Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46200 articles
Browse latest View live

JOKATE ,MPOTO NA INSPEKTA HAROUN WAWA KIVUTIO BANDA LA NGORONGORO

0
0
 Msanii wa Muziki wa Kughani Mrisho Mpoto akiimba mbele ya mashabiki waliomzunguka katika kituo cha taharifa cha Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kilichopo katika banda la Maonyesho ya 41 ya Saba saba jijini Dar es Salaam
 Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM,Jokate Mwegelo akicheza na wamasai katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM,Jokate Mwegelo akicheza na wamasai katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Msanii wa Muziki wa Bongofleva Nchini Haroun Kahena 'Inspector Haroun' Akizungumza na wadau     taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Wamasai waliofika katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya Wamasai waliofika katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam.


JOKATE ,MPOTO NA INSPECTOR WAWA KIVUTIO BANDA LA NGORONGORO

0
0
 Msanii wa Muziki wa Kughani Mrisho Mpoto akiimba mbele ya mashabiki waliomzunguka katika kituo cha taharifa cha Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kilichopo katika banda la Maonyesho ya 41 ya Saba saba jijini Dar es Salaam
Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM,Jokate Mwegelo akizungumza na wadau waliofika katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Muimbaji kutoka Bendi ya Mjomba inayoongozwa na Mrisho mpoto Ismail akionyesha umahiri wake wa kucheza na Sauti katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM,Jokate Mwegelo akicheza na wamasai katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana CCM,Jokate Mwegelo akicheza na wamasai katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Msanii wa Muziki wa Bongofleva Nchini Haroun Kahena 'Inspector Haroun' Akizungumza na wadau     taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Mashabiki  waliofika katika bandfa hilo
 Mtaalamu wa Wanyama wanaokula Nyama kutoka Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro,Zainab Suleiman akiungumza na watoto juu ya Sifa za Simba
 Sehemu ya Wamasai waliofika katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Feri kutoka Mjomba Band akitoa burudani katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Mjomba Band wakiwasha moto katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam
 Sehemu ya Wamasai waliofika katika kituo cha taharifa cha Ngorongoro kinachoongozwa na Mrisho  Mpoto katika Viwanja vya Maonyesho Sabasaba jijini Dar es Salaam

--

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungungumza na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni, 4, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mufindi Kusini, Medard Kigola kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Faida Bakari kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Msalala, Ezekiel  Maige (kulia) na Mbunge wa Bukene,  Selemani Zedi kwenye Jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Julai 4, 2017. 
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Abdallah Ulega wa Mkuranga  (kushoto) na Stephen Masele kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega kwenye Jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 59 MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JULAI 4, 2017.

0
0
  Naibu Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk.Tulia Ackson  akiongoza    kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof Palamagamba Kabudi akisoma maelezo kuhusu Sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali wa Mwaka 2017  kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Hamad Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Angeline Kairuki  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge   katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Mbunge wa Bukombe Mhe.Dotto Biteko akiuliza swali  katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Mbunge wa Kuteuliwa Mhe.Salma Kikwete akiuliza swali katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dk Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba   katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Mshindi wa Tuzo ya Stephen Thomas Award Bw.Samwel Edward Mwanyika mwenye ugonjwa wa Down Syndrome akionyesha tuzo yake Bungeni baada ya kushinda tuzo hiyo ya Dunia nchini Uingereza kwa kupiga picha inayovutia leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.Wengine ni Mama yake Bi.Sophia Mshangama na Kaka yake Ndg Elias Mwanyika
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza  jambo na Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye  katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
 Walimu na wanafunzi kutoka Sekondari ya Nyangao kutoka Mtama Mkoani Lindi wakiwa Bungeni kujifunza shughuli mbalimbali katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dk Hussein Mwinyi  akizungumza jambo  na Mbunge  wa Viti Maalum Mhe.Martha Mlata katika kikao cha hamsini na tisa cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Julai 4, 2017.

Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, PROF. JUMANNE MAGHEMBE AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA HIFADHI YA NGORONGORO NA SERENGETI

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amefanya ziara ya kushtukiza tarehe 02 Julai, 2017 katika Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuona maendeleo ya shughuli za utalii na changamoto zilizopo. HAYA NI MATUKIO YA ZIARA HIYO KATIKA PICHA.

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS SUDAN KUSINI

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudani Kusini Mhe. Jenerali Taban Deng Gai ambapo mazungumzo yao yalihusu kuendelea kudumisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.Mazungumzo hayo yamefanyika wakati mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika, jijini Addis Ababa ukihitimishwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

ANKAL MICHUZI ATEMBELEA WADAU KATIKA MAONESHO YA SABASABA

0
0
 Ankal Michuzi akizungumza na Wadau Abdul Malik wa Globala Education Link na Pascala Mayala wa PPR Katika Maonyesho ya Sabasaba
  Ankal Michuzi akizungumza na Wafanyakazi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali DailyNews na Habari Leo katika Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Ankal Michuzi  akisalimiana na wafanyakazi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali DailyNews na  Habari leo
Habari Leo katika Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam katika picha ya pamoja na wafanyakazi  wafanyakazi wa kampuni ya Magazeti ya Serikali DailyNews na Habari leo

TEHAMA yaongeza ufanisi a kazi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC)

0
0
Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Usikose kuangalia kipindi hiki.

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA MRADI MKUBWA WA MAJI SENGEREMA MKOANI MWANZA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine  akifungua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi huo mkubwa wa maji kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Antony Sanga wakati alipoanza ukaguzi wa mradi huo kabla ya kuufungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Maji Eng. Gerson Lwenge wakati akielekea kukagua mradi wa maji katika kijiji cha Nyamazugo Wilayani Sengerema. Mradi huo unatarajiwa kuhudumia wakazi wa Sengereza kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 33 ya awali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kufungua mradi huo wa maji Wilayani Sengerema.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Kada maarufu wa CHADEMA kanda ya Ziwa Hamis Tabasamu mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ameshikana mikono na waandishi wa habari  mbalimbali wa mkoani Mwanza ambao walishiriki katika kazi ya ufunguzi wa mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya amani ya Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke mara baada ya kufungua mradi huo wa maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Sengerema mjini wakati akielekea  Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Kada maarufu wa CHADEMA kanda ya Ziwa Hamis Tabasamu wakati akihutubia wakazi wa Sengerema mara mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanafunzi wa Sekondari mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema vijijini wakati akielekea kuzindua mradi wa Maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Geita mara baada ya kuwasili mkoani humo. 
PICHA NA IKULU

JARIDA LA NCHI YETU LA MWEZI JUNI

0
0

Mkurugenzi Taasisi ya Doris Mollel Azinduwa Duka la Kadi

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses na Mkurugenzi Mkuu, Raimond Njuu (kushoto) wakishuhudia.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (katikati) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Plus Events Cards, Raimond Njuu (kushoto) mara baada ya kuzindua tawi jipya la Kampuni ya Plus Events Cards, Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses akishuhudia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses (kushoto) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (kulia) sehemu ya bidhaa zinazouzwa na duka hilo mara baada ya kuzinduliwa. Kampuni ya Plus Events Cards, wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja imezinduwa tawi jipya Mwenge Sokoni jijini Dar es Salaam.
Hapa ikikatwa keki ya pongezi na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards.
Picha ya pamoja ya wageni waalikwa baada ya uzinduzi


MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi. Doris Mollel amezinduwa tawi jipya la duka la kadi la Kampuni ya ‘Plus Events Cards’ Mwenge, Sokoni Jijini Dar es Salaam huku akiwataka wajasiliamali wadogo na wakubwa wauzaji wa bidhaa hizo kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo ili wajipatie kipato. Bi. Mollel ametoa kauli hiyo alipokuwa akizinduwa tawi hilo, linalofunguliwa kusogeza huduma za uuzaji kadi za kisasa jumla na rejareja kwa wananchi eneo hilo.

Pamoja na hayo, Bi. Doris Mollel aliwashauri wananchi kupenda kununua bidhaa halisi na kuachana na bidhaa feki kwani zimekuwa na madhara huku zikilikoseshea taifa mapato. Alisema bidhaa nyingi feki haziingii kwa utaratibu rasmi nchini hivyo licha ya madhara kwa watumiaji zimekuwa zikilikosesha taifa mapato.

“…Nashauri Watanzania wenzangu tupende kununua bidhaa halisi zinazoendana na thamani ya fedha tunazotoa. Uzuri sasa hivi wauzaji wengine wamekuwa wawazi wanakwambia hii ni bei rahisi kwa kuwa ni feki na hii ndio bidhaa halisi…tujenge utamaduni wa kutumia bidhaa bora na halisi kwa manufaa yetu na taifa,” alisisitiza Bi. Doris Mollel.

Aidha aliipongeza kampuni ya Plus Events Cards wauzaji wa kadi na maua ya maharusi kwa kusogeza huduma zake eneo la Mwenge na kutoa fursa kwa wajasiriamali kuwatembelea kwa ajili ya kusambaza bidhaa hizo Dar es Salaam na hata mikoani. Aliongeza kuwa hatua hiyo si tu imesogeza huduma kwa wahitaji bali imetoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kupata bidhaa za kadi kirahisi na kuzisambaza kwa wahitaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Plus Events Cards mara baada ya uzinduzi. Wa kwanza kushoto na kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa duka hilo tawi la Mwenge Sokoni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses (kushoto) akimlisha keki ya pongezi Mkurugenzi Mkuu, Raimond Njuu (kushoto) mara baada ya uzinduzi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Plus Events Cards, Raimond Njuu (kulia) akiwashukuru baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa tawi lao lililopo Mwenge Sokoni wauzaji wa kadi mbalimbali na maua ya maharusi jumla na rejareja jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Plus Events Cards, Bi. Rehema Moses ameiomba Serikali kujenga mazingira ya ulipaji kodi na malipo anuai ya vibali vya biashara kufanyika eneo moja ili kupunguza urasimu ambao wamekuwa wakiupata wafanyabiashara wanapoitaji kulipia tozo hizo. Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa kauli hiyo kwenye uzinduzi wa tawi jipya la uuzaji kadi jumla na rejareja kwa ajili ya matukio mbalimbali ya sherehe eneo la Mwenge, Sokoni jijini Dar es Salaam.

Bi. Moses alisema wapo wafanyabiashara waadilifu ambao wanajua umuhimu wa kulipia tozo mbalimbali na vibali vya biashara wanazozifanya lakini baadhi wamekuwa wakikwazwa na urasimu uliopo katika ufuatiliaji wa vibali hivyo na mtawanyiko wa ofisi anuai za kufanyia malipo, jambo ambalo linachangia kujikuta wanashindwa kulipia kwa wakati.

Mfanyabiashara huyo mwanamama na Mtanzania wa kwanza kusambaza bidhaa hizo za kisasa aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa vibali vyote na malipo kuwa yakifanyika eneo moja ili kumrahisishia mfanyabiashara kukamilisha vibali husika kwa wakati, na kumpunguzia mfanyabiashara vikwazo ambavyo wakati mwingine vimekuwa vikimpotezea muda mwingi katika ufuatiliaji.

Aidha alivishauri vyombo vya kudhibiti ubora wa bidhaa kuongeza nguvu ili kudhibiti baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakichapisha kadi feki nchini na kuwalaghai watanzania kuwa ni halisi, jamboa ambalo linawaharibia wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa halisi. Alisema kampuni yake ambayo imekuwa ikisambaza kadi za kisasa za matukio mbalimbali ya sherehe jumla na rejareja kutoka nchini China ipo tayari kuwasaidia wajasiliamali waaminifu kutoka popote nchini kufanya biashara hiyo bila udanganyifu ili kumpatia mlaji wa mwisho bidhaa halisi kwa bei nzuri.
Kulia ni mfanyakazi wa Kampuni ya Plus Events Cards, akimuonesha mmoja wa wateja baadhi ya bidhaa mara baada ya uzinduzi huo.
Picha ya pamoja ya wageni waalikwa baada ya uzinduzi

SPIKA NDUGAI APATA UGENI KUTOKA CRDB BENKI LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza wakati alipotembelewa na ugeni kutoka CRDB Benki Tawi la Dodoma, Katikati ni Meneja wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi na kulia ni Meneja Biashara Ndg. Danny Shemdoe, katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Airtel na DTB wazindua maabara ya kompyuta kwa wanafunzi wa Dar kujifunza kutengeneza programu

0
0
 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) leo imezundua maabara ya kompyuta ilijulikanayo kama  “Airtel Fursa Lab” katika shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnologia
  
Maabara hiyo ya “Airtel Fursa Lab” itatoa mafunzo ya msingi ya kompyuta kwa hatua ya awali  na mafunzo ya hatua ya juu zaidi kwa  wanafunzi wa shule za msingi, sekondari, chuo kikuu na jamii nzima kwa ujumla. Walimu pia watapata mafunzo ya kompyuta yatakayowawezesha kutoa msaada kwa wanafunzi watakaotumia maabara hiyo

Akizindua maabara hiyo mgeni rasmi ambaye ni  Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, Prof. Faustin Kamuzora aliwapongeza Airtel na DTBi kwa kuweka nguvu pamoja  katika ushirikiano huu ambao utachochea mapinduzi kwa vijana wa kitanzania katika sekta ya habari namawasiliano (ICT).  Hii itasaidi kujenga jamii yenye msukumo wa kutafuta masuluhisho na kujiongezea wigo katika ujasiliamalia ambayo utasaidia kukuza uchumi wa viwanda kwa taifa”

Pia alitoa wito kwa wadau wengine kuunganisha nguvu katika ushirikiano kama huo ili kuleta maendeleo zaidi”

Akiongea katika uzinduzi huo pia, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya alisema “ wakati Tanzania imejipanga kufikia uchumi wa viwanda mahitaji ya wafanyakazi wenye ueledi katika teknologia wanahitajika sana ili kufikia malengo haya. Hivyo ni muhimu kujenga vijana wenye ujuzi  na ueledi wakiwa katika umri mdogo na hivyo tunajisikia fahari kuwa sehemu ya kutoa ujuzi na kukuza maendeleo ya watanzania katika Teknologia ya Tehama kupitia maabara ya Airtel Fursa  tunayozindua leo.

Maabara ya Airtel Fursa ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutumia teknologia ya mawasiliano ya simu pamoja na Tehama katika kustawisha biashara na kukuza ujuzi katika teknologia  na hivyo kuwa na nguvukazi yenye ueledi zaidi.  Natoa wito kwa vijana na jamii nzima kuchangamkia fursa hii na kuitumia maabara hii ya kompyuta ipasavyo. Aliongeza Mallya

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Eng. George Mulamula alisema “Tanzania tuna changamoto katika kutoa mafunzo kwa vitendo  ili kuchochea na  kuendeleza ubunifu wa teknolojia itakayoleta tija katika  biashara na jamii kwa ujumla hususani kwa wanafunzi wanaofanya masomo ya Kompyuta, sayansi na teknologia ya habari”

“Programu hii imewekwa katika mfumo mzuri ili kuwapa wasichana na wavulana nafasi ya kujiendeleza kuwa wajasiliamali kupitia teknolojia.  Itawasaidia kuwa wabunifu na kujitengenezea ajira kwa kutengeneza program  na bidhaa za kiubunifu zitakazotumika katika jamii zao au mashirika ya umma na kuingiza kipato kikubwa kwa taifa. Kupitia Programu kama ya afriCoderdojo, Science robotics na nyingine nyingi ikiwemo masomo kwa njia ya mtandao yaani E lerning, program za uhandisi, Sanaa na Hisabati, zote hizo ni program zitazotofaidisha jamii na kutoa  suluhisho katika maisha yao ya kila siku”

Dhamira yetu ni kujenga kizazi kipya ambapo katika umri mdogo wataweza kutumia teknolojia ya TEHAMA na kuingia katika elimu ya juu wakiwa tayari na uelewa wa kujihusisha na utengezaji wa programu mbalimbali zitakazoenda sambamba na karne ya sasa na kuleta tija katika kukuza uchumi wa nchi” alisema Mulamula.
  Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora (katikati) akiongea wakati wa uzinduzi wa maabara ya Kompyuta itakayojulikana kama“Airtel Fursa Lab” ili kufundisha watoto na vijana mafunzo ya TEHAMA chini ya usimamizi na ushirikiano kati ya Airtel na Dar Teknohama Bussiness Incubator (DTBI)  kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na Mkurugenzi Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula (kushoto). “Airtel Fursa Lab” imezinduliawa leo kwenye shule ya msingi ya kijitonyama iliyoko wilaya ya Kinondoni.
 Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora (wapili kulia) akikata utepe ili kuzinduzia  maabara ya Kompyuta ya “Airtel Fursa Lab” ili kufundisha watoto na vijana mafunzo ya TEHAMA chini ya usimamizi na ushirikiano kati ya Airtel na Dar Teknohama Bussiness Incubator (DTBI)  kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na Mkurugenzi na kushoto kwake ni Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula na Mwenyekiti wa kamisheni ya ICT Tanzania Maharage Chande na Mweyekiti wa Bodi ya Shule ya msingi Kijitonyama John Mutajwaha “Airtel Fursa Lab” imezinduliawa leo kwenye shule ya msingi ya kijitonyama iliyoko wilaya ya Kinondoni.
 kushoto ni Mwanafunzi wa shule ya msingi  Aghakan Serira Telerico akielezea jinsi alivyotengeneza program ya Robot  kwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora wakati alipozindua Maabara hiyo  kwenye shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya kinondoni, wanaoshudia ni Mkuu wa DTBI Eng. George Mulamula na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano ambao ndio wasimamizi na wadhamini wa  Maabara hiyo. “Airtel Fursa Lab” imezinduliwa leo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnolojia
Mwanafunzi wa shule ya msingi  Aghakan mzizima Brayan Basimaki (wakwanza kushoto) akielezea jinsi anavyotengeneza program zake za kompyuta  kwa Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais , Prof. Faustin Kamuzora wakati alipozindua Maabara hiyo  kwenye shule ya msingi ya kijitonyama wilaya ya kinondoni, Maabara hiyo. “Airtel Fursa Lab” imezinduliwa leo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi katika masomo ya Tehama na kukuza ujuzi katika maswala ya kitechnologia.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA NYANGAO WATEMBELEA BUNGE NA KUKUTANA NA MAJALIWA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyangao iliyopo Jimbo la Mtama mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Kushoto kwake ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete na wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye  wakisalimiana na wananfunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge jini Dodoma Julai 4, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao iliyopo katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma Kikwete na kulia ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyangao iliyopo katika Jimbo la Mtama Mkoani Lindi kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wapili kushoto kwake ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA MSHINDI WA TUZO YA UINGEREZA

0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Samuel Mwanyika, mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Katikati ni Mama wa mtoto huyo Sophie Mshangama.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel Mwanyika aliyeshinda tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa Juni 8, 2017 na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo (Down's Syndrome Association) ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel. 
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akiwa na Samuel Mwanyika (wa pili kushoto), mshindi wa tuzo ya Stephen Thomas iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Watu wenye Mtindio wa Ubongo ya Uingereza kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 4, 2017. Wa kwanza kushoto ni Elias Mwanyika (kaka yake Samuel) akiwa na picha iliyoshinda tuzo hiyo na wa kwanza kulia ni Sophie Mshangama ambaye ni mama yake Samuel.

MPAMBANO WA YANGA NA KOREA JUMAMOSI JUNI 8, 2017 UWANJA WA UHURU WA TAIFA UHURU - DAR

0
0

SABASABA YAZIDI KUWA TAMU KWA WATOTO

0
0
 Watoto wakicheza katika Mgari yanayopita katika Reli Maalum Ndani ya Viwanja vya Sabasaba
 watoto wakifurahi katika Maputo ya Mtelezo yaliyowekwa ndani ya Viwanja hivyo
 watoto wakifurahi katika Maputo ya Mtelezo yaliyowekwa ndani ya Viwanja hivyo
 Watoto wakicheza katika Mgari yanayopita katika Reli Maalum Ndani ya Viwanja vya Sabasaba

Dr. Mengi ataka wasambazaji kushawishi uwekezaji

0
0
Makampuni ya Tanzania ya uwakala wa usambazaji wa bidhaa za kutoka nje ya nchi, wameshauriwa kuyashawishi makampuni ya nje kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hapa hapa nchini. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi ametoa ushauri huo jijini Dar es salaam wakati akitembelea mabanda ya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara, na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kutaka kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda.  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akielekea kukagua baadhi ya matrekta katika banda la Kampuni ya Agricom akiambatana na Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kulia kwa Dr.Mengi) alipotembelea kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

 Akifuatana na Mkurugenzi wa TPSF Bw. Louis Accaro, Afisa Biashara wa Tan-Trade Bw. Mohamed Mkadara, na Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wajasiriamali Bi. Jacquiline Maleko, Dr Mengi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo yaliyopo chini ya mwamvuli wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda, na Kilimo – TCCIA, Mfuko wa Fursa sawa kwa wote-EOTF, na Banda la Kampuni ya Agricom, ambayo Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Angelina Ngalula alielezea jinsi ilivyojipanga kusambaza zana za kisasa za kilimo ili kumpunguzia mkulima gharama za uzalishaji. Katika majumuisho yake Dr Mengi alishauri Tan-Trade na TPSF washirikiane katika kuangalia namna ya kuboresha zaidi maonyesho hayo, hususan katika kuboresha mabanda ya maonyesho ili yalingane na hadhi halisi ya kimataifa.  Meneja Mkakati wa Kampuni ya Agricom Afrika, Eric Mwidunda (kushoto) akitoa maelezo kuhusu ubora wa matrekta hayo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi (wa pili kushoto) alipotembelea kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Agricom, Bi. Angelina Ngalula (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi alipotembelea banda la kampuni hiyo kujionea huduma zao kwenye Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mratibu wa miradi na mshauri wa Maisha Finance Ltd, ambao ni wakopeshaji wa zana zote za kilimo yakiwemo Matrekta ya kampuni ya Agricom, Erasmus Erneus akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wateja, Apollos Rweikiza aliyetembelea banda la Agricom katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko (wa pili kushoto) alipowasili kwenye banda la TWCC yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Fedha, Masoko na Usafirishaji wa C.E Holdings Ltd, wauzaji wa vito vya Afrika, Maria Pagama akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha juu na chini ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akifurahia jambo na wanawake wafanyabiashara kwenye banda la TWCC katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Picha ya juu kulia ni Noreed Mawalla wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC). Mkurugenzi wa Tanfood and Spice Co. Investment watengenezaji wa bidhaa za kutunza ngozi zinazotokana na mimea, Bi. Rona akitoa maelezo ya bidhaa halisi za kutunza ngozi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi alipotembelea banda la TWCC kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitoa maelekezo kwa Noreed Mawalla wa TWCC (katikati) wakati akitembelea banda la Chama cha wafanyabiashara wanawake kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama bidhaa mbalimbali katika banda la Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) lililopo katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa akimuongoza Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi mara baada ya kuwasili katika banda la EOTF kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr Reginald Mengi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Joane Art Craft, Culture & Desigin, Bi. Joane Baigana (kulia) alipotembelea banda la EOTF kwenye maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama kazi mbalimbali za wakinamama wajasiriamali kwenye banda la EOTF katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisalimiana na wanawake wajasiriamali wanaofadhiliwa na EOTF akiendelea kutembelea wajasiriamali katika maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Anayemuongoza ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF yanakoendelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika Uwanja wa Maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.[/caption] [caption id="attachment_2397" align="aligncenter" width="1404"] Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akitazama moja ya vitabu katika banda la Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu lililopo ndani ya banda la EOTF. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa. Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania – TPSF Dr. Reginald Mengi akipata maelezo ya huduma mbalimbali za mikopo riba nafuu kwa wanawake kutoka kwa Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanzania Women's Bank, Renita Michael (kulia) ndani banda la EOTF wakati alipotembelea maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Uwanja wa maonesho ya Biashara wa Mwl J.K Nyerere (Saba Saba) barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. 

Katikati ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa na Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Jacqueline Maleko.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULY 5, 2017

0
0



















KAIMU JAJI MKUU, WAZIRI MWIJAGE WATEMBELEA BANDA LA WCF

0
0

 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto), akikaribishwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Sebera Fulgence, alipotembela banda hilo kwenye hema la Jakaya Kikwete viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Julai 4, 2017. Mhe Profesa Hamisi  alitumia kwa uchache dakika 15 akiwa na shauku ya kupata taarifa zaidi kuhusu kazi na majukumu ya Mfuko huo. 

Mhe Profesa Hamisi alielezwa kuwa Mfuo huo umeundwa mahsusi kwa ajili ya kutoa fidia stahiki kwa Mfanyakazi aliyepata ugojnwa au kuumia mahala pa kazi. Hali kadhalika, alielezwa kuwa pamoja na kwamba Mfuko huo  ni wa Hifadhi ya Jamii, namna ya uchangiaji wake unatofautiana na Mifuko mingine, ambapo Mwajiri ndiye anawajibika kisheria kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi wakati Mifuko mingine, wachangiaji ni wote, mwajiri na mwajiriwa. 

Wakati hyuo huo, Waziri anayehusika na sekta ya Viwanda na Biashara, sekta ambayo inatoa ajira kubwa kwa wafanyakazi, naye alipata fursa ya kutembelea banda hilo ambapo kama ilivyokuwa kwa Kaimu Jaji Mkuu naye alielezwa majukumu yanayotekelezwa na Mfuko ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Sebera Fulgence, alimueleza kuwa sekta ya viwanda na biashara ni miongoni mwa sekta zinazotoa wanachama wengi kwenye Mfuko huo, ukiachilia elimu na afya na kwamba Mfuko umekuwa ukiendelea kutoa elimu zaidi kwa waajiri kuhusu umuhimu wa kuchangia wafanyakazi wao kwa manufaa ya mwajiri na mwajiriwa pindi yanapotokea madhara. 

Mfuko wa WCF ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi (sura 263 marejeo ya mwaka 2015).
 Profesa Ibrahim Hamisi Juma, akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence.(hayupo pichani)
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia maeelzo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Sebera Fulgence(kulia), akimpatia maelezo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma (kushoto) na ujumbe wake kuhusu shughuli zifanywazo na WCF.
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akizungumza jambo na Maafisa wa WCF, Bw. Sebera Fulgence (wapili kushoto) ambaye ni Afisa Uhusiano Mwandamizi na Bi.Bi.Inocencia William
 Mhe. Waziri Mwijage, (kulia), akiagana na Bw. Sebera baada ya kutembeela banda hilo na kuelimishwa kuhsuu majukumu ya Mfuko.
 Maafisa wa WCF wakiwa tayari kuwahudumia wananachi
 Bi.Bi.Inocencia William, (kushoto), afisa wa WCF akiwahudumia wananchi hawa waliofika kwenye banda la Mfuko huo
 Mwananchi akisoma kipeperushi chenye taarifa mbalimbali za shughuli na majukumu yanayotekelezwa na WCF
 
Mhe. Profesa Hamisi akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka
 Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Profesa Ibrahim Hamisi Juma, (kushoto) akiaghana na wafanyakazi wa WCF

 Bw. Sebera akisalimiana naMchambuzi wa soka hapa nchini, Bw. Ally Mayai kwenye banda la Mfuko wa WCF


Viewing all 46200 articles
Browse latest View live




Latest Images