Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1335 | 1336 | (Page 1337) | 1338 | 1339 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kiongozi wa Timu ya wataalamu wanaofanya maboresho ya mfumo wa kielektroniki wa PlanRep, Bi. Nseya Kipilyango akizungumza wakati wa mafunzo kwa watumiaji wa mfumo huo yanayoendelea Mjini Kigoma.
  Mmoja wa Wawezeshaji wa Mfumo wa mfumo wa kielektroniki wa PlanRep Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Jacqueline Manyanga akiwasilisha mada kwa watumiaji wa mfumo huo yanayofanyika Mkoani Kigoma yakihusisha Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.
  Washiriki wa Mafunzo wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea mjini Kigoma.

  Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Afrika kuanza kutumia  mfumo wa kielektroniki wa PlanRep ulioboreshwa ambao husaidia katika mipango, bajeti na kutoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini kote.

  Akizungumza katika mahojiano maalum mjini Kigoma, Mkuu wa Timu ya Mifumo ya TEHAMA kutoka mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)  Desderi Wengaa, amesema kuwa  mfumo huo utasaidia Taifa kufikia maendeleo endelevu kwa wakati kwani utaunganishwa na mifumo mingine iliyopo sasa na utawashirikisha wananchi wote.

  “Mfumo huu utawezesha kutolewa kwa taarifa za miradi ya maendeleo zinazohusu sekta zote zilizoainishwa katika mipango na bajeti kwa wakati katika kipindi chote cha mwaka” alisema Wengaa.

  Aliendelea kusema kuwa PlanRep iliyoboreshwa inaunganisha sekta zote katika mfumo mmoja ambao ni wa kitaifa tofauti na ilivyokuwa awali ambapo kila sekta ilikuwa na mfumo wake. Awali mfumo uliokuwa ukitumika haukuwa unaendana na mahitaji ya wakati hivyo kushindwa kufanya uchambuzi wa kina katika kusimamia rasilimali zilizokuwepo ikiwemo fedha. 

  Aidha,watumiaji wa mfumo huo  wataweza kuutumia mahali popote  kwa kuwa ni wa kitaifa na utaondoa changamoto ya kuwepo kwa matoleo tofauti tofauti. Hali hii itasaidia kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika kwa watoa huduma wa mifumo ya awali katika halmashauri na mikoa yote nchini.

  Kuwepo kwa mradi wa maboresho ya mifumo katika sekta za umma (PS3) kumesaidia wataalamu wa TEHAMA na watumiaji wengine wa mfumo wa PlanRep iliyoboreshwa kujengewa uwezo ili kuimarisha utendaji wao katika kuwahudumia wananchi. Miongoni mwa wanufaika wa mfumo huu ni waganga wakuu,wachumi, maafisa mipango, makatibu wa afya na watoa huduma katika ngazi mbalimbali hasa katika zahanati, vituo vya afya na shule.

   Kuunganishwa kwa mfumo huu katika mifumo ya malipo, kukusanya mapato,  kukusanya taarifa za sekta ya afya na mifumo mingine iliyokuwepo awali kutawezesha uchambuzi wa bajeti kufanyika kwa njia ya mtandao, hivyo kuifanya Mikoa, Wizara, halmashuri na taasisi za Serikali kuwa na toleo moja la bajeti.

  Mfumo wa PlanRep iliyoboreshwa umetengenezwa na wataalamu wazalendo hivyo itakuwa rahisi katika kufanya maboresho endapo yatahitajika kwa kuzingatia mahitaji ya wakati na mikoa husika. Mradi huu wa kuboresha mifumo ya sekta za umma unatekelezwa katika Mikoa 13, Halmashauri 93 na baadaye utatumika nchi nzima.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, akizungumza na waandishi wakati akitangaza matokeo ya mashindano ya afya na Usafi wa Mazingira leo jijini leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohamed Kambi.

   Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
  HALMASHAURI ya Meru uliypo mkoani Arusha inaongoza kwa asilimia 96  kwa usafi wa ujenzi wa na matumizi ya vyoo bora katika kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira iliyohusisha halmashauri 185.

  Hayo ameyasema leo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitangaza matokeo ya mashindano ya afya na Usafi wa Mazingira leo jijini, amesema kuwa halmashauri ya Meru imeweza kufanya vizuri usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora pamoja na kuwa na sehemu ya kunawa mikono.

  Amesema nafasi ya pili kwa  usafi wa mazingira na matumizi bora ya vyoo ni Halmashauri ya Njombe kwa asilimia 95.1 ikifuatiwa na Halmashauri ya Makete kwa asilimia 80.4.

  Waziri Ummy amesema  katika kutekeleza kampeni hiyo  kwa upande wa kijiji bora na mtaa kwa usafi kwa vilivyoshindaniwa ni 80 , kijiji cha Kanikale kinaongoza  wilayanii Njombe kimeongoza asilimia 95.8 , nafasi ya pili imechukuliwa kijiji cha Nambala wilaya Meru kwa asilimia 95.3 na kijiji cha tatu ni Lyalalo kwa asilimia 93.5 wilayani Njombe.

  Amesema majiji na Manispaa ambazo zimefanya kampeni  ya  usafi wa mazingira, vyoo bora pamoja na udhibiti wa taka ngumu kwa Manispaa ni Manispaa ya Moshi kwa asilimia 78.5 mshindi wa Pili Jiji la Arusha kwa 78.1 ikifuatiwa na Manispaa ya Iringa kwa asilimia 67.2 

  Waziri Ummy amesema kampeni ya 2018 wataongeza ofisi za serikali, shule za msingi na sekondari kushindanisha katika usafi wa mazingira na vyoo bora.

  0 0

    Mkuu wa Utawala wa Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Leonard Paulo, akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao kazi cha Inspekta Jenerali wa polisi nchini IGP Simon Sirro na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania salama isiyo na uhalifu.
   
  Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Zarau Mpangule, akitoa mada wakati wa kikao kazi cha Inspekta Jenerali wa polisi nchini IGP Simon Sirro na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania isiyo na uhalifu. 
  Picha na Jeshi La Polisi.

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, akitoa maelekezo kwa  Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini katika kikao kazi cha maelekezo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania salama isiyo na uhalifu.
    Mkuu wa Utawala wa Makao Makuu ya Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Leonard Paulo, akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa kikao kazi cha Inspekta Jenerali wa polisi nchini IGP Simon Sirro na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania salama isiyo na uhalifu.
   
  Mkuu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Kidatu, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Zarau Mpangule, akitoa mada wakati wa kikao kazi cha Inspekta Jenerali wa polisi nchini IGP Simon Sirro na Maofisa Wakuu Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Vikosi na Vyuo vya Polisi nchini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Katika kikao kazi hicho IGP Sirro aliwaelekeza Maofisa hao kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kufikia malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ya kuwa na Tanzania isiyo na uhalifu. 
  Picha na Jeshi La Polisi.

  0 0

  Ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kila mtoto kuanzia chekechekea mpaka kidato cha nne wanapata elimu bure, kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania leo imetoa vitabu vya sayansi kwa shule za mkoa wa Sumbawanga vyenye thamani ya shilingi milioni kumi TZS 10,000,000. Vitabu hivyo vimepokelewa na Mbunge wa Jimbo la kalambo Mh, Josephat Kandege na kugaiwa kwa shule zenye uhabu wa vitabu jimboni humo.

   Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Mbunge wa Jimbo la kalambo Mh, Josephat Kandege alisema “ muhimu kutambua mchango wa makampuni binafsi kama Airtel Tanzania kwa juhudi za dhati za kuunga mkononi serikali yetu katika kuninua sekta ya elimu hapa nchini. sote tunajua ya kwamba serikali yetu inaongozwa na sera ya serikali ya viwanda. Kwa maana hiyo hatuwezi kuwa na viwanda bila ya kuwa na wanasayansi, hiyo basi vitabu hivi vitaongeza chachu kwa wanafunzi wetu wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo ya sayansi na hatimaye kufanikisha ndoto zao pamoja na serikali”.

  Mh Kandege aliendelea kusema kwamba “nawaomba Airtel na wadau wengine waendelee kutusaidia kwenye nyaja zingine mbali mbali ili kuendelea kutengeneza mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi”.
  Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Airtel Rukwa na Katavi Bw, Hapson Kamanya  alisema “Airtel tunaamini jamii iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vya kutosha hususani vitabu,  ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi”.

  Tunaamini ya kwamba msaada wa vitabu utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa na  pia utaongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi” Aliongeza Kamenya.

  Kwa upande Mkuu wa shule ya Mwazye Bw, Haron Mwaibabu akiongea kwa niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu hivyo alisema “Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".

  Aliongeza, ni ukweli kuwa shule zetu zina uhaba wa vitabu vya sayansi kitu ambacho kilikuwa kinatupa ugumu kwenye kufundisha na hata kupelekea baadhi ya wanafunzi wetu kutotamani kuchukua masomo ya sayansi. Tunashukuru sana Airtel kwa kuwa mkombozi kwenye hili’.
  Diwani wa Kata ya Mambo Nkose Kanowalya Siwale (kushoto), Meneja Mauzo Airtel Tanzania Kanda ya Rukwa Hudson Kamenya (wa pili kushoto), Jimbo la Kalambo mkoani Sumbawanga Josephat Kandege wakimkabidhi vitabu vya sayansi Makamu wa shule ya Sekondari ya Kalambe Charles Mnkonya (kulia). Vitabu hivyo vyenye thamani ya TZS10,000,000 vimetolewa na Airtel Tanzania kwa shule za sekondari zenye uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye Jimbo la Kalambo.
  Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kalembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja Mauzo Airtel Tanzania kanda ya Rukwa Hudson Kamenya baada ya kampuni ya Airtel Tanzania kukabidhi vitabu vya sayansi vyenye thamani ya Tzs10,000,000/- mwishoni mwa wiki kwa jimbo la Kalambo mkoani Sumbawanga.
  Meneja Mauzo Airtel Tanzania kanda ya Rukwa Hudson Kamenya (katikati) na Mbunge wa Jimbo la Kalambo mkoani Sumbawanga wakimkabidhi Mwalimu wa somo la Kemia kwenye shule ya sekondari ya Mwazye Aidin Mwaibabu baadhi ya vitabu vilivyotolewa na kampuni ya Airtel Tanzania kwa shule za sekondari zenye uhaba wa vitabu vya sayansi kwenye Jimbo la Kalambo.

  0 0

   Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akizungumza na wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
   Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (Kulia), wakati alipokagua sehemu ya kuingilia abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), wakati alipofanya kikao cha pamoja, leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


  WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa Mwezi mmoja kwa wafanyabiashara wanaotoa huduma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) kulipa kodi ya Majengo kama mikataba yao inavyolekeza.

  Waziri Mbarawa ametoa agizo hilo leo wakati alipokutana na wafanyabiashara hao ili kujadili changamoto mbalimbali zilizopo na jinsi ya kuzitatua ili kuendelea kutoa huduma bora katika uwanja huo.

  “Kulipa kodi za majengo hapa ni suala la lazima, hivyo ifikapo Septemba mwishoni nataka kuona wafanyabiaashara wote mmeshalipa kodi ya pango, makusanyo haya ni muhimu kwetu ili tuendelee na hatua nyingine za uboreshaji wa viwanja vya ndege na huduma nyinginezo.” Amesisitiza Profesa Mbarawa.


  0 0

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Bibi Patrica  Baroness Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa katika ziara ya siku moja na ujumbe aliofuatana nao.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Bibi Patrica  Baroness Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya siku moja. 
  /Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na mgeni wake mara baada ya kumaliza mazungumza na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Bibi Patrica  Baroness Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo. 
  Picha na Ikulu


  JUMUIYA ya Madola imeahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo kama ilivyo kwa wanachama wengine wote 52 wa Jumiya hiyo.

  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi Patricia Baroness Scotland aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.

  Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa Jumuiya ya Madola inaendelea kutekeleza mipango na mikakati kabambe ambayo imeiweka kwa wanancha wake ikiwemo Tanzania ambapo Zanzibar pia, ni miongoni mwao.

  Bi Scotland alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa juhudi kubwa anazozichukua katika kuhakikisha Zanzibar inakuza uchumi na kuimarisha amani na utulivu na kusisitiza kuwa Jumuiya anayoiongoza haitokuwa nyuma kumuunga mkono.

  Aidha, Bi Scotland alimueleza Dk. Shein miongoni mwa mipango ya Jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake wote 52 ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa katika sekta ya biashara nan uchumi, kuwasaidia wanawake, vijana, upatikanaji ajira kwa vijana, elimu, kutunza mazingira, uwezeshaji na mengineyo.

  Aliongeza kuwa uchumi kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo umekuwa ukiimarika kwa kiasi kikubwa kwa zile nchi za Bara la Afrika na hata nchi za Bara la Asia uchumi wake umeimarika kwa asilimia 5 hadi asilimia 8.

  Katika mazungumzo hayo, Bi Scotland alimueleza Dk. Shein kuwa miongoni mwa maeneo yaliopewa kipaumbele na Jumuiya hiyo ni katika kuhakikisha nchi zake wanachama zinaimarika kiuchumi ni pamoja na miundombinu na nishati.

  Akieleza juu ya Jumuiya hiyo ilivyoweka mikakati katika kusaidia katika kupambana na changamoto ya hali ya mabadiliko ya tabia nchi hasa kwa nchi za Visiwa, Bi Scotland alitoa mfano wa nchi yake ya kisiwa cha Jamhuri ya Dominica jinsi ilivyopata athari zilizotokana na hali hiyo.

  Nae Rais Dk. Shein kwa upande wake alitoa pongezi kwa kiongozi huyo kwa ujio wake hapa Zanzibar sambamba na juhudi kubwa zinazochukuliwa na Jumuiya hiyo katika kuendelea kuiounga mkono Zanzibar.

  Dk. Shein kwa upande wake alimueleza kiongozi huyo kuwa Zanzibar iko salama na usalama wake unatokana na kuwepo kwa amani na utulivu mkubwa hatua ambayo inapelekea hata uchumi wake kuzidi kuimarika siku hadi siku.

  Aliongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza kupata mafanikio makubwa katika kuimarisha uchumi wake kutokana na sekta ya utalii, sekta ambayo bila ya kuwepo kwa amani na utulivu ni vigumu kuimarika.

  Dk. Shein alitumia fursa hiyo kueleza juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jinsi inavyochukua hatua katika kuimarisha sekta za maendeleo na kueleza azma ya ujenzi wa bandari mpya ya Mpiga Duri pamoja na kuuimarisha uwanja wake wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa kujenga jengo jipya la abiria.

  Aidha, Dk. Shein alieleza mafaniki yaliopatikana katika kuimarisha demokrasia na utawala bora hapa nchini huku akimueleza juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kutunga sheria ya maadili kwta viongozi  wa umma.

  Dk. Shein, pia, alitumia fursa hiyo kumueleza Katibu Mkuu huyo hatua zinazochukuliwa na Serikali anayoiongoza katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa akina mama na watoto sambamba na juhudi za Serikali za kuanzisha Pencheni Jamii kwa wazee kuanzia miaka 70, jambo ambalo Bi Scotland alilipongeza.

  Pia, alimueleza hali ya mabadiliko ya tabia nchi jinsi inavyoathiri mazingira ya Zanzibar hasa katika kasiwa cha Pemba na sehemu nyenginezo na kueleza hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali pamoja na Jumuiya za Kimataifa katika kupambana na hali hiyo huku akitolea mfano mkutano wa nchi zinazoendelea za visiwa (SIDS) uliofanyika mwaka 2014 huko Samoa na maazimio yake juu ya hali hiyo.

  Akijibu masuali ya waandishi wa habari baada ya mazungumzo hayo, Bi Scotland aliwataka wapinzani kushirikiana na Serikali anayoiongoza Dk. Shein kwa lengo la kuwaletea maendeleo endelevu wananchi wa Zanzibar na kusisitiza kuwa Zanzibar inafaidika na misaada ya Jumuiya hiyo kupitia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Jumuiya ya Madola  ilianzishwa karne ya 20 kwa lengo la kuikutanisha Uingereza na yaliyokuwa makoloni yake duniani kwa jukumu la kuhakikisha wanachama wake wanajikwamua katika Nyanja mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo kisiasa, kiuchumi, kijamii, michezo na burudani huku Malkia wa Uingereza akiwa ndiye Kiongozi Mkuu wa Jumuiya hiyo.

   Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

  0 0


  Benki Kuu ya Tanzania imetoa leseni kwa kampuni mpya ya kutoa mikopo ya nyumba inayoitwa “First Housing Company (Tanzania) Limited”.

  Taarifa iliyotolewa na Idara ya Sera na Leseni katika Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki imeeleza kwamba leseni hiyo inaipa nafasi kampuni hiyo mpya kufanya biashara ya kutoa mikopo ya nyumba nchini. Makao makuu ya kampuni hiyo ni jijini Dar es Salaam. 

  Hii ni mara ya kwanza kwa Benki Kuu kutoa leseni kwa kampuni ya mikopo ya nyumba nchini. 

  Benki Kuu pia inatoa leseni na kusimamia benki, taasisi za fedha, maduka ya kubadilisha fedha, kampuni za karadha na zinazotunza kumbukumbu za ukopaji za wananchi (credit reference bureaus).

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Zanzibar jioni ya leo tayari kuhudhuria sherehe ya Siku  ya Kizimkazi itakayoadhimishwa kesho tarehe 12 Agosti, 2017.

  Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa  Abeid Amani Karume, Makamu wa Rais amekutana na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam.

  Bi. Scotland alikuwa mjini Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam jioni ya leo. Pichani kati ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha-Rose Migiro 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Bi. Patricia Scotland ambaye alikuwa safarini kuelekea Dar es Salaam jioni ya leo. Pichani kati ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha-Rose Migiro .

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Seriakli Dkt.Hassan Abbas.

  0 0


  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Mtanzania anayecheza mchezo wa kikapu nje ya nchi, Hasheem Thabeet (kushoto), walipokutana kwa ajili ya Maandalizi ya Tamasha la Usalama Barabarani, linalotarajiwa kufanyika kesho Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mtanzania anayecheza mchezo wa kikapu nje ya nchi. Hasheem Thabeet (wapili kushoto), baada ya mazungumzo ya Maandalizi ya Tamasha la Usalama Barabarani, linalotarajiwa kufanyika kesho Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.Wengine ni ujumbe ulioongozana na mchezaji huyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKLALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na katika ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya katika ukumbi wa Arnautoglou jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Afisa Mtendaji  Mkuu (RITA) Emmy Hudson akizungumza na waandishi  wa habari katika mkutano wa viongozi wa gazi ya Mkoa na Wilaya kuhusu usajili wa matukio muhimu ya Binadamu na kutambulisha majaribio ya mfumo wa Tehama katika ukumbi wa Arnautoglou, jijini Dar es Dalaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


  0 0

  Siku moja baada ya Marekani kutangaza kutoa fedha za nyongeza katika mwaka ujao kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hapa nchini, nchi hiyo imetiliana saini na Wizara ya Fedha na Mipango makubaliano ya kutoa Dola Milioni 225. 

  Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya, Kilimo na Utawala bora. 

  Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini Bw. Andy Karas. 

  Akizungumza baada ya kutiliana saini makubaliano hayo Bw. Doto James ameishukuru Marekani kwa kuendeleza uhusiano mzuri uliopo na Tanzania na amesema fedha hizo zitasaidia kuimarisha juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi. 

  Nae Bw. Andy Karas amesema Serikali na watu wa Marekani wanafurahishwa na kuendelea kwa ushirikiano mwema kati yao na Serikali ya Tanzania katika maendeleo na ameahidi kuwa ushirikiano huo utadumishwa. 

  Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe. Dkt. Inmi Patterson ambaye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto)akisaini mkataba wa Makubaliano (Strategic Assistance Agreement )na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas(katikati) kuhusu utoaji wa fedha hizo dola za kimarekani Millioni 225 , tukio lililofanyika katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Wakwanza kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson akishuhudia.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto) akibadilishana mkataba ya makubaliano (Strategic Assistance Agreement) na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (wakwanza kushoto) akipiga makofi pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas(katikati), na Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano (Strategic Assistance Agreement ) katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini Dkt. Inmi Patterson mara baada ya kusaini mkataba huo utakaowezesha Tanzania kupatiwa fedha hizo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akimshukuru Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Marekani nchini USAID Andy Karas mara baada ya tukio hilo la mkataba wa makubaliano katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa CUF Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya Agosti 11. 2017, Waziri Mkuu yupo wilayani Kaliua kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Tabora 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akiongea na wananchi wa kitongoji cha Mwamnange kilichopo Wilaya ya Kaliua leo Agosti 11, 2017 .Wananchi hao walisimamisha msafara wake ili kumuomba serekali iwasaidie kupata umeme. 

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihotubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Veta Jimbo la Ulyankulu wilayani Kaliua mkoani Tabora leo August 11, 2017, ambapo amewataka wananchi waliopewa uraia kuheshimu sheria za nchi vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Ulyankulu waache kujihusisha na matukio ya uhalifu. 

  Ametoa onyo hilo leo mchana (Ijumaa, Agosti 11, 2017) wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa tarafa ya Ulyankulu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya VETA, wilayani Kaliua mkoani Tabora. 

  Amesema matukio ya ujambazi, mauaji na umiliki wa silaha yanayofanyika kwenye tarafa hiyo ni mengi ikilinganishwa hali ilivyo kwenye maeneo mengine ya mkoa huo. 

  "Taarifa nilizonazo zinaonyesha katika kipindi cha miaka miwili kumekuwa na matukio ya mauaji 35, ujambazi matukio 12, umiliki wa silaha nao unatisha. Yamekamatwa magobole 11, bunduki aina ya SMG saba na Mark Four mbili."

  "Tulikamata pia risasi 714 za SMG zikiwa kwenye ndoo za mafuta na juu yake wamepaka mafuta ya mawese. Pia risasi mbili za Mark Four zilikamatwa," amesema Waziri Mkuu. 

  Waziri Mkuu amewataka wakazi hao ambao baadhi yao wamepewa uraia na wengine bado ni wakimbizi waonyane wanapokutana kwenye vikao vyao kwa sababu matendo yao yanaikwaza Serikali ambayo iliamua kuwapa hifadhi. "Ni vema mkikutana kwenye vikao vyenu muelezane na kuonyana," amesema Waziri Mkuu. 

  "Ninawasihi matukio haya myadhibiti la sivyo mtaharibu nia njema iliyoleta uwepo wenu.  Bunduki na risasi zinakuja kufanya nini wakati nyie mko maeneo salama? Mauaji ya nini?  Kama kuna tatizo limekupata, muone mwenyekiti wa kijiji,  atakusaidia," alisisitiza.

  Alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi yao ambao wamegeuka mawakala na wameanza kuwaleta ndugu zao bila kufuata utaratibu. "Hatuzuii mtu kutembelewa na ndugu yake, lakini ni lazima mfuate taratibu. Tunataka tudumishe amani iliyopo nchini lakini pia tudumishe urafiki wa nchi zetu mbili za Burundi na Tanzania," aliongeza. 

  Mapema, Mbunge wa jimbo la Ulyankulu, Bw. John Kadutu alimuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la upatikanaji wa maji kwenye tarafa hiyo, pia aliomba wasaidiwe ili kata tatu za Kanindo, Igombenkulu na Milambo ziwezeshwe kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa. 

  0 0

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewaagiza Makatibu tawala wa mikoa yote Tanzania bara kuratibu zoezi la Hospitali tembezi katika mikoa yao ili kuwasaidia wananchi wa hali ya chini kupata huduma ya kibingwa. 

  Jafo ametoa agizo hilo leo alipokuwa akizindua huduma za hospitali tembezi kwa wilaya ya Chemba na Kondoa zoezi ambalo limefanyikia mjini Kondoa.Mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika katika wilaya ya Kongwa, Mpwapwa, Chamwino na sasa linaendelea kwa wilaya za Chemba na Kondoa.

  Akizindua huduma hiyo, Jafo ameumwagia sifa uongozi wa mkoa wa Dodoma kwa kuratibu vyema zoezi hilo ambapo zaidi ya wagonjwa 8,000 wamefanyiwa uchunguzi huku 500 wakifanyiwa upasuaji mdogo na mkubwa.

  Amewataka wananchi wa wilaya hizo kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizo za kibingwa huku akiwataka kupima tezi dume kwa kuwa umekuwa ugonjwa tishio kwa wanaume.

  Ameeleza kuwa huduma hizo za kibingwa zinatolewa kwa gharama nafuu na hivyo kuwawezesha wananchi wasio na uwezo kupata matibabu.Jafo amewapongeza madaktari bingwa wa mkoa wa Dodoma kwa kazi kubwa wanayoifanya na amewataka wengine waige mfano wa Dodoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya ya Kondoa na Chemba.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.James Kiologwe na viongozi wa wilaya ya Chemba na Kondoa.
  Mbunge wa Chemba Juma Nkamia akizungumza katika uzinduzi wa Hospitali tembezi katika wilaya za Kondoa na Chemba.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wagonjwa na viongozi katika uzinduzi wa Hospitali tembezi.
  Wananchi waliofika katika uzinduzi wa hospitali tembezi.

  0 0

  Katibu wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Iringa ndg:James mgego akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya uchaguzi wa jumuiya ya Umoja wa Vijana kwa Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka alipowasili kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi za CCM Mkoa .
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akipitia kwa umakini Taarifa ya uchaguzi ya Uvccm Mkoa wa Iringa alipowasili kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi za CCM Mkoa wakati akielekea katika chuo cha mafunzo Ihemi .
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akisalimiana na viongozi na wanachama wa chama cha mapinduzi alipowasili katika chuo cha Mafunzo IHEMI Iringa.
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka (pili kulia) akisalimiana na watumishi walio katika maandalizi ya mwisho ya kukamilisha utekelezaji wa kukifufua chuo cha mafunzo ihemi Iringa.
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi,wanachama pamoja na watumishi walio katika maandalizi ya mwisho ya kukamilisha utekelezaji wa kukifufua chuo cha mafunzo ihemi Iringa.

  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akitazama baadhi ya
  nyaraka na vitabu mbali mbali vilivyokua vikitumika wakati wa mafunzo
  katika chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka (wa tatu)akielekea kukagua baadhi ya majengo ya Chuo cha mafunzo Ihemi Mkoan Iringa.
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akikagua majengo ya madarasa katika chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka(wa nne kushoto) akitazama jengo la Utawala katika chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.
  Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akipata maelekezo katika mchoro wa ramani wa kubadilisha majengo na muonekano wa chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.
  Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe:Amina Masenza (kushoto) akizungumza jambo alipokutana na Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka katika mazungumzo juu ya hatua za kukifufua chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa.
  Pich ya pamoja ndg:Ndg:Kaimu katibu mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka (wa pili kushoto)Mhe:Amina masenza Mkuu wa mkoa Iringa (wa tatu kushoto), mkuu wa Wilaya ya kilolo Asia Abdallah,pamoja na ndg:John Melele Msaidizi wa Kaimu Katibu Mkuu Umoja wa Vijana wa CCM Taifa mara mazungumzo juu ya hatua za kukifufua chuo cha mafunzo Ihemi Mkoani Iringa. katika za mkuu wa mkoa wa Iringa.

  (PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)

  0 0


  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kushoto), wakitia saini mkataba huo wa ushirikiano kati ya taasisi zao hizo. Kulia anayemsaidia Postamasta Mkuu ni Mwanasheria wa TPC, Bi. Zuhura Pinde.
  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kushoto), wakitia saini mkataba huo wa ushirikiano kati ya taasisi zao hizo. Aliyesimama kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TPC, Elia Madulesi.
  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kulia), wakibadilishan hati za mkataba huo, mara baada ya kuusaini jijini Dar es Salaam leo.
  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kushoto) na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (kulia), wakiuonesha kwa waandishi wa habari mkataba huo, mara baada ya kuusaini jijini Dar es Salaam leo. 


  Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, akizungumza na waandishi wa habari, wakati akielezea kuhusu makubaliano ya ushirikiano ya kutoa huduma na Shirika la Posta Tanzania (TPC), jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa. Makubaliano kati ya taasisi hizo, ni katika nyanja za 1. Usafirishaji wafanyakazi, wanaposafiri kikazi, 2.Usafirishaji wa mizigo, vifurushi na barua kupitia ndege za ATCL, 3. Kubadilishana uzoefu wa namna ya kuhudumia wateja, 4. Ushirikiano wa matumizi ya majengo ya Ofisi na 5. Kushirikishana kwenye tovuti kuhusu mambo yote ya Masoko. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
  Baadhi ya Maofisa wa TPC na waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, wakati wa mkutano huo.
  Baadhi ya Maofisa wa TPC na waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi, wakati wa mkutano huo, wa makubaliano ya ushirikiano wa taasisi hizo wa kutoa huduma.
  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano huo.
  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (kulia), akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano huo.

  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deo Kwiyukwa (kulia), akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi, kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara na Masoko wa ATCL, Josephat Kagirwa na aliyesimama ni Mwanasheria wa ATCL, Phillipo Mahenge.
   
  Postamasta Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPC, Deo Kwiyukwa (kulia) akimtambulisha baadhi ya watendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mwendeshaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi (wa pili kulia), mara baada ya kumalizika shughuli hiyo, Dar es Salaam leo.

  0 0


  0 0


  Baadhi ya wananchii wakiwa wamezunguka Banda la Tigo wakipata Huduma Mbalimbalia katika maonesho ya kilimo ya Nane nane yaliyopo Ngongo Mkoa wa Lindi.
  Meneja wa kanda ya Kusini wa Kampuni ya Tigo Uthman Madata akigawa Kofia Katika Banda la Tigo katika Maonesho ya Kitaifa ya Kilimo ya Ngongo Mkoani Lindi
  Meneja wa kanda ya Kusini wa kampuni ya mtandao wa Tigo Uthman Madata akimuonesha Simu ya Mkononi Aina ya Tekno S1 Mwanafunzi wa Sekondari ya Lindi Charles Shirima katika maonesho ya Kilimo ya Nanenane yaliyofanyika Mkoani Lindi.
  .Meneja wa kanda ya Kusini kampuni ya mtandao wa Tigo akiongea na baadhi ya wateja wa Tigo waliofika kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali katika maonesho ya kilimo ya Nanenane
  .Meneja wa kanda ya Kusini kampuni ya mtandao wa Tigo akiongea na baadhi ya wateja wa Tigo waliofika kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali katika maonesho ya kilimo ya Nanenane​

  0 0


  Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma (kushoto), akimkabidhi simu aina ya S1 mmoja kati ya washindi 120 wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, Margteth Taumbe katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma (kushoto), akimkabidhi simu aina ya S1 mmoja kati ya washindi 120 wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, Pili Mohamed katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma (kushoto), akimkabidhi simu aina ya S1 mmoja kati ya washindi 120 wa promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi, Rajabu Ngorongo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Tigo Tanzania, mtandao unaoongoza kwa maisha bora ya kidijitali, inaendelea kuwazawadia wateja wake na kwa wakati huu imezawadia wateja wake 120 na simu mpya za mkononi za smartphone Tecno S1. Hii ni sehemu ya kampeni inayoendelea ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi kwa wiki ya kwanza ya Agosti.

  Akizungumza kwenye hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Dar es Salaam, Afisa Mzinduzi wa Bidhaa za Tigo, Jacqueline Nnunduma, alibainisha kuwa tofauti na promosheni nyingine ambapo wateja wachache tu wanapata zawadi, Tigo inatoa simu moja ya Tecno S1, kila saa kwa masaa 24 kila siku ya wiki kwa muda wote wa kampeni hiyo ya kusisimua.

  "Promosheni ya Tigo Jaza Ujazwe, Ujaziwe Zaidi ni bora zaidi na tofauti na promosheni nyingine kwa sababu kila mteja anapata zawadi kila mara anapoongeza muda wa maongezi . Kwa kuongeza salio tu, kila mteja pia anapata nafasi ya kushinda simu moja ya Tecno S1 smartphone inayoshindaniwa kila saa ya kila siku, kwa siku saba za wiki. 
   
  Washindi wa simu ya smartphone ya Tecno S1 pia watafurahia mawasiliano ya bure ya simu kwa mwaka mmoja. Zawadi nyingine anazoweza kushinda mteja ni pamoja na bonasi ya bure kwenye huduma ya sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno SMS kulingana na matumizi ya mteja husika, "alisema.

  Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za mkononi 720 zipo tayari kunyakuliwa katika promosheni inayoendelea sasa ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi. Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa kirahisi kwa kuongeza muda wa maongezi wa Tigo kupitia kadi za kukwangua, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo ya nafasi ya kushinda moja ya simu za mkononi zinazoshindaniwa kila saa , ya kila siku kwa siku saba za wiki.

  Aliendelea kuongeza kuwa Waratibu wa Biashara na Masoko wa Tigo tayari wamejiandaa kukabidhi simu za smartphones kwa washindi wengine wa droo ya wiki hii waliopatikana kutoka Dodoma, Tanga, Kagera, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Singida, Tanga na Zanzibar.

  "Kama kawaida, Tigo inasikiliza na kuitikia mahitaji ya wateja wake, na sasa tunawapatia zawadi kemkem kama njia mojawapo ya kuwashukuru kwa kuendelea kutumia bidhaa na huduma zetu bora. Nachukua fursa hii kuwakumbusha wateja wote wa Tigo kwamba zawadi ni nyingi na wote wanaoshiriki wanashinda zawadi, kwa hiyo wachangamkie fursa hii ya kusisimua ya kuvuna zawadi kupitia promosheni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi ", alisema Nnunduma.


  Mwisho

older | 1 | .... | 1335 | 1336 | (Page 1337) | 1338 | 1339 | .... | 1897 | newer