Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

JIMMIE MAGGETTE MILIONEA NA MFANYABIASHARA MAARUFU AMWALIKA MPIGANAJI WETU DAVIS MOSHA KATIKA KUSHEREHEKEA BIRTHDAY YAKE HOLLYWOOD, L.A

$
0
0
Davis Mosha "The CEO", Deo Temba "Mayor wa LA" na milionea Jimmie Maggette wakiwa katika Supper Club Hollywood jana usiku kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa tajiri Jimmie ambaye ni mdogo wa mcheza basketball maarufu na tajiri Corey Maggette. MC wa party alikuwa mwanamuziki maarufu J Cole. Wamarekani weusi wanajisikia proud sana wanapokutana na successful people kutoka Afrika.

The CEO Davis Mosha, D. Temba, Jimmie Maggettte na Alex King.
 Deo Temba "Mayor wa L.A." katikati ni Mlinzi (BodyGuard) wa Davis Mosha " The CEO"

Baada ya The CEO Davis Mosha kukubali mwaliko wa Jimmie Maggette alitumiwa mlinzi maalum (Body Guard) wa kumlinda, maana sehemu hiyo hawaendi watu wa kawaida, lazima uwe na mlinzi. Hapa Boss Mosha akiteta jambo na Body Guard wake.

   Mayor wa L.A. Deo Temba akikaribishwa kwenye gari na Boss Mosha

Ricardo Emmanuel Brown Rapper maarufu na aliyewahi kuwa Excutive Vice President wa Death Row records, jina la kisanii  Kurupt aka Kurupt tha Kingpin, aka Kurupt young Gotti au Young Gostra, ni member wa kundi kali la hip-hop la Tha Dogg Pound na HRSMN akiwa na The CEO Davis Mosha katika birthday party ya Jimmie Maggette Super Club, Hollywood Los Angeles.
  Deo Temba "L.A Mayor," Davis Mosha" The CEO" na Comedian Maarufu Funny Man Red Grant

Alex King na tajiri na mmiliki wa Kiota maarufu cha R n B LIVe Hollywood. L.A.

 Bathroom ina kila aina ya perfumes, zote expensive ukiingia lazima utoke na unyunyu mpya na pipi za bei ghali.

 Alex king akiwa na Bodyguard wa Davis Mosha Super club L.A.
PICHA ZOTE NA SWAHILI TV 
kwa picha zaidi tembelea www.swahilitv.blogspot.com


MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU JIJINI NAIROBI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake kutoka nchi za Maziwa Makuu, wakati walipokuwa katika Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Maziwa Makuu, alipoiwakilisha Tanzania katika majadiliano ya mkutano huo uliofanyika Jijini Nairobi, nchini Kenya jana Julai 31, 2013. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mkewe Mama Asha Bilal, (wa pili kulia) Balozi wa Tanzania Nchini Kenya, Dk. Batrida Burian, na viongozi wengine wakati alipowasili Jijini Nairobi juzi Julai 30, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu, uliofanyika Jiji humo jana Julai, 31, 2013. Makamu anaondoka leo Jijini Nairobi kurejea nchini baada ya kumalizika kwa majadiliano hayo. Picha na OMR  

===========   ========  =========
MAKAMU WA RAIS AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU JIJINI NAIROBI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika jijini Nairobi Kenya, jana Jumatano ya tarehe 31, 2013. Mkutano huu ulihudhuriwa na Mwenyeji wa Mkutano huo, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Mwenyekiti wa nchi za Maziwa Makuu na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, Katibu Mtendaji wa Kamisheni yas Nchi za Maziwa Makuu Prof.Ntumba Luaba, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, wawakilishi wan chi za DRC, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.

Mkutano huo umepokea taarifa kutoka kwa Mawaziri wa Ulinzi kutoka katika nchi za Maziwa Makuu ambayo imepokelewa na kisha kujadiliwa. Pia ripoti kutoka kwa Kamati ya Kimataifa inayoshughulikia suala la Mazungumzo kati ya Serikali ya Kongo (DRC) na wapiganaji wa kikundi cha M23 kinachojihusisha na upingaji wa serikali ya DRC kikifanya machafuko katika Mashariki mwa Kongo (DRC) imepokelewa kujadiliwa na kisha kupitishwa mapendekezo ambayo nchi washiriki zimeyasaini.
Wakati wa uzinduzi wa mkutano huo, nchi washirika walisisitiza kutaka kuona amani inapatikana katika nchi za Maziwa Makuu na hasa DRC, Afrika ya Kati na Sudan. Wawakilishi hao walielezea kusikitika kwao kutokana na machafuko ya amani katika nchi hizo na wakawataka viongozi mbalimbali wanaotajwa kuhusika na machafuko haya kutambua kuwa athari inayotokana na machafuko haya ni kubwa na inaathiri wananchi wengi.
Viongozi hao walisema, nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu zinahitaji utulivu na kwamba mgogoro wa uvunjaji amani katika Kongo DRC unaotokana na kuwepo kwa kikundi cha M23, lazima upewe tiba ya kudumu ili eneo hilo libakie tulivu na watu wake waweze kupata fursa ya utulivu utakjaowasaidia kushiriki katika kazi zao za kila siku.

Akifunga mkutano huo kwa niaba ya Mwenyekiti Yoweri Museveni, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alisema ni wakati sasa nchi za Maziwa Makuu kutambua na kuazimia kwa kauli moja kuwa amani inahitajika katika nchi zote za ukanda huu. Akifafanua zaidi Mheshimiwa Rais Kenyatta alisema wananchi wa ukanda huu wanataka ajira na sio mapigano.

“Hata vijana wanaotumika katika mapigano, tukumbuke kuwa baada ya mapigano watakachohitaji ni ajira. Akina mama na watoto wanataka kuona maisha yao yanaboreshwa na sio vionginevyo. Kwa namna nilivyoona tukishiriki katika mkutano huu ni dhaihiri tumeonesha nia ya dhati ya kuhakikisha maeneo yetu yanakuwa na amani. Tudumishe nia hii nzuri,” alisema Rais Kenyatta.
Makamu wa Rais na msafara wake wanarejea nyumbani leo Alhamisi Agosti Mosi, 2013 tayari kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Nairobi, Kenya
Agosti 01, 2013

Breastfeeding is the cheapest and most effective life-saver in history – UNICEF

$
0
0


NEW YORK, 1 August 2013 – During World Breastfeeding Week starting today, UNICEF is focusing on breastfeeding as the most effective and inexpensive way of saving a child’s life. But with less than half of all children under six months benefitting from exclusive breastfeeding, strong leadership in promoting the practice is essential.


“There is no other single health intervention that has such a high impact for babies and mothers as breastfeeding and which costs so little for governments,” said UNICEF Deputy Executive Director Geeta Rao Gupta. “Breastfeeding is a baby’s ‘first immunization’ and the most effective and inexpensive life-saver ever.”


Children who are exclusively breastfed are 14 times more likely to survive the first six months of life than non-breastfed children. Starting breastfeeding in the first day after birth can reduce the risk of new-born death by up to 45 per cent.


Breastfeeding also supports a child’s ability to learn and helps prevent obesity and chronic diseases later in life. Recent studies in the United States and United Kingdom point to large health care savings resulting from breastfeeding, given that breastfed children fall ill much less often than non-breastfed children.


Apart from the benefits to the baby, mothers who breastfeed exclusively are less likely to become pregnant in the first six months following delivery, recover faster from giving birth, and return to their pre-pregnancy weight sooner. Evidence shows that they experience less post-partum depression and also have a lower risk of ovarian and breast cancers later in life.


Despite these well documented benefits of breastfeeding worldwide, only 39 per cent of children aged less than six months were exclusively breastfed in 2012. This global figure has improved very little for the past several decades, due in part to large countries where the breastfeeding rate is low, and to the general lack of a supportive environment for breastfeeding mothers.

 
However, countries with supportive policies and comprehensive programmes that reach all communities have been able to increase their breastfeeding rates significantly.


China, which recently attracted media attention because its strong consumer demand for baby formula caused shortages in other countries, has an exclusive breastfeeding rate of only 28 per cent.


In a bid to boost such low rates in the world’s most populous country, UNICEF and the National Centre for Women’s and Children’s Health in May launched a “10m2of Love” campaign to locate, register, certify and publicize breastfeeding rooms in order to raise awareness and support for breastfeeding.


The campaign has established a web portal (unicef.cn/10m2) where any organization can register breastfeeding rooms for staff, patrons or customers that adhere to simple international standards. A mobile phone application to map the locations of all 10m2of Lovefacilities is under development


Cambodia has had notable success in raising exclusive breastfeeding rates from 11.7 per cent of infants less than six months in 2000 to a very high 74 per cent in 2010. Togo and Zambia also increased the rates from 10 and 20 per cent respectively in the late 1990s to over 60 per cent by 2000.


At the other end of the scale, Tunisia’s exclusive breastfeeding rate fell dramatically from 46.5 per cent in 2000 to only 6.2 per cent by the end of the decade.


The exclusive breastfeeding rate in Indonesia is declining; Nigeria has made no improvement over many years; and some of the lowest rates in the world are in Somalia, Chad and South Africa.


Such examples reflect insufficient global leadership on breastfeeding, as it continues to be undervalued relative to its importance in the life of child. There needs to be higher prioritization and commitment, targeted policies and greater consensus to engage the world in promoting this life-saving and vital practice.


Although breastfeeding is natural and may seem instinctive, it is essential to create an enabling environment for it to become the norm.  Mothers benefit from the help of skilled health providers and community workers to support them to breastfeed, as well as culturally-sensitive communication, and protective laws and policies, particularly around the marketing of breastmilk substitutes and maternity leave.



UNICEF campaigns for exclusive breastfeeding for the first six months and continued breastfeeding for two years or beyond, using creative tactics to draw attention to the issue. It recently rolled out a campaign in Uruguay and Argentina, “Giving the breast is giving the best of you,” starring Uruguayan actress Natalia Oreiro, aiming to boost breastfeeding among working mothers.

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA KAMPUNI YA BIA (TBL) MBEYA

$
0
0

Meneja uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na waandishi wa habari
Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera, akielezea mafanikio ya kampuni ya Bia.

Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.


Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.

Baada ya kutembelea kiwanda  sasa ilifika wakati wa kuonja Bia na kuitambua radha yake.


Unaonja na kutaja ni bia gani kama ni NDOVU au KILIMANJARO kunaalama za rangi zimewekwa katika grass
Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akionja na kujaza katika fomu kuwa hiyo aliyoinja ni Bia gani
 Meneja kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi zawadi Joseph mwaisango mara baada ya kuibuka mshindi wa uwonjaji bia
 Meneja kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akimkabidhi zawadi Emmanuel Madafa baada ya kushinda uonjaji wa Bia
Mshindi wa pili Joachim Nyambo akipokea zawadi yake toka kwa meneja wa kampuni ya bia 
Picha ya pamoja


ZAIDI ya Tani 60,000 za Shayiri  zinatarajiwa kuvunwa kutoka kwa Wakulima wa  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini baada ya kupatiwa mafunzo juu ya kilimo cha mazao yenye tija na uwepo wa soko la uhakika.

Aidha zaidi ya Wakulima 400 kutoka Kanda hiyo ndiyo walionufaika na Kilimo hicho na kujihakikishia Soko la zao ambalo hutumika zaidi katika utengenezaji wa Vinywaji moto ambavyo ni Bia na uzalishaji mwingine kutokana na uwepo wa Viwanda vikubwa vya kuzalisha vinywaji hivyo.

Hayo yalibainishwa juzi na Meneja masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kanda ya Mbeya, Raymond  Degera,wakati wa Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kiwanda cha Bia kilichopo Iyunga Jijini Mbeya.

Alisema  kutokana na uwepo wa Kiwanda cha Bia Mkoani Mbeya na kuhudumia Wananchi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini waliona si vema Malighafi zikatoka Nje ya Mikoa hiyo ili hali ardhi na hali ya Hewa inaruhusu kilimo cha mazao hayo na kuamua kutoa elimu namna ya kunufaika na Kilimo.

Degera alisema Kampuni  ilianzisha Programu ya kuwawezesha Wakulima kuhusu kilimo cha mazao yenye tija ambapo Wakulima wa Wilaya ya Mbozi, Sumbawanga na Iringa wanaofikia 400 ambao waliitikia na kuanza uzalishaji ambao baada ya mavuno kiwanda kitanunua moja kwa moja kutoka kwa wakulima ambao wanatarajia kuvuna Tani 60,000.

Kwa upande wake  Mpishi Mkuu wa Bia wa Kampuni ya Tbl, Tito alisema Sheria za Tanzania zinatakiwa kusimamiwa ipasavyo kuhusu matumizi ya Vilevi kwa kuwashtaki wanaozidisha pombe na wengine wanaokunywa mida ya kazi na kuleta usumbufu kwa wengine.

Alisema Utaratibu wa Nchi zingine  huwalazimisha wananchi wake kutumia Chupa mbili za Bia kwa siku na kwamba anayehitaji kuongeza zaidi ya hapo wauzaji huwakatalia, Sheria ambayo alishauri kutumika ili kuongeza uzalishaji na kuiondoa nchi katika majanga yanayotokana na ushawishi wa Pombe.

Aliongeza kuwa  kama wamiliki na watengenezaji wa Pombe wanahitaji wananchi wanywe kwa utaratibu ili waendelee kuwa wateja wao na  kusaidia kuchangia kodi kwa Taifa kutokana na Kampuni hiyo kuongoza kwa kuchangia kodi katika pato la Taifa.

Aidha katika Ziara hiyo Wanahabari walipata fursa ya kuelezwa sheria za unywaji wa Pombe na madhara yake, umri wa mtu kuanza kunywa pombe pamoja na madhara yake ambapo baada ya zoezi hilo walitembelea maeneo mbali mbali ya Kiwanda hicho.

Mbali na hilo wanahabari hao pia walishindanishwa kuonja Bia na kuzitambua kwa majina zoezi ambalo lilikuwa gumu kwa waandishi wengi huku Waandishi wanne wakiibuka washindi baada ya wawili kushika nafasi ya kuanza kwa kupata alama tatu kati ya Tano ambao ni Emmanuel Madafa na Joseph Mwaisango huku walioshika nafasi ya pili kwa kupata alama mbili kwa tano wakiwa ni Joachim Nyambo na Kenneth Ngelesi.



Waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakitembelea kapuni ya Bia TBL
Moja ya watumishi wa kampuni hiyo ya Bia akiwaeleza waandishi wa habari jinsi bia inavyotengenezwa
Ziara inaendelea
 Meneja kiwanda cha kampuni ya Bia TBL  Mbeya Nicolaus  Kanyamala akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kiwanda hicho.
Baadhi ya wa watumishi wa kampuni ya Bia wakijitambulisha mbele ya waandishi wa habari

TCRA ILIPOKUTANA NA WADAU WA HABARI NA MAWASILIANO HAPA JANA JIJINI DAR

UNIC YAHAMASISHA VILABU VYA KUJISOMEA KWA SHULE ZA MSINGI.

$
0
0
IMG_1445
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akielezea jukumu lao kubwa wao kama Unic ni kuelimisha jamii ambapo kwa kufanya hivyo wamehamasika kuanzisha vilabu vya kujisomea kwa shule za msingi vitakavyowajengea watoto msingi mzuri wa kupenda kujisomea ili kufahamu mambo mengi zaidi yanayoendelea duniani katika nyanja ya Sayansi, Teknolojia na habari.
IMG_1488
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha ( wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga ( wa nne kushoto) wakikabidhi vitabu vya kujisomea kwa walimu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa kushirkiana na Soma Book Café walihamasisha kuanzishwa kwa Klabu za Kujisomea katika shule tatu za msingi ambazo ni Hananasif, Kumbukumbu na Oysterbay ili kujenga tabia ya kujisomea kwa watoto tangu utotoni. Klabu ya Kujisomea ya Shule ya Msingi Oysterbay imezinduliwa rasmi jana tarehe 31 Julai 2013 kwa kukabidhiwa mashelfu na vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Soma Book Café pamoja na Book Aid International kupitia Maktaba Kuu ya Taifa.
IMG_1498
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Stella Vuzo akishiriki zoezi hilo la kukabidhi vitabu kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Oysterbay wakihamasisha wanafunzi kujenga tabia ya kujisomea tangu wakiwa wadogo.
IMG_1494
Afisa Habari wa UNIC Usia Nkhoma Ledama naye alishiriki zoezi hilo.
IMG_1508
Mwalimu Salome Makanza (kushoto) akitoa shukrani kwa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa msaada huo ambapo waliahidi kuleta mabadiliko ya maendeleo kwa wanafunzi wao kujijengea tabia ya kujisomea na hata kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la saba shuleni hapo. Katikati ni Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga.
IMG_1398
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akitoa ushauri wa namna ya upangaji vitabu kwa Msimamizi wa Maktaba ya shule hiyo Mwl. Veronica Kassidy.
IMG_1401
Unic team wakijikumbushia baadhi ya vitabu walivyowahi kuvisoma walipokuwa shule za msingi.
IMG_1415
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay wakichagulia vitabu vya kujisomea katika maktaba ya shule yao.
IMG_1513
Mkurugenzi wa Taasisi ya Soma Book Café , mshiriki katika kuhamasisha uanzishwaji wa Klabu za Kujisomea mashuleni Mama Demere Kitunga na Afisa Habari wa UNIC Stella Vuzo wakiteta jambo na baadhi ya wanafunzi wa shule mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi vitabu wanafunzi hao.

Exim Bank unveils additional ATM facility at Mlimani City

$
0
0

Exim Bank Customer Service Manager Frank Matoro
=========   =========  =======
Exim Bank unveils additional ATM facility at Mlimani City

EXIM Bank Tanzania has unveiled a second Automated Teller Machine (ATM) facility at Mlimani City (Hill Park) in Dar es Salaam as part of the bank’s strategy to offer convenient banking services. The new facility brings the bank’s ATM coverage to 32 in Dar e Salaam region and 52 across the country.

According to a statement release by the bank’s Customer Service Manager Frank Matoro in Dar es Salaam yesterday, the bank is committed to providing tailor-made banking services across the country.

Matoro said the new facility will help shoppers’ access additional funds to enhance their shopping spree at Mlimani City adding customers from other banks with Visa and Master cards can also make use of the facility. He said the bank has already embarked on quality service delivery strategy that seeks to make the bank become Tanzania’s preferred bank by choice.

“We are glad to expand our ATM coverage in Dar es Salaam region today. This step is expression of our commitment to the important growth market of Dar es Salaam region, and at the same time the continuation of our country-wide expansion strategy. “We are optimistic that the new facility will offer flexible banking services to our clients around Mlimani City and surrounding areas,” He said.

Matoro cautioned the bank’s clients to be vigilant with their passwords adding that exposing their passwords puts their money at a greater risk of fraudsters. He said his bank has already introduced a Queue Management System to its key branches with larger number of customer influx in a bid to enhance customer service delivery.

“In addition we have also introduced an Online Chat Service for customers to chat online with the bank’s representatives that will help them their queries / grievances resolved timely,” Matoro said.  Matoro added that the bank also launched a mobile money platform that enables the bank’s customers access to their accounts via mobile phones.

“All these efforts underline our bank’s ongoing commitment to meet increasing customer’s needs for instant and straightforward access to their finances. “We shall continue investing in research to come up with more and convenient ways to serve our clients better,” he said.

Exim Bank presently boasts branch network coverage of 25 branches across the country with two subsidiaries in Djibouti and Comoros.

WASHINDI WA TUZO ZA HABARI ZA TANAPA WAMALIZIA ZIARA YAO KWA KUTEMBELEA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA AFRIKA YA KUSINI (SABC)

$
0
0
3       Meneja Uhusiano wa TANAPA Pascal Shelutete akifanya mahojiano katika Studio za SABC.
4  Festo Sikagonamo wa ITV ambaye ni mshindi wa Tuzo za Habari za TANAPA akiwa katika studio za SABC.5Lilian Shirima wa TBC 1 ambaye ni mshindi wa Tuzo za Habari za TANAPA akiwa katika studio za SABC.6Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja ndani ya chumba cha habari cha SABC na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili Mike Arareng( wa kwanza kushoto)  na mtangazaji wa SABC kutoka Kenya Christina ( wa tatu kushoto).

LINEX AIBUKA NA SINGO YAKE MPYA IITWAYO KIMUGINA.!

$
0
0


HATIMAYE LINEX SUNDAY MJEDA!!  LEO HII AMEACHIA TRACK YAKE MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA” KIMUGINA”, WIMBO HUU MPYA AMBAO UMETENGENEZA KWENYE STUDIO ZA SEDUCTIVE RECORD AMBAYO KWA SASA , STUDIO HII NI GUMZO MTAANI  KWA JINSI INAVYOTENGENEZA NYIMBO  ZILIZOSIMAMA KIKWELIKWELI  CHINI YA PRODUCER  WA UKWELI MR. T  TOUCHES . LINEX KWA MARA NYINGINE TENA ANAONYESHA UFUNDI NA LADHA YA PEKEE YENYE VIONYO VYA HUBA NDANI YAKE….ANAMLALAMIKIA KIMUGINA…MTOTO TOKA KANDA YA ZIWA..! HAKIKA WIMBO HUU NI TASWIRA TOSHA YA LINEX JINSI ANAVYOUMIA KWA MTOTO KIMUGINA. EBU SIKILIZA WIMBO HUU. KWA HISANI YA http://www.annapita.com
.!!.

KARIBU ZuRii FASHION & BEAUTY BOUTIQUE ILIYOPO SINZA LEGHO DAR ES SALAAM.

$
0
0
HABARI NZURI KWA WALE WATEJA WETU VIBONGE aka PLUS SIZE NI KWAMBA MZIGO UMESHAFIKA DUKANI.  KWA WALE KAKA ZETU MNAO TAKA RABA ZA MTOKO ORIGINAL CONVERSE, TOMS NA VANS PIA ZINAPATIKANA. 

WALE WA SIZE NDOGO PIA KUNA NGUO NZURI SANA ZINAPATIKANA.
WAZAZI WAPENDEZESHE PIA WATOTO WAKO NA ZuRii KIDS COLLECTION.
KARIBUNI MJIPATIE VITU VYA SIKUKUU, MAKAZINI, MITOKO NA KANISANI. 

NGUO NZURI, QUALITY NZURI NA BEI NAFUU. 
LOOK GOOD, FEEL GOOD WITH ZuRii FASHION & BEAUTY BOUTIQUE. 
TUNAPATIKANA SIZA LEGHO, NYUMA YA ROMBO GREEN VIEW HOTEL (KUNA KIBAO BARABARNAI PIA). TUPIGIE +255659189769 or WHATSAPP +447404332910 (BUSINESS ONLY). 

NGUO ZA PLUS SIZE ZINAZOPATIKANA NI SIZE 14-20 (UK).  NA SIZE NDOGO NI 8-14 (UK).
KARIBUNI SANA.



WAZIRI MKUU WA THAILAND AONDOKA BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YA SIKU TATU NCHINI

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra wakati wa kuondoka kurejea nyumbani kwa mgeni wake huyo baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini leo Agosti 1, 2013.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini leo Agosti 1, 2013.
 Akiagana na Kamanda wa Mkoa maalumu wa kipolisi wa Dar es salaam Suleiman Kova.PICHA NA IKULU. 
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Uwekezaji na Uwezeshaji), Dkt. Mary Nagu wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini leo Agosti 1, 2013.
Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh Kagasheki, wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini leo Agosti 1, 2013.
 Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra akipeana mikono na Mkuu wa Mkoa wa  Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadick  wakati wa kuondoka kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini leo Agosti 1, 2013. 
Wasanii wakishangilia wakati ndege iliyomchukua Waziri Mkuu wa Thailand Mhe Yingluck Shinwatra ikipaa wakati wa kuondoka kurejea nyumbani kwa mgeni huyo baada ya kuhitimisha kwa mafanikio makubwa ziara rasmi ya siku tatu hapa nchini leo Agosti 1, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Waziri Mkuu wa Thailand kwa maafisa waandamizi mbalimbali wa serikali wakati wa kumsindikiza mgeni huyo aliyehitimisha ziara yake rasmi ya siku tatu nchini mchana huu. Hapo akipeana mkono na Mkumbwa Ally wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
 Akisalimiana na Dr Laurent Ndumbaro
 Akisalimiana na Dr Hamisi Mwinyimvua
 Akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Omar Mjenga
 Akiagana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MAMA WA WATOTO WAWILI WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU LA ARUSHA WALIOLAZWA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI NAIROBI.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Aisha Omari (kushoto) Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao. Katikati ni Balozi wa Tanzania, nchini Kenya, Batrida Buriani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Aisha Omari, Mama wa watoto wawili waanga wa mlipuko wa Bomu la Arusha, Sharifa Jumane (9) na Fatuma Jumanne (8) waliolazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Mama huyo alifika kuzungumza na Makamu akiwa jijini Nairobi leo asubuhi, Agosti 1, 2013 kuelezea hali ya watoto, ambapo pia alitoa shukrani zake kwa Serikali inayoendelea kuwahudumia watoto hao.PICHA NA OMR.

WAZIRI MKUU WA THAILAND BI. SHINAWATRA AMALIZA ZIARA YAKE NCHINI TANZANIA.

$
0
0
  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwapungia mkono kuwaaga baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi wa jiji la Dar es salaam wakipunga mkono kumuaga rasmi Waziri mkuu wa Thailand leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri mkuu wa Thailand Bi.Yingluck Shinawatra katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.
  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) akiwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara akiwa  ameambatana na  mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Kikwete (katikati) . Bi. Shinawatra amemaliza ziara yake  ya siku 3 nchini Tanzania. 

MASIKINI MLIMA WETU KILIMANJARO,BARAFU YOTE YAYEYUKA...!

$
0
0
 Taswira ya Mlima Kilimanjaro inavyoonekana kwa sasa baada ya kuyeyuka Barafu yote, ikiwa imebakia sehemu kidogo tu juu ya Kilele cha Mlima huo, ni kutokana na Mabadiliko ya Tabianchi na uhalibifu wa Mazingira uliokithiri. Picha na www.sufianimafoto.com
 Taswira ya mlima huo na Kilele cha Mlima Kibo. Picha na www.sufianimafoto.com
Mlima Kilimanjaro Kushney, kama unavyoonekana ukiwa hauna Barafu huku iliyobaki ikielekea kumalizika kwa kuyeyuka. Picha na www.sufianimafoto.com

NAPE AKUTANA NA MADIWANI NA WAJUMBE WA KAMATI ZA SIASA BUHIGWE NA KIBONDO

$
0
0
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Ndugu Charles Gishuli .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na madiwani wa CCM na Wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Buhigwe.
 Madiwani na Wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Buhigwe waliohdhuria kikao kilichoongozwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu wa NEC Itikadi  na Uenezi Nape Nnauye akivishwa skafu alipowasili katika ofisi za CCM wilaya ya Kibondo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni katika za ofisi za CCM wilaya ya Kibondo sanjali na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk.Amani Kaborou.
 Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wilaya ya Kibondo wakiwa wamefurika katika ofisi za wilaya ya Kibondo kumsalimia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati mkutano na madiwani na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Kibondo.

HATA KAMA MIMI NI MLEMAVU, KAMWE SITAKI KUWA TEGEMEZI

$
0
0
Bw. Fungo Kamili ambaye ni mlemavu wa mguu, akimwonesha mwandishi wetu miti aina ya mianzi ambayo anaitumia kwa shughuli za utengenezaji wa samani
 
Mara nyingi tumeshuhudia katika jamii watu mbalimbali wenye ulemavu hasa wa viungo wakiwa na mawazo kuwa wao ni watu wakutegemea kutoka kwa watu wengine hasa ambao hawana ulemavu, kwa madai kuwa wao hawawezi chochote zaidi ya kuomba

Na kutokana na kuomba huko kwa kuwa ni hiari ya mtu, wengi wamekuwa wakipata misaada michache ama wakati mwingine kupewa msaada mkubwa lakini hawawezi kusema kuwa wametosheka na badala yake zoezi hilo la kuwa tegemezi linazidi kushika kasi kwao

Ulemavu hutofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine, hapa kwa leo nazungumzia walemavu wale ambao ulemavu wao unawaruhusu kujishughulisha na baadhi ya kazi ambazo zinawaingizia kipato kikubwa kuliko hata wanavyodhania

Bw. Fungo Kamili ni mlemavu wa mguu kutoka wilaya ya Makete mkoani Njombe ambaye alikuwa na mawazo ya kuwa tegemezi toka awali lakini kutokana na ubababishaji uliopo kwenye utegemezi kutoka kwa baadhi ya watu na hata mashirika aliyokuwa akidhania kuwa ni msaada kwake, hivi sasa ameamua kuondokana na utegemezi huo na kuamua kujishughulisha na kazi ambayo inamuingizia kipato kinachomsaidia kuendesha familia yake

Fungo amesema alikuwa anafanya kazi kwenye shirika fulani hapa Makete(jina tunalihifadhi) ambalo lilimkabidhi kitengo cha karakana ya ufundi uashi ambapo kutokana na juhudi zake kitengo hicho kilikuwa kikiingiza zaidi ya milioni 30 kwa mwezi, lakini mshahara wake ulikuwa 80,000/= kwa mwezi, hata kama mapato hayo yataongezeka ama lah

Kutokana na ongezeko hilo la mapato aliamua kuwaomba wahusika wamuongezee mshahara kwa kuwa anayaona mapato anayoingiza ni mengi lakini hakuna aliyeonesha kumjali na badala yake walimpa maneneo matamu ya kumsihi awe mvumilivu ipo siku ataongezewa lakini kila akikumbushia ahadi hiyo aliambulia kupata maneno badala ya vitendo

Kufuatia hali hiyo aliamua kuomba likizo ya bila malipo ya miezi mitatu na hakurudi tena hapo kazini na badala yake aliamua kujiingiza kwenye shughuli binafsi za kutumia ubunifua wake ambazo zilimuingizia fedha za kumtosha tangu alipoacha kazi hadi hivi sasa

Kama ilivyoa ada kuwa kama utaamua kuumiza akili kuwa ufanye shughuli gani ikuingizie kipato kwa haraka na uhakika basi lazima iwe hivyo, kitu ambacho alikifanya Fungo Kamili na kumpa ahueni ya maisha hadi hii leo
miti aina ya mianzi

Wilaya ya Makete ina miti aina ya mianzi ambayo imegawanyika katika makundi ya aina mbili, aina ya kwanza hutumika kwa ajili ya kutengeneza pombe ya kienyeji aina ya ulanzi ambayo ni maarufu sana katika mkoa wa Njombe na Iringa na kundi la pili ni mianzi migumu ambayo hutumika kutengenezea samani mbalimbali (shughuli za ujenzi), hivyo Fungo aliamua kujiingiza kutengeneza samani mbalimbali kwa kutumia miti aina ya mianzi

Miongoni mwa vitu anavyotengeneza ni nyungo, vimikebe, vibakuli, makochi/viti vya kukalia na vingine vingi ambavyo huvitengeneza kwa wingi na soko lake kubwa ni wazungu ambao hufika mara kwa mara kwenye kituo alichokuwa akifanyia kazi awali na kuacha kazi baada ya kuona haina maslahi, na kwa kuwa wanamfahamu basi humpa 'oda' ya vitu ambavyo wanavitaka na yeye huwatengenezea kazi anayoifanyia nyumbani kwake
 
Baadhi ya samani anazotengeneza

Kutokana na kufanya shughuli hii ambayo anaipenda na kuitegemea amesema humpatia zaidi ya laki tatu kwa mwezi kama biashara ikiwa mbaya, lakini ikiwa nzuri humpatia hadi laki sita kwa mwezi, fedha ambazo huzitumia kusomesha watoto pamoja na kuendesha biashara hiyo na hata shughuli zingine zozote zinazojitokeza

Bw. Fungo anatoa wito kwa walemavu kote nchini kufanya kazi kulingana na ulemavu alionao na kuacha dhana potofu kuwa wao ni watu wa kusaidiwa tu, kwani kwa kufanya hivyo kutamkwamua na makali ya maisha yaliyomzonga

"Kuna mtu utakuta hana mkono mmoja umelemaa halafu anakaa na kutegemea kwenda kuwa omba omba, zipo kazi anazoweza kuzibuni na kuzifanya zikamuingizia hela nyingi tu, cha msingi walemavu tuwe wabunifu, tutatoka kimaisha"alisema Fungo
 

Appointed Tourism Technical Advisory Committee.!

$
0
0
The United Republic of Tanzania

MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM


 

Telephone: 255-22-2864230             

Fax:            255-22-2864234

Cables:        “UTALII”

In reply please quote:




       P.O. BOX 9372,

      DAR ES SALAAM.





The General Public is hereby informed that pursuant to the powers conferred upon him by section 4(1) of the Tourism Act No. 29 of 2008, the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Sued Kagashek has appointed the following as members of the Tourism Technical Advisory Committee for a period of three years with effect from 1st July, 2013:

1.     Dr. Wineaster Anderson – Chair person (Department of Marketing, University of Dar es Salaam).

2.      Mr. Charles Dobbie ( Selou Safari)

3.     Mr. Mbaraka Islam ( Journalist)

4.     Hon. Mustafa Akunaay (Executive Secretary, Tanzania  Association of Tour Operators)

5.     Mr. Donatius M.K.Kamamba   (Director of Antiquities)

6.     Mr. Allan Kijazi (Director General Tanzania National Parks)

7.     Mr. Bruno Kawasange (Ag. Conservator,  Ngorongoro Conservation Area Authority)

8.     Mr. George Msumi (Ag. Manager,  Marine Parks and reserves Unit- MPRU)

9.     Prof. Alexander Songorwa ( Director of Wildlife Management)

10.                    Ms. Latifa Sykes ( Executive  Secretary, Hotel Association of Tanzania)

11.                    Dr. Alois Nzuki ( Director General, Tanzania Tourism Board)

12.                    Mr. Richard Rugimbana (Executive  Secretary, Tourism  Confederation of        Tanzania)

13.                     Eng. T.Baya ( Director General, National Environment Management Council – (NEMC)

14.                    Mr. Bavoo Junus  (Representing Attorney General)

15.                    Mr. Haji Y. Janabi (Representing  Ministry of Home Affairs)



N. H. M. Millao

AG. PERMANENT SECRETARY


1st August, 2013

Uwekaji saini Mikataba ya Makubaliano ya Ushirikiano.

$
0
0
Na Benedict Liwenga-MAELEZO

02/08/2013.


WIZARA ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo saini na Kikundi cha Kimataifa cha Vijana International Youth Fellowship (IYF) cha Korea leo imetiliana Mikataba ya makubaliano ya Ushirikiano.


Naibu Katibu Mkuu Bi. Sihaba Nkinga wametia saini leo Mikataba ya makubalianjo ya Ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Kikundi cha Kimataifa cha Vijana International Youth Fellowship (IYF) kilichopo nchini Korea.

Utiaji saini huo ulishuhudiwa na Mwanzilishi wa IYF Mchungaji Ock Soo Park ambaye pia ni Mchungaji Mwandamizi wa Good News Gangnam Church la nchini Korea ambapo mwanzilishi huyo aliweka saini pia na kubadilishana mikataba hiyo na Waziri Dkt. Fenella Mukangara.


Aidha, mbali na utiaji saini wa mikataba hiyo ya Makubaliano ya Ushirikiano, Mchungaji Ock Soo Park alitoa tuzo ya kuthamini mchango wa kazi azifanyazo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara. Dkt. Fenella alimshukuru Mchungaji Ock Soo kwa tuzo aliyompatia pia alitoa shukrani zake za dhati kwa Kikundi kizima cha IYF kwa kazi nzuri  wanazozifanya za kushirikiana na Vijana wa Kitanzania hasa kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana wa kitanzania ambayo yatawafanya vijana wengi kubadilisha fikra zao kutoka mtazamo hasi kuwa chanya.

Kikundi cha vijana cha IYF kimekuwa kikifanya Kambi zake nyingi hapa nchini kwa mara ya tano ambapo kambi hizi zinaandaliwa na taasisi hiyo ya International Youth Fellowship (IYF) kutoka Korea kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Badilisha Fikra kutoka mtazomo hasi kuwa chanya”. 


MTANDAO WA MAWASILIANO WASAIDIA KUPUNGUZA UKATILI

$
0
0
 
Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto Bw.  Erasto Ching‘oro(Kushoto) azizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio waliyoyapata tangu kuzinduliwa kwaMtandao wa Mawasiliano ya Kuwasaidia Watoto wanaofanyiwa UkatiliNa. 116 (Child Help Line) kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.  PICHA NA ELIPHACE MARWA.


 ==============   =============    =============
MAELEZO YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MATUMIZI YA MTANDAO WA MAWASILIANO YA MSAADA DHIDI YA UKATILI WA WATOTO NA. 116 (CHILD HELP LINE)



Ndugu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari, MAELEZO,

Ndugu Wanahabari,

Mabibi na Mabwana,


Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi ya kukutana nanyi; napenda pia kuwashukuru ninyi Wanahabari kwa kuweza kuhudhuria kikao hiki.


Mnamo tarehe 14 Juni, 2013, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa masuala ya watoto ilizindua Mtandao wa Mawasiliano ya Kuwasaidia Watoto wanaofanyiwa Ukatili Na. 116 (Child Help Line). Mtandao huu ulizinduliwa kutokana na kuwepo kwa matukio mengi yaliyokithiri ambayo yamekuwa yakiwakabili watoto hapa nchini. Madhumuni ya uzinduzi wa mtandao wa mawasiliano na 116 ni kuwezesha watoto na jamii kwa kuripoti matukio ya ukatili wanaofanyiwa watoto ili kuwaunganisha na mamlaka husika kuhakikisha kuwa mtoto anapata huduma na ulinzi stahiki.


Ukatili huo ni pamoja na kubakwa, kuchomwa moto, kutelekezwa, unyanyasaji mbalimbali na wakatai mwingine kuuawa. Ukatili huo kwa kiasi kikubwa umekuwa ukiathiri maendeleo ya watoto, makuzi ya watoto pamoja na kuwasababishia madhara ya kisaikolojia.


Ndungu Wanahabari,

Matokeo ya Utafiti uliofanywa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (2009)  kwa kushirikiana  na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi na Tiba cha Muhimbili, UNICEF pamoja na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) ambao ulihusu kuelewa tatizo na sura ya ukatili wa kijinsia, kimwili na kiakili wanaofanyiwa  watoto nao ulichangia kuona umuhimu wa kuwa na mtandao wa mawasiliano ili kusaidia utoaji wa taarifa ya matukio ya ukatili na kuwaunganisha watoto na wasimamizi wa ulinzi wa mtoto.


Kutokana na ukweli kwamba, matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa kuna kiwango kikubwa cha ukatili dhidi ya watoto na matukio mengine ya ukatili dhidi ya watoto yamekuwa yakifanyika ama shuleni, nyumbani na ndani ya jamii. Hali hii ilipelekea wadau wa masuala ya watoto  kuandaa Mpango Mkakati wa mwaka mmoja wa Kushughulikia Tatizo la Ukatili Dhidi ya Watoto (2012 – 2013); na hatimaye kuandaa Mpango wa Miaka Mitatu wa kushughulikia tatizo hilo (2013 – 2016) ambao ulizinduliwa mkoani Dodoama mwezi Aprili, 2013.


Ndugu Wanahabari,

Pamoja na jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba kunakuwepo na Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008), Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009, uanzishaji wa Madawati ya Jinsia na Watoto katika vituo mbalimbali vya polisi nchini; bado Wizara na wadau tuliona kuna umuhimu wa kuwa na chombo kingine ambacho kitasaidia upatikanaji wa taarifa za matukio ya ukatili kwa watoto ili kuwaunganisha watoto na taasisi zinazotoa huduma ya stahiki kwa watoto walioathirika.


Mapema tarehe 3 Januari, 2013 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ilifikia makubaliano na Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya C-sema kuhusu uendeshaji wa mtandao wa mawasiliano ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto Na 116 ili kuripoti matukio ya ukataili wanaofanyiwa na kuwasilisha taarifa hizo kwa watoa huduma. Kwa kuanzia, Mtandao huu unafanya kazi katika Wilaya na  Manispaa za Temeke, Magu, Bukoba Vijijini, Musoma Mjini, Kasulu, Hai, Manispaa za Ilala na Kinondoni kama eneo la majaribio.


Mafanikio;

Ndugu wanahabari,

Toka mtandao huu ulipozinduliwa ni kipindi cha mwezi mmoja na takriban wiki tatu. Hata hivyo mtando umeonesha mafanikio kwa kuwepo mwitikio mkubwa kwa wananchi katika kutoa taarifa za ukatili kwa watoto na kuonesha umuhimu wa upatikanaji wa msaada wa kisheria na hivyo kuharakisha jukumu la utoaji wa huduma kwa mtoto aliyefanyiwa ukatili katika maeneo mbalimbali.


Tangu kuanzishwa Mtandao wa Mwasiliano ya Msaada wa Kuzuia Ukatili wa Watoto mapema tarehe 12 Mei 2013 kumekuwepo na mafanikio makubwa. Kwa kipindi kinachoishia tarehe 18 Julai 2013 kiasi cha simu 1,146 zilipokelewa kutoka mikoa mbalimbali. Kati ya simu hizo, simu 235 zilihitaji kufahamu jinsi mtandao unavyofanya kazi na namna ya kuripoti matukio ya ukatili. Simu 29 zilihitaji huduma ya ushauri na msaada zaidi ambapo taarifa za matukio ya ukatili zilipelekwa kwa Kamati za Ulinzi na Usalama wa Mtoto katika ngazi ya Wilaya kwa ajili ya ufuatiliji. Kamati hizi zinahusisha Maafisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri, Maafisa Maendeleo ya jamii, Polisi- Dawati la Jinsia na watoto.


Ndugu Wanahabari,

Takwimu hizi zinaonesha mafanikio makubwa ya matumizi ya namba 116, kutokana na ukweli kwamba wakati wa uzinduzi tarehe 14 Juni 2013 ilielezwa kuwa kulikuwa na jumla ya miito ya simu 267. Kati ya simu hizo, simu 64 zilipokelewa wiki ya kwanza, wiki ya pili miito 96 na hadi siku ya uzinduzi simu 107.


Hadi sasa kuna ongezeko la simu 939 kwa kipindi cha mwezi mmoja. Idadi hii ya miito ya simu inaashiria kuwa kunamwitikio mkubwa kutoka kwa wananchi katika kuripoti ukatili dhidi ya watoto katika maeneo tunakoishi. Vilevile, taarifa hizi ni kielelezo cha kuwepo kwa matukio ya ukatili wanaofanyiwa watoto katika familia na jamii kwa ujumla..  


Hili linathibitishwa na baadhi ya kesi ambazo zinaripotiwa na wananchi likiwemo tukio ambalo lilifanyika Mkoani Arusha ambapo raia mwema kwa niaba ya mama mzazi wa mtoto alipiga simu akiripoti tukio la ukatili aliofanyiwa mtoto wa kike (umri 12) ambaye alitekwa na bwana mmoja, alimbaka mtoto huyo na kisha mbakaji akamshikilia binti huyo mwanafunzi wa darasa la sita na kuendelea kuishi naye kama mke.


Ndugu wanahabari,

Kuwepo kwa mawasiliano ya msaada wa simu Namba 116 kuliweza kusaidia kumwokoa mtoto huyo kwa ushirikiano kutoka Jeshi la Polisi Arusha ambao waliweza kumrejesha mtoto huyo nyumbani na kuendelea na masomo yake. Hivyo, Wizara inazidi kuwaomba ninyi wanahabari kuendelea kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutumia huduma hii ili kwa pamoja tuweze kuzuia na kudhibiti ukatili dhidi ya watoto. Juhudi hizi zikiunganishwa na jitihada za vyombo vya habari na wadau wengine tutaendeleza azma ya kuwa na jamii inayowajali na kuwalinda watoto.


Aidha ni matumaini ya Wizara kuwa wadau mbalimbali wataendelea kujitokeza kushirikiana na Wizara na asasi ya C-Sema katika kuhakikisha kuwa huduma hii ya mawasilino inapatikana katika maeneo yote hapa nchini katika muda muafaka ili kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata ulinzi wa kutosha, na kwamba kila mwananchi anawajibu wa kuwalinda watoto na kuzuia vitendo vya ukatili.  


Ndugu Wanahabari,

Wizara inaendelea kuhimiza jamii kubadilika na kuhakikisha kuwa familia ambayo ndio kitovu cha jamii panakuwa ni mahala salama penye upendo amani na mshikamano miongoni mwa wanafamilia; na kuwapatia watoto haki zao za msingi ikiwemo haki ya kuishi, kulindwa, na kuendelezwa.


Jamii inapaswa kukumbuka kwamba Haki ya mtoto ya kuishi ni haki yao ya Kikatiba, hivyo kumnyima mtoto haki hiyo ni kukinzana na Mkataba wa Kimataifa wa Haki na Ustawi wa Mtoto, Sera ya Maendeleo ya Mtoto na Sheria ya Mtoto Na. 21 (2009). Hivyo, jamii inawajibu wa kulinda na kutetea utu na uhai wa mtoto, ili kuhakikisha kuwa watoto wanaishi kwa amani, furaha, uhuru na utulivu.


Mwisho napenda kuwashukuru wanahabari kwa kuendelea kufichua na kuripoti taarifa nyingi za ukatili wanaofanyiwa watoto kutoka katika maeneo mbalimbali. Napenda kuwathibitishia kuwa taarifa zenu zimekuwa kikifanyiwa kazi na mamlaka husika katika ngazi mbalimbali ili kuwasaidia watoto wetu wanaokumbwa na ukatili. Kwa pamoja tunaweza kumlinda mtoto wa Tanzania na kumwekea mazingira rafiki.



Asanteni kwa Kunisikiliza

  

ErastoT. Ching‘oro

Msemaji

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto






Tuma na kutoa pesa bure kupitia huduma ya Airtel money

$
0
0
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa , Meneja  masoko Airtel money Rwebu Mutahaba kwa pamoja wakionyesha Bango la hakatwi mtu wakati wa uzinduzi  wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini. 
  Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa akiongea na wahandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure itakayo wawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure, pichani MenejaUhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando, 
 Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando(katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure popote pale nchini. Kushoto Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa (kulia) Meneja  masoko Airtel money Rwebu Mutahaba.
========    ========   ========

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma za mawasilino leo imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha ijulikanayo kama ‘Hakatwi mtu hapa’ inayowawezesha wateja wake nchi nzima  kutuma na kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel money bila makato yoyote.

Promosheni ya Airtel money Bure itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.

akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa  kuzindua promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya  kifedha nchi nzima”.

Kwa upande wake Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza  kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.

“Tunayofuraha kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo hapo awali.  Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.

Airtel kwa sasa inaendesha promosheni maalumu  kwa wateja  wake ya Airtel yatosha. promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’  ni msisitizo unaoonyesha Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na  kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote  nchini. Huduma ya Airtel money sasa  bila shaka Yatosha. 

Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images