Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1287 | 1288 | (Page 1289) | 1290 | 1291 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dk,Ali Mohammed Shein akimvisha nishani ya Mapinduzi Bwana Aboud Talib Aboud katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapindizi Dk,Ali Mohammed Shein katikati akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi na waliotunukiwa nishani mbalimbali katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.
  Baadhi ya waalikwa waliohudhuria katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.
  Baadhi ya Waheshimiwa waliohudhuria katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.
  Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi kulia akipeana mikono na Makamo wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Gharib Mohammed Bilal katika hafla ya kutunuku nishani ya Mapinduzi,nishani ya Utumishi uliotukuka na nishani ya Ushujaa iliofanyika katika viwanja vya Ikulu mjini Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

  Viongozi mbali mbali na Wananchi waliohudhuria katika Sherehe za Kutunuku nishani iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
  Viongozi mbali mbali na Wananchi waliohudhuria katika Sherehe za Kutunuku nishani iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein 
  Baadhi ya Viongozi wa Kitaifa pamoja na Wananchi mbali mbali wakishuhudia na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitunuku Nishani mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja leo 
  Viongozi wakisiama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika Sherehe za Kutunuku nishani iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,shuhuli iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (mbele) pamoja na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi wakisimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika Sherehe za Kutunuku nishani iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja 
  Baadhi ya Viongozi na Wananchi mbali mbali ambao leo wamepewa Nishani mbali mbali na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,NIshani ya Mapinduzi,Viongozi na wananchi  wenyesifa maalum,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Watumishi wa Serikali,Nishani Watumishi wa Idara Maalum za SMZ na Nishani ya Ushujaa 
  Baadhi ya Viongozi na Wananchi mbali mbali ambao leo wamepewa Nishani mbali mbali na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,NIshani ya Mapinduzi,Viongozi na wananchi  wenyesifa maalum,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Watumishi wa Serikali,Nishani Watumishi wa Idara Maalum za SMZ na Nishani ya Ushujaa 
  Baadhi ya Viongozi na Wananchi mbali mbali ambao leo wamepewa Nishani mbali mbali na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,NIshani ya Mapinduzi,Viongozi na wananchi  wenyesifa maalum,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Watumishi wa Serikali,Nishani Watumishi wa Idara Maalum za SMZ na Nishani ya Ushujaa 
  Baadhi ya Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi wakiwa katika Sherehe za Kutunuku nishani iliyofanyika leo katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,ikiwa ni NIshani ya Mapinduzi,Nishani kwa Viongozi na wananchi wenyesifa maalum,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Watumishi wa Serikali,Nishani Watumishi wa Idara Maalum za SMZ na Nishani ya Ushujaa,[Picha na Ikulu.] 29/06/2017 
  Baadhi ya Viongozi na Wananchi mbali mbali ambao leo wamepewa Nishani mbali mbali na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja,NIshani ya Mapinduzi,Viongozi na wananchi  wenyesifa maalum,Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Watumishi wa Serikali,Nishani Watumishi wa Idara Maalum za SMZ na Nishani ya Ushujaa,[Picha na Ikulu.] 29/06/2017.

  0 0


   Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa na Katibu wake , Celestine Mwesigwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ambapo walisomewa mashtaka yao kadhaa ya matumizi mabaya ya ofisi ikiwe Kugushi nyaraka za shirikisho hilo pamoja na kutakatisha fedha zaidi ya laki tatu za kimarekani.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi akiwa na Katibu wake , Celestine Mwesigwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ambapo walisomewa mashtaka ya kadhaa ya matumizi mabaya ya ofisi ikiwa nipamoja na kutakatisha pesa zaidi ya laki tatu za kimarekani. washtakiwa hao wamepelekwa mahabusu Keko kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana hivyo wataletwa tena mahakamani  mpaka julai 3.
   Rais wa Simba ,Evance Aveva na Kaimu wake ,Godfrey Nyange(KABURU) wakiongea na aliyekuwa katibu wa Simba Evodius Mutawala katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu ambapo walipandishwa kwa mashtaka tofauti ikiwemo la matumizi mabaya ya ofisi
   Haji Manara , Said Tully na wadau wengine wa mpira wakiwa ndani ya mahakama ya hakimu Mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo
   Wadau wa mpira wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufatilia kesi inayowakabili viongozi wa Soka hapa nchini
    Wadau wa mpira wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufatilia kesi inayowakabili viongozi wa Soka hapa nchini
   Wadau wa mpira wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufatilia kesi inayowakabili viongozi wa Soka hapa nchini.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kuzuia usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi uko pale pale.

  Pia amesema mahindi iliyokamatwa mkoani Kilimanjaro yakisafirishwa kwenda nje ya nchi yataingizwa kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) na magari yatabaki polisi.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo ( Alhamisi Juni 29, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mheshimiwa Ritha Kabati (Viti Maalumu) aliyetaka ufafanuzi kuhusu zuio la kusafirisha mazao nje ya nchi kwa mikoa yenye chakula cha ziada.

  “Tumedhibiti na kuzuia usafirishaji wa chakula hasa mahindi kwenda nje ya nchi ili kuliepusha Taifa kukumbwa na baa la njaa kutokana na baadhi ya mikoa kutopata mavuno ya kutosha,”

  “Kuna maeneo kama ya Sengerema na Geita mahindi yamekauka, hivyo bado tuna upungu wa chakula. Na hata bei ya chakula ipo juu, hatuna namna nyingine zaidi ya kudhibiti utokaji wa chakula kwenda nje na nawasihi wananchi tushirikiane katika jambo hili,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema kama kunaulazima wa kusafirisha chakula kwenda nje ya nchi wahusika wakaombe kibali katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kibali kiwe cha kusafirisha unga na si mahindi.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema watumishi wote wa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Mkuu Dodoma (CDA) waliokuwa wanaolalamikiwa na wananchi kutokana na utendaji wao wataondolewa wakati wenzao wakihamishiwa Manispaa ya Dodoma.

  Waziri Mkuu amesema kwa sasa wanaendelea na ukaguzi na uhakiki wa kina kwenye masuala ya fedha na utumishi ili waweze kujua CDA ilipovunjwa iliacha fedha kiasi gani na shughuli zake zilifikia hatua gani ili ziendelezwe.

  Amesema majukumu yote ya CDA yatafanywa na Manispaa ya Dodoma na baada ya kukamilisha utaratibu huo mpango kazi wote utaendelea kama ulivyopangwa.Kuhusu waliolipia viwanja watakabidhiwa mara baada ya kukamisha utaratibu huo.

  Waziri Mkuu alikuwa akijibu swali la Mheshimiwa Matha Malata (Viti Maalumu) aliyetaka kupata tamko la Serikali kuhusu wananchi ambao waliolipia viwanja CDA ambao bado hawajakabidhiwa.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  ALHAMISI, JUNI 29, 2017.

  0 0

  Wadau wa Habari nchini wakiongozwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja kwa lengo la kuboresha mahusiano ya utendaji wa kazi iliyoshirikisha Serikali na wadau wa habari nchini.

  Semina hiyo pia ilihudhuriwa na maafisa wa Serikali wakiongozwa na Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii Bi Annastazia Wambura, Wabunge, wawakilishi wa vyuo vikuu, viongozi wa taasisi za Habari nchini, wahariri na waandishi.

  Naibu Waziri, Anastazia Wambura akizungumza kwenye mkutano huo amesema serikali iko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kufikia malengo waliyojiwekea katika kuhabarisha umma.
  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akizungumza kwenye mkutano wa wadau mbalimbali wa habari waliokutana kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ili kuleta ustawi wananchi leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili wa Magazeti, Bw. Patrick Kipangula akiwasilisha mada kuhusu sheria ya vyombo vya habari aliyoiwasilisha kwenye mkutano wa wadau wa vyombo vya habari waliokutana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura.
  Mjumbe wa Bodi ya MISA Tanzania, James Marenga akizungumza kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari hasa kwenye sheria ya vyombo vya habari.
  Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya serikali na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri, Maafisa habari na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa(kushoto) akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo  yanayohusu Idara ya Habari Maelezo yaliyoulizwa na wadau wa habari kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa habari waliokutana leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura.
  Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Paul Dotto Kuhenga akiwasilisha mada kwa wahariri, waandishi wa habari na maafisa habari wa Serikali waliokutana kujadili njia bora ya kufanya kazi kwa pamoja leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
  Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wabunge na baadhi ya wahariri, waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Serikali na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote. 
  Baadhi ya wadau mbalimbali wa vyombo vya habari wakichangia mada kuhusu namna ya kushirikiana kati ya Serikali na vyombo vya habari hapa nchini ili kuleta ufanisi katika tasnia ya habari.
  Baadhi ya wadau mbalimbali wa vyombo vya habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa kushirikiana kati ya Serikali na vyombo vya habari hapa nchini ili kuleta ufanisi katika tasnia ya habari.
  Picha ya pamoja


  0 0

  NA BASHIR NKOROMO

  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaridhishwa sana na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kwa kuwa serikali hiyo imejikita ipaswavyo katika kutekeleza ilani ya Chama ikiwemo kuipeleka Tanzania katika nchi ya Uchumi wa Viwanda.

  Akizungumza na Waandishi wa habari katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole, amesema, CCM imefikia hatua ya kutoa tamko rasmi la kuridhishwa kwake na utendaji kazi wa Serikali hiyo, baada ya Chama kufanya ziara ya uhakiki wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa viwanda vikubwa, vya kati na vidogo katika mkoa wa Pwani.

  Hivi karibuni CCM ilipata fursa ya kushiriki katika ziara ya Rais Dk. John Magufuli katika mkoa huo wa Pwani, kwa kuwakilishwa na Polepole, ambapo katika ziara hiyo ya siku tatu, Rais alitembelea na kuzindua viwanda kadhaa ambavyo vinaonyesha kuwa vitachangia kwa kasi kuleta mahuisha matumaini ya lengo la Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa Viwanda.

  "Katika kipindi cha miaka miwili cha Uongozi Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli, mkoa wa Pwani pekee, umeweza kuwa na viwanda vikubwa, vya kati na vidogo zaidi ya 370, hii ni hatua kubwa sana inayoonyesha kuwa Serikali hii imedhamiria kuifikisha Tanzania katika Uchumi wa Viwanda", alisema Polepole.

  Polepole amesema, kufuatia uhakiki iliofanya CCM katika hivyo viwanda zaidi ya 370, viwanda 87 ni vikubwa ambavyo vina uwezo wa uzalishaji bidhaa hadi za kwenda nje ya nchi na kwenda katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba viwanda hivyo vilivyopo mkoa wa Pwani baadhi vimejengwa kwa ubia wa serikali na wadau na vingine wadau wenyewe.

  Alisema, miongoni mwa viwanda vilivyoivutia CCM ni kile cha dawa za kuua viluwiluwi vya mbu ambacho ndicho pekee kilichopo Bara la Afrika na kwamba kiwanda hicho kimejengwa kwa ubia wa Serikali ya Tanzania ya Cuba. "Lakini cha kufurahisha zaidi ni kwamba Mheshimiwa Rais Dk.Magufuli ameshanunua lita 100,000 za dawa hiyo ambayo itasambazwa katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kupambana na malaria", alisema Polepole.

  Polepole alisema, kiwanda kingine ni cha kutengeneza Nondo kilichopo Mlandizi Kibaha, ambacho alisema, kina uwezo wa kuzalisha tani 1000 za nondo kwa siku, na kina uwezo wa kutengeneza mataruma ya reli kwa kutumia malighafi za hapa nchini.

  Kiwanda kingine alikitaja kuwa ni cha kuchakata matunda kilichopo Msoga, ambacho alisema, kina uwezo wa kuchakata tani 30 za matunda kwa siku, na kueleza kwamba uwepo wa kiwanda hiki utasaidia sana kuinua uchumi wa wakulima wa matunda katika mkoa wa Pwani, na kwa kutambua hivyo CCM imewaelekeza viongozi kuhakikisha maofisa ugani wanafika kwa wakulima kutoa elimu ya kilimo cha zao hilo, ili usije kutokea uhaba za matunda kiwanda kitakapoanza kuzalisha.

  Polepole alisema, kwa kuzingatia kuwa umadhubuti wa viwanda unaendana pia na Kilimo, CCM imefurahi kuona kuwa imejengwa karakana na kuunga matrekta na kwamba hadi sasa inamalizia matrekta 140 ambayo alisema, yatauzwa kwa bei nafuu kwa kuwa yanaunganishwa hapa nchini.

  Alisema, katika awamu ya pili Karakana hiyo ambayo imejengwa kwa ubia kati ya Tanzania na Uholanzi, mitambo itahamishiwa katika eneo la Tamco, Kibaha na badaa ya kuunganisha tu itakuwa ni kiwanda cha kutengenezea hapa nchini matrekta na pia kitakuwa kikiunganisha mabasi aina ya TATA.

  UCHAGUZI NDANI YA CHAMA

  Akizungumzia Uchaguzi ndani ya Chama, Polepole alisema, Chaguzi za Mashina zimeshakamilika nchini kote kwa asilimia 95, huku akiwataka Wanachama wa CCM wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za Jumuia na Kata huku akisisitiza kuwa fomu hizo zinatolewa bure.


  "Wewe ukijisikia kuwa ni Mwanachama ambaye kwa dhati ya moyo wako unakerwa na shida za wananchi, unajiheshimu, ni mnyenyekevu lakini mkali dhidi ya maovu kachukue fomu kuombe ridhaa ya kugombea nafasi unayotaka", alisema Polepole.

  Alisema, fomu katika ngazi za Jumuia na Kata zimeanza kutolewa tangu Juni 20, mwaka huu, na bdo zinaendelea kutolewa hadi mwezi ujao.


  PONGEZI KWA JPM

  Kadhalika, Polepole alisema CCM inaipongeza Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Magufuli kwa Ujenzi wa Bwawa la kufua umeme katika mto Rufiji na kwamba hiyo ni hatua muhimu kwa kuwa inaendana na lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Uchumi wa viwanda kwa sababu umeme ndiyo kichocheo kikubwa cha viwanda.


  Pia CCM imempongeza Rais Dk. John Magufuli kwa Serikali yake kupeleka miswada Bungeni kwa minajili ya kurekebisha sheria kuhusiana na ulinzi wa madini na maliasili za nchi.


  KUTOREJEA MASOMONI BAADA YA KUJIFUNGUA

  Akizungumzia kuhusu kauli aliyotoa hivi karibuni Rais Dk. John Magufuli kutoruhusu Wanafunzi kutorejea katika utaratibu wa kawaida wa masomo shuleni, Polepole alisema, CCM inampongeza Rais kwa kauli hiyo na inamuunga mkono kwa dhati kabisa.


  "Mnajua baada ya Rais kutoa kauli hii, kuna baadhi ya watu wanajaribu kupotosha, ukweli ni kwamba Rais yupo sahihi na sisi CCM tunamuunga mkono. Mnajua utaratibu na ni kwamba mtoto anapopelekwa shuleni anaanza masomo katika mfumo rasmi, sasa anapopata ujauzito na kwenda kujifungua, haiwezekani tena kurejea masomoni katika mfumo huo. Lakini Siyo kwamba mfumo huo ndiyo wa mwisho, akipenda kuendendelea na masomo ipo mifumo mingine nje ya mfumo rasmi ambayo anaweza akasoma", alisema.

  0 0

   Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akizungumza na wakazi wa Ilala Mchikichini wakati alipokuwa akifanya shoo ya uzinduzi wa Karanga zake zinazokwenda kwa jina la Diamond Karanga zitakazouzwa madukani kote katika mfumo wa kisasa.
  Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akitoa Burudani kwa mashabiki wake waliofika katika uzinduzi wa Karanga zake uliofanyika katika Viwanja vya soko la Mchikichini Karume Ilala Jijini Dar es Salaam 
  Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz)  akipongezwa na moja wa mashabiki wake waliofika kumuunga mkono kwa kununu karanga za shilingi 5000 mara baada ya uzindzui wa biashara hiyo. Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz)  akitoa burudani kwa mashabiki wake waliofik akumuunga mkono katika biashara yake ya Karanga
   Mama mzazi wa Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akiwa anakula Karanga za mtoto wake mara baada ya kuzinduliwa Karume jijini Dar es Salaam

   Mashabiki wa Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) wakigawana Karanga mara baada ya kuzinunua mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam
   Mashabiki wa Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) wakigawana Karanga mara baada ya kuzinunua mara baada ya uzinduzi uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam
   Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) ,akiwa amepiga picha ya pozi na mmoja wa wauza Karanga ambaye ameamua kuuza Karanga za Mwanamuziki huyo na kuachana na Karanga za Kawaida
   Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz)  katika picha ya pamoja na wadau wake walionunu Karanga
   Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akimfungulia mfuko wa Karanga  mmoja wa wauza Karanga ambaye ameamua kuuza Karanga za Mwanamuziki huyo na kuachana na Karanga za Kawaida
    Meneja wa Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz), Salaam SK akizungumza  katika Tamasha hilo
    Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akiwa na boksi la Karanga
   Mashabiki wa  Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz)
    Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz) akiwasili katika viwanja vya  soko la Mchikichini
   Mashabiki wa  Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz)
   Mwanamuziki wa Muziki wa Bongo Fleva nchini, Naseeb Abdul (Diamond Platnumz)


  0 0

   Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi kombe Nahodha wa timu ya Kundemba FC,Mohamed Haji Shaibu, baada ya kuibuka mshindi katika  mashindano ya Masauni - Jazeera Cup.Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani.Mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Visiwani Zanzibar. Picha na Abubakari Akida
   Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdulla Juma Saadala, akimkabidhi zawadi ya viatu  mchezaji bora wa mashindano ya Masauni - Jazeerah Cup,Shabani Makuka.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo,Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka mshindi  dhidi ya Kilimani Maghorofani, mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmmoja,Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida
   Mwamuzi Bora wa Mashindano ya Masauni - Jazeera Cup, Ramadhani Khamis Kombo akipokea zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala,b aada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali kati ya timu ya Kundemba FC na Kilimani Maghorofani.Mchezo huo ulifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida
   Nahodha wa timu ya Kundemba FC, Mohamed Haji Shaibu, akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza  wa mashindano ya Masauni-Jazeera Cup  kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt.Abdulla Juma Saadala.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni .Picha na Abubakari Akida
   Nahodha wa timu ya Kundemba FC, Mohamed Haji Shaibu, akipokea zawadi ya mshindi wa kwanza  wa mashindano ya Masauni-Jazeera Cup  kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , Dkt.Abdulla Juma Saadala.Kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera na watatu ni Mbunge wa jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni .Picha na Abubakari Akida
   Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Abdulla Juma Saadala, akizungumza na wananchi (hawapo pichani), waliofika kuangalia mchezo wa fainali wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup.Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani,uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmmoja, Visiwani Zanzibar.Picha na Abubakari Akida
   Mgeni Rasmi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar,Dkt.Abdulla Juma Saadala, akizungumza na vyombo vya habari baada ya  mchezo wa fainali wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup. Wapili kushoto ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Nassor Saleh Jazeera na wanne ni Mbunge wa jimbo hilo Mhandisi Hamad Masauni.Mchezo huo ulimalizika kwa mikwaju ya penati 8-7 iliyopelekea timu ya Kundemba FC  kuibuka bingwa dhidi ya Kilimani Maghorofani katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Visiwani Zanzibar.
  Wachezaji na mashabiki wa timu ya Kundemba FC, wakishangilia kuibuka mabingwa wa mashindano ya Masauni - Jazeera Cup, baada ya kuifunga timu ya Kilimani Maghorofani kwa ushindi wa mikwaju ya penati 8-7.Mchezo huo ulifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar

  0 0


  Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa maarufu kwa jina la Baucha (Kulia) na Mkuu wa huduma za Ezypesa Zantel, Shinuna Kassim (katikati) wakifurahia jambo na mteja wa Zantel katika hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Kampuni hiyo mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.
  Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa maarufu kwa jina la Baucha (Katikati) akipata futari na baadhi ya wateja wa Kampuni hiyo katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni hiyo mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.

  Ofisa Mauzo kwa wateja wakubwa wa Zantel, Salum Ally Said (kushoto) akiwa pamoja na mteja wa Kampuni hiyo wakati wa kupata futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa Zantel mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.
  Wafanyakazi wa Zantel kwa upande wa Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Benoit Janin (hayupo pichani) wakati wa kupata futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa Zantel mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.
  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni hiyo wa upande wa Zanzibar wakati wa kupata futari iliyoandaliwa kwa ajili yao mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.
  Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Khamis Mussa maarufu kwa jina la Baucha akizungumza katika hafla ya kupata futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo mwishoni mwa juma mjini Unguja-Zanzibar.

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee, Dk Khamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tano wa Madaktari uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga Makumbusho jijini Dar es Salaam .
  Sehemu ya madaktari na wanasayansi walioshiriki mkutano huo ambao unajadili masuala mbalimbali ya tiba katika bara la Afrika na hapa nchini 
  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee, Dkt Khamisi Kigwangalla akikagua maonyesho ya Dawa yaliyopo nje ya mkutano huo
  Sehemu ya madaktari na Wanasayansi walioshiriki mkutano huo ambao unajadili masula mbalimbali ya tiba katika bara la afrika na hapa nchini
  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee, Dk Khamisi Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa meza kuu na washirika wa Maendeleo nchini

  0 0


  Meneja wa Tigo Mkoa wa Dodoma Gidion Morris akimpa maelezo Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa alipotembelea banda la kampuni ya simu ya Tigo kwenye maonyesho ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya uwanja wa Nyerere Square mjini Dodoma jana.
  Meneja wa Tigo Mkoa wa Dodoma Gidion Morris akiagana na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa alipotembelea banda la kampuni ya simu ya Tigo kwenye maonyesho ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya uwanja wa Nyerere Square mjini Dodoma jana.

  0 0  0 0


  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtera Mwampamba (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA) Makao Makuu, Rose Majuva kuhusu kazi zinazofanywa na chama hicho ikiwemo kuwapa uwezo wanawake wa kujitambua na kujiamini alipokwenda kuzindua Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wilayani humo.

  Majuva aliwaasa wanawaje kuacha kutumia mikopo ya benki kuchezea ngoma bali waitumie kujiendeleza kibiashara na kuwa na tabia ya kulipa kwa wakati mikopo hiyo. Pia aliwaeleza mbinu mbalimbali za kufanya biashara na miiko yake. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDAKAMANDA WA MATUKIO BLOG.

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kisarawe, Mtera Mwampamba (kulia), akiangalia kiroba cha mkaa uliotengenezwa kiasili kwa kutumia taka mbalimbali alipokuwa akitembelea mabanda ya wajasiriamali kabla ya kuzindua Jukwaa hilo. Kushoto ni Gifti Mbaraka wa banda hilo la Vijana Wasiriamali Wakulima Kisarawe. Katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe, Mussa Gama.

  Wananchi wakisikiiza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa TGGA, Valentina Gonza jijsi ya kutengeneza jiko la kutumia mwanga wa jua kupikia vyakula mbalimbali kwa gharama nafuu wakati wa maonesho yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo mjini Kisarawe.

  Girl Guides wa TGGA, wakitengeneza Green House ya kupanda matunda na mbogamboga majumbani waliposhiriki uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wilayani Kisarawe. Kutoka kushoto ni Rachel Baganyire kutoka Uganda, Michelle kutoka Rwanda na Happy Mshana wa Makao Makuu ya TGGA, Dar es Salaam.
  Kamishna wa Makao Makuu ya TGGA, Rose Majuva (kulia) akisoma maadili ya kiongozi anavyotakiwa awe wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Wilaya ya Kisarawe.
  Mkufunzi wa TGGA, Makao Makuu Dar es Salaam, Ruth Namatanga akigawa karatasi ya kupigia kura kwa Wajasiriamali wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa hilo.
  Mkufunzi wa TGGA, Makao Makuu Dar es Salaam,Rehema Kijazi akigawa karatasi ya kupigia kura kwa Wajasiriamali wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa hilo.
  Mkufunzi wa TGGA, Makao Makuu Dar es Salaam, Valentina Gonza akigawa karatasi ya kupigia kura kwa Wajasiriamali wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa hilo.
  Mkufunzi wa TGGA, Makao Makuu Dar es Salaam, Ruth Namatanga akikusanya kura kwa Wajasiriamali wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Jukwaa hilo.
  Baadhi ya viongozi wa TGGA wakihesabu kura wakati wa uchaguzi huo
  Viongozi wa TGGA wakiwa kwenye banda lao wakati wa maonesho yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa Jukwaa hilo mjini Kisarawe
  Mwampamba akiangalia bidhaa mbalimbali za wajasiriamali
  Girl Guides kutoka Madagascar akijitambulisha wakati wa mkutano wa Jukwaa hilo. Kutoka kulia ni Rachel Baganyire kutoka Uganda na Michelle kutoka Rwanda. Vijana hao wapo nchini kwa miezi sita katika programu ya kubadilishana uozefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na ujasiriamali
  Mkufunzi kutoka Makao Makuu ta TGGA, Happy Mshana akielezea jinsi alivyopata uzoefu alipoiwakilisha TGGA kwenye mafunzo ya kubadilisha uzoefu nchini Madagascar

  0 0

  Mwakilishi kutoka Mtandao wa Kodi Tanzania (TTJC), Grace Masalakulangwa akiwasilisha ripoti ya utafiti ya One Billion Question iliyotafitiwa na shirika la ISCEJIE katika Mkutano uliowakutanisha wadau wa Elimu na Wenyeviti wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara  iliyofanyika jijini  Dar es Salaam. 
  Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Alistidia Kamugisha akifungua mkutano na kuwaelezea malengo ya mkutano huo wa siku mbili kwa wadau wa elimu na Chama cha Walimu Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
   Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET), Cathleen Sekwao akitoa mada kuhusu umuhimu wa ukusanyaji wa rasilimali za ndani na kuwekeza katika kuboresha sekta ya elimu hususani kwa mtoto wa kike na maslahi ya walimu katika mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU).
  Meneja Mradi wa Elimu kutoka shirika la ActionAid Tanzania Ndugu Karoli Kadeghe akiwasilisha changamoto zinazoikabili elimu msingi hapa nchini ikiwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa walimu kwenye mkutano uliowakutanisha wadau wa elimu pamoja baadhi ya viongozi wa Chama cha Walimu ngazi ya mikoa ya Tanzania Bara  iliyofanyika jijini  Dar es Salaam. 
    Baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania wakichangia mada kwenye mkutano uliowakutanisha ili kujadili kodi na ubora wa elimu hapa nchini Tanzania  kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar 

  Shirika la ActionAid-Tanzania, Mtandao wa Elimu Tanzania, Shirika la Maendeleo ya Elimu Singida-MEDO na Mtandao wa Asasi za Kiraia-KINGONET  kwa pamoja wanatekeleza mradi wa uhamasishaji utoaji elimu bora kupitia rasilmali zetu wenyewe ( PROMOTING QUALITY EDUCATION THROUGH PROGRESSIVE DOMESTIC RESOURCE MOBILIZATION) unaotekelezwa huko Kilwa na Singida Vijijini kwa ngazi ya wilaya kwa kufanya kazi na kamati za shule na klabu za haki za watoto shuleni. Kitaifa MRADI Huo unalenga kufanya  utetezi wa mabadiliko ya kisera na sheria  hasa suala la ulipaji kodi, ukusanyaji kodi kwa haki (tax Justice), uzibaji wa mianya ya uvujaji wa kodi  ili makusanyo yaongezeke na yagharimie huduma bora kwa wananchi wa Tanzania hususani kuboresha utoaji wa Elimu bora Nchini.

  Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bi. Cathleen Sekwao akifungua mkutano huo aligusia pia kuhusu “utoaji wa huduma za jamii hapa nchini unakabiliwa na ufinyu wa fedha, wote tu mashahidi kuwa hadi kufikia mwezi Machi, 2017 serikali ilikuwa imetoa asilimia 34 tu ya bajeti yote ya 2016/2017. Jambo hili lina madhara makubwa katika utoaji wa huduma za jamii hasa elimu msingi yenye ubora  hasakwa mtoto wa kike”.
  Aliongelea pia serikali kushindwa kutoa asilimia mia moja ya fedha za kutekeleza bajeti ya 2016/2017 tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza fedha nyingi kupitia misamaha ya kodi.

  Meneja Mradi wa Elimu kutoka shirika la ActionAid Tanzania Ndugu Karoli Kadeghe aliwasilisha changamoto zinazoikabili elimu msingi hapa nchini ikiwa ni pamoja na: Upungufu wa vyumba vya madarasa, Upungufu wa ofisi za walimu, Upungufu wa vyoo vya wanafunzi,Uwiano usiokubalika kitaratibu wa mwalimu na wanafunzi, Shule nyingine kukosa kabisa walimu wa kike.

   Upungufu wa nyumba za walimu, fedha za ruzuku zisizotosheleza, utegemezi wa bajeti ya nchi za nje unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu, mgawanyo wa ruzuku usiozingatia mahitaji halisi ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe, Kuwa na mipango ya kibaguzi-Shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa fedha(payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule, Kukosekana kwa mafunzo kazini kwa walimu, Kutopandishwa madaraja walimu, Kutolipwa kwa wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.

  Mratibu wa Inter Faith Standing Committee Bi. Grace Masalakulangwa aliwasilisha kuhusu Utafiti wa Ripoti ya “1 Billion Question” iliyojikita kubaini upotevu wa kodi katika sekta ya madini au uziduaji katika wilaya za Kilwa, Tarime na Geita. Utafiti huo umebaini serikali inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi.

  Washiriki mbalimbali wakichangia katika mkutano huo, walishauri serikali kuboresha ukusanyaji wa kodi na utengaji wa bajeti katika sekta ya maendeleo hususani sekta ya elimu. Baadhi ya washiriki walichangia pia kukosekana kwa ufanisi na maendeleo yenye tija katika sekta ya Elimu kutokana na usimamizi mbovu wa elimu, serikali kushindwa kuwekeza katika elimu, kuwepo kwa wizara mbili zinazosimamia elimu na muda mwingine kuingiliana kwa majukumu pamoja na kutozingatiwa katika maslahi ya walimu.  

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

  ENEO la njia Panda linalounganisha barabara za Moshi/Arusha,Tanga/Dar es Salaam na ile ya Holili mpakani mwa nchi jirani ya Kenya linatajwa kama kituo kikuu cha Malori yanayosafirisha Nafaka kwenda nchi jirani ya Kenya.
  Uchunguzi uliofanywa na Globu ya Jamii umebaini kuwepo kwa maeneo yasiyo rasmi ya kuegesha Malori hayo ,mengine yakiwa na Matela yake ,ambako shughuli za kupakua mahindi na kupakia katika Magari Madogo aina ya fuso zinazotoka nchi jirani ya Kenya hufanyika.
  Maeneo mengine yanayotajwa kuwepo na Magulio  ya Mahindi ni katika sehemu za maegesho ya magari  zilizopo katika  vituo mbalimbali vya kuuza Mafuta ,pamoja na baadhi ya nyumba za wageni ambazo zimegeuzwa Maghala ya kuhifadhia Mahindi.
  Magari zaidi ya 103 yanashikiiwa katika maeneo ya Njia Panda na Himo yakiwa yamebeba Shehena ya Mahindi tayari kusafirishwa huku baadhi ya madereva wakiyatelekeza Malori yao kwa siku ya tano sasa na kwenda kusiko julikana .
  Hatua iliwasukuma Wafanyabiashara wa Mahindi pamoja na Madereva kufika ofisi za Mkuu wa mkoa kuwasilisha malalamiko yao juu ya kukamatwa kwa Malori hayo yakiwa Njia Panda badala ya mpakani kama alivyo agiza Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.
  Wakizungumza nje ya jingo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa,Wafanyabiashara hao ,Laurance Kanyota,Nuru Madai na Mariam Ramadhan walisema wameshangazwa na hatua ya jeshi la Polisi kushikilia magari yao yalikuwa na Mahindi yakisafirishwa kuelekea mikoa ya Arusha na Moshi.
  “Magari yetu yapo pale Sheli Maount Meru,yalitokea Tunduma kwenda Arusha,yalipofika pale siku ya Jumamosi madereva walienda kula siku kuu ya Idd,jana (Juzi) asubuhi  Matandiboi wakapiga simu kwamba tumezungukwa na Polisi ,tukaenda pale tukaonana na OCD tukaliza kwanini mnatushikia magari ambayo yako Njia Panda yanayoenda Arusha au Moshi ,wakajibu tumetumwa kushika magari yote ya Mahindi.”alisema Mfanyabiashara Mariam.
  Alisema alimuelewa Waziri Mkuu katika agizo lake kwamba magari yaliyopo mpakani ndio yashikiliwe  na si kama lilivyofanya jeshi la Polisi kukamata magari yaliyokuwa Njia Panda kuelekea Moshi na Arusha huku wakimuomba Waziri Mkuu kutoa ufafanuzi  kwa wasaidizi wake juu ya agizo lake.
  Mfanyabiashara Kanyota alisema amekuwa akifanya biashara ya kusafirisha mazao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na ulipaji wa kodi lakini anashangazwa na hatua ya kuzuiliwa kwa  Mahindi yake ambayo amekuwa akinunua na kuyauza katika viwanda vya kutengeneza unga kwa ajili ya Chakula.
  “Tulikua tunaomba Mkuu wa mkoa ajue kwamba sisi ni wafanyabiashara tunaolipa kodi halali ya serikali atusaidie tufikishe mazao yetu sehemu yanapotakiwa kufika ,Mahindi yangu yanatoka Mbeya ,mkulima aiyeniletea mimi kama Dalali ametoka Tunduma.”alisema Kanyota.
  Kauli ya Serikali ya mkoa wa Kilimanjaro.
  Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Kilimanjaro imepigiria msumari katika Agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kutaifisha Mahindi pamoja na gari litakalokutwa kuanzia June 26 mwka huu likiwa limebeba na kusafirisha Mahindi kwenda nje  ya nchi.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa alisema jana ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari kuwa magari 103 yaliyokamatwa Himo na Njia Panda yatahesabiwa kama sehemu ya uhujumu uchumi na kwamba yatataifishwa .
  “Magari yaliyokamatwa kule Siha ,tayari tulikwisha amua kwamba yatapelekwa Nationa Milling(Ghala la chakula la taifa)  Arusha ,lakini haya ya Himo ,Waziri Mkuu Alisha agiza kwamba kuanzia tarehe 26 ,magari yote yatakayokamatwa ,Bidhaa pamoja na magari yenyewe yatahesabiwa kuwa ni sehemu ya uhujumu Uchumi ,kwa hiyo yatataifishwa.”alisema Mghwira.
  Mghwira alisema baada ya mfululizo wa vikao vya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro juu swala zima la uuzaji na usafirishaji wa chakula nje ya nchi,kamati imefanyia kazi tamko la Waziri Mkuu kutaka kujiridhisha vya kutosha juu ya hali ya chakula iliyopo Kilimanjaro na mikoa ya jirani.
  “Uogozi wa mkoa wa Kilimanjaro unapenda kuwatangazia wananchi wote,hususani Wafanyabiashara wa Sukari na Nafaka za Mpunga,Mchele ,Mahindi na Unga wa Mahindi ya kuwa ni marufuku kwa mfanyabiashara yoyote au mwananchi yoyote kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi bila kibali cha serikali”alisema Mkuu huyo wa Mkoa .
  Alisema kukiuka agizo hilo ni kuhujumu uchumi wa nchi  kama ilivyo ainishwa kwenye kifungu cha 3 cha jedwali la kwanza la sheria ya uhujumu Uchumi sura ya 200 ya sheria za Tanzania na pia ni kukiuka agizo la Waziri Mkuu,kupitia waraka wake alioutoa  Mei 30,2017,uliozuia utokaji  wa vyakula na sukari kwenda nchi jirani .
  Alisema kwa kukiuka sheria hiyo kunaweza kusababisha upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo nchini na kusababisha Mamlaka ya Mapato hapa nchini (TRA)  kukosa takwimu muhimu wa bidhaa zinazosafirishwa nje
  “Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro imejiridhisha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari  na nafaka hizo nyakati za usiku na hiki ndicho kinaleteleza kukosa takwimu muhimu kwa kupitia njia ambazo si rasmi kwa kushirikiana na baadhi ya askari polisi ambao sio waaminifu.
  Wakati wa baraza la Idd lilifanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha mjini Moshi,Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa alitangaza kupiga marufuku usafirishaji wa Mahindi kwenda nchi jirani na kwamba atakaye kiuka utaratibu huo atahukuliwa hatua kali za kisheria.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akiwa ameongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo Kamanda wa Polisi ,Hamis Issah na Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba wakitembelea maeneo ambayo yameshikiliwa magari yaliyobeba shehena ya Mahindi .
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizunbgumza na baadhi ya wafanyabaishara wa Mahindi ambao magari yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro.
  Baadhi ya Wafanyabiashara ambao Mahindi yao yanashikiliwa katika eneo la Njia Panda mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipofika eneo hilo kwa lengo la kuzungumza nao.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiangalia magari yaliyobeba shehena ya Mahindi yanayoshikiliwa katika eneo la Njia Panda ya Himo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akizungumza na baadhi ya madereva na Wafanyabaisahara ambao Mahindi yao yanashikiliwa eneo la Njia Panda ya Himo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akitizama Malori yenye Shehena ya Mahindi yakiwa yamehifadhiwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyuma ya vituo vya Mafuta .
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akiongozana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issa wakiodoka katika eneo hilo baada ya kuangalia malori yanayoshikiliwa yakiwa na shehena ya Mahindi.
  Baadhi ya Magari yakiwa yameegeshwa katika maeneo tofauti tofauti yakiwa na shehena ya Mahindi.


  0 0


  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Mh Charles Mwijage (kushoto), akizungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Mh. Almas Maige (kulia), huku Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka akisikiliza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana.
  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akilakiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Almas Maige (kushoto), na Mratibu wa Mradi wa Mwanamke wa Wakati Ujao, Lilian Machera (kulia) alipokuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho, Dar es Salaam jana.
  Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Mama Jayne Nyimbo (wa pili kushoto), akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo wakati wa Mkutano Mkuuu wa Mwaka wa chama hicho jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka, aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Mhe. Almas Maige na Makamu Mwenyekiti mpya, Felix Kagisa.
  Mkurugenzi​Mtendaji ​ wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk. Aggrey Mlimuka (kushoto), akiwa na baadhi ya maofisa wa chama hicho wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea.
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
  Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage ambaye alisema serikali itaendela kujenga mazingira mazuri ya utoaji vibali vya uwekezaji ili kuweza kufikia ajenda yake ya kuimarisha uchumi wa viwanda.
  Aliyekuwa Mwenyekiti Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Mhe. Almas Maige akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika pamoja na mkutano kujadili masuala mbali mbali kuhusu ajira na uwekezaji.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga amewataka wanawake wa Wilaya hiyo kuachana na masuala ya utegemezi kwa wanaume na zaidi wajikite katika kujiendeleza kiuchumi kwa kuanzisha miradi midogo midogo ikiwemo kuanzisha vikundi vya ujasiriamali  ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi..

  Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuvikutanisha zaidi ya vikundi 30 kutoka Wilaya ya Mkuranga na kuelezea matatizo wanayokumbana katika vikundi vyao.

  Sanga amewaambia kuwa wanawake bila kuwezeshwa wanaweza wakajiendeleza wenyewe kwani utakapomuelimisha mwanamk mmoja utakuwa umeelimisha watu wnegi sana.

  "wanawake mkijiwezesha wenyewe mnaweza sio lazima muwezeshwe kwani tunachoamini ni kuwa ukimuelimisha mwanamke umeelimisha dunia kwani nyinyi ndiyo msingi mkubwa wa familia katika jamii zinazotuzunguka mtakapoamua kukaa na kutokujishughulisha basi hakutakuwa na msingi mzuri wa kizazi kijacho,"amesem Sanga.

  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji  WanawakeWilaya ya Mkuranga Mariam Ulega alisema kuwa anashukuru sana kwa Mkuu wa Wilaya kuja kuwazindulia jukwaa lao na cha zaidi kwa kuwa wameshapatikana viongozi wa Jukwaa hilo kwa wilaya ya Mkuranga na zaidi anaomba umoja na ushirikiano kutoka kwa wakina mama kutoka kata mbalimbali ili kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

  Kabla ya kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ulifanyika uchaguzi na kupatikana kwa Mwenyekiti Mariam Ulega. 
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akizindua Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega akizungumza na wakina mama wa wilaya hiyo kutoka kata mbalimbali kuhusiana na kuviendeleza vikundi vyao kwa ajili ya kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akipokea maandamano ya wakina mama wa Mkuranga wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
   Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga  akisaini kitabu cha wageni wakati alivyowasili katika uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.
    Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filbert Sanga akioneshwa baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na wakina mama hao wa Wilaya ya Mkuranga kutoka katika Vikundi mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wanawake lililofanyika jana na kuwasihi wanawake kuachana na masuala ya utegemezi zaidi wanatakiwa kujiendeleza ili kujiinua kiuchumi na pia kuviendeleza vikundi vyao na kuvisajili ikiwa ni katika kutekeleza maagizo ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kila Wilaya kuwa na vikundi vya kujiinua kiuchumi.

  0 0

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

  Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji  katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.

  Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

  Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu  na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.

  “Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.

  Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.

  Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro.
  12
  MKUU WA OPERESHENI ZA POLISI, NAIBU KAMISHNA DCP LIBERATUS SABAS, AKIONYESHA BUNDUKI AINA YA SMG ZILIZOPATIKANA JUZI USIKU WAKATI WA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI  BAINA YA WAHALIFU NA POLISI KATIKA KIJIJI CHA PAGAE WILAYANI KIBITI MKOANI PWANI. BUNDUKI 2 AINA YA SMG ZILIPATIKANA PAMOJA NA MAGAZINI 2 NA RISASI 17. PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.
  ……………………..

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wanne kutoka (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga wanne kutoka (kulia)pamoja na vingozi wengine wa Tanzania na Norway mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwatazama Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Borge Brende wakati akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Mbeya.
  WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 18, Linda Mhewa, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji University (TEKU), kilichopo jijini Mbeya.
  Mshindi wa droo ya 18 ya Biko, Linda Mhewa, akiwa anazishangaa fedha zake kiasi cha Sh Milioni 20 alizokabidhiwa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo ya Biko Tanzania, leo jijini Mbeya.

  Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul William Ntinika mwenye suti, akimpongeza mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Linda Mhewa, aliyeibuka kidedea katika droo ya 18 iliyochezeshwa Jumatano iliyopita. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mbeya. Kushoto aliyeshika kipaza sauti ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Kulia ni Afisa wa Benki ya NMB, jijini Mbeya. Picha na Mpigapicha wetu Mbeya.

  Mwanafunzi huyo ambaye ni msichana wa pili kufanikiwa kuzoa mamilioni ya Biko kupitia bahati nasibu ya Biko, aling’ara katika droo ya Jumatano iliyopita, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kumwaga mamilioni kwa kupitia mchezo wao unaotoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau droo kubwa ya Jumatano na Jumapili ya Sh Milioni 20.
  Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven kushoto, akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wao Linda Mhewa wa pili kutoka kushoto.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mhewa aliyetangazwa kuwa mshindi wa donge nono la Milioni 20, alisema kwamba ni furaha yake kuona Mungu amemchagua katika bahati nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini tangu kuanzishwa kwake.

  Alisema amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku akiamini kuwa kushinda kwake ni sehemu ya kubadilisha maisha yake kiuchumi jambo ambalo ndilo alilokusudia kiasi cha kuamua kucheza Biko.

  “Wakati napigiwa simu na Kajala sijaamini kabisa, nikaamini baada ya kuona ni kweli hususan baada ya kukabidhiwa fedha zangu ikiwa ni matokeo ya kucheza kwangu Biko, huku ukiwa mchezo rahisi kwa sababu kwa kutumia simu za mikononi za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456, huku kianzio cha kucheza kikianzia Sh 1,000 na kuendelea,” Alisema Mhewa.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alimpongeza mshindi wao wa jijini Mbeya, huku akimtaka ahakikishe kuwa uchumi wake unakua kwa kuhakikisha kwamba anazitumia vyema fedha alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu yao.

  “Ni jambo zuri kuinuka kiuchumi kwa kupitia mchezo huu wa kubahatisha wa Biko, ambapo tumeshuhudia mamia ya Watanzania wakiibuka kidedea katika droo za wiki pamoja na ushindi wa papo kwa hapo unaotoka kila dakika,” Alisema.

  Kwa mwezi Mei pekee, zaidi ya Sh Milioni 500 zimetolewa kwa washindi, huku donge nono la Sh Milioni 20 likienda kwa washindi wawili kwa droo ya Jumatano na Jumapili.

older | 1 | .... | 1287 | 1288 | (Page 1289) | 1290 | 1291 | .... | 1897 | newer