Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1316 | 1317 | (Page 1318) | 1319 | 1320 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayojengwa Hospital ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa 100%.

  Wodi hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 150 ambapo ndani yake kutakuwa na Vifaa vya kisasa vya kutolea huduma, Vyumba vya Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na sehemu ya kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.

  Ujenzi wa Wodi hiyo ni unafadhiliwa na Kampuni tanzu ya Mafuta na Saruji ya Amsons Group ambayo imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Makonda kwa kujenga wodi tatu wazazi na watoto kwenye Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala ambapo zote zitakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 450.

  “Ujenzi huu na hatua iliyofikia inatoa matumaini mapya kwa kinamama, watoto na wakazi wa Dar es salaam juu ya upatikanaji wa huduma bora na nzuri kwenye Hospital zetu za Serikali,watu walishazoea huduma nzuri zinapatikana nje ya Hospital za Serikali lakini kwa sasa hali itabadilika, na nina uhakika ndani ya muda mfupi tutamuomba Rais Dr.Magufuli aje atuzindulie hizi wodi kama ishara ya kumbukumbu ya kazi aliyoianza alipotembelea Hospital ya Muhimbili na kukuta watu wamelala chini na kutafuta majibu, sisi wasaidizi wake ametupa kazi ya kutatua kero za wananchi, hivi ndivyo tunavyozitatua kwa vitendo” Alisema.

  Aidha Makonda amesema wodi hiyo itazidisha upatikanaji mzuri wa huduma bora za Afya kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam huku akieleza kuwa lengo lake ni kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa mkoa unaotoa huduma bora za Afya.

  “Kama mnakumbuka wakati tunakuja wodi iliyokuwa ikitumik akinamama walikuwa wakilundikana chini na wengine wanatumia kitanda kimoja zaidi ya watatu hadi wanne na wakati mwingine walikuwa wakilazimika kurudi nyumbani kabla ya muda wa madaktari kuruhusu kutokana na mazingira duni yaliyokuwa yakikabili wodi hiyo, lakini wodi hii itamaliza kero hiyo” Aliongeza Makonda.

  Hata hivyo Makonda amewataka wadau wa maendeleo wenye dhamira ya kuchangia shughuli za Maendeleo kwenye Mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi Ofisini kwake na Ofisi za Wilaya kuungana na Serikali kuujenga Mkoa huo.

  “Nawapongeza watumishi na wafanyakazi wa Afya kwenye Hospital za Amana, Temeke na Mwananyamala kwa kazi kubwa wanayoifanya kupunguza kero kwenye Sekta ya Afya” Alisema Makonda.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda jana ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayojengwa Hospital ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa 100%.

  Wodi hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 150 ambapo ndani yake kutakuwa na Vifaa vya kisasa vya kutolea huduma, Vyumba vya Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na sehemu ya kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda akikagua maendeleo ya ujenzi kwenye moja ya chumba katika wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayojengwa Hospital ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa 100%.

  Wodi hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 150 ambapo ndani yake kutakuwa na Vifaa vya kisasa vya kutolea huduma, Vyumba vya Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na sehemu ya kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda akizungumza na Wanahabari mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayojengwa Hospital ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa 100%.

  Wodi hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 150 ambapo ndani yake kutakuwa na Vifaa vya kisasa vya kutolea huduma, Vyumba vya Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na sehemu ya kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.


  0 0

  Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani imezindua visima vitano virefu vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini vilivyotolewa msaada na ubalozi wa Kuwait nchini.

  Visima hivyo vitano vilivyozinduliwa vimejengwa katika kijiji cha Kisayani, Kerekese, Mpafu, Sotele na Sangasanga vya Mkuranga.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo wilayani mkuranga mkoani pwani balozi wa Kuwait Mhe. Jasem Al-Najem alisema serikali ya Kuwait kupitia ubalozi uliyopo nchini inafanya jitihada kubwa kusaidia Tanzania katika nyanja mbalimbali zinazohusu Jamii ikiwemo afya pamoja na maji.

  Aidha balozi Jasem alisema katika kuunga mkono sera ya Rais wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli ya elimu bure wameamua kuanzisha mradi ujulilanao wa kisima kila shule ili kupinguza changamoto ya maji pamoja na kuakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama kwa wakati lengo nikuboresha elimu nchini."maji no muhimu sana uchimbaji wa maji mashuleni sio utasaidia wanafunzi na wanachi wanaoishi karibu na kusaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kupata huduma kamili ya masomo"alisema.

  Pia ubalozi huo umetoa mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya akina mama wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya ya mkuranga ili kuboresha huduma ya afya.

  Aidha Mbunge wa viti maalum mkoa wa pwani Zainabu Vulu alisema afya ya Mama na mtoto ni muhimu sana na kukikosekana vifaa afya ya mama itakuwa hatarishi."tunashukuru sana kwa msaada wenu huu utasaidia sana mama kujifungua mtoto mwenye afya na mwenyewe kubaki mwenye afya "alisema.

  Hata hivyo Mbunge wa jimbo la mkuranga mh. Abdalah Hamis Ulega amewashuru kuwait kwa msaada huo na kusema mpaka sasa wameshachimba visima ishirini visima nane kati ya hivyo ni vya serikali.

  Aidha aliongeza kama Mbunge wa mkuranga aliguswa na kuamua kutafuta wafadhili baada ya kupata barua kutoka kwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi kisayani kutaka kuifunga shule hiyo kutokana na changamoto ya maji,ndipo akawatafuta wafadhili hao ambao wamechima visima virefu vitano vya maji wilayani humo.

  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya mkuranga Filiberto Sanga alitoa wito kwa wanachi kuhakikisha wanakitunza kisima hicho kisiharibike.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Sanga akizunguma na wanacnhi wa kijiji cha Mpafu katika hafala ya uzidunzi wa visima vitano vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini vilivyotolewa msaada na ubalozi wa Kuwait nchini Visima hivyo vitano vilivyozinduliwa vimejengwa katika vijiji vya Kisayani, Kerekese, Mpafu, Sotele na Sangasanga
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akizungumza na wanchi wa kijiji cha Mpafu kataika uzinduzi wa visima virefu vitano vilivyo fadhiliwa na Ubalozo wa Kuwet nchini leo mkoani Pwani.
  Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega akimshukuru Balozi wa Kuwait nchini, Mhe. Jaseem Al Najem kwakuchimba visima hivyo.
  Mganga Mkuu Wilaya ya Mkuranga Dkt.Steven Mwandambo wa (kwanza kushoto) akitoa maelekezo mbele ya Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem,watendaji wakuu wa wilaya katika hafla ya uzidunzi wa visima virefu vitano vilivyo vyenye thamani ya zaidi ya milioni hamsini.
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wa (pili kushoto) akikabidhi watendaji wa wilaya ya mkuranga mabeseni hamsini pamoja na vifaa vya akina mama wakati wa kujifungua katika hospital ya wilaya hiyo.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem akizindua kisima katika kijiji cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdalah ulega.
  Picha ya pamoja
  Balozi wa Kuwait nchini, Mhe Jaseem Al Najem wakionja maji baada ya kuzindua kisima katika kijiji cha Mpafu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Filberto Sanga, Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah ulega.Picha na habari na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii

  0 0








  Kaimu Jaji Mkuu Wa Tanznaia Mhe. Prof. Ibrahim Juma Akifungua Pazia Kuashiria Uzinduzi Wa Mahakama Ya Watoto Leoi Jijini Mbeya. Katikati Ni Mwakilishi Wa Unicef Nchini, Stephanie Shanler Na Kushoto Ni Jaji Kiongozi Wa Mahakama Kuu Ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.
  Kaimu Hjaji Mkuiu Wa Tanznaia Mhe. Porof. Ibrahim Juma Akikata Utepe Kuzindua Jengo La Mahakama Ya Watoto Leo Jijini Mbeya.
  Kaimu Jaji Mkuu Wa Tanznaia Akizungumza Wakati Wa Hafla Hiyo
  Kaimu Jaji Mkuu Wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma Akiwa Katika Picha Ya Pamoja Na Viongozi Wa Mahakama Ya Tanzania Mara Baada Ya Kuzindua Mahakama Ya Watoto Leo Jijini Mbeya
  Msajili Mkuu Wa Mahakama Ya Tanzania Mhe. Katarina Revokati Akiwa Pamoja Na Mwakilishi Wa Unicef Nchini, Stephanie Shanler Na Jaji Wa Mahakama Kuu Mbeya Mhe. Mary Levira Wakati Wa Uzinduzi Wa Mahakama Ya Watoto.
  Jaji Mfawidhi Wa Mahakama Kuu Kanda Ya Mbeya Mhe. Noel Chocha Akizungumza Wakati Wa Hafla Hiyo

  ………………………………………………………………

  Na Lydia Churi-Mahakama, Mbeya

  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma leo amezindua rasmi Mahakama ya watoto katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo nchini kufikia mbili. Mahakama ya kwanza ya watoto iko Kisutu jijini Dar es salaam.

  Mahakama hii ya Watoto iliyoanza kufanya kazi rasmi Aprili 18 mwaka huu jijini Mbeya pamoja na ile ya Kisutu zina kazi kubwa ya kuamua kesi za watoto wanaojikuta wana ukinzani na Sheria zinazohusu watoto nchini pamoja na kutafsiri sheria hizo.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania alisema maendeleo endelevu ya Tanzania yatajengwa kwa misingi ya haki za watoto huku akinukuu andiko la shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na watoto (UNICEF) lisemalo maendeleo ya taifa lolote yatakamilika baada ya watoto kuwa na afya njema, salama pamoja na kupata elimu.

  Alisema uzinduzi wa jengo la Mahakama hiyo ya watoto unaashiria safari ndefu iliyonayo Tanzania ya kuhakikisha haki za watoto zinalindwa kwa kuwa pia bado kuna mikoa mingi ambayo inahitaji huduma hii muhimu.

  Prof. Juma alisema kazi kubwa ya Mahakama ya Tanzania ni kutoa tafsiri pana ya sheria zinazohusu haki za watoto ili kupanua wigo wa ulinzi kwa watoto huku akiwataka Majaji na Mahakimu nchini kutafsiri sheria hizo ili zitekeleze wajibu wao kisheria.

  Akitolea mfano wa Sheria ya Watoto namba 21 ya mwaka 2009, Kaimu Jaji Mkuu alisema sheria hii inashirikisha mihimili yote mitatu hivyo haki zote zinazotajwa na sheria hii ni lazima zipatikane inavyostahili. Prof. Juma pia amewataka Mahakimu wanaosikiliza kesi za watoto kuainisha mapungufu ya sheria hii na kuyawasilisha kwenye kamati ya Jaji Mkuu inayohusu masuala ya Sheria.

  Aidha, Kaimu Jaji Mkuu amewataka Majaji na Mahakimu nchini wanaosikiliza kesi za watoto kujisomea zaidi masuala yanayohusu maendeleo ya haki za watoto kwa kuzisoma taarifa za utekelezaji za nchini pamoja na zile za nchi nyingine ili kupanua uelewa wa sheria hizo.

  Kaimu Jaji Mkuu pia amewataka Majaji na Mahakimu wote kusimamia na kuhakikisha masuala yote yaliyotajwa na Sheria pamoja na mikataba ya kimataifa kuhusu watoto yanatekelezwa pindi wanapofanya ukaguzi kwenye magereza mbalimbali.

  Wakati huo huo, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali amewaomba UNICEF kufikiria na kuangalia uwezekano wa kujenga majengo mengine manne ya mahakama za watoto katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Tabora ili kuwapatia Mahakimu fursa ya kujifunza kwa vitendo namna Mahakama za watoto zinavyofanya kazi.

  Jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya lililojengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na UNICEF limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 415 ambapo Mahakama imechangia kiasi cha shilingi milioni 214 na UNICEF shilingi milioni 201.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakati wa ufunguzi wa sherehe za miaka 100 ya Skauti Tanzania kwenye ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania kuanzia mwaka 1985 mpaka 1995 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Bi. Fatma Karume kwa niaba ya Hayati Mhe. Abeid Amani Karume ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza shughuli za Vijana wa skauti katika visiwa vya Unguja na Pemba kwenye  sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Rais Mstaafu wa Awamu wa Sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume ambaye alikuwa mlezi wa pili wa chama cha Skauti Tanzania kuanzia mwaka 2000 mpaka 2010 wakati wa sherehe za miaka 100 ya Skauti nchini zilizofanyika kwenye ukumbi wa Chimwaga mjini Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvisha nishani Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye alikuwa skauti tangia shuleni na alipokuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika ambapo mwaka 2001 alipendekeza kuwe na siku ya SKAUTI AFRIKA itakayokuwa inaadhimishwa kila tarehe 13 mwezi Machi .

  0 0

  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza (TAKUKURU) imethibitisha kuwahoji wanafamilia wa soka wakiwemo Mjumbe Chama cha Soka Wilaya ya Ubungo (UFA) Shaffih Dauda na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es salaam (DRFA) Almas Kasongo.

  Mbali na hao TAKUKURU wamethibitisha pia kuwahoji Elias Mwanjali, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo, Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwanjaa , Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Mguu mkoa wa Shinyanga Benasta Lugola na wajumbe wa mikoa ya jirani kwa sababu ya kuwepo kwa viashiria vya rushwa na kampeni.

  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale amethibitisha kuwahoji kwa wanafamilia hao wa mpira ambapo waliwashikilia tokea jana saa 3 usiku na wameachiwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea na watakapojiridhisha wanaweza kuwakamata tena.

  Taarifa inasema kuwa wanafamilia hao walitumia mgongo wa Ndondo Cup kufanya jambo lao usiku wa saa 3 jana na ndipo walipotiliwa shaka na kufuatiliwa na kutiwa mikononi mwa Takukuru ambao wamethibitisha kuwashikilia tokea jana usiku na kuwaachia kwa dhamana

  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Mwanza Mhandisi Ernest Makale.

  0 0

  MFANYABIASHARA mdogo wa kuuza duka Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Leonard Bagumako, amekumbwa na mafuriko ya mamilioni kutoka bahati nasibu ya Biko, baada ya kutangazwa kushinda Sh Milioni 20 za droo ya 26 iliyochezeshwa leo.

  Bagumako aliibuka kidedea ikiwa ni siku chache baada ya donge nono kama hilo katika droo ya 25 kwenda kwa Ally Hassan Lukinga wa Mtwara.

  Akizungumza saa chache baada ya kupatikana mshindi huyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano, Hassan Melles, alimpongeza Bagumako kwa kuibuka mshindi kwenye droo hiyo ya aina yake, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa ya uwapo wa Biko kutajirika.

  Alisema biko ni mchezo rahisi unaotoaa ushindi wa zawadi za fedha za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka Jumatano na Jumapili.

  “Kila mtu anaweza kuibuka na shangwe kutoka Biko kwa kutwaa Sh Milioni 20, ambapo kucheza biko ni rahisi kwa sababu inachezwa kwa simu za mikononi ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa wachezaji kufanya miamala kuanzia Sh 1000 na kuendelea, ambapo Sh 1000 ina nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye kuwania sh Milioni 20, huku namba ya kampuni ya Biko ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema.

  Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, aliwataka Watanzania wote kuuamini mchezo wa Biko kwa kwakuwa umekuwa ukiendeshwa kwa kuzingatia kanuni na sheria walizokubaliwa na nchi yetu.
  “Biko ni mchezo ambao kila mtu anaweza kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo pamoja na mamilioni ya mwisho wa wiki, hivyo nawaomba wacheze kwa kujiamini maana unafuata kanuni zote,” Alisema.

  Naye mshindi huyo wa Sh Milioni 20 kutoka Kigamboni, Leonard Bagumako, alipokea ushindi huo kwa furaha, ingawa alisisitiza kuwa bado haamini kama ni yeye aliyepigiwa simu ya kupewa taarifa za ushindi.

  “Ndio mimi huyu huyu unayesema nimeshinda Sh Milioni 20 za Biko” alisema Bagumako huku akisisitiza kwamba amekuwa mchezaji mzuri wa Biko kwa muda mrefu.

  Kwa kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, mchezo wa Biko umeshakabidhi zaidi ya Shilingi Bilioni moja kutoka kwa washindi wao katika mikoa mbalimbali, ikiwa ni mwelekezo mzuri wa uwapo wa mchezo huo wa Biko Tanzania.

  Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki kushoto akiandika kumbukumbu muhimu baada ya kumpata mshindi wa droo ya 26 ya Bahati Nasibu ya Biko, ambapo Leonard Bagumako aliibuka kidedea kwa kujizolea Sh Milioni 20. Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
   

  0 0

  Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala. 
  Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu (BGML) uliopo katika Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga leo Jumatano Julai 26,2017 umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi 460,732,841.08/= kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
  Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew alisema kiasi hicho ni asilimia 67 ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka huu ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma wa mgodi huo katika kipindi hicho.
  “Jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania 687,660,956.84/=,ambapo malipo hayo yamegawanywa katika halmashauri mbili ambazo ni Msalala inayopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopo mkoani Geita inapata asilimia 33”,alifafanua Crew.
  Alisema kutokana na mgawanyo huo,halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 460 (460,732,841.08/= ) na Nyang’wale shilingi Milioni 226 (226,928,115.76/=.
  "Ushuru umepungua kwa kuwa mgodi haujafanya mauzo ya makinikia ambayo yamezuiwa tangu mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu, hivyo tunafahamu kuwa tutalipa zaidi tutakapouza makinikia ambayo yapo yanaendelea kukusanywa mgodini",aliongeza Crew.
  Katika hatua nyingine Crew alisema tangu mwaka 2000 mpaka sasa mgodi huo umelipa zaidi ya shilingi 10,247,742,957/= za kodi ya ushuru wa huduma na kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014.
  “Mgodi wetu unaendelea kuwa na matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji madini katika halmashauri ya Msalala huku tukiendelea kutekeleza mkakati wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa mwaka 2016 kwa kushauriana na wadau lengo likiwa ni kuchangia maendeleo ya Jamii Endelevu inayonufaika na kukua kwa uchumi ndani ya jamii ili kujenga mahusiano ya kuaminika”,alisema Crew.
  Akipokea hundi hiyo kisha kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliushukuru mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa huduma kwa jami.
  “Hiki kiwango cha shilingi milioni 460 tulichopokea ni kiwango kizuri ingawa kimepungua ulikinganisha na kipindi cha miezi sita cha Mwezi Juni hadi Desemba 2016,furaha inatujaza kwamba ile shilingi milioni 300 na zaidi ipo ndani ya Makinikia, yatakapouzwa tutaipata na tutaendelea kuboresha huduma za kijamii”,alieleza Nkurlu.
  Nkurulu alimuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha zilizotolewa na mgodi huo zitumike kwa huduma za kijamii kama zilivyokusudiwa ikiwemo kuboresha huduma za afya na miundombinu.
  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege alisema mapato waliyopokea kutoka mgodi huo yako chini kwa shilingi milioni 300 ukilinganisha na kipindi kilichopita cha kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2016 ambapo mgodi huo ulipokea shilingi milioni 760.
  “Sisi tumepokea mapato haya kama tunavyopkea mapato mengine tunayopata katika halmashauri zetu,mapato haya ni yako chini ukilinganisha na kipindi kilichopita,tunaambiwa mapato yamepungua kutokana na Makinikia ambapo sasa yamesimama,hii inaleta changamoto katika ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu, tunaamini mazungumzo baina Acacia na serikali yakiisha halmashauri yetu itapata mapato mengi zaidi”,aliongeza Berege.

  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama leo Jumatano Julai 26,2017 katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
  Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 iliyotolewa na Mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
  Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala. 
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (kulia) akishikana mkono na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew wakati wa zoezi la kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala. 
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati akimkabidhi hundi hiyo Kaimu Mweka Hazina wa halmashauri hiyo Saleh Bugege (kushoto). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah Ezra Terry.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
  Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.  Aggrey Mwanri amezindua rasmi kambi maalum ya huduma za Afya juu ya upimaji wa Afya bure kwa wananchi mbalimbali Wilayani Nzega, ndani ya Hospitali ya Wilaya ya Nzega. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanri ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwapongeza waandaaji wa kambi hiyo kwani itasaidia kuboresha afya za wananchi ili kuwa na afya njema.

  “Wananchi wanahitaji Afya njema, tunapongeza kwa kambi hii kwani madaktari bingwa waliokuja hapa watatua matatizo ya msingi kwenye afya zetu. Hivyo wananchi mujitokeze kwa wingi” aleleza RC Mwanri. Aidha, Mh. Mwanri amewapongeza  Madaktari bingwa kutoka China ambao wanaendesha kambi hiyo ya siku Sita, iliyoanza rasmi Julai 24 na inatarajia kumalizika Julai 30.
  Hata hivyo, Mh. Mwanri aliwaagiza Wakurugenzi wote wa Mkoa wa Tabora waupokee mpango huo wa kambi za huduma za Afya ili uende mkoa mzima kwani wanakosa fursa ya kuonana na Madaktari bingwa.

  “Ni jambo zuri, tunaomba Wakurugenzi wote mulipokee suala ili wa Mkoa wa Tabora ili liendelee Mkoa mzima. Pia ni wasaha kwa wananchi wote kupeana taarifa ili zienee kwa watu wote wajitokeze hapa Nzega kupatiwa huduma za upimaji na matibabu.” 
  Alieleza Mh. Mwanri huku akimuagiza Mganga Mkuu ahakikishe anaratibu mpango huo uenee Mkoa nzima wa Tabora.

  Kwa upande wake,Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini ameshukuru Serikali ya China kwa kufanikisha tukio hilo ikiwemo kutoa dawa za Maralia kwani kwa msingi huo utasaidia kuokoa maisha ya wananchi wa Nzega.
  “Tunapokea kwa mikono miwili msaada huu wa kutoka Serikali ya China hasa kupitia kwa Balozi wake hapa nchini Tanzania. Dawa hizi ni nyingi nahakika zitasaidia wananchi wote kuanzia wilaya ya Nzega na Mkoa nzima wa Tabora kwa ujumla. Nawashukuru sana wananchi wanaojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuja kupata  huduma za matibabu kwenye kambi hii ya madaktari bingwa hapa Nzega” alieleza Dak. Kigwangalla.

  Zoezi hilo la Upimajj wa Afya Bure Wilayani Nzega, limeandaliwa na Wabunge wa majimbo yote ya  Nzega ambapo imeanza kuanzia hiyo Julai 24 na itatarajiakumalizika Julai 30, huku kwa wakazi wote wa Nzega na jirani wata pima afya zao bure na kupata huduma za matibabu bure, ikiwemo upasuaji. Tayari timu ya Madaktari bingwa wa kila fani ya tiba wapo kwenye kambi hiyo inayoendelea kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nzega.

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa neno la shukrani kwa wote walioshiriki katika kumfariji kipindi cha msiba wa mke wake mpendwa Bi. Linah George Mwakyembe.

  Napenda kutumia fursa hii kwanza kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka zake na pili kutoa shukrani zangu za dhati kwa Watanzania wote kwa upendo na ushirikiano mkubwa mlionipa mimi na familia yangu katika kuomboleza kifo cha mke wangu mpendwa Bi.Linah Widmel-George Mwakyembe na baadaye katika mazishi yake wilayani Kyela.

  Familia inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli; Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kwa mchango wao mkubwa katika kumuuguza marehemu wakati wa uhai wake.

  Aidha, familia inawashukuru viongozi hao waandamizi wa nchi pamoja na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Naibu Spika, Mhe. Tulia Ackson Mwansasu, wake wa viongozi, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, viongozi wetu wa nchi wastaafu, Wabunge, Majaji, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Maaskofu wa Kanisa la Kiluteri, Makanisa ya Moravian na makanisa ya kiroho (Mito ya Baraka, Living Water, Evangelical Brotherhood nk) kwa ushirikiano wao katika maombolezi na mazishi ya marehemu.

  Wana-familia tutakumbuka daima moyo adhimu wa upendo na ushirikiano tulioupata toka kwa Katibu wa Bunge na maafisa wake, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na timu yake mzima ya Wizara, Makatibu Wakuu wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, watendaji wakuu wa taasisi, asasi na kampuni mbalimbali, na wananchi wote kwa ujumla katika kipindi hicho kigumu.

  Pia napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru Wana-Kyela wote kwa uvumilivu waliouonesha kipindi chote cha kumuuguza marehemu na ushirikiano wao wa dhati katika mazishi yake.

  Mwisho lakini si kwa umuhimu, nawashukuru sana madaktari na wauguzi waliomhudumia marehemu kwa kujituma, kwa weledi na ustahimilivu wao ili kuokoa maisha yake lakini Mungu akampenda zaidi. Vilevile wamiliki wa vyombo vya habari, waandishi na watangazaji kwa kukesha nasi kipindi chote cha msiba Dar es

  Salaam na Kyela wakitekeleza wajibu wao wa kitaaluma na vilevile kutufariji wafiwa kwa hali na mali.

  Nawaomba wote mpokee shukrani zangu za dhati na Mwenyezi Mungu awabariki kwa moyo wa ushirikiano na upendo mliouonyesha kwetu.

  Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe.

  Dkt. Harrison George Mwakyembe (Mb),
  WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO,
  26/07/2017.

  0 0

  MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa akikabidhi magari matatu ya wagonjwa (ambulance) ambayo yatasaidia kubeba wagonjwa katika jimbo la Kibaha Vijijini.


  ………………………………………………………………………….

  Na Mwamvua Mwinyi ,Kibaha Vijijini

  MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaa amekabidhi magari matatu ya wagonjwa (ambulance )ambayo yatasaidia kupunguza adha ya usafiri kwa wagonjwa hasa mahututi na warufaa.

  Kati ya magari hayo ,mawili yametokana na nguvu zake na moja ni msaada kutoka kwa Rais John Magufuli ikiwa ni kati ya magari ya wagonjwa 67 yaliyogawanywa katika maeneo mbalimbali nchini .

  Aidha mbunge huyo ,ameiomba wizara ya afya kukipandisha hadhi kituo cha afya cha Mlandizi kuwa hospitali ya wilaya ombi ambalo waziri wa afya,jinsia ,wazee na watoto Ummy Mwalimu amekubali ombi hilo .

  Jumaa aliyasema hayo ,viwanja vya shule ya msingi Mtongani ,Mlandizi wakati Ummy Mwalimu alipokwenda kukabidhi magari hayo kwa niaba yake kwa halmashauri na mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha.

  Alieleza ,ameamua kujikita kutatua kero zinazowakabili kwa kwenda sambamba na kauli mbiu yake ya SISI KWANZA SERIKALI BAADAE .“Ninamshukuru waziri Ummy kwa dhati ya moyo wangu kwa jitihada zake za kupigania gari moja kuletwa Kibaha Vijijini ,”

  “Ni bahati kwetu kwani zilikuwa ambulance 67 ambapo 50 zilielekezwa mikoa ya kanda ya ziwa ambako idadi ya vifo vya mama wajawazito ni kubwa hivyo zilibaki 17 hivyo moja wapo ndio hiyo imekuja kwetu ” alisema Jumaa .Alibainisha kuwa ,magari hayo ni sehemu ya kupunguza tatizo la usafiri linalokabili vituo na zahanati jimboni hapo .

  Alisema ,serikali iangalie uwezekano wa kuwaongezea magari ya wagonjwa katika maeneo ya mbali kama Kwala na Magindu .Hata hivyo Jumaa akizungumzia ombi la kituo cha afya Mlandizi kupandishwa hadhi ,alisema anaendelea kufanya jitihada za kutimiza vigezo vinavyotakiwa kupandishwa hadhi ikiwemo kujenga uzio .

  Alimshukuru makamu wa rais kwa harakati zake za kuhakikisha juhudi hizo zinazaa matunda kwa kuwachangia mifuko ya saruji 500 ,waziri mkuu nae alichangia mifuko hiyo 150 .

  Wadau wengine wamechangia kokoto tani 7 kwa sh. mil. 9.1, mchanga mil. 2.4 tofali sh. mil 8.4, nondo tani moja sh. mil. 3.6 na fedha zake mwenyewe na hadi sasa zimeshatumia sh .milioni 50 .Jumaa aliwaomba wadau wa afya na serikali kuendelea kumuunga mkono ili tatizo hilo libakie historia.

  Alichukua fursa hiyo pia ,kukabidhi vitanda 25 na mashuka 50 vilivyotolewa na Rais katika majimbo mbalimbali nchini .Katika vitanda hivyo 20 ni vya kawaida na vitanda vitano ni kwa ajili ya kujifungulia .

  Akikabidhi magari hayo ya wagonjwa ,waziri wa afya ,jinsia ,wazee na watototo Ummy alisema atachangia mifuko ya saruji 100 ili kuunga mkono ujenzi wa uzio.“Nampongeza Jumaa na mmepata mbunge anaejua kujiongeza ,mtumieni ,mtieni nguvu kwa mambo anayowapigania ” alisema Ummy .

  Alisema kutoka na ahadi walizowahi kutoa wakubwa wake kupandisha hadhi kituo hicho cha afya na kwa kuwa ni wakubwa wake amekubali ombi hilo .

  Ummy alisema pia kuna fedha anaitegemea ambayo atawezesha kujenga wodi ya uzazi yenye sehemu mbili na maabara ya damu kwa lengo la kuboresha huduma za afya .

  “Vigezo vikikamilika kwa namna hiii ,idadi ya watu wanaohudumiwa ,uzio ,idadi ya majengo na mengineyo naamini tutapata hospital ya wilaya iliyo nzuri na iliyokamilika ” alifafanua Ummy .

  Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Mansoor Kisebengo ,alisema watahakikisha wananchi hawagharamii mafuta kwa magari hayo .

  Kisebengo alisema ,halmashauri hiyo itakuwa inachangia gharama za mahitaji ya mafuta ili kuondoa bugudha kwa wananchi .

  0 0

  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri katika jiji la Dar es Salaam ndani ya siku 20 kusiwepo nyumba za wageni pamoja na kumbi za starehe katika maeneo yanayozunguka shule.

  Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na wakuu wa shule za sekondari na Msingi uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es salaam. ambapo amesema kuwa  shule ni kwa ajili ya kutoa elimu hivyo kuwepo kwa vitu hivyo vinafanya kuhalibu na kuwahadaa wanafunzi.

  Amesema kuwa maeneo yote ya shule yapimwe ili kusiwepo kwa mazingira ya kuweza watu kufanya kujenga maeneo hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na maafisa elimu, waalimu wakuu shule za sekondari na msingi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akizungumza na katika Mkutano wa Walimu Wakuu Shule za Sekondari na Msingi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Shule Kisarawe 11, Elieshi Emmanuel akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Shule juu.
  Mkutano ukiendelea.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii

  0 0


   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi Mkoani Simiyu.
  PICHA B
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akifuaahia jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kumaliza mahojiano na waandishi wa habari wakati wa ziara yake mkoani Simiyu.
  PICHA C (2)
  Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro(hayupo pichani) katika kikao alichofanya akiwa ziarani mkoani humo.
  PICHA D
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akisalimiana na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu
  PICHA E
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (kulia) na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo wakati wa ziara yake mkoani humo.
  PICHA F
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro (kulia) akizungumza na Kamati ya Ulizi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani humo,(baadhi ya wajumbe hawapo pichani).
  PICHA J
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro akisalimiana na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Chele Ndaki mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu
  PICHA K
  Kaimu Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Simiyu(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu
  PICHA L
  Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Ndg.Simon Maganga(kulia) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu.
  ……………………………………………………………………
  Na Stella Kalinga, Simiyu
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Inspekta Generali Simon Sirro amesema Makamanda wa Polisi wa Mikoa wataendelea kubaki katika vituo vyao vya kazi endapo watatimiza wajibu wao na kupunguza uhalifu katika mikoa yao.
  IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kamaliza mazungumzo yake na Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
  IGP Sirro amesema Makamanda wa Polisi Mikoa wanapaswa kutimiza wajibu wao  katika kujali na kusimamia suala la Ulinzi na Usalama katika mikoa yao ili wananchi wakae kwa amani na mali zao ziwe salama.
  “ Moja ya lengo la ziara yangu ni kuwakumbusha askari wa jeshi la polisi uwajibikaji na kuwajibika ni pamoja na kulinda watu na mali zao,  makamanda wa polisi mikoa nimewaambia kamanda ataendelea kukaa kwenye mkoa ule kama uhalifu utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa” amesema Sirro
  Inspekta Sirro amesema ziara yake pia imelenga kuwakumbusha askari majukumu yao katika kuhakikisha wanawajibika kutimiza kiapo chao na kutenda haki ili wananchi waendelee kuliamini Jeshi la Polisi.
  Kiongozi huyo pia ameelekeza viongozi wa jeshi la polisi wasiwanyime haki ya  dhamana watu wenye makosa ya kawaida ambayo yana  dhamana isipokuwa kwa makosa makubwa yakiwepo ya mauaji, kughushi na mengine yanayohitaji upelelezi.
  Kuhusu suala la kuwepo kwa mahusiano mabaya kati ya baadhi ya Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Waandishi wa habari, Inspekta Sirro amefafanua kuwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa watimize wajibu wao kama watumishi wa Umma kwa kuwajali waandishi kama wanavyowajali wateja wengine kwa kufuata sheria na akawataka waandishi wa habari wafuate sheria, kanuni na taratibu pasipo kuvuka mipaka.
  Akakimkaribisha Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini, katika Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka amemshukuru Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Boniventure Mshongi na Jeshi la Polisi kwa ujumla kwa namna wanavyoshirikiana katika suala la ulinzi na usalama.
  Aidha, amemuomba Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini kuona uwezekano wa kusaidia kujenga majengo ya Ofisi na nyumba za makazi kwa ajili ya  Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.
  Inspekta Simon Sirro amewasili Mkoani Simiyu akitokea Mkoani Mara akiwa katika ziara yake ya kikazi ambapo pamoja na kuzungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Wilaya ambao pni Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya,  pia  amezungumza na viongozi na askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

  0 0










  Mwenyekiti wa Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Young Human Rights Advocates (TYHRA) Samwel Shami akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu wachimbaji wadogo wa dhahabu kumpongeza Rais Magufuli leo Jijini Dar es Salaam.

  …………………..

  Na. Neema Mathias- MAELEZO

  Wachimbaji wadogo wa dhahabu kutoka wilaya ya Kahama wanatarajia kutembea kwa miguu kutoka Kahama mpaka Dar es salaam kwa ajili ya kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa juhudi zake za kuijenga Tanzania mpya.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Young Human Rights Advocates (TYHRA) Samwel Shami kwa niaba ya wachimbaji hao, alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam.

  “Tumeamua kwa hiyari yetu kutembea kwa miguu na baiskeli kutoka Kahama mpaka Dar es Salaam kumpongeza Rais wetu mpendwa na tunaomba Watanzania wenzetu wanaoipenda nchi yetu watuunge mkono”, alisema Bw. Shami.

  Bw. Shami amesema kuwa wachimbaji hao wamefurahishwa na juhudi za serikali ya awamu ya tano pamoja na moyo wa utu wa Mhe. Raisi katika kuhakikisha rasilimali za Tanzania zinawanufaisha Watanzania wote.

  “Kuna wakati tulijiona kama yatima kwenye nchi yetu, na tulianza kuamini kuwa dhahabu yetu imegeuka laana badala ya baraka alizotupatia mwenyezi Mungu bure, lakini sasa tunaiona nuru kubwa kupita Raisi wetu”, amesisitiza Bw. Shami.

  Aliendelea kusema kuwa mwaka 2008, Shirika la TYHRA kwa kushirikiana na wachimbaji wadogo, wadau wa maendeleo na wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu walianzisha harakati zilizojulikana kama ‘Native Solidarity Movement’ kwa lengo la kudai haki zao za msingi katika migodi lakini hazikuzaa matunda.

  Hata hivyo Bw. Shami ameyaomba mashirika mengine yasiyo ya kiserikali na yeyote anayeitazama Serikali kwa jicho la maendeleo na mwenye mapenzi mema na nchi yake wajaribu kutumia nguvu kubwa kuipongeza, kuishauri na kuitia moyo serikali kama wanavyotumia nguvu kubwa kukosoa na kulaani mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali.

  Bw. Shami alifananisha matatizo na changamoto za Watanzania sawa na kupewa tembo mkubwa kumla, jambo ambalo linahitaji hatua kwa hatua, kipande kwa kipande, hivyo aliwataka Watanzania wampe Rais muda wa kutatua changamoto zao kwani juhudi zake zimeonekana toka alipoingia madarakani.

  Shirika la Young Human Right Advocates linajihusisha na utetezi wa haki za binadamu na wadau wa maendeleo. Shirika hilo linashirikiana na wachimbaji wadogo wa wilaya ya Kahama kuchangia maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa na pia kukemea na kuelimisha jamii.

  0 0



  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu toka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila (kushoto) akitoa neno la utangulizi kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


  Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo toka kwa mshiriki toka Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelekezo toka kwa mshiriki toka Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelekezo toka kwa mshiriki toka Chuo Kikuu Nelson Mandela wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Vyuo Vikuu nchini Prof. Jacob Mtabaji (kushoto) akitoa neno la utangulizi kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wanafunzi wakipata maelekezo ya namna ya kujiunga na vyuo vikuu wakati wa uzinduzi wa maonesho ya 12 ya vyuo Vikuu nchini mapema hii leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

  ………………………….

  Na. Paschal Dotto – MAELEZO

  Vyuo vikuu vilivyofungiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018 vimetakiwa kukamilisha matakwa yanayohitajika kwa kufuata taratibu zilizowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).

  Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo, wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 12 ya vyuo vikuu nchini yanayofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini, Dar es Salaam.

  “Vyuo vikuu vyote nchini vinatakiwa kutoa elimu bora kwa wahitimu ili kuwawezesha kujiajiri na kuendana na Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kujenga Tanzania yenye viwanda,” amesema Majaliwa.

  Majaliwa ameongeza kuwa, ili kujenga uchumi wa viwanda vyuo vikuu hapa nchini vinatakiwa kufundisha na kuwawezesha wahitimu kujiajiri ili kuendana na ushindani katika soko la ajira kitaifa, kimataifa na Dunia kwa ujumla.

  Vile vile vinatakiwa kukuza stadi katika sekta ya viwanda kwa kupata wasomi waliofundishwa kwa vitendo kutoka katika vyuo mbalimbali, kuweka mikakati na kuboresha elimu ili kuendana na dhamira ya Serikali pamoja na kuweka mitaala mizuri kwa wanafunzi katika vyuo hivyo ili kuendana na mabadiliko yaliyofanywa katika udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2017/2018.

  Aidha Majaliwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa bajeti Shilingi Tril. 4.7 kwa Wizara ya Elimu ili kuboresha elimu ambayo itahusisha katika kujenga na kuboresha miundombinu ya elimu hapa nchini ikiwemo mikopo ya elimu ya juu na mahitaji mengine ya vitabu kwa shule za Sekondari.

  Naye Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amevitaka vyuo vikuu hususani vile vilivyofungiwa kwa kutokidhi matakwa ya utoaji elimu hapa nchini, kukaa na kuweka mambo sawa ili waweze kufanyiwa uhakiki upya na TCU.

  “Ili chuo kiweze kukamilika kutoa elimu bora lazima kiwe na miundombinu bora, wahadhili waliobobea, mitaala safi, wanafunzi wenye sifa na kujituma,” amefafanua Mwijage.

  Maonesho hayo ni ya 12 tangu yalivyoanzishwa mwaka 2005 ambapo kwa mwaka huu zaidi ya vyuo vikuu 80 kutoka ndani na nje ya nchi vinashiriki. Maonesho yatafanyika kwa siku Nne kuanzia Julai 26 hadi Julai 29 mwaka huu.

  0 0


   Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Angelina Kwinga, akizungumza na maofisa Ugani wa wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani kutoka kata zote na vijiji vya wilaya hiyo wilayani humo leo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Martha Susu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adam Malunkwi.
   Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Margareth Nakainga, akizungumza katika mafunzo hayo.
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Adam Malunkwi, akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya hiyo kufungua mafunzo hayo. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Paschal Byemelwa.
   Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange akitoa mada.
   Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa wilaya hiyo, Abdulusalam Kajuna, akizungumza.


  Mtafiti wa zao la Pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ugirigulu Mwanza, Stellah Chilimi akitoa mada.
   Maofisa ugani wakiwa katika mafunzo.
   Mafunzo yakiendelea.
   Mafunzo yakiendelea.
  Semina hiyo

  Maofisa ugani wa wilaya hiyo wakijitambulisha kwa mkuu wa wilaya.
  Wanahabari wakiandaa taarifa hiyo. Kulia ni Doreen Mlay wa TBC na Hellen wa Time FM.


  Picha ya pamoja ya maofisa ugani na mgeni rasmi mkuu wa wilaya.

  Na Dotto Mwaibale

  MKUU wa wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora, Angelina Kwingwa ameomba watafiti nchini kufanya utafiti wa mazao ya chakula yanayostahimili ukame ili kuwezesha wananchi kupata chakula cha kutosha kutokana na ukame kuathiri mazao hayo wilayani humo.
  Ombi hilo amelitoa leo wakati akifungua mafunzo kwa maafisa ugani wote wa wilaya hiyo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia( COSTECH),  kupitia Jukwaa la Bioteknojia kwa maendeleo ya kilimo (OFAB)  yenye lengo la kuwawezesha maofisa ugani kutumia teknolojia na tafiti katika kupunguza changamoto zinazowakabili wakulima na kuongeza tija.

  Amesema wananchi wa wilaya hiyo zao lao kuu ni Tumbaku ambalo nilo zao la biashara lakini wanategemea sana Mahindi pamoja na mpunga ingawa mabadiriko ya tabia ya nchi yamekuwa yakiathiri sana uzalishaji wa mazao hayo ya chakula na kupelekea baadhi yao kuwa na upungufu wa chakula.

  “Watafiti tunaomba mtuletee mbegu bora za mihogo  ambazo zinakinzana na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia kama zamamani kwani mihogo ya wakulima ya asili ambayo ilikuwa mizuri na iliyowapa tija wakulima miaka ya nyuma  imepotea kutokana na kushambuliwa na magonjwa” alisema  Kwingwa.

  Ameishurkuru COSTECH kwa kupeleka mafunzo hayo kwenye wilaya yake ili kuwakumbusha wataalamu hao wa ugani mbinu bora za mazao ya mihogo,mahindi,mpunga na viazi lishe ambayo ni mazao muhimu kwa chaula kwa wakazi wa wilaya na zao la biashara la pamba kama ambalo litasaidia na zao la Tumbaku katika kuongeza uchumi kwenye kaya.

  Ameahidi msimu ujao kutembea kila kata kuangalia kama wakulima wamepelekea mbinu hizo walizofundishwa kwa kukagua mashamba na kuwauliza maswali ili kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanaleta tija iliyokusudiwa ikizingatiwa kuwa Rais Dk.John Magufuli  alishasema hataki kusikia njaa wilaya yoyote.

  “Hakuna uchumi wa kati na viwanda endapo wakulima hawataweza kuzalisha mazao na malighafi za kutosha kulisha viwanda ambavyo serikali ya awamu ya tano inavihamasisha kujengwa na wataalamu hawa  ndio watakaowezesha wakulima kuzalisha malighafi hizo za kutosha  sipo tayari kuonekana siendani na kasi ” alisisitiza 
  Kwingwa.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo ya Urambo Magreth   Nakainga amesema wakulima wengi hivi sasa wanaotegemea zao la Tumbaku hawana hela na wanashindwa kumudu kujikumu kwenye mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kutokana na wanunuzi wa zao la Tumbaku kutofika kununua tumbaku ya wakulima kwa  wakati.

  Amesema wakulima wamelima vizuri na kuzalisha Tumbaku ya kutosha lakini wamebaki  na Tumbaku yao majumbani mwao hali ambayo inawadhoofisha kimaisha kutokana na fedha walizozitegemea kwenye kupeleka watoto shule,kununua mahitaji mengine  hazijanunuliwa na wanunuzi wa tumbaku na hivyo kukwamisha maendeleo ya wakulima.

  “ Hivi sasa tunahimiza zao la Pamba kwa wakulima wetu kwenye wilaya nzima kutokana  na soko la Tumbaku kutokuaminika husussani soko lake kwahiyo mafunzo haya yatasaidia sana kuamsha maafisa ugani wetu kupata dozi ya kutosha kuwafundisha  wakulima kukimbilia zao la Pamba” alisema Nakainga.

  Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Adam Malunkwi amesema halamashauri hiyo  itahakikisha mafunzo hayo yanatekelezwa kwa vitendo kwenye mashamba ya wakulima  kwakuwa wamewawezesha kila afisa ugani kupata baiskeli katika awamu ya kwanza lakini pia sasa wamewapatia pikipiki maafisa ugani wote ili waweze kutekeleza  majukumu yao kwa ufanisi.

  Amesema umefika wakati sasa wakulima wapewe mbegu bora za mpunga ambazo  zinastahimili ukame kutokana na hasara kubwa waliyoipata wakulima msimu uliopita  ambapo pamoja na kulima vizuri lakini mpunga wao umekauka na hivyo kuwakosesha 
  chakula wakulima wengi ambao wanalima kwenye mabonde.

  Katika hatua nyingine amelalamikia baaadhi ya mbegu za kilimo wanazouziwa wakulima  hazioti na hazifanyi vizuri kwenye wilaya hiyo na hivyo kuomba watafiti na wauzaji 
  wa mbegu kuwapelekea wakulima mbegu ambazo zinastahili kulimwa kwenye udongo wao.

  "Watafiti na serikali mtusaidie kufanya uchunguzi wa mbegu hizi zinazoletwa kwa wakulima wetu maana wanazinunua dukani na zina nembo zote ila hazioti na zikiota 


  0 0

  Kufuatia barua aliyopokea Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai kutoka kwa Mwenyekiti Prof. Ibrahim Haruna Lipumba na Kaimu Katibu Mkuu Mhe. Magdalena Hamisi Sakaya (Mb) wa Chama cha Wananchi (CUF), Mheshimiwa Spika angependa kuwaarifu Watanzania wote kwamba amejiridhisha kuwa Wabunge hao wamefukuzwa Uanachama kulingana na taratibu za Chama hicho na hivyo wamekosa sifa za kuendelea na Ubunge. Wabunge hao ni: - 


  1. Mhe. Severina Silvanus Mwijage, (MB);

  2. Mhe. Saumu Heri Sakala, (MB);

  3. Mhe. Salma Mohamed Mwassa, (MB);

  4. Mhe. Riziki Shahari Mngwali, (MB);

  5. Mhe. Raisa Abdallah Mussa, (MB);

  6. Mhe. Miza Bakari Haji, (MB);

  7. Mhe. Hadija Salum Ally Al-Qassmy, (MB); na

  8. Mhe. Halima Ali Mohamed, (MB).

  Hivyo, kwa mamlaka aliyonayo kwa kuzingatia kifungu cha 67(1)(b) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 kikisomwa pamoja na kifungu 37(3) cha Sheria ya Uchaguzi Sura 343 kama ilivyojadidiwa Mwaka 2015, Mheshimiwa Spika ametangaza nafasi hizo kuwa wazi na pia kumuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili aendelee na hatua zinazostahili kujaza nafasi hizo kwa Mujibu wa Sheria na Taratibu zilizopo.

  Imetolewa na: 
  Ofisi ya Spika,
  S. L. P. 941,
  DODOMA.
  26 Julai, 2017

  0 0


  1Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – George Simbachawene akisikiliza kwa makini taarifa ya wananchi wa Kijiji cha Lukole wakati wa ziara yake katika Jimo la Kibakwe.
  2Baada ya Waziri wa George Simbachawene (Kulia) kupokea malalamiko ya wananchi wa Kijiji cha Lukole kuhusu shida ya maji alikwenda kwenye bomba la Kijiji kuzungumza na wakina mama ambao ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo na kuwataarifu namna ambavyo amekwishaanza kushughulikia kero hiyo.
  3Wananchi wa Kijiji cha Kingiti walimsimika WaziriSimbachawene kuwa Chief wa Kigogo na kumkabidhi vifaa Vya Kimila.
  4Waziri wa Tamisemi George Simbachawene (katikatialiyekaa) akisimikwa kuwa chief wa Kigogo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kingiti.
  5Waziri wa Tamisemi Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kingiti wakati wa zaiara yake katika Jimbo la Kibakwe.

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimsalimia Mama mwenye ulemavu na kumpatia kiasi cha fedha alipokutananae wakati wa msafara wake kuelekea katika uzinduzi wa Ofisi ya Tawi la Bugarika Kata ya pamba.


  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiweka jiwe la msingi katika ofisi ya Tawi Bugarika wilayani nyamagana Mkoa wa Mwanza

  jiwe la msingi lililo wekwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
  Shaka Hamdu Shaka (MNEC) wilayani nyamagana Mkoa wa Mwanza.

   Injinia wa Barabara Ndg:Emilly Mbaga (kwanza kulia) akitolea ufafanuzi namna ya kuandaa mawe kabla ya kutengeneza barabara ya mawe kwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) (wa kwanza kushoto) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Ndg:Stanslaus Mabula wakati wa kushiriki ujenzi wa Barabara ya mawe Wilayani Nyamagana kata ya pamba Bugando.

   Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) (wa pili kulia)akishiriki Ujenzi wa barabara ya mawe kata ya Pamba Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza.

   Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) pamoja na Wanachama ,Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake wakiwa na shamra shamra alipowasili katika kikao cha ndani pa

  Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM Wilaya ya Nyamagana bi:Odilia Batimayo akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL.


  Baadhi ya mabango yakiwa na jumbe mbalimbali kwa ndg:Kaimu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa ccm Ndg:Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

  Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg:Hussein Kim akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL

  Naibu Mstaiki Meya wa jiji la mwanza Mhe: Biku kotecha akisalimia na kuwakaribisha Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL

  Mbunge wa jimbo la nyamagana Mhe:Stanslaus mabula akisalimia
  na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya mbunge jimbo la
  nyamagana kwa vijana katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL

  ndg:Rooben Sixbert Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Mkoa wa Mwanza akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) kuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL

  Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akuzungumza na Viongozi mbali mbali wa chama na jumuiya zake katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)


  Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa
  umesema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM na Jumuiya zake zote hakiokoti
  wanachama barabani, uchochoroni, ama mtaani kama ilivyo katika vyama
  vingine ambavyo sio CCM.

  Umoja huo umesema kuwa kuokota Viongozi barabarani ni
  kuzalilisha Chama na Jumuiya zake na kupoteza Misingi ya uwajibikaji na
  utendaji ya kupata viongozi walioandaliwa kuanzia ngazi ya Shina, Tawi,
  Mpaka Taifa.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg
  Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Leo Julai 25, 2017 katika Ukumbi wa BELMOUNT
  FIRMOUNT HOTEL uliopo Manispaa ya Nyamagana Wakati wa ziara ya siku moja
  alipokuwa akizungumza na Vijana wa Jumuiya ya Chama hicho (UVCCM)
  pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM).

  Shaka alisema kuwa Chama cha Mapinduzi hufanya maandalizi
  ya uchaguzi Mkuu pindi tu unapomalizika uchaguzi kwa kuwapata Madiwani,
  Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza Kusimamia
  na kufatilia utekelezaji wa ilani ya ushindi ya CCM.

  Alisema kuwa anavionea huruma vyama vya upinzani kwani
  havitaweza kuwa na mgombea Mwenye uwezo wa kushindana na Mwenyekiti wa
  CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe
  Magufuli kwani kazi kubwa anayoifanya nchini katika kipindi cha utendaji
  wake kinaungwa mkono na Wananchi wote wakiwemo wale wa Chama vya
  upinzani na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi.

  “Vijana wenzangu napenda mtambue kuwa siku zote Kizuri
  Chajiuza na kibaya chajitembeza, Hivyo Rais Magufuli ni KIZURI ambacho
  kinajiuza chenyewe bila hata kutembezwa na mtu yeyote” Alisema Shaka

  Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kitaendelea kushinda
  kwa haki, Amani na Demokrasia pasina vurugu, Ghubu, na visilani kama
  inavyofanywa na vyama vingine visivyo CCM.
  “Nataka niwakumbushe tu ndugu zangu wanachama wenzangu wa
  Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa nchi yetu ya Tanzania haijawahi kuwa na
  vyama vya upinzani Bali imewahi kuwa na vyama vya vurugu na kejeli dhidi
  ya Serikali yao”

  “Ninazo taarifa kuwa kuna Kata moja wamepitishwa wahenga
  kwenye uchaguzi wa Vijana sasa natoa maelekezo kwa Katibu wa UVCCM
  Wilaya ya Nyamagana na Mkoa wa Mwanza kusimamia na kuwatoa haraka kwani wakiwaacha mpaka wakaingia kwenye uchaguzi watakuwa wamekiuka taratibu na Kanuni za Uchaguzi” Alisisitiza Shaka

  Katika Ziara hiyo Kaimu Katibu Mkuu huyo ameshiriki ujenzi
  wa Ofisi ya CCM Tawi la Bugarika Kaskazini na kuahidi kumalizia katika
  upauaji jambo ambalo limemfanya pia Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe
  Stanislaus Mabula kuchangia Bando tatu za bati ili kumuunga mkono Kaimu
  Katibu Mkuu UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka.

  Aidha, Shaka ameshiriki ujenzi wa barabara inayojengwa kwa
  kiwango cha Mawe yenye urefu wa Kilomita moja kwani itatoa urahisi wa
  Huduma za kijamii hususani kwa Wakati wa Kaya ya Mahina na Kata ya
  Pamba.

  Shaka amesisitiza mipaka ya kazi na kuwepo heshima kwa
  kuchagua viongozi wenye sifa za kuchaguliwa huku akiwakumbusha Vijana
  Kujiunga katika vikundi Mbalimbali ambavyo watavisajili na hatimaye
  kuandika barua ya kuomba mikopo ambayo inatolewa na Serikali kwa riba
  nafuu ya shilingi 50,000 kwa kila wanapokopa Milioni Moja.

  0 0


   Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akipokelewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari na Mawasiliano, Utawala wa Mitandao kutoka Jamhuri ya watu wa China, Bibi.Tang Song alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na Mawasiliano ya Mitandao ya China.
  2
  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz akielezea jambo wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na Mawasiliano ya Mitandao ya China. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Rodney Thadeus
  3
  Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na Mawasiliano ya Mitandao ya China. Kutoka kulia ni  Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz  na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Rodney Thadeus (katikati).
  4
  Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akizungumza mbele ya wadau wa habari na mawasiliano mtandao kutoka China na Tanzania wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na Mawasiliano ya Mitandao ya China.
  5
  Naibu Waziri wa Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akifurahia jambo akiwa pamoja na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Rodney Thadeus (kushoto) alipokuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mkutano wa majadiliano kuhusu Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Mtandao leo  Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umefanyika kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya mitandao chini ya uratibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania na Wizara ya Habari, na Mawasiliano ya Mitandao ya China.

  0 0

  Muonekano wa ramani ya Mji mpya wa Fumba unaosimamiwa na Kampuni ya DSG kutoka Ujerumani ambao utatambulishwa rasmi kwa wananchi tarehe tano na sita mwezi ujao.
  Ofisa Mkuu wa Operesheni katika Kampuni ya DSG inayojenga mji wa kisasa Fumba, Tobias Dietzold, akizungumza na waandishi wa habari kuelezea maandalizi ya kuutambulisha mradi wao. Mkutano huo umefanyika ofisini kwao Migombani mjini Zanzibar.
  Meneja Mauzo wa Kampuni ya DSG inayojenga mji wa kisasa na nyumba za makaazi katika kijiji cha Fumba, Said Ally Said, akitoa ufafanuzi wa masuali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano wa kuutambulisha mradi wao kwa wananchi.

  Picha na Makame Mshenga.

  …………………………………………………………

  Na Salum Vuai Maelezo Zanzibar.

  Kampuni ya DSG inayoendesha ujenzi wa mji wa kisasa katika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi B, imeandaa maonesho maalumu ili kuutambulisha mradi huo kwa wananchi wa Zanzibar na watu mbalimbali kutoka maeneo mengine.

  Ofisa Mkuu wa Operesheni katika kampuni hiyo Tobias Dietzold, amewaambia waandishi wa habari kuwa, maonesho hayo yatakayofanyika Agosti 5 na 6 mwaka huu, yatahudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud, Mkurugenzi wa ZIPA Salum Khamis Nassor na wananchi mbalimbali.

  Alisema mradi huo uliopewa jina la ‘Fumba Town Development’, unalenga kuunga mkono mipango ya serikali katika kuyabadilisha maisha ya Wazanzibari, ambao kama walivyo watu wa nchi nyengine, wanahitaji makaazi bora pamoja na huduma nyengine muhimu za kijamii.

  Dietzold aliwatoa wasiwasi wananchi wa visiwa hivi ambao hawana uwezo mkubwa wa kifedha, akiwataka wafute dhana kwamba nyumba hizo zinajengwa kwa ajili ya matajiri, akisema bei zake zinapishana kulingana na aina ya nyumba zenyewe.

  Alifahamisha kuwa kampuni yake imeandaa usafiri wa mabasi wa uhakika na wa kutosha kuweza kuwasafirisha watu watakaopenda kwenda Fumba kujionea maonesho na jinsi mji huo unavyojengwa.

  Aidha amesema maandalizi yamefanywa kwa watu watakaohudhuria kupata huduma mbalimbali zikiwemo za chakula na vinywaji.

  Naye Mkuu wa kitengo cha mauzo katika kampuni hiyo Said Ali Said, amesema mradi huo uliofunguliwa rasmi mwezi wa Agosti 2015, na kuanza ujenzi Oktoba mwaka jana, umefikia hatua nzuri ambapo takriban nyumba 75 zimeshaezekwa zikiwemo za ghorofa nne.

older | 1 | .... | 1316 | 1317 | (Page 1318) | 1319 | 1320 | .... | 1897 | newer