Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

Mkuu wa wilaya Kibaha awapogeza washindi wa Biko

0
0
MKUU wa Wilaya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama, amewapongeza washindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ na kuwataka kuweka umakini na malengo katika fedha zao wanazokabidhiwa ili wanufaike kiuchumi.
Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya Biko, Goodhope Heaven kushoto akimuelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Asumpter Mshama katikati wakati wa kumkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 19 ya Biko, Elisiana Laizer kulia mwenye gauni jekundu ndani ya benki ya NMB, Tawi la Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

DC Asumpter ameyasema hayo jana katika tawi la NMB, Mlandizi, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 zilizokabidhiwa kwa Mshindi wa droo ya 19, Elisiana Simon Laizer, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, mwenye maskani yake Mlandizi, aliyeibuka kidedea katika droo ya 19 ya bahati nasibu hiyo ya aina yake inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu za mikononi za Tigo, Vodacom na Airtel.

Akizungumzia bahati nasibu hiyo ya Biko, DC Mshama alisema michezo ya kubahatisha ina nafasi kubwa ya kukuza uchumi wao na uchumi wa Taifa kwa kuhakikisha kwamba wanafanya shughuli zenye kuleta maendeleo badala ya kuzitumia kwa mambo yasiyokuwa na msingi.


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Asumpter Mshama kulia akimkabidhi jumlaa ya Sh Milioni 20, mshindi wa Biko droo ya 19, mjasiriamali wa kutengeneza sabuni, Elisiana Laizer, mwenye maskani yake Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani jana. Kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani, Mheshimiwa Asumpter Mshama wa pili kutoka kulia, akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wa Biko wa Sh Milioni 20 aliyepatikana katika droo ya 19, mkazi wa Mlandizi, Elisiana Laizer kulia kwake mwenye gauni jekundu. Kushoto ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven na mmoja wa watendaji wa juu wa benki ya NMB kwenye tawi la Mlandizi.

“Nimeshuhudia kwa macho yangu umekabidhiwa fedha hizi Sh Milioni 20 kutoka kwa watu wa Biko, hivyo nitaanza kukufuatilia hatua kwa hatua ukizingatia kuwa upo katika wilaya yangu na mimi kama DC nimekuja hapa kushirikiana na wananchi ili tupige hatua kiuchumi,” Alisema DC Mshama.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha zake, Elisiana Laizer alisema mbali na kuwa ni mjasiriamali wa kuuza sabuni, lakini hatakuwa na papara katika matumizi ya fedha zake alizokabidhiwa baada ya kushinda Biko droo ya 19, huku akiwa ni mchezaji mzuri wa mchezo huo.

“Nashukuru kwa kupewa fedha hizi lakini kwakuwa ni nyingi sana, nitatuliza akili yangu badala ya kufanya papara katika kuzitumia, maana ndoto yangu ni kuhakikisha kuwa fedha zinakuza uchumi wangu, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu tucheze Biko ili tuweze kuibuka na ushindi wa droo kubwa ya Sh Milioni 20 ya Jumatano na Jumapili,” Alisema.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kuendelea kuchangamkia mchezo wao ili waweze kuvuna donge nono la Jumatano na Jumapili pamoja na kuzoa zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku gharama ya mchezo ikianzia Sh 1000 na kuendelea na ukichezwa kwa kutumia simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

“Leo tumemkabidhi mshindi wetu wa Mlandizi sambamba na kupewa elimu ya kifedha kutoka kwa wataalam wa benki ya NMB wa tawi la Mlandizi, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, huku ikiwa Biko imeendelea kutoa ushindi kwa wachezaji wetu wa mikoa mbalimbali ya Tanzania, hivyo tunaomba Watanzania wacheze kwa wingi na mara nyingi zaidi ili waweze kuibuka na mamilioni ya Biko,” Alisema Heaven.

Kwa miezi miwili tangu kuanza kwa bahati nasibu ya
Biko, Biko imetoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi katika miezi miwili ya Mei na Juni, ikiwa ni njia ya kuwanufaisha wachezaji wao hapa nchini.

StarTimes yawataka wateja kumiminika sabasaba kwa ofa kemkem.

0
0

Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii.

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali nchini ya  StarTimes, imetangaza kushusha ofa ya Ving'amuzi katika Maonyesho ya 41 ya Sabasaba inawatangazia wateja wake na watanzania kwa ujumla kutembelea banda lao.


Akizungumza na Globu ya Jamii Meneja Mauzo wa Star Times Tanzania amesema kampuni hiyo  inawapa  wateja  ving’amuzi vya bei rahisi vilivyounganishwa na kifurushi  cha bure kwa mwezi moja vinapatikana kwa shilingi 78,000  kwa dishi na 47000 kwa antena.


amesmea kuwa pia wateja wataweza kununua televisheni ya kidigitali kwa bei nafuu zaidi na kupewa punguzo la asilimia  8%  ambapo kutakuwa na inchi 40,32 na 24 yenye kingamuzi ndani yake na kukupa chaneli zaidi ya 100 za kitaifa na kimataifa ili kufurahia ulimwengu wa kidigitali .


"Mbali na hayo,kutakuwa na bidhaa nyingine kama simu za kisasa na projekta ambazo zinapatikana kwa bei nafuu ambayo kila mtanzania anaweza kumudu.

Lengo la kufanya hivi ni kumuwezesha kila mtanzania aweze kumudu gharama za matangazo  na kufurahia  ulimwengu wa kidijitali.

Pia tungependa kuwahamasisha wateja wetu kulipia vifurushi tulivyonavyo ili kuweza kutazama chaneli na vipindi vingi zaidi tulivyonavyo  vya kitaifa na kimataifa." Amesema Kisaka.


Amesema kuwa  wateja wa StarTimes wanafurahia matangazo ya moja kwa moja ya kombe la mabara, Mwezi ujao tutaanza kuonyesha kombe la mabingwa kimataifa ( ICC),ligi kuu ya ujerumani (Bundersliga),ligi kuu Italia (Serie A), ligi kuu Ufaransa (League 1) na mwakani kombe la dunia litakalofanyika nchini Urusi.

Tunazo tamthiliya, filamu za kiafrika na ulaya, kichina kihindi, vipindi vya watoto na kadhalika.Vilevile utaweza kuangalia chaneli zaidi ya 37 mubashara na Bure kupitia APP yetu inayopatikana kupitia Google store, App store au www.startimestv.com. 


 Wafanyakazi wa kampuni ya Star Times wakitoa huduma kwa mmoja wa wadau waliotemlea banda hilo kwa nje kwa ajili ya kupata huduma za Ving'amuzi
 Martin Emmanuel wa Star Times Tanzania akitoa huduma ya kuseti Tv kwa mmoja wa wadau waliofika  katika banda la Star katika Maonyesho ya Sabasaba
 Meneja Mauzo wa Star Times Tanzania ,David Kisaka akisikiliza maelezo ya mmoja wa Mteja aliyefika kupata huduma katika Banda la Star Times
Ofisa Huduma kwa Wateja ,Maria Mtoi akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika  katika banda la StarTimes Tanzania  katika Maonyesho ya Sabasaba
 Ofisa Huduma kwa Wateja ,Abdul Mweta kitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika  katika banda la StarTimes Tanzania  katika Maonyesho ya Sabasaba
Muonekanao kwa nje wa Bnada la Star Times Tanzania katika Maonyesho ya Sabasaba

VIONGOZI WA KIMILA MKOANI MBEYA WAUNGA MKONO KAULI MBIU YA HAPA KAZI TU.

0
0
Na Zawadi Msalla-WHUSM

Viongozi wa kimila Mkoani Mbeya waunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika hatua mbalimbali za kuhakikisha Tanzania inafika katika uchumi wa kati wa Viwanda .

Wameyasema hayo walipokuwa wakizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katika ziara yake Mkoani humo na kuongeza kuwa ni vema Watanzania waungane kwa pamoja kufanikisha nia njema ya Rais, Dkt. Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi hao ,Chifu Rocket Mwashinga kutoka Igawilo alisema kuwa Rais anasisitiza wananchi kufanya  kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini na kulijenga taifa.

“Tufikishie ujumbe huu kwa Mhe. Rais ili hao vijana wetu wanaokimbilia mijini badala ya kukaa na sisi wazee kulima nchi isiwe na njaa warudishwe vijijini waje walime na kwa maendeleo yao binafsi na taifa” 

“Inasikitisha sana kuona siku hizi vijana wakilalamikia Serikali kuwa maisha ni magumu wakati wameacha mashamba na wao ndiyo watu wenye nguvu ambapo magenge makubwa ya ujambazi, wabakaji na walevi waliopitiliza yaliyopo huko mijini yanatokana na vijana wasio na ajira” Alisema Chifu Mwashinga.

Aidha Wakuu hao wa kimila walieleza kuwa ili kauli mbiu ya Hapa Kazi tu iweze kutekelezeka wameiomba Serikali iangalie utaratibu wa kuwarudisha vijijini vijana wasio na ajira waliopo mijini kwa kuwa wao ndio nguvu kazi na chachu ya maendeleo. 

Pia viongozi hao waliishauri Serikali kufufua kilimo shuleni ambapo hapo awali watoto walifundishwa elimu ya kujitegemea kwa kulima mashamba na kujenga majengo ya shuleni mambo ambayo kwa sasa hayafanyiki.

“Tulifundishwa kupenda kilimo tukiwa shuleni ,watoto wa siku hizi hata jembe hawajui kulishika” Alieleza Chifu Joseph Mwalawa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel aliiomba ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwatambua wakuu hao wa kimila ili kwa pamoja waweze kusukuma gurudumu la Maendeleo ya taifa.

DUKA LA KADI ZA KISASA ZA MIALIKO MBALIMBALI YA SHEREHE LAZINDULIWA MWENGE

0
0
Duka la kadi mbalilmbali za mialiko ya sherehe limezinduliwa Mwenge,jana jijini Dar, ambapo kila mtu anaweza kumudu gharama.

Akizungumza baada ya kufunguliwa duka hilo Mkurugenzi Mtendaji wa R Plus , Rehema Moses amesema kuwa wameweka kadi zinazoendana na wakati katika sherehe na hafla  mbalimbali.

Amesema Kadi za mialiko walizo nazo ni Send off ,KitchenParty , Harusi pamoja na mialiko ya Kiofisi zinazokwenda kisasa na wakati zaidi.

Rehema amesema katika biashara hiyo wajasirimali wengine wanaweza kununua hapo kwa bei ya jumla kutokana na mahitaji yao.

Amesema kadi zinazopatikana  za aina zote za kumfanya kila mtu kuweza kumudu kwa gharama nafuu kutokana na uwezo wake.
Mgeni Maalum wa Ufunguzi wa Duka la Kadi Mwenge, Doris Mollel Foundation, Doris Mollel akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la kadi Mwenge.
Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akimuonesha kadi mbalimba mgeni maalum wa ufunguzi wa Duka, Doris Mollel katika hafla iliyofanyika Mwenge.
Mkurugenzi Mtendaji R Plus na Mmiliki wa Duka la Kadi za Mialiko, Rehema Moses akiwa na Mwenza wake wakikata keki mara baada ya duka hilo kufunguliwa.
Mgeni Maalum, Doris Mollel akiwa na Mmiliki wa Duka, Rehema Moses na wadau mbalimbali waliofika katika duka hilo wakibadilishana mawazo mara baada ya uzinduzi
Picha ya Pamoja.

Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi ya Tigo imeingia mtaani kwa kishindo na kutoa simu za Samsung S8 zenye ofa ya mwaka mzima.

0
0
Meneja Chapa wa Tigo Tanzania, William Mpinga, akizungumza na wakazi wa Tegeta Nyuki, Dar es Salaam, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000.

Balozi wa Tigo Jaza Ujazwe, Lukas Mwavile ‘Joti’, akiwaburudisha wakazi wa Tegeta Nyuki, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000.
Balozi wa Tigo Jaza Ujazwe, Lukas Mwavile ‘Joti’, akiwaburudisha wakazi wa Tegeta Nyuki, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000.

Balozi wa Tigo Jaza Ujazwe, Lukas Mwavile ‘Joti’, akionyesha umahiri wake wa kupiga debe katika moja ya daladala zinazofanya safari zake Tegeta Nyuki Wazo, wakati wa kampeni ya Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi iliyofanyika katika viwanja vya stendi ya eneo la hilo ambapo wateja wa tigo walizawadiwa zawadi mbalimbali, ikiwamo simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1,900,000
Jijini Dar es salaam leo Jumanne tarehe 4 Julai 2017, Kampuni inayoongoza ya maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania, baada ya mafaniko ya promosheni ya Jaza Ujazwe, sasa  inaendelea na promosheni za kusisimua zaidi ya Jaza Ujazwa, Ujaziwe Zaidi ambapo wateja watakuwa wanaendelea kupokea bonas za papo kwa hapo kwa kushiriki katika droo za kila siku na kila wiki ambazo zitatoa zawadi za bure za muda wa maongezi, data na Ujumbe mfupi kwa washindi kwa muda wa mwaka mzima pamoja na smartphone za Samsung S8. Wanachotakiwa kufanya wateja wote ni kuongeza salio kwa njia ya vocha za kukwangua, Tigo Pesa au Tigo Rusha.


Promosheni hii imekuwa gumzo hapa jijini baada ya kampuni ya mawasiliano ya simu ya Tigo kuamua kuigia katika mitaa ya jiji la Dar es salaam na kutoa simu ya smartphone ya kisasa ya Samsung S8 ambayo ina GB 30, dakika 3,000 na SMS 3,000 kila mwezi kwa mwaka mzima. Kwa mujibu wa Tigo, promosheni hii imekuja sokoni kama sehemu ya kampeni ya ‘Jaza Ujazwe’ ambayo ni shukurani kwa wateja wa Tigo kwa uaminifu wao usiobadilika kwa kampuni hiyo.

Mpaka sasa, wateja wenye bahati wapatao 36 kutoka sehemu mbalimbali nchini wameibuka washindi katika droo za kila siku na kila wiki, ambapo baadhi yao wameondoka na muda wa maongezi usio na kikomo na data za kutumia mwaka mzima.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni za Jaza Ujazwe Ujaziwe Zaidi kwenye mitaa katika viwanja vya Tegeta Nyuki, Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo, Bwana William Mpinga amesema “Tigo inathamini mchango mkubwa ambao wateja wetu wamekuwa wanatupatia kwa muda wa miaka mingi, hii ndio sababu tunaamini kwamba wanapaswa kupewa shukurani kwa uaminifu wao endelevu. Kama kampuni tuna furaha kuwa zawadia wateja wetu kwa mara nyingine ili kuwawezesha kuendelea kufurahia huduma zetu zenye ubora wa hali ya juu.”


Zaidi ya kupata washindi wa kila siku na kila wiki, tumeamua kupeleka promosheni yetu mitaani na kuongeza fursa ya wateja wetu kushiriki katika uzinduzi wetu unaoambatana na burudani kutoka kwa msanii maarufu Joti na kushinda Samsung S8 ambayo inakuja na GB 30, dakika 3,000 na SMS 3,000 kila mwezi kwa muda wa mwaka mzima.


Mpaka sasa Lukinga Hamisi kutoka Kigamboni, Musa Banji kutoka Karume na Rajabu Mabela wa Mbagala wamejishindia kila mmoja simu ya Samsung S8 kutoka katika uzinduzi wa unaoendelea  mitaani na pia watapokea GB30, dakika 3,000 za muda wa maongezi na SMS 3,000 kila mwezi kwa muda wa mwaka mzima.

Mpinga alibainisha kwamba promosheni mpya ita imarisha Tigo kuwa ndio kampuni inayotoa bidhaa na huduma zenye bei nafuu, wakati huo huo itakuwa inaimarisha jukumu lake kama kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu zaidi Tanzania.

“Promosheni hii imekuja kufuatia uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wetu uliofanyika hivi karibuni ambao unahakikisha utendaji wa hali ya juu wa utoaji wa huduma. Kwetu sisi Tigo, kila wakati tunakuwa wabunifu katika kutengeneza mbinu mpya za kusisimua ambazo zinazoimarisha uhusiano wetu na wataja wetu. Promosheni hii ya uaminifu ni njia bora ya kuwazawadia na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendela kutumia huduma na bidhaa zetu.” Alisema Mpinga.

Alithibitisha tena kwamba Tigo imekusudia kuendelea kuwazawadia wateja wake kwa bidhaa na huduma za kusisimua zaidi na akaongeza kwamba “ Ubunifu wa huduma na bidhaa zetu unatokana na utafiti wa kina unaolenga kuwaridhisha wateja wetu. Kwa hiyo Jaza Ujazwe, Ujaziwe zaidi inakuja kukabiliana na mahitaji ya wateja ya kuwa na hisia ya msisimko kila mara wanapo tumia huduma zetu. Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia dakika, SMS au data za ziada wanazo zawadiwa kila mara wanapoongeza salio na hivyo itaboresha mwenendo wa mawasiliano yao” alielezea Mpinga

“ TUNDURU MPYA INAKUJA,TUPIGE KAZI KWA KUSHIRIKIANA ,HAKUNA KITAKACHOSHINDIKANA” DC TUNDURU

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera
Wilaya ya Tunduru ni moja kati ya Wilaya tano za Mkoa wa Ruvuma, Ni wilaya iliyokuwa nyuma kimaendelea kuanzia miundo mbalimbali japo ni wilaya iliyojaa utajili wa madini. Mkuu wa wilaya hiyo Juma Homera anakuja na na mkakati wa Tunduru Mpya , fuatilia ujue ni upya gani anakuja nao ambao utaiweka tunduru kuwa ya kisasa.

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII ALIPOTEMBELEA MAONYESHO SABASABA

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi wa akifurahia jambo na baadhi ya Wakurugenzi na waoneshaji nje ya banda la Wizara ya Maliasili naUtalii mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 – Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salam( Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi wa akizungumza jana na baadhi ya Wakurugenzi na waoneshaji nje ya banda la Wizara ya Maliasili naUtalii mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 – Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salam( Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi wa akizungumza jana na Baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili naUtalii mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 – Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa hivi karibuni jijini Dar es salam( Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii).
Mwenyekiti wa Bodi ya TTB, Jaji mstaafu Thomas Mihayo (katikati) akizungumza na Waoneshaji alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili naUtalii, (wa pili kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi (Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi (wa tatu kuli) akizungumza na Waoneshaji jana alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili naUtalii, Mwenyekiti wa Bodi ya TTB, Jaji mstaafu Thomas Mihayo (wa pili kulia) akiwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Taifa ya Utalii, Devotha Mdachi( wa kwanza kulia) 
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye lango la bustani ya wanyamapori hai wakielekea kuwaangalia wanyama kama vile simba , nyati, chui mamba, chatu pamoja na ndege wa aina mbalimbali. (Picha na Lusungu Helela- Maliasili na Utalii)

MKURUGENZI IDARA YA HABARI ATEMBELEA MAONESHO YA 41 YA KIMATAIFA YA BIASHARA

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi(katikati) na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz(kulia) wakijadili jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji) Prof.Adolf Mkenda walipotembele katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi akipata maelezo kutoka kwa Afisa Masoko wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Bw.Ally Mayai alipotembele banda hilo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi(katikati), Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz(kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari-MAELEZO(Huduma za Habari) Bw.Rodney Thadeus wakipata maelezo kutoka kwa Paul Michael Mkurugenzi wa Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha P.M.Tito’s walipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi na Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz wakipata maelezo ya namna picha za video za zamani zilivyokuwa zinahifadhiwa alipotembelea banda la Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara leo Jijini Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk. Jimmy Yonaz akimpa maelezo Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi namna wanavyofanya shughuli zao, alipotembelea banda la hilo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara leo Jijini Dar es Salaam
1- Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbasi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Leo Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimmy Yonaz



PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO

KAMPUNI YA PUMA ENERGY YATOA GAWIO KWA SERIKALI SH. BILIONI 7

0
0
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika,Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo pamoja na viongozi waanndamizi kutoka Wizara hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto), akipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited Dkt.Ben Moshi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti  mfano wa hundi yenye thamani ya sh. bilioni 7 ikiwa ni gawio la serikali yenye hisa ya asilimia 50 katika hafla iliyofanyika mjini Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni ,anaeshuhudia kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika

Dk. Mpango akifafanua jambo kwa kusisitiza Taasisi mbalimbali za Serikali kuboresha huduma zao na kuipatia serikali gawio kubwa.
Dk Mapango akipongezana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Philippe Corsalettti pamoja na Mwenyekiti wa Puma, Dkt. Moshi
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania Limited, Dk. Ben Moshi (katikati) akijadiliana jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango (kushoto) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma, Philippe Corsalettti wakati wa hafla ya kampuni hiyo kukabidhi gawio la sh. bilioni 7 kwa serikali mjini Dodoma,pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dk. Pallangyo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mpango (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Puma, pamoja na manaibu makatibu wakuu.. Kutoka kulia ni Katibu wa Bodi ya Puma, Gibson Mgima, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, CEO wa Puma, Corsaletti, Mwenyekiti wa Puma, Dk. Moshi na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, D. Juliana Palangyo.
 
=====  ======  =========
 
SERIKALI imekubali kulifanyia kazi ombi la Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy la kutaka taasisi za umma ziweze kununua mafuta ya kampuni hiyo yenye ubia wa asilimia 50 kwa 50 na Serikali ili faida inayopatikana itumike kwenye kutatua changamoto za Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa Mjini Dodoma mapema leo baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Dk Ben Moshi kutoa ombi hilo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango wakati wa tukio la kampuni hiyo kutoa gawio la Sh bilioni 7 kwa Serikali ambayo ni faida iliyopatikana kutokana na biashara ya mafuta.

Akikubali ombi hilo Dk.Mpango alisema kuwa watalifanyia kazi ombi hilo hasa kwa kutambua hata mchango wa kampuni ambazo zimewekeza nchini na zina ubia na Serikali, huku akitoa angalizo kuwa pamoja na ombi hilo
kufanyiwa kazi,hakuna sababu ya Puma kubweteka kwani lazima ushindani uwepo ili kupatikana kwa bidhaa bora."Serikali tumefurahi kwa gawio hili ambalo mmelitoa kwani fedha hizi zitakwenda kuhudumia Watanzania masikiniambao wanahitaji kupata huduma muhimu.Hivyo niwahakikishie Puma ombi lenu nimelisikia na tunalifanyia kazi lazima tuendelee kushirikiana ili kuwa na uwekezaji wenye tija kwa nchi yetu,"alisema Dk.Mpango.

Pia alitumia nafasi hiyo kuitaka kampuni ya Puma kuendelea kufanya kazi yao kwa ufanisi zaidi ili mwaka ujao wa fedha, gawio liongezeke zaidi na kuwahakikisha Serikali inalo jicho lake ambalo linaangalia kwa kampuni zote na mashirika ambayo wana ubia nayo.

Awali kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh bilioni 7 kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mwenyekiti wa Bodi yaPuma Dk. Mosha alisema kuwa wanatambua majukumu yao kwenye kufanyabiashara ya mafuta na ndio kampuniambayo inaongoza kwenye soko lakini ombi lao kwa Serikali ni kwamba itoe maelekezo kwa taasisi na mashirika yaumma kununua mafuta kutoka kwao.

Alisema wanaamini ombi hilo likifanikiwa wataongeza mapato na faida kwa kampuni hiyo ambayo kwa sehemu kubwani kama ya Serikali na hivyo gawio litaongezeka zaidi ya lilitolewa jana huku akisisitiza jukumu lililopo mbele yao nikuhakikisha wanaendelea kuwa bora katika utoaji wa huduma ya mafuta nchini.

"Kampuni yetu ina ubia na Serikali, hivyo tunaomba kama Waziri utaona inafaa mtoe maelekezo maalumu ili kuzifanya taasisi za umma kununua mafuta kwetu.Hii itatuwezesha kupata fedha nyingi na hivyo kuongeza gawio kwa Serikali 

.Tunatamani kuona tukija tena mwakani tunatoa fedha nyingi zaidi ya hizi Sh bilioni 7,"alisisitiza.Wakati huo huo, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Limited Philippe Corsaletti, alisema kuwa uongozi wa 

kampuni hiyo unapongeza juhudi za Rais John Magufuli ya kuhakikisha Serikali inatekeleza mikakati yake ya kukusanyakodi na kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani.

Pia alisema kuwa ufanisi wa kibiashara wa kampuni hiyo kwa mwaka 2016 ulikua mzuri kwa pande zote za mauzopamoja na mapato. "Ufanisi wetu mkubwa unatokana zaidi na biashara ya mafuta ya ndege ambako kwa sasa sisi ndiotunaongoza katika soko."

Alisisitiza wakati wakitoa gawio hilo la Sh bilioni 7 kwa Serikali, jambo kubwa ambalo linawapa faraja ni juhudi zaSerikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais ,Dk.John Magufuli ambaye pamoja na mambo mengine ya kuletamaendeleo ameimarisha mfumo wa kukusanya kodi na kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje na ndani kamailivyooneshwa kwenye bajeti ya 2017/2018. 

"Puma imekuwa ikifuatilia kwa karibu utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya tano, na kuridhishwa na utendaji wake,hivyo uongozi wa Puma Energy utaendelea kutoa ushrikiano kama ambavyo wamekua wakishirikiana siku zote.

"Pia tunafurahishwa na hatua ambazo Rais wetu anachukua katika kuhakikisha rasilimali zilizopo nchini zinawanufaisha Watanzania wote, hivyo Puma tutaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano,"alisema.

Akifafanua zaidi kuhusu gawio ambalo wamelitoa kwa Serikali Meneja huyo wa Puma alisema kufikia mwisho wamwaka ulioishia Desemba 31 mwaka 2016 kampuni hiyo ilitengeneza faida kabla ya kodi ya jumla yaSh bilioni 35.5 na kufafanua Puma Energy iliwekeza kwa nguvu katika kipindi cha mwaka 2016 ili kuboresha miundombinu yake ya ndani na rasilimali zake.

"Lengo letu lilikuwa ni kuimarisha uwepo wake sehemu mbalimbali na kukuza biashara yake. Hivyo kutokana na mazingira mazuri ya biashara bodi ya wakurugenzi imependekeza gawio la Sh.bilioni kwa mwaka ulioishia 2016 iwezekulipwa kwa Serikali kutokana na utendaji mzuri wa kampuni.Mwaka 2015 gawio lilikua Sh bilioni 4.5 bilioni na hivyo 

hiyo inawakilisha ongezeko la asilimia 56 ukilinganisha na mwaka jana na hii ni sambamba kabisa na mkakati wakampuni,"aliongeza.

Alitumia nafasi hiyo kuelezea majukumu ya kampuni hiyo ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania na kufafanua wanao uwezo wa kuhifadhi lita za mafuta milioni  94, vituo 47 vya mafuta maeneo mbalimbalinchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwashukuru wahisani Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).kwa kukabidhi gari leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu kakizungumza machache kabla ya kukabidhi gali hilo leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhiwa gari na Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akilikagua gari hilo
Muonekano wa gari hilo. Picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa gari aina ya Wingle 5 na Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).

Akielezea sababu ya kukabidhi gari hiyo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu ameeleza kuwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli katika suala zima la ujenzi wa uchumi wa kati wa Viwanda.

Meneja Liu ameeleza kuwa gari hiyo inathamani ya shilingi milioni 55, hivyo itumike kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi.

Kwa upande wake RC Makonda amewashukuru wahisani hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia msaada huo kama ilivyokusudiwa, huku akieleza kuwa utaratibu wa kulitumia gari hilo utatokana na maoni ya wananchi ambapo watapiga kura kupitia namba maalumu na kueleza gari hilo liende kwenye idara ipi, kwa mfano idara ya elimu, afya, polisi nakadhalika, zoezi hilo litachukua siku kumi.

RC Makonda ameongeza kuwa serikali yake itaendelea na utaratibu huo wa kupigia kura magari yaende kwenye idara ipi ili kuchochea ufanisi wa kazi na wanachi ndiyo watakao kuwa waamuzi wa hilo.

Phillip Luberege wa Dar es Salaam azoa Sh Milioni 20 za Biko

0
0
FUNDI ujenzi Phillip Luberege mwenye maskani yake Gongolamboto jijini Dar es Salaam, ametangazwa kuwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, akipatikana katika droo ya 20 ya kuwania Sh Milioni 20.

Luberege ametangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam katika droo ya 20 iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, akishirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo amepatikana baada ya kupatikana kwa washindi wa mikoani kiasi cha kuashiria kwamba kumekuwa na mwamko mkubwa kutoka kona zote za Tanzania kuchangamkia mchezo wao kwa watu kuchangamkia fursa ya ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

Alisema kwamba mchezo wao wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, kwa sababu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni yao ni 505050 na kumbukumbu yao ni 2456, huku kiasi cha kuanzia kucheza kikiwa ni Sh 1000 na kuendelea.

“Sh 1000 ya kucheza Biko inampa mshiriki wetu nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambapo hufanyika Jumatano na Jumapili, huku mpaka sasa Biko ikitoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi miwili ya Mei na Juni pekee,” Alisema.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe alisema kwamba maofisa wa Bodi yao wamekuwa wakihudhuria droo zote za Biko, huku wakisema kuwa mchezo huo umekuwa ukichezeshwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote.

“Biko ni mchezo unaofuata sheria zote, hivyo ni salama ambapo kwa wiki hii amepatikana mshindi wa Gongolamboto, baada ya kuchezeshwa droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 ya Jumatano,” Alisema.

Kwa Mwezi Mei na Juni pekee, waendeshaji hao wa mchezo wa kubahaisha wa Biko wametoa zaidi ya Sh Milioni Bilioni moja tangu kuanzishwa kwa mchezo huo unaotikisa katika viunga mbalimbali vya Tanzania.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Gongolamboto, Phillip Luberege. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Kajala Masanja kulia akiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
 

UCHAGUZI WA CHAMA CHA MPIRA WA WAVU WASOGEZWA MBELE

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

UCHAGUZI wa Chama cha Mpira wa Wavu Nchini umesogezwa mbele mpaka Agosti 13 ili kutoa nafasi kwa vyama vya mpira huo mikoani kupata viongozi wake.

Awali uchaguzi huo ulitakiw aufanyike Julai 8 mwaka huu umeweza kusogezwa mbele na Baraza la Michezo Taifa (BMT) ili kuwapa nafasi vyama vya mikoa kumaliza chaguzi zao za viongozi wa mikoa ili kwenda katika uchaguzi mkuu.

Taarifa hiyo imetolewa leo na BMT huku ikisisitiza vyama vya mikoa kufanya chaguzi zao kwa wakati pia kamati za michezo za mikoa kusimamia chaguzi zote za chama za mpira wa  wavu katika mikoa yao.

BMT imevitaka vyama vya mpira wa wavu vya mikoa ambavyo vimesajiliwa katika mikoa yao vihakikishe vinafanya uchaguzi kwa wakati ili viweze kupata haki ya kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Jijini Dodoma ukiwa ni uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi watakaosimamia mpira wa wavu nchini.

Simu za Motorola zarudi sokoni, zapatikana kwenye maduka ya Tigo

0
0

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akiwaonyesha waandishi wa habari simu aina ya Motorola MotoE+ na Moto E ambazo zipo sokoni kwenye maonesho ya 41ya biashara sabasaba jijini Dar Es Salaam leo.Pichani kushoto ni Meneja wa Vifaa vya intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga na Christina Julius wa Motorola.
Mtoa huduma wa kampuni ya simu za Motorola, Dalha Suleiman akiongea na wateja waliokuja kwenye banda Tigo kwenye maonesho ya 41ya biashara sabasaba jijini Dar Es Salaam leo.
Mtoa huduma wa kampuni ya simu za Motorola, Dalha Suleiman akiongea na wateja waliokuja kwenye banda Tigo kwenye maonesho ya 41ya biashara sabasaba jijini Dar Es Salaam leo.
Mtoa huduma wa kampuni ya simu za Motorola, Dalha Suleiman akiongea na wateja waliokuja kwenye banda Tigo kwenye maonesho ya 41ya biashara sabasaba jijini Dar Es Salaam leo.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari simu aina ya Motorola MotoE+ na Moto E ambazo zipo sokoni kwenye maonesho ya 41ya biashara sabasaba jijini Dar Es Salaam leo.Pichani kushoto ni Meneja wa Vifaa vya intaneti wa Tigo, Mkumbo Myonga na Christina Julius wa Motorola.

Waandishi wakichukua matukio wakati wa kutambulisha simu aina ya motorola

MAKAMU WA RAIS AREJEA NCHINI AKITOKEA ADDIS ABABA

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amerejea nchini akitokea jijini Addis Ababa,Ethiopia ambapo alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU).

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Makamu wa Rais wa akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaviva .Katika Ujumbe wa Mkutano huo Makamu wa Rais pia aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Shirika la Posta Tanzania Lapata Gawio la Fedha kutoka Benki ya Posta

0
0
Awamu ya Tano ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutekeleza azma yake ya kukusanya kodi, mapato na gawio kutoka kwa wananchi, wafanyabiashara mbalimbali, wawekezaji na Taasisi na mashirika ya umma ili kuongeza makusanyo ya ndani ya nchi kwa lengo la kuiwezesha Serikali kujiendesha yenyewe na kupunguza misaada na mikopo kutoka nchi wahisani, wabia wa maendeleo na mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa. Taasisi za Serikali na mashirika ya umma yanaendelea kutekeleza agizo la Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutoa gawio kwa Serikali ili kuchangia pato la Taifa.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango amepokea hundi ya shilingi bilioni 1.032 kutoka kwa Benki ya Posta Tanzania ikiwa ni gawio la hisa ya asilimia 86.17 kwa Serikali kama mmoja wa wanahisa kwenye Benki hiyo. Hundi hiyo imekabidhiwa na Prof. Lettice Rutashobya, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania. Vile vile Prof. Rutashobya amemkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania Dkt. Haruni Ramadhan Kondo hundi ya shilingi milioni 97.8 ikiwa ni gawio la hisa ya asilimia 7.98 kama mmoja wa wanahisa wa Benki hiyo.

Aidha, Mhe. Dkt. Philip Mpango amezitaka Taasisi za Serikali na mashirika ya umma kuilipa Serikali gawio la hisa zake na zijiendeshe kwa ufanisi na kwa faida ili makusanyo hayo yaweze kuwahudumia wananchi.

Katika tukio hilo, Dkt. Kondo ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iweze kuilipa Shirika la Posta Tanzania shilingi bilioni 3.6 ambazo ni malipo ya pensheni ya wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Shirika limelipa pensheni hizo kwa niaba ya Serikali.

Utaratibu wa Taasisi za Serikali na mashirika ya umma kulipa gawio la hisa kwa Serikali na wanahisa wengine ni maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuhakikisha kuwa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma yanafanya kazi kwa ufanisi, kuzalisha faida na kutoa gawio kwa Serikali ili mapato hayo yaweze kuhudumia wananchi katika Nyanja mbali mbali kama vile huduma za afya, elimu, maji na barabara.

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma na kushuhudiwa na Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Dkt. Maria Sasabo, Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bwana Deogratius Kwiyukwa.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea gawio la hisa la shilingi bilioni 1.032 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania, Prof. Lettice Rutashobya. Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Eng. Dkt. Maria Sasabo ( wa tatu kushoto) akiwa maeshika hundi hiyo.
Katibu Mkuu wa Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Dkt. Maria Sasabo (wa pili kushoto) akipokea gawio la hisa shilingi milioni 97.8 ya Shirika la Posta Tanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta Tanzania, Prof. Lettice Rutashobya. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wanne kulia) akishuhudia tukio hilo pamoja na Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Deo Kwiyukwa (wa tano kushoto).

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOZUNGUMZA NA WANANCHI WA MKOA WA GEITA WAKATI AKIELEKEA CHATO JANA JIONI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpungia mkono Mama mmoja mlemavu mkazi wa Buseresere mara baada ya kumaliza kuhutubia mamia ya wakazi wa Katoro na Buseresere waliojitokeza pembezoni mwa barabara katika eneo hilo kumsalimia wakati akielekea Chato Mkoani Geita jana jioni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Bwanga njia panda ya kuelekea Makao makuu ya Wilaya ya Chato jana jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Katoro na Buseresere mara baada ya kusimama wakati akielekea Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Geita mjini wakati akielekea Chato.
Wananchi wa Geita waliokuwa na Shauku ya kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakiwa wamepanda juu ya magari pembezoni mwa barabara ya Usagara-Sengerema-Geita jana jioni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mama Rosemary Lucas ambaye alikuwa akiwasilisha kero yake ya kuvunjiwa nyumba Sengerema mkoani Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela akichukua maelezo ya mama huyo Rosemary Lucas aliyevunjiwa nyumba yake Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kada wa zamani wa CHADEMA Hamis Tabasamu ambaye alikuwa akionesha Kadi yake mpya ya CCM mara baada ya kuhamia. Kadi hiyo alikabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza katika Wilaya ya Sengerema.PICHA NA IKULU

WAGOMBEA WAANZA KUJINADI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA CHAMA CHA SOKA CHA WANAWAKE JULAI 08.

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KUELEKEA uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka la Wanawake unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Julai 08  wagombea wa nafasi mbalimbali wameanza kujinadi sera zao wakiahidi kuendeleza vyema soka la wanawake linaloanza kushika kasi kwa sasa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wagombea hao wanaotetea nafasi zao wamesema kuwa wanatarajiwa kuendeleza pale walipoishia katika awamu waliyotoka kwani wanaamini kuwa wakirejea katika nafasi zao maendeleo ya soka la wanawake yatazidi kukua.

Mwenyekiti anayetetea nafasi yake, Amina Kaluma amesema kuwa atahakikisha anazidisha mahusiano mazuri na mashirikisho mengine ya soka kutoka nchi tofauti ikiwemo kujitangaza zaidi kwenye soka la wanawake.

Amina amesema kuwa, atatumia nafasi yake kama Mwenyekiti kuwashawishi wakina mama kuwaruhusu watoto wao kucheza mpira wa miguu ikiwemo kuwahamasisha wao kama wanawake kusaidia katika kuinua soka la wanawake kwani asilimia kubwa nao ni mashabiki wa mpira.

"Nitatumia nafasi yangu kuwahamasisha wakina mama kujiwekeza zaidi katika soka la wanawake kwani asilimia kubwa wao ni mashabiki na pia waweze kuwaruhusu watoto wao wa kike kucheza mpira wa miguu kwani
hauna uhuni kama wengi wanavyosema,"amesema Amina.

Kwa upande wa Mgombe wa nafasi ya Katibu Mkuu anayetetea nafasi yake Somoe Ng'itu amesema kuwa katika kipindi chao cha miaka minne iliyopita wameweza kuhakikisha ligi ya wanawake inachezwa na ikiwa katika ubora wa hali ya juu pamoja na kupata udhamini.

Mbali ba hilo wameweza kushiriki katika Kombe la Afrika Mashariki na Kati na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza, TWFA imeweza kuwa na timu za vijana za Taifa kwa upande wa wanawake kwa umri wa miaka 17 na 20 huku kwa mara ya kwanza ikijumuisha wachezaji kutoka nchi nzima.

Uchaguzi wa wanawake utafanyika Jumamosi huku kampeni za Uchaguzi zikiwa zimeanza Julai 4 mwaka huu.
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha soka la Wanawake Amina Kaluma akinadi sera zake mbele ya wanahabari.

IGP SIRRO APOKEA MSAADA WA MAGARI MANNE LEO JIJINI DAR

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na Meneja Mkuu wa kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari manne yaliyotolewa na kampuni hiyo ikiwa ni juhudi zake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akisikiliza maelekezo ya jinsi inavyotumika moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Anayemuelekeza ni Meneja wa Kampuni ya Kifaru, Mario Gaspari. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akikagua moja ya magari manne waliyokabidhiwa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval. Ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu. Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu, akizungumza wakati wa Hafla ya makabidhiano magari manne yaliyotolewa na Kampuni hiyo ambapo aliahidi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu nchini.Kushoto aliyesimama ni mkalimani wa lugha ya kichina.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro akipita mbele ya magari manne yaliyotolewa na Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika vita ya kupambana na uhalifu.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval, Jianguo Liu(watatu kushoto), baada ya makabidhiano ya magari manne kutoka kwa kampuni hiyo ikiwa ni mchango wao katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupambana na uhalifu nchini.Wengine ni viongozi wa juu wa jeshi na viongozi wa kampuni ya Haval.Hafla hiyo imefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Polisi,Oysterbay,jijini Dar es Salaam .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI MKUU NI MARUFUKU KUSAFIRISHA MAHINDI NJE YA NCHI BILA KIBALI

0
0

WAZIRI MKUU MHE.MAJALIWA AELEKEZA BARAZA LA MICHEZO TANZANIA(BMT) LIVUNJWE.

0
0
Na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameelekeza Baraza la Michezo Tanzania(BMT) livunjwe na shughuli zake kufanywa na Sekretarieti hadi hapo Baraza jipya litakapoundwa tena.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Bungeni Mjini Dodoma wakati akisoma hotuba ya kuhairisha mkutano wa saba wa Bunge la kumi na moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Serikali ya awamu ya tano haitafumbia macho usimamizi mbovu na utawala wa michezo usiojali maslahi ya Taifa,Serikali imeazimia kuimarisha utendaji kwa vyombo vya michezo nchini ili kila mwenye dhamana awajibike ipasavyo”,Aliongeza Mhe.Majaliwa.

Aidha katika hotuba yake amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk John Pombe Magufuli kwa kuunga mkono jitihada za michezo nchini kwa dhamira yake ya kujenga Uwanja mkubwa wa Michezo hapa mjini Dodoma kwa kushawishi mataifa rafiki kama vile Moroco ambao wanajenga uwanja huo.

Pia amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa michezo kwa Afya,umoja wa kitaifa na kama fursa ya ajira kwa vijana wetu ambapo ivi karibuni mkoani Mwanza yamehitimishwa mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA yaliyoibua vipaji na hamasa kubwa iliyo miongoni mwa vijana nchini.

“Tutaendelea kuratibu michezo shuleni,ikiwa ni pamoja na kusimamia ufundishaji wa michezo kama somo,maelekezo yetu ni kwamba kila mkoa uwe na shule angalau mbili zenye mchepuo wa michezo na walimu wenye sifa stahiki za kufundisha michezo,Ameeleza Mhe.Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia ameipongeza kwa dhati timu ya Serengeti Boys kwa kutoa upinzani mkubwa kwenye mashindano ya shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika na kuweka msisitizo kwa Chama cha Mpira nchini(TFF) kuendelea kuwatunza vijana hao.

“Msisitizo wangu kwa TFF ni kuendelea kuwatunza vijana hao na kusimamia vilabu vya michezo nchini, kuwekeza kwenye soka la vijana ili kujenga timu imara kwa miaka michache ijayo”,Aliongeza Mhe.Majaliwa.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images