Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1288 | 1289 | (Page 1290) | 1291 | 1292 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 06/30/17--07:20: TANGAZO KWA UMMA

 • Menejimenti ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF inapenda kuwafahamisha Wanachama na Umma kwa ujumla kuwa Ofisi ya Kanda ya Dar es Salaam iliyopo Mtaa wa Mkwepu, Jengo la Diplomatic House, katikati ya jiji la Dar es Salaam itahamia rasmi kwenye jengo la LAPF Millenium Towers, ghorofa ya tatu, lililopo barabara ya Ali Hassan mwinyi eneo la Makumbusho kuanzia tarehe 01/07/2017. Hivyo wanachama na wadau wote wa Mfuko wataendelea kupata huduma kulingana na matarajio yao katika mazingira yaliyoboreshwa zaidi. Karibuni sana tuwahudumie.

  “Ishi na Staafu kwa Ufahari na LAPF”

  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. wa pili kulia ni Mwenyeji na kiongozi wa Msafara Bishop Oscar John.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikat) akimsikiliza Mheshimiwa William Ngeleja akizungumza wakati Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Bishop Oscar John (aliesimama) akizungumza, pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (katikati) na Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo (kushoto) uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya kimataifa ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg. Ibrahim Rashid, anaefuata ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa pili kulia ni Ndg. Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya, waliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (kushoto waliokaa) baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Ndg. Mwadini Jecha (katikati) pale ugeni kutoka Chama hicho ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne kilimo.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufalme wa Norway, Mhe. Borge Brende wakiweka saini Mkataba wa Makubaliano kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway.Ttukio hilo lilifanyika jijini Dar Es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne Marie Kaarstad, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Mary Matari, pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (hawapo pichani). 
  Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana mikataba mara baada ya kuweka saini 
  Dkt. Mahiga akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza zoezi la uwekaji saini na Mgeni wake. 
  Mhe. Brende naye akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa Habari. 
  Balozi wa Tanzania nchini Norway mwenye makazi yake nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu (wa pili kutoka kulia), Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Hanne Marie Kaarstad (wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, Bi. Mary Matari (wa kwanza kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga wakifuatilia kwa makini mkutano wa waandishi wa habari na Mawaziri wa Mambo ya Nje. 
  Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Waziri wa Norway nao wakifuatilia mkutano wa waandishi wa habari na Mawaziri wa Mambo ya Nje. 
  sehemu ya waandishi wa habari wakiwasikiliza kwa makini Mawaziri walipokuwa wakiendelea kuzungumza (hawapo pichani). 

   

  Tanznaia na Norway kushirikiana katika masuala ya siasa na diplomasia

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ameeleza kuwa kusainiwa kwa Mkataba wa Makubaliano (MoU) kuhusu kushirikiana katika Mashauriano ya Kisiasa na Kidiplomasia kati ya Tanzania na Norway kumefungua sura mpya ya mahusiano kati ya nchi hizo mbili. 

  Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar Es Salaam wakati anaongea na waandishi wa habari baada ya shughuli ya uwekaji saini wa makubaliano hayo aliyoifanya kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende kukamilika.

  Alisema kusainiwa kwa MoU hiyo kutazifanya nchi hizo kuwa na mahusiano ya karibu zaidi katika kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kisiasa na kidiplomasia ambayo kimsingi yalikuwepo tokea zamani lakini leo yamerasimishwa. 

  Mhe. Mahiga amewambia wanahabari kuwa Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana kiuchumi, kiteknolojia na kijamii kwa takribani miaka 55 sasa. Baadhi ya maeneo aliyoyataja ambayo nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika kipindi hicho ni pamoja na uzalishaji wa nishati ya umeme hususan vijijini, afya, elimu, kilimo na utunzaji wa misitu. 

  Mhe. Mahiga aliendelea kueleza kuwa katika kikao chao, wamejadili maeneo mapya ya ushirikiano yakiwemo utunzaji wa mazingira na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa sekta binafsi za nchi hizo mbili kinyume na awali mahusiano zaidi yalikuwa baina ya Serikali mbili.

  Waziri Mahiga ameishukuru Norway kwa jitihada zake ziliozasaidia uvumbuzi na uchimbaji wa gesi asilia nchini kupitia kampuni ya Statoil ambayo imewekeza nchini mtaji mkubwa kuliko mahali popote Afrika.

  Alihitimisha hotuba yake kwa kusema kuwa Tanzania itaendelea kufaidika kwa kiasi kikubwa na ushirikiano wake na Norway kwa kuwa nchi hiyo ina utajiri mkubwa katika sekta ya mafuta misitu na teknolojia ya hali ya juu katika sekta mbalimbali.

  Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway alieleza kuwa Norway imekuwa ikishirikiana na Tanznaia katika sekta za maendeleo tokea mwaka 1964 na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania hadi hapo nchi hiyo itakapokuwa na uwezo wa kugharamia miradi yake yenywe. 

  Waziri Borge kabla ya kuondoka nchini leo join, atashiriki uzinduzi wa programu ya kushirikiana katika masuala ya kodi na uzinduzi wa awamu ya pili ya programu ya kuendeleza mafuta(oil for development program) utakaofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. 


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Dar es Salaam, 30 Juni 2017


  0 0


  Prof. Ninatubu Lema, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, (aliyenyoosha mikono) akimweleza jambo Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kulia), leo wakati akianza ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA_TBIII).
  Meneja wa Mradi wa Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII), Bw. Ray Blumrick (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye ujenzi wa jengo hilo, ambapo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof Makame Mbarawa (wa tatu kutoka kushoto) akimsikiliza kwa makini.
  Mhandisi Simba Charles (aliyenyoosha mkono) akionesha eneo la maegesho ya magari kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), leo alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
  Bw. Ray Blumrick, Meneja Mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBIII) akimwelekeza namna paa lilivyo imara, Prof. Makame Mbarawa (Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano) aliyetazama juu katikati wakati wa ziara yake kwenye jengo hilo leo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Prof Ninatubu Lema akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (wa pili kutoka kushoto) leo alipofanya ziara ya kutembelea jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa TAA, Bw. Richard Malulu.

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akifuatilia mjadala katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Pamoja iliyokuwa ikijadili miswada miwili ya sheria kuhusiana na usimamizi wa maliasili za Nchi.kikao hicho kilifanyika Mjini Dodoma jana Katika Ukumbi wa Msekwa.

  0 0
  Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo William Mpinga akiongea na waandishi wa habari wakati wa mwendelezo wa uzinduzi 'Jaza Ujazwe Ujaziwe zaidi' Pichani kushoto ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha Tanzania, Bakari Majjid na kulia Mchekeshaji Lucas Mhavile JOTI.

  Meneja wa Mawasiliano Tigo, Woinde Shisael akielezea jambo wakati wa uzinduzi wa J'aza Ujazwe Ujaziwe zaidi' jijini Dar Es Salaam leo
  Waandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa mkutano huo mapema leo.  Kampuni inayoongoza maisha ya kidigitali, Tigo Tanzania, leo Tarehe 30Juni 2017, imezindua promosheni mpya na ya kusisimua inayoitwa ‘JazaUjazwe Ujaziwe zaidi’ambapo wateja watakuwa wanazawadiwa vifurushi vya muda wamaongezi, data na ujumbe mfupi kila mwezi kwa mwaka moja mzima wanapokuwa wanaongeza salio,iwe ni kwa njia ya vocha za kawaida, e-pin au Tigopesa.

  Washindi wa zawadi watapatikana kwa droo ambazo zitachezeshwa kila siku na kila wiki ambapo wateja wote wa Tigo watakuwa na nafasi ya kujishindia GB 30 za data, dakika 3,000 za muda wa maongezi wa kupiga mitandao yote, meseji 3,000 au kujishindia Samsung S8 kwa muda wa mwaka mzima.

  Kwa mujibu waTigo, promosheni hii inakuja sokoni kama sehemu ya kampeni inayoendelea ya ‘JazaUjazwe’ ambayo ni shukurani za Tigo kwa wateja wake kwa uaminifu wao usio badilika kwa kampuni hiyo.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,Kaimu Meneja wa Huduma za Masoko wa Tigo William Mpinga amesema, “Tigoinathamini mchango mkubwa usio badilika ambao wateja wetu wamekuwa wakitupatia kwa miaka mingi. Hii ndio sababu inayotufanya tuamini kuwa wana haki ya kushukuriwa kwa uaminifu wao. Kama kampuni tunafuraha kwa mara nyingine kuwazawaidia wateja wetu kwa kuwawezesha kuendelea kufurahia dunia yetu -Huduma zetu zaki pekee”

  Mpinga alibainisha kwamba promosheni mpya itaimarisha Tigo kuwa ndio kampuni inayotoa bidhaa na huduma zenye bei nafuu, wakati huohuo itakuwa inaimarisha jukumu lake kama kampuni ya mawasiliano yenye ubunifu zaidi Tanzania.

  “Promosheni hii imekuja kufuatia uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wetu uliofanyika hivi karibuni ambao unahakikisha utendaji wa hali ya juu wa utoaji wa huduma. Kwetu sisiTigo, kila wakati tunakuwa wabunifu katika kutengeneza mbinu mpya za kusisimua ambazo zinazo imarisha uhusiano wetu na wateja wetu. Promosheni hii ya uaminifu ni njia bora ya kuwazawadia na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma na bidhaa zetu.” AlisemaMpinga.

  Alithibitisha tena kwamba Tigo imekusudia kuendelea kuwazawadia wateja wake kwa bidhaa na huduma za kusisimua zaidi na akaongeza kwamba“Ubunifu wa huduma na bidhaa zetu unatokanana utafitiwa kina unaolenga kuwaridhisha wateja wetu. Kwa hiyo JazaUjazwe, Ujaziwe zaidi inakuja kukabiliana na mahitaji ya wateja ya kuwa na hisia ya msisimko kila mara wanapotumia huduma zetu. Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia dakika, SMS au data za ziada wanazo zawadiwa kila mara wanapoongeza salio na hivyo itaboresha mwenendo wa mawasiliano yao” alielezea Mpinga

  0 0


  Bi. Joyce Msigwa ambaye ni Mratibu wa Faru Arts and Sports Development Organization (FASDO) akitoa maelezo kwa washiriki wa  'Bongo Style Competition'  2017, kuhusiana na asasi ya FASDO
  Mwezeshaji Bw. Erick Chrispin akitoa semina kwa washiriki wa Bongo Style namna ya kujiongoza wenyewe katika maswala ya Fedha,Muda na uongozi.
  Baadhi ya washiriki wa shindano la Bongo Style 2017, wakiwemo wapiga picha,waandishi wa miswada ya Filamu na wabunifu wa mitindo upande wa mavazi wakiwa wanafanya zoezi waliopewa na mwezeshaji Bw. Erick Chrispin (ambaye hayupo pichani)
  Baadhi ya Washiriki wa Bongo Style Competition 2017 wakiwa wanafanya kazi waliyopewa na mwezeshaji Bw. Erick Chrispin (hayupo pichani) baada ya kumaliza semina yake.
   Mkufunzi na Mtaalam wa maswala ya Picha Bw. Iddy John akitoa somo juu ya maswala ya picha kwa washiriki wa Shindano la Bongo Style kundi la  Picha
  Mbunifu maarufu wa Mitindo ya mavazi Martin Kadinda akitoa somo kwa washiriki  kundi la mitindo
  Washiriki wa kundi la  Ubunifu wa mitindo upande wa  mavazi wakipewa vitendea kazi.
  Bi. Christina Pande(aliyesimama) ambaye ni Mtunzi na muongozaji wa Filamu, akiwapa darasa vijana ambao wapo katika kundi la Uandishi wa  miswada ya Filamu shindano la Bongo Style 2017.
  Picha zote na Fredy Njeje.


  0 0

  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Nzasa.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akibeba zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Nzasa.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akichanganya zege kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Nzasa.


  Wananchi wa Nzasa wakishiriki katika ujenzi wa miundombinu ya shule ya msingi ya Nzasa wakiwa na Mbunge wao Anthony Mavunde
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wazee wa kijiji cha Nzasa.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki ujenzi wa moja ya majengo ya shule ya msingi Nzasa akiwa na wananchi wake.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akishiriki ujenzi wa moja ya majengo ya shule ya msingi Nzasa akiwa na wananchi wake.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Nzasa
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akisalimiana na wakazi wa kijiji cha Nzasa
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nzasa katika ujenzi wa majengo ya shule ya msingi.
  Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa viongozi wa kijiji hicho.
  ………………………..

  MBUNGE wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde leo ameshirikiana na wananchi wa Kijiji cha Nzasa,Kata ya Chihanga katika ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa na matundu ya vyoo.

  Ujenzi huo unahusisha nyumba tatu za walimu, ,madarasa matatu na matundu ya vyoo 7.

  Katika ujenzi huo, unatarajiwa kugharimu Sh.205,500,000 ambazo zinazotokana na mradi wa ‘Pay 4 Results’(P4R) uliopo chini ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia.

  Akizungumza na wananchi hao, Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, aliwapongeza kwa kujitolea kuhakikisha mradi unafanikiwa.

  Alibainisha kuwa changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo ni kukosekana kwa nyumba za walimu na hivyo kuwafanya walimu kuishi umbali wa kilomita zaidi ya 25.

  Mbali na hilo alisema kulikuwa na upungufu wa madarasa pamoja na uchakavu wa vyoo.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende wakielezana jambo kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Mafuta, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (wa tatu kushoto) akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja akitoa dondoo na kuwakaribisha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Waziri wa Mambo ya nje wa Norway Mhe. Borge Brende muda mfupi kabla ya kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende akielezea kuhusu kuendelea kwa ushirikiano wenye tija na Tanzania wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya program ya maendeleo ya Sekta za Mafuta jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo wakinukuu maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (hayupo pichani) wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya program ya maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akizungumza jambo wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Borge Brende (katikati) na Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne Marie Kaarstad wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) wakati akielezea umuhimu wa Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya maafisa waandamizi wa Serikali na waandishi wa habari wakiwa katika uzinduzi rasmi wa Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es Salaam.
  Maafisa waandamizi wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia ushirikiano wenye lengo la kuboresha uchumi unaofanywa na nchi ya Norway wakati wa kuzindua rasmi Mpango wa miaka mitatu wa Maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uzinduzi wa awamu ya pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta za Mafuta, Jijini Dar es salaam.(Picha: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)  Benny Mwaipaja, WFM, DAR ES SALAAM

  SERIKALI ya Norway imeipatia Tanzania msaada wa Dola Milioni 10.5 za Marekani kupitia programu ya miaka mitatu ya maboresho ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, inayotarajiwa kuanza Mwaka Mpya wa Fedha- Julai Mosi mwaka huu.

  Mpango huo pamoja na uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Program ya Maendeleo ya Sekta ya Mafuta, umezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo kwa niaba ya Serikali zao.

  Dkt. Mpango ameishukuru Serikali ya Norway kwa msaada huo mkubwa utakaochangia kuboresha utendajikazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuijengea uwezo zaidi wa kitaalamu, miundombinu na vitendeakazi vingine vitakavyo changia kuongeza uwezo wa Mamlaka hiyo wa kukusanya mapato ya Serikali.

  Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt. Juliana Pallangyo amesema kuwa hatua ya Serikali ya Norway kuendelea kufadhili programu ya pili ya Mpango wa kuendeleza Sekta ya Mafuta utaiwezesha Serikali kubobea katika masuala ya utaalamu wa masuala ya sheria na usimamizi wa sekta hiyo.

  Nae Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende amesifu utendaji kazi mahili wa Mhe. Rais Dokta John Pombe Magufuli wa kupambana na ufisadi na vitendo vya rushwa pamoja na kuimarisha ukusanyaji kodi, hatua ambayo itaifanya nchi ipige hatua za maendeleo haraka.

  Amesema kuwa hajawahi kuona nchi yoyote duniani ikiendelea bila kuweka nidhamu na uwajibikaji serikali pamoja na kutokusanya mapato yake ipasavyo na kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya tano kufanikisha mipango yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.

  0 0

  NA BASHIR NKOROMO, DAR.

  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Amina Makilagi leo ametangaza rami tarehe ya Wanachama wa Jumuia hiyo kuanza kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi tangu ngazi ya Kata hadi Taifa, na kusema fomu zinatolewa bure, huku akionya kuwa atakayejaribu kutumia rushwa kuomba nafasi yoyote atakatwa.

  Pia ametumia ameaema UWT inaunga mkono tamko la Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Magufuli alilolitoa hvi kribuni kwamba, ni marufuku kwa msichana atakayepata ujauzito akiwa shuleni katika mfumo rasmi kurudi masomoni katika mfumo huo rasmi.

  Makilangi amesema, UWT inaunga mkono tamko hilo kwa sababu ndiyo maelekezo yaliyomo katika Ilaniya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020, na pia ndiyo Sera ya Serikali katika kusimamia utoaji elimu katika mfumo rasmi hapa nchini.

  "Tafiti mbalimbali za Jumuia na Taasisi nyingine hapa nchini na za Kimataifa likiwemo Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataida (UNICEF), Mwanafunzi mjamzito au aliyejifungua ni vigumu kuendelea na masomo katika mfumo ambao umeandaliwa kulingana na Saikolojia ya akili ya mtoto asiye na majukumu ya malezi na ndiyo maana upomfumo uliopendekezwa na sera na ilani ya CCM kwamba anayekatiza masomo katika mfumo rasmi anaweza kuendelea katika mfumo usio rasmi, Mifumo isyo rasmi kwa ajili ya wanafunzi wa aina hiyo na wengine waliokosa masomo katika mfumo wa kawaida ni  kama MEMKWA na QT" , alisema Makilagi.

  Alisema UWT inatambua na kuheshimu mapendekezo  ya tafiti hizo kuhusu watoto na pia inakubaliana na sera ya Serikali na Ilani ya CCM kuweka utaratibu bora na wenye manufaa  zaidi wa kuwazuia wajawazito na wazazi  kuendelea na masomo katika mfumo rasmi na badala yake kutengeneza mfumo mbadala wa kupata elimu kwa kuwa kufanya hivyo kumaimarisha nidhamu, na uwezo wa kitaaluma wa watoto.

  "Pia UWT inawapongeza Wabunge kwa kupitisha sheria kali kwa wale watakaobainika kusababisha upatikanaji wamimba  kwa wanafunzi, kutetea na kufanikisha ndo za utotoni.  Sheria ya maraekebisho ya sheria mbalimbali namba 2 ya mwaka 2016 ilyofanyiwa marekebisho ya sheria ya elimu ya Sura 353 inaweka wazi dhamira ya Serikali ya kumlinda mtoto wa kike na kutoa onyo kali kwa wale wenye tabia za kuwarubuni na kuwasababishaia mimba zisizotarajiwa  na za utotoni",

  "pamoja nakuunga mkono kauli ya Mheshimiwa Rais, pia UWT inawashauri na kuwaomba Wazazi , Walezi na Jamii kwa ujumla, kuwalinda watoto wa kike na kutoa elimu ya kutosha kuhusu masuala ya jinsia, athari za mimba za utotoni na athari za maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi", alisema Makilagi.

  UWT imetoa mwito kwa wasichana waliopo shuleni kujizatiti kwenye masomo na kujiepusha na vishawishi kwa kuwa dira ya Tanzania ni kuwa na Taifa lenye uwiano na fursa sawa baina ya wanaume na wanawake hivyo mwito ni kwamba wasichana wajitahidi zaidi ili kulifikia lengo la kuwa washiriki katika ujenzi wa Taifa.

  UFUATAYO NI TAARIFA KAMILI KUHUSU UCHAGUZI WA KATIKA UWT

  TAARIFA KWA WANACHAMA WA UWT/CCM KUPITIA VYOMBO VYA HABARI – TAREHE 30/06/2017

  Mwaka 2017 ni mwaka wa Uchaguzi wa Viongozi ndani Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake ambazo ni Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), UVCCM na WAZAZI kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa.

  UCHAGUZI WA MATAWI
  Kwa upande wa UWT Uchaguzi wa Viongozi ngazi ya Matawi, Matawi yaliyofanya Uchaguzi ni 19,927 sawa na 87% na Matawi ambayo bado kufanya Uchaguzi ni 3,118 sawa na 13%.

  UCHAGUZI NGAZI YA KATA/WADI
  Tarehe 04/06/2017 hadi tarehe 11/06/2017 tulitoa na kupokea fomu za wanachama walioomba kuteuliwa kuwa Viongozi wa UWT ngazi ya Kata/Wadi. Hatua inayoendelea hivi sasa ni mchakato wa vikao kwa mujibu wa Katiba ya UWT. Uchaguzi wa Kata/Wadi utafanyika kati ya tarehe 25/07/2017 hadi tarehe 28/07/2017.

  UCHAGUZI NGAZI YA JIMBO
  Tarehe 29/06/2017 hadi tarehe 04/07/2017 kutoa na kupokea fomu na Uchaguzi wa Viongozi wa UWT ngazi ya Jimbo unatarajiwa kufanyika kati ya tarehe 25 – 26/08/2017.


  UCHAGUZI WA VIONGOZI WA WILAYA, MKOA NA TAIFA
  Tarehe 02/07/2017 hadi 10/07/2017 tutaanza kutoa na kupokea fomu za wanachama wanaoomba kuteuliwa kugombea Uongozi wa Wilaya, Mkoa na Taifa.


  Utaratibu wa Fomu
  Fomu za kugombea Uongozi wa UWT wa Wilaya, Mkoa na Taifa zinapatikana katika Ofisi za UWT Wilaya zote na Mikoa.

  Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti
  Fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti UWT, zitatolewa katika Vituo vitatu.

  1.       Ofisi ya UWT Makao Makuu Dodoma;
  2.       Ofisi Ndogo ya UWT Dar es Salaam;
  3.       Afisi Kuu ya UWT Zanzibar;

  Nafasi zingine za Kitaifa

  1.     Nafasi tano (5) za Halmashauri Kuu ya Taifa, nafasi tatu (3) Bara na nafasi mbili (2) Zanzibar.

  2.     Nafasi kumi (10) za Baraza Kuu la UWT, nafasi tano (5) Bara nafasi tano (5) Zanzibar.

  3.     Nafasi ya Uwakilishi wa UWT kwenda Jumuiya ya Vijana nafasi moja (1) na nafasi moja ya Mjumbe mmoja kuiwakilisha UWT Wazazi.

  4.     Fomu za kugombea nafasi hizo zitapatikana katika Ofisi ya UWT Wilaya na Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.

  5.     MIKUTANO MIKUU YA WILAYA, MIKOA NA TAIFA

  (1)       Mikutano Mikuu ya UWT ngazi ya Wilaya itafanyika tarehe kati ya tarehe 21 – 22/09/2017.

  (2)        Mikutano Mikuu ya UWT ngazi ya Mikoa itafanyika tarehe kati ya tarehe 25 – 26/10/2017.

  (3)       Mkutano Mkuu wa UWT ngazi ya Taifa utafanyika tarehe 01 – 03/11/2017.


  GHARAMA ZA FOMU
  Fomu zote za kugombea Uongozi wa Tawi hadi Taifa zitatolewa bila malipo yoyote.

  WITO KWA WANACHAMA
  Nitumie nafasi hii kupitia Vyombo vya Habari kuhamasisha wanachama wote wa UWT/CCM wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali ndani ya UWT kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa ifikapo tarehe 02 – 10/07/2017.


  ANGALIZO KWA WATENDAJI/VIONGOZI NA WANACHAMA
  Mipango ya kutafuta fedha kwa ajili ya gharama za Mikutano ya Wilaya, Mikoa na Taifa iendelee bila kuhusisha uchukuaji wa fomu na kugombea Uongozi ndani ya UWT.

  KUZINGATIA KANUNI YA UCHAGUZI
  Aidha, ninasisitiza umuhimu wa kuzingatia Katiba na Kanuni ya Uchaguzi wa UWT na Kanuni ya Uchaguzi ya Maadili ya Viongozi wa CCM, lengo ni kuhakikisha Uchaguzi kwa ngazi zote unakuwa Huru na Haki kwa wanachama wote wa UWT/CCM.


  RUSHWA
  Uchaguzi wa 2017 tunahitaji kupata Viongozi wasiotoa Rushwa  kwa wanachama na wajumbe wasiopokea wala kutoa Rushwa. Lengo ni kupata Viongozi waadilifu na wachapa kazi na wenye moyo wa kufanya kazi za UWT bila kutanguliza maslahi yao binafsi.

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

   Imetolewa na:
  Ndugu Amina Nassor Makillagi (MNEC, MB)
  KATIBU MKUU WA UWT
    30/06/2017

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu –TAWA Bw. Martin Loibooki akisoma risala mbele ya mgeni Rasmi
  katibu mkuu akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa jinsia ya kike 10 kati ya 97 waliyohitimu, wa tatu kutoka kushoto waliyokaa ni kaimu mkurugenzi mkuu-tawa
  wahitimu wakitoa heshima mbele ya mgeni rasmi  KM akisoma kiapo cha wahitimu

  …………………….

  Na Mwandishi wetu, Katavi

  Wizara ya Maliasili na utalii imewataka wadau wa uhifadhi kote nchini kuunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji kwenye pori la akiba la Selous ambao ukikamilika unatarajiwa kuzalisha zaidi ya megawati 2,100.

  Katibu Mkuu wizara ya Maliasili na utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi amesema utekelezaji wa mradi huo wa umeme ni wa muhimu kwa taifa kwani utasaidia kuharakisha maendeleo ya taifa kuelekea azima yake ya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati.

  Akiongea wakati akifunga mafunzo ya askari wa wanyamapaori kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania -TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Katibu mkuu Meja Jenerali Gudance Milanzi amesema mradi huo wa umeme pamoja na mradi wa bwawa la maji la Kidunda utachukua eneo dogo tu la pori la akiba la Selou lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba elfu 50.

  Amesema pori hilo ndilo kubwa miongoni mwa mapori ya aina hiyo ulimwenguni na ukubwa wake ni zaidi ya nchi za Rwanda na Burundi zikiunganishwa kwa pamoja.

  Katibu Mkuu amesema ujenzi wa miradi hiyo hauna tafsiri kwamba Tanzania haithamini masuala ya uhifadhi bali unazingatia uhifadhi wenye manufaa kwa jamii na maendeleo ya taifa na hasa dhamira ya serikali ya rais Dk John Pombe Magufuli kuelekea Tanzania ya viwanda ambayo inahitaji nishati ya umeme itakayoyotosheleza mahitaji ya taifa.

  Amesema Tanzania inatambua umuhimu wa uhifadhi ndiyo maana imetenga eneo la zaidi ya asilimia 28 ya eneo lote la nchi kavu Tanzania bara kwaajili ya uhifadhi wa aina mbalimbali ukiwemo wa wanayamapori na misitu ya vyanzo vya maji ambayo ni muhimu kwa shughuli za kijamii na kiuchumi, “ ni nchi chache sana duniani zenye eneo kubwa la uhifadhi kama Tanzania” alisisitiza katibu mkuu.

  Katibu mkuu amewataka wafanyakazi wa wizara na watanzania kwa ujumla kutokuwa kikwazo kwa utekelezaji wa mradi huo na kwamba wadau wanaotaka kuisaidia Tanzania wasaidie kuhakikisha inatumia maliasili zake kupiga hatua ya kimaendeleo ikiwemo misaada ya teknolojia za kisasa na rafiki wa mazingira kusaidia kufikia malengo yake kimaendeleo.

  “Mtakumbuka mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli hivi karibuni alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Pwani amezungumzia kwa kirefu sana umuhimu wa miradi hiyo ukiwemo wa bwawa la Kidunda na wa umeme wa Stieglars Gorge, sasa sisi kama wahifadhi na kama watumishi lazima tumuunge mkono na tusiwe kikwazo katika dhamira hii njema” alisema Jenerali Milanzi’’.

  Ametoa mfano wa nchi ya Qatar ambayo amesema ilikuwa na eneo la uhifadhi lililokuwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia kutokana na uwepo wa baadhi ya viumbe adimu lakini walipogundua mafuta, waliamua kujitoa kwenye urithi wa dunia ili wachimbe mafuta na kuinufaisha nchi hiyo na maendeleo ya wananchi wake.

  Akizungumzia kuhusu tatizo la mifugo kwenye maeneo yaliyohifadhiwa, Katibu mkuu amewataka wahifadhi kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hiyo na kusimamia sheria zilizotungwa na Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania ambazo zinakataza mifugo kuingia hifadhini kinyume cha sheria.

  Amesema ndiyo maana serikali inatumia fedha nyingi kugharamia mafunzo ya askari wa wanyamapori na wahifadhi ili kuwaongezea ujuzi na weledi wa kulinda maliasili za taifa kwa kuzingatia sheria zilizopo.

  Katibu Mkuu Meja Jenerali Gaudance Milanzi amezungumzia pia umuhimu wa kuhakikisha mapori ya uhifadhi yanatumiwa kwa uhifadhi badala ya kutumika kwa mambo mengine ikiwemo kilimo cha bangi na maficho ya majambazi na majangili na amewataka wahifadhi na askari kushirikiana na vyombo vingene vya ulinzi na usalama kuwafichua wahalifu wanaojificha kwenye mapori hayo na kufanya ujangili na uhalifu mwingine.

  Mapema katika taarifa yake kwa katibu mkuu, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania -TAWA Martin Loibooki alieleza kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuimarisha uhifadhi kwenye mapori mbalimbali ya akiba nchini na maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori.

  Aliwashukuru wadau mbalimbali wa uhifadhi wa ndani na nje ya nchi wanaofadhili mafunzo hayo na vitendea kazi juhudi ambazo amesema zimeanza kuzaa matunda ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya tembo na wanyamapori wengine kwenye mapori mengi nchini.

  Mfunzo hayo yaliyowashirikisha askari wa wanyamapori wapatao 98 kutoka Mamlaka ya wanayamapori Tanzania TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ni mwendelezo wa mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Maliasili na utalii kwa askari wa wanyamapori na watumishi wengine wa wizara hiyo katika hatua za kuelekea mfumo wa jeshi usu.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Anna Mghwira, (kulia), akipokea kadi ya uanachama wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, kupitia mpango wa hiari, (PSS), kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakati wa semina ya wastaafu watarajiwa mkoani Kilimanjaro Juni 30, 2017.
  Bw. Mayingu akitoa hotuba yake
  Mhe. Anna Ngwira, Mkuu wa Mkaow a Kilimanjaro, akionyesha kadi yake ya uanachama wa PSPF kupitia mpango wa PSS
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira,akiagana na wanachama wasitaafu watarajiwa,wa mfuko wa pesheni wa PSPF,mara baada ya kufungua semina hiyo Mkoa wa Kilimanjaro Juni 30, 2017
  Baadhi ya wastaafu watarajiwa wakiwa kwenye semina ya mafunzo iliyoandaliwa na PSPF mkoani Kilimanjaro.
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSPF 
  Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo.
  Baadhi ya wastaafu watarajiwa wakiwa kwenye semina ya mafunzo iliyoandaliwa na PSPF mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda wa kwanza kulia akiwa amembeba mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto Uwemba Mission.Kulia kwake ni Afisa Maendeleo na Afisa Ustawi wa Jamii Hosea yusto
  Mtoto Imelda Msola kutoka kituo cha watoto Compassion akitoa mkono wa asante kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda mara baada ya kukabidhiwa misaada mbalimbali katika kituo hicho
  Misaada iliyokabidhiwa katika kituo cha watoto Uwemba Mission.  HYASINTA KISSIMA-NJOMBE 

  Halmashauri ya Mji Njombe imetoa misaada yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki moja na arobaini kwa vituo viwili vya watoto yatima Compassion na Uwemba Mission ikiwa ni sehemu ya mapato ya ndani ya Halmashauri yaliyokusanywa katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2016/2017. 

  Akizungumza wakati akikabidhi misaada hiyo katika kituo cha watoto Yatima Compassion, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminatha Mwenda amesema kuwa Halmashauri yake imejiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa katika kila robo ya mwaka wa fedha inatenga fedha kwa ajili ya kusaidia jamii ya wenye uhitaji wakiwemo watoto yatima ili kuonesha upendo lakini pia kuijengea jamii tabia ya kuonesha upendo na kusaidia wale wote wenye mahitaji mbalimbali. 

  “Kila tunapokusanya mapato imekua ni utaratibu wa Halmashauri kwa kushirikiana na idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa jamii kuangalia makundi yenye uhitaji na kuona ni kwa namna gani tunayaongezea nguvu zaidi ili nao waweze kujikwamua kimaisha na kuona kuwa wao pia ni sehemu ya jamii inayotambulika na kuheshimika. 
   
  Tumekua tukifanya hivi mara kwa mara na leo tunapofunga mwaka na kuanza mwaka mpya wa fedha tumeona kwa kile kidogo tulichokipata tuweze pia kugawana na watoto hawa na furaha yangu imeongezeka kwani mpaka sasa Halmashauri yangu tumefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia mia na kuvuka lengo .”Alisema Mwenda. 

  Kwa upande wake Afisa Ustawi Halmashauri ya Mji Njombe Hosea Yusto amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya wazazi kuwatelekeza na kutowajali watoto wao matukio ambayo yamekuwa yakiongeza idadi ya watoto yatima katika vituo, watoto wa mitaani na amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanalea, kuwalinda na kuwa karibu na watoto wao ili kuepusha matukio mbalimbali yakiwemo ya ubakaji kwa watoto wadogo. 

  Akizungumza kwa niaba ya watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima Compassion Imelda Msola amesema wanaishukuru Halmashauri kwa kuendelea kuwapatia misaada ya mara kwa mara, na misaada waliyopata hususani vifaa vya shule vitawasaidia katika kipindi hiki wanapoenda kuanza muhula mpya wa masomo na wameomba wadau mbalimbali kuendelea kuwasaidia ili waweze kufanikisha malengo yao kimaisha. 

  Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Sukari, Mafuta, chumvi, Unga, Sabuni za kufulia, Mafuta ya Kujipaka nguo za watoto, Nepi, nguo za watoto, maziwa ya Kopo, dawa za meno, miswaki, daftari, kalamu.

  0 0


  Na Christina Mwangosi, MOHA

  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dk. Juma Malewa amesema Jeshi la Magereza nchini litatoa elimu ya namna kila Mtanzania hata aishie kwenye nyumba za ghorofa ama maeneo yenye nafasi ndogo ya kuanzisha kilimo cha mbogamboga, anavyoweza kutumia eneo dogo kuendeshea shughuli za kilimo cha mbogamboga wakati huu Maonyesho ya SabaSaba yanayoendelea katika Viwanja vya SabaSaba jijini Dar es salaam.

  Kamishna Jenerali Dk. Malewa amesema kuwa pamoja na kuandaa Shamba Darasa kwa ajili ya kutoa elimu ya shughuli mbalimbali za kilimo, Jeshi la Magereza limeandaa bidhaa mbalimbali ambazo zitaonyeshwa wakati wote wa Maonyesho pamoja na kuuzwa wakati wote wa Maonyesho hayo.

  Dk. Malewa amesema miongoni mwa bidhaa hizo ambazo ziko kwenye Banda la Magereza ni samani mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi na nyumbani ikiwemo makabati ya vyombo na nguo, meza na viti, madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari, vitanda, sofa, ‘dressing table’ pamoja na viatu vya ngozi vya kike na kiume.

  Amesema Jeshi la Magereza pia litauza pia majiko sanifu yanayotumia kuni kidogo, mashuka, foronya, vikoi pamoja na sabuni zenye ubora kwa ajili ya kufua nguo ambazo zinatengenezwa katika Kiwanda cha Sabuni kilichopo Mkoa wa Mbeya.

  Amesema Jeshi la Magereza katika kipindi hiki cha Maonyesho litatoa elimu ya shughuli za kilimo cha kisasa bure na kwa wale wananchi ambao maeneo yao yanafikika Wataalamu wa Magereza wanaweza kuwatembelea wananchi kwenye maeneo yao na kuwafundisha namna ya kuanzisha kilimo hicho kinachojulikana kama ‘kilimo cha jikoni’.

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyabiashara mbalimbali waliokuwa katika Ukumbi wa Mikutano wakati wa Ufunguzi wa Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017.
   Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabishi tuzo Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala ambao wameibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017.Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi tuzo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba baada ya Kampuni yake kuibuka washindi sekta ya mawasilioano, katika Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa TPDC.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi tuzo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi kwa niaba ya moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Property International Bw. A. Haleem  ambao waliibuka washindi wa tatu wa jumla katika Maonyesho ya Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa, yaliyoanza Juni 28 - Julai 8, 2017 ambapo kwa mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017, yaliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es salaam.
   Wakuu wa Wilaya za Dar es salaam, Sophia Mjema (kulia - Ilala), Felix Lyaviva (katikati - Temeke) pamoja na Hashim Mgandilwa (kushoto - Kigamboni) wakiwa kwenye ufunguzi huo.
  Wakuu wa vikosi vya Ulinzi na Usalama.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala.
  0 0

   Rais John Magufuli akimkabidhi Tuzo ya ushindi wa kipengele cha mawasiliano ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa sabasaba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari, jijini Dar Es Salaam jana. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. (Na Mpiga Picha Wetu).

  0 0

  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pension wa LAPF Bwana James Mlowe akipokea tuzo kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya LAPF kuwa mshindi wa Kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba katika kategori ya mifuko ya Hifadhi ya jamii, Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage Mapema leo Jijini Dar es salaam. 
  Meneja masoko na mawasiliano wa Mfuko wa Pension wa LAPF Bwana James Mlowe Akipokea tuzo kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli baada ya LAPF kuwa mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba Mapema leo Jijini Dar es salaam. 
  Tuzo ya Mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 41 ya sabasaba katika viwanja vya Mwl JK Nyerere barabara ya Kilwa DSM. Tuzo hii ilikabidhiwa kwa Mfuko wa Pensheni wa LAPF na Raisi Dr. John Pombe Magufuli Mapema leo Jijini Dar es salaam.
  Rehema Mkamba afisa mwandamizi masoko na mawalisiliano Bi Rehema mkamba akoionyesha tuzo baada ya LAPF Kuibuka mshindi wa kwanza katika kategori ua mifuko ya hifadhi ya jamii na bima kwenye maonyesho ya 41 ya sabasaba 2017 Mapema leo Jijini Dar es salaam. 
  Wafanyakazi wa LAPF nje ya banda lao wakifurahia tuzo yao ya kuwa mshindi wa kwanza kategori ya mifuko ya Pensheni na Bima katika maonyesho ya 41 ya sabasaba waliyokabidhiwa na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk John Pombe . Magufuli mapema leo. 

  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM-Dar es Salaam
  BENKI ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kusaidia mpango wa Serikali wa miaka 11 wa Elimu bila malipo kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari nchini.
  Kiasi hicho cha fedha ni nyongeza ya Dola milioni 122 zilizotolewa na Benki hiyo katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa maboresho ya elimu kupitia Mpango wa Tekeleza kwa Matokeo Makubwa sasa-BRN, uliolenga kuondoa changamoto za elimu nchini.
  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird amesema wakati wa utiaji saini mkataba wa nyongeza ya fedha hizo kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kuwa nyongeza ya Dola milioni 80 imetokana na Benki hiyo kuridhishwa na namna Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dokt. John Pombe Magufuli, ilivyosimamia kikamilifu mpango huo wa utoaji elimu bure na kuwanufaisha wanafunzi wengi wakiwemo wanaotoka katika familia masikini.
  Amesema kuwa uamuzi huo umesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi, kuongezeka kwa ufaulu, wanafunzi kujua maarifa ya hesabu, kusoma na kuandika, utoaji wa ruzuku  ya elimu kwa wakati, hatua ambayo pia imesababisha kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa miundombinu ya shule, changamoto ambazo anaamini zinapungua kupitia mkopo huo wenye masharti nafuu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James ameishukuru Benki ya Dunia kwa kutoa fedha hizo ambazo amesema zitasaidia kwa kiasi kikubwa mipango ya Serikali ya kuboresha elimu nchini na kuondoa changamoto zinazoukabili mpango huo likiwemo ongezeko hilo kubwa la wanafunzi.
  Bw. James ameeleza kuwa fedha hizo zitasaidia ujenzi wa miundombinu ya madarasa, ubora wa eimu, ukaguzi wa shule, upelekaji wa walimu, na kuwasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki hiyo ya msingi ya elimu.
  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila, amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa elimu wa lipa kulingana na matokeo upitia mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 122 zimetumika kujenga madarasa 1,400, matundu 3,390 ya vyoo, mabweni 261, majengo ya utawala 9, mabwalo ya chakula 9 nyumba za walimu 11, uchimaji wa visima vya maji katika shule nne na kukarabati vyuo vya ualimu.
  Amesema kuwa  mkopo mpya wa dola za Marekani milioni 80 uliotolewa na Benki ya Dunia hata kabla ya awamu ya kwanza ya mradi huo kumalizika hapo mwakani, umeonesha nia ya dhati ya Benki ya Dunia kusaidia maendeleo ya elimu nchini.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakitia saini makubaliano ya Benki ya Dunia kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (Kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bella Bird, wakibadilishana hati (mkataba) ya mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw, Doto James akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kutia saini makubaliano na Benki ya Dunia ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Somalia, Malawi na Burundi, Bi. Bella Bird, akisisitiza jambo mbele ya  waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya Benki yake ya kuipatia Tanzania mkopo wenye riba nafuu wa Dola za Marekani milioni 80 kwa ajili ya kutekeleza maboresho ya elimu ya msingi na sekondari kupitia mpango wa  lipa kwa matokeo (elimu bila malipo), Jijini Dar es Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0

  Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto ameteuliwa kuwa balozi wa hifadhi ya wanyama ya Ngorongoro kwaajili ya kuwahamasisha watanzania kutembelea kivutio hicho na kujionea ufahari wake.
  Mshairi huyo ameteuliwa na Wizara ya Utalii baada ya kuonyesha jitihada mbalimbali anazozifanya katika hatua ya kuitangaza nchi ya Tanzania katika nyanja mbalimbali.
  Akiongea na mwandishi wetu Jumamosi hii akiwa katika viwanja vya Sabasaba ndani ya banda la Ngorongoro, Kaimu Mhifadhi wa Mamlaka ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Samson Mtunga amesema wameona Mrisho Mpoto ni mtu sahihi ambaye ataweza kuitangaza nchini katika mambo ya kitalii.
  “Tumemteua Mrisho Mpoto kuwa balozi wetu wa utalii, tumeona ni mtu ambaye anaweza kufanya kazi hiyo vizuri kwa sababu tayari kuna baadhi ya juhudi zake binafsi tumekuwa tukiziona katika shughuli zake mbalimbali. Kwahiyo kama mnavyojua wizara ina bidhaa nyingi Mpoto anaanza na Ngorongoro lakini baadaye anaweza kuongezewa majukumu kwa sababu tuna vitu vingi sana tunahitaji vitangazwe,” alisema Samson Mtunga.
  Kwa upande wa Mpoto amesema ataitumia nafasi hiyo kuwahamasicha Watanzania juu ya ufahari wa hifadhi hiyo pamoja na kuvitangaza vitu pekee vinavyopatikana.
  “Kazi iliyopo mbele yangu kwa sasa ni kuhakikisha Watanzania wanatembelea vivutio vyetu, tukiizungumzia Ngorongoro ni hifadhi ambayo ndani yake pia kuna binadamu wanaishi, kuna wanyama wengi. Kwahiyo huu ndio wakati ya kuthamini vya nyumbani na kuvitumia ipasavyo. Kwa mfano umechukua likizo ya mwezi mmoja tembelea kule ukiwa na familia yako ukaone mambo mazuri ambayo huwenda hayapatikani duniani kote,” alisema Mpoto.Mpoto amewataka Watanzania ambao wanatembelea maonyesho ya Sabasaba wasiache kutembelea banda hilo ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu hifadhi ya Ngorongoro.
  “Kwa sasa hivi nipo kwenye banda la Ngorongoro kwahiyo ukifika hapa tunaweza kuongea mengi kuhusu hifadhi hii ili na wewe ukirudi nyumbani ukawaeleze wengine kwamba Ngorongoro sio sehemu ya mchezo mchezo,”
  Alisema Watanzania wakitembelea hifadhi hiyo kwa wingi kwanza watafurahia upekee wa hifadhi hiyo pia wataweza kuchangia kuongeza pato la taifa hela ambazo zinaenda kutatua kero mbalimbali za watanzania iliwemo maji, barabara na huduma ya afya.

older | 1 | .... | 1288 | 1289 | (Page 1290) | 1291 | 1292 | .... | 1898 | newer