Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1307 | 1308 | (Page 1309) | 1310 | 1311 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0


   Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (kushoto)akisalimiana na Katibu wa CCM Wilaya ya UVINZA ndg Evarist Mkuluge alipopokelewa Katika kata ya Nguluka Wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma.
   Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (kushoto)akivalishwa Skafu
   Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka (katikati) akikaribishwa rasmi na gwaride la vijana wa Green Guard Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
   Shamrashamra za Vijana wa Boda boda katika mapokezi ya Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
   Shamra Shamra za wanachama wa Chama cha mapinduzi katika mapokezi ya Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka Mkoani kigoma kata ya Nguluka Wilayani Uvinza
   Katibu wa Chama cha mapinduzi Wilayani Uvinza akiwasilisha taarifa Utekelezaji pamoja na maendeleo ya uchaguzi wa Chama Wilayani Uvinza katika Ukumbi wa CCM NGULUKA
   Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha mapinduzi (UVCCM)mkoa wa kigoma ndg:Peter Joseph Msanjira akizungumza katika mkutano wa Ndani  uliofanyika katika ukumbi wa CCM NGULUKA.
  Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa CCM Wilaya ya Uvinza Mkoan Kigoma katika mkutano wa Ndani  uliofanyika katika ukumbi wa CCM NGULUKA.(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)


  0 0

  MSIMU wa tatu wa michuano ya BRAZUKA KIBENKI unaoshirikisha taasisi za kibenki katika michezo ya mpira wa miguu na kikapu unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.
  Katika msimu huu michuano hiyo itashirikisha timu 15 ambazo ni NMB (Mabingwa watetezi), DTB, Barclay’s, BancABC, Exim, Stanbic, BOA, UBA, Letshego, EcoBank, CRDB, BOT, Azania, TPB, Access na UBA.
  Mmoja wa maofisa wa benki ya Exim, Frank Rweyemamu ambaye pia ni mwanachama wa tawi la Simba Makini linalomiliki mtandao huu alivitaja viwanja vitakavyotumika kuwa ni Gymkhana na DonBosco.

  Martin Komba wa DTB (kulia) akimtoka
  Hezbo wa NMB katika pambano la jana
  “Michuano ya mwaka huu itafanyika katika viwanja vya Gymkhana kwa mpira wa miguu huku mechi za mpira wa kikapu zikitarajiwa kuchezwa katika uwanja wa DonBosco.” Alisema Rweyemamu.
  Jana kulikuwa na mchezo wa ngao ya hisani ambapo mabingwa watetezi NMB walikubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa DTB katika mchezo wa kuashiria kuanza kwa michuano hiyo.
  Bingwa wa msimu huu atakabidhiwa kikombe pamoja na medali.

  0 0


   Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart ikishirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),sambamba na Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,wanatarajia kuanzisha msako mkali kwa wale wote wanaofanya biashara ya uharamia wa kazi za Wasanii hapa nchini.

  Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,Mkurugenzi wa Msama Auction Mart,Alex Msama alisema kuwa tayari wameishapata kibali na kupewa baraka zote za kuifanya kazi hiyo,ya kuhakikisha wizi/uharamia wa kazi za Wasanii unapungua ama kufika kikomo kabisa.

  “Tayari tumepata kibali,hivyo Sisi kama kampuni tumejipanga vyema kukabiliana na hayo mapambano ya wizi wa kazi za Wasanii,tutakae mkuta anauza nyimbo za CD feki,ama anauza nyimbo za wasanii kwa kuziweka kwenye flash,kwenye simu sambamba na wale wote wanaomiliki kompyuta kwa kufanyia kazi hiyo ya kuuza nyimbo za wasanii kinyume cha sheria, tutawakamata popote pale walipo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria”alisema Msama.

  Amesema kuwa Wasanii wameibiwa vya kutosha,ifike mahali nao sasa wanufaike na jasho la kazi yao,na si kumnufaisha mtu mwingine,alisema na kuongeza kuwa Wasanii wamekuwa wakilalamika muda mrefu kuhusiana na hili jambo la kuibiwa kazi zao na kusambazwa hovyo hovyo bila utaratibu wa aina yoyote,wao kama kampuni watalibeba jukumu hilo huku wakiamini ushirikiano ndio jambo kubwa la kuifanikisha kazi hiyo  yenye changamoto kubwa.

  “Tunawaomba wasanii mbalimbali na Wadau wa sanaa ya Muziki,watuunge mkono ikiwemo na kutupa ushirikiano wa taarifa,zikihusu maeneo yoyote ambako uharamia wa kazi zao unafanyika,nasi tutachukua hatua za haraka na kuwakamata wahusika”alisema Msema.

  Msama alimaliza kuwa kuwapa tahadhari ya mapema kwa wale wote wanaouza kazi wasanii kinyume cha sheria,hasa katika vituo vya mabasi,nyumbani,kwenye Maduka ya biashara waache mara moja,wakipuuza wajue kabisa kiama chao kimefika.


  0 0  0 0

  Standard Chartered Bank’s Group Chief Information Officer, Dr. Michael Gorriz is expected to visit the Bank’s offices in Tanzania today.

  According to a statement issued by Standard Chartered Bank Tanzania Limited, during his visit Dr. Gorriz will meet with various internal and external stakeholders of the Bank in Tanzania with a view of exploring ways in which the Bank can further enhance its business and support economic growth in the country.

  Dr. Gorriz was appointed Group Chief Information Officer on 25 March 2015 and is responsible for the banking operations, systems development and technology infrastructure which underpin the Bank’s client services, and defines and implements the Bank’s digital and innovation agenda.

  His visit to Tanzania comes as the Bank commemorates its centenary anniversary since it first opened its doors in Tanzania in 1917. The visit is a continuation of key Group visits that have been taking place to mark the Bank’s historical milestone in Tanzania as well as further reiterate the Group’s commitment to Tanzania.

  Dr. Gorriz will be accompanied by Top Team Members of the Group’s Information Technology and Operations Segment. These include; Bhupendra Warathe, the Global Head of the Bank’s Operations, Venkatesh Rathnam, the Global Head of Business Operations covering the Bank’s Retail Banking, Wealth Management and Private Banking Segments, and Toby Blythen, the Chief Financial Officer for the Information Technology and Operations Segment.

  In March this year the Bank also hosted over thirty of its Top Management Team members from its Africa and Middle East Region. The delegation, the biggest ever to have visited the country at one go, was led by the Regional Chief Executive, Africa and Middle East, Sunil Kaushal. The members held business meetings with various Government Officials and members of the business community, as well as joined the staff in Tanzania to launch its centenary anniversary.

  Africa, and the Bank’s business in Tanzania, continue to be a key market for the Standard Chartered Group. The Group’s highly ranked officials, therefore, continue to visit Tanzania with a view of further understanding the business on the ground thereby offering the necessary support to enhance its banking solutions leading towards further enhancing the country’s economy.

  Standard Chartered Bank in Tanzania is known to have revolutionized Banking in Tanzania leveraging on its innovation in technology. The Bank introduced the country’s first Automated Teller Machine in 1997, the country’s first Visa Electron Debit card, and the country’s first Web Banking services for corporate clients.Last year in July, the Bank became the first to launch a unique biometric enabled Mobile App. which has now attracted more than ten thousand downloads.

  Dr. Gorriz, who is responsible for the Bank’s operations, systems development and technology infrastructure which underpin the Bank’s client services, has wide experience in the Technology field. Prior to joining Standard Chartered, Dr. Gorriz was the Vice President and Chief Information Officer at Daimler AG where he was globally responsible for strategy, planning and development of the Group’s IT systems, as well as the operation of its technical infrastructure.

  During his 14 years at Daimler, Dr. Gorriz progressed through specialist research and design roles in aerospace to general management roles.He is a physicist and engineer by background and obtained a PhD in Engineering.

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua jambo kwa viongozi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara alipokutana nao mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
  4
  Muonekano wa jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga ambalo limekamilika na ujenzi wake umesimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
  5
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua moja ya nyumba za watumishi eneo la Rubaga zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoani Shinyanga.
  6
  Muonekano wa jengo la Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambalo ujenzi wake unasimamiwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
  3
  Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoa wa Shinyanga Eng. Amosi Manyete akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, mfumo wa maji taka uliowekwa nje ya jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania, kanda ya Shinyanga iliyopo mkoani humo. Kushoto ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda hiyo Mhe. Jaji Richard Kibella.

  1
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Tellack, mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi.

  …………………………………………………………………
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), kuhakikisha ndani ya miezi sita wanakamilisha ujenzi wa nyumba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga.

  Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani humo wakati alipokagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala huo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa kuwapatia waheshimiwa majaji mahali pazuri pa kuishi ili waweze kutimiza wajibu wao wa kutenda haki kwa wananchi ipasavyo.

  “Hakikisheni mnakamilisha ujenzi wa nyumba hii haraka iwezekanavyo ili Mheshimiwa huyu apate mahali pazuri pa kuishi, kufanya hivi kutarahisisha majukumu yake na kufanikish utendaji wa kazi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Amesisitiza umuhimu wa Wakala huo kuongeza kasi katika miradi mbalimbali inayoendelea ya ujenzi wa nyumba za viongozi ili kuondoa adha ya kodi za pango kubwa zinazopotea kwa viongozi hao kupanga kwa watu binafsi.

  Naye, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga Mhe. Jaji Richard Kibella amemshukuru Prof. Mbarawa kwa niaba ya taasisi zake za TBA na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kwa namna ambavyo wameshirikiana na Mahakama kukamilisha ujenzi wa jengo hilo na kuwapatia huduma nyingine za uendeshaji.

  Aidha, ameiomba Serikali kukamilisha kwa haraka ujenzi wa nyumba za viongozi na watumishi wa mahakama kwani gharama kubwa zinatumika katika malipo ya upangaji wa nyumba za viongozi.

  “Mhe. Prof. Mbarawa suala la nyumba ni changamoto, nyumba za kupanga zina gharama kubwa ambapo kwa namna moja au nyingine inaongeza gharama za uendeshaji wa mahakama na kupunguza usalama”, amefafanua Jaji Kibella.

  Kwa upande wake Mtendaji wa Mahakama hiyo Bwana Ernest Masanja, amemueleza Prof. Mbarawa kuwa kukamilka kwa jengo la Mahakama hiyo kumewezesha Majaji na watendaji wengine wa mahakama kufanya kazi kwa bidii, ufanisi na kwa wakati katika kuwapatia wananchi haki.

  Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Mkoa huo unaosimamiwa na TBA na ameuelekeza Wakala huo kushirikiana na Mamlaka husika kuhakikisha kuwa ujenzi wake unazingatia viwango na ubora na kukamilika kwa wakati.

  0 0

    TSN Group Tanzania, katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, imeingia mkataba na MIMOSA CONCIERGE inayotoa MIMOSA Black Card ambayo ni kadi maalum kwa wateja wanaofika kupatiwa huduma kupitia kadi hizo. 

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusaini mkataba huo na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, leo Meneja Masoko wa TSN alisema, Jahu M. Kessy amesema TSN imelenga kuongeza tija katika kutoa huduma zake.
   “Tunarahisisha na kuboresha huduma zetu kuwa bora na za kisasa. Pengine huduma hii itapanua wigo wa wateja wetu watumiao Black Cards kwa Dar es salaam lakini kwa Mwanza TSN Hypermarket inakuwa kampuni ya kwanza kupokea na kukubali malipo kupitia Black card ya Mimosa. Hatua ambayo ni kubwa kuchukuliwa na TSN katika kuwajali wateja wake.”
   “Sasa ukifanya malipo kupitia kadi ya Mimosa kwenye supermarket zetu na Petrol station unajiweka katika nafasi ya kushinda punguzo la zaidi ya asilimia 5 pamoja na kuponi ya zawadi wa kwateja watakao tumia kiasi cha shillingi laki moja kwa manunuzi ya mara moja,” alisema Jahu. 

  Akieleza zaidi juu ya huduma na faida wazipatazo wateja watumiayo kadi hizo, Mkurugenzi Msiaidizi wa MIMOSA, Leonce Mongi alisema kupitia kadi hii Mteja wa TSN hatapata tu punguzo la bei kutoka TSN pekee lakini pia atapata offer mbalimbali zitokanazo na kadi hiyo kupitia discount partners wengine ambao ni zaidi ya watoa huduma 71 Nchi Nzima.  
   Jahu alisema TSN inajiimarisha katika kutoa huduma zake kwa wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia, hivyo basi kuona umuhimu wa kuwapatia wateja wake wenye MIMISA black card nafasi ya kufanya malipo yao kwa uhuru na furaha. 

  Alisema,”hatua hii inafuatia hatua nyinginezo nyingi tulizochukua kuhakikisha wateja wa TSN wanafurahia huduma zetu, ikiwemo malipo kutupitia miamala ya simu, bank cheques, malipo ya dola na sasa pia kupitia Mimosa Black Card. 
  Leonce alisema kupitia kadi hii TSN itakuwa ikipokea malipo na kuongezaa tija kwa mteja, lengo ni kuhakikisha mteja mwenye kadi ya Mimosa hashindwi kufanya malipo yake akiwepo katika vionga vyao, na pia kufurahia ofa na punguzo mbalimbali zipatikanazo na mtangamano huu. 

   “Teknolojia imeendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya jamii yetu kwa kurahisisha na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Kukua kwa teknolojia katika nyanja mbalimbali za kiuchumi kisiasa na kijamii kumeendelea kuleta matokeo chanya siku hadi siku. Sambamba na kurahisishwa kwa utendaji kazi lakini pia upokeaji wa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi wa kawaida kumerahisishwa.” Alisema Jahu.

  Katika kutambua fursa hiyo, TSN itaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi zinaenda sambamba na mabadiliko hayo ya teknolojia.

  Leonce aliipongeza TSN kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaweka urahisi kwa wateja wake na hiyo imekuwa ni chachu kubwa katika kurahisisha utoaji huduma kwa wateja wao.

  0 0

  Naibu Mkurugenzi mtendaji wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Wasia Mushi akikabidhi mfano wa funguo kuashiria makabidhiano ya Greda kwa Mteja Bw. T Hitesh Vishram ambae ni Project Supervisor wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Limited, Katikati ni meneja wa masoko, Utafiti na maendeleo wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Muganyizi Bisheko.


  BANK OF AFRICA hii leo imekabidhi rasmi mtambo wa ujenzi (Greda jipya aina ya JCB) lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kampuni ya Dezo Civil Contactors Limited, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo kandarasi ya ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi.

  Makabidhiano ya mtambo huu ni sehemu ya mpango endelevu wa benki wa kununua na kukodisha mitambo (lease finance), ambayo inawawezesha wateja kujiongeza kiutendaji kwa kupata vifaa vya kisasa bila ya kulazimika kuwa na pesa taslimu za manunuzi ya vifaa hivyo.

  Makubaliano haya ya ukodishaji wa mitambo yanaakisi katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii, madini, mafuta na gesi.

  BANK OF AFRICA imebaini huu ni mpango ambao una tija kubwa kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo, kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa biashara zao ambao utaongeza uzalishaji na faida kubwa. Mteja kupitia mpango huu anapewa fursa pana ya kufanya chaguo lake bila kikwazo chochote na bila ya uhitaji wa amana ya awali au dhamana nyingine. Marejesho ni malipo ya ukodishaji ya kila mwezi na mteja ana uwezo wa kuchagua kua mmiliki wa mali husika pindi ifikapo mwisho wa mkataba wa ukodishaji.

  Benki humsaidia mteja kuhakiki chombo anachotaka kuingianacho mkataba kama kina ubora ili kuweza kuinua uchumi wake na uchumi wataifa kwa ujumla.

  BANK OF AFRICA ilianza shughuli zake Juni mwaka 2007, baada ya kuinunua Benki ya Euroafrican ambayo ilianza kazi Tanzania kutokea September 1995.

  BANK OF AFRICA inafanya kazi katika mtandao wa benki za biashara katika nchi 18 zikiwamo nchi za Benin, Burkina Faso, Burundi, Cote d”ivoire, Djibouti, DRC, Ethiopia, France, Ghana, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Rwanda, Senegal, Tanzania, Togo na Uganda.

  Kundi la Group BANK OF AFRICA lina makao makuu yake jijini Dakar, Senegal ikiwa na mtandao wa watu 500 wale wanaotoa huduma na sapoti kwa ofisi. Kuanzia mwaka 2010, Group BANK OF AFRICA ilimilikiwa kwa wingi wa hisa BMCE Bank, ambayo ni benki ya pili kwa ukubwa nchini Morocco.

  BMCE Bank huleta mikakati mizito ya msaada wa uendeshaji katika kuunga mkono shughuli za BANK OF AFRICA Group, vilevile na muunganiko na ukaribu wa kufikia masoko ya kimataifa kutokana na uwepo wake katika nchi za Ulaya na Asia.

  0 0

  Na Humphrey Shao-Globu ya Jamii.

  Kada wa chama caha Mapinduzi (CCM) kutoka wilaya ya Sengerema Lawrence Mabawa ametangaza kampeni yake mpya itakayo kwenda kwa jina la 'MAGUFULI BAKI'.

  Mabawa amesema kuwa Kama jinsi Watanzania na wasio Watanzania tunavyotambua kazi kubwa na nzuri ya kutetea na kupigania rasilimali za Taifa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, Rais wa wananyonge na masikini wa Watanzania wote bila kujali jinsia, dini,kabila, kuchukuwa jukumu la kumpongeza na kumtia moyo Rais na Serikali yake na si kumkatisha tamaa.

  " Mimi kama Mtanzania mzalendo na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nimeamua kuchukuwa jukumu la kuanzisha kampeni ya ‘Magufuli Baki’ yenye lengo kumpongeza Rais kazi anayoifanya bila kujali itikadi zao. 

  Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha Mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wanafunzi wa Sekondary na wananchi kwa kufanya mikutano yenye nia njema ya kumwomba Mhe. Rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea Watanzania wanyonge na masikini"Amesema Mabawa.

  Amesema kuwa Kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kupitia mikutano tutakayoifanya ambapo wataweza kutoa maoni kuhusu utendaji wa serikali kwa ujumla ikiwa ni kupongeza na hata kukosoa.

  ametaja kuwa hili kukamilisha kampeni hii tutatumia Kurasa za Mitandao ya Kijamii maalum ambazo zimeandaliwa kwa kampeni hiyo ambapo tutaweka maoni na pongezi za kila mshiriki wa kampeni hiyo. Mbali na kutumia mitandao ya kijamii tutashirikiana bega kwa bega na vyombo vya habari pamoja na wanahabari kufanikisha kampeni hii.

  Ameongeza kuwa lengo la kampeni hii mbali na kompongeza Mhe. Rais na Serikali yake pia tutapata fursa ya kuwasikiliza wananchi moja kwa moja ili kugundua ukweli halisi kutoka kwao wa namna gani wanaona utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
  Kada wa Chama cah Mapinduzi kutoka Wilaya ya Sengerema ,Lawrence Mabawa akizungumza na waandishi wa haabri juu ya kampmeni yake ya Magufuli baki ambayo ameitambulisha kwa Wanahabari kuhusu kuanza kampeni ya kumshinikiza Rais Magufuli aendelee kusimamia misimamo yake katika kuongoza nchi na kuacha kuyumbishwa na maneno ya kwenye mitandao
  Afisa Habrai Idara ya Habari MAELEZO , Georgina Misama akimtambulisha Kada wa Chama cah Mapinduzi kutoka Wilaya ya Sengerema ,Lawrence Mabawa kwa Waandishi wa Habari.
  Sehemu ya Waandishi walioshiriki mkutano huo wakimsikiliza Kada wa Chama cah Mapinduzi kutoka Wilaya ya Sengerema ,Lawrence Mabawa kwa makini

  0 0


  NA EVELYN MKOKOI.

  NAIBU  Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga  Mpina ,amesitisha uchimbaji na uchotaji wa mchanga kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.

  Pia ametoa siku 30 kwa Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kubaini na kutenga maeneo ya uchimbaji ya mchanga ambayo yapo ndani ya manispaa zao yatakayo ruhusiwa kwa zoezi hilo kisheria.

  Akitoa agizo hilo Dar es Salaan leo,wakati wa ziara ya kutembelea Mto Nyakasangwe uliopo maeneo ya Boko Kata ya Bunju alisema kama kuna maeneo ambayo wananchi wanaweza kufika Kwa urahisi, manispaa zinapaswa kuyatembelea maeneo hayo na kuyabaini kama kunauwezekano wakuchimba mchanga.

  Alisema ndani ya mwezi mmoja manispaa hizo zinatakiwa  kuandaa utaratibu mfupi wa kutenga maeneo hayo ikiwemo utoaji wa vibali kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Halmashauri pamoja na Nemc.

  “Halmashauri zote zilizo na eneo ambalo linaweza kuruhusiwa kuchota mchanga hakikisheni mnatembelea maeneo hayo na kufata taratibu zote za utoaji wa vibali ambapo maeneo mengine yawe ya uchotaji wa mchanga,”alisisitiza Mpina

  Alisema watafanya Operasheni ya  usiku na mchana kuhakikisha watu watakaoendelea kuchimba  mchanga na kuchota mchanga sehemu ambazo haziruhusiwi watachukuliwa  hatua ikiwa ni pamoja na kutozwa faini zilizopo kisheria na kufikishwa mahakamani.

  Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunju Bw. Kateni Nassor Msangi alimshukuru Mpina kwa kufanya ziara katika eneo hilo na kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kujengea mawe katika kuta za kingo yam to huo ambao umeharibika vibaya, ili kuweza kunusuru mazingira ya mto huo kuharibika pamoja na kunusuru makazi yao.
   Eneo la mto Nyakasangwe lililopo kaika kata ya Bunju linavyoonekana kuharibika vibaya kutokana na uchimbaji wa mchanga , na kupelekea makazi ya wananchi kuwa hatarini.
  DSC_0025
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina  akizungumza na vyombo vya habari baada ya kukamilika kwa zoezi la kukagua mto Nyakasangwe, uliopo katika kata ya Bunju ulioharibiwa vibaya na uchimbaji wa mchanga.
  DSC_0044
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mwandishi wa Habari wa kituo cha Radio cha Efm kinachopatikana katika masafa ya 93.7 katika jiji la Dar es Saalam alipokuwa akimuuliza maswali kuhusu uchafuuzi wa mazingira utokanao na uchimbaji wa mchanga katika eneo la Boko.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) akifafanua jambo mbele ya nwaandishi wa habari (hawapo pichani) akitangaza uamuzi wa kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) pamoja na uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa NEMC ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustine Kamuzola na kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Richard Muyungi.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa mkutano wao na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. Januari Makamba (MB) alipokuwa akitangaza uamuzi wa kusitisha uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) na wajumbe saba wa Bodi ya baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.Picha na: Frank Shija - MAELEZO.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na akiwa kwenye kikao na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu kinachomuelezea Jane Goodall na miaka 50 alioishi Gombe kutoka kwa Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Dk. Jane Goodall, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Katika Ujumbe wake Dk. Goodall aliambata na Mama Getrude Mongela na Hadija Simba ambao ni wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Roots and Shoots pamoja na watendaji wengine wa Taasisi hiyo.

  Katika mazungumzo yao Dk. Goodall pamoja na mambo mengine amezungumzia uharibifu wa shoroba za wanyama pamoja na makazi yao katika hifadhi ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma ambayo ni maarifu kwa uhifadhi wa Sokwe. Alisema kwa sasa hifadhi hiyo imezungukwa na maakazi ya binadamu hali iliyosababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya wanyama hao.

  Aidha Dk. Goodall alimuelezea Makamu wa Rais jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kupambana na uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya Gombe ikiwemo kuhimiza uwepo wa mipango bora ya matumizi ya ardhi.

  “inawezekana tatizo kubwa linalosababisha uharibu wa mazingira ni umasikini na uelewa mdogo wa wananchi” alieleza Dk.Goodall. Hata hivyo alisema zipo jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kutoa elimu kwa umma. 
   
  Kwa sasa wananchi kutoka katika vijiji zaidi 52 mkoani wa Kigoma wanapatiwa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira. Vilevile, jumla ya shilingi Milioni 400 zimekopeshwa kwa wananchi wa vijiji 32 ili kujiwezesha kiuchumi na kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira hususan yenye leno la kulinda shoroba na makazi ya Sokwe. Hali hii imeanza kuleta mafanikio.

  Dk. Goodall ametaja changamoto kubwa katika uhifadhi wa mazingira ya Gombe kuwa ni kuwepo kwa wakimbizi kutoka Burundi ambao kwa kiasi kikubwa hushiriki katika shughuli ambazo husababisha uharibu wa mazingira kama vile kilimo na ufugaji usio endelevu.

  Kwa upande wake Makamu wa Rais alisema serikali inafanya kazi kubwa katika kuhakikisha mazingira ya hifadhi za Taifa pamoja na ikolojia yake yanatunzwa. Makamu wa Rais amemhakikishia Dk. Goodall kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti ili kuhakiksha wananchi wanafanya shughuli za kujiletea maendeleo bila kuharibu mazingira.

   “Ni muhimu kuishirikisha jamii inayoishi pembezoni mwa hifadhi zetu katika suala la uhifadhi wa mazingira lakini pia kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi”, alisema Makamu wa Rais. Kuhusu suala la wakimbizi kuharibu mazingira, Makamu wa Rais aliahidi kutoa maelekezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ili kuona namna bora ya kulipatia ufumbuzi suala hilo.

  Mwisho, Makamu wa Rais alimpongeza Dk. Goodall kwa kupewa tuzo ya heshima na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) kama ishara ya kutambua mchango wake katika masuala ya uhifadhi wa Sokwe na mazingira kwa ujumla.

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akionyesha moja kati ya vifaa vya maabara ambayo wilaya ya Muheza imepatiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari wilayani humo juzi wakati alipokwenda kukabidhi kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Luiza Mlelwa kushoto ni Afisa Elimu Sekondari wilaya hiyo Julitha Akko

  Mwanafunzi wa kidato cha sita shule ya Sekondari Muheza High School,Luqman Mustapha akimueleza Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu juzi namna wanayotumia vifaa vya maabara walivyopatiwa wakati alipokabidhi vifaa vya maabara kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa nchini  MBUNGE wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi wa shule za Sekondari wilayani humo kuongeza bidii ikiwemo kujikita kwenye masomo ya sayansi ili kuweza kuendana na sera ya viwanda ilivyopo hapa nchini.
  Balozi Adadi aliyasema hayo jana wakati alipokabidhi vifaa vya maabara kwa shule za sekondari wilayani humo vilivyotolewa na Wizara ya ElimuSayansi na Teknologia kwa ajili ya shule zote za sekondari hapa chini. 

  Alisema vifaa hivyo ambayo vimetolewa katika shule 7 kati ya 24
  wilayani humo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuweza kufikia malengo yao ya kufanya vizuri katika masomo yao katika hafla hiyo iliyofanyika shule ya sekondari ya Muheza.
  “Jambo hilo ni nzuri na hasa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutaka vifaa hivyo vikabidhiwe katika shule ambazo zitakuwa zimekamilisha ujenzi wa maabara na vitaweza kuwapa mwanga mzuri kusoma kwa bidii “Alisema. 

  Alisema ni jambo la ajabu iwapo vifaa ambazo vimekabidhiwa vitatumika vibaya kitendo ambacho kitakwamisha juhudi za serikali za kutaka wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili waweze kuendana na sera ya viwanda. “ Vifaa hivi ambavyo mmekabidhiwa leo hii vinagharama kubwa hivyo niwaombe ndugu zangu mhakikishe mnavitunza ili viweze kutumika katika matumizi yaliyokusudiwa lakini pia niwatake wanafunzi mhakikishe mnasoma kwa bidii “Alisema .

  Mbunge huyo alisema lipo tatizo la kubwa la kutokuwepo vifaa vya maabara katika shule nyingi za sekondari hapa nchini jambo ambalo limeanza kupatiwa ufumbuzi na serikali ya awamu ya tano kupitia wizara ya elimu ili kuona namna ya kulimaliza. 

  Awali akizungumza katika hafla hiyo, Afisa elimu sekondari wilaya Muheza Julitha Akko amewaagiza walimu wakuu wa shule za sekondari zilizopatiwa vifaa hivyo kuacha tabia ya kufungia ndani ya makabati na badala yake vitumike kama ilivyokusudiwa. 

  Aidha alisema kuwa lazima kuwekwe utaratibu wa namna ya kuvitunza vifaa hivyo na kuagiza visitumike kinyume na makusudio yake na kuwataka wanafunzi waelekeze nguvu zao kwenye masomo ili kuongeza wataalamu wengi. 

  Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Muheza(Muheza high school) Alex Birumo alisema yapo mategemeo makubwa ya kuongeza ufaulu hasa kwa masomo ya sayansi kutokana na kupatikana kwa vifaa hivyo ambavyo wanafunzi walikosa fursa kwa miaka mingi kujifunza kwa vitendo. 

  “Shule yetu hii ni ya masomo ya sayansi ya michepuo ya PCB NA CBG na ni ya kidato cha tano na sita unapokuwa na wanafunzi zaidi ya 150 unawafundisha bila ya vifaa vya maabara kiukweli mafunzo yetu kwa wanafunzi hao yahakuwa na tija”Alisema

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wafanyakazi wakati wa mafunzo ya kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

  Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfuatilia kwa makini mwenzeshaji kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. Andrew Mbwambo wakati wa mafunzo ya kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

  Wawezeshaji wa kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kipindi cha miaka mitano kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe wakimsililiza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi wakati akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfuatilia kwa makini mwenzeshaji kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof. AndrewMbwambo wakati wa mafunzo ya kuandaa mpango mkakati wa utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

  Picha na JKCI.

  0 0


  WITO umetolewa kwa washindi wa bahati nasibu ya Biko wanaoendelea kupatikana kila siku wafanye vitu vya maendeleo mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake.

  Alisema ni wakati wao sasa washindi wote wa Biko wale wanaopata zawadi nono ya Sh Milioni 20 inayotoka kila Jumatano na Jumapili pamoja na zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja wanakuza uchumi wao.

  “Kwa kuanzia Sh 1,000 tu mtu anaweza kushinda 5,000 hadi Milioni 20 kwa droo zetu kubwa, ambapo ni rai yetu kwa washindi wote kuwataka maisha yao yabadilike kwa kutumia vyema fedha zao baada ya kucheza Biko, mchezo unaochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za TIGO Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.

  Naye Nyari, mshindi huyo wa droo ya 23 aliyotangazwa juzi jijini Dar es Salaam, alisema ni jambo la kumshukuru Mungu kwa hatua yake ya kuibuka na ushindi wa Sh Milioni 20 uliokuja kuyabadili maisha yake baada ya kukabidhiwa jana katika Tawi la Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.

  “Wakati napigiwa simu ya ushindi na balozi wa Biko, Kajala Masanja, hakika nilikuwa siamini, ukizingatia kuwa wanaocheza Biko ni wengi na kila mtu anataka yeye awe mshindi wa Jumatano au Jumapili, hivyo kwangu mamilioni haya niliyokabidhiwa leo yamekuja kunibadilisha kwa hatua moja kwenda nyingine.

  “Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba napiga hatua kubwa, ili pamoja na mambo mengine, niweze kutimiza ndoto zangu na kuwaaminisha waendeshaji wa mchezo wa Biko kuwa fedha zao zinabadilisha maisha yangu kiuchumi,” Alisema.

  Moja ya sifa kubwa ya bahati nasibu ya Biko ni kitendo chake cha kuwakabidhi washindi wao fedha zao wanazoshinda siku moja tu baada ya kutangazwa washindi jambo linaloongeza chachu ya kupiga hatua kimaendeleo, huku kwa kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, wakiweza kuwapa washindi wao zaidi ya Sh Bilioni moja tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu yao.

  Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kulia akimkabidhi kiasi cha Sh Milioni 20 mshindi wao Fredy Nyari wa Kigamboni aliyeibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 katika droo ya 23 juzi. Kushoto ni Afisa wa NMB.


  Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alipokuwa anamkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Jumadili (Jumapili), Fredy Nyari, akiwa ni mshindi wa droo ya 23 ya Biko.

  Akizungumzia hatua ya makabidhiano ya fedha hizo, Heaven, alisema kwamba ikiwa siku zote mtu anakosa mtaji wa kuanzisha au kuendeleza biashara zake, kupata Milioni 20 kwa mara moja si jambo la mzaha.

  Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko droo ya 23, Fredy Nyari, akiwa na uso wa furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam.

  Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa na mshindi wao wa Sh Milioni 20 Fredy Nyari baada ya kumkabidhi fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam leo mchana.
     0 0

   Mbunge wa Manonga / Igunga Seif Khamis Gulamali akimpokea na kumpa sapoti ya safari yake Muigizaji wa Filamu za Kihindi Sanjay Dutt kwenda Mapumzikoni Mbuga za Wanyama Ngorongoro Mkoani Arusha Mapema leo
   Mbunge wa Manonga / Igunga Seif Khamis Gulamali akimpokea na kumpa sapoti ya safari yake Muigizaji wa Filamu za Kihindi Sanjay Dutt kwenda Mapumzikoni Mbuga za Wanyama Ngorongoro Mkoani Arusha Mapem leo
  Muingizaji wa Filamu za Kihindi Sanjay Dutt akipanda ndege tayari kwa kuruka  kwenda Mapumzikoni Mbuga za Wanyama Ngorongoro Mkoani Arusha Mapema leo

  0 0

   Rais Mtaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akilakiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipofika kumpa pole kwa msiba wa mke wa Waziri huyo mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Rais Mtaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiongea na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipofika kumpa pole kwa msiba wa mke wa Waziri huyo mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda (kulia) akiongea na baadhi ya waombolezaji alipofika kumpa pole Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar e s Salaam Mhe. Paul Makonda (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa msiba wa mke wa Waziri huyo mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi (kulia) akiteta jambo na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda wakati walipofika kumpa pole Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz (kulia) akimpa mkono wa pole  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe (kulia) akimpa pole Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu (kulia) akimpa pole Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati walipoenda kumpa pole Waziri Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam, kulia ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu na kushoto ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakati alipoenda kumpa pole Waziri Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akimpa pole Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Mhandisi Stella Manyanya akimpa pole Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kwa msiba wa Mke wake mapema hii leo nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo
   Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma akimpa pole Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe kwa kufiwa na Mkewe, Linah Mwakyembe Nyumbani Kunduchi jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Mssaka,Globu ya jamii.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju akimpa pole Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe kwa kufiwa na Mkewe, Linah Mwakyembe Nyumbani Kunduchi jijini Dar es Salaam. 
   Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Razalo Nyalandu akimpa pole Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe kwa kufiwa na Mkewe, Linah Mwakyembe Nyumbani Kunduchi jijini Dar es Salaam. 

   Msanii wa Kizazi kipya Nasbu Abdul (Diamond Platnumz) akimpa Pole Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe kwa kufiwa na Mkewe, Linah Mwakyembe Nyumbani kwake Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Bernad Membe akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Razalo Nyalandu pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika Msiba wa Mke wa Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Linah Mwakyembe nyumbani Kunduchi jijini Dar es Salaam.

  Kaimu Jaji Mkuu , Profesa Ibrahim Juma  akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika Msiba wa Mke wa Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Linah Mwakyembe nyumbani Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola , wakimpa pole Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Dk. Harrison Mwakyembe kwa kufiwa na Mkewe, Linah Mwakyembe Nyumbani Kunduchi jijini Dar es Salaam.
   Picha mbalimbali waliofika katika Msiba wa Mke wa Waziri wa Habari, Michezo , Utamaduni na Sanaa, Linah Mwakyembe nyumbani Kunduchi jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awasili mkoani Tanga kutatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo pamoja na mikoa inayopakana nayo.

  Katika ziara hii Waziri Lukuvi leo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Iliyopo Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi iliyopo mkoani Tanga ikiwa muendeleo zo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.

  Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.

  Ikumbukwe mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.

  Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
  Aidha, wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto walimlalamikia Waziri Lukuvi kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo ajulikanae kwa jina la Le-Mash Enterprises Limited.

  Baada ya Waziri Lukuvi kusikiliza malalamiko hayo, ameahidi kutembelea mashamba hayo kesho ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wanakabiliwa na mgogoro huu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera wakiwasikiliza wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi katika kutatua mgogoro wa mpaka unaoikabili mikoa hiyo.
   Wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto wakiwasilisha malalamiko yao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi baada ya kukutana nae.
   Eneo la Mji wa Lushoto mkoani Tanga.
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi  (katikati) alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela (wanne kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera na (watatu kushoto) pamoja na viongozi wengine.
   Wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto wakiongozwa na Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi (wasita Kulia) walipokutana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametoa siku saba kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam DCP Lucas Mkondya kuhakikisha wizi wa vifaa vya Magari unakomeshwa mara moja.

  Akitoa maagizo hayo, Mheshimiwa Makonda amesema wizi wa vifaa vya magari vikiwemo Vioo, Radio, Side mirrow, Power Window,Taa pamoja na Shoo ya mbele na nyuma ya Gari vimekuwa vikishamiri kila kukicha jambo linalowakera wananchi na kuwapa hofu ya kuweka magari yao kwenye maegesho kwa kuhofia kuibiwa kitendo ambacho amesema hakivumiliki.

  “Sitaki kusikia watu wanaibiwa vifaa vya Magari yao,watu wanaibiwa Vioo, Power Window,Radio, Taa,Side Mirror na wakati mwingine wanavunja vioo vya gari na kuiba Pochi na Laptop, sasa haiwezekani wizi wa namna hii uendelee kwenye Mkoa  wangu, sasa Kaimu Kamanda Kanda Maalumu nakuagiza na ninakupa siku saba sitaki kusikia wizi wa vifaa vya magari ukiendelea, nataka ifikie hatua mtu aweze kuegesha Gari lake na kulikuta likiwa salama” Alisema Makonda.

  “Mwananchi yoyote atakaeibiwa na akapeleka taarifa Polisi na hatua za kisheria zichukuliwe atoe taarifa kwangu bahati nzuri wananchi wana namba zangu, haiwezekani Mwananchi anajikusanya na kununua gari alafu anaibiwa watu wanaiba vifaa vyake, wizi wa namna hii nasema Mwisho ndio umefika leo," Alisisitiza Makonda.

  Aidha Makonda ameagiza Maduka na Vijiwe vyote vinavyouza vifaa vya Magari kujisajili mara moja iliviweze kutambulika na Serikali.“Kinachoshangaza ni kwamba hawa wanaoiba wana vijiwe vyao ambapo wanauza hivyo vifaa, ukienda Kariakoo, Magomeni na pia Temeke (Keko) kuna vijiwe ambavyo ukienda kule unakuta kifaa kilichoibiwa kwenye Gari lako kipo mtaani kinauzwa” Aliongeza Makonda.

  Akipokea Maagizo hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  DCP Lucas Mkondya amesema kuwa maagizo hayo yanaanza kutekelezwa leo ambapo msako utaanza leo kuhakikisha Genge la wezi wa vifaa vya magari vinasambaratishwa.

  Aidha amewaagiza Makamanda wa polisi Temeke, Ilala na Kinondoni kuanza utekelezaji wa maagizo hayo kuanzia leo na kuwataka wote wanaouza vifaa vya wizi kujisalimisha mara moja kwa Jeshi la Polisi.

older | 1 | .... | 1307 | 1308 | (Page 1309) | 1310 | 1311 | .... | 1898 | newer