Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1314 | 1315 | (Page 1316) | 1317 | 1318 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Baada ya Matokeo ya Kidato cha Sita , Global Education Link (GEL) ambao ni mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vikuu vya nje udahili ni papo kwa papo na vyuo hivyo viko wazi.

  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema katika azma ya serikali ya awamu ya tano ya viwanda, inahitaji rasilimali watu ya kutosha ambao ndio watasukuma gurudumu hilo la viwanda na ujuzi upo katika vyuo vya nje ambapo nchi zenye vyuo vina uatajiri wa viwanda.

  Mollel amesema kuwa vyuo ambavyo anashirikiana na vina uwezo wa kutosha katika uzalishaji wa rasilimali watu katika sekta ya viwanda.Amesema kuwa wazazi wanaotaka kupeleka wanafunzi katika vyuo vikuu vya nje hawatajutia kutokana na mazingira wanayokwenda kusoma huko.

  Mollel amesema kuwa wazazi na wanafunzi wafike katika ofisi zao ziko katika mikoa ya Dar es Salaam viwanja vya Saba saba , Dodoma , Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Arusha pamoja na nchi ya Zambia.

  Amesema kuwa mwanafunzi atayekuwa anapitia katika wakala hiyo atapata uangalizi kwa muda wote masomo yake katika kuhakikisha mzazi kile anachokifanya kwa kijana wake hawezi kujutia.

  Mollel amesema kuwa wazazi na wanafunzi wanaweza kufika katika ofisi zao kwa maelezo na jinsi kuwafanyia udahili wa papo kwa papo.
  Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Afisa Masoko wa Global Education Link (GEL) Damaricy Peter akiwapa maelekezo wateja waliofika kupata huduma katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Afisa wa Hati ya Kusafiria Passport , Abdul Milanzi akimsainisha fomu ya hati ya kusafiria mteja wa Global Education Link GEL leo katika ofisi za Global Education Link zilizopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
  Meneja Masoko wa Chuo Kikuu cha Lovely Professional, Love Kumas akizungumza na mteja katika ofisi za Global Education Link (GEL) leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0


    Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora Mhe Rais yupo mkoani humo kwa  ziara ya kiserikali
   Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mke wake Mama Janeth Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Tabora  Agrey Mwanri wakiondoa kitambaa kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 

  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa Barabara ya Tabora Ndono - Urambo yenye urefu wa kilometa  94 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 

   Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiondoa kitambaa kwenye jiwe la Msingi kuashiria kufunguliwa kwa Barabara Kariua - Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli,akiwapungia Mikono kwa Kuwasalimia Wananchi wa Kariua na Viunga vyake Walio jitokeza kumsikimsikiliza Mh Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
   Maelfu ya wananchi wa Kariua na Viunga vyake Wakimsikiliza Mh Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwahutubia wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora 
  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Wananchi wa Kariua Mkoani Tabora wakati wa Ufunguzi wa Barabara ya Kariua -Kazirambwa yenye urefu wa kilometa 56 iliyojengwa kwa kiwango cha lami Mkoani Tabora. Picha na IKULU

  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewasihi wanafunzi wa kike nchini kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha kukatisha masomo yao.
  Amesema ni vema wanafunzi hao wakatumia muda wao vizuri kwa kusoma kwa mfululizo kutoka kiwango kimoja cha taaluma kwenda kingine.
  Mama Mary aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 23, 2017) alipozungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Vwawa wilayani Mbozi.
  Mke wa Waziri Mkuu ambaye ameambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika ziara ya mkoa Songwe, aliwaasa wanafunzi hao kutumia wakati huu kwa kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo viovu.
  “Nawasihi mtumie muda huu kusoma kwa bidii ili muweke msingi imara kwa ajili ya kujenga maisha yenu ya baadae. Msikatishe masomo yenu.”
  Mama Mary aliongeza kwamba “utumieni muda huu vizuri ili msije mkaujutia baadae, kwani wakati ni mali ukipita umepita.”
  Alisema ni vizuri wakasoma hadi chuo kikuu na kwamba wasikimbilie kufanya mambo yasiyowahusu kwa sasa kwani mshika mawili moja lazima limponyoke.Mke wa Waziri Mkuu alisema wanafunzi hao wakisoma hadi elimu ya juu watakuwa na uwezo wa kutambua jambo lipi ni jema na lipi ni baya.
  “Kilichonifurahisha zaidi ni kwa sababu mimi pia ni mwalimu kwa hiyo inavyoona wanafunzi wako vizuri kama hivi nafurahi sana, hivyo nawaomba msome kwa bidii.”
  Serikali imetunga sheria kali dhidi ya watu wanaosababisha watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kuwapa mimba au kuwaoa.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, JULAI 24, 2017

  Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majalwa akizungumza na wanafujnzi wa Shule ya Sekondari ya Vwawa iliyop[o Mbozi baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na watumishi wa umma, viongozi wa dini na viongozi wa taasisi za binafsi kwenye ukumbi wa shule hiyo Julai 23, 2017 . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Shule tano kufaidika na vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 5 

  Mbeya; Katika kuinua sekta ya elimu nchini , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa msaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa shule 5 za sekondari mkoani Mbeya.

  Vitabu hivyo vimetolewa na Airtel kwa kushirikiana na Tulia Ackson foundation kwaajili ya shule za sekondari za Ikuti, Kayuki , Bujeli, Ntaba na Ikupa

  Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Naibu Spika Mh Dkt, Tulia Ackson alisema aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana na taasisi yake ya Tulia Ackson ili kusaidia shule za sekondari zenye uhaba wa nyenzo za kujifunzia mkoani Mbeya. Dr. Ackson alisema” ni muhimu kwa makapuni binafsi ya umma kushirikiana katika kuinua sekta ya elimu nchini ili kuweka mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na kuwa na taifa lenye ueledi

  Tumeshuhudia uhaba mkubwa wa vitabu katika mashule ambapo uwiano upo kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi 5 hadi 10. Tunaamini msaada huu tunaoutoa leo utasaidia kuzalisha nguvukazi yenye ueledi itakayowawezesha kujiajiri au kuajiriwa na kujenga uchumi wenye nguvu. Natoa wito kwa makapuni mbalimbali kuungana nasi na kuzifikia shule zenye uhitaji wa vifaa vya kufundishia nchini

  Kwa upande wake Meneja Mauzo mkoani Mbeya, Bartholomew Masatu alisema” Airtel tunaamini jamaa iliyoelimika inajengwa kutoka katika shule zenye vifaa vya kufundishia vyakutosha hususani vitabu. Ili kuwa na maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi hapa Mbeya”.

  Tunaamini msaada utachochea ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi katika mkoa wetu.” Aliongeza Masatu

  Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa sekondari ya Kayuki Bi Bertha Sarufu Kwa niaba ya shule zilizofaidika na msaada wa vitabu alisema “ Tunashukuru sana Airtel kwa kutufikishia msaada huu na napenda kutoa wito kwa wanafunzi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa lengo la kuboresha ufaulu. Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu zimekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia ipasavyo".

  WAZIRI wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamja na Naibu Spika wa Bunge, Dkt.Tulia Akson wakipokea vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.Anayewakabidhi vitabu hivyo ni Meneja mauzo wa Airtel mkoa wa Mbeya bw, Bartholomew Masatu. Airtel imekabidhi vitabu hivyo mwishoni mwa wiki hii ikiwa ni ahadi yake ya kuendeleza masomo ya sayansi nchini.
  WAZIRI wa Elimu Profesa, Joyce Ndalichako (Kushoto)akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania , Dkt.Tulia Akson , wakimkabidhi vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa sekondari ya Kayuki, Bertha  Sarufu, vitabu vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel. Mbali ya Kayuki, shule nyingine za sekondari zilizonufaika na msaada huo ni Ikuti, Bujela, Ntaba na Ikapu, zote zipo wilayani Rungwe. Airtel imekabidhi vitabu vya sayansi mwishoni mwa wiki vyenye thamani ya shilingi milioni 15.

  0 0

  Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akifungua mkutano wa sita wa watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya Afya, wataalamu wa Afya kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na mataifa ya nje ambao unaogozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu Pamoja na mabalozi na viongozi mbali mbali wa serikalini na sekta binafsi kujadili mustakabali wa sekta ya afya wa Tanzania na nchi shiriki hasa jinsi ya kuboresha sekta binafsi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine wa meza kuu wakimshikiliza Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati akitoa hotuba yake katika kufungua mkutano wa sita wa watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya Afya, wataalamu wa Afya kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Uganda, Burundi, na mataifa ya nje, unaofanyika kwa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya washiriki wa mkutano wa sita wa watoa huduma za afya, wamiliki wa vituo vya Afya, wataalamu wa Afya kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na mataifa ya nje ambao unaongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu Pamoja na mabalozi na viongozi mbali mbali wa serikalini na sekta binafsi kujadili mustakabali wa sekta ya afya wa Tanzania na nchi shiriki hasa jinsi ya kuboresha sekta binafsi. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Picha na Kajunason, Globu ya Jamii.

  0 0

  Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Rais chama cha Mawakili nchini (TLS),Mh. Tundu Lissu akishuka kwenye gari maalum mara baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema hii leo jijini Dar,akituhumiwa kwa makosa ya Uchochezi.

  Tundu Lisu alikamatwa  Julai 20 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alikokuwa akielekea Kigali, Rwanda kwenye Mkutano wa Marais wa Vyama vya Mawakili Afrika Mashariki.
  Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Rais wa chama cha Mawaikili nchini (TLS),Mh. Tundu Lissu akiingizwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mapema hii leo jijini Dar,kujibu tuhuma za kesi yake inayomkabili ya ya Uchochezi.

  Tundu Lisu alikamatwa  Julai 20 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) alikokuwa akielekea Kigali, Rwanda kwenye Mkutano wa Marais wa Vyama vya Mawakili Afrika Mashariki.
   
  HABARI ZAIDI TUTAWALETEA HIVI PUNDE.

  0 0

  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amezitaka halmashauri kuwawezesha vijana na kinamama kwa vitendo kwa kuyapa makundi hayo baadhi ya kazi zilizo chini ya halmashauri ambazo wanao uwezo wa kuzifanya ili wajiongezee kipato.

  Jafo ameyasema hayo leo katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh. milioni 70 iliyotolewa na Manispaa ya Dodoma kwa vikundi vya ujasiliamali vya vijana na kinamama ndani ya manispaa hiyo.

  Ameeleza kwamba haipendezi kwa halmashauri yeyote kuwanyima fursa ya kazi vikundi vya vijana na kinamama ambapo kazi hizo zinaweza kufanywa na makundi hayo.

  Jafo ametolea mfano kikundi cha vijana cha DOYODO ambacho kina kiwanda cha kisasa cha kufyatua Matofali lakini wanahangaika soko  la kuuzia matofali wakati kuna ujenzi mkubwa wa madarasa na vyoo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

  “Kwa mfano kuna ujenzi unatarajia kuanza kwenye shule za msingi za Nkuhungu, Mwenge, na Ihumwa ambapo kuna zaidi ya vyumba 12 vya madarasa na vyoo matundu zaidi 18,”amesema

  Naibu Waziri Jafo ameipongeza manispaa hiyo kwa kuvitumia vikundi vya vijana katika utengenezaji wa madawati ya shule za msingi na sekondari na amezitaka halmashauri nyingine hapa nchini kuiga mfano huo.
  Wawakilishi wa vikundi vya vijana na kinamama wa Manispaa ya Dodoma wakipokea hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya shughuli za ujasiriamali.
   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza na wajasiriamali wa Manispaa ya Dodoma katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya vikundi vya Kinamama na Vijana.
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi akitoa taarifa ya mikopo ya vijana na kinamama kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
   Meya wa Manispaa ya Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akimkaribisha Nabu Waziri Ofisi ya Rais, Selemani Jafo kuzungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya Sh.Milioni 70 kwa ajili ya vikundi vya kinamama na vijana.
   Mwakilishi wa kikundi cha vijana akimpongeza Naibu Waziri kwa maelekezo aliyoyatoa.
   Mmoja wa kinamama wajasiriamali akitoa shukrani kwa serikali baada ya kuwezeshwa.

  0 0

   Rais Dkt John Pombe Magufuli akipewa akisikiliza maelezo mafupi mara baada kufungua mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora. Rais Dkt Magufuli ameagiza Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano kujenga jengo la abiria 500 badala ya jengo lililopo la abiria 50.Pia ameagiza urefu wa uwanja uongezwe hadi kufikia kilometa 2.5 badala ya kilometa 1.9 zilizopangwa ili ndege kubwa na ndogo ziweze kuutumia uwanja huo.
  Rais Dkt John Pombe Magufuli ameweka jiwe la Msingi la mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda miji ya Tabora, Nzega na Igunga. Mradi huo utagharimu Shilingi Bilioni 600 na unatekelezwa kwa fedha za mkopo nafuu kutoka India. Una uwezo wa kuzalisha lita Milioni 80 kwa ajili ya Mji wa Tabora.
   Rais Dkt John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo mafupi ya mradi hu wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora,kutoka kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Prof Makame Mbarawa mapema leo mkoani humo

  Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo amefungua mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Tabora,Wakati wa uzinduzi wa mradi huo,Rais Dkt Magufuli ameagiza Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano kujenga jengo la abiria 500 badala ya jengo lililopo la abiria 50.Pia ameagiza urefu wa uwanja uongezwe hadi kufikia kilometa 2.5 badala ya kilometa 1.9 zilizopangwa ili ndege kubwa na ndogo ziweze kuutumia uwanja huo.

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amezindua Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa lengo la kuimarisha ufanisi wa Taasisi  na uangalizi wa karibu.

  Akizungumza hivi karibuni wakati wa uzinduzi huo uliofanyika  Taasisi ya Uhasibu Tanzania kampasi ya Singida  Dkt. Kijaji amesema Bodi hiyo itamsaidia Waziri wa Fedha na Mipango kupata ushauri wa kitaalam  na hatimaye kutoa maamuzi  yenye tija kwa Taasisi na Taifa kwa ujumla.

   "Bodi hii ya Ushauri inategemewa kutoa mchango  wa mawazo na  kitaalam yanayohusu uendeshaji  na uboreshaji wa  Taasisi yetu ya TIA ili kuendana na mabadiliko yanayoendelea duniani katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa na kijamii", amesema Dkt. Kijaji.

  Dkt. Kijaji ameongeza kuwa Bodi hiyo ina wajibu wa kujua ubora wa wanafunzi wanaohitimu katika chuo hicho ikiwa ni pamoja na ubora wa vyeti vyao kuendana na uwezo wao wa kufanya kazi katika fani walizosomea na kukabiliana na changamoto kwenye maeneo ya kazi.

  Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Said Chiguma amesema Taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchache wa miundombinu kama vile kumbi za mihadhala, madarasa, maktaba na maabara za kompyuta ambavyo ni nyenzo muhimu katika utoaji wa elimu iliyo bora.

  Chiguma amesema ili kupunguza changamoto hizo, Taasisi inajitahidi kutenga fedha inazozikusanya ili kukarabati na kujenga majengo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu na kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi.

  Taasisi ya Uhasibu Tanzania ni chuo cha Serikali ambacho kinatoa mafunzo katika fani za Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, Uongozi wa Rasilimali Watu, Masoko na Uhusiano wa Umma pamoja na Uhasibu wa Fedha za Umma kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashada (Diploma)  na Shahada (Degree).
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza muda mfupi kabla hajazindua Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
   Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Said Chiguma akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Joseph Kihanda, akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi hiyo. Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA tawi la Singida mjini.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa  Bodi mpya ya Ushauri ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA). Uzinduzi huo umefanyika hivi karibuni katika kampasi ya TIA Singida mjini. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Ushauri TIA Said Chiguma na Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA Joseph Kihanda na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhe. Elias Tarimo na Mjumbe wa Bodi Dkt. Leonada.

  0 0

   Katibu Tawala Msaidizi,Uchumi na Mipango Mkoa wa Mwanza, Johansen Bukwali akifungua Mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) kwa maafisa Mipango, Wachumi, Wahasibu, Maafisa Tehema na Makatibu wa Afya wa Halmashauri kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.
  Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka TAMISEMI,  Elisa Rwamiago akitoa mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) kwa maafisa Mipango, Wachumi, Wahasibu, Maafisa Tehema na Makatibu wa Afya wa Halmashauri kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.
   Washiriki wa Mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) wakifuatilia mafunzo yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.
  Mgeni rasmi (katikati walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Mfumo Mpya wakuaandaa Mipango na Bajeti za Serikali za Mitaa (PlanRep) kutoka Mkoa wa Geita yaliyofanyika Jijini Mwanza, leo Tarehe 24 Julai 2017.

  0 0

  Na: Paschal Dotto - MAELEZO.

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Kenya zimefanya mazungumzo ya pamoja na kutatua  vikwazo vilivyokuwa vikiikabili  sekta ya biashara baina ya nchi hizo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga ametoa taarifa juu ya kumalizika kwa tofauti za kibiashara baina ya nchi hizo. 

   “Bidhaa za Tanzania zilizowekewa vikwazo na nchi ya Kenya ni unga wa ngano pamoja na  gesi ya kupikia (LPG). Aidha juhudi, za Serikali ya Tanzania kuona vikwazo hivyo vinaondolewa na Serikali ya Kenya kwa wakati hazikuzaa matunda, hivyo Serikali ya Tanzania nayo iliweka vikwazo kwa bidhaa za maziwa na sigara kutoka Kenya kuingia katika soko la Tanzania,” amefafanua Dkt. Mahiga.

  Amesema kuwa kutokana na mahusiano mazuri ya udugu yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya na  kwa kujali manufaa mapana ya Jumuiya ya Afrika Mashariki viongozi wakuu wa nchi hizo mbili, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli walikubaliana kuzungumza na kutoa vikwazo vya biashara hizo. 

  Aidha, Dkt. Mahiga amesema, nchi hizo zimekubaliana kuunda Tume ya pamoja ambayo itakuwa na jukumu la kuepusha tofauti za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kutolea ufumbuzi changamoto za kibiashara kati ya nchi hizo mbili pindi zinapojitokeza.

  Tume hiyo itaongozwa na Mawaziri wa mambo ya Nje wa Tanzania na Kenya na kujumuisha mawaziri wanaohusika na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Biashara, Fedha, Mambo ya Ndani ya Nchi, Kilimo, Uchukuzi na Utalii wa nchi hizo. 
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo na kushoto ni Kaimu Balozi wa Kenya nchini Tanzania Peter Sang.
   Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kikanda toka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Innocent Shiyo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Balozi Dkt. Augustine Mahiga (hayupo pichani) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu mazungumzo ya pamoja kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. Kulia ni mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Songwe, Erasto Zambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
   Baadhi ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi wakimsikiliza  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao  katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya  Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea silaha za jadi kutoka kwa Chifu  Muleshwelwa Mzunda wa Mbozi ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chief wa Songwe Julai 24, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe . Kushoto kwake ni mkewe Mary na watatu kulia  ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto kwake) wakiagana na viongozi wa Mkoa wa Songwe kabla ya kuondoka kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa huo kwenda kwenye uwanja wa ndege wa Songwae baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo Julai 24, 2017. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanyara wilayani Mbozi ambao walikusanyika barabarani wakitaka asimame na kuzungumza nao . Alikuwa akitoka Vwawa kwenda Uwanja wa Ndege wa Songwe Julai 24, 2017.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi.
  Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
  Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakimsikiliza Waziri Maghembe.
  ................................................................................

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amewapokea Mabilionea 26 wa taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika Hifadhi ya Taifa  Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

  Mabilionea hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda, Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.

  Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake,  Prof. Maghembe aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza "hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores) na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti". 

  Prof. Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye  amani na vivutio vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea Tanzania mapato.

  Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.

  (SOURCE: WWW.WIZARAYAMALIASILINAUTALII.BLOGSPOT.COM)

  0 0

    Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kikosi cha Yanga kimeendelea tena na mazoezi mapema leo baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili kutoka kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo  Mzambia George Lwandamina.

  Yanga waliokuwa wanafanya mazoezi ya Gym kwa takribani wiki  moja na nusu ikiwa ni katika programu ya Mwalimu Lwandamina ya kuwaweka fit wachezaji hao baada ya kuwa mapumzikoni kwa kipindi kirefu.

  Leo mapema asubuhi kikosi hicho kiliingia katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu 2017/18 huku wakitarajiwa kuwa mechi kadhaa za kirafiki.

  Mechi ya kwanza ya kirafiki itakuwa ni Agosti 5 dhidi ya timu ya Singida inayonolewa na aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo Mholanzi Hans Van De Pluijm mchezo utakapigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.
   
  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi Amis Tambwe akiwa katikati akipambana na wachezaji wa Yanga katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
   Beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul akiwa amemiliki mpira akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake  katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
   Wachezaji wa Yanga wakiwa katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
  Kocha George Lwandamina akijadiliana jambo na Beki kisiki Kelvin Yondani katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.


  0 0

  Visiwa vya Zanzibar na Mauritius vina fursa ya kubadilishana uzoefu katika miradi ya Maendeleo ili kujiongezea ujuzi na maarifa yanatayowawezesha Wananchi wake kuimarika zaidi kiuchumi hali itakayosababisha Mataifa yao kuongeza mapato.

  Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Kisiwa cha Mauritius { Moneo Consulting } Bwana Devanand Virahsawmy akiuongoza ujumbe wa viongozi wa Kampuni hiyo alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.

  Bwana Devanand Virahsawmy alisema Sekta ya elimu ambayo ndiyo mama katika Taifa lolote Duniani inaweza kuwa mwanzo wa ushirikiano huo unaoweza kutoa nafasi kwa vijana wa pande hizo mbili kujipatia Elimu ya Msingi, Sekondari hadi vyuo Vikuu .

  Alisema mpango huo wa pamoja kupitia Kaisheni ya pamoja kwa Nchi zilizozunguukwa na Bahari ya Hindi utaongeza chachu ya uchumi kwa Vijana waliobobea Kitaaluma sambamba na ongezeko la ajira.

  Bwana Devanand alisema Visiwa vya Mauritius tayari vimeshapiga hatua kubwa ya maendeleo hasa katika Sekta ya Utalii kiwango ambacho wanaweza kusaidia Taaluma kwa Nchi zilizo jirani na Visiwa hivyo.

  Mwenyekiti huyo wa Kampuni ya Moneo Consulting alimueleza Balozi Seif pamoja na Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa SMZ Kwamba Uongozi wa Kampuni yake upo Zanzibar kuitika wito Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuangalia fursa za Uwekezaji.

  Alieleza kwamba Kampuni hiyo tayari imeshijengea uwezo wa kuendesha miradi mbali mbali ya Kiuchumi na Maendeleo akiitaja baadhi yake kuwa ni pamoja na Miradi ya Umeme, Bara bara, Utalii, Benki ya Ufukweni { Off show Bank } Viwanda vya vidogo vidogo pamoja na Uvuvi wa Bahari Kuu.

  Akitoa ufafanuzi wa mipango ya Uwekezaji Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} Nd. Salum Nassor Khamis alisema Zanzibar imeanza kufanya mabadiliko ya uchumi wake katika Miaka ya 90 ili kutoka nafasi kwa Taasisi yenye uwezo wa uwekezaji kushiriki kwenye mabadiliko hayo. 

  Ndugu Salum alisema ushirikishwaji wa Sekta binafsi katika kuchangia uchumi wa Taifa umezingatiwa ili kujenga jamii itakayokwenda sambamba na mabadiliko ya Kiuchumi Duniani.

  Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliueleza Ujumbe huo wa Kampuni ya Ushauri ya Moneo kwamba Zanzibar ina mtazamo wa kuwekeza katika sekta ya Uvuvi wa Bahari Kuu.

  Alisema Rasilmali ya Bahari ni eneo linaloweza kujenga uchumi imara utakaoweza kuongeza mapato ya Taifa sambamba na kupunguza ufinyu wa ajira uliowakumba Vijana wengi wanaomaliza masomo yao Nchini.

  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  24/7/2017.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Mauritius (Moneo Consulting) Bw. Devanand Virahsawmy Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Balozi Seif na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ, Makatibu Wakuu na Watendahi Wakuu wa SMZ akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya Moneo Consulting kutoka Mauritius.
  Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Ushauri kutoka Mauritius (Moneo Consulting) Bw. Devanand Virahsawmy akisisitiza jambo wakati ujumbe wake ulipofanya mazungumzo na Balozi Seif.
  Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Kampuni ya Moneo Consulting na badhi ya Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wa SMZ. Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipenya ili kuvuka katika daraja la mto Songwe kwenye mpaka wa mikoa ya Mbeya na Songwa baada ya Lori lililokuwa limebeba vinywaji baridi kupinduka katika daraja hilo na kuziba barabara. Ajali hiyo ilisababisha msururu mrefu wa magari yaliyokuwa yakitoka Tunduma na yale yaliyokuwa yakitoka Mbeya Julai 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  Msururu wa magari uliosababishwa na ajali ya lori lililopinduka kwenye daraja la mto Songwe katika barabara Mbeya- Tunduma Julai 24, 2017. Lori hilo lilikuwa limebeba vinywaji baridi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Kulia kwa Mh Rais ni Balozi wa India Nchini Mhe Sandeep Arya, Kulia kwa Mh Rais ni Waziri Maji Mhandisi Gerson Lwenge, akifuatiwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na viongozi balimbali wa Mkoa wa Tabora wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa mradi wa Maji toka Ziwa Victoria Kwenda Kwenye Mji wa Tabora, Igunga na Nzega Julai 24, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Balozi wa India Nchini Mhe Sandeep Arya,wakiteta jambo mara baada ya Rais kuweka Jiwe la Msingi na Ufunguzi rasmi wa mradi wa Maji toka Ziwa Victoria Kwenda Kwenye Miji ya Tabora, Igunga na Nzega leo Julai 24, 2017.
  Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa mara baada ya ufunguzi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege Tabora leo Julai 24, 2017.
  Rais wa Jamhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo ya Mradi Ukarabati, Ujenzi na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege Tabora toka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Uwanja huo Mhandisi Neema Joseph.
  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akikata utepe kwenye Ufunguzi wa barabara ya Tabora -Puge -Ngeza yenye Urefu wa Kilometa 114.9 akiwa na  Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Prof Makame Mbarawa na viongozi wengine wa mkoa wa Tabora.
  Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia wananchi wakati wa ziara mkoani Tabora.

  0 0


  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yamefikia katika hatua ya nusu fainali kwa timu nne kuumana mwishoni mwa wikiendi iliyopita huku Mchenga Bball Stars na Kurasini wakiibuka na ushindi.  Michezo hiyo iliyochezwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay ilikuwa ni hatua ya kwanza ya mechi za nusu fainali ambapo wikiendi ijayo itaendelea tena ikiwa ni hatua ya pili.  Baada ya kumalizika kwa hatua tatu za mechi ya nusu fanilai, mshindi wa jumla wa mechi hizo ataingia moja kwa moja katika fainali ya Sprite BBall Kings inayotarajiwa kufanyika mwezi Agost mwaka huu kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.


  Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wikiendi iliyopita, wiki ijayo timu hizo zitaumana tena mpaka katika hatua ya tatu na timu zilizopata alama nyingi ndiyo zitafanikiwa kuingia hatua iya fainali.

  "Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya leo na katika michezo ya hatua zijazo ndiyo watakaofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings,"amesema Basilisa.

  Katika mechi zilizochezwa wikiendi hii mchezo wa kwanza uliwakutanisha TMT dhidi ya Kurasini ambapo Kurasini walitoka na ushindi wa vikapu 87 kwa 80, na mchezo wa pili timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers 

  Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio inaendelea tena wiki ijayo katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay na mshindi kamili ataondoka na kitita cha shiling milion 10.
  Mchezaji wa timu ya Mchenga (jezi nyeusi) akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Flying Dribblers katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.
  Mchezaji wa timu ya Flying Dribblers (jezi nyeupe) akiwa amemiliki mpira katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.
  Mchezaji wa timu ya Flying Dribblers (jezi nyeupe) akiwa amemiliki mpira katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.

  Mchezaji wa timu ya Mchenga (jezi nyeusi) akijaribu kumtoka mchezaji wa timu ya Flying Dribblers katika mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza ambapo timu ya Mchenga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa vikapu 119 dhidi ya vikapu 70 vya Flying Dribblers.

older | 1 | .... | 1314 | 1315 | (Page 1316) | 1317 | 1318 | .... | 1897 | newer