Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live

KAMPUNI YA TRUMARK YATOA ZAWADI YA EID EL-FITR KWA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwa amekaa na watoto wa kituo hicho.
 Mratibu wa Miradi wa Kampuni hiyo, Gasparino Haule akiongoza kucheza katika hafla hiyo.
 Ofisa  Rasilimali Watu wa Kampuni hiyo, Grace Zikwaze, akizungumza na watoto hao.
 Keki maalumu ya hafla hiyo ikikatwa kwa pamoja. Kushoto ni Makamu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobald Truphone na katikati ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo. Wengine ni maofisa wa Kampuni ya Trumark.
 Zawadi zikitolewa.
 Mwanafunzi Shafii Hassan wa kituo hicho akizungumza 
kwenye hafla hiyo.
 Mwanafunzi Wanswekula Zacharia akizungumza na wanahabari kuhusu changamoto walizonazo.
 Nguo zikiandaliwa tayari kukabidhiwa watoto hao.
 Keki maalumu kwa ajili hayo iliyotolewa na Kampuni hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwalisha keki watoto hao.
 Watoto wakiserebuka.
 Ofisa Utawala wa Kampuni hiyo, Azavery Phares akimkabidhi keki hiyo maalumu, mtoto Godwin Steven.
 Picha ya pamoja kabla ya kuicharanga keki hiyo tayari kwa kuila.



 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwa na watoto wake kwenye hafla hiyo.


Na Dotto Mwaibale

JAMII imetakiwa kujenga moyo wa kusaidia watu waliopo katika makundi yenye uhitaji ili nao wajisikie kama watu wengine waliopo katika familia.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark inayojishughulisha na uwezeshaji  jamii, Agnes Mgongo wakati kampuni hiyo  ilipokuwa ikitoa zawadi ya Sikukuu ya Eid El-Fitr katika Kituo cha watoto Yatima  cha Mtoto Wetu Tanzania kilichopo Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo hii.

"Ni vizuri jamii ikajenga tabia ya kuwakumbuka watoto na watu wengine waliopo  katika makundi maalumu kwa kuwafariji badala ya kuiachia serikali ambayo ina mambo mengi ya kufanya" alisema Mgongo.

Alisema kampuni yake iliguswa na changamoto walizonazo watoto waishio katika kituo hicho ikaona ni vizuri katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El-Fitr wakajumuike nao kwa kula na kucheza pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.

Mgongo alitaja zawadi walizotoa kupitia wadau wengine marafiki wa taasisi hiyo kuwa ni nguo, vinywaji na chakula ambacho kilipikwa katika kituo hicho.

Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo watoto waliopo katika makundi yenye  uhitaji, Wanswekula Zacharia alisema ni pamoja na vitabu, karo, sare za shule na  mahitaji mengine.

Alisema pamoja na kuwepo kwa changamoto hizo mwanafunzi anapaswa kujua wajibu wake akiwa shuleni ni kusoma na si vinginevyo.

Alisema kupokea misaada ni jambo moja lakini hata mtu kufika tu kituoni hapo na  kuwajulia hali bila ya kuwa na kitu chochote ni jambo la heri kwani wanachohitaji  zaidi ni kujumuika na jamii na kupata faraja.

Mwanafunzi wa kidato cha sita, Shafii Hassan ambaye analelewa katika kituo hicho  tangu akiwa mdogo anasema misaada wanayoipata imekuwa ikiwafanya wapate faraja  ukizingatia ukubwa wa changamoto walizonazo.

Makamu Mkurugenzi wa Kituo hicho,Theobald Tryphone aliishukuru kampuni hiyo kwa  msaada huo na kueleza changamoto kubwa walizonazo ni ada za wanafunzi, chakula,  ulipaji wa umeme na kuwa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) wameweka alama za x  katika majengo yao waondoke lakini suala hilo linashughulikiwa na Manispaa ya  Ubungo kuona jinsi itakavyowasaidia kuwasaidia kupata eneo jingine kwa ajili ya 
kujenga kituo hicho.

Mtoto analelewa katika kituo hicho, Godwin Steven alitoa shukurani kwa kampuni  hiyo kwa niaba ya wenzake kwa msaada huo.

HIVI NDIVYO COCO BEACH ILIVYOFURIKA JIONI YA JANA JIJINI DAR

$
0
0
Hivi ndivyo Ufukwe wa Coco (Coo Beach) ulivyofurika watu wa aina mbalimbali hapo jana jioni, katika kusherehekea sikukuu ya Iddi pili,Mabasi/Daladala kutoka kona kadhaa za jiji la Dar zilionekana zikishusha watu kwa wingi katika ufukwe huo ambao ulisheheni pia vyakula vya kila aina ikiwemo Mihogo,Chips mayai na wengine walikutwa na Camera ya Blogu ya jamii wakiwa wemebeba vyakula vyao na kujibweda kando kando ya ufukwe,ama kwa hakika ilikuwa burudani kwa wakazi wa jiji la Dar.Picha na Michuzi Jr.



Kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha unakuwepo,Jeshi la Polsi lilipiga kambi kabisa eneo hilo,kwa idadi ya watu ilikuwa ni kubwa.
Sehemu za kupaki magari zikaonekana hazitoshi kabisa
Foleni ya kuingia kando kando ya ufukwe nayo ilikuwa kubwa kiasi ambacho magari mengine yalipita kwa taabu kuendelea na safari zake.

Chopa ya Jeshi la polisi nayo ilikuwa na kazi ya ziada kama hivi ya kukagua meneo mbalimbali yaliyokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu,Pichani chini Chopa ikionekana kwa mbali ilipokuwa ikikatiza maeneo hayo

VIJUSO VYA MAGAZETI YA JUMATANO LEO JUNE 28,2017

MAVUNDE AAHIDI KUZITATUA KERO ZA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya kutembelea maeneo ya katikati ya mji na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hasa wafanyabiashara ndogo ndogo.

Hatua hiyo ya Mavunde imetokana na Ofisi yake ya Mbunge kuweka utaratibu wa kuwasikiliza wananchi kero zao na matatizo yao kila Alhamis(kero za Ardhi) na Ijumaa(Mambo ya kijamii).

Hata hivyo kwa siku ya leo kutokana na mapumziko ya Sikukuu ya Eid El Fitr, Mavunde ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ameamua kutembea maeneo mbalimbali ya mjini katikati na kusikiliza kero za wananchi.

Maeneo aliyotembelea ni pamoja na eneo la ‘One way’ ambalo kuna wafanyabiashara wengi wakubwa na wadogo na barabara ya sita ambako ni maarufu kwa maduka ya simu katika kata ya Madukani.

Akizungumza mara baada ya kuwatembelea wananchi hao, Mavunde ameahidi kuzipatia ufumbuzi baadhi ya kero zinazowasibu wafanyabiashara hao.
 Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyabiashara katika maduka ya simu barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye moja ya maduka ya simu eneo la barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Dodoma wakati alipotembelea maeneo mbalimbali ya mji.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akisalimiana na mmoja wa walinzi katika eneo la barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi katika maeneo aliyotembelea.

MAPOROMOKO YA MAJI MWALALO.

$
0
0
Ni maporomoko yanayopatikana katika safu za milima ya LIVINGSTONE karibu na kingo za ziwa Nyasa (MATEMA BEACH), kijiji cha Matema, wilaya ya Kyela mkoani Mbeya. Mto huu humwaga maji yake ziwa Nyasa.

Maporomoko haya yapo sehemu ambayo ni nzuri kwa (ku hike) ambapo huchukua takribani saa 1 (1hr) kutembea kwa mwendo wa kawaida (kwa miguu) kutoka katika kijiji cha Matema.

Ni nzuri kutembelea eneo hilo kwa muda wa ziada pale unapotembelea fukwe za ziwa Nyasa kwaajili ya mapumziko au sababu za kitalii kwa ajili ya zoezi la mwili, moja kati ya interesting moment ni pale katika kakilima ka mwisho kanakohitaji kupanda kwa kujivuta katika kamba.

Eneo lina sifa ya muonekano mzuri hasa wa rangi nyeupe ya maji yanayoporomoka katika miamba ya rangi ya mvuto ya kijivu.

Maporomoko haya yametengeneza bwawa zuri na la asili katikati ya miamba (mawe) ambacho ni kizuri kwa kuogelea, na kupigia picha

Ungependa kufika mahali hapa? Wasiliana na UYOLE CULTURAL TOURISM ENTERPRISE
Simu 0783545464,
Barua pepe: uyolecte@gmail.com

17 Big Bets for a Better World” launched in Tanzania

$
0
0


Ruge Mutahaba, Co-founder Clouds Media Group (right) speaking during the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. Also in the panel is, Chief Executive Officer of Benjamin Mkapa Foundation, Dr Ellen Mkondya- Senkoro (left) and Executive Director of the Dalberg Group, James Mwangi (middle) moderating the panel discussion
Executive Director of the Dalberg Group, James Mwangi (middle) moderating the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’. Also in the panel is, Chief Executive Officer of Benjamin Mkapa Foundation, Dr Ellen Mkondya- Senkoro (left) and Ruge Mutahaba, Co-founder Clouds Media Group.
Guests following the panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’ during the launch of the book ’17 Big Bets for a Better World’.


150+ business leaders engage in panel discussion on solutions for ‘off-grid societies’.

Dar es Salaam, Tanzania: Dalberg Group, The Africa List and the CEO Roundtable hosted an Iftar dinner to celebrate Dalberg’s 10 years in Africa by launching the book “17 Big Bets for a Better World”. The purpose of the launch was to kick off a discussion on Tanzania’s future and the role that the private sector plays in building the economy while addressing issues that affect Tanzanians.

The event was attended by more than 150 business leaders in Tanzania representing a diverse range of sectors including finance and banking, telecoms, agribusiness and manufacturing. Reflecting on the launch in the Tanzanian context, Dalberg Group’s Executive Director - James Mwangi - remarked, “The book presents 17 bold and innovative ideas to reduce global poverty and improve lives. It tackles the types of questions that Dalberg has been addressing in Tanzania and the rest of Africa for the past decade. The private sector is a major driving force in developing our economies and a key partner in the type of work we do – working on the most pressing development challenges.”

In the book, some of the world’s most renowned thought leaders detail how we collectively can reach the global goals (Sustainable Development Goals) set forth by the UN last year. From a bank president and a Nobel Peace Prize winner to an artist and Michelin-chef, contributors include Amina Mohammed – current Deputy Secretary-General of the United Nations and a former Minister of Environment of Nigeria, Ashish J. Thakkar – the founder of the Mara Group and Mara Foundation, James Mwangi – Managing Director and CEO of Equity Bank among others.

The book presents fresh and credible solutions to the challenges humanity faces through 17 transformational ideas for positive change. Reviews of 17 Big Bets Ban Ki-moon, Secretary General, United Nations.

“The Sustainable Development Goals embody the aspirations of people everywhere for lives of peace, prosperity and dignity on a healthy planet. To uphold our core promise to leave no one behind, we need action from everyone, everywhere. The United Nations looks forward to working with all partners to mobilize the leadership and investments that will turn this transformative vision into tangible progress.”

Muhammed Yunus, Nobel Peace Prize Laureate “What drives the world forward is transformative and game-changing solutions and innovations. Leveraging the big bets of global thinkers, this book is an important contribution to the new Global Goals.”

To further the discussion on Big Bets in the Tanzanian context, James Mwangi, spoke about a new concept called “off-grid societies” and why solutions must be created for serving them.

“In the past, “off-grid” has been used to refer to those without energy access, but we need to look beyond that to define off-grid societies as those that do not have access to 20th century infrastructure, such as roads, bank branches, hospitals, and schools. Finding solutions to reach these unconnected populations is extremely important if we are to achieve truly inclusive growth. Creating effective solutions for off-grid societies often requires us to devise new business models and leapfrog technologies that require formal infrastructure, such as phone networks or roads, to function. These are challenges that could unlock a huge amount of growth in Tanzania, but that need the private sector’s leaders to get behind.”

The off-grid societies discussion focused on five key sectors that were well represented in the audience: Finance, Retail, Energy, Healthcare and Finance. After the main session, participants were invited to engage further in coming up with off-grid solutions and big bet ideas for Tanzania.

Korogwe waishukuru Airtel kwa Kufungua duka la kisasa

$
0
0
Wakati uhalifu wa mtandao ukionekana kushika kasi duniani, Jamii imetakiwa kuzitumia simu za mkononi katika kulisaidia jeshi la polisi kubainisha watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kama sehemu ya kutekeleza haki yao ya kikatiba

Wito huo ulitolewa na Mkaguzi wa Polisi Merkiad Makumba jana kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Korogwe , wakati akizindua duka la Kisasa la kampuni ya simu za mkononi la Airtel katika wilaya hiyo mkoani Tanga. Hatua hiyo itasaidia kukabiliana na vitendo vya namna hiyo ambavyo vinahatarisha ustawi wa raia na mali zao…alisema Mkaguzi Makumba.

“ Wahalifu wengi wanatumia mawasiliano ya simu za mkononi na wamekuwa wakiwasiliana nanyi,iwapo mtazitumia simu kwa nia njema Tanzania itakuwa sehemu salama ya kuishi” alisema Mkaguzi Mkumba. Meneja mauzo wa Airtel Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.

Kiango aliongeza kwa kusema duka hili litatoa huduma nyingi pamoja na kusajili line, kutoa huduma za kifedha za Airtel Money, kuunganisha wateja na huduma za intaneti na nyingine nyingi , aidha alitumia fursa hilo kuwakaribisha wakazi wa Korogwe kulitembelea duka hilo.

Mpaka sasa Airtel imeshazindua maduka mengine kama hili katika mikoa ya Shinyanga, Dodoma, Arusha , Manyara , Dar na Morogoro. Mpango huo wa kuzindua maduka ya kutoa hudma kwa wateja unalenga kupanua na kusogeza huduma za AIRTEL karibu na jamii hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma hizi muhimu na kutatua changamoto za wateja kwa urahisi na haraka zaidi. Mpaka ifikapo mwisho wa mwaka Airtel itazindua zaidi ya maduka 2000 nchini
Mkaguzi wa Polisi wa wilaya ya Korogwe, Merkiad Makumba akikata utepe wakati wa kuzindua duka la Airtel katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, akishuhudia ni Afisa wa wateja wa Airtel Korogwe, Bi Elen na Meneja mauzo wa Airtel Tanga, Habibu Kiango.

Mahojiano ya Mubelwa Bandio na Shose Kombe kuhusu Diaspora

$
0
0
Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Mkuu wa Mawasiliano wa Diaspora kutoka KCB Bank Shose Kombe.Mahojiano haya yalifanyika ndani ya Kilimanjaro Studio iliyopo Beltsville, Maryland nchini Marekani


MASALIA YA MIJUSI MIKUBWA KUTORUDISHWA NCHINI

$
0
0
Na Octavian Kimario-WHUSM Dodoma.

Wazo la kuwarudisha nchini Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Mchinga Mhe. Hamidu Hassan Bobali lililo uliza,Ni nini kauli ya mwisho ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wananufaika kutokana na mabaki hayo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza kupata manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujererumani.

“Kufuatia majadiliano ya kina yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Malikale kutoka pande zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha shughuli za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika maeneo hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za Utalii zifanyike katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini na nje ya nchi” alisisitiza Mhe. Makani.

Kuhusu Serikali kupunjwa mapato yatokanayo na viingilio katika Makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin,Mhandisi Makani amesema jambo hilo halina ukweli wowote kwani ni ngumu kufahamu ni kiasi gani hupatikana kama kiingilio kuwaona Mijusi kutoka Tanzania kwakuwa Makumbusho hiyo ina kumbi nyingi zenye masalia kutoka nchi mbali mbali za Afrika na gharama za kuendesha Makumbusho hiyo hutolewa na Serikali ya Ujerumani.

Ameeleza kuwa Serikali ya Ujerumani itafadhili zoezi la uimarishaji idara inayohusika na Malikale katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwezesha upatikanaji wa wataalamu wa kutosha wa fani husika ilikuendeleza Utalii wa Malikale nchini.

Mijusi mikubwa (Dinosaria) ilichimbwa katika Kilima cha Tendaguru,mkoani Lindi kati ya waka 1909 na mwaka 1913 na kupelekwa katika makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin nchini Ujerumani.

Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao

$
0
0

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mheshimiwa Anthony Mavunde, amewataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa Dodoma kunufaika kiuchumi kwa kuutumia vyema uwapo wa mchezo wa bahati nasibu wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’.

Mh Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa makabidhiano ya Sh Milioni 20 kutoka kwa mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, ambaye ni fundi cherehani mwenye maskani yake mjini Dodoma, akitangazwa mshindi katika droo ya 17.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Mavunde alisema kwamba serikali ya awamu ya Tano ni ya viwanda, hivyo ni jukumu la washindi hao kuhakikisha kwamba wanaanzisha na kusimamia biashara kubwa kwa kutumia mamilioni ya Biko.

Alisema fedha za Biko zinaweza kutumiwa vizuri na washindi wao, huku katika jimbo lake, mbali na watu kuibuka na ushindi wa papo kwa hapo unaonzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa kwa kupitia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni ya Biko 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

“Nawataka kila mtu ahakikishe kwamba akipata fedha hizi anazitumia vizuri na mimi kama mbunge wao wa Dodoma nitasimamia katika kuwapatia mwangaza mzuri wakati wowote wakihitaji, maana lengo la serikali ni kupiga hatua kiuchumi,” Alisema.

Naye Evodi Mlingi aliwapongeza Biko kwa kuhakikisha kwamba wamemfikishia fedha zake haraka tofauti na matarajio yake, licha ya kuwa na imani kubwa na waendeshaji wa mchezo wa Biko ambao umekuwa ukitoa fedha nyingi kwa washindi wao.

“Nimekuwa mchezaji mzuri wa Biko kila siku na kila saa ambapo ninapopokea fedha ya ushindi wa papo kwa hapo naipeleka tena Biko jambo ambalo nimepata ushindi mnono kwa kuchanganya na maombi yangu kwa Mungu, maana nina uhitaji mkubwa wa fedha na hizi nilizopata naahidi kuzipeleka kwenye fungu la kumi kama nilivyotaka tangu mwanzo,” Alisema Mlingi huku akiwashauri Watanzania kucheza kwa wingi ili wapate ushindi.

Wakati huo huo, Mshindi wa droo ya 18 ya Biko ametangazwa jana, huku akiwa ni binti mwenye miaka 25 anayeishi jijini Mbeya, Linda Mhewa, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu Teofilo Kisanji University (TEKU), kilichopo jijini Mbeya.

Mwanafunzi huyo amepatikana katika droo iliyofanyika jana na kuchezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo, ikiwa ni mwendelezo wakutoka mamilioni kwa washindi wao.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema ni wakati wa kutajirika kwa kuhakikisha kwamba kila anayeibuka na ushindi wa Sh Milioni 20 za Biko anazitumia katika kuanzisha au kuendeleza miradi ya maendeleo kwa kupitia bahati nasibu ya Biko.

“Watu watumie vizuri uwapo wa Biko kwa kuhakikisha wanacheza mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza kuanzia Sh 1,000 na kuendelea huku Sh 1,000 ikitoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20 ambapo droo kubwa hufanyika Jumatano na Jumapili,” Alisema.

Huku mamilioni ya fedha yakiendelea kwenda kwa Watanzania, Biko wameshalipa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa mwezi Mei pekee, ikiwa ni zawadi za papo kwa hapo na ile ya droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili.



Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde, kulia akiwa na mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mjini Dodoma. Waziri Mavunde amepongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu ili afanikiwe kiuchumi.


Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde kulia akiwa na wananchi wake wa Dodoma Mjini walioshinda Sh Milioni 20 za Biko kila mmoja. Evodi Mlingi katikati amekabidhiwa fedha zake jana wakati kushoto ni Ramadhan Juma Hussein aliyeshinda Milioni 20 hivi karibuni ambapo tayari ameshapokea fedha zake kutoka Biko.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa kwenye tukio la kumkabidhi fedha zake mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, kushoto, mjini Dodoma jana.

TAKUKURU YAENDELEA KUWASHIKILIA RAIS WA TFF MALINZI NA KATIBU WAKE MWESIGWA

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kuwashikilia Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa kwa mahojiano.

Afisa uhusiano wa TAKUKURU Musa Misalaba amesema, ni kweli wanawashikilia viongozi wa TFF kwa ajili ya mahojiano ambapo wamekuwa wakifanya uchunguzi kwa muda mrefu kabla ya kuamua kuwashikilia kwa ajili ya mahojiano.

“Ni kweli kwamba tunaendelea na uchunguzi dhidi ya viongozi mbalimbali wa TFF na uchunguzi huo tumekuwa nao kwa muda mrefu lakini kuhusu kuwashikilia kwa nini, bado ni siri yetu upande wa uchunguzi, katika uchunguzi tunaongozwa na misingi ya sheria, kanuni na taratibu hatuwezi tukaweka wazi kila jambo.”

Misalaba amesema kuwa Jambo la msingi ambalo wananchi wanatakiwa kuelewa ni kwamba, kuna uchunguzi ambao wanaendelea nao ambao umekuwa ukifanywa kwa muda mrefu na kuhusiana kuwashikilia Malinzi na Mwesigwa wamesema muda wa uchunguzi ukikamilika watawapeleka mahakamani.

“Tunawashikilia na bado tuko nao chini ya ulinzi wetu , tunaongozwa na sheria tutakapomaliza uchunguzi wetu tutaweka wazi kama ni kuwaachia ila ushahidi ndio utakaoamua lakini ni lini ni swala kiuchiunguzi, lakini ni siri ya uchunguzi.”

Hivi karibuni gazeti la Nipashe liliandika mfululizo wa makala zilizokuwa zikielezea tuhuma za ufisadi zilielekezwa kwa Malinzi na viongozi wenzake wa TFF.

JAMALI AMEFANYA HAYA UFISADI WA KUTISHA TFF

Ripoti ya ukaguzi wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania kwa Taifa Stars iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inaelezwa kuwa, mbali na mambo mengine, TBL iliamua kufanya ukaguzi huo ili kujiridhisha kama shirikisho linazingatia makubaliano yaliyomo kwenye mkataba.

Inaelezwa katika ripoti hiyo ambayo uongozi wa juu wa TBL uliithibitishia Nipashe jana kwamba ilifanywa na Mkaguzi Mkuu wake wa ndani, Richard Magongo, kuwa kati ya Novemba 13, 2013 (siku 11 tangu uongozi wa sasa wa TFF uingie madarakani) na Februari 15, 2014, Dola za Marekani 315,577 (Sh. milioni 688.368) zilitumika bila ya nyaraka za kuthibitisha matumizi yake kinyume cha makubaliano ya mkataba wa pande hizo mbili.

Kati ya Novemba 11, 2013 na Machi 11, 2014, Dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) pia zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF, ripoti inabainisha.

Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonesha kuwa, miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia fedha hiyo ni pamoja na rais wa TFF, Jamal Malinzi, ambaye Desemba 24, 2013 alilipwa Dola za Marekani 159 kupitia vocha yenye namba 1075 zikiwa ni gharama za malazi hotelini (Hotel accommodation).

Ripoti inaonesha kuwa, siku hiyo hiyo (Desemba 24, 2013), Malinzi alilipwa na TFF Dola 10,000 kupitia vocha namba 1077 (Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya fedha za Jamal Malinzi), kisha Februari 6, 2014 akalipwa Dola 15,934 (Loan Repayment to Jamal Malinzi/Marejesho ya mkopo kutoka kwa Jamal Malinzi) na baadaye kulipwa Dola 69,471 kupitia vocha namba 1098 na Dola 63,735 kupitia vocha namba 1401.

Wengine waliopewa fedha hiyo ya udhamini wa TBL kwa Taifa Stars ni aliyekuwa msaidizi wa Malinzi, Juma Matandika, Ali Ruvu na mwingine aliyetajwa kwa jina la S. Madadi ambao kwa pamoja walilipwa Dola 1,084 kupitia vocha namba 828 Februari 6, 2014.

Ripoti pia inabainisha malipo ya Dola 3,500 Januari 16, 2014 kwa ajili ya ziara ya Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF jijini Nairobi.

Pia zimo Dola 4,630 zilizochotwa Desemba 24, 2013 kugharamia mtihani wa utimamu wa mwili kwa waamuzi (Cooper test for referees), Dola 4,120 zilizotolewa siku hiyo hiyo kwa ajili ya Ally Mayay na Ayubu Nyenzi kufanya ziara Uganda na Dola 1,638 ambazo zilitolewa siku hiyo hiyo zikiwa fidia ya malipo ya deni la TFF kulipia ziara ya uongozi wa shirikisho mkoani Mwanza.

Dola 4,023 zilitolewa Desemba 24, 2013 kwa ajili ya posho ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kwa wafanyakazi wa TFF na Dola 30,000 zilitumika kwa semina elekezi kwa makocha iliyofanyika Lushoto (coach retreat at Lushoto), ripoti inasema.

Inaongeza: “Dola 2,829 zilitumika kutoa rambirambi na misaada, Dola 3,298 zikakopeshwa kwa Chama cha Soka Mbeya huku Dola 989 zikitolewa kwa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara zikiwa ni msaada.”

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa, Dola 90,000 zilitumika kulipia fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wa aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen na Dola 34,177 zikatumika kununua magari mawili aina ya Toyota Hiace.

Ripoti inaeleza kuwa, kulikuwa na mawasiliano rasmi kati ya maofisa wa TFF na TBL kabla ya kufanya malipo kwa Poulsen na ununuzi wa magari hayo.
Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa.

Halotel ilivyotoa Mkono wa Eid kwa Vituo 10 vya Yatima Dar

$
0
0
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Halotel imetoa msaada wa vyakula, mbuzi na mafuta ya kupikia kwa vituo 10 vya Watoto Yatima na wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mkono wa Siku Kuu ya Eid Mubarak. Akikabidhi zawadi hizo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyan Thanh Binh alisema msaada huo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni hiyo kuikumbuka jamii hasa watoto waliopo katika mazingira magumu.

Alisema mbali na kampuni hiyo kutoa msaada huo kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu Dar es Salaam, wamezielekeza ofisi zao mikoa mbalimbali Tanzania kusaidia makundi hayo kama walivyofanya jijini Dar es Salaam. Alisema utaratibu huo utakuwa wa kila mara ili kujenga mahusiano mazuri na jamii hiyo ambayo pia ni wateja wa kampuni yao.

"...Kwanza tumeanza kuwaita na kuzungumza nao kujua masuala mbalimbali yanayowakabili na huu utakuwa ni utaratibu wa kawaida kabisa kujumuika na makundi haya na kusaidiana," alisema Nguyan Thanh Binh akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa vikundi.

Kila kikundi kimepewa mfuko wa mchele, galoni la mafuta ya kula pamoja na mbuzi wawili ikiwa ni mkono wa Siku Kuu ya Eid Mubarak inayotarajia kuadhimishwa kesho duniani pote.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyan Thanh Binh (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda (mwenye kanzu) wakikabidhi kiroba cha mchele, mafuta pamoja na mbuzi wawili kwa baadhi ya viongozi na watoto wa Kituo cha Yatima cha Mwandaliwa cha jijini Dar es Salaam ikiwa ni zawadi ya Eid Mubarak.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyan Thanh Binh (wa tatu kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda (wa pili kushoto) wakikabidhi kiroba cha mchele, mafuta pamoja na mbuzi wawili kwa viongozi na watoto wa Yatima Group Trust Fund cha Chamazi jijini Dar es Salaam ikiwa ni zawadi ya Eid Mubarak.Baadhi ya viongoni na wawakilishi wa vituo vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam pamoja na watoto wakiwa wamesimama kabla ya kupokea mkono wa Eid Mubarak kutoka Kampuni ya Halotel.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyan Thanh Binh (wa nne kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda (wa kwanza kulia) wakikabidhi mbuzi wawili kwa baadhi ya viongozi na watoto wa Kituo cha Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Kigamboni cha jijini Dar es Salaam ikiwa ni zawadi ya Eid Mubarak. Kituo hicho pia kilikabidhiwa kiroba cha mchele na mafuta ya kupikia kwa ajili ya watoto kusherehekea siku kuu ya Eid Mubarak.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyan Thanh Binh (wa nne kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda (wa kwanza kulia) wakikabidhi mbuzi wawili kwa baadhi ya viongozi na watoto wa Kituo cha Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu cha Kigamboni cha jijini Dar es Salaam ikiwa ni zawadi ya Eid Mubarak. Kituo hicho pia kilikabidhiwa kiroba cha mchele na mafuta ya kupikia kwa ajili ya watoto kusherehekea siku kuu ya Eid Mubarak.Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyan Thanh Binh akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya zoezi la kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo 10 vya Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu ikiwa ni zawadi ya Eid Mubarak.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Halotel, Mhina Semwenda (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya zoezi la kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo 10 vya Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu ikiwa ni zawadi ya Eid Mubarak. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Nguyan Thanh Binh.

UTENDAJI KAZI WA DAWASA WAIRIDHISHA SERIKALI

$
0
0
Serikali imesema imeridhishwa na Utendaji kazi wa Mamalaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika kutekeleza miradi mikubwa ya maji kwa kuzingatia Sheria na Kanuni hali inayoongeza tija katika mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesema moja ya miradi hiyo ni ule wa kupanua na kusambaza maji katika mji wa Chalinze utakaonufaisha wakazi zaidi ya laki mbili.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua moja ya mitambo katika chanzo cha maji ruvu juu,kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus Mwangi’ngo.

“Kwa ujumla naridhishwa na kazi inayofanywa na DAWASA katika kutekeleza miradi ya maji nawatia moyo muendelee kufanya kazi hii kwa bidii ili azma ya Serikali kuwafikishia wananchi huduma ya maji kwa wakati itimie” Alisisitiza Prof. Mkumbo.

Akifafanua Prof. Mkumbo amesema katika ziara yake amejionea na kukagua miundo mbinu ya kusambaza maji,ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji na miundo mbinu yote katika chanzo cha maji Wami kinachopanuliwa ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa Chalinze .
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua miundo mbinu ya chanzo cha maji ruvu juu wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA.

“Wananchi wajenge utamaduni wa kutunza rasilimali zilizopo ikiwemo miundo mbinu ya maji mbayo inajengwa kwa gharama kubwa ili iweze kuwanufaisha Wananchi wote na kuchochea maendeleo” Alisisitiza Prof. Mkumbo Mradi mwingine uliotembelewa ni ule wa uchimbaji visima vyenye urefu wa mita 600 kila kimoja vipatavyo 20 na kati ya hivyo 17 vimekamilika hivyo kuongeza upatikanaji wa maji ambao utachochea maendeleo na ukuaji wa sekta ya Viwanda.

Visima hivyo vitawezesha kuzalishwa kwa lita milioni 260 za maji kwa siku zitakazotumika katika Wilaya ya Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam. Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA mhandisi Romanus Mwangi’ngo amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini na Visima vya Kimbiji na Mpera vitasaidia kufikisha kiwango cha maji yanayozalishwa kufikia lita milioni 756 zitakazosaidia katika kuondoa tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (katikati) akisisitiza jambo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA.Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus Mwangi’ngo na kushoto ni Meneja wa Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Juu Bw. Emmanuel Makusa.

Aliongeza kuwa kwa upande wa mradi wa Chalinze vituo vya kusambaza maji takribani 236 vimeshajengwa kati ya 351 vilivyopangwa hali inayoonyesha kuwa mradi huo unaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa na utakamilika mwezi oktoba 2017.

Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na umwagiliaji kukagua miradi inayotelezwa na DAWASA katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani imehusisha vyanzo vya maji vya Ruvu Juu,Mradi wa uchimbaji Visima virefu Kimbiji na Mpera,Chanzo cha maji Wami unakotekelezwa mradi mkubwa wa upanuzi na ulazaji mabomba, ujenzi wa vituo vya kusambazia maji na matanki ya kuhifadhi maji Chalinze.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akioneshwa ramani ya mradi huo na hatua iliyofikiwa katika ulazaji wa mabomba kutoka kwa meneja wa mradi huo unaoanzia katika chanzo cha mto wami,mradi unaotekelezwa na Kampuni ya WAPCOS ya India chini ya usimamizi wa DAWASA.

SERIKALI YAJIPANGA KUKUZA LUGHA YA KISWAHILI

$
0
0
Na Zawadi Msalla-WHUSM

Serikali imeahidi kuweka misingi madhubuti ya kukuza lugha ya Kiswahili kwa kuhakikisha lugha hiyo inatumika katika ngazi mbalimbali ikiwemo kufundishia katika taasisi za kielimu, Mahakamani na Bunge.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 60 ya kuzaliwa kwa Idhaa ya Kiswahili BBC yaliyofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro-Hyatt Regency jana Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa Wizara yake ipo katika hatua za ukamilishaji wa kuundwa kwa sera mpya ya Lugha ambayo itasimamia matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili na kufanya matumizi ya lugha hiyo kukuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

“Serikali imejipanga kukifanya kiswahili kuwa kati ya lugha tatu bora duniani,kwa sasa ni miongoni mwa Lugha 10 maarufu kati ya Lugha 6000 na Lugha ya pili kutumika barani Afrika” alieleza Waziri Mwakyembe.

Aliongeza kwa kueleza kuwa uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa lugha hiyo adhimu huku Serikali ikihakikisha Kamusi hiyo inasambazwa katika maeneo yote muhimu zikiwemo ofisi zote za Balozi za Tanzania nje ya nchi, Taasisi za Elimu kuanzia ngazi za awali hadi za juu na mahakamani .

Vilevile Mhe. Mwakyembe amewapongeza wafanyakazi na uongozi wa Idhaa ya Kiswahili BBC kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Lugha ya Kiswahili inatumika katika matangazo yao na kukifanya kusikiwa dunia kote.

Aidha Waziri Mwakyembe alitoa wito kwa watanzania wote kukipenda na kukienzi Kiswahili kwani ndiyo kitu pekee kinachoweza kumtambulisha kila mtanzania mahali popote pale duniani.

SPIKA NDUGAI AGAWA VITABU KWA SHULE ZA SEKONDARI ZILIZOPO WILAYANI KOGWA

$
0
0
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini Ndg. Mungwe Athuman (kulia) wakimkabidhi  kitabu Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Manghweta Ndg. Elinetha Kimaro (kushoto) wakati wakigawa vitabu Mbali mbali kwa Shule za Sekondari zilizopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. 
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa pili kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Mtandao wa Kuondoa Umasikini Ndg. Mungwe Athumani (kulia) wakikabidhi vitabu kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya sekondari Iduo Ndg. Cathbert Kalindo, Shule iliyopo Wilaya ni Kongwa Mkoani Dodoma.
 Spika wa Bunge Mhe Job  Ndugai (wa pili kushoto) akizungumza na Wazazi wa Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Sekondari Laikala iliyopo Wilayani Kongwa, Dodoma wakati wa zoezi la kugawa Vitabu shuleni hapo  vilivyotolewa na Mtandao Kuondoa Umasikini, kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa.
   Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa tatu kulia) akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ibwaga iliyopo Wilayani Kongwa, Dodoma baada ya kugawa vitabu shuleni hapo, vitabu hivyo  vimetolewa na Mtandao wa kuondoa Umasikini. Kulia kwa Spika ni Mweyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athuman  na kushoto kwake ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa. Zoezi la ugwaji wa vitabu hivyo lilianza  toka wiki iliyopita ambapo takribani shule thelathini za Sekondari zilizopo Wilaya ya Kogwa, Dodoma zimenufaika na msaada huo. (Picha na Ofisi ya Bunge).

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIZUNGUMZA JAMBO NA MBUNGE SERUKAMABA

$
0
0
Waziri  Mkuu Kassim  Majaliwa  akisikiliza jambo kutoka  kwa  Mbunge  wa Kigoma  Kaskazini  Peter  Serukamba  (CCM).  walipo kutana katika viwanja vya Bunge  Mjini Dododma  leo June 28, 2017.

JESHI LA ZIMAMOTO LAFANIKIWA KUZIMA MOTO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Watanzania wenye asili ya kihindi wakiwa kwenye kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam, kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla ya kuleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Askari wa  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam,kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Askari wa  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakijiandaa kupokea waathirika wa janga la moto  katika shughuli za uzimaji moto baada ya jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam,kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
 Jengo la ghorofa 12 lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi lililoshika moto na kufanikiwa kuzimwa na askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,leo jijini Dar es Salaam. Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji
Kifaa kinachotumika na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  kuzima moto,kuokolea watu na mali kwenye majengo marefu, kikisaidia uokoaji  katika  jengo lililopo Mtaa wa Indira Ghandhi,jijini Dar es Salaam, baada ya kushika moto ambao ulifanikiwa kuzimwa na askari wa jeshi hilo kabla haujaleta madhara.Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

NCAA KUSHIRIKIANA NA TFF KUKUZA SOKA LA TANZANIA

$
0
0
 
Naibu Mhifadhi (Huduma za Shirika) wa Mamlaka ya  Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye N. Bangu, akipeana mkono na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa TFF wa Maendeleo ya Soka (TFDF), Derek Murusuri. Bw Bangu alizitembelea ofisi za TFDF ili kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano kati ya Mamlaka yake na Mfuko huo. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi za TFDF zilizoko Mikocheni jijini Dar Es Salaam leo (28 June 2017).

Katika mazungumzo hayo, Bw Bangu ameahidi kushirikiana na Mfuko huo katika kuendeleza soka la Tanzania. Timu ya Taifa ya vijana walio chini ya miaka 20 (U-20), Ngorongoro Heroes, inatumia jina la Mamlaka hiyo ya Taifa ambayo pia ni mojawapo ya maajabu saba ya dunia.

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MWONGOZ KWA WAPELELEZI NA WAENDESHA MASHITAKA WA KESI ZA WANYAMAPORI NA MISITU

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria Uzinduzi Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wengine pichani ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia),Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodrigues na kushoto ni Muendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga na Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni Kitabu cha Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, katikati ni Muendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali Biswalo Mganga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mwongozo kwa Wapelelezi na Waendesha Mashitaka wa Kesi za Wanyamapori na Misitu kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais - Ikulu)
 
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Makamu wa Rais Samia Suluhu azindua muongozo kwa watumishi katika kesi za wanyamapori.

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha mashitaka, polisi na wapelelezi wa kesi za wanyamapori na misitu kubadilika katika kazi zao ili kulinda rasilimali hizo kwa vizazi vya sasa na vijavyo.Aidha, ameitaka mahakama kutoa muongozo kwa watumishi wake kuhusu namna ya kuendesha kesi zinazohusiana na nyara za serikali kwa lengo la kuwa na uwiano sawa katika utoaji amri.

Samia amesema hayo leo mjini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mwongozo kwa wapelelezi, waendesha mashitaka na Polisi wa kesi za wanyamapori na misitu ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

Amesema wote hao wanatakiwa kufanya kazi zao ipasavyo kuhakikisha usalama wa wanyamapori na misitu kwani kwa kupoteza maloiasili hizo kunafanya uchumi wa nchi kushuka na kwamba wasifanye kazi hiyo kwa kuweka mazingira ya rushwa.

Amesema, kazi za kupeleleza na kuendesha kesi za wanyamapori zimekuwa na ushawishi mkubwa wa rushwa kutoka kwa wahusika na kuwataka kufikiria maslahi mapana ya nchi na sio wao binafsi.

"Jamani, msiogope kufa, kifo kipo na kila mmoja wetu atakufa hata mnyama ikiwemo huyo FaruJohn, muhumu ni namna ya kujua aina ya kifo utakachokufa, lakini Jambo la kusikitisha mmekuwa mkiponzwa na fedha, wahenga walisema 'fedha ni sabuni ya roho lakini pia walisema fedha ni fedheha," amesema Samia.

ameongeza kuwa, Rais Magufuli ana lengo kubwa la kulinda maliasili za nchi hii na kwamba kutaka kwake kuwepo kuwepo kwa miongozo hiyo katika mahakama kutasaidia mahakimu na majaji kutoa adhabu na dhamana zinazowiana.

Ameongeza, mara kadhaa kumejitokeza majaji na mahakimu kutoa adhabu zinazotofautiana au masharti yanayo tofautiana katika kesi zenye mazingira sawa.

Aidha amemtaka DPP kufanya namna ya kuwapeka watumishi hao kwenye mbuga za wanyama, vyanzo vya maji na maeneo ya mbali mbali yenye misitu ili kujionea ni kwa namna gani rasilimali za nchi zinavyopotea kwa wanyama kuuawa kwa kukosa maji.

Amesema, mwongozo huo uliotolewa utasaidia kuboresha upelelezi na uendeshaji wa mashitaka na kwamba mapambano dhidi ya ujangili na uhalifu yatakoma na matokeo chanya yatakuwa yakipatikana katika kesi mbali mbali na serikali kuweza kupata mapato yake katika sekta ya utalii.

Akitoa takwimu za sekta ya wanyamapori, Samia amesema, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ya mwaka 2009, ilionesha kuwa Tanzania ilikuwa na tembo 109,051 na sensa ya mwaka 2014 ilionesha idadi ya tembo imepungua na kufikia tembo 43,330 ambao sawa na asilimia 60.3 ya tembo wote.

Alisema sababu kuu ya kupungua kwa tembo hao ni ujangili na kwamba takwimu rasmi za Sekretarieti ya Maktaba wa Kimataifa unaoratibu biashara ya wanyama waliohatarini kutoweka (CITES), ilionesha asilimia 70 ya meno ya tembo yaliyokamatwa duniani kote kati ya mwaka 2008 na 2013, yalitokea Afrika Mashariki nchi za Tanzania na Kenya ambapo kiasi kikubwa kilitokea Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa ya Taasisi ya International Union for the Conservation of Nature (IUCN) ya mwaka 2013, Tanzania ilishuka hadi namba tatu kwa idadi ya tembo kwa asilimia 13 ya tembo wote waliopo barani Afrika ikiwa nyuma ya Botswana (asilimia 33) na Zimbabwe (asilimia 16).

Naye DPP Biswalo Mganga amesema katika kipindi cha mwaka 2014 na 2017, washitakiwa 100 walihukumiwa kulipa faini ya bilioni 1.1 na vifungo virefu ambazo tayari imeshalipwa serikalini.Aidha, watuhumiwa 80 walihukumiwa kifungo cha miaka 20 na 30 gerezani na faini ya bilioni 164.7 ambayo bado haijalipwa.

Alisema suala la dhamana kwa makosa makubwa yanayohusu wanyamapori waliohatarini kutoweka ikiwemo tembo na faru, watuhumiwa wengi wamekuwa wakitoroka na kusababisha kesi kutoendelea dhidi yao.

Ameongeza mwaka kati ya 2010 na 2015 mashauri 13 yanayohusiana na nyara za serikali zenye thamani ya milioni 800 yalifikishwa katika Mahakama za Mkoa wa Dar es Salaam lakini watuhumiwa wake walitoweka baada ya kupewa dhamana.

Hata hivyo, alisema asilimia 69 ya watuhumiwa hao ni raia wa kigeni na asilimia 31 ni Watanzania; wakati mahakama inapotoa dhamana, moja ya masharti yake ni kunyang'anywa hati zao za kusafiria.Alifafanua kuwa kati ya kesi hizo 13 watuhumiwa waliua jumla ya tembo 300, chui nane, Kobe 210, twiga,kiboko, pundamilia na ndege wa aina mbalimbali wenye thamani ya milioni 800.

Amesema, takwimu zinaonesha kuwa asilimia 70 ya washitakiwa huruka dhamana na kukimbia kesi pindi wanapopewa dhamana kwa hiyo, anajitahidi kuchukua hatua madhubuti kwenye suala la dhamana hasa kwenye kesi zinazohusu meno ya tembo na faru wanaokaribia kutoweka nchin.

NGUVU KAZI YA TAIFA INATEKETEA KWA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA- RC DODOMA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Dodoma

Vijana wengi wanaangamia kutokana na kutumia dawa za kulevya na kufanya Taifa kukosa nguvu kazi ya kufanya uzalishaji.

Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square mkoani hapa, amesema kuwa vijana kuwa na familia wameshindwa kuwa wazalishaji kwa kuishia katika matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema vita ya dawa za kulevya ilishatangazwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli na wengine ni kufanya utekelezaji kuhakikisha linafanikiwa dhidi vita ya dawa za kulevya.

Rugimbana amesema kuwa Dodoma inalengwa na kuwindwa kutokana na vyuo vingi kuwepo hali ambayo vijana wanaweza kungeuka na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku matumizi ya shisha katika hoteli zilizopo katika mkoa wake kutokana na kuwa sehemu ya dawa za kulevya.

Aidha amemuomba Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji kujenga sober house katika mkoa wa Dodoma kutokana na kuwepo kwa kundi la vijana ambao wameathrika na matumizi ya dawa za kulevya.

Bhanji amesema kuwa wanaangalia uwezo katika kuweza kujenga kituo ili kuweza kuwarudisha vijana kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya na kuwa wazalishaji katika taifa lao.

Amesema kuwa vijana wanaathirika sana na matumizi dawa za kulevya na kufanya familia zao kuwa na mzigo wa kuwategemea wazazi wakati wazazi hao walitakiwa kusaidiwa na vijana wao.

Katika maonesho hayo yameshirikisha umoja wa vituo vya kuhudumia walioathirika na dawa za kulevya Voice of Sober Houses (VOS).
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji jana wakati maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Jana.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji wakati alipotembelea banda la Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipata maelezo katika banda la Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya kutoka kwa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Anastazia Sauli katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akizungumza na katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma .
Kamishina Msaidizi wa Idara ya Kinga , Tiba na Utafiti ,DK. Cassian Nyadindi akitoa maelezo juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Wananchi waktembelea mabanda mbambali juu ya huduma wanazozitoa katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
 Picha ya pamoja.
Sehemu ya wananchi wakiwa katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live




Latest Images