Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog



Channel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1282 | 1283 | (Page 1284) | 1285 | 1286 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Azzan Zungu  akiongoza kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 23, 2017.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk Ashatu Kijaji  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 23, 2017.
   Naibu Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng Stella Manyanya akijibu maswali mbalimbali ya wabunge  katika kikao cha hamsini na nne  cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 23, 2017.
   Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 23, 2017.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akijadili jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk Ashatu Kijaji  katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 23, 2017.
   Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof Jumanne Maghembe akiteta jambo na Mbunge wa Viti Maalum Bi Martha Mlata   katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 22, 2017.
   Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi  wakifuatilia jambo na Mbunge wa Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy  katika kikao cha hamsini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 23, 2017.
  Naibu Waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwelwe  akimskiliza Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe. Daniel Nsanzugwako  katika kikao cha hamsini na nne  cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 23, 2017.

  Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea Tanzania itakavyokuwa wenyeji wa kuandaa Kongamano la ‘Global Logistics Summit 2017’ linalotarajia kufanyika Agost 23-26, 2017 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna.
  Kongamano hili la kiulimwengu litakaribisha zaidi ya wageni 350 wakiwa mawakala wa kusafirisha mizigo, wajumbe wa kibiashara, washiriki wa kibiashara, maafisa wa serikali, mabalozi kutoka ukanda wa Afrika na Mashariki ya Kati, n.k. Zaidi ya nchi 32 toka ulimwengu mzima zinategemewa kuhudhuria na kushiriki mkutano huu toka dunia nzima. Mhe. Prof. Makame Mbarawa ameipongeza TAFFA kwa jitihada zake za kutengeneza ufahamu ambao ulihitajika kwa muda mrefu katika sekta ya uchukuzi ambayo ni muhimu katika taifa lolote sababu inawezesha usafirishaji wa watu na mizigo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea Tanzania itakavyokuwa wenyeji wa kuandaa Kongamano la ‘Global Logistics Summit 2017’ linalotarajia kufanyika Agost 23-26, 2017 jijini Dar es Salaam. Kulia ni Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), Stephen Ngatunga na kushono ni makamu wa Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), Edward Urio.
  Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa akitilia msisitizo jambo.
  Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), Stephen Ngatunga (kulia) alisema kuwa Kongamano hili pia litaiwezesha Tanzania kupata fursa ya kukuza uchumi wake kupitia sekta ya usafirishaji na usambazaji na baadhi ya maswala kama uboreshaji wa bandari na kuifanya iwe ya kisasa, kuongeza vyanzo vya mapato na changamoto zingine zitapewa kipaumbele kwenye majadiliano. 

  Kongamano hili linafanyika wakati ambao wafanyabiashara wa Kitanzania wanahitaji uelewa zaidi pamoja na maarifa kuhusu njia bora za utendaji kazi zinazotumika katika dunia hii ya kidijitali ambapo teknolojia inatawala. Kwa hakika kuna fursa nyingi za ukuzaji wa biashara Tanzania kwa maana ya usafirisaji na uhifadhi wa mizigo hasa katika nchi zisizo na bahari kama Burundi, DRC, Rwanda, Zambia, Malawi na Uganda zinaweza kutumia bandari ya Dar es Salaam kama njia ya usafirishaji mizigo.

   “Sisi kama TAFFA tunapiga hatua kuhakikisha tunaziwezesha biashara kupitia kongamano hili la GLS ambapo wadau mashuhuri na waliobobea katika fani hizi watatoa maarifa bora kwa wasafirishaji wa kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa sisi kuwa wenyeji wa mkutano huu wa kiulimwengu. Tunafurahia sana kupata fursa hii ambayo itaitangaza Tanzania kama kituo kizuri cha usafirishaji.” Alielezea Ngatunga.

   “Hii ni fursa muhimu kwa taasisi yoyote yenye maslahi na sekta ya usafirishaji iwe kama, wakala, kampuni ya bima, mtoa huduma, mwanasheria, mtoa bidhaa ama afisa biashara kutengeneza wigo na mahusiano ya kibiashara. Tunataka kuionyesha dunia kupitia mkutano huu kwamba Tanzania ni sehemu sahihi kwa biashara za ukanda huu.

  0 0

  Kambi ya Watoto na Vijana “Ariel Camp” iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi nchini Tanzania iliyoanza June 19,2017 jijini Mwanza, imefungwa leo Ijumaa June 23,2017.
  Kambi hiyo ilikutanisha watoto na vijana 50,walezi 11 walioambatana nao kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita.
   
  Miongoni mwa mambo waliyojifunza katika kambi hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tano, ni pamoja na masuala ya lishe,ufuasi mzuri wa dawa,stadi za maisha,unyanyapaa na ubaguzi,haki na wajibu wa watoto pamoja na elimu ya afya ya ujana na makuzi.
   
  Washiriki wa kambi hiyo pia walitembelea makumbusho ya Wasukuma ya Bujora na kufanya michezo mbalimbali nje ya darasa yenye kuashiria umoja,ushirikiano,upendo na kujenga mtazamo chanya kwenye maisha yao.
  Akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel jijini Mwanza,mgeni rasmi,Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Silas Wambura,aliwataka watoto na vijana hao kuwa mabalozi wazuri wanaporudi nyumbani huku akiwasihi kuzingatia masomo na kanuni za afya ili kufikia malengo yao ya kimaisha.
   
  Aidha, Dk. Wambura alisema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na shirika la AGPAHI katika sekta ya afya na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao ili watanzania wengi zaidi waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na shirika hilo hususani katika mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.
   
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela alisema takribani watoto na vijana 400 wameshapata fursa ya kushiriki Kambi ya Ariel tangu shirika hilo lilipoanzishwa mwaka 2011,ambapo washiriki hutoka kwenye klabu za vijana na watoto kwenye mikoa ambayo AGPAHI inafanya kazi zake.

  “Mshiriki wa kambi lazima awe mwanachama wa klabu za vijana na watoto,lakini kwa mikoa hii mipya (Mwanza,Geita,Tanga na Mara),shirika liliamua kuwachukua vijana,watoto na walezi kushiriki kwenye kambi ndipo baadae uanze mchakato wa kuunda klabu/vikundi ili kutoa huduma za kisaikolojia kwa watoto”,aliongeza Dk. Telatela.
   
  “Hii ni kambi ya nane tangu kuanza kwa shirika letu ,tulianza kufanya kazi katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu,na kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016,tuliongeza mikoa minne ya Mwanza,Tanga,Geita na Mara hivyo kufikisha idadi ya mikoa sita ambako tunafanya kazi”,alieleza Dk. Telatela.
   
  Katika hatua nyingine alisema shirika la AGPAHI linatekeleza majukumu yake kwa hisani ya Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease Control and Preventation (CDC),mfuko wa kusaidia Watoto wenye VVU kwa hisani ya Watu wa Uingereza (CIFF) na Shirika la Development Aid From People to People (ADPP – Mozambique).
   
  ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA KUFUNGA KAMBI YA ARIEL MWAKA 2017 JIJINI MWANZA.
  Washiriki wa Kambi ya Ariel 2017 wakiandamana kuelekea ukumbini wakati wa kufunga kambi hiyo leo Ijumaa June 23,2017 katika Hoteli ya Lesa Garden jijini Mwanza.
  Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akitambulisha washiriki wa kambi ya Ariel kwa mgeni rasmi wakati wa kufunga kambi hiyo.
  Mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura akitoa hotuba wakati wa kufunga kambi ya Ariel mwaka 2017.
  Dk.Wambura akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel.Wa kwanza kulia ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Mwanza, Olympia Laswai akifuatiwa na Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela.Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Miradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Dk. Gastor Njau akifuatiwa na Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita Dk. Joseph Odero.
  Watoto na vijana wakinyoosha mikono juu baada ya kuulizwa na Dk. Wambura kama wamefurahia kambi ya Ariel.
  Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel jijini Mwanza. Alisema watoto na vijana walioshiriki kambi ya Ariel ni wale walioko kwenye umri balehe (miaka 10 – 17).
  Washiriki wa kambi ya Ariel wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea.
  Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela akizungumza wakati wa kufunga kambi ya Ariel.
  Watoto na vijana wakiimba na kucheza wimbo mbele ya mgeni rasmi,Dk. Silas Wambura.
  Vijana wakicheza muziki.
  Mtoto akionesha vazi la ubunifu kwa kutumia magazeti alilolitengeneza akiwa kambini baada ya kufundishwa somo la stadi za maisha.
  Mtoto akielezea jinsi alivyofurahishwa na mambo mbalimbali akiwa kambini.
  Mtoto akitoa ushuhuda wa mambo aliyojifunza akiwa kambini.
  Vijana wakionesha igizo kuhusu ugonjwa wa Ukimwi.
  Keki maalum kwa ajili ya washiriki wa kambi ya Ariel mwaka 2017.
  Mgeni rasmi,Dk. Silas Wambura,Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela na watoto walioshiriki Kambi ya Ariel wakikata keki.
  Mgeni rasmi / Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura akimlisha keki mtoto.
  Mtoto akimlisha keki mgeni rasmi Dk. Silas Wambura.
  Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela akilishwa keki na mtoto.
  Muelimisha rika Mahene James kutoka Mwanza akishikana mkono na Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura wakati akipokea cheti cha ushiriki wa kambi ya Ariel.
  Mtumishi wa afya kutoka mkoa wa Shinyanga aliyeambatana na watoto na vijana kutoka Shinyanga,Glory Assey akishikana mkono na Mkurugenzi wa Miradi AGPAHI, Dk. Safila Telatela baada ya kupokea zawadi ya cheti cha ushiriki wa kambi ya Ariel.
  Mtumishi wa afya kutoka mkoani Geita Awipu Piniel akipokea zawadi ya cheti cha ushiriki wa kambi ya Ariel.
  Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura akiangalia michoro ya miti ya maisha iliyochorwa na watoto na vijana walioshiriki kambi ya Ariel wakielezea kwa ufupi mambo wanayoyapenda katika maisha yao.
  Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dk. Silas Wambura akiendelea kuangalia michoro ya miti ya maisha ya washiriki wa kambi ya Ariel. Kushoto ni Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Geita, Dk. Joseph Odero akiangalia michoro hiyo.
  Kijana akimwelezea Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Dk. Silas Wambura kuhusu mti wake wa maisha aliochora kuhusu historia yake ya maisha.
  Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Geita,Richard Kambarangwe akimwelezea mgeni rasmi,Dk. Wambura kuhusu shindano la ‘Mkali Wao’ ambapo washiriki hushindanishwa katika masuala mbalimbali mfano kujiamini,ucheshi,usikivu, utulivu,uchezaji mzuri wa muziki,kujibu maswali vizuri,uongozi mzuri,kutunza muda,nidhamu na utii na uchangamfu kambini na mshindi anayepatikana hupigwa picha katika bango hilo.
  Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na washiriki wa kambi ya Ariel. 
  Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na wafanyakazi wa AGPAHI.
  Picha ya pamoja: Mgeni rasmi na watumishi wa afya waliombatana na watoto na vijana kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita.
  Watumishi wa afya waliombatana na watoto na vijana kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza na Geita wakiwa katika picha ya pamoja.
  Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

  0 0


  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  WAKATI siku ya Wiki ya Utumishi wa Umma imefikia kilele leo Juni 23, 2017, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, aliiacha ofisi yake na kujiunga na kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Mfuko huo Makao Makuu ya PPF barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam ambapo alifanya kazi ya kuwahudumia wateja.

  Awali Bw. Erio alizungumza na baadhi ya wanachama wa Mfuko waliofika kwenye kitengo hicho kuhudumiwa, na kusikiliza maoni yao ni jinsi gani wanahudumiwa na Wafanyakazi wa Kitengo hicho.

  Idha Mkurugenzi Mkuu Erio pia aliwahudumia wanachama wengine akiwemo mzee Clemence Munisi ambaye ni mstaafu wa kampuni ya Narco.

  Kwa mujibu wa Mzee Munisi, yeye alisema, amefurahishwa na huduma zitolewazo na Mfuko ambapo zimekuwa ni za haraka na zisizokuwa na usumbufu.

  Baada ya kutembelea kitengo hicho, Bw. Erio alikutana na baadhi ya wafanyakazi ili kusikiliza maoni yao kuhusu namna uongozi wa Mfuko unavyoshirikiana na wafanyakazi katika kulihudumia taifa.

  “Kama mjuavyo hii ni siku ya mwisho ya wiki ya utumishi, nimeona nikutane nanyi ili kuwasikiliza, maana mara nyingi sisi viongozi ndio tunasema tu, lakini leo ni zamu yenu ninyi watumishi kusema jambo lolote linalohusu Shirika letu, lakini hata wewe binafsi kama mfanyakazi.” Alisema Bw. Erio.

  Bw. Erio pia aliwakumbusha wafanyakazi kuwajibika ipasavyo katika kuwahudumia wananchi, lakini pia kuzingatia suala la afya bora.

  “ Ili uweze kuwahudumia vema wananchi, ni lazima uwe na afya bora, mimi kama mwenyekiti wa kamati ya UKIMWI ya shirika letu, bado nasisitiza, chukueni tahadhari kubwa, kwani ugonjwa huu bado upo ingawa hauzungumzwi sana kwa sasa.” Alionya Bw. Erio.

  Bw Erio pia aliwataka wafanyaakzi hao kutojihusisha kwa namna yoyote na matumizi ya madawa ya kulevya au biashara ya madawa ya kulevya.

  Mimi siko serikalini, lakini ninao wajibu kama kiongozi wenu, kuwakumbusha mambo ambayo jamii inapaswa kujiepusha nayo, na nyinyi kama sehemu ya jamii, hamna budi kutojihusisha kwa namna yoyote na matumizi au biashara ya madawa ya kulevya.” Alisema.

  Kwa upande wao wafanyakazi walishukuru uongozi wa Mfuko kwa kuwa karibu na wafanyakazi.

  “Ukiona hupati maneno mengi ujue mambo yako poa, sisi kwakweli tunashukuru sana kwa kiongozi kama wewe kuja kusungumza nasi tena kwa kutusikilzia sisi tuna lipi la ksuema, lakini nikuhakikishie tu kwa niaba ya vijana wenzangu, mimi naona mambo yako safi na sikukuu hii tutasherehekea kwa furaha kabisa.” Alisema mfanyakazi mmoja kutoma idara ya fedha, Bw.Joseph Fungo.

  Naye Meneja wa fedha wa PPF, Bw.Dozitte Msoffe, yeye alisema, mahusiano mema kati ya uongozi na wafanyakazi ndiyo yanayoboresha utoaji huduma kwa wananchi na kwa PPF, kumekuwepo na mahusiano mazuri sana baina ya pande hizi mbili kwa hivyo mimi nikupongeze tu ndugu Mkurugenzi Mkuu, kwa uamjzi wako wa kuja kutusikiliza hii huwezi kuisikia mahala pengine, lakini hapa PPF imetokea hongera sana.” Alisiema Bw. Msoffe.

   Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (kushoto), akismikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, Bw.Clemence Munisi, aliyefika kitengo cha huduma kwa wateja ili kuhudumiwa wakati wa kilele cha wiki ya utumishi Makao Makuu ya PPF Barabara za Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam, Ijumaa Juni 23, 2017.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, aliiacha ofisi yake na kujiunga na kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Mfuko huo Makao Makuu ya PPF barabara ya Samora na Morogoro jijini Dar es Salaam ambapo alifanya kazi ya kuwahudumia wateja.
   Bw. Erio akizungumza na baadhi ya wanachama waliofika kitengo cha huduma kwa wateja cha Mfuko huo ili kupaiwa huduma
   Meneja wa Fedha wa PPF, Bw. Dozitte Msoffe akizungumza. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele.
   Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Bw. Erio
   Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (katikati), akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko huo Makao Makuu, PPF House, barabara ya Samora/Morogoro jijini Dar es Salaam, Ijumaa Juni 23, 2017 wakati wa kilele cha wiki ya utumishi. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mfuko huo, Bi.Gladness Mteta, na kulia ni Kaimu Katibu M,uu wa TUICO, Bw.Laurent Mwombeki.
   Bw. Msoffe akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio na watumishi wengine wakimsikilizia
   Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Bw. Erio kwa makini
   Afisa Fedha wa PPF, Bw. Joseph Fungo akizungumza
   Baadhi ya wafanyakazi wakipiga makofi kufuatia mazungumzo mafupi ya Bw. Erio
  Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bi. Gladness Mteta, (kulia) akiwa na Meneja wa Huduma za Utawala wa PPF, Bi.Cecilia Obeid Katikaza.

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza na wananchi wa Jimbo hilo mara wakati wa futari iliyoandiandaa nyumbani kwake kwa wananchi
  Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza wakiwa na wageni waalikwa wakipiga dua
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa futari hiyo
  Wageni waalikuwa wakipata futari hiyo ambayo iliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu nyumbani kwake
   Wageni waalikuwa wakipata futari hiyo ambayo iliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu nyumbani kwake
   MNEC wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mkinga,Mwasingo naye akipata futari hiyo



  Mbunge wa Jimbo la Muheza(CCM) Balozi Adadi Rajabu akiwa na wananchi wa Jimbo lake wakipata futari
   Mwandishi wa AZAM TV mkoani Tang,Mariam Shedafa kulia na Anna Peter wakipata futari 
   Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto mwenye kikombe cha chai akipata futari na wageni wengine.
   Katiby Tawala wa wilaya ya Muheza (DAS) Desderia Haulekulia akipata futari na wageni wengine waalikuwa nyumbani kwa Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu

  Mbunge wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga,Balozi Adadi Rajabu kushoto akiteta jambo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati wa futari hiyo 
  Mbunge wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga,Balozi Adadi Rajabu akiagana na wananchi waliofika kupata futari nyumbani kwake
  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0





  0 0

  Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akipata Futari na waumini wengine katika Msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai baada ya kushiriki pia katika miskiti mingine mitatu .
  Mmoja wa viongozi wa Dini ya Kiislamu Mwl Mohamed Mbowe akizungumza wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe katika Msikiti wa Lambo .
  Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji ,Habib Nasiwa akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe kwa jitihada zake za kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali katika wilaya hiyo.
  Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akionesha zawadi ya Cheti alichokabidhiwa na Waislamu katika wilaya ya Hai.
  Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi zawadi ya Cheti kwa Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu ili afungue na kusoma kilichoandikwa ndani.
  Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu (Mwenye suti) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Cheti kilichotolewa na Waislamu wa wilaya ya Hai,kwa Mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe. 
  Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akishiriki Dua mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliyoandaliwa katika misikiti minne tofauti ukiwemo msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai.
  Baadhi ya wauimini wa Dini ya Kiislamu wakiwasiliza viongozi mara bada ya kushiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
  Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Helga Mchomvu wakati wa Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti.
  Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakipata Futari katika msikiti wa Kibaoni wilayani Hai.
  Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Omar Mohamoud akizungumza wakati wa hafla ya kupata Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
  Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki ,Fahad Lema akisoma Risala kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe mara baada ya kumalizika hafa ya kupaa futari kwa pamoja katika msikit wa Kibaoni wilayani humo.
  Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimiana na Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki Fahad Lema mara baada ya kuwasilisha ombi la kusaidiwa ujenzi wa vyumba vya madrasa ambapo Mh Mbowe alichangia kiasi cha Sh Mil,2 kwa ajili ya kununua mbao za kuezekea Paa.  
  Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimana na Waumini katika Msikiti wa Kibaoni uliopo Bomang'ombe wilayani Hai ,mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti katika jimbo hilo.

  Msikiti wa Lambo uliopo Machame ambao Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe amechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wake.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
  MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni,Mh ,Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali.
  “Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji  na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
  Mh Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo katika misikiti minne tofauti ya Modio ,Rundugai,Kibaoni na Lambo.
  Cheti hicho kilichosainiwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Sheakh ,Omary Mahmoud ambaye pia ni katibu wa msikiti wa Kibaboni Bomangombe kimetolewa ikiwa ni ni ishara ya kutambua mchango mkubwa unatolewa na Mbunge huo kwa Waislamu.
  AkIzinunguza mara baada ya kukabidi cheti hMjumbe wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa alitoa shukrani kwa niaba ya waislamu wa jimbo la Hai kwa namna ambavyo ameendelea kujitoa pamoja na kuchangia ujenzi wa msikiti wa Lambo.
  “Nimehemewa sana ,sidhani kama naweza kusema kiasi cha kutoshereza ,nimehemewa na kujaaa furaha ya kufikiwa na Mh Mbowe,halikua jambo rahisi la kumpata leo ,kwanza tukijua Bunge linaendelea kadharika tukijua kwamba ana majukumu mengine mengi lakini akaona ashiriki na sisi wilaya ya Hai.”alisema Nasiwa.
  “Jambo fupi la kukushirikisha jioni ya leo,mheshimwa tunakupongeza kwa kujua umuhimu wa ramadhan kwa kuacha shughuli zako na kuja kushiriki nasi katika kutufuturisha,tunakupa asante sana na mungu akubariki sana,”aliongeza Alhaji Nasiwa.
  Katika hafla hiyo ya kufuturisha ,Mh Mbwe alishiriki katika misikiti yote minne ambapokatika msikiti wa Mudio alitoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi inayomilikiwa na msikiti huo na pia alikabidhi kiasi cha sh Mil moja kwa msikiti wa Rundugai kwa ajili ya mwalimu anayefundisha masomo ya dini katika shule ya Msingi na Sekondari za Rundugai .

  0 0

  Maafisa wa Mamalaka ya Mapato Nchini (TRA) wameendelea  kufanya zoezi la ukaguzi wa maduka ya wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao pasipo kuwapatia risiti za mashine za Kielektroniki (Efd) jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo imeendelea kufanyika katika eneo la Kibiashara la Kariakoo na itakuwa endelevu kuhakikisha wafanya biashara wanazingatia sheria, kanuni na taratibu za biashara katika mauzo ya bidhaa zao. 
  Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart na askari polisi wakisimamia zoezi la kuingiza ndani bidhaa za wafanya biashara walikutwa wakiendelea kutoa huduma ilhali awali walikutwa wakiuza bidhaa hizo pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine. Hatua ya ukamatwaji kwa wafanya biashara hao inatokana na kitendo cha kutokuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot)

  Add caption
  Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart akifunga kofuli la wafanyabiashara walikamatwa katika Mtaa wa Aggrey Kariakoo Dar es Salaam wakifanya biashara bila pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine hiyo. Hatua ya kuwakamata wafanya biashara hao imetokana na kushindwa kuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Hivyo basi watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
  Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart akifunga kofuli kwenye lango duka la wafanya biashara waliokamatwa katika Mtaa wa Aggrey Kariakoo Dar es Salaam wakifanya biashara bila pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine. Hatua ya kuwakamata wafanya biashara hao imetokana na kushindwa kwao  kuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
  Afisa wa Mamlaka ya Mapato Nchini (kushoto) akisubiri mmiliki wa duka la urembo  lililokutwa likiendelea kufanya biashara hata baada ya kukutwa wakiuza bidhaa zao pasipo kutoa risiti za kielekroniki licha kuwa na machine inayotakiwa kutumika kwa utoaji wa risiti kwa wateja wao iliyotolewa na TRA. Hatua ya kuwakamata wafanyabiashara hao imetokana na kitendo cha uongozi wa duka hilo kutokuitikia wito wa TRA kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Wafanya biashara hao watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
  Wafanya biashara waliokamatwa eneo la Kariakoo Mtaa wa Congo Dar es Salaam, kwa kosa la kutoitikia wito wa mamlaka hiyo kwenda kulipia faini ya utoaji wa huduma pasipo kutoa risiti za kielektoniki licha ya kuwa na mashine wakifunga duka lao walipokamatwa na maofisa wa TRA Juni 22 2017. Kwa mujibu wa sheria za nchi wafanyabiashara hao watatakiwa kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.
  Afisa wa Kampuni ya Yono Auction Mart (kulia) na mmoja wa wafanya biashara wakifunga makofuli kwenye duka la madera katika mtaa wa Congo Kariakoo Dar es Salaam Juni 22 2017 baada ya kukutwa duka hilo likiendelea kutoa huduma ilhali awali walishakutwa wakiuza bidhaa hizo pasipo kutoa risiti ya kielektoniki licha ya kuwa na mashine ya risiti za kieletroniki (Efd). Hatua ya kuwakamata wafanyabiashara wa jinsi hiyo ilitokana na kitendo cha kutokuitikia wito wa mamlaka ya Mapato Nchini wa kwenda kulipa faini baada kufanya kosa hilo. Kwa kosa hilo watalazimika kulipa kati ya shilingi milioni 3 mpaka 4 na nusu ili waruhusiwe kuendelea na biashara.



  0 0


  0 0


  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

  Serikali imewashauri wakazi wa Wilaya ya Malinyi mkoa wa Morogoro, kutumia njia mbadala kupata huduma za kibenki ikiwemo kupitia simu za mkononi yaani (simbanking) ya CRDB na Banking on the Wheel ya NMB iliyoko Mlimba kwa kipindi hiki ambacho mchakato wa kufungua matawi rasmi ya benki unaendelea.

  Hayo yameelezwa Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Malinyi Dkt. Hadji Hussein Mponda (CCM), aliyetaka kujua ni lini huduma rasmi za kibenki zitaanzishwa katika wilaya ya Malinyi ama kama kulikuwa na mpango wa taasisi za fedha kuanzisha huduma za matawi ya benki yanayohamishika (mobile banking) wilayani humo.

  Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema kuwa, wilaya ya Malinyi ni moja ya wilaya ambazo zinanufaika na mfumo wa utoaji huduma kupitia mawakala wa Fahari Huduma (Malinyi SACCOS  na Zidua Waziri Shop) zinazoendeshwa na benki ya ‘CRDB Bank’ ambapo wateja wanapata huduma za kibenki ikiwemo kufungua akaunti,  kuweka na kuchukua fedha, kuomba mikopo na kupata ushauri wa huduma za kifedha.

  “Gharama za kuanzisha na kuendesha tawi kuwa kubwa Benki ya NMB na CRDB zinaendelea na upembuzi yakinifu kwa ajili ya kufungua tawi katika wilaya ya Malinyi utakaotoa mwelekeo wa kufungua tawi au la, kwa sababu Tawi linatakiwa liwe endelevu na kujiendesha kwa faida”. Alisema Dkt. Kijaji.

  Dkt. Kijaji aliongeza kuwa Serikali inatambua umuhimu wa wananchi wa Tanzania kupata huduma za kibenki karibu na maeneo yao na kwamba  huduma hizo lazima ziwe na faida kwa pande zote yaani kwa mabenki na wateja pia.

  Aidha Dkt. Kijaji alifafanua kuwa mabadiliko ya mfumo wa fedha nchini ya mwaka 1991, yaliitoa Serikali katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za mabenki nchini ili kuruhusu ushindani huru na kuwezesha kuboresha huduma  katika sekta ya fedha.

  Katika swali la nyongeza Mbunge wa Malinyi Dkt. Hadji Hussein Mponda (CCM), alitaka kujua namna Jeshi la polisi linavyoweza kuwasaidia wakazi wa wilaya hiyo wanaotembea na fedha nyingi kufuata huduma za kibenki mbali na wilaya hiyo ili wasipoteze mali zao.

  Akijibu swali hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha usalama katika maeneo hayo ili kuweka ushawishi kwa Taasisi za kifedha kuweza kufungua mabenki ili kupunguza changamoto ya huduma za kibenki.

  0 0

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (Wa tatu kulia), akifuatilia taarifa ya utekelezaji iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (Wa pili kulia) kabla ya kukutana na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.
  KIZ2
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Antony Mtaka (katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia), alipokuwa akizungumza nae kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Simiyu. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
  KIZ3
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na kulia kwake ni Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mathias Kabunduguru.
  KIZ4
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bw. Mariano Mwanyigu akitoa maoni wakati wa kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
  KIZ5
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akipata maelezo ya usindikaji maziwa kutoka kwa Mthibiti Ubora wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bw. Gerald Baruti alipotembelea Kiwanda cha kusindika Maziwa (Meatu Milk) kilichoanzishwa na vikundi vya vijana kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
  KIZ6
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiangalia bustani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, alipotembelea shughuli za maendeleo za Wilaya ya Meatu ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kushoto kwake ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Bi. Upendo Naftali.

  0 0



   
   Mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi misaada kwa Mwenyekiti wa Taasisi  inayoshughulikia masuala mbalimbali ya Wajane na Watoto Yatima ijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya, Ahmed Chebe ya Mwanayamala B jijini Dar es Salaam. Jokate ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi kilo 250 za unga na mchele, mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za watoto wa kike na wa kiume, mafuta yakupikia na  nguo za watu wazima kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa faraja zaidi.
  1
  Mmoja wa wajane wa Taasisi  ya Ahbaabul Khairiya, Nawili Saidi akibeba nguo mbalimbali zilizotolewa na Mwanamitindo, Jokate Mwegelo kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr.
  2
  Jokate akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kituo cha Ahbaabul Khairiya  pamoja na wajane na yatima.
  3
  Wanawake wajane wakimshukuru Jokate mara baada ya kutoa msaada katika kituo hicho.
  …………………..

  Mwanamitindo, Miss Tanzania namba mbili 2006 na mbunifu wa mavazi, Jokate Mwegelo ametoa sadaka ya sikukuu ya Eid El Fitr kwa taasisi ya wanawake wajane na watoto yatima ilijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya cha Mwanayamala B jijini Dar es Salaam.

  Jokate ametoa zawadi hiyo kwa kituo hicho chenye jumla ya wajane 32 na watoto yatima 41 kama sehemu ya kuwafanya wajane na yatima hao kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa faraja zaidi.

  Mrembo huyo ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi kilo 250 za unga na mchele, Mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za watoto wa kike na wa kiume, mafuta yakupikia na  nguo za watu wazima.

  Amesema kuwa ameguswa na changamoto za kituo hicho ambacho kimefanya kazi kubwa kujua changamoto mbalimbali za wajane na watoto yatima wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

  “Nimegushwa sana na kuamua kidogo nilichonacho kugawana na ninyi, sikukuu ya Eid El Fitr inakaribia na natarajia kila mmoja wetu atasheherekea kwa faraja zaidi, naomba mpokee msaada huu na matarajio yangu ni kuendelea kuwasaidia pindi ninapata nafasi,” alisema Jokate.

  Mmoja wa wasanii wa luninga nchini, Juma Chikoka ambaye alikuwa katika makabidhiano hayo alitoa wito kwa jamii kuunga mkono juhudi za Jokate za kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

  Mwenyekiti (Amiri) wa Taasisi hiyo, Ahmed Shebe alimshukuru Jokate kwa msaada huo na kuomba wadau mbalimbali kujitokeza kutatua changamoto hizo.

  “Taasisi inahudumia wajane wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, wapo wengine Chalinze na Bagamoyo mbali ya hapa wa jijini, tunajitahidi kutafuta michango sehemu mbalimbali ili kuweza kuondoa changamoto hizi, hata hivyo bado hatujafikia lengo, tunahitaji msaada kwa wasamaria ili kuwapa faraja zaidi,”

  “Kuna wajane wanaosaidiwa kulipia kodi yay a nyumba na watoto yatima wanaolipiwa ada, hatuna uwezo mkubwa wa kufanya hivyo na zaidi fedha za msaada zinatokana na michango yetu,” alsema Shebe.

  0 0


  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu (katikati) akiongea na wadau (hawapo pichani) katika kikao cha wadau hao  kilichojadili namna bora ya kuboresha mahusiano kati ya TEMESA na wadau hao kilichofanyika  katika ukumbi wa MT Depot jijini Dar es Salaam, Kikao hicho ni maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma nchini, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko na kushoto ni Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Bw. Slylivester Semfukwe
  1
  Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Bw. Sylivester Semfukwe kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) akitoa ufafanuzi kutoka kwa wadau (hawapo pichani) ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini, wa pili kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu.
  2
  MSTAHIKI MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akichangia mada katika Kikao  kilichojadili namna bora ya kuboresha mahusiano kati ya TEMESA na wadau hao kilichofanyika katika ukumbi wa MT Depot jijini Dar es Salaam, Kikao hicho ni Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini.
  3
  Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Hans Lyimo akiongea katika Kikao cha kujadili namna bora ya kuboresha mahusiano kati yao na TEMESA kilichofanyika katika ukumbi wa MT Depot jijini Dar es Salaam ikiwa ni Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini, wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Japhet Maselle.
  4
  Mdau wa TEMESA akitoa maoni katika  Kikao  kilichojadili namna bora ya kuboresha mahusiano kati ya TEMESA na wadau hao kilichofanyika katika ukumbi wa MT Depot jijini Dar es Salaam ikiwa ni Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini.
  5
  Mwanasheria Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Gatian Mali akitoa ufafanuzi wa Kisheria kwa wadau (hawapo pichani) katika kikao cha kuboresha mahusiano ya pande mbili ikiwa ni Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa MT Depot jijini Dar es Salaam.
  6
  Baadhi ya Wadau wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Mgwatu (watatu kutoka kulia waliokaa) mara baada ya kikao cha kuboresha mahusiano kati ya TEMESA na wadau hao kilichofanyika  katika ukumbi wa MT Depot jijini Dar es Salaam, Kikao hicho ni Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma nchini

  0 0

  Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo.
  Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubakary Zubery akitia aini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimajaro (KIA).
  Mufti Mkuu wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiteta jambo na Sheakh Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
  Msafara wa Mufti ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) .
  Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
  Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery.
  Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akiwasili katika mmoja wa miskiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
  Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akifungua kitambaa katika jiwe la Msini kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jingo hilo litakalo tumika kama Madrasa.
  Jengo la Ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai ambalo Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubakary Zubery amefika kwa ajili ya uzinduzi wake.
  Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai ka ajili ya ufunguzi wake.
  Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akizindua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
  Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akitia saini katika kitabu cha ageni mara baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
  Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai
  Mufti Mkuu wa Tanzania ,Abubakar Zubery akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika mskiti wa masjid Shafi kwa ajili ya uzinduzi.
  Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akizindua rasmi Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
  Katibu wa Bakwata wilaya ya Hai,Mwl Mohamed Mbowe akisoma risala wakati wa uzinduzi rasmi wa msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.
  Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akizungumza mara baada ya kuzindua Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0
 • 06/24/17--04:25: SALAMU ZA EID EL FITRI


 • 0 0


  Mlezi wa kituo cha watoto cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma Shekhe Mohamed Thabiti (kushoto) akipokea masaada wa vyakula kutoka kwa Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia) jana kampuni hiyo iliandaa futari kwa Watoto wa kituo hicho na kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5.

  Meneja wa tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia) akimkabidhi msaada mtoto Halima Bakari kwa niaba ya watoto wa kituo cha kulelea watoto cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma jana usiku wakati kampuni hiyo ilipoandaa futari kwa Watoto wa kituo hicho na kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5.

  Meneja wa tigo kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Dodoma ,Singida na Manyara Aidan Komba (kulia) akishiriki kugawa futari kwa Watoto wa kituo cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma jana usiku wakati kampuni hiyo iliandaa futari kwa Watoto wa kituo hicho na kukabidhi msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5.

  Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo wakishiriki futari ya jioni na watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Rahman Ophanage Centre cha mjini Dodoma jana usiku wakati kampuni hiyo iliandaa futari na kutoa msaada wa vyakula ,mafuta na sabauni vyote vikiwa na thamani zaidi ya milioni 1.5.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imekabidhi msaada wa chakula na kuandaa futari kwa ajili ya Watoto wanaishi kwenye kituo cha kulelea watoto cha Rahaman Ophanage center cha mjini Dodoma .

  Msaada huo ulikabidhiwa jana kwenye kituo hicho na timu ya Wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Tigo Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini Aidan Komba .

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo meneja wa Tigo kanda ya kaskazini inayojumisha mikoa ya Dodoma ,Singida na manyara Aidan Komba alisema kampuni ya tigo wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kushirikiana na jamii hasa wenye mazingira magumu.

  Komba alisema msaada huo ni sehemu ya faida ambayo kampuni inarudisha kwenye jamii kwa kuwaunga mkono katika kununua na kutumia mtandao wao.

  Alisema mwaka huu tigo walichagua kushiriki kuandaa futari na kutoa msaada wa vyakula kwa Watoto wanaotunzwa katika kituo hicho ili wao waone kuwa Kampuni inawajali na kushirikiana nao .

  Alitaja aina ya vitu walivyokabidhi hapo jana katika kituo hicho kuwa ni mchele ,unga wa ngano,unga wa chakula,mafuta ya kupikia na sabuni za kufulia na kuogea.


  Aidha laisema vifaa hivyo walivyokabidhi thamani yake ni zaidi y ash milioni 1.5 na kuwa vyakula hivyo walivyokabidhi vitasaidia kuendelea kupata futari kwa siku za kufunga zilizobaki.

  Naye mmoja wa Watoto wanaotunzwa katika kituo cha Rahaman Ophanage Center cha Chang'ombe mjini Dodoma , Halima Bakari aliwashukuru wafanyakazi wa kampuni ya tigo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia msaada huo mkubwa.

  Kwa upande wake mwalimu wa kituo hicho Ustadhi Umas Mafita aliishukuru menejimenti ya kampuni ya Tigo kwa kutoa msaada na kuwapa futari watoto wa kituo hicho

  Alitoa wito kwa makapuni mengine kuiga mfano wa kampuni ya tigo na kijitokokeza kukisaidia kituo hicho chenye watoto zaidi ya 100 wanaotunzwa hapo .Alisema idadi hiyo ya watoto wanaotunzwa pamoja na kupewa mafunzo ya kidini ya kislamu na elimu ya kawaida .

  Mafita aliwaomba tigo kuendelea kuwasaidia kituo hicho kwani kinamahitaji mengi kama vifaa vya shule,magodoro, vitanda na ujenzi wa mabweni .

  0 0

  Na. Lilian Lundo - MAELEZO
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi ya Idd El Fitri zenye thamani ya shilingi 10,922,000 kwa vituo 9 vya Mkoa wa Dar es Salaam, vituo 2 vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.

  Zawadi hizo zimekabidhiwa leo katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Simon Panga kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

  Panga amezitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengi.
  “Mhe. Rais kwa upendo wake wa dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee  wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa  katika makazi, katika kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri mwaka 2017,” amesema Panga.

  Aidha, amevitaja vituo vilivyonufaika na zawadi za Mhe. Rais kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN Kathry- Ilala, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima Chakuwama, Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke, Makao ya Watoto Yatima Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization), Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam – Upanga, Makazi ya Wazee na Wasojiweza Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya Watoto Wenye Ulemavu Yombo.

  Vile vile, amevitaja vituo vilivyonufaika kwa upande wa mikoa ya Tanzania Bara kuwa ni Makao ya Watoto Tosamaganga – Iringa, Makao ya Watoto Yatima Malaika Kids Home, Mkuranga – Pwani, Makao ya Watoto  Yatima Karibu Nyumbani, Kibaha – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Miyuji Cheshire – Dodoma, Shule ya Maadilisho Irambo – Mbeya na Mahabusu ya Watoto – Mbeya.

  Vituo vingine ni Mahabusu ya Watoto – Arusha, Makao ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto – Sinyanga, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ngehe – Ruvuma, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kiilima – Bukoba, Kagera, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Magugu – Manyara, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ipuli – Tabora, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi – Mwanza.
  Kwa upande wa Zanzibar, vituo vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Yatima Mabaoni – Chakechake – Pemba na Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Sebleni – Unguja.

  Utoaji wa zawadi hizo ni utaratibu wa Waheshimiwa Marais tangu awamu nne zilizopita ambapo wamekuuwa wakiwapatia makundi hayo maalum zawadi za vyakula katika sikukuu mbalimbali.
   Kamishna Msaidizi katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Simon Panga akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi ya Idd El Fitri kwa niaba ya Rais Dk. John Magufuli  kwaVituo vya Yatima na Makundi Maalumu katika Maabusu ya Watoto Dar es Salaam, leo.
   Kamishna Panga, akikabidi zawadi kwa Ofisa Ustawi  wa Jamii Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Yatima Kurasini, Dar es Salaam, Beatrice Mgumiro.
   Kamishna Panga, akikabidhi zawadi wa Sister Stella Selugenge wa Makao ya Yatima Msimbazi, Dar es Salaam.

  (Picha Zote Na. Frank Shija)


  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye miwani) akisikiliza  maelekezo kutoka kwa  Mkurugenzi  Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  Bw. Alex Nkenyenge (wa Tatu kulia) alipotembelea uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo  wa Wizara hiyo Bw. Alex Nkenyenge (katikati) alipokuwa akiwatambulisha vijana ambao ni Maafisa kilimo (wenye makoti)  leo Jijini Dar es Salaam , mwingine ni  Mkurugenzi wa Utawala  na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas(mwenye shati jeupe).
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipata maelekezo kuhusu mbegu za nyasi mpya kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa mashine zinazotumika katika ukarabati wa picth katika uwanja wa Taifa kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge (aliyechuchumaa), katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala  na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas  leo Jijini Dar es Salaam .
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akielezwa jambo kuhusu matumizi    mashine ya kuchorea mistari kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius  Mgaya(aliyeinama) na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge  leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo. 9picha na Lorietha Laurence WHUSM).

  Na Lorietha Laurence WHUSM.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa eneo la kuchezea mpira (picth) la Uwanja wa Taifa wakati wa ziara yake leo Jijini Dar es Salaam. 

  Akizungumza  katika ziara hiyo ya kukagua hatua iliyofikiwa katika matengenezo ya uwanja huo   Waziri  Mhe.Dkt.  Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya awali ya ukarabati na anatarajia mabadiliko makubwa  zaidi baada ya hatua zinazofuata kukamilika .

   “Nimefurahishwa na mabadiliko niliyoyaona katika hatua hii ya awali naamini ukarabati utakapokamilika milango itakuwa wazi kwa mechi za kimataifa ikiwemo mashindano ya AFCON yanayoratajiwa kufanyika nchini kwetu  mwaka 2019” alisema Dkt.Mwakyembe

  Aidha aliongeza kwa kusema kuwa Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha viwanja vingine vikiwemo vya mikoani  vinafanyiwa ukarabati ili kuboresha sekta ya michezo nchini.

  Waziri Dkt. Mwakyembe ameushukuru uongozi wa SPORTPESA kwa kuonyesha ushirikiano wa karibu na Serikali katika kuhakikisha inaweka mchango wake  katika michezo kwa kukarabati sehemu ya kuchezea mpira (picth) ya Uwanja wa Taifa pamoja na vifaa mbalimbali vilivyotolewa katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.

  Naye Mkurugenzi wa Utawala Na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas ameeleza kuwa kampuni yao imefanya hivyo ikiwa ni njia ya kuonyesha uzalendo wa kupenda na kuthamini vya nyumbani.
  “Hatua hii ni ya awali baada ya mechi ya Everton na Gorimahiya mnamo Julai 13 mwaka huu  hatua itakayofuata ni ya   kuondoa nyasi zote  na kuotesha mpya ambazo zitachukuwa miezi mitatu kuwa sawa” alisema Bw.Tarimba.

  Uwanja wa Taifa ulianza matengenezo ya eneo la kucheze (pitch) rasmi katikati wa mwezi wa sita lengo ni kuhakikisha nyasi zilizochakaa zinaondolewa na kuwekwa nyasi mpya zitazodumu zaidi ya miaka 10 .


  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi Dkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi,  wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  MAFUNZO ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.
  Mafunzo hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.
  Mafunzo hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.
  Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo,  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw  Masha Mshomba, alisema kuwa  ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa kazini.

   Dkt.Benjamin Najimu Mohammed, akizungumz kwa niaba ya madaktari wenzake. "Nia ya mafunzo haya ni kwenda kuwasaidia watanzania wenzetu kwa niaba ya wenzangu napenda kuushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kwa kutambua umuhimu wa ushiriki wetu katika mafunzo haya ili hatimaye kuwasaidia walengwa ambao ni watanzania wenetu." Alisema Dkt. Mohammed kutoka hospitali ya Kairuki ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Mwenyekiti wa jopo la wataalamu walioendesha mafunzo hayo, Dkt.Robert Mhina kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
   Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Arnold Mtenga
    Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Aida O. Salim
     Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Alex Shuli
   Dkt. Machumani Kiwanga akisikilzia kwa makini hotuba ya ufungaji

   Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia),  akifuatilia kwa makini hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo kwa wataalamu hao wa afya.
   Washiriki wakisikiliza hotuba
  Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu, WCF akiwa na Daktari bingwa wa upasuaji na majeruhi kutoka tasisi ya Mifupa MOI, Dkt. Robert Mhina, ambaye ndiye alijkuwa mwenyekiti wa jopo la wataalamu waliotoa mafunzo hayo

older | 1 | .... | 1282 | 1283 | (Page 1284) | 1285 | 1286 | .... | 1897 | newer