Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

AKINAMAMA WALIMA NYANYA KINYEREZI DAR WAJIFUNZA KILIMO CHA UYOGA

0
0

Mafunzo kwa vitendo. Akinamama wa Kinyerezi Green Voices wakiweka udongo kwenye mifuko kama maandalizi ya kilimo cha uyoga.

Mafunzo ya nadharia: Mkufunzi wa kilimo chau yoga wa kikundi cha Bunju Tunza Women, Bi. Esther Chiombola, akitoa mafunzo kwa wanakikundi wa Kinyerezi Green Voices waliotembelea mradi wa akinamama wa Bunju kwa nia ya kubadilishana uzoefu.
Mshiriki kiongozi wa kikundi cha akinamama walima uyoga Bunju, Bi. Magdalena Bukuku, akimkabidhi Dkt. Sophia Mlote kitabu cha namna ya kulima uyoga.

Mkufunzi wa kilimo chau yoga, Bi. Esther Chiombola, akiwapatia vipeperushi washiriki wa mafunzo hayo ya siku moja.
Akinamama wa kikundi cha Kinyerezi Green Voices wakipita kwenye banda (shamba) la uyoga walipokwenda hivi karibuni kwa mafunzo ya siku moja ya kubadilishana uzoefu.





AKINAMAMA wanaojishughulisha na kilimo cha nyanya, spinachi, kabichi na mapapai kutoka Kinyerezi jijini Dar es Salaam wameamua kujifunza pia kilimo cha uyoga kutoka kwa wenzao wa Bunju ikiwa ni hatua ya kuongeza fursa ya ujasiriamali pamoja na kubadilishana uzoefu.


Wakiongozwa na Dkt. Sophia Mlote, akinamama hao wa kikundi cha Kinyerezi Green Voice wameamua kuchukua hatua hiyo katika awamu ya pili ya kutekeleza Mradi wa Green Voices unaolenga kuwawezesha wanawake kujihusisha na shughuli za kiuchumi zinazoendana na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uhifadhi wa mazingira.

Ziara hiyo ya mafunzo ya siku moja ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwahusisha akinamama 13 wa kikundi hicho cha Kinyerezi ambao wanashiriki kilimo hai katika maeneo yao kwa kutumia mabanda maalum ambapo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita wameweza kunufaika na bidhaa wanazozalisha.

Awamu ya pili ya mradi huo wa Green Voices imeanza mwezi Aprili 2017 na itaishia Aprili 2018, ambapo mradi huo unafadhiliwa na taasisi inayojihusisha na maendeleo ya wanawake wa Afrika, ijulikanayo kama Foundation for Women of Africa inayoongozwa na Makamu wa Rais mstaafu wa Hispania, María Teresa Fernández de la Vega.

Dkt. Mlote alisema kwamba, wameamua kwenda kujifunza kilimo chau yoga siyo tu katika kubadilishana uzoefu, bali pia kuongeza ujuzi ili kupata tija katika shughuli za kilimo rafiki wa mazingira katika utekelezaji wa mradi huo wa Green Voices.

“Tunataka kujifunza aina mbalimbali za kilimo kwa sababu hii ni fursa nzuri ya kumwezesha mwanamke kujiajiri na kuongeza pato kiuchumi,” alisema Dkt. Mlote.

Dkt. Mlote, ambaye ni Ofisa Mwandamizi katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Mifugo, alisema mazingira walioyonayo katika kuendesha kilimo hifadhi cha nyanya, kabichi na mapapai huko Kinyerezi hhayana tofauti na mazingira ya kilimo cha uyoga kwani shughuli zote zinafanyika katika maeneo madogo ya nyumba zao huku wakihitaji kiasi kidogo cha maji.

“Ni rahisi kuendesha miradi hii kwa kuwa shughuli zote zipo nyumbani na hata utarudi usiku kutoka kazini, bado unaweza kuingia shambani na kuhudumia mimea kwa kutumia mwanga wa taa zilizomo kwenye banda,” alisema.

Kikundi hicho cha ‘Kinyerezi Green Voices’ kinaundwa na wanawake 10, ambao baada ya mafunzo walioyoyapata katika awamu ya kwanza ya mradi wa Green Voices walijikita katika kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo nyanya, kabichi, pilipili hoho, matango na matikiti maji.


Esther Chiombola ‘Mama Uyoga’, Ofisa Kilimo Msaidizi Mwandamizi wa Manispaa ya Kinondoni ndiye mkufunzi wa kikundi cha ‘Bunju Tunza Women Group’ kinachojihusisha na kilimo cha uyoga, ambaye allitumia muda mwingi kuwaelimisha akinamama wa Kinyerezi kuelezea umuhimu wa kilimo chau yoga pamoja na faida zake.

Alisema uyoga ni lishe bora iliyojaa kiasi cha asilimia 20 hadi 49 cha protini pamoja na Vitamini B, C, D, E, na K, na madini joto, chuma, fosforas, potashi, zinki na shaba na kwamba hauna lehemu (cholesterol).

Alisema baadhi ya aina za uyoga kama Ganoderma husaidia kuzuia na kupunguza kasi ya magonjwa sugu kama saratani, kisukari, kifua kikuu, moyo, shinikizo la damu na figo.

“Kilimo cha uyoga ni ajira kubwa kwa akinamama, vijana, wazee na wastaafu na ni kilimo rafiki kinachopunguza uchafuzi wa mazingira kwa vile kinatumia mabaki ya shambani na viwandani,” alisema na kuongeza kwamba kilimo hicho ni endelevu ambacho hakina msimu.

Bi. Magdalena Bukuku ni mshiriki kiongozi wa Bunju Tunza Women Group ambaye alisema kwamba, tangu walipoanzisha mradi huo mwaka 2016 akinamama wameweza kunufaika na kuongeza mapato kutokana na bidhaa zao kupata soko kubwa katika maeneo mengi ya jijini Dar es Salaam.

“Hata kwenye maduka makubwa (super markets) wamekuwa wakiuhitaji kwa ajili ya wateja, hivyo soko la uhakika lipo la kutosha,” alisema Bi. Magdalena.

Aidha, aliongeza kwamba, kikundi chao kimekuwa kama darasa kwani watu wengi, wanawake kwa wanaume, kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar wamekuwa wakienda kujifunza kila mara kuhusu kilimo hicho.

“Ni mradi mzuri, unatumia gharama kidogo huku mavuno yake yakiwa endelevu hasa ukiwa na nia, dhamira na jitihada, soko lake lipo kubwa,” alieleza Magdalena.

Dkt. Mlote na Bi. Magdalena Bukuku ni miongoni mwa akinamama 15 wanaotekeleza Mradi wa Green Voices nchini Tanzania baada ya kupatiwa mafunzo nchini Hispania mwaka 2016 ambapo lengo ni kupaza sauti za wanawake kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kushiriki shughuli za kilimo rafiki wa mazingira.

Akinamama wengine wanatekeleza miradi mbalimbali ya ujasiriamali unaoendana na mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Kigoma, Kilimanjaro, Pwani na Mwanza.

Mratibu wa mradi wa Green Voices nchini Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, alisema katika awamu ya pili, mbali ya akinamama hao kuendeleza miradi yao ya awali, pia watapata fursa ya kubadilisha uzoefu na kuona uwezekano wa kutekeleza mmiradi mingine tofauti kwa faida yao.

huo wa kilimo hai cha nyanya kwa kutumia green house ni sehemu ya miradi 10 inayoendeshwa nchini Tanzania kupitia Green Voices ambapo inaendeshwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara.

Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Kigoma, Morogoro na Kilimanjaro ambapo inahusisha kilimo, usindikaji, ufugaji na utafiti.

“Jumla kuna miradi 10 ikiwemo ya kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani, ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro, usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga, kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanajro,” alifafanua Secelela Balisidya.

Aidha, alisema, lengo kubwa la mradi wa Green Voices ni kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya Kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

WATOTO NA VIJANA WA KAMBI YA ARIEL WATEMBELEA MAKUMBUSHO YA KISUKUMA – BUJORA MWANZA

0
0

Watoto na vijana 50 kutoka mikoa ya Geita,Mwanza na Shinyanga wanaoshiriki katika kambi ya Ariel 'Ariel Camp 2017’ jijini Mwanza iliyoandaliwa na shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi, wametembelea makumbusho ya kabila la Kisukuma ‘Sukuma Museum’ ya Bujora Kisesa Mwanza ili kujifunza tamaduni na mila za Kisukuma.

Kambi ya Ariel imeanza Juni 19,2017 itafungwa Juni 23,2017 ambapo washiriki wanajifunza mambo mbalimbali ikiwemo afya ya ujana na makuzi, lishe, stadi za maisha, elimu sahihi kuhusu VVU na Ukimwi,kushiriki katika michezo sambamba na kubadilishana mawazo.

Katika siku ya tatu ya kambi hiyo,Jumatano Juni 21,2017 ,watoto na vijana hao walitembelea Makumbusho ya Kisukuma ya Bujora na kucheza michezo mbalimbali katika ufukwe wa Ndorosi katika ziwa Victoria.

Watoto na vijana hao wakiwa wameambatana na watumishi wa afya,madaktari wa watoto na wafanyakazi wa AGPAHI walijionea zana mbalimbali zinazotumiwa na wasukuma katika maisha yao ya kila siku pia walijifunza historia ya wasukuma.

Makumbusho ya Kisukuma ya Bujora yalianzishwa mwaka 1968 na padre David Clement Fumbuka aliyeamua kukusanya mabaki mbalimbali ya zana za Kisukuma na kuandika historia ya wasukuma.

Mwongozaji wa wageni katika makumbusho hayo,Yasinta Salum alisema Fumbuka aliyekuwa raia wa Canada mwenye asili ya Ufaransa alifika kanda ya ziwa mwaka 1952 na kuanzisha chama cha Mtakatifu Sesilia ambacho kazi yake ilikuwa ni kuimba nyimbo za Kilatini kisha kuzitafsiri kwa lugha ya Kisukuma lengo likiwa ni kuangalia namna ya kuchanganya masuala ya dini na utamaduni.

“Mwaka 1958 ,Padre Fumbuka alifungua kanisa Katoliki hapa Bujora kisha akapata wazo la kuanzisha makumbusho,akaanza kukusanya mabaki ya zana za Kisukuma na kuandika historia ya wasukuma na kufanikiwa kufungua makumbusho haya mwaka 1968”,alieleza Yasinta.

Alisema makumbusho hayo yamesheheni mambo kadha wa kadha ya wasukuma ikiwemo historia ya falme za kisukuma,utawala wa machifu wa kisukuma,familia za kisukuma na nyumba zao,ngoma na zana walizokuwa wanatumia katika maisha yao ya kila siku.

ANGALIA HAPA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WATOTO NA VIJANA WA KAMBI YA ARIEL WAKITEMBELEA MAKUMBUSHO YA KISUKUMA - BUJORA MWANZA

Bango linaloonesha makumbusho ya Kisukuma ya Bujora Mwanza,pichani kushoto ndiye mwanzilishi wa makumbusho hayo David Clement Fumbuka aliyezaliwa mwaka 1922 na kufariki dunia mwaka 1986.

Mwongozaji wa wageni katika makumbusho ya Kisukuma Bujora ,Yasinta Salum akielezea historia ya makumbusho hayo kwa watoto na vijana kutoka mikoa ya Shinyanga,Geita na Mwanza walioshiriki katika Kambi ya Ariel jijini Mwanza.

Yasinta akiendelea kutoa historia ya Makumbusho ya Bujora.



Baada ya kuwapatia historia ya Makumbusho ya Kisukuma Bujora,Yasinta akaanza kuwatembeza wageni wake katika makumbusho hayo.





Mwongozaji wa wageni katika makumbusho ya Kisukuma Bujora ,Yasinta Salum akielezea kuhusu chama cha Mt. Sesilia kilichoanzishwa na Padri David Clement Fumbuka na viongozi wengine wa kanisa katoliki waliofika katika makumbusho hayo.





Watoto,vijana na watumishi wa afya walioambatana na watoto hao wakimsikiliza Yasinta





Yasinta akionesha zana zilizokuwa zinatumiwa na wasukuma katika maisha yao ya kila siku.Hapo kuna zana za kuwashia moto,kuyeyushia chuma na vinginevyo.





Yasinta akionesha zana ya kuwashia moto 'ulimbombo'.





Hapa ni nje ya nyumba iliyokuwa inatumiwa na wahunzi.





Yasinta akiwaonesha wanakambi kifaa kwa ajili ya mchezo wa bao.





Yasinta akionesha ramani inayoonyesha jinsi falme za Kisukuma zilivyokuwa.





Sehemu ya ramani ya falme za Kisukuma ikionyesha majina ya machifu.





Yasinta akionesha kifaa kinachotumika kuhesabu namba kwa lugha ya Kisukuma.





Watoto na vijana wakipanda katika eneo la kutunzia ngoma za Kichifu.





Yasinta akionesha ngoma zilizokuwa zinatumiwa na Machifu wa Kisukuma.





Kijana muelimisha rika akipiga ngoma ya Kichifu.





Mfano wa nyumba ya Kisukuma.





Nje ya nyumba ya Kisukuma na vitu mbalimbali ambavyo lazima utakutana navyo ambavyo ni pamoja zizi la ng'ombe na maghala ya chakula.





Haya ni mawe yanayotumika kusagia nafaka katika familia za Kisukuma.





Hapa ni ndani ya nyumba ya Msukuma na vitu mbalimbali





Vijana wakiangalia vitu mbalimbali vinavyopatikana katika nyumba ya msukuma.





Vijana wakiangalia vyungu katika familia ya Msukuma.





Hii ni nyumba ya mganga wa kienyeji/Mganga wa Kisukuma.





Vijana wakiangalia vitendea kazi vya mganga wa kienyeji alivyohifadhi ndani ya nyumba yake.





Vijana wakiangalia vibuyu vya mganga wa kienyeji.





Vijana wakiangalia ngozi za wanyama zinazotumiwa na mganga wa kienyeji.





Kikundi cha ngoma za asili cha Mt. Sesilia- Bujora kikitoa burudani ya ngoma ya Bhucheye inayochezwa wakati wanawake wanapotaka wachumba na wanawake hao hucheza wakiwa wanasaga nafaka kwenye mawe.





Ngoma ya Bhucheye ikiendelea.





Ngoma ya Sogota ikiendelea.Ngoma hii huchezwa na wasukuma wakati wa mavuno.





Mchezaji wa ngoma ya Bhuyeye akicheza na nyoka.





Mcheza ngoma ya Bhuyeye akiingiza nyoka kwenye kaptura yake.





Mmoja wa vijana kutoka kambi ya Ariel akiwa na mcheza ngoma ya Bhuyeye wakiwa wameshikilia nyoka.





HAPA NI KATIKA UFUKWE WA NDOROSI : Vijana wakionesha mapozi ya Ki Miss.





Vijana wakipiga picha ufukweni.





Watoto na vijana wakicheza mchezo wa kuruka.





Watoto na vijana wakicheza mchezo wa kujifunza umuhimu wa ushirikiano.





Michezo ikiendelea.



Wafanyakazi wa AGPAHI wakicheza na mmoja wa vijana hao.

Mchezo wa mbio za magunia nao ulikuwepo.

Mchezo wa kuruka kamba ukiendelea.

Michezo inaendelea.

Watoto wakiendelea na michezo.

Watoto wanacheza.

Mchezo wa kubembea ukiendelea.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Fanya yafuatayo kunogesha sikukuu ya Eid-al-Fitr

0
0
 Na Jumia Travel Tanzania

Ni siku chache zimebakia kabla ya waumini wa dini ya kiislamu nchini na duniani kote kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. Zipo namna tofauti za kusherehekea sikukuu hii kulingana na sehemu watu walipo.

Jumia Travel ingependa kukushirikisha mambo yafuatayo ambayo yanaweza kuifanya sikukuu hii kuwa ya tofauti na kipekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka.   

Fanya maandalizi pamoja na familia. Katika kuhakikisha kwamba kila mtu anafurahia sikukuu basi ni vema ukawashirikisha kwenye maandalizi yake. Kama baba au mama wa familia na una watoto au ndugu unaishi nao litakuwa ni jambo zuri kama mtafanya hata kikao kidogo na kujadili. Kwa mfano, shughuli zote zitakazofanyika kipindi cha sikukuu, chakula kitakachopikwa, vinywaji, zawadi, wapi kwa kusherehekea, wageni gani wa kuwaalika, kupamba nyumba nakadhalika. Hii itasaidia siku hiyo ikifika kila mtu anafurahia na sio kufanya mambo ambayo yatakufurahisha wewe tu kuwaacha baadhi ya wengine kunung’unika.

Sherehekea pamoja na familia na majirani. Mara nyingi sikukuu hupendeza pale zinaposherehekewa kwa pamoja na ndugu na jamaa. Haijalishi familia uliyonayo ina ukubwa gani, kujumuika kwa pamoja kunaleta furaha na muunganiko zaidi miongoni mwa watu. Pia, hata kama una familia ndogo ni vema ukawashirikisha majirani zako. Unaweza ukapika chakula cha kutosha na ukaamua kuwaalika au kuwagawia lengo ni kuifanya iwe na shamrashamra zaidi.

Sherekea pamoja na watu wenye mahitaji maalum. Sio kila mtu huwa anapata fursa au kuwa na uwezo wa kusherehekea sikukuu. Na kwa sababu sikukuu ya Eid al-Fitr husherehekewa kwa siku mbili mpaka tatu (kwa sehemu zingine), unaweza ukapanga kwamba sikukuu ya moja au mbili ukasherehekea na familia yako na nyingine ukajumuika pamoja na watu wenye mahitaji maalumu kama vile watoto wa mitaani, watoto wa mitaani, wagonjwa mahospitalini, wazee, wafungwa na wengineo.

Wasimulie watoto kuhusu maisha ya Mtume na namna waislamu wa wakati walivyokuwa wakisherehekea sikukuu ya Eid-al-Fitr. Sio siku zote watoto wakishamaliza kupata chakula cha pamoja na familia wakaenda kutembea. Unaweza kuitumia siku hiyo kwa muda mchache tu ukawakusanya watoto na kuwasomea hadithi za Mtume Mohammad na namna waislamu wa kipindi hiko walikuwa wanasherehekea vipi sikukuu hii.  Hii itawafanya si tu kufurahia kwa kuwaongezea maarifa lakini pia kuelewa ni nini maana zaidi ya siku hii.


Safiri pamoja na familia. Unaweza ukaamua kusherehekea sikukuu hii kwa kusafiri mahali tofauti na nyumbani. Mnaweza kutumia gari binafsi kama usafiri, mkawa mnapumzika kwenye vituo kadhaa kwa ajili ya chakula na kuswali mpaka mkafika mahali muendapo.

Toa zawadi kwa ndugu, jamaa na marafiki. Kipindi cha Ramadhan mbali tu na kuwa ni kipindi cha kufanya toba na kumuomba Mwenyezi Mungu kukupunguzia dhambi zako lakini pia kutoa zawadi kunaweza kuwa ni njia mojawapo ya kukuongezea thawabu. Kutoa zawadi ni jambo jema kumfanyia mtu hususani unapolifanya kwa moyo mkunjufu. Basi kama utakuwa na uwezo unaweza kununua zawadi kadhaa na kuwapatia ndugu na majirani zako.

Badili muonekano wa nyumba yako. Itapendeza kama siku ya sikukuu mtaisherehekea kwenye nyumba yenye muonekano tofauti. Unaweza kufanya hivi kwa kushirikiana na familia yako ili kupata mwonekano utakaovutia. Mambo yanayoweza kubadili mwonekano wa zamani ni kama vile kupaka rangi mpya, kubadili samani za ndani, kununua mapambo, kufanya usafi au hata mpangilio wa vitu ndani ya nyumba.

Valia mavazi nadhifu. Tumezoea kwamba linapokuja suala la kuvaa nguo mpya siku za sikukuu huwa ni watoto pekee wanaopenda kufanya hivyo. Kwenye familia nyingi imekuwa ni kawaida wazazi kuweka kipaumbele kwa kuwanunulia watoto nguo mpya. Kutokana na desturi hiyo kuzoeleka miongoni mwa watu wengi, imewafanya watu wazima kupuuzia kuvaa nguo mpya kipindi cha sikukuu. Hiyo ni dhana na mawazo ya watu tu na wala isikufanye ujisikie vibaya kuvaa nguo mpya siku ya sikukuu. Unastahili kuutendea vema mwili wako kwa kuuvika na mavazi mapya na nadhifu siku hiyo, kama una uwezo lakini.   

Dhumuni la kukupatia dondoo hizi ni kuifanya sikukuu hiyo iwe na upekee tofauti na unavyosherehekea kila mwaka. Jaribu kufanya baadhi ya mambo hayo na utagundua utofauti mkubwa. Sio lazima ufanye yote yaliyoorodheshwa kwenye makala haya, machache tu yanatosha. Tofauti na hapo, Jumia Travel ingependa kukutakia maandalizi na mapumziko mema ya sikukuu ya Eid al-Fitr!

MSIWATOZE KODI YA MAJENGO WAZEE WA MIAKA 60

0
0

*Ataka TRA wafanye sensa ya majengo kwenye miji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maafisa wa Mamlaka ya Kodi ya Mapato nchini (TRA) wakusanye kodi za majengo kwa kuzingatia sheria na wasitoze kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60.

"TRA ijipange kukusanya kodi za majengo kuanzia Julai Mosi 2017. Katika kutekeleza jukumu hilo, zingatieni sheria. Tusisikie mnawadai kodi ya majengo wazee wenye umri zaidi ya miaka 60 kwa majengo wanayotumia kama makazi yao," amesema. 

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Juni 22, 2017) wakati akizungumza na wananchi na viongozi wa wilaya ya Chato waliohudhuria uzinduzi wa jengo la TRA, wilayani humo, mkoani Geita. 

Waziri Mkuu amewataka maafisa hao wakusanye kodi ya majengo kwenye maeneo ya mjini na siyo vijijini kwani kodi hiyo haiwahusu. "Msiende vijijini. Nyumba za nyasi au za tembe hazihusiki. Tembeleeni nyumba za mijini.  Piteni kwenye mitaa, muainishe aina zote za nyumba zinazostahili kulipiwa kodi. Mkishafanya sensa, wekeni utaratibu wa kuwawezesha wananchi kulipia kodi hizo," amesema huku akishangiliwa.

Pia amewataka wananchi wanaonunua bidhaa wadai risiti lakini wahakikishe wanapewa risiti yenye kiwango halisi walicholipia.  "Ukipewa risiti uiangalie kama ina kiwango halisi cha fedha uliyotoa. Kuna watu wachache wasio waaminifu wanaamua kukupa risiti lakini imeandikwa bei ndogo kuliko ile uliyolipia, ukitoa laki moja anakuparisiti ya sh 10,000."

Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo la ghorofa moja, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw.  Charles Kicheere alisema ujenzi huo ulianza Julai 12, mwaka jana na ulikamilika Juni 12, mwaka huu. 

"Ujenzi wa jengo hili umegharimu sh. bilioni 1.4 na ulichochewa na ongezeko kubwa la idadi ya walipakodi wa Chato kutoka watu 150 mwaka 2010/2011 hadi kufikia watu 600 mwaka 2016/2017", alisema. 

Pia alisema wamejenga ofisi hizo ili kuwapunguzia umbali wafanyabiashara wa wilaya hiyo ambao walilazimika kwenda Geita mjini kupata huduma za TRA ambako ni umbali wa zaidi km.120.

Alisema hivi karibuni watakamilisha ukarabati wa ofisi za mikoa ya Mara, Iringa, ikiwemo kujenga ofisi kwenye mikoa mipya ya Simiyu, Katavi, Njombe na Manyara. "Pia tutajenga ofisi kwenye mkoa mpya wa kikodi wa Kahama," alisema. 

Alizitaja wilaya ambazo ziko mbioni kupatiwa ofisi zake kuwa ni Kondoa, Longido, Bunda na Arumeru. 

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, TRA imelenga kukusanya sh. trilioni 17.106 na watahakikisha wanafikia lengo hilo. 

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,            
ALHAMISI, JUNI 22, 2017.

MADEREVA WAASWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI KUEPUKA AJALI

0
0
 Askari wa Usalama Barabarani akichukua maelezo ya gari Noah yenye namba za usajili T338 BVU iliopata ajali mapema jana,njia panda Goba,Mbezi Beach jijini Dar.Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari dogo (daladala pichani chini yenye namba za usajili T912 CVY),iliyokuwa imebeba abiria ikitokea Goba kwenda Mwenge,na hivyo gari hiyo kukosa mwelekeo kufuatia kona iliyopoo eneo hilo,Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha.

Mashuhuda hao pia wakatoa wito kwa baadhi ya Madereva kuwa makini,kufuata sheria na kuzingatia alama za barabarani,kwani kwa kufanya hivyo ajali nyingi zitapungua kutokea. 
  Daladala yenye namba za usajili T912 CVY ikiwa imeacha barabara na kuvamia mtaro kufuatia gari hiyo kupoteza uelekeo kwa kile lichodaiwa na Mashuhuda kuwa ni mwendo kasi na kutaka kugongana uso kwa uso na gari nyingine aina ya Noah (pichani juu),sehemu yenye kona kali.
Baadhi ya watu wakishuhudia ajali ya gari aina  daladala pichani yenye namba za usajili T912 CVY,ikiwa imeacha njia na kuvamia mtaro,kama ionekavyo pichani.katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza Maisha

CRDB YAWAKARIBISHA WATEJA WAKE KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

0
0

TAARIFA KUTOKA BARAZA KUU LA WAISLAM TANZANIA (BAKWATA).

0
0

KAMATI YA KUDUMU YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA KUTOKA BUNGE LA MSUMBIJI YATEMBELEA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Chomera Jeremiah (kushoto) Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015 wakati Kamati hiyo ilipotembelea Ofisi za Tume leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya Tume kwa Wabunge wa Bunge la Msumbiji ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa waliotembelea Ofisi za NEC jijini Dar es salaam kujifunza namna Tume hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Lucas Chomera Jeremiah na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Hamis Mkunga.



Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Emmanuel Kawishe (kushoto) akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji namna Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Chomera Jeremiah (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Wajumbe wa Kamati hiyo kutoka Msumbiji na watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania leo jijini Dar es salaam, Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji wamezitembelea Ofisi za NEC kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala ya Uchaguzi.Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia) akisalimiana na Wabunge wa Bunge la Msumbiji na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa wa nchi hiyo waliotembelea Ofisi za NEC kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu uendeshaji wa chaguzi mbalimbali.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ya Bunge la Msumbiji waliozitembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam. PICHA/Aron Msigwa - NEC

Muuza simu Dodoma ajazwa Milioni 20 za Biko

0
0
MFANYABIASHARA wa simu za mikononi mjini Dodoma, Ramadhan Juma Hussein, jana amejazwa Sh milioni 20 zake alizoshinda kutoka kwa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko, aliyoshinda katika droo ya 16, iliyochezeshwa Jumatano iliyopita.

“Nashukuru nimekuwa mchezaji mzuri wa Biko na huwa nashinda mara kwa mara zawadi za papo kwa hapo ambazo hupatikana kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.
“Binafsi ninawaamini Biko kwa sababu si mara ya kwanza kushinda zawadi za papo kwa hapo, hivyo nawaomba Watanzania wenzangu tujitokeze kwa wingi kucheza Biko ili tushinde zawadi mbalimbali ikiwamo hii ya Milioni 20 ambayo leo nimekabidhiwa, huku nikiahidi kuwa nitaendelea kucheza Biko zaidi na zaidi,” Alisema.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba wanaendelea kusambaza mamilioni kutoka kwa washindi wao mbalimbali wanaojitokeza kwa wingi kucheza bahati nasibu yetu rahisi katika uchezaji wake.
“Huu ni wakati wa kulala masikini na kumka tajiri kwa sababu kwa kupitia Biko kila mtu anaweza kuvuna mamilioni yetu ya papo kwa hapo pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili,” Alisema.
Biko ni mchezo wa bahati nasibu uliojizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania kwa siku chache tangu kuanzishwa kwake, huku kwa mwezi Mei pekee zaidi ya Sh Milioni 500 zikiwa zimekwenda kwa washindi waliobuka katika nafasi mbalimbali za ushindi.
Mshindi wa droo ya 16 ya Sh Milioni 20 kutoka Biko, Ramadhan Juma Hussein katikati akiwa amebeba fedha zake alizokabidhiwa jana na waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko mjini Dodoma katika benki ya NMB. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Kupokea kwa pesa zake kumekuja baada ya kuwa miongoni mwa Watanzania lukuki wanaocheza bahati nasibu ya Biko kuwania zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni 1,000,000, pamoja na donge nono la Sh Milioni 20 linalotoka Jumatano na Jumapili.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa Dodoma, Ramadhan Juma Hussein. Wengine wanaoshuhudia ni familia ya Ramadhan wakati wa makabidhiano hayo.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika katika benki ya NMB mjini Dodoma, Juma anasema kwamba pesa hizo atazitumia vizuri katika kukuza biashara zake kama alivyokuwa akimuomba Mungu aweze kushinda mamilioni ya Biko.
Ramadhan Juma Hussein akiwa kwenye fyraha baada ya kukabidhiwa jumla ya Sh Milioni 20 kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika benki ya NMB Mjini Dodoma.

Diamond Platnumz - I miss you (Official Video)

0
0

ASKOFU MTEULE BLASTON GAVILLE WA KKKT DAYOSISI YA IRINGA KUANZA KAZI RASMI

0
0
Katibu mkuu KKKT dayosisi ya Iringa Nayman chavala akizungumza na wanahabari

Na Fredy Mgunda, Iringa

KANISA la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa limesema maandalizi ya kumwingiza kazini askofu mteule litafanyika jumapili huku likimpongeza Rais Dkt John pombe Magufuli kwa utendaji kazi.

Katibu mkuu wa KKKT dayosisi ya Iringa Nayman Chavala ameyasema hayo leo

wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari kuhusu maandalizi yaliyofikiwa ya sherehe kubwa ya kuwekwa wasifu kwa askofu mteule Mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Mchungaji Himidi Saga.

Alisema kuwa sherehe za kumpa madaraka ya kuanza kufanya kazi kama askofu wa kanisa la KKT Jimbo la Iringa mchungaji Gavile na msaidizi wake Saga itafanyika jumapili ya june 25 mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi kwenye viwanja vya shule ya msingi Gangilonga .

Kuwa ibada hiyo itaongozwa na askofu mkuu wa KKKT Dkt Frederick Shoo pamoja na askofu mstaafu Dkt Owdenburg Mdegella na kuwa kabla ya idaba kutakuwa na maandamano ya wachungaji na washarika yatakayoanzia usharika wa kanisa kuu hadi Gangilonga.
" Tunaomba wananchi wote na washarika kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria pia tunategemea kuwa na viongozi mbali mbali wa serikali na wageni mashuhuri kutoka ndani na nje ya Tanzania"

Chavala alisema maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya tukio hilo kubwa ambalo lilikuwa likisubiliwa kwa shauku kubwa .

Askofu Gavile amechukua nafasi ya aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Dkt Mdegella ambaye alistaafu kwa heshima kubwa na kuacha heshima ya aina yake ndani ya KKKT .

Wakati huo huo Katibu huyo amempongeza Rais Dkt Magufuli kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya ya kuwatumikia watanzania kwa uadilifu mkubwa na kuwa kazi kubwa kwa watanzania ni kuendelea kumpa ushirikiano .

Kwani alisema kuwa hatua ya kuwabana wasio waadilifu pamoja na kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu (MAKINIKIA) ni hatua ya kupongezwa kwani suala hilo lilikuwa likiwanufaisha wachache huku Taifa likibaki patupu .

" Sisi kama kanisa tumekuwa tukimuombea kila wakati tena kwa kumtaja kwa jina na hatutachoka kuendelea kumuombea maana kazi anayoifanya ni ngumu ambayo silaha kubwa ni maombi "

KIJIJI CHA SHUJAAZ CHAFUNGULIWA KATIKA MASHINDANO YA EAC 2017 MJINI MOSHI.

0
0
Mwakilishi wa Taasisi ya Wel tel Story ,watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz,Alan Lucky akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu kufunguliwa kwa kijiji cha Shujaaz katika Mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki maarufu kama East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika shule ya Sekondari Moshi Ufundi .
Baadhi ya Wageni wakijiandikisha kabla ya kuingia katika kijiji hicho ambako kumekuwa kukitolewa mafunzo mbalimbali hasa ya Kilimo .
Mratibu wa Tafiti wa Mradi wa Shujaaz,Winnie Nyato akitoa tiketi kwa mmoja wa watoto waliotembelea kijiji cha Shujaaz .
Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma ,Mohamed Kombo anayejishughulisha na Kilimo cha matunda akizungumza na vijana waliofika katika kijiji cha Shujaaz kuona namna gani wanaweza kuhamasika na kuingia katika shghuli za Kilimo.
Mjasiliamali Khalfa Muslim akitoa elimu jinsi ya kutengeneza mchanganiko wa Matunda kwa vijana waliotembelea kijiji cha Shujaaz kilichopo katka viwanja vya Shule ya sekondari Moshi Ufundi yanapofanyika mashindano ya East Africa Cup 2017.
Mjasiliamali Holo Bukombe akionesha bidhaa mbalimbali ambazo amekuwa akiziweka katika vifungashio maalumu na kuongeza thamani ya bidhaa husika.
Afisa Masoko wa kamuni ya YARA Ltd ,Linda Byaba akitoa elimu kuhusu kilimo bora na chenye tija na jinsi ya kuongeza thamani ya mazao mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya Mbolea kwa Mwakilishi wa taasisi ya Wel tel Story ,Alan Lucky.
Muonekano wa kijiji cha Shujaaz kilichopo katika Shule ya Sekondari Moshi Ufundi ambako elimu mbalimbali hususani za Kilimo pamoja na michez kwa vijana imekuwa ikitolewa.
Baadhi ya watoto wakishindana michezo mbalimbali (Games) katika kijiji cha Shujaaz.
Vijana wengine wamepaa fursa ya kucheza mchezo wa mitupo ndani ya kijiji hicho.
Vijana wengine walipata nafasi ya kuonesha vipaji vyao hasa vya kuimba na kucheza na kuambulia zawadi kutoka Shujaaz.

Na Dixon Busagaga wa Glob ya Jami ,Kanda ya Kaskazini.

KATIBU MKUU WA CCM APIGA MARUFUKU WAGOMBEA KUUZIWA FOMU.

0
0
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana amepiga marufuku uuzaji wa fomu za uchaguzi kwa ngazi zote za uongozi ndani ya Chama.

Taarifa iliyosainiwa na Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Rodrick Mpogolo kwenda kwa Makatibu Wakuu wa Jumuiya imeeleza kuwa kwa mwanachama yeyote aliyeuziwa fomu arejeshewe pesa yake.

RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA VITANDA,MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA LEVOLOSI

0
0
 Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa Arusha  Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 Picha ikionyesha  wa kwanza kulia Mbunge wa viti maalum(CCM)Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais  John Magufuli   msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda  25 katika  kituo cha afya cha Levolosi  ,ambapo msaada wa vitu hivi umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja wapo ya ahadi zake alizozitoa katika kipindi cha kampeni  ,katikati ni Mganga  mkuu wa kituo cha Afya cha Levolosi  Feksi Edward ,wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha (picha na Woinde Shizza,Arusha)
 Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo
 Mkuu  wa wilaya ya Arusha  Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi  wa jiji la Arusha


 Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo
  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji  mara baada ya kupokea msaada huo na kuhadi kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa
 Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo
Baadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda ,mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)

 Na Woinde Shizza,Arusha.
Wananchi wametakiwa kuwapiga vita na kutokubaliana na wale wote ambao wanapinga jitihada za maendeleo ambazo zinafanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwani jitiada hizo zinamanufaa makubwa kwa wananchi.

Aidha  kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakiziponda kazi ambazo anazifanya   Rasi kitu  ambacho sio kizuri kwani Rais amekuwa akijitaidi kufanya kazi vizuri ya kuwaletea maendeleo wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyosema

 Hayo yamesemwa   leo jijini hapa  na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha  Catherine Magige  wakati akikiabidhi kwa niaba ya Raisi  vitanda 25 ,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

Alisema k uwa  kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi  za Rais na kusema kuwa  afanyikitu chochote 

"Rais  wetu anafanyakazi mtu anaesema afanyikazi kweli ni wakupuunzwa kabisa au naweza sema ana akili angalieni jinsi alivyozuia makontena  ya madini,angalieni jinsi alivyowakamata waujumu uchumi wa Escrow na sasa ivi ameunda tume ya kwenda kuchunguza Tanzanite one mbali na apo ata leo ametambua umuimu wawananchi wa mkoa wa Arusha na  ameamua kutoa msaada wa  magodoro ,mashuka pamoja na vitanda "alisema Magige

Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kazi ziazofanywa na Rais  ,pia alitumia muda huho kuwasihi madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi

Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo mkurugenzi wa jiji la Arusha  Mh: Athuman Kihamia aliishukuru serikali kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuhaidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa  huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya aina mbalimbali.

Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda 25  uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  ikiwani moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA KILWA YAFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA SONGO SONGO

0
0
 Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Wapili kushoto) walipotembelea mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi.
 Ofisa Usalama wa Kampuni ya Pan African Energy  inayochakata na kusafirisha Gesi kutoka Kisiwa cha Songo Songo, Baraka Melchiory (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (kushoto) kuhusu hali ya usalama na namna ya kujikinga na majanga pindi itokeapo itilafu katika mradi huo. Mkuu wa Wilaya aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya katika ziara yake kutembelea mradi wa Songas juzi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai (Kushoto) akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas katika kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (kulia) kutoka Kampuni ya Pan African Energy. Mkuu wa Wilaya ya Kilwa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya katika ziara yake juzi. 

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Zablon Bugingo akizungumza na Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi Songas kutoka Kampuni ya Pan African Energy, Andrew Hooper wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama walipotembelea Kisiwa cha Songo Songo kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hizo kijijini hapo.

 Meneja Mradi wa kuchakata na kusafirisha Gesi katika Kisiwa cha Songo Songo, Andrew Hooper (katikati) kutoka Kampuni ya Pan African Energy akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na  Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai namna  mitambo ya kuchakata Gesi inavyofanya kazi wakati wa ziara yao walipotembelea chumba maalumu (Control room) katika mitambo ya Gesi Songas iliyopo katika kisiwa hicho juzi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na Viongozi wa Kijiji cha Songo Songo baada ya kukagua ujenzi ya nyumba ya mwalimu kijini hapo na kubaini mapungufu kadhaa, mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo juzi.

 Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizindua Choo katika Shule ya Msingi iliyopo katika Kijiji cha Songo Songo kilichojengwa na Taasisi ya  Fanjove, mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini hapo juzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ndubiagai akizungumza na wanakijiji cha Songo Songo baada ya kukagua miradi mbalimbali ya kijiji hicho iliyojengwa na makampuni yanayo endesha shughuli mbalimbali kijijini hapo. Mkuu wa wilaya huyo aliambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutembelea kijijini. (PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY)

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL FITR

0
0
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera John Bulimba.

SPIKA NDUGAI AKABIDHI VITABU VYA KUJIFUNZIA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI KONGWA

0
0
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na wanafunzi wa Shule Secondari ya Banyibanyi iliyopo wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma, baada ya kuwapatia vitabu vilivyotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini.
 Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akimkabidhi vitabu Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Sejeli Ndg.Gerald Kagali ikiwa ni zawadi kwa Shule hiyo, Msaada uliotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini, tukio lililofanyika leo kijijini Mbande Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya sekondari Banyibanyi  katika tukio lililofanyika leo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.

WAHAMIAJI HARAMU 45 WAKAMATWA WILAYANI MKINGA.

0
0






IDARA ya Uhamiaji Mkoani Tanga imewakamata wahamiaji haramu 45 kutoka nchini Ethiopia katika Kijiji cha Horohoro wilayani Mkinga mkoani Tanga kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria wakiwa shambani kwa wananchi wanakula mahindi kabla ya kutiwa nguvuni. 

Licha ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao lakini pia idara hiyo inamshikilia raia mmoja kutoka nchini Kenya ambaye ndio alikuwa akiwaongoza wahamiaji haramu hapa. 

Akizungumza na waandishi wa habari,Afisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Crispin Ngonyani alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa June 18 mwaka huu katika kijiji hicho baada kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wa eneo hilo. 

Alisema wahamiaji haramu hao walikamatwa wakiwa porini katika jiji hicho wakati wakisafiri kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo waligunduliwa na wananchi baada ya kufika mashambani mwao wakawakuta wanakula mahindi ndio walipotoa taarifa kwa askari wa Polisi wa Horohoro na hivyo wakaenda kuwakamata. 

Aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni Melesa Manesha, Asaf
Erisid,Ashnif Agide,Mulugeta Menano,Demek Sorebeto,Samal
Latbo,Temesgen Tefera,Tememi Juheri,Mubarc Lamago,Temesa
Kibemo,Haftamu Tumiso,Teshum Assfe,Yohanness Ayano na Daniel Abbate. 

Aidha Ofisa Uhamiaji huyo aliwataka wengine walio kamatwa kuwa ni Kibmam Abab,Temesgzeen Ayele,Akilu Abraham,Pxirose Makore,Munyasha Lombaso,Berekei Cezenzeni ,Detebo Erikato, Ayele Kebamo,Tamrat Mamo.
Wengine waliokamatwa kuwa ni Saniel Wolde,Tomiot Deto Gem,Abeje Alemeyo, Ashenaf Waje,Tariko Dutamo,Birhanu Atso,Tesefaye Dena,Tekel Abush,Tesyfe Landu na Abdi Hassani. 

Kwa mujibu wa ofisa uhamiaji huyo aliwataja wengine kuwa ni Daafa Daimo,Getahun Zeleke,Yonas Liliso, Amanei Ashebo, Xesabo Womago,Isagay Tikie Mubarik Analo,Begaye Ganorem,Dawit Teso,Teshele Kemiso,Samweli Hyle na Tamasgen Sorsa. 

Alisema wahamiaji haramu hao wamefikishwa mahakamani jana kujibu tuhuma zinazowakabili akiwemo msindikizaji Mongela Kidhome ambaye ni Mkenya na mkazi wa mpakani mwa Kenya na Tanzania Horohoro. 

Hata hivyo aliwataka mawakala wa wahamiaji haramu kuacha mara moja vitendo vya kuwaingiza nchini kwani watakaobainika watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kujibu tuhuma zinazowakabili.


Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

UNDP YACHANGIA MILIONI 110 HUDUMA YA MAJI KIKWAJUNI

0
0
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez(kulia) na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib, walipotembelea maeneo yatakayopita mabomba yakusamabaza maji kwa wakazi wa jimbo hilo.UNDP wameahidi kuchangia  kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha mradi huo. Picha na Abubakari Akida.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib,baada ya kumaliza kutembelea maeneo ya Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha mradi huo.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez,akifunga bomba la maji katika moja ya maeneo ambayo Mradi wa Maji Kikwajuni ushakamilika. UNDP wameahidi kuchangia   kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akisadiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), kumtwisha mkazi wa jimbo hilo ndoo ya maji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maeneo ulikopitia Mradi wa Maji Kikwajuni. UNDP wameahidi kuchangia   kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.Kulia ni Katibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYI inayosimamia mradi huo, Abdallah Ahmed Suleiman.
 Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akizungumza katika mkutano na wananchi wa eneo la Kikwajuni Mao, alipowatembelea baada ya kukagua maeneo unakopita Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 110 kupitia UNDP kukamilisha mradi huo.
 Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa Kikwajuni Mao, katika mkutano huo aliongozana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib.UNDP wameahidi kuchangia  kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha Mradi wa maji katika jimbo hilo.
Mkazi wa Jimbo la Kikwajuni, Mohamed Seif Said, akijiandaa kumvisha zawadi ya kofiaMratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez baada ya kuzungumza na wananchi katika mkutano uliohusu Mradi wa Maji jimboni hapo ambapo UNDP waliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika.Kulia ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib.

Na Abubakari Akida
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limechangia kiasi cha shilingi 110 milioni katika kuwezesha huduma za maji kwa wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kupitia Mradi wa Maji Kikwajuni uliozinduliwa na Rais wa Zanzibar,Dk. Mohamed Shein miaka miwili iliyopita.

Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo baada ya kutembelea vituo na vyanzo vya mradi huo vya Migombani na Kilimani, Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP, Alvaro Rodriguez alisema lengo lao ni kuona jamii zinapata huduma mbalimbali ili kuweza kuleta maendeleo na wao wanachangia kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika.
“Nimeridhishwa na maendeleo ya mradi unaotarajiwa kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 10,000 wa jimbo hili, UNDP inajitolea kiasi cha shilingi milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika na wananchi wapate huduma ya maji,” alisema mwakilishi huyo wa UNDP
Akizungumza kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira,Salama Abood Talib, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha inashirikisha wadau mbalimbali katika kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa wananchi wa maeneo mbalimbali visiwani humo na amemshukuru mwakilishi wa UNDP kwa msaada waliotoa katika kumalizia mradi huo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni amesema mradi huo una awamu tatu huku awamu mbili zikiwa  zishakamilika na wapo katika awamu ya mwisho ya kukamilisha mradi huo na  amemshukuru mwakilishi huyo  kwa msaada huo ambao utasaidia kukamilika haraka ili wananchi wafaidike na huduma hiyo.
Akizunguma kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Ahmed Said Makame alisema jimbo la Kikwajuni limekua na changamoto ya huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo na anashukuru mradi huo utakapokamilika tatizo hilo litakua limekwisha.
Mradi wa Maji Kikwajuni unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi milioni 344,000,000 ambapo awamu ya kwanza na ya pili ikiwezeshwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Mbunge wa Jimbo hilo, michango ya wananchi na Serikali ya Japan. Mradi huo utakapokamilika utanufaisha wakazi zaidi ya 10,000 wa jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar.

Jafo akitaka kikundi cha DOYODO kuongeza ubunifu

0
0
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwasha mtambo wa kufyatulia matofali.
 Naibu Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akizungumza na Wanafunzi waliokuwa wanafundishwa masomo ya ziada(tution) katika ofisi ya DOYODO.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa taasisi ya DOYODO na Afisa Vijana kutoka Manispaa ya Dodoma alipokuwa anakagua miradi mbalimbali mapema leo ofisini kwao mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari akiwataka vijana wa taasisi ya DOYODO kuwa mfano wa kuigwa Dodoma na nchi nzima katika kampeni yao ya kujiajiri wenyewe.



Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI)Mhe.Selemani Jafo amewataka vijana wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana Dodoma(DOYODO) kuongeza ubunifu ili waweze kuwa washindani katika soko la biashara kwa kutumia fursa ya  wahamiaji wanaokuja Dodoma.

Mhe.Jafo aliyazungumza hayo alipokuwa anakagua miradi mbalimbali ya taasisi hiyo mapema leo na kuwataka kuwekeza kwenye kilimo  kwa kuwa   wanafikilia kupata eneo lao wenyenye ni vyema  kupata hekari moja kwa ajili ya kilimo cha mboga mboga na matunda kwani kinalipa.

’’Kumekuwa na tabia ya vijana kuchagua kazi na baadhi yao kusubiri kupata ajira kutoka Serikalini lakini nyie mmetoa mfano badala ya kutegemea ajira, mmejiajiri na ntahakikisha baadhi ya wabunge wanakuwa wa kwanza kuja kununua matofali hasa kwa wale wanaojenga Dodoma ’’

“Nitaongea na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma ili mpatiwe milioni moja kutoka mfuko wa 5% ya makusanyo ya Manispaa ya Mapato ya vijana na milioni kumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na mimi nachangia  kwa kununua matofali mia tano “Mhe.Jafo aliahidi.

Naye Afisa Mipango na Muhasibu wa DOYODO Elias Mbogo amesema taasisi inajipatia kipato chake kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo ada ya uanachama,tozo,miradi yao na misaada kutoka kwa wadau wa Taasisi. 

Taasisi ya DOYODO imesajiliwa kisheria mwaka 2002 na kuanza kufanya shughuli zake rasmi toka 2015 na miradi waliyonayo ni mradi wa matofali,tuition(elimu),ufundi chelehani na kukodisha ukumbi kwa ajili ya semina na sherehe mbalimbali.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images