Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 11 | 12 | (Page 13) | 14 | 15 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Tunawashukuru wadau wote wa Mtandao huu wa WWW.FULLSHAANGWEBLOG.COM kwa uvumilivu wenu baada ya mtandao wetu kutokuwa hewani kwa siku mbili kutokana na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wetu, Mtandao wa FULLSHANGWEBLOG umerejea usiku wa kuamkia leo mara baada timu ya wataalam wetu kukamilisha kazi ya marekebisho na tayari tulishaanza kumuvuzisha matukio usiku huohuo.

  Tunasema asante kwa uvumilivu wenu na kutuelewa kila mlipotupigia simu kuulizia hali ikoje,tunawashukuru pia kwa simu zenu kwani tumejiona ni wenye bahati na kumbe mchango wetu mnautambua vizuri asanteni sana wadau
  Tunatoa shukurani kwa wadau wetu wawezeshaji Benki ya NBC, Benki ya NMB,NHIF, TTB, SERENGETI BREWERIERS , WILNA INTERNATIONAL ,BAYPORTna R&R kwa uvumulivu wenu tunasema asanteni sana na Mablogger wote ambao walitusemea wakati tulipokuwa na tatizo hili.

  Shukurani za Pekee zimwendee Mustafa Selemani mtaalam wetu na timu yake kwa kuhakikisha wanarekebisha tatizo hilo mpaka tunarejea tena hewani usiku wa kuamkia leo tunakushukuru Mustafa na timu yako ya G5CLICK. Mwisho tunasema kazi inaendelea mbele na wadau wote mnakaribishwa ktutumia habari na matukio mbalimbali kupitia Email ya johnbukuku@gmail.com na info@fullshangweblog.com nasi tutazimuvuzisha mtandaoni kama kawaida.

  0 0

  Additional Financing for Tanzania’s Bus Rapid Transit System to benefit 300,000 Commuters and Create 80,000 Jobs


  WASHINGTON, January 15, 2012 – The World Bank Board of Executive Directors has today approved US$100 million as additional financing for completion of the Bus Rapid Transit (BRT) system in Dar es Salaam. The initiative will save the economy billions of shillings lost daily in the jams and provide relief to at least 300,000 commuters.

  The additional $100 million from the Bank’s International Development Association will bring the total cost of the Second Central Transport Corridor Project (CTCP2 to $290 million).

  “Dar es Salaam is growing rapidly”, said Philippe Dongier, World Bank’s Country Director for Tanzania, Uganda and Burundi. “Traffic jams are a significant problem for the economy. They reduce productivity by wasting the time of road users; they threaten future growth prospects for the city and the country, and they pollute the environment.”
  shu
  The BRT is implemented by the Dar es Salaam Rapid Transport (DART) agency and is aligned to Tanzania’s development strategy which underscores the need for improved transport infrastructure to achieve social and economic objectives. The combined works on the project including the construction of the road works, bus-passenger terminal buildings, feeder stations, utility power relocation will provide some 80,000 jobs by completion in 2015. 

  The BRT system will be operated by a US$40.9 million public private partnership (PPP) arrangement with two private bus operators, one fare collector and a fund manager. The modern system will provide rapid boarding and dedicated right of way for 148 buses with a capacity of 140 passengers each, providing both normal and express services. Additionally, another 100 buses with a capacity of 60 passengers will transport passengers to the trunk system through feeder stations. The entire 20.9 kilometers will be provided with tree-shaded bicycle and pedestrian ways on both sides of the road with an average distance of 500 meters between bus stops.

  “We are happy with the momentum of implementation of the BRT infrastructure as all works contracts have been awarded and the construction is proceeding,” said Yonas Mchomvu, the World Bank’s Transport Specialist in Tanzania.

  DART in collaboration with the Surface and Marine Transport Authority (SUMATRA) and the Daladala Owners Association (DARCOBOA) are currently mobilizing local transport operators to form companies that are expected to participate in the bidding for the BRT bus operation through joint venture agreements and/or operation contracts with experienced international operators. Further, preferential access to shares in the BRT bus operation will be given to the 1,800 daladalas (commuter mini-buses) that are expected to be displaced by the BRT operation.  0 0
 • 01/16/13--01:26: kamuzi la mabest's night.


 • 0 0


  0 0
 • 01/16/13--02:07: KUMRADHI WASOMAJI WETU

 • http://api.ning.com/files/YwgxESvlyQ7MAiAkeI1920Bv5KpUD62CflsKrq*BbdeRWepRd4ZZ5Q3Xuph3*57bl44ZCwGLImS-N0yH0XsJXcmmY7*4bOgH/GLOBALWEBSITELOGO.jpg
  KUMRADHI WASOMAJI WETU
  Mtandao wako uupendao wa www.globalpublishers.info hauko hewani kwa sasa kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza mapema leo ambayo yanashughulikiwa na wataalamu wetu. Ni maratajio yetu kuwa tatizo lililopo litatatuliwa mapema na Mtandao kurudi katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo kwa wale wanaosoma magazeti yetu On Line, wataendelea kusoma kama kawaida kwa kwenda moja kwa moja kwenye anuani hii: http://www.mypublications.info/globalpublishersltd 
  Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote utaojitokeza katika kipindi hiki.

  Asanteni kwa uvumilivu wenu

  Web Master
  Global Publishers Ltd

  0 0


   .Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisisitiza kwa wajumbe wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kuhusu serikali kufuatiliaji  maendeleo ya miradi inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge mjini Zanzbar.
   Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ali Nassoro Lufunga akizungumza na viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.Mkoa wa shinyanga ulikuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa mwaka 2012.
   ======   ========= ========

  SERIKALI KUFUATILIA MAENDELEO YA MIRADI INAYOZINDULIWA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU.
  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  16/1/2013. Zanzibar.
  Serikali inaandaa utaratibu wa kufuatilia maendeleo ya miradi yote inayozinduliwa wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakua endelevu na kuwanufaisha wananchi.
  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana nchini kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akitoa tathmini ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2012 na maendeleo ya miradi iliyozinduliwa wakati wa mbio hizo kwenye mkutano wa viongozi na waratibu wa mbio za Mwenge kutoka maeneo mbalimbali nchini.
  Amesema serikali ina wajibu wa kufuatilia kwa karibu miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2012 katika Halmashauri za wilaya, manispaa na Miji ili kuhakikisha kuwa gharama kubwa iliyotumika wakati wa uanzishaji na ujenzi wa miradi hiyo inawanufaisha wananchi kutoka kizazi kimoja hadi kingine ili kutunza hadhi na heshima ya Mwenge wa Uhuru.
  Amesema mbio za Mwenge wa uhuru zimezindua miradi mingi nchini yenye thamani ya mabilioni ya fedha na kuongeza  kuwa si dhamira ya serikali kuona kuwa mwenge wa uhuru unatumika tu kuzindua miradi ya maendeleo bali kuhakikisha uendelevu wa miradi hiyo.
  “Mbio za Mwenge wa Uhuru kila mwaka zinazindua miradi mikubwa inayogharimu fedha nyingi, lazima tufanye tathmini ya miradi yote inayozinduliwa na hatutapenda kuona mwenge unatumika tu kuzindua miradi kwa maana sherehe, tutapenda kuwa na taarifa za maandishi juu ya hali ya miradi hiyo ili itolewe kwenye tathmini ya mbio za mwenge kwa miaka inayofuata” amesisitiza Prof. Gabriel.    
  Amesema  kuwa utaratibu  huo wa ufuatiliaji  utawahusisha wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri zote ambazo Mwenge wa Uhuru utazindua miradi katika maeneo yao ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea kunufaika na miradi hiyo na mbio za Mwenge wa Uhuru.
  Aidha Prof. Gabriel ametoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa miradi yote inayozinduliwa na Mwenge wa Uhuru  inapewa kipaumbele katika usimamizi na ufuatiliaji.
  Kwa upande wake Bw. Wito Mlemelwa mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru mwaka 2012  akitoa taarifa ya tathmini ya mbio za Mwenge kwa wajumbe wa mkutano huo kwa niaba ya kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa ametoa wito kwa watendaji na viongozi wa maeneo mbalimbali kuhakikisha kuwa miradi yote inayotarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru inakamilishwa kwa ubora na viwango ili kuepuka kukataliwa.
  “Natoa wito kwa watendaji wa maeneo mbalimbali wawe makini wahakikikishe kuwa miradi yote inayozinduliwa na Mwenge wa uhuru inakidhi ubora na viwango vilivyowekwa kulingana na  gharama halisi ya fedha iliyotumika kwa sababu Mwenge wa Uhuru hautahusika kuzindua miradi iliyo chini ya kiwango” amesisitiza Bw. Mlemelwa.
  Katika kipindi cha mwaka 2012 mbio za Mwenge wa Uhuru nchini zilizidua miradi 273 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 158.

  0 0


  Kumradhi wadau kwa picha hii kama itakuwa imewakwaza kwa namna moja ama nyingine,lakini ndiyo hali halisi ya tukio lenyewe,pichani ni mwili wa dada huyo wa kazi za ndani ukining'inia mara baada ya kujinyonga na kupoteza uhai wake,ambapo mpaka shuhuda wa tukio hili anaondoka kwenye tukio chanzo cha kujinyonga kwa mwanadada huyo hakijulikani.Tukio hilo limetokea eneo la la Tabata Barakuda jana usiku mnamo majira ya saa moja usiku na bado chanzo hakijulikani.
  Gari la Polisi likiwa limewasili na kuuchukua mwili wa marehemu na kuupakia katika gari na kuondoka nao.habari zaidi ingia www.tzdadaz.blogspot.com 
  Umati wa watu ukiangalia mahala alipokuwa amejinyongea mdada huyo wa kazi za ndani,ambapo sababu za kujinyonga kwake hazikufahamika mapema.

  0 0

    Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa 
   Mstaiki Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Ilala Mhe Jerry Silaa amewakaribisha na kuwaeleza jinsi walivyoweza na wanavyoendelea kukusanya mapato.
  Mstaiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe.Stanslaus Mabula na ujumbe wa kamati yake ya fedha wametembelea halmashauri ya manispaa ya Ilala kwa maagizo ya Mhe.Waziri Mkuu kuja kujionea mbinu za kisasa za kukusanya mapato.

  0 0  Photo: THE MIC KING: SADAM OUT, WATATU DANGER ZONE! MSHIRIKI wa Shindano la The Mic King lililoendelea kutimua vumbi kila Jumapili katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar, Sadam Rashid ‘KM 18’ ameliaga shindano hilo huku washiriki wengine watatu wakiingia kwenye eneo la hatari (danger zone). Awali, wasanii wawiliwawili kutoka katika makundi ya Risasi, Championi, Uwazi na Ijumaa waliwasilisha jukwaani kazi walizokuwa wamepewa huku majaji wa shindano hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, Ally Baucha na John Dilinga ‘DJ JD’ wakitoa komenti zao. Mwishoni, MC wa shindano hilo alimtangaza Sadam (pichani)kuwa ametolewa kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji huku Hamza ‘KM 11’, Paizo ‘KM 17’ na Salum ‘KM 20’ wakitangazwa kuingia kwenye danger zone. Shindano huoneshwa kila Jumanne saa nne usiku katika Runinga ya DTV na marudio ni Alhamisi saa 10 jioni na Jumamosi kuanzia saa 8 mchana ambapo mashabiki hupata fursa ya kuwapigia kura washiriki wakati wakijinadi runingani.

  MSHIRIKI wa Shindano la The Mic King lililoendelea kutimua vumbi kila Jumapili katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar, Sadam Rashid  ‘KM 18’ ameliaga shindano hilo huku washiriki wengine watatu wakiingia kwenye eneo la hatari (danger zone). Awali, wasanii wawiliwawili kutoka katika makundi ya Risasi, Championi, Uwazi na Ijumaa waliwasilisha jukwaani kazi walizokuwa wamepewa huku majaji wa shindano hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, Ally Baucha na John Dilinga ‘DJ JD’ wakitoa komenti zao. Mwishoni, MC wa shindano hilo alimtangaza Sadam kuwa ametolewa kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji huku Hamza ‘KM 11’, Paizo ‘KM 17’ na Salum ‘KM 20’ wakitangazwa kuingia kwenye danger zone. Shindano huoneshwa kila Jumanne saa nne usiku katika Runinga ya DTV na marudio ni Alhamisi saa 10 jioni na Jumamosi kuanzia saa 8 mchana ambapo mashabiki hupata fursa ya kuwapigia kura washiriki wakati  wakijinadi runingani.

  0 0

  Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam .
  Bondia Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala  Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam 
  Bondia Iddy Mnyeke kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Mussa Sunga katika Mazoezi yanayoendelea Kambi ya Ilala Dar es salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


  Na Mwandishi Wetu Ilala
  BONDIA Iddy Mnyeke yupo katika maandalizi mazito ya kujiandaa na mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika  February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam

  Bondia huyo kwa sasa ananolewa na kocha wa kimataifa wa Mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo wameweka kambi ili kumkabili Momba
  Akizungumza Super D alisema kuwa amemwingiza kambini bondia wake ili aweze kumtengeneza vizuri kwa ajili ya mpambano wake na Sadiki Momba

  Super D alisema kuwa mpambano huo utakuwa wa utangulizi kabla ya Deo Njiku na Omary Ramadhani kutwangana kugombea Ubingwa wa Taifa wa PST
  Kocha huyo alisema kuwa kambi yao itahakikisha inaendeleza ubabe baada ya bondia tegemeo wa kambi hiyo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kumdunda Saidi Mundi Kutoka Tanga.

  Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.

  Michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.

   Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.

  Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
  timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mgeni wake ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi wakiongea katika mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi wakiangalia ngoma katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.
  Jakaya Mrisho Kikwete akiandika jambo huku akiangaliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin Mhe Boni Yayi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere leo Januari 16, 2013.PICHA NA IKULU

  0 0


   Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Usalama, wakitembelea mwishoni mwa wiki Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), cha Arusha, walipofanya ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho.
   Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC), Usalama, wakitembelea mwishoni mwa wiki Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), cha Arusha, walipofanya ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho.

   Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam, wakiangalia eneo ambapo maji yaliyotumika kiwandani yanachujwa tayari kwa matumizi mengine, walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.

   Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
   Baadhi ya maofisa kutoka Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri (wa pili kushoto), walipotembelea Kiwanda cha Bia cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) cha Arusha, wakati wa  ziara ya siku moja kujionea shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
  Kiongozi wa ujumbe wa maofisa wa Jeshi kutoka Chuo ChaTaifa cha  Ulinzi (NDC) Mafunzo ya Kijeshi na Usalama, S.M Minja  (kushoto) akimkabidhi zawadi  Meneja wa Uzalishaji Bia wa Kiwanda cha Bia cha TBL Arusha, Ben Mwanri, walipotembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akfungua rasmi jengo jipya la hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na baadhi ya Wafanyakazi wa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia baadhi ya wafanyakazi na uongozi wa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam mara baada ya kufungua jengo lake jipya leo Januari 16, 2013. PICHA NA IKULU

  0 0

  Tamasha la Muziki la Sauti za Busara kwa mwaka huu litafanyika eneo la mji mkongwe Zanzibar, kuanzia tarehe 14 hadi 17 Februari, jitihada zimefanyika katika kufanikisha tamasha la 10 na kuhakikisha kuwepo kwa uhuru wa kujieleza kupitia nyimbo mbalimbali za wasanii wa Kiafrika ambao nyimbo zao zimepigwa marufuku au kuzuiwa katika nchi wanazotoka.

  Kutakuwa na waimbaji wengi mahiri, akiwemo muimbaji  mwenye misimamo kutoka jamii ya kiisilam nchini Mali, anaejulikana kwa jina la Khaira Arby ambae alifungiwa kuimba licha ya kwamba nyimbo zake zinamsifu/ elezea Mtume Mohammad (SAW). Mwengine ni Comrade Fasto anayetoka Zimbabwe, msanii mahiri wa kurap na mshauri, ambae nyimbo zake zinakosea serikali ya Mugabe hali iliyopelekea nyimbo zake kutopigwa katika radio na Televishen ya taifa. “Tuna uwezo wa kufikisha ujumbe wetu kwa walengwa. 

  Tuna timu  nzuri( mitaani) zenye uwezo wa kusambaza kopi nyingi za albam katika maeneo mbalimbali na hata katika mabasi ya abiria ambayo mengi yanatumiwa na wazimbabwe wa kawaida. Tumebuni njia mbadala “Radio Watu” na albam imekuwa zikichezwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri”. Alisema Comrade Fasto.  

  Wakati wa kongamano lijulikanalo kama Movers & Shakers ya Sauti za Busara, jopo la wasanii litafanya majadiliano ya kuangalia umuhimu wa kulinda uhuru wa kujieleza kwa wasanii. Nae Rebecca Corey, Mkurugenzi Mtendaji wa Busara Promotions anaamini kwamba ni muhimu kwa wasanii kupata nafasi ya kupaza  sauti zao. “Muziki ni njia moja yenye nguvu, lazima tuseme hali ya kutokuwa na usawa, tufurahie maisha, na kueleza hali ya utu wa mtu. Uhuru wa kujieleza ni haki za binadamu, na unatunufaisha sote ikiangaliwa na kuheshimiwa. Ndio maana Sauti za Busara ina jivunia kukuza sauti za wasanii kama Khaira Arby na Comrade Fastoambao wamepigwa marufuku katika nchi wanazotoka”.

  Msanii Khaira Arby kutoka Mali atafanya onesho lake katika tamasha la 10 la Sauti za Busara siku ya mwisho ya tamasha litakaloanza tarehe 14 hadi 17 Februari pale Ngome Kongwe, Zanzibar. Akivutiwa na binamu yake  Ali Farka Toure, Khaira Arby katika muziki wake ameweka vionjo vya chimbuko la  Berber na Songhai ambapo umekuwa ukileta mchanganyiko mzuri wa kuvutia wa desert blues na  wakati wa kurikodi huchanganya na kinanda cha guitar la umeme, ngoni, ngoma na muziki wa kitamaduni na kuufanya mziki wake uvutie sana. Arby, amezaliwa katika kijiji ambacho hakipo mbali na mji wa Timbutku, ambao umezungukwa na jangwa.

  Kwa upande mwingine,  Samm Farai Monro, anaejulikana zaidi kama  Comrade Fatso, ni mmoja wa msanii ambae ni maarufu na anavuma kwa mashairi Zimbabwe.  Anaimba mashairi ya Toyi Toyi, mashairi ya mtaani yenye msimamo ambayo anachanganya na lugha ya Shona na kiingereza na mbira pamoja na hip hop. Atafanya onyesho lake sambamba na kundi la Tanzania Mlimani Park Orchestra wajulikanao pia kama Sikinde, Atongo Zimba kutoka Ghana, N'Faly Kouyaté kutoka Guinea, Owiny Sigoma Band kutoka Kenya, pamoja na wazimbabwe wenzake Mokoomba.

  Miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania watakao shiriki katika tamasha la mwaka huu ni pamoja na  Msafiri Zawose na Sauti Band, Lumumba Theatre GroupSuper Maya Baikoko, Peter Msechu na wengineo wengi..

  Kiingilio kwa watanzania ni shilingi 3,000 na kiingilio maalumu kwa wakaazi wa Africa Mashariki.

  Kwa maelezo zaidi na picha downloads:  Tafadhali tembelea wovuti ya www.busaramusic.org                                                                                   


  0 0
 • 01/17/13--00:31: Nice, smaller house for rent
 •  FRONT YARD.

  Nice, smaller house for rent with 3 bedrooms in Arusha Ngaramtoni on the way to National Forest near SOS school. One of the bedrooms​ is self-contained. The house comes fully furnished with good furniture and asking rent is USD 1,000 per month. 
   
  If interested please send text with your name to +255786223333 or email at neemashau@gmail.com


   BACK YARD
   SITTING ROOM

  KITCHEN

  DINNING ROOM

  0 0


  Mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa tawi la Mitunduruni.

  Foleni ya viongozi wa matawi katika jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa kuanza Januari 20 mwaka huu.
  Baadhi ya wa viongozi ngazi za matawi jimbo la Singida mjini,wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa CCM manispaa ya Singida, Hamisi Nguli (hayupo kwenye picha) wakati akitoa nasaha zake muda mfupi kabla ya kukabidhi vifaa vya michezo.
  Baadhi ya msaada wa vifaa vya michezo vilivyotolewa na mbunge wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa soka jimboni kwake. (Picha zote na Nathaniel Limu).

  Mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 vitakavyotumika kwenye ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi januari 20 mwaka huu.

  Vifaa hivyo ni pamoja na jezi pea 854,mipira 122,soksi pea 854 na cloves za magolikipa 61.Vifaa hivyo ni kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi ngazi ya kitongoji katika jimbo la Singida mjini.Baada ya ligi hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.

  Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa misaada mikubwa mbalimbali katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza wapiga kura wake na wananchi kwa ujumla.
  “Dewji toka awe mbunge wa jimbo la Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi na vijana. Amewasaidia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa ajili ya vijana wa bodaboda watakaojiunga katika vikundi”,alisema.

  Awali msaidizi wa mbunge Dewji, Duda Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni mwendelezo wa Dewji kuhakikisha vijana wanatumia michezo kujiendeleza kimaisha.

  0 0


  Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.
  Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
   Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda.
  Marehemu Judith  alizikwa jana katika makaburi ya Kibada maeneo ya Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEME MAHALI PEMA PEPONI. 
  AMEN.
  Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga.
  Marehemu Judith Chikaka alifariki siku ya Jumapili  ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa bahati mbaya na mapenzi yake muumba alifariki kabla ya kujifungua.
  Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe.
  Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka
  Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi
  Padre kutoka Parokia ya Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya Kigamboni Kibada.
  Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa rambi rambi zao.
  Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
  Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
  Kushoto ni mwakilishi wa Familia ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa marehemu kutoka wizara ya Ardhi
  Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake.

  0 0


  3-- Mama Jk akiangalia ngoma ya utamaduni wakati wa mapakeezi, (mwenye miwani) ni Mk wa uwt -kILIMANJARO MAMA FLORA ZELOTE
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete(kulia) akiangalia vikundi vya sanaa ya  ngoma mbalimbali za utamaduni  alipowasili  katika  kiwanja  cha ndege cha Kimataifa cha Kilimnjaro (KIA) jan 16.2013 kwaajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya ya Mama na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani  Arusha. Aliengozana nae  wapili ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoa wa Arusha (UWT) Flora Zelote (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

  4-KIKUNDI CHA NGOMA YA MSANJA KIKITUMBUIZA
  Kikundi cha kinamama  cha ngoma ya Msanja  kikitumbuiza katika mapokezi ya Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama salma Kikwete (hayupo pichani)   kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro  (KIA ) Jan 16,2013.

  7-MAMA JK (KULIA) AKISALIMIANA NA MKUU WA MKOA WA ARSMwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo  Wanawake(WAMA) kulia, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mkuu wa Mkoa Arusha Magesa Mulongo (kushoto)  wakati  alipowasil katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013.
  8- Mama jk (kulia) akisalimiana na mkuu wa wilaya ya ars John Mongela- KIaMke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Jan 16,2013.

  1- Mama Jk (kushoto) akielekea ARS ((kushoto) NW wa Afya Dr. Seif RashidMke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete(kushoto) pamoja na Naibu wa Wizara ya Afya Dkt.Seif Rashid (mwenye miwani) wakielekea kupanda ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa- JK- Nyerere jijini Dar es Salaam 16-jan 2013 kuelekea  Arusha kwa ajili ya kufunga mkutano wa masuala ya Afya na Mtoto jan. 17,2013. Mkutano huo unawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi. 
  2- MMama Salma akisalimiana na wafanyakazi wa ndege- (kulia) NW wa Afya Dr. Seif RashidMke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akisalimiana na wafanyakazi wa ndani ya ndege katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam Jan 16,2013 wakati akielekea kufunga mkutano wa Masuala ya Afya na Mtoto hapo Jan 17,2013 mkoani Arusha. Mkutano huo anawashirikisha wajumbe wapatao 700 wa ndani na nje ya nchi, (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid. 

  0 0

  HOTUBA YA KUFUNGA MWAKA 2012 YA JUMUIYA YA WATANZANIA ITALIA ILIYOTOLEWA NA MWENYEKITI Nd. ABDULRAHAMANI A. ALLI.


  Ndugu Abdulrahamani A.Alli
  Mwenyekiti
   Jumuiya ya Watanzania Italia

  Ndugu zangu,
  Watanzania Wenzangu hapa Italia,
  Nina furaha na faraja kubwa kuukaribisha mwaka 2013.
   Ni jambo la bahati ambayo hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kuumaliza mwaka wa 2012 salama.
   Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao wangependa kuuona mwaka huu  lakini hawakujaaliwa. Wametangulia mbele ya haki. kama mnavyojua tumekwisha safirisha miili ya Watanzania wenzetu watatu na mwili mmoja bado tupo katika hatua za mwisho ili tuweze kuusafirisha.

  Tuendelee kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape mapumziko mema. Nasi tumuombe Mola wetu atujaalie baraka katika mwaka huu mpya 2013. AMIN!

  Mwaka tulioumaliza  ulikuwa wenye mambo mengi mazuri na mafanikio, lakini, pia, bado ulikuwa na changamoto zake. Baadhi zilikuwa ngumu na zipo zilizokuwa za kusikitisha na kuhuzunisha hasa za misiba.

  Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote kwa ushirikiano wenu kwa kujitolea kwa hali na mali katika kutatua matatizo makubwa yanayotufika hasa ya misiba. Nawashukuru viongozi na Watanzania wote wa matawi ya jumuiya yetu na jumuiya zingine za Watanzania hapa Italia. Kwa kweli mnastahili pongezi kubwa.Napenda kusisitiza umoja,ushirikiano na upendo baina yetu.
  Nachukua nafasi hii pia kumshukuru Mh. Alex James Msekela Balozi wa Tanzania Rome Italy, na maofisa na watendaji wote wa Ubalozi wetu kwa ushirikiano wao wakati wote tunapowahitaji,kwenye furaha,matatizo mbalimbali.
  Mafanikio:

  Katika mwaka uliopita 2012 Jumuiya yetu kama nilivyosema mwanzo kuwa tulipata mafanikio na matatizo pia ambayo zaidi ilikuwa ni ya misiba na kuuguliwa.

  Mafanikio tuliyoyapata ni kama ifuatavyo:
  • Kwanza kabisa katika mwaka wa 2012 idadi ya Wanajumuiya imeongezeka zaidi, hii inaonyesha jinsi gani Watanzania wanavyoridhika na utendaji mbalimbali wa Jumuiya yetu.
  • Vilevile kwa mwaka wa 2012 Jumuiya yetu ilishiriki mikutano kadhaa ya jumuiya zingine na kupata mialiko mbalimbali ya kuhudhuria sherehe za kitaifa pamoja na ufunguzi wa jumuiya mpya za mataifa mengine.Hili limetuongezea zaidi uzoefu na kujifunza mengi kutoka kwa wenzetu.
  • Mwaka 2012 tulipata heshima kubwa ya kushiriki mapokezi ya ugeni mkubwa wa serikali yetu ulioongozwa na spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda ,kwa ajili ya mkutano wa mzingira wa kimataifa uliofanyika mjini Napoli, Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na balozi wa Tanzania Rome, Mh Alex James Msekela, mheshimiwa balozi alipata fursa ya kuongea na Watanzania na kujitambulisha rasmi kuwa Balozi mpya wa Tanzania baada ya M h. Ali Karume.
  • Jumuiya yetu pia tuliweza kuitisha kikao cha kujadili na kuchangia maoni ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao hicho kilihudhuriwa na msaidizi balozi na Mkuu wa utawala wa ubalozi wa Tanzania Rome, Mh.Salvator M.J.Mbilinyi. Kikao hiki kilikuwa na mafanikio makubwa kwani watanzania walipata maelezo ya kina na jinsi ya kuchangia maoni ya katiba mpya.
  • Mwezi wa desemba 2012,Jumuiya ilipata mualiko wa kuhudhuria mkutano wa Chama cha Radicale italiani, kuchangia maoni kuhusu masuala ya wageni wahamiaji.
  Matukio haya yote ni mafanikio ya Jumuiya yetu kwa kiasi kikubwa na kama nilivyoelezea kuwa matatizo yetu makubwa yaliyotukuta ni misiba, lakini tunamshukuru MwenyeziMungu kwa kutuwezesha kukusanya michango iliyofanikisha kusafirisha miili nyumbani, hili ni kati  ya mafanikio makubwa  ya Jumuiya ya Watanzania Italia tangu ilipoundwa rasmi na kupata  matawi na uwakilishi sehemu mbalimbali mikoani . Jumuiya imefanya kazi kubwa sana ya kuwaunganisha Watanzania  na kuhakikisha kuwa Watanzania wanakuwa pamoja katika matatizo na furaha.Vile vile kwa upande wa Wagonjwa tumeweza kuwashughulikia kwa kadiri ya uwezo wetu.

  Mwito wa 2013/2014:
   Katika mwaka huu mpya napenda kuto mwito kwa Watanzania wote na wanajumuiya wa Jumuiya ya Watanzania Italia kama ifuatavyo:
  •  Natoa wito kwa Watanzania wote kujiandikisha kwenye Jumuiya ili tuwe na idadi kamili ya Watanzania, wapi wanaishi na anuani zao.Vilevile kwa walio na watoto pia ni muhimu kuwandikisha. Hii itatusaidia kwa mambo mbalimbali pamoja na kuwasiliana pale inapohitajika.
  • Matawi yote na wawakilishi wa  jumuiya ya Watanzania Italia lazima kufuata taratibu za katiba yetu, kuwa na mikutano ya viongozi na Watanzania wote katika sehemu zao. Viongozi wa jumuiya wakae na kupanga taratibu za mikutano na tarehe kwa mwaka huu wa 2013. Ratiba za vikao ziwafikie Watanzania wote.

  • Ndugu zangu Watanzania, kama mnavyojua Jumuiya yetu tunaiendesha kwa kujitolea, kwa hiyo nazidi kusisitiza zaidi kuwa kila Mwanajumuiya  ni wajibu wake kutoa mchango wa kila mwaka wa Euro 20,00 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji  na kazi za Jumuiya.
  • Na kwa wale ambao bado hawajajiandisha tafadhali mfike katika ofisi zetu,au muwasiliane na katibu au mwakilishi wetu wa eneo lako ili uweze kupata fomu na maelezo zaidi ya kujiandikisha.
  • Utaratibu wetu wa kufungua matawi ya jumuiya utakuwa na umuhimu mkubwa kwa kipindi hiki cha 2013/2014 kutokana na maombi mengi ambayo tumeyapokea kutoka kwa Watanzania mbalimbali walioko mikoa mingine.
  • Wanajumuiya wazingatie mahudhurio ya vikao vyote vya jumuiya  ili tuweze kujadili mambo yanayotuhusu kwa pamoja na kuhudhuria vikao tunavyoalikwa na jumuiya za mataifa mengine na zile za wenyeji wetu Wataliani.
  • Kila mwaka kutakuwa na mikutano miwili ya Jumuiya, itakayoshirikisha Watanzania wote, kukusanya maoni na kutoa maelezo na taarifa muhimu zinazohusu watanzania wote. Kila mmoja wetu ana wajibu wa kuhudhuria vikao hivi muhimu. Vikao hivi viwili vimetofautiana hivi: Kikao cha kwanza yaani mwanzoni mwa mwaka  kitafanyika katika kila tawi la Jumuiya ya Watanzania Italia na kile cha pili ambacho ni kikubwa kitafanyika makao makuu ya jumuiya mjini NAPOLI. Ambacho kitakutanisha Watanzania wote kutoka kila mkoa wa Italia. Katika kikao hiki cha mwisho wa mwaka viongozi watatoa taarifa za maendeleo ya jumuiya kutoka matawi yote, pamoja na taarifa zote muhimu. Tarehe za vikao hivi zitatolewa rasmi na makao makuu ya Jumuiya.
  Namaliza kwa kutumia nafasi hii kuwashukuru sana Watanzania wote kwa kuwa na moyo wa kujitolea kwa hali na mali, napenda kuwafahamisha kuwa michango yenu inatambulika na tunaithamini sana.
   Jumuiya bado inahitaji msaada zaidi kwa hiyo nasisitiza sote tujitokeze katika kusaidia jumuiya hii ambayo ni chombo muhimu sana kwa Watanzania wote. Serikali yetu inalitambua hili na inathamini sana mchango wa Watanzania wote ughaibuni.( Tanzania Diaspora)
  Nachukua nafasi hii kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh. Raisi Jakaya Kikwete kwa kutoa nafasi kwa Wataalaam mbalimbali walioko ughaibuni (diaspora) kushiriki katika ujenzi wa nchi yetu kwa kutuma CVs zao ili waweze kupata mikataba ya kazi katika sekta mbalimbali.
  Ndugu zangu hii ni nafasi nzuri sana kwetu katika kushiriki kikamilifu kujenga nchi yetu naamini tunayo mengi mazuri ya kuchangia katika ujenzi wa nchi yetu, hima wote walio na ujuzi kupeleka maelezo yao kwani nafasi hii inaonyesha jinsi gani Serikali yetu inavyothamini Watanzania waliopo nje.
  Mwisho Nawatakia kila la heri na mafanikio katika mwaka huu mpya wa 2013.
  Mungu ibariki Jumuiya yetu, Mungu ibariki TANZANIA!

  Kagutta N.M

  0 0

  Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao ‘ Valentine Day’ iliyoandaliwa kwa kushirikiana na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM. Kushoto ni AFISA Masoko na Mauzo wa AMG,  Prosper Vedasto 
  =====   =======
  Push Mobile, Channel Ten kutoa zawadi ya gari Valentine Day
  KAMPUNI ya Push Media Mobile itatoa zawadi ya gari aina ya Vitz lenye thamani ya shs milioni 8 kwa mshindi wa kampeni maalum ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanoa “Valentine Day” ikayoa adhimishwa Februari 14.
  Hayo yalisemwa na Meneja Mauzo na Masoko wa Push Media Mobile, Rodney Rugambo katika uzinduzi wa kampeni hiyi pamoja na Kampuni ya African Media group (AMG) kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten na Redio Magic FM.
  Rugambo alisema kuwa wameamua kutoa zawadi kubwa hiyo ili kuwafanya wapendanao wegi kushiriki na kupata nafasi ya kushinda. Alisema kuwa ili kuingia katika droo ya shindano hilo, unatakiwa kutuma neno “Penzi” kwenda namba 15678 na kujibu maswali mbali mbali yahusiyo masuala ya mapenzi na siku ya Valentine.
  “Hii ni promosheni ya kwanza kubwa hapa nchini na mshindi kujishindia gari, lengo kubwa ni kutoa ufahamu kuhusiana na sikukuu ya wapendanao na vile vile kuwazawadia wadau waokwa kushiriki katika shughuli zao za ujenzi wa taifa,” alisema Rugambo.
  Alisema kuwa mbali ya zawadi hizo, washiriki wa promosheni hiyo pia watapata nafasi ya kujisha kompyuta (Laptop) aina ya HP yenye thamani ya shs milioni 1.5, simu aina ya Blackberry Curve yenye thamani ya shs 500,000 na Home theatre ya thamani ya shs 400,000 na Ipad.
  Kwa mujibu wa Rugambo, lengo lao kubwa ni kuifanya sikukuu ya wapendanao kuwa kubwa kama nyingine kwani mapenzi ni kitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.
  Alisema kuwa mipango yao ni kuwekeza katika sikukuu hiyo ambayo jamii imeanza kuitilia mkazo japo si siku ya mapumziko kama sikukuu nyingine. Alisema kuwa kwa mwaka huu, wameweka bajeti ya shs milioni 30 ili kufanikisha zaoezi hilo.

older | 1 | .... | 11 | 12 | (Page 13) | 14 | 15 | .... | 1897 | newer