Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1330 | 1331 | (Page 1332) | 1333 | 1334 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Pichani ni eneo la stendi mpya na ya kisasa ya mabasi mjini Korogowe Mkoani Tanga, iliyozinduliwa rasmi na Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo. PICHA NA IKULU
  Sehemu ya Wananchi wa Korogwe wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye eneo la stendi hiyo, kumsikiliza Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kabla ya kuizindua rasmi leo.
  RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUNGUA STENDI YA MABASI YA KOROGWE MJINI MKOANI TANGA

  0 0


  Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.(Picha na Pamela Mollel)
  Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na wananchi hili katika maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.
  Wananchi wakiwa wanaangalia bwawa la samaki katika banda la halmashauri ya mji wa Babati katika maonyesho ya nane nane

  WATANZANIA wameshauriwa kutumia teknolojia za kisasa katika kada za kilimo,mifugo na uvuvi ili kujipatia ajira na kipato na hatimaye kukuza lengo la uchumi wa viwanda.

  Ushauri huo ulitolewa jana jijini Arusha na Mkuu wa Idara ya Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati Bw,Daniel Luther wakati akiongea na gazeti hili kwenye maonesho ya kilimo na mifugo Nane nane yenye kauli mbiu Zalisha kwa tija,mazao na bidhaa za kilimo,mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati ambapo kwa kanda ya Kaskazini yanafanyika mkoani Arusha.

  Luther alisema kuwa endapo watanzania wataamua kuwekeza nguvu zao katika teknolojia hizo ikiwemo ufugaji wa samaki wataweza kujiingizia kipato katika ngazi ya kaya kupitia samaki watakazozalisha.

  "Ufugaji wa samaki kisasa si lazima uwe na eneo kubwa hata eneo dogo nyumbani kwako unaweza ukafuga ama hata katika simtank,madyaba ama pipa ili mradi eneo hilo liwe na hewa pamoja na usafi wa mazingira ya maji ya kuhifadhia samaki wako.

  "Mradi huu unawezesha ajira na thamani ya utengenezaji wake ni ndogo sana ukizingatia na faida utakayoipata baadae hivyo vijana wachangamkie hii fursa kuliko kusubiri ajira serikalini"alisema Luther.

  Aidha aliwataka watanzania kuwekeza katika kilimo cha mazao yenye thamani ikiwemo kilimo cha uyoga, mbogamboga za majani,matunda na mizizi kwa kusindika mazao hayo ili kuendeleza soko lake na kujipatia kipato.

  imu wa mavuno mazao yanakuwa mengi na mengine yanaweza kuharibika lakini yakiweza kuongezewa thamani kwa kukaushwa hasa mbogamboga tunaweza kuendelea kuwa na soko hili na kujiongezea kipato.

  "Mfano zao la uyoga linaweza kuendelea kupatikana katika soko kwakuwa umekaushwa tofauti na ukiwa mbichi kwani huaribika kwa haraka

  0 0

  Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. 
  Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017. Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017. Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) akimshukuru Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya michezo leo jijini Dar es Salaam vilivyotolewa na NMB kuwezesha timu ya JWTZ kushiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017. Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.

    BENKI ya NMB leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) inayotarajia kushiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki itakayofanyika jijini Bujumbura - Burundi. Vifaa vilivyokabidhiwa leo ni pamoja na mipira kwaajili ya timu ya mpira wa miguu, mipira ya mchezo wa mikono (wasichana) na mipira mchezo wa kikapu kwa wanaume (Basket ball).

   Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ - Kanali Richard Mwandike, Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa alisema vifaa vingine ni pamoja na mipira 10 ya mchezo wa volebo (Volleyball), jezi 42 za mpira wa miguu, seti mbili za jezi mpira wa kikapu (wasichana), seti mbili za jezi mpira wa basket na seti mbili za jezi mpira wa Volleyball.

   Vifaa vingine vilivyokabidhiwa ni pamoja na seti mbili za jezi za waamuzi kwa michezo ya Netball, Basketball, Volleyball na mabegi 30 ya wachezaji ambapo vyote kwa ujumla vina thamani ya shilingi milioni 10 za Kitanzania. Bw. Raballa alisema kuwa msaada huo umetokana na ushirikiano mzuri na wa muda mrefu kati ya benki ya NMB na jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na ndiyo maana wakaona umuhimu wa kuendelea kuwashika Mkono kupitia msaada kwa timu za jeshi zinazoenda kushiriki mashindano ya majeshi ya jumuia ya afrika ya mashariki. 

   "...Hii si mara ya kwanza kusaidia katika mashindano haya, kwani nakumbuka hata mwaka jana tuliwasaidia baadhi ya vifaa vya michezo kushiriki katika mashindano haya. Tunaamini vifaa hivi mbali na kuendeleza ushirikiano wetu mzuri, vitakuwa chachu ya kufanya vizuri katika mashindano haya muhimu kwa jumuia ya Afrika ya Mashariki," alisema Raballa. 

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ - Kanali Richard Mwandike akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya JWTZ alisema anaishukuru NMB kwa msaada wa vifaa hivyo na kuongeza kuwa msaada huo umewapa morali ya kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano hayo. Kanali Mwandike aliongeza kuwa timu hiyo itatumia jezi na vifaa vingine walivyo kabidhiwa kwenye mashindano hayo huku wakiahidi kuwa mabalozi wazuri wa NMB nan chi kwa ujumla. Kwa Mwaka wa 6 mfululizo, NMB imekuwa ikisaidia timu za Majeshi wanapoenda kuwakilisha nchi kupitia michezo mbalimbali na katika mashindano mbalimbali.   Meneja Mahusiano Kitengo cha Mikopo NMB, Emmanuel Mahodanga (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) katika hafla hiyo. Kaimu Afisa Mkuu wa Wateja wadogo na Wakati wa NMB - Boma Raballa (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali vya michezo Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) - Kanali Richard Mwandike (kulia) leo jijini Dar es Salaam. Vifaa hivyo mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi, mipira na vifaa vingine vyenye thamani ya shilingi milioni 10, vitatumiwa na wachezaji wa timu ya JWTZ wanaotarajia kusjiriki Mashindano ya Kijeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotarajia kuanza Agosti 24, 2017.

  0 0

   Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa umma kutoka mikoa ya Songwe, Iringa, Njombe na Mbeya alipokuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Kisekta  (PlanRep)  leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa hiyo
   Kiongozi wa wawezeshaji Bw. Frank Makua Charles akichokoza mada wakati wa semina katika akichokoza mada wakati siku ya kwanza ya semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hii ya siku nane inaendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID)ambapo imeshirikisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
   Mwakilishi wa Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Makao Makuu Dar es Salaam Dkt. Gemini Mtei akielezea jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
  Mwakilishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Bw. James Mtatifikolo akifafanua jambo wakati wa  hafla ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
   Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja akiagana na Meneja Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Mkoa wa Mbeya Bw. Gasper Materu mara baada ya ufunguzi wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inahusisha watumishi wa umma kutoka kada za Maafisa Mipango, Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu kutoka Halmashauri na Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.Katikati ni Mwakilishi wa Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) Dar es Salaam Dkt. Gemini Mtei.
   Baadhi ya washiriki wa semina ya siku nane kuhusu Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia mada wakati wa ufunguzi wa semina hiyo leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inayoendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya  Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID). Semina hii imewahusisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama,  Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
   Mmoja ya wawasilisha mada kutoka OR – TAMISEMI Bw. Jeremia Mtawa akiwasilisha mada kuhusu namna mfumo wa PlanRep utakavysaidia katika kuimarisha utendaji wa Halmashauri nchini wakati wa semina semina ya siku nane kuhusu Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma katika upangaji  mipango na bajeti (PlanRep) leo Jijini Mbeya. Semina hii ya siku nane inaendeshwa kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inashirikisha watumishi kutoka kada za Maafisa Mipango, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu katika ngazi za Mikoa na Halmashauri za mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Songwe.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bi. Mariam A. Mtunguja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki washiriki wa semina ya siku nane juu ya Mfumo mpya wa  kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (PlanRep) mara baada ya kufungua semina hiyo leo Jijini Mbeya. Semina hiyo inaendeshwa Kupitia Programu ya Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Marekani (USAID) ambapo inahusisha watumishi wa umma kutoka kada za Maafisa Mipango,Wachumi, Makatibu wa Afya, Wahasibu, Maafisa Tehama, Waganga Wakuu kutoka Halmashauri na Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.

   
  Picha zote na: Idara ya Habari – MAELEZO, Mbeya.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, amewaagiza Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma na Manyara kuhakikisha wanatafuta eneo la kujenga kituo cha mizani ili kudhibiti madereva wanaozidisha uzito katika barabara ya Dodoma- Babati (km 263), inayojengwa kwa kiwango cha lami.
  Akizungumza katika eneo la Bonga, mkoani Manyara Eng. Nyamhanga, amesema kuwa barabara hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika baadae mwezi huu inahitaji uwepo wa mizani kwa haraka ili kudhibiti  magari yanayozidisha uzito na kuharibu barabara. 

  "Hakikisheni mnatafuta eneo la kujenga mizani ndani ya miezi miwilli ambapo wakandarasi bado wapo hapa ili iwe rahisi kwenu kumtumia mmoja wa wakandarasi hawa kuweza kujenga kituo hiki haraka, uwepo wa mizani hii utasaidia kudhibiti magari makubwa yanayozidisha uzito", amesema Katibu Mkuu Nyamhanga.
  Aidha, Eng. Nyamhanga amewaagiza mameneja wote nchini kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote wanaopitisha mifugo katika barabara ili kudhibiti uharibifu wa barabara.

  Amewataka  madereva wote nchini kuendesha magari yao kwa tahadhari na kuzingatia alama za barabarani ili kudhibiti ajali zinazoepukika.
  Katibu Mkuu Nyamhanga ametoa wito kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hiyo kuhakikisha wanatumia fursa ya kukamilika kwa barabara hiyo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika maeneo yao ili kukuza uchumi kwa familia zao na Taifa kwa ujumla.
  Amemataka  mkandarasi wa sehemu ya barabara ya Mela - Bonga (km88.8)  kuhakikisha anakamilisha kazi zilizobaki kwa wakati na kwa viwango vilivyo kwenye mkataba.
  Katika hatua nyingine, Eng.Nyamhanga, ametembelea na kukagua barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35) kwa kiwango cha lami na daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 na kuridhishwa na ujenzi wake na kumtaka mkandarasi wa mradi huo kukabidhi mradi huo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.
  Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri wa barabara ya Mayamaya- Mela (km 99.35), Leornado Licari,  amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kumaliza mradi huo kwa wakati kwani kazi  zilizobaki kwa sasa ni ndogo kama kumaliza tabaka la mwisho la lami na uwekaji wa alama za barabarani.
  Barabara ya Dodoma- Babati (km 263) ni sehemu ya barabara kuu ya kaskazini (Great North road), inayoanzia Capetown nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri ambapo hapa nchini barabara hiyo inayopitia Tunduma mkoani Mbeya, hadi Namanga mkoani Arusha ina urefu wa kilomita 1500,hivyo kukamilika kwa sehemu ya barabara ya Dodoma – Babati (km 263), kunaiunganisha barabara yote kutoka Capetown hadi Cairo yenye  urefu wa kilomita 100000 kwa kiwango cha lami.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
   Mhandisi Mshauri wa barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), Eng. Leornado Licari, akitoa maelezo ya mradi wa barabara hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wapili kushoto), alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa kampuni ya CHICO anayejenga sehemu ya barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), alipofanya ukaguzi mkoani Dodoma.
   Muonekano wa sehemu ya juu ya daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akikagua kingo za daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 linalounganisha wilaya ya Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (wapili kushoto), akiwa na wataalamu wanaosimamia ujenzi wa barabara ya Mayamaya – Mela (km 99.35), inayojengwa kwa kiwango cha lami mara baada ya kuikagua mkoani Dodoma. Wanne kushoto ni Mkurugenzi wa barabara Eng. Ven Ndyamukama.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akikagua sehemu ya barabara ya Mela – Bonga (km 88.8), inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Manyara.

   Ujenzi wa barabara ya Dodoma – Babati kwa kiwango cha lami sehemu ya Mela – Bonga (km 88.8), ukiendelea.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Manyara, Eng. Bashiri Rwesingisa (kulia), na mkandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group Co. Ltd anayejenga sehemu ya Mela – Bonga (km 88.8), mkoani Dodoma.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


  0 0

   Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi  akizungumza leo na wananchi wa mtaa Lungule juu ya kudhibiti matapeli wa ardhi, na migogoro mbalimbali ya ardhi hapa nchini.
  Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akizungumza mbele ya Wananchi leo katika hafla ya kukabidhi hati 88  kwa wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wananchi mtaa Lungule waliokabidhiwa hati wakiwa katika picha ya pamoja.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Na Jonas Kamaleki-MAELEZO

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amekabidhi hatimiliki 88 kwa wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam kati ya 4333 ambazo ziko kwenye hatua za mwisho katika mradi wa urasimishaji wa makazi holela.

  Akikabidhi hatimiliki hizo, Mhe. Lukuvi amesema hizi hati ni mtaji uliofufuliwa baada ya wakazi kukakaa na kuendeleza maeneo yasiyopimwa yaani mtaji mfu kwani hakuna mtu yeyote ambaye angewezakupata mkopo bila hati.

  Mhe. Lukuvi amesema kuwa Serikali ya Aawamu ya Tano inayo dhamira ya dhati ya kurasimisha makazi nchi nzima ili kuongeza thamani ya ardhi au maeneo husika. Ardhi yenye hatimiliki thamani yake inaongezeka kwani inatambuliwa na taasisi za fedha ambazo ni rahisi kukuopesha wenye hati.

  “Kwa hati hizi zilizotolewa takribani 4333 tukisema kila nyumba ikopeshwe kwa kiwango cha chini cha shilingi milioni 10, kwa siku ya leo Kimara inapata mtaji wa karibu bilioni 40.5,”alisema Mhe. Lukuvi.

  Aliongeza kuwa maeneo yote ya miji ambayo hayajapimwa, yapimwe na halmashauri na manispaa zote nchini ili kuyaongezea thamani na kuondokana adha ya watu kujenga kwenye makazi holela.

  Waziri huyo wa Ardhi amesema kuwa kwa sasa wakazi wa Kimara wameondoka kwenye kuitwa watu wanaokaa kwenye makazi holela na sasa wanajulikana kuwa wakazi wa maeneo rasmi.

  Aidha, Mhe. Lukuvi ametoa onyo kali kwa matepeli wa ardhi kuacha vitendo hivyo mara moja kwani dawa yao ipo tayari. Ameongeza kuwa na madalali uchwara wa ardhi waache tabia ya kuwaonea wanyonge na kusababisha mali zao ziuzwe kwa njia ya udanganyifu.

  “Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya matapeli hao ambao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya maafisa wasiowaaminifu,”alisisitiza Lukuvi.

  Amewaonya wanaotunza mapori mijini kuwa wakae makini kwani watanyang’anywa wasipoendeleza maeneo hayo. Ameongeza kuwa na wale waliokuwa wanamiliki maeneo makubwa bila kuwa na hati itabidi waanze kulipa kodi ya pango la ardhi ili Serikali ipate mapato.

  Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amempongeza Mhe. Lukuvi kuwa ni mtu anayejali maendeleo ya wananchi bila kujali vyama vyao wala itikadi zao. Amesema Lukuvi anafuata nyayo za Mhe. Rais John Pombe Magufuli ambaye anafanya maendeleo kwa watanzania wote bila kujali vyama vyao.

  Hivyo, amewataka wanasiasa wengine waige mfano wa Mhe. Rais Magufuli na William Lukuvi ili kuwaletea wananchi maendeleo pasipokuangalia vyama wala dini.

  Naye mkazi wa Kilungule, Kimara ambaye amekadhiwa hati na Mhe. Lukuvi, Bwana Prackson Lugazia amesema hatua hii ya kupata hati ni jambo zuri na la kimaendeleo kwani ataweza kupata mikopo kwenye taasisi za fedha kwa kutumia hati hiyo.

  “Nimefurahi sana kupata hati hii kwani kwa sasa ardhi yangu imeongezeka thamani kuliko ilivyokuwa awali,” alisema Lugazia.

  Hati hizo zimetolewa kwenye mpango wa Urasmishaji wa Makazi Holela katika kata za Saranga na Kimara, jijini Dar es Salaam. Mpango huu umesimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na ni mpango darasa ambao unaweka msingi kwa ajili ya urasimishaji wa makazi nchi nzima.

  0 0


  Na Bushiri Matenda Na Agness Moshi - MAELEZO

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imetoa rai kwa wadau wa Takwimu Nchini kufuata kanuni na taratibu za utoaji takwimu ili kuepusha sintofahamu baina yao, wapokeaji taarifa na Taasisi husika .

  Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo kufuatia taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Kampuni ya Utafiti ya Geopoll yenye ofisi ya Kanda ya Afrika, mjini Nairobi, Kenya kuhusiana Viwango na Idadi ya watazamaji wa vituo mbali mbali vya habari vinavyorushwa hapa nchini .

  “Taarifa zozote zinazohusu utafiti ni lazima zihusishe wadau mbalimbali, na kwa kuzingatia vigezo vyote vinavyotakiwa na mamlaka iliyoidhinishwa kisheria kuhusiana na utoaji takwimu”, Dkt.Chuwa alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na uwazi na ukweli, uhusishwaji wa Wadau na kwa kuzingatia weledi.

  Aidha, amefafanua kuwa ni vyema Taasisi yoyote inayotaka kukusanya taarifa mbalimbali za takwimu ni budi kushirikisha wahusika ili kuepusha mkanganyiko na upotoshwaji kama ilivyofanywa na Kampuni hiyo kutoka Nairobi, Kenya.

  “Takwimu zinazotolewa bila kuzingatia taratibu zinazohitajika hazitatambulika na Serikali kwani utoaji wa Takwimu haufanywi kama unavyohesabu migomba shambani, hivyo ni lazima wahusika wafuate taratibu zote”, alifafanua Dkt.Chuwa.

  Dkt.Chuwa amesema, Serikali haitambui Takwimu zilizotolewa hivi karibuni kupitia mitandao ya kijamii kwani hazikufuata Sheria ya Takwimu na hazijakidhi vigezo rasmi vya Takwimu na hivyo kuathiri mahusiano ya kiutendaji baina ya vyombo vya habari hapa nchini.

  Kufuatia tukio hili, Ofisi ya Takwimu nchini inapenda kuzijulisha Taasisi zinazojihusisha na utoaji wa taarifa zinazotokana na utafiti nchini kwamba kwa mujibu wa Sheria ya 2015 NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya matumizi ya Serikali na Wadau wa Takwimu.

  Amesema, kwa mujibu wa Kifungu cha 6 cha Sheria hiyo, kinaipa NBS jukumu la kutoa na kusimamia miongozo na viwango vya utoaji rasmi wa Takwimu. “Hapo awali Ofisi ya Taifa ya Takwimu haikua na meno lakini mara baada ya marekebisho ya Sheria hiyo, sasa inayo meno ya kuiwezesha kudhibiti utoaji holea wa Takwimu nchini” Amesisitiza Dkt. Chuwa.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa amewataka Waandishi wa Habari kuacha kuandika taarifa ambazo hazijathibitishwa na NBS, pia ambazo hazina mashiko kwa Wananchi na Serikali kwa ujumla.

  “Vyombo vya habari nchini viache kushabikia taarifa zinazotolewa na Taasisi zozote zisizo tambulika na kuthibitishwa na NBS hususani katika maswala ya Takwimu”, alisisitiza Bi. Zamaradi.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa Takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya Serikali na Wadau wa Takwimu.
  Mkurugenzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Habari maelezo Jijini Dar es Salaam , kushoto Bw. Ephraim Kwisigabo Mkurugenzi Sensa na Takwimu za jamii.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bunju wakati akirejea jioni ya leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoa wa Tanga. 
   Baadhi ya wananchi wa eneo la Bunju wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza aliposimama eneo hilo kwa ajili ya kuwasalimia wakati akirejea jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tano katika mkoani  Tanga. PICHA NA IKULU

  0 0

  Mshindi wa Tuzo ya International Confederation of Midwives (ICM), Loveluck Mwasha akiwasilisha mada kwenye kongamano la kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani lililofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo. Maadhimisho hayo yalianza wiki iliyopita kwa kupima afya watu mbalimbali waliojitokeza katika hospitali hiyo. Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa Mei 5, kila mwaka, lakini TAMA tawi la Muhimbili iliamua kuadhimisha siku hii katika wiki ya unyonyeshaji duniani.
  Baadhi ya Wakunga na maofisa wengine wakifuatilia kongamano hilo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  0 0  0 0

   Afisa Rasilimali watu wa Kurugenzi ya Rasilimali Watu na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Peter Valerian akiwapa maelezo wananchi waliotembelea Banda la BoT  katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Afisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Tawi la Mtwara, Denis Malosha akitoa maelezo ya utoafautishaji Noti bandia na Noti halali  kwa wananchi waliotembelea banda la BoT katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Afisa wa BoT, akionesha noti chakavu ambazo wananchi hawapo (pichani) wamezipeleka katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Wananchi wakipata maelezo katika maeneo tofauti ndani ya banda la BoT katika  maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Afisa Uhusiano wa Tazara, Regina Tarimo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea Banda la Tazara katika maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Meneja wa Kitengo cha Hali ya Hewa Kilimo wa TMAA , Isack Yona akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la mamlaka ya hali hewa nchini TMAA, katika  maonesho ya Nanenane kwenye  viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

  0 0

  Spika Mstaafu Anna Makinda ameipongeza DCB Commercial Bank kwa huduma bora za kibenki inayotoa hasa huduma za mikopo kwa wajasirimali wadogo wadogo na kuwakwamua katika hali ya umasikini.

  Makinda amewaasa DCB Commercial Bank kujikita zaidi kutoa huduma hii kwa  wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambao ndiyo wengi nchini ili kuboresha hali za maisha yao kwa kuwapatia mikopo.

  Hayo aliyasema wakati alipotembelea banda la DCB Commercial bank katika maonesho ya nane nane kanda ya kati yanayoendelea mkoani Dodoma. Makinda aliongezea kuwa ili kuwezesha wajasiriamali wengi DCB Benki haina budi kupeleka huduma hii ya mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii ya mikopo ya vikundi Sambamba na utoaji wa mikopo hii ya vikundi kwa wajasiriamali wadogo wadogo.

  Makinda ameasa DCB kuwaunganisha wajasiriamali hawa na huduma ya bima ya afya kutoka NHIF na pia bima ya taifa ya Jamii ili wateja hawa au familia zao wanapougua wapate msaada wa matibabu kwa unafuu hivyo kuwafanya wawe na afya na kuweza kurejesha mikopo .

  Alisisituza kuwa mteja akiugua ile pesa ya marejesho ataitumia katika kugharamia matibabu hivyo kuitia hasara benki, kumbe akijiunga na mifuko ya afya ya jamii atapata matibabu bure hivyo benki haitaathirika. Alisema makinda.

  Akimkaribisha kwenye banda na kuelezea huduma zinazotolewa na DCB Commecral Bank, Meneja masoko wa DCB benki Boyd Mwaisame alitaja huduma za DCB zinazopatikana katika banda la benki hiyo viwanja vya maonesho nane nane Mzuguni Dodoma kuwa ni pamoja na kufungua akaunti za kuweka akiba kwa watu binafsi, akaunti za wanafunzi, akaunti za muda maalumu, akaunti za biashara  na huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa.

  Mteja akisha fungua akaunti ya akiba na biashara anunganishwa bure na huduma ya DCB Pesa, huduma mpya ya kufanya miamala ya benki kupitia simu ya mkononi, yaani kuweka na kutoa pesa na kulipia bili mbalimbali. Huduma hii si lazima mteja awe na akunti DCB, bali mtu yeyote mtaani anaweza kujiunga mradi tu awe na namba yoyote ya simu ya mkononi iliyosajiliwa na mojawapo ya kitambulisha cha mpiga kura, utaifa, udereva na paspoti.

  Huduma hii inapatikana kwa kupiga *150*85#.  Pia Meneja masoko alimueleza Mh. Makinda kuwa huduma za DCB Commercial Bank mbali na Dar es Salaam kwa sasa pia zinapatikana mkoani Dodoma kupitia tawi lake  lilifunguliwa hivi karibuni katika jengo la LAPF mtaa wa Makole na mikoa mbali mbali kupitia huduma ya uwakala wa benki yaani DCB Jirani.

  Naye afisa wa benki Cecilia Msikula akimuelezea Mh. Makinda huduma ya akiba ya watoto akaunti za watoto –Young saver account ambayo alivutiwa sana nayo hasa Meli ya mtoto, alisema kuwa DCB inatoa huduma hii bila makato ya mwezi ambapo mteja akisha fungua akaunti ya mtoto kwa shi. 5,000 tu anapewa Meli ya Mtoto/ kibubu  bure kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba akiwa bado mdogo kwa ajili ya matumizi yake ya baadaye. Pesa ikisha jaa kwenye Meli ya mtoto yaani kibubu mzazi analeta benki kwa ajili ya kuziweka kwenye akaunti ya mtoto baada ya kuzihesabu.

  Katika msafara huo, Spika mstaafu Makinda aliongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Mh. Jabir Shekimweri.
  Spika Mstaafu Anna Makinda akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma.
  Spika Mstaafu Anna Makinda akisoma moja ya kipeperushi cha benki ya DCB
   katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame

  Wananchi wakipatiwa huduma katika banda la benki ya DCB katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani Dodoma.

  0 0

   Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruyaya kilichopo Kata ya Lihmalyao wilayani Kilwa Mkoa wa Lindi, Hassan Amanzi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kilimo kwa wakulima wa Kijiji hicho yaliyofanyika wilayani humo jana. Wengine ni viongozi na wajumbe wa kijiji hicho. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

  Wazee na vijana wakiwa kwenye mafunzo hayo. 


   Mkulima Athuman Hassan akizungumzia kukosekana kwa dawa ya salfa ya kuua wadudu kwenye mikorosho.
   Mkulima Mohamed Sadiki akichangia jambo kuhusu zao la mhogo.
   Selemani Mbanga, akizungumzia jinsi wanyama waharibifu tembo na nguruwe wanavyo haribu mazao yao.
   Mkulima Mohamed Dege akielezea ugonjwa unaofanana na Ukimwi unavyoshambulia mihogo yao.
   Wakina mama wa kijiji hicho wakiwa kwenye mafunzo hayo.
   Mwezesha wa mafunzo hayo kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Hamalord Mneney, akitoa mafunzo ya kilimo cha kisayansi na Bioteknolojia kwa wakulima hao.
   Wakulima wakiwa kwenye moja ya shamba la mihogo katika kijiji hicho kwa mafunzo.
   Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia, OFAB, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Morogoro, SUA, Philbert Nyinondi akiangalia mhogo katika moja ya mashamba ya kijiji hicho wakati akipatiwa maelezo ya ugonjwa unaoshambulia mihogo kutoka kwa mkulima, Mohamed Maundu.
  Majadiliano yakiendelea katika shama hilo.

  Na Dotto Mwaibale, Kilwa-Lindi

  WAKULIMA  wa mihogo katika Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wamefananisha ugonjwa unaoshambulia mihogo yao kuwa kama  ukimwi uliokosa dawa kutokana na mihogo kuooza na kunyauka majani yake ambapo wameomba wataalamu wa kilimo na serikali kuwasaidia ili waondokane na changamoto hiyo.

  Hayo yamebainika katika ziara ya watafiti wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ya kutoa mafunzo ya kilimo bora cha mihogo kwa wakulima wa Kijiji cha Ruyaya kilichopo Kata ya Lihmalyao wilayani Kilwa mkoani Lindi jana.

  Akizungumza katika mafunzo hayo mkulima Mohamed Rashid Dege alisema changamoto kubwa waliyonayo ni ugonjwa wa ukimwi wa mihogo ambao unawasumbua kwa muda mrefu ambao unashambulia mihogo yao na hauna dawa.

  "Ugonjwa huu wa ukimwi wa mihogo unaifanya mihogo kuliwa au kuoza na majani yake kukauka hatujui ni ugonjwa gani ni ugonjwa ambao unatusumbua sana tunaomba wataalamu na serikali watusaidi kutuondolea  kero hii" alisema Dege.

  Mkulima Athuman Mwamba alisema changamoto nyingine waliyonayo ni kukosekana kwa mbegu bora zilizozalishwa kitaalamu hivyo waliwaomba watafiti kuwapelekea mbegu bora.

  Selemani Mbanga ambaye ni mkulima wa kijiji hicho alisema changamoto nyingine waliyo nayo ni kukosekana kwa soko la uhakiki la kuuza mihogo yao na wanyama waharibifu kama tembo na nguruwe kushambulia mihogo yao.

  Mkulima Hamisi Mohamed alisisitiza kukosekana kwa soko la mihogo na barabara ya ambayo haipitiki vizuri wakati wa mvua.

  Athumani Hassan alililamikia changamoto ya kutopatika dawa ya salfa kwa ajili ya kupulizia mikorosho ambayo katika msimu huu wa kilimo hawajapata ya kutosha  na kusabibisha mashamba ya mikorosho kushambuliwa na wadudu.

  Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Kilimo ya Halmshauri ya Wilaya ya Kilwa, Manyusi  Ngilangwa alisema dawa ya salfa kwa ajili ya kupulizia mihogo ya wakulima hao haikuweza kutosheleza kwa sababu ya kukosekana kwa idadi halisi ya wakulima kutokana na kuuza korosho zao maeneo ya mbali ya kijiji hicho.

  "Dawa ya salfa imetolewa kidogo kwa kuwa hakukuwa na taarifa ya idadi ya wakulima ambayo hupatikana wakati wakiuza korosho zao kwa walanguzi bila ya kutumia ghala lao ambalo lipo kijijini hapo jambo lililosabisha kuto kuwa na idadi kamili ya wakulima" alisema Ngilangwa.

  Alisema wakulima wanapotumia kuuza korosho zao katika ghala hilo inakuwa rahisi kupata idadi yao hivyo kuletewa pembejeo zao kwa urahisi.

  Mwezesha wa mafunzo hayo kutoka Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Hamalord Mneney aliwaambia wakulima hao ugonjwa wa mihogo wanaoufananisha na ukimwi kuwa ni ugonjwa batoto na michirizi ya kahawia ambapo aliwata wakulima hao kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo na kutumia mbegu bora zenye zisizo na magonjwa.

  Dk. Mneney aliwaambia wakulima hao kuwa waongeze bidii katika kilimo chao na kuwa waondoe dhana ya kudai soko la mihogo halipo ambapo aliwahakikishia kuwa soko lipo iwapo watalima na kuvuna mihogo isiyo na magonjwa.

  Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hassan Amanzi aliishukuru COSTECH kwa kuwapelekea mafunzo hayo ambayo yameongeza mori kwa wakulima hao.

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Lindi.

  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo ameiomba Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kubuni mpango maalum wa mafunzo ya ufundi stadi kwa vijana wanaoingia katika mafunzo ya JKT ili wakitoka katika makambi waweze kupata fursa za ajira katika maeneo mbalimbali.

  Meja Isamuhyo alitoa ombi hilo Jumatatu, Agosti 7, 2017 alipotembelea kwenye banda la VETA, katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Ngongo, mkoani Lindi.

  Alisema vijana wanapoingia katika makambi ya JKT hupata mafunzo ya uzalendo na ukakamavu kwa kipindi cha takribani miezi mitatu na kisha kuingia katika  mafunzo ya stadi za maisha na stadi za kazi kwa kipindi kipatacho miezi 18.

  Alifafanua kutokana na mgawanyiko huo wa mafunzo ya JKT, VETA kwa kushirikiana na jeshi hilo wanaweza kuweka mpango maalum wa kutumia kipindi cha miezi 18 ya mafunzo ya stadi za kazi na stadi za maisha kuandaa mafunzo ya ufundi stadi ili kuwapatia vijana ujuzi utakaowawezesha kuajirika baada ya kuhitimu JKT.

  Alisema JKT wamekuwa wakitoa mafunzo ya ufundi stadi mbalimbali, lakini changamoto imekuwa ni kukidhi vigezo vya kutunuku vyeti vinavyotambulika na VETA, kwani kipindi cha miezi minane ni kifupi katika kukidhi matakwa ya mitaala ya VETA.

  Alisema kutokana na vijana hao kushindwa kupata vyeti vinavyotambulika na VETA ambayo ni mamlaka ya kitaifa inayodhibiti na kusimamia mafunzo ya ufundi stadi, inakuwa vigumu kwao kukubalika katika ajira au kujiendeleza katika maeneo mbalimbali ya stadi walizozipata.

  Alishauri kuwa, kama mazungumzo na mipango mizuri itawekwa na VETA kwa ushirikiano na JKT, kipindi hicho cha miezi 18 ya mafunzo ya JKT kinaweza kupangwa vyema katika namna ambayo vijana watatimiza masaa yanayohitajika kufuzu mafunzo ya ufundi stadi katika ngazi husika, hivyo kutunukiwa vyeti vinavyotambulika na VETA.

  Akijibu juu ya suala hilo, Meneja Uhusiano wa VETA, Sitta Peter alimshukuru Mkuu wa JKT huyo kwa ushauri na mawazo mazuri na kuahidi kuyafikisha katika Menejimenti ya VETA kwa majadiliano na utekelezaji.

  Alikiri kuwa ni kweli kundi hilo la vijana wanaoingia katika mafunzo ya JKT ni nguvukazi muhimu ikiwa wataandaliwa vyema katika mafunzo ya ufundi stadi baada ya mafunzo ya ukakamavu na uzalendo yanayotolewa na JKT.
   Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata maelezo kutoka  Mtaalam wa Kutathimini mafunzo  wa VETA  Joyce Mwinuka  juu ya VETA inavyofanya kazi katika kuwajenga vijana katika mafunzo ya elimu ya ufundi stadi katika maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata maelezo kutoka kwa Meneja uhusiano wa VETA, Sitta Peter wakati mkuu wa JKT alipotembelea maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Michael Isamuhyo akipata maelezo wa tofari ambazo zinaokoa gharama kutokana mazingira ambayo kila mwananchi anaweza kumudu wakati mkuu wa JKT alipotembelea maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
   Shamba darasa la JKT ndani maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.


  0 0

  Na Mathias Canal, Lindi

  Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ambayo yalianza tokea tarehe 1/8/2017 katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi yanaendela kushika kasi huku kivutio kikubwa ikiwa ni baaada ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa kwenye mabanda na Halmashauri mbalimbali kutoka mikoa yote miwili inayounda kanda ya kusini ambayo ni Lindi na Mtwara.

  Kwa ujumla wake maonyesho ni mazuri kwani yamehusisha shughuli nyingi za Kilimo, Uvuvi na mifugo kama kauli mbiu inavyosema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” kauli mbiu hii ikiwa na msisitizo na hamasa zaidi kwa wananchi kutambua mbinu bora za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kuwa na kipato kikubwa kitakachopelekea wananchi kwa ujumla wao kufikia uchumi wa kati.

  Pia kumekua na wajasiriamali wengi sana ambao wamefika katika Maonesho hayo wakiwa na bidhaa mbalimali zikiwemo bidhaa za ngozi, mikoba, viungo, asali, vyakula vya asili, mashine Ndogondogo na vingine vingi vya kuvutia.

  Maonyesho ya mwaka huu yamekua chachu na kuwa na mvuto mkubwa kwani tangu kufunguliwa kwake kumekuwa na mgeni rasmi anayetembelea kila siku ambao ni mwaaziri, ama wakuu wa mikoa kutoka katika mikoa husika jambo ambalo limefanya maandalizi kuwa makubwa na mazuri zaidi.

  Kanda ya kusini ina fursa nyingi za kiuchumi kama vile Hali ya hewa nzuri, na Uzalishaji mazao mbalimbali hususani zao kubwa la Korosho, Jambo la msingi ni kujipanga vizuri  na kuhakikisha tunatumia fursa hizi  kikamilifu ili kupunguza umasikini na kuleta utajirisho.

  Katika hotuba nyingi zinazotolewa na wageni mbalimbali wanaozuru katika Maonesho hayo ni kuhusu Tatizo kubwa linalokabili sekta ya kilimo na ufugaji nchini kwa wahusika kutozingatia kanuni bora na za kisasa za kilimo na Ufugaji.

  Hivyo katika maonesho haya kuwapo kwa Taasisi za utafiti zinazozalisha mbegu za kisasa, Kuwapo kwa teknolojia na zana za kilimo za kisasa ni njia mojawapo ya kuongeza tija kwa jambo ambalo litawasaidia wananchi kufahamu zaidi kanuni bora za kilimo.

  Ufugaji nyuki ni fursa mpya ambayo endapo Watanzania wataichangamkia itawaletea kipato na kuwaondolea umasikini. Fursa haihitaji gharama kubwa kuazisha gharama kubwa ni kununua mizinga na kuweka maeneo rafiki ya nyuki ili waweze kuingia.

  Baada ya hatua hiyo hakuna gharama yeyote zaidi ya kuvuna na kuchakata asali ili iwe na ubora wa kimataifa.

  Nyuki wanatoa mazao mengi ikiwa ni pamoja na nta ambayo inatumika kutengeneza mishumaa na bidhaa nyingine.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzirasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji wa Korogwe mkoani Tanga katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzirasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji wa Korogwe mkoani Tanga katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Korogwe kwenye uzinduzi rasmi wa Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza madiwani na viongozi wengine baada ya kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akienda kuagana na wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mmoja wa wa wananchi baada ya  kuzindua rasmi Stendi ya mabasi mpya na ya kisasa ya mji huo katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Moja ya mabango yaliyokuwa na ujumbe wa changamoto mbalimbali za Korogwe
   Wengi walikuwa na kiu ya kusikilizwa kero zao
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza diwani wa kata ya Msima  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Wananchi wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama kwa muda na kuongea nao katika kata ya Msima  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

    Kikosi kazi cha TBC kikirusha mubashara matukio yote ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Hapa ni katika Msima  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Kikosi kazi cha TBC kikirusha mubashara matukio yote ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Hapa ni katika Msima  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulisha viongozi alioongozana nao kwa wananchi wa kata ya Msima  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsimiliza mwalimu wa shule ya msingi ya Msima aliposimama kuzungumza na wananchi  kata ya Msima  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella akielezea changamoto mbalimbali za wananchi wa kata ya Msima  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi shilingi milioni 5 taslimu  Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ya Msima kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukiingia mjini Handeni  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika nyumba ya aliyekuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Alhaj Dkt. Abfdallah Kigoda  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga  leo Agosti 7, 2017. Pamoja naye ni mjane wa marehemu Mama Kigoda, dada wa Marehemu Mhe, Asha Kigoda na mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Omari Abdallah Kigoda
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  waakitoa heshima zao kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Alhaj Dkt. Abfdallah Kigoda  nyumbani kwa marehemu mjini Handeni katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga  leo Agosti 7, 2017. Pamoja naye ni mjane wa marehemu Mama Kigoda, dada wa Marehemu Mhe, Asha Kigoda na mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Omari Abdallah Kigoda
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  waakitoa heshima zao kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Alhaj Dkt. Abfdallah Kigoda  nyumbani kwa marehemu mjini Handeni katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga  leo Agosti 7, 2017. Pamoja naye ni mjane wa marehemu Mama Kigoda, dada wa Marehemu Mhe, Asha Kigoda na mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Omari Abdallah Kigoda
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli  waakitoa heshima zao kwenye kaburi la aliyekuwa Mbunge wa Handeni Marehemu Alhaj Dkt. Abfdallah Kigoda  nyumbani kwa marehemu mjini Handeni katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani Tanga  leo Agosti 7, 2017. Pamoja naye ni mjane wa marehemu Mama Kigoda, dada wa Marehemu Mhe, Asha Kigoda na mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Omari Abdallah Kigoda
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe alipowasili wilayani humo  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akipungia wanannchi alipowasili katika uwanja wa mikutano wa Kibaoni kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Mke wa Rais Mama Janeth  Magufuli akiwakipungia wananchi wa Handeni alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia  wananchi alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia  wananchi alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia  wananchi alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia  viongozi wa dini na wananchi alipowasili katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akikaribisha wageni wake wilayani humo  katika siku ya mwisho ya ziara  Rais ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
  Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017

   Mke wa Rais Mama Janeth  Magufuli akisalimia wananchi wa Handeni katika uwanja wa mikutano kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara ya Rais ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Handeni  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Sehemu ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa mikutano alipofika kuzungumza nao  katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
    Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akitolea ufafanuzi baadhi ya changamoto  wilayani humo  leo Agosti 7, 2017
   Mmoja wa wananchi wa Handeni akitoa kero zake mbele ya Rais Magufuli
   Rais Magufuli akimfariji mwananchi huyo kwa matatizo yaliyomsibu
   Mmoja wa wananchi wa Handeni akitoa kero zake mbele ya Rais Magufuli
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakiagana na viongozi na wananchi wa Handeni baada ya kuwahutubia katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuliakiagana na viongozi na wananchi wa Handeni baada ya kuwahutubia katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Msafara wa Rais Magufuli ukiendelea na safari
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi wa Manga aliposimama kwa muda kuongea nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi ya siku tano mkoani humo leo Agosti 7, 2017
   Mbunge wa Handeni Vijijini  Mhe. Mboni Mhita akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali wakati Rais Magufuli aliposimama kwa muda katika kijiji cha Kwachaga 
   Mafundi mitambo wa TBC wakiwa makini kuhakikisha matangazo yanaruka mubashara bila shida
   Mkulima wa kijiji cha Manga akieleza kero wazipatazo kwa wafugaji katika kata ya Kwachuma
   Mmoja wa viongozi wa wafugaji akifafanua hali ilivyo kata ya Kwachuma
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akitoa maelezo ya changamoto mbalimbali katika kata ya Kwachuma
   Rais Dkt. Magufuli akiagiza kuondolewa kwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Mazingara baada ya wananchi na Mkuu wa Wilaya kudai amekuwa akitoa uamuzi usiotoa haki kwa wakulima
   Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella akimuaga rasmi Rais Dkt. Magufuli na kumshukuru kwa kutembelea mkoa huo kwa siku tano
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia wananchi wa kata ya Kwachuma
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimia wananchi wa kata ya Kwachuma
   Rais Dkt. Magufuli akiaga wananchi wa kata ya Kwachuma
   Rais Dkt. Magufuli akiagana na viongozi wa mkoa wa Tanga baada ya kuongea na  wananchi wa kata ya Kwachuma
    Rais Dkt. Magufuli akiagana na viongozi wa mkoa wa Tanga baada ya kuongea na  wananchi wa kata ya Kwachuma
    Rais Dkt. Magufuli akiagana na viongozi wa mkoa wa Tanga baada ya kuongea na  wananchi wa kata ya Kwachuma
    Kabla ya kuondoka Rais Dkt. Magufuli aliongea na wanafunzi wa shule za kata ya  Kwachuma
  Rais Dkt. Magufuli akiongea na wanafunzi wa shule za kata ya  Kwachuma
    Rais Dkt. Magufuli akimsikiliza mwanafunzi  Mwajuma Omari Mbwewe 
   Rais Dkt. Magufuli akijibu maswali ya mwanafunzi huyo wa shule za kata ya  Kwachuma
   Rais Dkt Magufuli akiagana na mwanafunzi Mwajuma Omari Mbwewe baada ya kujibu maswali yake
   Akiwa njiani msafara wa Rais Dkt. Magufuli ulisimamishwa na umati mkubwa wa watu maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ambapo ikambidi asimame na kuongea nao
   Umati mkubwa wa watu maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam ambapo ukimsikiliza Rais Magufuli
   Rais Dkt. Magufuli akiongea na umati mkubwa wa wananchi uliomsimamisha  maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam 
   Rais Dkt. Magufuli akisikiliza kero za wafanyabiashara wadogo maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam 
   Kama kawaida ujumbe ulikuwepo
   Rais Dkt. Magufuli akimfariji mmoja wa wafanyabiashara wadogo waliopata changamoto eneo la Bunju A
  Rais Dkt. Magufuli akishangiliwa na umati wa  wananchi uliomsimamisha  maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
   Rais Dkt. Magufuli akishangiliwa na umati wa  wananchi uliomsimamisha  maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
   Rais Dkt. Magufuli akishangiliwa na umati wa  wananchi uliomsimamisha  maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
   Rais Dkt. Magufuli akiagana na umati wa  wananchi uliomsimamisha  maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam
  Rais Dkt. Magufuli akiagana na umati wa  wananchi uliomsimamisha  maeneo ya Bunju A wilaya ya Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Picha na IKULU

  0 0

   Meneja wa Mwalimu Commercial Bank, Plc, (MCB), tawi la Samora katikati ya jiji la Dar es Salaam, Bi. Leticia Ndongole, (wapili kushoto), akimkabidhi zawadi ya IPAP, Bw. Khamisi Mmuka, kutoka wilayani Newala mkoani Mtwara, baada ya kuibuka mshindi kwenye droo ya kampeni ya "weka akiba na ushinde" iliyochezeshwa na benki hiyo. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.
  BENKI ya Mawlimu, (Mwalimu Commercial Bank plc), imewakabidhi zawadi washindi watatu wa kampeni ya “weka akiba na ushinde’ ambapo mteja wa benki hiyo kutoka wilayani Newala, Bw.Khamisi Mmuka, alijinyakulia zawadi ya IPAD.
  Katika hafla hiyo ya kukabidhi zawadi iliyofanyika alasiri ya Agosti 7, 2017 kwenye tawi la Samora la benki hiyo, washindi wengine ni Bi.Flora Mbaule na Bi.Macrina Yoram Kyando wote kutoka Temeke jijini Dar es Salaam ambao walijnyakulia vocha za manunuzi.
  Akizungumza kweney hafla ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa alisema, kampeni hiyo ilianza Mei 18, 2017 ambapo mteja mwenye akaunti kila anapoweka akiba ya fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini (50,000) kwenyeakaunti yake, aliingia moja kwa moja kwenye droo hiyo. “Na sio mteja wetu tu hata mwananchi aliyefungua akaunti na kuweka kiasi kama hicho cha fedha naye pia alipata fursa ya kushiriki.” Alifafanua Bi. Rahma.
  Naye Meneja wa tawi la Samora wa benki hiyo, Bi.Leticia Mmuka, alisema ingawa kampeni hiyo imemalizika lakini amewahimiza wananchi kufungua akaunti kwenye benki hiyo na wale wenye akaunti waendelee kuweka fedha zao kwani benki inatoa huduma bora na zenye kuvutia wateja.
  Alisema huduma huizo ni pamoja na kutoa gharama nafuu na rafiki za kibenki na ni sukuhisho la kifedha kwa walimu, watumishi wa serikali, wafanyabiashara, wakulima na wananchi kwa ujumla.
  “Huduma za kibenki zitolewazo na MCB ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu, huduma ya ATM iliyounganishwa na mtandao mpana wa UMOJA SWITCH uliosambaa nchi nzima.” Alifafanua zaidi.
  Aidha kwa upande wao washindi wa zawadi hizo walisema, wamefurahishwa na jinsi benki inavyowashirikisha wananchi na wateja kwenye kampuni kama hiyo na kuwataka wananhi kufungua akaunti na benki hiyo ambapo huenda nao wakapata zawadi kubwa zaidi ya walizopata wao.
  “Nimefurahi sana kushinda zawadi hii, kwani mimi ni mteja wa MCB kutoka mbali kidogo, hko Neawala mkoani Mtwara, laini nimeibuka mshindi, nah ii inaonyesha hapakuwepo na upendeleo wowote, nawashukuru sana MCB kwa zawadi hii.” Alisema mshindi wa IPD Bw. Khamisi Mmuka.

   Meneja Masoko wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, akizungumza na waandishi wa habari baada ya zoezi la kutoa zawadi.
   Mshindi wa vocha ya manunuzi, Bi. Macrina Yoram Kyando, (kushoto), kutoka wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akielezea furaha yake baada ya kuibuka mshindi.
    Mshindi wa vocha ya manunuzi, Bi. Flora Mbaule, (kushoto), kutoka wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, akielezea furaha yake baada ya kuibuka mshindi.
   Afisa wa Huduma kwa wateja wa MCB, Bi.Martha Gambosi, (kushoto), akimkabidhi vocha ya manunuzi mshindi wa kampeni ya "weka akiba na ushinde" Bi. Flora Mbaule kutoka wilayani Temeke.
   Meneja wa tawi la Samora wa MCB, Bi. Leticia Ndongole, (Kushoto), akimpongeza Bi. Flora Mbaule kwa ushindi wake uliompatia zawadi.
  Kiongozi wa watumishi wa MCB tawi la Samora, Bw.Ombeni Kaale, (wapili kulia), akimkabidhi zawadi ya vocha ya manunuzi, Bi. Macrina Yoram Kyando, kitoka wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, baada ya kuwa miongoni mwa washindi wa droo ya "weka akiba na ushinde" iliyochezesha na MCB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Bi. Rahma Ngassa, (wakwanza kushoto) na Menja wa tawi la MCB, Samora, Bi. Leticia Ndongole

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NHIF Mhe. Anne Makinda akisaini
  kitabu cha wageni kwenye banda la NHIF jijini Dodoma alipotembelea maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Nzuguni jijini humo.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga na viongozi wengine wa NHIF wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF alipotembelea banda hilo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mmoja wa maofisa wa NHIF waliokua wakishiriki maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma.

  Meneja wa NHIF mkoani Dodoma Bi. Salome Manyama akielezea jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Mhe. Anne Makinda ambaye
  pia alitembelea banda hilo kama mgeni Rasmi wa maonesho hayo ya Nanenane yaliyokua yakifanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya Nzuguni.
  ……………………………

  Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mhe. Anne Makinda ametembelea Maonesho ya Nanenane katika Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi wa siku hiyo. Mhe. Makinda alisisitiza umuhimu wa kila mtanzania kuwa na bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu na kuweza kutimiza majukumu yake ya kila siku na kuepukana na umaskini.

  Alisema ‘…. tunajua kuwa katika zama hizi tunatakiwa kuchapa kazi kama Mhe. Rais wetu anavyotuhimiza, lakini ili tuweze kuendana na kasi hii hatuna budi kuwa na uhakika na afya zetu na Serikali imetuletea utaratibu huu wa bima ya afya ambao ni rahisi kwa kila mtu kujiunga na kuwa na uhakika wa matibabu pindi anapougua”

  Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga amesema NHIF imejipanga kutoka na kwenda kuwafuata watu walipo ili kuweza kuwasajili na huduma za Mfuko huo. Alisema kwa sasa Mfuko unafanya kampeni ya uhamasishaji wa huduma ya bima ya afya kwa watoto walio chini ya miaka 18 ijulikanayo kama TOTO AFYA KADI. “Mfuko umeanza kufanya usajili kwa wingi katika maeneo mbalimbali karibu na watu walipo ambapo kila mtoto anachangiwa sh. 50,400 tu kwa mwaka” alisema Bw. Konga.

  Huduma hii ya TOTO AFYA KADI imezinduliwa rasmi na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wiki iliyopita ambaye alisema kuwa watoto ambao ni asilimia 51 ya watanzania wote wanahitaji kuwa na uhakika wa matibabu na alihimiza kuweka mikakati madhubuti kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma hiyo.

  Naye Meneja wa NHIF Mkoani Dodoma, Bi. Salome Manyama amesema wazazi na walezi wamepata mwitikio na kufika kusajili watoto wao katika huduma ya TOTO AFYA KADI katika maonesho hayo. Ameongeza kusema kuwa umma uko tayari na wamejipanga kuendeleza kampeni hiyo katika maeneo ya karibu zaidi na wananchi.

  0 0

   Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (kushoto), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour (hayupo pichani), alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kwenye Maonyesho ya Nanenane viwanja vya Ngongo mkoani Lindi leo. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendegu. Maonyesho hayo yatafungwa na Makamu wa Rais leo mchana.
  Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, HusseinMansour (kushoto), akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, alipotembelea banda la COSTECH.
  Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la COSTECH katika maonyesho hayo.
  Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Christina Kidulile, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la COSTECH jinsi ya kuotesha mimea kwa kutumia chupa.
   Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Philbert Nyinondi, kushoto akizungumza na wadau wa kilimo jinsi Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya Kilimo-SNAL itakavyowawezesha wakulima wa Tanzania kupata taarifa za kilimo kwa njia rahisi.
   Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Patric Ngwediage (wa nne kulia), akiwa na Crew nzima ya COSTECH katika banda hilo.
  Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Philbert Nyinondi (katikati) akigawa vipeperushi kwa wakulima ambao ni makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), vinavyohusu Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya Kilimo-SNAL. Kushoto ni Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Christina Kidulile.
  Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro, Ismail Ngolinda, akitoa maelekezo kwa wakulima jinsi ya kuotesha miche kwa njia ya chupa.older | 1 | .... | 1330 | 1331 | (Page 1332) | 1333 | 1334 | .... | 1898 | newer