Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKOA WA KIGOMA

$
0
0
 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji toka Ziwa Tanganyika toka kwa mhandisi mshauri wa mradi huo ndugu Michael Mwamkinga 
 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata maelezo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji toka Ziwa Tanganyika toka kwa mhandisi mshauri wa mradi huo ndugu Michael Mwamkinga 
 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Waziri Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe pamoja  na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi  wa mradi wa maji toka ziwa Tanganyika 
  Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Waziri Maji Mhandisi Gerson Lwenge, Mbunge wa Kigoma mjini Mhe. Zitto Kabwe pamoja  na viongozi wengine akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi  wa mradi wa maji toka Ziwa Tanganyika 
 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Mamia ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. 
  Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia Mamia ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. 
 Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli,akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Bulombora Kikosi cha 821KJ.
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa Bulombora Kikosi cha 821kj wakishangilia mara baada ya kukutana na kupiga picha kusalimiana na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli. 
  Maelfu ya waanchi wakimsikiliza Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati akiwahutubia a katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. 
Maelfu ya waanchi wakimsikiliza Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli wakati akiwahutubia a katika Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. PICHA NA IKULU

JAJI UPENDO MSUYA AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR

$
0
0

Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka undogo kwenye kaburi la Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya aliyewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Juma akiweka undogo kwenye kaburi la Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Anne Makinda akiweka undogo kwenye kaburi la Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Mume wa Marehemu Hilary Msuya akiweka undogo kwenye kaburi la Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Prof. Ibrahim Juma akizungumza jambo na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakati wakishiriki mazishi ya Marehemu Jaji Upendo Hilary Msuya aliyewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam leo

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI JULAI 23,2017

ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBBAINI WA UFISADI

$
0
0
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville (kushoto).
Askofu Blaston Gaville wakati akiwekwa wakfu kuongoza Dayosisi ya Iringa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). 


KUKAMILIKA kwa mchakato wa uaandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutasaidia kuweka misingi imara na kuondoa changamoto zilizopo katika Katiba ya sasa, hivyo kukomesha ufisadi na kuinua uchumi wa Tanzania.

Aidha, kukamilika huko kwa Katiba Mpya kutaakisi jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, ambaye alimtaka Rais Magufuli kuumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, kwani alisema mbali ya kuakisi kasi yake anayoifanya ya kukuza uchumi pia kutasaidia kuhimiza uwajibikaji.

“Wakristo na Watanzania kwa ujumla tuna imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano na ni matarajio yetu kwamba mchakato wa kuandika Katiba utamalizwa kama lengo lilivyokuwa,” alisema. 

Askofu Gaville amesimikwa ili kuchukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella ambaye amestaafu.Alisema wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dkt. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote. 

Alisema Tanzania ina wanyonge wengi kuliko wenye nguvu, hivyo wanatiwa moyo na jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli na serikali yake hasa anapowatetea wanyonge.Aidha, pamoja na kupongeza jitihada hizo, Askofu Gaville, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa kodi akisema hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo bila mapato hayo.

“Tunaiomba serikali iangalie upya suala la kodi kwa mashirika ya dini kwani baadhi ya kodi tunazolipa, ikiwemo ya kuendeleza vyuo vya ufundi na ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, zimekuwa mzigo mkubwa kwaetu.

“Kazi ya Kanisa ni kutoa huduma, siyo kutengeneza faida, kodi hizo zimeleta changamoto kubwa kwa uendeshaji wa taasisi, tunaomba serikali iziangalie upya,” alisema.

Kuhusu elimu, Askofu Gaville alisema Kanisa linasaidia watoto maskini ili wapate haki yao ya elimu na akaiomba serikali isiwaingize katika kundi la watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo kwa sababu wanasoma shule binafsi. 

“Wanapojiunga na vyuo vikuu, tunaomba Bodi ya Mikopo isiwanyime mikopo stahiki kwa kisingizio cha shule wanazotoka, ufanyike upembuzi ili kutoa msaada kwa walengwa wote,” alisema.

Aidha, alisema Dayosisi ya Iringa inatoa mwaliko kwa vyama vyote vya kisiasa na jamii nzima ya Watanzania kuendeleza na kukuza tunu ya ushirikiano na moyo wa kizalendo ili kuwa na maendeleo yenye tija, badala ya kujenga uhasama kwa sababu za kiitikadi.

Katika salamu zake kwa waumini wa dayosisi hiyo, Askofu Mkuu wa KKKT Tanzania, Dkt. Fredrick Shoo, alizipongeza kamati mbili za madini zilizoundwa na Rais Magufuli akisema zimewaumbua baadhi ya Watanzania waliodhani ni sifa kusaini mikataba ya madini inayonyonya haki ya Watanzania.

“Kama hao watu waliosaini hiyo mikataba walidhani wanaisadia nchi huku wakijua mikataba hiyo inalenga kuiibia nchi, wajue hayo ni mambo ya aibu na ni upumbavu mkubwa kufanya mambo kama hayo kwa ajili ya matumbo yao binafsi,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri William, akitoa salamu za serikali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, alisema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini ili kufikia malengo yake ya maendeleo.

William alizungumzia fursa mbalimbali za maendeleo zilizopo mkoani Iringa na akawaomba Watanzania na wawekezaji kuzitumia ipasavyo kuunga mkono jitihada za Rais za kuifanya nchi kuwa ya viwanda.

Katika hatua nyingine, Askofu Mstaafu wa Dayosisi hiyo, Dkt. Owdenburg Mdegela, aliipongeza serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa hatua mbalimbali inazochukua kujirekebisha.

Akiungana na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Iringa katika maandamano ya amani siku moja kabla ya kumsimika Askofu Gaville, Dkt. Mdegela alisema moja ya makosa makubwa yaliyofanywa na serikali lilikuwa ni kuua Azimio la Arusha la mwaka 1967.

Maandamano hayo yalifanyika mjini Iringa kwa nia ya kupongeza juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. Magufuli katika kushughulikia changamoto zinazolikabili Taifa, ambapo yalipokelewa katika viwanja vya Mwembetogwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, siasa na serikali, watumishi, wanafunzi, wafanyabiashara na wadau wengine wa maendeleo kutoka wilaya zote za mkoa huo.

“Hatukupaswa kuua Azimio la Arusha pamoja na kwamba kuna mambo yalipaswa kubadilishwa. Kimsingi azimio lile lilikuwa na mambo mengi ya msingi ambayo ni ya faida kwa Taifa, hayo ni pamoja na maadili kwa viongozi na msingi wa kujitegemea,” alisema.

Alibainisha wazi kwamba, serikali ya CCM ilichoka, lakini kupitia kwa Rais Magufuli imeanza kujirekebisha ikiwa ni pamoja na kutembea katika misingi ya Azimio la Arusha, hatua inayopaswa kupongezwa hadharani.

“Anayempinga Rais anayekamata wezi, watumishi hewa na anayepambana kulinda rasilimali za nchi kwa manufaa ya Watanzania wote na kuhimiza uwajibikaji lazima atakuwa alipata matokeo mabaya ya mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne.

“Tunapaswa kuiona falsafa ya kiongozi wetu pamoja na kwamba wapo watu wanambeza kwa maneno mengi ya kuudhi lakini wanaombeza Magufuli wakumbuke kwamba hata Mungu alibezwa na theluthi moja ya malaika zake,” alisema.

Amina Masenza, katika utangulizi wake, alisema Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 inasema katika miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuondoa umaskini, kutatua tatizo la ajira hasa kwa vijana, katika vita dhidi ya rushwa na ubadhilifu wa mali za umma na kudumisha amani, ulinzi na usalama.

UBALOZI WA JAPAN NCHINI WAAHIDI KUENDELEA KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI YA KIMAENDELEO MKOANI IRINGA

$
0
0
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida na Waziri Lukuvi wa pili kulia na wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ,mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakishiriki kukata utepe kuzindua bweni Shule ya Idodi sekondari leo 
Vitanda vilivyopo katika bweni hilo 
Hili ndilo bweni la kisasa lililojengwa na ubalozi wa Japan nchini 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akimkaribisha balozi wa Japan nchini 
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akizungumza na wananchi na wanafunzi wa sekondari ya Idodi 
Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida akikabidhi taa za mionzi ya jua kwa mkuu wa shule ya sekondari Idodi kulia kwake ni mbunge wa Isiman Wiliam Lukuvi na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na katibu wa CCM Iringa vijijini Dodo Sambo 
Balozi wa Japan nchini akimkabidhi taa hizo mbunge wa Isimani wiliam Lukuvi 
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi ambae ni mbunge wa Ismani akimsaidia balozi wa Japan nchini kukaa katika kiti cha asili ya Kihehe baada ya kuvishwa nguo hizo za heshima 
Balozi wa Japan nchini akivishwa nguo za kichifu wa wahehe 
Balozi wa Japan Masaharu Yoshida akivishwa nguo za kichifu 
balozi wa japan nchini akiwa na nguo za kijadi za kihehe akisema hapa KAZI TU 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto na waziri Lukuvi na DC Iringa Kasesela wakiwa na balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida 
Mbunge wa Ismani na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi akimpongeza balozi wa Japan kwa msaada wa ujenzi wa Bweni 
NA MatukiodaimaBlog 

UBALOZI wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli. 

ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa Bweni hilo la wanafunzi shule ya sekondari ya Idodi Iringa balozi Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania. 

Alisema kuwa hatua Japan kufika kusaidia ujenzi wa bweni hilo katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Ismani Wiliam Lukuvi ambaye ni waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliloomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali kuteketea kwa Moto.

"waziri Lukuvi lileta maombi ya mradi wa kujengewa miradi hiyo ya maendeleo ambayo ni Hostel ya wasichana shale ya wasichana Ismani ambayo ilijengwa toka mwaka 2005 na mwaka2008 kujenga jengo la OPD na wodi ya wagonjwa katika zahanati ya Mlowa na mwaka 2010 kununua gari la wagonjwa katika zahanati ya Mlowa... namshukuru Waziri Lukuvi kwa kusimamia vema miradi hiyo"

Balozi huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo. 

" Leo nimefurahi kuona ujenzi umekamilika kwa kiwango kizuri vitanda vya kutosha, mfumo wa kuhifadhi maji, Hosteli hii sasa inauwezo wa kulaza wanafunzi 208 kama kusudio la ujenzi ni matumaini yangu mradi huu utatunzwa vema"

Balozi huyo alisema kutokana na usimamizi mzuri walioufanya kampuni ya Koyo Corporation kampuni ya kijapani imetoa msaada wa taa zinazotumia nguvu ya mionzi ya jua kwa ajili ya kutumia wanafunzi wote watakaoishi katika bweni hilo. 

Hata hivyo alisema ubalozi wa Japan nchini utaendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania chini ya kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awali akimkaribisha balozi huyo alisema kuwa serikali ya mkoa inafurahishwa na msaada huo ambao umesaidia kupunguza msongamano ya wanafunzi bwenini na hivyo bweni hilo ambalo litatunzwa vizuri. 

Mbunge wa Ismani waziri Lukuvi pamoja na kupongeza msaada huo wa kujengewa bweni na miradi mingine bado amepongeza kwa hatua ya balozi huyu kubariki zaidi ya shilingi milioni 11 zilizobaki katika ujenzi wa bweni hilo kutumika kununua vifaa vya kusambaza maji ya kisima kitakachochimbwa shuleni hapo.

MSANII BONGO FLAVA AT MFALME WA MIDUARA BONGO, MR TZ WANOGESHA RAHA ZA PWANI COLLEGE PARK, MARYLAND

$
0
0
Msanii wa Bongo flava na mfalme wa miduara AT, akiongelea utamaduni wa kiswahili na raha za pwani kwenye jopo la kongamano la raha za pwani kwa lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na baadae kuonesha onesho kali ya nyimbo zake zilizotamba na zinazoendelea kutamba kwenye anga ya bongo na kimataifa. Kongamano hilo linaloambatana na tamasha la Mswahili na lugha yake huandaliwa na Swahili Media Network na hufanyika mara moja kila mwezi. Picha na Vijimambo Blog na Kwanza Production.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT akichengua mashabiki wake kwa wimbo mmoja wapo wa mduara.
Msanii wa Bongo flava mfalme wa miduara AT usipime ni balaa
Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye  jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 Hampton Inn, College Park, Maryland.
Msanii wa Bongo Flava Mr. Tz akitoa buradani kwenye  jopo la kongamano la raha za pwani
Aisha akifungua pazia kwenye jopo la kongamano la raha za pwani kwa lengo la kudumisha na kutangaza utamaduni wa Mswahili na lugha yake.na baadae kumkaribisha mratibu wake Bwn. Mgaza (hayupo pichani).
Mratibu wa Raha za Pwani Bwn. Mgaza akiuelezea Utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Bi Rukia akichangia nini maana ya Utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland na huku akitoa rai kwa wazazi ughaibuni kuacha kudharau utamaduni wa wetu na wafanye kazi ya ziada kuwafundisha watoto wa ughaibuni lugha ya Kiswahili na utamaduni wake.
Mama mitindo na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA MaWiny Casey akichangia vazi la khanga na utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.

Mama mitindo na mkurugenzi wa Miss Tanzania USA MaWiny Casey akimkabidhi tuzo Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza linalosimamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) - Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA, aliefuatana na Msanii maarufu wa nyimbo na ngoma ya Muduara- Bwana ALI RAMADHAN ALI, al-maarufu kwa jina la MR. AT kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Mwenyekiti Mtendaji wa Baraza linalosimamia shughuli za utamaduni na Sanaa nchini Tanzania (BASATA) - Bwana GODFREY LEBEJO MNGEREZA akiongelea muziki unavyodumisha utamaduni wa Kiswahili na lugha yake kwenye jopo la kongamano la raha za pwani lililofanyika siku ya Jumamosi July 22, 2017 College Park, Maryland.
Watoto Imani (kushoto)naAaliyah wakicheza moja ya mchezo ya watoto wanavyocheza kwa Kiswahili kama moja ya kudumisha Kiswahili na utamaduni wake.
 

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NGURUKA WILAYANI UVINZA MAPEMA LEO.

$
0
0
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi mbalimbali wa mji wa Nguruka mapema leo asubuhi,waliojitokeza mapema leo kumshuhudia Rais akiweka jiwe la msingi la Mradi wa maji.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,ambapo pia ameweka jiwe la msingi la mradi huo unaotarajia kukamilika Desemba 31, 2017,ukamilishwaji wa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.
 Rais Dkt Magufuli akipeana mkono na Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini,Mh Daniel Nsanzugwako mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi mkubwa wa maji mapema leo mjini Nguruka mkoni Kigoma.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,na kuwamba Mradi huo unatarajia kukamilika Desemba 31,2017,kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.
 Rais Dkt Magufuli akitoka kukagua mradi huo wa maji unaotarajia kukamilika Desemba 31,2017.kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.Rais Dkt Magufuli yuko njiani akielekea mkoani Tabora,ambapo atasimama Wilayani Kaliua na kuzindua barabara ya Kaliua hadi Kazilambwa yenye urefu wa kilometa 56.

NAIBU WAZIRI KIGWANGALLA AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA BWENI LA WAZEE KAMBI YA KOLANDOTO NA KUZINDUA JIKO LA NISHATI YA GESI

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akilsililiza Katibu wa Baraza la wazee wa Mkoa wa Shinyanga Mzee Faustine Sengerema mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo la bweni la wazee katika makazi ya wazee waisiojiweza ya Kolandoto mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Ujenzi wa Bweni la wazee waishio katika makazi ya wazee wasiojiweza ya Kolandoto Mhandisi Harold Jackson Mtyana wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo na kuweka jiwe la msingi.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akisililiza matumizi ya nishati ya jiko la gesi kutoka kwa Afisa Mfawdhi ya Makao ya wazee Kolandoto katika Manispaa ya Shinyanga, muda mfupi kabla ya uzinduzi wa matumizi ya majiko hayo katika vituo vya makao ya wazee na watoto hapa nchini.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akikata utepe katika moja ya bajaji kuashiria ugawaji na matumizi rasimi ya bajaji hizo katika makazi ya kulea wazee wasiojiweza ya Kolandoto Shinyanga kwa niaba ya Makazi mengine nchini.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akimkabidhi funguo ya bajaji Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea wazee wasiojiweza ya Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe kwa niaba ya maafisa Wafawidhi katika makazi mengine nchini.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla(Mb) akimkabidhi Sanduku la Huduma ya kwanza Afisa Mfawidhi wa Makazi ya Kulea Wazee wasiojiwezaya Kolandoto Bi Sophia Kang’ombe kwa niaba ya maafisa Wafawidhi katika makazi mengine nchini.


TENGA ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA KAMATI YA UFUNDI NA MAENDELEO CAF,TFF YAMPONGEZA.

$
0
0
Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace John Karia amempongeza Leodegar Chilla Tenga - Rais wa Heshima wa TFF kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Ufundi na Maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Leodegar Chilla Tenga aliteuliwa Ijumaa iliyopita katika Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika mjini Rabat nchini Morocco ambako katika kamati hiyo muhimu, Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zambia (FAZ), Kalusha Bwalya.

“Hii ni sifa kwa nchi. Na ni sifa kwa Mheshimiwa Tenga. Tunajisikia fahari Tanzania kung’ara katika medani za uteuzi katika vyombo vya kimataifa kama CAF. Uteuzi wake ni kwamba anafungua njia kwa nchi na wengine ili kufanya vema,” anasema.

Karia amesema ana imani na Tenga na Bwalya katika kamati yao kwa sababu ni wachezaji na manahodha wa zamani wa timu za taifa. Itakumbukwa kwamba Tenga alikuwa akicheza kama mlinzi Bwalya alikuwa mshambuliaji. “Wote ni wataalamu. wanajua, tutafanikiwa.”

Katika mkutano huo mbali na kuteua akina Tenga na kuunda kamati nyingine, pia ulifanya marekebisho ya muundo wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na sasa yatakuwa yakifanyika katikati ya mwaka badala ya mwanzoni mwa mwaka. 

Kwa miaka ya nyuma hadi mwaka huu ambako michuano hiyo ilifanyika Gabon, ilikuwa ikifanyika kuanzia katikati ya Januari hadi Februari. Mbali na kuzitoa Fainali za AFCON katikati ya mwaka hadi mwanzoni, pia idadi ya timu za kushiriki zimeongezwa kutoka 16 hadi 24 ambako sasa utakuwa na timu washindwa 10 badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.

“Watanzania wasikate tamaa, hata kama kwa mfumo wa sasa unaofutwa au tuseme kubadilishwa, bado tuna malengo yetu yalikuwa ni kufuzu, Tunajipanga kwa hali ya sasa na hatujaanza vibaya na Lesotho. Bado tuna nafasi,” amesema Karia.

Michuano hiyo kuhamishwa kutoka Januari na Februari hadi Juni na Julai kuanzia Fainali za mwaka 2019 nchini Cameroon.

Hii si mara ya kwanza kwa Tenga aliyepata kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), bali amekuwa akiteuliwa mara kwa mara kuwa Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF. Hongera sana Rais wa Heshima wa TFF, Leodegar Chilla Tenga.

RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO

$
0
0
Mh.David Kafulila
Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma

RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nguruka,leo Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana.

Amesema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwasababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa.

"Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulila kwa uzalendo wake kwa nchi na nitaendelea kumpongeza maisha yangu yote"alisema Magufuli.Magufuli alisema maendeleo hayana chama ndio maana Kafulila alijitoa kwa hali ya juu na kutetea fedha za Wananchi zilizo kuwa zikiibiwa na mafisadi wachache na kujinufaisha wao.

"Ninajua Kafulila ulitukanwa sana wakati wa kuibua sakata la Escrow, wapo watu walikuita tumbili mimi najua wewe sio tumbili ,matumbili ni wao wewe najua ni wa Chama kingine lakini umefanya kazi kubwa ya kulinda maslahi ya nchi, kwahiyo nitakuwa mnafiki sana nisipo kupongeza kitu ulichokifanya ni kikubwa Kwa,Taifa naomba nikupongeze kwa hilo",

Alisema Kiongozi mzuri ni yule ambae anatetea wananchi bila kujali chama wala siasa za uchochezi , hivyo atahakikisha kuwa Wananchi hawateseki na Wale ambao wameiba fedha za serikali na Wananchi wanazirudisha bila kujali nyadhifa walizonazo, ili pesa hizo zitumike katika kuleta maendeleo.

Rais Magufuli aliwaahidi Wananchi wa Nguruka atahakikisha anatatua kero ya Maji na umeme katika kata yao,kuhusu suala la umeme atamtuma Waziri wa Nishati na madini ili aweze kutatua tatizo hilo na kuwasaidia Wananchi kuepukana na shida hizo.

Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji mkubwa katika kata ya Nguruka uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 ambao unatarajiwa kukamilika desemba 30 mwaka huu ambao utafuta kero ya maji kwa wananchi wa kata ya Nguruka.

Akiongea kwa njia ya simu na mtandao huu akiwa jijini Dar es Salaam aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kigoma kusini kupitia tiketi ya chama cha NCCR Mageuzi David Kafulila kuhusu kauli ya Rais Kafulila amesema kuwa Rais amekuwa akimtia moyo kwani anaona kazi aliyokuwa akiifabya sasa imeanza kuleta matokeo mazuri.

"Kwakweli nafarijika na inanipa moyo wa kizalendo zaidi ninapo ona Rais anaunga mkono sakata la Escrow ambalo mimi ndo nililiibua wakati nikiwa mbunge japo nilipitia kwenye kipindi kigumu "alisema Kafulila

Kafulila alisema kuwa wakati akiwa mbunge kwenye sakata la Escrow msimamo wake na Rais ulikuwa unafanana toka bungeni.

Mfanyakazi wa Tanesco Mtwara aibuka na Sh Milioni 20 za Biko

$
0
0

MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko katika droo ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.

Lukinga fundi wa Tanesco alitangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed kushoto akiandika maelezo ya mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20 alilopata mfanyakazi wa TANESCO Mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga mara baada ya kupatikana kwenye droo ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja. Picha na Mpigapicha Wetu.
Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha pozi nzito baada ya kupatikana mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyetengazwa katika droo ya 25 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema ni mara ya kwanza kumpata mshindi wa droo kubwa ya Sh Milioni kutoka Mkoa wa Mtwara.

Alisema kupatikana kwa mshindi huyo kunaongeza wigo wa washindi wa Biko kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wanaoshinda droo kubwa pamoja na wanaoibuka na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mchezo wetu wa kubahatisha tumempata mshindi kutoka Mtwara, ambaye ni fundi wa Tanesco, huku tukiamini kuwa kila mtu anaweza kuibuka na ushindi kutoka Biko endapo atacheza mara nyingi zaidi kwa kupitia mitandao ya simu.

“Biko inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku gharama za uchezaji zikianzia Sh 1,000 na kuendelea, ambapo shilingi 1000 inatoa nafasi mbili ambazo ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotolewa kila Jumatano na Jumapili,” Alisema Melles.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed, alimpongeza Lukinga kwa kuibuka na ushindi huo mnono, huku akisema Biko ni mchezo unaochezwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote zilizowekwa katika tasnia ya michezo ya kubahatisha.

“Bodi yetu inakuwa karibu kuhakikisha kwamba washindi wetu wanapatikana kihalali, ambapo safari hii mkazi wa Mtwara, Lukinga ameibuka kidedea kwa kupata donge nono la Biko la Sh Milioni 20,” Alisema.

Naye Lukinga akizungumza kwa simu wakati anahojiana na Kajala, Balozi wa Biko, alisema haamini kabisa kama ameshinda zawadi nono ya Biko, akipigiwa simu kuambiwa hilo dakika chache baada ya namba yake kushinda.

“Nashukuru sana kwa kushinda zawadi hiyo nono kutoka Biko, maana siku ushindi huo umeniaminisha kuwa watu wanashinda kihalali, hivyo huu ni wakati wangu kufurahia maana hata jana nilicheza Biko,” Alisema.

Kwa kushinda donge nono la Biko, Lukinga anatarajia kupokea fedha zake haraka wiki hii, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kutoa zawadi za fedha za papo kwa hapo pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 zinazotolewa Jumatano na Jumapili, huku mwezi Mei na Juni pekee Biko wakitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wao.

MAKONDA: KAMPUNI YA PROPERTY INTERNATIONAL INASAIDIA KUONDOA TATIZO LA MIGOGOLO YA ARDHI

$
0
0

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema miongoni mwa Makampuni Binafsi yanayoisaidia Serikali kwa kufanya kazi ya uuzaji na upimaji wa Viwanja vya Viwanda na Makazi, ni Kampuni ya Property International pekee ambayo mpaka sasa kama mkuu wa mkoa bado hajapata malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu migogolo ya ardhi.

Akizungumza katika Kipindi cha Sema Kweli kinachorushwa kila Ijumaa na Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, alisema kuwa, amekuwa akipata malalamiko kadhaa kutoka kwa wananchi juu ya migogolo hiyo inayotokana na kuuziwa ama kupimiwa viwanja na makampuni ambayo hayajajitosheleza katika kufanya kazi hiyo baada ya kuidhinishwa na Serikali.

Aidha alisema kuwa kutokana na suala hilo kumekuwa na ugumu wa Serikali kukusanya mapato 'Kodi ya majengo' kutokana na wananchi kujijengea makazi holela bila kupata vibali vya ujenzi, baada ya kuuziana maeneo kienyeji bila kupimwa na kupatiwa hati, jambo ambalo kwa sasa linafanyiwa kazi kwa kasi na baadhi ya makampuni binafsi ikiwamo ya Property International, yanayoshirikiana na Selikali katika kifanya kazi hiyo.

Makonda alimpongeza Waziri William Lukuvi, kwa kazi ngumu anayofanya ikiwa ni pamoja na ya ulasimishaji wa makazi ili kwenda na viwango vinavyotakiwa kwa ajili ya kuzitambua nyumba na kuzipa madaraja tofauti kurahisisha upatikanaji wa kodi ya majengo, na mpangilio wa miji unaotakiwa huku Serikali ikiendelea kuwakaribisha wapimaji biasfi ili kuendana na kasi.

''Wapimaji binafsi watasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa Watumishi na Vifaa vya kisasa vinavyorahisisha upimaji wa haraka na kwa wakati, lakini Manispaa zinatakiwa kuwapa ushirikiano makampuni hayo kwa kuwapa na kuwatambua ili Serikali inapotoa Hati isitokee mgongano kutokana na maeneo husika kupimwa na watu watatu tofauti''. alisema

Akiongelea kuhusu Makampuni binafsi yanayotambulika na kuisaidia Serikali kufanya kazi ya Upimaji, aliitaja Kampuni ya Property International, ambayo ina jumla ya Viwanja 240 vya Viwanda huko eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambapo anayehitaji Heka hata 500 hadi 1000 anaweza kupata ambavyo tayari vimepimwa na zaidi ya Viwanja 800 vya Makazi na Biashara vilivyopimwa katika mradi huo.

Akizungumza na Mtandao huu, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Property International, Haleem Zahran , alisema kuwa Kampuni imefarijika sana .

baada ya kusikia taarifa za serikali kutambua mchango na juhudi zinazofanywa na kampuni yake katika kufanya kazi kubwa ya kuhamasisha suala la kupanga na kupima Viwanja katika maeneo mbalimbali ili wananchi kuweza kupata makazi yaliyo salama.

Hata hivyo alimpongeza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda na Waziri Lukuvi kwa kazi kubwa wanavyofanya katika Sekta hiyo ili kuendana na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo baada ya muda kila mwananchi atakuwa akiishi katika eneo linalotambulika na kupunguza migogolo ya ardhi.

‘’Kama kampuni bado tuna mikakati mikubwa ya kuendelea kuongeza mashine za kisasa za kurahisisha upimaji wa maeneo kwa haraka na uhakika''. Alisema Haleem

Aidha alisema kuwa Kampuni yake inaendelea na juhudi za kuiunga mkono Serikali na kwamba haitalewa sifa kwa kutambulika huko bali itaongeza jitihada na kupambana ili kuhakikisha inaisadia Serikali kupanga na kupima maeneo mbalimbali.

RIPOTI: HOTELI ZA NYOTA MBILI NA TATU HUPENDELEWA ZAIDI NA WATEJA

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Je ushawahi kupanga kwamba unataka kwenda kulala kwenye hoteli ya nyota ngapi? Ni vigezo gani ambavyo huwa unavitumia kutambua kwamba hoteli hiyo hadhi yake ni nyota fulani? Ni vigezo gani huja kwanza akilini pindi unapofanya uchaguzi wa hoteli hiyo? Ni maswali magumu ambayo mtu wa kawaida hawezi kuyajibu labda awe anajihusisha au kufanya kazi kwenye sekta ya hoteli au mtu anayesafiri mara kwa mara.

Mara nyingi linapokuja suala la kuchagua hoteli ya kwenda miongoni mwa vitu vinavyopewa kipaumbele ni pamoja na kiwango cha huduma za hoteli husika, miundombinu, vyumba, mahali ilipo na gharama.

Suala la kuzipa hoteli hadhi ya nyota fulani limekuwa likizua mijadala kwenye nchi tofauti kutokana na changamoto ya vigezo vinavyotumika kufanikisha zoezi hilo kutofautiana kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kwa mfano hoteli ya nyota nne kwa nchini Tanzania inaweza kuwa ni ya nyota mbili huko Misri kutegemea vigezo vilivyotumika. Katika kujaribu kutatua changamoto hiyo nchi nyingi duniani zimeunda mamlaka maalum kusimamia zoezi hilo ambapo mara nyingi huwa ni serikali au taasisi.

Hivi karibuni kampuni inayojihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika, Jumia Travel ilizindua ripoti ya Utalii mwaka 2017 ambapo ndani yake imebainisha kuwa kati ya hoteli zenye nyota moja mpaka tano watanzania wengi wanapendelea zaidi za nyota mbili (41%) na tatu (39%).

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa maeneo yanayotembelewa zaidi pamoja na gharama za hoteli zake ni Zanzibar (30%) ambapo chumba huanzia USD 134, Dar es Salaam (26%) gharama ni kuanzia USD 100, Arusha (10%) gharama ni kuanzia USD 50, Mwanza (4%) gharama ni kuanzia USD 34, Bagamoyo (3%) gharama ni kuanzia USD 58, Mbeya (2.5%) gharama ni kuanzia USD 24, Moshi (2%) gharama ni kuanzia USD 42 na Dodoma (1.5%) gharama ni kuanzia USD 23.

Intaneti imekuja kubadili mfumo mzima wa namna biashara na huduma mbalimbali zinazovyotolewa siku za hivi karibuni. Baadhi ya faida zake ni pamoja na kuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara kuwafikia na kuwakutanisha na wateja tofauti ndani ya muda mfupi, kujitangaza kwa gharama nafuu pamoja na kurahisisha namna ya upatikanaji wa huduma zao.




Jumia Travel katika ripoti yake hiyo kwa kutumia mtandao wake mpana wa hoteli takribani 1300 nchini Tanzania, zaidi ya 30,000 barani Afrika na zaidi ya 300,000 duniani kote, imekuwa ikihamasisha na kupendekeza mifumo rahisi kwa wamiliki na mameneja wa hoteli inayowawezesha kufanya shughuli zao muda na mahali popote walipo sio lazima mpaka wawe kwenye vituo vyao vya kazi.

Mfumo huo ambao unaitwa Extranet husaidia kupokea huduma kutoka kwa wateja, kukubali au kukataa, kupata maoni na pia kutambua wateja wao ni watu wa aina gani na wanapendelea huduma zipi zaidi kwenye hoteli wanazozitembelea. Hivyo huwa inawarahisishia kwenye kufanya maboresho kwenye maeneo ambayo wateja hawapendelei pamoja na kuongeza huduma ambazo wateja wanazipendelea lakini hawakuzipata.

Vivyo hivyo kwa upande wa wateja ambao hapo awali iliwabidi kwenda moja kwa moja hoteli au kutembelea tovuti moja baada ya nyingine kutafuta huduma sasa wamewezeshwa kufanya huduma za hoteli tofauti sehemu moja. Hivi sasa wanayo fursa kubwa ya kufanya huduma ya hoteli ndani ya muda mfupi mtandaoni kama vile kuchagua hoteli, mahali ilipo, aina ya chumba, bei, upatikanaji wake na namna ya kufanya malipo.

Ripoti hiyo iliangazia pia mchango wa sekta utalii nchini kwenye pato la taifa ambapo takwimu zinaonyesha kwamba 72.4% ya mapato hutokana na matumizi ya wageni wanaotoka nje ya nchi huku 27.6% hutokana na ya watalii wa ndani. Kwa kuongezea, 85.5% ya matumizi hayo ni kwa ajili ya kustarehe au kutalii huku 14.5% ni kibiashara.

Tamasha la Castle Lite Unlocks Iilivyofanyika Leaders, Dar Jumamosi hii

$
0
0
Angalia Full Video ya Show Hiyo.

 Cassper Nyovest kutoka Afrika Kusini akitoa burudani wakati wa tamasha la Castle Lite Unlocks limefanyika katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam Julai 23, 2017 ambapo kubwa zaidi ameshuhudiwa rapper Future kutoka Marekani na Cassper Nyovest wa Afrika Kusini wakitumbuiza kwa mara ya kwanza hapa nchini.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
 Rapper Future kutoka Marekani akitoa burudani.
 Vanessa Mdee. 
 Mashabiki.
 Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kupanda jukwaani.
 Cassper Nyovest kutoka Afrika Kusini akizungumza.
 Navy Kenzo 
Rapper Future kutoka Marekani  akikabidhiwa zawadi ya picha.

BARABARA YA MPEMBA/ISONGOLE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto) wakisalimiana na wanakwaya baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye stendi ya mabasi ya Ileje mkoani Songwe, Julai 22 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Ileje kwamba Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mpemba-Isongole.

Amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 58 ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwani itafungua fursa za kiuchumi na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Julai 22, 2017) alipozungumza na wananchi wa wilaya ya Ileje kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Stendi.

Waziri Mkuu alisema barabara hiyo itawawezesha wananchi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe, ambao wana mazao mengi kuyafikia masoko kwa urahisi.

“Ujenzi wa barabara hiyo utaongeza fursa za kiuchumi katika Wilaya ya Ileje, hasa kufungua biashara za mipakani kati ya nchi ya Tanzania na Malawi.”Alisema Serikali imedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto mbalimbali hasa miundombinu ya barabara, hivyo aliwaomba waendelee kuiamini na kushirikiana nayo.

Awali Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Joseph Mkude alisema kiasi cha fedha kinachotolewa kwa matengenezo ya barabara hakitoshi ukilinganisha na ubovu wa barabara zao.

Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa wilaya aliiomba Serikali kuipa kipaumbele miradi ya ujenzi wa barabara iliyo kwenye ukanda wa mvua nyingi ili zipitike wakati wote.Pia alisema wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo la uharibifu wa barabara unaofanywa na wananchi wasio waadilifu, hivyo kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.

Hata hivyo alisema kwa sasa wanatoa elimu ya utunzaji na ulinzi wa miundombinu ya barabara kwa wananchi ili kupunguza gharama za matengenezo ya kila mara.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 23, 2017

MSANII FUTURE KUTOKA MAREKANI NA DIAMOND PLATINUM WA TANZANIA WAACHA GUMZO KATIKA TAMASHA LA CASTLE LITE UNLOCKS JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
MSANII wa muziki wa Hip Hop ambae pia ni mtunzi na mtayarishaji wa muziki mahiri wa nchini Marekani, Nayvadius DeMun Wilburn maarufu kama Future akifanya shoo katika tamasha la Castle Lite Unlocks iliyofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Julai 23, 2017. PICHA ZOTE NA KAJUNASON BLOG/MMG/CATHBERT KAJUNA.
Msanii wa Kizazi Kipya Vannessa Mdee akiwaburudisha katika tamasha la Castle Lite Unlocks lililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Vijana waliojitokeza katika tamasha la Castle Lite Unlocks lililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Kila mmoja alikuwa na furaha.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz akiburudisha tamasha la Castle Lite Unlocks lililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Wapenda Burudani kutoka nchini Zambia na Kenya ambao walipata udhamini wa bia ya Castle Lite wakifurahi katika tamasha la Castle Lite Unlocks lililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Marafiki wanapokutana huwa wanashow love pamoja.
Nami pia mmilikiwa wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo Kajuna (kulia) ambaye nimekuletea picha hizi, nikiwakilisha na mdau Alex.
Pia Mmiliki wa Kajunason Blog, Cathbert Kajuna (kushoto) nikishow love na timu Zambia na Kenya walihudhuria tamasha la Castle Lite Unlocks lililofanyika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Jimbo la Tungu Mhe Simai Mohammed na Mbunge wa Jimbo Hilo Mhe Khalifa Salum Washiriki Ujenzi wa Soko la Samaki Katika Kijiji cha Tindini

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe Khalafa Salum Suleima wakishiriki katika ujenzi wa Taifa wa kujenga Soko la Samaki katika ufukwe wa pwani ya Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja, wakikata majengo ya kuezekea bati katika soko hilo. Pia wamekabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi huo ili kutowa mazingira mazuri ya Soko hilo wakati wa kufanya mnada wa samaki kwa wavuvi wanaporudi baharini kuvua.
Wananchi wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakishirikiana na Mbunge wao na Mwakilishi katika ujenzi wa Taifa wa Soko la Samaki katika ufukwe wa Bahari ya Unguja Ukuu Zanzibar.
Mbunge nas Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said ma Mhe Khalifa Salum Suleiman wakikabidhi mabati kwa Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bi. Sauda Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ya Mabati hayo na miti yamefanyika katika viwanja vya Soko hilo Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja Mkoa wa Kusini.
Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao.. 
Wananchi wa Kijiji cha Tindini wakishiriki katika ujenzi wa Soko la Samaki Tindini likiwa katika hatua ya kuezeka.na kuhudumiwa wananchi wavuvi wa kijiji hicho kuuzia samaki wao
Kiongozi wa Kijiji cha Tindini akitowa maelezo ya ujenzi wa Soko hilo la Samaki katika ufukwe wa bahari yao litakalotowa huduma ya kuuzia samaki kwa wavuvi katika soko la mnada. 
Mwakilishi wa Jimbo las Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Soko la Samaki katika kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitumia soko hilo kwa shughuli zao za biashara ya samaki na minada kwa wavuvi wanaorudi bahari kuvua.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akisisitiza jambo wakati wa hafla hiyo kwa Wananchi wa Jimbo lake. 
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Bi Sauda Ramadhani akizungumza wakati wa hafla hiyo ujenzi wa taifa na kukabidhi mabati na vifaa vya ujenzi wa Soko la Samaki katika Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu Wilaya ya Kati Unguja.
Wananchi na wavuvi wa kijiji cha Tindini Unguja Ukuu wakimsikiliza mgeni rasmin wakati wa hafla hiyo ya ujenzi wa Taifa na kukabidhi mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Soko hilo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge na Mwakilishi na Wananchi wa Kijiji cha Tindini Unguja Ukuu baada yas hafla hiyo.
Imetayarishwa na Othman Mapara.Blogspots.com
Zanzinewes.com.
Email.othmanmaulid@gmail.com 

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NGURUKA WILAYANI UVINZA MKOANI KIGOMA AKIWA NJIANI KUELEKEA MKOANI TABORA KWA ZIARA YA KISERIKALI

$
0
0
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli mapema asubuhi ya tarehe 23 Julai 2017 akihutubia wananchi wa kijiji cha LUCHUGI-UVINZA Mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea Mkoani Tabora Kuanza Ziara ya Kiserikali Mkoani Humo Julai 23,2917.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo akiwa kwenye mikutano yake mbalimbali ya njiani aliyosimma uili kuzungumza na wananchi wa vijiji vya mkoa wa Kigoma akielekea Mkoani Tabora kuanza Ziara ya KIserikali Mkoani humo, Julai 23,2017.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo akiwa kwenye mikutano yake mbalimbali ya njiani aliyosimma uili kuzungumza na wananchi wa vijiji vya mkoa wa Kigoma akielekea Mkoani Tabora kuanza Ziara ya KIserikali Mkoani humo, Julai 23,2017.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza mwenyekiti wa kijijji cha Uvinza Ndugu Nilisi Noa Ntabai alipokuwa akieleza kero ya maji ya eneo hilo la uvinza ikiwemo kusimama kwa kiwanda cha chumvi Uvinza ambacho kilikuwa tegemeo kwa wananchi wa eneo hilo,ambapo Mhe,Rais amewaahidi wananchi hao kumtuma Waziri wa Viwanda na Biashara kushughulikia tatizo hilo. Julai 23,2017.


Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikagua tanki la kuhifadhia maji toka mto Maragarasi kabla ya kuweka jiwe la msingi la maradi huo utakao hudumia waananchi wa Nguruka Uvinza mkoani Kigoma,kushoto kwa Mhe Rais ni Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa ameambatana na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge wakishuka ngazi mara baada ya Mh,Rais Kukagua Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia Maji kwaajili ya Wananchi wa Nguruka kabla ya kuhutubia wananchi. Julai 23,2017.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge mara bada ya kuweka jiwe la msingi la maradi wa maji Nguruka. Julai 23,2017.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wananchi wa Nguruka Uvinza Mkoani Kigoma,wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia Maji kwaajili ya Wananchi wa Nguruka. Julai 23,2017.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia Mamia ya Wananchi wa Nguruka Uvinza Mkoani Kigoma mara baada ya kuhitimisha kuwahutubia wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia Maji kwaajili ya Wananchi wa Nguruka Julai 23,2017.
Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia Mamia ya Wananchi wa Nguruka Uvinza Mkoani Kigoma mara baada ya kuhitimisha kuwahutubia wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia Maji kwaajili ya Wananchi wa Nguruka Julai 23,2017.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI DED WA MBOZI KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, Bw. Eliseyi Mgoyi pamoja na maofisa wengine watatu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma. 
 Pia amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Songwe, Bw. Damian Sutta kuwakamata na kuanza kuwachunguza haraka maofisa hao na kisha ampelekee taarifa ofisini kwake. 
 Waziri Mkuu amewasimamisha kazi maofisa hao leo (Jumapili, Julai 23, 2017) wakati alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Vwawa, akiwa katika ziara ya mkoa wa Songwe.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa  Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wa wilaya ya Mbozi kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vwawa wilayani Mbozi Julai 23, 2017. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa  Wapili  kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Limdi, Erasto Zambi
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe nje kidogo ya mji wa Vwawa mkoani Songwe Julai 23, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (kulia kwake) wakitazama Kimondo wakati walipotembelea Kituo cha Mambo ya Kale cha Mbozi mkoani Songwe
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwapungia wananchi wa wilaya ya Mbozi wakati walipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kyalele wilayani humo kuhutubia mkutano wa hadhara, Julai 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. 
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama nguo za batiki  wakati walipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wa Mbozi kabla ya  mkutano wa hadahara uliohutubia wa Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari ya Nalyelye wilayani Mbozi, Februari 23, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

SHAKA AMALIZA ZIARA YA KIKAZI WILAYA YA MAGU, ATUA WILANI UKEREWE

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akishiriki Kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mwamanga wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizindua shina la vijana wakereketwa wa CCM wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka,(kulia) akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Mwamanga wilayani Magu
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, akizindua shina la vijana wakereketwa wa CCM wilayani Magu
Mwenyekiti wa UVCCM mkoani Mwanza Ruben Sixtus, akitoa salamu zake
kwenye ziara ya Katibu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali wa CCM wilayani Magu wakiwemo mabalozi, wanachama pamoja na viongozi wa jumuiya za CCM wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka, alipokuwa akizungumza nao kwenye ofisi za CCM wilayani humo
Kaimu Katibu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza wilayani Magu
Kaimu Katibu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akipokelewa wilayani Magu majira ya Usiku.picha zote na Fahadi siraji
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images