Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 129 | 130 | (Page 131) | 132 | 133 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

  NI jambo lisilowezekana hata kidogo kukaa wiki moja au mbili bila kuona tamko lolote kutoka kinywani mwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

  Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliwahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha mwaka (2005-2010).

  Kiti cha sita baadaye kilikaliwa na Spika Anne Makinda, ambapo bila woga wala soni, Sitta aliwaambia wafuasi wake kuwa nafasi yake imehujumiwa kwasababu ya kuchukia ufisadi.  Waziri Sitta amesema hayo, akiamini kuwa mafisadi wamehujumu cheo chake kwa kisingizio cha jinsia. Yani mwanamke ashike nafasi hiyo ambayo yeye hakutaka iwe hivyo.

  Mengi amekuwa akisema, lakini anasahau kuwa hata yeye alipoingia katika nafasi hiyo mwaka 2005, ililazimika kumuondoa Spika Pius Msekwa, akiitwa ‘Agano la Kale’. Nani asiyejua utawala wa Sitta bungeni ulivyokuwa na mshike mshike mwingi kiasi cha kumlazimisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ajiuzulu nafasi hiyo mwaka 2008, akisema kuwa tatizo ni Uwaziri Mkuu.

  Nimekuwa nikifuatilia kwa kina maneno ya Sitta kila wakati, huku nikiamini kuwa mengi anayotoa, anayatumia kama mtaji wake kisiasa, akiwashughulikia wabaya wake kwa kisingizio cha kuuchukia ufisadi uliotuwama ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Sitta anapotembea magharibi na mashariki kupinga ufisadi wa viongozi wengine wa serikali inayoongozwa na chama chake, hakika kinachekesha watu walionuna.Ni kiongozi wa serikali kwa kupitia CCM anayoituhumu usiku na mchana bila kujua athari zinazoweza kukiangusha chama chao.

  Ni kutokana na hayo, naendelea kupekua huku na kule kuutafuta utukufu wa Sitta, ndani ya CCM na serikali kwa ujumla. Inawezekana wapo watu ambao ni wachafu, ila kwa ujasili huo huo anaousema mtaani, basi angeutumia kuwataja watu hao ama kupeleka ushahidi wake mahakamani ili tufanye kazi kivitendo zaidi badala ya porojo zisizokuwa na tija.
   
  Kwanini Sitta amekuwa akiidhalilisha CCM, japo mwenyewe kwa utashi wake anaamini unafurahisha baadhi yake? Usafi wa Sitta unatoka wapi? Haiwezekani. Hii ni kwasababu Sitta ni miongoni mwa watu wanaotumia fedha nyingi bungeni wakati Watanzania wengi wanaishi kwa kubangaiza.

  Sijamuona Sitta akipinga ulaji huo kwa wanasiasa ambao wengi wao wapo bungeni kulala, kupiga makofi, kufanyiana fitina na kusaini posho za vikao, wakati walimu, askari polisi, madaktari wanaofanya kazi ngumu ya kuokoa roho za watu wakiishi kwa mshahara mdogo.

  Watu hawa hawajui kesho yao itakuwaje na ndio maana tumeshuhudia walimu wengi wakishindwa kuhudhuria sehemu zao kazi kutokana na changamoto wanazokutana nazo. Akiwa kama Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ana fursa ya kuingia katika vikao mbalimbali vya Baraza la Mawaziri, ameridhika na kuingizwa kwa hoja ya kulipia simcard kwa Sh 1000 kwa mwezi.

  Mpango huu umekuwa mchungu kwa Tanzania kwa sasa, huku vyama vya siasa na viongozi mbalimbali wakipaza sauti zao, akiwamo Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, John Mnyika, Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wengineo kutoka chama tawala na upinzani. Sitta anajua kuwa vipo vijiji vingi vinavyostahili umeme lakini tangu nchi ipate uhuru havijawahi kupewa huduma hiyo muhimu na kila siku yamekuwa yakisemwa katika kila vikao vya Bunge?

  Je, anajua kuwa watoto wa wapiga kura wake kule Urambo wanasaga na rumba, wakivuja jasho, huku yeye akibaki mjini kutoa matamko ya kuwatusi au kuwadhalilisha viongozi wenzake?. Huu ni mgogoro gani kama kweli upo kati ya Sitta na viongozi wengine kutoka ndani ya serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete, moja ya viongozi wanaofanya kazi nzuri kiasi cha kuwafanya waje kukumbukwa usiku na mchana?

  Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli, alijiuzulu uwaziri mkuu wake huku akitoa lawama kwa baadhi ya watu waliokuwa wakitolea macho nafasi yake hiyo, kabla ya kuhusishwa na kashfa ya Kampuni tata ya kufua Umeme ya Richmond. Ndio hapo matamko mengi ya Sitta yanapoingizwa kwenye kejeli kwa Lowassa, hasa kwa hoja zake za ufisadi, akiamini zitakuwa mbeleko katika mchakato wake kisiasa.

  Labda hayo yanapamba moto kutokana na spidi ya Lowassa, mmoja wa watu wenye wingi wa watu wanaomuunga mkono. Kila pembe ya nchi anatajwa usiku na mchana. Ingawa si mjuzi wa vuta nikuvute ya machaguo ya urais hasa ndani ya CCM, ila ni ngumu mno kumfanya Lowassa ashindwe kwenye mchakato huo kama atahitaji nafasi hiyo mwaka 2015.

  Japo hajatangaza wazi juu ya adhma hiyo, lakini Lowassa anatajwa sambamba na wanachama wengine wa CCM, akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Sitta asiyelala kwa ajili ya kutangaza mabaya ya wenzake, bila kujua kuwa kauli zake ni kama bomu kwa chama chake. Ni kwasababu Watanzania wengi siku hizi tumezoea kuishi kwa kukariri. Ama tunaishi kwa mazoea. Kama hivyo sivyo, basi mmoja ajitokeze hadharani kumuuliza Sitta juu ya kukaa kwenye CCM ya mafisadi na wenye majungu?

  Kama Rais Kikwete alimuhujumu kwenye uspika, kwanini alikubali uwaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki? Nafasi ambayo ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wenzetu, hasa wale wanaofanya kazi ya kutoka nje ya mipaka yetu katika Bara hili wanaishi kwa kuhabatisha. Watanzania hao wakiwapo madereva wanaishi kwa manyanyaso ya aina yake, hasa nchi za Uganda, Rwanda, Malawi, Burundi, pale watu hao wanapotaka kuingia au kutoka.

  Ningetaka kuona utendaji kazi wa Sitta juu ya manyanyaso ya Watanzania hao kwa kuimarisha ushirikiano kama cheo chake kinavyosema, badala ya kuikandamiza CCM miaka nenda rudi. Ndio, Sitta ametangaza kung’atuka katika ubunge ifikapo mwaka 2015, ila sitaki kuamini kuwa hana ndoto za kuona chama chake kinaendelea kuwa lulu ya Watanzania wote.

  Ama Sitta anataka CCM ife? Najua Sitta ni miongoni mwa wanasiasa makini, ila si sahihi kuendelea na malumbano yasiyokijenga chama chake, akiamini ndio njia ya kuwasulubu wabaya wake. Tunahitaji kauli thabiti na utendaji kazi uliotukuka kutoka katika kinywa cha Sitta. Endapo anaona chama kinakwenda ndivyo sivyo, basi awe wa kwanza yeye kusimama hadharani na kukemea na sio kubaki nusu kuzimu na nusu peponi.

  Nayasema haya nikiamini Sitta ataona jambo jema la kufanya kwa ajili ya Tanzania. Hatuhitaji tena kupoteza muda. Tunahitaji vitendo, maana siasa zisizokuwa na tija ndio zilizotufikisha hapa. Kuna mengi ya kufanya kwa ajili ya kufanikisha maisha bora kwa kila Mtanzania.

  Mnyukano unaofanywa na Sitta dhidi ya serikali yake una faida gani? Anajenga au anabomoa? Sitta ana mapenzi na CCM au lengo lake ni chama hicho kutoweka katika historia ya Taifa letu?

  Waswahili wanaamini kuwa mwanamke anayetumia muda wake mwingi kuunadi upungufu wa mume wake basi huyo si muungwana. Hana sifa stahili za kuwa mke wa ndoa.Huyo ana lake jambo. Ama ameingia katika ndoa hiyo kwa ajili ya kuondoa mkosi au pia kuna kitu amefuata hapo, hasa maslahi.

  Hili si tusi kwake, maana aliwahi kuitoa dhidi ya Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, akisema kuwa mara nyingi yanayojiri baada ya ndoa huwa hayaonekanai kwenye uchumba.
  Haya Sitta anayajua. Mnyukano wao kisiasa waufanye ndani ya vikao halali vya chama, ili apate nafasi ya kuwatumikia Watanzania.

  Huo ndio ukweli wa mambo. Japo kuusema kunahitaji moyo, ukizingatia kuwa hali ya siasa ilivyokuwa sasa, imeongeza joto na kuzalisha makundi ya kutisha.Hao ndio wanaopita huku wakituhumu upande mwingine, huku hoja ya ufisadi ikitumika tofauti kwa kila mtu asiyekubaliana naye.

  Hatuwezi kwenda hivyo. Tujaribu kuwa waungwana, maana maneno mengi yanayotolewa katika jamii yamekuwa hayana tija. Tunatumia vibaya nafasi zetu na kuwapotezea muda wao bure, huku tukijua fika ugumu wa maisha wanaokutana nao mtaani kwao.

  Tutumie fursa zetu vizuri kwa ajili ya maisha ya Watanzania kwa kuhakikisha kuwa rasilimali watu, rasilimali fedha na maliasili zote kwa Taifa zinanufaisha watu wote. Hata iweje, bado siwezi kumtofautisha mbunge yoyote ndani ya CCM au Waziri, hasa wale wanaotumia muda mwingi kutusi wenzao ili waonekane wapo sahihi.

  Watu watajiuliza na baadaye kupata majibu sahihi, hasa kwa kukiwajibisha chama tawala CCM. Ama hajui kuwa maneno yanaumba na wapo watakaofuata ushauri wake, matusi yake dhidi ya viongozi wenzake na chama kwa ujumla, wakati siku zote tunaambiwa samaki mmoja akioza ni wote?

  Je, huo utukufu wa Sitta utaendelea kubaki mioyoni mwa Watanzania hata kama muda wake mwingi aliutumia kumtusi Kikwete, Lowassa na wengine anaopingana nao?

  0 0

  Mpigapicha wa New Habari Anthony Siyame akidhalilishwa na askari wa Idara ya Usalama wa Taifa wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa Thailand, Yungluck Shinawatra baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam  jana,Julai 30 2013.
  (Picha kwa hisani ya Selemani Mpochi) .
   
  Cha ajabu ni kwamba wakati mpigapicha huyo akifanyiwa visa na kushindwa kufanya kazi yake kwa utulivu wanahabari wengine wa kigeni walipewa ushirikiano mzuri na kufanya kazi yao bila bughuza  kabisa.

  0 0

    Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (kulia), akichukua futari katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mjini Zanzibar jana. 
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji  wa Benki ya NBC, Bi. Mizinga Melu katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Kushoto ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe. 
   Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  wa Zanzibar, Zahra Ali Hamadi (kulia), Katibu Mkuu katika wizara hiyo, Mwanaidi Saleh  Abdallah (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) wakichukua mlo wa futari iliyondaliwa na benki hiyo mjini Zanzibar jana.
    Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akilakiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na NBC Kwa wateja wake mjini Zanzibar jana. Katikati ni Meneja Mkuu Kitengo cha Uhusiano cha benki hiyo, William Kallaghe.
    Mjumbe wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Kassim Hussein (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Khamis baada ya hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao mjini Zanzibar jana. Nyuma ya Dk Kassim ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Mizinga Melu.
   Baadhi ya waalikwa katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Kisiwani Zanzibar jana.
   Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto), akiwa na Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NBC, Dk Mussa Assad (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji NBC, Mizinga Melu katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibar jana.


  0 0
  0 0

   Msanii wa muziki wa asili Tanzania ambaye pia ni msanii wa maigizo na filamu, Mrisho Mpoto akizungumza jambo mbele ya waaandishi wa habari na wamiliki wa blogs mbalimbali katika uzinduzi wa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii. Mrisho alisimama kuzungumza dakika chache baada ya wimbo alioimba na Banana Zoro kuzinduliwa, unaojulikana kama 'Futa, Delete Kabisa'. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),John Nkomo katika uzinduzi huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkomo, akizungumza mbele ya wamiliki wa blogs mbalimbali Tanzania, waandishi wa habari katika warsha ya kampeni ya kuzindua matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuhamasisha suala zima la maendeleo.

   Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), waandishi mbalimbali wa habari pamoja na wamiliki wa mitandao ya kijamii, Blogs, wakisikiliza maneno mazuri kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Tanzania, Profesa John Nkomo, hayupo pichani. Hii ni sehemu maalumu ya kuonyesha kuwa TCRA wanatambua mchango wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na wamiliki wao kwa ujumla.
  Afisa Uhusiano wa TCRA,Innocent Mungi akiwakaribisha wadau mbalimbali wa mambo ya habari za kwenye mitandao,kuhusiana na uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi mazuri ya Mitandao ya Mawasiliano,Warsha hiyo imefanyika leo Makao makuu ya Ofisi hizo,zilizopo barabara ya Sam Nujoma jijini Dar.
   Wadau wa mawasiliano wa mitandao ya kijamii, blogs, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa na viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA katika uzinduzi wao wa matumizi mazuri ya mitandao kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya Taifa.

  0 0

   Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa (kulia) akizungumza na waumini wa kiislam (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa wa Benki ya Azania jijini Dar es Salaam juzi yenye lengo la kuimarisha mahusiano baina ya benki hiyo na wateja wake katika msimu huu wa Ramadhan. Kushoto ni Afisa Mkuu Maendeleo ya Biashaara wa Benki ya Azania, Bw. Othman Jibrea.
   Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa (kulia) akishiriki kwenye hafla ya kufuturisha wateja wa kiislam wa Benki ya Azania ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya benki hiyo na wateja wake katika msimu huu wa Ramadhan
   Baadhi ya wateja wa Benki ya Azania wakishiriki katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya benki hiyo na wateja wake katika msimu huu wa Ramadhan. Picha na mpiga picha wetu.
   Watoto nao walipata nafasi ya kujumuika kwenye hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na Benki ya Azania ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya benki hiyo na wateja wake katika msimu huu wa Ramadhan. 
   Afisa Mkuu Maendeleo ya Biashaara wa Benki ya Azania, Othman Jibrea akitoa machache wakati wa hafla hiyo.
   Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Benki ya Azania Bernard Haule (kushoto) akiwakaribisha wateja wa benki hiyo kwenye hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki yake jana ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya benki hiyo na wateja wake katika msimu huu wa Ramadhan. Kushoto ni Afisa Mkuu Maendeleo ya Biashaara wa Benki ya Azania, Othman Jibrea. 
  Baadhi ya wateja wa Benki ya Azania wakishiriki katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya benki hiyo na wateja wake katika msimu huu wa Ramadhan. 

  0 0

  Mhe Pereira Silima Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa Usalama Barabarani leo amezungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara na kutoa taarifa ya maadhimisho ya Kitaifa ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Mkoani Mwanza 23/09/13 - 27/09/13. 
  ======  =======  =======  0 0


   Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake baada ya kumtwanga  Ekkalak Saenchan  wa Thailand kwa KO raundi ya kwanza  PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com.
  Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa akimsukumia makonde mazito mfululizi bondia Ekkalak Saenchan  wa Thailand na kufanikiwa kumtwanga kwa kwa KO raundi ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita picha kwa niaba ya Mtandao wa SUPER D.
  Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia akimsikilizia mpinzani wake baada ya kumtwanga kumi nzito na kuhesabilwa wakati wa mpambano wake ata hivyo mpinzani wake akuendelea na kufanikiwa kupata ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza

  0 0

  Bagamoyo 2

  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid na Balozi wa Italia nchini Pierluigi Velardi wakizindua maabara ya kisasa kwenye majengo ya Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) huko Bagamoyo hivi karibuni. Maabara hiyo ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inajulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3, na ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI).
  Bagamoyo 1
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr Seif Rashid hivi karibuni amezindua maabara ya kisasa kabisa ambayo ina uwezo wa kutambua magonjwa mapya na yale ya hatari sana ikiwemo Ebola bila kuhatarisha maisha ya watafiti inayojulikana kitaalamu kama Biosafety Lab 3 ambayo ni ya kwanza ya aina yake katika eneo la Afrika Mashariki na Kati. Maabara hiyo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2 imejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Italia na inasimamiwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) kwenye maabara zake za Bagamoyo. Pichani anaonekana Mratibu wa mradi wa maabara hiyo Bw.Francesco Vairo akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afyya (wa pili kushoto), Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani ( WHO) Dr. Rufaro Chatora na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi wakiwa ndani ya maabara hiyo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF) Phares Magesa leo asubuhi akiongea na wapenzi wa michezo kupitia Radio kuhusu maendeleo ya Mchezo huo nchini ikiwemo ziara ya mchezaji Nyota wa NBA Steve Curry ambae ataendesha clinic ya vijana wadogo 100 tarehe 1 Aug, viwanja vya Don Bosco Oysterbay, wote mnakaribishwa.

  0 0

  Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar    

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa ruhusa ya kuendelea kwa ujenzi wa Jengo jipya la Abiria katika Uwanja wa ndege wa  Zanzibar lililosita kwa muda baada ya kuonekana kasoro za kiufundi zilizojitokeza hapo awali katika jengo hilo.

  Hayo yameelezwa leo huko Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar na  Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif  Suleiman wakati  alipokuwa akiwasilisha Bajeti yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo.

  Amesema katika kutekeleza hilo ujenzi huo umeanza mara baada kukamilika kwa taratibu za Michoro mipya kwa baadhi ya sehemu za jengo baada ya kupata Mshauri elekezi kutoka Nchini Ufaransa.

  “Mnamo mwezi wa Machi mwaka huu tulimpata mshauri elekezi na kuaza kazi mwezi April na kutoa ripoti yake mwezi juni mwaka huu ambavyo ilionesha namna ya kasoro zilivyojitokeza na kuweza kutatuliwa haraka ipasavyo .”alisema Waziri Rashid Seif.

  Aidha alifahamisha kuwa baada ya matokeo ya Ripoti hiyo mpya ya michoro Serikali ilifuatilia suala hilo kwa kuwasiliana na Benk ya Exim ya China na kuwasilisha ombi la kuongezewa muda wa mkopo ambapo ungefikia ukingoni tarehe 31 Julai mwaka huu.

  Amesema hali hiyo ilifanikiwa pamoja na kuiomba Serikali ya Mapinduzi  pesa za ziada ya mkopo ili kugharamia ongezeko  linalotokana na kubadilika kwa baadhi ya michoro ya jengo hilo na mazingira iliyo lizunguka .

  Waziri Rashid ameongeza kuwa ujenzi wa Uwanja huo unaendelea chini ya Mkandarasi yule yule wa kampuni ya Beijing Construction Engineering Group ya China chini ya usimamizi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mshauri Muelekezi kutoka kampuni ya ADPI ya Ufaransa.

  Kwa upande wake Kamati ya Miundonbinu na Mawasiliano imependekeza kufanyiwa Marekebisho Makubwa Barabara zilizochakaa katika maeneo ya Unguja na Pemba.

  Aidha Wamependekeza Bandari ya Mkoani Pemba kupewa kipaumbele cha pekee kwa kufanyiwa marekebisho ya haraka kutokana eneo lake kudidimia.

  Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imeliomba Baraza kuidhinisha jumla ya shl. Bilioni 20.092 ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza majukumu yake iliyojipangia kwa mwaka wa Fedha 2013/2014

  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   
  Siku za hivi karibuni, ongezeko la huduma za mawasiliano nchini limekuwa kwa kasi sana. Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi kifupi zimekuwa sana na kuwafikia Watanzania wengi zaidi. Kutoka laini za simu za mkononi  milioni tatu tu mwaka 2000 hadi kufikia laini 28,000,000.  

  Watanzania walio wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, yakiwemo mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji. Vile vile huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi zimeongezeka maradufu. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.

  Hali kadhalika kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi kutoka watumiaji laki tatu miaka mitatu iliyopita hadi watumiaji milioni 7.6 kwa takwimu za hivi karibuni. Wengi wa watumiaji wa intaneti matumizi yao ni katika kujifunza na kujielimisha pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali zinazotoa habari mbalimbali zikiwemo za kimaendeleo, burudani pamoja na michezo.

  Matumizi haya ya intaneti yamewanufaisha watanzaia walio wengi kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.

  Hata hivyo pamoja na maendeleo haya, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo vurugu, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.

  Leo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inazindua kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya mawasiliano na inawatahadharisha wananchi kwamba kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010 ni makosa. Katika kampeni hii, Mamlaka inakusudia kuwasihi wananchi kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri ili kudumisha amani, mshikamano na upendo miongoni mwa watanzania.
   Katika uzinduzi huu, Mamlaka imewaalika baadhi ya watumiaji mahiri wa mitandao ya kijamii ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania walio wengi wanafaidika na mawasiliano. Miongoni mwao wako wamiliki wa blog mbalimbali, wasimamizi wa makundi mbalimbali katika mtandao wa FB na mengineyo. Nia ya Mamlaka ni kuomba ushirikiano kwao ili waweze kushiriki katika kampeni hii na kuwahamasisha mashabiki wao kutumia vizuri mitandao ya kijamii ili kunufaisha Taifa letu kwa matumizi mazuri.
   Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wote wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha kampeni hii kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta ya Mawasiliano inaendelea kuchangia uchumi wa Taifa na kuiweka Tanzania katika mazingira mazuri zaidi kijamii, kiuchumi na kisiasa.

  Tunawasihi wananchi na watumiaji wa huduma za mawasiliano kuwa wakipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.

  Pichani Juu: Mkurugenzi wa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, John Nkomo, akiongea na baadhi ya Wanahabari mapema leo asubuhi, jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizindua rasmi uzio wa ukuta katika kituo cha kulelea watoto yatima St. Martin De Pores Katandala Mkoani Rukwa leo. Uzio huo ambao ni msaada wa wahisani kutoka Marekani pamoja na upanuzi wa jiko, nyumba ya kufulia nguo (Laundry), ununuzi wa mashine za kufulia nguo za watoto na ujenzi wa nyumba ya ng'ombe umegharimu fedha za kitanzania  shilingi milioni 190. Kushoto ni Baba Askofu Kiharuzi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga. 
  Baba Askofu Kiharuzi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga katikati akibariki tukio hilo. Geti linaloonekana ni sehem ya uzio wa huo uliojengwa kwa fedha za wahisani kutoka Marekani. Katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliendesha harambee fupi ya kuchangia kituo hicho ambapo jumla ya Tsh. 835, 000/ zilipatikana.  
    Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi zawadi ya batiki kwa Mama Ann Marie English pamoja na wahisani wengine sita kutoka Marekani ambao ni mmoja kati ya wahisani waliofadhili miradi hiyo mbalimbali katika kituo hicho cha St. Martin De Pores.   
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi Hati ya Pongezi kwa Mama Ann Marie English pamoja na wahisani wengine sita kutoka Marekani ambao ni mmoja kati ya wahisani waliofadhili miradi hiyo mbalimbali katika kituo hicho cha St. Martin De Pores. 
   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akikabidhi zawadi ya nembo ya bendera ya Taifa kwa Mwenyekiti wa jumuiya ya St. Martin Kids ya Marekani Mama Marry Lynne Cassleman na wahisani wengine sita kama kumbukumbu kwako kwa kufika Mkoani Rukwa. 
  Mwenyekiti wa jumuiya ya St. Martin Kids ya Marekani Mama Marry Lynne Cassleman akizungumza katika hafla hiyo. 
  Ndugu Michael Caraway ambaye ni mmoja ya wahisani hao kutoka Marekani akizungumza katika hafla hiyo. Kulia anaeonekana kichwa kwa nyuma ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya. 
   Ndugu Michael Caraway kulia aliomba kupiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. 
  Picha ya pamoja (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa "www.rukwareview.blogspot.com")

  0 0  0 0

  Pichani ni Mwili wa Mtu aliyekutwa katupwa katika Msitu wa Kibamba Hospitali na Makondeko Luguruni, ukiwa katika hali mbaya kutokana na kudhaniwa kuwepo kwa takribani siku 4 na zaidi, mpaka sasa hajatambulika kwa jina, kutokana na kuharibika. Kikosi cha Askari kwa kushirikiana na Mjumbe wa Nyumba kumi kumi, Serikali ya Mitaa, kwa pamoja wamekubaliana kuuzika Mwili huo Pale alipokutwa katelekezwa. Halii hiyo imesababisha hofu kwa wakazi wa Maeneo ya Kibamba, Mbezi na Vitogoji vya Jirani. hivyo wameitaka serikali kuongeza jitihada za Ulinzi ususani wakati wa Usiku katika Bonde la Makondeko kuelekea Kibamba Hospitali.(Picha Zote na Shaaban Mpalule).
   Baadhi ya wakazi wa Maeneo ya Kibamba na Makondeko, wakijaribu kutambua  Mwili huo ambao umekutwa Eneo alikokutwa katelekezwa, Bondeni kutoka katika Daraja la Kibamba Hospitali na Makondeko.
   Baadhi ya Askari wakiwa eneo la Tukio kwa Maziko na Uchunguzi.
  Baadhi ya wakazi wa Maeneo ya Kibamba na Makondeko, wakijaribu kutambua  Mwili huo ambao umekutwa Eneo alikokutwa katelekezwa, Bondeni kutoka katika Daraja la Kibamba Hospitali na Makondeko.


  0 0


  0 0

   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akifuturu pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk.Amani Kaborou,Katibu wa CCM Mkoa wa Kigoma Mohamed Nyawenga na Mbunge wa Manyovu Albert Obama.
   Baadhi ya Mabalozi wa nyumba kumi na wakazi wa Kigoma mjini wakifuturu leo 31Julai 2013 katika ofisi za CCM wilaya ya Kigoma Mjini.
   Baadhi ya Mabalozi na wakazi wa Kigoma mjini wakipata futari
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache baada ya kufuturu na Mabalozi wa nyumba 10 ambapo alisisitiza Watanzania kutunza amani waliokuwa nayo.
   Sheikh Mustafa Halfan Kiumbe akisema maneno machache kabla ya kumkaribisha Sheikh Mkuu wa Kigoma
   Katibu wa NEC itikadi na Uenezi akishiriki dua iliyoongozwa na Sheikh Hassan Idd Kiburwa leo baada ya kufuturu na mabalozi wa nyumba 10 wa Kigoma mjini.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya mabalozi wa nyumba 10 kutoka Kigoma mjini ambao alifuturu nao pamoja.
  Wajumbe wa kamati ya utekelezaji kutoka wilaya ya Kigoma mjini wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufturu .

  0 0

  Ms. Susan Muyang Tatah, CEO of the International African Festival Tübingen
  The International African Festival Tübingen 2013 will take place in Tübingen, Germany from8th to 11th August.

  It will feature Africa’s top bands including Ngoma Africa Band - a German based Tanzanian band, Susubilibi – a West African band, Osumare Band from Nigeria, Richard Amougou from Cameroon and Wamali Percussions from Senegal. David Presna from Haiti will also perform.

  The festival will also feature a huge market with more than 70 traders selling beautiful African artefacts, children’s programs, exotic African culinary and Gospel music.


  Business and social forums will provide guests with information on business opportunities in Africa.

  At least 10 African Ambassadors in Germany have confirmed their participation at the festival together with dignitaries from the city of Tübingen.

  For more information about the International African Festival Tübingen 2013, please visit:www.afrikafestival.net.


  0 0

  Kampuni ya Glitz Entertainment imeandaa Toto Party kwa ajili ya watoto wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake linayotarajiwa kufanyika katika Art Gallery iliyopo Mbezi Beach siku ya Iddi Mosi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muandaaji wa tamasha hilo, Deniss Ssebo alisema kuwa hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto, na wanatarajia kuanza kulipeleka na mikoani.

  Katika Tamasha hilo, watoto watapata nafasi ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama soka, kuogelea, kusaka hazina (Treasure hunt) na kujipaka rangi usoni (Face painting) na mengine mengi. Aidha watoto hao pia wataweza kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu.

  Mbali na watoto kucheza na kufurahi michezo mbalimbali pia wazazi wao watachuana katika mchezo wa kuvuta kamba ambapo washindi katika michezo hiyo watazawadiwa zawadi mbalimbali na viingilio ni Sh 3,000 kwa watoto na wakubwa Sh 7,000.

  0 0

    Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akipokea funguo za Bajaji mpya aliyojishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na tTgo kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga ambapo washindi wa wiki ya pili ya Promotion hiyo wamekabidhiwa zawadi  zao jana Jijini Dar es Salaam. 
   Mkazi wa Makumbusho Isabela Edwad Msemo akipokea funguo ya Bajaji akiwa mwenye furaha kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo, Wiliam Mpinga  mara baada ya kujishindia  kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili  wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam. 
   Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akishuka ndani ya bajaji yake aliyokabidhiwa na Tigo  baada ya kujishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo, kushoto ni  Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.

   Mkazi wa Mabibo Khalid Jafari Gomani akikagua Bajaji  mpya aliyojishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili ya wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.

older | 1 | .... | 129 | 130 | (Page 131) | 132 | 133 | .... | 1898 | newer