Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1291 | 1292 | (Page 1293) | 1294 | 1295 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) anayeshughulikia huduma za jamii, Asangye Bangu amewataka watanzania kuanza kuhamasika kutembelea hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro ili kujionea mambo mbalimbali yanayopatikana ndani ya hifadhi hiyo.

  Bangu amesema hayo akiwa katika banda la balozi wa hifadhi hiyo Mrisho Mpoto lililopo katika viwanja maonesho ya biashara vya Babasaba jijini Dar es salaam.

  “Hii ni fursa ya pekee kwa watanzania kuanza kuhamisika na kwenda kuangalia maajabu ya hifadhi ya Ngorongoro, kusema kweli tunakosa uhondo kabisa. Kwa sababu wewe jiulize mzungu anapanda ndege na kutumia gharama kubwa kuja Ngorongoro wakati sisi wenyewe tupo karibu hapa tunashindwa kuwapeleka watoto wetu kijifunza mambo mbalimbali,” alisema Bangu.

  Alisema Ngorongoro Crater ni mbuga ya wanyama mfano wa bakuli kubwa lililoundwa miaka 25 elfu iliyopita baada ya milima miwili Makaroti na Satiman kulipuka na kutoa tope lenye moto. Tope hili ndilo lilikuwa na tabaka tatu za udongo na kuumba bonde lililofanana na bakuli kubwa ambalo wenyeji wa kabila la Kimasai walilipa jina la Ngorongoro Kaldera.

  “Kijiji cha Malanja ni cha pekee katika bonde la Ngorongoro katikati ya Milima ya Makaroti ambao ni mkubwa na Satiman ambao ni mdogo. Wenyeji wa kijiji hicho huendesha Maisha yao kama kawaida ya kufuga mifugo yao ndani ya mbuga wakichanganyika na wanyama pori,” alisema

  Pia katika bonde hilo kuna mto mmoja ambao unatoka Olmot Crater, Ziwa Magadi ambalo wakati wa kiangazi hukauka na kutoa vumbi aina ya majivu ambayo wenyeji wa Kimasai hutumia kuwalisha Ng’ombe kama dawa ya kudhibiti magonjwa.

  Alisema huwezi kuitaja Hifadhi ya Ngorongoro Crater bila kuwataja wanyama wakubwa wajulikanao kama “Big Five”, ambao ni Faru, Tembo, Chui, Nyati na Simba.

  “Kinachovutia zaidi ni kuona wanyama wote, wakali na wapole jinsi wanavyoishi kwa pamoja hadi pale tu wanapokuwa na njaa ndio hubadilikianana. Penye kundi la Nyumbu, Faru, Punda milia, Ngiri, Nguruwe na kadhalika utawakuta pia Simba pembeni wamelala wakipunga upepo baada ya kupata mlo wa mchana. Hii ni kuonyesha kwa jinsi gani wanaishi kama familia moja na wako katika nyumba moja,” alisema B

  Bangu aliwataka watanzania kuacha kusimuliwa kuhusu ufahari wa Ngorongoro bali watembelee mbuga hiyo kwaajili ya kujionea wenyewe

  0 0


  0 0

  Na,Jumbe Ismailly SINGIDA July,03,2017 Nyalandu 


  MBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini,Lazaro Nyalandu ametangaza donge nono kwa timu itakayokuwa bingwa wa mashindano ya kombe la Mbunge huyo,maarufu kwa jina la “NYALANDU CUP” linalotarajia kuanza mwezi wa nane mwaka huu.

  Kombe hilo litakaloanza mwezi ujao,litashirikisha timu za mpira wa miguu kwa wanaume na mpira wa miguu kwa wanawake na kilele cha mashindano ya kombe hilo kitafanyika katika Kijiji cha Ngamu,kilichopo katika Kata ya Mwasauya.

  Akitangaza msimamo wake huo mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour,Nyalandu alisema kwamba tangu alipochaguliwa kuwa mwakilisha wa wananchi wa jimbo hilo la Singida Kaskazini hajawahi kuandaa ligi ya aina yake kama hiyo inayotarajiwa kuanza kuchezwa katika jimbo zima.

  “Nilimwambia Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru nafikiri nilikuwa namnong’oneza kwamba mwenge ukipita na hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu nimekuwa Mbunge halafu kuchezesha mambo hii ya mechi”alifafanua ‘Mimi nafanyaaga maskolashipu,wasome sekondari,wafanye nini,mambo ya maji nafikiri sasa hivi tutaenda kwa zote, kwa hiyo ningependa kuanzisha ligi ambayo itafanyika ya mpira wa miguu lakini nataka iende sambamba na ligi ya wanawake” alisisitiza Mbunge Nyalandu.

  Kwa mujibu wa Mbunge huyo kutakuwa na ligi ya wanaume na itafungwa pamoja na ligi ambayo itakuwa ni ya wanawake na ligi hiyo watashirikiana kuitangaza,kuiunda na kuiandaa na serikali ya wilaya hiyo pamoja na Halmashauri hiyo kwa ujumla.

  “Kwa hiyo itafanyika kwa uwazi kabisa na kwa wale wataalamu ambao ndiyo waandaa ligi watahusika katika kuiandaa kitaaalamu na mwisho wa ligi,mwisho wa yote na leo nilikuwa nimepanga tu kusema zawadi kwa upande wa mpira wa miguu”aliweka bayana Mbunge huyo wa jimbo la Singida Kaskazini.

  Aidha Mbunge huyo hata hivyo pamoja na kutangaza zawadi kwa washindi wa mashindano hayo,vile vile alitangaza mapendekezo yake ya mahali patakapochezwa mchezo wa fainali ya ligi hiyo kuwa ni katika Kijiji alichokiita Kijiji pendwa cha Ngamu.

  Akitoa sababu za mapendekezo hayo ya mchezo wa mwisho,Nyalandu alitanabaisha kwamba Kijiji cha Ngamu katika kata ya Mwasauya kutokana na kuwepo kwa mradi mkubwa wa Benki ya dunia wa kusambaza maji katika nyumba za watu.

  “Halafu mshindi wa kwanza atapata zawadi,mshindi wa pili atapata zawadi na mshindi wa tatu atapata zawadi,ambapo kwa mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi milioni tatu na kombe,jezi na mpira,mshindi wa pili zawadi shilingi milioni mbili,jezi na mpira na mshindi wa tatu zawadi shilingi milioni moja,jezi na mpira”aliweka bayana zawadi hizo kwa washindi.

  Hata hivyo Nyalandu alitangaza pia zawadi kwa washindi wa mpira wa miguu wanawake kuwa ni shilingi milioni tatu kwa bingwa wa mashindano hayo,shilingi milioni mbili kwa mshindi wa pili na mshindi wa tatu shilingi milioni moja.

  Naye Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaaifa mwaka huu,Amour Hamad Amour alishauri ushirikishwaji ufanyike ili kupata jina la ligi hiyo na hata hivyo hakusita kusisitiza kujittokeza kwa timu nyingi kushiriki katika mashindano hayo ili yawe mashindano ya kweli.
  Mchezaji wa timu ya Mtinko Fc,Yusufu Samsoni (mwenye jesi yenye rangi ya bluu) alipomtoka mchezaji wa timu ya Msange Fc,Yasini Athumani na kwenda kuifungia timu yake bao la pili na la ushindi.
  Baadhi ya wachezaji wa timu ya Msange FC wakifanya mazoezi katika uwanja wa michezo wa shule ya msingi Mtinko kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao matokeo yalikuwa Mtinko FC 2 na Msange FC 1.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

  0 0

   Meneja Masoko wa Benki ya Access Bank ,Sijaona Simon akizungumza na Mmoja wa Wateja waliotembelea Banda la benki hiyo hili kuweza kujipatia huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo mikopo na akaunti ya malengo Maalum

   Afisa Mikopo wa Access Bank , Marggoreth Riziki  akizungumza na mmoja  wateja juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo kwa wajasiliamali wadogo
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Godbless Exaud  akizungumza na mmoja  wateja juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo kwa wajasiliamali wadogo
   Afisa Mikopo wa Access Bank ,  Isaak Malaba akikabidhi zawadi ya mfuko wa Acces Bank kwa mmoja wa wateja waliotembelea banda lao
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Marggoreth Riziki na Godbless Exaud wakiwahudumia wateja ndani ya Sabsaba
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Magdalena Kijuu akikabidhi Zawadi ya T-Shirt kwa mteja aliyefungua Akaunti katika banda lao la Maonyesho  ya Sabasaba
  Afisa Mikopo wa Access Bank , Alex akitoa huduma mteja
   Sehemu ya Wateja waliofika katika Banda hilo
  wafanyakazi wa Accs Bank wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda la Maonyesho Sabasaba

  0 0

  Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutoa huduma za Elimu ya afya Nchini Marekani Bi. Asha Mustafa Nyang’anyi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu ujio wao hapa Zanzibar.
  Bwana. Amiri Muhammed Amiri akimuonesha fangas Daktari bingwa wa ngozi Mamotheo alipokuwa akitoa matibabu katika hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. 
  Baba wa mtoto Abdulmajid akiwaonesha madaktari bingwa wa maradhi ya ngozi namna mwanawe alivyodhurika kwa kufanya mabaka mwilini katika hospitali ya Mnazimmoja mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.


  Na Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar 03-07-2017

  Wananchi wa Tanzania wanaoishi Marekani wanadiaspora wakishirikiana na Madaktari bingwa wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi.

  Zoezi la kutoa huduma hizo za matibabu bure linafanyika kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya Mnazi mmoja.

  Akizungumza na waandishi wa habari huko katika kitengo cha maradhi ya ngozi kwenye hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Mwanadiaspora Idi Seif Sandaly amesema wameamua kuja nchini hapa kutoa huduma hizo ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo mbalimbali.

  “Tumekuja Zanzibar kwa lengo la kuwasaidia wananchi ambao wana maradhi mbali mbali na kuwapatia matibabu kwa kupitia jumuiya yetu ya marekani Health Education Development kwa kutibu maradhi ya ngozi , sukari na pressure pamoja na maradhi ya akinamama.” Amesema Mwanadiaspora huyo.

  Sandaly amesema wapo kwa muda wa siku tatu na wamekuja na dawa za kutibia maradhi hayo ambapo dawa hizo wanazitoa bure bila ya gharama zozote kwa wananchi.

  Amesema katika matibabu yao wanatarajia kutoa huduma kwa zaidi ya Wananchi 3,000 watakaofika katika Hospital hiyo ya Mnazi mmoja.

  Akifafanua kuhusu gharama za Dawa hizo ambazo wamekuja nazo kutoka Marekani amesema zaidi ya Dola Million moja za Marekeni zimetumika kwa ajili ya kununulia Dawa hizo.

  Hata hivyo ameongeza kuwa Nusu za Dawa hizo zitatumika Zanzibar na Nusu yake zitapelekwa Mkoa wa Bukoba kwa lengo la kusaidia matibabu mkoani huko

  Nae Daktari wa maradhi ya Ngozi kutoka Marekeni Dkt Mamotheo Lepheana amesema amefarijika kuona wananchi wamejitokeza kwa wingi hasa wa maradhi ya ngozi.

  Sambamba na hayo mgonjwa aliyepata matibabu hayo ya ngozi Masika Juma Mussa mkaazi wa Mwera amesema ameshukuru kupatiwa huduma hiyo na kuiomba serikali iendeleze kuleta wataalam kama hao wanaotaka kusaidia jamii .

  Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo la kutoa huduma za Elimu ya afya Asha Mustafa Nyang’anyi amesema ameamua kuja Zanzibar kwa sababu wananchi wa hapa ni wakarimu na wanaojali kusaidiwa.

  0 0

  NA CHRISTINA MWAGALA ,OFISI YA MEYA WA JIJI

  MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema watanzania hawajafikia hatua ya kubaguana kwa kiitikadi ya vyama, Dini, Kabila badala yake wote wanapaswa kutangaza hali ya Umoja, Upendo na Mshikamano katika nchi yao.

  Meya Mwita alitoa kauli hiyo jijini hapa jana, wakati wa harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Kanisa la kisasa la Tanzania Assemblies Of God (TAG) lililopo Kivule ,Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini hapa ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa watanzania wanapaswa kuwa wamoja ili nchi iendelee kuwa na amani.

  Alisema yapo mambo mbalimbali ambayo yanajitokeza ndani ya nchi ambapo kama watanzania , kwakushirikiana na viongozi wa dini kwa pamaoja wanapaswa kusimama na kuliombea Taifa ili kuendelea kudumisha amani iliyopo.

  " Tangu nimezaliwa sijawahi kushuhudia vita, machafuko katika nchi yetu, kikubwa huwa naona amani iliyotawala, Upendo, na umoja , sasa nawasishi sana ndugu zangu tuendelee kuwa wamoja tusibaguane, kwa namna yoyote ile , ili nchi yetu iendelee kuwa na amani" alisema Meya Mwita.

  "Baba wataifa Hayati Mwalim Julius Nyerere enzi ya uhali wake alikuwa akisisitiza sana kulinda amani ya nchi yetu, na sisi ambao tupo hai hadi sasa , mambo ya vyama, Udini, Ukabila tuweke pembeni tusimame kama Taifa moja.

  Awali akijibu risala iliyoandaliwa na uongozi wa kanisa hilo, Meya Mwita aliahidi kuchangia katika ujenzi huo mifuko 100 ya Simenti na kiasi cha Fedha shilingi 500,000 huku aliwataka waumini wa kanisa hilo kujitolea ili kufanikisha ujenzi huo.

  Risala hiyo ilieleza kujenga kanisa la kisasa lenye uwezo wa kuchukua waumini 600 ambapo jumla ya shilingi milioni 95 zinahitajika ili kukamilisha ujenzi huo.

  0 0
 • 07/03/17--08:40: WOTE MNAKARIBISHWA

 • Ni ijumaa hii ya tarehe 7...yaani 77. Katika ukumbi wa kiteto Hall...njooni tyjumuike pamoja, tule tunywe, tucheze na tuelimike. Ni maalum kwa watu wanaojiamini, wenye malengo makubwa na kiu ya kutaka kufika mbali. Kwa sh 25,000 tu. Kuanzia saa 11 jioni hadi saa nne usiku. 

  Ni kwa ajili yako mwanamke unayejitafutia kipato. Tiketi zinapatikana Luluz Hair Kinondoni...Happy Massage ndani ya hoteli ya Lamada Ilala...Kwa Junaither Kinondoni, Pendomackay Plussize Sinza Kamanyola, Becket Boutique Namanga, Shekinah Vipodozi Asilia Kimara Korogwe, Loves Design Sinza...pia ukihitaji kuletewa tiketi utafikishiwa. 

  kwa mawasiliano zaidi tupigie simu 0752910910, 0714898481 au 0786625969. @kitengeprintmedia @kitengeprintmedia

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena juzi katika uwanja wa chuo kikuu cha Dar es salaam, ikiwa ni hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

  Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Mchenga na The fighter na timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 109 dhidi ya 41 za The fighter .

  Mechi ya pili iliwakutanisha Flying dribblers ambaye alitoka na ushindi wa vikapu 91 dhidi ya Osterbay aliyepata vikapu 82, TMT wakaumana na Dream chaser na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 96 dhidi ya vikapu 73.

  Mechi ya nne iliyowakutanisha Kurasini Heat na Kigamboni Heroes ilimalizika kwa vikapu 64 vya Kurasini Heat dhidi ya 59 vya Kigamboni Heroes. 

  Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za Robo fainali na kupatikana kwa timu nne zitakazoendelea kwenye hatua ya nusu fainali kutachezeshwa kwa droo maalumu kwa ajili ya kuzipanga timu zitakazochuana kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano haya ya Sprite BBall Kings kwa mwaka 2017.

  "Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya wiki hii ndizo zilizofanikiwa kuendelea katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Sprite Bball kings 2017 "amesema Basilisa.

  Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio huku mshindi akitarajiwa kuondoka na kitita cha shiling milion 15.
  Timu ya The fighter (jezi nyeupe) ikisalimiana na timu ya Mchenga (jezi nyeusi) wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali ya shindano la Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya Mchenga kushinda kwa vikapu 109 dhidi ya vikapu 41
  Mchezaji wa timu ya The Fighter akiambaa na mpira wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Mchenga  wa mashindano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 109 dhidi ya 41.
  Mchezaji wa timu ya kikapu ya TMT  akipiga pigo la adhabu kwa upande wa timu yake wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Dream Chaser  wa mashindano ya Sprite Bball Kings uliomalizika kwa timu ya TMT  kuibuka na ushindi wa vikapu 96 dhidi ya 73.
   Timu ya Dream Chaser  (jezi nyeupe) na TMT (Jezi buluu) wakikaguliwa na waamuzi wa mchezo huo kabla ya  kuanza kwa mchezo wa hatua ya robo fainali ya shindano la Sprite Bball Kings.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Dini mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ngoma za asili kutoka kikundi cha Bujora mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiombewa sala na Viongozi mbalimbali wa dini kutoka Kanda ya ziwa mara baada ya kuwasili mkoani Mwanza. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kona ya bwiru katika barabara ya Airport wakati akitokea uwanja wa ndege wa Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinunua Karanga kutoka kwa Mmachinga anayefanya biashara katikati ya jiji la Mwanza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa katikati ya jiji la Mwanza wakati akielekea Uwanja wa Nyamagana kuangalia mechi kati ya Buhongwa United na Timu ya Nyamwaga.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono washabiki wa mpira wa miguu wakati akitoka katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. PICHA NA IKULU


  0 0


  Mtafiti Mkuu Kiongozi Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR) Leonard Mboera akizungumza kwenye mkutano wao wa Watafiti,uliohusu Utafiti kuhusu taarifa za vifo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania,uliofanyika katika taasisi hiyo mapema leo mchana,ambapo watafiti mbalimbali walihudhuria na kuwasilicha mada zao sambamba na kuzijadili kwa pamoja.


  Katika mkutano huo,Dkt Leonard alisema kuwa wamefanya utafiti wa kuangali eneo kubwa na vyanzo na sababu za vyanzo katika hospitali zetu hapa nchini,alisema kuwa katika utafiti huo vya wameufanya kwa kujumuisha hospitali ya Taifa Muhimbili,hospitali tatu za rufaa,hospitali maalum ambazo ni Kibong'oto,Mirembe,taasisi ya saratani ya ocean road,taasisi ya MOI na pia wakajumlisha hospitali zote za mikoa na asilimia kumi ya hospitali za Wilaya.

  Dkt Leonard alisema kuwa dhumuni la kufanya utafiti huo ni kuangalia upatikanaji wa takwimu za vifo katika hospitali hizo na pili kuangalia ni magonnjwa gani ambayo yanasababisha vifo hospitalini "na zoezi hilo lilianza Julai 20016 na ukusanyaji wa takwimu ulikamilika mwezi Novemba,2016 ,baada ya hapo tukawa tunafanya uchanganuzi",alisema Dkt Leonard.

  Alisema kuwa walichobaini katika uchanganuzi huo katika makundi ya magonjwa kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO),Magonjwa ya kuambukiza,maradhi yanawakuta Wakina mama wakati wa uja uzito na maradhi yanayohusiana na Lishe ndio yanayoongoza (kundi kubwa) kwa kuwa na asilimia 57,kundi kubwa, na Magonjwa yasiambukizwa ni asilimia 30 (kundi la kati) na kuna kundi dogo la Maradhi linalosabishwa na ajali ambalo linachukua asilimia 15.


  kutokana hali hiyo Magonjwa yasio ambukiza yameanza kuchukua nafasi,lakini kwa upande mwingine ugonjwa wa Malaria ndio una oongoza kuleta vifo katika hospitali zetu.

  Baadhi ya Watafiti waliokutana leo katika mkutano wao,ambao ulibeba dhima ya 'Utafiti kuhusu taarifa za vifo vinavyotokea katika hospitali za Tanzania'.

  0 0


  0 0


  *TAARIFA MUHIMU KWA WAGOMBEA WA UVCCM KATIKA DHAMIRA  YA KUJENGA HAIBA YA DEMOKRASIA YA KWELI NA KURUDISHA UPYA MAADILI NA NIDHAMU YA  UCHAGUZI HURU*

  Demokrasia ni jambo muhimu linalohitajika kuheshimiwa na kuenziwa ndani na nje ya Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa miaka kadhaa kumekuwa na shutuma pia tuhuma zilizokaribia kuotesha mizizi ya kuwepo  rushwa ambazo nusra zivunje heshima ya chama chetu  na jumuiya zake. Jambo hilo sasa  halitaruhusiwa tena wala kuachiwa lifanyike .

  Kiongozi wa UVCCM mahali popote atachaguliwa baada ya kufanyika chaguzi huru na za haki, kuzingatia Kanuni na Taratibu za Uchaguzi kama zilivyoagizwa na vikao husika bila ya kukiuka, kupuuzwa au kuvunjwa.

  Nia ya UVCCM ni kujenga haiba mpya na njema ya kuheshimu misingi ya demokraia ya kweli, kuwa na adabu na kufuata nidhamu, miiko na maadili kwa kila anayetaka kuchagua au kuchaguliwa.

  Jana Jumapili tarehe 02/07/2017 zoezi la utoaji fomu kwa Waombaji wa nafasi mbali mbali za Uongozi katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM lilianza rasmi ngazi ya Wilaya, Mikoa na Taifa.

  • Kwa Ngazi ya Taifa nafasi zote fomu zinatolewa Dodoma ghorofa ya 3 chumba Na. 45, Ofisi Ndogo za UVCCM Dar es Salaam ghorofa ya 7 na Afisi Kuu ya UVCCM Gymkana Zanzibar.

  Fomu zote zirejeshwe si zaidi ya tarehe 10/07/2017 Saa 10.00 Jioni katika maeneo yaliyoainishwa.

  Ifahamike kuwa kila  Kijana wa Chama Cha Mapinduzi  ana haki ya msingi kugombea nafasi yoyote ile kwa mujibu wa Kanuni ya UVCCM na katiba ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM).

  •Kama iliyo Haki na Wajibu wa mwanachama kugombea, kuchagua au kuchaguliwa, ndivyo inayostahili mwanachama kufuata taratibu na kuheshimu kanuni pamoja na taratibu za uchaguzi.

  •UVCCM imekusudia kurudisha nidhamu ya Chama hasa katika suala zima la kugombea nafasi za uongozi na haki ya kuchagua au kuchaguliwa.

  •Muomba nafasi anayo haki ya kutia nia, kuchukua fomu ya kuwania Uongozi bila ya kufanya mbwembwe, shengesha au mikogo ambayo kwa namna moja au nyingine itaonyesha hali ya kujinadi mapema, kujitangaza na kufanya kampeni.

  •  Muomba nafasi yoyote ajaze fomu zake kwa uangalifu, azingatie tarehe na siku ya kurudisha mahali husika tena kwa kujali wakati uliopangwa kikanuni na kuheshimu taratibu.

  •Sifa au wasifu wa kila muomba nafasi kwa kadri atakavyojaza fomu yake utajielekeza na kuandikwa kama ilivyo katika kitabu maalum cha wagombea wote ambacho kitasomwa na wajumbe wapiga kura siku ya uchaguzi husika hivyo ni vyema kuwa makini na taarifa zako.

  •Ni marufuku na hatakiwi kabisa muomba nafasi yoyote ile Mara baada kuchukua au kurejesha fomu kuandika bango au kipepeprushi na kuvigawa, kuvieneza au kuwatuma wapambe wake wakati taratibu nyengine za vikao bado hazijakamilika.

  *Kila muomba nafasi atapata nafasi ya kujieleza, kutoa wasifu wake, kutaja dhamira na malengo yake mbele ya wajumbe wa Mkutano husika wa kuchaguliwa si kinyume na hivyo baada ya taratibu za Vikao kukamilika.

  •Kuanza mapema kampeni au wapambe kufanya ushabiki wa kisiasa na kumnadi, kumpiiga debe pia kwenda katika vyombo vya habari na kueleza wasifu, sifa au kutaja nafasi anayogombea na kujinadi kutahesabika ni kufanya kampeni mapema na kumfanya apoteze sifa.

  •Ni marufuku na haitaruhusiwa kabisa muda ukifika kwa mgombea yeyote kufanya kampeni za kihuni kwa kutumia lugha chafu, siasa za maji taka, matusi, dharau kinyume na ubinadamu pia kushiriki kejeli dhidi ya wenzake.

  •Muomba nafasi katika ngazi yeyote ambaye hatazingatia wala kuheshimu na kutofuata maelekezo haya anaweza kujipotezea sifa ya kuteuliwa na kushiriki kwake katika chaguzi huru na za kidemokrasia ndani ya UVCCM

  *ANGALIZO:*

  • Kuachia hayo yote yafanyike bila ya kuyadhibiti , kuyaasa na kuyakemea ni mwanzo wa kuiruhusu au kufungua milango atakayopita adui rushwa .

  •Rushwa ni kikwazo cha maendeleo ya demokrasia na adui hatari wa haki, haitakubalika wala kuruhusiwa muomba nafasi  kutoa au kupokea na kugawa rushwa ndani ya chaguzi za jumuiya yetu.

  •Chaguzi za jumuiya zitafanyika kwa njia huru na za  uwazi huku kila na mgombea akipitishwa jina lake na vikao husika vya Kikanuni na Kikatiba  baada ya kuonekana kuwa amekidhi masharti  na kufuata kanuni za uchaguzi katika kila hatua husika bila kukiuka.

  •Uchaguzi ni kipimo cha ukomavu wa demokrasia ya kweli bila kufanyika mizengwe na hila ndani ya jumuiya kwa lengo la kusimamia shabaha na misingi sahihi itokanayo na miongozo, maelekezo na kuheshimu utaratibu unaohimizwa na  Chama Cha Mapinduzi na kutii maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Mwenyekiti wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

  •Waomba nafasi hawaruhusiwa kutembea toka Wilaya au  Mkoa mmoja hadi mwingine, kukusanya wajumbe, kujinadi au kuelezea dhamira yake ya kuchukua fomu kabla ya siku ya uchaguzi kwani kuyaachia hayo na mengine yafanyike huko ni kuipalilia rushwa istawi ndani ya chaguzi zetu .

  Ni matumaini yangu kuwa Vijana mtaendelea kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuomba Uongozi kutimiza haki yenu ya Kidemokrasia ndani ya Jumuiya yetu.

  Nawatakia kila la heri.

  *KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI*

  *Shaka Hamdu Shaka* *(MNEC)*
  *KAIMU KATIBU MKUU*

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa bodi ya Bodi ya Utalii Tanzania ,Jaji Thomas Mihayo  akizungumza na wadau wa mikutano wakati wa ufunguzi Semina Maalum ya wadau hao kuhusu utalii wa mikutano hapa nchini ambao utaweza  kusaidia mapato ya sekta ya utalii na Taifa kwa ujumla.
   Mwenyekiti wa Bodi ya AICC, Balozi Dkt  Ladislaus Komba  akizungumza katika Semina ya wadau wa mikutano juu ya utalii wa mikutano ambao utaweza kukuza utalii nchini  na mapato ya mwekezaji mmoja mmoja kupitia mikutano hiyo
   Washiriki wa mkutano huo kutoka bodi ya utali nchini TTB wakifatilia kwa ukaribu yanayozunmzwa katika mkutano huo
   Mkurugenzi wa Mikutano kutoka AICC,Mkunde Senyangwa akizungumza na wadau walioshiriki Semina hiyo juu ya umuhimu wa utalii wa mikutano nchini
   Sehemu ya wadau walioshiriki mkutano huo wakisilikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa
   Mkufunzi kutoka kampuni ya Business Tourism  ya Afrika Kusini ,Rick Taylor akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nchi nyingi zilivyofanikiwa kupitia Utaliihuo wa Mikutano
  Wajumbe wa mkutano huo wakizungumza jambo na  Mwenyekiti wa bodi ya Bodi ya Utalii Tanzania ,Jaji Thomas Mihayo

  0 0

  Msanii wa muziki wa asili ambaye pia ni Balozi wa Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Mrisho Mpoto ametangaza deal kwa waimbaji pamoja na wapiga ala za muziki kujitokeza kwa wingi Sabasaba jijini Dar es salaam katika banda la maonyesho la Hifadhi ya Ngorongoro kwaajili ya kupata wasanii wapya watakao unda bendi mpya ya hifadhi hiyo.
  Akiongea wa wadau waliojitokeza kwa wingi katika banda hilo, Mrisho Mpoto ambaye ni balozi wa hifadhi hiyo, alisema vijana hao wanatakiwa kujua kuimba pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na vitu vinavyopatikana.

  “Hii fursa kwa waimbaji wa muziki pamoja na wapiga ala za muziki, tunatakiwa kuanzisha bendi ya muziki ‘Ngorongoro Band’, kuandaa nyimbo maalum ambazo zitakuwa zinawaelimisha watanzania juu ya ufahari wa hifadhi hii. Kuandaa wimbo ambazo zitawafanya watanzania kuijua zaidi mbuga zao , masuala ya utalii pamoja na vitu mbalimbali vilivyomo ndani yake,” alisema Mpoto.

  Katika hatua nyingine Mrisho amesema anashukuru wadau mbalimbali wanajitokeza kwa wingi katika banda la Ngorongoro kwaajili ya kujifunza mambo mbalimbali kuhusu hifadhi ya Ngorongoro pamoja na wanyama wanaopatika.

  “Kuwema kweli mambo yamekuwa mazuri sana katika banda letu, watu wanakuja kwa wingi sana kwa sababu sisi tunatoa burudani na elimu, burudani na elimu, kuna bendi hapa In African ambio inatoa burudani kila siku, kuna mastaa mbalimbali wanakuja kutoa burudani kama mlivyowana akina Stara Thomas, Solid Ground, Steve B&B na wengine wengi ambao wanakuja na kuondoka. Kwa hiyo kikubwa zaidi kwetu ni burudani na elimu,” alisema Mpoto.

  Aliongeza, “Pia tumekuwa na kipengele cha elimu kuhusu wanyama kila siku na baada ya haps tunawaita watoto waeleze vitu ambavyo wanajifunza kila siku na tumekuwa tukitoa zawadi ya mpaka tsh milioni moja kwa siku na tumeona matunda kabisa watoto wanakuja hapa hawajuhi chochote lakini wakiondoka hapa wanaweza kueleza vitu mbalimbali ambavyo vinapatika katika hifadhi ya Ngorongoro,”

  Mshairi huyo amewataka watanzania kwa ujumla kutembelea banda hili pamoja na watoto wao ili wapate kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Hifadhi ya Ngorongoro.

  0 0

   Muonekano wa Banda la Kampuni ya Zurich Insurance kwa nje katika Viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba mwaka huu.
    Meneja wa Operesheni Kampuni ya Zurich Insurance Brokers EA, Abdallah Mahamba (kushoto) akimfafanulia jambo mteja wake aliyefika katika Banda lao la Maonyesho katika Maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Zurich Insurance Brokers EA, wakiwa katika Banda lao la Maonyesho.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Zurich Insurance Brokers EA, wakiendelea kutoa huduma kwa wateja wao katika Banda lao la Maonyesho.

  0 0

   Mkurugenzi wa Huduma zaTiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akizungumza wakati akiwa kwenye banda la Mfuko huo
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  WAAJIRI na wafanyakazi wamejitokeza kwa wingi kupata elimu kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
  Maonesho hayo ya kila mwaka huwaleta pamoja wafanyabiashara ya makampuni makubwa ya kimataifa kutoka nje na dnani ya nchi, lakini pia kunakuwepo na mkusanyiko mkubwa wa wafanyakazi wa umma na binafsi wanaotoa huduma mbalimbali kwa watu wanofika kutembeela maonesho hayo.
  Mfuko wa Fidia kwa wWafanyakazi, (WCF) imetumia fursa hiyo kutoa elimu kwa waajiri na wafanyakazi ambao walifika kwenye banda la Mfuko huo na kupatiwa maelezo ya kina kuhusu kazi za Mfuko kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wake Bw. Masha Mshomba, wakurugenzi na wakuu wa idara pia.
  “WCF ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ulioanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 263 ya mwaka 2015.” Bw. Mshomba aliyasema hayo akiwa kwenye banda hilo ambapo waajiri na wafanyakazi walifika kupata elimu zaidi ya kuhusu Mfuko huo.
  Bw. Mshomba aliendelea kufafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria iliyoanzasha Mfuko huo, tofauti na Mifuko mingine ya Hifadhio ya Jamii, ambapo mwajiri na mfanyakazi hutoa michango ya kila mwezi, kwa upande wa WCF, ni mwajiri pekee ndiye anawajipika kumchangia mfanyakazi wake kila mwezi na mfanyakazi hawajibiki kutoa mchango wowote. Aidha Bw. Mshomba alieleza kuwa, dhumuni kuu la kuanzishwa kwa Mfuko huo ni kutoa Mafao ya kutosha na stahili  kwa Mfanyakazi aliyepatwa na maradhi au majeraha yaliyotokana na kazi anazozifanya Mfanyakazi huyo.
  “Na ifahamike kwamba, Mafao haya analipwa Mfanyaakzi aliyepatwa na madhara hayo imma wakati akiwa kazini au madhara hayo yanapojitokeza hata baada ya kuacha kazi ilimradi madaktari wathibitishe kuwa madhara hayo yametokana na kazi alizokuwa akifanya au kifo ambapo watalipwa wategemezi wake.” Alifafanua Bw. Mshomba.
  Miongoni mwa Mafao ambayo Mfuko utatoa kwa Mfanyakazi aliyepatwa na maradhi au majeraha ni pamoja na fao la matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, (Temporary disability), Msaada wa uangalizi wa kudumu, Msaada wa mazishi kwa mfanyakazi aliyefariki kutokana na kazi aifanyayo, lakini pia Fidia kwa wategemezi wa marehemu aliyepatwa na umauti akiwa kazini.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma zaTiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar, alisema Mfanyakazi aliyeumia kutokana na kazi aifanyayo au maradhi yaliyosababishwa na kazi aifanyayo, Mfuko utagharimia huduma za gari la kubeba wagonjwa, kumuona daktari, upasuaji, pamoja na matibabu kwa ujumla baada ya kufanyiwa tathmini na madaktari ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya namna ya kufanya tathmini kwa Mfanyakazi aliyeumia au kupata maradhi kutokana na kazi anayoifanya.
  Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasilianonna Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, aliwahimiza waajiri na wafanyakazi kutembelea banda hilo ili kupata elimu lakini pia kujua haki za Mfanyakazi na mwajiri pia.
  “Mfulo huu unatoa nafuu sio tu unasaidia Mfanyakazi kulipwa Fidia Stahili bali pia unatoa nafuu kwa mwajiri kwani ghara hizo zitasimamiwa na WCF na sio Mwajiri. “Ndio maana tunawahizimiza waajiri kote nchini kutoka sekta binafsi na umma, kutoa michango ya kila mwezi kama sheria inavyotaka.” Alisema Bi. Laura.
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akizungumza na Posta Masta Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Bw. Deo Kwiyukwa, wakati alipotembelea banda hilo.
    Mkurugenzi wa Huduma zaTiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCD), Dkt. Abdulsalaam Omar, akimfafanulia mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko kwenye hema kubwa la Jakaya Kikwete, kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam 2017, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuhusu hatua ambazo mfanyakazi anapaswa kuchukua baada ya kupata maradhi au kuumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kabla ya kupatiwa Fidia na WCF.
   Wafanyakazi hawa wakipatiwa maelezo mbalimbali yahusuyo huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), walipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam
   Afisa Uhsuiano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, (wapili kushoto), akimpatia maelezo mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo.
   Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), akizunguzma jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Elimu wa Mamlaka ya Udhibiti Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Bi. Saraha Kibonde Msika, ambaye alitembelea banda hilo. SSRA imeweka maafsia wake kila banda linalotoa huduma ya hifadhi ya jamii kwenye maonesho ya mwaka huu.
   Afisa wa WCF, (kulia), akimuhudumia mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la WCF
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Laura Kunenge, (kushoto), akimsikilzia mwananchi huyu aliyefika kwenye banda la Mfuko huo.

   Afisa wa WCF, Bi.Inocencia William, (kulia), akimpatia maelezo yenye kuhusu huduma za WCF mwananchi huyu aliyefika kujua nini hasa kazi ya Mfuko huo na faida zake kwa Mfanyakazi na Mwajiri
   Bw. Mshomba, (kulia), akiongongozana na Bi Laura, (kushoto) wakati akiwasuli kwenye banda hilo ili kuwahudumia wananchi. Kushoto ni Sebera Fulgence, Afisa Uhusiano mwandamizi wa Mfuko.


  0 0


  Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Cricket waliotoka katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea Dubai ambapo walishiriki mashindano ya Dunia yajulikanayo kama Memon World Cup na kufanikiwa kuchukua nafasi ya tano.
  Wachezaji wa timu ya Taifa ya Cricket wakiwasili nchini kutoka Dubai walikokwenda kushiriki mashindano ya Dunia ya Memon World Cup na kufanikiwa kushika nafasi ya tano na kurudi na Vikombe Viwili na Medali ,ambapo mashindano hayo yalijumuisha timu 12 kutoka nchi mbalimbali zilizofuzu
   Sehemu ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Cricket  wakiwa na mizigo yao ndani ya uwanja wa ndege wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam
   Wachezaji wa timu ya Taifa ya Cricket wakionyesha vikombe walivyopata na Medali katika mashindano ya Dunia ya mchezo huo
   Viongozi na Wachezaji wa mchezo huo wakiwa wanatoka na mizigo ndani ya uwanja wa  Kimataifa wa Ndege wa JK Nyerere wakitokea nchini Dubai kwenye mashindano ya Dunia ya Mchezo wa Cricket ambapo Tanzania imefanikiwa kushika nafasi ya tano

  0 0

  --
   Meneja Masoko wa Benki ya Access Bank ,Sijaona Simon akizungumza na Mmoja wa Wateja waliotembelea Banda la benki hiyo hili kuweza kujipatia huduma mbalimbali zinazotolewa ikiwemo mikopo na akaunti ya malengo Maalum

   Afisa Mikopo wa Access Bank , Marggoreth Riziki  akizungumza na mmoja  wateja juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo kwa wajasiliamali wadogo
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Godbless Exaud  akizungumza na mmoja  wateja juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo kwa wajasiliamali wadogo
   Afisa Mikopo wa Access Bank ,  Isaak Malaba akikabidhi zawadi ya mfuko wa Acces Bank kwa mmoja wa wateja waliotembelea banda lao
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Marggoreth Riziki na Godbless Exaud wakiwahudumia wateja ndani ya Sabsaba
   Afisa Mikopo wa Access Bank , Magdalena Kijuu akikabidhi Zawadi ya T-Shirt kwa mteja aliyefungua Akaunti katika banda lao la Maonyesho  ya Sabasaba
  Afisa Mikopo wa Access Bank , Alex akitoa huduma mteja
   Sehemu ya Wateja waliofika katika Banda hilo
  wafanyakazi wa Accs Bank wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda la Maonyesho Sabasaba

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Shirika la Ndege la ATCL Bi. Lilian Fungamtama akifurahia jambo na wananchi waliotembelea banda la shirika hilo lililopo katika banda la Maliasili katika maonyesho ya Maonyesho ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam, Maonyesho hayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Nje TANTRADE na kufanyika kila mwaka mwezi Julai.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali wakitembelea banda la Shirika la Ndege la ATCL katika viwanja vya maonyesho vya J.K.Nyerere Barabara ya Kilwa.
  Octavian Nshiu Makamu wa Rais Viwanda Shirika la TCCIA akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa shirika hilo katika banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaa,
  Baadhi ya wadau wa TCCIA wanaoshughulika na mavazi ya viwandani na ujenzi wakiwa katika banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam

older | 1 | .... | 1291 | 1292 | (Page 1293) | 1294 | 1295 | .... | 1897 | newer