Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

MTEMVU ATOA MSAADA WA VYAKULA KWENYE VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA TEMEKE

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akiwakabidhi msaada wa vyakula watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Dar Alqaama Tandika katika sherehe ya kutoa misaa kwa vikundi mbalimbali vya yatima, Dar es Salaam hivi karibuni.
                                        Akiwakabidhi watoto wa Kituo cha Hiyari Chang'ombe
                                              Upendo Maganga wakipata msaada huo
                                                                  Upendo Bokolani wakipata msaada huo
                                        Kituo cha WAVIBA KILAKALA wakipokea msaada
                                               Kituo cha Faraja kikipokea msaada huo
 Mwenye ulemavu wa viungo, Zamda akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Mtemvu
                                                  Aisha Shabani akipokea msaada huo
                                        Mwasiti Mtebwa akipata msaada
 Mama Mwandoro akipata msaada
                                                           Ashura Sadiki


Kituo cha Ungindoni kikikabidhiwa msaada wa vyakula na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu

ANAKUJA.

0
0

kumekucha Twanga pepeta na shangwe za Idd pili ndani ya Mango Garden-Kinondoni jijini Dar

0
0

FLAVIANA MATATA ATAJWA KWENYE LIST YA FORBES AFRICA MAGAZINE MODEL

0
0

FORBES AFRICA Releases Forbes Africa's Magazine Model List for 2013. Angolan Model Maria Borges Tops The List

Announced a few days ago by FORBES AFRICA, a 21-year-old Angolan model Maria Borges makes the tops Forbes Africa's Magazine Model List for 2013 making her the hottest item of the moment in the catwalk. The magazine will hit stands on August 1st, so grab your copy for the list where other African models that came close to snatching the title for number 1 include Ajak Deng from Sudan, Grace Bol from Sudan, Candice Swanepoel of South Africa, Liya Kebede of Ethiopia, Katryn Kruger of South African and Miss Universe competitor Flaviana matata.
Maria-Borges-Forbes-Africa-Top-Model-BellaNaija-July2013-8-400x600
Maria Borgas
Flanianamatata

RAIS KIWETE AFUTURISHA WASANII WA BONGO FLEVA IKULU

0
0
 
 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Filamu na  Bongofleva,Hemed Suleiman.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu na mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,TV,Mbwiga Mbwiguke.

 Rais Kikwete akiwa akiwa katika picha ya pamoja na Msanii Mkongwe wa Bongofleva,Gwamaka Kaihula a.k.a King Crazy G K.

 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa bongofleva na muigizaji wa Filamu hapa nchini,atambulikae kwa jina la kisanii Zuwena Mohamed a.k.a. Shilole.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii wa Bongofleva,Ally Kiba na mdogo wake Abdull Kiba.
 
Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongofleva mara baada ya kufturu.Kutoka kushoto,Snura,Keisha,Mwasiti,aliyechuchumaa ni Shilole,Dj Fetty ,Mwanahawa Abdul a.k.a Quee Doreen.
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya pichani shoto Mwasiti Almas na kulia Zuwena Mohamed a.k.a Shilole wakiwa sambamba na Mtangazaji wa Clouds FM,Dj Fetty wakipakua ftari kufuatia mualiko wa Rais Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar jana.

 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakipata ftari kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar jana kufuatia mualiko wa Rais Kikwete.
 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wa bongofleva,Lawrence Malima a.k.a Marlow,kulia kwake ni Ally Kiba pamoja na Abdul Kiba na kushoto ni Mtangazaji wa East Africa Radio,Samisango

 Rais Kikwete akisalimiana na msanii wamuziki wa kizazi kipya,Chege Chigunda na kulia kwake ni msanii wa bongofleva,Cassim Mganga,wakati wa kupata ftari jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar.

 Rais Kikwete akiwasabahi baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya,mara baada ya kupata ftari mapema jana jioni kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar,Rais Kikwete aliwaalika wasanii mbalimbali kupata ftari ya pamoja Ikulu jana jioni. 

MKUU WA MKOA WA RUKWA STELLA MANYANYA AONANA NA WALIMU WA KIKE WA MANISPAA YA SUMBAWANGA LEO KUJADILI KERO ZAO MBALIMBALI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na walimu wa kike wa Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 02 Agosti 2013 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la mkutano huo likiwa kujadili kero mbalimbali za walimu pamoja na kuzitaftia ufumbuzi. Pamoja na kero mbalimbali zilizowasilishwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa maelekezo kwa Halmsahauri ya Manispaa kushughulikia kero zinazowezekana ikiwepo madai ya likizo na mengineyo. Kwa yale yaliyo nje ya uwezo wa Manispaa aliahidi kuyachukua na kuyafikisha panapohusika ili yaweze kutaftiwa ufumbuzi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Kushoto ni Afsa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa Bi Catherine Mashalla.  
 Katika kikao hicho walimu walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kufuta chama cha waalim (CWT) kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiwakata waalim mishahara kwa mda mrefu bila kuwa na msaada wowote kwao pindi wanapouhitaji.Mapendekezo mengine ni kupunguza idadi ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka tisa hivi sasa na kuwawekea masomo yatakayowawezesha kusoma na kuandika kuliko hivi sasa ambapo masomo ni mengi na huwachanganya watoto. Hata hivo Mkuu wa Mkoa aliweka bayana kuwa ni vyema chama hicho kikaona ni jinsi gani ya kuwanufaisha zaidi walimu kwa kujiwekea utaratibu wa kuwakopesha au kuwasaidia kwa njia nyingine kiuchumi.

Sehemu ya waalimu waliohudhuria katika Mkutano huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwashauri waalim kutokopa katika taasisi zisizo rasmi ambazo riba zake ni kubwa kupita kiasi. Alisema taasisi nyingi za namna hiyo zimechangia kufanya maisha ya walimu wengi kuwa magumu na badala ya kuwa msaada kwao inageuka na kuwa kero.

Mkuu wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi Witness Maeda akitoa kero mbalimbali wanazokabiliana nazo waalim ikiwepo uhaba madarasa, mabweni, bwalo na maabara chuoni hapo. Kwa ujumla kero zilizowasilishwa ziligusia mishahara hafifu ya walimu, uhaba na ubovu wa vyumba vya madarasa, kucheleweshewa madai yao ya mishahara na nauli (Salary Arears), kupandiswa madaraja na uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kuweza kukabiliana ni mabadiliko ya mitaala mipya.  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa www.rukwareview.blogspot.com)

Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake

0
0


Kampuni ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto, na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.

Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi. Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.

 Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

RAIS KIKWETE AAGANA NA BALOZI WA VIETNAM NCHINI

0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga Balozi wa Vietnam aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mhe Nguyen Duy Thien  Ikulu jijini Dar es salaam jana. PICHA NA IKULU.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza Balozi wa Vietnam aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Mhe Nguyen Duy Thien baada ya kuagana naye Ikulu jijini Dar es salaam jana.

KCB BANK WAFUTURISHA JIJINI DAR

0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara (CCM) Philiph Mangula muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni mwenyekiti wa bodi ya KCB Benki Docta Edmund Mndolwa.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara (CCM) Philiph Mangula muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni mwenyekiti wa bodi ya KCB Benki Docta Edmund Mndolwa.
 Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya KCB Moezz Mir akiteta jambo bna Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Twaha Taslima, mmoja wa Wanazuoni wa Kiislam walioalikwa kwenye futari 
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, akisoma hotuba muda mfupi kabla ya kuanza kwa futari liyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania jijini Dar es Salaam jana
 Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Philiph Mangula akichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania jijini Dar es Salaam jana. Anayemfuatia ni Babu Othman mmoja ya waalikwa wa futari pamoja na Dr Edmund Mndolwa ambaye ni mwenyekiti wa bodi wa benki 
Baadhi ya akina mama wakiwa kwenye foleni ya kuchukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya KCB jijini Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye foleni ya kuchukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na benki ya KCB Tanzania jijini Dar es Salaam jana. 
  1. Mwenyekiti wa bodi ya benki ya KCB Tanzania Dkt Edmund Mndolowa akitoa neon la shukrani kwa wawakilishi kutoka jumuiya za Waislamu walioshiriki katika futari iliyoandaliwa na benki yake jijini Dar es Salaam jana


==========   ========  ========
BENKI ya KCB Tanzania inatarajia kufungua tawi jipya jijini Dar es Salaam mwezi huu, litakalokuwa maalum kwa ajili ya kutoa huduma za kibenki zinazofuata sharia za kiislamu
 
Akizungumza muda mfupi kabla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo Moizz Mir alisema mahitaji ya huduma za kibenki zinayofuata sharia imekuwa ikikuwa kwa kasi katika nchi mbali mbali ulimwenguni ikiwamo Tanzania.Mkurugenzi huyo alisema kuwa, kutokana na mahitaji ya huduma hiyo hapa nchini benki yake ilianzisha huduma hiyo mwaka 2008 na kuongeza kuwa mahitaji yameendelea kuongezeka tangu kipindi hicho
 
“Kwa kutambua umuhimu wa huduma hii pamoja na kukwa kwa mahitaji, tumeamuamua kuanzisha tawi ambalo litakuwa malum kwa ajili ya kutoa huduma mbali mbali za kibenki zinazofuata sharia,” alisema
 
Mgeni rasmi katika hafala hiyo ambaye ni Rais mstaafu wa wawamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi aliipongeza benki hiyo kwa huduma hiyo kwa ajili ya waislamu huku akiwasisitiza waislamu kujitokeza kujiunga nayo ili kunufaika
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo Dkt Edmund Mndolwa Pili aliushukuru  Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania  kwa  kuungana na KCB bank katika hafla hiyo na aliwapongeza kwa kazi nzuri za kijamii na kidini wanazozifanya ikiwemo pamoja na kutoa ushauri wa kibenki kwa benki mbalimbali nchini ikiwemo KCB Bank katika kuunda, kusimamia  na kuuza huduma zinazofuata sharia.
 
“Napenda pia kuwapongeza kwa jitihada zenu zakusuluhisha migogoro mbalimbali nchini ili kudumisha amani ambayo ndicho kitambulisho kikuu cha nchi yetu ulimwenguni kote,” alisema. 
 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA KIONGOZI WA TAASISI YA IYF YA KOREA KUSINI NA UJUMBE WAKE

0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na ujumbe wa IYF Ikulu jijini Dar es salaam jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Ock Soo Park Ikulu jijini Dar es salaam jana.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadili chapisho la kitabu na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni mkalimani. 

HOTUBA YA RAIS KIKWETE YA MWISHO WA MWEZI WA JULAI 2013

0
0

MTANZANIA MSHIRIKI ALIYETOLEWA KATIKA MJENGO WA BIG BROTHER AFRIKA ARMY NANDO ATUA JIJINI LOS ANGELELS CALIFORNIA.

0
0
Army Nando awasili Los Angeles, California.
 Mpiganaji Davis Mosha, Edgar D. Mosha, Mayor wa L.A. Deo Temba (Katikati nyuma) na Army Nando.
  Mpiganaji Davis Mosha akimpa ushauri Army Nando kuwa asahau yaliyopita na aangalie ya mbele na kumweleza kuwa hiyo ilikuwa ni mchezo tu (It was just a game).
 Nancy Assenga ( Mama wa Army Nando), Army Nando, na Deo Temba L.A. Mayor.
 Mayor wa L.A. Deo Temba, Army Nando, Nancy Assenga (Mama na Meneja) na Mkurugenzi mtendaji wa Swahili TV Bwana Alex Kassuwi mara baada ya kumpokea Nando Los Angeles, California.


 Juliet Luangisa, Army Nando na Nancy Assenga (Mama na Meneja wa Nando)
Mkurugenzi Mtendaji Swahili TV Bwana Alex Kassuwi, Army Nando, Walter Minja, Deo Temba na Nancy Assenga-Meneja wa Nando wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumpokea Army Nando Marekani.

MPIGANAJI DAVIS MOSHA "THE CEO" BAADA YA KUONANA NA WATANZANIA WAISHIO  L.A.  AMWANDALIA HAFLA (BASH) NZITO YA HADHI YA KISTAA (CELEB STATUS) ARMY NANDO KATIKA HOTELI GHALI YA YARD HOUSE L.A. MAREKANI.

 Mpiganaji "THE CEO" Davis Mosha katika msafara aliwakaribisha pia chakula cha jioni watanzania zaidi ya ishirini katika hoteli ya bei ghali L.A. Yard House ambayo ipo Downton katikati ya Uwanja wa Lakers (Staples Center) na JW Marriott Hoteli.

 Army Nando na Nancy Assenga (Mama mzazi na Meneja wake) wakifurahia chakula katika Yard House Hoteli Downtown L.A.

 Mayor wa L.A. Deo Temba naye aliwakilisha jiji lake.

Juliet Luangisa na Walter Minja wakiburudika kwa misosi ya Yard House.

USIKOSE KUANGALIA EXCLUSIVE INTERVIEW NA SWAHILI TV








   USIKOSE KUANGALIA INTERVIEW HII ENDELEA KUANGALIA SWAHILI TV
  www.swahilitv.blogspot.com
www.swahilitv.info
PICHA ZOTE NA SWAHILI TV COPYRIGHT 2013





MAKAMU WA RAIS AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA SHINDANO LA TATU LA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU JIJINI DAR

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza za waumini wa dini ya Kiislamu, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Qur'an Tukufu, iliyofanyika jana usiku Agosti 2, 2013 katika Msikiti wa Istiqaama, jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya waumini wa dini ya Kiislamu, waliohudhuria hafla hiyo. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 2, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 30, Abdulkarim Khamis, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa  washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013. 
  Mtoto Maryam Nassor (8) akisoma moja ya haya iliyo katika kitabu cha Juzuu kwa kichwa, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 1.5, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi Juzuu 20, Maryam Nassor (8), wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.
  Mtoto Maryam Nassor (8) akisoma moja ya haya iliyo katika kitabu cha Juzuu kwa kichwa, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam, jana usiku Agosti 2, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Juzuu, wakati wa hafla ya kuwakirimu wasindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku Julai, 2, 2013. Picha na OMR-

wawekezaji zanzibar wafutarisha kijiji cha paje mkoa wa kusini unguja

0
0
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslim Hija (wa kati alievaa koti) akiungana na mafsa mbalimbali wa Mkoa huo katika futari iliyoanaliwa na Ivan Kodeh Mejeja wa Hoteli ya Cristal Resort ya Paje iliyofanyika huko Hoteli kwake Paje Mkoa wa Kusini Unguja.
Mke wa Meneja ya Hoteli ya Cristal Resort ya Paje, Bi. Deva Monique akiwa na mwanawe Thalia akiungana na wanakijiji cha Paje katika futari iliyoandaliwa  Mumewe Ivan Kodeh Mejeja wa Hoteli ya Cristal Resort.
 Mejeja wa Hoteli ya Cristal Resort ya Paje Bw. Ivan Kodeh, akitoa shukran mara baada ya futari aliyowandalia, huko Hotelini kwake Paje.
  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Dkt. Idrisa Muslim Hija na Mejeja wa Hoteli ya Cristal Resort Ivan Kodeh na wananchi wa Paje wakitikia dua mara baada ya futari.
 Familia ya Ivan Kodeh Mejeja wa Hoteli ya Cristal Resort nayo ikijumuika na wananchi kuitikia dua mara baada ya kuftari huko Hotelini kwao Paje Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar) .

Mbeya Yetu Blog Big up sana katika hili.!

0
0
Pichani ni banda la wadau wa mtandao wa Mbeya Yetu Blog,likiwa katika maonesho ya wakulima Nane Nane,jijini Mbeya.Ama kwa hakika mtandao wa JIACHIE unawapa hongera na pongezi kubwa kwa ubunifu huo mlioubuni wa kujitangaza.Uongozi mzima wa Mbeya Yetu Blog hizo ndizo fursa zenyewe na namna ya kuzitumia,nafasi inapotokea basi hakuna kufanya makosa-yaani mpaka kieleweke.Kama mlivyoona na kusikia TCRA ndio hao wamekwisha zitambua juhudi zetu tunazozionesha katika suala zima la kuielimisha,kuiburudisha na kuionya jamii kwa namna moja ama nyingi kupitia mitandao yetu ya Kijamii.Mbeya Yetu Big Up sana katika hili,




MAKUNDI MBALI MBALI MBALI YA VIJANA MKOA WA MWANZA WASHIRIKI MJADALA WA KATIBA MPYA

0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa ufafanuzi wa CCM juu ya Rasimu ya Katiba mpya katika mkutano uliofanyika Mwanza leo na kuwakutanisha vijana wa makundi mbali mbali.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Stephen Wasira akifafanua juu ya mstakabali wa vijana katika mchakato wa Katiba mpya.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dk.Anthony Dialo akichangia mada juu ya umuhimu wa serikali mbili kwa Tanzania.
Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Mkoani Mwanza Sixbert Ruben akielezea umuhimu wa vijana wa Mwanza katika kushiriki kwa kwenye mchakato wa Katiba mpya.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Martin Shigela akifafanua juu ya umuhimu wa vijana katika suala la  Katiba mpya
Sehemu ya Vijana walioshiriki katika  mjadala wa mchakato wa Katiba mpya uliofanyika leo katika ukumbi wa chuo cha mafunzo Benki Kuu mkoani Mwanza ambapo vijana zaidi ya mia sita walihudhuria.

TSN, TCRA, AICC, TTCL, YARA WASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE DODOMA 2013

0
0
 Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao lililopo ndani ya Viwanja vya Nzuguni Mjini Dodoma yanapofanyika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima Nane Nane. Mwaka huu TCRA wanakuambia 'FUTA-DELETE' ujumbe wowote usio na maana katika simu yako au mtandao wa Barua pepe. Ila Father Kidevu Blog, inaongezea Ujumbe 'PUUZIA-IGNORE' taarifa yeyote isiyo na manufaa kwa jamii katika Mitandao ya Kijamii.
 Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mwasiliano Tanzania (TCRA) anaeshughulika na Uratibu wa Kanda, Victor Nkya akitoa elimu ya FUTA-DELETE kwa vijana waliotembelea banda hilo leo.
 Kikosi kazi cha Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Standard Newspapers (TSN) Limited ambacho kipo ndani ya viwanja vya Nzuguni katika Banda la Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo katika Maonesho ya siku ya Wakulima Nane Nane yaliyoanza Agosti Mosi na kutaraji kumalizika Agosti 8, 2013 kitaifa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Afisa Masoko, Francis Kihinga akiwa na Afisa Mauzo na Masoko, Chikira Mgheni. TSN ndio wachapishaji na wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO, HABARILEO Jumapili na SpotiLEO.
 Afisa Masoko wa TSN, Francis Kahinga akigawa majarida ya Elimika na Academy kwa wanafunzi walio tembelea banda la TSN. TSN ndio wachapishaji na wasambazaji wa Magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARILEO, HABARILEO Jumapili na SpotiLEO.
 Kampuni Kongwe ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL) nayo ipo katika Viwanja vya Nzuguni, kuelimisha umma juu ya huduma zake. Pichani ni Maofisa wa Kampuni hiyo Thomas Lemunge ambaye ni Afisa Biashara wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (katikati) akitoa elkimu kwa mwananchi huku Afisa Habari, Amanda Luhanga akifuatilia.
 Wafanyakazi mbalimbali wa TTCL wakiwa bandani hapo wakitoa elimu ya huduma zao.
Ofisa Masoko na Utafiti wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Linda Nyanda, akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.

Ofisa Habari Mwandamizi na Itifaki wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), Catherine Kilinda akiwapa maelezio wanafunzi wa kidato cha tatu wa Sekondari ya Maria de-Mathias ya mjini Dodoma juu ya shughuli mbalimbali za AICC walipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Wakulima nane nane katika Uwanja wa Nzuguni mjini Dodoma.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya YARA Tanzania Limited, Catherine Assenga (kushoto) akimsadia mwananchi aliyetembelea banda lao lililopo ndani ya Banda la NMB katika Viwanja vya Maonesho Nane Nane, Nzuguni Mjini Dodoma. YARA ndio wasambazaji wa Mbolea CHAPA MELI.

Makamu wa Rais Dk Bilal ahudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Iran

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya IRAN alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Ogast 03-2013 kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhan  Al-Quds  anaetarajiwa kuapishwa kesho baada ya kushinda kwenye uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Agosti 03-2013 kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhan  Al-Quds  anaetarajiwa kuapishwa kesho baada ya kushinda kwenye uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mshauri Maalum wa Waziri wa Mambo ya nje wa Serikali ya Jamhuri ya Kiislam ya IRAN bw. Mohammad Valulleh kwenye chumba maalum cha mapumziko VIP katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Teheran leo Ogast 03-2013 alipowasili Nchini Irani kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mpya wa Nchi hiyo Bw. Hassan Rouhani Al-Quds anaetarajiwa kuapishwa kesho baaada ya kushinda kwenye Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni. (Picha na OMR).

Nyota wa NBA Stephen Curry aendesha Clinic ya kikapu na kugawa vyandarua "Nothing but Net"

0
0
Viongozi wa juu wa TBF Magesa, Maluwe na Msoffe wakiwa na NBA stars Stephen Curry na Hasheem Thabeet mara baada ya Wachezaji hao kuendesha clinic ya kikapu kwa Vijana 100 wa chini ya miaka 18 ... Katika kampung ya Nothing but Net ambapo Curry anagawa vyandarua ili kupitia vita Malaria.... Urey alikuja nchini katika ziara iliyoratibiwa na UN Foundation, US Embassy kwa kushirikiana na TBF, clinic hiyo ilisaidiwa na Cocacola, BBall Kitaa, Redcross na wadau wengi wa kikapu wa DSM.

WANACHAMA WA HABARI GROUP WAPELEKA MISAADA VITUO VYA WATOTO YATIMA

0
0

Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Fonditioni, Aisha Sururu kulia akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia watoto yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group  Rabia Bakari kushoto na Asha Bani kwa ajili ya kupeleaka kwa watoto yatima katika vituo mbalimbali  Misaada mingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba,Mmiliki wa Maduka ya Silva Botique, Madam Nora, Katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa kiislam Sheikh  Khamisi Mataka, na Mkurugenzi wa Kampuni ya QUALITY Printers And Stationers Amani Sokko.

Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Foundation, Aisha Sururu kushoto akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia watoto yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group  Rabia Bakari kushoto na Asha Bani kwa ajili ya kupeleaka kwa watoto yatima katika vituo mbalimbali  Misaada mingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba,Mmiliki wa Maduka ya Silva Botique, Madam Nora, Katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa kiislam Sheikh  Khamisi Mataka, na Mkurugenzi wa Kampuni ya QUALITY Printers And Stationers Amani Sokko PIcha na  BLOG YASUPER D

Wanachama wa kikundi cha Habari Group Rabia Bakari kulia na Asha Bani wakiangalia baadhi ya vyakula na vitu mbalimbali walivyokabidhiwa kwa ajili ya kwenda kugawa kwa watoto yatima.Picha na  BLOG YA SUPER D
Diwani wa Viti Maalumu na Mwenyekiti Mtendaji wa Aisha Sururu Foundationi, Aisha Sururu kulia akiwakabidhi sehemu ya msaada alioutoa kwa ajili ya kuchangia watoto yatima kwa wanachama wa kikundi cha Habari Group  Rabia Bakari kushoto na Asha Bani kwa ajili ya kupeleaka kwa watoto yatima katika vituo mbalimbali  Misaada mingine ilitolewa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba,Mmiliki wa Maduka ya Silva Botique, Madam Nora, Katibu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa kiislam Sheikh  Khamisi Mataka, na Mkurugenzi wa Kampuni ya QUALITY Printers And Stationers Amani Sokko PIcha na  BLOG YASUPER D

Wanachama wa Habari Group wakia katika picha ya pamoja na na mwenyekiti mtendaji wa Aisha Sururu fondition bi, Aisha Sururu
Moja ya kituo cha kilichopewa misaada na Habari Group Leo

Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group Asha Bani kulia akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Katibu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni Bw. Abubakari Simba Dar es salaam leo Picha na
www.burudan.blogspot.com

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha habari Group wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni baada ya kutoa misaada mbalimbali leo

Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group Asha Bani kulia akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Katibu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Al-Hidaya Orphans Center and Tahfidhil-qur-an cha Buguruni Bw. Abubakari Simba Dar es salaam leo Picha na
www.burudan.blogspot.com


Mwanachama wa Kikundi cha Habari Group Asha Bani kulia akikabidhi sehemu ya msaada  walioutoa kwa  Msimamizi Mkuu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Al Furqan Islamic Center cha Chanika Bw,Hamisi Omari  Dar es salaam leo Picha na
www.burudan.blogspot.com

Baadhi ya wanachama wa kikundi cha habari Group wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Al Furqan Islamic Center cha Chanika baada ya kutoa misaada mbalimbali leo
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images