Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1284 | 1285 | (Page 1286) | 1287 | 1288 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare akiwasili katika Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Haraka cha Kimara Mwisho. Mhandisi Rwakatare alipokewa na Kaimu Meneja Usafirishaji wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dkt Philemon Mzee (kushoto).
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare akipita sehemu ya ukaguzi wa tiketi na kadi zitumiwazo na Mabasi Yaendayo Haraka. Mhandisi Rwakatare alipata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali vya Kituo Kikuu cha Kimara mwisho na kujionea huduma za usafiri zinavyofanyika katika kituo hicho.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare akizungumza na mmoja wa abiria wa Mabasi yaendayo haraka katika Kituo Kikuu cha Mabasi hayo katika eneo la Kimara Mwisho.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare (kulia) akitembelea vitengo mbalimbali vya kutoa huduma katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo haraka kilichopo Kimara mwisho. Mhandisi Rwakatare aliambatana na Kaimu Meneja Usafirishaji wa DART Dkt Philemon Mzee, na Kushoto ni Afisa Habari Mkuu wa DART bwana Mathew Kwembe.
  Sehemu ya daraja linalotumiwa na wananchi pindi wanapoingia na kutoka katika Kituo Kikuu cha Mabasi Yaendayo Haraka kilichopo Kimara Mwisho. Daraja hili ni miongoni mwa miundombinu iliyojengwa na Serikali kwa ushirikiano na Benki ya Dunia.  Na Mathew Kwembe

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Rwakatare ameeleza kuwa mradi huo umepata mafanikio makubwa katika kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es salaam hususani katika barabara ya Morogoro.

  Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kituo kikuu cha Kimara mwisho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma, Mhandisi Rwakatare alisema kuwa katika kipindi hicho cha mpito, Mabasi yaendayo haraka yameweza kusafirisha watu 200,000 kila siku kutoka watu 50,000 iliyokuwa ikisafirisha mwaka jana, wakati mradi unaanza.

  Mhandisi Rwakatare alieleza kuwa Mradi huo umeweza kuokoa muda wa wananchi ambao kabla ya mradi kuanza walikuwa wakitumia usafiri mwingine uliokuwa ukichukua kutoka masaa mawili, wakati sasa wanatumia dakika 45 tu kwa safari ya kutoka Kimara hadi Posta kwa kutumia mabasi yaendayo haraka.

  Alifafanua kuwa huduma hiyo mbali na kuwapunguzia mzigo wa nauli watumiaji wa kawaida wa mabasi ya daladala, mradi wa mabasi yaendayo haraka imeokoa gharama ya usafiri kwa wenye magari binafsi ambapo wengi wao wamekuwa wakiutumia zaidi usafiri huo.

  Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma Mhandisi Rwakatare alisema kwa wakala umeona ni vyema kutumia maadhimisho hayo kusikiliza kero na maoni ya wananchi hasa watumiaji wa huduma hiyo ili kuona namna nzuri ya kuiboresha.

  “Watumishi wa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka wamekuwepo katika vituo vya Gerezani na Kimara mwisho kwa siku hizi mbili ili kusikiliza kero na maoni kutoka kwa wananchi wetu, na tunafurahi kuona huduma hii ikizidi kushika kasi, hasa kwa kuzingatia kuwa tupo katika kipindi cha mpito,” alisema.

  Hata hivyo alisema kuwa maoni na ushauri walioupata kutoka kwa wananchi wataufanyia kazi na kurekebisha kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika kipindi cha mpito ili kuhakikisha kuwa huduma hiyo inakuwa bora zaidi.

  Aisema kuwa Wakala upo mbioni kumpata mtoa huduma ya ukusanyaji mapato ambapo ndiye atakuwa na jukumu la kushughulikia suala la kadi ili kuondokana na changamoto mbalimbali za usafiri zinazowakabili watumiaji wa mabasi hayo.

  “Natambua kuwa kadi zimeisha na wakala unalishughulikia jambo hili na tutahakikisha kuwa tunaongeza kadi, nawasihi wananchi watambue kuwa tupo katika kipindi cha mpito, mapungufu mengi yaliyojitokeza tutayarekebisha,” alisema.

  Mhandisi Rwakatare alibainisha kuwa suala la kadi limechukua muda mrefu kwa vile mchakato wake unahusisha mfumo wa kibenki na hivyo kuwataka wananchi wa jiji la Dar es salaam kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki cha mpito kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza hususani suala la kadi ambapo aliahidi kulitafutia ufumbuzi suala hilo mapema iwezekanavyo.

  Mhandisi Rwakatare alisema kuwa Mradi huo unatekelezwa kwa ubia baina ya Serikali na Kampuni binafsi ya UDART ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kutoa huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo haraka katika kipindi hiki cha mpito

  Alisema Serikali kwa upande wake imeshirikiana na Benki ya Dunia kujenga miundombinu mbalimbali inayotumiwa na mabasi hayo ambapo katika awamu ya kwanza ujenzi wake umehusisha barabara zenye jumla ya kilometa 20.9 ambazo ni Kimara – Kivukoni, Magomeni – Morocco na Faya – Karikaoo.

  Pia alisema kuwa Wakala wa Mabasi yaendayo haraka upo mbioni kumpata mtoa huduma kamili baada ya kipindi cha mwaka mmoja cha mpito. Alisema kuwa Wakala unatarajia kuongeza mabasi mengine 165 kwa ajili ya kutoa huduma zaidi za usafiri katika jiji la Dar es salaam.

  Alisema kuwa wakala unatarajia kuongeza njia za mrisho katika maeneo ya Mwenge, Kawe na Mabibo.

  Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka ulianza rasmi tarehe 16 Mei, 2016, ambapo umekwishatimiza mwaka mmoja katika kipindi cha mpito tangu kuanza kutolewa kwa huduma hiyo ambapo zimepangwa awamu sita za ujenzi wa miundombinu ya mradi huo katika maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam huku awamu ya kwanza imekwishakamilika.

  0 0  0 0  Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Catherine Magige akimkabidhi mkurugenzi na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Faraja orphance kilichopo jijini hapa,kituo hichi cha watoto yatima kina jumla ya watoto 200 na kati ya watoto hao watoto 30 wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
  wa pili kushoto mbunge wa viti maalumu akiwa anateta jambo na katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan ,wakwanza kulia ni katibu wa kanda ya kaskazini msikiti wa Twariqatul ndugu Abdi Ramathani
  mbunge wa viti maalumu akiwa anamkabidhi zawadi za iddi mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Samaritan villege Jospephat Mmnyi
  mbunge wa viti maalum akiwa pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima na wasiojiweza cha Faraja ,mkurugenzi wa kituo hicho pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha
  mbunge wa viti maalumu akiwa amembeba moja ya mtoto aliotelekezwa na mama yake akiwa mdogo anaeishi katika kituo cha watoto yatima cha Faraja kilichopo jijini hapa wakati alipowapelekea zawadi ya iddi

  mbunge wa viti maalumu akimkabidhi msaada wa chakula mmoja wa kijana wa kito cha Zawiani wakati alipotembelea kutoa zawadi za sikukuu ya iddi
  mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anapewa maelezo mafupi katika maabusu ya watoto Arusha ,Ambapo aliaambiwa mahabusu hiyo inauwezo wa kubeba watoto 50 wakike wakiwa 10 na wakiume wakiwa 40 lakini kwa sasa ina jumla ya mahabusu 12 tu na wote wakiwa ni wanaume (picha na Woinde Shizza,Arusha )
  Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anamkabidhi mbuzi ,mchele na mafuta kiongozi wa kituo cha mahabusu Arusha Mussa Mapunda ikiwa ni zawadi ya idi kwa watoto hao
  vijana wa kituo cha Zawiani wakisala kabla ya msaada kutolewa wakiwa na mbunge wa viti maalumu pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi

  Habari picha na Woinde shizza,Arusha


  Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Catherine Magige leo amekabidhi msaada wa mbuzi watano ,chakula na mafuta kwa vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja watoto wanoishi katika mahabusu ya watoto mkoani hapa ili kusherekea sikukuu ya idi .


  Akikabidhi msaada huo kwa katika vituo hivyo alisema kuwa watoto hao wanapaswa kusherehekea sikukuuu ya iddi kama wengine wanaoishi na wazazi wao majumbani kwao .


  Alisema kuwa vitu vyote hivyo alivyovigawa katika vituo vyote alivyo vitoa ametoa kwa moyo wake wote ,ambapo alisema kuwa yeye kama mama ameguswa na akaamua kwenda kuwapa watoto hawa msaada huo ili nao wakisherekea sikukuu hii wajisikie nao wapo na wazazi wao.


  "napenda kuwasihi wananchi wajijengee tabia ya kusaidia watoto hawa yatima pia wajifunze kutembelea hata hawa watoto mahabusu ata kama awana watoto katika mahabusu hizi lakini wanaweza wakatoka na misaada na kuamua kupelekea watoto hawa yatima au hawa watoto walioko mahabusu kwani ni watoto na wanahaki ya kupendwa kama watoto wengine"alisema Magige


  Alivitaja vituo ambavyo vimepewa msaada kuwa ni pamoja na Faraja ophas,Samaritan villege,kituo cha watoto yatima na wasio jiweza cha Zawiani pamoja na Mahabusu ya watoto Arusha


  Wakati huohuo, Ofisa Msimamizi wa kito hicho , Mussa Mapua aliiomba Serikali kujenga uzio katika mahabusu hiyo ili kuzuia watu wenye nia mbaya kuingiza dawa za kulevya au wale watoto ambao ni wakorofi kutoroka.


  Aidha alisema kuwa pia wanahitaji wanasheria wa watoto hao ili kesi zao zilizoko mahakamani ziishe kwa muda mfupi, tofauti na hali ilivyo sasa huku akisema kuwa mahabusu hiyo kwa sasa inawatoto wa kiume 12 wote wakiwa ni wanaume


  "unajua kesi zinachelewa kutokana na kukosekana kwa wanasherisa wa kuwatetea watoto hivyo tunaomba serikali ijitaidi kutuletea mwanasheria wa kutetea watoto hawapia napenda kutumia nafasi hii kuliomba Jeshi la Polisi kuwa makini katika upelelezi wa kesi mbalimbali ikiwamo kuzingatia umri wa watoto ili kuepuka kuwapeleka wakubwa katika mahabusi hiyo "alisema Mapua  0 0  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira mara baada ya kuwasili Mkoani hapo kwa ajili ya kuhudhuria ibada ya Eid Elfitr itakayo fanyika Kitaifa mjini Moshi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mwenyekiti wa TAMCO (Jumuiya ya Waislamu DMV) Bwn Ally Mohamed akitoa salamuza Eid El Fitr kwa Waislam na marafiki zao DMV kwenye sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika siku ya Jumapili June 25, 2017 Silver Spring, Maryland.Picha na Vijimambo Blog na Kwanza production.
  Kushoto ni Balozi Mustafa Nyang"anyi akijumuika kwenye sherehe ya Eid El Fitr na Watanzania DMV.
  Balozi Mustafa Nyang"anyi akifuatilia sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika Sliver Spring, Maryland siku ya Jumapili June 25, 2017, kulia ni Seif Ameir.
  Watanzania DMV wakijumuika pamoja katika sherehe ya Eid El Fitr iliyofanyika Silver Spring, Maryland siku ya Jumapili June 25, 2017.


   


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya Eidd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Wananchi mbali mbali baada ya Swala ya ElIdd Fitri iliyoswaliwa leo katika uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherekekea kumalizika kwa Mfungo wa MweziMtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
   Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga   alipokuwa akitoa khutba baada ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan aliyohudhuriwa na Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali wa Mkoa wa Mjini Magharibi  leo.
   Waislamu wanawake wakiwa katika Swala ya Eid  el fitri iliyoongozwa na Sheikh Fadhil Soraga katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjni Unguja leo katika Mkoa wa Mjini Magharibi ambapo  Viongozi  wa Kitaifa na Waislamu mbali mbali walihudhuria [Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
   Baadhi ya waislamu wanaume waliohudhuria katika swala ya EId elfitri wakimsikiliza  Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar  Sheikh Fadhil Soraga aklipokuwa akitoa khutba ya Swala ya El Idd elfitri iliyoswaliwa katika Uwanja wa Maisara Suleiman Mjini Unguja katika kusherehekea Sikukuu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.

  0 0

  KATIKA hali inayoonyesha ya kuchachamaa na kuchangamkia fursa, droo ya 17 ya Bahati ya Nasibu ya Biko ‘ijue Nguvu ya Buku, imefanyika jana jijini Dar es Salaam, huku fundi charahani wa Mjini Dododoma, Evodi Mlingi, kuibuka kidedea na kujinyakulia jumla ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na Biko.
  Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza na simu ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Dodoma, Evodi Mlingi aliyepatikana baada ya kuchezesha droo ya 17 ya Bahati Nasibu ya Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki.

  Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, akiandika dondoo baada ya kupatikana kwa mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 17 ambapo Evodi Mlingi mkazi wa Dodoma aliibuka kidedea. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

  Droo ya kumtafuta mshindi huyo wa Sh Milioni 20 imeendeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Mlingi ni mshindi wa pili wa anayetokea Dodoma mjini kujinyakulia Sh Milioni 20, akitanguliwa na Ramadhan Juma Hussein, aliyekabidhiwa fedha zake wiki iliyopita.
  Alisema mchezo wa Biko ni rahisi kucheza na rahisi pia kushinda kwa kutumia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo wanachotakiwa ni kufanya miamala kwenye simu zao kuanzia Sh 1,000 na kuendelea huku namba ya kampuni wakipaswa kuingiza 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.

  “Huu ni wakati wa kutajirika kwa kupitia Biko, hivyo tunampongeza mshindi wetu wa Dodoma, Mlingi kwa kushinda dodo la Sh Milioni 20, huku nikiwakumbusha kuwa kila mtu anaweza kushinda zawadi mbali mbali za fedha taslimu za papo kwa hapo kuanza Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washindi,” Alisema.

  Naye mshindi huyo wa Dodoma, Mlingi aliwashukuru Biko kwa kumtangaza mshindi katika droo ya 17, huku akisema sasa maisha yake yamekuwa mazuri kwa kuzitumia vizuri fedha za bahati nasibu hiyo atakazopewa.

  “Nilikuwa nacheza Biko kwa malengo ya kushinda, hivyo leo kutangazwa mshindi hatimae ndoto zangu zimetimia, maana pamoja na kucheza sana, pia nilikuwa namuomba Mungu anipe nafasi ya mimi kushinda ili niimudu familia yangu,” Alisema kwa hisia fundi charahani huyo kutoka Dodoma Mjini.

  Kwa upande wake mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, aliwapongeza Watanzania wote wanaojitokeza kwa wingi kucheza Biko akisisitiza kuwa ni eneo zuri la kunufaika kuichumi kwa kupitia sekta ya michezo ya kubahatisha.
  “Watanzania wacheze kwa wingi kwa sababu ni mchezo unaofuata vigezo vyote kutoka kwenye Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, nikiamini kuwa wanaweza kujikomboa kiuchumi kwa kupitia fursa ya michezo hii ya kubahatisha hapa nchini,” Alisema.

  Kwa kutangazwa mshindi kwenye droo ya 17, sasa Mlingi anajiandaa kupokea fedha zake haraka iwezekano kutoka kwa waendeshaji wa bahati nasibu hiyo ambao Mwezi Mei pekee waliweza kutoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa washindi wao.

  0 0

  Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba yake fupi wakati wa Swala ya Eid el Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja mapema leo, jijini Dar es Salaam. 


  Pichani kulia ni Rais mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi sambamba na waumini wengine wakiswali swala ya sikukuu ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.

  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum akitoa mawaidha yake wakati wa Swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

   Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika Swala ya Eid El Fitr,iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar
    Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika Swala ya Eid El Fitr,iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar
    Waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia mawaidha mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika Swala ya Eid El Fitr,iliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar
   
    Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Eid El Fitr,katika viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar.
     Waumini wa dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Eid El Fitr,katika viwanja vya mnazi mmoja mapema,leo jijini Dar  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dkt Hussein Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi mara baada ya kuwasili katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,Pichani kati ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum .
  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi mara baada ya kuwasili katika Swala ya Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CUF,Prof Haroun Lipumba na waumini wengine wakiwasili katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa ajili ya kushiriki swala ya Eid El Fitr jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim akiongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa Salum pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mhe.Salum Hapi kushiriki kwenye swala ya sikukuu ya
  Eid El Fitr iliyofanyika mapema leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akitoa nasaha za Eid, tarehe 26 Juni, 2017. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa nasaha kwa waumini (hawapo pichani) waliohudhuria Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally wakati wa stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mara baada ya Swala ya Eid el Fitr na Baraza la Eid Kitaifa mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally mara baada ya stafutahi kwenye Ikulu ndogo ya Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha maombolezo, nyumbani kwa marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa pole na neno la faraja kwa wanafamilia, nyumbani kwa marehemu Dk. Philemon Ndesamburo, eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro tarehe 26 Juni, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa pole mjane wa marehemu, mama Ndehorio P. Ndesamburo alipofika nyumbani kwao eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro kuwafariji kutokana na msiba wa Dk. Philemon Ndesamburo, leo tarehe 26 Juni, 2017. 
  Kaka wa marerehemu Dk. Philemon Ndesamburo, Bw. Zablon Sindato Kihwelu akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika nyumbani kwao eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro kuwafariji kutokana na msiba wa Dk. Philemon Ndesamburo, leo tarehe 26 Juni, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Anna Mgwira (wa tatu kushoto), mjane wa marehemu na Kaka wa marehemu wakiomba dua na wanafamilia kwenye kaburi la Dk. Philemon Ndesamburo, aliyezikwa nyumbani kwake eneo la Kiboriloni, Moshi, mkoani Kilimanjaro. Wa kwanza kulia ni mtoto wa marehemu.

  ……………………………………………………………………….

  *Ahimiza nyumba za ibada zisaidie vita ya dawa za kulevya 

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi kuanzia leo. “Kuanzia leo, ni marufuku kwa mtu yoyote kusafirisha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi bila ya vibali. Serikali inahamasisha uwekezaji kwenye ujenzi wa viwanda nchini. Kama tutatoa vibali, ni lazima mtu alazimike kusaga nafaka ili kutoa ajira nchini,” amesema. 

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Juni 26, 2017) wakati akitoa nasaha kwenye Baraza la Eid lililofanyika kitaifa kwenye msikiti wa Masjid Riadha, mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro mara baada ya kuswali sala ya Eid. 

  “Jana nimeona kwenye televisheni taarifa kuhusu malori 10 yaliyokamatwa Tarakea yakiwa na mahindi tayari kuvushwa mpaka. Mheshimiwa RC akasema chakula hicho ni lazima yarudishwe kwa ajili ya usagaji.”

  “Mimi nasema kuanzia leo, yeyote atakayekamatwa akitorosha chakula kwenda nje ya nchi, chakula hicho kitataifishwa na kupelekwa ghala la Taifa na gari lake tutalitaifisha na litaishia Jeshi la Polisi. Tunafanya hayo kwa lengo la kuwalinda Watanzania tusikumbwe na baa la njaa.” 

  Akitoa tahadhari kuhusu uuzwaji wa chakula nje ya nchi, Waziri Mkuu amesema kumekuwa na wimbi kubwa la usafirishaji wa chakula kwenda nje ya nchi bila kibali. “Hilo ni kosa kubwa kwa sababu litasababisha nchi yetu kupata baa la njaa huko mbele,” amesema.

  Amesema mipaka ya Tarakea, Holili, Mwanga, Horohoro, Siha, Namanga na Sirari imekuwa inapitisha kiasi kikubwa cha mazao ya chakula kwenda nje ya nchi jambo ambalo ni hatari sana. “Hii ni kwa sababu chakula cha ndani hakitoshelezi mahitaji. Kwa sababu nchi zote za jirani hazina chakula cha kutosha. Tusipokuwa makini, tutabaki tunalia njaa.”

  Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwasihi wafanyabiashara wa ndani, wachukue mahindi kutoka maeneo yenye mavuno mengi na kuyapeleka kwenye sehemu zenye mavuno kidogo. “Watanzania tushirikiane, kama ni biashara tutoe huku kwenye mavuno mengi na tuyapeleke Shinyanga na Geita ambako wanayahitaji au tukanunue Sumbawanga na kuyapeleka kwenye mikoa mingine yenye upungufu,” alisisitiza. 

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka viongozi wa dini waisadie Serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kupitia kwenye nyumba za ibada. “Naomba tuendelee kushirikiana kupambana na janga hili la dawa za kulevya kwa ustawi wa nchi yetu. Naamini viongozi wa dini mnayo nafasi kubwa katika mapambano haya, kwa kuwafunda vijana wetu kuishi katika maadili ya kidini na kutojiingiza kwenye janga hilo.”

  Alisema Serikali kwa upande wake itaendeleza mapambano hayo bila ajizi wala mzaha. “Tunaomba wananchi wote watuunge mkono kwa kutoa taarifa sahihi za wanaojihusisha na uzalishaji, utengenezaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya pindi tu wanapowabaini.”

  Wakati huo huo, akitoa tafsiri ya Qur’aan tukufu kwenye Baraza la Eid, Sheikh wa Mkoa wa Arusha, Sheikh Shaaban Juma alisema kila nguzo katika Uislamu inapaswa kufuatwa na kwamba mtu akiharibu nguzo moja tu anakuwa ameharibu nguzo zote tano.

  Alisema siku ya kiyama, watatokea watu wenye thawabu kama milima ya Usambara ama Upareni na akawataka Waislamu wote nchini wadumu katika kutenda mema ili wapate thawabu.

  Mapema, akitoa khutba katika swala ya Eid el Fitr iliyoswaliwa kwenye msikiti huohuo wa Masjid Riadha, Sheikh Mlewa Shaban alisema sikukuu ya Eid ni siku ya kujiepusha na madhambi kama ulevi, kamari na lugha chafu, bali aliwataka waumini wote waitumie siku hiyo kuwapa furaha maskini, yatima na wajane.

  “Mtu asiseme mwezi wa Ramadhan umepita, sasa narudia mambo yangu ya zamani. Adhabu za Mwenyezi Mungu hazina mipaka na wale waliotulizana watapata thawabu yao, kumbukeni neema na Mwenyezi Mungu na mcheni Mwenyezi Mungu.”

  “Kitu tunachopaswa kufanya kila wakati ni kumcha Mwenyezi Mungu. Lazima tupendane, tuondoe tofauti zetu na tuujenge Uislam. Hatuwezi kuujenga uislam kama hatupendani. Lazima tuilinde ibada yetu kwa sababu hatuna garantii, ni lini tutaondoka,” alisema.

  Sherehe hizo zilihudhuriwa na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally; Wajumbe wa Baraza la Ulamaa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe; Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mama Anna Mghwira; IGP Mstaafu, Bw. Said Mwema; Mbunge wa Moshi Mjini, Bw. Jaffary Michael; Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.

  0 0

  Picha mbalimbali zikimuonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri leo tarehe 26/06/2017 Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika Ikulu Mjini Unguja leo kumtakia Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) pampja na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika Ikulu Mjini Unguja leo kumtakia Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wakiitikia Dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibae Sheikh Saleh Omar Kabi,(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pampja na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi wakiaagana na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika Ikulu Mjini Unguja leo baada ya kutakiana Kheri katika Sikukuu ya Eid El Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na Mjukuu wake Ali Abdalla Mitawi katika Kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akifanya mahojiano na Watoto Nabil Mohamed Said na Ahmed Mohamed Said (kushoto) waliofika Ikulu Mjini Unguja kutoka Shirika la Utangazaji ZBC kwa ajili ya kutayarisha Kipindi cha Watoto sambamba na Sikukuu ya Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
  Baadhi ya Akinamama na Watoto waliofika katika viwaja vya Ikulu Mjini Unguja kwa ajili ya kusalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) na Kupokea Mkono wa Eid katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mzee Juma Kesi (kulia) alipojumuika na Wazee mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mzee Salum Othman Haji (kulia) alipojumuika na Wazee mbali mbali waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)alipokuwa akitoa Sikukuu kwa Mtoto Othman Khamis (mwenye ulemavu) alipojumuika na Wazee mbali mbali na Wananchi waliofika katika viwanja vya Ikulu Mjini Unguja kupokea mkono Eid el Fitri katika kusherehekea Sikukuu ya Eid el Fitri iliyoanza leo baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.

  0 0

  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba akizungumza wakati wa baraza la Eid lililofanyika kwenye shule ya Sekondari Jumuiya mjini Tanga kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella kushoto ni Shehe wa mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza katika baraza hilo kushoto ni  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
  Shehe wa mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akizungumza katika baraza hilo ambapo aliwataka waislamu kuendelea kutenda mambo mema kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba na mkuu wa mkoa wa Tanga,Martine Shigella
   Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akilakiwa na waumini wa dini ya kiislamu wakati akipokwenda kwenye baraza la Eid ambalo lilifanyika katika shule ya Sekondari Jumuiya
   Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba akilakiwa na waumini wa dini hiyo wakati alipokwenda kwenye Baraza la Iddi ambalo lilifanyika katika shule ya sekondari Jumuiya
   Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika Baraza hilo
   Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo
    Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo
    Sehemu ya waumini wakimsikiliza Waziri Makamba kwenye Baraza hilo leo
   Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira January Makamba kulia akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella
   Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Inastaajabisha kuona watu wa mataifa ya nje wanajua vitu vingi zaidi vinavyopatikana Tanzania kuliko watanzania wenyewe. Sijui ni ile hulka ya kutopenda kufuatilia mambo au ni dhana kwamba waache wageni waje kushangaa maana hivyo vitu vitaendelea kuwepo tu.
  Nchi yetu imebarikiwa na inaendelea kubarikiwa kugunduliwa kwa mambo mengi zaidi ya kustaajabisha ambayo hayapatikani kwingineko duniani. Jumia Travel ingependa kukufumbua macho kwamba yafuatayo ni baadhi tu ya mambo yanayopatikana na unaweza kuyashuhudia ukiwa nchini Tanzania.
  Mti mrefu zaidi barani Afrika. Hivi karibuni mtafiti kutokea Chuo Kikuu cha Byreuth cha nchini Ujerumani, Dkt. Andreas Hemp baada ya utafiti wa takribani miaka 20 amethibitisha kuwa Tanzania ina mti mrefu zaidi kuliko yote barani Afrika ukiwa na urefu wa mita 81.5. 

  Mti huo kwa jina la kitaalamu unajulikana kama ‘Entandrophragmaexcelsum’, ni aina adimu sana ya miti na inaweza kuwa na umri wa zaidi ya miaka 600. Ili kuweza kuuona mti huo unaopatikana katika safu ya misitu ya Mlima Kilimanjaro na kuwa kivutio kikubwa kwa watalii hivi sasa, itakupasa utembee umbali wa masaa 2.30 mpaka kutokea kijiji cha Tema ili kuufikia.

  Twiga mweupe aonekana kwa mara ya kwanza.  kubisha kwamba hiko kitu hakiwezekani lakini ndio maajabu ya Mungu hayo, twiga mweupe ameonekana Tanzania. Takribani mwaka mmoja uliopita, mwanzilishi na mwanasayansi katika Taasisi ya Misitu Asilia katika hifadhi ya taifa ya Tarangire inayopatikana mkoani Manyara, Dkt. Derek Lee alimuona twiga mwenye rangi nyeupe. Twiga huyo ambaye alikuwa na umri wa miezi 15 amepewa jina la ‘OMO,’ rangi yake inaonekana kama vile imechubuliwa tofauti na rangi asilia ya twiga tunaowajua. Mtafiti huyo amesema kuwa twiga huyo anasumbuliwa na ‘leucism,’ ni hali inayosababisha kupotea kwa baadhi ya rangi. Licha ya utofauti huo na wenzake lakini bado mnyama huyo anajichanganya na wengine na wenzie kutojali utofauti huo kabisa.   
   
  Asilimia 30% ya ardhi ya Tanzania ni hifadhi za wanyama pori. Kama ulikuwa haujui basi ni kwamba nchi ya Tanzania sehemu ya asilimia 30 ya ardhi yake ni hifadhi za wanyama pori wa aina mbalimbali duniani. Tanzania inazo hifadhi za taifa 16 ambazo zinasimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ambapo kwa ujumla wake zina ukubwa wa kilometa za mraba takribani 42,000. Kwa mfano, hifadhi ya taifa ya mbuga ya Serengeti ni mojawapo ya mbuga maarufu na inayopendwa zaidi duniani, ni makazi ya aina mbalimbali za wanyama zaidi ya milioni moja. Pia imetangazwa kuwa ni Eneo la Urithi wa Dunia na kutajwa mojawapo ya sehemu ya Maajabu Saba ya Dunia.
   
  Takribani wanyama milioni 2 hushiriki tukio la kuhama linalotokea kila mwaka mbuga ya Serengeti. Kila mwaka watalii hushuhudia tukio la kipekee la uhamaji wa makundi ya wanyama wa aina ya pundamilia na nyumbu zaidi ya milioni 1.5. Tukio hilo hutokea kati ya Kusini mwa bonde la mbuga ya Serengeti nchini Tanzania kuelekea eneo la Kaskazini mwa mbuga ya Masai Mara iliyopo Kenya.

   Lengo kubwa la tukio hilo ni katika harakati za kutafuta malisho mazuri kwa wanyama hao ambalo hutukia mnamo miezi ya Mei mpaka Desemba ingawa muda huwa unaweza kubadilika. Sehemu inayosisimua zaidi ni pale wanyama hao wanakatisha mto Mara kuuvuka kuelekea Masai Mara, wanyama hao kwa makundi na ujasiri mkubwa huvuka licha ya kuwa na mamba wakali.   
  Mbuyu unaweza kuishi mpaka miaka 1,000. Mibuyu ni miti mikubwa na inayovutia zaidi, hapa nchini Tanzania unaweza kuiona vizuri zaidi ukitembelea hifadhi ya taifa ya Tarangire. Kama ulikuwa haufahamu ni kwamba baadhi ya aina ya miti ya mibuyu huweza kuishi kwa takribani miaka 1,000 au zaidi. Inasemekana mbuyu mkongwe zaidi unapatikana nchini Afrika ya Kusini ni unaaminika kuwa na miaka takribani 6,000.  
   
  Uwepo wa vitu hivyo Tanzania ni uthibitisho wa namna nchi hii ilivyobarikiwa na vivutio mbalimbali ambavyo watu wengi hawavifahamu bado. Kwa hayo machache Jumia Travel inaamini utakuwa umejifunza na kupata shauku ya kutembelea maeneo hayo pamoja na kukuongezea ari ya kujifunza mengineyo zaidi.

  0 0


  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakiwa kwenye foleni kushiriki futari pamoja na watoto wa kituo cha Umra Orphanage kilichopo Magomeni Jijini Dar es Salaam
  Watoto wa kituo cha Umra Orphanage kilichopo Magomeni wakipata futari iliyoandaliwa na kampuni ya Tigo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar Es Salaam.
  Watoto wa kituo cha Umra Orphanage kilichopo Magomeni wakiwa katika foleni kupata futari iliyoandaliwa na kampuni ya Tigo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar Es Salaam.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Tigo wakiwa kwenye foleni kushiriki futari pamoja na watoto wa kituo cha Umra Orphanage kilichopo Magomeni Jijini Dar es Salaam
  Watoto wa kituo cha Umra Orphanage kilichopo Magomeni wakipata futari iliyoandaliwa na kampuni ya Tigo mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar Es Salaam.

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii-Kanda ya Kaskazini.

  Wachezaji 30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro ,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari.

  Rekodi nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) Jonesia Rukyaa  kuchezesha mchezo huo  wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila kufungana .
  Kundi la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
  Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
  Mhifadhi Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
  Wachezaji wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
  Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
  Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.

  0 0


  0 0

  Waumini wakiwa nje ya Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani wakisubiri kuswali swala ya Iddi El Fitri, jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
  Waumini wakiswali swala ya Iddi El Fitri kwenye Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, jijini Dar es Salaam leo. Swala hiyo iliongozwa na Msaidizi wa Imamu Mkuu, Sheikh Ally Bakari, hotuba ikasomwa na msaidizi wa pili wa Imamu, Sheikh Abubakar Khamisi na mawaidha yakatolewa na Imamu Mkuu, Sheikh Muhammad Idd Muhammad.
  Waumini wakiwa kwenye Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, jijini Dar es Salaam, wakisikiliza hotuba ya swala ya Iddi El Fitri iliyokuwa ikitolewa na Msaidizi wa pili wa Imamu, Sheikh Abubakar Khamisi.
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitoa tafsiri ya hotuba ya Swala ya Iddi El Fitri. 
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitoa tafsiri ya hotuba ya Swala ya Iddi El Fitri.  
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitoa mawaidha wakati wa Swala ya Iddi El Fitri.  
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitoa mawaidha wakati wa Swala ya Iddi El Fitri.  
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akimpa mkono wa Iddi El Fitri mmoja wa watoto waliofika msikitini hapo.  
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akipiga picha na mmoja wa waumini wakati wa kutakiana heri ya Sikukuu ya Iddi El Fitri na waumini. 
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitakiana heri ya Sikukuu ya Iddi El Fitri na watoto waliofika katika msikiti huo kwa ajili ya swala ya Iddi El Fitri. 
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitakiana heri ya Sikukuu ya Iddi El Fitri na waumini. 
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni kwa Mnyamani, Sheikh Muhammad Idd Muhammad, akitakiana heri ya Sikukuu ya Iddi El Fitri na waumini.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRNalipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na na watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB)waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017

  0 0

  IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imeanza mikakati ya kukabiliana kwa vitendo na wimbi la wahamiaji haramu kuingia mkoani hapa kwa kuanzisha kizuizi eneo la Mkata wilayani Handeni kwa muda wa saa 24. 

  Hayo yalibainishwa na Afisa Uhamiaji Mkoani Tanga DCI, Crispin Ngonyani wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mipango waliojiwekea kuzibiti vitendo vya namna hiyo. 

  Alisema wameamua kuanzisha mpango huo kutokana na asilimia kubwa ya wahamiaji haramu hao wanapokuwa wamefika kwenye eneo hilo la kizuizi wanashushwa na kupakia pikipiki maarufu kama bodaboda na kuingia mkoani Tanga. 

  “Kutokana na hali hiyo ndio maana tumeamua kuweka kizuizi hicho ambacho kimekuwa ni eneo ambalo linatumika kuwafaulisha wahamiaji haramu kwenye pikipiki maarufu kama bodaboda kwa lengo la kuzibiti suala hilo kwa vitendo “Alisema. 

  Aidha pia alisema hivi sasa wamejipanga kuhakikisha wanadhibiti maeneo yote ambayo yamekuwa na mianya ya kutumia kwa ajili ya kupitia ili kuweza kuhakikisha hawaingii mkoani Tanga. 

  “Lakini pia tuwatake wananchi kuhakikisha wanawafichua wahamiaji haramu pindi wanapokuwa wakiwaona kwenye maeneo yao kwani wamekuwa na madhara makubwa hivyo wanapaswa kutoa taarifa kwa mamlaka husika “Alisema. 

  Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa iwapo watabaini kuwepo kwa watu wasiowaelewa kwenye maeneo yao ili hatua kali ziweze kuchukuliwa.


  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0  MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi
  Robert Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative kulia ni Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu na Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada
  nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka 
  Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu kushoto akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka 
  Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka akizungumza katika halfa hiyo 
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Gorge Nyaronga akizungumza katika halfa hiyo 
  MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel kushoto akimpatia zawadi ya kitenge  Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu akimshukuru kwa msaada wa ujenzi wa madarasa na vyoo na uzio 
  Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu katikati akitazama kitenge chake 
  Risala ya shule hiyo ikisomwa 
  Sehemu ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Jitengeni wilayani Korogwe wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
  MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
  SERIKALI wilayani Korogwe Mkoani Tanga imepania kuhakikisha wanakomesha vitendo vya mimba za utotoni kwa kuwachukulia hatua kali watakaobinika kuhusika na matukio hayo ili kuweza kuondosha hali hiyo kwenye jamii.

  Lakini pia imesema watakaohusika kuwa kichocheo cha ndoa hizo zifanyike wakiwemo wazazi kutoka pande zote mbili watafikishwa mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake zaidi kwa lengo la kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.

  Hayo yalibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe ,Mhandisi,Robert Gabriel wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
  .

  Alisema hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha wanakomesha vitendo vinavyofanya na baadhi ya vijana vya kuwa sha wishi wananfunzi wa kike na kuwapatia ujauzito hivyo kupelekea wasichana hao kukatisha masomo yao.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema hivi sasa lazima wawe wakali na watu wanaocheza na maisha ya watoto ya wanafunzi ambao asilimia kubwa masomo yao yana haribiwa mara tu baada ya kushawishiwa na kupewa ujauzito.

  Alisema hatua ya kurubuniwa watoto wa kike kwenye masomo haiwezi kuvumiliwa hasa kipindi hiki ambacho hawatakuwa na nafasi tena ya kujiendeleza katika shule za serikali pindi watakapo jifungua.

  Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ,Mkuu wa shuele ya msingi Jitengeni,Mafikiri Twinzi alisema umalizikaji wa madarasa hayo utapunguza kero kwa wanafunzi shuleni hapo ambapo awali walikuwa wakikaa wanafunzi 100 hadi 120 kwenye chumba kimoja.

  Alisema shule hiyo iliyo na wanafunzi 816 imekuwa na tatizo la
  uchakavu wa madarasa hali iliyopelekea kuwajengea woga wanafunzi wa kuangukiwa na kuta za shule hiyo.

  Naye kwa upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka alisema taasisi hiyo lengo lake ni kuisadiana na serikali katika kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya na maji.

  Aidha alisema baada ya kumalizika kwa ujenzi wa madarasa hayo,matundu ya vyoo,uzio pamoja na kuweka mabomba ya maji na sasa mpango uliopo ni kuendelea kuvunja madara manne mengine yaliyochakaa shuleni hapo ili kujenga upya na kutoa fursa kwa wanafunzi kujisomea bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yeyote ile.

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

older | 1 | .... | 1284 | 1285 | (Page 1286) | 1287 | 1288 | .... | 1898 | newer