Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1331 | 1332 | (Page 1333) | 1334 | 1335 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Msanii chipukizi wa kizazi kipya kutoka mkoani Ruvuma anayejulikana kwa jina la LANISTER amefunga ya moyoni kupitia Exclusive Interview ya Ruvuma TV kuhusu uonevu uliopo katika Media .

  0 0

   Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney (kulia), akitoa mafunzo ya siku moja ya kilimo chenye tija  kwa maofisa Ugani wa Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani hapa juzi.
   Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Amina Pemba akizungumza kwenye mafunzo hayo.
   Maofisa Ugani wakipata mafunzo.

  Ofisa Kilimo kutoka Manispaa ya Lindi, Hussein Mwapili, akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya kupata mafunzo hayo.

   Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro (SUA), akizungumza na maofisa ugani hao katika mafunzo hayo.
   Mafunzo yakiendelea.
   Wahamasishai wa matumzi ya Bioteknolojia katika kilimo wakijadiliana wakati wa mafunzo hayo. Kulia ni Happiness John na Flaviana Anthony.
  Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya ya Kilwa, Ramadhan Hatibu akizungumza kwenye mafunzo hayo.

  Na Dotto Mwaibale, Lindi

  MAOFISA ugani mkoani Lindi wamesema wanashindwa kuwahudumia kikamilifu wakulima kutokana na kukosekana kwa usafiri wa kuwapeleka vijijini pamoja na kutelekezwa na 
  wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kushindwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara.

  Wakizungumza juzi katika mafunzo kuhusu kilimo bora yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia, COSTECH, maofisa ugavi hao walisema kutokana na 
  upungufu wa wataalam hao wamekuwa wanahudumia vijiji vingi na mtu mmoja anaweza kuhudumia vijiji hadi sita. 

  Pia walisema kwamba tatizo lignine wamekuwa hawapati 
  mafunzo ambayo yatawezesha waweze kwenda na wakati.

  Ofisa Ugani kutoka Manispaa ya Lindi Hussein Mwapili alisema wizara ya kilimo baada ya kuwakabidhi maafisa ugani kwa halmashauri imeshindwa hata kuwafuatilia na hata kuwajengea nyumba wakati wizara zingine kama elimu na afya zinawakumbuka wataalamu wao kwa kuwajenge nyumba na kuwapa miongozo ya mara kwa mara.

  “Sisi tumesahulika kabisa, tunakumbukwa wakati wa njaa tu ndipo utaona tunalaumiwa kwamba tunaishi mjini, lakini wizara ya kilimo imefanya nini kuhakikisha maafisa ugani wanaishi katika mazingira bora ya kufanyia kazi? Kule vijiji tunaambiwa 
  tukaishi huko je kuna nyumba za wagani? alihoji.

  Amina Pemba ambaye ni afisa ugavi kutoka manispaa ya Lindi alitaja changamoto zinazowakabili ni kukaa kwa muda mrefu bila kupata mafunzo au semina kuhusu taaluma yake ya kazi kwa vile kilimo ni sayansi na inabadilika mara kwa mara.

  Alisema hata kama anatembea kwa miguu hawezi kuwafikia watu wengi alisema maafisa ugavi hawana usafiri wa kwenda vijijini. “Tunashukuru juzi mkurugenzi ametupatia gari idra ya kilimo, hatujawahi kupatiwa usafiri tangu nianze kazi miaka 20 
  iliyopita.”

  Alisema maofisa ugavi hawana vifaa vya kupimia ardhi kujua aina ya madini yaliyoko pale ili waweze kuwashauri wakulima aina ya mazao anayotakiwa kupanda au aina ya mbolea anayotumia kulingana na hali ya udongo.

  Pemba alisema kwamba hata tafiti zinazofanywa na wataalamu wa wizara ni taasisi zingine za utafiti hazishuki kwa maafisa ugavi jamboa mbalo linafanya tafiti hizo zisiwe na msaada kwa mkulima.

  Alisema pamoja  na kuhamasishw akwenda vijijini lakini hakuna nyumba za maafisa ugavi na hilo linatokana na wizara ya kilimo kuwatekeleza wataalamu hao na hivyo kusababisha kufanya kazi katika mazingira magumu.

  “Sisi tukiwezeshwa wagani tutawajibika, lakini kwa hali ilivyo sasa ni ngumu kuwafikia wakulim wote, wagani wengi hawana usafiri,” alisema.

  Ofisa ugani wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Mligo Eisen   alisema katika idara ya mifugo kuna pikipiki tatu na idara yote ya kilimo kuna gari moja ambalo tangu lipatikane halina zaidi ya miezi sita na vifaa hivyo vya moto ndivyo vinavyotegemewa na maofisa ugani na maofisa mifugo ili kuwafikia wakulima hali 
  ambayo ni changamoto kubwa.

  Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa maofisa ugani jambo linalochangia wakulima kupata elimu ya kilimo kwani ofisa ugani mmoja anatakiwa kutembelea vijiji vitatu na kukutana na wakulima wa aina tofauti ambao wanalima mazao 
  tofauti.

  Alisema hali hiyo inamfanya ofisa ugani husika kushindwa kuwafikia wakulima wake wote hivyo kuwa chanzo cha wao kukosa elimu ya kilimo na kupata chakula kidogo na 
  mazao ya biashara.

  Katika maonesho ya nanenane yanayoendela mjini hapa, wakulima ambao wamekuwa wanapatiwa mafunzo na tume ya taifa ya sayansi na teknolojia wamekuwa wanawalalamikia wagani wa kilimo kwa kushindwa kuwafikia na kuwapatia huduma za 
  ushauri wa kitaalamu wanazohitaji.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akiukaribisha ugeni wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (kushoto) ulipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akizungumza wakati ugeni wa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (kulia) ulipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Simon Migangala (kulia) akieleza machache kuhusu umuhimu wa Benki ya Kilimo kwenye uchumi wa viwanda.
  Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed (katikati) akizungumza na viongozi wa TADB alipotembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.
  Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed akihimiza jambo kwa uongozi wa Benki ya Kilimo.
  Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Sarah V. Chiwamba akizungumza wakati wa Ziara hiyo.
  Mhe. Hamad akitembelea mabanda ya wakulima walionufaika na Mikopo ya TADB.

  ………………………………….

  Na Mwandishi wetu,

  Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameiasa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwezesha wakulima ili waweze kuchangamkia fursa za kuuza mazao ya kilimo nje ya nchi ili kuwaongezea kipato wakulima hao.

  Waziri Hamad aliyasema hayo alipolitembelea Banda la TADB katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini humo.

  Mhe. Hamad alisema kuwa Tanzania inapata fursa nyingi za masoko nje ya nchi kwa mazao mbalimbali ikiwemo zao la karafuu, korosho na mazao ya mikunde ikiwemo dengu na mbaazi zinazotakiwa sana nchini India na Arabuni.

  “Naiomba Benki ya Kilimo kuwawezesha wakulima wanaolima kibiashara ili kuchangamkia fursa za masoko kwa mazao ya kimkakati yakiwemo zao la karafuu, korosho na mazao ya mikunde ikiwemo dengu na mbaazi ambazo nchi nyingi marafiki wanahitaji,” alisema Mhe. Hamad.

  Aliongeza kuwa wizara yake inaletewa maombi mengi ya mazao kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nchi hizo.

  Kwa mujibu wa Waziri Hamad kuna wafanyabiashara wa kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wanaohitaji zaidi ya kontena mbili za korosho kwa wiki hivyo Benki ya Kilimo ina wajibu wa kuwezesha wakulima ili waweze kuchangamkia fursa hizo.

  “Naamini Benki ikiwawezesha wakulima wanaweza kuchangamkia fursa za masoko ya nje ikiwemo ya wafanyabiashara kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu wanaohitaji zaidi ya kontena mbili za korosho kwa wiki,” aliongeza.

  Akizungumza wakati wa akipokea ugeni huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa TADB ni kuchagiza juhudi za serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania.

  Aliongeza kuwa katika kutekeleza hayo Benki ya kilimo imedhamiria na kujizatiti katika kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.

  “Lengo letu ni kuhakikisha tuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.

  Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta hizo ili kuongeza tija sekta hizo ili kupambana na umaskini nchini.

  0 0

  Msanii wa filamu nchini, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

   MUDA mfupi baada channel ya mtandaoni ya Global TV Online kuendesha kampeni maalum yakumchangia fedha za kusaidia matibabu na huduma kwa msanii wa filamu nchini, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’,wadau mbalimbali wameonekana kuiunga mkono kampeni hiyo. Kampeni hiyo iliyopewa jina la Support Treatment For Jini Kabula, imeonekana kuwagusa watu mbalimbali hivyo kuahidi kujitolea kwa moyo japo kwa kidogo chochote kadiri watakavyojaaliwa.Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ enzi akiwa salama.
   Kwa nyakati tofauti, wadau kadhaa wamezungumza na kusema kuwa wameumizwa na kuguswa na tatizo la msanii huyo baada ya kutazama mahojiano kupitia Global TV Online.“Binafsi nimeguswa sana tatizo la Jini Kabula hivyo kwa chochote nitakachojaaliwa nitajitolea kwa ajili ya kusaidia kidogo, naamini na wengine wataguswa kama mimi, maana najua Watanzania tuna moyo wa upendo na mshikamano kwenye matatizo,” alisema mmoja wa wadau waliozungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wetu. Ndugu wa karibu wa Kabula wameliambia gazeti hili kuwa kwa yeyote aliyeguswa na tatizo hilo basi atume mchango wake kupitia namba 0712 56 53 69, ambapo jina litasomeka Daynes Jolwa ambaye ni dada wa Jini Kabula.

  0 0

  KUTOKANA na changamoto nyingi za ukosefu wa makazi ya kuaminika kwa watu wengi, mshindi wa Sh Milioni 20, Innocent Nyeriga, amesema anatafakari fedha zake alizokabidhiwa jana mjini Dodoma aziweke kwenye ujenzi wa nyumba.

  Nyeriga mkazi wa Dodoma na mshindi wa Biko droo ya 29 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alikabidhiwa fedha zake jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma tayari kwa kuanza kuzitumia kwa matumizi yake ya kawaida.

  Akizungumza kwa furaha kubwa, Nyeriga anayejighulisha na kibarua cha kuhudumia mifugo mjini Dodoma, alisema kwamba lengo lake haswa ni kujenga nyumba nzuri ili familia yake iondokane na changamoto ya ukosefu wa makazi bora.

  “Nawashukuru Biko bahati nasibu iliyokomboa maisha yangu, hivyo fedha hizi tangu mwanzo nilizipanga nijengee nyumba saa chache baada ya kupewa taarifa ya ushindi wangu, nikiamini haya yote yameletwa na Mungu kwa kuwatumia Biko,” Alisema Nyeriga.

  Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema mchezo wa Biko ni mzuri na rahisi kucheza pamoja na kushinda kwake, huku akiwataka Watanzania kuchangamkia ili waweze kuvuna mamilioni ya zawadi kwa kuanzia zile papo kwa hapo bila kusahau donge nono la Jumatano na Jumapili la Sh Milioni 20 kama alizonyakua Nyeriga.

  “Mchezo huu wa Biko unachezwa kwa kutumia simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo wanachotakiwa ni kufanya miamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya Kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.

  “Mbali na kushinda zawadi kubwa ya Sh Milioni 20 ambayo ni lazima iende kwa mshindi Jumatano na Jumapili, lakini pia zawadi za papo kwa hapo zinatoka kila dakika ambazo ni zile za Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja inayoenda kwa mshindi mara baada ya kupokea ujumbe wa ushindi kwenye simu anayotumia kuchezea Biko,” Alisema Melles.

  Kwa kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Dodoma, mshindi mwingine wa Milioni 20 anatarajiwa kujulikana katika droo ya kesho Jumatano maarufu kama Jumatamu na nyingine itakuwa Jumapili huku ikiitwa Jumadili na waendeshaji hao wa Biko.
  Mshindi wa Droo ya 29 ya Biko, Innocent Nyeriga wa pili kutoka kulia akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles wa pili kutoka kushoto mwenye fulana ya Biko.
  Shughuli ya makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wa Dodoma, Innocent Nyeriga ikiendelea katika benki ya NMB jana mjini Dodoma.
  Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kushoto akimkabidhi mshindi wao wa Sh Milioni 20 fedha zake jana Jumatatu katika benki ya NMB, Mjini Dodoma anayejulikana kwa jina la Innocent Nyeriga aliyeibuka kidedea kwenye droo ya 29
  Mshindi wa Sh Milioni 20 wa mjini Dodoma, Innocent Nyeriga, akiwa amezilalia fedha zake baada ya kukabidhiwa jana Jumatatu katika benki ya NMB, mjini Dodoma. Nyeriga aliibuka mshindi wa Biko droo ya 29.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Patterson ofisini kwake Jijini Arusha.

  Katika mazungumzo yao Bi Inmi Patterson amempongeza Mkuu huyo wa mkoa kwa kufanikiwa kuirudisha Arusha katika hali ya amani na utulivu.
  “Kwa kweli sisi kama wamarekai tunafurahi sana kuiona Arusha ikiwa katika hali hii kwani Taifa letu ndio linaloongoza kwa kuleta watalii wengi hapa kwenu na sisi kama balozi tuna wajibu wa kuangalia viashiria vyote vya vurugu na machafuko, ila kwa sasa tunawasemea vizuri sana kwa watu wetu, hongera sana Kamishna kwa jitihada zako sasa Arusha ni mahali salama” amesema Kaimu balozi huyo.

  Bwana Gambo alimshukuru sana Balozi huyo kwa kumtembelea Ofisini kwake na amemweleza wao kama mkoa wa Arusha wana wajibu wa kukuza Utalii Mkoani humo kwa asilimia kubwa ya mapato ya utalii yanatokana na mkoa wa Arusha.

  “Utalii ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu sisi watu Arusha na pato la taifa kwa sekta ya utalii inachangiwa na Arusha kwa zaidi ya asilimia 80% hivyo unaweza kuona namna ambavyo amani na utulivu visipotiliwa mkazo vinaweza kuleta hasara kubwa kwa watu wa Arusha na taifa kwa ujumla wake.” Amesema Mhe Gambo.

  Kaimu balozi huyo wa Marekani ameambatana na Bwana Steve Mshauri wa masuala ya Sheria wa Ubalozi huo na Bi. Brinille Eliane Ellis Afisa wa masuala ya Uhusiano wa Ubalozi huo. 
  Mhe Gambo akiwa katika mazungumzo na Kaimu balozi wa Marekani Bi Inmi Patterson
  Kutoka kushoto ni Afisa Mahusiano wa Ubalozi wa Marekani Bi. Brilliane Ellis, Bwana Steve mshauri wa masuala ya kisheria wa ubalozi huo
  Kaimu Balozi wa MArekani Bi Seoung akimkabidhi Mkuu wa Mkoa zawadi ya kitabu chenye historia ya Rais wa Marekani Bwana Barrack Obama. “Ninajua unampenda sana Kiongozi huyu na umekua unamsoma sana, haya ninakupa kitabu kingine kilichoandikwa na New York times” alisema Balozi huyo wakati anamkabidhi Mhe Gambo kitabu hicho.
  Mhe Gambo na Kaimu balozi wa Marekani katika picha ya pamoja.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha akimsindikiza mgeni wake kutoka nje ya ofisi yake.
  RC Gambo katika picha na mgeni wake nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha.

  0 0

  Mashabiki wa Simba waliojitokeza kwenye Tamasha la Simba Day linalofanyika Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam .. Klabu ya Simba yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam ina utaratibu wake wa kuenzi vitu vyake vya klabu kwa kuanzisha siku maalumu ambayo wanasimba wote hukusanyika pamoja kujadiliana mambo mbalimbali.Agosti 8 ya kila mwaka huwa ndiyo siku hiyo iliyopewa jina la ‘Simba Day’, wameichagua wao Wanasimba kama sehemu ya kumbukumbu ambapo huchagizwa na mambo mengi ikiwemo kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka, kubadilishana mawazo, na mwisho huchezwa mechi ambayo ndiyo huitimisha kila kitu.  0 0

  Na Agness Francis, Globu ya Jamii
  Mgombea wa Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Shija Richard ameanza rasmi harakati za kufungua kampeni yake ya kuwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo hapa nchini. 

  Shija amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam nia na madhumuni ni kufungua rasmi zoezi la kampeni yake ambayo imejikita  kuzungumzia sera zaidi ya TFF  badala ya  maswala ya kiutendaji

  Mgombea huyo amesema kuwa atahakikisha  kunakuwepo na sport Academi katika kanda sita hapa nchini, hii itaongeza vipaji vingi vya kabumbu na  kuwashawishi  wazazi wanapeleka watoto wao wenye vipaji katika  shule hizo za mafunzo ya mpira.

  Hata hivyo Shija amesema kumekuwa na tatizo kubwa kwa klabu kukosa kuwa na uwanja, na hilo pia husababisha kutofanya vizuri kimataifa hivyo amesema atahakikisha anatafuta wadhamini kujikita katika swala zima la miundo mbinu ili kila klabu kujengewa kiwanja chake

  Amesema ili kucheza mpira kwa amani na utulivu bila kupendelea upande mmoja wa timu  ataweka mkakati kwa kushirikiana na vyama vingine vya michezo duniani kote ili kuleta ufanisi kwenye mchezo huo hapa nchini.

  Uchanguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti  mwaka huu mjini Dodoma ambapo wagombea hao wa  kiti cha urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) ni Shija Richard, Wallace Karia, Iman Madega, Ally Mayay,  na Emmanuel Kimbe.
  Mgombea urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Shija Richard akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna atakavyofanya kampeni zake alizozizundua leo rasmi na akiahidi maendeleo ikiwemo na kujenga shule za akadeni ya kabumbu katika kanda sita 6 nchini.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Lindi
  Kwa mara nyingine tena Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imepata ushindi wa kwanza kwenye kundi la Taasisi za Utafiti na Mafunzo katika maonesho ya Wakulima Nanenane, 2017 yaliyokuwa yakifanyika kitaifa kwenye uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.

  Baada ya kutangazwa mshindi katika sherehe za ufungaji rasmi wa Maonesho, VETA imekabidhiwa kombe na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli za ufungaji wa maonesho hayo zilizofanyika leo 8 Agosti, 2017. 

  VETA ilifuatiwa na Chuo cha Maji katika nafasi ya pili na Chuo cha Uhasibu Arusha ambacho kilishika nafasi ya tatu katika kundi hilo. 

  Kaulimbiu ya maonesho hayo ilikuwa, "Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati." 

  Katika maonesho hayo, VETA ililenga kutoa taarifa na kuhamasisha wananchi kutumia fursa mbalimbali za mafunzo ya ufundi stadi ili kuboresha shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi, hivyo kuzalisha kwa tija. 

  Vilevile VETA ilionesha ubunifu wa teknolojia bora na rahisi katika kilimo, mifugo na uvuvi na kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii ya wananchi wa kijijini. 

  Mfano wa ubunifu na teknolojia ni pamoja na mashine za kufukuza ndege waharibifu wa mazao mashambani, vifaa vya kumwagilia, ujenzi wa nyumba kwa gharama nafuu,   mashine za kisasa za usanifu wa nguo, jiko la kisasa linalotumia mafuta ya taa na nyinginezo. 

  Katika maonesho hayo VETA imepokea wageni mbalimbali ikiwemo viongozi wa kitaifa ambao kwa pamoja walikiri kufurahishwa na juhudi zinazofanywa na vyuo vya ufundi stadi nchini hasa kupunguza tatizo la ajira kwa vijana nchini huku wakishauri kutanua wigo wa utoaji mafunzo ili kufikia makundi mengi zaidi. 

  Mkuu wa JKT Meja Jenerali Michael Isamuhyo aliiomba VETA kushirikiana na jeshi hilo kuandaa mafunzo maalum ya ufundi stadi kwa vijana wanaojiunga na kambi za JKT katika maeneo mbalimbali nchini. Lengo la ombi hilo ni kuhakikisha kuwa vijana hao wakimaliza mafunzo ya jeshi watoke pia na ujuzi na vyeti vinavyotambulika na VETA na kukubalika kitaifa. 

  Akizungumzia ushindi huo, Meneja Uhusiano wa VETA, Sitta Peter alisema, ni ishara  kuwa jamii na mamlaka mbalimbali wanazidi kutambua na kuamini mchango muhimu unaotolewa na VETA. 

  Aliwaasa wakulima na wanajamii kuendelea kutumia fursa mbalimbali za mafunzo zinazotolewa na VETA ili waweze kunufaika kwa kupata ujuzi utakaoweza kuwasaidia kuongeza tija katika uzalishaji na kujipatia ajira na kuongeza vipato vyao. 
   Mkuu wa Chuo cha VETA Lindi akipeana mkono na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu baada ya VETA kuchukua kikombe cha mshindi wa kwanza wa Taasisi Mafunzo ya Ufundi Stadi katika kilele cha maonesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja Ngongo mkoani Lindi.
  Watendaji na Veta wakishangalia baada ya kupata kikombe cha mshindi wa kwanza wa Taasisi Mafunzo ya Ufundi Stadi katika kilele cha maonesho ya Kitaifa ya Nanenane katika viwanja Ngongo mkoani Lindi

  0 0

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Banda la maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Makamu wa Rais alipokelewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Rose Mdami

  Makamu wa Rais anapokea taarifa ya shughuli za Usajili ambazo zimekuwa zikifanyika katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakati wa Maonyesho ya Nanenane kwenye Viwanja vya Ngongo – Lindi.
  Makamu wa Rais akikagua Vitambulisho vinavyogawanywa kwa wananchi Wananchi wakati wa maonyesho ya Nanenane mkoani Lindi.

  Mhe. Makamu wa Rais akikagua fomu za Usajili zinavyohakikiwa kabla ya mwananchi kuchukuliwa alama za Vidole, Picha na Saini ya Kielektroniki.
  Makamu wa Rais akikagua mashine za Usajili zinazotumika kuwasajili wananchi; ikiwemo uchukuaji wa alama za kibaiolojia, Picha na Saini ya Kielektroniki
  Watumishi wa NIDA wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupata ushindi kwenye maonyesho ya Nanenane kwa mwaka 2017.

  ……………………….

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA na kufurahishwa na ufanisi mkubwa katika kuunganisha mifumo ya Serikali yenye kulenga utoaji huduma bora na kurahisisha shughuli ya Utambuzi kwa wananchi.

  Mheshimiwa Makamu wa Rais ametembelea Banda la NIDA akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha maonyesho ya sikukuu ya Wakulima Kitaifa maarufu Nanenane yaliyofanyika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Mhe. Samia aliambatana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dr. Charles Tizeba.

  Katika maonyesho hayo NIDA ni miongoni mwa Taasisi zilizofanya vizuri na kupata ushindi katika makundi 15 yaliyotangazwa.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Wizara zilizoshiriki Maonesho ya 24 ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (kulia) akipata ufafanuzi wa Utaratibu wa malipo ya kiinua mgongo, pensheni na mirathi alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Mipango Bi. Joyce Mkinga pamoja na Mkuu wa Hazina Ndogo Lindi Bi. Pili Kamali
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) anayesaini kitabu cha wageni, katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya Nanenane, Ngongo, mkoani Lindi.

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), (wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara na Taasisi zake walioshiriki Maonesho ya 24 ya Nanenane, yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Kulia kwake ni Meneja Takwimu Mkoa wa Lindi Bw. Moses Sagala, kushoto kwake ni Mkuu wa Hazina Ndogo Lindi Bi. Pili Kamali, na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  ………………………………..

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amewataka watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi na Serikali yao.


  Dkt Mpango aliyasema hayo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya maonesho Nanenane katika eneo la Ngongo mkoani Lindi.

  Alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inategemewa na wananchi wengi hivyo ni vyema wahudumiwe vizuripamoja na kutoa elimu kwa umma vya kutosha ili waweze kuelewa na kuridhika na huduma zinazotolewa na wizara.

  “Tujitahidi kuwaelezea wananchi juu ya kazi na huduma zetu ili waweze kuzitumia kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla na tuweze kufikia uchumi wa viwanda kama lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipangia ” Alisisitiza Dkt. Mpango.

  Kauli mbiu ya maonesho ya Nanenane mwaka huu ambayo ni ya 24 kufanyika kitaifa huku yakifanyika mwaka wan ne mfululizo mkoani Lindi inasema “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  Wizara ya Fedha na Mipango
  Ngongo Lindi

  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na baadhi ya Wadau wa mpira wa miguu kuhusu namna bora ya kukuza na kendeleza mchezo huo leo jijini Dar es salaam.
  Baadhi ya Viongozi Wastaafu wa mpira wa miguu nchini wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati wa majadiliano ya namna bora ya kukuza na kendeleza mchezo huo leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia ni Rais wa Heshima wa TFF na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Shrikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF).
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyekaa katikati) baada majadiliano ya namna bora ya kukuza na kendeleza mpira wa miguu leo jijini Dar es salaam.

  (Picha na Eleuteri Mangi-WHUSM)

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia mkaa ulotengenezwa kutokana na makaratasi yaliotumika wakati alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
  Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Charles Tizeba akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ubanguaji wa korosho wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya magonjwa na wadudu wanaoshambulia mikorosho na namna ya kutibu mimea kutoka kwa Mtafiti kiongozi wa Zao la Korosho wa Taasisi ya utafiti wa Kilimo Nahendele Bw.Fortunus Kapinga wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Ndendegu na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama Salma Kikwete (MB) wakiangalia ufugaji wa samaki wa kwenye matenki unaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia karoti wakati alipotembelea na kujionea shughuli za kilimo cha mboga mboga zinazofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakati wa kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha sherehe ya maadhimisho ya 24 ya sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mkoani Lindi.

  Sehemu ya wananchi waliohudhuria.

  0 0


  Shirika la Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), limezindua mfumo mpya wa Mawasiliano ambao unalenga kumrahisisha mteja kupata na kutoa taharifa.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu amesema lengo la mfumo huu ni kumuweka mteja karibu kihuduma.

  "Smartphone itamuwezesha kila mwananchi kupakua huduma hii hili aweze kupata huduma kwa kujisajili kwa kuingiza akaunti namba yake ya DAWASCO Ambapo baada ya kufuata hatua zote za kujisajiri mteja atatumiwa neno la Siri" amesema Kingu.

  Naye, Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi. 
   
  “Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.

  Amesema kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akionyesha mfumo wa Huduma Mtandaoni unavyofanya kupitia simu za mkononi
  Mkurugenzi wa Mawasiliano na Teknolojia wa DAWASCO, Kiula Kingu akifafanua jambo kwa wanahabari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa mawasiliano katika simu za mikononi inayowawezesha kupata taarifa zote muhimu za shirika hil kwenye simu. Pamoja naye ni Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro.
  Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro, akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa kuzindua huduma ya simu mtandaoni

  Waandishiwa habari waliohudhuria mkutano huo.

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akitowa shukrani zake kwa Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar kwa ushirikiano wao kuwezesha kupa umeme kwa wakati na katika kijiji cha Tunguu Uwandani Wilaya ya Kati Unguja, wakiwa katika sehemu iliowekwa Transfoma kwa ajili ya kupokea umeme katika kijiji hicho na kutowa huduma hiyo kwa wananchi zaidi ya mia moja kupata huduma hiyo. 
  Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO Hassan Ali akitowa maelezo wakati wa hafla hiyo ya kupokea shukrani zilizotoka kwa Wananchi wa Jimbo hilo na Mwakilishi wao kwa msaada wao wa usambazaji wa umeme kwa wakati na kupata fursa ya kupata hudumi hiyo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kijiji cha Tunguu Uwandani akitowa shukrani za wananchi wa kijiji hicho wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika eneo lililowekwa transfoma ya kusabaza umeme katika eneo hilo na kutowa huduma kwa wananchi zaidi ya mia moja.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kutowa shukarani kwa Shirika la Umeme Zanzibar kwa msaada wao kukamilisha zoezi hilo la usambazaji wa umeme katika Kijiji cha Tunguu Uwandani Wilaya ya Kati Unguja.hafka hiyo imefanyika katika kijiji hicho tunguu. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Ally Halil Milza akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuwataka wananchi wa kijiji hicho kuitumza miundo mbinu hiyo na kuahidi kusambaza umeme kwa wananchi wa vijiji jirani kwa kuongeza nguzo 16 zilizobakia ili kuweza kupatikana kwa huduma hiyo kwa wananchi hao. 
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Tunguu Uwandani wakiwa katika eneo la hafla hiyo wakisikiliza nasaha zilizokuwa zikitolewa na wahusika.  
  Sheha wa Shehia ya Tunguu Uwangani akisoma dua baada ya hafla hiyo kumalizika ya kutowa shukrani  
  Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Mazingira Ally Halil Mirza Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu na Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar ZECO wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kijiji hicho baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe, Simai Mohammed Said akizungumza na wananchi wa Jimbo lake baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.

  0 0


   Kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda.
  Kikosi cha Simba.


  Mashabiki wa Simba waliojitokeza kwenye Tamasha la Simba Day linalofanyika Kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam .. Klabu ya Simba yenye maskani yake Msimbazi jijini Dar es Salaam ina utaratibu wake wa kuenzi vitu vyake vya klabu kwa kuanzisha siku maalumu ambayo wanasimba wote hukusanyika pamoja kujadiliana mambo mbalimbali.Agosti 8 ya kila mwaka huwa ndiyo siku hiyo iliyopewa jina la ‘Simba Day’, wameichagua wao Wanasimba kama sehemu ya kumbukumbu ambapo huchagizwa na mambo mengi ikiwemo kutoa misaada kwa jamii inayowazunguka, kubadilishana mawazo, na mwisho huchezwa mechi ambayo ndiyo huitimisha kila kitu.
  0 0


  0 0

  Mgeni rasmi katika kilele cha Maonyesho haya alikuwa waziri wa ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za Mitaa MHE. George B. Simbachawene akimkabidhi mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah tuzo ya mshindi wa tatu sambamba na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kilolo Aloyce Kwezi.Katikati DC wa kilolo Asia Abdallah , kushoto aliyeshika hati, Mkurugenzi Halmashauri ya Kilolo Aloyce Kwezi na mwishoni kwa Mkurugenzi ni Dkt. Mwingira Afisa Mifugo mkuu Wilaya na kulia tena huku ni Afisa Kilimo mkuu Wilaya ndgu. Kuziwa..

  Na Fredy Mgunda, Mbeya

  Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani iringa imeshika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane ambao huhusisha maswala ya kilimo yaliyofanyikia jijini mbeya kwa kanda ya nyanda za juu kusini na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali kutoka mikoa yote ya nyanda za juu kusini.

  Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi ya kuwa washidi wa tatu wa maonyesho hayo ya nane nane  mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah aliwapongeza wananchi na viongozi wa wilaya hiyo kwa kufanya vizuri katika maonyesho hayo kwa kile walichokifanya na kuonyesha kuwa Kilolo Kilimo kinasaidia kuinua kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

  "Mimi niwashukuru sana kwa zawadi waliyotupa wananchi na viongozi wa Wilaya ya Kilolo maana ushindani ulikuwa mkubwa mno hasa ukiangalia wilaya zote za nyanda za juu kusini zinasifika sana kwa Kilimo cha mazao mbalimbali na ufugaji hivyo haikuwa rahisi sana kufika hapa mwaka huu"alisema Abdallah

  Abdallah alisema kuwa atakaa na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Kupanga mikakati madhubuti ili mwakani waweze kushika nafasi ya kwanza na kuwa wilaya ya mfano huku nyanda za juu kusini hata Tanzania kwa ujumla.

  "Sasa kazi imeanza na nitahakikisha kila kitu mwakani kitakuwa vizuri na tutafanya vizuri sana kwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri ya uwekezaji kwenye sekta ya Kilimo na ufugaji hivyo lazima tutatafuta njia mbada ya kuinua Kilimo cha wilaya ya Kilolo" alisema Abdallah

  Aidha Abdallah alisema mikakati yake ni kuboresha pale walipokwama ili kupata matokeo chanya katika maonyesho yajayo.

  "Mikakati iliyopo ni kwamba mwisho wa maonesho haya ndiyo mwanzo wa maonesho mengine, tumegundua vitu vilivyotufanya kuwa namba tatu ni pamoja na ubunifu, hivyo tutazidi kuwa wabunifu kwa maonesho yajayo ili tufikie ushindi mnono zaidi" alisema Abdallah

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo Aloyce Kwezi alisema kuwa halmashauri inamikakati mingi ya kuboresha maeneo ya Kilimo kuwaomba wadau mbali mbali wanaotaka kuwekeza kwenye Kilimo wafike katika ofisi halmashauri ili kujadiliana namna ya uwezaji na maeneo wanayoweza kuwekeza.

  "Halmashauri ya wilaya ya Kilolo ina maeneo mengi mazuri kwa ajili ya Kilimo ambayo bado hayafanyiwa Kilimo hivyo naomba wadau wenye nia ya kuwekeza kwenye Kilimo waje kuweza maana maeneo ni rafiki kwa Kilimo cha aina yoyote ile kutokana na hali ya hewa iliyopo huku" alisema Kwezi

  Naye afisa mifugo mkuu wa wilaya ya kilolo Dkt. Mwingira aliupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo kwa jitihada za kuinua Kilimo na ufugaji kwa wananchi wa Wilaya hiyo na ndio sababu kubwa kupata mafanikio ya kushika nafasi ya tatu katika maonyesho ya nane nane.

  "Mimi nampongeza sana Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi kwa ubunifu wao ambao umetusaidia kufika hapa hivyo naomba tuwape ushirikiano katika kukuza Kilimo cha Wilaya ya Kilolo "alisema Dr mwingira

  Katika maonyesho hayo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa George Simbachawene na huku nafasi ya kwanza ilichukuliwa na halmashauri ya Mpanda na nafasi ya pili ilishikwa na Tunduru.

  0 0


  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Prof Kitila Mkumbo akiwabebesha maji wawakilishi wa wananchi wa kijiji cha Newland mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika eneo hilo.
  Diwani wa kata ya Mabogini kilipo kijiji cha Newland ,Emanuel Mzava akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji hicho ambacho wakazi wake wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji hicho. 

  Baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika uzinduzi huo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA wakiwa katika uzinduzi huo.
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi ,(MUWSA) Joyce Msiru akitoa taarifa ya Mamlaka hiyo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji ,Prof ,Kitila Mkumbo (Hayupo pichani) alipofanya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Newland.
  Mkurugenzi MUWSA ,Joyce Msiru akikabidhi taarifa kwa katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof Kitila Mkumbo. 
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof ,Faustine Bee akizungumza kaika uzinduzi huo.
  Mjumbe wa Bodi a Wakurugenzi wa MAMLAKA YA mAJI SAFI NA uSAFI WA mazngira mjini Moshi(MUWSA) Hajira Mmambe akisalimia wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa katika kijiji cha Newland.
  Katibu tawala mkoa a Kilimanjaro na Mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi ,Aisha Amour akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa mradi huo. 
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji safi katika kijiji cha Newland kilichopo kata ya Mabogini wilaya ya Moshi. 
  Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Newland akicheza kwa furaha baada ya maji kuanza kutoka katika kijiji hicho.
  Kikundi cha Burudani cha Msanja kikitoa burudani wakati wa uzinduzi wa mradi wa majisafi katika kijiji cha Newland kilichopo kata ya Mabogini wilaya ya Moshi.

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo akitia saini katika kitabu cha wageni alipotembelea Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kwa ajili ya uzinduzi wa mradi wa Maji katika kijiji cha Newland. 
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Joyce Msiru akizungumza wakati wa utamburisho wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka hiyo kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Prof Kitila Mkumbo alipotembelea Mamlaka hiyo. 
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa MAzingira mjini Moshi (MUWSA) .
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof,Kitila Mkumbo katika eneo la Shabaha kwa ajili ya uzinduzi wa tanki la Maji linalohifadhi maji kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.
  Tenki la kuhifadhia Maji kwa ajili ya Mradi wa Maji yanayosambazwa katika kijiji cha Newland.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Utalii,Prof Kitila Mkumbo akizindua tenki la Maji katika eneo la Shabaha kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Newland.kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakuruenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi,(MUWSA) Prof Faustine Bee na kushoto mwa katbu Mkuu ni Mjumbe wa Bodi hiyo ,Bi Hajira Mmambe.
  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  Wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakitoa elimu jinsi ya kutumia mfumo wa Government electronic Payment Gateway kwa watendaji wa Halmashauri ya Kinondoni. Watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Kinondoni wakipewa mafunzo jinsi mfumo mpya wa ukusanyaji maduhuli ya Serikali utakavyokuwa unatumika. Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ikitolewa kwa watendaji wa manipaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

  …………………….  Na ELIAFILE SOLLA

  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini.

  Mfumo huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya ardhi. Pia mfumo wa GePG, utamuwezesha mwananchi au mmiliki wa kipande cha ardhi, kujua anadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.

  Majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, baada ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.

  Mwananchi yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kuwa na hati, ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi pia.

  Kwa zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama vile upekuzi katika daftari la msajili (official serach), mwananchi atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.

  Kwa sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni kuongeza ufanisi katilka ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini,

older | 1 | .... | 1331 | 1332 | (Page 1333) | 1334 | 1335 | .... | 1897 | newer