same kwa upande wa mkoa wa Kilimanjaro ambao kwa sasa upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 79 na mijini mkoa wa Kilimanjaro unakimbilia asilimia 98.
Mradi huo unajengwa kwa ufadhili wa Benki ya Kiarabu inayosimamia Maendeleo ya Nchi za Afrika (Badea), Mfuko wa Ofd unaojumuisha nchi zinazozalisha mafuta (Opec) na Mfuko wa Maendeleo wa Kimataifa wa Saud na Mfuko wa Misaada wa Kuwait.
Mwisho.

WANAFUNZI JITEGEMEE SEKONDARY WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA AJILI YA KUJIFUNZIA

$
0
0

 Gwaride la ukakamavu la wanafunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT Mgulani likipita mbele ya mgeni rasmi katika hafla iliyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam jana.
 Gwaride lilipita jukwaa kuu.
 Meza kuu ikitoa Saluti  wakati gwaride likipita mbele yao.

 Maofisa wa Jeshi wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Mmoja wa makamanda wa gwaride hilo, Ibrahim Mrisho akipongezwa na mgeni rasmi baada ya kupokea zawadi yake. Ibrahim alikuwa miongoni mwa makanda sita waliozawadiwa kwa kufanya vyema kwenye gwaride hilo, wengine ni Moses Peter, Azan Mohamed, Kidali Saidi na Clementina Joseph.
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Jitegeme, Robert Kessy akizungumza
 Kanali Emanuel Mwaigobeko ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Makongo inayomilikiwa na jeshi akimpongeza mgeni rasmi Mgombolwa kwa hotuba nzuri aliyoitoa kwa wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ukakamavu.
 Gadi ya wasichana ikiwa imetulia wakari wa hafla hiyo.
 Mgeni rasmi akipiga saluti wakati akipokea heshima wakati gwaride hilo lililopita mbele yake.
Brass Bendi ya JKT iliwajibika ipasavyo wakati wa kufungwa kwa mafunzo hayo ya ukakamavu.

Na Dotto Mwaibale

KANALI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Anchila Kagombola ambaye ni Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Kujenga Taifa Makao Makuu jijini Dar es Salaam, amewaasa wanafunzi kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujifunza na siyo kutumiana jumbe zisizofaa zinazoweza kuhatarisha maisha yao.
          
Kagombola aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya kufunga mafunzo ya ukakamavu ya Kidato cha Tano kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jitegemee JKT High School 2017, alitoa rai hiyo jana.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kagombola aliwapongeza wanafunzi wa Jitegemee kwa kujiunga na shule hiyo inayotoa elimu bora na kusisitiza ukakamavu, maadili, uzalendo,umoja na nidhamu kwa jumla.

Kanali Kagombola, amewaasa wanafunzi hao watumie mitandao ya kijamii kwa kujifunza na siyo kutumiana jumbe hatarishi kwa ajili ya usalama wao na usalama wa taifa.

“Aidha, niwahusie wanafunzi wote wa shule hii kuwa mkwepe vishawishi vyote vya ujana, msome kwa bidii, muache kutazama nafsi zenu hasa watoto wangu wa kike na kupata faraja, kwani zaweza kukatisha ndoto zenu, hivyo muwakatae wote wanaowashawishi kuingia kwenye mienendo hatarishi, mfano kufanya ngono, utumiaji wa madawa na vitendo vya uhalifu.

Aidha, mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Youtube na mingine itumike kwa ajili ya kujifunza, siyo kutumiana jumbe hatarishi kwenu na kwa usalama wa nchi. Tafadhali sana, mmenisikia?”

Kagombola ametoa pongezi kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee, Luteni Kanali Robert Kessy kwa kuendesha mafunzo hayo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza, kidato cha tano na kwa wahamiaji.

Alibainisha kuwa katika mtazamo wa nje mafunzo ya ukakamavu huonekana hayana umuhimu kwa walengwa, lakini yanasaidia vijana kuishi kwa nidhamu wawapo shuleni na uraiani na bila tabu yoyote.

“Faida  za mafunzo haya ya ukakamavu ni pamoja kudumisha nidhamu, utimamu wa mwili, uwezo wa kufikiri haraka, uvumilivu, uadilifu, kujiamini na suala zima la kutenda na kuamua kwa wakati ili kupata matokeo mazuri katika masomo,” alisema Kagombola.
Hata hivyo, ameomba mpango wa kutoa mafunzo ya ukakamavu mashuleni uliokuwepo miaka ya nyuma urejeshwe ili kujenga ukakamavu , uzalendo na wanafunzi kuwa na maadili.

Pia aliwasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha mtoto wa kike anapatiwa  elimu bora kwa kuwa ndio walezi wa jamii.

Akizungumzia mafunzo hayo,Luteni Kanali Kessy alisema yalianza 1985 na kwamba wakati huo yalikuwa yakichukua wiki mbili sasa wiki tatu na yanafanyika baada ya muda wa masomo.

‘Mafunzo haya ya ukakamavu yalianzishwa ili kuwafanya wanafunzi wawe wazalendo, wakakamavu, wenye maadili na nidhamu.

Gwaride hilo la wanafunzi wa kidato cha tano liliongozwa na Gwaride Kamanda, ambaye ni mwanafunzi  aitwaye Zulfa Ally likihusisha wanafunzi 256 na gadi nane.

The Commonwealth Secretary General Rt Hon Barones Patricia Scotland QC meets Zanzibar President, visits some of the Isles attractions

$
0
0
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC (left) accompanied by Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro and Ambassador Celestine MushyDirector of  Multilateral Cooperation in the Ministry of Foreign Affairs and Regional Affairs head to the plane ready to take off  for their one day trip of  Zanzibar
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC greets the crew before boarding
Top Zanzibar government officials receive The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia atScotland QC at the Karume International Airport in the isles
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC signs the visitor's book upon arrival at the Abeid Amani Karume International Airport. On her right is Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma and left is Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro

The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC upon arrival at the Abeid Amani Karume International Airport. On her left  is Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma and Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC arrives at the Zanzibar State House accompanies by Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein receives The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC at the State House
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein and The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC fields questions from journalists at the State House
 The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC poses for a souvernier photo with Isles based ITV and Radio One journalist Farouq Karim  at the State House
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC is taken to a tour of Stone Town with The House of Wonders in the background
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage pose for a group photo
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage pose for another group photo
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC and her entourage take a guided walking tour through spice plantations
During the Spice tour the Baroness  and her entourage saw how the spices, herbs and fruits are cultivated, with the  tour guide describing in detail all about them as well as tropical fruits such as cloves, lemongrass, nutmeg, cinnamon, turmeric, vanilla, coconuts, papaya, chilli, black pepper, jackfruit, cardamom, cassava and oranges.
The  tour guide describes in  detail  how the spices, herbs and fruits  can be used
Visibly happy with the tour, our visitor is
More spices and herbs are shows
Even lipstick from plants was applied 
Some of the many tourists taking the spice tour cool off the day with coconut juice under clove trees
The baroness joins in
Neatly packed spices and herbs are on display
The visitors take their leave after a satisfying spice tour
Off to the State House where a sumptious luncheon in her hnour awaits
After  the luncheon and on behalf of the entourage Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro thanks their host President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein 
Thank you, Your Excellency, for the sumptious luncheon....
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein  leads the Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC outside for souvenir photos.
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein take the first photo with the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC at the State House
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein and the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC are joined by the Zanzibar Chief Secretary Dr.  Abdulhamid Yahya Mzee (left)  Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma, Tanzania's High Commissioner to the UK Dr. Asha-Rose Migiro and Minister for Finance and Planning Dr. Khalid Salum Mohamed
The VVIPs are joined by the rest of the entourage
The President of Zanzibar and Chairman of the Revolutionary Council Dr. Ali Mohamed Shein bids farewell to the  Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC
At the airport The Vice President of the United  Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan meets the Baroness
The Vice President of the United  Republic of Tanzania Hon. Samia Suluhu Hassan bids farewell to  the Baroness
Its time for the Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC to depart
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC is bid farewell 
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC  bids farewell to Zanzibar's Minister for Education and Vocational Training Hon. Riziki Pembe Juma

The Baroness waves goodbye...
....and blows kisses to her hosts
Salutes welcome them back to Dar es salaam
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC greets the police officers
"...What a tour"
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC caps off the day with a courtesy call on  Prof Palamagamba Kabudi,  Minister for Justice and Constitutional Affairs at his office in Dar es salaam
The Baroness greetsb Prof Sifuni Mchome, Permanent Secretary in the Ministry of Justice and Constitutional Affairs
The Commonwealth Secretary General Rt Hon Patricia Scotland QC  holds talks with   Prof Palamagamba Kabudi,  Minister for Justice and Constitutional Affairs at his office in Dar es salaam.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMTEUA BERNARD HEZRON KONGA KUWA MKURUGENZI MKUU WA NHIF

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF,Bw.Bernard Hezron Konga



Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Muliro J. Muliro awaongoza askari katika mazoezi

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Muliro J. Muliro (watatu kushoto) akiwaongoza askari na maofisa wa vyeo mbalimbali leo jijini Dar es salaam, katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano na ujasiri hususan katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi na kukabiliana na matukio ya kihalifu. Picha na Jeshi al Polisi.
Askari na maofisa wa vyeo mbalimbali wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, leo jijini Dar es salaam, wakiwa katika mazoezi baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano na ujasiri hususan katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi na kukabiliana na matukio ya kihalifu, matembezi hayo yaliongozwa na kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Muliro J. Muliro. Picha na Jeshi al Polisi.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakifanya mazoezi leo jijini Dar es salaam, baada ya kumaliza matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano na ujasiri hususan katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi na kukabiliana na matukio ya kihalifu, matembezi hayo yaliongozwa na kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Muliro J. Muliro. Picha na Jeshi al Polisi.

Baadhi ya askari wa vyeo mbalimbali kutoka mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, leo jijini Dar es salaa, wakiwa katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano na ujasiri hususan katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi na kukabiliana na matukio ya kihalifu, matembezi hayo yaliongozwa na kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Muliro J. Muliro. Picha na Jeshi al Polisi.
Baadhi ya askari wa vyeo mbalimbali kutoka mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, leo jijini Dar es salaa, wakiwa katika matembezi ya pamoja ya kuimarisha afya na kujenga ushirikiano na ujasiri hususan katika kutekeleza majukumu ya kazi za Polisi na kukabiliana na matukio ya kihalifu, matembezi hayo yaliongozwa na kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Muliro J. Muliro. Picha na Jeshi al Polisi.

RIDHIWANI ATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU ZA WILAYA YA BAGAMOYO

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na mchezaji anayeshiriki katika mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akitoa vifaa kwa washiriki wa mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, akitoa vifaa kwa washiriki wa mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa tatu kutoka kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo wa pili toka kulia Majid Mwanga wakiangalia mashindano ya Kombe la Mazingira,yaliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akionyesha moja ya jezi zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la chalinze Ridhiwani Kikwete.


Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo hilo zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Ridhiwani, amesema kuwa atawapatia washindi wa pili wa michuano hiyo pikipiki ya miguu miwili na jezi kwa timu zote tatu za juu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga,ambaye pia ndio muaandaji wa mashindano hayo ametoa zawadi ya pikipiki ya Toyo ya miguu mitatu kwa mshindi wa kwanza ili itumike kwa shughuli za kuwaingizia kipato kwa vijana.

DIWANI WA KATA SAMBASHA ( CCM) AACHIWA KWA DHAMANA DHIDI YA KESI INAYOMKABILI

$
0
0
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akiwa nje ya mahakama mara baada ya kuachiwa kwa dhamana kutokana na kesi inayomkabili.Picha na Vero Ignatus Blog.
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa UVCCM,na Diwani wa Kata ya Sambasha mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya (aliyevaa suti nyeusi)akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama.Picha na Vero Ignatus Blog.
Akizungumza na mwenyekiti wa CCM katika kata ya Sambasha Lesion Letionoki Njoki.Picha na Vero Ignatus Blog.

Akisalimiana na wananchi wa kata ya Sambasha mara baada ya kuachiwa kwa dhamana.Picha na Vero Ignatus Blog.


Na Vero Ignatus.Arusha

Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .

Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).

Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serekali Penina Joakim amesema kuwa Mnamo May 18 katika hotel ya Skyway iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .

Wakili Penina alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .

Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Nestory Barro alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na mahakama hiyo.

Hata hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukithi vigezo vilivyowekwa na mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye sifa ambapo kwanza awe mtumishi wa serikali pili awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.

Hata hivyo wakili Edina Mndeme anayemtetea Lengai Ole Sabaya amesema kuwa mteja wake amekuwa akifikishwa mahakamani na amesomewa mashitaka yaleyale na hii ni mara ya nne .

Kesi imeaihishwa na hakimu mkazi hadi itakapotajwa tena 30/8/2017 ambapo uchunguzi unatarajiwa kukamilika na kesi hiyo kuanza kusikilizwa.

SERIKALI YASITISHA UTOAJI WA MAENEO MAPYA YA UTAWALA

$
0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imesitisha zoezi la kutoa maeneo mapya ya utawala hadi itakapotangazwa vinginevyo. 

"Kwa sasa tumesitisha kutoa maeneo mapya ya utawala ili tuimarishe kwanza yale ya awali. Tunaimarisha kwanza miundombinu ya majengo ya ofisi,  nyumba za watumishi kwenye wilaya na Halmashauri mpya, zikitengamaa tutafanya maamuzi mapya, " alisema. 

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Ijumaa,  Agosti 11, 2017) katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Ulyankulu na Kaliua, wilayani Kaliua mkoani Tabora. 

Alikuwa akijibu maombi ya wabunge wa majimbo ya Ulyankulu na Kaliua ambao walisema kuna haja ya kuigawa wilaya ya Kaliua ili kusogeza huduma kwa wananchi waishio kwenye kata zilizo mbali na tarafa. 

Akizungumzia kuhusu migogoro baina ya wanavijiji na maeneo ya hifadhi, Waziri Mkuu alisema Serikali bado inafanya uhakiki wa mipaka katika maeneo ya hifadhi na ikikamilisha zoezi hilo itatoa taarifa. 

Ili kuharakisha zoezi hilo,  Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaoishi pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na maeneo ya hifadhi, wasifanye upanuzi wowote hadi zoezi la kuhakiki mipaka ya hifadhi litakapokamilika.

"Tumeamua kuweka beacons katika maeneo yote ya hifadhi ili kubaini mipaka imepita wapi.  Wananchi mkiwaona watu wa hifadhi wanapita huko msigombane nao. Ni hatua ya awali ya kubaini maeneo ya mipaka. "

"Niwasihi wanavijiji wote, vijiji vilivyomo kwenye hifadhi visiendelee kupanua maeneo yake. Mbaki hivyo hivyo hadi Serikali itakapoamua vinginevyo, " alisema. 

Alisema zoezi la uhakiki wa mipaka ya hifadhi likikamilika na taarifa kutolewa, Serikali itatoa uamuzi juu ya vijiji vilivyobainika kuwa ndani ya maeneo ya Hifadhi.

Akiwa Kaliua, Waziri Mkuu alielezwa na Mbunge wa jimbo hilo,  Mheshimiwa Magdalena Sakaya kuwa wananchi wanashindwa kujenga makazi ya kudumu katika maeneo waliyopo kwa sababu wanatishiwa kwamba wapo hifadhini. 

Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya mapitio na ikilazimu itabidi ifanye marekebisho ya Sheria inayohusu Misitu ya Hifadhi pamoja na Sheria inayohusu masula ya Wakimbizi. 

(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAMOSI, AGOSTI 12, 2017.

GRACA MACHEL AFUNGA MKUTANO WA MAENDELEO KWA WANAWAKE ,KIUCHUMI NA JAMII (WOMEN ADVANCE IN AFRICA)

$
0
0
Mjane wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Mama Graca Machel akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
Mjane wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Mama Graca Machel akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
Mjane wa Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Mama Graca Machel akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Zamani Nchini ,Jaji Joseph Sinde Warioba kabla ya kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
Baadhi ya Wanawake kutoka nchi Mbalimbali Walioshiriki Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika
Waziri Mkuu Mstaafu ,Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza jambo na Mwanaharakati wa siku nyingi Getrude Mongela wakati wa Kufunga Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika 
Baadhi ya Wanawake kutoka nchi Mbalimbali Walioshiriki Mkutano wa Maendeleo ya Wanawake kwenye Uchumi na Jamii(Women Advance in Africa ) Uliofanyika Jijini Dar es Salaam anakwa takribani siku tatu na kuwakutanisha Wanawake kutoka kila pembe ya Afrika

MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.

Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.

Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani michezo hudumisha umoja na kuleta mshikamano katika jamii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi
Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa shrehe ya Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kukuna nazi yawa kizutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kusokota kamba 
Vijana kutoka Kusini mwa Kizimkazi wakivuta kamba wakishindana na vijana wa kaskazini wakati wa sherehe za Siku ya Wakizimkazi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bw. Sudi Simba ambaye alifika Kizimkazi kutambulisha huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vipeperushi vyenye taarifa ya huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.
Wakazi wa Kizimkazi wakiangalia ngalawa 15 zikichuznz vikali ikiwa sehemu ya sherehe ya siku ya Wakizimkazi
Wananchi wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pongezi kijana aliyeshinda kwenye mashindano ya Ngalawa Bw. Ali Khamisi Mgeni akiwa na chombo chenye jina la Sea Never Dry.

WAKULIMA WA TUMBAKU MKOANI TABORA WATAKIWA KUJIPANGA ILI WAACHE KUENDELEA NA UKOPAJI WA MBOLEA.

$
0
0

Na Tiganya Vincent-Tabora

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim ametoa wito kwa Wakulima wa tumbaku mkoani Tabora kuanza kujipanga ili waanze kilimo cha zao hilo kwa kunununua mbolea kwa kutumia fedha zao badala ya kuendelea kutegemea mbolea za mkopo kupitia vyama vya msingi.

Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana katika maeneo mbalimbali wilayani Uyui wakati akiwahutubia wananchi.

Alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia wakulima hilo kuwa na huru hata wakati wa kupanga bei ya zao wanapokwenda kuwauzia wanunuzi wa tumbaku.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa tabia ya kuendelea kusubiri mbolea ya mkopo inawafanya wakulima wengi washindwe kusonga mbele kwa sababu pesa nyingi inakwenda katika kulipia deni la mbolea.

“Ndugu zangu wakulima watumbaku ni vema kuanzia sasa mkaanza kujipanga kwa msimu ujao wa kilimo kwa kununua mbolea kidogo kidogo ili ikiwezekana ulime kwa kutumia mbolea ulionunua mwenyewe……..hali hii itakufanya uwe uhuru hata wa kuamua bei unayotaka” alisisitiza Mhe. Majaliwa.

Alisema kuwa ni wakulima wakaanza kwa kununua kidogo dogo mbolea ya tumbaku kupitia mapato yanayotokana na mauzo ya tumbaku yao kama hatua ya kuelekea katika kujikomboa na kuondokana na utegemezi wa mbolea za mikopo ambayo zimewaingiza katika matatizo mbalimbali ikiwemo kuwa siku nyuma kimaendeleo.

Aidha Waziri Mkuu amepiga marufuku Kampuni zinazonunua tumbaku hapa nchini kununua zao hilo kutoka kwa Mkulima kwa njia ya fedha ya Kimarekani (Dola) na kusema kuwa vitendo hivyo ndio vinasababisha unyonyaji wakulima.

Alisema tumbaku yote kuanzia sasa itakuwa ikinunuliwa kwa fedha ya kitanzania na sio vinginevyo. Mhe. Majaliwa alisisitiza kuwa wakulima wengi hajui dola jambo ambalo limefanya viongozi wengi wakiwemo wa vyama vya msingi kumibia mkulima.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alisema kuwa mtu akayekamatwa ananunua tumbaku ya mkulima kwa njia ya vishada Serikali haitamuachia na kama atakuwa ana chombo cha usafiri kitashikiliwa na Polisi ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kuwavizia wakulima walime kisha wao waende kurubuni na kununua tumbaku yao kwa nia ya ulanguzi.

Alisisitiza kuwa tumbaku yote itauzwa kupitia Vyama vya Msingi na sio vinginevyo na mtu yoyote atakayekutwa akiuza tumbaku nje ya utaratibu wa Serikali atachukuliwa hatua kali.

DOKTA MPANGO AWASIMAMISHAKAZI WATUMISHI 4 WA TRA MPAKANI TUNDUMA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Songwe/Mbeya

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewasimamisha kazi watumishi wanne wa Idara ya Forodha, katika Mpaka wa Tanzania na Zambia, Mjini Tunduma, ili kupisha uchunguzi wa kudaiwa kuhusika na upotevu wa lakiri 10 zinazotumika kufunga kwenye shehena ya mizigo inayopita mpakati hapo kutoka nje ya nchi.

Mpango amewataja watumishi hao kuwa ni pamoja na Harrison Mwampashi, John Makorere, Stephene Josia na Frank Kessy na kuviagiza vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama mpakani hapo viwahoji huku wakiwa wamesimamishwa kazi.

Watumishi hao wanadaiwa kuiba lakiri hizo kumi kutoka ofisi za TRA-Tunduma wanakofanyiakazi, ambapo 4 kati ya hizo lakiri zilikutwa zimefungwa kwenye mizigo ya malori yanayoshikiliwa katika mpaka huo baada ya uchunguzi kufanyika huku malori mengine 5 yakizuiwa baada ya kuonekana lakiri zao zimechezewa.

Taarifa zinasema kuwa baada ya uchunguzi, mawakala ama wamiliki wa malori hayo wamedai walipewa lakiri hizo na watuhumiwa na kwamba uchunguzi zaidi umebaini kuwa kiwango cha mizigo kilichomo kwenye makontena yaliyobeba mizigo ya magogo na kufungwa lakiri hizo za wizi hakilingani na idadi ya mizigo iliyoko kwenye nyaraka jambo linaloashiria kuwa wanazitumia lakiri hizo kudanganya idadi na uzito wa mizigo yao ili kukwepa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali.

“Hakuna kitu muhimu kama uadilifu kwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato na hatutasita wala hatutamwonei aibu mtu yeyote, tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria ili kulinda fedha za umma” alionya Dkt. Mpango

Alisema kuwa Serikali imebaini baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato na Idara za Forodha mipakani wanashirikiana na wafanyabishara wasio waaminifu kuingilia mifumo ya kukusanyia mapato, kitendo ambacho kinaweza kurudisha nyuma juhudi za serikali kuwahudumia wananchi wake.

Dkt. Mpango amewaonya wafanyakazi wote wa forodha na Mamlaka ya Mapato nchini, kuwa wazalendo na waaminifu katika kukusanya mapato ya Serikali na kuacha kujihusisha na vitendo vinavyokwaza ufanisi wa Mamlaka hayo.

BIASHARA YA KUBADILISHA FEDHA MPAKANI

Wakati huo huo, Dkt. Mpango, ametoa muda wa siku thelathini, kwa wanaobadilisha fedha za kigeni kiholela mipakani, waache mara moja, badala yake waheshimu sheria za Nchi, na kuunda vikundi vinavyoweza kuanzisha maduka ya kubadilisha fedha hizo.

Alitoa kauli hiyo Mjini Tunduma, wakati akizungumza na wabadilisha fedha mpakani humo, kwamba serikali itawaheshimu tu wale watakaojiundia vikundi na kuwa na sehemu wanakoweza kubadilisha fedha kwa kufuata utaratibu na wala si vinginevyo.

ATEMBELEA UJENZI WA KITUO KIPYA CHA FORODHA NA IDARA YA FORODHA TUNDUMA

Akiwa Mjini Tunduma, Dkt. Mpango, pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha pamoja cha Forodha cha Mpaka kati ya Tanzania na Zambia Mjini Tunduma.

Pia ametembela Ofisi ya Idara ya Forodha mpakani hapa, na kupata taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017, ambapo maafisa wamekusanya mapato zaidi ya Bilioni 75 na kuvuka lengo la mapato waliyokuwa wameyatarajia.

Meneja wa Idara ya Forodha mikoa ya Mbeya na Songwe, Bw. Jimmy Nsindo amesema kuwa pamoja na mafanikio hayo, Mpaka huo wa Tanzania na Zambia, ni mpaka unaoweza kuingilika kirahisi, matokeo yake udhibiti wa mapato unaingia dosari, huku baadhi ya watanzania wanafanya biashara zinazodaiwa kuliingizia hasara taifa, zikiwemo za kubadili fedha za kigeni kwa mfumo usio rasmi.

ASHITUKIZA VITUO VYA MAFUTA

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ametoa muda wa siku ishirini kwa wamiliki wote wa vituo vya mafuta ambao wameomba kupatiwa mashine za Kielectroniki kwaajili ya kuunganishwa na mfumo wa kodi na utoaji wa risti wawe wamepata mashine hizo vinginevyo watafungiwa vituo vyao.

Aidha, amesema ifikapo Jumatano Juma lijalo wamiliki wote wa maduka mkoani Mbeya, waanze kutumia mashine za Kielekroniki za kutolea risiti (EFDs) na kuonya kwamba Serikali haitasita kuyafunga maduka yao wasipotekeleza maagizo hayo.

Waziri wa Fedha na Mipango ametumia ziara hii kutoa shukrani kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya namna walivyoitikia kulipa kodi za nyumba.

MPINA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA , WAZUNGUMZIA MASUALA YA HIFADHI YA MAZINGIRA NA SULALA LA MABADILIKO YA TABIANCHI YAPEWA KIPAUMBELE

$
0
0
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Nje ya Ofisi ya Makamu wa Rais Baada ya kumaliza mkutano ulohusu suala zima la usimamizi na Utunzaji wa Mazingira.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akiongea jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, baada ya mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaan Leo.
Mhe. Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza AshaRose Migiro, akizungumza baada ya kikao na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mpina na wataalaam kuhusu masuala ya Mazingira, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na wajumbe walioshiriki mkutano wa masuala ya hifadhi ya mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina 

Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. AshaRose Migiro baada ya kumaliza mazungumzo yaliyoohusu masuala ya mazingira.

………………………………………………………………..

Katibu wa Jumuiya ya madola Mhe. Patricia Scotland amefanya mazungumzo na Naibu Waziri Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga kuhusu suala zima la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira huku eneo la mabadiliko ya Tabianchi likipewa kipaumbele.

Katika mazungumzo hayo Bi. Scotland alisema kuwa kuna kila sababu ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuelewa zaidi suala zima la mabadiliko ya tabianchi akieleza kuwa wanasayansi wanasema ifikapo mwaka 2050 dunia inaweza kabisa kuepukana na suala la athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi endapo itawezekana kulifanyia kazi kwa pamoja.

Kwa upande wake Naibu Waziri Mpina alieleza kuwa Tanzania imeathiriwa na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali na jitihada zimefanyika katika kuwezesha jamii kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi (2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.

Aidha, Mhe. Mpina alipokumbushwa kuhusu jitihada zake zinazoonekana wazi katika suala zima la utunzaji wa mazingira hususan katika oparasheni zake za viwandani, na Balozi Migiro; Mpina alisema kuwa viwanda vingi nchini alivyovipitia havina mifumo ya kisasa ya kutibu majitaka akitolea mfano wa jiji la Dar es Salaam Mpina lisema mfumo wa majitaka katika jiji hilo kwa sasa ni asilimia 13% tuu ndiyo yenye mfumo mzuri na kuongeza kuwa asilimia iliyobakia haijakaa vizuri, jambo ambalo si salama kwa viumbe hai na mazingira.

Awali, akiongea katika mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Uingerea Mhe. Asharose Migiro akitolea mfano wa athari za mabadiliko ya tabia nchi katika maeneo ya ufukwe ya ocean road ambayo imelika, alisema wakati umefika sasa kwa Tanzania kuonyesha ushirikiano katika suala hili na wananchi kuelewa shughuli za kibinadamu zinazochangia kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Amefanya mazungumzo hayo leo na Naibu waziri Mpina na Team ya wataalam baada ya kutembelea kisiwa cha Zanzibar.

Rais wa Zanzibar Dkt. Shein ziarani Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja mradi  katika Kanda ya Afrika Mashariki katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Nd,Tushar Mehta  alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Meneja wa Mawasiliano katika Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Fatma Salum Ali (kulia) wa  Kampuni ya ETG inayoendesha Kiwanda hicho wakati alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji pia Kaimu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Mhe.Ali Abeid Karume wakati alipowasili katika ukaguzi wa maendeleo ya Kiwanda cha Sukari cha Mahonda na kupata maelezo mbali mbali kutoka kwa Wasimamizi wa Kiwanda hicho Kampuni ya ETG  alipofanya ziara katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja leo

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa  Meneja mradi  katika Kanda ya Afrika Mashariki katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Ndg. Tushar Mehta  (wa pili kushoto) alipofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mkuu wa mradi   katika Kampuni ya ETG inayoendesha  Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Bw. Mahesh  Patel (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya Kiwanda hicho leo katika Wilaya ya Kaskazini "B" Mkoa wa Kaskazini Unguja,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Vuai Mwinyi Mohamed.
Picha na IKULU

MBUNGE WA UBUNGO SAED KUBENEA AKAGUA BARABARA YA MAKOKA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI MMOJAMMOJA

$
0
0
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na Mmoja wa Madereva wa Daladala ambao hufanya safari zao kituo cha River Side kwenda Makoka mara baada ya kuchonga barabara hiyo kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo .
  Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, akizungumza na Dereva wa Bodaboda katika barabara ya Riverside Makoka mara baada ya kukagua barabara hiyo iliyochongwa kwa fedha za Mfuko wa jimbo
 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akizungumza na  Wakazi wa eneo la Ubungo Makoka mara alipo fika katika kituo cha Daladala eneo la Riverside kupata maoni yao nini kifanyike kuboresha barabara hiyo ili iweze kupitika muda wote 
Mjumbe wa shina Makoka Phinias  akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea  juu ya barabara ya Makoka River side   mara baada ya kuchonga barabara hiyo kwa kutumia fedha za mfuko wa jimbo 

RAIS DKT MAGUFULI ASHIRIKI MISA YA JUMAPILI KANISA LA MTAKATIFU JOSEPH JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika  Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017.  Picha na IKULU
IMGS0060
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakitakiana amani na watawa wakati wa Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
IMGS0071
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakijumuika na waumini wengine kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
IMGS0074
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
IMGS0177
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
IMGS0181
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017
IMGS0187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakipata picha ya kumbukumbu na  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam  Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Padre Vicent na baadhi ya wanafunzi shule ya Sekondari ya St. Joseph baada ya kushiriki Ibada ya Misa takatifu, Dominica ya 19 ya mwaka A wa Kanisa, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam leo Agosti 13, 2017

TFF kuanza kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi ya fedha kwenye magazeti

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na wajumbe wa TFF (hawapo pichani) baada ya kutangazwa na kuapishwa kwa viongozi wapya wa TFF Mkoani Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia akitoa neno la shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF kumwezesha kushika nafasi ya urais, wakati wa Mkutano Mkuu wa TFF uliofanyika katika Ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta na Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Michael Wambura (kushoto) baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa TFF uliofanyika jana katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma.

 Na Genofeva Matemu - WHUSM

Uongozi mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) umetakiwa kufikia Januari mwakani kuwajibika kama mashirika mengine ya mpira wa miguu duniani yanavyowajibika kuchapisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye magazeti ili wananchi wapate fursa ya kufahamu namna fedha zinavyopatikana na jinsi zinavyotumika katika kuboresha na kuendeleza usimamizi bora wa soka nchini.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na katika ukumbi wa St. Gasper Mkoani Dodoma Aidha Mhe. Mwakyembe amewapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne kwa kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku huku akiwapongeza washiriki wote waliothubutu kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi Mkuu wa TFF wa mwaka huu.

Kwa upande wake Rais mpya wa TFF Bw. Wallace Karia amewaahidi wapiga kuwa wake kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu kwani nafasi aliyopewa na wajumbe hao kwa kumuamini ni deni ambalo atalilipa kwa kuleta mafanikio makubwa katika mchezo wa soka.

Bw. Karia amesema kuwa furaha waliyonayo viongozi wote waliochaguliwa kuiongoza TFF kwa muda wa miaka minne iende kuwa furaha ya kazi kwa kufanya yale watanzania wanatarajia kutoka kwao.

DED MNASI: AKAGUA MRADI WA UMWAGILIAJI KATIKA HALMASHAURI YA ILEJE MKOANI SONGWE

$
0
0
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Haji Mnasi akiwa anakagua mradi wa mfereji mkubwa wa umwagiliaji kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo kwa wananchi wa Ileje akiwa Sambamba na viongozi na wananchi wakati wa ukaguzi.
Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akisikiliza maelezo ya mradi huo kutoka kwa wataalamu ambao pia ni wafanyakazi wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje.


Na fredy Mgunda, Ileje

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe Leo amefanya ziara ya kushitukiza kukagua miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa kutokana na ila ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2015 kwenda 2020 chini ya uongozi wa chama cha mapinduzi CCM taifa.

Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ukaguzi  wa maendeleo ya ujenzi mfereji mkuu wa umwagiliaji wenye urefu wa km 6  wa sasenga maeneo ya kata ya mbebe lengo ni kuona mradi huu unakamilika kwa wakati na unawanugaisha wananchi wa vijiji vyote vya mradi.

"Mradi huu ni mkubwa sana naomba wananchi wautumie vizuri na kuutunza kwa kuwa unamanufaa ya muda mrefu kutokana na ujenzi wake kuwa mkubwa na wagharama kubwa na unaubora unaokidhi vigezo vyote kuwa mradi wa kutumu"alisema Mnasi

Mnasi aliwataka wananchi kuutunza na kuulinda mreji huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia katika Kilimo cha mazao mbalimbali yanayolimwa katika ukanda huo wa halmashauri ya wilaya ya Ileje.

"Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje wametegemea Kilimo katika kuendesha maisha yao hivyo uwepo wa mradi huu utakuwa na tija ya kimaendeleo kwa wakulima na wafanyabiasha mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika halmashauri hii" alisema Mnasi

Aidha Mnasi aliwaomba wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Mkoani Songwe kuitumia vizuri fursa za uwepo wa mfereji mkubwa kwenye eneo hilo ambao unaweza kutumiwa kwa kuzalisha vitu vingi ambavyo vitakuwa na tija kwa maendeleo yako.

"Wananchi wangu itumieni vizuri fulsa hii kuleta maendeleo katika halmashauri hii sihitaji kusikia malumbano yoyote juu ya matumizi ya mradi huu wa umwagiliaji ambao unatija sana kwa maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla"alisema Mnasi

Mnasi alitoa onyo kwa wafugaji wenye mifugo yao husani ngombe ambao wamekuwaa wakizagaa katika eneo hilo ,alimwagiza mtendaji wa kata mwashitete kusimamia agizo hilo na kuongeza kinyume cha hapa mifugo hiyo itatozwa faini kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ileje Joseph Mkude aliwataka wananchi kuulinda na kuutunza mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa serikali imefanya kazi kuwa kuwaletea maendeleo ya Kilimo kwa wakulima ili kupunguza idadi ya wananchi tegemezi.

"Unajua huu mfereji utaongeza ajira kutokana na Kilimo kinacholimwa katika wilaya hii hivyo ni lazima wananchi kuutunza na kuuthamini mradi huu" alisema mkude

Lakini mkude alimtaka Mkurugenzi na kamati zake kuhakikisha mradi huo unadumu kwa muda mrefu kwani serikali imetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini ili nao waweze kuinuka hapo mlipo kwenda hatua nyingine ya kimaendeleo.

"Mkurugenzi hakikisha kuwa huu mradi unasimamiwa vizuri na kuutunza ili uweze kudumu kwa muda mrefu kama lengo la serikali litimizwe kama ilivyopangwa"alisema mkude

Nao baadhi ya wananchi ambao niwakulima wameishukuru serikali kwa mradi huo wa umwagiliaji kwa kuwa Kilimo ndio maisha yao hivyo wanatarajia kunufaika na kukuza uchumi katika maeneo hayo.

DC IKUNGI AHIMIZA UFANYAJI MAZOEZI ILI KUEPUKA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA NA KUUNGA MKONO KAULI MBIU YA HAPA KAZI TU

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akifanya moja ya mazoezi ya viungo pamoja na wananchi.
mtatu (4)
Sifa ya kiongozi ni kumsikiliza mwananchi yoyote,wakati wote,mahali popote ikiwa ni pamoja na kutatua kero na haja za wananchi ambayo ndio dhamira ya serikali ya awamu ya tano,mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu analitimiza hilo pichani akimsikiliza mmoja wa wananchi waliojumuika nae kufanya mazoezi.
mtatu (5)
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akiwaongoza wakazi wa kata ya Makiungu na Mungaa katika jogging ikiwa ni ufanyaji wa mazoezi ya viungo.
mtatu (6)
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akifanya moja ya mazoezi ya viungo pamoja na wananchi.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu ameshiriki kufanya mazoezi ya viungo na  wananchi  wa Kata ya Makiungu na Mungaa zilizopo wilayani humo huku akitilia mkazo ufanyaji wa mazoezi hayo sambamba na uzingatiaji wa  ulaji wa vyakula visivyo na mafuta mengi ili kuepukana na maradhi yasiyoambukiza.

Hatua hiyo ni kuunga mkono maelekezo ya makamu wa Rais Samiah Suluhu Hassan ya kufanya mazoezi kila jumamosi ya pili ya kila mwezi.
Akizungumza katika mazoezi hayo Mtaturu amesema magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa yakichukua maisha ya watu wengi duniani hivyo ni wakati wa kuweka jitihada kupambana  nayo.

“Mbali na kufanya mazoezi haya kila mwezi lakini ni vizuri pia kuweka utaratibu wa kutembea walau mara moja kwa siku iwe asubuhi au jioni lakini pia kuweka msisitizo kwenye ulaji wa matunda na mboga za majani kwa wingi huku tukiepuka matumizi ya mafuta mengi kwenye vyakula vyetu,”alisema Mtaturu.

Alisema rais John Magufuli anasisitiza kauli mbiu yake ya hapa kazi tu na ili kauli mbiu hiyo iweze kufanikiwa ni lazima tuwe na afya iliyo imara kwa kujenga tabia ya kupima mara kwa mara na kufanya mazoezi.

“Ili kuweka mazoea ya ufanyaji wa mazoezi tunapaswa tuanze kuwazoesha vijana wadogo na ili kutilia mkazo hili hivi karibuni tutaanzisha ligi ya mpira wa miguu itakayoitwa Elimu Cup ambayo  itakashirikisha kata zote 28 wilayani hapa,”aliongeza mkuu huyo.

Aliweka bayana lengo la kuanzisha ligi hiyo kuwa ni  kuhamasisha uchangiaji wa mfuko wa elimu na hapo hapo kubaini vipaji vya vijana.
Kauli mbiu ya kuhamasisha mazoezi hayo ni mazoezi ni  afya tokomeza magonjwa  yasiyoambukizwa.

RIDHIWAN KIKWETE-AHIMIZA WANANCHI WAJITOLEE KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete ,akizungumza wakati wa uzinduzi wa madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete kushoto akiagana na balozi wa Pakistan nchini Amir Khan baada ya kuzindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na Mwamvua Mwinyi)



Balozi wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete,wakizindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na Mwamvua Mwinyi)


Balozi wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete,wakikagua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na Mwamvua Mwinyi)


Balozi wa Pakistan nchini,Amir khan wa kushoto na mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete,wakiingia katika lango kuu la majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan utete kata ya Pera,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan.(Picha na Mwamvua Mwinyi)



Balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan akizungumza baada ya kuzindua majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu yaliyokarabatiwa na marafiki wa Pakistan katika shule ya msingi Pakistan utete iliyopo kata ya Pera,kushoto kwake ni mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete.(Picha na Mwamvua Mwinyi)

……………………………………………………………….

Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

MBUNGE wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,amewahimiza wananchi kujenga tabia ya kujitolea katika shughuli za kimaendeleo pasipo kuachia serikali/halmashauri na wahisani pekee.

Aidha amesema ofisi yake na halmashauri wataendelea kuunga mkono juhudi za wafadhili na wadau wanaojitokeza kushirikiana nao kutatua changamoto zinazowakabili jimboni hapo ikiwemo elimu.

Ridhiwani alitoa rai hiyo, wakati wa uzinduzi wa majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan Utete iliyopo kata ya Pera,Chalinze wilayani Bagamoyo,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan,kwa gharama ya sh.milioni.30.

Alisema baadhi ya wafadhili wanasaidia endapo wanaona jamii husika ikichukua juhudi na kufikia hatua mbalimbali . Aliwataka wananchi wa Chalinze kushirikiana na serikali,halmashauri na wafadhili wanaojitokeza ili kukamilisha miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao. “Ajenda kubwa tuliyonayo ni kuboresha na kutatua changamoto katika sekta ya elimu” 

“Pamoja na shughuli zinazofanywa na wahisani lakini haina budi wananchi mkajitolea katika shughuli za maendeleo ili tukienda kuomba msaada kwa wafadhili waweze kukubali kirahisi kwa kuona hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa “alisema Ridhiwani. 

Ridhiwani alisema wakati marafiki wa Pakistan wakiwezesha ukarabati huo,lakini halmashauri ya Chalinze imeshatenga fedha kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo nane katika shule ya Pakistan Utete. Hata hivyo,mbunge huyo alieleza kwamba,pia wanajenga matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mbala sanjali na madarasa mawili ya shule ya msingi Makombe. 

Ridhiwani alieleza,ujenzi wa matundu ya vyoo utasaidia kuondoa kero ya uchafu wa mazingira ambapo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakijisaidia ovyo maporini ,vichakani . “Kwasasa kilichobakia ni usimamizi katika hatua ya ujenzi unaoendelea kwenye shule hizo ”alisema Ridhiwani. 

Akizungumzia msaada walioupata kutoka kwa marafiki wa Pakistan,Ridhiwani aliomba ushirikiano ulioonyeshwa usiishie hapo .
Alimpongeza mwenyekiti wa kitongoji Hussein Mramba na diwani wa kata ya Pera kwa jitihada walizozichukua kusukuma jambo hilo. 

Ridhiwani hakusita kumuomba balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan ,kuwasaidia ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa na mashine za kupima magonjwa katika kituo cha afya Chalinze. Akizindua majengo hayo,balozi wa Pakistan nchini Khan,alisema amefurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania,na alishauri kuwepo na mahusiano kati ya wabunge wa Pakistan na Tanzania. 

“Nilipoambiwa kuja shuleni hapa ni km 120 kutoka Dar es salaam nikaona nije kutembea na kuona kilichofanyika,Nawapongeza kwa kuanzisha ujenzi huu ili watoto wapate elimu”alisema Khan. Alisema ili watoto hao wasome vizuri ni vyema kukajengwa uzio katika shule hiyo ili kuweka usalama zaidi hivyo wanatasaidia kuujenga. 

Balozi huyo,aliahidi na kukubali ombi la kusaidia mashine na vifaa vya kituo hicho cha afya lakini kwasasa wanachotakiwa kufanya ni kuandika maombi ya msaada huo.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images