Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

TIGO KUTOA SMARTPHONE ZENYE MUDA WA BURE WA MAONGEZI KILA SAA KWA SAA 24

$
0
0
 Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu promosheni mpya ya Jaza Ujazwe ambapo simu za kisasa 720 zitatolewa kila siku kwa washindi wa promosheni hiyo. Kulia ni  Mtaalamu wa  Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Wiliam Mpinga, akionesha moja ya simu aina ya Teco S1 zitakazotolewa katika promosheni hiyo.
Mtaalamu wa  Bidhaa Mpya za Tigo, Jaqualine Nnunduma, akizungumzia promosheni hiyo.
Na Dotto Mwaibale
 ……………………………………………
 
Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo  Tanzania, bado inawavutia wateja wake tena na prmosheni kubwa ambayo itashuhudia wateja hao  wakiondoka na simu za mkononi za kisasa (Smartphones) kila saa kwa saa 24 kila siku. Simu za mkononi zitatolewa zikiwa na muda wa  bure wa  mawasiliano kwa mwaka mmoja.
 
 Kwa mujibu wa Tigo, jumla ya simu za kisasa (Smartphones) 720  zipo tayari kuchukuliwa katika kampeni ya promosheni hii mpya.  Wateja wanaweza kushinda simu za mkononi kila saa tu kwa kuzijaza simu zao muda wa maongezi  kwa kukwangua kadi, e-pin au TigoPesa, ambapo namba yao ya simu itaingia kwenye droo kwa ajili ya kushinda  moja ya Smartphones za Tecno S1 ambayo itakuwa tayari kuchukuliwa  kila saa,  kila siku, katika siku saba za wiki.
                                             
Tofauti na promosheni nyingine ambapo ni wateja wachache tu wanapata zawadi chache, promosheni hii ya Tigo imethibitisha kusimama mahali ambapo  kila mteja mmoja anazawadiwa  kila anapojaza. Washindi wa Smartphone ya Tecno S1  watafurahia mawasiliano ya bure kwa mwaka mmoja ambapo zawadi nyingine za kushinda zinajumuisha bonasi ya bure katika  sauti, data na ujumbe mfupi wa maneno ( SMS) kulingana na muundo wa matumizi wa wateja.
 
Akitangaza zawadi hizo mpya, Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa kampuni hiyo kwa mara nyingine tena imefurahishwa na mwitiko chanya wa wateja kwa kampeni maarufu ya  Jaza Ujazwe na ndiyo sababu imewafanya waongeze zawadi za kuvutia zaidi pamoja na bonasi zaidi za kusisimua kama ishara ya shukrani.
 
  “Ni sehemu ya utamaduni wa Tigo katika  kutambua kuungwa mkono kusiko na ukomo ambao wateja wetu wametupa. Ndiyo maana, tunaamini kwamba wanastahili kupewa shukrani  kwa kujitoa kwao kwa kwa ajili ya  bidhaa  na huduma zetu. Tuna furaha  mara nyingine tena, kuwapatia  wateja wetu zawadi hizi, zitakazowawezesha kuendelea kufurahia huduma zetu za maisha ya kidijitali “, alisema Mpinga. 
 
 Tuzo za kusisimua zinaendana na  kuongezeka kwa miundombinu ya mtandao wa kisasa ya Tigo, aliongeza Mpinga akibainisha kuwa kipaumbele muhimu cha kampuni kilikuwa kikizingatia mahitaji ya wateja na kutoa suluhisho linalofaa kushughulikia mahitaji hayo.
 “Wateja wote wa Tigo wanastahili kupokea tuzo; tunatarajia kukidhi mahitaji ya mteja ya kuwa na uzoefu usio na  dosari kila wakati wanapowasiliana kwa chapa zetu.
 
Tunaamini kuwa wateja wetu watafurahishwa na zawadi hizi  mpya ikiwa ni pamoja na bonasi kwa dakika, ujumbe mfupi wa maneno (SMS) au data wanazozawadiwa na hivyo  kuimarisha utamaduni wao wa mawasiliano, “alibainisha Mpinga.

MAREHEMU PROF NAGU KUZIKWA ALHAMISI NYUMBANI KWAKE ENDASAKI,WILAYANI HANANG

$
0
0



Marehemu Prof. Nagu alikuwa Mhadhiri ktk chuo kikuu Mzumbe. Marehemu pia ni mume wa Mbunge wa Hanang- Mhe. Mary Nagu ambaye pia alikuwa Waziri katika serikali ya awamu ya tatu na ya nne. Marehemu Prof. Nagu ni baba wa Dr. Tumaini, Neema na Deogratias. 

Tunapenda kuwajulisha kuwa Marehemu atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwake Endasaki Wilaya ya Hanang siku ya Alhamisi tarehe 3/8/2017 

leo saa kumi jioni kutakuwa na Ibada ya kumuaga Marehemu katika kanisa katoliki St Peters, kisha mwili utaenda kulala nyumbani kwake Regent Estate Mikocheni tayari kusafirishwa siku ya tarehe 02/07/2017 kuelekea Manyara, Hanang', Kijiji cha Endasaki. 

Raha ya milele umpe ee Bwanana na mwanga wa milele umwangazie.

Apumzike kwa Amani Mzee wetu Prof Joseph Nagu.

MASAUNI AWATAKA WANAFUNZI VYUO VIKUU NCHINI KUONGEZA KASI YA UBUNIFU, AFUNGUA MAONYESHO YA SAYANSI CHUO CHA ST. JOSEPH DAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria kufungua Maonyesho Makubwa ya Sayansi na Teknolijia yaliyoandaliwa na wanafunzi wanaosoma fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Prakabahran Anath. Masauni baada ya kuangalia kazi za ubunifu mbalimbali uliofanywa na wanafunzi hao, aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akimsikiliza Mwanafunzi wa mwaka wanne fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, Tumaini Lutufyo (kushoto) wakati alipokuwa anatoa maelezo ya gari la kuzima moto ambalo linatumia gesi lililotengenezwa na wanafunzi wa chuo hicho. Masauni alifungua Maonyesho ya Sayansi na Teknolojia chuoni hao ambapo aliangalia kazi mbalimbali za ubunifu uliofanywa na wanafunzi hao, pia aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiliendesha gari linalotumia umeme wa jua lililotengenezwa na wanafunzi wa fani ya uhandisi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam. Masauni alifungua Maonyesho ya Sayansi na Teknolojia chuoni hao ambapo aliangalia kazi mbalimbali za ubunifu uliofanywa na wanafunzi hao, pia aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo .
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufungua Maonyesho ya siku mbili ya Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Chuo hicho kwa lengo l kuonyesha ubunifu mbalimbali wa wanafunzi hao. Masauni baada ya kuangalia kazi za ubunifu mbalimbali uliofanywa na wanafunzi hao, aliwataka wanafunzi hao kuongeza kasi zaidi ya kuongeza ubunifu kutokana na taaluma wanayoipata chuoni hapo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha jijini Dar es Salaam, Dk. Prakabahran Anath alipokua anatoa historia ya chuo hicho kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri huyo kufungua Maonyesho Makubwa ya Sayansi na Teknolijia yaliyoandaliwa na wanafunzi wanaosoma fani ya uhandisi chuoni hapo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NC

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI NA WATENDAJI WAKE WAKUU WAPITIA MPANGO WA MANUNUZI WA MWAKA WA FEDHA 2017/2018

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara yake wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala, akifuatiwa na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa pamoja na Kamishna wa Polisi wa Fedha na Logistiki Albert Nyamuhanga.
 Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi David Mwangosi, akiwasilisha Mpango wa Ununuzi wa Wizara hiyo wa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara hiyo wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa hiyo.
 Kamishna wa Polisi wa Fedha na Logistiki Albert Nyamuhanga    akichangia hoja kwa Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia ni Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa. 
Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha Edward Peter Chogero akichangia hoja kwa Watendaji Wakuu, Maofisa Bajeti na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani) wakati wa Kikao cha kupitia Mpango wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa mwaka wa fedha 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Jeshi hilo. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala. 

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA BALOZI WA MAURITIUS HAPA NCHINI NA WAWEKEZAJI WA SUKARI

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiagana na  Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu jijini Dar Es Salaam
17
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiagana na  Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji aliyeongozana na Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari ambao wameonyesha utayari wa kuwekeza nchini Tanzania.
15
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na  Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji , Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.WilliamErio .Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
……………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji aliyeongozana na Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari ambao wameonyesha nia na utayari wa kuwekeza nchini.

Mbali ya ujumbe kutoka Mauritius, wengine waliohudhuria mazungumzo hayo ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.WilliamErio .
Katika mazungumzo hayo  Makamu wa Rais amewahakikishia wawekezaji hao ushirikiano wa Serikali na kuwaeleza kuwa Tanzania ina mazingira bora ya uwekezaji.

Mbali ya fursa ya uwekezaji katika Sukari, Makamu wa Rais aliainisha maeneo mengine ya kuwekeza kama vile viwanda na TEHAMA.
Aidha alisema pindi uwekezaji huo ukifanikiwa , Tanzania itafaidika na soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na masoko mengine duniani kwa ujumla.
Uwekezaji huu utakuwa wa Ubia kati mashirika ya hifadhi ya mifuko ya jamii na pia kampuni nyingine za wazawa.

TAARIFA ZA MICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

$
0
0
DK. NDUMBARO, MGONGOLWA WATEULIWA TFF
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imeteua Kamati ya Rufaa ya Leseni za Klabu, ikiwa ni maandalizi ya kuanza msimu mpya wa mashindano ya soka yanayosimamiwa na kuendeshwa na TFF.
Viongozi na wajumbe waliteuliwa na kupitishwa Jumapili Julai 30, 2017 katika Mkutano wa Kamati ya Utendaji uliofanyika Ukumbi wa Hosteli za TFF, zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam yaliko Makao Makuu ya shirikisho.
Viongozi na Wajumbe walioteuliwa ni Msomi Wakili Dk. Damas Ndumbaro atayekuwa Mwenyekiti; Msomi Wakili Alex Mngongolwa (Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo) wakati Wajumbe ni Meneja wa zamani wa Uwanja wa Taifa, Charles Matoke, Tumainiel Mlango na Ahmed Menye.
Viongozi wa Kamati hiyo watakuwa na majukumu ya kusililiza rufaa kutokana na uamuzi wa Kamati ya Leseni za Klabu inayoongozwa na Msomi Wakili Lloyd Nchunga ambayo inasimamia utekelezaji wa Kanuni ya 11 ya Ligi Kuu.
Kwa mujibu wa kanuni hiyo ya 11, Klabu za Ligi Kuu zinawajibika na kutakiwa kuwasilisha maombi ya kupatiwa Leseni ya Klabu kwa TFF katika muda utakaotangazwa na Kamati ya Utendaji ya TFF na kuhakikisha zinakidhi masharti na vigezo vyote vya msingi kupatiwa leseni ili kuweza kushiriki Ligi Kuu.
Kanuni hiyo ya 11 inasema kwamba Klabu itakayoshindwa kukidhi kiasi cha kukosa Leseni haitashiriki Ligi Kuu kwa msimu husika. Vigezo hitajika kwenye kupata leseni ya klabu ni kuwa na Uwanja wa nyumbani wa mechi, uwanja wa mazoezi, umiliki wa klabu moja, kuwa na timu ya vijana, uwepo wa ofisi rasmi na watendaji wake akiwamo mtendaji mkuu (CEO) na maofisa masoko, habari na mhasibu mwenye taaluma ya uhasibu.
Tayari Klabu zilielekezwa kuwasiliana na Meneja wa Leseni za Klabu, Jemedari Said ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania wa TFF kwa ajili ya maelezo ya kuchukua na kurejesha fomu kwa mujibu wa taratibu na kanuni za mashindano kabla ya kuanza rasmi mashindano.


LIGI DARAJA LA KWANZA TANZANIA BARA 2017/18
Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kundi.
Tayari TFF, ilikwisha kutangaza makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19.
Kwa mujibu wa makundi hayo yaliyoratibiwa na Bodi ya Ligi ya TFF, kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga, Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.
Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za Dar es Salaam.
Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya  Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
Kadhalika, TFF imeagiza timu za Ashanti United, Friends Rangers, KMC na Polisi Dar ya Dar es Salaam kuwasilisha majina ya viwanja vitakavyotumiwa na timu zao wakati wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao.
Kutaja viwanja hivyo ni matakwa ya Kanuni ya 6 (1) za kanuni Mama ya VPL inayozungumzia Viwanja kadhalika kusomwa pamoja na Kanuni ya 11 inayozungumzia Leseni za Klabu kwamba kila timu haina budi kuwa na viwanja vya mcehi za nyumbani ikiwa ni masharti ya kupata leseni ya klabu.

SEMINA YA MADAKTARI WA TIMU ZA LIGI KUU BARA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeita semina ya siku moja kwa Madaktari wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayofanyika Ijumaa Agosti 4, mwaka huu kuanzia saa 2.00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 73 ya Ligi Kuu, kila klabu ya Ligi Kuu inatakiwa kuwa na daktari wa timu ambaye pamoja na mambo mengine atahakiki afya za wachezaji na viongozi wa timu.
Kila klabu inatakiwa kuhakikisha daktari wake anahudhuria semina hii muhimu itakayoendeshwa na Kamati ya Tiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Paul Marealle.
Bodi ya Ligi itagharamia nauli ya basi ya kuja na kurudi Dar es Salaam kwa kila mshiriki. Tunawatakia kila la kheri katika maandalizi ya ushiriki wa semina hiyo ambayo ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2017/2018.
  UCHAGUZI MKUU TAFCA AGOSTI 10, 2017
Uchahuzi Mkuu wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA utafanyika Agosti 10, mwaka huu mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi), Ramadhani Mambosasa ametangaza orodha ya majina sita ya mwisho ya wagombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.
Kwa mujibu Mambosasa, wagombea hao kwa sasa hawana budi kuendelea na kampeni hadi Agosti 9, mwaka huu.
Waliopitishwa katika orodha ya mwisho kuwania nafasi mbalimbali za uongozi - ngazi ya taifa ni pamoja na Kidao Wilfred, Lister Manyara, Michael Bundala, Dismas Haonga, Jamhuri Kihwelo, George Komba, Samuel Moja na Maka Mwalwasi na Mohammed Tajdin.
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
……………………………………………………………..………………………………
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

SERIKALI YASAJILI VIWANDA 2,536

$
0
0
Na Bushiri Matenda- MAELEZO

Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji imekanusha taarifa iliyotolewa na uongozi wa CHADEMA kuhusu suala la ubinafsishaji na kuwa hakuna viwanda vipya vilivyojengwa katika awamu hii kwa vile hakuna mkopo wa kuanzisha viwanda .

Taarifa iliyotolewa Jijini Dar es Salam imesema kuwa viwanda vilivyokuwepo viliuzwa kwa bei rahisi kwa kuwa wawekezaji waliovichukua waliingia mikataba ya kuviendeleza na Serikali, hivyo vilichangia mapato ya serikali na kutoa ajira.

Aidha baadhi ya wawekezaji wa viwanda vilivyobinafsishwa waliviendeleza na mpaka sasa vimeendelea kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa nchi. Baadhi ya viwanda hivyo ni kiwanda cha Bia (TBL),KIWANDA CHA Sigara (TCC), viwanda vya saruji vya Mbeya,Tanga na Twiga.

Hata hivyo viwanda vilivyokiuka mkataba vitarudishwa serikalini ili vitangazwe kwa wawekezaji wenye uwezo wa kuviendeleza ili viendelee na uzalishaji ambao utatoa fursa ya ajira na kuingiza mapato serikalini.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kwa kuwa viwanda hivyo vilijengwa kwa fedha za watanzania na kuuzwa kwa wawekezaji ili waviendeleze na wao wakavunja mikataba kwa makusudi nia ya kuvirejesha serikalini haina ubaya wowote.

Serikali imeendelea kujenga viwanda kutokana na kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha za ndani.Viwanda hivyo ni Pipeline industries, Masasi Food Industries na CATA mining Ltd. Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya viwanda 224 vilisajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji (TIC), 41 kupitia Mamlaka ya maeneo maalum ya uwekezaji( EPZA), 128 kupitia BRELA na 2,143 kupitia shirika la viwanda vidogo(SIDO ).

Aidha wizara imetoa tahadhari kwa wawekezaji waliobinafsishiwa viwanda na hawajaviendeleza kuharakisha kuvifufua kwa mujibu wa mikataba yao kwani zoezi la kuvirejesha serikalini limeanza kwa kasi.

Watanzania wametakiwa kuendelea kutumia fursa zilizopo za kujenga viwanda ili kuipeleka nchi yetu katika uchumi wa kati.

WAUZA DAWA FEKI ZA KUUWA WADUDU WA ZAO LA PAMBA KUKIONA –MPINA

$
0
0
NA EVELYN MKOKOI – MWABUSALU MEATU

Hatua kali zitachuliwa kwa wafanyabiashara wanaouza dawa feki za kuuwa wadudu wa zao la Pamba nchini, Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipokuwa akizungmza na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba katika kata ya Mwabusalu Wilayani Meatu Mkoani Simiyu, wakati wa ziara yake jimboni Kisesa.

Mpina alisema kuwa wapo wafayabiashara wanaodhoofisha wakulima wa zao la Pamba kwa kuwauzia madawa yasiyo na nguvu na kutoweza kufanya kazi kabisa katika zao la Pamba na kupelekea kufa kwa zao hilo na kuwataka watu hao kuwaletea wakulima dawa bora kabisa na kinyume na hapo wizara husika itachukua hatua dhidi yao.

Aidha amewataka wakulima wa kijiji hicho kinacholima zao hilo la mfano nakutoa mbegu Bora Pekee ya pamba nchini kuacha kilimo cha mazoea na kutumia fursa hiyo kuangalia kwanza maeneo wanayoishi kutokana na faida itokanayo na biashara ya zao la pamba kuninunulia chakula cha kutosha na kutoka kwenye nyumba za tembe na kujenga nyumba za kisasa.

Sambamba na hilo Mpina amewataka wakulima hao kuzingatia sauala la utunzaji wa mazingira kwa kuyaandaa mashamba yao kwa wakati huku wakizingatia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi wanayokabilina nayo.

Awali, Naibu Waziri Mpina alikitembelea kiwanda cha Pamba cha Geki Investiment limited na kuutaka uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji mapema mwakani ili wakulima wa kata ya Mwabusalu waweze kunufaika kutokanana mauzo ya pamba yao karibu. “Serikali hii inalenga katika kuinua na kuimarisha uchumi wa viwanda hivyo kiwanda hiki sasa wakati umefika wakuanza uzalishaji kisikae hapa na kutumika kama ghala kianze kazi mara moja, vinginevyo hatuta mvumilia muwekezaji huyu kama atashindwa Wizara husika itafanya kazi yake”. Alisisitiza Mpina.

Serikai ya awamu ya tano toka iingie madarakani imepandisha bei ya zao la pamba kutoka bei ya awali ya shilingi 600 kwa kilo mpaka mpaka sh. 1,200 imeelezwa kuwa kata ya Mwabusalu, ni kata ambayo imepata upendeleo kwa wakulima kuuza Pamba hiyo kwa kiasi cha shilingi 1,320 kwa kilo.

Tafiti zinaonyesha kuwa kata ya Mwabusalu inalima Pamba ambayo pamoja namatumizi mengine inatoa Mbegu ambayo inapatika pia katika maeneo mawili tuu nchini yanii mwabusalu na Ingunga Mkoani Tabora.
katika Picha Roli lililobeba pamba za wakulima tayari kwenda kuuzwa
Naibu Waziri Mpina akingalia ubora wa Pamba ya wakulima katika kijiji cha Mwabusalu leo.
Naibu Waziri Mpina akipima furushi la Pamba katika Mzani Maalum kabla ya kuongea na baadhi ya wakulima wa Pamba katika kijiji cha Mwabusalu jimboni kisesa leo.
Baadhi ya wakulima wa Pamba wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (hayupo pichani) alipokuwa akingumzanao katika kijiji cha Mwabusalu mapema leo.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa na baadhi ya wakulima wa zao la Pamba kijijini Mwabusalu, Meatu Mkoani Simiyu leo.

ATE yaanza kundi la pili la Programu ya Mwanamke wa Wakati Ujao (Female Future)

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Plc, Sabasaba Moshingi (katikati) akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya miezi tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao ya kundi la pili yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bi. Jayne Nyimbo (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya Sheria ya ATE, Suzan Ndomba (kushoto) ma Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka (katikati), wakifurahi na Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na maendeleo wa Acacia Mining, Janeth Lekashingo katika hafla hiyo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bi. Jayne Nyimbo (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzu wa Kampuni ya Statoil Tz,  Gunnar Mentzsen    huku Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akiangalia  wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya  program ya Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam.

 Mhadhiri wa Taasisi ya  Uongozi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI), Prof. Apollonia Kerenge (kulia), akizungumza na washiriki wa kundi la pili wa mafunzo ya miezi tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  kwa kushirikiana na Shireikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa wafanyakazi wanawake  kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.  

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate, Frank Mugeta (kulia), akizungumza na washiriki  wa mafunzo ya miezi tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE)  kwa kushirikiana na Shireikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam juzi. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa wafanyakazi wanawake  kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.   
 Mratibu wa Program ya Mwanamke wa Wakati Ujao ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Lilian Machera akizungumza na washiriki hao kuhusu utaratibu wa mafunzo hayo yenye malengo ya kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.   


 Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya program ya Wanawake wa Wakati Ujao, Bi. Anna Nyimbo akijitambulisha kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo yatakayochukua kipindi cha miezi tisa.  

Washiriki wa kundi la pili la mafunzo ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya viongozi wa ATE pamoja na wakurugenzi wa makampuni 16 yanayofadhili mafunzo hayo. Makampuni hayo ni; Acacia Mining, Alistair Equipment Services (T) Ltd, AngloGold Ashanti, Geita Gold Mine, Cartrack Tanzania Limited, EFC Microfinance Bank, Ubalozi wa Denmark, Global Health Program-Tanzania, HJFMRI, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  Benki ya NMB Plc, Mfuko wa PPF , Songas Limited, Benki ya Standard Chartered, Statoil Tanzania AS, Benki ya TIB Corporate, Benki ya TPB Bank Plc na Under The Same Sun.

Uchumi wa Tanzania Waendelea Kuimarika-Dkt. Abbasi

$
0
0










Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Sehemu ya Habari na Picha Bw. Rodney Thadeus.





Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu hali ya uchumi mbele ya waandishi wa habari leo Jijiji Dar es Salaam.



Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu hali ya uchumi wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: MAELEZO


By Bushiri Matenda-MAELEZO

Licha ya kuyumba kwa uchumi na kuongezeka kwa mfumuko wa bei duniani, Tanzania imeendelea kuongoza kwa ukuaji wa uchumi miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) zimetaja uchumi wa Tanzania kuwa imara.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alibainisha hayo wakati akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya uchumi nchini.

“Uchumi wa Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo sasa bado uko katika ukuaji usiopungua asilimia 7.0 hadi 7.2 ikiwa ni ukuaji wa juu katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Rwanda inakua kwa asilimia 6, Uganda asilimia 5 na Kenya asilimia 6.4”, alisema Dkt. Abbasi.

Alieleza kuwa sambamba na ukuaji wa uchumi, Tanzania imeendelea kudhibiti mfumuko wa bei ambapo taarifa ya hivi karibuni zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonesha kuwa mfumuko wa bei nchini umeshuka kutoka asilimia 6.1 mwezi Mei hadi kufikia asilimia 5.4 mwezi Juni mwaka huu.

Aidha, Mkurugenzi Dkt. Abbasi alieleza kuwa katika eneo la mazingira bora ya uwekezaji, Tanzania imeendelea kufanya vizuri ambapo alitoa takwimu za taasisi ya Quantum Global Research Lab ya Uingereza kuhusu Farihisi ya Uwekezaji Afrika ambazo zilionesha Tanzania ikiongoza miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki na ya nane Barani Afrika, ikiwa imepanda kutoka nafasi ya 19 mwaka 2015.

“Mashirika ya Kimataifa kama IMF, Benki ya Dunia katika ripoti zao za hivi karibuni yamesisitiza kuwa uchumi wa Tanzania ni imara na wamesifu mageuzi makubwa yanayofanywa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli”, alieleza Dkt. Abbasi na kusema kuwa mashirika hayo yameitaka Serikali iendeleze mapambano zaidi dhidi rushwa na udhibiti wa mapato ya Serikali.

Alieleza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kufanyia kazi maoni hayo ya IMF na Benki ya Dunia na kwamba mabadiliko makubwa yamefanyika katika kupambana na rushwa na kudhibiti mapato ya Serikali ambapo ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa shilingi bilioni 925 kwa mwaka 2015 hadi shilingi trilioni 1.069 kwa mwaka 2016/17 ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.


Dkt. Abassi ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, alieleza kuwa kutokana na uchumi wa Tanzania kuwa imara kumeiwezesha Serikali kufanya maboresho makubwa katika sekta mbalimali zikiwemo afya, elimu, miundombinu na nishati ambapo katika sekta ya afya Serikali imetenga shilingi trilioni 1.077 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kulinganisha na shilingi bilioni 796 zilizotengwa mwaka fedha 2016/17.

Alieleza kwa kwa upande dawa na vifaa tiba, Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kutekeleza ahadi yake kwa kuongeza fedha katika ununuzi wa dawa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu fedha za ununuzi wa dawa na vifaa tiba zimeongezea kutoaka shilingi bilioni 30 mwaka 2015/16 mpaka kufikia shilingi bilioni 261 katika bajeti ya mwaka 2017/18.

“Katika kuhakikisha Watanzania wengi wanaelimika, Serikali imeendelea kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ambapo takribani shilingi bilioni 18 hutumika kwa mwezi na zinawafikia walengwa na kwa wakati”, alieleza Dkt. Abbasi na kuongeza kuwa wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani kulikuwa na shilingi bilioni 341 kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu lakini Rais John Pombe Magufuli akaongeza hadi kufikia shilingi bilioni 475 na kwa mwaka 2016/17 bajeti ya mikopo ya elimu juu iliongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 483.

Alieleza kuwa kutokana na uchumi imara, Tanzania imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo ikiwemo ile ya umeme, maji, reli ya kisasa, barabara na pia mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mapka Tanga nchini Tanzania, ambapo mradi huu unatekelezwa kwa pamoja na nchi hizo mbili.

Changamkieni fursa Mradi wa Bomba la Mafuta – Dkt. Pallangyo

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari na mwongozaji wa kipindi cha 360 cha Clouds TV, Hassan Ngoma katika mahojiano maalum kuhusu uzinduzi wa mradi wa wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu yaliyofanyika mapema Julai 31, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwandishi wa habari na mwongozaji wa kipindi cha 360 cha Clouds TV, Hassan Ngoma akiuliza swali kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia) kwenye mahojiano hayo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amewataka wananchi wanaoishi katika mikoa itakayopitiwa na miundombinu ya bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika Bandari ya Tanga nchini Tanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

Dkt. Pallangyo aliyasema hayo mapema jana jijini Dar es Salaam kupitia kipindi maalum cha 360 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds wakati akielezea maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania unaotarajiwa kufanyika Agosti 05, mwaka huu.

Alisema kuwa wananchi katika maeneo husika wanatakiwa kujiandaa kwa ajira wakati wa maandalizi na utekelezaji wa mradi, ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali za vyakula, usafiri na ufundi.

“Fursa zitakazokuwepo ni nyingi mno, vijana waliomaliza Vyuo vya Ufundi wataweza kufanya kazi za uchomeleaji wa vyuma, madereva wenye leseni kupata kazi, wakina mama lishe kuuza vyakula, wakulima kuuza mazao kwa walaji watakaoongezeka kutokana na uwepo wa mradi huo, alisema Dkt. Pallangyo.

Akielezea manufaa ya mradi huo, Dkt. Pallangyo alieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaleta mabadiliko ya kiuchumi katika nchi za Uganda na Tanzania.Alisisitiza kuwa mradi utatoa takribani ajira 10,000 na kufungua fursa za biashara katika mikoa itakayopitiwa na mradi

“Mradi utapelekea kufunguka kwa Ukanda wa Biashara kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kama vile Rwanda, Burundi, Kongo, Sudan ambapo wanaweza kuunganishwa na miundombinu hiyo na kusafirisha mafuta kwa urahisi,” alisisitiza Dkt. Pallangyo.

Aliendelea kusema kuwa, kukamilika kwa mradi huo nchi za Tanzania na Uganda zitapata mapato na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wake.Dkt. Pallangyo alieleza faida nyingine kuwa ni pamoja na gharama za mafuta kupungua kutokana na nchi za Afrika Mashariki kutumia mafuta yake yenyewe kwenye magari pamoja na ndege hivyo kuchochea kasi ya utalii katika nchi husika pamoja na ajira.

Awali akielezea mradi huo, Dkt. Pallangyo alisema kuwa mradi ulikuwa na ushindani mkubwa hata hivyo bado ilionekana Tanzania kuwa na vigezo vya bomba hilo kupita katika sehemu kubwa ya ardhi yake ambapo alieleza vigezo hivyo kuwa ni pamoja na hali ya tambarare katika ardhi ya Tanzania hivyo gharama za uwekezaji kuwa rahisi.

Aliongeza kuwa ardhi ya Tanzania ni rahisi pamoja na kuwepo kwa hifadhi ya barabara katika maeneo mengi hali inayopelekea gharama za fidia kuwa ndogo.Dkt. Pallangyo alieleza vigezo vingine kuwa ni pamoja na Tanzania kuwa na uzoefu mkubwa katika usimamizi wa bomba la Mafuta la TAZAMA na la Gesi linalotoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam.

“Pia bandari ya Tanga imeonekana inafaa kwa kuwa itawezesha mafuta kusafirishwa kwa mwaka mzima bila tatizo lolote,” alisema Dkt. Pallangyo.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MTAMBO WA KUSAFISHA DHAHABU CHUNYA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea na kujionea mtambo wa kisasa wa kusafisha dhahabu kwa asilimia 99 unaomilikiwa na kampuni ya Sunshine Group uliopo katika kata ya Matundasi wilayani Chunya mkoani Mbeya.

Ametembelea mtambo huo leo (Jumanne, Agosti 1, 2017) wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya na kusema kuwa mtambo huo ni wa kwanza kuweza kusafisha dhahabu kwa kiwango hicho hapa nchini.

Amesema kwa Tanzania kampuni ya Sunshine Group ndiyo yenye mtambo wa kuweza kusafisha dhahabu na kufikia asilimia 99 ukilinganisha na makampuni mengine yanayomiliki migodi.Pia Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia makinikia ili kuweza kusafirisha dhahabu halisi.

Naye Ofisa Madini Mkoa wa Mbeya, Mhadisi Said Makwama amesema dhahabu inayosafishwa katika mtambo huo ikipelekwa nje ya nchi inaingizwa sokoni moja kwa moja tofauti na migodi mingine.

Mhandisi huyo alisema Sheria mpya ya Madini imesaidia Serikali kupata kodi ya juu itokanayo na Mrabaha wa asilimia 6 na ‘clearance and inspection fee’ ya asilimia moja ya thamani ya madini yanayosafirishwa ukilinganisha na mrabaha wa awali wa asilimia nne.

“Uzalishaji uliofanyika kwa mwezi Julai tu Serikali imepata mrabaha wa sh. milioni 333 ukilinganisha na sheria ya zamani Serikali ingepata shilingi milioni 191. Sheria mpya imewezesha Serikali kupata mapato zaidi ya sh. milioni 142. Awali ilikuwa inapata sh. milioni 191 kwa gramu 52. 518 kwa mgodi mmoja wa Sunshine.”

Kwa upande wake mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Victor Mwambalaswa ameiomba Serikali kukubali maombi ya Kampuni ya Sunshine ya kujenga mtambo wa kuchenjulia mabaki ya mchanga wa dhahabu wilayani Chunya ili kuweza kuongeza fursa za ajira, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sunshine Group Bw Leo Le alisema kampuni ya Sunshine Group ni ni miongoni mwa makampuni makubwa kutoka nchini China yaliyowekeza Tanzania, ambapo thamani ya uwekezaji wao ni zaidi ya Dola za Marekani milioni 100.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


JUMANNE, AGOSTI 1, 2017

Kuwait Yatoa Vifaa Vya Upasuaji Vyenye Thamani Ya Shilingi Mil. 325

$
0
0
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kulia) akiangalia baadhi ya zawadi za watoto wenye matatizo ya moyo toka kwa Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem (kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem (katikati) akimkabidhi mmoja ya watoto wenye matatizo ya moyo zawadi ya madaftari wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (kulia) akimkabidhi mmoja ya watoto wenye matatizo ya moyo zawadi ya madaftari wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wazazi wenye watoto wenye matatizo ya moyo wakati wa hafla ya kupokea vifaa tiba toka Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.

Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

…………………………….

Na Thobias Robert- MAELEZO

Serikali ya Kuwait imetoa msaada wa vifaa vya upasuaji vyenye thamani ya Shilingi Milioni 325kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kuboresha huduma za upasuaji katika Taasisi hiyo.

Hayo yamebainishwa leo, Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al Najem wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Taasisi hiyo.

“Leo tumekuja hapa kutoa msaada wa vifaa vya upasuaji kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, lakini pia Serikali ya Kuwait itatoa msaada wa zaidi ya dola milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Mnazi Mmoja Visiwani Zanzibar,” amesema Balozi Jasem.

Ameongeza kwa kueleza kuwa Serikali ya nchi yake kupitia shirika lisilo la kiserikali la Help Patient Society litasaidia kutoa msaada wa damu salama katika Taasisi ya Mifupa (MOI) na kwamba zoezi hilo litafanyika mwezi huu wa Agosti.

Vile vile amesema kuwa Kuwait inatarajia kutoa mabeseni 1,000 yenye vifaa mbalimbali vya kujifungulia kwa ajili ya mama na mtoto katika hospitali mbalimbali za Serikali hapa nchini, ambapo mpaka sasa mabeseni 250 yameshatolewa kwa hospitali za Mbagala Zakhem na Mkurunga.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada huo ambao utaimarisha utoaji wa huduma katika Taasisi hiyo.

Aidha amesema kuwa, msaada huo uliotolewa na Serikali ya Kuwait utasaidia utoaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa sita kwa siku kutoka idadi ya wagonjwa watatu iliyokuwepo hapo awali.

“Ninaridhishwa na huduma zinazotolewa na JKCI, ambapo kwa sasa tumepunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya Nchi hasa wagonjwa wa Moyo, kutoka wagonjwa 85 mwaka 2015/2016 hadi Wagonjwa 17 kwa mwaka 2016/2017,” ameeleza Ummy.

Ameendelea kwa kusema kuwa, hapo awali Taasisi hiyo ilikuwa ikifanya upasuaji wa wagonjwa 15 kwa mwezi lakini kwa sasa inatoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa 30 kwa mwezi. Kuongezeka kwa vifaa vilivyotolewa na Serikali ya Kuwait vitaongeza utoaji wa huduma ya upasuaji kwa zaidi ya wagonjwa 120 kwa mwezi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janubi amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Taaasisi hiyo mwaka 2005 imesaidia kutoa huduma ya upasuaji kwa zaidi ya wagonjwa 700. Hivyo kutolewa kwa msaada wa vifaa vipya utasadia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa ambao hawajapata huduma hiyo kwa wakati.

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa msaada kwa Wananchi wa Tanzania lakini pia hata kwa Mataifa ya nje ikiwemo Kenya, Uganda na Malawi ambao wanaitumia Taasisi hiyo kama hospitali ya Rufaa.

Tigo yafungua duka kubwa, la kisasa Dodoma

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma, Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa usimamizi na masuala ya kiserikali wa Tigo,Sylvia Balwire, Meneja usimamizi wa wateja wa Tigo kanda kaskazini, Vitalis Stephen na kushoto ni George Lugata mkurugenzi wa Tigo kanda kaskazini.

Meneja usimamizi wa wateja wa Tigo kanda kaskazini, Vitalis Stephen akimuonesha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari baadhi ya simu zinazouzwa kwenye duka jipya la kisasa lililozinduliwa leo mkoani Dodoma . Pembeni ni mkuu wa huduma kwa wateja wa Tigo Dodoma,Scolastica Kisori.
Mteja akipata huduma mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma,
Mteja akipata huduma mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la kisasa lililofunguliwa leo mkoani Dodoma,


Dodoma, Agosti 1, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali, Tigo Tanzania imeendelea kuishi kulingana na ahadi yake ya kuwapatia wateja huduma wanazozifikia kwa urahisi zaidi kwa huduma za Tigo kwa kufungua duka la huduma kwa wateja ambalo ni jipya lililofamnyiwa ukarabati mkubwa leo katikati ya jiji la Dodoma .

Akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi wa duka, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema duka iliyofanyiwa ukarabati ikiwa ni mkakati wa upanuzi wa kampuni wa kuzileta bidhaa na huduma zake sehemu moja.

Duka hilo jipya lililokarabatiwa miongoni mwa vitu vilivyomo ni pamoja na sehemu ya watu mashuhuri (VIP) kwa ajili ya kuhudumia wateja ambao ni VIP na wale wanaohitaji huduma za ufuatiliaji wa kasi, kaunta zimeongezwa na eneo la kufanyia majaribio ambapo wateja wanaoingia wanaweza kufurahia uzoefu wa kwanza wa kujifunza jinsi ya kutumia bidhaa za Tigo kama vile simu za kisasa (smartphones) na bidhaa na huduma nyingine za mtindo wa maisha ya kidijitali kama vile Tigo Pesa ambazo zinatolewa na kampuni.

'Tigo imepania kutumia rasilimali zake zote ikatika kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma za daraja la juu duniani, kuhakikisha ufanisi, wakati halisi wa majibu kwa maswali yao katika maduka yetu yote 52 ya huduma za wateja yaliyopo nchini, "alisema Karikari, na kuongeza kuwa duka hilo mpya Iimewekwa vifaa vya kisasa, likihudumiwa na wafanyakazi waliopata mafunzo sawasawa na ambao ni wachapa kazi ambao wako tayari kutoa huduma bora kwa idadi ya watu inayoongezeka kwa haraka jijini humo.

Akizungumza juu ya uendeshaji wake, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata alisema kuwa duka hilo jipya la Tigo mpya litakuwa wazi siku zote saba za wiki.

"Kimkakati kuwepo kwa duka hilo eneo la katikati ya jiji kunafanya iwe rahisi kufikiwa na wakazi wa mji wa Dodoma, maeneo jirani na watu wanaotembelea kitovu hicho cha nchi, " aliongeza Lugata.

Aliendelea kufafanua zaidi kuwa duka kubwa, la kisasa limekuwa pia linaenda bega kwa bega na mkakati wa Tigo kupeleka huduma kwa wateja kwa wakazi wa Dodoma kama mji ambao unatarajia kuwa ‘ mlipuko’ wa idadi ya watu kufuatia uamuzi wa serikali kuhamishia shughuli zake za kiutawala kutoka Dar es Salaam , na hivyo kufanya mji wa Dodoma makao makuu ya nchi.

Duka lipo mkabala na mzunguko wa CDA kwenye sakafu ya chini ya Jengo la CDA Barabara ya Uhindini katika Manispaa ya Dodoma, na linatarajiwa kuhudumia wateja zaidi ya 300 kwa siku.

VIKOSI VYA MAJESHI YA SADC KUFANYA ZOEZI LA PAMOJA MKOANI TANGA

$
0
0

Msimamizi wa Zoezi la pamoja kwa vikosi maalumu vya Majeshi
ya SADC ambalo limepewa jina la Matumbawe,Meja Generali Harison Msebu katika kupambana na matishio mbalimbali ya usalama kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanza zoezi hilo ambalo litaanza Agosti 2 hadi Septemba 1 Jijini Tanga,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

VIKOSI vya Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwaafrika (SADC SPECIAL FORECES) vimeamua kupambana na ugaidi,Uharamia kwa kushirikiana kufanya zoezi la pamoja lililopewa jina la “EX MATUMBAWE” ikiwa ni mkakati wa kutokomeza vitendo hivyo. 

Zoezi hilo litakaloshirikisha vikosi vya Makomandoo, Ndege za
kivita,meli za kivita na makomandoo watakao ruka na miavuli huku wote kwa pamoja kutoka nchi zote shiriki watafanya mazoezi hayo kubadilishana uzoefu litafanyika kuanzia Agosti 2 mpaka Septemba 1 mwaka huu katika maeneo ya Mapango ya Mleni. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga,Msimamizi wa Mazoezi hayo,Meja Generali Harison Msebu alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni kufanya mazoezi ya pamoja kwa vikosi maalumu vya Majeshi ya SADC,ili kuviwezesha kuwa na utayari na harakati katika kupambana na matishio mbalimbali ya usalama. 

Aidha alisema kuwa kutasaidia kuviwezesha vikosi hivyo kukabiliana na masuala ya Ugaidi,Uharamia na maafa yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia vikundi vya kulinda amani kama ilivyoelekezwa na Jumuiya ya SADC pamoja na umoja wa Afrika (AU).

Alisema Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Mwaafrika zimejiwekea mikakati ya kuondoa uhasama wao na zaidi kuunganisha mahusiano ikiwa na lengo la kupambana mambo ambayo yanaweza kuleta madhara katika nchi zote za Jumuiya hiyo na Afrika kwa ujumla.

Alisema yapo madhumuni ya kimkakati,utendaji kivita na kimbinu haya yote yakitekelezwa kwa ufanisi zaidi kwa nchi zote upo uwezekano wa hali ya juu katika mafanikio ya mapambano ya kigaidi na kiharamia. 

“Tunajenga misingi mizuri kwa majeshi yetu na kuondoa dhana ya kupambana wenyewe kwa wenyewe sasa tunaelekeza nguvu zetu katika mapamabano ya kigaidi na kiharamia zaidi jambo ambalo litasumbu katika nchi hizi za Afrika”Alisema Meja Jenerali Masebu. 

Alisema zoezi hilo litashirikisha Nchi saba za Jumuiya hiyo zikiwa Botswana,Lesotho,Malawi, Jumuiya ya Afrika ya kusini,Zambia, Zimbabwe na Tanzania ambao ndio watakauwa wenyeji katika zoezi hilo ambalo linafanyika hapa kwa mara ya kwanza.

Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigela aliwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi pindi watakapokutana na vikosi hivyo vikiwa vinaendelea na majukumu yao huku akiwataka kutoa ushirikiano pindi watakapo hitajika.
Alisema wananchi wasiokote vitu vyovyote wasivyovielewa na watoe taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kitu ambacho watakiona kinawapa mashaka.


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MHANDISI MAKANI ASISITIZA UTALII WA MISITU YA ASILI NCHINI KAMA CHANZO MUHIMU CHA KUONGEZA PATO LA TAIFA NA JAMII KWA UJUMLA

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU
.........................................................................................
Katika kuhakikisha sekta ya utalii nchini inaendelea kukua kwa kasi, Serikali imesema itaimarisha utalii wa Misitu ya Asili nchini iweze kutoa mchango mkubwa kwenye pato la taifa tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hutegemea zaidi utalii wa wanyamapori.


Hayo yamesemwa jana wilayani Lushoto na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kutatua migogoro mbalimbali ya uhifadhi.


Alisema sekta ya utalii nchini imekuwa ikitegemea sana wanyamapori na kusahau vivutio vingine kama vile misitu ya asili ambayo ndani yake kuna mimea na viumbe hai mbalimbali adimu duniani na ambavyo hupatikana Tanzania pekee.


“Tumezoea zaidi utalii wa wanyamapori, utalii wa misitu unaweza kuzidi hata wa wanyamapori, kwenye misitu yetu ya asili tunajivunia mimea adimu ya asili na viumbe hai mbali mbali kama vile ndege, vyura, vipepeo, mijusi nakadhalika, tunachotakiwa kufanya ni kutunza misitu yote ya asili, tuiboreshe na kuitangaza ili kupata watalii wengi zaidi na pato la taifa liendelee kukua”, alisema Makani.


Kwa mujibu wa tovuti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Tanzania ina jumla ya Hifadhi za Misitu ya Asili 100, idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na hifadhi za taifa ambazo zipo 16 pekee, idadi hiyo kubwa pamoja na upekee wake inatoa fursa pana ya kuendeleza sekta ya utalii nchini.


Akizungumzia mafanikio, Makani alisema sekta hiyo inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni. Alisema pamoja na faida hizo, sekta hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya uharibifu wa misitu ya asili ambayo ni muhimu kutafutiwa suluhu ya kudumu ili kunusuru misitu hiyo.


“Ni lazima tutafute njia endelevu ya ulinzi wa misitu, hatuwezi kuwa na askari wa kutosha, walinzi na mitutu, njia sahihi ni ulinzi shirikishi, tuwaelimishe wananchi umuhimu wa misitu na tuwaeleze watanufaikaje, tofauti na zile faida za ujumla za upatikanaji wa mvua na hali nzuri ya hewa, hii itasaidia sana kuwaleta karibu kwenye uhifadhi wa pamoja”, alisema Makani.


Akizungumza na wananchi wa kijiji Nywelo wilayani humo kuhusu mgogoro wa mpaka baina ya kijiji hicho na shamba la miti Shume, Makani alisema tatizo lililopo ni uelewa tofauti kuhusu mpaka huo baina ya pande hizo mbili,  hivyo akuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kutuma wataalamu wa upimaji waliopima eneo hilo awali waje wafanye uhakiki wa mpaka huo kwa kushirikisha uongozi wa wilaya, halmashauri na kijiji hicho ili kuondoa tofauti hizo na kumaliza mgogoro huo ndani ya wiki mbili zijazo.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Januari Lugangika alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali za uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti ya asili, uchimbaji wa madini kwenye maeneo ya hifadhi, uchomaji moto misitu na uhaba wa watumishi.


Katika ziara yake hiyo wilayani Lushoto, Naibu Waziri Makani alitembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Magamba na Shamba la Miti la Shume, alifanya pia vikao vinne vya ndani na mkutano mmoja wa hadhara ambapo alijibu kero mbalimbali za wananchi.

Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akijibu kero mbalimbali za uhifadhi kwa wananchi wa Kijiji cha Shume Nywelo, Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo jana. 
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kushoto) akisikiliza moja ya kero kuhusu uhifadhi kutoka kwa Abunio Abraham Shangali (wa pili kulia) ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Shume Nywelo, Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga jana wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo. 
 Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kulia) akizungumza na viongozi wa kikundi cha uhifadhi na utalii cha Friends of Usambara kilichopo Lushoto Mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo jana.
Naibu Waziri wa Maliasili, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Januari Sigareti Lugangika katika kijiji cha Shume Nywelo wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutatua migogoro ya hifadhi wilayani humo jana.
Muwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mwalimu Elias Mkwilima akijibu baadhi ya hoja katika mkutano huo uliofanyika katika kijiji cha Nywelo jana wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga.

RAIS DKT MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO ZA MABALOZI WATANO NA AMUAPISHA BALOZI BENEDICT MASHIBA

DAWASCO YASHAURIWA KUTOA HUDUMA KWA UWAZI

$
0
0
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.  PICHA NA KAJUNASON BLOG/MMG.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) wakati wa halfa ya kutangaza DAWASCO kujiandaa kuingia katika mchakato wa Mfumo wa Usimamizi wa Ubora wa Kimataifa (ISO) iliyofanyika katika ofisi yao makao makuu jijini Dar es Salaam.
Watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco).
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja wakiwa na watendaji wengine wakati wakiimba wimbo wa 'Tanzani', 'Tanzania'.
Katibu Mkuu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema ameapa kuwashughulikia watumishi wachache chini ya wizara yake ambao bado wanaendekeza maisha ya ujanja ujanja kazini. Profesa Kitila ameitoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akizungumza na watendaji na mameneja wa Shirika la Maji Safi na Taka Dar es Salaam (Dawasco) kwenye ofisi za makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam. 

Amesema ingawa Dawasco imefanikiwa kuboresha huduma zake, lakini wapo watumishi wa chache ambao bado wanafanya kazi kwa ubabaishaji. Amesisitiza kuwa zama za ujanjaujanja zimekwisha na wale wachache wanaoshiriki mbinu za kulihujumu shirika hilo hawatavumiliwa na watendaji wa shirika hilo kutoa taarifa kwa watakaobainika. 

Wakati huo mhuo, Profesa Mkumbo amewashukuru watendaji na watumishi wa Dawasco akibainisha kuwa siku hizi simu za malalamiko anazopigiwa na wateja kuhusu huduma za maji zinazotolewa na Shirika hilo zimepungua sana. Amesema hali hiyo inatokana na Dawasco kuboresha huduma zake. Amesema hivi sasa anatumiwa ujumbe mfupi wa kupongezwa kuhusu huduma za zinatolewa na Dawasco na kulitaka shirika hilo kuendelea kuchapa kazi ya kutoa ya kuwahudumia wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

 “Hongereni kwa huduma nzuri mnazitoa kwa wakazi wa mikoa hii. Nyie ndiyo taswira ya Serikali katika utoaji wa huduma za maji. Bila nyie Ukatibu wa Mkuu hauna maana kwa mkoa wa Dar es Salaam hata waziri na wizara kwa ujumla,” amesema Profesa Mkumbo. Profesa Mkumbo amesema wizara yake haina mipaka katika utendaji kazi na kwamba ipo wazi kuwasiliana mtendaji yeyote atakayetaka huduma.

PPF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYA SH.MILIONI 6 KWA HALMASHAURI YA MJI MAFINGA

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa na viongozi kutoka mfuko wa pensheni wa PPF wakiwa katika Ardhi ya Hospitali ya halmashauri ya Mji wa Mafinga wakati wa kukabidhi vifaa tiba vyenye dhamani ya shilingi million sits.
 Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa Sambamba n Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga wakati wa kupokea msaada huu mkubwa wa vifaa tiba kutoka PPF
Baadhi ya madiwani na viongozi wa halmashauri ya Mafinga Mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupokea msaada wa vifaa Tiba vyenye thamani ya shilingi million sita kutoka mfuko wa pensheni wa PPF

Na fredy Mgunda, Iringa

Mfuko wa pensheni wa PPF umetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni sita katika hospitali ya halmashauri ya mji wa mafinga mkoani iringa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo afisa mawasiliano kutoka PPF Lulu Mengele alisema kuwa msadaa huo ni muendelezo wa kurudisha huduma kwa wananchi kwa kile wanachochangia kwenye mfuko huo.

"Wananchi ambao wamekuwa wadau wetu wakubwa wamekuwa wakichangia katika mfuko wetu kitu kichosababisha turudishe fadhila kwa kuleta maendeleo ya moja kwa moja kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo serikali imezidiwa na ukiangalia maeneo ya afya ndio imekuwa changamoto kubwa kwa serikali ndio maana tumeanzia huku ili kuisaidia serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John pombe Magufuli"alisema Mengele

Aidha Mengele aliwataka wananchi kujiunga katika mfuko huo wa pensheni ambao umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi hasa kwenye huduma ya afya kwa kuwa bima zao ni za bei nafuu lakini unatibu unachostahili kutokana na bima yako hivyo naomba muendelee kujiunga kwenye mfuko wa PPF kwa usalama wa maisha yenu.

"Ukitoa elfu ishirini tu inakusaidia kupata hudumu nzuri za afya hivyo naomba mjiunge na mfuko huu kwa kuwa ni msaada mkubwa sana kwenu hasa hapa Mafinga ambako kunashughuli nyingi za kijamii ambazo ni hatarishi kwa maisha yenu" alisema Mengele

Naye katibu wa hospitali ya mafinga Bernard Makupa ameshukuru msaada huo wa vifaa tiba kutoka PPF kwa kuwa vifaa hivyo vitakuwa Masada kwa hospitali.

"Tulikuwa na changamoto katika wodi za wazazi nilikuwa na upungufu mkubwa wa vitanda pamoja na magodoro yake hivyo kupata msaada huu unatusaidia kupunguza changamoto hivyo hivyo nawashukuru na kuwapongeza sana PPF kwa kurudi na kutoa huduma kwa jamii husika"alisema Makupa.

Mbunge wa jimbo la mafinga COSATO CHUMI amewashukuru PPF kwa msaada wa vifaa tiba ambavyo vitaendelea kupunguza changamoto zilizopo katika hospitali hivyo.

"Vifaa hivi vya Tiba ni muhimu sana katika idara yetu ya afya kwa kuwa inatupunguzia changamoto kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi na mikoa ya Jirani wanayoitumia hospitali yetu ya Mafinga" alisema Chumi

Chumi aliwataka wananchi wa Mafinga Mjini kujiunga na mfuko huo wa pensheni kwa kuwa unamanufaa mengi sana hasa upande wa afya na ni muhimu kuwa na bimaa ya afya ya PPF kwa kuwa hudama yao ni ya ukahika na salama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga aliwashukuru mfuko wa pensheni wa PPF na mbunge Cosato Chumi kwa msaada huu mkubwa ambao kama halmashauri ingekuwa vigumu kutekeleza kutokana halmashauri hiyo kuwa Mpya.

"Chumi amekuwa mpambanaji mkubwa wa halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa kuleta maendeleo katika idara mbalimbali hivyo tunakuomba uendelee kutusaidia kutatua changamoto za halmashauri hii"alisema Makoga

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATANO LEO AUG 2,2017

Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images