Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

NEWS ALERT: SHABIKI WA YANGA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

0
0
Globu ya Jamii imepokea taarifa ya kifo cha shabiki maarufu wa timu ya Yanga Ally Mohamed almaarufu kwa jina la Ally Yanga. Taarifa zinaeleza kuwa Ally Yanga amefariki Dunia mapema leo katika ajali ya gari eneo la kijiji cha Chipogoro wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Taarifa  rasmi tutawaletea kutoka Jeshi la Polisi kutoka mkoani humo. Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amin.

Taarifa zinasema Ally Yanga alikuwa kwenye msafara wa mbio za Mwenge kabla ya kupata ajali hiyo barabara ya Wiyenzele kuelekea Chipogoro na kufariki hapo hapo.

Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.
Pichani juu na chini ni gari iliyopelekea kifo cha Shabiki huyo wa Yanga,Ally yanga

UBA’S DEBUT $500M EUROBOND OVERSUBSCRIBED 240% BY GLOBAL INVESTORS – FURTHER VALIDATION OF UBA’S PAN-AFRICAN GROWTH STRATEGY

0
0

  Lagos, Nigeria – June 12, 2017 – United Bank for Africa Plc (UBA) successfully raised USD500 million, though a debut Eurobond, which was 240% over-subscribed. The significant investor demand reflects the strong global investor appetite for UBA’s credit and support for the Group’s pan-African financial services strategy. The Global Offering is a five-year senior unsecured benchmark bond (144A/Reg S) listed on the Irish Stock Exchange and will further support the Group’s strategic vision, as it continues to grow its franchise across the continent and client segments.
 The bond, which is rated by both Fitch (B, stable outlook) and S&P (B, stable outlook), matures in June 2022 and was issued with a coupon rate of 7.75%, priced at an effective yield of 7.875%. This pricing is seen by the global investor community as the best possible pricing for a debut issue from a financial institution of Nigerian origin in current markets. The pricing was at par to the recent bond issue by the Federal Republic of Nigeria, which issued USD1 billion in February 2017.
 Investor interest was global, including the United Kingdom, Europe, Asia, the Middle East and the US.
 Speaking on the offering, the Group Managing Director/CEO of UBA Plc, Mr. Kennedy Uzoka stated: “This successful dollar-denominated offering further illustrates global investor confidence in the strong fundamentals of our Group. The USD500 million bond will complement our stable funding base and support the growth of our balance sheet and the overall business. More importantly, this medium-term funding will further enhance our strength in financing profitable, impactful projects on the African continent.” 
Also commenting on the Eurobond, the Group CFO, Mr. Ugo Nwaghodoh said: “UBA’s debut global offering is another milestone for us. It is timely in the Group’s growth phase and aligns with our strategic plan to profitably grow the balance sheet, as we maintain our prudent risk management and benchmark asset quality ratios.”
The United Bank for Africa Plc is a leading pan-African financial institution, offering banking services to more than 14 million customers, across over 1,000 business offices and customer touch points in 19 African countries. With presence in New York, London and Paris, UBA is connecting people and businesses across Africa through retail, commercial and corporate banking, innovative cross border payments and remittances, trade finance and ancillary banking services.

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI VIFAA VYA KUSAIDIA WAKINA MAMA WAJAWAZITO WAKATI WA KUJIFUNGUA KATIKA HOSPITALI MBILI MBAGALA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla maalum ya kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati na baada ya kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo mabeseni 100 yenye vifaa hivyo kati ya 1000 yalikabidhiwa kwa hospitali ya Mbagala Rangi Tatu, Dar Es Salaam.
 Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akihutubia mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100,Mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Baadhi ya mabeseni yenye vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania wakiangalia mbabeseni yanya vifaa vya kusaidia wakina mama kujifungua yaliotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bi.Arafa Nurdin wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala Rangi Dkt. Joseph Kiani wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali ya Mbagala Rangi 3 kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsalimia mtoto mwenye miezi miwili Jenifer Mathias, kulia ni baba wa mtoto Bw. Mathias Miano mkazi wa Kingugi, Mbagala kabla uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar ,hospitali ya Mbagala Rangi 3 ilikabidhiwa mabeseni hayo yenye vifaa 100 pamoja na kituo cha Afya cha Mbagala Round Table nacho kilipokea mabeseni 100
 Sehemu ya wananchi wa Mbagala Kizuiani kwenye kituo cha Afya cha Mbagala Round Table waliojitokeza kumsikiliza  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vifaa vya kusaidia wakina mama wajawazito wakati kujifungua vilivyotolewa na Shirika la Red Crescent la Kuwait ambapo zaidi ya mabeseni 1000 yatatolewa kwa hospitali za Tanzania Bara na Zanzibar.

                           .............................................................. 
     Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua zoezi la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 200 yaliyotolewa na Ubalozi wa Kuwait nchini kwa ajili ya wanawake wajawazito katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu  na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Lengo la mpango huo ni kutoa mabeseni hayo zaidi ya 1,000 kwa wanawake wajawazito wasio na uwezo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kama hatua ya kukabiliana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito nchini.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vifaa tiba hivyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mpango huo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito kwa kukosa vifaa tiba kutokana na umaskini unaowakabili.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kwa maeneo yaliyopatiwa mabeseni yenye vifaa tiba yahakikishe vifaa hivyo vinatolewa kwa wanawake wajawazito ambao baadhi yao wanakata tamaa kwenda kujifungulia kwenye hospitali au kwenye vituo vya afya  kwa kukosa vifaa hivyo kwa sababu ya umaskini.

Amesema mkakati uliopo wa Serikali ni kuhakikisha huduma za afya nchini zinaendelea kuboreshwa hasa huduma ya mama na mtoto ambapo kutokana na umuhimu wa sekta ya afya Serikali imetenga fedha za kutoka katika bajeti ya mwaka 2017/2018.

Makamu wa Rais ameeleza kuwa mradi huo wa ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba katika mradi huo kuanzia sasa utasimamia na wake wa viongozi wastaafu na wakiwemo wake wa mawaziri baada ya kuuzindua rasmi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa msaada wake huo ambao amesema utakuwa ni chachu ya kupambana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa upande wake, Balozi wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesema Serikali ya Kuwait kupitia kwa Jumuiya ya Red Crescent ya nchini hiyo itaendelea kusaidia vifaa tiba mbalimbali kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya karibu na maeneo yao.

Balozi huyo wa Kuwait hapa nchini Jasem Al- Najem amesisitiza kuwa milango ya ubalozi wa Kuwait ipo wazi kwa Taasisi mbalimbali za Kiserikali kupeleka maandiko mbalimbali kwa ajili ya kuomba kupatiwa misaada lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma za viwango vya juu katika sekta mbalimbali.

Amesema kwa sasa Serikali ya Kuwait ipo mbioni kutiliana saini ya makubaliano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja iliyopo Unguja.
Ameeleza kuwa ukarabati huo utaiwezesha hospitali hiyo kuongeza utoaji wa huduma bora kwa wananchi wengi zaidi.

Halfa ya makabidhiano ya mabeseni 200 ya vifaa tiba katika hospitali ya Mbagala Rangi Tatu na Kituo cha Afya cha Mbagala Round Table katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

SPIKA NDUGAI APATA UGENI KUTOKA BUNGE LA MSUMBIJI LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias (katikati) pale ugeni kutoka kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Beatriz Chaguala.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisisitiza jambo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias na kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Beatriz Chagula.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akizungumza  mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, wa pili kushoto ni Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kutoka Bunge la Msumbiji, Mhe. Lucas Jeremias.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA KIBAHA MKOA WA PWANI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mwananchi Azilongwa Buhali alipokuwa akimuelezea shida yake mara baada ya kuhutubia wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Bondeni Mjini Kibaha kwa ajili ya kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Kibaha Maili moja katika viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu
Mkoani humo.
 Mmoja wa Wananchi akionesha hisia zake wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia Wananchi wa Kibaha Maili moja katika Viwanja vya Bondeni Mkoani Pwani.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka kabla ya kuhutubia Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza katika mkutano huo.
 Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka kabla ya kuhutubia Wananchi wa Kibaha Mkoani Pwani.
Wananchi wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akihutubia mjini Kibaha.

 PICHA NA IKULU

MTOTO SHUKURU ARUHUSIWA MUHIMBILI , AFYA YAKE YAIMARIKA

0
0
Mtoto Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kupatiwa matibabu na afya yake kuimarika.
Mtoto Shukuru alifikishwa  katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili Mei 16, mwaka huu akitokea Tunduru ambako aliripotiwa kuishi kwa kunywa mafuta , sukari na maziwa.

Baada ya kufikishwa MNH alifanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari Bingwa  na kubaini kwamba ana ugonjwa wa Selimundu pamoja na upungufu wa madini ya chuma na kwamba upungufu wa madini hayo ulisababisha anywe mafuta, sukari na maziwa.

Kwa upande wake Mama mzazi wa mtoto Shukuru,  Mwanabibi Mtenje amesema amepata faraja kuona afya ya mtoto wake imeimarika na sasa anaweza kula chakula chochote.

“Kwakweli namshukuru Mungu, pia nawashukuru  sana madaktari na wauguzi wa Muhimbili  kwani  hali ya mwanangu ilikuwa mbaya, alikuwa hawezi kula chochote  zaidi ya kunywa mafuta, maziwa na sukari, lakini baada ya kupatiwa matibabu,  afya yake imeimarika na sasa anaweza kula vyakula vyote,’’ amesema Mama Shukuru.

Awali mtoto Shukuru  alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Tunduru kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini ugonjwa haukooneka na baadaye alipelekwa hospitali  Nyangao mkoani Lindi.
 Mtoto Shukuru Kisonga (16) akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alifikishwa Mei 16, 2017 kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa na Selimundu na upungufu wa madini chuma. Mtoto huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na madaktari wa hospitali hiyo.
Mtoto Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa selimundu na upungufu wa madini chuma.  Kushoto ni mama yake Shukuru, Mwanabibi Ntenje.

WAZIRI MWAKYEMBE ''MSIMAMO WA MWALIMU ULIOKOA MENGI YA NCHI HII''

0
0

HAKI ELIMU YAZINDUA KAMPENI YA KUMUWEZESHA MTOTO WA KIKE APATE ELIMU

0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Elimu Nchini , John Kalaghe akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuondoa Vikwazo kwa Mtoto wa Kike katika hafla iliyofanyika katika ofsi za Tasisi hiyo Upanga jijini Dar es Salaam,Kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa kwa jamii kumpa fursa msichana hili aweze kupata mafanikio na kufikia maelengo yake
Msemaji kutoka TGNP, Grace Kisetu akichangia jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ondoa Vikwazo asome iliyofnyika katika ukumbi wa Haki Elimu Upanga Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya Waandishi waliohudhuria kampeni ya ondoa Vikwazo asome iliyozinduliwa na Tasisi ya Haki elmu kwa kushilikiakana na mashirika mbalimbali ya za kijamii
Sehemu ya Waandishi waliohudhuria kampeni ya ondoa Vikwazo asome iliyozinduliwa na Tasisi ya Haki elmu kwa kushilikiakana na mashirika mbalimbali ya za kijamii
Sehemu ya Waandishi waliohudhuria kampeni ya ondoa Vikwazo asome iliyozinduliwa na Tasisi ya Haki elmu kwa kushilikiakana na mashirika mbalimbali ya za kijamii

WATANZANIA WANG'ARA MAREKANI.

0
0
 Wanafunzi watatu wa shule ya sekondari ya FEZA BOYS Dar es Salaam wamenyakua medali za dhahabu huko Marekani katika mashindano ya uwezo wa kitaaluma ya GENIUS OLYMPIAD yaliyoshirikisha nchi 63 Duniani. Walionyakua medali hizo ni wanafunzi Abdulrazak Juma Mkamia,Rashid Jakaya Kikwete na Abdallah Rubeya

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA CHAMA CHA ASKARI WASTAAFU WA VITA KUU YA PILI YA DUNIA LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

0
0
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akipokea Barua ya kujitambulisha na kuomba msaada wa mchango kwa ajili ya kufanya Mkutano Mkuu wa Chama cha Askari wastaafu kwa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 – 1945 kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho ambae ni Ndg. Bakari Ngonja, katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisisitiza jambo pale alipokutana na kufanya mazungumzo na Chama cha Askari wastaafu wa Vita kuu ya pili ya dunia waliopigana Mwaka 1939 -1945 katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNE 21,2017

0
0

BAJETI KUU YA SERIKALI YAPITISHWA KWA KISHINDO MJINI DODOMA

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), pamoja na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), pamoja na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Bustani kilichoko wilayani Kondoa mkoani Dodoma, walipotembelea bungeni mjini Dodoma, siku ambayo Bunge limepitisha kwa kishindo Bajeti ya Sh. trilioni 31.7 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Bw. Doto James (wa nne kulia-mbele), akiongoza Vongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango kufuatilia tukio la Wabunge wakipiga kura kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, Bungeni Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Chakwa-Zanzibar, Mhe. Bhagwanji Meisuria (katikati), na mkewe Kissum Biin Bhagwanji Meisuria, wakimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Mhe. Charles Kitwanga akimkumbatia kwa furaha na bashasha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Mnauye akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb), akimpongeza kwa furaha na bashasha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kwa kufanikisha kuandaa na hatimaye kupitishwa kwa Bajeti Kuu ya Serikali ya kihistoria ya shilingi trilioni 31.7 ya Mwaka wa Fedha 2017/2018, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto), akiteta jambo na maafisa waandamizi wa Wizara yake nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akipongezwa na Askari wastaafu wa Jeshi la KAR waliopigana Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1939-1945 baada ya Bunge kupitisha kwa kishindo Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7, bungeni mjini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara hiyo baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya Shilingi trilioni 31.7 mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akimshukuru na kumpongeza Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), kwa ushirikiano mkubwa aliompatia hadi kufanikisha kazi kubwa ya kuandaa na kusimamia Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 31.7 iliyopitishwa na Bunge kwa kishindo mjini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

UVUMILIVU WAWASHINDA WAKAZI WA BULYANHULU MKOANI SHINYANGA.

0
0
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kakola, wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga, Emmanuel Bombeda, akiongoza kongamano la wananchi wa kijiji hicho lililokuwa na ajenda ya kutoka na maazimio ya kudai fidia zao kutoka mgogi wa Bulyanhulu. Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, John Kiganga, akizungumza kwenye kongamano hilo Mkazi wa Kakola, Erasto Mapato, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mjumbe serikali ya Kijiji cha Kakola, Jedidiah Kitundu, akizungumza kwenye kongamano hilo Mkazi wa Kakola, John Mutemankamba, akizungumza kwenye kongamano hilo Mchimbaji mdogo wa dhahabu, Aziz Mbaga, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Kakola, Erasto Mapato, akizungumza kwenye kongamano hilo Mkazi wa Bulyanhulu, Waziri Bakari, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Bulyanhulu, akizungumza kwenye kongamano hilo. Mkazi wa Bulyanhulu akizungumza kwenye kongamano hilo. Mzee Nikodemas Mabe ambaye ni Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Bulyanhulu akielezea kero zao Magdalena Lusana akielezea kero za Bulyanhulu Mzee Geremiah Wangaluke akielezea kero za Bulyanhulu Kijana Masumbuko Kafula mkazi wa Bulyanhulu akieleza madhira waliyoyapata kutokana na wawekezaji Mama Melania Baesi akieleza juu ya wanae kupoteza maisha kwenye sakata la Bulyanhulu Wakazi wa Bulyanhulu wilayani Msalala Wakazi wa Bulyanhulu wilayani Msalala Kongamano la wananchi wa kijiji cha Kakola lililokuwa na ajenda ya kutoka na maazimio ya kudai fidia zao kutoka mgogi wa Bulyanhulu.

Wakazi wa Kijiji cha Kakola, Kata ya Bulyanhulu, Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wameazimia kufanya maandamano yasiyo na ukomo kushinikiza mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kuwalipa fidia zao.

Wakizungumza kwenye kongamano la Kijiji hicho lililofanyika jana juni 20,2017, wakazi hao wamepanga kupeleka kero zao Jijini Dar es salaam kwa Rais John Pombe Magufuli pamoja na kufanya maandamano ya kufunga barabara kushinikiza kulipwa fidia zao.

"Kongamano la leo ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kwa kugundua kwamba tulikuwa tunaibiwa kwa muda mrefu. Tangu mwaka 1996 mpaka leo sisi tumeibiwa tu, hatujapata haki hata moja. Hakuna huduma za jamii zinazotambulika ambazo zimefanywa na mgodi". Alisema mchimbaji mdogo Aziz Mbaga.

Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Bulyanhulu, Mhidini Mfwanguro alisema maazimio ya wananchi wa Kijiji hicho ni fidia kwa wafukiwa na waathirika wa Bulyanhulu mwaka 1996 pamoja na waathirika wengine wakiwemo wafanyakazi waliochishwa kazi kwa kuumia kazini bila kulipwa na kwamba watawasilisha madai hayo kwa wamiliki wa mgodi huo, kampuni ya Barrick Gold Mine.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kakola, Emmanuel Bombeda amesema kijiji hicho kilikuwa na vitongoji tisa lakini vitongoji vinne vilichukuliwa na mgodi wa Bulyanhulu bila wananchi kulipwa fidia huku nyumba zao zikibomolewa.

"Tunataka maandamano ya kufunga barabara tulipwe, siwezi kufanya maandamano halafu tusambae, nataka maandamano kama tuliyofanya umeme ukaletwa kijiji cha Kakola, maandamano kama yale ya Musoma ya kupigwa mabomu lakini tulipwe". Alisema Bombeda.

Diwani wa Kata ya Bulyanhulu, John Kiganga alikiri wananchi wengi kukosa stahiki zao baada ya kuondolewa kwenye maeneo yao ili kupisha uwekezaji wa mgodi wa Bulyanhulu na kusisita kwamba wanapaswa kulipwa fidia zao maana fomu za tathimini zipo na kwamba hata wale waliolipwa fidia, walilipwa kinyume na tathimini ambapo mmoja wa wananchi aliyepaswa kulipwa shilingi milioni 375 alilipwa shilingi laki tano.

Wananchi wa Kijiji cha Kakola wanalalamika kutolipwa fidia zao baada ya maeneo na makazi yao kuchukuliwa na mgodi wa Bulyanhulu, wengine ndugu zao kufukiwa kwenye mashimo, waliokuwa wafanyakazi wa mgodi huo kutaka stahiki zao baada ya kuumia kazini na kuachishwa kazi pamoja na kutaka huduma bora za kijamii ikiwemo barabara za lami na vituo vya afya/hospitali kutokana na uwepo wa mgodi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA USHIRIKIANO, UPENDO KWA DINI ZOTE TANZANIA

0
0
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akitoa salamu za Shukurani kwa niaba ya Wabunge na wafanyakazi wa Bunge, kwa Spika wa Bunge Job Ndugai, kwa kuwafuturisha, June 20, 2017 katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma. Waziri Mkuu aliwaasa Watanzania wote kuwa na ushirikiano kwa dini zote na kupendana.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibadilishana mawazo na Spika wa Bunge Job Ndugai katika Futari iliyoandaliwa na Spika kwa ajili ya Wabunge, Wafanyakazi wa Bunge na Wageni waalikwa katika viwanja vya Bunge Mjini Dododma, June 20, 2017
Baadhi ya Wabunge wakibadilishina mawazo wakati wa futari iliyo andaliwa na Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai , kutoka kulia, Mbunge wa Ilala Idd Zungu. katikati Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge .na kushoto ni Mbunge wa Mbarali Haroon Mulla .Futari hiyo ilifuturiwa katika viwanja vya Bunge June 20, 2017 Mjini Dodoma Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAKAZI WA PWANI WAIFURAHIA HUDUMA YA UKARIMU YA VODACOM

0
0

Wakazi wa kanda ya Pwani wameipokea kwa furaha kubwa huduma mpya ya Ukarimu inayotolewa na Vodacom Tanzania wakati huu wa msimu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani inayolenga kutoa ushirika na utoaji.
Ukarimu huu wa Vodacom unakwenda sambamba na kuwapatia wateja kifurushi kinachowawezesha kupata Qaswida, Mawaidha, Hadith, Facebook yenye picha na kuzungumza usiku wanaposubiri daku BURE kabisa. Ili mteja aweze kunufaika na bando hili la Ukarimu anatakiwa kupiga *149*01# kisha kuchagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha. Lipo bando linalodumu kwa muda wa saa 24 na linalodumu kwa siku saba.

Kwa kiasi cha shilingi 1000, mteja atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 10 kwenda mitandao yote, ujumbe mfupi wa maandishi wa maandhishi bila kikomo, simu kupitia mtandao pamoja na ujumbe wa didi bure.

Kwa mteja atakayenunua bando la shilingi 3000 atapata dakika 150 Vodacom kwenda Vodacom, dakika 30 kwenda mitandao mingine, ujumbe mfupi wa maandishi bila kikomo, simu za bure usiku Vodacom kwenda pamoja na ujumbe mfupi wa maandishi wa dini bure kwa siku saba.

Siku ya leo Vodacom wanaendelea na futurisha katika maeneo yafuatayo

Tangax
Nyako
Mtindiro Kwabeda
Korogwe mjini

Mtwara
Newala

Lindi
Kilwa somanga
Kilwa chumo
Ruangwa namungo

UTUMISHI YAWAAGA WATAALAM 14 WA KUJITOLEA KUTOKA NCHINI JAPAN WALIOKUJA KUTOA HUDUMA KATIKA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

0
0
  Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bw.Hiroki TAMURA akielezea namna alivyofanya kazi katika Chuo cha Utalii Zanzibar, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI  leo.
  Mtaalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani Bi. Moemi Ikeda akielezea namna alivyofanya kazi katika Shule ya Msingi Lusanga-Morogoro, katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo.
 Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Fundikira Ekerege (kulia) akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya elimu yaliyowasilishwa katika hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Roxana Kijazi (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa kujitolea kutoka nchini Japan Bi. MIDORI MIYAZAKI  aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo. 
 Mkurugenzi Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Roxana Kijazi (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa kujitolea kutoka nchini Japan Bw. Shota Yanagisawa aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini  katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa UTUMISHI leo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-UTUMISHI Bi.Roxana Kijazi (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika UTUMISHI leo.

Ziara ya TTB Israel yaleta mafanikio sekta ya utalii

0
0
 Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi akitoa mada katika mkutano nchini Israel alipofanya ziara ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na fursa za biashara kupitia sekta hiyo. Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki akichangia mada katika mkutano nchini Israel alipofanya ziara ya kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na fursa za biashara kupitia sekta hiyo. Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi akizungumza na waandishi   wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam akitoa mrejesho kuhusiana na ziara yao iliyofanyika nchini Israel ikiwa na lengo la kutangaza utalii wa Tanzania iliyofanyika kuanzia Juni 11 hadi 15 mwaka huu.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi. Devota Mdachi(wapili kushoto) katika picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania nchini Israel Job Massima (wapili kulia) mara baada ya kumaliza mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta ya utalii wa nchini Israel kutambua fursa za utalii zilizopo Tanzania. Ziara ya siku tatu aliyoifanya nchini humo imeleta ushawishi kwa bodi ya utalii ya Israel kushirikiana na Tanzania katika sekta hii. Kulia ni Balozi mdogo wa Tanzania nchini Israel Kasbian Chirich na Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce Nzuki.

BODI ya Utalii Israel imeahidi kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kutangaza vivutio vilivyopo na kukuza sekta ya utalii nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devota Mdachi,  aliyeongozana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki, kuitembelea Israeli kwa siku tatu mwezi huu, amesema  ziara yao nchini Israel imeleta mafaikio katika sekta ya utalii  Tanzania.

Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni  kukutana na wadau wa sekta ya utalii wakiwemo mawakala wa utalii na sekta ya malazi.
“Israel imeonyesha shauku kubwa ya kushirikiana na sisi katika kuutangaza utalii wa Tanzania. Mwaka jana tulipata watalii 22,000 kutoka nchini humo ambapo wameahidi mwaka huu watakuja watalii wengi zaidi.

“Vilevile kupitia vyombo vyao vya habari tumeeleza namna vivutio vyetu vilivyo na mwonekano wa kipekee duniani, tumepokea maombi mengi ya kuja kutembelea fukwe na hifadhi za wanyamapori.”

Alieleza kuwa hifadhi zilizotajwa sana ni Katavi, Mahale, Ngorongoro na Zanzibar: “Tunafahamu Waisraeli wanapenda kuangalia wanyamapori.Nilipokuwa nikiwatajia wanayama tulio nao walionyesha kufurahi hasa nilipowaeleza kuwa faru Fausta (55) mwenye umri mkubwa kuliko wote barani Afrika yupo katika ardhi ya Tanzania walionyesha kuvutiwa zaidi.”

Bw. Nzuki aliuambia mkutano na wadau wa utalii nchini Israel katika Mji waTel Aviv, : “Tanzania kuna fursa nyingi katika uwekezaji,  upande wa hoteli za kitalii.  Ikiwa una kampuni ya kitalii pamoja nyumba ya wageni ya kisasa unajiwekea uhakika wa kupata wageni wengi.“Ukiwa tayari unaweza kuja na kufuata utaratibu wa kisheria katika mamlaka husika utapewa maelekezo. Tunawakaribisha kuwekeza katika utalii.”

Miongoni mwa wawekezaji wanaofanya shughuli za kitalii nchini , Bwana Alon Hovev anayemiliki kampuni ya utalii ya Sima Safari , ameuambia mkutano huo kuwa sababu zilizomfanya kuwekeza Tanzania ni hali ya hewa na watu wake.

“Watanzania ni wakarimu,  nimevutiwa na mtindo wao wa maisha, vilevile kuna maeneo mengi ya kuvutia ikiwemo pwani safi na mbuga za wanyama,” amesema Bw. Hovev ambaye ameoa raia wa Tanzania.Utalii ni miongoni mwa vyanzo vikubwa vya mapato nchini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, ameliambia bunge la bajeti hivi karibuni na kueleza kuwa mwaka 2016 Tanzania ilipokea watalii  milioni 1.2 ikiwa ni ongezeko la asilimia 12.9 mwaka 2015 walipokuja watalii milioni 1.1.

Mwaka jana sekta ya utalii iliingiza kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 2 ikiwa ni sawa na Sh Trilioni 4, mwaka 2015 iliingiza Dola bilioni 1.9.
Kiwango hicho cha mapato kiliifanya sekta ya utalii kuchangia asilimia 17.5 ya pato la taifa katika bajeti ya mwaka 2016/17 pamoja na kuingiza asilimia 25 ya fedha za kigeni.

TPSC YAANZISHA MAFUNZO YA SHAHADA YA UHAZILI NA UTUNZAJI KUMBUKUMBU,TAARIFA NA NYARAKA

0
0
Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa mara ya kwanza kimeanzisha Masomo ya Shahada ya kwanza (Degree) katika fani za Uhazili na Utunzaji wa Kumbukumbu, Taarifa na Nyaraka.

Kufuatia kuanzishwa kwa masomo ya Shahada ya kwanza katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Mkuu wa Chuo Dkt. Henry Mambo ametoa wito kwa watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa kuchangamkia nafasi hizo za masomo kwa manufaa yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Dkt. Mambo alisema masomo hayo ya Shahada ya kwanza yataanza Mwezi Septemba,2017 katika Matawi ya Dar es Salaam na Tabora, nayo ni hatua kubwa kwa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania katika kuwaendeleza Watumishi na Watanzania Kitaaluma.

Kwa upande wa sifa za kujiunga na masomo hayo ya shahada ya kwanza, Dkt. Mambo alisema muombaji anatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha sita pamoja na ufaulu katika masomo mawili au Diploma katika fani husika yenye ufaulu au GPA alama 3.

Mkuu wa Chuo pia aliendelea kufafanua kwamba Masomo hayo ya ngazi ya Shahada yameanzishwa ili kuhakikisha kwamba watumishi wa umma na Watanzania wenye sifa za kujiunga wanakabiliana na changamoto zinazojitokeza katika soko la ajira kufuatia mabadiliko ya teknolojia na mifumo mbalimbali ya utendaji kazi.“Kutokana na mabadiliko hayo ni vema Watumishi wa Umma na Watanzania wenye sifa kwa ujumla nao wakapata mafunzo ambayo yatawawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali katika soko la ajira,”.

Kuhusu shahada ya Uhazili na Utawala, Mkuu wa Chuo alisisitiza kwamba Wahitimu wataweza kukabiliana na changamoto mbalimbali za mawasiliano  katika utendaji wao wa kazi wa kila siku na hivyo kuwawezesha kufanya kazi kwa ufasaha katika sekta ya umma na hata sekta binafsi. “Mafunzo hayo pia yatawawezesha wahitimu kumudu nafasi ya Maofisa Wasaidizi Waandamizi ambao watafanya kazi katika taasisi mbalimbali hapa nchini na hata nje ya nchi kulingana na soko la ajira litakavyowahitaji” alisema.

Kuhusu Shahada ya Utunzaji Kukumbukumbu, Taarifa na Nyaraka, Mkuu wa Chuo cha Utumishi alibainisha kwamba mafunzo hayo yatawawezesha wahitimu kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha mkubwa zaidi katika eneo hilo na hivyo kuchangia katika uendelezaji na ukuaji wa Taaluma ya Utunzaji Kukumbukumbu, Taarifa na Nyaraka. 

Mafunzo ya ngazi ya shahada (Degree) yatatolewa kwa muda wa miaka mitatu, wakati yale ya Diploma na Cheti yataendelea kutolewa kwa kipindi cha miaka miwili na mwaka mmoja kama kawaida na akatoa wito kwa watumishi wa umma na watu wote wenye sifa za kujiunga na masomo hayo kuchangamkia fursa hizo kwa kujaza fomu za kujiunga na Chuo zinazopatikana katika matawi yote ya Chuo cha Utumishi wa Umma ya Dar es Salaam, Tabora, Singida,Mtwara, Tanga na Mbeya, na katika tovuti ya Chuo www.tpsc.go.tz

Katika kongamano la Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama Cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) lililofanyika hivi karibuni Mkoani Dododma, Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa kufungua Mkutano huo, aliwataka makatibu Mahsusi hao kuichangamkia kozi hiyo, kwa kuwa ni fursa nzuri kwa Makatibu Mahsusi na itawasaidia sana katika kuongeza weledi na ufanisi kazini.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angellah Jasmine Kairuki, ambae pia alihudhuria Kongamano hilo na ambaye Chuo cha utumishi wa Umma kiko chini ya Wizara yake, aliwatoa hofu waombaji wa kozi hizo mpya zilizoanzishwa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kwa kusema Ofisi yake inalitambua hilo na inalifanyia kazi suala hilo ili Wahitimu watakapomaliza mafunzo yao ya miaka mitatu(3), waweze kutambulika nafasi zao katika Muundo wa Utumishi wa Umma. Hivyo akawahimiza Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu Taarifa na Nyaraka kuchangamkia nafasi hizo.

Mwandishi wa gazeti hili pia aliweza kuongea na Katibu Mkuu wa TAPSEA, Festo Melikiory ambaye alisema kuwa kuanzishwa kwa kozi hizo ni fursa kwa Watanzania hususan Makatibu Mahsusi na Watunza Kumbukumbu na kwamba ni matumaini yake kuwa kozi hizo zitaongeza weledi na ujuzi miongoni mwa watumishi wa umma na watanzania kwa jumla. “Hiki kilikuwa ni kilio chetu cha siku nyingi, sasa kimesikilizwa, ni matumaini yangu kuwa Makatibu Mahsusi wengi wataichangamkia fursa hii,”alisema.

Katibu Mkuu huyo wa TAPSEA alitoa wito kwa Makatibu Mahsusi kuichangamkia kozi hiyo kwani itaongeza uwezo wao wa utendaji wa kazi.Alisema kozi hiyo ni fursa nzuri kwa Makatibu hao kwani itawasaidia sana katika kuongeza weledi na ufanisi kazini.

Baadhi ya Watumishi wa Umma na wananchi wamekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma kwa kuanzisha masomo ya Shahada katika fani hizo na kusema kwamba mafunzo hayo ni hatua kubwa katika mchakato wa kuendeleza taaluma ya elimu hapa nchini. 

Pamoja na kutoa Mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi majukumu mengine ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ni kutoa Huduma ya Shauri za Kitaaluma, Tafiti na Machapisho mbalimbali yanayohusiana na uendeshaji wa Utumishi wa Umma.

Mafunzo ya muda mfupi yanatolewa kwa Watumishi wa Umma pamoja na watumishi wa sekta binafsi ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Mafunzo yatolewayo na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yamejikita katika maeneo ya Menejimenti, Utawala na Uongozi, Usimamizi wa Rasilimali Watu, Utunzaji wa kumbukumbu Taarifa na Nyaraka, Usimamizi wa Fedha, Uendeshaji wa Ofisi, Ununuzi na Ugavi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt.Henry Mambo, katika moja ya hafla jijini Dar es Salaam hivi karibuni(Picha na Maktaba)

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

0
0
Afisa Utumishi Mkuu Ally Juma Ally (Kushoto) akisikiliza maswali mbalimbali ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakati wa kikao cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Yamo Wambura
Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Mariam Maliwa akifatilia kwa karibu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo Ndg Alute Joseph akitoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma


Leo June 20, 2017 watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameanza kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano mkubwa uliohudhuriwa na watumishi wote wa makao makuu katika ukumbi wa Manispaa hiyo mkutano ambao umeongozwa na Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa hiyo Ndg Ally Juma Ally kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.

Akiongea katika kikao hicho mara baada ya kufungua kikao Afisa Utumishi mkuu aliwajulisha kuanza rasmi kwa wiki ya utumishi na kutoa utaratibu wa jinsi Halmashauri itakavyotimiza maadhimisho hayo ambapo alisema kuwa kwa wiki hii ya maadhimisho muda wa kutoka kazini utaongezeka kwa saa moja badala ya kutoka saa tisa na nusu mchana itakuwa ni saa kumi na nusu, hali kadhalika alisisitiza mambo ya kuzingatia katika wiki hii na hata baada ya maadhimisho no pamoja na Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma, Kufanya kazi zetu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, na Kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa bila ya viashiria vya kupokea rushwa au hongo katika kutoa huduma katika ofisi za serikali au umma.

Mengine ni Kuongeza Ari na kujituma katika kutekeleza majukumu yetu, Kufanya kazi kwa maarifa na kuwasikiliza wanaanchi wanapofika kupata huduma katika ofisi za umma/serikali na Kuweka vizuri kumbukumbu za wananchi watakaohudumiwa kwa kipindi hiki ili kuzitolea taarifa kwenye mamlaka husika.

Pia wamesisitizwa kutoa Huduma bora, Utii kwa serikali, Kuongeza bidii ya kazi, Kutoa huduma bila upendeleo, Kufanya kazi kwa Uadilifu, Uwajibikaji kwa Umma, Kuheshimu sheria na taratibu za kazi, na Matumizi sahihi ya Taarifa.


IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

UPATIKANAJI WA DAWA KWENYE VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA WAFIKIA ASILIMIA 80

0
0

 Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga(CMO), Jairy Khanga akifungua mafunzo ya  mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfukowa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri mjini Tanga kulia ni Msimamizi wa Mfuko huo,Dina Mlwilo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga
Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya MkoaniTanga (NHIF) Dinna Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga wakatiwa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi kutokahalmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko waTaifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga uliofanyika mjini hapa  ambapo
alisema asilimia 70 wakina mama wajawazito wamejiunga na mradi watumaini la mama kwa ajili ya kupata matibabu
 Mwezeshaji wa mafunzo wa Tumaini la Mama,Ally Omari akisisitiza jambo wakati  akitoa somo kwenye mafunzo hayo


Mmoja wa wasimamizi wa mradi wa Tumaini la Mama Tanzania Irine Meaki akielezea masuala mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Jiji. 
 Baadhi ya wauguzi  wanaohudumia wakina anama wajawazito wakimsikiliza mgeni rasmi wakati alipofungua mafunzo ya mradi wa tumaini la mamauliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutokahalmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko waTaifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzowakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mamauliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutokahalmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko waTaifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.



Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzowakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mamauliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutokahalmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko waTaifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
 Msimamizi wa Mfuko huo,Dina Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo

UPATIKANAJI wa dawa kwenye vituo vya Afya kwenye Halmashauri ya Jijila Tanga umeelezwa kufikia asilimia 80 kwa wagonjwa wanao kwendakupata matibabu wakiwemo wanaohudumiwa na mfuko wa Taifa wa Bima yaAfya (NHIF).

Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga(CMO), JairyKhanga wakati alipofungua mafunzo ya mradi wa tumaini la mamauliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutokahalmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko waTaifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.

Alisema upatikanaji huo wa dawa umesaidia kuweza kuwadumia wakina mamawajawazito ambao wamekuwa wakijitokeza kupata huduma za matibabu navifaa tiba pamoja na wategemezi wao.

Aidha alisema jambo hilo limeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguzana kuondokana na vifo vya wakina mama wajawazito ambavyo vilikuwavikijitokeze kutokana na kukosa huduma muhimu za matibabu wakatiwanapojifungua.

Alisema kutokana na umuhimu wa mradi huo watoa huduma wanapaswa kuwekamipango mizuri ya kuwahudumia wakina mama wajawazito wakati wanapofikakwenye vituo vyao vya afya ili waweze kuepukana na athari zinazowezakujitokeza kutokana na hali walizokuwa nazo.

“Mradi huu una zaidi ya miaka minne nyie kama watoa huduma mnauzoefumkubwa hivyo kupitia mafunzo hayo jaribuni kushirikiana na wawezeshajikuhusu changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji wake “Alisema.

Aidha pia aliwataka watoa huduma wafanye uhamasishaji mkubwa kwawakina mama wajawazito waliopo kwenye maeneo yao kwa lengo la kuongezawigo mpana wa kuwaandikisha kwenye mradi huo ambao ni muhimu kwao.

Akichangia wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali katika mafunzohayo,Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wilayani MkingaElizaberth Dickson alisema moja kati ya changamoto kubwa zilizopo hivisasa ni ucheleweshwaji wa kadi za bima ya afya kwa wakina mamawajawazito jambo ambalo linakwamisha huduma kwa baadhi yaowanapohitaji
matibabu.

“Lakini nisema upatikanaji wa kadi za mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwawakina mama wajawazito na wategemezi kwa wakati zitarahisishaupatinaji wa huduma za matibabu katika vituo mbalimbali vya afya ndanina nje ya mkoa”Alisema

Katika kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wakina mama wengi mkoaniTanga, Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF)Dinna Mlwilo aliwataka watoa huduma kuihamasisha jamii kuona umuhimuwa kuajiandikisha katika vituo vya afya wakati wa ujauzito kupitiamradi huo

“Kwani kujiandikisha huko wanaweza kupata fursa muhimu ya kupitiamradi wa tumaini la mama kwa kupata huduma za matibabu wao nawategemezi wao kwenye vituo vya afya “Alisema.

Aidha alisema kwa mkoa wa Tanga tayari wamekwisha kuandikisha wakinamama wajawazito asilimia 70 ambao wananufaika kupitia mpango huo ambaouna lengo la kupambana na vifo wakati wanapojifungua.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images