Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNE 16,2017


DKT HAMISI KIGWANGALLA AZINDUA KONGAMANO LA WATOTO KUELEKEA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

UNIC Yakutana na Wanafunzi Mbalimbali Kujadili Mkutano wa Bahari

$
0
0
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akizungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vijana (hawapo pichani) kwenye mkutano kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na vijana na wanafunzi kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (mbele) akizungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vijana kwenye mkutano kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Sehemu ya maofisa kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), wakiwa katika mkutano huo na wanafunzi kutoka shule mbalimbali na pamoja na vijana kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Sehemu ya wanafunzi wakiwa kwenye mkutano huo ulioandaliwa na UNIC, Tanzania kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (mbele) akizungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vijana kwenye mkutano kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (mbele) akizungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vijana kwenye mkutano kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (mbele) akizungumza na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vijana kwenye mkutano kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Baadhi ya wanafunzi wakichangia hoja kwenye mkutano huo ulioandaliwa na UNIC, Tanzania kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Baadhi ya wanafunzi wakichangia hoja kwenye mkutano huo ulioandaliwa na UNIC, Tanzania kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani.

KITUO cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) leo kimekutana na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vijana kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Mkubwa wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York kuanzia Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa Bahari.

 Akizungumza na wanafunzi na vijana katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo aliwataka vijana kuwa mstari wa mbele kwa kutoa elimu na kushiriki katika jitihada za kuifadhi mazingira ya bahari pamoja na viumbe waliomo kwa matumizi endelevu. Alisema kwa mujibu wa majadiliano katika mkutano uliopita, kasi ya uharibifu wa mazingira ya bahari na viumbe waliomo ni kubwa kiasi ambacho inatishia baadhi ya viumbe kutoweka kabisa kama si kuadimika katika vizazi vya baadaye. 

Alisema taka aina ya nailoni ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitupwa baharini na kwenye fukwe zinatishia viumbe waliomo baharini na huwenda zikawa na madhara makubwa kwa binadamu hapo baadaye kama jitihada za makusudi hazita chukuliwa. Aliwataka vijana kuwa mabalozi katika kutoa elimu juu ya umuhimu wa kusafisha fukwe na kufanya uvuvi mzuri kwa wavuvi ili kulinda mazalia ya samaki na viumbe wengine majini kwa manufaa ya baadaye. Aliongeza kuwa kuna kila sababu ya kuhifadhi mazingira ya bahari kutokana na umuhimu wake kwa maisha ya binadamu.

 "...Tunapata chakula kutoka baharini (samaki), tunanufaika kwa shughuli mbalimbali kama utalii, ajira katika uvuvi na kazi zingine, biashara, usafiri wa watu na mizigo na shughuli anuai zimekuwa na manufaa makubwa hivyo kuna kila haja ya kila mmoja kuchangia katika kulinda uharibifu wa bahari na mazingira yake," alisema Bi. Stella Vuzo na kuwataka vijana kujitolea mmoja mmoja na katika kusafisha fukwe zetu. 

Aidha katika mkutano wa 'The Ocean Conference, United Nations' takribani makubaliano ya ahadi 700 zimetolewa kwa nchi mbalimbali washiriki katika mkutano huo wakiahidi kulinda na kutunza mazingira ya bahari pamoja na viumbe vyake ili visije kutoweka na kutishia manufaa lukuki yatokanayo na uwepo wa bahari na mazingira yake. 

 Aliongeza kuwa wameamua kuwapa elimu zaidi vijana kwa kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana hivyo wakiwa na elimu ya kutunza na kuhifadhi fukwe watakuwa mabalozi wazuri wa mapambano hayo ya kulinda mazingira ya bahari. 

Hata hivyo, Ofisa huyo wa UNIC aliyakaribisha makundi mbalimbali ya vijana kutembelea ofisi za UNIC, Tanzania kujua shughuli mbalimbali wanazozifanya na kuungana katika kampeni anuai zenye manufaa kwa jamii nzima. Baadhi ya wanafunzi wakichangia hoja kwenye mkutano huo ulioandaliwa na UNIC, Tanzania kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Mmoja wa waratibu wa mkutano huo (kushoto), ofisa kutoka Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), akizungumza jambo na wanafunzi na vijana walioshiriki mkutano huo. Baadhi ya wanafunzi wakichangia hoja kwenye mkutano huo ulioandaliwa na UNIC, Tanzania kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa bahari duniani. Picha ya pamoja ya washiriki katika mkutano huo pamoja na baadhi ya maofisa wa UNIC, Tanzania.

UBA Bank Tanzania yaingiza sokoni Kadi zake Mpya za Mastercard

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha malipo ya kiditali wa bank ya UBA Tanzania, Mr. Priscussy Kessy akiongea na baadhi ya wafanyakazi na wateja wa benki hio wakati wa uzinduzi wa Kadi za Mastercard zitakazoanza kutolewa kwa wateja wa UBA Bank Tanzania.
 Mkurugenzi mkuu wa bank ya UBA Tanzania, Mr Peter Makau akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kadi za mastercard kwa wateja wa bank hiyo ya UBA Tanzania
 Mkurugenzi Mkazi wa Mastercard Tanzania Mr. Anthony Karingi (kushoto) akikata utepe na mkurugenzi mkuu wa bank ya UBA Mr Peter Makau (kulia) kuashiria uzinduzi wa huduma mpya ya kadi za mastercard kutoka Benki ya UBA Tanzania.
 Mkurugenzi mkazi wa Mastercard Tanzania Mr. Anthony Karingi (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa bank ya UBA Tanzania Mr Peter Makau (wa pili kushoto)wakikata keki kuashiria uzinduzi wa huduma hio ya kadi za mastercard ya bank ya UBA Bank uzinduzi uliofanyika leo katika tawi la benki hio lililopo barabara ya Pugu
 Mmoja wa wateja wakubwa wa benki ya UBA Tanzania, Mr Jitendra Kumar Bhardwayi akizungumzia ujio wa mastercard ya UBA Bank ambayo amesema itamsaidia katika kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao na kumrahisishia shughuli zake za kibiashara
 Baadhi ya wafanyakazi wa UBA bank Tanzania wakifurahi mara baada ya uzinduzi huo wa kadi za Mastercard za UBA Bank.
Wafanyakazi wa benki ya UBA wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa kadi za mastercard kutoka benki ya UBA leo
Wafanyakazi wa benki ya UBA na baadhi ya wafanyakazi wa Mastercard Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa Kadi mpya za Mastercard za benki ya UBA Tanzania.

Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

 Benki ya UBA Tanzania imezindua huduma yake mpya ya kadi za mastercard ambazo zitaanza kutolewa kwa wateja wake nchni Nzima. Wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa kitengo cha digitali za benki hio ya UBA Bank Bw Priscussy Kessy amesema kuletwa kwa kadi hizo za mastercard kwa benki yao itawasaidia wateja wao kufanya manunuzi kwenye tovuti mbalimbali na pia zitatumika pia kutolea pesa katika mashine za kutolea pesa zote duniani zenye nembo ya mastercard iwe ndani ya nchi au nje ya nchi.
Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wafanyakazi wa UBA bank na Mastercard Tanzania umefanyika katika tawi la UBA Bank lililopo barabara ya Pugu huku baadhi ya wateja wa benki hio wakipata fursa pia ya kushuhudia uzinduzi huo wa huduma mpya ya kadi ya mastercard kutoka Bank ya UBA Tanzania.
Benki ya UBA Tanzania ambayo yenye matawi yake Posta, Kariakoo na Barabara ya Pugu huku ikiwa na mashine za kutolea pesa sehemu mbalimbali za jiji la Dar Es Salaam ikiwemo Segerea, Mikocheni, Mabibo na kwingineko.TAARIFA ZAIDI KUTOKA KWA MKURUGENZI MKUU WA UBA BANK TANZANIA.
 
On behalf of Board of Directors UBAT Ltd , UBA Group, and management of UBAT,  I wellcome  our valued customers, Business partners, and UBA staff  to our luanch of MasterCard issuance by UBATZ.
I also take this opportunity to recognise the presence of Mastercard representatives here with us today. Specifically we have with us today Mr. Anthony Karingi Mastercard country manager, and, Amy Etiang Mastercard leader Product management.
This event is an important milestone for our business objective to continuously diversify and increase the range of our products and services to provide efficient and convenient means of serving our customers. 

We are therefore delighted to now extent our range of products and services to MasterCard issuance by UBATZ.  The Launch of MasterCard  issuance today by UBA Tanzania effectively means that our customer will now have the benefit of being issued with MasterCard debit cards and will be able to Benefit from the convenience and good efficiency of Master Card Global network payments  technology and service. 
We would also like to thank MasterCard for partnering with UBA in the provision of high quality products and services to serve our customers better. Further , we look forward to enhancement of our business partnership with with Mastercard to in future cover other new products services to our customers. 

UBA is committed to customer Excellence and the  launch of Master Card issuance by UBAT today is confirmation of this commitment.


Asanteni

Benki ya NMB yafuturu pamoja na wateja wake Mjini Zanzibar

$
0
0
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud (kulia) akimshukuru Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Abdulmajid Nsekela baada ya kupokea zawadi maalumu kwa ajili ya Ramadhani mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Hafla hii ya Futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi. Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani mjini Zanzibar wakiwa kwenye hafla ya futari Mjini Zanzibar. Hafla hiyo ya futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi. Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB – Abdulmajid Nsekela (wa kwanza kulia) akijiandaa kumkabidhi zawadi ya ramadhani Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud ikiwa ni zawadi maalumu kwa ajili ya Ramadhani mara baada ya kumalizika kwa tafrija ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Wateja wake walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani. Hafla hii ya Futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi Baadhi ya wateja wa Benki ya NMB walio kwenye mfungo Mtukufu wa Ramadhani mjini Zanzibar wakiwa kwenye hafla ya futari Mjini Zanzibar. Hafla hiyo ya futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi. Baadhi ya viongozi mbalimbali na wa Benki ya NMB wakiwa kwenye hafla ya futari Mjini Zanzibar. Hafla hiyo ya futari ilifanyika Mjini Zanzibar- Unguja juzi.

Magreth Sinyangwa wa Kilosa Morogoro apokea Milioni 20 za Biko

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MJASIRIAMALI mwanamke mwenye umri wa miaka 26, Magreth Sinyangwa amekabidhiwa jumla ya Sh Milioni 20 za ushindi wa bahati nasibu ya Biko, aliyoupata katika droo kubwa iliyochezeshwa juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam, huku akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na ushindi huo.

Sinyangwa amekabidhiwa fedha hizo Kilosa katika benki ya NMB, mkoani Morogoro na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ambaye pamoja na mambo mengine, alimpongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu pamoja na kuboresha maisha yake ya kila siku.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Heaven alisema ni wakati wa kutajirika kwa kutumia vyema bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyozidi kuchanja mbuga na kutoa mamilioni ya Sh kwa washindi wa droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili, sanjari na zawadi za papo kwa hapo.

“Tunajivunia kumpata mshindi mwanamke ambaye leo (jana) tumemkabidhi zawadi yake ya Sh Milioni 20, tukiamini kuwa atazitumia vizuri katika kuhakikisha kwamba anakuza biashara zake, ukizingatia kuwa tayari yupo kwenye tasnia ya biashara kabla ya kupata donge nono la Biko.

“Kucheza ni rahisi kwa sababu Biko inachezwa kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo mtu atafanya muamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo ataweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku mbali na donge nono la Sh Milioni 20 linatoka kila Jumatano na Jumapili, pia zipo zawadi za papo hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni,” Alisema Heaven.

Naye Sinyangwa alishindwa kuzuia furaha yake baada ya kukabidhiwa fedha zake, akisema kuwa ameshukuru ushindi wake huo akisema maisha yake yatabadilika kwa sababu atatumia biashara zake zipanuke kwa kutumia vyema ushindi huo wa Biko uliompatia mamilioni ya fedha.

“Huu ni wakati wa kusonga mbele kiuchumi kwa kutumia fedha hizi ambazo nimezipata bila kutarajia, hivyo nawaomba akina mama wenzangu pamoja na Watanzania wote kucheza Biko kwa sababu kila mtu anaweza kushinda bila kuangalia yupo wapi na anaishi vipi.

“Mimi nipo Kilosa Morogoro, lakini nilishangaa nilipopigiwa simu na mtu anayeitwa Kajala Masanja na kuniambia kuwa nimeshinda Biko, lakini nzuri zaidi leo (jana) wameniletea fedha zangu hadi ninapoishi jambo ambalo naona si la kawaida na ni la pekee kwa hawa Biko,” Alisema.

Mbali na kukabidhiwa fedha hizo jumla ya Sh Milioni 20, Biko pia tayari wametoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa washindi wake walioshinda katika mwezi Mei pekee, ikiwa ni siku chache tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu hiyo inayotikisa katika kona mbalimbali hapa nchini..
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wao wa Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa aliyeibuka kidedea katika droo kubwa iliyofanyika Jumatano iliyopita. Kushoto ni mume wa Magreth, Bahati Ramadhani na mwingine ni Ofisa wa NMB Tawi la Kilosa, akiwa kwenye makabidhiano hayo.
Mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa kutoka kwa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kushoto akiwa ameshika hundi tayari kwa kumkabidhi mshindi wao wa Sh Milioni 20 wa Kilosa Morogoro, Magreth Senyangwa, wa pili kutoka kushoto akifuatiwa na mumewe Bahati Ramadhan pamoja na familia yao.
Mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Biko, Magreth Senyangwa, akiwa amebeba fedha zake mara baada ya kukabidhiwa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 kwa mshindi wao wa Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa aliyeibuka kidedea katika droo kubwa iliyofanyika Jumatano iliyopita. Kushoto ni Ofisa wa NMB Tawi la Kilosa, akiwa kwenye makabidhiano hayo.

UWT Zanzibar yawataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

UMOJA wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi  Tanzania (UWT)  umewataka wanawake kuchangamkia fursa za Uongozi wa ngazi mbali mbali  kupitia uchaguzi unaondelea hivi sasa ndani ya Chama na jumuiya zake.

Wito huo umetolewa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo Zanzibar  Bi.Tunu Juma Kondo    katika mwendelezo wa ziara ya  UWT  ya kuzungumza na Viongozi wapya wa ngazi za matawi wa umoja huo uko Jimbo la Kijini  Wilaya ya Kaskazini "A" kichama Unguja.

Awambia  Akina Mama hao kuwa Uchaguzi  wa ngazi mbali mbali unaoendelea  katika taasisi hiyo ndio fursa moja wapo ya wanawake  kupata nafasi za uongozi ili waweze kufikia malengo ya kupata uwakilishi wa viongozi wenye idadi sawa na wanaume ndani ya Chama hicho.

Alifafanua kuwa wanawake wanatakiwa kuondokana na dhana ya kuendelea  kuongozwa kwa kila nafasi za uongozi ndani ya CCM bali wanatakiwa kujiongeza kwa kuwania wenyewe uongozi ndani ya chama hicho ili kuleta maendeleo endelevu ndani ya chama na jumuiya zake.

Pia alisisitiza viongozi hao kuwa pamoja na majukumu ya kiuongozi waliyonayo ni lazima wawahamasishe  kwa wingi wanawake  kuwania nafasi za uongozi ili kupata viongozi makini na wenye  uwezo  wa kwenda na kasi  za kiutendaji za chama hicho.

"Wanawake wenzangu tutumieni fursa ya Uchaguzi wa Chama kuwania nafasi mbali mbali za uongozi , tusisubiri nafasi za uteuzi  bali tusimame wenyewe  kupambana kwa kuhakikisha nasi tunakuwa na nyadhifa za uongozi kama walivyo wanaume kwani tunaweza wenyewe bila ya kuwezeshwa’’,. Alisema Bi.Tunu.

Akizungumza katika ziara hiyo Katibu Msaidizi Idara ya Organazesheni UWT Zanzibar, Bi. Mgeni Ottow Alisema CCM atadumu madarakani endapo viongozi mbali mbali wanaopatikana kupitia uchaguzi wa chama hicho watakuwa na uzalendo wa kweli katika kulinda maslahi ya taasisi hiyo kwa vitendo.

Bi. Mgeni aliwasihi  Akina Mama wa Umoja huo kuhakikisha wanachagua viongozi waadilifu na wenye uwezo wa kubuni fursa mbali mbali za maendeleo zitakazowanufaisha wanawake wenzao na chama kwa ujumla.

“ Wanawake ndio tegemeo la Chama chetu na jumuiya kwa ujumla hivyo lazima tuwe wa kwanza kujitokeza kwa kila tukio linalohusu uimarishaji wa chama chetu hasa michakato ya uchaguzi na tukiwa wengi katika nafasi za uongozi ndipo tutakapopata nguvu za pamoja kutetea haki zetu na kupinga kisheria udhalilishaji wa Wanawake”,. Aliseleza Bi. Mgeni.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi. Miza Ali Kombo amesema zoezi la Uchaguzi kwa ngazi ya Wadi linaendelea vizuri kwani wagombea tayari wamejaza fomu na kinachosubiriwa kwa sasa ni upigaji wa kura ili kupata viongozi watakaoongoza ngazi hiyo kwa miaka mitano.

Naye Katibu wa UWT Tawi la Muange, Bi. Waja Mnadhani Ali  alieleza maratajio yake baada ya kupata nafasi hiyo atafanya kazi za jumuiya na chama kwa umakini na uadilifu ili kuwawakilisha vyema wanawake waliomuamini na kumpa ridhaa ya uongozi huo.
 Kaimu  Naibu  Mkuu wa UWT Zanzibar, Bi. Tunu Juma Kondo akizungumza na viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
  Katibu Msaidizi wa  Idara ya  Organazesheni  UWT Zanzibar, Bi. Mgeni  Ottow akitoa nasaha kwa viongozi wa Matawi ya Jimbo Kijini Wilaya ya Kaskazini “A” kichama Unguja.
Baadhi ya viongozi wa UWT  wa Matawi jimbo la kijini Wilaya ya Kaskazini “A”  kichama Unguja wakisikiliza kwa makini nasaha zinazotolewa na viongozi wa UWT Zanzibar  uko Tawi la CCM Muange.

CRDB YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA KUWAPATIA ZAWADI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BENKI ya CRDB imeadhimisha siku ya  Mtoto wa Afrika kwa kuwapatia zawadi watoto mbalimbali ambao wazazi wao waliwafungulia akaunti za Junior Jumbo huku wakiwa wamewekewa fedha mara kwa mara.

Akitoa zawadi hizo, Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe  Nomina Msoka amesema kuwa watoto hao waliopatiwa zawadi ni kutokana na wazazi wao kuwawekea fedha mara kwa mara na hata akiba za akaunti zao zina kiasi kikubwa cha fedha.

Nomina amesema kuwa, wazazi wanatakiwa kuwafungulia na kuwawekea watoto wao fedha mara kwa mara iili kuwandaa na maisha ya baadae ikiwemo katika kulipia ada za masomo yao na pia upo taratibu wa wazazi kuwaekea hela kupitia akaunti zao..

Amesema mbali na hilo, CRDB wameweza kuandaa michezo mbalimbali ya watoto kwa ajili ya kujumuika pamoja na wenzao na kufahamiana zaidi.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe  Nomina Msoka akiwa amembeba mtoto Kinora Brown na kumkabidhi zawadi yake ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  kwa mama yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka. 
 Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Orley Mwanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
 Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Tonia Naivasha  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti  mtoto Rashidi Jumbe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka  akiwa katika picha ya pamoja na watoto aliowakabidhi zawadi za mebegi ya Junior Jumbo Akaunti  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
  Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka   akizungumza na watoto hao baada ya kumalizika kwa zoezi la ugawaji zawadi  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Watoto waliojitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wakiwa wanacheza michezo mbalimbali iliyoandaliwa na tawi la benki ya CRDB Azikiwe. Picha zote na Zainab Nyamka.



UCHAGUZI TFF: IMANI MADEGA ACHUKUA FOMU YA URAIS WA TFF

$
0
0

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga Seneta Imani  Maugila Madega


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga Seneta Imani  Maugila Madega amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.

Madega anakua ni mtu wa pili kuchukua fomu ya Urais baada ya Rais anaemaliza muda wake Jamal Malinzi kuchukua mapema asubuhi ya leo.


SIKU YA MTOTO AFRIKA : MAKAMU WA RAIS AFUNGA TAMASHA LA UELIMISHAJI NA UPIMAJI KWA WATOTO NA VIJANA KINYEREZI DAR ES SALAAM

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangalla wakati Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Meza Kuu Ifurahia Jambo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwaaga wageni mbalimbali waliofika kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana kwenye uwanja wa michezo wa shule ya msingi Kinyerezi. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe.Sophia Mjema
Burudani mbalimbali zilitolewa kwenye tamasha hilo




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kote nchi kuwafichua watu wanaonyanyasa na kudhalilisha watoto kijinsia ili waweze kukamatwa na kuchukua hatua za kisheria kama hatua ya kukomesha vitendo hivyo ambayo vimeanza kushamiri katika baadhi ya jamii nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kuhitimisha kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ilitoa huduma bure za vipimo na matibabu kwa watoto na vijana zaidi ya 1500 kampeni ambayo iliambatana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika viwanja vya Shule ya msingi Kinyerezi mkoani Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa watenda maovu hao lazima vifichuliwe na wananchi, walezi pamoja na wazazi kwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa watoto wapo miongoni mwa jamii.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola kutofumbua macho vitendo hivyo bali pindi wanapopata taarifa za matukio ya udhalilishaji wa watoto wachukue hatua za haraka za kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki watu wanaofanya vitendo hivyo vibaya.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kote nchini waache kuwaficha watu wanaotendea vitendo hivyo vibaya bali wawapatie taarifa walimu wao na polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa kufanya hivyo watoto watakuwa salama katika mazingira ya nyumbani na wakiwa mashuleni kwani watu wabaya wanaofanya vitendo hivyo watawajibishwa kulingana na matendo maovu waliyokuwa wanawafanyia watoto hao.

“Mtoto anaweza kufaidika na fursa sawa iwapo tu atalindwa kwa kuwezeshwa kuwa afya bora”, Amesisitiza Makamu wa Rais.

Kuhusu kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameendelea kuua watu kwa kasi katika nchi zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.

Amesema ipo haja ya kuimarisha juhudi za kukabiliana na tatizo hilo kwa ushirikiano wa wadau wote kwani janga hilo linagharimu taifa na wananchi wake wakiwemo watu wazima, watoto na vijana.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yasipodhibitiwa yatapunguza uzalishaji mali,ufanisi mahali pa kazi na hata shughuli za ulinzi na usalama nchini mwetu na hivyo pato la taifa litapungua na taifa kuwa watu maskini kutokana na magonjwa hayo”, Alifafanua Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza Serikali imeweza kupanua maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa saratani nchini kwa kujenga jengo jipya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kuongeza majengo mapya ya huduma za saratani kwenye Hospitali za Rufaa ya kanda ya Bugando mkoani Mwanza.

Amesema Serikali pia imejenga Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambayo ni taasisi ya mfano ya kutibu maradhi ya moyo ambapo kutokana na kujengwa kwa taasisi hiyo Serikali imefanikiwa kuokoa mabilioni ya fedha ambayo yangetumika kuwagharamia wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamisi Kingwangala amemhakikishia Makamu wa Raia kuwa Wizara hiyo itaendelea kuweka mipango na mikakati imara ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini.

Dkt Kingwangala ameomba wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kidini na wadau wengine kushirikiana na Wizara ya Afya katika kuongeza kasi ya kukabiliana na magonjwa hayo ili yasiendelee kuteketeza maisha ya watu nchini

DIASPORA WAMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI

DARUSO YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
 Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Mhandisi John Jilili(katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga kupongeza juhudi za kuleta ukombozi wa kiuchumi zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli. Kulia ni Makamu wa Rais wa Serikali hiyo bi Anastazia Anthony na kushoto ni Waziri wa michezo,Haiba na Burudani Bw. Mabina David. 
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo.
  (Picha na frank Mvungi-MAELEZO)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kazi za kizalendo anazoendelea kuzifanya kwa maslahi mapana ya Taifa .

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), Mhandisi John Jeremiah amesema wanaunga mkono jinsi suala la mchanga wa madini (makinikia) linavyoshughulikiwa na Serikali ikiwa ni moja ya hatua za kuleta mageuzi ya kweli na kujenga Tanzania mpya.

“Tofauti na wale wanasiasa wanaobeza juhudi za Rais Mgufuli sisi wana DARUSO tunapenda kumuhakikishia kuwa tuko pamoja nae kifikra, kimikakati na kimaombi na tunaamini kuwa fedha iliyopaswa kulipwa na ACACIA kwa Tanzania tangu 1998 hadi 2017 zitalipwa mara moja”Alisisitiza Jeremiah.

Aliongeza kuwa ripoti ya kamati iliyoongozwa na Profesa Michael Ossoro imebainisha kuwa fedha zilizopotea zingeweza hudumia bajeti ya miaka mitatu hivyo juhudi za kulinda rasilimali za Taifa zinapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania 

“DARUSO tunapenda kukumbusha kuwa vita hii sio ya chama chochote cha siasa bali ni vita ya watanzania wote kwa hivyo tusimame na kuungana na Mhe. Rais wetu Dkt. Magufuli kwenye mapambano haya.” Alisisitiza Mhandisi Jeremiah

Mwandisi Jeremiah amesema kuwa kiwango hicho cha fedha kingetosha kuhudumia huduma za kijamii hivyo kuwapa Watanzania unafuu wa maisha.  

“Tunapenda kumpongeza Mhe. Rais kwa muelekeo mzuri wa juhudi zake za kizalendo zilizomfanya Mwenyekti Mtendaji wa Kampuni ya (Afica) Barrick Gold Mining Professor John Thornton kuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu”.Alisisitiza Mwandisi Jeremiah.

KATIBU WA BUNGE DKT. KASHILILAH AONGOZA KIKAO CHA MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA BUNGE LEO UKUMBI WA SPIKA MJINI DODOMA

$
0
0
 Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akiongoza kikao cha Menejimenti ya Utumishi wa Bunge kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha Menejimenti ya Utumishi wa Bunge wakimsikiliza Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WAZIRI MAKAMBA AZUNGUMZIA MAADHIMISHO YA SIKU JANGWA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (katikati) akiongea na waandishi wa habari juu ya Maadhimisho ya Siku ya Kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na Ukame. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa hazina Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora na Bw. Timothy Mande Afisa Misitu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utoaji wa tamko la kuadhimisha siku ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame, mkutano huo umefanyika leo katika ukumbi wa hazina Dodoma

WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR WAELIMISHWA KUHUSU KIPINDUPINDU

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas akifungua mafunzo ya waandishi wa habari  juu ya maradhi ya kipindupindu yaliyoandaliwa na Idara ya Kinga katika Ukumbi wa  RCH Kidongochekundu Mjini Zanzibar.
 Afisa  Afya Juma Mohd Juma akitoa maelezo ya historia ya kipindupindu duniani na hatimae kuingia Zanzibar katika miaka ya 1976 na kurejea kila baada ya kipindi.
 Mwandishi wa habari wa Redio Coconut Tabia Makame akitoa mchango katika mafunzo ya waandishi wa habari ulioandaliwa na Idara ya Kinga na Elimu ya Afya kuhusu maradhi ya kipindupindu.
 Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya Halima Ali Khamis akieleza malengo ya Wizara ya Afya katika kukabiliana na maradhi ya kipindupindu ili kuhakikisha yanaondoka Zanzibar. 
 Daktari dhamana Wilaya ya Mjini Ramadhani Mikidadi Suleiman akieleza dalili za maradhi  ya kipindupindu Zanzibar na dalili zake katika hatua za awali katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa RCH.
 Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Vuai akifunga mafunzo  ya waandishi wa habari kuhusu maradhi ya kipindupindu katika ukumbi wa RCH Kidongochekundu.

KESI YA UHUJUMU CHUMI;KITILYA NA WENZAKE WAPOKEA AWAMU YA KWANZA YA VIELELEZO KUTOKA NCHINI UINGEREZA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umeieleza mahakama kuwa wamepokea awamu ya kwanza ya vielelezo kutoka nchini Uingereza.

Hayo yameelezwa Leo na wakili wa Serikali, Christopher Msigwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Msigwa ameiambia mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wanatarajia awamu ya pili ya vielelezo kuwasili nchini Tanzania wakati wowote kuanzia sasa.

Hata hivyo wakili wa utetezi, Mwanahamisi Adam ameuomba upande wa mashtaka kueleza muda muafaka ambao utatumika kwa vielelezo hivyo kufika nchini.

Aidha Hakimu Mkeha amewaambia upande wa mashtaka huo muda wowote wanaoutaja wahakikishe unaangukia ndani ya siku 14 na ikishindikana basi Juni 30 mwaka huu waeleze vielelezo hivyo vitafika ndani ya siku ngapi.

Miezi miwili iliyopita upande wa mashtaka uliieleza mahakama kuwa upalelezi dhidi ya kesi hiyo uliokuwa unafanywa ndani ya nchi umekamilika na kuwa bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza

Kampuni ya Tigo Yaadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwa kushirikiana na wadau kwenye viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Meneja mauzo na masoko wa taasisi ya Shule Direct Shaweji Steven (kushoto) akimuonesha Meneja Mawasiliano ya Umma kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael (kulia) kifaa cha kusoma vitabu kwa njia ya mtandao kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya sekondari wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam mapema leo.
Mtaalamu wa kutengeneza roboti inayotumika kwa kuchezea watoto,Mkufu Tindi (aliyekaa) akitoa maelezo kwa Meneja Mawasiliano ya Umma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael (katikati) wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam mapema leo.
Meneja Mawasiliano ya Umma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Woinde Shisael akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam mapema leo.
Watoto mbalimbali waliofika kwenye maadhimisho  maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam mapema leo.
Watoto wakiwa katika picha ya pamoja katika  maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam mapema jana.

IJUMAA KAREEM KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. PAUL MAKONDA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amekutana na Masheikh na Viongozi wa Misikitini zaidi ya Mia sita (600) ya Mkoa wa Dar es salaam.

Hatua hii ni muendelezo wa Mikutano yake na Makundi ya watu mbalimbali, ambapo katika kuenzi mwezi wa Mfungo wa Ramadhani.

Mhe Makonda ametoa vitu mbalimbali kama SADAKA KWA KILA KIONGOZI vifuatavyo kwa kila Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam :-
1. Mchele Kg 25
2. Ngano Kg 25
3. Sukari Kg 25
4. Mafuta ya kupikia Lita 20

Akizungumza na Masheikh na  Viongozi wa Dini ya KIISLAMU, Mhe Makonda kwanza amewapongeza kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali pamoja na kumuunga mkono Mhe, Rais, Dot. John Pombe Magufuli kwa jinsi ambavyo anatekeleza utendaji wake wa kazi kwa kuhakikisha anaipeleka Tanzania kwenye nchi ya Uchumi na kipato cha kati kupitia mapinduzi ya VIWANDA.

Mhe Makonda pia, amewaomba viongozi wa Dini kuutumia mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kuhubiri AMANI, UTULIVU NA KUVUMILIANA katika kila mambo wanayofanya waumini wao.

Katika hatua nyingi, Mhe Makonda amefanikiwa KUWASHAWISHI wafanyabiashara haswa wa SUPERMARKET Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi mpaka saa sita za usiku, ili kutoa fursa kwa wananchi kujipatia mahitaji yao muhimu kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
16/06/2017

Mtoto wa miaka sita, darasa la kwanza azindua kitabu katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika

$
0
0
Mtoto Ethan Thedore Yona akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kitabu chake kwa njia ya mtandao(App) kijulikanacho kama Ethan Man, hafla hiyo imefanyika leo kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam.

Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo.
Mtoto Ethan Thedore Yona akitoa maelezo kwa watoto wenzie jinsi ya kutumia App yake ya Ethan Man kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika viwanja vya JKY Park Jijini Dar Es Salaam leo.



JUNI 16, 2017: Dar es Salaam, Tanzania. Katika maadhimisho ya Siku yaMtoto wa Afrika mwaka huu  mtoto mwenye umri wa miaka sita  Ethan Theodore Yona  anayesoma darasa la kwanza  amezindua zana(App) yake ya android  ambayo inaonesha shujaa wa hali ya juu akiwa ni muhusika  anayejulikana kama EthanMan. Mhusika  anaegemea upande wake  ni mwenye kipaji kikubwa, ameandika vitabu vya kuvutia,  kubuni michezo ya kijifunza  na kuwapelekea watoto katika  safari za mafunzo.
 Ethan alianza kujishughulisha na mradi huo  alipokuwa na umri wa miaka mitano katika shule ya awali  ikiwa ni matokeo ya mapenzi yake katika  michezo na kujifunza. “Kila mara nilikuwa na nguvu , kufurahia kujifunza  vitu vipya  na kupenda kucheza michezo mbalimbali. 

Siku moja niliwaambia wazazi wangu  ningependa kuanzisha  mhusika mkuu  jasiri  kwa kuzingatia ubora wangu. Baadaye waliniuliza  ubora huo ni upi  na nikawaambia  mimi ninakipaji kikubwa  na ninaweza kuwa kitu chochote ninachokipenda , naweza kuwa mchezaji soka, nyota wa muziki, mhandisi n.k. Na hivyo ndivyo wazo la mhusika shujaa mkuu  lilivyoanza.”
 
Ethan  alifanya kazi hiyo na mshauri wa  teknolojia ya elimu katika i-LearnEast Africa, na ambayo inatoa kozi kwa njia ya mtandao  na mafunzo ya mabadiliko  kuunda mhusika huyo  na kuanzisha  kitabu chake cha kwanza cha picha  alichokiita “Nitakapokuwa Mkubwa”. Tulivutiwa sana kufanya kazi na Ethan  katika mradi huu. 

Inafurahisha kwamba  mtoto mdogo namna hii  kutaka kufanya jambo hili kubwa tulitaka kuwa sehemu  ya huu mradi tangu mwanzo. Ikiwa ni kampuni ya ushauri katika masuala ya elimu tuliona umuhimu wa kujifunza  ambao mradi huu utawapatia watoto. Mchango wa Ethan katika kuandaa kitabu hiki ni wa kushangaza,” alisema Ofisa Mtendaji wa Learn Tech, Deus Ntukamanzina. 
 
Zana hiyo na michezo  ilianzishwa kwa ushirikiana  na kampuni ya Tujenge Technology  ambayo imejikita katika kuanzisha masuluhisho ya kidijitali  ambayo  yatawezesha  kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii.
 “Tulipoombwa  kuanzisha michezo ya EthanMan  tulifurahi. Kuwa sehemu ya  mradi huu wa kipekee  ndicho kilichotufanya  kuingia katika teknolojia na  kuianzisha. Mchango wetu ilikuwa ni  kuunganisha  mhusika EthanMan na vipaji vyake vingi katika jukwaa ambalo  itakuwa ni rahisi kufikiwa  na kuanzisha  uzoefu mkubwa wa kutumia miongoni mwa watoto. Mchango wa ethan katika kuanzisha michezo ni wa hali ya juu, kwa sababu  kila kitu kimejielekeza katika maisha yake  kama mhusika. Tulikuwa na muda mzuri wa  wa kuunda  kile ambacho tunaamini  kuwa ni bidhaa ya kwanza ya mchezo katika anga ya teknolojia nchini Tanzania.
Zana (App) ya EthnMan  inapatikana kwa kupakua katika hifadhi ya michezo ya android , watoto wataweza kusoma vitabu, kucheza michezo. Na kuwa pamoja na muundaji wa EthanMan, Ethan Theodore Yona.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA DAR

$
0
0
 Watoto wakikimbia walipokuwa wakiandamana kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kinyerezi, ambapo yalifanyika kimkoa wilayani Ilala, Dar es Salaam leo.Maadhimisho hayo yaliongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Maandamano yalielekea kwenye viwanja hivyo
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwashukuru na kuwapatia vyeti wauguzi wa kujitolea  walioshiriki kampeni kupima magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watoto na vijana  wakati wa T
 WATOTO WAKIPIMWA UREFU
 Maandamano
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwasalimia watoto pacha Brighton na Bright Shirima alipokuwa akikagua mabanda ya tiba kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
 Kikundi cha hamasa cha Ilala kikihamasisha wakati wa maadhimisho hayo
 Brass Band ya Polisi ikiongoza maandamano 
 Makamu wa Rais Samia akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akihutubia 

 Kikundi cha ngoma cha Shule ya Msingi Umoja kikitumbuiza kwa ngoma ya kibati wakati wa maadhimisho hayo

 Kikundi cha Umoja kikitumbuiza kwa ngoma ya Makhirikhiri


 Makamu wa Rais, Samia akimkabidhi cheti cha shukrani DkNg'wege aliyekuwa mmoja wa madaktari walioshiriki kupma afya za watoto na vijana wakati wa maadhimisho hayo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akihutubia katika maadhimisho hayo.Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigangwala na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kote nchi kuwafichua watu wanaonyanyasa na kudhalilisha watoto kijinsia ili waweze kukamatwa na kuchukua hatua za kisheria kama hatua ya kukomesha vitendo hivyo ambayo vimeanza kushamiri katika baadhi ya jamii nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kuhitimisha kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ilitoa huduma bure za vipimo na matibabu kwa watoto na vijana zaidi ya 1500 kampeni ambayo iliambatana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika viwanja vya Shule ya msingi Kinyerezi mkoani Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa watenda maovu hao lazima vifichuliwe na wananchi, walezi pamoja na wazazi kwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa watoto wapo miongoni mwa jamii.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola kutofumbua macho vitendo hivyo bali pindi wanapopata taarifa za matukio ya udhalilishaji wa watoto wachukue hatua za haraka za kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki watu wanaofanya vitendo hivyo vibaya.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kote nchini waache kuwaficha watu wanaotendea vitendo hivyo vibaya bali wawapatie taarifa walimu wao na polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa kufanya hivyo watoto watakuwa salama katika mazingira ya nyumbani na wakiwa mashuleni kwani watu wabaya wanaofanya vitendo hivyo watawajibishwa kulingana na matendo maovu waliyokuwa wanawafanyia watoto hao.

“Mtoto anaweza kufaidika na fursa sawa iwapo tu atalindwa kwa kuwezeshwa kuwa afya bora”, Amesisitiza Makamu wa Rais.

Kuhusu kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameendelea kuua watu kwa kasi katika nchi zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.

Amesema ipo haja ya kuimarisha juhudi za kukabiliana na tatizo hilo kwa ushirikiano wa wadau wote kwani janga hilo linagharimu taifa na wananchi wake wakiwemo watu wazima, watoto na vijana.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yasipodhibitiwa yatapunguza uzalishaji mali,ufanisi mahali pa kazi na hata shughuli za ulinzi na usalama nchini mwetu na hivyo pato la taifa litapungua na taifa kuwa watu maskini kutokana na magonjwa hayo”, Alifafanua Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza Serikali imeweza kupanua maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa saratani nchini kwa kujenga jengo jipya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kuongeza majengo mapya ya huduma za saratani kwenye Hospitali za Rufaa ya kanda ya Bugando mkoani Mwanza.

Amesema Serikali pia imejenga Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambayo ni taasisi ya mfano ya kutibu maradhi ya moyo ambapo kutokana na kujengwa kwa taasisi hiyo Serikali imefanikiwa kuokoa mabilioni ya fedha ambayo yangetumika kuwagharamia wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamisi Kingwangala amemhakikishia Makamu wa Raia kuwa Wizara hiyo itaendelea kuweka mipango na mikakati imara ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini.

Dkt Kingwangala ameomba wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kidini na wadau wengine kushirikiana na Wizara ya Afya katika kuongeza kasi ya kukabiliana na magonjwa hayo ili yasiendelee kuteketeza maisha ya watu nchini
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images