Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 126 | 127 | (Page 128) | 129 | 130 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja na Balozi Radhia Msuya (wane kushoto). Wengine katika picha ni Jasper Masika Mtanzania anayeishi Afrika Kusini, Phinias Bashaya wa Mwananchi, Pascal Shelutete Meneja Uhusiano TANAPA, Lilian Shirima (TBC) , Alex Magwiza (TBC), Albano Midelo (Nipashe) na Afisa wa Ubalozi.
  Wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja nje ya Hospitali ya Med Clinic alikolazwa Rais wa Kwanza Mzalendo Nelson Mandela akiendelea na matibabu.
  Wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA katika picha ya pamoja nje ya Kijiji cha Makumbusho cha Lesedi. 
  Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mheshimiwa Radhia Msuya akizungumza na wanahabari walioshinda Tuzo za Habari za TANAPA waliomtembelea ofisini kwake jijini Pretoria.

  0 0


  0 0

  "Hongera...Weruweru,umlezi wetuuu...."If this line reminds you of our beloved school,then this is for you.
  In preparations for our big celebrations of Weruweru's Golden Jubilee,we have a meeting on Sunday at Cine Club...Yes,This Sunday from 3pm.

  If you are a Weruweru girl or you know one,please pass the message along. Use the numbers above on the poster to confirm and/or ask for more info.

  Remember to come with a scarf of the color of your skirt during them good days...Or if you still have your Shamba dress :)

  Looking forward to seeing you,

  xoxo
  Missie Popular

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu kulia na Meneja kampuni ya bia (TBL) Nicolaus Kanyamala wakizindua kisima cha kijiji cha Isnura.
  Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akimtwisha maji mwenyekiti wa kijiji cha isnura Josephine ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima hicho

   
  Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gulam Kiffu akiwashukuru TBL kwa kusaidia maji katika kijiji cha isnura na kuahidi kukitunza kisima hicho
  Meneja uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na wakazi wa Isnura ambapo amesema kuwa TBL imekuwa na sera ya kusaidia maeneo mbali mbali hapa nchini kupitia faida kidogo inayopata kwa kuamua kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa wananchi baada ya kubaini uhitaji wa msaada eneo husika, ambapo pamoja na mambo mengine meneja huyo alitoa rai kwa jamii kuona umuhimu wa kuisaidia serikali hapa nchini.
  Mwenyekiti wa Kijiji cha Isnura  Josphine Ndimilage akisoma risala kwa niaba ya wananchi
  Uchimbaji wa kisima katika Kijiji hicho umefadhiliwa na Kampuni ya Vinywaji ya Tbl kwa gharama ya Shilingi milion 28  ikiwa ni pamoja na Jenereta ndogo kwa ajili ya kupandisha maji katika Tanki kubwa lenye ujazo wa Lita 45,000.Picha na Mbeya yetu

  0 0

  The EAC Brand 2013 survey team embarked on a week-long mission to Uganda on how citizens perceive the regional integration activities, programme and how much they understand of the Community. The survey will be undertaken in all Partner States between 16 July and 27 August. The first two teams set out for Uganda and Burundi. In the picture, the Brand Survey Team poses for a group picture with acting Uganda's Permanent Secretary Steven Niyonzima(with tie) and on his right is the EAC Brand Team leader, Sukhdev Chhatbar., after paying a courtesy call at the Uganda EAC Ministry in Kampala.

  0 0

   Meneja wa Vodashop  Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro(kulia)akimuelekeza jinsi ya kutoa Pesa,Anatori E.Chogolo-mkazi wa Iringa,(katikati)ambae ni mshindi kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja katika Promosheni ya Cheka Plus,alizotumiwa kwa njia ya M-PESA  kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu,anaeshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.
   Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)na Meneja wa Vodashop  Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro(katikati)wakimshuhudia Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Plus Bw.Anatori E.Chogolo-mkazi wa Iringa,ambae ni mshindi ,kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu,akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Pesa alizokabidhiwa mara baada ya kuzitoa kwa njia ya M-PESA,alizotumiwa kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo,ili kujiunga na promosheni hiyo wateja wanatakiwa kupiga *149*01#
   Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)akimkabidhi Tsh milioni 2  Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Plus Bw. Anatori Emmanuel Chogolo-mkazi wa Iringa,ambae ni mshindi ,kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja,baada ya kuzitoa kwenye M PESA alizotumiwa toka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu.Ili kujiunga na promosheni hiyo piga *149*01#
  Mmoja wa washindi wa droo kubwa kati ya washindi 5 wa Promosheni ya Cheka Plus Bw. Anatori E. Chogolo-mkazi wa Iringa(katikati)akihesabu Pesa zake Shilingi Milioni 2 mara baada ya kuzitoa kwa njia ya M-PESA,alizotumiwa kutoka makao makuu ya Vodacom kwa ushindi wake kwenye Promosheni hiyo,wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom,Matina Nkurlu na kulia ni Meneja wa Vodashop Mlimani City jijini Dar es Salaam Bi.Rosemary Maro.

  0 0

  Vikundi vya ngoma vikitumbuiza wageni.
  Wananchi wa Muleba wakimshangilia Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili wilayani humo akiwa katika ziara yake ya siku sita Mkoani Kagera
  Rais Kikwete akivikwa skafu na skauti baada ya kuwasili Muleba
  Rais Kikwete akisalimiana na mama wa Profesa Anna Tibaijuka
  Waziri wa Ardhi Profesa Anna Tibaijuka akishiriki katika ngoma ya utamaduni wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete wilayani Muleba
  Rais Kikwete akiongea na viongozi wa wilaya ya Muleba baada ya kupokea taarifa ya maendeleo, akiwa na mawaziri watano anaoongozana nao katika ziara hiyo
  Mbunge wa Muleba akitoa  maoni na kero za jimbo lake
  Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akiwahakikishia viongozi wa Muleba juu ya mipango ya serikali kuleta meli za abiria mpya mbili katika ziwa Victoria
  Rais Kikwete akipata maelezo ya mpango kabambe wa maji wilaya ya Muleba
  Rais Kikwete akizindua mradi mkubwa wa maji wilayani Muleba
  Rais Kikwete akikata utepe kuzindua mradi wa maji
  Rais Kikwete akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi wa Muleba baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji kwa wilaya hiyo
  Mwananchi mwingine akitwishwa maji
  Ngoma ya utamaduni ikimlaki Rais Kikwete alipowasili katika mkutano wa hadhara
  Rais Kikwete akisalimia wananchi
  Rais Kikwete akiangalia mazao yatokanayo na uzalishaji mbegu ya kampuni ya Itente ya Muleba
  Rais Kikwete akipozi na wafanyakazi wa kampuni ya uzalishaji mbegu ya Itente
  Rais Kikwete akifurahia ngoma
  Umati wa wananchi Muleba ukimsikiliza Rais Kikwete
  Rais Kikwete akiongea na wananchi wa Muleba
  Rais Kikwete akihutubia wana Muleba
  Sehemu ya umati mkutanoni
  Rais Kikwete akiendelea kungea na wananchi
  Umati  katika mkutano wa hadhara
  Umati katika mkutano wa hadhara
  Rais Kikwete akijiunga na waumini wa Muleba kusali swala ya Magharibi kabla ya kufuturu
  Dua ikisomwa baada ya futari aliyoandaa Rais Kikwete kwa wananchi wa Muleba
  Dua ikiombwa baada ya futari
  Dua
  Wananchi wa Muleba katika futari aliyoandaa Rais Kikwete wilayani Muleba

  0 0

   Msemaji toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Innocent Mungy(kushoto)akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu madhara ya kutumia visivyo huduma ya mawasiliano  na utumiaji wa majina yasiyo sahihi katika usajili wa namba za simu kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar Es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa. Picha na Hassan Silayo.
  =========  =======  =======

  MATUMIZI MABAYA YA MAWASILIANO NA UDANGANYIFU KATIKA Usajili wa namba za simu za mkononi NCHINI nikosa la jinai . 


  1.  Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi cha miaka kumi iliyopita zimekuwa sana na kuwafikia watu wengi zaidi. Ni ukweli usiopingika kuwa watanzania wengi hivi sasa wanafaidika kwa huduma za mawasiliano, hususani katika mawasiliano ya simu za mikononi, utangazaji, intaneti na huduma za ziada kama kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao na simu za mkononi. Wananchi wengi wanapata huduma za kibenki kwa kutumia simu zao, wanawasiliana kwa kutumia simu zao kupitia sauti, SMS na kadhalika.

  2.    Aidha kumekuwa na ongezeko la matumizi ya intaneti kwa watanzania walio wengi hususani matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile Facebook, twitter, BBM, LinkedIn na blog mbalimbali. Matumizi haya yamewanufaisha watanzaia kwani ni fursa murua ya kujifunza kupitia mitandao hiyo ya kijamii kwa kupata habari mpya, kujifunza na kuelimishana kuhusu shughuli za maendeleo na kuleta amani miongoni mwa watanzania.

  3.    Pamoja na maendeleo haya chanya kwa nchi yetu, kumekuwepo na baadhi ya watu wachache wanaotumia mawasiliano ya simu, mitandao ya kijamii, redio, TV na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga amani, kuchocheo ugomvi, kuchonganisha watu, kusababisha ugomvi, kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli, kupotosha jamii na hata kuvuruga maendeleo kwa ujumla.

  4.    Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inawatahadharisha wananchi kwamba ni kosa la jinai kutumia mawasiliano vibaya kama ilivyoainishwa katika sheria ya Mawasiliano ya Kielectroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010. Wananchi wanashauriwa kuhakikisha wanatumia mawasiliano vizuri na kuhakikisha tunadumisha amani na upendo miongoni mwa watanzania.

  5.    Aidha mamlaka inapenda kuwakumbusha wananchi kuwa kusajili laini yako ya simu, kwa kutumia utambulisho wa udanganyifu pia ni kosa la jinai. Mtumiaji wa huduma za mawasiliano unatakiwa kwenda kwa mtoa huduma au wakala wake ukiwa na kitambulisho sahihi chenye picha yako na kutoa taarifa sahihi. Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, kifungu cha 131, kimeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au kuwezesha kutumika namba ya simu isiyosajiliwa. Adhabu ya faini ya shilingi laki tano (Tshs 500,000.00) au kifungo cha miezi mitatu itatolewa kwa yeyote atakayekiuka sheria hii.

  6.    Kuanzia tarehe 1 Juni 2013 saa sita usiku, laini zote za simu ambazo hazijaanza kutumika zilifungwa (locked) na haziruhusiwi kutumika hadi mtumiaji atakapoisajili laini yake mpya kwa watoa huduma. Kama kuna mwananchi atakaenunua laini, na kuweza kuitumia bila ya kuisajili, anaombwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).   

  7.    Watumiaji wote wa simu za mkononi ambao hawakuwa wamesajili namba zao za simu wafanye hivyo mara moja. Ifahamike kwamba ilipofika tarehe 10 Julai 2013 saa sita usiku, laini za simu ambazo zilikuwa zinatumika na zilikuwa bado hazijasajiliwa hadi wakati huo, zilifungwa. Kufungua laini iliyofungwa, mtumiaji atapaswa kwenda kwenye ofisi ya mtoa huduma wake au wakala wake kusajili upya na kuthibitishwa ili laini yake ifunguliwe.

  8.    Watumiaji wa simu za mkononi na wananchi wanashauriwa kuunga mkono juhudi zinazofanyika ili kufanikisha usajili wa namba za simu kwa ajili ya kudumisha na kuendeleza amani na usalama na kuharakisha maendeleo ya sekta na ya Taifa kwa ujumla.

  9.    Faida za kusajili laini ya simu ni nyingi zikiwemo usalama katika huduma za kutuma na kupokea pesa kwa mitandao ya simu. Kununua na kulipia gharama mbalimbali zikiwemo za bili za umeme, maji, na ushuru na pia kusaidia upelelezi iwapo kuna matumizi mabaya ya simu.

  10. Mamlaka inapenda kuukumbusha umma kuwa ni kosa la jinai:
  a)    Kuuza laini za simu kama wewe si wakala wa mtoa huduma: Iwapo mtu atakamatwa na kutiwa hatiani akiuza laini za simu ikiwa yeye si wakala wa kampuni ya simu atahukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kufungwa jela miaka miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja.
  b)   Kutumia simu isiyosajiliwa: Mtu yeyote anayetumia simu isiyosajiliwa anatenda kosa la jinai na akitiwa hatiani atahukumiwa kulipa faini isiyozidi shilingi laki tano, au kifungo cha miezi mitatu jela.

  c)    Kutoa taarifa za uongo wakati wa kusajili namba ya simu: Mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo akijua kuwa taarifa hizo si za kweli anatenda kosa la jinai na akitiwa hatiani atahukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni tatu au kifungo cha miezi kumi na miwili au adhabu zote kwa pamoja.

  d)   Kumsaidia mtu mwingine atende kosa kwa mujibu wa sheria za mawasiliano naye anatenda kosa na akitiwa hatiani atahukumiwa kulipa faini isiyozidi shilingi milioni tatu au kufungwa jela miezi kumi na miwili au adhabu zote mbili kwa pamoja.

  e) Kutumia njia yeyote ya mawasiliano kuvuruga amani, kugombanisha watu, kufanya uchochezi wa kidini au kisiasa, kueneza chuki, kusambaza uongo na kuleta vurugu katika jamii ni kosa la jinai na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobanika kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

  f)Mwananchi ukipokea ujumbe wowote wa kueneza chuki, unaopelekea kuvuruga amani, uchochezi na kuvuruga amani, toa taarifa kwa vyombo husika, kisha futa ujumbe huo. Usiueneze kwa wengine kwani utakuwa sehemu ya uhalifu.

  Imetolewa na:
   

  MSEMAJI MAMLAKA YA MAWASILIANO
  Mamlaka ya mawasiliano TaNzania
  26 July 2013

   


  0 0

  Na Miza Kona        Maelezo – Zanzibar      

  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wameishauri Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupiga marufuku bishara ya uingizwaji wa Kuku kutoka nje ya nchi ili kuwawezesha Wananchi wa Zanzibar kufanya biashara hiyo.
  Wamesema kwa vile biashara hiyo imedumaza juhudi za Wazawa kujiajiri wenyewe hivyo ni vyema Serikali kupiga marufuku ili kutoa nafasi za ajira kwa Wazawa.

  Wajumbe hao wametoa kauli hiyo walipokuwa wakichangia Bajeti ya Waizara ya Mifugo na Uvuvi katika kikao cha Bajeti kinachoendelea katika Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanizibar.

  Mmoja ya Wajumbe hao Hamza Hassan Juma amesema kuiondoa Biashara hiyo hakutosababisha matatizo yoyote katika Sheria za kimataifa hasa ikizingatiwa kuwa Suala la uingizwaji wa Kuku lilipitia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amefahamisha kuwa licha ya Bunge kuidhinisha bishara hiyo siku za nyuma chini ya Waziri David Matayo lakini kwa upande wa Bara bishara hiyo haifanyiki.

  “Wenzetu Bara ndio ambao walihusika kuidhinisha Biashara hiyo lakini cha kushangaza wao wameipiga marufuku kwa nini nasisi tusiiondoe ili kuwawezesha Wananchi wetu kujipatia ajira?” Alisema Hamza.
  Kwa upande wake Mwakilishi wa Viti Maalum Asha Bakari Makame ameiomba Serikali kukubali matakwa ya Wakalishi hao ili kuinua biashara ambayo inaweza kufanywa na Wazawa hasa kinamama.

  Amedai kuwa Afya na ubora wa Kuku hao pia unatia mashaka hivyo ni vyema Wenyeji Wakaachiwa kufanya biashara hiyo ili kuzidi kuongeza fursa za ajira kwa Wazanzibari hasa kinamama.

  Akijibu hoja za Wawakilishi hao Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdillah Jihad Hassan amesema biashara hiyo inafanyika kutokana na Wafanyabiashara Wazawa kutotimiza kiwango cha mahitaji ya Kitoweo cha Kuku kinachotakiwa Zanzibar. Amesema kutokana na hoja hiyo na kwa vile sheria zinaruhusu Serikali iliamua kuwaruhusu wawekezaji kuingiza Kuku hao wanaotoka nje ya Nchi.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed amesema Serikali haiwezi kupiga marufuku biashara hiyo bila kufanya tathimini ya kutosha.

  Amesema kwa Vile Kuku hao huingizwa nchini kwa kufuata taratibu zote ikiwemo pia ya kujua ubora na Afya zao ni vyema Suala hilo likapatiwa muda kabla ya kufanyiwa uamuzi. Kutokana na kuibuliwa hoja hiyo bila kupatiwa ufumbuzi Baraza limeghairishwa hadi Jumatatu ili kupatikana muda wa kutosha wa kujadili Bajeti hiyo.

  IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR  26/07/2013

  0 0

  Oliver Mtukudzi alitoa burudani bure kwa wakazi wa New York katika eneo la kupumzika  Free Park, maelfu ya wamarekani walifurika katika show yake. Hii inafundisha nini wasanii wa nyumbani Tanzania? Nafikiri kuna jambo kubwa sana la kujifunza toka kwa mkongwe huyu. 
  Oliver si mjinga kutoa burudani ya bure, wasanii wetu toka Tanzania inabidi waige mfano huu ili mziki wao uanze kuwaingia wamarekani na hata mataifa mengine ya nje. Nazungumzia msanii kujulikana na kukubalika katika kiwango cha kimataifa  katika soko la mziki la dunia.

  Namalizia kwa kuwapongeza mapromota wote wanaowatafutia show wasanii toka nyumbani kutoa burudani nje ya nchi. Kwa kweli wanafanya kazi nzuri. Sasa nawaomba waanze kutafuta masoko nje ya jamii zetu za kitanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Hii namaanisha sio kuimba pekee katika klabu za wabongo ama wakenya. 

  Mtakubaliana nami wasanii mliowahi kutoka nje ya Tanzania nadhani mnaelewa nachosema. Sisi mashabiki wenu tunataka kuona mkipanda na kushiriki katika majukwaa makubwa yanayoheshimika duniani. Ni furaha yangu nitakapoona msanii wetu anatoa burudani katika viwanja vikubwa hapa Marekani na kwingineko, naamini inawezekana.

  Video na Joshua Mmali.

  kuona mengi toka Swahili TV Mtaani Kunani tembelea www.swahilitv.blogspot.com

  0 0

  Hong Kong Customs yesterday (July 25) detected three drug trafficking cases, with seizures totally valued at $4.78 million, in the department's escalated anti-narcotics efforts to combat drugs.

       Customs officers at the Hong Kong International Airport (HKIA) intercepted a 26-year-old incoming male passenger arriving from Tanzania for clearance yesterday afternoon and seized 1.6 kilogrammes of heroin concealed in two false compartments of his hand carry briefcase. The drugs would fetch a value of about $1.28 million.

       Later in the evening, Customs officers at the HKIA intercepted another 45-year-old man from Tanzania for clearance. On suspicion of concealment of drugs inside his body, the suspect was escorted to hospital where he discharged 204 grammes of heroin after staying for one day. The value of the drugs was about $0.16 million. The suspect is still in the hospital.

       In the same evening, Customs officers intercepted a 28-year-old man at a carpark in Tai Kok Tsui. Approximately 2.03 kg of cocaine camouflaged as snacks were found inside a plastic bag carried by him.

       Customs officers later escorted the suspect to a domestic flat nearby for a search and seized 1 kg of cocaine and 290 grammes of crack cocaine there. The total value of the seizure was about $3.34 million.

       A Customs spokesperson said today (July 26) that all three suspects in the three cases were arrested for drug trafficking. The cases are still under investigation.

       Under the Dangerous Drugs Ordinance, drug trafficking is a serious offence. The maximum penalty is life imprisonment and a fine of $5 million.


  Ends/Friday, July 26, 2013
  Issued at HKT 23:43

  NNNN

  0 0
  0 0

   Afisa Habari na Mawasiliano Bw.  Munir Shemweta toka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bw.  Munir Shemweta juu ya faida za kuimarishwa kwa mfumo wa sheria wa huduma za jamii kwa wazee utakaowezesha upatikanaji wa huduma muhimu za maisha kwa kundi hilo ,wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam katikati ni Afisa Habari toka Idara ya Habari Bw. Frank Mvungi na kulia ni Afisa Sheria Mkuu wa Tume hiyo Bi. Anjela Shila.
   Afisa Sheria Mkuu toka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Anjela Shila(kulia) akisisitiza jambo juu ya faida za kuimarishwa kwa mfumo wa sheria wa huduma za jamii kwa wazee utakaowezesha upatikanaji wa huduma muhimu za maisha kwa kundi hilo ,wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
  Katibu Msaidizi Elimu ya Sheria kwa Umma toka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Bi. Agnes Mgeyekwa(kushoto) akitoa ufafafanuzi kuhusu namna tume hiyo inavyotimiza majukumu yake katika kurekebisha sheria mbalimbali nchini,wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam kulia ni Afisa Habari na Mawasiliano wa tume hiyo Bw.  Munir Shemweta.


   ===========      ========  =======
   

  MAPITIO YAANZA YA MFUMO WA SHERIA WA HUDUMA ZA JAMII KWA WAZEE

  Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza kupitia mfumo wa sheria wa huduma za jamii kwa wazee (elderly social care) kwa nia ya kubaini mapungufu yaliyoko kwenye mfumo huo na kutoa mapendekezo  stahiki ili kuweza kuwa na mfumo mzuri wa sheria   utakaolenga ustawi na hifadhi kwa wazee wote waliohitimu miaka 60 na zaidi wa mijini na vijijini. 

  Wazee wanapofikia umri mkubwa, uwezo wao wa kujihusisha na shughuli mbalimbali hupungua na hivyo hushindwa kijihudumia mahitaji yao muhimu ya kila siku kama vile chakula, mavazi, malazi, pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa ziwe za kitamaduni, kijamii au kiuchumi.

  Tume imeona kuna umuhimu wa kuimarisha mfumo wa sheria  wa huduma za jamii kwa wazee ili kuwezesha wao kupata huduma muhimu za maisha.   Pamoja na kuwa na Sera ya Taifa ya Wazee (National Ageing Policy, 2003) Tanzania haina sheria maalum katika eneo hili.   Sheria mbalimbali za mafao zinawagusa wazee wanaostaafu kazi serikalini na sekta binafsi ambao ni sehemu ndogo sana ya kundi la wazee wengi wanaokosa huduma muhimu za maisha.

  Ikumbukwe kuwa wazee hawa ni wale waliotumikia taifa kwa nguvu na moyo wote kwenye ngazi mbalimbali wakati wakiwa na nguvu zao hivyo wanapokuwa wamezeeka ni muhimu wakawekewa mfumo bora wa kisheria ili kuhakikisha wanaishi maisha mazuri bila kujali kupungua kwa uwezo wao wa kujishughulisha katika nyanja mbalimbali.

  Kwa sasa Tume inaendelea na rasimu ya awali ya kuangalia hali halisi ya Tanzania kuhusiana na suala zima la wazee ikiwemo mikataba ya kimataifa, mifumo ya kisheria na kijamii pamoja na sera na na baada ya hapo itatembelea mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kwa nia ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya mfumo huo wa kisheria.  Maoni hayo yatahusisha wazee wenyewe, maofisa kazi, afya, ustawi wa jamii, watendaji wa vijiji, taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazojishughulisha na wazee pamoja na wananchi kwa ujumla.

  Ni Matarajio ya Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kuwa baada ya kukamilika kwa mapitio ya mfumo huo wa kisheria kuhusiana na huduma za jamii kwa wazee, Tume itakuja na mapendekezo ya kisheria na yasiyo ya kisheria ambayo yataleta tija kwa taifa kwa ujumla.
  Kuhusu Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania

  Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania ni Idara ya Serikali inayojitegemea chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.  Ilianzishwa kwa mujibu wa sheria kupitia kifungu cha 3 cha Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Namba 11 ya mwaka 1980.  Sheria hii kwa sasa ni Sura ya 171 ya Sheria za Tanzania kama sheria zilivyorekebishwa katika toleo la mwaka 2002.  

  Majukumu ya Tume katika ujumla wake ni kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria mbalimbali kwa Serikali, kwa kutafiti na kutathmini maeneo yote ya sheria husika na kuyatolea mapendekezo kwa lengo la kuyaboresha.  Baada ya utafiti, Tume huwasilisha taarifa yake kwa Waziri anayehusika na masuala ya sheria.

  Moja ya mafanikio ya Tume yaliyopatikana kutokana na mapendekezo ya Taarifa zake zinazopelekwa kwa Waziri anayehusika na masuala ya sheria ni pamoja na kutungwa kwa sheria mbalimbali ikiwa ni pamoja na:-

  ·         Marekebisho ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 Kuhusu Kuwalipa Fidia Wahanga Wa Makosa Ya Jinai;
  ·         Kuchapishwa kwa Tangazo la Serikali Na. 192 la mwaka 1988 kuhusu Uharakishwaji wa Mashauri Mahakamani;
  ·         Mapitio ya Sheria ya Udhibiti wa Ubadilishaji wa Fedha za Kigeni;
  ·         Uanzishwaji wa Mfumo wa Wafungwa Kutumikia Sehemu ya Vifungo Nje ya Gereza;
  ·         Marekebisho Makubwa Yalifanywa Kwenye Sheria 28 Kati ya 40 Zilizopendekezwa na Tume ya Nyalali Ikiwa ni Sehemu ya Mapendekezo Yaliyotolewa na Tume ya Kurekebisha Sheria Baada ya Kusoma Taarifa Hiyo ya Tume ya Nyalali
  ·         Kutungwa kwa Sheria ya “Makosa ya Kujamiiana” Na. 4 ya 1998;’
  ·         Marekebisho ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai Ili Kutambua Utatuzi wa Migogoro kwa Njia za Usuluhishi;
  ·         Kutungwa kwa Sheria za Kazi za Mwaka  2004;
  ·         Kurekebishwa Sheria ya Ushahidi Ili Kutambua Ushahidi wa TEKNOHAMA (Electronic Evidence) Mwaka 2007;
  ·         Kutungwa kwa Sheria ya Vinasaba vya BinadamuMwaka 2009;
  ·         Kutungwa kwa Kanuni Mpya za Mahakama ya Rufaa (Court of Appeal Rules) za Mwaka 2009
  ·         Kutungwa kwa Sheria Zinazohusu Haki za Watu Wenye Ulemavu za Mwaka 2009;na
  ·         Kutungwa kwa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009.  Imetolewa na:

  Munir Shemweta
  Afisa Habari na Mawasiliano
  TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA
  27 JULAI 2013  0 0  Na Georgina Misama-MAELEZO


  Jumla ya shilingi trilioni 44.5 za kitanzania zinatarajiwa kutumika katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, ambapo Tanzania imedhamiria kufikia hadhi ya nchi zenye kipato cha kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025.


  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Joyce Mkinga alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo.


  Joyce alitaja malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, ambapo alisema katika miaka mitano ya kwanza vipaumbele vipo katika makundi ya Miundombinu ambayo inahusisha nishati, usafirishaji, TEHAMA, maji safi na maji taka na umwagiliaji, Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara,Viwanda, Rasilimali watu na uendeshaji wa huduma za utalii, Biashara na fedha ni miongoni mwa vipaumbele vitano vya Taifa ambavyo serikali inatarajia kutekeleza.


  “Mkazo mkubwa unatiliwa katika miradi ya maendeleo, tunaamini miradi ikiendelea vizuri, umasini utapungua. Tume ya mipango ina wajibu wa kufatilia miradi iliyowekewa kipaumbele na utekelezaji wake” alisema Joyce Mkinga.


  Aidha Bi. Joyce alisema  kuwa  ili kufikia malengo jumla ya shilingi tirioni 8.9 zinahitajika kwa mwaka na kuongeza kuwa Serikali inakadiria kuwekeza kiasi cha wastani wa takriban shilingi trilioni 2.9, kwa mwaka wakati wastani wa shilingi trilioni 6.0 kwa mwaka zinatarajiwa kutokana na uwekezaji binafsi au ubia.


  Itakumbuwa kuwa mpango wa matoke sasa ambao ulizundiliwa ambao ulizundiliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mpango huu umelenga kuhakikisha utekekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inafiiwa ifikapo mwaka 2025.


  0 0

   Rais Kikwete akihutubia umati Ngara.
   Rais Kikwete akisalimiana na  wananchi  wa Rulenge
   Rais Kikwete akiwasili Ngara huku akipokelewa kwa shangwe na wananchi
   umati wa watu ukimsikikliza rais kikwete kijiji cha Rulenge.
   waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi profesa anna tibaijuka akielezea baraza la ardhi
   waziri wa kilimo christopher chizza akielezea mipango kabambe ya kilimo
   Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe aklieleza mipango kabambe ya maji.

  0 0

   Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bi. Joyce Mkinga akionesha kwa waandishi wa habari kijitabu cha Dira ya Taifa ya Maendeleo hadi kufikia 2025, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam.

   Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bi. Joyce Mkinga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa dira ya Taifa ya Maendeleo hadi kufikia 2025 wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam kushoto ni Afisa Habari toka Idara ya Habari Bi. Fatma Salum.PICHA ZOTE NA FRANK MVUNGI-MAELEZO
   
  0 0

    The cleaner Production Centre of Tanzania (CPCT) dealing with Resource Efficiency and Cleaner Production (RECP) has conducted training on RECP to all manufacturing industries in Tanzania.

  The training was aiming at minimizing of Energy use, Water use, Profitable production, Lowest possible pollution of environment - Particularly Lake Victoria under Lake Victoria Environment Project (LVEMP II).

  In this regard CPCT conducted RECP Award Competition for Lake Zone in which 63 manufacturing industries participate among them was Mutex - Musoma Textile Mills (T) Ltd, a subsidiary of MeTL group of Companies.
  Out of 63 participants, 10 contestants were short listed for 4 categories, unto which MUTEX emerged SOLID WASTE MANAGEMENT WINNER 2013.
  Verification team was comprised of East African members on Cleaner Production, which are Uganda Cleaner Production Centre, Kenya National Cleaner Production Centre, Cleaner Production Centre of Tanzania and OSHA officials.

  The ceremony was conducted in Mwanza on 28th June, 2013 by CPCT, under Ministry of Water and Irrigation, headed by Permanent Secretary in the Ministry where the Chief Guest was Hon. Minister of State for Enviornment in the Vice President ‘s Office Hon Dr. Therezya Huvisa.
  NEMC and Lake Victoria Environmental Project (East Africa) Officials also attended.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro.
  Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamtandao wa Jumuiya ya wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi maandamano ya wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, mmoja kati ya wachangiaji bora wa kuendeleza Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) Justice Shekilango, wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo Julai 26, 2013 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Wasanii wa kikundi cha ngoma ya Muhembe cha mjini Dodoma, wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya ya Mtandao wa wakulima wa Tanzania (MVUWATA) yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro.
  Wakulima wa Jumuiya ya Mtandao wa Wakulima wa Tanzania (MVUWATA) wakiwasili kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa maandamano leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo, yaliyopokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, aliyekuwa mgeni rasmi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanamtandao wa Jumuiya ya wakulima wa Tanzania (MVUWATA) baada ya kupokea rasmi maandamano ya wakulima ya maadhimisho ya miaka 20 ya Jumuiya hiyo iliyofanyika leo katika uwanja wa Jamhuri mijini Morogoro. Picha na OMR.

  0 0

  Kambi ya Wasanii wa Filamu na Maigizo pamoja na Kambi ya Wanahabari Makapela Tanzania imepata pigo kubwa baada ya Mwanachama wake Nguli, Simon Simalenga kuamua kuiaga kambi hiyo na kuingia rasmi katika Kambi Tawala ya Wanandoa baada ya kufunga Ndoa na Bi. Neema Inana.

  Wawili hao wameamua kuingia kambi hiyo ya Upinzani katika mahusiano leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi Sinza jijini Dar es Salaam na baadae katika tafrija kubwa inayofanyika usiku huu wa Julai 27, 2013 katika ukumbi qa Grande Hall uliopo ndani ya Hoteli ya Picolo Beach Mbezi. 
  Production: MD Digital Company: +255 373 999/+255 717 002303 
  Whatsapp +255 788 207274.
older | 1 | .... | 126 | 127 | (Page 128) | 129 | 130 | .... | 1897 | newer