Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live

MASAUNI AAMURU UJENZI GEREZA MUHEZA UANZE MARA MOJA, AKAGUA OFISI, NYUMBA ZA TAASISI ZAKE WILAYANI PANGANI

0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimuangalia mhamiaji haramu katika dirisha dogo la chumba cha mahabusu, Kituo cha Polisi Pangani mkoani Tanga. Mhamiaji huyo kutoka nchini Somalia alikamatwa wilayani Pangani katika mwambao wa Bahari ya Hindi. Masauni akiwa mjini Tanga aliwaagiza Maafisa Uhamiaji na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Kituo Polisi mjini Pangani, Christina Musyani. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani wakati alipokua anamfafanulia masuala ya ulinzi na usalama wilayani humo. Masauni alikikagua kituo hicho pamoja na nyumba za askari polisi ambazo zipo katika hali mbaya zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani alipokuwa anamuonyesha moja ya nyumba ambazo zipo katika hali mbaya zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoka kulikagua Gereza la Wilaya ya Pangani mkoani Tanga. Masauni pia alizungumza na mahabusu wa Gereza hilo kwa kusikiliza kero zao na kuzitolea maamuzi hapo hapo na baadhi kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka zaidi. Kwa nyuma ni Mkuu wa Gereza hilo, Elishinikizo Moshi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsalimia Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu, wakati Naibu Waziri huyo alipowasili wilayani Muheza mkoani Tanga kwa ajili ya ziara yake ya kikazi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mwanaasha Tumbo. Kulia ni Mkuu wa Gereza Muheza ambalo ujenzi wake unatarajiwa kujengwa hivi karibuni baada ya Masauni kuamuru ujenzi huo uanze mara moja. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo alipokua anatoa taarifa yake ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo. Mara baada ya kusomewa taarifa hiyo na kuona kuna changamoto mbalimbali ikwemo ya kutokuwepo Gereza wilayani humo, Masauni aliamuru ujenzi wa Gereza hilo uanze mara moja ikiwa mahitaji yote ya nguvu kazi na mengineyo yapo. Wapili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Dkt. Abbasi Kuongoza Kamati ya Kuchunguza Ubia wa TBC na Star Times

0
0
 Dkt.Hassan Abbasi


IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI KENYA

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasili uwanja wa ndege kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), kushoto ni kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa Ali Mussa. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro,  akizungumza na Kaimu kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Lucas Mkondya (wa kwanza kushoto), muda mfupi alipowasili nchini akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), kulia ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa Ali Mussa. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro (wa kwanza kulia), akifurahia jambo baada ya kuwasili nchini akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), anayefuata ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa Ali Mussa na Kaimu kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP) Lucas Mkondya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro(wa kwanza kulia),akitafakari jambo baada ya kuwasili nchini akitokea Nairobi nchini Kenya kuhudhuria hafla ya ufungaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), anayefuata ni Kamishna wa Polisi Jamii nchini (CP) Mussa Ali Mussa na Kaimu kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP) Lucas Mkondya
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya makamanda na washiriki kutoka Majeshi ya Polisi ambao ni wanachama wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO),  waliohudhuria mafunzo ya kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka, mafunzo yaliyofanyika katika chuo cha Jeshi la Ulinzi la Kenya kilichopo katika eneo la Embakasi, jijini Nairobi
Baaadhi ya vikosi vya Jeshi la Polisi kutoka nchi wanachama wa Shirikisho la Wakuu kwa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki (EAPCCO), walioshiriki katika mafunzo ya kujengewa uwezo wa kukabiliana na matishio ya kigaidi na uhalifu mwingine unaovuka mipaka, mafunzo yaliyofanyika katika chuo cha Jeshi la Ulinzi la Kenya kilichopo katika eneo la Embakasi, jijini Nairobi.

TRA YAONGEZA MUDA WA KULIPIA KODI YA MAJENGO MPAKA JULAI 30, 2017

0
0

TAARIFA KWA UMMA: KUISHA KWA MUDA WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (e-VERIFICATION)

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
IDARA YA UHAMIAJI
     


KUISHA KWA MUDA WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI (e-VERIFICATION)

Idara ya Uhamiaji inapenda kuwakumbusha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni wote kuhakikisha wamehakiki vibali vyao kupitia Mfumo wa Uhakiki ambao unapatikana kupitia Tovuti ya Idara ya www.immigration.go.tzkabla ya zoezi la uhakiki kuisha tarehe 19/07/2017.

Kwa wale ambao kumbukumbu za vibali vyao hazitaonekana katika mfumo wa uhakiki au kuwa na tatizo lolote wanashauriwa kuripoti katika Ofisi za Uhamiaji za Mikoa au kwa Mamlaka husika ndani ya muda uliotolewa.

Baada ya kuisha kwa muda uliotolewa, Idara itafanya ukaguzi nchi nzima na kuwachukulia hatua za kisheria Wageni binafsi, Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo wageni wao watabainika kuwa na vibali vya kughushi au vilivyopatikana nje ya utaratibu wa utoaji vibali.

Idara ya Uhamiaji ilitoa muda wa siku 90 kwa wale wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki vibali vyao; tangu tarehe ya kuzindua mfumo huo tarehe 19 Aprili, 2017.

Imetolewa na;
KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
14 JULAI, 2017.

CRB yatahadharisha wakandarasi dhidi ya matapeli

0
0
BODI ya Usajili wa Wakandarasi Nchini (CRB), imewatahadharisha wananchi, watu  wenye miradi ya ujenzi pamoja na wakandarasi nchini kuwa makini na watu wanaotumia jina la bodi hiyo na kufanya utapeli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msajili wa bodi hiyo, Rhoben Nkori, bodi imewataka wananchi na wakandarasi wawe wanatoa taarifa katika ofisi za bodi za Makao Makuu Dar es Salaam na Kanda zake ili kuwakamata na kuwafikisha mahahani watu wa aina hiyo.

“CRB ina ofisi za kanda ambazo zinafanya kazi nchi nzima, kanda hizo ni Kanda ya mashariki – Dar es salaam, Kanda ya kaskazini  Arusha, Kanda ya kusini Mbeya,  Kanda ya ziwa Mwanza

na Kanda ya kati  Dodoma, watumie ofisi hizi wasirubuniwe na matapeli,” alisema Nkori.

Aidha, alisema watumishi wa CRB wamekuwa wakienda kwenye ukaguzi wakiwa na vitambulisho vya bodi hiyo na vizibao vyenye nembo ya CRB vinayowatambulisha kuwa wanatoka bodi hiyo.

Alisema kuna watu ambao wamekuwa wakijiita wawakilishi wa Bodi hiyo na kufanya shughuli za bodi hiyo kwa njia ya utapeli na kuchukua rushwa kwa wakandarasi na wenye miradi.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa jana na  CRB, watu hao wamekuwa wakijitambumbulisha kama wawakilishi wa bodi hiyo ambao huwa wanakwenda kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi maeneo mbalimbali.

Alisema watu hao hutembelea sehemu zenye miradi na kuwatisha watu wanaofanya shughuli za ujenzi na kuwaomba rushwa ili wasiwashtaki wanapobaini kasoro kwenye miradi yao.

Aidha, alisema watu hao wamekuwa wakiwaandikia barua watu wenye miradi ya ujenzi wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua na bodi kwa kufanyakazi zao bila kuzingatia masharti ya ujenzi kama vile kuweka vibao vya kuonyesha mkandarasi anayejenga.

“Sisi CRB hatuwatambui watu hao na tunawaomba wananchi na watu wenye miradi ya ujenzi wawe makini na wakiwa na tatizo waende kwenye ofisi za kanda zetu ambazo tumezitaja kama kuna watu anahisi wanataka kumtapeli awasiliane na bodi ili tumkamate na kumfikisha mahakamani,” alisema

Gazeti hili lilifanikiwa kupata nakala ya barua yenye nembo ya CRB iliyoandikwa na mmoja wa matapeli hao kwenda kwa mmoja wa wateja akidai kutaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo kwenye mradi wake wa ujenzi unaoendelea.

 Kwenye barua hiyo kwenda kwa mteja tapeli huyo  aliandika hivi “ I need the following drawings, architectural drawing, structural drawing and Building permit and sign board.

“Hapo anamaanisha kuwa mteja huyo amuonyeshe mchoro wa jengo, kibali cha ujenzi na kibao ambacho kisheria kinapaswa kuwekwa sehemu ya ujenzi kikionyesha jina la mteja, mkandarasi, mhandisi mshauri na  mkandarasi”alisema

SHINDANO LA "MAVUNDE NA UTAMADUNI WETU" LAFANA DODOMA

0
0
SHINDANO la ngoma za utamaduni liitwalo ‘Mavunde na utamaduni wetu’ limefanyika leo mjini Dodoma likiwa na lengo la kuenzi, kulinda na kuhifadhi utamaduni wa watu wa Dodoma.

Shindano hilo limeandaliwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na lilihusisha vikundi vya ngoma za asili ya Dodoma 7.Vikundi hivyo ni Simba dume, changamoto, Noti mtemi, Neema Yerusalem, Chipukizi, Finga Vikonje na Imani Makulu.

Akizungumza katika shindano hilo, Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema uwepo wa shindano hilo ni utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu 2015 na kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuhamishia shughuli za serikali Dodoma, kupiga vita Rushwa na Ubadhirifu na Kulinda Maliasili za Taifa kwa manufaa ya watanzania wote.

“Tamaduni zetu zilikuwa zimeanza kusahaulika watu hawakuona tena umuhimu wa ngoma za jadi na hii ni kutokana na utandawazi na kuwa watu wa mjini sana tumesahau tumetoka wapi,”amesema Mavunde

Amebainisha katika kampeni hizo aliahidi kwa nafasi yake atajitahidi kuviunganisha vya kutoka maeneo mbalimbali ili kuenzi na kulinda utamaduni wa Dodoma.

“Hatua yetu ya kwanza ni kukusanya vikundi na kuvipambanisha lakini baadaye tutakuwa na makubwa ya kimkoa kila mwaka na hii nawashawishi na wenzangu pia, ili mkoa wetu uendelee kutunza na kuhifadhi utamaduni wetu,”amesema

Mavunde amesema shindano hilo linalenga kuwakumbusha vijana kuwa mababu zao waliishi kwa namna gani.Kwa upande wake, Chifu wa Dodoma mjini Lazaro Chihoma amempongeza mavunde kwa kuandaa tamasha hilo na kudai kuwa wamepita viongozi wengi lakini hawakuona umuhimu wa kuenzi utamaduni wao.

Vikundi vilivyoibuka kidedea ni pamoja na kikundi cha Imani Makulu ambacho kimepata kombe na fedha Sh.300,000, mshini wa pili ni Kikundi cha Chipukizi kimepata Sh.250,000 na ngao na mshindi wa tatu Figa Vikonje kimepata Sh.150,000 huku vingine vikipatiwa Sh.80,000 kila kimoja.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akizungumza katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu lililofanyika mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akizungumza katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu lililofanyika mjini Dodoma.
Chifu wa Dodoma mjini Lazaro Chihoma akizungumza katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu, mjini Dodoma 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Anthony Mavunde akiwa na viongozi mbalimbali katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu. 
Umati wa wakazi wa Dodoma waliohudhuria shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.
Umati wa wakazi wa Dodoma waliohudhuria shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoshiriki katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoshiriki katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.
Vikundi mbalimbali vya ngoma vilivyoshiriki katika Shindano la Mavunde na Utamaduni wetu.

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2017 pamoja na Ualimu 2017 haya hapa


VIONGOZI 6 WA CHADEMA AKIWEMO MBUNGE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA

0
0
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Gemini Mushy Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia viongozi 6 wa kitaifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma kupitia chama hicho ZUBEDA SAKURO , kwa kosa la kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa na kuzua vurugu wilayani Nyasa mkoani Ruvuma. Hii hapa taarifa yake.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAPILI LEO JULAI 16,2017

0
0

TANZIA: WAZIRI HARRISON MWAKYEMBE AFIWA NA MKEWE

0
0

WAZIRI PROF. MBARAWA AAGIZA CHUO CHA RELI TABORA KUANDAA WATAALAMU

0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Reli cha Tabora Eng. Richard Lauwo (kulia), wakati alipotembelea chuoni hapo jana katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mwalimu Queen Mlozi.
Mkuu wa Chuo cha Reli cha Tabora Eng. Richard Lauwo (kushoto), akifafanua jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati alipotembelea chuoni hapo.
Mkuu wa Chuo cha Reli cha Tabora Eng. Richard Lauwo (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, baadhi ya majengo yaliyopo chuoni hapo, wakati alipotembelea kuona maendeleo ya chuo hicho.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na walimu na wanafunzi wa Chuo cha Reli cha Tabora, wakati alipofanya ziara yake chuoni hapo.
Waziri Mkuu Serikali ya Wanafunzi kutoka Chuo cha Reli cha Tabora Bw. Isaac Fundisha akiuliza swali kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati alipofanya ziara yake ya kikazi chuoni hapo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiwa katika picha ya pamoja na uongozi na wanafunzi wa Chuo cha Reli cha Tabora nje ya jengo la chuo hicho.

………………………………………………………………………………..

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wito kwa uongozi wa Chuo cha Reli cha Tabora kuwajengea uwezo wanachuo ili kupata wataalamu wenye ujuzi, weledi, maarifa na uadilifu katika kusimamia mradi mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge).

Waziri Prof. Mbarawa ametoa wito huo alipotembelea chuo hicho ambacho kinatoa mafunzo mbalimbali yahusuyo reli na kusisitiza ushirikishwaji wa wanachuo hao katika kusimamia ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), ili kuwajengea uwezo.

“Serikali inawategemea ninyi kuendesha Reli ya Kisasa kwa kuwa ujenzi wa reli ni kitu kimoja na usimamizi na uendeshaji ni kitu kingine”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Amewataka wanachuo hao kusoma kwa bidii, kuwa waadilifu na wazalendo ili kuweza kuendesha Reli ya Kisasa (Standard Gauge) na Serikali itahakikisha kuwa inawapatia mafunzo kwa vitendo ya kutosha ili wawe na umahiri unaotakiwa.

Aidha, ameongeza kuwa Mkoa wa Tabora utakuwa ni kiungo muhimu cha Reli ya Kisasa kwani utaunganisha Mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Mwanza na nchi za jirani.

Prof. Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge), utagharimu takribani shilingi Trilioni 16 hivyo kuwataka watanzania kutumia fursa hiyo ya kujipatia ajira na kufanya kazi kwa uzalendo.

Ujenzi wa reli ya kisasa utabadilisha maisha ya watanzania na raia wa nchi za jirani kwani utarahisisha huduma za usafiri wa abiria na uchukuzi wa mizigo kutoka Rwanda, Uganda na D.R.C Congo.

Naye, Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Reli cha Tabora, Bwana Isaac Fundisha, amemshukuru Prof. Mbarawa kwa kutembelea Chuo hapo, kuzungumza na wanafunzi na kuonesha utayari wa Serikali wa kuwapatia wanachuo hao mafunzo kwa vitendo wakati wa mradi wa ujenzi wa reli hiyo na wengine kupata fursa ya ajira.

Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya kukagua miradi ya miundombinu iliyopo mkoani Tabora.

Ujenzi wa Barabara ya Ipembe-Msongole Kuanza Mwezi Juni Mwaka huu.

0
0



Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akipata maeleozo ya mtandao wa ramani ya barabara za Mkoa wa Songwe kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM).
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akitoa maelekezo kwa kaimu Meneja wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS)Mkoa wa Songwe Eng. Yona Kasaini (Kulia) alipokagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM) ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaanza mwezi juni Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipokea maoni ya mkazi wa wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM) ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaanza mwezi juni Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM) kupitia radi Ileje Fm mara baada ya kukagua barabara hiyo Mkoani Songwe.
Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International ltd, Canada akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto) kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Barabara ya Mafinga-Nyigo KM 74.1 wakati Eng. Ngoyani alipokagua maendeleo ya mradi huo Mkoani Njombe.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International ltd, Canada kuhusu kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara Mafinga-Nyigo KM 74.1 wakati alipokagua maendeleo ya mradi huo Mkoani Njombe.

……………………………………………………………………….

Serikali imetenga kiasi cha sh. bilioni 107.56 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Ipemba hadi Isongole wilayani Ileje yenye urefu wa kilomita 50.3 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa wa Songwe na Nchi jirani ya Malawi.

Naibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo amesema ujenzi huo utaanza mwezi juni Mwaka huu na kukamilka mwezi June, 2019.

“Tayari mkandarasi ameshapatikana na sasa ameanza kufanya maandalizi ya kuleta vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huu, Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kukamilisha ahadi hii kwa miezi ishirini na nne toka pale ujenzi utakapoanza”. amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng. Ngonyani amesema kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ni katika hatua za kutekeleza ahadi iliyotolewa na Serikali kwa wanachi wa mkoa huu katika vipindi tofauti tofauti vya uongozi.

“Wananchi wa hapa wana shauku kubwa na barabara hivyo kukamilika kwake kutasaidia kuufungua mkoa huu kwa upande wa Malawi ambao tunapakana nao na hivyo kukuza shughuli za kibiaahara baini ya nchi hizi mbili na kupelekea kukuza uchumi kwa wakazi hawa,” amesisitiza Eng Ngonyani.

Naye Meneja wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Songwe amemuhakikishia Waziri Ngonyani kuwa wakala utasimamia ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati na viwango vinavyokubalika,” amesema Eng. Yona Kasaini

“Barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami ya daraja la kwanza ili kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu zaidi, sisi tutahakikisha kazi hii inakamilika kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wetu,” amesema Eng.Yona Kasaini

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bi. Chiku Galawa ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuamua kujenga barabara hii na ameahidi kutoa ushirikiano kwa TANROADS na mkandarasi wa M/s China Engineering Corporation atakayejenga barabara hiyo.

Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amekagua mradi wa ukarabati wa barabara ya Mafinga-Nyigo (74.1 KM) na kipande cha Nyigo-Igawa (63.8 KM) ambapo amemtaka mkandarasi anayejenga barabara hiyo kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.

“Ninakuagiza baada ya miezi miwili nitarudi hapa nikute ujenzi umefikia asilimia 65 sababu mmeshindwa na kasi tunayoitaka wakati fedha mmepewa,” alisisitiza Eng. Ngonyani.

Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Kampuni ya China Civil Engineering CONsturtcion Corporation (CCECC), Bw. Martin Bai amemuhakikishia Eng. Nyongani kuwa watakwenda na kasi kwani wameongeza idadi ya vifaa vya kufanyia kazi na kuahidi atakaporudi ataona maendeleo makubwa.

RAIS DKT JONH MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBI RAMBI WAZIRI DKT MWAKYEMBE KWA KUFIWA NA MKEWE

0
0

RAIS DKT MAGUFULI ASALI CHATO NA KUCHANGISHA KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA

0
0
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na mke wake Mama Janeth Magufuli wakitoa sadaka wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita, leo julai 16, 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mkewe Janeth Magufuli wakisikiliza mahubiri toka kwa Padri Henry Mulinganisa wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita, leo Julai 16 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisisitiza jambo wakati wa ibada ya jumapili katika kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita.Leo 16 julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka toka kwa Mke wake Bi Janeth Magufuli wakati wa kuchangia ujenzi na upanuzi wa katika kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita, leo Julai 16, 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli aliyeshika kikapu cha sadaka akipokea sadaka kutoka kwa waumini wakati wa kuchangia ujenzi na upanuzi wa katika kanisa la Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa ameshika kikapu chenye michango ya fedha zilizotolewa na waumini wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa hilo, leo Julai 16, 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Mwita Chacha mara baada ya kuchangia mifuko mitano ya saruji kwaaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita .
Mama Janeth Magufuli mke wa Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiahidi mchango wake wa ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akishuhudia mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Deogratius Ambrosi mwenye ulemavu wa mkono,akitoa mchango wake wa kiasi cha shilingi elfu tano kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimshukuru mmoja wa waumini wa kanisa hilo ndugu Deogratius Ambrosi mwenye ulemavu wa mkono,akitoa mchango wake wa kiasi cha shilingi elfu tano kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwashukuru waumini walioshiki kuchangia ya ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita,ambapo zilikusanywa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni kumi na tatu pamoja na ahadi mbalimbali za vikiwemo vifaa vya ujenzi.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa nje ya kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita, ambalo linaendelea kupanuliwa na kujengwa hapo akielekea kuwasalimia waumini walio kuwa nje ya kanisa na kuwaaga baada ya ibada.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiondoka kwenye kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita, mara baada ya ibada.
Katibu wa Rais Ndugu Ngusa Samike (kushoto) akikabidhi mchango wa Mhe Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli jumla ya shilingi milioni kumi kwaajili ya ujenzi na upanuzi wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita,
Waumini wa kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita wakiwa kwenye ibada.
Jengo la kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita linaloendelea kupanuliwa na kujengwa
Waumini wa kanisa Katoliki la Bikira MariaParokia ya Chato Mkoani Geita wakitoka kwenye ibada ya jumapili. (PICHA NA IKULU)

Fredy Nyari wa Kigamboni achomoza na Milioni 20 za Biko

0
0

MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo amefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutesa hapa nchini.
Droo iliyompa ushindi mnono mkazi huyo wa Kigamboni maarufu kama ‘Jumadili’, imechezeshwa jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.

Akizungumza katika droo hiyo ya aina yake, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kumpata mshindi wao wa Kigamboni ni sehemu ya kuhakikisha kuwa washindi wao wanaendelea kuzoa mamilioni kutoka kwao baada ya kucheza Biko.
Alisema kila anayecheza Biko anasehemu kubwa ya kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo pamoja kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja bila kusahau donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka katika droo kubwa za Jumatano na Jumapili.
“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu mchezo wetu wa kubahatisha unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kupitia miamala ya kifedha kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.
“Ili mtu aweze kushinda anapaswa kucheza mara nyingi zaidi kwa kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo mbali na ushindi wa papo kwa hapo unaotoka kila wakati, pia ni fursa nzuri ya droo kubwa ya Sh Milioni 20 ambazo tunaamini mtu akifanikiwa kuzipata kama alivyopata mshindi wetu wa Kigamboni bwana Nyari maisha yake yatapiga hatua kubwa,” Alisema.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, alimpongeza Nyari wa Kigamboni kwa kuwa mmoja kati ya vijana wadogo wanaoibuka na mamilioni ya Biko tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu inayotesa nchini inayochezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi.
“Kuwapo kwetu katika droo kuna maana kuwa bahati nasibu hii ni halali na ina nia njema kwa Watanzania, hivyo tunawajulisha Watanzania wote juu ya kutumia michezo kama hii ili kuboresha kipato chao endapo mtu atafanikiwa kushinda zawadi mbalimbali kama wanavyoshinda watu tofauti kutoka kila pembe za nchi yetu ya Tanzania,” Alisema.
Wiki iliyopita, mshindi wa Morogoro Mjini, Elizabeth Damian alifanikiwa kukabidhiwa zawadi yake ya Sh Milioni 20 ikiwa ni siku moja baada ya kutangazwa mshindi katika droo ya 22 ya Biko, huku bahati nasibu hiyo ikiweza kuwapa washindi zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi miwili ya Mei na Juni pekee kama sehemu ya ushindi wa pesa mbalimbali walizoshinda.

Mwakilishyi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid kushoto akiandika dondoo muhimu katika droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku' leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Temeke, Fredy Nyari alifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko. Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.
Picha na Mpigapicha Wetu.
Harakati za kumtafuta mshindi wa droo ya 23 Fredy Nyari wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, zilipofikia ukomo kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja kutoa neno kwa wadau na Watanzania kwa ujumla juu ya bahati nasibu ya Biko.

.

PROF. MBARAWA ATOA MIEZI 10 KWA MKANDARASI CICO

0
0
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndibalinze, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa barabara ya Tabora –Nyahua KM 85, wakati alipokagua ujenzi wake, Mkoani humo jana.
Muonekano wa sehemu ya KM 6 ya barabara ya Tabora–Nyahua yenye jumla ya urefu wa KM 85, inayojengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitazama mchoro wa ujenzi wa kalvati itakayojengwa katika barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30, Mkoani humo jana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi anayesimamia ujenzi wa barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30 Eng. Golam Shahid, kumaliza mradi huo kwa viwango na ubora unaostahili, Mkoani humo jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw. Abeli Busalama, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, wakati alipokuwa akikagua barabara ya Kaliua-Kazilambwa yenye urefu wa KM 56 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani humo jana.

……………………………………………………………………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amempa muda wa miezi kumi Mkandarasi wa Kampuni ya CICO anayejenga barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30 kwa kiwango cha lami kukamilisha kazi hiyo.

Prof. Mbarawa ameyasema hayo mkoani Tabora mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kuelezea kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake.

“Nakupa miezi kumi tangu sasa hadi mwezi Mei mwakani uwe umeikabidhi Serikali barabara hii”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa ukamilishaji wa barabara hiyo uendane na viwango na ubora vinavyoendana na thamani ya fedha waliyopewa ili barabara hiyo iweze kudumu kwa muda uliopangwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mwalimu Queen Mlozi, amemshukuru Waziri Prof. Mbarawa kwa kuufuatilia kwa karibu mradi huo ambao utachochea kasi ya maendeleo mkoani humo.

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndabalinze, amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa atamsimamia mkandarasi huyo kikamilifu ili barabara hiyo ikamilike katika kipindi cha miezi kumi.

Pia, Waziri Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Tabora-Nyahua yenye urefu wa KM 85 na kumtaka mkandarasi CICO anayejenga barabara hiyo kukamilisha KM 6 zilizobaki ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa amempongeza Mkandarasi CHICO anayejenga barabara ya Kaliua-Kazilambwa yenye urefu wa KM 56 iliyokamilika kwa kiwango cha lami na kusisitiza wananchi kuilinda na kuitunza barabara hiyo kwa kutoiharibu miundombinu yake.

Ametoa nafasi nyingine kwa mkandarasi huyo kuomba kazi nyingine za ujenzi wa barabara katika maeneo mengine mbalimbali ya nchi kwani utendaji wao ni wa viwango na wanamaliza kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Bw. Abel Busalama, ameipongeza Serikali kwa jitahada zake za kufungua Mikoa na Wilaya nchini kwa kujenga barabara za lami kwani barabara hiyo imefungua shughuli za kiuchumi na kimaendeleo wilayani kwake.

Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya kukagua miradi ya miundombinu iliyopo mkoani Tabora.

WATANZANIA KUACHANA NA NGUO ZA MITUMBA-MAJALIWA

0
0

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akingalia mitambo ya kutengeneza Nguo katika Kiwanda cha NIDA kilichopo Jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu alifanya ziara katika kiwanda hicho Jumamosi 15 july 2017 kushoto anaye toa maelezo ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza Nguo cha NIDA Bwana Muhammadhamza Rafiki na kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha NIDA Bwana Muhammad Waseem ,Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katikati akionyeshwa Ubora wa Kanga zinazo tengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha NIDA wakati alipofanya ziara Jumamosi 15 july 2017 katika kiwanda hicho kilichopo Jijini Dar es salaam wanao muonyesha kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza Nguo cha NIDA Bwana Muhammadhamza Rafiki na kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha NIDA Bwana Muhammad Waseem

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

……………………………………………………………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.

Pia amesema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika hivyo amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda vipate malighafi.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Julai 15, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar Es Salaam.

Alisema viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.

Alisema kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.

“Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”

Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji ya nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.

Katika kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani 700,000 kwa mwaka kimeajiri watu 2000 na kinalipa kodi ya sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe waadilifu.

Pia Waziti Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUDHURIA MSIBA WA LINAH MWAKYEMBE

0
0

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri  Julai 16, 2017.
 Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa, akisaini kitabu cha maombolezo,alip hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri Julai 16, 2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe, alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mke wa Dr. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe, aliyefariki katika Hospitali ya Agakhan leo alfajiri Julai 16, 2017. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RC SHINYANGA AKABIDHI MWENGE WA UHURU RC TABORA, MIRADI KABAMBE YAPITIWA SHINYANGA

0
0
 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa ili aukabidhi mwenge huo kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mheshimiwa Aggrey Mwanri (wa kwanza kushoto) leo Jumapili Julai 16,2017katika Kijiji cha Sigiri kata ya Sigiri halmashauri ya wilaya ya Nzega -Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mheshimiwa Aggrey Mwanri.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akitoa hotuba fupi kuhusu mbio za mwenge mkoani Shinyanga wakati akikabidhi mwenge huo kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mheshimiwa Aggrey Mwanri.Kulia ni Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour.
Mwenge wa uhuru ukiwa katika kijiji cha Sigiri kata ya Sigiri Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora ambapo makabidhiano yamefanyika
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio baada ya kumaliza mbio za mwenge mkoani Shinyanga,wakijiandaa kukabidhi mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Tabora.
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakifurahia eneo la tukio
Viongozi wakiendelea kufurahia kwa kumaliza salama mbio za mwenge mkoani Shinyanga.
Wakimbiza mwenge wakipiga ngoma eneo la makabidhiano
Viongozi wa mkoa wa Tabora wakijiandaa kupokea mwenge wa uhuru ili ukimbizwe katika mkoa huo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akitoa hotuba fupi kuhusu mbio za mwenge mkoani Shinyanga 
Wakimbiza mwenge wa uhuru wakiwa eneo la tukio
Viongozi wa mkoa wa Shinyanga wakiwa eneo la makabidhiano
Tunafuatilia kinachoendelea hapa…
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akitoa hotuba fupi kuhusu mbio za mwenge mkoani Shinyanga 
Mmoja wa wakimbiza Mwenge akishikana mkono na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack 
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akizungumza eneo la tukio ambapo alisema kati ya miradi yote aliyoipitia mkoani Shinyanga,hakuna mradi alioukataa
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Mkuu wa mkoa wa Tabora,Aggrey Mwanri akimkaribisha Tabora Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa ili aukabidhi mwenge huo kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mheshimiwa Aggrey Mwanri (wa kwanza kushoto)
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akikabidhi Mwengewa Uhuru kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mheshimiwa Aggrey Mwanri
Zoezi la makabidhiano likiendelea
Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mheshimiwa Aggrey Mwanri akisoma taarifa ya miradi ya maendeleo itakayozinduliwa na mwenge wa uhuru mkoani humo
Viongozi wa mkoa wa Tabora wakijiandaa kukimbiza mwenge wa uhuru
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,mheshimiwa Josephine Matiro akiwa na mkuu wa wilaya ya Tabora,mheshimiwa Queen Mlozi wakipiga kumbukumbu
Viongozi wilayani Kahama na Shinyanga wakibadilishana mawazo baada ya zoezi la kukabidhi mwenge wa uhuru kumalizika.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Viewing all 46129 articles
Browse latest View live




Latest Images