Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 128 | 129 | (Page 130) | 131 | 132 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 07/29/13--08:14: CCM YAKOMALIA SERIKALI MBILI
 • VIDEO 2

  0 0

  TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI
  TAREHE 29/07/2013
  Ndugu Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam,

  Napenda nichukue fursa hii kuwajulisha rasmi kwamba Nchi yetu imepata heshima ya kutembelewa na Waziri Mkuu wa Thailand ambaye atawasili Nchini tarehe 30/07/2013.  Ziara hii ni ya kikazi (state visit) na atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kumbukumbu ya Mwalimu J. K. Nyerere majira ya saa 6:30 mchana na kulakiwa na mwenyeji wake Mhe. Rais wetu mpendwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatana na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Mkoa.

  Ndugu Wananchi,
  Baada ya kuwasili Mhe. Waziri Mkuu wa Thailand atakagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na pia atapata fursa ya kukagua vikundi mbalimbali vya ngoma ambavyo vitakuwa vikitumbuiza na kutoa burudani kwa Mgeni wetu na msafara wake.

  Ndugu Wananchi,
  Mgeni wetu baada ya kukagua vikundi vya ngoma na burudani ataondoka kuelekea Ikulu kupitia barabara ya Nyerere, Railway, Gerezani, Sokoine Drive hadi Ikulu. Akiwa Ikulu atasaini mikataba mbalimbali kati ya Serikali ya Tanzania na Thailand. Usiku atashiriki katika dhifa maalumu iliyoandaliwa na Mwenyeji wake.

  Ndugu Wananchi,
  Tunaomba radhi kwamba barabara hizi nilizozitaja zitafungwa kwa muda kupisha misafara ya Viongozi wetu Wakuu watakaoelekea Uwanja wa Ndege wa Kumbukumbu ya  Mwalimu J. K. Nyerere kumlaki Mgeni wetu hususan barabara ya Nyerere kuanzia saa 6.00 mchana hadi saa 7.30 mchana.

  Ndugu Wananchi,
  Tarehe 31/07/2013 Waziri Mkuu wa Thailand atatembelea Mbuga za Wanyama za Serengeti.Tarehe 01/08/2013 atarejea Dar es Salaam na kuagwa rasmi katika Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere na kuendelea na ziara yake huko Uganda.

  Ndugu Wananchi,
  Kama ilivyo ada tunaombwa kumlaki mgeni wetu kwa shangwe na bashasha katika maeneo yote atakayopita.

  Asanteni kwa kunisikiliza.

       Saidi Meck Sadiki
           MKUU WA MKOA
          DAR ES SALAAM

  0 0


  Na Miza Othaman – Maelezo Za nzibar
  Wizara ya kilimo na Maliasili Zanzibar imesema inajukumu la kusimamia
  maendeleo ya uzalishaji wa mazao ya chakula na Biashara katika
  upatikanaji na usambazaji wa huduma za pembejeo na dhana za kilimo kwa
  wakulima.
  uhifadhi na ukaguzi wa mazao na kutowa mafunzo kwa wazalishaji.
  Hayo yameelezwa huko Baraza la Wakilishi na kaimu Waziri wa Kilimo na
  Maliasili Ramadhani Abdalla Shabani wakati alipokuwa akiwasilisha
  Bajeti ya Wizara hiyo ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa
  mwaka  2013/2014 barazani hapo.

  Amesema katika kufikia azma hiyo wizara itazia uimarishaji wa mimea
  kwa kuitia dawa ambapo jumla ya  lita 500 za dawa  za asili
  zimetayarishwa kwa  kuulia wadudu waharibifu wa mimea.

  “ tutatia dawa mimea lakini pia Tutawelimisha wakulima 1500,juu ya
  mbinu zakilimo bora pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi
  kwamabibi/mwabwanashamba 95 juu ya mbinubora za kilimo,”alisema
  waziri.

  Aidha ameeleza kua watazalisha Tani nane za mbegu ya mahindi , tani
  mbili za mbegu yam tama na 570 za mbegu ya mpunga ikiwemo NERICA.

  Waziri huyo alizieleza kua pamoja na hayo wizara inakabiliwa na
  changamota ambazo  ni pamaja na ongezeko kubwa la mahitaji ya mazao ya
  maliasili kuliko uwezo wa udhalilishaji, matumizi mabaya  ya dhana
  yanayopelekea uharibifu wa mazingira ukiwemo msumeno wa moto.

  Alitaja Nyengine ni uhaba wa uchakavu wa Matrekta, uvamizi wa maeneo
  ya kilimo kwaajili ya makaazi, uchimbaji wa mchanga na wizi wa mazao
  wa kilimo wa maliasili.

  Pia alisema kuwa Wizara hiyo inakabiliwa uchache wa mabwanashamba,
  mabadiliko ya hali ya hewa na mvua zisizo tabirika, na ushiriki kuwa
  mdodo  waskta bimafsi katika kuwekeza maendeleo ya kilimo.

  Akieleza mafanikio alisema jumla ya tani 535 za mbegu ya mpunga
  zimesambazwa kwa wakulima ( sawa na asilimia 94 ya lengo), kati ya
  mbegu hizo tani 300 zimenunuliwa kutoka T anzania Bara na tani 235
  zimenunuliwa kupitia wakulima wa mikataba Zanzibar.

  Wizara hiyo amepanga kutekeleza malengo yake kutimiza  dira 2020
  kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUZA II),malengo ya milenia
  MDGs na mikakati ya kisekta pamoja na mpango wa mageuzi ya sekta ya
  kilimo (ATI)

  Aidha kuimarisha udhlishaji wa zao la karafuu, mpunga, utowaji wa
  huduma za matrekta, pembejeo za kilimo, kuzalisha matunda,mboga mboga,
  asali, utalii wa kimaubile, pamoja na kuhamasisha ushirika wa vijana
  katika uzalishaji kilimo cha biashara.

  Wizara hiyo iliomba kuidhinishiwa 30,320,998,000 kwa kazi za kawaida
  na kimaedeleo.

  0 0

   
  Imeelezwa kuwa Jeshi la polisi linashindwa kujenga vituo vidogo vya polisi pembezoni mwa mji kutokana na ufinyu wa bajeti katika jeshi hilo.
   
  Akizungumza  kamanda wa polisi mjini Iringa,RAMADHAN MUNGI amesema kuwa jeshi linatamani sana kuwa na vituo kila sehemu inayozungukwa na watu lakini linashindwa kufanya hivyo kutokana na kuwa na bajeti ndogo.Mungi amesema kuwa kwa kushirikiana na serikali za mitaa pamoja na manispaa wanaweza kujenga vituo hivyo kwani hizo ndizo zenye watu.

  Amesema kuwa kutokana na hali hiyo ya upungufu wa vituo vya polisi jeshi limeanza kutoa elimu juu ya ulinzi na usalama kuanzia ngazi ya familia pamoja na kitongoji juu ya kujilinda.
   
  Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na uchache wa polisi wanashindwa kufika kila mahali hivyo jeshi la polisi linawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi pindi matukio ya kihalifu yanapotokea.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelefu ya wananchi wa mkoa wa Kagera waliofurika katika uwanja wa michezo wa Kaitaba kumsikiliza siku ya mwisho ya ziara yake ya siku sita mkoani humo. PICHA NA IKULU

   Rais Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.

  0 0

  Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar .
   
  Spika wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema
  Baraza la wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo
  utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali
  kuja kuingia katika kitahanani kwa lile ambalo kulitimizia Taifa
  mahitaji yake muhimu.

  Hayo ameyasema  leo huko Baraza la wakilishi  wakati alipokuwa akitoa
  ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM  Hamza Hassan Juma wakati
  alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa
  kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuuliwe kwani una uwasokosesha
  mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.

  Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo
  kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wa
  kutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.

   “sivizuri kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali
  tuwachie Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae
  watuleteeripoti,”alisema Spika.

  Aidha ali sema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana
  wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio
  lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe
  makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.

  Nae waziri wa Nchi afisi ya Makamo wapili wa Rais Muhamed Abuod
  Mohaamed alisema kuku wanao zalishwa na wanaanchi wa ndani ni tani 163
  na nchi inahitaji tani 585 kwakujitosheleza kimahitaji ,hivyo
  wazalishaji wa ndani bado uzalishaji wao mdogo.

  Waziri huyo alilitaka baraza kua, wakiachie kifungu hicho na serikali
  ya mapinduzi ya Zanzibar haina ajizi kuwapatia manufaa wananchi wake
  juu ya suala zima la uzalishaji kuku nchini, na wataliondoa pale
  uzalishaji wa kutosha ukiwepo.

  Ukiendelea mjadala huo waziri wa Afya Juma Duni alisema kumeingizwa
  kuku bandarini na kamapuni ya Malik Fereji ambao wamezuiliwa kutokana
  na mmiliki wa kuku hao kuidanganya Serikali kwa kutoa Risiti feki
  zisizo kuwa za kihalali ,kuibabaisha serikali juu ya kuku hao
  wanakotoka.

  Wazri huyo ameseam kuku hao wazima lakini  watangamizwa na mmiliki
  huyo atalazimika kulipia gharama za uangamizaji  kutokana na kukosa
  uaminifu.

  Nae  mwakilishi aliokuwa amezuia kifungu hicho Hamza Hasssa Juma
  alikubali kukiachia kifungu hicho kwa shingo upande kwa kuilaumu
  serikali kua Bazara la Mapinduzi mapema washapitisha maamuzi
  kuwasaidia wananchi kuinua zao la kuku lakini wahusika wake bado
  wamelikalia kimya jambo ambalo halipendezi.

  Alisema karibu duniani kote wazalishaji kuku katika nchi hupewa kipau
  mbele kwa kupewa msukumo wa kifedha ili zao hilo kuzalisha kwa kiwango
  kikubwa kwa wazalendo na kulimiliki wenyewe wazalishaji wa ndani.

  Aidha alisema haitowezekana kontena la futi 20 lililipiwa milioni 30
  haponyuma na kwasasa kontena la futi 40 kulipiwa milioni nane
  haiwezekani lazima ichnguzwe.

  Mwakilishi aliishauri Serikali kumchukulia hatua za kisheria
  muingizaji kuku kutoka kampuni ya Malik Fereji kwa kuidanganya
  serikali kwa hati za ungo kuingizia kuku kutoka nchi sio.
  “Inawezekana hata hao waliopita walingizwa kwa njia hiyo hiyo”alisema Hamza.
  Hata hivyo alimuomba Spika ampe uhuru wa kuunda tume itayo weza
  kujitegemea wenyewe kulifuatilia suala zima la kuku hapa Nchini na
  Nnje ya Nchi kulifuatilia, na bila ajizi spika alikubali kuundatume
  hiyo na kutakiwa kutafuta wezake wakufuatilia jambohilo.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha  Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha  Bunazi, mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya siku sita mkoani humo.PICHA NA IKULU


  0 0

   
  MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Idi Azzan, amejilisalimisha' polisi na kutaka jeshi hilo, kufanyia uchunguzi tuhuma za kuhusishwa na biashara za dawa za kulevya na iwapo itabainika anahusika, hatua za kisheria zichukue mkondo wake.

  Mbunge huyo alifikia hatua hiyo jijini Dar es Salaam jana baada ya barua zilizoandikwa na watu wanaodai ni wafungwa wa Tanzania wanaotukia adhabu zao mjini Hong Khong, nchini China, kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimhusisha yeye (Azzan) kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo akiwatumia vijana hao. Wafungwa hao wanadaiwa kuwa wanatumikia adhabu zao baada ya kupatikana na makosa ya dawa za kulevya.


  Mbunge huyo alisema alienda kutoa taarifa hizo mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaa.

  "Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainika na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azza, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana.

  Azzan alibainisha kuwa ameamua kwenda kutoa taarifa polisi ili waanze uchunguzi wao. Alisema barua hizo ambazo hazina anuani ya eneo zilipotoka wala majina ya waandishi wake zina lengo baya dhidi yake na kutaka kuposha umma.

  "Mimi sipo juu ya sheria itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza;

  "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao."

  Mwishoni wiki hii katika mitandao mbalimbali ya kijamii ziliwekwa barua zinazodaiwa kuandikwa na wafungwa waliokamatwa na dawa za kulevya nchini China zikimhusisha mbunge huyo na biashara hiyo.

  Barua hizo pia zinawataja baadhi ya viongozi wa serikalini kuwa wanajihusisha na mtandao wadawa za kulevya, lakini hazikuainisha majina yao.


  0 0

  IMG_1336
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
  IMG_1345
  Pichani juu na chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto) aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
  IMG_1339
  IMG_1344
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
  IMG_1360
  Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
  IMG_1372
  Uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa.

  0 0

  WATU tisa, wawili kati yao wakiwa ni askari wa Jeshi la Polisi kituo cha Osterbay jijini Dar esalaam wamekamatwa wilayani Kisarawe Mkoani Pwani kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha meno ya tembo (ndovu) 70 sawa na kilo 305 kinyume na sheria.
  Meno hayo ya tembo kwa mahesabu ya kawaida ni sawa na Tembo 35 ndiyo wameuawa na kwamba thamani ya meno hayo ni  zaidi ya sh, milioni 850 fedha za kitanzania.

  Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa saa 5.30 usiku wa Julai 28 huko Kisarawe na Askari Polisi na maliasili wilayani humo waliokuwa kwenye operesheni ya kukamata pembe za ndovu.

  Matei amesema watuhumiwa hao walikamatwa katika kizuizi cha Kauzen kata ya Vikumbulu tarafa ya Chole ambapo walikuwa wakisafirisha meno hayo kwa kutumia gari T 357 ABK Toyota Surf kutoka wilayani humo kwenda jijini Dar esalaam

   Kamanda huyo wa Polisi Pwani amewataja watuhumiwa hao ni Hamidu  Hamadi wa Tandika Yombo, Musa Muhamed Ali wa Kinondoni Studio, Prospa Maleto mkazi wa Tandika hewa, Amir Bakar mkazi wa Mbagala Chalambe,Seif Mdumuka, Said Kadro na Ramadhan Athumani  wa Chanika.

  Matei amewataja pia askari Polisi  wawili waliokamatwa pia kuwa ni Koplo Senga Idd Nyembo na PC Issa Mtama ambao wote wanadaiwa ni watumishi wa Jeshi la Polisi kituo cha Ostabay  jijini Dar esalaam na wanatarajiwa kutolewa Kisarawe walikokamatiwa na kufikishwa Kibaha makao makuu wa jeshi hilo mkoani Pwani kwa ajili ya hatua zingine za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.

  Chanzo: tabianchi

  0 0
 • 07/30/13--03:15: WAZEE WA KAZI KAZINI


 • 0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, kwa ajili ya kutoa mkono wa pole kwa famili ya mhasibu huyo aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Juma Haji Mkina, Kibibi Juma Mkina, aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahani leo Julai 30, 2013 kwa ajili ua kutoka mkono wa pole, kabla ya marehemu kusafirishwa kwenda kuzikwa kijijini kwao Rufiji.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika pamoja na waombolezaji nyumbani aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkina, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. Makamu alifika nyumbani kwa marehemu Kigogo Mburahati, leo Julai 30 kwa ajili ya kutoa mkono wa pole na kuwafariji wafiwa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka Kigogo Mburahati, jijini Dar es Salaam, leo Julai 30, 2013 nyumbani kwa aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Juma Haji Mkima, baada ya kufika kutoka mkono wa pole na kuwafariji wafiwa kutokana na msiba huo. Marehemu Juma, anatarajia kuzikwa leo kijijini kwao, Rufiji. Picha na OMR

  0 0

   Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akipokea mifuko 30 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Vodacom Foundatio Hassan Saleh ikiwa ni sehemu ya vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Sh 10 Milioni vilivyotolewa na Vodacom kumalizia ujenzi wa kituo cha uendelezaji na ukuzaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Msingi Kisiwandui. Wengine pichani kutoka kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni  Mahmoud Mohamed Mussa na Mbunge wa Jimbo hilo Masauni Hamad Masauni. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Taifa.
   Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akipokea kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Masauni Hamad Masauni maelezo ya michoro ya ujenzi wa kituo cha ukuzaji na uendelezaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Msingi Kikwajuni. Kushoto ni Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh ambae alimkabidhi Makamu wa Rais vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya Sh 10 Milioni kumalizia ujenzi wa kituo hicho.
  Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh akiongea na jumuiya ya Shule ya Msingi Kisiwandui wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh. 10 Milioni vilivyotolewa na Vodacom kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha ukuzaji na uendelezaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Misngi Kisiwandui Zanzibar. Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal mwishoni mwa wiki Zanzibar.
   Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh kompyuta kumi zenye thamani ya Sh 13 Milioni kwa ajili ya kusaidia kituo cha jamii cha mafunzo ya komyuta cha Chwaka Mjini Zanzibar. Makabidhiano hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki Zanzibar.
  ==========  =======  ===========
  Dk Bilal ahimiza Tehama kwa vijana
  *       Asifu juhudi za Vodacom za kusaidia maendeleo
  Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal ametoa rai ya kuongezwa kwa kasi ya uwekezaji wa elimu na uwezo wa matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano - Tehama kwa vijana nchini ili waweze kuishi kwenye enzi waliyomo inayotawaliwa na teknolojia..

  Dk Bilal ametoa rai hiyo wakati akipokea msaada wa vifaa vya ujenzi kumalizia ujenzi wa kituo cha uendelezaji na ukuzaji matumizi ya Tehama cha Shule ya Msingi Kisiwandui pamoja na kompyuta kumi kwa ajili ya kituo cha kompyuta cha kijamii cha Chwaka vyote vya Mjini Zanzibar vilivyotolewa na Mfuko wa Kampuni ya Vodacom wa kusaidia jamii - Vodacom Foundation ambavyo kwa pamoja vina thamani ya Sh 23 Milioni.

  Makamu wa Rais amesema uwekezaji kwenye Tehama ni moja ya mambo yanayopaswa kupewa kipaumbele kwa wakati huu hasa kwa vijana ambao hawana sababu ya kuishi nje ya mfumo na zama zinazotawaliwa na matumizi makubwa ya teknlojia katika kila Nyanja ya maisha ikiwemo mfumo rasmi wa elimu. Amesema maisha ya sasa yanahitaji kompyuta na Tehama kwa kiaisi kikubwa na hivyo kuipongeza Vodacom Foundation kwa kuona umuhimu wa kusaidia vituo hivyo viwili msaada ambao ni wa wakati na wa umuhimu kulingana na mahitaji ya wakati.

  "Viongozi wa ngazi zote za serikali tuweke ajenda ya Tehama ili kuviwezesha vizazi vya sasa kuishi na wakati wao."Alisema Dk Bilal na kuongeza kuwa "Sisi tuliozaliwa na kukulia katika zama za BBC(Born Before Computer) tunapoona mapinduzi haya makubwa ya kiteknolojia tunakumbuka tulipotoka na tunawaza ni vipi maisha yatakuwa katika miaka michache ijayo kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya Tehama."Alisema Makamu wa Rais Dk Bilal.

  "Tunachotaka ni kuona vijana ambao ndio wa kizazi cha Tehama wasiulize wanachokitaka leo bali wajiulize na kupata suluhu ya nini kitakachohitajika miaka ijayo na ili tufikie huko ni lazima tuwaandae vijana na tuwekeze kisawaswa kwenye Tehama na kutokana na hilo basi ndio maana nawashukuru sana Vodacom kwa kuona umuhumi wa Tehama kwa jamii na kutoa misaada hii."Aliongeza Dk Bilal katika hafla hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mjini Zanzibar-

  Amesema vituo hivyo vitawasaidia sana vijana kujifunza mambo ambayo hawajayasoma darasani  kupata uelewa na ufahamu wa mambo ambayo hawajawahi kuyafahamu.

  "Kila kitu siku hizi kipo kwenye mtandao hakuna haja ya kusumbuka kama ilivyokuwa wakati wetu ambapo Mwalimu kwa mfano alilazimika kutumia muda mwingi sana kusoma kitabu kizima ili kupata notisi za kufundishia darasani, lakini sasa kila kitu ni kudadavua tu."

  Dk Bilal ambae alitumia muda mwingi kuelezea utofauti wa maisha yalivyokuwa enzi za bila ya kompyuta na hali ilivyo hivi sasa amewaomba wadau wengi zaidi kujitokeza na kusiadia juhudi za ukuzaji na uendelzaji wa matumizi ya Tehama kwa vijana ili kwualinda vijana hao kutosihi kizamani.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Foundation Hassan Saleh amesema muono wa Vodacom ni kuona kila mtanzania anafikiwa kwa urahisi na huduma za Intaneti ili kuweza kunufaika na mapinduzi ya kiteknolojia yanayotoeka ulimwenguni.

  "Nia ya kampuni ya Vodacom ni kuona kila Mtanzania anafikiwa na huduma za Intaneti na kuwa na uwezo wa kuzitumia kwa kuwa tunatambua umuhimu wake kwa maisha ya watu na maendeleo yao kwa sasa bila kujali aina ya kazi au  kipato, na ndio maana tumejitoa kusiadia vituo hivi vinavyoleta huduma za Tehama karibu na watu."

  Saleh amesema Vodacom Foundation imekuwa karibu na jamii kwa kusaidia ustawi wa maendeleo ya jamii hasa katika maeno ya elimu, afya na ustawi wa jamii kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za serikali zinazofanywa katika kuleta maendeleo. "Tumekuwa tukifanya uwekezaji mkubwa kwa jamii yote hii ni kuunga mkono juhudi za dhati zinazofanywa na serikali zote mbili ya Muungano na ya Zanzibar katika kutatua changamoto mbalimbali za kijamii."Alisema Saleh na kuongeza "Azima yetu ya kusaidia jamii bado ipo imara na tunaedela nayo."

  Sale ameongeza kuwa hata misaada hiyo ni kielelezo na mwendelezo wa mchango wa Vodacom katika maendeleo ya wananchi ikitambua na kuheshmu mchango wa jamii inamofanyia biashara kwenye maendeleo ya kibiashara ya kampuni yake.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto)  akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao jijini Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akiwakaribisha baadhi  ya wateja wao katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
   Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu jana.
  Wateja wa Airtel Tanzania wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar se Salaam jana.
   Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications, Bakari Machumu (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Kolaso (kulia kwake) wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wake jijini Dar es Salaam jana.
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam, Said Salim Bakhresa (wa pili kushoto),  akichukua mlo wa futari pamoja na baadhi ya wateja wa Airtel katika hafla iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam jana.
  Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakifuturu katika hafla iiliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu jana.

  0 0  Na Ali Issa – Maelezo Zanzibar              30/7/2013

  Wizara ya kilimo na Maliasili Zanzibar imeiangamiza misumeno 57 ya
  moto ili kuepusha ukataji wa miti kwa idadi kubwa na kupelekea
  uharibifu wa mazingira Nchini.

  Hayo yamesemwa leo huko Baraza lawakilishi na Naibu Waziri wa Wizara
  hiyo Amina Iddi Mabruok wakati alipokuwa akitoa Majumuisho ya michango
  na maswali ya wakilishi wa wananchi majimboni.

  Amsema wametekeleza azma hiyo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya
  ukataji wa miti jambo ambalo lina tishia kukifanya kisiwa kuathiriwa
  na mabadiliko mabaya ya tabia ya nchi na kukipotezea uhalisi wake.

  “tume ingamiza misumeno hii kuinusuru miti,”alisema Naibu Waziri huyo.

  Aidha alisema Rasimu ya kuwea mikakati suala hilo tayari imeandaliwa
  kulikomesha suala hilo na wizara ishapiga marufuku kuletwa misomeno
  hiyo katika nchi ya Zanzibar.

  Nae kaimu wa Wziri wa Wizara hiyo Ramadhani Abdalla Shabani akijibu
  hoja za wakilishi mbali mbali juu ya suala la mazao ya Machungwa
  kuvamiwa na wadudu huko katika kijiji cha kitogani mkoa wa kusini
  Unguja, alisema wizara yake itaongeza mitego ya kuwatega wadudu
  waharibifu juu ya zao hilo.

  Alisema katika kuhakikisha zao hilo lina fanikiwa alisema atakwenda
  yeye na tume yake kuwaonawakulima hao ili kuiona hali hiyo. 
  Waziri aliwatahadharisha wakulima mara wanapo ona hali mbaya ya
  machungwa kuharibiwa na wadudu wayazike ili wadudu wasiendelee kuenea
  kuharibu zaidi.

  Pia akijibu suala la shamba la Makurunge kupewa chuo cha kizimbani kwa
  shughuli za kiutafiti alisema kua tayari wizara imeshaanda hakimiliki
  kupewa chuo hicho kuliendeleza eneo hilo kwa shughuli za chuo cha
  kizimbani.

  Waziri alisema upungufu wakushuka mazao ya chakula kua tani 6000 mwaka
  2012 -13 kulitokana na hali mbaya ya hali ya hewa.

  Aidha akijibu suala la Serikali kuwa na mpango wa kuweka cha kula cha
  hakiba, alisema Wizara yake tayari imeshaanda maelekezo namna ya
  kuhifadhi chakula hicho na rasimu ya maelekezo iko serikalini.

  “Hifadhi ya chakula inahitaji utaalamu kwani chakula cha kuhifadhiwa
  sio mchele , ngano ,sukari vitu hivi vina haribika mapemasana tafauti
  na ulivyo ngano,mahindi na vyakula vyote vya maganda.

  Mengine waziri huyo akijibu alisema wizara katika kuwapa elimu
  wakulima ataongeza na kuwasomesha Mabwana shamba kutoa elimu zaidi kwa
  wakulima ilikufanikiwa katika mavuno yao.

  0 0

  Serikali imetupiwa lawama kwa kushindwa kudhibiti matukio ya kijangiri yanayoendelea kushamiri katika hifadhi mbalimbali hapa nchini.
  Hayo yamesemwa na waziri kivuli maliasili na mazingira PETER MSIGWA wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake, kutokana na vitendo hivyo kushamiri na watu wengi kukamatwa wakiwemo askali polisi maafisa wapelelezi wanajeshi pamoja na viongozi ambao wananchi wanawaamini na kuwapa dhaman za uongozi.
  Msigwa amesema kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa nchini lakini cha kushangaza waziri mwenye dhamana bado analifumbia macho kwa kuwatetea wahalifu licha ya wapinzani kuwataja wahusika.
  Msigwa amesema kuwa wahusika wakubwa katika vitendo hivyo ni watu ambao wananchi wanawategemea katika kulinda maliasili ya taifa lakini cha kushangaza wao ndio wanakuwa watuhumiwa nambamoja jambo ambalo linasikitiasha taifa.
  Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kwa bahati mbaya tumewapa watu dhamana ambao hawajui majukumu yao badala ya kulinda watu wao wapo katika masilahi yao binafsi.
  hata hivyo amewaomba wananchi kushirikiana katika kuchagua viongozi watakaotunza maliasiri za nchi ili kuleta faida kwa nchi na wananchi kwa ujumla kuliko kuweka viongozi wasiojua wajibu wao na kusababisha uchumi wa nchi kushuka.

  WAKATI HUO HUO........!.

  Kutokana na vitendo vya ubakaji kushamiri katika mkoa wa Iringa ,Kamanda wa jeshi la polisi RAMADHANI MUNGI amekemea vikali vitendo hivyo na kusema kuwa ni makosa dhidi ya Binadamu.
  Akizungumza,Kamanda  Mungi amesema kuwa mtu yoyote anayefanya mapenzi na msichana au binti chini ya umri wa miaka 18 hata kama atakuwa amekubali kwa hiari yake bado atahesabiwa kuwa mbakaji.
  Mungi amesema kuwa vitendo hivyo vinasababishwa na matatizo ya kisaikolojia hivyo watalamu wa saikolojia wanapaswa kulishugulikia suala hilo ili kusaidia kupunguza matukio kama hayo.
  Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na wananchi wengi kulalamika juu ya kuachiwa huru kwa watuhumiwa wenye makosa ya ubakaji, amesema kuwa ni haki yao kupewa dhamana kwa mujibu wa sheria na sio kwamba polisi wanafanya makusudi.

  0 0

   Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bi.Constantina Martin(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu Mpango Mpya wa uchangiaji wa hiari mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi wasio wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii fursa ya kujiunga na mfuko huo, kushoto ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, mipango na Utafiti Bw. Gabriel Silayo.

  Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mipango na Utafiti kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) Bw. Gabriel Silayo(kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo yaliyofikiwa na mfuko huo tangu kuanzishwa kwake kulia ni Meneja Mawasiliano,Masoko na Uenezi kutoka Mfuko huo Bi.Constantina Martin. PICHA NA FRANK MVUNGI> MAELEZO.


  ===========   ============
  MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF)


  1.0            UTANGULIZI

  PSPF ni Taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa kwa Sheria Namba 2 ya Mafao ya Hitimisho la Kazi kwa Watumishi wa Umma ya mwaka 1999 (The Public Service Retirement Benefits Act No.2 of 1999) sura ya 371.

  Hapo awali Mfuko huu ulikuwa unahudumia watumishi wa Serikali Kuu na Wakala wa Serikali tu. Hata hivyo, kufuatia kupitishwa kwa Sheria ya Msimamizi na Mdhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (Sheria Na.8 ya mwaka 2008); fursa zaidi zimefunguliwa ambapo sasa Mfuko wa PSPF unaweza kusajili wanachama kutoka sekta zote iwe sekta binafsi, sekta rasmi na isiyo rasmi.  Aidha  mabadiliko haya yameleta uhuru kwa mtumishi kuchagua Mfuko autakao.

  Kutokana na hili PSPF inapenda kuwakaribisha wote na inatoa taarifa rasmi kwamba sasa kila Mtanzania aliyepo ndani au nje ya nchi anaweza kuwa mwanachama wa PSPF!

  Ili kuweza kuwahudumia Watanzania wote haswa waliopo katika sekta isiyo rasmi PSPF imeanzisha Mpango wa Uchangiaji wa Hiari (PSPF Supplimentary Scheme) maarufu kama PSS.

  Mpango huu ulizinduliwa rasmi tarehe 07 Machi 2013 wakati wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Wadau wa PSPF, hadi kufikia tarehe 25/07/2013 mpango huu una wanachama 730 na makusanyo ya kiasi cha shilingi milioni 135.83.

  2.0    MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME- PSS)

  Mpango huu wa hiari ni mahsusi kwa ajili ya kuwapatia huduma ya hifadhi ya jamii wale wote ambao awali kutokana na matakwa ya kisheria hawakuweza kujiunga na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.  Vile vile mpango huu ni fursa nzuri ya kujiwekea akiba ya ziada wanachama ambao tayari wamo katika Mifuko mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii.

  Uanachama katika mpango huu uko wazi kwa kila Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.  Kiasi cha mchango kwa mwezi ni shilingi 10,000/= kiwango ambacho wengi wanaweza kukimudu kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu. Michango inaweza kuwasilishwa kwa siku, wiki, mwezi na hata kwa msimu kutegemeana na upatikanaji wa kipato cha ziada. Michango hii huwekewa faida kila baada ya miezi sita.

  Michango inaweza kuwasilishwa kupitia akaunti ya benki, au kupitia Wakala wa malipo wa M-Pesa, Tigo-Pesa na Airtel money. Mwanachama atajaza fomu na kupewa kitambulisho na nambari ya uanachama.

  Mafao yatolewayo katika mpango huu wa hiari ni kama yafuatavyo:

  ·         Fao la Elimu, 

  ·         Fao la Ujasiriamali,

  ·         Fao la Uzeeni,

  ·         Fao la Ugonjwa,

  ·         Fao la Kifo.

  Pia mwanachama anapolazimika kuchukua michango yake yote na faida kutokana na sababu zozote zile, anaweza tena kuanza kuchangia upya bila masharti yoyote.

  Taarifa hii imetolewa na:

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu

  Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)

  Golden Jubilee Towers, Front Tower,

  Ghorofa ya 6 -13, Mtaa wa Ohio/Kibo,

  S.L.P 4843, Dar es Salaam, Tanzania

  Simu: +255 22 2120912/52, +255 222127375/76

  Nukushi: +255 22 2120930,

  Barua Pepe: pspf@pspf-tz.org: Tovuti: www.pspf-tz.org


  0 0

  Na Edwin Moshi, Makete
   
  Kero ya muda mrefu ya ukosefu wa maji katika shule ya msingi Ndulamo wilaya ya Makete mkoani Njombe hatimaye imetatuliwa baada ya idara ya maji wilayani hapo kuamua kutilia mkazo suala hilo
   
  Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Bosco Godigodi Malangalila (pichani) amesema maji yanapatikana kwa wingi shuleni hapo baada ya kuyakosa kwa kipindi kirefu hali iliyokuwa inaleta picha mbaya shuleni hapo.
   
  Amesema tatizo hili limeondoka shuleni hapo baada ya idara ya maji kupeleka mabomba na kuyafunga kufidia yale ya awali yaliyokuwa yakivujisha maji ilihali yalikuwa mapya hali iliyosababisha kijiji cha Ndulamo kukosa maji ikiwemo na shule hiyo.Mwalimu Godigodi amesema awali walifanya maandamano hadi kwenye ofisi za serikali ya kijiji kushinikiza tatizo hilo la maji kuondolewa shuleni hapo na waliohusika na uzembe uliosababisha maji yasifike shuleni hapo wawajibishwe
   
  “Hivi sasa ndugu mwandishi kuna uafadhali mkubwa kwani maji yapo, hata waalimu wanaoishi shuleni hapa wanauwezo wa kulima hata kabustani ka mbogamboga” alisema Mwalimu mkuu huyo.Mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Alexander Marko amesema kutokana na maji kutoka shuleni hapo yanawasaidia kunywa maji na kunawa mikono ukizingatia msimu huu ni wa kiangazi
   
  Amesema hivi sasa ile kero ya kwenda kutafuta maji wakati wa masomo na wakati mwingine wanafunzi kuja na maji ya kunywa shuleni kwa sasa haipo kwa kuwa yapo maji ya kutosha.Naye mwanafunzi mwingine Timotheo Ibrahim amesema hivi sasa usafi wa vyoo ni mzuri tofauti na awali lakini pia hata mazingira ya shule yamekuwa masafi kwa kuwa maji hayo hutumia kupigia deki madarasani na vyooni
   
  Katika hatua nyingine mwalimu Godogodi amesema ujenzi wa nyumba ya mwalimu uliokuwa ukamilike mwezi huu, hivi sasa unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba mwaka huu kwa kuwa ujenzi huo utaendelea kwa kasi baada ya maji kufika shuleni hapo
   
  Amesema ujenzi huo ulisuasua kutokana na kukosekana kwa maji shuleni hapo lakini kwa kuwa kila kitu cha ujenzi hivi sasa kipo ujenzi huo utakamilika mwezi Septemba

  0 0

   
   Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
    Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akikagua gwaride la heshima la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo.
   Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es salaam.
   Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.
   Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
   Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
   Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam.
   Naibu Waziri mkuu wa Thailand ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Dr. Surapong Tovichakchaikul (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Tanzania Mh. William Mgimwa (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya kudumisha , kutunza na kuendeleza uwekezaji kati ya Tanzania na Thailand Ikulu jijini Dar es salaam.
   Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Tanzania na Thailand walioongozwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Yingluck Shinawatra ambapo Tanzania na Thailand zimesaini mikataba minne ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa, uendelezaji wa shughuli za uwekezaji, ushirikiano katika masuala ya Ufundi na ushirikiano katika sekta ya Nishati na Madini.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

  0 0  Si nyingine bali ni Ngoma Africa band a.k.a FFU ughaibuni,bendi maarufu yenye
  ngome yake kule Ujerumani,chini ya kamanda wao Ras Makunja,bendi hiyo
  imefanya kweli siku ya jumapili 28.08.2013 katika maonyesho ya Jambo Seeheim Festival,yaliyofanyika mjini Jugenheim-Seeheim,nchini Ujerumani kuliko ungua shoka mpini ukabaki,kama kawaida yake Ngoma Africa band ilianza kuwasha muziki mkali na kuwatia kiwewe washabiki waliokuwapo katika onyesho hilo,bendi hiyo yenye utajili wa wanamuziki wenye vipaji akiwemo afande Christian aka Chris-B,
  na yule kijana Jonathan Souza a.k.a Jo Jo. Usikose kupata burudani za FFU at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

older | 1 | .... | 128 | 129 | (Page 130) | 131 | 132 | .... | 1898 | newer