Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS, SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI

0
0
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akimfariji Mjane wa Marehemu, Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akishiriki katika Dua ya kumuombea Marehemu Hassan Rashid Shebuge wakati alipofika msibani hapo, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha Maombolezo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi wakiwa katika Msiba wa Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.

 Sehemu ya Waombolezaji wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge pindi ulipowasili nyumbani kwake, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo tayari kwa maandalizi ya mazishi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza machache.
Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata akisoma taarifa fupi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakiwa wamejumuika na waombolezaji wengine kwenye Msiba wa Marehemu Hassan Rashid Shebuge aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri, nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu Jijini Dar es salaam leo.

BEI YA DAWA ZA SERIKALI YASHUKA NCHINI

0
0
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa bei za dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutokana na uamuzi wa serikali wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akisisitiza jambo katika mkutano huo.
 Viongozi wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria Elangwa, Mkurugenzi Mkuu MSD, Laurian Bwanakunu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Kaimu Mfamasia Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya,  Siana  Mapunjo na Mfamasia kutoka Wizara hiyo, Mercy Masuki.
 Taarifa ikitolewa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari Ibrahim Yamola akiuliza swali.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanahabari, Philip David akiuliza swali.
Picha ya pamoja.

Na Dotto Mwaibale


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu amesema bei za dawa, vifaa tiba na Vitendanishi vya maabara zinazonunuliwa na kusambazwa Boahari ya Dawa (MSD) zimepungua bei kwa asilimia 15 hadi 80 ukulinganisha na mwaka jana kutokana na hatua ya MSD kuanza utaratibu wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, kama alivyo agiza Rais Dk.John Magufuli.

Waziri huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, alioufanya ofisi za Makao Makuu ya Bohari ya Dawa MSD, Keko, Dar es Salaam leo huku akizielekeza Halmashauri,  Hospitali na Vituo vya Afya kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa ma Wizara ya Afya ambayo ipo kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.

MSD  kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji  wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India, Bangladesh, Pakistan, Jamuhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani, Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania, Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu,  na Tanzania. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh, India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.

Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na dawa ya chanjo ya homa ya ini (hepatitis B Vaccine ) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 22,000 sasa inauzwa shilingi 5,300, Dawa ya sindano ya Diclofenac kwa ajili ya maumivu (vichupa 10) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 2,000 sasa inauzwa shilingi 800 na Dawa ya kupambana na maambukizi ya bacteria (Amoxicillin/Clavulanic Acid Potassium 625mg) yenye Vidonge 15 awali iliuzwa shilingi 9,800 sasa inauzwa shilingi 4,000.

Kwa upande wa vifaa tiba amesema jumla ya wazalishaji 18 wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili ya aina 178 za vitendanishi vya maabara.   

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Serikali ya awamu ya tano imeboresha kwa kiasi kikubwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini ambapo bajeti ya dawa,vifaa tiba, vitendanishi vya maabara na chanjo kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni shilingi Bilioni 269 kutoka Bilioni 251 ya mwaka jana wa fedha 92016/2017)

TANZIA: KARANI WA BARAZA LA MAWAZIRI, HASSAN SHEBUGE AFARIKI DUNIA

0
0
Katibu Mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi anasikitika kutangaza kifo cha Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge (pichani) kilichotokea Julai 06, 2017 katika Hospitali ya Taifa Muhimbini Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Kabla ya kufikwa na Mauti, inaelezwa kuwa Marehemu Shebuge aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Mbagara Majimatutu mnamo Julai 03, 2017 na kukimbizwa katika Hospitali ya Rangi tatu ili kupatiwa huduma ya dharula na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbini kwa matibabu zaidi hadi hapo matuti yalipomfika.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitaama iliyotolewa na madaktari, inaelezwa kuwa Maremu Shebuge alipatwa na shinikizo la damu ambalo limepeleka kupoteza kwake maisha.

Tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu, aiweke roho ya Marehemu Hassan Rashid Shebuge mahapa pema peponi, Amin.

Msiba upo nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu.

IFUATAYO NI RATIBA NZIMA YA MSIBA 

RC MAKONDA AHAHIDI KUPELEKA WANAFUNZI 50 NGORONGORO WATAKAOFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI WA MOCK

0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akipokelewa na Msani Mrisho Mpoto katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba ambapo kupita banda hilo mkuu wa mkoa amehahidi kuwapeleka wanafunzi 50 wa mkoa wa Dar es Salaam bonde la hifadhi ya Ngorongoro
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiasalimaina na Watendaji wa Ngorongoro  katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akisaini katikabu cha wageni katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda  akiteta na  Msani Mrisho Mpoto banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba
 Msani Mrisho Mpoto, akizungumza na wadau waliofika katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda, akikabidhi zawadi kwa watoto waliojibu maswali vizuri juu ya hifadhi ya Ngorongoro
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makondaakikabidhi zawadi kwa watoto waliojibu maswali vizuri juu ya hifadhi ya Ngorongoro
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaaam waliofika katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba

 
 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paula Makonda katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba
 Kikundi cha Sarakasi kikitoa burudani kwa wadau waliofika  katika banda la Elimu kwa Umma la Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro katika Maonesho ya Sabasaba
 Wasanii wa kundi la Mjomba Band wakiwa wanacheza kwa mtindo wa Salute Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda


ALIYEKUWA KARANhttps://www.blogger.com/blogger.g?blogID=3447083346505731795#editor/src=sidebarI WA BARAZA LA MAWAZIRI AAGWA DAR

0
0
 
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akishiriki dua ya kumuombea marehemu ya aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, akisaini kitabu cha maombolezo, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akitoa pole kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, Julai 7, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro, wakati akiwasili kwenye msiba wa aliyekua Karani wa Baraza la Mawaziri, Hassan Rashid Shebuge, nyumbani kwa marehemu, Mbagala Majimatitu, (katikati) ni Katibu Mkuu Ikulu Alphayo Kidata, Julai 7, 2017.
……………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, viongozi waandamizi wa Serikali na mamia ya wananchi kuuaga mwili wa aliyekuwa Karani wa Baraza la Mawaziri Bw. Hassan Shebuge.

Marehemu Bw. Shebuge ameagwa leo (Ijumaa, Julai 7,2017) nyumbani kwake Mbagala- Majimatitu jijini Dar es Salaam na anatarajiwa kuzikwa kesho (Jumamosi, Julai 8, 2017), katika kijiji cha Funta, Bumbuli mkoani Tanga.

Bw. Shebuge amefariki dunia jana (Alhamisi, Julai 6, 2017) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata na shinikizo la damu.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia, Waziri Mkuu amesema kifo hicho ni pigo kwa Serikali.

Amesema enzi za uhai wake marehemu Bw. Shebuge alikuwa mpole na muadilifu na kutoa mchango mkubwa kwenye kufanikisha maamuzi na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa ufanisi.

“Kwa kweli hatuna budi kwa sasa “Wajibu wetu sote ni kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.”

Awali, Katibu Mkuu Ikulu, Bw. Alphayo Kidata akisoma wasifu wa marehemu Bw. Shebuge alisema marehemu alizaliwa Mei 25, 1969 wilayani Korogwe, Tanga.

Alisema marehemu alipata elimu ya msingi katika shule ya Mkwakwani kuanzia mwaka 1977 hadi mwaka 1983, ambapo alipata elimu ya sekondari katika shule ya Usagara kuanzia mwaka 1984 hadi mwaka 1987, zote za mkoani Tanga.

Bw. Kidata alisema mwaka 1988, marehemu alijiunga na shule ya sekondari ya Ilboru mkoani Arusha kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na cha sita.

Alisema mwaka 1992 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada ya Sanaa na Ustawi wa Jamii mwaka 1995, mwaka 1998 alipata shahada ya uzamili ya Sanaa na Ustawi wa jamii. Pia marehemu alipata mafunzo mengine mbalimbali ndani na nje ya nchi.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

IJUMAA, JULAI 07, 2017

WATENDAJI WA WIZARA YA AFYA ZANZIBAR WAKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KIJITOUPELE

0
0


Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Ali Sleiman Shihata akitoa maelezo ya ujenzi wa kituo kipya cha Afya kwa timu ya watalamu kutoka Wizara ya Afya walipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho. Wa katikati ni Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla na (kulia) ni Diwani wa Kijitoupele Saleh Kinana.
1
Mkurugenzi kinga na elimu ya afya Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akisoma ramani ya kituo hicho na kutoa maelekezo kwa mafundi wanaojenga kituo hicho (katikati) Mwakilishi wa Jimbo la Kijitoupele Ali Sleiman Shihata na wapili (kulia) ni Msaidizi daktari dhamana kanda Unguja Ali Kassim Amour.
2
Muonekano wa jengo jipya la kituo cha Afya cha Kijitoupele linalojengwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mwakilishi Mhe. Ali Sleiman Shihata kwa kushirikiana na wananchi wao.
Picha na Makame Mshenga.

………………………
NA Mwashungi Tahir,  Maelezo Zanzibar  .
            
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema kujengwa vituo vya afya katika maeneo mbali mbali kutaweza kusaidia kupungua msongomano wa wagonjwa  katika Hospital kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja .

Hayo amesema Dkt Fadhil Mohammed Abdullah mkurugenzi wa kinga na elimu ya afya  kwa niaba ya waziri wa afya  wakati alipokuwa akikaguwa  kituo cha afya kilichokuwa meli nne katika jimbo la kijitoupele.

Amesema kituo hiki cha afya kilichojengwa hapo kina umuhimu mkubwa  sana hasa ukizingatia katika jimbo hilo  linaishi watu wengi sana hivyo kitakapokamilika na kuanza kazi kutaweza kupunguza idadi ya wagonjwa wengi wanaokwenda katika hospitali ya Fuoni au Mnazi mmoja.

Dr Fadhil amesema wananchi katika majimbo yao wana chachu kubwa ya kupatiwa maendeleo hivyo amewashukuru viongozi wa jimbo hilo kwa kuamua kujenga kituo hicho.

“labda niwashukuru viongozi wa jimbo hili kwa uamuzi walioufanya kwa kujenga kituo hiki cha afya katika eneo hili kwani kutaweza kuwaletea faraja kubwa wananchi wa jimbo hilo,” alisema mkurugenzi huyo.

Pia amesema kituo hiki kitakapokamilika kitakuwa kinatoa huduma zote muhimu ambazo zinatolewa katika hospital kuu ya mnazi mmoja ikiwemo sehemu ya kujifunguliya akinamama , ushauri nasaha, chanjo kwa akinamama na watoto, meno, na kupima presha na baadhi ya maradhi mengine.

Vile vile amewashauri wananchi hao kuwa na utaratibu wa kwenda vituo vya afya kwenda kupima afya zao kila baada ya muda na kupata kujua afya zao kwani kinga bora kuliko kutibu.

Nae mwakilishi wa jimbo hilo Ali Suleiman Shihata akitoa shukurani zake kwa viongozi wa jimbo hilo wakiwemo waliopita na wa sasa hivi kwa kukamilisha kituo hichi ikiwa ni moja ya ahadi zake alizoziahidi wakati wa kampeni  na sasa wanatimiza ahadi zao akiwemo mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo.

Pia mwakilishi huyo ameahidi kuwa kitakapomaliza kituo hicho madaktari na manesi pamoja na wahudumu wengine watatoka katika jimbo hilo ili kupunguza usumbufu wa kwenda masafa marefu.

Jumla ya million 84 na laki nne zimetolewa na viongozi wa jimbo hilo wakiwemo mwakilishi na mbunge katika kukamilisha kituo hicho.
Nao wananchi wa jimbo hilo wametoa pongezi zao kwa viongozi wao wa jimbo kwa kupatiwa kituo cha afya  ndani ya jimbo lao na kusema kuwa watapunguziwa kwenda masafa marefu kuifata huduma hiyo hasa akinamama na watoto.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar atembelea banda la Global Education Link

0
0
Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link Ltd Zakia Nassor akimuelezea jambo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar Moudline Castico wakati alipotembelea banda Global Eductaion Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.
Mtaalamu wa Udahili wa Global Education Link Medadi Sota akimuelezea  Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar Moudline namna ya kuwasaidia wanafunzi kudahili wanafunzi katika nchi mbalimbali wakati alipotembelea banda la Global Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.
Wanafunzi wakiendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata mwongozo wa wa namna ya kujiunga na vyuo vya nje ya nchi kupitia Global Education Link katika maonesho ya biashara ya 41 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar es salaam.

ASAS YATAKIWA KUONGEZA UZALISHAJI ZAIDI WA MAZIWA

0
0
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwasili katika banda la kampuni ya Maziwa ya Asas katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba
Meneja Masoko Jimy Kiwelu akitoa Maelezo kwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipotembelea banda la kampuni ya Maziwa la Asas katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiasaini katabu cha wageni wakati alipotembelea banda la kampuni ya Maziwa la Asas katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba
Meneja Masoko Jimy Kiwelu akitoa Maelezo kwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wakati alipotembelea banda la kampuni ya Maziwa la Asas katika Maonesho ya 41 ya Sabasaba

Naibu Waziri Ole Nasha awaasa watanzania kula korosho

0
0

Na Chalila Kibuda , Gobu ya Jamii 

Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha amewasaa watanzania kula korosho kwa wingi ili kuweza kuepukana na magonjwa mbalimbali ambayo yanagharimu na kukosa nguvu kazi ya taif. 

Nasha ameyasema hayo leo katika Siku ya Korosho katika maonesho ya 41 biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba), amesema kuwa korosho inasaidia kuepukana na mafuta mwilini ambayo yanasababisha magojwa ya moyo kwa kiasi kikubwa. 

Amesema kuwa katika utumiaji wa kurosho kwa kula inafanya kuongezeka kwa pato la taifa na kuwafanya wananchi kuwa nguvu kazi yenye kuzalisha kwa tija kwa maendeleo uchumi hasa katika kuelekea uchumi wa viwanda. 

Nasha amesema kuwa kilimo cha korosho kimeboreshwa na kuwataka wakulima kulima mbegu za kisasa pamoja na kufuata ushauri wa watalaam wa kilimo katika maeneo yao. 

Aidha amesema kuwa katika maonesho hayo watu watumie fursa ya kujifunza kilimo cha kurosho katika kujenga uchumi wa viwanda wa adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Dk. John Pombe Magufuli. 

Makamu Mwenyekiti Bodi ya Korosho, Makola Majogo amesema kuwa wanaendelea katika utoaji wa ulimaji wa kilimo cha kisasa cha kurosho katika kuwa ni zao kuleta maendeleo uchumi wa nchi pamoja na mkulima kunufaika na kilimo hicho.
 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akizungumza katika siku ya Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti  wa Bodi ya Korosho, Makola Majogo akizungumza na waandishi wa habari juu umuhimu wa zao la korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Kilimo , Uvuvi na Mifugo, William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na mifuko ya korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wa waliofika katika Siku Korosho katika maonesho ya 41 ya biashara Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

MAZISHI YA GWIJI WA MUZIKI WA DANSI NCHINI, SHABAAN DEDE YAFANYIKA MAKABURI YA KISUTU JIJINI DAR

0
0

BALOZI DK.PINDI CHANA NA MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI WA LAPF WATEMBELEA BANDA LA LAPF MAONESHO YA SABASABA

0
0
Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akisalimiana na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam,mapema jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya LAPF Prof. Faustine Bee (katikati aliyeshika tuzo ya ushindi wa Lapf )akiwa katika picha ya pamoja na Meneja masoko wa LAPF Bw.James Mlowe pamoja na wafanyakazi wa mfuko huo wakati alipotembelea banda la mfuko wa Pensheni wa LAPF katika viwanja vya Sabasaba mapema jana . 
Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Dr. Pindi Chana akipokea zawadi kutoka kwa mtumishi wa LAPF Simboninsia Ndosi alipotembelea banda la LAPF katika maonyesho ya biashara ya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, kulia anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe mapema jana 
Wanachama wapya wa LAPF wakielekezwa kujaza fomu ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika viwanja vya sabasaba mapema jana. 
Mtumishi wa LAPF akimsajili mmoja wa wanachama wa LAPF alietembelea banda hilo. 
Wateja wakiwa wanasubiri kupata kadi zao za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mapema jana katika maonesho ya sabasaba.
Maafisa wa LAPF wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika kwenye banda la LAPF na kujiunga na uanachama kwenye mfuko katika maonesho ya SabaSaba mapema jana.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMAMOSI LEO JULAI 8,2017

0
0

Kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi yatikisa maonesho ya biashara ya 41 sabasaba leo

0
0
Meneja wa Huduma za  Biashara Tigo, Suleiman Bushagama akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha droo ya Jaza Ujazwe ujaziwe zaidi ya kila wiki ambapo mshindi, Alishady Kihongo Msaji toka Arusha alijishindia simu aina ya Samsung S8. Pichani  kushoto ni Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed na Balozi wa Tigo Jaza ujazwe ujaziwe zaidi Lucas Mhavile JOTI .
Balozi wa Tigo Jaza ujazwe Ujaziwe zaidi JOTI akiwa na mteja wa Tigo, Jane Mushi wa salasala  Dar wakati wa kampeni za klia wiki za Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi kwenye banda la Tigo Sabasaba leo. Kampeni ambazo washindi ujipatia simu aina ya samsung S8, muda wa maongezi na intaneti ya bure mwaka mzima
Balozi wa Tigo Jaza ujazwe Ujaziwe zaidi JOTI akisherehesha umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojaa katika banda la tigo
Meneja wa Huduma za  Biashara Tigo, Suleiman Bushagama akichezesha droo ya Jaza Ujazwe ujaziwe zaidi ya kila wiki ambapo mshindi, Alishady Kihongo Msaji toka Arusha alijishindia simu aina ya Samsung S8. Pichani  kushoto ni Msimamizi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed na Balozi wa Tigo Jaza ujazwe ujaziwe zaidi Lucas Mhavile JOTI
JOTI akifanya yake kwenye kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi

UJENZI WA DARAJA LA KAVUU UMEKAMILIKA

0
0
Ujenzi wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ujenzi wake umekamilika na litaanza kutumika ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Daraja hilo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na Mizigo kutoka Mkoa wa katavi kwenda mikoa ya jirani.

“Serikali iliona kero kubwa wanazozipata wananchi wa mkoa huu hasa kwenye usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye kipindi cha mavuno, hivyo baada ya kukamilisha Daraja hili wananchi wataweza kupita vipindi vyote vya Mwaka,” alisema Naibu Waziri Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng. Ngonyani amemuagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi Kuhakikisha Mzani unaohamishika unawekwa ili kudhibiti magari yatakayozidisha Tani 36.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Katavi Eng. Abdon Maregesi amemuhakikisha Naibu Waziri, Eng. Ngonyani kuwa wakala utaweka mzani huo ili kutoruhusu magari yaliyozidisha Uzito wa Mzigo kupita kwenye Daraja hilo.

Wakati huo huo, Naibu Waziri Eng. Ngonyani amekagua ujenzi wa Nyumba za Viongozi Mkoani humo na kuuagiza Wakala wa Majengo nchini (TBA), kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizo unakamilika ifikapo Novemba mwaka huu.

“Serikali imeshatoa fedha za kukamilisha ujenzi wa nyumba hizi, ujenzi huu ulisimama kwa takribani miezi minne kwa sasa hakuna sababu ya ujenzi kusuasua wakati fedha zipo, ninakuhakikishia Mkuu wa Wilaya nyumba hizi zitakamilika kwa wakati ili zianze kutumika,” alisisitiza Naibu Waziri Eng. Ngonyani.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Eng. Nyonyani amekagua ujenzi wa Barabara ya Sitalike-Mpanda yenye urefu wa kilomita 36.9 ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, barabara hii ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Tunduma kupitia Sumbawanga, Mpanda, Uvinza, Kibondo, Nyakanazazi hadi Mutukula. 

Naibu Waziri Eng. Ngonyani yupo katika Ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Viwanja vya Ndege, Ujenzi wa Nyumba za viongozi na Madaraja katika Mkoa wa Katavi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto), akikagua ujenzi wa Nyumba za viongozi zinazojengwa na Wakala Wa Majengo nchini (TBA) Mkoani Katavi, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bi. Rachel Kassanda.


Meneja Wa Wakala Wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Abdon Maregesi (kulia), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Katikati) juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Kivuu wakati Naibu Waziri huyo alipokagua, Mkoani Katavi.


Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiongea na wananchi wa kata ya MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kukagua Daraja la Kavuu ambalo ujenzi wake umekamilika na linatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa mwezi huu..

 Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akisalimiana na wakazi wa kata ya MajiMoto Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi mara baada ya kuongea nao.
 Naibu Waziri Wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akiongea na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi Mhe. Omary Yahya Massare (Kulia), Wakati Waziri Ngonyani alipotembelea Jimboni kwake mwishoni mwa wiki.
 Muonekano wa Daraja la Kavuu lenye urefu wa Mita 89 linalounganisha Halmashauri ya  Wilaya ya Mlele na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwimbwe Mkoani Katavi ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
Muonekano wa Barabara ya Sitalike-Mpanda yenye urefu wa kilomita 36.9 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99, barabara hii ni sehemu ya barabara kuu inayoanzia Tunduma kupitia Sumbawanga, Mpanda, Uvinza, Kibondo, Nyakanazazi hadi Mutukula.

MAONESHO YA SABASABA 2017;FINCA MICROFINANCE BANK WANG'ARA KATIKA KUTUMIA TEKNOLOJIA KUHUDUMIA WATEJA

0
0

Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.

Wakala wa Finca Express Grace Kimaro akiwa anamsajili mteja mpya wa Finca kwa kutumia Tablet katika banda lao mapema jana katika maonesho ya sabasaba.Jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa FINCA Microfinance Bank Beatrice kimaro akimpiga picha katika kumsajili mteja mpya wa FINCA kwa kutumia mfumo wa kisasa ambao hutumia Tablet mapema jana katika maonesho ya sabasaba ,Jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa Finca Microfinance Bank Bi ;Irene Kijangwa akimpa maelezo mteja aliyetembelea banda lao kuhusu hatua jinsi ya kufungua akaunti za Finca .mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Finca Microfinance Bank wakitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda la FINCA kufungua akaunti Mapema jana katika maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es salaam.
Wateja waliofika katika banda la Finca Microfinance Bank wakipata maelezo jinsi ya kufungua akaunti na huduma za mikop zinazotolewa na Benki,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

TAARIFA KWA WAPENZI WA FM ACADEMIA BAND

0
0
Wamiliki wa bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” wametoa ufafanuzi juu ya kile kilichopelekea Nyoshi el Saadat kuvuliwa cheo cha urais wa bendi.

Wiki mbili zilizopita Nyoshi alivuliwa cheo hicho alichokitumikia kwa takriban miaka 20 na nafasi yeke kuchukuliwa na Patcho Mwamba, hatua ambayo imezua fikra tofauti miongoni mwa mashabiki wa muziki wa dansi – wengine wakiona Nyoshi kaonewa na wengine wakiunga mkono mabadiliko.

Blake Mwambona ambaye amejitambulisha kama mdogo wa aliyekuwa mmiliki wa FM Academia (Marehemu Martin Kasyanju), amesema kwamba kwa zaidi miezi sita iliyopita, maendeleo ya bendi yamekuwa yakididimia kwa kasi kuwa, ikiwa ni pamoja kukosekana ari kwa wanamuziki wengi.

Mwambona amesema wanaamini mfumo wa kubadilishana uongozi, ndio bora zaidi badala kumsimika mtu uongozi kwa miaka mingi na mwisho wa siku anageuka kuwa mtawala. 

Naye Nsajigwa Martin Kasyanju ambaye ni mtoto wa marehemu Martin Kasyanju, amesema kuwa wao hawajamfukuza Nyoshi, ila akiamua kuondoka hawana kizuizi.Tayari imedaiwa kuwa Nyoshi yuko chimbo akisuka bendi yake mpya na hajakanyaga show za FM tangu avuliwe urais wa bendi.

Katika mahojiano yake na Jembe FM ya Mwanza wiki mbili ziliyopita, Nyoshi alifunguka kuwa ameachana na FM Academia na ataibuka na bendi mpya. 

“Hatujamfukuza, tumebadili uongozi wa bendi kwa manufaa ya biashara yetu, kama yeye hawezi kuishi FM bila cheo cha urais, hatutakuwa na namna ya kumsaidia. Kwetu sisi biashara kwanza halafu mambo mengine baadae", Japo yanasemwa mengi, hata hivyo sisi tunatambua Nyoshi bado ni muajiliwa wa FM Academia kama mikataba inavyojieleza na taratibu za kazi zilivyo, anaeleza Nsajigwa.

“Tunathamini sana mchango wa Nyoshi, lakini ni lazima ifahamike kuwa FM Academia inafanya biashara, kuna wakati maamuzi magumu lazima yachukuliwe kwaajili kulinda biashara” aliongeza Nsajigwa na kufichua kuwa mabadiliko hayo yameongeza furaha, amani na ari kwa wanamuziki wa FM Academia.

Waziri wa usalama wa Kenya Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery afariki dunia.

0
0


Jenerali Joseph Ole Nkaissery enzi za Uhai wake.
 
Waziri huyo amefariki dunia saa chache baada yake kulazwa katika hospitali ya kibinafsi ya Karen kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. 
Taarifa za kifo chake zimetangazwa na mkuu wa utumishi wa umma Bw Joseph Kinyua mwendo wa saa kumi na moja alfajiri. 

“Ni kwa huzuni kubwa na mshangao kwamba tunatangaza kifo cha ghafla cha Waziri wa Usalama wa Ndani Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery,” taarifa ya Bw Kinyua imesema. 

“Taifa litaendelea kupashwa habari zaidi punde maelezo yatakapopatikana.” 
Jenerali Nkaissery amefariki siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe G.G Gitahi aliyekuwa seneta wa jimbo la Laikipia kufariki dunia.
Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i (pichani) ameteuliwa kuwa kaimu waziri wa usalama wa ndani kufuatia kifo cha aliyekuwa waziri Meja Jenerali Mstaafu Joseph Nkaissery.

WAKAZI WA JIJI LA DAR WAFURIKA KATIKA BANDA LA UBER NA KUJIUNGA NA HUDUMA

0
0
Wafanyakazi kampuni ya Uber Godfrey Mabula na Ibrahimu Kunguya wakitoa maelezo kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam waliofurika katika banda kujua jinsi Program ya Uber inayorahisisha usafiri wa kutumia teknolojia ya kisasa na gharama nafuu pia wateja wote waliopakua Program hiyo walipata punguzo la kiasi cha 8200Tsh kwa safari yao ya kwanza.Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 
Mfanyakazi wa Uber Ibrahim Kunguya akimsaidia mteja jinsi ya kutumia Program ya uber ambayo imekuwa msaada kwa wakazi wa jiji la Dar kusaidia kurahisisha usafiri kwa njia ya kiteknolojia ,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar Es Salaam. 
Balozi wa Uber akimsaidia mteja jinsi ya kupakua na kutumia program ya Uber katika banda lao katiika maonesho ya sabasaba mapema jana Jijini Dar es salaam. 
Wateja waliofika katika banda la uber wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa Uber Jinsi ya kupakua na kutumia Progamu ya Uber ambayo inarahisisha usafiri na kwa gharama nafuu,Mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam. 

Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakipata maelekezo jini ya kujiunga na programu ya Uber katika maonesho ya sabasaba mapema jana Jijini Dar Es salaam. 
Bango linaloonyesha jinis ya kuipata program ya Uber katika APP store na Google play na kutumia kutumia usafiri kwa bei nafuu na kwa kisasa zaidi . 
Balozi wa Uber akitoa maelekezo kwa mteja aliyefika katika banda lao ambapo pia wateja walijipatia punguzo la kiasi cha 8200 Tsh mara baada ya kupakua na kutumia program ya uber katika kuagiza usafiri kwa bei nafuu na kwa teknolojia ya kisasa mapema jana katika maonesho ya saba saba. 
Huduma zikiendelea kutolewa katika banda la Uber mapema jana katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es salaam.

MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) PROF. MOHAMED JANABI ATEMBELEA MAONESHO YA SABASABA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza viongozi mbalimbali waliotembelea viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi Taasisi yake inavyofanya kazi za kutibu magonjwa ya Moyo na umuhimu wa kupima afya mara kwa mara japo mara moja kwa mwaka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi wakati alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. 

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Aika Nnkya akimsikiliza Haubert Makoke ambaye alimuuliza swali kuhusu magonjwa ya Moyo wakati alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpa ushauri kuhusu afya ya Moyo Mzee John Lihame aliyembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akiwaonyesha wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jinsi upasuaji wa Moyo unavyofanyika.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akijibu maswali mbalimbali kuhusu magonjwa ya moyo aliyoulizwa na wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wananchi hao walifika katika banda hilo kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Fatuma Mkomwa akimpima mapigo ya moyo (BP) Mzee Mwanga ambaye alifika katika banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ally Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali wanazozitoa.
Neema Juma akimsikiliza kwa makini Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo wakati akimweleza namna anavyoweza kuishi na kuepukana na magonjwa ya moyo. Neema alitembelea banda la Taasisi hiyo lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kupima magonjwa ya Moyo bure, kupata ushauri na kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo wanazozitoa.
Wananchi wakiwa katika mstari wa kupima magonjwa ya Moyo bure na kupata ushauri katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo ndani ya Hema la Ali Hassan Mwinyi katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tan trade Edwin Rutageruka (kulia) na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa Tan Trade Fidelis Mugenyi (katikati) alipotembelea maonyesho ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Picha na JKCI

MKURUGENZI MADABA AKIFUNGUA KITUO CHA TIBA ASILI

0
0
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma Shafi Mpenda, amekifungia kituo cha kitengo cha utafiti wa sayansi ya tiba asili na tiba mbadala kinachojishughulisha na kupima afya za binadamu na kutibu magonjwa mbalimbali cha The King Solomon of Sanitarium clinik hadi hapo wataalam wa afya watakapojiridhisha uhalali wake.

Mbali na kukifungia kituo hicho,Mpenda amesema atawachukulia hatua kali baadhi ya wataalam wake wa idara ya afya walioshiriki kutoa vibali feki vilivyohalalisha kituo hicho kufanya kazi ambayo imeonekana kama kuwatapeli wananchi.

Kwa mujibu wa Mpenda ni kwamba, kituo hicho kupitia kwa mmiliki wake Selemani Nzaganya kimekuwa kikifanya shughuli zake kinyume na taratibu ambapo hata leseni kutoka kwa baraza la tiba asili kimekwisha muda wake tangu tarehe 1 januari mwaka huu,hata hivyo bado akifanya shughuli zake bila kupata leseni mpya jambo ambalo ni kosa kinyume cha sheria.

Alisema, amelazimika kufunga kituo hicho kwa ajili ya kuokoa maisha ya wansanchi kwani hata mtu aliyekutwa akihudumia wananchi hana taaluma yoyote inayomwezesha kuhudumia wagonjwa jambo linaloonekana ni hatari kwa afya za watu.

Kwa mujibu wa Mpenda hii ni mara ya pili kufunga kituo kama hicho na ni kampeni ya kudumu kwa wale wote wanaofanya shughuli za kuwatapeli wananchi wa Madaba ambapo ametoa onyo kwa watu wengine wenye tama ya kupata fedha kwa njia ya ujanja ujanja kutafuta maeneo mengine ya kufanya shughuli zao.

Hata hivyo kwa mujibu wa majirani ambao hawakutaka kutaja majina yao,wameipongeza serikali kwa uamuzi wa kukifungia kituo hicho kwani wamiliki wake walikuwa wakiwaibia wananchi.

Walisema, kituo hicho kimekuwa sehemu ya tatizo kwa sababu hata wananchi wanaohitajika kupata ushauri na matibabu hospitalini wamekuwa wakifika katika kituo hicho kwa kuamini kwamba watapata suluhu ya matatizo yao kumbe wanazidisha ukubwa wa matizo waliyonayo.

Kwa upande wake mtu aliyekutwa akitoa huduma katika kituo hicho Ezakiel Mwakatumbula alisema, wamekuwa wanatoa huduma za matibabu kwa wa magonjwa mbalimbali hasa magonjwa sugu kwa kutumkia dawa za mimea,chakula na matunda.

Hata hivyo alikanusha kufanya shughuli zao kitapeli na kusisitiza kuwa huduma wanazotoa zimekuwa zikiwasaidia sana wananchi kuokoa maisha yao.
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images