Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

CUF KUIFIKISHA KORTINI WAKALA WA USAJILI, UFILISI NA UDHAMINI (RITA)

$
0
0

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi(CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu madai ya muendelezo wa hujuma dhidi ya chama hicho zinazofanywa na ofisi ya msaji wa vyama vya siasa nchini. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Seveline Mwijage.
 Maofisa wa Chama hicho wakiwa meza kuu wakati wa mkutano na wanahabari.
 Wabunge wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Wananchi (CUF), kinatarajia kumfikisha mahakamani  Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) 
 kwa kukiuka taratibu za sheria ya wadhamini kwa kutojiridhisha juu ya uhalali wa majina ya Bodi ya Wadhamini yaliyofikishwa kwake kama yalipitishwa na kikao halali cha chama kwa mujibu wa katiba.

Kauli hiyo ameitoa Katibu  Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seifjijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema wanachukua hautua hiyo kutokana RITA kushindwa kutumia mwongozo na weledi katika kutekeleza majukumu yao na badala yake wamesukumwa na utashi binafsi kwa ajili ya hujuma dhidi ya chama hicho.

“Chama chetu kimepatwa na mshituko mkubwa sana, kuona taasisi kubwa nan yeti yenye dhamana kubwa katika nchi inaweza kufanya vitendo vya ovyo. RITA ni taasisi inayobeba maisha ya watu ya kila siku. Licha ya kusajili Bodi za Wadhamini, inasajili vizazi na vifo, ndoa, talaka na inatunza wosia kwa ajili ya mirathi,” alisema Maalim.

Alisema michakato wa kufungua kesi hiyo inaanza leo ambapo alieleza kuwa tayari wamekwisha agiza mwawakili kulishughulikia. Kutokana na matarajio ya ufunguzi wa kesi hiyo watawasilisha maombi mbele ya Mahakama Kuu kuitaka isimamishe kesi nyingine zote walizofungua kuhusiana na kadhia hiyo hadi hapo shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya RITA  litakapoamuliwa.

Maalim alisema kusajiliwa kwa bodi hiyo ambayo aliiita kuwa ni bodi feki, alieleza kwamba ni mwendelezo wa kukihujumu na kukidhoofisha chama kunakofanywa dola kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa pamoja na Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake.

Alitaja mambo manne ambayo yalikuwa msukumo wa kusajiliwa kwa bodi hiyo. Alisema kuwa ni kwa ajili ya kufuta kesi zote zilizofunguliwa na ambazo zinawaelemea licha ya kutumia nguvu kubwa ya dola, kufungua akaunti mpya ya benki ili kumwezesha Profesa Lipumba kupata ruzuku.

Aliongeza mengine kuwa ni Bodi hiyo kuwezesha udhibiti wa Ofisi za Makao Makuu, Zanzibar pamoaja na kumwondoa madarakani Katibu Mkuu Maalim Seif Hamad na hivyo kufanikisha njama za kuwapokonya haki Wazanzibar kwa maamuzi yao ya Oktoba 25 mwaka 2015.

Hamadi alisema kamwe  haki ya Wazanzibar haitapotea na kuahidi kuwa ndani ya miezi mitatu haki hiyo itakuwa imepatikana.


RAIS DKT MAGUFURI AKUTANA NA WATAALAMU WA NISHATI KUTOKA ETHIOPIA NA TANZANIA, KAMATI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI (MAKINIKIA)

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele anayaongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017

 Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi (kulia) akiongea na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Ing Seleshi Bekele anayaongoza ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge kabla ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele na ujumbe kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  pamoja na jopo la wataalamu wa Tanzania wanaosimamia mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono  na Waziri wa Maji, Umwagiliaji na Umeme wa Ethiopia Dkt. Seleshi Bekele baada ya kupata picha ya pamoja na ujumbe wake kutoka kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo iliyopo nchini kusaidia mchakato wa ujenzi wa Dam (bwawa la kuzalisha umeme)  la Steigler’s Gorge  pamoja na jopo la wataalamu wa Tanzania wanaosimamia mradi huo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 28, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wajumbe wa Kamati mbili alizoziteua za Uchunguzi wa Mchanga wa  Madini (Makinikia) Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2017.PICHA NA IKULU




TGGA YAKABIDHI VYETI KWA WALIOHITIMU MAFUNZO YA MWANAMKE KUJIAMINI, KUJITAMBUA NA KUWA JASIRI

$
0
0
 Viongozi na walimu wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wakishangilia baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujiamini, kujitambua na ujasiri katika kambi iliyofanyika hivi karibuni  eneo la Mombasa, Dar es Salaam. Zaidi ya 36 kutoka mikoa mbalimbali walishiriki kwenye mafunzo hayo. Pia katika mafunmzo hayo yaliyofanyika kwa wiki moja yalihudhuriwa na viongozi kutoka nchi za Uganda, Rwanda na Madagascar

Mgeni rasmi katika hafla ya kufungakambi hiyo yalifanywa na Katibu Mkuu wa TGGA Tanzania, Grace Shaba, ambaye aliwaasa kuyatumia vizuri mafunzo hayo kwenda kuanzisha kambi za kuwafundisha wanachama mikoani wanakotoka. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wakiruka kwa furaha
 Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba akimkabidhi cheti mmoja wa walimu waliohitimu mafunzo hayo.
 Grace Shaba akimkabidhi m cheti mmoja wa wahitimu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Jestina Philip
 Grace Shaba akimkabidhi cheti Makamu Mwenyekiti wa TGGA Mkoa wa  Lindi, Sharifa
 Grace Shaba akimkabidhi cheti Happy wa Makao Makuu ya TGGA Dar es Salaam

 Mwalimu wa Girl Guides , Valentina akikabidhiwa cheti
 Kiongozi wa Girl Guides wa TGGA, Makao Makuu, Rehema Kijazi akipokea cheti kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Grace Shsba. Katikati ni Kamishna Rose.
 Michelle kutoka Rwanda akifurahi baada ya kukabidhiwa cheti
 Kiongozi wa Girl Guides kutoka Madagascar akipokea cheti
 Katibu wa TGGA Mkoa wa Lindi, akipokea cheti
 Kiongozi kutoka Tanga, akipokea cheti
 Twarhiya Hussein kutoka Lindi  mtoto pekee aliyehitimu mafunzo hayo na kufanya vizuri, akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba.

 Rachel Baganyila kutoka Uganda akifurahi kupokea cheti
 Ni wakati wa kucheza ngoma

KANALI LUBINGA AFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA CCM TAWI LA UINGEREZA (UK), LEO

$
0
0





Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimkaribisha Ofisini kwake, Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza (UK), Kangoma Kapinga, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mwenyekiti huyo ambaye alifuatana na Katibu wa CCM wa tawi hilo Leybab Mdegela alifanya mazungumzo na Kanali Lubinga ikiwemo haja ya kuimarishwa matawi ya CCM yaliyopo nchi za nje.
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwa Kanali Ngemela (katikati), kabla ya mazungumzo yao kuanza. Kushoto ni Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Leybab Mdegela.
Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Lebab Mdegela akisaini Kitabu cha wageni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga na Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Katibu wa CCM Tawi la Uingereza Lebab Mdegela akisaini Kitabu cha wageni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga na Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akifafanua jambo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Uingereza Kangoma Kapinga (kulia), katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Katibu wa CCM wa tawi hilo Laybab Mdegela. PICHA: BASHIR NKOROMO-CCM Blog.

KAULI YA MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN KWA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHTAKA NCHINI

VIJUSO VYA MAGAZETI YA ALHAMIS LEO JUNE 29,2017

VIONGOZI WA MAJI MAJI WATUHUMIWA KUCHOTA PESA ZA CLUB

$
0
0
Baadhi ya wanachama wa majimaji wameutuhumu uongozi uliopo madarakani kwa ubadhilifu wa mali za clabu hiyo na ndio chanzo cha kuchelewesha uchaguzi wa viongozi wapya.

RAIS DKT.MAGUFULI APANIA KUJENGA BWAWA KUBWA LA KUZALISHA UMEME STEIGLER'S GORGE


KAMTI HURU YA UCHAGUZI YA TIMU YA MAJIMAJI YA TANGAZA RATIBA YA KUCHUKUA FOMU

$
0
0
Hatimaye kamati ya huru ya uchaguzi ya klabu ya MAJIMAJI imejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kutangaza tarehe rasimi ya uchaguzi huo baada ya wanachama kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi, ambapo nafasi zinazowania ni mwenyekiti wa klabu,makamu mwnyekiti wa klabu na mjumbe wa bodi .

IGP SIRRO AWAFARIJI WAFIWA KIBITI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua nyumba iliyochomwa moto na wahalifu waliofanya mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji  hayo. picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.
 Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la polisi.
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya mwenyekiti wa kitongoji na afisa mtendaji wa kijiji hicho. IGP Sirro alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kijijini hapo kutowafumbia macho wahalifu wanaotenda mauaji hayo na kuwataka kuwa na kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu hao.  picha na hassan mndeme-jeshi la polisi.
 Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa rambirambi ya msiba kwa wananchi wa kijiji cha mangwi, kata ya mchukwi wilayani kibiti jana alipokwenda kuwapa pole baada ya kutokea mauaji ya Mwenyekiti wa kitongoji na Afisa Mtendaji wa kijiji hicho. picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.


SPIKA WA BUNGE AONGOZA KIKAO CHA UONGOZI YA BUNGE

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokutana jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokutana jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama.
 Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge wakiwa tayari kwa ajili ya kuanza kwa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kilichokutana jana usiku katika Ofisi za Bunge Mjini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Jenista Mhagama.

MAKALA YA MATUMIZI ENDELEVU YA ARDHI YATAEPUSHA JANGWA NA UKAME NCHINI

$
0
0
Jovina Bujulu-MAELEZO.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 193 zilizosaini mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kupambana na kuenea hali ya jangwa duniani (UNCCD). Mkataba huu unalenga kupambana na tatizo la uharibifu wa ardhi katika maeneo yenye ukame na kufanya juhudi za kuyahifadhi.

Mkataba huu ni muhimu kwa nchi yetu ambayo uchumi wake unategemea ardhi kwa ajili ya kilimo ambacho kinachochea maendeleo na ajira kwa wananchi walio wengi.

Hivi karibuni dunia iliadhimisha siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame ambayo ilikiongozwa na kauli mbiu isemayo “Ardhi ni makazi yetu tuitunze kwa manufaa ya baadaye”. Kauli mbiu hii inahamasisha jamii kutunza ardhi kwa kuwa ndiyo makazi yetu.

Akiongea hivi karibuni mjini Dodoma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alisema kuwa kauli mbiu hii inahimiza jamii kuongeza juhudi za kutunza ardhi, na kuzingatia maendeleo endelevu ya rasilimali tulizo nazo kwa ajili ya maendeleo ya sasa na kwa vizazi vijavyo.

Madhumuni ya kuadhimisha siku hii ni pamoja na kuongeza uelewa miongoni mwa jamii na kujua athari za jangwa na ukame katika maisha ya kila siku ya binadamu na jinsi ya kuthibiti hali hiyo.

“Malengo hayo yanadhihirisha umuhimu wa utunzaji wa ardhi na udongo kwa matumizi endelevu hasa kwa ajili ya kilimo, mifugo, na huduma nyingine kama utalii wa wanyama pori na uwindaji.” Aliongeza Mhe. Makamba.

Umuhimu wa kutunza ardhi pia unaonekana katika kuhifadhi vyanzo vya maji na miti ili kuwezesha shughuli za uzalishaji mali na uwekezaji katika viwanda ili kuleta ustawi wa jamii.

Hali ya uharibifu wa ardhi na vyanzo vya maji imeongezeka kwa kasi na kuongeza ukame, upungufu wa mazao ya kilimo na kuongeza umaskini miongoni mwa jamii.

Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 61 ya eneo la nchi yetu liko hatarini kugeuka jangwa. Hali hii ni tishio kubwa kwa maendeleo ya nchi kwani uwepo wa jangwa ni kikwazo kikubwa kinachosababisha kushuka kwa uchumi, hasa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa kwa kiasi kikubwa na hatari ya kuenea kwa jangwa na ukame. Waziri Makamba aliitaja mikoa mbayo iko katika hatari kubwa ya kugeuka jangwa kuwa ni pamoja na Singida, Dodoma, Shinyanga, Geita, Simiyu, Manyara na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Arusha.

Madhara ambayo yameanza kuonekana ni pamoja na kukauka kwa vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali, vifo vya mifugo na wanyama pori, upungufu wa mvua kutokana na kukata miti holela, kupungua kwa maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo.

Aidha, jangwa na ukame vinasababisha tabaka la juu la ardhi kuwa wazi na hivyo kusababisha mmomonyoko wa udongo, hali ambayo inapunguza rutuba na hivyo kupunguza uzalishaji wa mazao kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na kuwepo kwa hatari ya kuwepo kwa jangwa na ukame, Serikali ya Awamu ya Tano inafanya jitihada kubwa za kukabiliana na janga hilo kwa kusimamia Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2016/2017 hadi 2020/2021 ili kusimamia maliasili, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Malengo ya mpango huu ni pamoja na kuhakikisha kuwa mchango wa pato la taifa unaotokana na matumizi endelevu ya misitu, maji, na rasilimali za bahari linafikia asilimia 10, ongezeko la eneo la misitu kwa hekta 130,000, upandaji wa miti 100,000,000 kwa nchi nzima ifikapo 2020.

Hatua za kimkakati za mpango huo ni pamoja na kulinda, kurejesha na kuhamasisha matumizi endelevu ya mifumo ya mazingira ya nchi kavu na misitu ili kukabiliana na jangwa na shughuli zinazosababisha jangwa.

Mikakati mingine pamoja na kutekeleza Mpango Kazi wa Kitaifa wa kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa mwaka 2014 hadi 2018 ambao unahusisha programu za upandaji miti, kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi, kulima kilimo kinachofuata njia za kisasa, ufugaji bora na wa kisasa na kuanzisha maeneo ya hifadhi na kulinda yaliyopo.

Kwa upande wa ushiriki wa wananchi katika kukabiliana na hali hii, mkakati huu utatekelezwa kila kijiji, kitongoji, mtaa, kaya, na taasisi, na utamshirikisha kila mwananchi.

Lengo ni kuhakikisha nchi yetu inakuwa ya kijani ikiwa ni pamoja na kurekebisha changamoto zilizojitokeza katika mikakati na kampeni zilizopita, pamoja na motisha na ushiriki wa sekta binafsi. Mkakati huu umeanza kutekelezwa katika baadhi ya maeneo.

Serikali pia imeweka mkakati wa kutoa elimu kwa wananchi kwa kuwaelekeza shughuli nyingine za uzalishaji mali ili waepuke utegemezi wa maliasili ya misitu ambapo programu ya upandaji miti ya mwaka 2016 hadi 2021 inalenga kupanda miti zaidi ya milioni 280 kila mwaka hasa katika maeneo yaliyo katika hatari zaidi ya kugeuka jangwa.

Mikakati yote hii itafanikiwa endapo kila mwananchi atakuwa sehemu ya kupunguza kuenea kwa tatizo hilo kwa kuzingatia matumizi endelevu ya ardhi.

Matumizi hayo ni pamoja na kupanda na kutunza miti ambako kutasaidia ulinganifu katika shughuli za kilimo, ufugaji, misitu, uhifadhi wa vyanzo vya maji na kuhakikisha mifumo ya ikolijia inategemeana na haiingiliwi.

Ni wakati sasa muafaka kwa wananchi kuunga mkono wito wa Mhe. Makamba kushiriki kikamilifu katika kutekeleza kauli mbiu ya mwaka 2017 ya siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame ili kutunza ardhi kwa vizazi vijavyo.

ZIARA YA MWANAMUZIKI FERRE GOLA, CHRISTIAN BELLA SHULE YA UHURU MCHANGANYIKO

$
0
0
 Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Ltd, Teddy Mapunda (kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru mchanganyiko, Anna Mshana, kwa pamoja wakipaka rangi katika ukuta wa chumba cha darasa la Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakati walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kujionea mazingira ya shule hiyo, baada ya kuomba kusaidiwa mahitaji hayo, ambapo msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
 Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola, (kushoto) na Christian Bella,  kwa pamoja wakipaka rangi katika ukuta wa chumba cha darasa la Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, wakati walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kujionea mazingira ya shule hiyo, baada ya kuomba kusaidiwa mahitaji hayo, ambapo msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
 Mwanamuzki wa Kimataifa kutoka nchini Congo, Ferre Gola (kulia) akisaini katika moja ya picha ya kujifunzia iliyobandikwa kwenye Chumba ca darasa katika Shule ya Uhuru Mchanganyiko, baada ya kumaliza kupaka rangi katika chumba hicho, walipofika kukabidhi ndoo za rangi ikiwa ni msaada uliotokana na mauzo ya Meza za onyesho maalumu la mwanamuzki huyo. Kushoto ni Mwanamuziki Christiani Bella. 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Ltd, Teddy Mapunda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika SHule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Anna Mshana, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika Shule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwanamuziki Christian Bella, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mwanamuziki wa kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola (wa pili kulia) na Christian Bella (kulia) walipofika Shule ya Uhuru Mchanganyiko kwa ajili ya kukabidhi na kupaka rangi katika baadhi ya vyumba vya madarasa ya shule hiyo. msaada huo umetokana na mauzo ya meza za Onyesho maalumu la mwanamuziki huyo linalofanyika leo Alhamisi kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Wakitembelea maeneo ya shule hiyo.....
 Ferre Gola, akisaini katika kitabu cha wageni
Christiani Bella, akisaini katika kitabu cha wageni....

Mawakili wapya 248 kutoka vyuo mbali mbali waapishwa leo

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma amewaasa mawakili kutokuwa mawakala wa kupeleka rushwa mahakamani badala yake wawe mawakala wa kutenda haki na kufuata maadili ya sheria.

Aidha, amewaasa mawakili hao wasome zaidi sheria za nje ya Tanzania ili pindi wanapotayarisha mikataba iwe mizuri kwa kuwa mikataba mingi inayoingiwa haitegemei sheria ya hapa nchini pekee.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawakili 248 kutoka vyuo mbalimbali nchini, ambao wameingizwa katika orodha ya mawakili waliopo Tanzania.

Profesa Juma amesema Tanzania inaingia mikataba mingi ambayo haitegemei sheria zilizopo nchini, hivyo wanapaswa kusoma zaidi ili wanapoandaa mikataba hiyo iwe kwa maslahi ya taifa.Ameongeza kuwa, wananchi wengi wamekuwa wakitoa maoni yao kwamba kuna tatizo la rushwa mahakamani ambalo halipaswi kufumbiwa macho.

Amesema ni vema mawakili wakafuata sheria na kuwa na maadili ya kufanya kazi kwa weredi na na siyo kupeleka rushwa mahakamani.

Aidha amewaambia mawakili hao kuwa, karne ya hii ya sasa inawataka mawakili kutumia ujuzi wao wa sheria sio kutafsiri na kuelewa sheria za Tanzania pekee bali na za Kimataifa pamoja na kupambana na changamoto zinazoikabili nchi.

Profesa Juma amesema mapambano yao yanatakiwa kulenga kuondoa umasikini kwa kuwa wanasheria wa wanyonge na kuisaidia nchi kufikia malengo yanayotakiwa.

Pia amewaasa mawakili hao kuangalia gharama walizotumia wazazi wao hadi walipokubaliwa ili wawasaidie na kuisaidia serikali kutoka ilipo.

Hata hivyo, aliwatoa hofu mawakili hao kwamba Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), hakiwezi kufutwa kwa kuwa imependekezwa kuwepo kwa mabadiliko ya sheria ambayo hayalengi mtu wala taasisi binafsi bali inaangalia sheria kwa upana wake.

Alisema wanataka kuangalia mawakili wenye viwango, vyuo vinavyotoa sheria vinakidhi viwango hivyo hawapaswi kuwa na hofu.

"Tunatarajia vijana hawa wadogo walioapishwa leo wataweza kulitumikia taifa kwa zaidi ya miaka 30, katika umri wa kustaafu wa miaka hivyo tunategemea matokeo chanya kutoka kwao," ameeleza Kaimu Jaji.

Naye, Rais wa TLS, Tundu Lissu amesema mawakili hao ni wasaidizi wa mahakama katika kutenda haki na kwamba wanatakiwa kuielekeza jamii njia ya utawala wa sheria, haki za binadamu na demokrasia.

"Idadi ya mawakili Tanzania ni ya pili katika Afrika Mashariki ikiongozwa na Kenya na mwisho Uganda. Kuapishwa kwa mawakili hawa ni jambo jema ambalo Tanzania inajipanua katika utoaji wa huduma," alisema Lissu.
Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akifuatilia jambo wakati wa sherehe za 56 za kuwakubali na kuwasajiri, Mawakili wapya 248 mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya ndugu wa Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa kwa ndugu zao mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Mawakili wapya wakisubiri zoezi la kuapishwa mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (wanne toka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji na Mawakili wapya mara baada ya kuwaapisha mapema hii leo katika viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa -Maelezo

TAA Yajivunia Kujenga Shule ya Mafumbo Bukoba

$
0
0
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imejivunia kujenga shule ya kisasa ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba Mjini ili iwe mbadala wa shule ya Tumaini iliyopo eneo la karibu na uzio wa Kiwanja cha ndege.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi amesema shule hiyo inamajengo tisa yenye madarasa 24 kati ya hayo 21 ni ya watoto wasio na mahitaji maalum na matatu ni ya watoto wenye mahitaji maalum; zipo ofisi za walimu, vyoo vya shule na vya walimu, na nyumba ya kukaa mwalimu mmoja.

“Ninaona fahari kubwa na nimefarijika sana kuona shule imekamilika kwa kiwango kikubwa na sasa watoto wetu watasoma katika mazingira ya ya utulivu na amani tofauti na awali katika shule ya Tumaini kulikuwa na kelele za ndege kila zinapotua na zinaporuka,” amesema bw. Msangi.

Pia Bw. Msangi amesema shule ya zamani ilikuwa katika maeneo hatarishi ya karibu na barabara ya kutua na kuruka kwa ndege, jambo ambalo lingeweza kuleta maafa makubwa endapo kungetokea ajali maeneo hayo.

Naye mkandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya ujenzi ya CMG ya Mwanza, Mhandisi Jumanne Warema amesema pia madarasa hayo yatawekewa madawadi 315, meza na viti 16 za walimu na madarasa ya watoto wenye mahitaji yatawekwa viti maalumu 48.

Mkuu wa shule ya Tumaini, Bw. Theophil Ndyakowa ameishukuru TAA kwa msaada huo mkubwa walioutoa kwa ujenzi wa shule ya kisasa, ambapo sasa wanafunzi watasoma kwa bidii zaidi.

Hata hivyo mradi huo wa shule umedhaminiwa na Benki ya Dunia, ambapo pia wamefanikisha ujenzi wa jengo la kisasa la abiria, jengo la kuhifadhi umeme na kukarabati barabara ya kutua na kuruka kwa ndege.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (watatu kushoto) akiwafafanulia jambo wahandisi Diana Munubi na Mbila Mdemu (kushoto) huku Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (mwenye suti nyeusi) akisikiliza mara baada ya kukagua shule mpya ya msingi ya kisasa ya Tumaini iliyopo Bukoba.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa shule ya kisasa ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba Mjini.
Wanafunzi waliohamishiwa kutoka katika shule ya msingi Tumaini iliyokuwa maeneo ya karibu na kiwanja cha ndege cha Bukoba, sasa wakiwa mapumziko kwenye shule mpya iliyojengwa maeneo ya Mafumbo kwa usimamizi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), wakiwa nje ya madarasa ya shule mpya ya kisasa ya msingi ya Tumaini baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), Prof. Ninatubu Lema (aliyevaa fulana nyeupe mbele), na wajumbe wengine wakimsikiliza mmoja wa walimu wa shule hiyo wakiwa ndani ya ofisi ya walimu wa shule hiyo.
Shule ya zamani ya msingi ya Tumaini iliyokuwa karibu na eneo la iwanja cha Ndege cha Bukoba, na sasa imehamishiwa mbali eneo la Mafumbo kutokana na usalama.

Dkt. Tizeba: Walioshindwa kutimiza malengo miradi ya kilimo watupishe

$
0
0
WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amewataka viongozi wa miradi ya kilimo inayofadhiliwa na serikalipamoja na mashirika ya misaada kuzingatia malengo ya kuanzishwa miradi hiyo ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

Akizungumza katika skimu ya umwagiliaji ya Dakawa mkoani Morogoro hivi karibuni Dkt. Tizeba alisema wakulima hawana sababu ya kuwa na hiyari kwani fedha zinazotolewa ni nyingi na wahisani pamoja na serikali wanataka kuona matokeo ya misaada hiyo.

“Naomba unisikilize ndugu mwenyekiti, waliopewa pesa kwa ajili ya kilimo wasiwe na hiyari ya kulima, hatuwezi kuendelea kusikia tu wenzetu wanavuna tani nyingi katika mataifa mengine ikiwa sisi bado tunaendelea hivi hivi,” alisema Dkt. Tizeba na kusisitiza:“Anayetaka kukaa hapa kwenye skimu akae kwa kufuata masharti na asiyetaka aondoke apishe wengine. 

USAID (Shirika la misaada la watu wa Marekani) kiasi walichotoa kinafikia Sh bilioni 29, tukizigawa kila mmoja anapata Sh milioni 60. Naombeni make halafu mkubaliane kuwa suala la kufanya kilimo cha hiyari katika maeneo tuliyofadhili hatutaki kusikia. Msimu ujao tunataka tuvune tani 12 katika skimu hii.”

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo, Dkt. Filimini Mizambwa amesema ili taasisi zinazosaidia wakulima ziendelee kuwepo lazima wakulima hasa wadogo waonyeshe tija katika shughuli wanazofanya ikiwemo kuonyesha matokeo mazuri wakati wa mavuno.

“Ili sisi tuendelee kuwepo lazima wakulima hasa mkulima mdogo fanikiwe, wito wangu wakulima wajifunze kilimo chenye tija na kufanya kazi kwa juhudi ili kuwaonyesha wafadhili fedha zao hazipotei bure kwa uzembe.

“Kazi yetu ni kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora na kuongeza tija katika uzalishaji mazao, tunafanya kazi na sekta binafsi na sekta za umma, majukumu yetu ni kuongeza uzalishaji mbegu bora,” alisema Dkt. Mizambwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bwana Geoffrey Kirenga alisema malengo ya ziara hiyo katika skimu ya umwagiliaji ya wakulima wadogo Mkondo na skimukubwa ya Dakawa yenye ukubwa wa Hekta 2000 inalenga kuangalia shughuli zinazofanyika na kuangalia changamoto zilizopo.

“Huu ni mfano mzuri wa utekelezaji wa dhana ya SAGCOT, ambayo ni ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma. Katika ziara hii kuna watu wa serikali na sekta binafsi, wakulima ni sehemu ya sekta binafsi,” alisema na kuongeza:

“Nawashauri wakulima wadogo wafuate kanuni bora za kilimo ili kuonyesha tija, zamani suala hili ilikuwa ni utashi wa mkulima lakini kwa sasa si suala la hiyari tena. Kama alivyosema Mheshimiwa Waziri wa Kilimo asiyetaka atupishe ili tulete watu wengine.

Tumwekeza fedha nyingi za walipa kodi na fedha za wahisani lengo ni kuona mkulima anapata faida, ikiwa kinyume chake haitakuwa na maana hiki tunachokifanya.”Ziara hiyo ni sehemu ya maandalizi ya uzinduzi wa skimu hizo za umwagiliaji mkoani Morogoro utakaofanywa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli.

Miongoni mwa wafadhili wa shughuli za SAGCOT ni Serikali ya Tanzania, Ubalozi wa Norway, USAID, UKAID, Benki ya Dunia, UNDP na AGRA.

RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakati wa ziara yake wilayani humo. Wengine pichani kulia ni Kamanda wa Polisi mkoa huo, Muliro Jumanne Muliro.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akiangalia mashine za kukoboa na kusaga nafaka pamoja na kusindika alizeti kutoka mjasiriamali Mzee Nassoro alipokuwa kata ya Mwamamalasa.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akiwa na Katibu Tawala Mkoa, Albert Msovela (katikati) pamoja na Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese (kushoto) wakati wa ziara.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga.
Mjasirimalia Mabela Msolwa kutoka wilayani Kishapu akitoa maelezo kuhusu mradi wake wa mashine za kuchakata nafaka na ghala kuhifdhi nafaka kwa Mkuu wa mkoa (kulia) na viongozi wengine wakati wa ziara hiyo.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Kishapu, Lucas Said (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa huduma ya maji ya Ziwa Victoria kwa wananchi kata ya Maganzo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akitoa maelekezo wakati alipotembelea ghala la nafaka la Mabela mjini Mhunze kata ya Kishapu wakati wa ziara yake.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kulia) akifafanua jambo kwa viongozi mbalimbali wakati wa ziara hiyo kijiji cha Kinampanda kata ya Mwamalasa.


Na Robert Hokororo

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack amefanya ziara wilayani Kishapu kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Telack alikagua mradi wa huduma ya maji kutoka Ziwa Victoria uliopo kata ya Maganzo na maendeleo ya ujenzi wa zahanati kata ya Shagihilu.

Mradi mwingine ni wa mjasiriamali wa kusindika alizeti na kukoboa nafaka za mpunga na mahindi ambao unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Kwenye kata ya Kishapu eneo la Mhunze alitembelea mradi mwingine wa ghala la kuhifadhi nafaka na mashine za kukoboa nafaka za mahindi na mpunga.

Katika ziara hiyo kiongozi huyo aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa (RAS), Albert Msovela na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa akiwemo Kamanda wa Polisi Mkoa was Shinyanga, Muliro Jumanne Muliro.

Alikaribishwa na mwenyeji wake, Mkuu wa wilaya, Nyabaganga Talaba, Katibu Tawala Wilaya, Shadrack Kangese, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga, Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya na wakuu wa idara katika halmashauri hiyo.

MAJARIBIO YA UTAFITI WA HALI YA UMASIKINI UNAENDELEA KUFANYIKA MKOANI DODOMA NA KILIMANJARO

$
0
0

Benny Mwaipaja, WFM - Dodoma

29 Juni, 2017.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), inakamilisha majaribio ya utafiti wa hali ya umasikini katika mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro kabla ya kuanza utafiti huo nchi nzima mwezi Agosti, mwaka huu.

Hayo yamesemwa mjini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa wakati Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini humo.

Amesema kuwa ana matarajio kwamba mchakato wa taarifa za utafiti huo zitafanywa mjini Dodoma baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi hiyo inayojengwa kwa gharama ya shilingi 11.6 bilioni, zikiwa ni fedha za mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.

Dkt. Chuwa ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wakusanya taarifa za utafiti huo ili Serikali iweze kupata takwimu sahihi za hali ya umasikini nchini kwa ajili ya kutathmini programu mbalimbali na kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wake.

Nae Mshauri wa Masuala ya Kitakwimu kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania, Elizabeth Talbert amesema kuwa Benki yake imetoa mkopo huo kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Bara na Zanzibar kutokana na Benki hiyo kuona mchango mkubwa wa takwimu katika maendeleo ya nchi yoyote ile duniani.

“Tumefurahishwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi hii hapa mjini Dodoma na tunaamini ujenzi wake utakamilika kwa wakati ili kazi za kitakwimu ziweze kufanyika katika mazingira mazuri na tunaamini hatua hii italeta mchango mkubwa katika masuala ya kitakwimu hapa nchini” alisema Bibi Talbert.

Amesema kuwa Jengo la Ofisi ya Takwimu kwa upande wa Zanzibar limekamilika na huenda likaanza kutumika mapema Julai mwaka huu hatua ambayo inaleta mageuzi makubwa katika tasnia hiyo ya ukusanyaji wa takwimu mbalimbali zinazoisaidia nchi kupanga mipango ya maendeleo ya watu wake.

Kwa upande wake Mkandarasi Msanifu Majengo Mhandisi Ramadhani Shomvi anayesimamia ujenzi wa jengo hilo litakalo kuwa na ghorofa 6, amesema kuwa kampuni yake itakamilisha ujenzi huo mwezi Februari, 2018.

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina chuwa (wa pili kushoto) akingalia kitofali kinachotengezwa na mkandarasi anayejenga jengo la Taasisi hiyo wakati Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
Mshauri wa Masuala ya Kitakwimu kutoka Benki ya Dunia nchini Tanzania, Elizabeth Talbert (kushoto) akisisitiza jambo wakati Ujumbe kutoka Benki hiyo ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.
Mkandarasi Msanifu Majengo, Mhandisi Shomvi (aliyevaa sweta kulia) anayesimamia ujenzi wa jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa Mkoani Dodoma akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo wakati Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo hilo mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina chuwa (wa pili kushoto) akifurahia jambo na timu ya wataalamu wa ujenzi na ujumbe kutoka Benki ya Dunia ulipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo Jipya la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu linalojengwa mkoani Dodoma.

(Picha: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Airtel yatoa ofa kabambe katika maonesho ya sabasaba

$
0
0

Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando (kulia) na Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Bi Veronica Valentine (kushoto) wakionesha simu aina ya ZTE na Motorola katika banda la Airtel lililoko katika viwanja vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba, simu hizo zitauzwa kwa bei ya ofa ya shilingi 16,000 tu na mteja ataunganishwa na kufurushi cha muda wa maongezi kwa mwezi mzima cha shilingi 10,000 BURE. katikati ni Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Tumwidike Michael
Kutoka kulia ni Afisa huduma kwa wateja wa Airtel Digna Paul na Tumwidike Michael wakitoa huduma katika banda la Airtel lilipo katika vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba leo. katika banda hilo airtel itauza simu original kwa bei ya shilingi 16,000 ikiwa imeunganishwa na laini ya airtel na bando la mwezi mzima la shilingi 10,000 BURE.




fisa huduma kwa wateja wa Airtel Tumwidike Michael akionesha baadhi ya simu na vocha zinazouzwa katika banda la Airtel lililoko katika viwanja vya maonesho ya biashara maarufu kama sabasaba, simu hizo zitauzwa kwa bei ya ofa ya shilingi 16,000 tu na mteja ataunganishwa na kufurushi cha muda wa maongezi kwa mwezi mzima cha shilingi 10,000 BURE.







· Airtel kuuza simu kwa bei nafuu sabasaba
· Simu ya Airtel kuuzwa 16,000 ikiwa na bando la 10,00 mwezi mzima BURE

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetangaza ofa kabambe wakati wote wa maonyesho ya biashara ya sabasaba mwaka huu zitakazowawezesha wateja wake na wale wapya kuunganishwa na huduma za mtandao kwa gharama nafuu na pia kujipatia simu bomba kwa bei nafuu.

Akiongea na waandishi wa habari katika banda la Airtel lililopo viwanja vya sabasaba Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “dhamira yetu Airtel ni kuendelea kuunganisha jamii kwa bidhaa na huduma, hivyo kwa msimu huu maonesho ya saba saba tutatoa ofa nyingi sana ikiwemo simu aina ya ZTE GS 500, Motorola C113, Motorola F3 na Motorola C117 kwa shilingi 16,000 tu na mteja akishanunua ataunganishwa na bando la shilingi 10,000 litakalodumu kwa muda wa mwezi mmoja”

“Unaweza ukaona hapo gharama ya simu inakuwa nafuu na kisha unaunganishwa na kifurushi cha mwezi mzima BURE kuongea na ndugu, jamaa, na marafiki huku ukifaidi huduma zingine za Airtel” alieleza Mmbando.

Katika banda letu ndani ya saba saba mwaka huu pia huduma zitakazopatikana ni pamoja na kubadilisha laini, huduma za Airtel Money, simu za smartphone za kisasa na origino, huduma ya Timiza Vicoba, kuelekezwa jinsi yakusoma masomo ya ufundi kwa njia ya simu VETA kupitia Vsomo pamoja na kujua jinsi yakufungua biashara ya Duka la Airtel popote na jinsi ya kupata faida yako”

Mmbando alisema kuwa “Airtel imekuwa ni desturi yetu kuleta huduma na bidhaa zetu katika maonyesho haya ya biashara kila mwaka na kukutana na wateja wetu ana kwa ana ili kutoa elimu zaidi kuhusu huduma zetu mpya na za kibunifu tunazozitoa kila mwaka”.

“Natoa wito kwa watanzania kutembelea banda letu na kujipatia simu huduma za kimtandao zote kwa gharama nafuu na vilevile kukutana na watoa huduma wetu na kupata elimu juu ya huduma mbalimbali ikiwemo Kupata maelekezo ya kupata mikopo ya vikundi kupitia huduma ya Timiza vikoba. Kupata maelekezo ya kuweza kufanya biashara za Airtel kokote Tanzania kupitia mfumo wa Maduka ya Airtel AMSHA pamoja na huduma nyingine nyingi” aliongeza Mmbando.

BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA KUWA HISTORIA-WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha inakuwa historia nchini.

Pia ametoa wito kwa wazazi wote nchini waendelee kufuatilia nyendo za watoto ili wasijiingize kwenye mtego wa dawa za kulevya na wala wasisubiri vijana wao waanze kutumia.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Juni 29, 2017) kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, iliyoadhimishwa mjini Dodoma.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya unadhibitiwa kikamilifu nchini.

Amesema katika kutimiza azma hiyo, ambayo pia inaelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Dawa za Kulevya kwa kuanzisha chombo cha kisheria cha kupambana na biashara hiyo, ambayo imeongeza adhabu kwa wanaoshiriki.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuimarisha chombo hicho kinachoongoza mapambano ya dawa za kulevya ili kiendelee kufanya kazi kwa weledi na kwa kutumia mbinu za kisayansi.

“Tunaponadi uchumi wa viwanda lazima tuwe na nguvu kazi yenye siha njema kuweza kushiriki kwenye kazi halali za kujenga Taifa letu na yeyote anayetaka kudhohofisha nguvu kazi ya Taifa letu au kuhujumu jitihada za uchumi wa viwanda atashughulikiwa bila huruma,” amesema.

Aidha, kauli mbiu ya maadhimisho hayo kitaifa ni ‘Tuwasikilize na Kuwashauri Vijana na Watoto ili Kuwaepusha na Dawa za kulevya.’

Waziri Mkuu amesema kauli mbiu hiyo imetokana nan a takwimu za waathirika wakubwa wa dawa za kulevya ambao ni vijana wenye umri kati ya miaka 15-35.

“Hili ndilo kundi kubwa kwenye jamii jetu na ndilo tegemeo kubwa kwa ustawi wa nchi yetu. Hili ndilo kundi litakalotoa askari wa kulinda Nchi yetu, wanasiasa wa kuongoza Taifa letu na wataalamu mbalimbali wa kuisaidia Tanzania,” amesema.

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu), Mheshimiwa Jenista Mhagama alisema matumizi ya dawa za kulevya yamelisababishia Taifa madhara makubwa ya kiafya na kiuchumi hivyo kila mwananchi ashiriki katika mapambano hayo.

Mapema Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la Kituo cha Kutoa Huduma ya Tiba kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya katika eneo la Itega mkoani Dodoma na kuwashauri wakazi wa mkoa huo kutojihusisha na biashara hiyo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, JUNI 29, 2017
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017. 
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akizungumza katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama dawa mbalimbali za kulevya katika maonyesho yaliyokwenda sambamba na Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Kutoa Huduma kwa Waathirika wa Dawa za Kulevya mjini Dodoma Juni 29, 2017. Kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na kulia ni Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga 
Wasanii wa Kikundi cha Mchoyi cha Dodoma wakicheza ngoma ya kabila la Wagogo katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za ulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya  Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Gaudensia Simwanza wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017.
Baadhi ya wananchi na Viongozi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kwenye uwanja wa Nyerere mjini Dodoma Juni 29, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images