Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1280 | 1281 | (Page 1282) | 1283 | 1284 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (kushoto) baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Singida kutoka kwa Katibu Tawala huyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
   Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na watumishi wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akipokea maoni na malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watumishi hao mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
   Mmoja wa watumishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida akitoa maoni wakati wa kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua jambo kwa mmoja wa watumishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida alipokuwa akisikiliza malalamiko ya mtumishi huyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
  Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais - Menejementi ya Utumishi wa Umma, Bi, Jeanfrida Mushumbusi akihakiki taarifa za mmoja wa watumishi kutoka mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

  0 0

    Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi akizungumza na wakina mama wajasiriamali kwenye kata ya Nguvumali wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo aliyaandaa kwa ajili ya kukabiliana na fursa mbalimbali za kujiwekeza kiuchum ambapo mafunzo hayo yatafika kwenye kata 27 za Jiji hilo
   Baadhi ya wanawake wajasiriamali katika Kata ya Nguvumali Jijini Tanga wakiwa kwenye mafunzo hayo
  WANAWAKE wajasiriamali Jiji la Tanga wanatarajiwa kunufaika na mafunzoya kuwajengea uwezo katika utengenezaji na ubinifu wa bidhaambalimbali ili waweze kujikwamua kichumi jambo ambalo litasaidiakuondokana na utegemezi kwenye jamii.

  Mafunzo hayo ambayo yamekwisha kuanza katika kata ya Nguvumaliyanatarajiwa kuwafikia wanawake wajasiriamali 120 na baadae kuendeleakwenye maeneo mengine katika Jiji la Tanga.

  Akizungumza juzi wakati akifungua mafunzo hayo,Mstahiki Meya wa Jijila Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi alisema mpango huo utasaidiakuwakomboa wanawake kiuchumi lakini pia kuwaandaa na ujio wa miradimikubwa miwili mkoani hapa ikiwemo wa bomba la mafuta na kiwandakikubwa cha kuzalishia saruji.

  Alisema pia licha ya kuwapa uelewa masuala hayo lakini namna bora yakuzitumia kwa malengo yatakayokuwa na tija fedha wanazokopa kutokakwenye taasisi za kibenki kwani baadhi yao wanashindwa kutambuawazitumie vipi na kuzirejesha.

  “Utakuta wakina mama wajasiriamali wanakopa fedha kwenye taasisimbalimbali kwa malengo ya kufanya biashara lakini kutokana na kutokuwana elimu hivyo wanaishia kuzitumia kwenye mambo mengine na kusababishamadeni “Alisema.

  “Lakini pia wanawake wajasiriamali wanapaswa kutumia fursa ya mafunzohayo kuweza kujiongezea wigo mpana kwani ujio wa mradi wa bomba lamafuta wenzetu wanaokuja kutoka nchini Uganda hivyo lazima waweze nauwezo wa juu “Alisema.

  Aidha pia alisema wanatumia nafasi hiyo kuwaandaa kwa kusaidia iliwaweze kujiandaa kwa kuongeza uzalishaji wa kilimo cha mboga mboga namatunda ikiwemo uuzaji wa mayai.

  Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Kata ya Nguvumali,Saumu Omari mafunzo hayo yamewaongezea maarifa ambayo wanawezakuyatumia ili kuweza kuongeza uzalishaji lakini pia kukabiliana nasoko la ushindani wa bidhaa.

  Alisema kupitia elimu hiyo ya ujasiriamali wanaweza kuona namna ganibora ya kuanzisha na kubuni miradi ya kuwainua kiuchumi kwa kuzitumiafursa zitakazo patikana
  kutokana kwa kuwawezesha kukuza kipato chake.

   Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki  katika swala ya magaharibi katika  futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu mjini  Chato, mkoani Geita, Juni 21, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifuturu pamoja na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC)  Dayosisi ya Geita (kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alhaj Yusuph Kabaju(kulia) katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli, mjini  Chato, mkoani Geita  Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Dayosisi ya Geita katika futari iliyoandaliwa na Waziri Mkuu kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli  mjini  Chato mkoani Geita  Juni 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza  na wananchi wa eneo la Kigongo feri Wilaya ya Misungwi, wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Chato kwa ziara ya siku mbili  Juni 21, 2017.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu,  Ezekiel Kyunga wakati alipowasili mjini Chato mkoani Geita  Juni 21, 2017 kwa ziara ya siku mbili mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  *Ahimiza nyumba za ibada zisitumiwe vibaya

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba waumini wa dini za Kiislamu na Kikristo nchini wahakikishe nyumba zao za ibada hazitumiki kuleta migogoro.

  Ametoa ombi hilo jana usiku (Jumatano, Juni 21, 2017) wakati akizungumza na mamia ya waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu pamoja na viongozi wa dini walioshiriki ibada ya futari wilayani Chato, mkoani Geita.

  Akizungumza na waumini hao kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema Mheshimiwa Rais alishapanga kufika Chato ili kushiriki nao ibada ya iftar lakini ametingwa na majukumu ya kitaifa akaona ni vema amtume yeye ili amwakilishe.

  “Mheshimiwa Rais alishapanga kuja Chato kufuturu pamoja na wana-Chato lakini kadri siku zinavyozidi kwenda anajikuta anabanwa na majukumu mengi ikiwemo kukutana na wageni wa kimataifa, kwa hiyo akaona ni vema nije kumwakilisha katika shughuli hii,” alisema.

  “Mheshimiwa Rais anawaombea heri katika siku zilizobakia za mfungo wa Ramadhan ili mmalize salama na Mungu akijalia muweze kusherehekea pamoja, na pia anawatakia heri wale watakaoendelea na sita tushawal.”

  Akisisitiza kuhusu amani na utulivu nchini, Waziri Mkuu alisema: “Hatupendi kusikia kuwa msikiti fulani wamechapana viboko kwa sababu ya kugombea uongozi au kwenye kanisa fulani waumini wamepigana wakigombea mchungaji wao.”

  “Tutumie nyumba zetu za ibada kudumisha amani na mshikamano wetu. Napenda niwahakikishie kuwa Serikali yenu chini ya Rais John Pombe Magufuli itaendelea kuheshimu dini zote.”

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwakumbusha waumini hao kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhan ni wa toba kwa kila muumini. “Huu mwezi mafundisho yake yanasisitiza amani, uvumilivu na kusameheana. Nipende kuwasihi kwamba tuendelee kudumisha utulivu tulionao,” aliongeza.

  “Nipende kusisitiza kwenu wana-Geita na wana-Chato kwamba jukumu kubwa mlilonalo ni kuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais ili Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, busara na uongozi wa kimungu katika maamuzi yake. Niwasihi ndugu zangu Waislamu na Wakristo, tuendelee kuwaombea viongozi wote wa kitaifa kila siku ili wafanye kazi kwa kuongozwa na Mungu,” alisema.

  Awali, akisoma risala mbele ya Waziri Mkuu, Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Chato, Sheikh Ally Moto alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapa fursa ya kuweza kushiriki ibada ya iftar pamoja na watoto yatima na wajane.

  Alisema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano na ili kudumisha amani wilayani humo, waumini wa Kiislamu na Kikisto wameunda Kamati ya Amani ya wilaya hiyo inayojulikana kama Interfaith Committee.

  Naye Mbunge wa Chato ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuandaa futari hiyo ambayo imejumuisha wana Chato kutoka pembe nne za wilaya hiyo.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Geita, Askofu Mussa Magwesera wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Dayosisi ya Geita alitoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Magufuli na kuwapongeza viongozi wakuu wa kitaifa kutokana na utendaji wao unaogusa mioyo ya Watanzania.

  “Ninyi wote watatu ni viongozi ambao Mungu amewaweka kuongoza nchi yetu. Katika miezi hii 18, mmefanya mambo makubwa, ni imani yetu kuwa ataendelea kuwaongoza katika utendaji kazi wenu,” alisema.

  Akitoa shukrani, Sheikh wa Mkoa wa Geita, Sheikh Yusuph Kabaju ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Mkoa huo, alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapa fursa wana-Geita kujumuika pamoja katika futari hiyo na kuahidi kudumisha amani ya Tanzania.

  “Tunakushukuru kwa kutuunganisha wana Geita katika futari hii japo umeamua kufanyia ibada hii hapa Chato. Maneno ya Quran tukufu yanasema malipo ya waliofunga anayapata pia yule aliyefuturisha waliofunga,” alisema.

  Sheikh Kabaju pia alisoma dua ya kumuombea Mheshimiwa Rais Magufuli pamoja na viongozi wa kitaifa. Pia aliombea amani kwa ajili ya Taifa la Tanzania.  IMETOLEWA NA:

  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  ALHAMISI, JUNI 22, 2017.

  0 0

    The Ngorongoro District Authorities, in collaboration with the UNESCO Dar es Salaam Office, will welcome the Permanent Secretary of the Ministry of Health (MoHCDGEC), Dr. Mpoki Ulisubisya, the Vice-Chancellor of the Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS), Prof. Ephata Kaaya and the UNESCO Representative, Ms. Zulmira Rodrigues on 23 June 2017 for a visit to the first Tele-health Centre in the country. The mission is taking place in the context of the preparations of the handover from UNESCO to Government of this innovative model for provision of specialised health care to remote rural populations. 

  The Tele-Clinic is part of a UNESCO/Samsung Digital Village programme in a remote Maasai village in Ngorongoro, Arusha. It is an innovation platform, testing health services provision in maternal and infant care, dental and Ear, Nose and Throat (ENT) services that utilizes connectivity and smart technologies. It will be the first tele-health pilot to connect all levels of the Tanzanian healthcare system reaching out to the remotest communities. The pilot is in the initial service trial phase, focusing first on the operationalization of remote maternal consultations.  The Digital Village is a pioneering example that demonstrates how remote communities can be empowered by modern technology improving their access to quality health and education services and build capacities to generate decent income. 

  UNESCO’s innovation approach is unique in its focus on incorporating the cultural specifics in the programme by working in close collaboration with the local community, traditional leaders and healers and by building on traditional Maasai livelihoods such as Maasai crafts to tap into the opportunities for sustained development of the Northern Circuit. The visitors will also be introduced to other Digital Village programme components including e-learning, livelihoods development and cultural tourism development activities.

  0 0

  --
   Mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam akiwa amempakia mwanawe katika baiskeli huku wakifanya Manunuzi ya vitu kadhaa kwa ajili ya maandalizi ya sikuu ya Eid  El Fitri kama walivyokutwa na Camera yetu katika mtaa wa Congo Soko Kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam
   Mchuuzi wa miwani na Saa za watoto akimajribisah mmoja ya mtoto aliyeongozana na Baba yake kufnya manunuzi katika soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam
   Wanawake wakichagua nguo za watoto wao wa kike ambazo zimemwagwa chini katika barabara ya mtaa wa Congo, katika soko kuu la jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya sikuu ya Eid el Fitri
   Mzazi akimjaribisha nguo mtoto wake wa kiume kutoka kwa wamachinga wa soko la Kariakoo kwa ajili ya maandalizi ya sikuu ya Eid el Fitri
   Wanawake wakiwa wanachgua  viatu vya kuvaa  kwa ajili ya maandalizi ya sikuu ya Eid el Fitri
  Sehemu ya umatai wa watu uliofurika katika mtaa wa Congo katika soko kuu la Kariakoo jijini Dar es Salaam

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge pamoja na watendaji wake kuhakikisha Mji wa Kisarawe uliopo mkoani Pwani unapata huduma ya maji safi na salama.

  Rais Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo jana mkoani Pwani wakati akizindua Mradi wa upanuzi wa Mtambo wa  maji wa Ruvu Juu na ulazaji wa Mabomba Makuu kutoka Mlandizi kwenda Jijini Dar es Salaam.

  Mh. Magufuli amesema kuwa Mkoa wa Pwani umefanya kazi kubwa ya kutunza miundombinu ya maji ambayo imewezesha kuhudumia wananchi wa Dar es Salaam hivyo ni haki kwa wananchi wa Mkoa huo kufaidika na maji wanayoyatunza kwa muda mrefu.

  “Ninafahamu Mji wa Kibaha kwa sasa hauna shida ya maji, shida iliyopo ni kuzidi kwa presha ya maji ambayo sio tatizo la DAWASA wala DAWASCO hivyo ili kutatua tatizo hilo ni jukumu la Wizara husika na watendaji wake kujipanga na wahandisi wa maji kuunganisha bomba kutoka Wilaya ya Kibaha hadi Kisarawe ambapo kuna changamoto ya maji safi na salama,” alisema Rais Magufuli.

  Akiongelea utunzaji wa miundombinu ya maji, Rais Dkt. Magufuli amewataka watendaji wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kuhakikisha wanashughulikia maji yanayopotea kwa kurekebisha miundombinu ambayo imeharibika na kuweka miundo mbinu mipya inayoweza kuhimili wingi wa maji.

  Aidha, Rais Magufuli ameishukuru Serikali ya India kwa kutoa trilioni 1.3 kwa ajili ya kuendeleza miradi ya maji kwa Miji 16 nchini ambayo ikikamilika itawezesha wananchi wengi kupata maji safi na salama hivyo amewaahidi kudumisha ushirikiano uliopo katika sekta ya maji baina ya nchi hizo mbili.

  Kwa upande wake Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema kuwa Mradi huo ni sehemu ya miradi mikubwa saba ya kimkakati inayoendelea kupanuliwa ikiwemo ya upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini, Ruvu Juu, Uchimbaji visima virefu, Ujenzi wa bwawa la Kidunda, upanuzi wa mtandao wa usambazaji maji, mradi wa kupunguza upotevu wa maji na uboreshaji wa mfumo wa majitaka. 

  “Mradi huu umejengwa na fedha za mkopo jumla ya shilingi bilioni 87 kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim ambapo umesaidia pia kujenga nyumba 17 za wafanyakazi katika eneo la mradi,” alisema Mhandisi Lwenge.

  Mhandisi Lwenge amefafanua kuwa baada ya upanuzi huo mashine zinauwezo wa kuvuta maji kati ya lita milioni 182 - 196 kwa siku hivyo hadi kufikia mwezi Machi, 2016 wananchi 742,611 wa mkoani Pwani wanapata maji safi na salama.

  Nae Balozi wa India nchini Tanzania, Sandeep Arya amesema kuwa uhusiano wa sekta ya maji kati ya Tanzania na India ulianza miaka 35 iliyopita na maji ndiyo sekta ya kipaumbele inayounganisha Tanzania na India hivyo uhusiano baina ya nchi hizo ni wa kindugu.

  “Uamuzi wa kutoa mkopo wa shilingi Trilioni 1.1 kwa ajili ya mradi wa usambazaji maji katika Miji 17 nchini Tanzania unaendelea kudhihirisha ushirikiano wetu,” alisema Balozi Arya.

  Uzalishaji wa sasa wa mitambo yote unafikisha jumla ya lita Milioni 502 kwa siku ambazo ni majumuisho ya maji ya Ruvu Juu lita milioni 196, Ruvu chini lita milioni 270 pamoja na mtambo mdogo wa Mtoni unaozalisha kiasi kidogo kwa siku.
  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli

  0 0


  0 0

  Loveluck Mwasha, a midwife and lecturer at The Aga Khan University (AKU) School of Nursing and Midwifery – Tanzania has received the coveted Midwife for Life Award 2017.

  Amina Sultani of Afghanistan also received a similar Award presented by Save the Children, and the International Confederation of Midwives (ICM) at the ICM 31st Triennial Congress in Toronto, Canada.

  The midwives have been awarded for their outstanding roles in developing the profession in their countries despite all odds. ICM President Frances Day-Stirk and Save the Children President and Chief Executive Officer Patricia Erb jointly presented the awards.

  Mwasha who has practiced midwifery for 30 years is a staunch advocate for the midwifery profession, midwives’ improved working conditions and improved health for mothers and new-borns in Tanzania.

  She has also been a “steadfast advocate for and mentor” to midwives through her work on the board of the Tanzania Nursing and Midwifery Council and at The Aga Khan Hospital and AKU School of Nursing and Midwifery.

  “My work is an opportunity to advocate for better support and training of midwives,” Mwasha said. “We work with stakeholders to help them appreciate midwives’ role in supporting women’s reproductive health, from community groups to members of parliament.”

  In Tanzania, 257 women and their babies die due to complications of pregnancy or childbirth which means 93,800 deaths each year, 70 percent or more of which are preventable with proven and effective interventions.

  Midwives are seen as the single most important cadre for preventing maternal and new-born deaths and stillbirths.

  Especially in humanitarian contexts and for poor or hard-to-reach populations, midwives provide the majority of immediate care to mothers and new-borns, often without support, materials, training, or recognition.

  Mwasha has been a lecturer at the University since July 2015 and teaches Reproductive Health Nursing –midwifery, coordinating electives course. Her research interests are in midwifery focused care during labour, delivery, immediate postnatal care for mother and neonatal.

  Her debut in midwifery practice was when she single-handedly attended to a woman who had just delivered and her baby was in poor condition.

  “It was in the evening and I was alone with all the candle lights. The baby was flat, not crying and in poor condition but I managed to resuscitate her and she survived. From that moment I gained the confidence and that is where my career as a midwife took off,” said Mwasha in an interview ahead of the ICM Congress.

  She said the Award has motivated her to pursue her passion for imparting knowledge that will boost quality healthcare for women and children in Tanzania.

  “I commit to help my students discover themselves and become midwives who are competent and can confidently deliver quality maternal and new-born care,” said Mwasha.

  Mwasha attributes her exemplary achievements to the training she received at AKU and senior midwives she worked with at the time she began practising midwifery.

  She holds a Master’s of Science in nursing degree from AKU School of Nursing and Midwifery Karachi, Pakistan and a Bachelor of Science in Nursing from the AKU School of Nursing, Tanzania Institute of Higher Education (TIHE).

  The ICM President said the needs of midwifery across multiple settings – humanitarian, marginalised, or hard to reach – are remarkably similar.

  “Both Loveluck and Amina are working for the same goals in very different settings: for the recognition of their work, supportive policies, and the training and resources they need to enable mothers to give birth safely and their new-borns to get a healthy start in life,” she said.

  Save the Children President said she was “impressed” by the level of interest in the awards this year.

  Of the more than 50 nominations from 18 countries, Erb said, “It’s heartening to see this clear evidence of midwives speaking up and making a difference in policies and practices that affect midwifery and the conditions under which midwives work.”

  The ICM is highlighting some of the challenges midwifery faces at the policy and facility level this week at its 2017 Triennial Congress in Toronto.

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (kushoto) akizungumza na maafisa wakuu wa Jeshi la Polisi alipofanya kikao na maafisa hao akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar kabla ya kwenda kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Ali Mohamed Shein. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamdani makame. Picha na Hassan Mndeme.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya zanzibar alipokwenda kufanya kikao na kamati hiyo akiwa kwenye ziara ya kikazi visiwani Zanzibar. IGP alikwenda pia kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar mheshimiwa, Dk Ali Mohamed Shein. Picha na Hassan Mndeme.

  0 0

  Mtaalamu  kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (kushoto) akitoa maelekezo ya matumizi ya  mashine ya kushindilia na kutoa uchafu kwa ajili ya kusafishia uwanja  kwa uongozi na maafisa wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa.
   Mtaalamu  kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (kulia) akionyesha   mashine ya kukatia majani  na  kusafishia uwanja  kwa uongozi na maafisa wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa.
  Mtaalamu  kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (Mwenye kofia) akionyesha  mashine ya kubebea uchafu  katika ziara ya kukagua vifaa vinavyoyumika katika ukarabati wa uwanja  kwa uongozi na maafisa wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  leo Jijini Dar es Salaam katika Uwanja wa Taifa .
  Mkurungezi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yussuph Singo (kulia) akimpa mkono wa shukrani Mtaalamu wa Uwanja kutoka Timu ya Everton Bw. Shane Mcgeown (kushoto) baada ya kutoa maelekezo ya vifaa mbalimbali vya kutunza mazingira ya Uwanja wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence WHUSM).

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na mmoja wa wazee waliofika kupatiwa huduma katika viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo ofisi nzima ya Manispaa hiyo imehamia viwanjani hapo kwa ajili ya kuhudumia watu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
   Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akiwa na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto wakitoa huduma kwa wadau waliofika kutaka msaada juu ya mambo yanayowakabili . Ofisi za Manispaa hiyo zimahamia hapo kwa muda kwa ajili ya kuhudumia watu, ikiwa ni sehemu ya mahadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma katika wilaya hiyo.
  Mkurugenzi  wa Manispaa ya Ilala Msongela Palela akimuhudumia mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliofika katika viwanja vya mnazi mmoja.
    Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni ya kuuza vifaa vya kuzimia moto inayojulikana kwa jina la Zima Moto  
   Afisa mkaguzi  Msaidiz wa jeshi la Zima Moto , akitoa maelezo kwa  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema wakati wa maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ilala ambo wanatoa huduma kwa wananchi katika Viwanja vya mnazi mmoja 

  0 0


  Mwili wa Shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga aliyefariki dunia juzi katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma umezikwa leo katika makaburi ya Nguzo Nane mjini Shinyanga.

  Mbali na kuwa mshabiki wa Yanga Ally Yanga pia alikuwa mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na siyo kwamba alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.

  Ally alizaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.
  Mwili wa marehemu Ally Yanga ukiwa umebebwa kwa ajili ya mazishi katika makaburi ya Nguzo Nane Mjini Shinyanga leo Ijumaa June 22,2017.Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
  Mwili wa Marehemu Ally Yanga ukizikwa kwenye makaburi ya Nguzo Nane mjini Shinyanga
  Awali kabla ya mazishi,Sheikh  wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiombea mwili wa marehemu Ally Yanga 
   Naibu katibu mkuu CCM bara Rodrick Mpogolo akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais John Pombe Magufuli 
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali
  Naibu kartbu mkuu CCM bara Rodrick Mpogolo akisaini kitabu cha rambirambi nyumbani kwa Marehemu Ally Yanga Stendi ya Mabasi ya wilaya mjini Shinyanga
  Mkuu wa Wilaya Josephine Matiro( wa tatu kutoka kulia) , akifuatiwa na mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa msibani
  Wananchi,wapenzi wa mpira wa miguu na viongozi wa serikali ,wabunge wakiwa kwenye maombolezo nyumbani kwao na marehemu Ally Yanga mjini Shinyanga
  Wananchi wakiwa msibani
  Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

  0 0

   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea vitabu kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Ndg. Mungwe Athman (katikati) kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tukio lililofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa na Wageni wengine ni Wajumbe wa tume ya Utumishi wa Bunge wakiongozwa na Mhe. Mussa Zungu(nyuma kulia).
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akikata utepe ili aweze kufungua  boksi lenye vitabu alivyokabidhiwa na Mtandao wa kuondoa umasikini kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katikati ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman, wa pili kushoto ni Meneja wa Mtandao huo Ndg. Peter Yobwa na wengine ni Wajumbe Mbali mbali wa tume ya utumishi wa Bunge wakiongozwa na Mhe. Mussa Zungu (nyuma kulia).
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akionyesha moja ya kitabu alichokabidhiwa na Mtandao wa kuondoa umasikini, vitabu walivyokabidhi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman na kulia ni Mjumbe wa tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Peter Msigwa, nyuma yake pia ni Wajumbe wa tume ya utumishi wa Bunge ambao ni Mhe. Mussa Zungu na Mhe. Mary Chatanda.
   Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza baada ya makabidhiano ya vitabu kwa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Msaada uliotolewa na Mtandao wa kuondoa umasikini, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Mtandao huo Ndg. Mungwe Athman, tukio hilo pia lililouzuliwa na Wajumbe wa tume ya Utumishi wa Bunge katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na  Mwenyekiti wa Mtandao wa kuondoa umasikini, Ndg. Mungwe Athman (kushoto)kabla ya Makabidhiano ya vitabu kwa Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tukio lililofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili akihutubia na kutoa uzoefu wa nchi yake dhidi ya mapambano dhidi ya rushwa wakati wa ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa uliofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakiangalia kitabu kinachoelezea mapambano dhidi ya rushwa na Rais wa zamani wa nchi ya Georgia Mhe. Mikheil Saakshvili (kushoto) wakati Ufunguzi Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
  Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Ngazi za juu wa Mapambano dhidi ya Rushwa , Rais huyo wa zamani alitoa uzoefu wake na wa nchi yake katika kupambana na rushwa.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali haitarudi nyuma kamwe katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini mpaka hapo vitendo hivyo vitakapokoma.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua Mkutano wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa vita ya kupambana na vitendo vya rushwa na ufisadi ni kipaumbele cha kwanza katika Serikali ya awamu ya Tano na wale wote wanaowezesha, kunufaika na kuhusika na vitendo hivyo wataendelea kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo nchini.

  “Kupambana na rushwa ni jambo la msingi na muhimu kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo endelevu katika nchi yeyote Duniani,” Amesisitiza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu Tano chini ya Uongozi Shupavu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli inaendelea kukaza kamba katika mapambano dhidi ya rushwa ambayo kwa muda mrefu sasa yamechangia kurudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

  Amesema Serikali ya Tanzania inalenga kufikia kipato cha kati na kuimarisha uchumi wa viwanda hadi ifikapo mwaka 2015 hivyo malengo hayo yatafanikiwa haraka iwapo tu vitendo vya rushwa vitakomeshwa katika ngazi zote nchini.

  Rushwa ni baya na imeharibu sana maisha ya watu na maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii hivyo ni lazima ikomeshwe ili jamii iishi maisha mazuri“Ameeleza Makamu wa Rais.

  Amesema kuwa hakuna nchi yeyote ambayo haijagushwa na misukosuko ya vitendo vya rushwa Duniani lakini Bara la Afrika limeendelea kuteseka sana na vitendo hivyo kwa miongo kadhaa sasa hivyo jitihada za pamoja zinatakiwa katika kutokomesha vitendo hivyo.

  Kwa upande wake, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa wizara yake itaendelea kupambana na vitendo vya rushwa ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali kwa watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao ya kazi.

  Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia bi Bella Bird amepongeza jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano za kupambana na vitendo vya rushwa na kusisitiza kuwa Benki hiyo ataendelea kutoa mchango wake wa hali na mali katika kuisaidia Tanzania katika uimarishaji wa mapambano hayo.

  Mkutano huo wa Kimataifa wa ngazi ya Juu wenye lengo la kubadilishana uzoefu katika mapambano dhidi ya Rushwa unaofanyika nchini unahudhuriwa na viongozi mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wenye uelewa na uzoefu katika mapambano dhidi ya rushwa.

  0 0

  Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Harmorapa na Juma Nature (Sir Nature) watapamba tamasha la muziki Raha ya Rocky City lililopangwa kufanyika wakati wa sikukuu ya Eid El Fitr kwenye ukumbi wa Buzuruga Plaza.

  Mbali ya Sir Nature na Harmorapa ambao wanatamba na wimbo wa Kiboko ya Mabishoo, muandaaji nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, P-Funk naye atashiriki katika tamasha hilo lililoandaliwa na kituo cha redio nyota ya kanda ya Ziwa, 102.5 Lake FM.
  Mkurugenzi Mkuu wa 102.5 Lake FM, Doreen Noni amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo lililopangwa kuanza saa 12.00 jioni yamekamilika na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya watarajie burudani safi kutoka kwa wasanii mbalimbali mbali ya Sir Nature na Harmorapa.

  Doreen alisema kuwa Nature na Harmorapa watafanya onyesho la kwanza ‘live’ kutambulisha wimbo wa Kiboko ya Mabishoo kwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa muziki huo wa mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani.

  “Harmorapa pia atatambulisha nyimbo zake mbalimbali kama, Nundu, Usigawe Pasi wakati Nature atawakumbusha mashabiki wake wa zamani kwa nyimbo nyota za zamani kama Ugali, Hili Game, Utajiju, Naja, Hakuna Kulala, Inaniuma Sana, Ubinadamu Kazi, Kighetogheto na Mgambo.

  “Tamasha hili ni sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya Eid El Fitr, tumeandaa burudani mbalimbali ambazo hazita wachosha mashabiki, lengo ni kuleta msisimko wa aina yake kwa mashabiki wa Kanda ya Ziwa,” alisema Doreen.

  Alifafanua kuwa Lake fm imedhamiria kutoa nafasi kwa wasanii wa mkoa wa Mwanza hivyo kutakuwa na wasanii mbalimbali wa Mwanza ambao nao ni moto wa kuotea mbali. Wasanii hao ni Jimmy Chansa, Future JNL, kundi la Lakezonia, Ngeta na Dogo D, Abu Mkali, vile vile kutakua na makundi ya kudans TYT na MCB pia jopo la warembo lukuki kutoka 21plus models na Blackfox models.

  Mbali na hayo, pia kutakuwa a burudani safi ya muziki kutoka Ma-DJ wa 102.5 Lake FM. Ma DJ hao deejays hao ni DJ Ten Ten, DJ Jabir, DJ Basta na DJ Steve wa Mitindo.

  0 0

   Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.
  Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.
   Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro.
  Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kulia) akimkabidhi Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe zawadi ya picha ya kumbukumbu ambayo ilipigwa wakati wawili hao wakitua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Matambwe, Selous, Kwa mujibu wa balozi huyo siku hiyo haikuwa rahisi kwa ndege hiyo kutua kwa kuwa mvua zilikuwa zinanyesha. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

  0 0


  0 0


  . Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Nyanda za juu kusini Bwana Jackson Kiswaga akizungumza na wananchi waliojitokeza wakati wa kugawa msaada katika kituo cha watoto Dairlybread kilichopo kata ya Nzihi, akiwa na baadhi ya viongozi wa kata hiyo.
  Mwenyekiti wa kata ya Nzihi akifafanua jambo mbele ya wananchi na watoto wa kituo cha Dairlbread kilichopo kata ya Nzihi mkoani Iringa.
  Baadhi ya watumishi wa kituo cha kulea watoto cha Dairlbread cha kata ya Nzihi  wakijitambulisha wao na watoto mbele ya mkurugenzo wa kampuni ya Tigo nyanda za juu kusini Bw. Jackson Kiswaga hayupo pichani.
  Mkurugenzi wa Tigo kanda ya nyanda za juu kusini, Jackson Kiswaga akikabidhi misaada ya vyakula na mahitaji mengine  kwa vituo vya watoto wenye uhitaji  vya Daily Bread Ahsante Sana na Kipera Disabled  mkoani Iringa juzi.

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) pamoja na Meneja Uwajibikaji wa SBL, Hawa Ladha (kulia) wakimtwika ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni Hamisi Ramadhani leo ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) pamoja na Diwani Kata ya Chang'ombe, Benjamin Ndalichako (kushoto) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

  Baadhi ya wananchi wakiwa katika mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).

  Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Temeke, Primy Damas (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya mradi huo mara baada ya kuzinduliwa. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie na Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamin Ndalichako wakishuhudia.

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.

  KAMPUNI ya Bia Serengeti leo imezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.

  Ukiwa na uwezo kwa kuhudumia watu 4,000 mradi huo unajumuisha kisima pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila masaa ishirini na nne.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni miongoni mwa mikakati kama hiyo ambayo kampuni ya bia imeiendesha katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.

  Weesie alisema kwamba mradi wa Chang’ombe sio tu kwamba utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia utaongeza tija kiuchumi, “hususani kwa watoto wa kike na wanawake ambao hawatahitaji kutumia saa nyingi kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule wakiwa huru.”

  “SBL ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu na Maji kwa Uhai ikiwa ni mojawapo ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyabainisha katika lengo lake kuipatia jamii msaada katika jumuia inamohudumia”, alisema Weesie akielezea vipaumbele vingine hivyo kama: Kutoa Stadi za Maisha, Undelevu wa mazingira na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

  Mkurugenzi huyo Mtedaji aliendelea kusema SBL ina programu ya kilimo ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imewasaidia wakulima zaidi ya 100 nchini kwa kuwapatia msaada wa kiufundi na kifedha iliyowasaaidia kuboresha maisha yao na maisha ya jumuia zao.

  Weesie alisema kutokana na juhudi hizo, “SBL imeweza kuibua tani za malighafi inazotumia kutoka wa wakulima wa hapa nchini kutoka 0 hadi tani 10,000 na hili limechangia katika kukua kwa kampuni na kukuza kipato cha wakulima.”

  Aliendelea kubainisha: “Licha ya kuchangia katika kukua kwa uchumi wa taifa kupitia malipo ya kodi ya mara kwa mara, SBL imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa hususani katika kutoa huduma ya maji safi na salama ndani ya nchi.”

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) pamoja na Diwani Kata ya Chang'ombe, Benjamin Ndalichako (kushoto) wakisfurahia mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji.

  Muonekano wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

  Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva aliipongeza SBL kwa kutoa msaada uliokuwa unahitajika mno, akisema kwamba kampuni hiyo ya bia imekuwa mstari wa mbele katika kukuza miradi ya maendeleo nchini ambayo inawezesha kuwepo kwa jamii inayozalisha na iliyo na afya.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB kwa ajili ya wateja wao mkoani Tanga  iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort,kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu na kushoto ni Meneja wa Benki ya DTB Mkoani Tanga,Athumani Juhudi
   MKUU wa wilaya ya Tanga,Thobias mwilapwa akizungumza wakati wa futari hiyo
   Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akitoa neno kwenye futari hiyo
   Meneja wa Benki ya Diamond Trust BankMkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi akizungumza na waandishi wa habari
   Wageni waalikw
   Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto akisalimiana na Aliyekuwa Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Kassim Kisauji wakati wa hafla ya futari hiyo
   sehemu ya wageni waalikwa wakipata futari

  BENKI ya Diamond Trust(DTB) Tawi la Tanga wanakusudia kupanua wigo wahuduma zao kwa wateja kwa kukarabati na kuongeza namba ya wahudumuikiwa ni mkakakti wa ujio wa fursa mbalimbali mkoani hapa ukiwemomradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka hoima nchini Uganda hadiBandari ya Tanga.

  Hayo yalibainishwa juzi na Meneja wa Benki ya Diamond Trust BankMkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi wakati futari iliyoandaliwa naBenki hiyo kwa wateja wao wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenyeukumbi wa Tanga Beach Resort mjini hapa na kuhu dhuiwa na viongozimbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za Handeni na Tanga.

  Alisema wao wanakusudia kufanya hivyo ili kuweza kuendana na wigompana wa ukuaji wa uchumi kwa mkoa wa Tanga ambao unatarajiwakufanyika kutokana na mradi huo mkubwa .

  “Benki yetu ipo kwenye nafasi ya tano kati ya mabenki zenye amanakubwa za wateja hivyo tumeona kuwaandalia futari hiyo ni namna bora yakuwashukuru wao kwa kuwasapoti”Alisema.

  “Unajua wateja wetu wamekuwa wakitusapoti hivyo ndio maana tumeonavizuri kuwaandalia futari lakini pia niwaambie kuwa  wanaweza kutumana  kusafirisha fedha kwa haraka kutoka nje ya nchi na ndani yanchi”Alisema

  Awali akizungumza katika hafla hiyo,Mkuu  wa Mkoa wa Tanga,MartineShigella aliwataka wakazi wa mkoa huu kuendelea kumuombea Rais JohnMagufuli aweze kuendelea kupigania haki za watanzania wanyonge ambazozimekuwa zikipotea.

  Alisema kuwa kiongozi huyo mkuu wa nchi amekuwa akifanya mambo makubwaya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo haraka na kukuza uchumiambao utatufikisha kwenye mafanikio.

  “Ndugu zangu waislamu tuendelee kuombea nchi yetu na Rais wetu iliyeye na viongozi wote waendelee kutenda yaliyomema na yanayompendezamwenyezi mungu”Alisema RC Shigella.

  “Lakini pia niendelee kuwashukuru kwa kuendelea kudumisha amani namshikamano kwa mkoa huu kwa kipindi cha tokea mwezi ulipoanza mpakasasa  hivyo muendelee kuwa na upendo kwa watu wote.

  Awali akizungumza katika futari hiyo,Shehe wa Mkoa wa Tanga, JumaLuwuchu  aliwataka waislamu mkoano hapa kuendelea mshikamano waliokuwanao kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kuendeleakutenda yaliyo mema.

  “Tuendelee kushikamana tupendane lakini kubwa zaidi tuhakikishatunazingati kufanya ibada mara kwa mara na sio kipindi cha mwezi huutu hata baada ya kumalizika kwake “Alisema.
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

older | 1 | .... | 1280 | 1281 | (Page 1282) | 1283 | 1284 | .... | 1897 | newer