Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

MBUNGE MUSSA AINGILIA KATI MGOMO WA MADEREVA DALADALA AWATAKA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku akizungumza na madereva wanaofanya safari zao kati ya Masiwani,Magomeni,Majengo na Raskaone Jijini Tanga   waliogoma kutoa huduma kwa siku nzima wakiishinikiza Halmashauri kuikarabati barabara wanazozitumia kutokana na ubovu ambapo Mbunge huyo aliwataka kuendelea shughuli zao wakati kilio chao kikifanyiwa kazi
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani (RTO)Nassoro Sisiwaya akizungumza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na waansdishi wa habari kuhusu namna halmashauri ilivyoweza kulitatua tatizo hilo mara moja kwa kupitisha greda kuichonga
 Kaimu DTO wa wilaya ya Tanga,Imani Raphael akizungumza katika tukio hilo la mgomo wa madereva hao
Kaimu DTO wa wilaya ya Tanga,Imani Raphael akizungumza na  madereva hao ambapo aliwataka kuendelea na shughuli zao wakati suala lao likishughuliwa na mamlaka husika
Diwani wa Kata ya Duga (CUF) Khalid Rashid akizungumza katika mgomo huohabari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

KUKAMATA VIONGOZI WA KISIASA NA VIONGOZI WA DINI SI KOSA“ IGP SIMON SIRRO ”

$
0
0
Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amesema kukamata viongozi wa kisiasa na dini si kosa bali ni sehemu ya majukumu ya Jeshi la polisi kukamata kama amevunja sheria. Hii hapa video yenye habari yake.  
Kazi yetu Ruvuma TV ni kuhabarisha umma, hivyo tumekusogezea matukio sita yaliyotokea mkoani Ruvuma kuanzia Jul 17 – Jul 23, 2017.

VIJUSO VYA MAGAETI YA JUMANNE LEO JULY 25,2017

Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara akabidhiwa Sh Milioni 20 za Biko

$
0
0
MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, jana amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko, jumla ya Sh Milioni 20.
Makabidhiano hayo yamefanyika jana mkoani Mtwara katika benki ya NMB, ambapo Lukinga aliishukuru Biko na kusema kuwa fedha hizo atazitumia vizuri kuhakikisha zinakuza uchumi wake.
“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha hizi ambazo kwa hakika nitazitumia vizuri kama sehemu ya kupiga hatua kiuchumi kama dhamira ya Biko kuanzisha bahati nasibu yao.


“Awali sikuamini kama naweza kushinda donge nono la Sh Milioni 20, hivyo ni wakati huu Watanzania wote kuamini kwamba Biko ni mchezo wa kubahatisha wa watu wote, maana kama hata mimi wa Mtwara nashinda, ndio kusema yoyote anaweza kushinda,” Alisema.

Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan Melles, alimpongeza Lukinga kwa kukabidhiwa fedha zake, huku akiwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa ya Biko ili washinde zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kila wakati, sambamba na droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka Jumatano na Jumapili.

“Jumapili hii amepata Lukinga ambapo leo tumemkabidhi fedha zake, hivyo wote mnaweza kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ya kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea kikiwa Sh 1,000 na kuendelea,” Alisema.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Biko inaendelea kutoa zawadi mbalimbali zikiwapo za papo kwa hapo na zile za Milioni 20, hivyo yoyote atakayeshinda katika Mkoa wa Tanzania atafikishiwa fedha zake haraka iwezekanavyo ili azitumie kwa ajili ya maendeleo yake.

“Kumpatia fedha zake Lukinga wa mjini Mtwara ni nafasi ya kumsubiri mwingine aibuke na mamilioni ya Biko ili naye apate chake, maana Biko ipo kwa ajili ya Watanzania wote, hivyo dawa ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi wakati wowote na mahala popote kwenye mikoa yote ya Tanzania,” Alisema.

Baada ya kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Mtwara, mshindi mwingine wa Sh Milioni 20 anatarajiwa kupatikana Jumatano ama (Jumatamu) kama wanavyoita, ikiwa tayari Biko wameshakabidhi zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi ya Mei na Juni pekee.


Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven mwenye fulana ya Biko kushoto akiwa ameshika hundi saa chache kabla ya kumkabidhi kiasi cha fedha cha Sh Milioni 20 mshindi wa Mtwara, Ally Hassan Lukinga katikati. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.


Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko Tanzania, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia, akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa mjini Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyeshinda katika droo ya 24 Jumapili. Kulia ni Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.
Ally Hassan Lukinga kulia akifurahia fedha zake alizokabidhiwa na Biko mkoani Mtwara.

DC ASIA ABDALLAH :IRINGA ACHENI MAJUNGU FANYENI KAZI KUKUZA KIPATO CHENU

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza na wanachama na wadau wa timu ya lipuli kwenye mkutano wa uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa timu ya lipuli uliofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Mwembetogwa.
Baadhi ya wadau na wanachama wa timu ya lipuli wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo bi Asia Abdallah

Na fredy Mgunda, Iringa.

Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah aliwataka wananchi wa Mkoa wa Iringa kuishi bila kuwa na majungu kwa sababu majungu yanarudisha nyuma maendeleo.

Hayo yamesemwa wakati wa hotuba ya uchaguzi wa kuwapa viongozi wapya wa timu ya Lipuli katika ukumbi wa shule ya sekondari ya mwembetogwa  ulipo Manispaa ya Iringa.

Abdallah alisema kuwa Iringa kumekuwa na majungu ambayo yamekuwa yakileta uchonganishi baina ya watu na watu pia viongozi na viongozi hivyo inatakuwa kubadilika na tusiishi kwa mazoea.

"Ukiiinga huku majungu kule majungu hasa mtu hana pesa ya kula lakini anashinda kwenye mitandao ya kijamii kuleta majungu,fanyeni kazi kwa nguvu zenu zote maana mnaendekeza tu majungu ambayo hayana manufaa kwako binafsi hata taifa kwa ujumla"alisema Abdallah

Aidha Abdallah alisema kuwa viongozi wa timu ya lipuli watakaoingia madarakani kuhakikisha wanavunga makundi yote ya majungu na kuhakikisha timu inakuwa na umoja na ushirikiano kila nyanja ili kupata mafanikio makubwa ambaya yataleta faraja kwa wakazi wa Iringa na wapenda Soka.

"Haiwezikani kila kona ni majungu tu hivi nyie hamna kazi za kufanya tena afadhali wanawake wangekuwa na majungu lakini majungu hayo yanaongozwa na wanaume kwenye magroup ya what's up,achaneni na magroup ambayo hayana faida kwako wala hanaya afya kwa taifa la Tanzania" alisema Abdallah

Mohammed aliongeza kwa kusema kuwa Rais wa jamhuli ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli anahimiza wananchi kufanya kazi na sio kutengeneza majungu ambayo yamekuwa yakikwamisha maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake Katibu wa chama cha Soka Mkoani Iringa Dr Ally Ngalla alimshukuru Mkuu wa wilaya huyo kwa hotuba nzuri na kumuahidi kuwa Iringa itabadilika na kufuta majungu kutokana na tayari wamepata viongozi wapya wa timu ya lipuli.

"Nikiwa kama kiongozi nitahakikisha makundi yote ya majungu yanavunjwa na kuwa kitu kimoja ambapo tutafanya kazi kama siafu ili kuinua Mpira wa miguu Mkoani Iringa "alisema Ngalla

Ngalla aliwata wadau wa mpira miguu Mkoani Iringa kusahau yaliyopita na kuangalia nini cha kufanya ili kuisadia timu ya lipuli ifanye vizuri kwenye ligi kuu Tanzania bara na kulejesha furaha ya wananchi wa Iringa.

Naye Mwenyekiti Mpya wa timu ya lipuli Ramadhani Mahano aliwaomba wadau wa Mpira na wapenzi wa timu ya lipuli kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja kuvunja makundi yote yaliyokuwa yanasababisha migogoro ya lipuli na Mpira wa miguu kwa ujumla.

Nawaombeni sana kuyaka kichwani vizuri maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Kilolo bi Asia Abdallah kwa kuacha majungu au kusababisha migogoro ambayo haina maana bali naomba tushauriane kwa kila jambo kwa manufaa ya lipuli na wadau wa mpira.

MWENGE WA UHURU KITAIFA WAWASILI MKOANI KIGOMA,YAIBUA MIRADI LUKUKI ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO

$
0
0
 
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga  akikabidhi mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mwanamvua Mrindoko.


Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
 
Mwege wa uhuru kitaifa umeanza kutimua vumbi mkoani Kigoma kwa kuibua miradi lukuki iliyojengwa chini ya kiwango katika halmashauri ya wilaya ya uvinza huku kukiwa na hofu ya ufujaji wa fedha za umma katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Kufuatia hali hiyo Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017 Amour Amour amekataa kuweka mawe ya msingi katika miradi hiyo mitano inayohusisha ujezi wa nyumba za walimu vyumba vya madarasa na hofisi mbalimbali na kuagiza kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa mhandisi wa ujenzi wa halmashauri hiyo
 
Aidha Kiongozi huyo ametoa muda wa siku tatu kwa muhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Uvinza na mkandarasi aliyejenga mradi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Nguruka iliyopo katika kata ya nguruka kurekebisha baadhi ya kasoro zilizobainika katika mradi huo kwa kutumia fedha zao .

Maagizo hayo aliyatoa jana mara baada ya kuanza kukagua na Kuzindua Miradi sita ya halmashauri hiyo katika Shule ya Sekondari Nguruka, ambapo katika mradi wa Nyumba za shule hiyo walibaini kuwepo na nyufa katika majengo hayo na matumizi yafedha nyingi katika kukamilika kwa Mradi huo na kumuagiza mkurugenzi kuwasimamia muhandisi wa halmashauri na Mkandarasi wa mradi kufanya marekebisho ndani ya siku tatu na kupelekewa taarifa ya marekebisho hayo.

Hata hivyo Kiongozi huyo aliahirisha zoezi la uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya kijiji cha Malagalasi kata ya Nguluka Wilayani uvinza mkoani kigoma kufuatia jengo hilo kujengwa chini ya kiwango.

Pia Amour aliwaagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuchunguza mradi huo kama kuna vitendo vya rushwa vilifanyika, kutokana na mkandarasi huyo alieshindwa kufanyia marekebisho, mapungufu ya awali ambapo baada ya Mkandarasi mwingine kukabidhiwa mradi huo bado mapungufu yaliendelea kuwepo katika mradi.

Amour alisema atahitaji apatiwe taarifa ya marekebisho hayo baada ya siku tatu na taarifa hiyo ataifikisha mahari usika, pia alisema hawawezi kuvumilia fedha za serikali ziendelee kuibiwa kwa kutekeleza miradi mibovu isiyo na viwango ni lazima miradi yote inayotekelezwa ya Maendeleo iwe imara na inayodumu kwa muda mrefu kutokana na fedha wanazozitoa.

" sisi tumekuja kufanya kazi hatuta kubali kuzindua wala kupokea taarifa ya miradi mobov, ninaomba marekebisho haya yafanyike haraka sana na kabla hatujaenda Mkoa mwingine hii taarifa niipate na niifikishe sehemu husika hatuwezi kuvumilia mapungufu haya yaendele katika halmashauri zetu nilazima muwe na uangalizi na usimamizi mzuri wa miradi ilikuhakikisha tunapata miradi iliyo imara",alisema Amour.

Alisema Miradi ya Nyumba za Walimu imetofautiana hata katika fedha kutokana na uzembe wa usimamizi wa Miradi kwa halmashauri, Wakandarasi wana Lugha nzuri za kuwadanganya Wakurugenzi na Wasimamizi ilikulinda vibarua vyao, kupasuka kwa Nyufa za Nyumba inatokana na uzembe wa Mkandarasi na usimamizi Mbovu wa halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenz wa halmashauri, Weja Ng'olo alisema Mradi huo ulighalimu zaidi ya milioni 162 hadi kukamilika, na wao kama Halmashauri walitembelea mradi huo na kubaini baadhi ya Mapungufu ambapo walimuomba Mkandarasi kuyafanyia marekebisho na aliposhindwa waliamua kumpa kazi hiyo mkandarasi mwingine.

Alisema marekebisho hayo watayafanya kwa kutumia fedha ya Mkandalasi aliyobaki anaidai halmashauri hiyo ilikuhakikisha Mapungufu yote yaliyokatika Mradi yanamalizika na kuendlea kutumiwa na Walimu na familia zao.

MADUKA YA NGUO YA WOOLWORTHS YAJA NA PUNGUZO LA HADI 50%

$
0
0
Maduka ya nguo ya Woolworths yenye matawi yake jijini Dar es Salaam na Arusha, yametangaza punguzo kubwa la bei kwa bidhaa tofauti tofauti zinazopatikana katika maduka yake. Mkurugenzi wa fedha wa Woolworths Tanzania Samson Katemi alisema punguzo hilo kubwa la bei ni la hadi kufikia asilimia hamsini na litadumu kwa wiki moja kuanzia leo Jumanne. “Lengo la Woolworths ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anaweza kumudu kununua nguo mpya na za kisasa kwa gharama nafuu na kuachana na mitumba na ndiyo maana huwa tunakuwa na punguzo la bei mara kwa mara,” alisema. Mkurugenzi wa fedha wa maduka ya nguo ya Woolorths Samson Katemi, akimkabidhi mshindi wa hivi karibuni wa droo ya mwezi Lilian William Divas vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi laki tano. Wateja wa Woolworths wanaofanya manunuzi kupitia kadi maalum za manunuzi (Wrewards) wanayo nafasi ya kujishindia vocha hizo.

Katemi alisema punguzo hili litawawezesha wateja wa Woolworths watakafanya manunuzi katika maduka yake yaliyopo PPF Towers na Mikocheni kwa jijini Dar es Salaam pamoja na TFA na Njiro Complex kwa jijini Arusha wataweza kupata punguzo hilo katika bidhaa kama nguo za watoto, wanawake na wanaume “Kwa wateja wenye kadi maalum za manunuzi za Wrewards, watapata asilimia 10 zaidi ya punguzo. Kama mteja hana kadi ya Wrewards afike katika maduka yetu ili aweze kuipata bila malipo na aweze kunufaika na asilimia10 zaidi,” alieleza . Baadhi ya bidhaa mpya zilizopo katika maduka ya Woolworths kama ambavyo kamera yetu ilifanikiwa kuzinasa katika moja ya maduka ya Woolworths yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Katemi aliongeza kuwa, wateja wanaofanya manunuzi kwa kutumia kadi za Wrewards wanayo nafasi yakuingia kwenye droo zinazofanyika kila mwezi na kujishindia vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi laki tano ambazo huweza kutumika ndani ya kipindi cha miezi sita. “Katika droo ya mwezi Aprili, Lilian William Divas aliweza kuibuka mshindi. Kila mteja anayetumia Wrewards kadi kufanya manunuzi anaweza kuwa mshindi kama alivyokuwa Lilian,” aliongeza . Na katika droo ya mwezi wa sita Amina Shaban na Abdul Karim Ngarama waliibuka washindi. 
Baadhi ya wateja wakihudumiwa mara baada ya kufanya manunuzi kama ambavyo kamera ilivyokamata katika dula la Woolworths lililopo katika jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam 
Picha juu na chini ni baadhi ya wateja wakichagua nguo mara baada ya dula la Woolworths kutangaza punguzo la bei la hadi asilimia 50 kwa bidhaa tofauti tofauti kama ambavyo kamera yetu iliwakuta katika dula la lililopo katika jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam[/caption]  

SPIKA NDUNGAI APOKEA BARUA YA PR.LIPUMBA


WAZIRI MKUU KASSI MAJALIWA AKUTANA NA MWALIMU WAKE WA SEKONDARI

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwalimu wake, Agrias Sichone ambaye alimfundisha katika Shule ya Sekondari ya Kigonsera mwaka 1977 hadi 1980. Alikuwa katika kikao cha kuhitimisha ziara yake mkoani Songwe kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Sunrise mkoani humo Julai 24, 2017. kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KAIMU MENEJA MKUU WA BANDARI YA KIGOMA AKANUSHA MADAI JUU YA KUTOKULIPWA WANANCHI 1228 WA ENEO KATOSHO

$
0
0

KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao kushoto ni Meneja wa Mawasiliano TPA Janeth Ruzangi
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika  kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao kushoto ni Maneja wa Mawasilino TPA Janeth Ruzangi
 PRO wa TPA Tanga Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo
 Waanmdishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia matukio
 Waandishi wa habari wakiwa kazini kuchukua stori
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza kushoto akimpa ufafanuzi mwandishi wa gazeti la Dail News Mkoani Tanga,Amina Kingazi
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza amekanusha madai yanayoenezwa juu ya kutokulipwa wananchi 1228 wa eneo la Katosho katika Manispaa hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa bandari kavu ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 12 zimetengwa kwa ajili ya gharama za fidia.
 
Hayo ameyazungumza jana Jijini Tanga alipokuwepo kwenye kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao.

Aidha alisema jumla ya hekari 158 ndizo zilizochukuliwa na mamlaka ya bandari(TPA) kwa ajili ya mradi huo huku wananchi 1196 kati 1228 tayari wamekwisha lipwa fedha zao kama semehemu ya fidia za ardhi,mazao na makazi jambo ambalo limefanyika kwa mujibu wa kisheria na ushirikishwaji wa pande zote.
 
Mchindiuza alizidi kufafanua kuwa kutokana na hatua hiyo wananchi 32 kati yao walishindwa kulipwa fidia zao kutokana na kushindwa kuwakilisha akaunti zao katika Halmashauri ya manispaa ya Mji wa Ujiji jambo ambalo linapotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari.
 
“Yapo malalamiko mengi ya utaratibu wa ulipwaji wa fidia hizo kwa wananchi walioko katika maeneo ya ya maradi lakini labda niseme kitu tayari tumekwisha walipa wananchi 1196 kati 1228 na waliobakia ni 32 tu na fedha zao zipo wapeleke akauti zao tuweze kuwalipa”Alisema.

Alisema Mamlaka hiyo baada ya kukua kutokana na kuongezeka kwa shehena mamlaka ilitafuta eneo kwa ajili ya kujenga mradi wa bandari kavu ambalo litatumika kuhudumia nchi jirani za maziwa makuu kama DRC,Burundi na Rwanda.

Taratibu za kupatikana kwa eneo hilo ambalo lilikuwa mali ya wananchi katika eneo hilo la Katosho Mkoani humo zilifanyika kisheria na kuishirikisha Halmashauri ya Mji huo ambao wao ndio wanaozijua kaya zinazoishi katika maeneo hayo.
 
“Lengo letu la kuishirikisha Halmashauri ya manispaa hiyo ni
kuhakikisha wanafanya tathmini ya kina dhidi ya wananchi hao na tunatambua kuwa wanazitambua kaya zote zinazostahili kulipwa na hivi ndivyo tulivyo fanya”Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi hao kama wanamadai kuhusiana na kiwango kidogo cha fidia wanaweza kufika katika mamlaka za sheria za ardhi na kufuata mkondo wa sheria ili waweze kupata msaada wa kisheria zaidi.
 
“Wananchi wasipotoshwe na wajanja wajanja idadi ya wafidiwa
inatambuliwa na na kama kuna kitu hakijafuatwa wafuate sheria ili mkondo huo uchukue maamuzi ya kisheria bila ya kuonea mtu na sisi kama viongozi wa mamlaka tupo salama na kwa wale ambao hawajalipwa wafike na vielelezo katika ofisi husika wachukue fedha zao.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hao waache kupotoshwa na watu wachache ambao hawataweza kuwasaidia kitu chochote jambo la msingi kujenga ushirikiano katika miradi hiyo ya maendeleo ya Taifa.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

WAZIRI LUKUVI AWEZESHA UJENZI WA MABWENI IRINGA

$
0
0
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa mbele.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa nyuma.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa ndani.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Vitanda kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.
Eneo la kunawia lililo ndani ya Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa.

………………………….

Na Hassan Mabuye

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ismani Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan amesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi Iringa Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania.

Ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Isimani Mhe. Wiliam Lukuvi aliyoyaomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali la shule hiyo kuteketea kwa Moto.

Balozi huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.

Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.

“waziri Lukuvi lileta maombi ya miradi mbalimbali ambayo miongoni mwake ni kujengewa Hostel ya wasichana ya shule ya Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka 2008, kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa, kwa hiyo namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo”

“Leo nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji wa Hosteli hii umekamilika ikiwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi, na ni matumaini yangu mradi huu utatunzwa vema”

Balozi huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika bweni hilo.

Hata hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo litatunzwa vizuri.

Waziri Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa bweni na miradi mingine amewataka wanafunzi hao kutunza mabweni hayo na kujiepusha na hatari zozote za kuchoma moto, kitendo ambacho kinasababisha upotevu mkubwa wa mali na uhai wa wanafunzi hao.

NDG:BUKWALI:MFUMO MPYA WA BAJETI UTATATUA CHANGAMOTO ZILIZOKUWEPO KWENYE MFUMO WA ZAMANI

Rais Magufuli afungua barabara ya Itigi - Manyoni

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wapili kushoto na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida, wakiondoa kitambaa kuashiria kufunguliwa rasmi kwa barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5. mkoani Singida leo Julai 25, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Viongozi wengine wa Mkoa wa Singida na Tabora wakikata utepe kama ishara ya kufunguliwa Rasmi kwa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiteta jambo na Mwakilishi wa Kampuni ya PowerChina International Group Limited nchini Bw. Wang Chao wakati wa Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 mkoani Singida leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwaaga kwa kupunga mikono wananchi wa Itigi na Manyoni walioshiriki na Kushuhudia Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya mkoani Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Itigi na Manyoni wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Itigi - Manyoni - Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali.
 Wananchi wa Itigi na Manyoni wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwatubia kwenye Ufunguzi wa  Barabara ya Itigi - Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa kwa fedha za Serikali kwa  asilimia mia moja.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi Kijiji cha Tula Uyui mkoani Tabora waliojitokeza barabarani kumsalimia akiwa njiani kuelekea mkoani Singida leo Julai 25, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi wakati mheshimiwa Rais alipowasili Mkoani Singida eneo la Itigi ili kufungua Barabara ya Itigi -Manyoni -Chaya yenye urefu wa kilometa 89.5 iliyojengwa na Serikali kwa asilimia mia moja.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MSUMBIJI AMEWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZILIZOPO.

$
0
0
Watanzania waishio katika mikoa ya MTWARA,RUVUMA wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo hususani katika majimbo mawaili ya CABO DELGADO NA NIASSA nchini MSUMBIJI,hayo yamesemwa na balozi wa tanzania nchini MSUMBIJI RAJABU LUHAVI wakati wa mkutano mkutano mkuu wa ujirani mwema kati ya TANZANIA NA MSUMBIJI mkoani RUVUMA.HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE.

Wakulima wa mahindi Handeni wanogewa na mbegu za mradi wa WEMA

$
0
0


Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) pamoja na wakulima na wageni mbalimbali walipotembelea shamba hilo. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA) Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) pamoja na wakulima na wageni mbalimbali walipotembelea shamba hilo. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA). Mratibu wa Mradi wa WEMA, na Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti Ilonga, Dk. Justin Ringo (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali (wa pili kushoto) juu ya ubora wa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA), katika moja ya shamba darasa la mkulima. Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa Shamba darasa la mkulima, Kidika Swai lililotembelewa na washiriki wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani. Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA). Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali akimenya moja ya hindi katika shamba darasa Ofisa Mawasiliano wa jopo la watafiti wa Mradi wa WEMA Tanzania, Dk. Janet Kaya (kushoto mwenye kofia) akifafanua jambo kwa mgeni rasmi na viongozi wengine walipotembelea moja ya shamba mfano lililopandwa kwa mbegu chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA). Mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe (wa pili kulia) wakiangalia moja ya hindi kwenye shamba mfano lililohudumiwa na mbegu za mradi wa WEMA. Mkulima, Kidika Swai (mwenye suti ya kijivu) akitoa darasa kwa wakulima wenzake ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani.

 Na Joachim Mushi, Handeni 

 WAKULIMA wa Mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA), wilayani Handeni wameiomba Serikali irekebishe sheria ya uzalishaji wa mbegu ili kutanua wigo wa uzalishaji mbegu kupitia taasisi za Serikali kama vile Jeshi la Kujenga Uchumi (JKT), Jeshi la Magereza pamoja na zinginezo zilizopo. 

Wakulima hao wametoa ombi hilo jana kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani, kilichopo Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kufuatia uwepo wa changamoto ya kutopatikana kwa uzalishaji wa mbegu ya kutosha kulingana na mahitaji kama ile ya WE 2109 ambazo zimeonekana kufanya vizuri zaidi maeneo ya Wilaya ya Handeni. Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mwakilishi wa Wakulima hao, Costansia Msola alibainisha kuwa bei kubwa ya mbegu zinazozalishwa na makampuni ya mbegu ulikuwa changamoto licha ya uwepo wa wadudu waharibifu waliojitokeza kwenye mashamba ya wakulima na kukwamisha matarajio ya uzalishaji. 

 Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, aliyewakilishwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, John Mahali aliwapongeza kikundi cha wakulima 22 waliokubali kushirikiana na watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi kuendesha mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA) ambao umeonesha mafanikio makubwa. Aidha aliwataka wakulima Wilayani Handeni kukubali mabadiliko na kuanza kutumia mbegu hizo za kisasa zaidi ya aina 11 zilizoonesha mafanikio makubwa katika utafiti. "...Huko nyuma tulikuwa tukitumia mbegu za asili ambazo zilikuwa hazifanyi vizuri, naombeni sasa tutumie mbegu hizi bora zilizofanyiwa utafiti na WEMA kwa kilimo bora," alisisitiza, Bw. John Mahali akizungumza na wakulima. 

Aliyaomba makampuni ya uzalishaji mbegu kujitokeza na kufanya uzalishaji wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame ili kuwasaidia wakulima upatikanaji wake kwa wakulima. Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Maendeleo ya Utafiti kutoka Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Jackson Nkuba akimwakilisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utafiti alisema Serikali ipo tayari kushirikiana na makampuni yatakayojitokeza kuzalisha mbegu hizo bora kwa wakulima hivyo kutoa rai kujitokeza kwa wingi. 

Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha mkulima anafanya kilimo cha kisasa chenye tija apate mazao mazuri na yakutosha ambayo yatamletea maendeleo. Alisema njia pekee ya kufanya vizuri kwenye kilimo ni kuendesha tafiti mbalimbali na ndio sababu Serikali kwa kushirikiana na mashirika anuai inaendelea kutoa fedha na kufanya tafiti tofauti. Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, William Makufwe akizungumza aliiomba Serikali kujenga viwanda vya kusindika Mahindi na mazao mengine yanayozalishwa na wakulima wilayani humo ili wakulima wanufaike zaidi na mazao hayo, tofauti na kutegemea kuuza nje ya eneo hilo.

 "Haiwezekani mahindi tulime sisi tuyauze Dar es Salaam na mikoa mingine wayasindike (unga) na kuja kuuziwa tena sisi wenyewe wakati mwingine kwa bei ya juu tofauti na tulivyo uza siye...," alisema Bw. Mkufwe. Mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA) ulianza mwaka 2009 ukiwa na lengo la kufanya utafiti shirikishi wa mbegu bora chatara za mahindi zinazostahimili ukame kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, ukiwa na mkulima mmoja tu lakini kwa sasa una kundi la wakulima 22 ambao walihamasika na kujiunga pamoja kushirikiana na watafiti. Baadhi ya wakulia wa Mradi wa utafiti wa mbegu bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA), wilayani Handeni wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani. Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa. Mtafiti na Mwenyekiti wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakulima Katika Kijiji cha Kabuku Ndani, Wilaya ya Handeni, Bw. Temu (kulia aliyesimama) akiwasalimia washiriki wa maadhimisho hayo Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa. Baadhi ya wakulima wakitembelea Shamba darasa la mkulima, Kidika Swai Shamba hilo limepandwa kwa mbegu aina 11 bora chotara za mahindi zinazostahimili ukame (WEMA) Sehemu ya shamba la utafiti wa mahindi yenye sifa zifuatazo; kustahimili ukame na magonjwa, kukomaa mapema, zinazostawi ukanda wa chini na wa kati na zilizokaribia kuidhinishwa.

Kamati ya Kuchunguza Mkataba ... Times na TBC Yaongezwa Muda

UMMY -AAGIZA MGANGA MFAWIDHI WA KITUO CHA AFYA MLANDIZI ASIMAMISHWE KAZI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa ,akizungumza mara baada ya waziri wa afya ,jinsia ,wazee na watoto Ummy Mwalimu kutembelea kituo cha afya cha Mlandizi
Waziri wa afya ,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu ,akitembelea kituo cha afya Mlandizi ,wa kwanza kushoto ni mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi,dk.Mpola Tamambele,ambae amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi .(Picha na Mwamvua Mwinyi )
………………………….

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha 

WAZIRI wa afya, jinsia ,wazee na watoto ,Ummy Mwalimu ,amemsimamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi,dk.Mpola Tamambele,kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo ya serikali ya kuhakikisha mama mjamzito ,mtoto chini ya miaka mitano na mzee wanapata huduma bure . 

Kutokana na kutokuwa na mamlaka ya moja kwa moja amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya halmashauri ya wilaya ya Kibaha ,Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiendelea . 

Amemuelekeza kaimu mkurugenzi huyo pia kuwafuatilia watumishi wa afya kituoni hapo waliohusika kumuagiza mama aliyejifungua Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya sh.180,000 ili apate huduma . Aliyasema hayo wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi ,kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo ,Hamoud Jumaa . 

Waziri huyo alisema yeye hana mamlaka ya moja kwa moja kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo hivyo anaiachia mamlaka husika isimamie jukumu hilo.
Alisema hatokubali kuona watumishi wachache kwenye vituo vya afya ,zahanati na hospitali wanachezea maagizo ya serikali. 

Alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mama aliyejifungua ambae alisema amenunua vifaa vya kufanyiwa operesheni kwa gharama ya sh .180,000 .
Ummy alisema haiwezekani kuona mama wajawazito ,wanalipishwa hadi gloves na pamba ili kujifungua wakati serikali yao ilishasema watahudumiwa bure . 

Alieleza kwamba ,kuanzia sasa waganga wakuu wa wilaya ,mikoa na watumishi wa afya wote nchini wahakikishe wanatimiza maelekezo ya serikali kuhudumia akinamama wajawazito na watoto ili kupunguza vifo vya uzazi . Ummy alisema kuwa ,watumishi na wauguzi wengi wanajituma na kufanya kazi zao kifanisi ila wapo wachache ambao wanakwamisha juhudi hizo . 

“Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume na serikali ,rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la kuboresha huduma za afya ,halafu akitokea mtu mmoja mzembe anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho “
“Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya ,namsimamisha mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika .” alisema Ummy . 

Mbali ya hayo Ummy alibainisha,bajeti ya dawa katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha imeongezeka ndani ya miaka miwili mfululizo kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano .
Ummy alisema mwaka 2015/2016 bajeti ya madawa katika halmashauri hiyo ilikuwa mil.24 na 2017 ilifikia mil.70 na bajeti ya sasa 2017/2018 imefikia sh. mil.101 . 

Kwa upande wake mama aliyejifungua kituoni hapo ,Salma Khalfani ,alimweleza Ummy kwamba aliandikiwa orodha ya dawa za kununua kwenye maduka ya dawa ya nje .
Alieleza ,alitakiwa kufanyiwa upasuaji na hivyo kutakiwa kununua madawa na vifaaa tiba ,pamba na gloves vya 180,000 akanunue ili aweze kujifungua . Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Mmbaga alisema maagizo aliyopewa na waziri ameyapokea na atayafanyia kazi . 

Nae mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini ,Hamoud Jumaaa alisema kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wananchi hasa akinamama kulipishwa fedha za dawa na vifaa tiba . 

Alisema baadhi ya wazee wamekuwa wakishindwa kupewa huduma za afya bila malipo .
Jumaa alimuomba Ummy kuendelea kushirikiana nae kuwadhibiti watumishi wazembe wanaodidimiza haki za wananchi .

BENKI YA CRDB YAUNGANISHA WATEJA WAKE NA HUDUMA YA SimBanking

$
0
0
 Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti mpya na kujiunga na huduma ya SimBanking ndani ya gari la mauzo la Benki ya CRDB katika maeneo ya Mbezi-Kimara jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti mpya na kujiunga na huduma ya SimBanking ndani ya gari la mauzo la Benki ya CRDB katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Benki ya CRDB, Edina Masawe, akimhudumia mteja wa benki hiyo, Christian Wilfred, aliyefika katika gari la mauzo la benki hiyo katika eneo la Mbezi Luis.
Ofisa Masoko wa Benki ya CRDB, Estherine Mtimba (kulia), akimsaidia kufungua akaunti pamoja na kumuunganisha na huduma ya SimBanking mteja mpya wa benki hiyo, Rehema Adam.
 Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Benjamin Banzi (wa pili kulia), akimuunganisha mteja, Christopher Mjata kwenye huduma ya SimBanking (huduma za benki ya CRDB kwa njia ya simu za mkononi) katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.
Mteja wa Benki ya CRDB, Khalid Hassan (kulia), akifungua akaunti katika gari la mauzo la benki hiyo katika eneo la Mbezi jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Benki ya CRDB, Eric Maro.
Baadhi ya wateja wa Benki ya CRDB wakitoka kufungua akaunti pamoja na kujiunga na huduma ya SimBanking katika gari la mauzo la benki hiyo katika eneo la Kimara jijini Dar es Salaam.
Wateja wakisubiri kupata huduma mbalimbal ndani ya gari la mauzo la Benki ya CRDB.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti mpya pamoja na kujiunga na huduma ya SimBanking ndani ya gari la mauzo la Benki ya CRDB katika eneo la Mbezi Luis.

HUAWEI YAENDELEA KUCHANGIA SEKTA YA ELIMU KUPITIA PROGRAMU YA ‘SEEDS FOR THE FUTURE’ KWA MWAKA 2017

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Gao Mengdong akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ kwa mwaka 2017 inayoratibiwa na Kampuni hiyo kila mwaka leo jijini Dodoma. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei kwa mwaka 2017 jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Mkurugenzi wa kitengo cha TEHAMA wa chuo Kikuu Dodoma Dkt. Hector Mongi akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (wa pili kulia) akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (kulia) na Mkurugenzi wa Huawei Tanzania, Gao Mengdong wakitia saini kwenye mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika programu ya ‘Seeds for the future’ wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu hiyo iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (kulia) na Mkurugenzi wa Huawei Tanzania, Gao Mengdong wakipeana mkono baada ya kutia saini kwenye mkataba wa makubaliano wa kushirikiana wakati wa uzinduzi wa programu ya ‘Seeds for the future’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Huawei jijini Dodoma leo. Programu hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya kampuni hiyo katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kwa kushirikiana na Wizara, Huawei huchukua wanafunzi 10 wa vyuo vikuu kila mwaka wanaochukua masomo ya TEHAMA na kuwapeleka nchini China kwenda kujifunza kwa vitendo ili kuongeza uwezo kwenye masuala ya TEHAMA.
Picha ya pamoja



Dodoma, 25 Julai, 2017: Katika kuchangia maendeleo ya elimu nchini Tanzania, Kampuni ya Huawei inayoongoza ulimwenguni katika utoaji wa huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) leo imeendeleza juhudi zake kwa kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania kwa kuzindua programu yake ya kila mwaka ya ‘Seeds for the future’.

Uzinduzi wa programu hiyo umefanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Huawei imeeleza dhamira yake ya dhati katika kupanua wigo wa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Mafunzo ya Ufundi katika kupanua maarifa ya masomo ya TEHAMA kwa wanafunzi na watendaji wanaofanya kazi kwenye sekta ya Mawasiliano na Teknolojia.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, alipongeza juhudi za Huawei katika kuibua vipaji kwenye sekta ya TEHAMA nchini Tanzania na kushirikiana kikamilifu na wananchi.

Dkt. Akwilapo alimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ambao walitarajiwa kuzindua programu hiyo ya TEHAMA.

Dkt. Akwalipo alisema Huawei imekuwa mshirika muhimu waTanzania katika kukuza maendeleo ya TEHAMA nchini na imeendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika uvumbuzi wa masuala hayo kutokana na Serikali kuendelea kuboresha Teknolojia kupitia miradi yake mbalimbali.

“Ninapenda kuwashukuru Huawei kwa kile walichokianzisha na kuendeleza Programu ya ‘Seeds for the Future’ kwa wanafunzi wa Tanzania. Ninawahakikisha kwamba Wizara ya Elimu itaendelea kushirikiana na Huawei kwa sababu tunatambua kwamba TEHAMA ni muhimu sana pia katika kusaidia maendeleo ya elimu,”

Aliongeza kuwa Programu ya Seeds for the Future inaendeshwa na Huawei ulimwenguni kote kupitia kitengo chake cha Corporate Social Responsibility (CSR). Kupitia programu hii Huawei Tanzania imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wanafunzi 100 kutoka hapa nchini wanashiriki katika mradi wa miaka 10 ambapo inamaanisha kwamba kila mwaka wanafunzi 10 kutoka hapa nchini watapata fursa ya kutembelea Beijing na kufanya kazi na kampuni hii katika makao makuu yake yaliyopo Shenzhen, China.

Katika tukio hilo, Huawei pia ilisaini mkataba na Wizara ya Elimu kuhusu utekelezaji wa kukuza vipaji katika kuendeleza ICT unaojulikana ‘Huawei ICT Talent Cultivation Plan’ ambapo utawanufaisha vijana wenye taaluma, maofisa wa serikali na wahadhiri.

Malengo ya mpango huo ni kutekeleza programu ya kuhamasisha elimu ya TEHAMA iliyolenga kuinua kiwango cha elimu na kuendeleza mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma ICT. Hususani kukuza ushirikiano na Huawei ambao utaendeleza vituo vya mafunzo na kuanzisha madarasa maalumu katika ofisi za Huawei Tanzania.

Kupitia mkataba huo wa makubaliano uliosainiwa leo, tutaimarisha vituo vya kitaaluma katika ofisi za Huawei, Huawei Tanzania Customer Solution Intergration & Innovation Experience Centre (CSIC) na madarasa.

Zaidi ya hayo tutatoa nafasi za mafunzo kwa wanafunzi wa ICT kufanya kazi za muda katika ofisi za Huawei Tanzania jambo ambalo litawasaidia kujifunza, kufanya tafiti na kuendelea ujuzi wao kwenye masuala ya TEHAMA,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Bwana Gao Mengdong.

Aidha, Huawei pia imedhamiria kutimiza ahadi yake ya kupanua ushirikiano wake na serikali katika kuanzisha mradi wa mafunzo kwa matandao ambao ushirikiano huo utatoa mchango mkubwa zaidi kwa sekta ya elimu nchini Tanzania na maendeleo ya ICT ili kuifanya Tanzania kufikia malengo ya dira ya maendeleo ya mwaka 2025.

Kwa mujibu wa Gao, falsafa ya Huawei ni ‘Expoloration’ ikiwa na maana kwamba kampuni itaendelea kubuni kila namna ili kuiwezesha nchi kuendelea kutimiza mipango yake ya maendeleo.

Miongoni mwa wanafunzi walioteuliwa kushiriki programu hii, Kadhija Mohammed aliipongeza Huawei kwa kuendelea kuibua vipaji vya ICT nchini Tanzania na kuendelea kushirikiana na wananchi.

Alisema Huawei imekuwa msharika muhimu kwa maendeleo ya ICT nchini Tanzania na imeendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania katika uvumbuzi wa ICT ambapo serikali imekuwa ikiendelea kuboresha ICT kupitia miradi yake mbalimbali.
“Ni matumaini yetu kwamba Serikali ya Tanzania itatumia vyema fursa iliyotolewa na Huawei na tunaamini kupitia Programu ya Seeds for the Future tutajifunza mambo mengi kutoka kwa Huawei Tanzania,” alisema.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 26,2017

Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images