Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

Barua kutoka kwa Watanzania waliofungwa Hong Kong kuhusiana na madawa ya kulevya,yawataja wahusika


PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA RAIS KIKWETE WILAYANI KARAGWE.

$
0
0
 Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo.
 Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Jumamosi Julai 27, 2013
 Rais Kikwete akihutubia umati Ngara
 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo.
 Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013
 Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara.
Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.

AISHA SURURU FOUNDATION YATOA MSAADA WA MAGODORO KWA WANAFUNZI WA MASJIDI IDRISA KARIAKOO

$
0
0
Wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari jijini Dar es salaam ambao wameweka kambi ya kujisomea katika Msikiti wa Idrisa Kariakoo Dar es salaam wakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Aisha Sururu Foundation Aisha Sululu kulia baada ya kuwakabizi magodoro na Mashika kwa ajili ya kulalia wawapo katika masomo yao ya ziadi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Aisha Sururu Foundation, Aisha Sururu kulia akimkabizi mmoja wa vijana wanaojisomea katika kambi ya msikiti wa Idrisa, Muhsin Juma magodoro aliyotoa kwa ajili ya vijana hawo kulalia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Aisha Sururu Foundation, Aisha Sururu kulia akimkabizi mmoja wa vijana wanaojisomea katika kambi ya msikiti wa Idrisa, Muhsin Juma magodoro aliyotoa kwa ajili ya vijana hawo kulalia .
Mkurugenzi Mtendaji wa Aisha Sururu Foundation, Aisha Sururu kulia akimkabizi mmoja wa vijana wanaojisomea katika kambi ya msikiti wa Idrisa, Muhsin Juma mashuka pamoja na magodoro aliyotoa kwa ajili ya vijana hawo kulalia  Picha na Blog ya SUPER D

BONDIA MTANZANIA OMARI KIMWERI 'LION BOY' AMTWANGA MTHAILAND KWA KO YA RAUNDI YA KWANZA

$
0
0

Omari Kimweri
BONDIA Mtanzania Omari Kimweri  'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini   Australia amendelea kutamba katika nchi hiyo baada ya jana kumtwanga kwa  KO ya raundi ya kwanza bondia Ekkalak Saenchan wa Thailand   ikiwa ni mchezo wake wa 16 tangia angie katika ngumi za kulipwa akiwa nchini humo .
 
Bondia huyo ambaye anaitangaza vema nchi ya Tanzania Kimataifa ameaidi kuwa ataenderea kutoa vipigo kwa mabondia  mbalimbali  pindi wakutanapo ulingoni .
 
Bondia huyo aliezaliwa Tanzania katika jiji la Dar es salaam mwaka 1982 amekuwa gumzo nchini humo kwa kuonesha mchezo mzuri unaowavutia raia wengi wa Australia na kuweza kuwa bondia namba moja katika nchi hiyo uku katika Dunia akishikilia nafasi ya 52 katika mabondia 450 duniani wenye uzito wa light flyweight
Anasema lengo lake kubwa ni kuukamata ubingwa unaotambulika kimataifa Duniani wa WBA World light flyweight title unaoshikiliwa na bingwa namba moja Duniani ,RomanGonzalez na IBF light flyweight title  unaoshikiliwa na John RielCasimero wa  Philippines ambao wananiumiza kichwa kwa sasa kwani ngumi ulimwengu mzima ni zile zile ila tunazidiana maarifa

Bondia huyo anaefanya shughuli zake za masumbwi nchini Australia ana mpango wa kuja kuwekeza nchini Tanzania mchezo wa masumbwi ili ukuwe hapa ambapo atafanya kila jitiadi ili mchezo wa masumbwi uweze kusonga mbele nchini habari hizi kwa ushirikiano mkubwa wa mtandao wa www.superdboxingcoach.blogspot.com

ZAIDI YA WANAWAKE 7500 WANUFAIKA NA"MWEI"MKOANI MOROGORO

$
0
0
 Baadhi ya wanawake  wajasiriamali wadogowadogo wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini wakipatiwa elimu na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania hawapo pichani,kabla ya kupatiwa mikopo yao ya pesa isiyokuwa na riba ya zaidi ya shilingi Milioni 327 iliyotolewa  na Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI".mikopo hiyo inawawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini kujiendeleza katika biashara zao,na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.
 Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane Bi.Rosena Rashid -Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akisaini kitabu cha orodha ya wakina mama wajasiriamali wadogowadogo waliokuwa wakipatiwa mikopo ya pesa isiyokuwa  na riba ya zaidi ya shilingi Milioni 327 toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI"unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini, na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi.Rukia Mtingwa.
 Mwenyekiti wa kikundi cha tupendane Bi.Rosena Rashid- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akipokea mkopo wa pesa kutoka kwa wakala wa M-PESA wa Vodacom Morogoro,Bw.Verus Bitahilo(alieketi)Kampuni hiyo inatoa mikopo kwa wanawake wadogowadogo wajasiriamali hapa nchini isiokuwa na riba wanawake hao walipokea mkopo huo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 327 kupitia mradi  wake wa "MWEI" na kurudisha mikopo hiyo kwa njia ya M-PESA.anaeshuhudia wapili toka kulia walioketi ni Meneja wa mradi huo Bi.Grace Lyon.
 Wakala wa M-PESA wa Vodacom Mkoani Morogoro,Bw.Verus Bitahilo(alieketi)akimkabidhi Mwenyekiti wa kikundi cha Mother support Bi.Veronica Nyemele- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini Mkazi wa,mkopo wa kiasi cha shilingi 100,000 usiokuwa na riba unaotolewa na Vodacom kupitia mradi  wake wa "MWEI"unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini,waliopatiwa mkopo wa zaidi ya shilingi Milioni 327 wilayani hapo.
  005. Mwenyekiti wa kikundi cha Mother support Bi.Veronica Nyemele- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini akihesabu pesa zake alizopewa mkopo usio na riba toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI"unaowawezesha wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini,wanawake 7500 walinufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni 327.
 Mwenyekiti wa kikundi cha Mother support Bi.Veronica Nyemele- Mkazi wa Tarafa ya Matombo Morogoro vijijini  akionesha na kufurahia  pesa zake alizopewa mkopo usio na riba toka Vodacom Tanzania kupitia mradi wake wa "MWEI"unaowawezesha  wanawake wajasiriamali wadogowadogo nchini, wanawake 7500 walinufaika na mkopo huo wa zaidi ya shilingi Milioni 327.

Hospitali Mwanza yapata mashine ya kisasa kuboresha uzazi salama

$
0
0
 Meneja wa KCB tawi la Mwanza, Joseph Njile (kushoto) akikabidhi mashine ya kisasa ya ultrasound kwa mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Ilemela Amina Masenza kabla ya kuikabidhi kwa uongozi wa hospitali ya SDA ya jijini Mwanza.Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 15 ni mahsusi kwa kupima afya ya wajawazito ili kuwawezesha wapate uzazi salama.
========  ======  =========
Mashine bora ya ultrasound  kusaidia maelfu ya wazazi Kanda ya Ziwa
 Na Mwandishi, Mwanza

Benki ya KCB tawi la Mwanza  imetoa msaada wa mashine ya kisasa ya na vifaa vengine vya upimaji  kwa kwa hospitali ya  Kanisa la Wasabato(SDA) ya  jijini hapa ikiwa ni azma yake  kuboresha uzazi salama katika mikoa ya Kanda ya ziwa.

Msaada huo ambao uliambatana na mashine ya kuchapa matokeo papo hapo, ulitolewa mwishoni mwa juma kwa hospitali hiyo na meneja wa KCB tawi la Mwanza, Joseph Njile mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemema , Amina Masenza na Askofu Mkuu wa jimbo la Nyanza, Joseph Bulengela.

"Mashine na vifaa hivi ni mahsusi  kwa upimaji na utoaji wa matokeo papo hapo kwa wajawazito na wagonjwa wengine wenye matatizo ya tumbo, uzazi, kansa na  udhaifu wa viungo vya ndani, kwa mwaka mzima, mashine hizi zinaweza kuhudumia zaidi ya watu 3,000,"  alisema Daktari Joseph Kajiru, Mganga Mfawizi wa hospitali hiyo.

Kwa upande wake, meneja wa KCB tawi la Mwanza,  Bw Njile alisema vifaa vya kidijitali vilivotolewa na benki yake vina jumla ya thamani ya shilingi milioni 15 ikiwa ni kutekeleza ahadi ya benki yake kwa wananchi wa Mwanza ambayo ilitolewa  mwaka jana wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Uratibu na Mahusiano, Steven Wassira.\

  "Mimi nafarijika sana kusikia  kwamba mashine mpya imefika kwa wakati muafaka na iko tayari kuanza kutumiwa  mara moja," alisema Bw Njile katika hafla iliyohudhuriwa pia na mamia ya waumini wa madehehebu ya Kisabato jijii.

Mmoja wa wakazi wanategemewa kunufaika na ujio wa mashine hizo, alikuwa ni mjamzito aitwaye Adela Misana, 28,  ambaye  alidai kuwa  mashine hizo za kisasa zimempa yeye  na akima mama wengine  uhakika wa uzazi salama ambao utaepusha vifo vya wazazi na watoto wakati wa kujifungua. 

"Mimi namshukuru Mungu kwa kuipa KCB moyo wa huruma na upendo  kwani mashine hii  itawapa ufanisi mkubwa  wafanyakazi wa hospitali katika kufuatilia afya za wajawazito  na hatimaye kuwawezesha wapate uzazi salama," alisema mama huyo mwenye watoto wawili.

Zaidi ya hayo, Askofu mkuu wa Jimbo la Nyanza,  Bulengela alitoa shukrani zake kwa KCB kwa msaada wa vifaa tiba vitakavyookoa maisha ya maelfu na kutoa wito kwa mamlaka ya hospitali kuvitunza vifaa hivyo ili viendelee kuhuduia watu kwa muda mrefu.

 "Mchango mkubwa ambao thamani yake ni zaidi ya Shilingi milioni 15 zilizotumika kwa ununuzi wake kwa sababu thamani ya uhai wa binadamu haipimiki kwa fedha,"
Kwa kumalizia meneja wa tawi bwana Njile, alisema: "Itakuwa faraja kubwa kusikia kuwa akina mama na wajawazito  mkoani Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla wamepata mafanikio makubwa ya kiafya kupitia hospitali hii na vifaa ambavo KCB imevikabidhi leo hapa."

UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha mawasiliano toka Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mkumbwa ally(Kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari juu ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa na kulia ni Mkuu wa Idara ya Asia na Australasia Balozi Mbelwa Kairuki.

 Mkuu wa Idara ya Mashariki ya kati toka Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano Balozi Hassan Simba(Kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari sababu za kufungua Balozi za Tanzania nchini Brazil na Malasia, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyikaleo Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano toka Wizara hiyo Bw. Mkumbwa ally.



Mkuu wa Idara ya Asia na Australasia toka Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano Balozi Mbelwa Kairuki(Kulia)akijibu moja ya maswali ya waandishi wa Habari juu ya Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyikaleo Jijini Dar es Salaam kushoto Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa. Picha zote na Hassan Silayo.
==========  ========  =========


UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imekuwa inatekeleza Sera Mpya ya Mambo ya Nje iliyoanza kutumika rasmi 2001. Lengo la sera hii ni kufanya mageuzi katika sera ya awali ya mambo ya nje ya Tanzania ili iendane na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyotokea ndani nan je ya nchi.

Sera mpya inaweka kipaumbele kwenye diplomasia ya uchumi, na kazi kubwa ya Wizara ya Mambo ya Nje ni kuratibu shughuli za wizara nyingine na Asasi za serikali na binafsi katika kukabiliana na changamoto za maendeleo kwa kufuata diplomasia ya uchumi madhubuti na endelevu.

Mikakati inayotumika kutekeleza sera ya mambo ya nje ni pamoja na kujenga mazingira wezeshi ya ndani ya kukuza uchumi;  kuimarisha ubia wa kimataifa; kuweka mbele malengo ya uchumi katika ushirikiano wa pande mbili (bilateral cooperation); kuimarisha uhusiano wa kimataifa (multilateral cooperation); kukuza ujirani mwema na kukuza ushirikiano wa kikanda.

Njanja zinazotumiwa kutekeleza malengo ya kukuza ushirikiano ni mikutano ya pande mbili, tume za pamoja za ushirikiano, mikutano ya kimataifa, balozi zetu nchi za nje na ziara za viongozi wetu wa kitaifa nchi za nje na viongozi wa mataifa ya nje hapa nchini.

Wizara imepata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi, ambayo yamejidhihirisha katika sekta mbali mbali, zikiwemo za afya, kilimo, nishati, mifugo na uvuvi, viwanda, miundombinu na uchukuzi.
Baadhi ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2011/12 hadi sasa ni pamoja na yafuatayo:-
 

                                                                                                                                           

Sekta ya Afya

Mwezi Oktoba, 2012, Bloomberg Philanthropies ya Marekani ilitoa Dola za Marekani milioni nane(US$8,000,000)  kwa ajili ya kuboresha vituo vya afya vijijini hapa nchini. Ufadhili huo ulizinduliwa mjini New York, Marekani, na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Msaada huo utatumika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya za dharura kwa wanawake wajawazito na kuendesha mafunzo kwa maafisa tabibu wasaidizi na wakunga.

Sekta ya kilimo

Katika mwaka wa fedha wa 2012, Mradi wa Rais Barack Obama wa Marekani wa kuendeleza uzalishaji wa chakula katika nchi zinazoendea (Feed the Future)  ulisaidia zaidi ya wakulima 14,000 kutumia mbinu mpya za kilimo katika mashamba yao ya jumla ya hekta 22,430, chini ya mpango wa Taifa was kukuza kilimo ukanda wa kusini (SAGCOT), wakati wakulima wengine 13,000 walisaidiwa kuongeza uzalishaji kwa hekta kwa asilimia 46. Mradi huo pia ulifadhili mipango ya lishe iliyofaidia watoto 96,000 nchini.
Aidha, wizara  ilifanikiwa kushawishi mamlaka za Chakula za Jamhuri ya Watu wa China kuruhusu tumbaku inayozalishwa Tanzania kuingia kwenye soko la China. China peke yake inanunua asilimia 46 ya tumbaku yote duniani na inalipa bei ya juu kuliko nchi nyingine.

Sekta ya Nishati

Serikali ya China imetoa mkopo wa masharti nafuu kujenga bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na mitambo ya kusafishia gesi hiyo. Jumla ya gharama za mradi huu utakaoongeza uzalishaji wa umeme nchini ni dola za Marekani bilioni 1.2.
Aidha, Tanzania ni kati ya nchi saba za Afrika zitakazofaidika na mradi wa upanuzi wa uzalishaji wa umeme utakaogharimiwa na Serikali ya Marekani (dola za Marekani bilioni 7) na Washirika wengine wa maendeleo (dola bilioni 9).



Sekta ya Mifugo na Uvuvi

Wizara iliratibu ziara ya ujumbe wa wataalam kutoka serikali ya Oman uliokuja nchini kutafuta fursa za biashara ya nyama na mazao yake. Mazungumzo yanaendelea kati ya Oman na Kampuni ya Ranchi za Taifa ili kuwezesha nchi yetu kufaidi9ka na biashara ya mifugo na kuboresha maisha ya wafugaji.

Sekta ya Viwanda

Wizara imeratibu mipango ya kampuni ya Nitori ya Japan kuwekeza katika sekta ya viwanda hapa nchini. Nitori itajenga kiwanda cha nguo katika Ukanda Maalum wa Uwekezaji uliopo Bagamoyo, na tayari imepatiwa eneo la kulima pamba huko Handeni, Tanga. Uwekezaji huo utatoa ajira kwa maelfu ya Watanzania.
Wakati huohuo, Wizara kwa kushirikiana na Ubalozi wetu New Delhi, india, inaratibu mpango wa Serikali ya India kufadhili miradi ya kuendeleza teknolojia ya viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO). India itatoa dola za Marekani milioni 2ikiwa ni sehemu ya msaada ulioahidiwa na Waziri Mkuu Dkt. Manmohan Singh alipotembelea Tanzania Mei, 2011.

Sekta ya Miundombinu na Uchukuzi

Wizara imeshiriki kuivutia kampuni ya China Merchant Holding International kuja kujenga bandari kubwa ya kisasa (4th generation port) huko Bagamoyo, ambako pia kampuni hiyo itajenga eneo la ukanda maalum wa uwekezaji (Export Processing Zone- EPZ), mji wa kisasa pamoja na miundombinu ya reli na barabara.

Mkataba wa Mwongozo (Framework Agreement) kuhusu uwekezaji huo ulitiwa saini wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping hapa nchini, Machi, 2013. Mradi huo mkubwa utatoa ajira za moja kwa moja kwa maelfu ya Watanzania na kuliingizia taifa mapato kutokana na kodi na mrabaha. Aidha utasaidia kupunguza foleni na msongamano katika jiji la Dar es Salaam.
                                                              

Kadhalika, Serikali ya Japan imekubali ombi la Tanzania kupitia Wizara yetu, kufadhili ujenzi wa barabara za kupita juu (flyovers) katika makutano ya Barabara za Nyerere na Mandela, eneo la TAZARA jijini Dar es Salaam.
Makubaliano hayo yalifikiwa katika mkutano uliofanyika Arusha Mei, 2012, kati Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa JICA. Mkataba wa makubaliano hayo umetiwa saini na Serikali ya Japan inafanya maandalizi ya ujenzi.

Sekta ya Maji

Wizara imeweza kushawishi nchi mbali mbali rafiki kusaidia ujenzi wa miradi ya maji hapa nchini. Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Serikali za Ujerumani na Tanzania, wamegharamia mradi wa maji wa Swaya mkoani Mbeya, ambao utafaidia wananchi 490,000. EU imechangia shilingi bilioni 36.9, Ujerumani shilingi bilioni 13.5 na Serikali ya Tanzania shilingi bilioni 29.1

Mradi huo ulifunguliwa na Mheshimiwa Rais Kikwete wakatiwa ziara ya Mheshimiwa Jose Manuel Barroso, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya hapa nchini Julai, 2012.
Aidha, Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund), imesaini makubaliano ya kugharamia mradi mkubwa wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe, utakaofaidia mamia ya maelfu ya wananchi wa mikoa ya Kilimanjaro na Tanga. Mradi huo utatekelezwa mwaka huu wa fedha.

Mafanikio mengine ya Wizara

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).  Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Kituo hicho jijini Dar es Salaam.  Kituo hicho kina uwezo wa kuchukua watu 1600 kwa wakati mmoja na ujenzi wake umegharimu USD Milioni 15.5.


Ufunguzi wa Balozi mpya: Tangu kipindi cha mwaka 2007 hadi2013 Tanzania imefungua Balozi mpya nne ambazo zimefunguliwa katika nchi za Brazil, Malaysia, Uholanzi na Comoro na kuifanya Tanzania kuwa na jumla ya Balozi 34, Balozi Ndogo 3 na Balozi za Heshima 17.





Heshima ya Tanzania Kimataifa: Tanzania ilikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka 2008 chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete  na Tanzania sasa ni Mwenyekiti wa Asasi ya Ulinzi, Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA) kuanzia Agosti 2012 hadi Agosti 2013.
 
·        Uteuzi wa Watanzania wengi kushika nyadhifa mbalimbali kimataifa na kikanda:  Mfano ni Dkt. Asha-Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na hivi sasa ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja huo katika Masuala ya UKIMWI Barani Afrika.  Mwingine ni Balozi Liberata Mulamula, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Maziwa Makuu (ICGLR), na wengine wengi. 

 Ziara za viongozi wa Mataifa Makubwa Duniani

Katika kipindi cha utakelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje, Tanzania imekuwa mwenyeji wa ziara kadhaa za viongozi wa juu wa mataifa makubwa duniani. Mwaka huu wa 2013 pekee, nchi yetu imetembelewa na Rais Xi Jinping wa Jamhuri ya Watu wa China na Rais Barack Obama wa Marekani.

                                                            
Rais Xi amekuwa kiongozi wa juu wa pili wa China kutembelea Tanzania ndani ya miaka mitano iliyopita wakati Rais Obama ni Rais wa tatu wa Marekani aliyeko madarakani kuzuru nchi yetu tangu mwaka 2000. Ziara hizi ni kilele cha mafanikio ya sera yetu mpya ya mambo ya nje na zinadhihirisha umaarufu ambao viongozi wetu wameijengea nchi yetu katika uwanja wa kimataifa.

Aidha, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Majadiliano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue), uliohudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali saba. Zaidi ya nchi 20 ziliwakilishwa kwenye mkutano huo.

Hitimisho

Sera mpya ya Mambo ya Nje inayoweka kipaumbele kwenye diplomasia ya uchumi, imeleta manufaa makubwa kwa nchi yetu na kuweka wazi zaidi jukumu la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa la kuratibu na kusukuma juhudi za kukuza uchumi wa taifa.


IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES N  `        SALAAM.
JULAI 28, 2013
 

VIJANA MKOANI IRINGA WATAKIWA KUSHIRIKI AFYA YA UZAZI

$
0
0
VIJANA mkoani Iringa wametakiwa kushiriki katika afya ya uzazi kwa vijana ili kuzijua na kuzitambua haki za afya ya uzazi kwa vijana na kutambua mahitaji yao muhimu.

Akizungumza leo,Ofisa utetezi na sera wa mradi wa haki ya afya ya uzazi kwa vijana Meshack Mollel alisema kuwa vijana wanatakiwa kushiriki na kupata elimu ya afya ya uzazi ili kujitambua na kujua haki zao na kuunda sera zinazowahusu.

Mollel alisema kuwa mradi huu unatekelezwa katika manispaa tatu ikiwamo  IRinga , Ilala na Kinondoni ili kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana kwa kushirikiana na  shirika la afya na tiba  AMREF chini ya ufadhili wa shirika maendeleo la nchini  swedeni(SIDA).

“Tamasha hili la vijana lenye kauli mbiu inayosema “hamasisha ushiriki wa vijana ili kutambua mahitaji muhimu katika afya ya uzazi”pia tukiwa na lengo la kutoa elimu na kuzijua haki  za afya ya uzazi kwa vijana na kuwapa fursa ya kuunda sera zinazo wahusu vijana”alisema Mollel.

Kwa upande wake naibu meya wa manispaa ya Iringa Gervas Ndaki ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa anafurahi kuwaona vijana wamejitokeza kwa wingi hivyo anaimani hata katiba mpya ya sasa itakuwa na maoni na sera zinazo muhusu kijana.

“dhana hii ya michezo ni dhana nzuri ya kuwakutanisha vijana kwa sababu kwanza michezo inapendwa na vijana wengi na  inajenga afya zao na kuwa fanya waondokane na makundi yasiyofaa kutokana na vijana kuwa na changamoto nyingi”alisema Ndaki.

DAVIS MOSHA AHOJIWA NA VOA (VOICE OF AMERICA)

$
0
0
Edgar Davis Mosha mtoto wa mfanyabiashara tajiri na maarufu boss wa kampuni ya DELINA  Bwana Davis Mosha ahojiwa na VOA (Voice of America). Edgar na baba yake wametua kwa kishindo nchini Marekani wakitokea Uingereza ambapo Edgar amepeperusha vyema bendera ya Tanzania kwa kuitwa  kufanya majaribio na klabu ya Chelsea ya Uingereza. Swahili TV itakuletea Exclusive video karibuni.


 Davis Mosha "The Boss" akifanya mahojiano na kituo cha VOA jijini Washington DC, kulia ni mwanae Edgar Mosha mwanafunzi mwenye kipaji cha masomo na soka.


 Davis Mosha "The Boss" akifurahia jambo katikati ya mahojiano na kituo cha VOA jijini Washington DC.
Kutoka kushoto; Juliet , Sunday Shomary, Edgar Mosha, Davis Mosha "The Boss" na Chief wa VOA Idhaa ya Kiswahili Dkt. Hamza Mwamoyo.

Davis Mosha "The Boss" na Edgar Davis wakipata picha ya kumbukumbu baada ya kuteta na VOA, Jijini jijini Washington DC
Edgar Davis, Davis Mosha "The Boss" na mtangazaji mahiri bwana Sunday Shomary 

Juliet, Alex Kassuwi, Edgar na The Boss wakipata picha ya ukumbusho VOA.




Baada ya mahojiano na kituo cha VOA msafara wa The Boss ulielekea SEquoia kwa hafla fupi .
Edgar na Juliet wakiwa Sequoia water front.

MANENO MBEGU NA QUEEN SENDIGA WAMEREMETA

$
0
0
 Bwana Harusi Maneno Mbegu akivishwa pete na mwandani wake, Queen Sendiga walipokuwa wanafunga ndoa hivi karibuni katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
                     Maneno Mbegu akiapa mbele Ofisa Tawala  Wilaya ya Kinondoni
                                    Queen akila kiapo
                                Mbegu akitia saini
 Queen akitia saini
Wakitoka baada ya kufunga pingu za maisha
Du! hivi kweli tumeoana?
                                                Maharusi wakiwa na sura za bashasha.
Baba akimpongeza binti yake kwa kuolewa
Mbegu na mkewe Queen akiw na katika picha ya pamoja na wakwe zake.
Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na ndugu zao pamoja na marafiki.
Queen akiwa na mamake mzazi katikati na mdogo wake
Queen akiwa na watoto wapambe

MTUHUMIWA WA WIZI ANUSURIKA KUFA KWA KIPIGO CHA WANANCHI KAWE

$
0
0
 Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa watu wenye hasira.
MTU mmoja aliyetuhumiwa kuwa ni mwizi amenusurika kufa baada ya kundi la wananchi kumpa kipigo cha maana, leo mchana katika eneo la Mbezi-Darajani, Kawe mjini Dar es Salaam. Mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja inadaiwa alikutwa akiruka geti kuingia ndani kwenye nyumba ya mkazi moja wa eneo hilo. Picha zifuatazo ni baadhi ya matukio wakati mtuhumiwa huyo alipokuwa akipata kichapo hicho.  
 Akisulubiwa kwa bakora na mmoja wa wananchi hao wenye hasira.
 Mtuhumiwa wa wizi akiomba kusamehewa wakati mtu mwenye hasira akijiandaa kumtupia tofali kichwani ambalo lilimjeruhi vibaya mtuhumiwa huyo
 Akiendelea kuslubiwa wakati wakipelekwa polisi.
 Mwenye hasira akimsulubu mtuhumiwa huyo kwa kumtandika teke. 
Lakini kutokana na kipigo akaanguka hadi hatua iliyofanya watu hao wenye hasira kutawanyika eneo la tukio, wakidhani mtuhumiwa amekufa. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO.

RAIS KIKWETE AKIWA WILAYANI MULEBA

$
0
0
Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera
Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni

Huawei contributes USD 30,000 to NM-AIST to build capacity in ICT research

$
0
0
 The Huawei Technologies Tanzania Public Affairs and Communication Director for East Africa , Mr David Wang (Right) and The Nelson Mandela African Institute of Science and Technology (NM-AIST) Vice Chancelloe, Professor Burton Mwamila (left) shake hands after signing the memorandum of Understanding (MoU), at the ceremony held in Arusha at the weekend. Witnessing the signing (standing) from right is the Minister of Communication, Science and Technology, Professor Makame Mbarawa and Chinese Ambassador to Tanzania, Mr. Lu Youqing. Huawei contributed USD 30,000 (About Sh48m/-) to the institute to build capacity in ICT researches.
 The Huawei Technologies Tanzania Public Affairs and Communication Director for East Africa , Mr David Wang (Right) and The Nelson Mandela African Institute of Science and Technology (NM-AIST) Vice Chancelloe, Professor Burton Mwamila (left) sign the memorandum of Understanding (MoU), at the ceremony held in Arusha at the weekend. Witnessing the signing (standing) from right is the Minister of Communication, Science and Technology, Professor Makame Mbarawa and Chinese Ambassador to Tanzania, Mr. Lu Youqing. Huawei contributed USD 30,000 (About Sh48m/-) to the institute to build capacity in ICT researches.
=======  ======  =======

Huawei contributes USD 30,000 to NM-AIST to build capacity in ICT research
By Our Correspondent, Arusha.

HUAWEI Technologies Tanzania Co. Limited, a global leading company in the information and communications Technology industry, has signed a Memorandum of Understanding (MoU) with Nelson Mandela African Institute of Science and Technology (NM-AIST) that aimed at building capacity in ICT research at the institute. 


The MoU will see Huawei Technologies for continuous 3 years releasing USD 30,000 (about Sh48m/-) each year to support ICT researches for the students who are studying Master program in ICT field at NM-AIST.

Speaking during the signing ceremony held at the Institute at the weekend, the Minister of Information, Science and Technology Prof. Makame Mbarawa said the agreement will see Tanzania through NM-AIST’s masters and PhD students build capacity in conducting ICT researches and help improve the country’s technology.


“Am sure that the agreement will be a catalyst for speedy development of ICT sector in the country as the university will now have the opportunity to embark more on doing research in the ICT field and the findings will enable us discover new technologies in the ICT industry,” said Prof. Mbarawa.


The Chinese Ambassador to Tanzania, Mr. Lu Youqing during the event in his remarks appreciated the contribution made by Huawei Technologies Tanzania to the development of ICT in Tanzania. “Am very pleased to see Huawei plays a vital role in bringing about ICT development in Tanzania. Huawei’s contribution to ICT sector in the country will not only bring technological advancement but also help grow the country’s economy as a whole.


“It is through Information, Communications and Technology development that enable any country achieve political, social and economic growth because ICT is an enabler of technology innovation, driving social and economic development, and creating value for individuals and society as a whole,” said Ambassador Youqing.


Huawei’s Technologies Public Affairs and Communication Director in the East African Region, Mr. Wang Shun Li during the event said the funds will be used to cater for the masters’ students ICT researches at Nelson Mandela African Institute of Science and Technology (NM-AIST) that will see the university build capacity on researching the ICT related topics.   


“As part of our ICT Star programme which supports the development of ICT sector in Tanzania, we are confident that the contribution will encourage students putting more efforts into their ICT researches as their findings will play a vital role in boosting ICT sector development in the country,” said Mr. Wang.


Mr. Wang, underscored his company’s commitment in supporting growth of the country’s ICT industry, pointing out that through support on ICT sector more and more ICT engineers and experts will be generated thus contributing to the ICT development in Tanzania.


On his part, the NM–AIST Vice Chancellor, Professor Burton Mwamila, said that Huawei’s support will be a great boost to the masters students at the institute to do their researches effectively.

“We thank Huawei for supporting our university, and we promise to use the funds provided accordingly in making sure that the funds are allocated into the ICT researches so as to enable boost the development ICT sector in the country,” said Prof. Mwamila.

WANACHAMA WA MFUKO WA MAENDELEO YA MTANDAO WA WANAMBWEWE WAISHIO DAR ES SALAAM, WAKUTANA NA MBUNGE WAO

$
0
0
 MBUNGE wa Chalinze, wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo, akizungumza na wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanambwewe waishio Dar es Salaam (MNDF), leo katika ukumbi wa Shule ya Msingi Ali Hassani Mwinyi, mjini Dar es Salaam. Wanachama hao walimwalika kwenye kikao chao cha kujadili jinsi ya kuuendesha mfuko huo kwa manufaa ya wananchi wengi
 MBUNGE huyo akisisitiza jambo
 Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Katibu wa wanachama wa Mfuko wa Maendeleo ya wanamtandao wa Mbwewe waishio Dar  es Salaam, Hassani Msonde akizungumza mwanzoni mwa kikao
 Mwenyekiti wa Umoja huo, Rajabu Papa akifungua kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati ya Umoja huo, Fatuma Kikwappe akisoma risala huku viongozi wakimsikiliza kwa makini akiwemo Mbunge Bwanamdogo
 Fatuma akiendelea kusoma risala hiyo
Kisha akaikabidhi risala hiyo kwa Mbunge wa Chalinze, Saidi Mwanamdogo
 Mbunge Saidi Mwanamdogo akiwakabidhi dola za Marekani, viongozi wa umoja huo, ikiwa ni mchango wake kwa ajili ya kufanikisha usajili.
 Mwenyekiti akimkabidi Mbunge Katiba ya Umoja
 Fatuma na mjumbe mwenzake wa Kamati katika Umoja huo wakipitia makabrasha kwa makini
 Mbunge wa Chalinze Saidi Mwanamdogo akiagana na viongozi wa Umoja huo baada ya kushiriki kikao>IMETAYARISHWA NA theNkoromo Blog

Sikiliza na angalia kwa makini Video ya Mahojiano ya Sunday Shomari na Mhe. Edward Lowassa. Washington DC (Part One & Two)

$
0
0
Sikiliza na angalia kwa makini Video ya Mahojiano ya Sunday Shomari na Mhe. Edward Lowassa. Washington DC (Part One & Two)


Karibu katika sehemu ya kwanza na ya pili ya mahojiano kati ya Sunday Shomari na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Siku ya Jumatano Julai 17, 2013 jijini Washington DC.

Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya Airtel yatosha.

$
0
0
 Mteja wa Airtel mkoani arusha bw, Robert Justin akihesabu pesa zake alizojishindia wakati wa promosheni ya Airtel yatosha mara baada ya kuzitoa kupitia njia ya Airtel Money katika ofisi za Airtel mkoani
Arusha.

 Meneja wa airte Mauzo wa kanda ya kaskazini Stephen Akyooo akikabidhi shilingi milioni 1 kwa Bw, Robert Justine wa jijini Arusha fedha alizojishindia katika promosheni  ya Airtel Yatosha inayoendeshwa na
Airtel maalum kwa wateja  wake wote wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kwa wiki, siku au mwezi mbapo pia mteja anaweza kujishindia moja kati ya Nyumba 3 za kisasa zilizopo dar es salaam.

Meneja wa airtel kanda ya kaskazini Stephen Akyoo akiwa na washindi wawili wa shilingi milion moja wa shindano la airtel yatosha kutoka  mkoani Arusha bw, Robert Justine and Balistus Mambo. Washindi wote
walikabidhiwa shilingi milioni moja kila mmoja walizojishindia katika promosheni ya Airtel yatosha na kuzitoa kwa Airtel Money.

=======  =======  =====

Airtel yakabidhi milioni 14 kwa washindi wa promosheni ya  Airtel yatosha.
•         Ni washindi wa shilingi milioni moja wa wiki ya kwanza na ya
pili ya promosheni

Jumapili 28 julai 2013, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo
imetangaa na kuwazawadia washindi 14 wa kila siku wa promosheni ya
Airtel yatosha shinda nyumba  kila mmoja shilingi milioni moja pesa
taslimu kupitia huduma ya Airtel Money.

Washindi hawa wamepatikana kupitia droo ya wiki ya kwanza na ya wiki
ya pili ambapo jumla ya washindi 14 kutoka katika mikoa mbalimbali ya
nchi walipatikana na hatimaye kukabithiwa pesa zao

Akiongea wakati wa kukabithi zawadi kwa washindi hao Meneja Mauzo wa
Kanda Mkoani Arusha  bwana Stephen Akyoo  alisema” leo tunayofuraha
kupata washindi wa promosheni ya Airtel yatosha na kuwakabithi zawadi
zao. Washindi hawa wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali na
kujishindia kila mmoja shilingi milioni moja pesa taslimu kwa kutumia
huduma za Airtel yatosha  na kujiunga na vifurushi vyetu mbalimbali.

nae Meneja Uhusiano wa Airtel Akitangaza majina ya washindi hao bwana
Jackson Mmbando alisema "washindi wetu wa wiki ya kwanza na ya pili ni
pamoja na  Hawa Said Mkazi wa Mtwara, John Masawe mkazi wa singida,
Joseph Emmanuel Nchimbi Songea,  Rosemary Michael na John Masanja
kutoka Tabora , Zuhura Sabuni kutoka Lindi, Balistus mambo kutoka
Moshi, Robert Faustine kutoka Arusha ,  Frank Ladislaus na Paulina
Michael kutoka Sengerema Mwanza, Flavian Adamson Malilo kutoka Katavi,
Jacob Muhole kutoka Dodoma,  Singodi Severin kutoka Kagera  na
Ephrasia Thadeo kutoka Ngara.

Ili kushiriki mteja anatakiwa kupiga  kupiga *149*99#  na kununua
kifurushi cha huduma ya Airtel yatosha cha siku, wiki au mwezi na
kuunganishwa mojakwamoja kushiriki kwenye promosheni na kupata nafasi
ya kushinda nyumba au pesa taslimu shilingi milioni moja kila siku.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo Bwana Robert Justine
moja kati ya washindi anayetokea mkoani Arusha alisema” nimefurahi
sana kuwa mshindi wa promosheni na ntaendelea kutumia huduma ya Airtel
yatosha ili kuendelea kufaidika na huduma hii na kupata nafasi ya
kushinda nyumba. Natoa wito kwa watanzania kutumia huduma hii na
kuhakikishia   hata wao wananafasi ya kushinda kama mimi nilivyoweza
leo kukabithiwa shilingi milioni moja kwa kutumia tu huduma ya Airtel
yatosha.

Promosheni ya Airtel yatosha bado inaendelea kwa mienzi mitatu hadi
hapo mwishoni mwa mwenzi wa tisa ambapo mbali na zawadi za pesa
taslimu wateja pia wanapata nafasi ya kujishindia nyumba 3 zilizopo
kigamboni jijini Dar es saalam.

RAIS KIKWETE AWAPONGEZA WANAHABARI WA KAGERA KWA KAZI NZURI WAKATI WA ZIARA YAKE

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanahabari wa Mkoa wa Kagera ambao amewapongeza kwa kazi nzuri waliyofanya wakati wa ziara yake ya siku sita mkoani humo. Hapa ni katika uwanja wa Kaitaba mara baada ya kuhutubia umati mkubwa wa wananchi katika kuhitimisha ziara hiyo
 Rais Kikwete akiwapongeza wanahabari wa Kagera kwa kazi nzuri
 Akisalimiana na mkongwe Meddy Mulisa wa Daily News
 Hongera kwa kazi nzuri dada...
Rais Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na wanahabari hao.

Wafanyakazi wa Benki ya NBC watembelea kituo cha watoto yatima na kuwakabidhi misaada.

$
0
0
 Wafanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha operesheni, wakipozi kwa picha na watoto wanaolelewa katika kituo cha Ijango Zaidia Orphanage cha Sinza walipokwenda kupeleka msaada wa vyakula, sabuni, mafuta ya kupikia na vyandarua ikiwa ni moja ya mikakati ya NBC kurudisha sehemu ya faida waipatayo katika jamii. Hafla ilifanyika kituoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Wengine ni watumishi wa kituo hicho.

 Mkurugenzi wa Uendeshaji na Huduma wa Benki ya NBC Tanzania, Cornie Loots (kulia) akikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua kwa Mkuu wa kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage , Bi. Zaidia Nuru Hasani, vilivyotolewa na NBC kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

 Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, Ramia Mahmoud , akipokea mafuta ya ngozi kwa niaba ya wenzake vyaliyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Ernest Paulo Mbepera (kulia) kituoni hapo, Sinza, jijini Dar es Salaam. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia, sabuni na vyandarua.

 Mfanyakazi wa Benki ya NBC, Mwanaisha Nassoro Ayosi (kulia) akikakabidhi misaada iliyotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi.

Mtoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima cha Ijango Zaidia Orphanage, Amina Twahilu, akipokea moja ya vyandarua kwa niaba ya wenzake vilivyotolewa msaada na Benki ya NBC kutoka kwa mfanyakazi wa benki hiyo, Anyelwisye Enock Mwakatobe (kulia) kituoni hapo, Sinza, Dar es Salaam juzi. Benki hiyo pia ilikabidhi msaada wa vyakula, mafuta ya kupikia na sabuni. 

SHARE YOUR EXPERIENCE.!

$
0
0
 Blogu yako ya www.tabianchi.blogspot.com inayotoa habari za usafiri wa anga, mazingira, maliasili na utalii, inakuletea kampeni ya ‘Share your experince’.
 
Ambapo wadau, watu binafsi na makampuni ya tours mnaombwa ku-share picha zenu za good moments, matukio mbalimbali ya safari za kwenye hifadhi na vivutio vingine vya utalii, picha za safarini kwenye ndege, ushuhuda wa safari zenu (testimonies) na picha za mazingira mbalimbali.
 
Share experience yako, kupitia blog yako ya tabianchi, email kingkahindi@gmail.com, au tupia kwa fb tabianchi
Asante sana!

DAR KUWA MWENYEJI WA MAONYESHO YA VODACOM ELIMU EXPO 2013

$
0
0


 Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Kivukoni, Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo, wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maonyesho ya siku tatu ya Vodacom Elimu Expo, yanayotarajia kuanza Agosti 30, mwaka huu katika Viwanja vya Michezo vya Chuo cha Posta, Kijitonyama jijini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa. 


 Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo (katikati) Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) na  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakigonganisha glasi, kama ishara ya uzinduzi wa maonyesho hayo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo leo, Katikati ni   Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo, na Mkurugenzi Mkuu wa Elimu Expo, Joel Njama.
 Sehemu ya waandishi wa habari, waliohudhuria mkutano huo.PICHA NA SUFIANIMAFOTO.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images