Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Mheshimiwa Spika ashiriki katika mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuia ya Madola Barani Afrika uliofanyika, mjini Abuja, Nigeria

$
0
0

Mhe Spika Job Ndugai akisalimiana na Spika wa Bunge la Nigeria,Mhe Alhaji Yakubu Dogara wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 18 wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaofanyika Abuja nchini humo.
IMG-20170726-WA0034 (1)
Mhe Spika Job Ndugai akisalimiana na Kaimu Rais wa Nigeria Mhe Prof.Yemi Osinbajo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 18 wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika unaofanyika Abuja nchini humo.

Tehama yaboresha utendaji wa kazi na utoaji wa huduma kwa TAKUKURU

$
0
0
Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma TAKUKURU. Usikose kuangalia kipindi hiki uone jinsi ambavyo TEHAMA imesaidia kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma hasa kupitia sims za mkononi.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO JULAI 27,2017

PROF MAGHEMBE AFUNGUA MKUTANO WA SITA WA TANAPA KWA WAHARIRI NA WANAHABARI WAANDAMIZI MKOANI TANGA

$
0
0
Wahariri na Wanahabari wametakiwa kuendelea kutumia kalamu zao katika kuandika masuala mbalimbali ya utalii wa Tanzania ili kuutangaza ikiwa sambamba na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa 

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 
 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 

Prof Maghembe amesema katika kufanikisha kukuza uchumi wa Tanzania kwa kutegemea utalii Wanahabari wanapaswa kushiriki moja kwa moja katika utoaji wa taarifa zilizo sahihi kwa Watanzania na wageni kwa kutumia kalamu zao. 

"Nyinyi waandishi wa habari msikubali kuandika jambo ambalo hamlijui kitaaluma, kwani ukifanya hivyo utakuwa hujengi jamii yako,hivyo ni muhimu sana kwa wanahabari kujua habari sahihi za uhifadhi hasa kwa kuzungumza na wataalamu kutoka sekta hiyo"amesema Prof. Maghembe. 

Nae Mkurugenzi wa TANAPA, Allan kijazi amesema kuwa utalii Utalii unachangia 17.2% ya pato la Taifa na 25% ya fedha za kigeni nchini,80% ya utalii unatokana na Hifadhi za Taifa.

Amesema kuwa TANAPA inajitegemea kwa asilimia 100, na mchango wao kwa serikali umeongezeka kutoka bilioni 27 mwaka 2015/16 mpaka bilioni 34 kwa mwaka 2016/17 sawa na ongezeko la bilioni saba.

"Tanzania ina vivutio vingi vya kipekee ukilinganisha na nchi nyingine Duniani,Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii nchini pamoja na Ofisi za Balozi zetu nchi mbalimbali inajitangaza ndani na nje ya Nchi ili kuongeza idadi ya Watalii",amesema Kijazi.

Akielezea Uvumi wa Mlima Kilimanjaro kuwa haupo Tanzania,anasema ni ni propaganda za ushindani wa kibiashara, lakini matumizi ya Teknolojia yamesaidia kutoa elimu,anasema na kuongeza kuwa hivi sasa idadi kubwa ya watalii kutoka Nje ya nchi wanaelewa Mlima huo upo Tanzania.

Akielezea changamoto ya Ujangili,Kijazi anaeleza kuwa kwa sasa matukio ya ujangili yamepungua kwa 80% na kwamba Mamlaka inashirikiana na Jumuia ya Kimataifa kutokomeza Soko la bidhaa zinazotokana na ujangili.

Kijazi alimaliza kwa kusema kuwa TANAPA ilianzishwa kisheria mwaka 1959 kukiwa na hifadhi moja tu ya Serengeti,lakini mpaka sasa hifadhi zimeendelea kuongezeka hadi kufikia 16 mwaka 2014. 

 Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe akizungumza jambo alipokuwa akifungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'. 
  Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia  yaliyaokuwa yakijiri kwenye mkutano huo ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Allan Kijazi akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Maliasili Prof.Jumanne Maghembe kufungua Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye Mkutano wa Sita wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa Wahariri na Waandishi waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanda'.
  Baadhi ya Wahariri na Wanahabari waandamizi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi Waandamizi ulioanza kufanyika leo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa jijini Tanga, ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni 'Utalii na Tanzania ya Viwanga'.

ETIHAD AIRWAYS INTRODUCES NEXT-GENERATION BOEING 787 BETWEEN ABU DHABI AND BEIRUT

$
0
0
Etihad Airways has introduced the Boeing 787-9 on its scheduled daily service from Abu Dhabi, the capital of the United Arab Emirates (UAE), to Beirut, Lebanon.
The new 787 Dreamliner service replaces the Airbus A321 aircraft previously operating the airline’s EY535/EY538 flights to and from the Lebanese capital. The Boeing 787-9 features Etihad Airways’ next-generation Business and Economy Class cabins and is configured with 299 seats – 28 Business Studios and 271 Economy Smart Seats.
“Beirut was the first international destination served by Etihad Airways in 2003 and it is fitting that we introduce the state-of-the-art 787 Dreamliner to this key market today,” Mohammad Al Bulooki, Etihad Airways Executive Vice President Commercial said.
“The new two-class 787-9 provides an increase of 125 seats per flight, with 4,186 weekly seats now offered in both directions. This reflects the strong demand to Lebanon from Abu Dhabi and the entire UAE, where a large Lebanese expatriate community resides.
“Additionally, a significant proportion of our customers travelling to Lebanon originate in Australia, home to a considerable Lebanese Australian community, with the vast majority based in the Sydney area. They can now enjoy an upgraded, seamless flying experience, connecting from A380 services via Abu Dhabi onto 787 Dreamliners onwards to Beirut,” he said.
The Boeing 787 is the backbone of Etihad Airways’ modern fleet of aircraft, boasting innovative, award-winning cabin designs and products, complemented by the airline’s acclaimed service and hospitality offering, which on Beirut flights now includes a Norland approved Flying Nanny in Economy Class to provide extra specialized care for families with young children.
The Business Studios offer direct aisle access, a fully-flat bed of up to 80.5 inches in length, and an increase of 20 per cent in personal space. Upholstered in fine Poltrona Frau Leather, the Business Studio is equipped with an in-seat massage and pneumatic cushion control system which enables guests to adjust the firmness and comfort of their seat.
Each Business Studio has an 18-inch personal touch-screen TV with noise-cancelling headsets. Guests can also enjoy mobile connectivity, onboard Wi-Fi and seven satellite channels of live TV.
Economy Smart Seats provide enhanced comfort with a unique ‘fixed wing’ headrest, adjustable lumbar support, a seat width of approximately 19 inches and an 11.1” personal TV monitor on each seat. The aircraft has been designed with enhancements including humidity controls while air pressure levels are set to ensure a smoother flight, allowing guests to arrive feeling fresher.
The airline’s Boeing 787 fleet is equipped with the latest inflight entertainment system featuring over 750 hours of movies and programmes, as well as hundreds of music choices and a selection of games for both adults and children.

UNAITUMIAJE MITANDAO YA KIJAMII KUTANGAZA BIASHARA YAKO ?

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Mitandao ya kijamii ni huduma zinazopatikana kwenye intaneti ambazo zinakuwezesha kuwasiliana, kutengeneza maudhui na kuwashirikisha watu wengine waliopo mitandaoni.

Tofauti na watu wanavyoitumia, Jumia Travel ingependa kukufunua macho kwamba mitandao ya kijamii imeleta fursa kubwa ya kutangaza biasahara za aina mbalimbali. Unaweza kuitumia mitandao hiyo kwa kufanikisha malengo kama vile; kukuza jina na biashara yako, kuwafahamisha wateja juu ya bidhaa na huduma zako, kujua wateja wanaichukuliaje biashara yako, kuwavutia wateja wapya pamoja na kujenga mahusiano thabiti na wateja ulionao.

Faida za kutumia mitandao ya kijamii

Kuwafikia watu wengi. Badala ya kutegemea wateja kuja moja kwa moja ofisini kwako mitandao ya kijamii huwafikia mamilioni ya watu sehemu mbalimbali ndani ya muda mfupi.

Kuwafikia wateja unaowakusudia. Uzuri wa mitandao ya kijamii ni kwamba hutofautiana kwa aina ya watumiaji wake kama vile vijana, watu wazima, wanasiasa, wanataaluma na matabaka mengine. Hivyo hii hutoa fursa kwa mfanyabiashara kulingana na huduma au bidhaa aliyonayo kujiwekea mkakati wa namna ya kuwafikia.

Unafuu. Haikuhitaji kuwa na fedha ndipo ufungue akaunti kwenye mtandao wa kijamii mara nyingi ni intaneti tu. Lakini kama unataka kuitumia kwa malengo ya kibiashara wamiliki wake hutoza kiasi kidogo cha fedha ambacho ni rahisi kukimudu.

Kumfikia mtu binafsi. Mitandao ya kijamii inakuruhusu kujenga ukaribu au kuwasiliana na wateja wako kwa ukaribu zaidi. Uwezo wa kuyapokea na kuyajibu maswali yao au kuyasikiliza na kuyafanyia kazi maoni yao vina ushawishi mkubwa katika kuwafanya wateja kutumia huduma na bidhaa zako.

Uharaka. Ndani ya muda mfupi unaweza kusambaza taarifa juu ya huduma na bidhaa zako kwa watu wengi kwenda sehemu mbalimbali.

Urahisi. Haikuhitaji kuwa na ‘madigrii’ ya vyuo vikuu ili kuweza kutumia mitandao ya kijamii. Ni rahisi kuitumia kwa njia mbalimbali kama vile kompyuta, tabiti au simu za mikononi ambazo watu wengi wanamiliki.   
Mitandao mikuu ya kijamii unayoweza kuitumia

Facebook. Mtandao huu hutoa fursa nzuri kwa wafanyabiashara kuwasiliana na wateja wao moja kwa moja, kuweka picha na video, kutangaza ofa walizonazo, bidhaa na huduma mpya na mambo mengine.

Twitter. Mara nyingi huduma hii hutumika kutuma na kupokea jumbe fupi kutoka kwa wateja wapya na waliopo. Siku hizi pia hutumika kama nyenzo muhimu kwa kuweka viungo ambavyo vitawapeleka wasomaji kwenye tovuti.

Youtube. Mtandao huu hutumika kwa kuweka video tofauti, zinaweza kuwa juu ya huduma na bidhaa ulizonazo, namna ya kuzitumia pamoja na taarifa mbalimbali ili wateja wako wazitazame.

Blogu. Kama mfanyabishara pia unaweza kufungua mtandao huu utakaokupatia fursa kubwa ya kuwashirikisha wasomaji wako juu ya huduma na bidha zako pamoja taarifa mbalimbali.

Instagram. Mbali na mtandao huu ipo mingine pia inayowawezesha watumiaji kuweka na kuwashirikisha watu wengine picha mbalimbali. Kwa mfano hivi karibuni Instagram wameuboresha mtandao wao kwa kuwawezesha watumiaji wake kuweka picha zaidi ya moja. Hivyo kutoa fursa nzuri kwa wafanyabishara kuweka picha mbalimbali za bidhaa na huduma zao.
Mbali na kuwepo kwa faida lukuki za mitandao ya kijamii, Jumia Travel ingependa kukuasa kwamba bado unahitajika umakini mkubwa katika nanma ya kuitumia. Miongoni mwa changamoto unazoweza kukumbana nazo ni pamoja na kupoteza muda na fedha zako kwa kuwekeza kwenye  kitu ambacho hakitoleta faida, kusambaa kwa habari zisizo sahihi kuhusu biashara yako kwa wateja na kukumbana na matatizo ya kisheria endapo usipofuata au kuvunja taratibu zilizowekwa na mamlaka husika.

NBC Yazindua Klabu ya Biashara mjini Kahama

$
0
0
 Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mjini Kahama, Shinyanga jana. Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Katikati ni mmoja wa wateja, Salum Selemani na Joshua John (kulia), Ofisa Masoko wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) kutoka ofisi ya Mwanza.
 Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kushoto), akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Kahama, katika semina iliyoandaliwa kabla ya  uzinduzi  rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC hiyo iliyoanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Hafla ya uzinduzi ilifanyika mjiini Kahama, Shinyanga jana.
 Meneja wa Kanda wa NBC, Daudi Mfalla (kulia), akizungumza wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi  rasmi wa Klabu ya Biashara ya NBC  iliyoanzishwa kusaidia mahitaji ya wateja wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashara wadogo na wakati wa NBC, Evance Luhimbo.
 Baadhi ya wateja wa NBC mjini Kahama waliohudhuria uzinduzi wa B-Club ya benki hiyo, wakijipiga picha ‘selfie’ pamoja na bango lenye picha inayoonyesha kilele cha Mlima Kilimanjaro ikiwa ni baadhi ya shamrashara zilizopamba uzinduzi huo.
  Wafanyakazi wa NBC tawi la Kahama wakipozi kwa katika hafla hiyo.
Wasanii wakionyesha umahiri wao kucheza ngoma ya kadete ya kabila la wasukuma katika hafla ya uzinduzi wa B-Club mjini Kahama, Shinyanga jana.

Rais Magufuli asimamishwa Morogoro aagiza wamachinga wasinyanyaswe na waliotelekeza viwanda wavirejeshe Serikalini

$
0
0

 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia Wananchi wa eneo la stendi ya mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro akitokea mkoani Dodoma leo Julai 27, 2017.
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wananchi wa eneo la stendi ya mabasi ya Msamvu  mkoani Morogoro akitokea Dodoma leo Julai 27, 2017.
 Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli Akimsikiliza Bi Maria Gabrieli aliyemweleza kero za wafanyabiasahara ndogondogo wa Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro kunyanyaswa. Julai 27, 2017.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Bi Halima Ali akimweleza juu ya kero za wafanyabiasahara ndogondogo wa Stendi ya Mabasi Msamvu  Mkoani Morogoro kunyanyaswa. Julai 27, 2017.
Picha na IKULU

Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa jimboni kwake

$
0
0


 Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,  lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.
 
 Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi gari jipya na la kisasa la kubebea wagonjwa lililokabidhiwa katika kituo cha Afya Busondo, Tarafa ya Puge,  lililotolewa na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla.

Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) mpya na la kisasa katika Kituo cha Afya Busondo kilichopo Tarafa ya Puge ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Nzega Vijijini.

Tukio hilo la kukabidhi gari hilo limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani  Tabora, Mh. Geofrey Ngupula ambaye alitoa agizo kali kwa Mganga Mkuu wa Kituo hicho kuhakikisha gari hilo linatumika kwa shughuli zilizokusudiwa ikiwemo za kubebea wagonjwa na akina mama wajawazito kuwawaisha sehemu muhimu za kutolea huduma stahiki.

Mkuu wa Wilaya huyo alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo Dk. Kigwangalla kwa kuweza kuwasaidia wananchi  wa Jimbo hilo kwa kuweza kuwasaidia gari hilo la Wagonjwa  kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi hao ambao wapo maeneo ya mbali na kituo cha Afya huku pia likitarajiwa kuwa msaada kwa kuwapeleka wateja katika  ngazi za juu za huduma hiyo ikiwemo Hospitali za  Wilaya, Mkoa, Kanda na Taifa.

Aidha, alisema ni marufuku wagonjwa kuombwa  kuchangia mafuta ya  ambulance hiyo au gharama yoyote ile, gari hili wagonjwa walitumie bure kwani limetolewa bure na pia huduma zote zikiwemo za mafuta zinalipwa na Halmashahuri hiyo.

“Gari hilo lipatikane kituoni  wakati wote pamoja na dereva. Tumeshahakikishiwa hapa Halmshauri imesema ina mafuta ya kutosha litakuwa linajazwa lita 90, kila yatakapokuwa yametumika hivyo kusiwe na kisingizio kingine cha kuweza kudai mafuta ama kuwatoza wananchi gharama na atakayefanya hivyo Serikali hii si ya mchezo hatua kali zitafuata , tutakutumbua tu” alieleza Mh. Ngupula.

Ameongeza kuwa gari hilo ambalo ni la kisasa, litunzwe na kulindwa ili liweze kutumika kwa miaka mingi ijayo na kuwa  msaada kwa Tarafa hiyo na wananchi wote watakaopata msaada.

Kwa upande wake, Dk. Kigwangalla amewaomba wananchi waendelee kumuombea kwa kazi anayofanya ikiwemo jukumu la kulitumikia Taifa katika nafasi yake ya Unaibu Uwaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Dk. Kigwangalla ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli  kwa kuweza kuwa karibu na Wananchi ikiwemo kushughulikia suala la maji kutoka Ziwa Victoria na kuja Mkoa wa Tabora ikiwemo kuanzia katika Wilaya hiyo ya Nzega na kisha kwenda maeneeo mengine.

“Tunampongeza Rais wetru Dk. Magufuli kwa kuwa karibu na wananchi wake. Tulikuwa nae Mkoani kwetu hapa Tabora na amezindua miradi mbalimbali ikiwemo ya barabara na ule wa maji safi yatakayotoka Ziwa Vitoria. Shida ya maji kwa wananchi wa Nzega inaenda kuwa histoa kwani Maji hayo yatakuja hapa na kisha kwenda maeneo mengine. Rais wetu anatupenda na tuendelee kumuunga mkono hasa juhudi zake za kulinda rasilimali za nchi yetu na pia katika kushughulikia mafisadi na wahujumu uchumi wa Taifa letu

Mimi Mbunge wenu pia muendelee kuniombea na kila siku mawazo yangu na akili yangu ipo pamoja nanyi ndio maana nimeweza kuwaletea gari hili la wagonjwa, na pia kufanikisha kuandaa kambi maalum ya matibabu bure ya wiki moja kwa wananchi wote wa Nzega bure” alieleza Dk. Kigwangalla.

Tukio hilo la ukabidhi wa gari hilo pia lilishuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani wa Jimbo hilo na wale wa jimbo jirani ikiwemo Bukuene, Viongozi wa ulinzi na Usalama pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nzega.

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI JIJINI DAR, AWAHUTUBIA WANANCHI WA TEGETA KWA NDEVU

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, baada ya wananchi hao kusimamisha msafara wake alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimshangilia Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017. PICHA NA IKULU.

NENO LA NAIBU WAZIRI DKT KIGWANGALLA KWA MAAFISA USTAWI NA MAENDELEO YA JAMII NCHINI

MAWAZIRI WATANO WAFANYA ZIARA MPAKA WA TANZANIA NA UGANDA

$
0
0
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Luteni Kanali Denice Mwila kuhusu changamoto za mpaka huo wngine ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba.
 Jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba 30.
 Ujumbe wa Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwa juu ya Jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda namba 30.
 Moja ya jiwe la mpaka wa Tanzania na Uganda ambalo Mawaziri wamefanya ziara ya kuliona.
   Ujumbe wa Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania wakipita katika eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani Kagera.
 Ujumbe wa Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania wakikagua huduma za vibali vya kuingia na kutoka nchini Tanzania na Uganda zilizopo Mtukula mkoani Kagera.

Eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda kwa upande unapo pita mto Kagera.


Na. Hassan Mabuye
Mawaziri watano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watembelea mpaka wa Tanzania na Uganda ili kutatua changamoto zinazoukabili mpaka huo na kuuboresha.

Mawaziri hao ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleman Jaffo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Suzan Kolimba na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe.

Miongoni mwa maeneo yaliyotembelewa na Mawaziri hao ni eneo la mpaka ya Tanzania na Uganda kwa upande unapo pita mto Kagera na eneo la kivuko cha mpaka wa Tanzania na Uganda kilichopo Mtukula mkoani Kagera.

Katika ziara hii Mawaziri hao wameweza kujionea hali halisi ya maisha ya wakazi wa mipakani na jinsi wanavyohusiana na wenzao wa nchi ya jirani ya Uganda ambapo wamekuwa wakishirikiana na kuishi kwa amani katika shughuli zao za kila siku.

Aidha, ziara hii ni maandalizi ya Mkutano wa ujirani mwema kati ya Mawaziri wa serikali ya Uganda na Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unatarajiwa kufanyika mnamo tarehe 29 Julai 2017, Bukoba mkoani Kagera.

prof dos santos kuwasilisha mada ya uhifadhi wa misitu na mpango mkakati wa utalii nchini

$
0
0
Mtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania, Ibrahim Mussa (kushoto) alipokuwa akimueleza mambo mbalimbali ya uhifadhi na changomoto zake inapokuja suala la kushirikisha vyombo vya habari kabla ya kufungua mkutano wa sita wa wahariri na wanahabari waandamizi unaohusu sekta ya utalii nchini ambao umeandaliwa na Hifadhi za Taifa (TANAPA) unaofanyika jijini Tanga 27 - 29, Julai 2017. 
 
Katika mkutano huo Prof  Silayo atawasilisha mada "uhifadhi wa misitu ya hifadhi ya asili na mpango mkakati wa utalii Kesho Ijumaa ya tarehe 28 Julai 2017 saa 05:45 asubuhi na kurushwa moja kwa moja kupitia ukurasa wa facebook wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (www.facebook.com/foresttz). 
 
usikose kuungana naye na atajibu maswali yatakayoibuka kutokana na mada atakayoiwakilisha!

Mratibu wa Mradi wa Misitu ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Tanzania, Gerald Kamwenda (Kushoto) akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof Dos Santos Silayo mara baada ya kupokea taarifa za wajumbe wa Mkuno Mkuu wa Mwaka wa Wahariri na Wanahabari Waandamizi ulioandaliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kutembelea Hifadhi ya Misitu Asilia ya Amani Siku ya Jumamosi (Julai 29,2017).

TUME YA UCHAGUZI YATEUA WABUNGE 8 WA VITI MAALUM KUPITIA CHAMA CHA ANANCHI CUF

SPIKA NDUGAI APONGEZWA BAADA YA KUSHINDA NAFASI YA MWENYEKITI WA MASPIKA KATIKA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipongezwa na Naibu Spika wa Cameroon, Mhe.  Monjowa Lifaka baada ya kushinda nafasi ya Mwenyekiti  wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika. Uchaguzi huo umefanyika leo katika Mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliomalizika leo Mjini Abuja.

SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA WAAJIRI KOTE NCHINI KUJISAJILI NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, (WCF), VINGINEVYO HATUA ZA ADHABU ZA VIFUNGO NA FAINI KUTEKELEZWA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (kulia), akizungumza leo Julai 27, 2017 wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa kushtukiza kwenye Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati jijini Mbeya ili kubaini kama mwajiri kwenye hospitali hiyo amejisajili katika  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF). Waziri ametoa siku 30 kwa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania Bara, kujisajili na Mfuko huo, vinginevyo watakabiliwa na adhabu mbalimbali ikiwemo faini ya shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdusalaam Omar.
NA MWANDISHI WETU MBEYA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ametoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao hawajasajili, kujisajili katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF), na kutoa michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri Mhagama alitoa agizo hilo jijini Mbeya Julai 27, 2017 wakati wa zoezi la ukaguzi wa kushtukiza jijini humo kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeleza Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 Marejeo ya Mwaka 2015 kifungu cha 5, ambayo inawataka waajiri wote kutoka sekta ya Umma na Binafsi, Tanzania Bara kujisajili kwenye Mfuko huo.

“Mwajiri ambaye hajajisajili kwenye Mfuko, anaweza kufikishwa mahakamani na adhabu ni pamoja na kutozwa faini ya kiasi cha fedha kisichozidi shilingi milioni 50 au kifungo kisichozidi miaka 5 jela au vyote kwa pamoja, hivyo nawasihi waajiri kutoka sekta binafsi na umma Tanzania Bara ambao hawajasajili kutekeleza sheria hiyo inayowataka kujisajili WCF katika muda huo nilioutoa.” Alisisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama.

Katika ziara hiyo ya ukaguzi wa kushtukiza Mhe. Waziri alifuatana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge na Afisa Kazi wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Mary Patrick Mwansisya ambapo taasisi ya kwanza ambayo Mhe. Mhagama aliikagua ni Hospitali ya K’s iliyoko eneo la Mafyati na St. Aggrey iliyoko Uyole na kubaini kuwa taasisi hizo hazijajisajili katika Mfuko.

Aidha Waziri alitoa siku saba kwa waajiri wote Mkoani Mbeya wapatao 107 ambao bado hawajajisajili ikiwemo Hospitali ya K’s na Shule ya sekondari St. Aggrey kujisajili ndani ya muda huo.

“Mkishindwa kutekeleza agizo hilo maana yake mnatuelekeza kutumia kifungu cha 71(4), cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kinachotamka adhabu ya faini ya kiasi cha fedha kisichopungua shilingi milioni 50, kifungo cha miaka 5 jela au vyote kwa pamoja.” Alisema.

Aidha Waziri Jenista alihimiza kuwa mwajiri anapojisajili na Mfuko pia atimize wajibu wa kisheria wa kuchangia katika Mfuko kwa wakati stahiki. Mhe. Waziri alisema nia ya Serikali ya awamu ya Tano sio kuwatisha waajiri bali ni kuhakikisha wanafuata sheria ili hatimaye, wafanyakazi wapate haki yao stahiki pindi wanapoumia, kuugua ama kufariki wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri wao kwa mujibu wa mkataba wa ajira.

Akifafanua zaidi Waziri alisema, takwimu zilizopo katika Mfuko za kipindi cha mwaka 2015/16 na 2016/17 zinaonesha kuna jumla ya waajiri 229 jijini Mbeya na kati yao ni waajiri 107 tu ndiyo waliojisajili katika Mfuko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Tathmini wa WCF, Dk. Abdulsalaam Omar alisema Mfuko unamshukuru Mhe. Waziri kwa kushiriki katika ukaguzi huu wa kwanza wa aina yake kufanyika tangu Mfuko huu uanzishwe mnamo mwaka 2015 na kwamba Mfuko utasimamia na kutekeleza maagizo ya Mhe. Waziri.

"Kwa kipindi chote hicho Mfuko umekuwa ukijikita zaidi katika kutoa elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo waajiri ili waweze kuelewa umuhimu wa kujisajili katika Mfuko na faida ambazo mwajiri na mfanyakazi atazipata pindi anapoumia, kuugua au kufariki wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri,” alisisitiza Dkt Omar.

Akifafanua zaidi, Mkurugenzi huyo alisema katika kazi ya uelimishaji kwa kipindi cha mwaka 2016/2017 Mfuko ulitoa elimu kwa waajiri wapatao 4,901 kuhusu haki na wajibu lakini pia kuelewa sheria kuhusu wajibu wa waajiri kujisajili katika Mfuko. Aidha Mfuko umekuwa ukitumia njia mbalimbali kama vile vyombo vya habari, semina lakini pia kwa kuwaandikia waajiri kuhusu umuhimu wa wao kutekeleza sheria hiyo kwa kujisajili katika Mfuko na kutoa Michango kwa wakati kama ambavyo sheria inaelekeza.

Dkt Omar alisema Mfuko ulianza kutekeleza majukumu yake tarehe 1 Julai 2015 kama ilivyoelekezwa katika tangazo la Serikali Na. 169/2015 ambapo majukumu hayo ni pamoja na kusajili waajiri, kukusanya michango na kulipa fidia stahiki.Tayari Mfuko umeanza kulipa fidia kwa wafanyakazi walioumia, kuugua ama kufariki kuanzia tarehe 1 Julai 2016.

Ili mfanyakazi aweze kulipwa fidia, ni lazima mwajiri wake awe amechangia katika Mfuko, hivyo waajiri wanao wajibu kisheria chini ya Vifungu vya 71 – 78 vya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kujisajili, kuwasilisha michango, kutoa taarifa ya matukio ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi pamoja na kuwasilisha mapato ya mwaka." Alifafanua Dkt. Omar.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge alisema, "Tamko alilotoa Mhe. Waziri wetu litakuwa chachu kwa waajiri wengine nchini kujiunga na Mfuko kwa kujisajili na kuwasilisha michango kwa wakati na hivyo kuwezesha kufikia lengo la Mfuko la kulipa Fidia Stahiki kwa wakati." Alisema.

Bi. Kunenge pia alisema, Ofisi za WCF ziko wazi na kwamba huduma za Mfuko huo zinapatikana kila mkoa hapa Tanzania Bara ambapo Maafisa Kazi wa Mikoa ndio wanafanya kazi kwa niaba ya Mfuko kwa sasa.
 Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge. (kushoto), na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya, (kulia), wakiuliza alipo mkurugenzi wa Hospitali ya K's mara baada ya kuwasili na waziri Mhagama katika ziara ya ukaguzi wa kushtukiza leo Julai 27, 2017.
 Waziri Mhagama, (wakwanza kulia), Bi. Laura na Dkt. Omar, wakimsubiri Mfanyakazi huyu wa K's Hospital akiwasiliana kwa simu na mwajiri wake ili kumjulisha uwepo wa Waziri na ujumbe wake kwenye hospitali hiyo.
 Maafisa wa polisi wakiwa tayari kuhakikisha usalama unazingatiwa wakati wa zoezi hilo.
 Waziri Mhagama na Dkt. Omar(kushoto), wakisubiri ujio wa Mkurugenzi wa hospitali ya K's
 Afisa Matekeelzo Mwandamizi wa WCF, Bw.Dan Kapogo, (kulia), akijadiliana jambo na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya.
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge. (kushoto), Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Dan Kapogo,na Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya, wakijadiliana jambo.
 Mhe. Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi wa Hospitali ya K's Dkt.Victoria Kanama, baada ya kuitwa ili aonane na waziri kueleza kwa nini hajajisajili na Mfuko licha ya kupatiwa elimu lakini pia kujulishwa kwa barua.
 Dkt. Omar, Kulia), akimuongoza waziri Mhagama wakati wakitoka kwenye Hospitali ya K's baada ya ukaguzi. (wakwazna kushoto) ni Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dkt.Victoria Kanama.
 Dkt. Omar akitoa shukrani za WCF kufuatia ziara hiyo ya kushtukiza aliyofanya Mhe. Waziri na kubainisha kuwa maagizo hayo yatasimamiwa na kutekelezwa.
 Bi. Kunenge na Bw. Kapogo kutoka WCF wakijadiliana jambo
 Mratibu wa Hospitali ya K's Bw.Mtunda Mwankwasya akizungumza.
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge
 Afisa Kazi Mkoa wa Mbeya, Bi.Mary Patrick Mwansisya akizungumza. "Tumewapa taarifa waajiri wote mkoani Mbeya hivyo wanajua fika kuhusu sheria hii inayowataka kujisajili na kutoa Michango katika Mfuko.
 Dkt. Omar akiteta jambo na Mhe. Waziri Mhagama.

 Waziri akitoka kwenye Hospitali ya K's akiongozana na Mratibu wa hospitali hiyo,Bw.Mtunda Mwankwasya
 Mkuu wa shule ya St. Aggrey.

Waziri Mhagama akizungumza mbele ya Meneja wa shule ya St. Aggrey, Bw.Melas Paul Mdemu

MAVUNDE AWADUWAZA WANAKIJIJI WA MATUMBULU KWA KUKAMILISHA AHADI YAKE.

$
0
0
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu.
Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akikabidhi mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu kwa wananchi.

.Mabomba ya kusambazia maji katika kijiji cha Matumbulu

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa na wananchi wa Matumbulu

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akifurahi jambo na wananchi wa Matumbulu.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na Diwani wa Kata ya Matumbulu Emmanuel Chibago.

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akiwa na viongozi wa kijiji cha Matumbulu.


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Anthony Mavunde ameendelea kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni ya uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo leo amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero ya maji katika kijiji cha Matumbulu.

Mavunde amekamilisha ahadi yake ya kutatua kero hiyo kwa kutoa mabomba ya kusambazia maji kijiji kizima yenye urefu wa Kilomita 1 yenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 8.

Kufuatia utekelezaji huo wa ahadi hiyo, wananchi hao walishikwa na butwaa kwa uharaka wa utekelezaji wa ahadi hiyo kwakuwa tatizo hilo la upatikanaji wa maji katika eneo ilikuwa ya muda mrefu hali iliyosababisha wananchi kutumia maji yasiyo safi na salama.

Wananchi walikuwa wanakosa fursa ya kupata maji kwa urahisi na hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji na muda mwingine kutumia maji ambayo si safi na salama kutoka na umbali wa kufuata maji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Matumbulu Alfred Malogo, amefurahishwa na utekelezaji wa ahadi hiyo na kwamba alichokifanya Mavunde kuwapatia wakazi wa kijiji hicho mabomba kwa ajili ya kusambazia maji kitatatua kero yao ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji.

“Tulikuwa tunapata shida juu ya shida lakini tunamshukuru sana huyu kijana(Mavunde) alituahidi katika uwanja huu huu kuwa atatupatia maji na leo ametimiza ahadi yake kwa kutuletea mabomba ya maji ambayo tutayasambaza na watu wataanza kupata maji,”amesema

Akizungumza wakati akikabidhi mabomba hayo, Mavunde amesema “Ni matumaini yangu kwamba ile adha kubwa ya upatikanaji wa wa maji katika eneo kubwa la kijijini Matumbulu itaisha na kusaidia wanakijiji kupata maji safi na salama kwa wakati”

Kwa upande wake, Diwani wa kata hiyo Emmanuel Chibago amempongeza Mavunde kwa anavyojitoa kuwatumikia wanadodoma na kuwaletea maendeleo na hivyo kuwaomba wanadodoma wampe ushirikiano ili afanye makubwa zaidi.

WAZIRI MAKAMBA AFANYA ZIARA KATIKA MTO MSIMBAZI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
ziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba akimsikiliza msimamizi wa ujenzi kingo za Mto Msimbazi katika eneo la Ilala Bungoni Mhandisi Jovinalis Kamugisha toka Kampuni ya Dezo Civil Constructions wakati wa ziara ya Waziri huyo kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kingo katika mto Msimbazi eneo la Ilala Bungoni wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Diwani wa Kata ya Ilala Mhe. Saady Khimji akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kingo katika mto Msimbazi eneo la Ilala Bungoni wakati wa ziara ya Waziri huyo kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa kingo za mto Msimbazi katika eneo la Ilala Bungoni wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba akitoa maelekezo kwa wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa kingo za mto Msimbazi eneo la Ilala Bungoni wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba akimsikiliza mfanyabiashara ya chakula (Mama Lishe) katika eneo la Ilala Bungoni alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba (kushoto) akipata maelekezo toka kwa Mhandisi Frank Juvenily toka Kampuni ya Dezo Civil Constructions wakati wa ziara ya Waziri huyo ya kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa, Shadrack Mwakalila wakati wa ziara ya Waziri huyo ya kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba (kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Profesa, Shadrack Mwakalila wakati wa ziara ya Waziri huyo ya kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.

Eneo la mradi wa ujenzi wa kingo katika Mto Msimbazi eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam.

Eneo la mradi wa ujenzi wa kingo katika bahari ya Hindi eneo la Barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam.
Eneo la mradi wa ujenzi wa kingo katika bahari ya Hindi eneo la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano Januari Makamba (kulia) akipata maelekezo toka kwa Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa kingo katika bahari ya Hindi eneo la Barabara ya Barack Obama Mhandisi Hillary Josiah toka Kampuni ya Dezo Civil Constructions wakati wa ziara ya Waziri huyo ya kukagua ujenzi wa kingo za Mto Msimbazi, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni na barabara ya Barack Obama mapema hii leo.Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

MH. PAUL MAKONDA AGAWA KOMPYUTA KATIKA HALMASHAURI ZA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Mkaonda akipanga kompyuta mara baada ya kupokea kuoka Kampuni ya TAMOBA Company Ltd ya jijini Dar es salaam.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akiangalia kompyuta mara baada ya kupokea kopmyuta hizo zilizotolewa na Kampuni ya TAMOBA Company Ltd ya jijini Dar es salaam.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda leo amekabidhi kompyuta za kisasa 50 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 170 kwa Manispaa tano za Mkoa wa Dar es salaam pamoja na Watu wa Jiji na Mkoa kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi.

Katika mgawanyo huo kila Manispaa imepatiwa kompyuta nane (8) huku Ofisi ya Jiji wakipatiwa kompyuta tano (5) na Ofisi ya Mkoa wakipatiwa kompyuta tano (5) ikiwa ni ufadhili wa kampuni ya ulinzi ya TAMOBA Company Ltd iliyomuunga Mkono RC Makonda kutokana na kuhamasika na utendaji kazi wake mzuri.

Makonda amesema Kompyuta hizo zitawekewa Mfumo wa kisasa ujulikanao kama Dar Ardhi E.System utakaoziunganisha idara zote zinazohusika na utoaji wa vibali vya ujenzi (One stop Center) ili kurahisisha Mwananchi kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi, ambapo mwananchi atakuwa na uwezo wa kutuma maombi ya kibali cha ujenzi kwa kutumia simu ya mkononi mwake au Computer hata akiwa nyumbani na akapewa majibu yake kwa haraka.

“Kazi yangu kubwa ni kupunguza mateso,malalamiko na kero za Wananchi dhidi ya maswala ya Ardhi, na namna mbili za kupunguza ni pamoja na kuwawezesha watendaji kuwa na nyenzo na vifaa vitakavyorahisisha kufanya kazi zao kisasa zaidi kuendana na kasi ya Rais wetu Dr.John Magufuli, na pili ni kusimamia uwajibikaji kwamba kila mmoja anatekeleza majukumu yake ili Mwananchi wa Mkoa wa Dar es salaam asipate adha na mateso aliyokuwa akiyapata kwenye Sekta ya Ardhi.

Umuhimu wa kutoa vibali vya ujenzi ni jambo lisilopingika hasa katika mji huu unaokuwa kwa kasi barani Afrika” Alisema Makonda. Aidha kompyuta hizo zitawekewa Mfumo maalumu utakao kuwa ukikusanya Maoni na mapendekezo ya wananchi ambapo wananchi watakuwa na fursa ya kutuma maoni yao na kero mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta ya Ardhi.

“Tumeishi sana kwenye mfumo wa makaratasi na mafaili, na wakati mwingine kumekuwa na changamoto ya kupotea kwa mafaili na mwananchi kupata adha ya kutoelewa nini afanye maana ataanza upya kutuma maombi, lakini si hivyo tu bali pia inafanya kazi kuwa ngumu, na mfumo huu wa kizamani unaonekana ni chanzo cha rushwa hasa pale mwananchi anapokuwa akisumbuliwa na mtumishi.

Naamini kompyuta hizi zinaenda kukata mzizi wa fitina,Wananchi kulundikana ofisini ni kero kubwa, wananchi kusumbuka kupata huduma ni kero kubwa”,alisema Makonda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya TAMOBA Bwana Joseph Kimisha amesema kuwa kampuni yao itaendelea kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Dar es salaam katika masuala mbalimbali ili kuhakikisha wanatatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Katika Makabidhiano hayo pia makamu Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TAMOBA Bwana Otieno Igogo ameahidi kuwa watatoa jumla ya Printer 12 kwa ajili ya kusaidia utendaji kwa manispaa za jiji la Dar es salaam ambapo kila manispaa itapata Printer mbili na idara ya ardhi Mkoa kupata printer mbili pia.

HATUA ZILIZOFIKIWA KATIKA MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA KUANDAA MIPANGO NA BAJETI ZA SERIKALI ZA MITA

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images