Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1305 | 1306 | (Page 1307) | 1308 | 1309 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Kaimu Afisa wa mafunzo Kikosi cha Zimamoto Zanzibar Inspekta Ibrahim Ali Hassan akionyesha utaratibu bora wa kubeba chupa ya gesi kwa ajili ya kuzima moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.
   Mmoja wa wafanyakazi wa bohari kuu ya dawa Zanzibar Ali Othman Omar (kushoto) akiuliza suala kuhusu matumizi sahihi ya mtungi wa kuzimia moto katika mafunzo hayo.
   Mkurugenzi Idara ya Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahrani Ali Hamad akifungua mafunzo ya siku moja ya kukabiliana na janga la moto kwa wafanyakazi wa Idara hiyo Ofisini kwao Maruhubi Mjini Zanzibar.

  Fatma Omar Said akiwa katika mafunzo ya vitendo ya kukabiliana na janga la moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar yaliyofanyika Maruhubi Mjini Zanzibar.
  Picha na Makame Mshenga.

  Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
  Sehemu zenye mikusanyiko ya watu zikiwemo Taasisi za Serikali na watu binafsi zinatakiwa kuwa na vifaa vya huduma ya kwanza vya kupambana na janga la moto na watu wenye taaluma ya kutumia vifaa hivyo.

  Kaimu Afisa wa mafunzo Inspekta Ibrahim Ali Hassan wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar amesema sheria No. 7 ya mwaka 1999 ya Idara hiyo imewapa uwezo wa kuzifungia sehemu hizo iwapo zitashindwa kuweka vifaa na watu wenye uwezo wa kuzima moto.

  Inspecta Ibrahim ametoa maelezo hayo alipokuwa akitoa mafunzo ya kukabiliana na moto kwa wafanyakazi wa Idara ya Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.

  Amesema lengo la kuwepo sheria hiyo ni kujaribu kuokoa maisha ya wananachi na mali zao wakati wa janga la moto ambalo linasababisha athari kubwa katika jamii.

  Hata hivyo amesema bado taasisi nyingi za Serikali na binafsi hazijaona umuhimu wa kuweka vifaa vya huduma ya kwanza vya kuzimia moto na kuwapa mafunzo wafanyakazi wao .

  Ameipongeza Wizara ya Afya kwa kujali kuwapatia mafunzo ya kukabiliana na moto wafanyakazi wa vitengo vyake mbali mbali na kuimarisha huduma hiyo katika taasisi zake kila mwaka.

  Katika kukabiliana na janga la moto, Inspekta Ibrahim Ali Hassan aliwataka wafanyakazi wa bohari kuu kuacha fadhaa na kutumia njia za kitaalamu kwa kuondosha vitu ambavyo havijaanza kuungua, kuunyima moto hewa na kutia maji kwa moto wa kuni.

  Aidha amewashauri wananchi kuanzisha utaratibu wa kuweka chupa ya kuzimia moto katika majumba yao na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kinatoa mafunzo ya matumizi sahihi ya kifaa hicho bila malipo.
  Amesema binadamu hawezi kuishi bila kutegemea moto na moto ni adui mpenzi wa binadamu hivyo tahadhari inahitajika wakati wote katika kujilinda.

  Akizindua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Bohari Kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad ametaka kila  mfanyakazi wa taasisi hiyo kuwa na uwezo wa kujilinda na moto yeye mwenyewe na mali iliyopo ndani.
  Amesema bohari kuu ni taasisi muhimu katika ustawi wa maisha ya wananchi wa Zanzibar na imeweka mkazo kuhusu mafunzo hayo kwa wafanyakazi wote hivyo amewashauri kuyapokea kwa umuhimu wake.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

    Kaimu Afisa wa mafunzo Kikosi cha Zimamoto Zanzibar Inspekta Ibrahim Ali Hassan akionyesha utaratibu bora wa kubeba chupa ya gesi kwa ajili ya kuzima moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.
   Mmoja wa wafanyakazi wa bohari kuu ya dawa Zanzibar Ali Othman Omar (kushoto) akiuliza suala kuhusu matumizi sahihi ya mtungi wa kuzimia moto katika mafunzo hayo.
   Mkurugenzi Idara ya Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahrani Ali Hamad akifungua mafunzo ya siku moja ya kukabiliana na janga la moto kwa wafanyakazi wa Idara hiyo Ofisini kwao Maruhubi Mjini Zanzibar.

  Fatma Omar Said akiwa katika mafunzo ya vitendo ya kukabiliana na janga la moto katika mafunzo ya wafanyakazi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar yaliyofanyika Maruhubi Mjini Zanzibar.
  Picha na Makame Mshenga.

  Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
  Sehemu zenye mikusanyiko ya watu zikiwemo Taasisi za Serikali na watu binafsi zinatakiwa kuwa na vifaa vya huduma ya kwanza vya kupambana na janga la moto na watu wenye taaluma ya kutumia vifaa hivyo.

  Kaimu Afisa wa mafunzo Inspekta Ibrahim Ali Hassan wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar amesema sheria No. 7 ya mwaka 1999 ya Idara hiyo imewapa uwezo wa kuzifungia sehemu hizo iwapo zitashindwa kuweka vifaa na watu wenye uwezo wa kuzima moto.

  Inspecta Ibrahim ametoa maelezo hayo alipokuwa akitoa mafunzo ya kukabiliana na moto kwa wafanyakazi wa Idara ya Bohari Kuu ya dawa Maruhubi.

  Amesema lengo la kuwepo sheria hiyo ni kujaribu kuokoa maisha ya wananachi na mali zao wakati wa janga la moto ambalo linasababisha athari kubwa katika jamii.

  Hata hivyo amesema bado taasisi nyingi za Serikali na binafsi hazijaona umuhimu wa kuweka vifaa vya huduma ya kwanza vya kuzimia moto na kuwapa mafunzo wafanyakazi wao .

  Ameipongeza Wizara ya Afya kwa kujali kuwapatia mafunzo ya kukabiliana na moto wafanyakazi wa vitengo vyake mbali mbali na kuimarisha huduma hiyo katika taasisi zake kila mwaka.

  Katika kukabiliana na janga la moto, Inspekta Ibrahim Ali Hassan aliwataka wafanyakazi wa bohari kuu kuacha fadhaa na kutumia njia za kitaalamu kwa kuondosha vitu ambavyo havijaanza kuungua, kuunyima moto hewa na kutia maji kwa moto wa kuni.

  Aidha amewashauri wananchi kuanzisha utaratibu wa kuweka chupa ya kuzimia moto katika majumba yao na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar kinatoa mafunzo ya matumizi sahihi ya kifaa hicho bila malipo.
  Amesema binadamu hawezi kuishi bila kutegemea moto na moto ni adui mpenzi wa binadamu hivyo tahadhari inahitajika wakati wote katika kujilinda.

  Akizindua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Idara ya Bohari Kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad ametaka kila  mfanyakazi wa taasisi hiyo kuwa na uwezo wa kujilinda na moto yeye mwenyewe na mali iliyopo ndani.
  Amesema bohari kuu ni taasisi muhimu katika ustawi wa maisha ya wananchi wa Zanzibar na imeweka mkazo kuhusu mafunzo hayo kwa wafanyakazi wote hivyo amewashauri kuyapokea kwa umuhimu wake.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 
   
  Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Hifadhi za Tanzania TANAPA, limempatia tuzo nne za Heshima, mwanasayansi na mtafiti wa kimataifa Dkt. Jane Goodall. Dkt. Jane amekabidhiwa tuzo mapema leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Magembe ambazo ni kinyago cha Sokwe, Kitenge, cheti cha heshima na ngao. 

  Tuzo hiyo ya heshima imetolewa maalumu kwa kutambua mchango wake katika masuala ya utafiti na uhifadhi wa Sokwe kwenye hifadhi ya taifa ya Gombe ambao ameufanya kwa zaidi ya miaka 60. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo, Waziri wa Magembe amesema, Tanzania ni nchi ya kwanza ya uhifadhi katika bara Africa. 

  Katika hifadhi zetu za taifa za wanyama mbali mbali ambazo ziko 16, ziko pia, hifadhi za taifa mbili, Gombe na Mahale ambazo wanyama wanaohifadhiwa humo kwa sehemu kubwa ni Sokwe ambapo hata katika dunia hizo mbili ndio hifadhi nzuri kupita zote. Amesema, Kazi kubwa iliyofanywa na mtafiti huyo imeiwezesha jamii kugundua kuwa, Sokwe, wanajitambua na kushirikiana. Wao kama wanyama, wana hisia zao kama viumbe na kama binadamu. 

  Amesema, kabla ya utafiti huo wa Sokwe, na katika ulimwengu wa sayansi binadamu ndio waliokuwa wa wanahisiwa kuwa ndio wenye hisia na kushirikiana kama viumbe wenye akili sana kumbe hata Sokwe kwani wao pia wanatumia nyenzo katika maisha yao. 

  Ameongeza kuwa tafiti anazofanya zimekusanya takwimu zenye maana kubwa sana katika uhifadhi wa Sokwe na pia katika uhifadhi wa wanyama pori. "Kwa mchango wake huu alioutoa, kidunia, kimataifa lakini kwa Tanzania kutoa mchango huu, tumeamua kumtunukia tuzo katika uhifadhi wa wanyamapori na zaidi Sokwe" amesema Waziri Maghembe. 

  Ameongeza, uharibifu wa mazingira unatokana na ukosefu mkubwa wa elimu, kabla ya Sokwe kufanyiwa utafiti huu uliofanywa, tulikuwa tunajua sisi binadamu ni tofauti na Sokwe,kumbe katika vinasaba vyetu kama binadamu asilimia 99 ni sawa sawa na Sokwe, tofauti ni moja asilimia moja tu, ya ubongo wetu na uwezo wetu ndio mkubwa kuliko wao, mambo mingine yote tuko sawa sawa", amesema Magembe. 

  Aidha Waziri amesisitiza kuwa, msimamo wa Serikali katika utafiti huu mgumu uliofanywa na Dkt. Jane ni kuendeleza kazi hizo, kupanua taasisi ya utafiti ya wanyama hao kama binadamu na kuileta iwe na ushirikiano na mashirika ya wanyama pori nchini kama Tanapa, Ngororo na mengineyo na kuhakikisha kazi ya utafiti inaendelea na kutufanya tuzidi kuwa viongozi duniani katika sekta hiyo. 

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Allan Kikazi amesema, Tanapa ina kila sababua ya kumpa tuzo ya Heshima, Dkt, Jane kwani amekuwa akitumia muda wake mwingi sana kufanya utafiti na kuwapatia taarifa za kutosha zinazowawezesha kujua mienendo na tabia za wanyama aina ya Sokwe ambao unaweza kuwapata kwenye hifadhi ya Gombe iloyopo Kigoma na kwenye Milima ya Mahale pekee. 

  Amesema taarifa hizo zinaisaidia Tanapa kuweka mikakati sahihi juu ya namna ya kusimamia hifadhi ya Gombe na kuwasimamia Sokwe ambao wako katika hatari ya kutoweka, kwani bila taarifa hizi, kungekuwa na uwezekano wa idadi ya wanyama hao kuwa ndogo kuliko sasa ambao wanakadiriwa kuwa zaidi ya 80.

  Pia Dkt. Jane amesaidia kutoa mafunzo na kuwawezesha wafanyakazi wa Tanapa kihakikisha Sokwe wanasimamiwa inavyopaswa. "Idadi ya wanyama walioko ndani ya hifadhi inaonekana inaongezeka lakini pia kama wanyama wanaoonelana kuwa wanaishi kwenye mazingira yao ya asilo wao huwa hawatambui mpaka iliyopo, wamekuwa na tabia ya kutoka na maeneo yaliyopo nje ya hifadhi mengi yameharibiwa na wamekuwa wakiuwawa kwa mambo mbali mbali, lakini tunafanya jitihada kuhakikisha tunaweka mifumo sahihi hata wakiwa nje ya hifadhi', amesema Kikazi. Kwa upande wake Dkt. Jane ameishukuru sana Serikali ya Tanzania na Tanapa kwa kutambua mchango wake.  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika hifadhi mbalimbali na baadaye kujikita katika Hifadhi ya Gombe. Picha zote na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna.  Dkt. Jane Goodall akionyesha cheti chake cha kutambua mchango wake katika Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe.  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, akimkabidhi Tuzo ya Uhifadhi Wanyama aina ya Sokwe, Dkt. Jane Goodall, aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60 katika hifadhi mbalimbali na baadaye kujikita katika Hifadhi ya Gombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanapa, George Waitara na Bi. Gertude Mongella.  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe Profesa Maghembe akizungumza wakati wa hafla ugawaji wa tuzo kwa Dk. Jane Goodall ambaye ametoa mchango mkubwa kwenye sekta ya uhifadhi na kubainisha tabia za sokwe ambazo watu wengi hawazijui. Profesa Maghembe aliongeza kuwa mtafiti huyo ambaye ni raia wa Uingereza amebainisha katika tafiti zake kwamba sokwe wana fikiri na wana hisia kama walivyo binadamu. Picha zote na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna.  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi akitoa machache wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo kwa Dk. Jane Goodall ambaye ni muhifadhi Wanyama aina ya Sokwe aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama hao kwa miaka 60.  Dkt. Jane Goodall, ambaye aliyekuwa akifanya utafiti wa Wanyama aina ya Sokwe kwa miaka 60 akitoa shukrani za pekee.    Wageni waalikwa waliofika kuhudhuria hafla hiyo. 

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda ( kushoto) akikabidhiwa Computer 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joseph Kimisha kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa.

  Baadhi ya Kompyuta hizo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (wakwanza kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiwa Computer 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na kampuni ya ulinzi ya TAMOBA kama namna ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri

  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa kizungumza mchache katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.


  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda amepokea Kompyuta 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 kutoka kwa kampuni ya ulinzi ya TAMOBA,ikiwa kama namna ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri unaofanywa na Ofisi hiyo.

  Upatikanaji wa Computer hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya shauku na utafutaji wa RC Makonda kwa ajili ya kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wa Dar es Salaam, ambapo itakumbukwa hivi karibuni Mh.Makonda alifanya mkutano na Watumishi wa sekta ya Ardhi wa Manispaa zote na moja ya kero kubwa iliyo bainishwa kuwasumbua wananchi ni namna ya kupata kibali cha ujenzi jambo lililomkera RC Makonda.

  Kucheleweshwa kwa huduma ya namna hii kwa wananchi huchochea utoaji Rushwa na ujenzi holela bila vibali unaosababisha Serikali kupoteza kodi ya viwanja na kodi zingine zinazohusiana na ardhi.

  Aidha amesema kuwa wananchi wamekuwa wakipata kero mbalimbali ikiwemo ile ya kupewa kibali na manispaa kisha wakaja watu wa zima moto wakakuzuia kuendelea kwa ujenzi sababu hawana taarifa, huku wakati mwingine ukimalizana na watu Zimamoto wanakuja watu wa OSHA nao wanakuzuia usiendelee na ujenzi.

  Hivyo basi badala ya hivi vitengo husika nane kuwa sehemu moja (one stop center) badala yake vimetawanyika na kuwa kero na usumbufu kwa wananchi hasa wanaotaka kufuata taratibu.

  kutokana na sababu zote hizo,Makonda ameamua kutengeneza mfumo mpya utakaomwezesha mwananchi kutokwenda kupanga foleni Manispaa yoyote ile, anapotaka kibali cha ujenzi badala yake anaweza kutuma kwa njia ya mtandao na vitengo vyote vinane vikapokea taarifa hizo kwa wakati mmoja na kumfanya kila mwenye kitengo chake kuwajibika kwa wakati pasipokuwa na kisingizio cha kupoteza taarifa za wateja, urasimu na hata lugha mbaya kwa wananchi wanaotaka huduma ya Serikali.

  Aidha mfumo huo utamwezesha Mkuu wa Mkoa kuona nani anakwamisha utendaji ili hatua za haraka zichukuliwe na mwananchi apate huduma ya haraka.

  Mfumo huu pia utamwezesha mwananchi kutuma kero inayohusu huduma ya ardhi popote alipo na ikapatiwa ufumbuzi pasipo yeye kuhangaika.

  Mkuu wa Mkoa ameahidi pia kuwapatia Pikipiki 50 watendaji wa idara ya ardhi ili waweze kufanya safari za haraka kwenda kwenye migogoro ya ardhi pale inapoibuka kabla ya madhara makubwa kutokea.

  “Nataka ifike mahali Mwananchi yoyote Yule bila kujali kipato chake akiomba kibali cha ujenzi apatiwe ndani ya mwezi mmoja,haiwezekani mtu anatuma maombi ya kupata kibali cha ujenzi anazungushwa na hatimae anakata tamaa na mwisho wa siku anajenga bila kibali na kusababisha ujenzi holela.*aliongea Makonda.

  Kwa hiyo ndio maana nikaona twende kwenye mfumo wa kupata kibali cha ujenzi ndani ya muda mfupi na serikali kupata mapato. Nikimaanisha ndani ya mwezi mmoja unatosha kupitia taarifa na kupitia maombi yao ili kamati ya mipango miji ifanye kazi yake ndani ya wakati.” alisisitiza Makonda.

  Sanjari na hayo Mkuu wa Mkoa ameushukuru uongozi wa kampuni ya TAMOBA kwa kutimiza ndoto aliyonayo na kueleza kuwa sasa ni wakati wa wataalamu kukamilisha mfumo ili wananchi waanze kupata huduma ya kisasa na aina yake.

  Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa amesema kuwa wameamua kutoa zawadi hizo kwa mkuu wa mkoa ili kusaidia kuboresha shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam huku akionyesha kushangazwa na watanzania wanaoingiza chuki na ubinafsi katika kazi nzuri anayoifanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Joseph Kimisha amesema kuwa kampuni yao inafarijika na namna ofisi ya mkuu wa mkoa inavyoshughulikia kero za wananchi kwa ufanisi na kueleza kuwa wataendelea kushirikiana na ofisi hiyo bega kwa bega.

  0 0


  Kikosi cha timu ya Azam kimeanza mazoezi ikiwa  ni maalumu kabisa katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu ujao, ambapo Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amepanga kutengeneza kikosi kikali kitakachoweza kufanya makubwa katika siku za usoni.

  Kikosi hicho leo kimeshafanya mazoezi mara mbili, saa 1.00 asubuhi na 3.30 asubuhi na kitamalizia mazoezi mwisho saa 11.00 jioni ndani ya viunga vya Azam Complex, Chamazi.

  Cioaba amesema faida kubwa ya kufanya mazoezi makali hivi sasa ni kuwajenga wachezaji kwenye maeneo mbalimbali, kiufundi uwanjani, stamina na ustahimilivu kwenye kupambana.

  Baada ya kumaliza programu hiyo ya mazoezi, Azam FC itasafiri Julai 20, mwaka huu kuelekea kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ikienda kucheza mechi tatu za kirafiki, ya kwanza ikiwa ya mwaliko dhidi ya Mbeya City, itakayofanyika Julai 22 katika siku watakayokuwa wakisherehekea Mbeya City Day.

  Mechi nyingine za kirafiki itacheza na timu mbili zilizopanda daraja. Njombe Mji Julai 24 mwaka huu mjini Njombe na ikimaliza ziara hiyo kwa kukipiga na Lipuli ya Iringa Julai 26 kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam Julai 27.
   Wachezaji wa Azam wakiwa katika mazoezi leo asubuhi ikiwa ni katika maandalizi ya msimu ujao chini ya  Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba na Iddy Cheche. 
  Wachezaji wa Azam wakiwa katika mazoezi ya viungo leo asubuhi ikiwa ni katika maandalizi ya msimu ujao chini ya  Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba. 


  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe (hawapo pichani) leo alipofanya ziara ya kikazi  katika Kata hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma Jijini Dar es Salaam. 
   Mhudumu wa Afya kutoka Hospitali ya Magomeni Bi. Rukia Mkapa akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Mwalimu Paschal Mugayana kutoka shule ya Sekondari ya Njechele  akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inaendelea kusanifu na kuboresha Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCIMS) ili uweze kutumika kutoa taarifa za msingi kwa watumishi  wa umma wengi zaidi kwa lengo la kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika sekta ya umma nchini.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya  Kinondoni – Kata ya Kawe, jijini Dar es Salaam.
  Mhe. Kairuki amesema Mfumo wa HCIMS awali ulikuwa unapatikana Ofisi ya Rais–Utumishi pekee, lakini baadae ukakasimishwa kwa Maafisa Utumishi lakini sasa lengo ni kuwafikia watumishi wa umma waweze kuona taarifa zao ili kupata taarifa sahihi na za uhakika katika kanzidata. 

  Amesema Tovuti ya Watumishi, Watumishi Portal, imeanzishwa maalum ili watumishi wa umma wajisajili kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais-Utumishi yenye anuani www.utumishi.go.tz na kuona taarifa zao za msingi.
  Waziri Kairuki, pamoja na hilo, amesema mfumo wa HCIMS umegatuliwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hivi sasa ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kufanya maamuzi kwa haraka zaidi.
   “Kwa kuwa mahitaji ya watumishi wa umma ni mengi hivyo tumeona ni vema tukakasimu Mfumo huu na kwa watumishi wa umma katika kada nyingine ili kurahisisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko” Mhe. Kairuki amesema.
  Waziri Kairuki ameongeza kuwa tayari mafunzo kuhusu namna ya kutumia mfumo yalikwishatolewa kwa Maafisa Elimu na Makatibu wa Afya wapatao 633.
   “Tumeamua kuanza na sekta hizi kwa sababu ni sekta zenye watumishi wa umma wengi zaidi ukilinganisha na sekta nyingine lakini tutaendelea kugatua mfumo wa HCIMS ili ufike katika sehemu nyingi zaidi za kutolea huduma (Service Delivery Points).” Mhe. Kairuki ameongeza.
  Mhe, Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam, ambapo leo ni siku yake ya tano aliyoitumia kukutana na Watendaji na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe.
  Lengo la ziara ni kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini. 

  IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
  OFISI YA RAIS-UTUMISHI
  14.07.2017

  0 0  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuweka mikakati endelevu ili kuwezesha kiwanja cha ndege cha Tabora kujisimamia na kujiendesha kutokana na miundombinu bora na ya kisasa inayoendelea kujengwa kiwanjani hapo.

  Amezungumza hayo jana mkoani humo, mara baada ya kuanza ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Prof. Mbarawa amekagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho ambapo mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 96 na umegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 27.

  “Hivi sasa huduma ya usafiri wa ndege katika kiwanja hichi unaridhisha, hivyo ongezeni ubunifu ili kuvutia abiria wengi na kuwezesha kiwanja kujiendesha”, amesema Prof. Mbarawa.

  Amesisitiza kuwa gharama za usafiri wa anga zitaendelea kupungua kadri huduma na ubora zitavyokuwa zinaendelea kuongezeka ili kuwezesha abiria wengi zaidi kutumia usafiri huo na hivyo kuwezesha pato la Taifa kuongezeka.

  Kwa upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege mkoani Tabora Eng. Danstan Komba amemueleza waziri kuwa idadi ya abiria wanaotumia kiwanja cha ndege hicho imeongezeka kutoka asilimia 10 kwa mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 62.3 mwaka 2016 kutokana na ndege za ATCL kuanza safari zake mkoani humo.

  Aidha, ameongeza kuwa baada ya mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho kukamilika, mashirika ya ndege yataongeza safari zake mkoani humo kwa kuzingatia uwepo wa miundombinu bora yenye kukidhi mahitaji na hivyo itatoa chachu ya maendeleo kwa wakazi wake na kuboresha shughuli za kiuchumi na kijamii.

  Naye, Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja hicho Eng. Neema Joseph, amemuahidi Waziri Prof. Mbarawa kumsimamia mkandarasi kumalizia kazi zilizobaki uwanjani hapo ndani ya siku 14 na kwa kuzingatia viwango na ubora.

  Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa amezungumza na viongozi na wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na kusisitiza kufanya kazi kwa kuzingatia uaminifu, weledi, kasi na uzalendo ili kuendeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kufikia uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

  Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili ya kukagua miradi ya miundombinu iliyopo mkoani Tabora.
   
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Kaya-Ceytun JV Eng. Ifran Sakrak (kushoto), wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanja cha ndege cha Tabora, jana.
  Muonekano wa Taa za kuongozea ndege wakati wa kutua zilizojengewa katika Kiwanja cha Ndege cha Tabora.
  Muonekano wa Mtambo wa kisasa wa kuongoza ndege unaonesha mwelekeo na umbali wa zaidi ya Kilomita 200 uliopo katika kiwanja cha ndege cha Tabora.

  Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Tabora Eng. Neema Joseph, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo ya ujenzi yaliyofikiwa kiwanjani hapo, wakati akikagua ujenzi wake, mkoani humo jana.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mradi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Tabora Eng. Neema Joseph, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanja hicho uwanjani hapo, jana.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiwasili na ndege aina ya Bombadier Q400 ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), mkoani Tabora katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo jana.

  0 0


  Na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna. 

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungulia vituo vya mafuta vipatavyo vitatu jijini Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti ya kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta (Automatic EFD).

  Akizungumza mara baada ya kufungua vituo hivyo, Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere amewashukuru wamiliki wa vituo hivyo kwa kuonyesha ushirikiano kwa serikali kwa kutimiza masharti waliyopewa ya kufunga mashine hizo na kusisitiza kuwa hakuna kituo kitakachofunguliwa kama hakitatimiza masharti. 

  "Niwaombe wamiliki wa vituo vilivyofungiwa kuwa kwa sasa hakuna kitakachofunguliwa bila kutimiza mashart, timiza masharti tuje tukague na tukufungulie uanze biashara yako," amesema Kamishna Kichere. Amesema vituo vilivyofunguliwa leo ni GBP kilichopo eneo la Majumba Sita, Simba Oil kilichopo eneo la Sitakishari, Ukonga na PETRO kilichopo eneo la Kigamboni. 

  "Kitendo cha kuunganisha mashine hizi na pampu za mafuta ni cha muda mfupi sana na wala hakichukui muda mrefu, angalia huyu tulimfungia siku ya jumanne tarehe 11 Julai na leo Ijumaa Julai 14 ameshafunga mashine na anaanza kufanya biashara bila kugombana na serikali;" amesema Kamishna Kichere. 

  Mpaka sasa vituo zaidi ya 40 vimefungiwa nchi nzima ikiwemo jijini Dar es Salaam kwa kosa la kushindwa kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta (Automatic EFD).  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikata utepe katika kituo cha mafuta cha Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kutimiza masharti ya kufunga mashine za kielekitroniki zinazotoa risiti moja kwa moja kutoka kwenye pampu ya mafuta. 
  Mfanyakazi wa kituo cha mafuta cha Kigamboni akitoa risiti mara baada ya kuuza mafuta. 
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikagua risiti mara baada ya kuuza mafuta.

   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akiuza mafuta katika kituo cha GBP kilichopo uwanja wa ndege mara baada ya kukifungulia.

  0 0


  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,wa pili kulia jana alipata fursa ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira na wa kwanza kulia ni Meneja mkuu Kilimanjaro Machine Tools Eng.Adriano Nyaluke akitoa taarifa za uzalishaji wa kiwanda hicho(Picha na Pamela Mollel Arusha).
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama akiteta jambo na wakurugenzi wa mifuko ya jamii jana katika ziara yake katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC),Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh..Daud Msangi ,kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF Mh. William Erio
  Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa GEPF Mh..Daud Msangiakizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho,alisema mfuko wa hifadhi ya jamii ya GEPF umeshakamilisha mkopo wa bilion 1.6 kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kutengeneza kinu cha kuyeyushia vyuma,kukarabati mfumo wa umeme,pamoja na kununua maligafi
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiwa anatoa maelekezo katika kiwanda hicho ambapo alisema kuboreshwa kwa kiwanda hicho kitasaidia ajira kwa vijana
  Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Wizara ya viwanda,Biashara na Uwekezaji Eng.Elli Pallangyo akitoa ufafanuzi kwa Waziri.
  Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam akiangalia baadhi ya vyuma vilivyo zalishwa katika kiwanda hicho


  Kaimu Mkurugenzi mwendeshaji shirikisho la Taifa Maendeleo (NDC)Mh.Ramson Mwilangali akitoa maelezo kwa Waziri jana Mkoani Kilimanjaro
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira akizungumza mara baada ya kutembelea kiwnda hicho amabapo alisema anaunga mkono jitihada za serikali katika kufufua viwnda hapa Nchini
  Mashine za uzalishaji
  Wa kwanza kushoto ni Joseph Mrina Ambaye ni kiongozi mkuu ndani ya kiwanda hicho akiwa Anna Mosha ambaye yeye ni Fundi wa mashine wakionyesha moja ya mashine ya kuranda mbao waliyoitengeneza hivi karibuni
  Wakurugenzi wa Key Media Arusha Sara Keiya na Anna Keiya wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagam jana Mkoani Kilimanjaro

  Moja ya wafanyakazi katika kiwanda hicho akiendelea na uzalishaji

  Katibu wa shirikisho la mifuko ya hifadhi ya jamii Nchini (TSSA)Meshach Bandewa akitoa utambulisho kwa Waziri jana .

  Serikali ipo katika hatua za mwisho katika kuhidhinisha bilioni 1.6 kutoka katika mfuko wa hifadhi za jamii GEPF kwaajili ya kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma katika kiwanda cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools Limited (KMTC).

  Akizungumza jana katika kiwanda hicho mara baada ya kutembelea Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh.Jenista Joakim Mhagama,alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwaajili ya kuboresha kiwanda hicho kwa lengo la kufufua kwa kuwa kiwanda hicho kinabeba dhana nzima ya maendeleo ya uchumi wa viwanda kwenye nchi ya Tanzania

  Alisema kuwa mfuko wa GEPF baada ya kupokea maagizo kutoka kwa Rais akihimiza Serikali ya viwanda ,wameweza kujiridhisha kuwa wanauwezo wa kuwekeza katika kiwanda hicho cha kutengeneza vipuri na mashine cha Kilimanjaro Machine Tools (KMTC)

  Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa Pensheni wa GEPF Daud Msangi alisema kuwa katika uwekezaji huo kiwanda hicho kitaweza kujenga kinu cha kuyeyushia vyuma ambayo ndio maligafi yao kubwa ya kuchonga vipuri na mashine mabalimbali

  Aidha aliongeza kuwa kiwnda hicho kinakabiliwa na chagamoto ya umeme ambapo pesa hizo zitatumika katika kukarabati mfumo wa umeme katika kiwanda hicho


  0 0

    Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee kulia, akimkabidhi Elizabert Tungu baiskeli (Wheel chair) kwa ajili ya  mwanaye Malale Mihayo (aliyekaa) ambaye ana tatizo la mtindio wa ubongo.Kushoto ni Abass Meghjee mmoja wa wafadhili na kiongozi wa taasisi hiyo yenye makao makuu nchini Uingereza. 
   Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foudation Tawi la Tanzania Sibtain Meghjee akimsaidia kumsukuma Malale Mihayo mkazi wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga baada ya kumkabidhi msaada wa baiskeli (Wheel chair) itakayomsaidia kwa usafiri. Mtoto huyo ana tatizo la mtindio wa ubongo.

  Na Baltazar Mashaka, Mwanza
  Familia ya mtoto Malale Mihayo (12) yenye makazi yake katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imeishukuru Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) Tawi la Tanzania kwa msaada wa baiskeli (Wheel Chair ) kwa ajili ya mtoto wao mwenye tatizo la Cerebral Polse (mtindio wa ubongo).

  Akizungumza na mtandao huu baada ya kukabidhiwa baiskeli hiyo mama mzazi wa mtoto huyo Elizabert Tungu alisema  itampunguzia adha ya kumbeba mwanaye huyo ambaye hana uwezo wa kufanya chochote kutokana na tatizo alilonalo.

  “ Mwanangu alizaliwa  mwaka 2008 akiwa mzima wa afya, alipata tatizo hili baadaye akiwa na umri  wa miaka 3 na nusu.Nilimpeleka kutibiwa hospitali huko Arusha na Moshi madaktari wakanieleza anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo, licha ya kutibiwa hakupata nafuu.Nawashukuru Desk & Chair kwa msaada huu,”alisema.

  Bi. Tungu mwenye familia ya watoto sita alisema alimpeleka kwa waganga wa tiba za jadi nako hakupata nafuu na hivyo akalazimika kurejea nyumbani ambapo mwanaye huyo aliendelea kukakamaa viungo vya mwili wake na kupoteza uwezo wa kukaa wala kutembea.

  Mtaalamu wa viungo (Physiotherapy) Prisla Paul Mselle alisema Malale alipata tatizo la kukosekana hewa ya oksjeni kwenye ubongo linalosababishwa na uzazi pingamizi  na homa kali kwa  watoto wa umri chini ya miaka mitano na kushambulia tishu ya ubongo kwa kuwa ubongo unakuwa haujakomaa.

  Alisema kuwa mtoto huyo kupinda mgongo kumesababishwa na kuchelewa kupata tiba haraka  na hivyo anaweza kupata nafuu kwa kupata vifaa saidizi vya kuchechemua misuli yake ambavyo kwa kitaalamu ni standing board, stratching na standing table lakini hawezi kupona.

  “ Baada ya kumbaini mtoto huyo niliangalia uwezo wake na kumwanzishia mazoezi ya kumnyoosha viungo kama magoti, vifundo vya miguu kwa kutumia vifaa vya kitaalamu ambavyo baadhi ni changamoto.Watoto wenye matatizo haya ni wengi changamoto ni kuwabaini,”alisema.

  Mtaalamu huyo alieleza kuwa inahitajika elimu ya kutosha kwa jamii nyumba kwa nyumna ili kuweza kuwafichua na kuwabaini watoto wengi wenye ulemavu ambao wanafichwa kwa sababu ya mila potofu kuwa kuzaa mtoto mlemevu ni laana, mikosi pamoja na imani za ushirikina.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation Sibtain Meghjee alisema mtoto huyo ingawa amesaidiwa baiskeli hiyo anakabiliwa na changamoto ya mavazi na mahitaji mengine na kumtaka mzazi wake kumfungulia akaunti huku akiwaomba wadau wengine wajitokeze kumsaidia mtoto huyo kwa hali na mali kwa sababu matunzo yake ni tofauti na ya watoto wengine.

  Alisema taasisi hiyo itaendelea kumsaidia lakini kutokana na changamoto ya kuwaibua watoto wenye matatizo hayo aliishauri serikali kuwa na mpango mahsusi wa kuwabaini watoto wenye matatizo ya aina hiyo na kuweka takwimu zao ili kurahisisha jinsi ya kuwahudumia na kuwapa misaada.

  0 0


  Ijumaa Julai 15,2017,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack ametembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya mchele kinachomilikiwa na kampuni ya Mwekezaji kutoka nchi ya China Jielong Holding kilichopo katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.

  Mkuu huyo wa mkoa aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na maafisa mbalimbali mkoa huo amejionea jinsi kampuni hiyo ilivyodhamiria kuzalisha mafuta ya kupikia yanatokana na mapumba laini ya mpunga “Mchele”.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Telack alisema kiwanda hicho ni cha pekee nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla na kitasaidia wamiliki wa mashine za kukobolea mpunga pamoja na wakulima kunufaika na zao la mpunga kwani wataweza kuuza mapumba kwa ajili ya kutumika kama malighafi kuzalishia mafuta hayo.

  “Niwapongeze wawekezaji hawa kwa ubunifu huu wa kiwanda cha aina yake, serikali ya mkoa wa Shinyanga inaunga mkono jitihada za kuhakikisha tunakuwa na uchumi wa viwanda,tushirikiana kuwahamasisha wananchi kulima mpunga kwa wingi na wale wenye mpunga basi wauze mapumba yao ili wajipatie kipato”,alieleza Telack.

  “Naamini watu wenye mashine za kukobolea mpunga wataongeza kipato kwa kuuza mabaki ya mpunga kwa ajili ya kuendeshea kiwanda hiki ambacho pia kinazalisha nishati ya umeme kwa kutumia mapumba”,alieleza Telack.

  Aidha aliwahamasisha wamiliki wa kampuni ya Jielong Holding kununua mapumba ya mchele kwani katika maeneo mbalimbali mkoani Shinyanga ili kiwanda hicho kianze kufanya kazi mara moja.

  Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kampuni ya Jielong Holding, Qi Shuwei aliiomba serikali kuendelea kushirikiana na kampuni hiyo na pale panapojitokeza mapungufu basi serikali iwape ushauri kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

  “Tunaishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa viwanda,lengo kampuni yetu inayojihusiha na mazao hususani uzalishaji wa mafuta ya alizeti,pamba na mchele na kutengeneza sabuni ni kuwainua kiuchumi wananchi kupitia mazao wanayolima”,alisema Shuwei.

  Hata hivyo alisema kiwanda hicho kimekwama kuanza uzalishaji wa mafuta ya mchele kutokana na uhaba wa malighafi kwani zinatakiwa tani 500 za mapumba kwa ajili ya kuanzisha uzalishaji lakini kiwango hicho hakijafika.

  Angalia picha za matukio yaliyojiri wakati wa ziara hiyo kutembelea viwanda mbalimbali ikiwemo kiwanda cha kutengenezea mafuta ya Mchele,alizeti,pamba na sabuni vinavyomilikiwa na kampuni ya Jielong Holding
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia) akitembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya mchele kinachomilikiwa na kampuni ya Mwekezaji kutoka nchi ya China Jielong Holding kilichopo katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga.Kulia kwake ni Mkalimani katika kampuni hiyo Joseph Warioba akifuatiwa na Mwenyekiti wa kampuni Jielong Holding,Qi Qi Shuwei.Wengine ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na maafisa kutoka mkoa huo.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa ndani ya kiwanda cha Jielong Holding.

  Qi Shuwei akiongoza msafara wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuangalia uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotokana na mazao yanayolimwa na wakulima.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiteta jambo na Mwenyekiti wa kampuni Jielong Holding,Qi Qi Shuwei.

  Kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Jielong Holding, Qi Shuwei akimweleza mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack kuhusu kiwanda cha mafuta ya mchele walichokianzisha ambapo watakuwa wananunua mapumba ya mpunga ili kupata mafuta ya kupikia.  Mwenyekiti wa Kampuni ya Jielong Holding, Qi Shuwei akionesha mapumba malaini yaliyoanza kutengenezwa ili kupata mafuta ya kupikia.  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akishika mapumba laini ya mpunga 'mchele' ambayo tayari yapo katika hatua za awali kwa ajili ya kutengeza mafuta ya kupikia.

  Mapumba ya mpunga yakiwa kiwandani.

  Mkuu wa mkoa,waandishi wa habari na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga wakiangalia moto mkali ndani ya kiwanda hicho unaotokana na mapumba/mabaki ya nafaka ambayo yanatumika kutengeneza nishati ya umeme katika kiwanda cha Jielong Holding.Kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Jielong Holding, Qi Shuwei.

  Dirisha dogo lililofunguliwa kuonesha moto mkali.

  Mwenyekiti wa Kampuni ya Jielong Holding, Qi Shuwei akimweleza jambo mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack wakati akimbelea viwanda vya kampuni hiyo.

  Mkalimani katika kiwanda cha Jielong Holding,Joseph Warioba akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack kuhusu malighafi mbalimbali zinazotumika katika kiwanda hicho cha kutengeneza mafuta ya alizeti,pamba,mchele na sabuni.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia zoezi la utengenezaji wa madumu ya plastiki kwa ajili ya kuwekea mafuta yanayotengenezwa katika kiwanda cha Jielong Holding.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia mitambo ya kutengenezea vifungashio vya plastiki/madumu ya mafuta.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa ndani ya kiwanda cha Jielong Holding.  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia ndoo ya plastiki iliyotengenezwa katika kiwanda hicho kwa ajili ya kuwekea mafuta ya alizeti.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akingalia shughuli ya uzalishaji mafuta ya alizeti inavyofanyika.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia mafuta ambayo yako tayari kwa ajili matumizi ya binadamu.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa ndani ya kiwanda hicho.

  Mwenyekiti wa Kampuni ya Jielong Holding, Qi Shuwei akimweleza jambo mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia mitambo ndani ya kiwanda.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiendelea kuangalia mitambo.

  Mfanyakazi wa kiwanda cha Jielong Holding,Joseph Warioba akionesha mitambo ya kutengenezea mafuta mbalimbali.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia sabuni ya gwanji iliyotengenezwa katika kiwanda cha sabuni cha Jielong Holding.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia sabuni.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani wakiangalia miche ya sabuni.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikagua mazingira nje ya viwanda

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiangalia shimo la majitaka.

  Kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Jielong Holding, Qi Shuwei akizungumza baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack kutembelea viwanda vinavyomilikiwa na kampuni ya Jielong Holding.Kushoto ni Mkalimani wa kampuni hiyo Joseph Warioba akitafsiri lugha ya Kichina na Kiswahili.

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza baada ya kutembelea viwanda,

  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa,maafisa mkoa na wafanyakazi wa kampuni ya Jielong Holding wakijadiliana namna ya kufanya ili viwanda viwanufaishe wananchi,wawekezaji na serikali.


  Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

  0 0

  Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru kuhakisha wanaboresha huduma za Afya katika Wilaya hiyo hasa kituo cha Afya Mkasale ambacho kimebainika kuwa na huduma mbovu huku pia kikiwa na uchakavu kwenye majengo yake hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama na afya za watumishi na wagonjwa wanaohudumiwa hapo.

  Akiwa katika ziara ya kikazi ya ukagazi wa utekelezajiwa agizo la uboreshaji wa vituo vya afya katika kila Kata nchini lilitolewa Desemba 2016, Dk. Kigwangalla akikagua kituo hicho cha Mkasale , aliweza kujionea mazingira hayo ambapo licha ya kupewa taarifa alitaka mara moja Uongozi wa Halmashahuri

  hiyo kushughulikia suala ndani ya miezi mitatu ikiwemo Mkandarasi wa Maji kuhakikisha anaingiza mifumo ya maji ndani ya kituo hicho, pia aliagiza uongozi wa kijiji kushiriki katika kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka kituo hicho cha Mkasale.

  Awali akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Tunduru baada ya ziara hiyo ya kukagua vituo vya Afya na Hospitali ya Wilaya, Dk Kigwangalla amesema Serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma za afya na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zenye ubora na kwa wakati na lengo la serikali ya awamu ya tano ni kupunguza kwa asilimia kubwa changamoto zinazoikabili wilaya ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, kukamilisha maboma yote ya vituo vya afya, zahanati na hospitali ambazo hazijakamilika, na kuhakikisha kuwa vifaa tiba na dawa zinapatikana za kutosha.

  “Hata hivyo nawasihi wananchi tumuunge mkono Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa vita aliyoianzisha ya kulinda rasilimali za nchi yetu, kwani taifa limekuwa likiibiwa kwa muda mrefu sana ila umefika muda kuhakikisha kuwa rasimali za nchi zinatunzwa na kulindwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati akiwahutubia wananchi hao.

  Aliendelea kusema kuwa ili mwananchi aweze kushiriki katika shughuliza uzalishaji ni lazima awe na afya njema na ili awe na afya njema ni lazima wananchi kwa kushirikiana na serikali kuboresha vituo vya kutoa huduma za afya na kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.

  “Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha kuwa dawa zinakuwepo za kutosha katika hospitali na vituo vya afya na katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga bajeti ya kutosha kuhakikisha kuwa vifaa tiba vinakuwepo katika vituo vya afya na hospitali zote nchini” Alieleza Dk. Kigwangalla katika mkutano huo.

  Samabamba na hayo serikali inahakikisha kuwa huduma za mama na mtoto zinatolewa bure kwenye hospitali za umma zote nchi ili kupunguza vifo vya wamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

  Dk Kigwangalla aliuagiza uongozi wa kijiji cha mkasale na mkotamo kutengeza barabara ya kuelekea katika kituo cha afya mkasale kutoka na barabara hivyo kuwa chafu sana hali inayoweza kuleta madhara kwa watumiaji hasa kwa wadudu kama nyoka.

  "Nakuagiza mwenyekiti wa kijiji mara baada ya kumaliza kikao hapa upange ratiba na wananchi wako namna bora ya kuweza kutengeza barabara inayokwenda katika kituo cha afya mkasale na pia mupange ratiba ya kufanya ausafi katika kituo kwani kazi ya usafi ni ya wananchi"alisema Dk kigwangalla.

  Aidha, katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma zilizo bora uongozi wa wilaya umeagizwa kufanya kuhakikisha vituo vyote vya afya vilivyopo wilayani Tunduru, vinajenga vyumba vya upasuaji katika vituo vyote vya afya, kukarabati maabara zote, na kuhakikisha kunakuwepo na mfumo wa maji safi wenye uhakika katika vituo vyote vya afya, kufanya matengenezo kwa vifaa vilivopata hitilafu ili kuboresha huduma.
  Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akilakiwa na wananchi wa Kijiji cha Mkasale wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo 
  Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akimsabahi mmoja wa watoto waliofika na wazazi wake wakati wa kumpokea katika Kijiji cha Mkasale wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo.
  Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza katika mkutano huo wa wazi kwa wananchi wa Halmashauri ya Tunduru, Mkoani Ruvuma


  0 0

   Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani akizindua mradi wa Umeme vijijini REA jana Nangale wilaya ya Itilima mkoani Simiyu akiwa ameambatana na viongozi wa mkoa huo.
   Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani akiwasalimia wabunge wa mkoa wa Simiyu wakati wa uzinduzi mradi wa Umeme vijijini REA jana.

   Wabunge  mkoa wa Simiyu  wakicheza na Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani wakati wa uzinduzi mradi wa Umeme vijijini REA jana  ikiwa ni katika kuhakikisha umeme unapatikana nchi nzima na kwa bei nafuu.
   Mbunge wa Itilima Njalu Silanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Umeme vijijini (REA) jana Katika kijiji cha Nangale wilayani Itilima katika mkoa wa Simiyu  ikiwa ni katika kuhakikisha umeme unapatikana nchi nzima na kwa bei nafuu..
    Wananchi  wakiwa wanafuatilia uzinduzi wa mradi wa Umeme vijijini REA jana wakati ulipozinduliwa na Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani ikiwa ni katika kuhakikisha umeme unapatikana nchi nzima na kwa bei nafuu.
  Picha ya pamoja ya wabunge na viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt Medard Kalemani wakati wa uzinduzi wa mradi wa umeme wa vijijini REA jana. .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka na Kulia ni wabunge Esther Midimu (Viti maalum),Mashimba Ndaki Maswa Magharibi na Njalu Silanga wa Itilima  ikiwa  ni muendelezo wa kuhakikisha umeme unapatikana nchi nzima na kwa bei nafuu. 


  0 0

  Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. George Daniel Yambesi (kulia) alipoitambulisha rasmi bodi hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wakimsikiliza Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwatambulisha wajumbe wapya wa bodi ya ushauri waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
  Wajumbe wakimsikiliza Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) jana Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwatambulisha wajumbe wapya wa bodi ya ushauri waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
  Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa wa bodi ya ushauri waTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).


  0 0

  Na Lorietha Laurence -WHSUM.

  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameunda kamati ya wajumbe 10 kwa ajili ya kufuatilia undani wa kutopatikana kwa faida kati ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kampuni ya Star Times kutoka China.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam alisema kuwa kamati hiyo imepewa siku saba kuhakikisha inakuja na taarifa kamili kuhusiana na suala hilo.

  “ nimeipa kamati hii muda wa siku saba ukimalizika siiongezi tena nitatoa labda siku moja mbili kumalizia tu ili inipatie majibu kamili kwa nini kwa miaka yote hiyo hakuna faida”alisema Mwakyembe.

  Aidha Dkt. Mwakyemba anaeleza kuwa uamuzi wa kuunda kamati hiyo ni kutokana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuonyesha kukerwa na kutokupatikana kwa faida kwenye ushirikiano huo wa TBC na Star Times alipofanya ziara yake mwezi Mei mwaka huu.

  Anazidi kufafanua kuwa Rais alikasirishwa na kitendo cha kampuni hiyo kufanya kazi nchini kwa kipindi cha miaka saba bila faida yoyote na hivyo kuagiza hatua stahiki kuchukuliwa juu ya suala hilo.

  Dkt. Mwakyembe anabainisha kuwa tangu kutolewa kwa kauli ya Rais Mhe. Dkt. Magufuli Wizara na watendaji wake tayari wameshafanya mikutano miwili mmoja Mjini Dodoma na mwingine Jijini Dar es Salaam wakajadili kwa kina sababu zinazopelekea kushindwa kupatikana kwa faida.

  Kabla ya mkutano na waandishi wa habari ,Waziri Dkt. Mwakyembe alitumia takribani saa tatu akijadiliana kwa kina na Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times kutokea nchini China, Xinxing Pang pamoja na wafanyakazi wa wizara akiwamo Katibu Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel na Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt.Hassan Abbas.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Star Times Bw. Xinxing Pang alisema kuwa ana imani kuna uwezekano wa kumalizwa kwa suala hilo kwa kutumia wataalamu wake watakaoangalia sababu za kutokupatikana kwa faida na nini kifanyike katika kuondokana na changamoto hiyo.
  Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiongea na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu kutoka Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Times Bw. Xinxing Pang.
  Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo katika picha) alipokuwa akieleza msimamo wa Serikali kuhusiana na Kampuni ya Star Times jana Jijini Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence.)

  0 0

  CHAMA cha riadha Mkoa wa Singida kimeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuzitafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazochangia idadi kubwa ya wanawake kutopenda na kisha kutoshiriki kabisa katika mchezo wa riadha.

  Akitoa ushauri huo kwenye viwanja vya michezo vya shule ya msingi Tambukareli,wilayani Manyoni,Mkoani Singida,mmoja wa washiriki wa mashindano hayo,Hamida Nasoro alisisitiza kuwa kutokana na idadi kubwa ya wanawake kutohamasishwa kushiriki katika mashsindano hayo,ndiko kulikochangia mashindano ya mchezo huo wa riadha kuwa na idadi ndogo ya washirki.

  “Mashindano haya tumeonekana wanawake wachache sana labda ni kwa ajili ya changamoto mbali mbali ikiwemo wanawake wengi kutopenda kujishirikisha katika mchezo wa riadha kunakotokana na ukuaji wao wa umri”alisisitiza Hamida.

  Akizungumza na kituo hiki,Hamida hata hivyo hakusita pia kutoa tahadhari kwa wanawake wanaopenda kushiriki katika mchezo huo wa riadha wasijihusishe katika mahusiano ya kimapenzi kwani endapo wataendelea kufanya hivyo,ndoto zao za mafanikio katika mchezo huo zitapotea.
  Hata hivyo Hamida alitumia fursa ya mashindano hayo kuwashauri wanawake wasiopenda kushiriki mchezo huo wajenge utamaduni wa kupenda kushiriki mchezo huo ili waweze kulitangaza soko la mchezo huo kwa wanawake.

  Kwa upande wake Diana Alphonce kutoka wilaya ya Ikungi pamoja na kuridhishwa na maandalizi ya mashindano hayo ya riadha,lakini hakusita kuwaomba waandaaji wa mashindano hayo,wawahamasishe watu wengi zaidi ili waweze kujitokeza kushiriki mashindano hayo.

  Kwa mujibu wa Diana aliwataka waandaaji hao wa mashindano kuangalia uwezekano wa kuwapatia zawadi washindi wa mashindano hayo ili waweze kuwatia moyo watu wasioupenda mchezo huo ili nao waweze kuona umuhimu wa kushiriki.

  “Katika mashindano haya wawe wanatutia moyo hata angalau watupatie zawadi hata kidogo ili kumhamasisha yule ambaye hajashiriki ili awe na moyo wa kushiriki”alisisitiza mshiriki huyo kutoka wilayani Ikungi.

  Naye mwanamke mwenye umri wa miaka 48 anayeshiriki katika mbio za kilomita 21 na aliyewahi kushiriki katika mashindano ya mbio za nusu marathon,Zainabu Ramadhani aliyataja malengo ya kushiriki katika mashindano hayo kuwa ni pamoja na kujenga mwili,kuwaunga mkono vijana na kuweka reodi nzuri ya ushiriki wake kwenye mchezo wa riadha.
  Baadhi ya washiriki wa mashindano ya mchezo wa riadha wa Mkoa wa Singida walioshiriki mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya michezo vya shule ya msingi Tambukareli,wilayani hapa.
  Mwanamke mwenye umri wa miaka 48,Zainabu Ramaddhani kutoka wilaya ya Ikungi akishiriki mbio za umbali wa kilomita 21 katika mashindano hayo na kufanikiwa kuchaguliwa kwenda kushiriki mashindano ya kimkoa.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikabidhiwa fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mfkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, (kulia), baada ya kufungua semina ya Mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoni Dodoma Julai 14, 2017.
  NA K-VIS BLOG, DODOMA


  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS) na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata Mafao yao wanapostaafu. 

  Mhe. Jafo aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa mkoani Dodoma Julai 14, 2017.Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wastaafu hao watajiwa ili kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali wakati muda wao wa utumishi wa umma utakapokoma.

  Mhe. Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka michango ya wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero kubwa pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia Mafao yao kutokana na taarifa za uwasilishaji michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kutokamilika.

  “Nitoe rai kwa ndugu zangu watumishi wa umma ambao katika kipindi cha miaka miwili ijayo mtaondoka kwenye utumishi wa umma, yatumieni vema mafunzo haya ili mtakapopata mafao yenu basi tayari mtakuwa na nyenzo ya kuwasaidia kutumia vema fedha mtakazopata kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo, lakini pia kilimo na ufugaji wa kisasa na hatimaye kuyafanya maisha yenu kuwa bora baada ya utumishi wa umma.” Aiasa Mhe. Jafo.

  Katika hatua nyingine, wimbi la viongozi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari yaani PSPF Supplementary Scheme, (PSS), Mhe. Jafo naye amejiunga na mpango huo na kuwahamasisha wastaafu hao watarajiwa na wananchi wengine kujiunga na Mpango huo kwani utawawezesha kuwa na hakikisho la kuweka fedha zao ili ziwasaidie kwenye miradi wanayotarajia kuibuni, ikiwa ni pamoja na kujipatia bima ya afya.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu, amebainisha kuwa mfuko huo unatarajia kulipa jumla ya Sh.Trilioni 1.3 katika kipindi cha 2017/18 ambazo ni Mafao ya watumishi 9,552 wanaojiandaa kustaafu katika kipindi cha kati ya Mwaka huu wa 2017 na mwaka ujao wa 2018.
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akitoa hotuba yake. "Mfuko umetenga kiasi cha shilingui Bilioni 1.3 kwa ajili ya kulipa mafao watumishi 9,552 wanaotarajiwa kustaafu kati ya mwaka huu wa 2017/2018."
  Naibu Waziri Jafo akitoa hotuba yake.
  Washiriki wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
  Mzee mstaafu akitoa ushuhuda kwa kundi la wanachama wa Mfuko wa PSPF wanaotarajiwa kustaafu katika semina iliyoandaliwa na mfuko huo mkoani Dodoma.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akitoa hotuba yake mbele ya maafisa wa Magereza pamoja na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, katika Ukumbi wa Magereza Karanga, Mjini Kilimanjaro Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. Waziri Mhagama alifanya ziara ya kutembelea na kukagua eneo la Mradi wa Ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha karanga kilichopo mkoni Kilimanjaro ambacho kipo chini ya Mfuko wa Pesheni wa PPF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini. Kiwanda hicho kilikuwa kinazalisha viatu 150 kwa siku na sasa kinatarajiwa kufikia viatu 400 baada ya kukamilika kwa ukarabati.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwira, Katibu mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Prof. Adof Mkenda pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt, Juma Malewa wakiangalia sehemu ya Bidhaa za Ngozi zinazotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, akichukuliwa kipimo cha mguu kwa ajili ya kutengenezewa Viatu vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakiangalia moja ya mashine za kutengeneza viatu, katika Kiwanda cha Viatu cha Magereza Karanga, Mkoani Kilimanjaro, Julai 14, 2017. Wengine ni Kamishna wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Hassan Bakari Mkwiche pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akitoa taarifa fupi ya uwekezaji uliofanywa na mfuko huo kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika ukarabati wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Magereza Karanga kilichopo Mkoni Kilimanjaro.  0 0


  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajikuta akikesha ofisini kwake pamoja na wananchi takriban 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.

  Mhe. Waziri ametumia takriban saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi. Kazi hiyo ilianza majira ya saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku.

  Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi hao.

  Wananachi wengi wenye matatizo na Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hii ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.

  Wananchi hao wamesifu hatua hii ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea. Nae Bwana Francis Kamara mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam amemuomba Waziri aweze kuwaajibisha watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kupelekea yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.

  Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambao wangependa kumuona, wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es Salaam iliyopo ghorofa ya pili, jengo la Wizara ya Ardhi – Magogoni, Kivukoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.

  Aidha, Mhe. Waziri atafanya ziara kama hii katika kanda nyingine mara baada ya kukamilisha zoezi hilo katika Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.
  Baadhi ya wananchi wa Pwani na Dar es Salaam wakiwa ofisi za Wizara ya ardhi mida ya saa 9 usiku kusubiri kusikilizwa kero zao za ardhi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
  Mkazi wa Goba jijini Dar es salaam Bibi Fatuma Shami akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake kuvamiwa na kupata miliki pandikizi.
  Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani Bibi Mariam Hamis akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake lililo na Mgogoro.
  Baadhi ya wananchi kutoka Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakimueleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu mgogoro wao wa ardhi katika ofisi za Wizara ya ardhi.
  Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Kanda ya Dare s salaam na Pwani waliokesha na Waziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi wakati wa kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi.

older | 1 | .... | 1305 | 1306 | (Page 1307) | 1308 | 1309 | .... | 1897 | newer