Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

Mfuko wa PSPF Wakabidhi Mashuka Kwa Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar

0
0
Maafisa wa Mfuko wa PSPF kulia Faidha Khatau na Hazina Konde wakimkabidhi mashukaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Ali Salum Ali anayefutia ni Mkurugenzi Utawala na Uendeshaji Dr. Abubakar Khamis Hamadi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa jengo jipya wa Hospitali ya Watoto Mnazi mmoja PSPF imekabidhi mashuka 75 kwa ajili ya wodi za watoto katika hospitali hiyo Kuu Zanzibar ikiwa ni moja ya kusaidia Jamii.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akipokea mashuka kutoka kwa Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Hazina Konde (katikati) na Afisa Mkuu wa Tawi la Zanzibar PSPF Bi. Faidha Thatau wakikabidhi mashuka hayo kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya Watoto katika hospitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika majengo mapya wa hospitali hiyo Zanzibar. 
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Faidha Thatau akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi mashuka kwa Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Mfuko wa PSPF hutowa huduma za mafao mbalimbali kwa Wanachama wake Bima ya Afya kwa wateja wao.  

Maafisa Wafawidhi wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya vitanda katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya kukabidhi mashuka hayo 75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto Zanzibar. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani

0
0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia  katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma
 Waziiri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sampuli mbalimbali za korosho katika wakati alipotembelea banda la Ushirika wa Ruangwa, Nachingwea Liwale Cooperative Union (RUNALI) Limited  katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma Julai 30, 2017. Kushoto  kwake ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Convenant, Sabetha Mwambenja
 Bendi ya Jeshi la Kujenga Taifa ikiongoza maandamano katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba (katikati) na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. Tate William Ole- Nasha baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma  kuhutubia katika kilele cha  Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani kwenye ukumbi wa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma

SHIRIKA LA POSTA LAIBUKA KIDEDE KWA WATOA HUDUMA BORA KUTOKA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI KWENYE MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli (katikati), akimkabidhi Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. Kulia anayesaidia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijange.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo leo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (katikati), akiwa ameishikilia Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo, mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo leo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (wa tatu kulia), Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Sabasaba, mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, jijini leo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (kushoto), akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (kulia), kwenye banda la shirika katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam leo.

MOBISOL YAZINDUA TV YA SOLA YENYE UWEZO WA KUENDESHA VIFAA VINGINE

0
0

Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni ya Mobisol, Leslie Katharina Otto, (kushoto)akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliotembelea kwenye banda la Mobisol kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Kaimu Balozi wa Ujereumani hapa nchini John Reyels (kushoto) akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Mobisol Afrika Mashariki, Henrik Axelsson Lilja , wakati wa uzinduzi wa kutoa huduma za Mobisol jijini Dar es Salaam, kwenye banda la Ujerumani lililopo kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam .
Ofisa Mkuu wa Kampuni ya Mobisol Afrika Mshariki, Henrik Axelsson Lilja, akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya TV ya Sola

Mwakilishi wa Mobisol kanda ya Dar es Salaam, Allan Rwechungura akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampuni Mobisol mkoani Dar e salaam na Sola Tv kwenye banda la maonyesho la kampuni hiyo lililopo uwanja wa SabaSaba ---Kampuni ya Mobisol kutoka nchini Ujerumani ambayo inafunga na kuuza vifaa bora vya nishati ya umeme imezindua bidhaa mpya ya kipekee kwenye soko la Tanzania, ambayo ni TV ya sola inayojitegemea kabisa.

Akiongea jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wake, kwenye banda la Ujerumani, katika viwanja vya sabasaba, Meneja Mkuu wa Mobisol Afrika Mashariki, Henrik Axelsson akiwa na mwakilishi wa Mobisol, kanda ya Dar es salaam, Allan Rwechungura, amesema TV hii mpya ya kioo bapa yenye ubora wa hali ya juu ya sola inajitegemea na inauwezo wa kuwasha taa na kuchaji simu hivyo ni ya kipekee na inajitegemea kwa upande wa nishati.

TV hii kisasa ya kioo bapa yenye ubora wa hali ya juu, ina betri inayofanya kazi hadi masaa 10, ina uwezo wa kuwasha taa, una waranti ya miaka 3 na huduma (service) baadaa ya mauzo.

Alisema katika msimu huu wa Sabasaba kampuni ya Mobisol imetoa punguzo maalumu kwa ajili ya kuwawezesha watanzania wengi kuunganishwa na umeme wa sola wa uhakika ikiwemo kujipatia vifaa imara na vya kisasa vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya Kijerumani kwa gharama nafuu na kuweza kulipia kwa awamu mpaka kufikia kipindi cha miaka mitatu.

”Ofa hii inawezesha wateja wetu watakaolipa fedha taslimu kuunganishwa na mtandao wa Mobisol kupata punguzo hadi asilimia 25% na watakaolipia kwa awamu gharama ya kuanzia ni shilingi 59,000/- ambapo makato ya kila mwezi itakuwa shilingi 33,500/- ambapo kwa miaka 3 itakuwa kiasi cha shilingi 1,266,000/-”. Alisema Rwechungura.

Hii ni fursa ya kuwapatia zawadi ya maendeleo familia yako na wale uwapendao kijijini! Aliongeza kuwa kampuni ya Mobisol ambayo sasa imeanza kutoa huduma zake hapa jijini Dar es Salaam, ina mitambo ya nguvu ya kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani ya wati 80, 120, na 200 mbayo inakuja pamoja na betri, taa, TV, redio, tochi na waya ya kuchaji simu. Hivyo kumwezesha mtu anayeishi eneo ambalo umeme haujafika kutokuwa na tofauti na mtu aishiye mjini.

Akibainisha zaidi uwezo wa kufanya kazi wa TV hii ya sola inayojitegemea ikitumika kwa TV, kuwasha taa 3 (za Wati 1) kwa muda wa masaa 6 na kuchaji simu 2 unaweza kufanya kazi kati ya masaa 6 hadi 9. Matumizi ya King’amuzi na kuwasha taa 3 kwa masaa 6 ya kuchaji simu 2 unaweza kufanya kazi kati ya masaa 5 na 7.

Rwechungura aliendelea kufafanua kuwa iwapo mteja atawasha TV kwa masaa 4 na kuchaji simu 2 ataweza kutumia taa kwa masaa 10 hadi 15.

“Mtambo huu wa Tv ya sola unaowezesha matumizi ya aina mbalimbali unapatikana kwa gharama ya shilingi 950,000 na vifaa vya umeme ambayo mteja ataweza kununua na kutumia kwenye mtambo huu ni seti ya taa ya umeme yenye 1W au 2W, kifurushi cha King’amuzi cha Zuku chenye chaneli za kulipia, Redio ndogo na seti ya kuchaji simu. Hii ni fursa nyingine ya pekee kwa wateja kujiunga na familia ya Mobisol na kufurahia maisha ya kisasa kwa kutumia vifaa vya teknolojia bora kutoka Ujerumani” Alisema.

Mobisol ni kampuni pekee katika kanda ya Afrika yenye mitambo ya kuzalisha umeme wa nishati ya jua wenye nguvu na inauza vifaa bora vya majumbani vya matumizi ya nishati ya umeme wa jua ambapo pia imekuwa inatekeleza mpango wa kusambaza nishati ya umeme wa jua kwa kulipia kwa awamu. Kufikia sasa inao mtandao wa wateja zaidi ya 62,000 nchini Tanzania na zaidi ya wateja 85,000 katika kanda ya nchi za Afrika Mashariki.

Mobisol sasa ipo katika mikoa 23 nchini Tanzania na inaendelea kusogeza huduma karibu na wahitaji.

AGPAHI YAENDESHA KAMPENI YA UPIMAJI MAAMBUKIZI YA VVU MSALALA NA MANISPAA YA SHINYANGA

0
0

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania limeendesha Kampeni ya Upimaji wa Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa watoto na vijana katika halmashauri ya Msalala na Manispaa ya Shinyanga katika mkoa wa Shinyanga. 

Zoezi la kupima watoto na vijana limefanyika Juni 30,2017 na Julai 1,2017 katika zanahati ya Buluma iliyopo katika kijiji cha Buuma kata ya Jana katika halmashauri ya Msalala na zanahati ya kijiji cha Galamba katika kata ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga.

Zaidi ya watoto na vijana 760 walipata fursa ya kupima afya zao.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la upimaji,Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon, alisema kampeni ya Upimaji VVU kwa vijana na watoto yenye kauli mbiu ya “Ijue Afya ya Mwanao” inalenga kuwafikia vijana na watoto wengi zaidi ili kujua afya zao.

“Hili ni zoezi endelevu,AGPAHI kwa kushirikiana na serikali tumekuwa tukipima afya za watoto na vijana na pale inapobainika wamepata maambukizi ya VVU huwa tunawaanzishia huduma ya tiba na matunzo”,alieleza Simon.

“Kupitia kampeni hii tunashirikiana na viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na tumekuwa tukiwahamasisha wazazi kuwaleta watoto na vijana ili wapimwe na zoezi hili limekuwa na manufaa makubwa kwani watoto wengi wameletwa na wazazi wao kupima afya zao”,aliongeza.

Naye Mratibu wa Masuala ya Watoto AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Jane Kashumba alisema wameamua kuanzisha kampeni hiyo ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma ya kupima VVU kwa hiari katika maeneo ya karibu yao ili waweze kujua afya zao.

“Tunaushukuru mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU Kwa hisani ya watu wa Uingereza (CIFF) kwa kuwezesha kampeni hii",alieleza Dk. Kashumba.

"Tumeanza zoezi hili katika halmashauri hizi mbili na tutaendelea na kampeni katika maeneo mengine kwani lengo la AGPAHI ni kuwafikia watoto na vijana zaidi”,aliongeza Dk. Kashumba.

Kwa Upande wake Mratibu wa Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii na Upimaji VVU wilaya ya Kahama, Peter Shimba alisema serikali itaendelea kushirikiana na shirika la AGPAHI katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

Shirika la AGPAHI linatekeleza shughuli zake katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Tanga,Geita na Mara kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU Kwa hisani ya watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP - Mozambique).
Ijumaa Juni 30,2017: Hapa ni katika Zahanati ya Buluma iliyopo katika kijiji cha Buluma kata ya Jana halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoa wa Shinyanga .

Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simon akiwaeleza wazazi na walezi walioleta watoto na vijana katika zahanati ya Buluma kuhusu lengo la Kampeni ya Upimaji wa Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa Watoto na Vijana.

Wazazi,vijana na watoto wakimsikiliza Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Charles Simonwakati akitolea ufafanuzi juu ya kampeni ya Upimaji VVU.

Mwenyekiti wa kijiji cha Buluma, Budila Teremka akisisitiza jambo kabla ya zoezi la kupima watoto na vijana halijaanza.

Mratibu wa Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii na Upimaji VVU wilaya ya Kahama, Peter Shimba akizungumza kabla ya zoezi la upimaji VVU halijaanza ambapo alilishukuru shirika la AGPAHI katika harakati zake za mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nalo katika mapambano hayo.

Mtoa huduma za afya akimtoa damu mtoto ili kumpima kama ana maambukizi ya VVU au la!

Kulia ni mzazi aliyeambatana na watoto wake katika zahanati ya Buluma kwa ajili ya kupima VVU.

Kushoto ni mama aliyekuwa ameambatana na watoto akishuhudia zoezi la upimaji VVU kwa watoto.

Zoezi la upimaji VVU likiendelea.

Mbali na kupima VVU, kulifanyika michezo ya watoto na vijana kama vile kukimbia na yai.Pichani kulia ni Charles Simon akitoa maelekezo kwa washiriki wa shindano la kukimbia na mayai.

Vijana wakikimbia na mayai yaliyowekwa kwenye vijiko.

Mchezo wa kukimbia na mayai ukiendelea.

Mratibu wa Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii na Upimaji VVU wilaya ya Kahama,Peter Shimba akiipongeza moja ya familia iliyojitokeza kupima VVU  na kubainika kuwa hawana maambukizi ya VVU. Katika zahanati ya Buluma  kati ya watoto na vijana 525 waliopimwa VVU,watano pekee walibainika kuwa na maambukizi ya VVU.

Jumamosi Julai 1,2017: Hapa ni katika Zahanati ya Kijiji cha Galamba iliyopo katika kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga ambapo pia Kampeni ya Upimaji wa Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa watoto na vijana imefanyika.

Mratibu wa Masuala ya Watoto AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Jane Kashumba akizungumza wakati wa zoezi la kupima VVU kwa vijana na watoto katika kijiji cha Galamba.

Dk. Kashumba akizungumza na wazazi,vijana na watoto katika zahanati ya Galamba.



Mtoa huduma za afya akimchukua damu mmoja wa vijana kutoka kijiji cha Galamba waliofika kupima VVU.

Vijana na watoto wakisubiri kupima VVU.
Afisa Mradi, Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Rehema Kivuyo akizungumza katika zahanati ya Galamba ambapo vijana na watoto 238 VVU na hakuna aliyepatikana kuwa na maambukizi ya VVU.

Michezo nayo ilikuwepo: Pichani ni Mratibu wa Masuala ya Watoto AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Jane Kashumba akiongoza vijana katika mchezo wa kukaa kwenye viti.

Mchezo wa kukimbia na mayai ukiendelea.

Rehema Kivuyo akiwapa zawadi ya mayai vijana walioshinda mchezo wa kukimbia na mayai.
Vijana na watoto wakicheza mchezo wa kukimbiza kuku.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

WAZIRI MWIJAGE AIPONGEZA PPF KWA KUWEKEZA KWENYE VIWANDA

0
0
 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kulia), akipeana mikono na Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele alipotembelea banda la Mfuko huo kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, leo Julai 1, 2017.
 Waziri Mwijage a,kizungumza na wafanyakazi wa PPF kwenye banda la Mfuko huo.
 Waziri Mwijage akipeana mikono na Afisa Uendeshaji Mwandamizi wa PPF, Bi. Pauline Msanga
 Waziri Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PPF baada ya kutembelea banda lao
 Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo alipotembela banda la Mfuko huo
 Wafanyakazi wa PPF wakiwahudumia wananchi waliotembela banda hilo
  Wafanyakazi wa PPF wakiwahudumia wananchi waliotembela banda hilo
Waziri Mwijage, akiagana na wafanyakazi wa PPF baada ya kutembelea banda hilo. Kulia ni Mkuu Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja.

DIASPORA GOSPEL TALENT

0
0

HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI WAKATI WA UFUNGUZI WA MAONESHO YA 41 YA SABASABA JULAY 1,2017

0
0

SUMA JKT WANYAKUA TUZO YA KILIMO NA UFUGAJI BORA WA MWAKA 2017

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT)  Brigedia Jenerali Charo Yateri amesema kuwa jitihada na juhudi zinazofanywa na vijana wake ndicho kitu kikubwa kilichopelekea kupata tuzo ya  masuala ya Kilimo na ufugaji.

Tuzo hiyo walikabidhiwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

Brigedia Jenerali Yateri alisema kuwa, mbali na kujihusisha na masuala ya ufugaji na kilimo amvapo wana dhana mbalimbali wanazozitumia ikiwemo Kilimo cha umwagiliaji pia wanajihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa ya kuwaweka.

Pmaoja na hilo,  SUMA JKT wamejikita zaidi katika utengenezaji wa samani za ndani kama makabati, vitanda, samani za maofisini na vitu mbalimbali pia wanatengeneza nguo mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT)  Brigedia Jenerali Charo Yateri akizungumza na Globu ya Jamii mara baada ya kupata tuzo katika masuala ya Kilimo na ufugaji waliyokabidhiwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli katika ufunguzin wa maadhimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Dhana mbalimbali za Kilimo zinazotumika kwa Kilimo cha Umwagiliaji vinavyotumika na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), dhana hizo ziliweza kuwekwa wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
 Baadhi ya wananchi wakiangalia Mabwawa ya Samaki yanayotumiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kwa ajili ya ufugaji ambapo kila tenki moja linachukua samaki 100 wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Wananchi wakiangalia mabanda ya kuku wanaofugwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
Samani zinazotengenezwa na Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) zikiwa katika banda lao wakati wa ufunguzi  maadhimimisho ya miaka 41 ya Sabasaba yaliyofanyika jana kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

Elisiana Laizer wa Mlandizi mkoani Pwani aibuka na Milioni 20 za Biko

0
0

MJASIRIAMALI mdogo wa Mlandizi, mkoani Pwani, Elisiana Laizer, leo ametangazwa kuwa mshindi wa droo ya 19 ya kuwania Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutikisa hapa nchini.

Droo ya kumpata mwanadada huyo ilichezeshwa jana jijini Dar es Salaam na balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehus Ngolo.

Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba ni furaha yake kuona droo tatu kati ya 19 zilizoendeshwa na Biko zimewapata wanawake watatu, jambo linaloonyesha kwamba mchezo wao umekuwa wa Watanzania wote.

“Ni jambo la kutia moyo kuona droo ya 19 imempata dada wa Mlandizi, Elisiana ambaye anajishughulisha na biashara ndogo ndogo maeneo ya Mlandizi, mkoani Pwani, nikiamini kuwa ni hatua nzuri kwake na Kwa Watanzania wote wanaocheza Biko,” Alisema.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Biko imezidi kukolea baada ya kutoka Dodoma, ikaenda Mbeya sasa imetua mkoani Pwani kwa mshindi wao Elisiana ambaye ameibuka kidedea kwa Sh Milioni 20, huku zawadi mbalimbali za Biko za hapo kwa hapo zikianzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.

“Tumetoka Mbeya juzi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wetu Linda Mhewa Sh Milioni 20 zake, huku leo tukimpata msichana mwingine anayeishi Mlandizi, mkoani Pwani aliyecheza Biko mchezo rahisi unaochezwa kwa ujumbe wa simu za mikononi wa Tigo Pesa, M-pesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, alisema Biko ni mchezo rahisi wa ujumbe mfupi wa maandishi unaotoa ushindi kwa Watanzania wote, hivyo Watanzania wachangamkie fursa.

“Biko ni mchezo unaofuata sheria, kanuni na taratibu zote, hivyo tunaomba Watanzania wacheze kwa wingi ili wavune mamilioni ya zawadi kutoka kwenye mchez huu,” Alisema.
Hadi sasa tayari zimeshafanyika droo 19 za kutoa ushindi mkubwa wa Sh Milioni 20, huku Biko wakitoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa Mwezi Mei pekee tangu mchezo huo wa kubahatisha ulipoasisiwa nchini Tanzania na kutoa fursa ya utajiri kwa Watanzania.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, kushoto akizungumza jambo na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja katika kuchezesha droo ya 19 ya Biko ambapo mjasiriamali Elisiana Laizer kutoka Mlandizi, mkoani Pwani alifanikiwa kuwa mshindi wa Sh Milioni 20.

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUTUMIA HUDUMA ZA HOTELI MTANDAONI

0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Kuna faida nyingi za kutumia mitandao inayotoa huduma za hoteli badala ya kuwasiliana nao au kutembelea tovuti zao moja kwa moja. Kwani unaweza kuperuzi aina tofauti za hoteli, kujua huduma walizonazo pamoja na bei kabla ya kufanya maamuzi ni hoteli gani umependezewa nayo.

Mbali na kuwepo kwa manufaa mengi kwa mteja pindi anafanya huduma za hoteli mtandaoni changamoto kubwa hujitokeza kwenye kufanya uchaguzi na maamuzi. Jumia Travel ingependa kukushirika mambo muhimu ya kuzingatia pindi unapoingia mtandaoni na kuchagua ni hoteli gani unayotaka kwenda.

Wapi unaweza kufanyia huduma hizo? Kwa wasafiri wengi wazoefu wanafahamu kuwa ni gharama kubwa kutumia huduma za hoteli kupitia kwenye tovuti zao. Badala yake hutumia mitandao inayotoa huduma hizo kwani huwa na bei nafuu tena na ofa kadha wa kadha. Kwa mfano, mmojawapo ya mitandao hiyo ni pamoja na Jumia Travel, ambao una aina mbalimbali za huduma za malazi kwa watu wa hadhi tofauti. Tofauti ya mitando hii na tovuti za hoteli ni kwamba zenyewe zinampatia mteja machaguo ya hoteli mbalimbali, mahali popote na kwa mujibu wa bajeti aliyonayo.
Fikiria kuhusu umbali, kufikika kwake na gharama za usafiri. Jambo linalofuatia baada ya kujua ni mtandao gani unaoweza kuutumia kupata huduma unayoitaka ni mahali unapotaka kwenda. Lakini pia ni vema kujiuliza je hapo unapotaka kwenda kunafikika kiurahisi na gharama za usafiri zikoje kukutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Usipokuwa makini unaweza kujikuta unakwenda kufikia sehemu ambayo itakupasa kutumia gharama kubwa za usafiri au ni ngumu kufika kwenda kwenye shughuli zako.

Chumba cha aina gani unachokipendelea? Hoteli au sehemu yoyote ile ya malazi inakuwa na machaguo tofauti kulingana na matakwa ya mteja. Kuna huduma ya chumba kimoja, chumba kimoja chenye vitanda viwili ndani, chumba chenye maliwato ndani yake na kadhalika. Hivyo lazima ujue ni chumba cha aina gani unakitaka ili hata iwe rahisi kumuelezea mtoa huduma hotelini, lakini hayo yote hutegemea bajeti yako kwani bei huwa tofauti.

Je unaweza kupata huduma siku hiyo hiyo? Dharura hutokea na huwa haiepukiki kwenye masuala ya kusafiri. Kwa mfano unaweza kupewa maagizo na bosi wako kusafiri kwenda mkoani siku hiyo hiyo na tayari tiketi ya usafiri umekwishakatiwa. Sio hoteli zote zinakubali au kupokea huduma kwa siku hiyo hiyo, hivyo yakupasa kutafiti ni hoteli gani zinafanya hivyo.
Pitia maoni ya wateja waliowahi kukaa hapo. Kuna umuhimu wa kutafiti wateja waliowahi kukaa sehemu unayotaka kwenda wanasemaje kuhusu huduma zao. Hii itakusaidia kujua kwamba itakufaa au la. Sidhani kama utashawishika kwenda kwenye hoteli ambayo wateja wameacha maoni mtandaoni kwamba wahudumu wa pale sio rafiki na wala hakuna ulinzi wa kutosha.

Wateja wanaopendelea sehemu hiyo ni watu wa aina gani? Hoteli huwa zinajengwa kwa malengo tofauti kulingana na aina fulani ya wateja. Zipo kwa ajili ya wafanyabiashara, familia, fungate kwa wanandoa, watalii na kadhalika. Kama wewe ni mfanyabiashara basi chagua hoteli itakayokufaa kwa dhumuni ulilonalo, usije kujikuta unakwenda kwenye hoteli ambayo wanafamilia na watoto huwa wanapenda kwenda kupumzika na ukakwazika.

Huduma nyinginezo - maegesho ya magari, kifungua kinywa, bwawa la kuogelea, sehemu ya kufanyia mazoezi. Kama msafiri na mara nyingi huwa sio wenyeji kwa mahali unapokwenda ni vema kujua ni huduma gani unaweza kuzipata kwenye hoteli unayotaka kwenda. Mfano wa huduma nyingi zinazotolewa na hoteli kwa sasa ni kama vile, kifungua kinywa, maegesho ya magari, mgahawa au chakula, kufuliwa na kupasiwa nguo na huduma ya usafiri. Kwa hiyo pindi unapoamua unakwenda kufikia wapi ulizia vitu hivyo ili kujua kama vinapatikana bure au kuna gharama utakazoziingia kama mteja.

Namna ya kufanya malipo. Sio hoteli zote zinaruhusu kufanya malipo taslimu pale unapofika hotelini na sio zote pia huruhusu mteja kutumia benki au mtandao. Kwa hiyo itakuwa ni jambo la msingi kujua sera ya malipo ya hoteli unayotaka kwenda. Kwani unaweza kukuta kuna hoteli nyingine inakupasa kulipia siku 2 kabla ya kwenda pale au hata wiki moja nyuma. Mara nyingi hii hufanyika ili kuzuia tabia ya wateja kusema wanakwenda halafu hubadili maamuzi, hoteli huwatoza kiasi kadhaa cha fedha wateja wenye tabia hizi ili kuepuka hasara.

Muda wa kuingia na kutoka. Kwa sababu umekwishalipia huduma kwenye hoteli fulani haimaanishi kwamba unaweza kwenda au kutoka muda wowote unaoutaka wewe. Kila hoteli inakuwa na utaratibu wake iliyojiwekee na ni muhimu kuzingatia kwani unaweza kujuikuta unakosa huduma uliyokwishailipia au kuingia matatizoni. Kwa mfano, sehemu nyingi za malazi hapa Tanzania muda wa wateja kuingia hotelini huwa ni saa 4 au 5 asubuhi na kutoka pia inakuwa ni hivyo hivyo siku inayofuatia.
Kwa dondoo hizo chache Jumia Travel inaamini kuwa utakuwa umepata mambo mapya ya kujifunza na wakati mwingine utakuwa makini kama ulikosea kipindi cha nyuma. Kufanya huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ni kitu ambacho kinatumika duniani kote kwa sasa kwani ni njia rahisi, uhakika na salama. Kikubwa ni kuweza kujifunza namna ya kufanya hivyo kwani kuna faida lukuki badala ya kutumia njia za kawaida tulizozioea kama vile kuwapigia simu ndugu, jamaa na marafiki zako wakusaidie kufanya hivyo huko uendako.

WAKONGWE 15 BONGO FLEVA WAPIGIWA ‘MIZINGA YA HESHIMA’ DAR LIVE

0
0
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, akiwasikilizisha nyimbo zake mashabiki waliofurika katika Ukumbi wa Dar Live usiku wa kuamikia leo katika shoo ya kuwapa heshima waanzilishi wa Muziki wa Bongo Flava nchini ambapo 'mizinga' mitano ya kuheshimu kazi yao hiyo ilipigwa. 
[/caption] Usiku wa kuamkia leo Jumapili ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar kulikuwa na shoo ya heshima kwa Bongo Flava waanzilishi wa muziki huo waliowahi kutamba enzi hizo walipigiwa mizinga mitano kabla kuanza mambo. Shoo hiyo iliyoandaliwa na kituo cha Redio na Runinga cha East Africa Television na Radio ya East Afrika kupitia kipindi chake cha Planet Bongo baada ya kupigwa mizinga hiyo umati uliofurika ukumbini hapo ulitulia dakika moja kuwakumbuka waanzilishi wa muziki huo waliotangulia mbele za haki. Baadhi ya wasanii waliotajwa majina yao wakiwa mbele za haki ni pamoja na Albert Mangwair, Mr Ebbo, Dogo Mfaume, Langa Kileo, Complex na Vivian ambao wote nyimbo zao zilizowahi kutikisa zilipigwa. ...Akiendelea kuwapagawisha mashabiki.[/caption] Tukio la kuwakumbuka waasisi hao lilipopita wasanii na makundi mbalimbali yaliyowahi kutikisa enzi hizo yalianza kuvamia jukwaa moja baada ya jingine na kupiga nyimbo zao zilizowahi kutamba. Mashabiki wa burudani walionekana kukunwa sana na burudani hiyo ambapo baadhi walisikika wakisema hiyo ndiyo ilikuwa Bongo Flava ya ukweli. Katika burudani hiyo alianza kuvamia jukwaa Z Anto, University Corner, LWP, Daz Nundaz Family chini ya Daz Baba, Wagosi wa Kaya, Solid Ground Family, Dully Sykes, Mandojo na Domokaya, Tid, Jaymoe, Dudu Baya, Manduli Boy, Mabaga Fresh, Afande Sele, Ispector Haruni ambapo mkali wa Temeke, Juma Nature ndiye aliyefunga kazi. Mashabiki wakimshangilia Dully Sykes.
[/caption] Katika burudani hiyo kila msanii aliyepanda jukwaani alitaka kujidhihirisha kama bado yuko vizuri kwenye gemu maana makamuziki hayakuwa ya chini, ambapo Kundi la Mabaga Fresh lilionekana kuupagawisha ukumbi huo hasa waliposhusha kibao chao kilichowawahi kutamba cha Tunataabika. Kibao hicho kiliufanya ukumbi huo ulipuke kwa mayowe ya kushangilia huku DJ Snox naye akiwachagiza kwa swaga za kiulemavu huku akiinadi tafsiri ya Mabaga Fresh kuwa Ulemavu fresh tu. [caption id="attachment_151493" align="aligncenter" width="800"] Msanii mkongwe Khalid Mohammed aka TID Mnyama akifanya makamuzi. [/caption] [caption id="attachment_151493" align="aligncenter" width="800"] ...TID akiendelea kufanya makamuzi.[/caption] [caption id="attachment_151497" align="aligncenter" width="534"] Msanii mkongwe mwengine, Dudu Baya, akiongea na mashabiki wakati wa shoo hiyo.[/caption] [caption id="attachment_151498" align="aligncenter" width="800"] ...Akipiga shoo. Kundi la Mabaga Freshi wakikumbushia enzi zao. ...Makamuzi yakiendelea. Msanii mkonge, Afande Sele, akiwapagawisha mashabiki wa Bongo Fleva. Inspekta Haroun akikumbushia enzi zake kwa mashabiki. Juma Nature (kushoto) na Dollo wakifanya makamuzi. Inspekta (kushoto) akiimba na Juma Nature Jay Moe akiwapa burudani mashabiki. Wagosi wa Kaya wakiwapa burudani mashabiki kwa nyimbo za tangu enzi zao mpaka sasa.
(Picha/Habari na Richard Bukos/GPL)

SHAKA AZINDUA SEMINA ELEKEZI YA UJASILIA MALI KWA VIJANA WA WILAYA YA UBUNGO

0
0
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kuliapamoja na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Kinondon ndg:Said Masanga wakionja bidhaa ya dagaa zinazookwa na wajasilia mali wadogowadogo wilaya ya Ubungo

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akionyeshwa shati la batiki moja ya bidhaa zinazotengenezwa wajasilia mali wadogowadogo wilaya ya Ubungo

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Ubungo Leah Mbeke akizungumza

Baadhi ya Vijana walioudhuria Mafunzo ya Ujasilia Mali UVCCM Ubungo
yalio fungulia na Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka katika
Ukumbi wa Texaz Manzese

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza katika Semina ya mafunzo yaUjasilia mali ya Vijana yaliofunguliwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka


Baadhi ya Vijana walioudhuria Mafunzo ya Ujasilia Mali UVCCM Ubungowakishangilia

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa Tatu kulia akicheza Burudani ya Muziki pamoja na Vikundi vya Sanaa Vilivyo tumbuiza.

Kijana akipiga pushap

”Viongozi wa UVCCM Wilaya zote nchini fuatilieni Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015-2020,Hakikisheni asilimia 5 inayotolewa na kila Halmashauri nchini zinawafikia Vijana”Aliyasema Ndg:Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakati akifungua Semina ya Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wa Wilaya Ya Ubungo Katika Ukumbu wa Texaz Manzese

TAMASHA LA MAJIMAJI SEREBUKA KUTIMU VUMBI JULAI 22 HADI 30

0
0
Msimu wa tatu wa tamasha la MAJIMAJI SEREBUKA linaloandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali Songea Mississipi, linatarajia kuanza julai 22 mwaka huu,Huku mishezo mbalimbali itahusishwa ikiwemo riadha,ngoma za asili,maonyesho ya kiabiahara na mdahalo,na nini hasa lengo la tamasha hilo huyu hapa mwenyekiti wa tamasha DAMASI NDUMBARO anabainisha. HABARI KAMILI HII HAPA VIDEO YAKE

MATUKIO KATIKA PICHA NAMNA KITUO CHA KISASA CHA MABASI KILIVYOFUNGULIWA SINGIDA.

0
0
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamad Amour akifungua rasmi kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja.
Muonekano wa sehemu ya kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida kikiwa katika hali ya usafi uliosifiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamad Amour wakati akifungua rasmi kituo hcho. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamad Amour akiwa na viongozi wa Manispaa ya Singida wakisubiria kupanda basi ambalo lilifungua rasmi huduma ya usafiri wa mabasi katika kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamad Amour akiwa na Mkimbiza Mwenge kitaifa Fredrick Ndahani wakiwa ndani ya basi lililowaingiza ndani ya kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida kama sehemu ya uzinduzi wa kituo hicho. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamad Amour akishuka kutoka ndani ya basi lililowaingiza ndani ya kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida kama sehemu ya uzinduzi wa kituo hicho. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja.
Mabasi na wananchi wa Singida wakianza kutumia rasmi kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida kilichozinduliwa na mwenge wa uhuru 2017. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja. Kituo hicho kimesifiwa kutokana na kuwa katika hali ya usafi huku mikoa mingine ikitakiwa kuiga mfano huo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamad Amour akiwa na viongozi wa Manispaa ya Singida wakikagua kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja.
Muonekano wa Moja ya Sehemu ya kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida kilichozinduliwa na mwenge wa uhuru 2017. Ujenzi wa kituo hicho ulianza Januari 2016, umegharimu shilingi bilioni 3.7 na kituo hicho kinaweza kuhudumia mabasi makubwa zaidi ya 70 kwa wakati mmoja.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Amour Hamad Amour akikabidhi mizinga mitano ikiwa ni sehemu ya mizinga 40 kwa timu ya Mpira wa Miguu ya Stendi Misuna mara baada ya kuzindua kituo kikuu na cha kisasa cha mabasi Singida. Timu hiyo inayoundwa na wakata tiketi imekuwa ni chachu ya kuhakikisha kituo hicho kinakua na ulinzi na usalama wa hali wa juu pamoja na kupinga vitendo vya kuvunja sheria kama utumiaji wa madawa ya kulevya.

WANAWAKE WAPONGEZA MWENGE WA UHURU KUWAEPUSHA KUCHANGIA MAJI NA MIFUGO.

0
0
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akimtwisha ndoo ya maji moja ya akina mama waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Merya Wilayani Singida.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akifungua maji katika bomba wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Merya Wilayani Singida, pembeni yake Mkimbiza Mwenge Kitaifa Fredrick Ndahani.


Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akitazama vitunguu katika shamba la mboga mboga la umwagiliaji kwa njia ya matone wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Msange Wilayani Singida.
Sehemu ya shamba la mbogamboga lenye kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone ambapo vitunguu vinaonekana vimestawi vizuri, shamba hilo lina ukubwa wa ekari 25.

…………………….

Wanawake wa Vijiji vya Merya na Ikugha katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida wameushukuru Mwenge wa Uhuru kwa kuwafungulia mradi ambao umewaepusha kutembea umbali mrefu kutafuta maji ya kutumia ambayo si safi wala salama huku wakiyachangia na mifugo yao.

Wanawake hao wametoa pongezi hizo mara baada ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour kufungua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 49 utakaohudumia vijiji hivyo ambao umegharimiwa na shirika la saving International, halmashauri ya Singida pamoja na michango ya wananchi.

Wamesema kabla ya kupatikana mradi huo wanawake wa vijiji hivyo wamekuwa wakifuata maji umbali mrefu sana kiasi cha kushindwa kutekeleza shughuli nyingine za kuzalisha mali.

“Tulikua tunatembea mpaka tunachoka, tunaamua kupumzika njiani kwanza ndio tuendelee na safari ya kuleta maji nyumbani, yani tunashukuru sana kwakweli”, ameongea Bi Greta Senge Mkazi wa kijiji cha Ikugha.

Aidha wameongeza kuwa mradi huo utawapatia maji safi na salama kwakuwa maji waliyokuwa wakiyafuata umbali mrefu hapo awali yalikuwa machafu na si salama.

“Yani tulikuwa tunachota maji ambayo unakuta ng’ombe anakunywa hapohapo, wakati mwingine anajisaidia na inabidi uchote hivyo hivyo, kwakweli tunaushukuru sana mwenge kutufungulia mradi huu, tulikua tunaumwa matumbo kila mara”, ameongeza Rehema Lazaro.

Wameongeza kuwa mradi huo utapunguza magonjwa ya tumbo na macho ambayo yamekuwa yakiwasumbua mara kwa mara hukua wakiridhia kulipia kiasi cha shilingi 50 kwa lita 20 za maji ili kupata fedha za kutunza mradi huo.

Kwa upande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour ameitaka jumuiya ya watumia maji ya mradi huo kuutunza mradi huo ili utoe maji kwa wingi na muda huo kutokanana kuonekana ni hitaji la muhimu.

“Nimefika hapa na kushuhudia akina mama wengi mnamiminika na ndoo ili mpate maji, hii ni ishara kuwa mradi huu ni muhimu hivyo basi jumuiya ya watumia maji hakikisheni mda wote maji yanatoka na sio kupanga masaa ya kutoa maji au mvua ikinyesha tu mnayafunga, hapana” amesisitiza Amour.

Amesema mradi huo usimamiwe vizuri kusiwe na upendeleo au ubaguzi wowote kwakuwa maendeleo hayo hayana ubaguzi wa rangi, dini, itikadi za kichama au makabila.

Amour amesema jumuiya hiyo ihakikishe miundombinu ya mradi huo inatunzwa ili kuepusha kuwarudisha akina mama hao katika shida waliyokuwa wakiipata awali huku akiwashauri kuangalia namna ya kuipatia mifugo maji pamoja na kuweka taratibu nzuri za mapato na matumizi ya mradi huo.

Wakati huo huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amezindua mradi wa umwagiliaji mbogamboga kwa njia matone wa ekari 25 wenye thamani ya shilingi milioni 326 katika kijiji cha Msange.

Akisoma taarifa ya mradi huo Afisa Kilimo wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Adam Mngale amesema mradi huo ulianzishwa mwaka 2012 na hadi sasa una wanachama 32 ambao wananufaika kwa kujiongezea kipato kutokana na kulima misimu miwili yani kiangazi na masika.

Mngale amesema malengo ya mradi huo ni kuongeza eneo la uzalishaji hadi kufikia ekari 1400, kupanua miundombinu ili waweze kutumia kutumia bwawa la suke na lililoko eneo jirani katika umwagiliaji na kutumia kiwanda cha kusindika mbogamboga kilichoko Msange kusindika mazao yao.

SPIKA NDUGAI AONGOZA WABUNGE KATIKA MECHI KATI YA TIMU YA BUNGE NA TIMU YA FC GRACE UNITED STATES KUTOKA NCHINI MAREKANI ILIYOFANYIKA LEO KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA.

0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akisalimiana na Mchezaji wa timu ya Bunge Mheshimiwa William Ngeleja (kushoto) wakati akikagua vikosi vya timu ya Bunge pamoja na timu ya FC GRACE UNITED STATES kutoka nchini Marekani kabla ya kuanza kwa mechi yao iliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akionyesha zawadi ya jezi ya timu ya Taifa ya Marekani aliyopewa na Mchezaji wa timu ya FC GRACE UNITED STATES Ndg. Robert Allen (kushoto) kabla ya kuanza kwa mechi kati ya timu ya Bunge pamoja na timu ya FC GRACE UNITED STATES kutoka nchini Marekani iliyofanyika leo uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akikabidhiwa jezi na Mchezaji wa timu ya FC GRACE UNITED STATES Ndg. Robert Allen (kushoto) kabla ya kuanza kwa mechi kati ya timu ya Bunge pamoja na timu ya FC GRACE UNITED STATES kutoka nchini Marekani iliyofanyika leo uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia)akifurahia jambo na Mchungaji Vicent Valentyn kutoka Afrika kusini (watatu kulia) wakati wakifuatilia mechi kati ya timu ya Bunge pamoja na timu ya FC GRACE UNITED STATES kutoka nchini Marekani iliyofanyika leo uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.


 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akikabidhiwa Mipira kutoka kwa Ndg. Robert Allen (kulia) kwa ajili ya timu ya Bunge, kabla ya kuanza kwa mechi kati ya timu ya Bunge na timu ya FC GRACE UNITED STATES kutoka nchini Marekani  iliyofanyika leo uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA UBORESHAJI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam katika eneo la Bandari hiyo.

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Baadhi ya mabalozi kutoka nchi mbalimbali wakifatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya kutoa hotuba yake kabla ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird alipokuwa akisoma hotuba yake.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird wakati wakitazama kipeperushi ya maelezo ya Mradi wa uboreshaji wa Bandari jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akicheza muziki pamoja na Banana Zorro, Mrisho Mpoto, pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma mara baada ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi wengine waliosimama wakati Banana Zorro pamoja na Mrisho Mpoto walipokuwa wakiimbawimbo wa Aamka Tufanye kazi kabla ya tukio la uwekaji wa jiwe la msingi Uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YASHIRIKI KIKAMILIFU MAONESHO YA SABASABA

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Samwel Kamanga akiweka saini katika kitabu chwa wageni alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Saba saba) yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Wizara ya Fedha na Mipango Josephine Majura.


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi akisaini kitabu cha wageni katika banda la GEPF wakati alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Saba saba) yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko Shirika la Bima la Taifa Bw. Elisante Maleko wakati alipotembelea Taasisi hiyo iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango katika banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Saba saba) yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dorothy Mwanyika (kushoto) akipokea kitabu kutoka Taasisi ya Uhasibu Arusha (T) (IAA) alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (Saba saba) yanayoendelea katika viwanja vya JK Nyerere barabara ya Kilwa, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio (katikati) akizungumza na Jumanne Nyamgunda Afisa Mwandamizi wa Bima wakati alipotembelea Shirika la Bima la Taifa katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba saba) jijini Dar es Salaam ambapo aliwapongeza kwa huduma nzuri, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja na kulia ni Mwanaidi Shemweta Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIC.

MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ADDIS ABABA USIKU HUU KUMUWAKILISHA RAIS KATIKA MKUTANO WA 29 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI YA UMOJA WA AFRIKA (AU).

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili usiku huu Jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo hapo kesho tarehe 03 Julai 2017 atahudhuria Mkutano wa 29 wa Wakuu wa  Nchi na Serikali  wa Umoja wa Afrika (AU).

Katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Ethiopia Pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Naimi Aziz na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga.

Katika Mkutano huo wa siku mbili kuanzia tarehe 03-hadi 04 Julai-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo.

 Kabla ya ufunguzi rasmi, Mkutano huo ulitanguliwa na vikao vya Baraza la Utendaji linalowashirikisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na Kamati ya Uwakilishi wa Kudumu  inayowahusisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje kutoka nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi  na Serikali  utafunguliwa rasmi kesho tarehe 03-Julai-2017 katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa, Ethiopia na  utajikita katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo.

Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na taarifa  kuhusu Maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maboresho ya kitaasisi katika AU na  hali ya Ulinzi na Usalama katika bara la Afrika.

Kuhusu  hali ya  ulinzi na usalama katika Bara la Afrika majadiliano ya Viongozi hao yatajikita zaidi kwenye nchi za Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Libya.  Aidha, majadiliano hayo pia yatagusa  hali ya usalama kwenye baadhi ya nchi ambazo ziliathiriwa na kundi la Boko Haram za  Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Mkutano huo 29 wa AU, unatarajiwa kuhuduhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Mkutano huo 29 wa AU utakaofanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia utaongozwa na Mheshimiwa  Alpha Conde  Rais wa Jamhuri ya Guinea ambaye ndiye Mwenyekiti wa AU.

Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni Kuimarisha Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia Uwekezaji katika Vijana (Harnessing Demographic Divident Through Investments in the Youth)

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 ADDIS ABABA- ETHIOPIA.      

03-Julai-2017
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili usiku huu Jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo hapo kesho tarehe 03 Julai 2017 atahudhuria Mkutano wa 29 wa Wakuu wa  Nchi na Serikali  wa Umoja wa Afrika (AU).Mhe.Samia amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Ethiopia Pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Naimi Aziz na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga mara baada ya kuwasili jijini Addis Ababa,nchini Ethiopia usiku huu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassa akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuwasili jijini Addis Ababa mapema usiku huu
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images