Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Wataalamu wasisitiza mazingira safi, lishe bora

$
0
0
 Mratibu wa kampeni ya kitaifa Bw. Anyitike Mwakitalima akizungumza wakati wa mkutano kujadili uhusiano kati ya usafi wa mazingira na lishe bora kwa watoto jijini Dar es Salaam juzi.
 Dkt Generose Mulokozi (kulia) kutoka shirika la IMA World Health akisema ‘Nipo Tayari’ kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira kwa lengo la kuzuia magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu yanayogharimu maisha ya Watanzania.
Mtaalamu wa lishe wa Unicef Mauro Brero akitoa ishara ya kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira yenye kauli mbiu ya Nipo Tayari ikiwa na lengo la kuzuia magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu yanayogharimu maisha ya Watanzania.


.Washirika wa maendeleo nchini wamekutana jijini Dar es Salaam leo kujadili, pamoja na mambo mengine, umuhimu wa usafi wa mazingira katika lishe bora kwa watoto na kuunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira yenye kauli mbiu ya “Nipo Tayari”.

Kampeni hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njisia, Wazee na Watoto imejikita katika kuhamasisha watu, mijini na vijijini, kujenga utamaduni wa kuwa na vyoo na kuvitumia kikamilifu na kunawa mikono na sabuni mara baada ya kutoka chooni.

“Bila kuzingatia usafi wa mazingira, lishe bora kwa mtoto inaweza kuathiriwa na magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu, hivyo kuondoa virutubisho vyote mwilini. Ndio maana usafi wa mazingira na lishe bora kwa watoto ni vitu vinavyotakiwa kwenda pamoja”, anasema Dkt Generose Mulokozi kutoka shirika la IMA World Health.

Akizungumza katika mkutano huo, Mratibu wa kampeni hiyo ya kitaifa Bw. Anyitike Mwakitalima alisema: “Mazingira machafu na ukosefu wa vyoo umethibitika kuwa chanzo kikubwa kinachosababisha kudumaa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. Takwimu zinaonyesha kwamba asilimia 34 ya watoto wa umri huo nchini wamedumaa kutokana na kuishi katika mazingira yasiyokuwa na vyoo na kutozingatia kanuni za afya.

Alisema kuwa ukosefu wa lise bora pia hupunguza kinga ya mwili kwa watoto hivyo kuugua mara kwa mara na kuwafanya kushindwa kukua vizuri kimwili na kiakili.

Utafiti wa afya uliofanywa nchini Tanzania 2015-16 umeonyesha mafanikio ambapo namba ya watoto waliodumaa imepungua hadi asilimia 34 ikilinganishwa na mwaka 1992 wakati nusu ya watoto walikuwa wamedumaa.

Utafiti mwingine uliofanyika nchini hivi karibuni umeonyesha kuwa madhara ya udumavu kwa watoto hauishii utotoni bali huwa na matokeo hasi kwa watu wazima na kuathiri kipato chao kwa asilimia 20. Hii inarudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Inatarajiwa kuwa asilima 75 ya Watanzania watakuwa wanaishi katika mazingira safi ifikapo mwaka 2025 na asilimia 100 mwaka 2030. Mafanikio hayo makumbwa yatafikiwa ikiwa serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu na washirika wa kimaendeleo wa kimataifa kufanikisha mpango huo.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau wa maendeleo kutoka Action against Hunger, Aga Khan Foundation-Tanzania, Catholic Relief Services, Child Investment Fund Foundation, Department for International Development, Doctors with Africa CUAMM, Embassy of Switzerland, Feed the Children na Global Affairs Canada.

Wengine ni Global Alliance for Improved Nutrition, Ifakara Health Institute, IMA World Health, Institute of International Programs Johns Hopkins University, and International Fund for Agricultural Development, International Potato Center, United Nation Children Fund, UN World Food Program, United States Agency for International Development, World Bank, World Health Organization na World Vision International.

TAARIFA KWA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA)




Juni 16, 2017

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatambua kuwa baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini hawajakamilisha miradi kwa mujibu wa MIKATABA waliyosaini na Wakala (REA). Aidha, kuna baadhi ya wakandarasi wamekamilisha miradi lakini hawajakabidhi rasmi miradi hiyo na vifaa au hawajafanya marekebisho kasoro zilizobainishwa na wasimamizi wa miradi kutoka (TANESCO na REA).

Kwa tangazo hili, Wakala unawataarifu wakandarasi wote ambao hawajakamilisha matakwa hayo ya kimikataba kufanya hivyo mara moja. Wakandarasi watakaoshindwa kutimiza masharti hayo hawataruhusiwa kushiriki katika zabuni zitakazotangazwa na Wakala (REA) baada ya TANGAZO hili na hatua nyingine zitachukuliwa juu yao kwa mujibu wa mikataba hiyo.


Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Jengo la Mawasiliano, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma, 14414
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania
Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ATC) NA TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM (DIT) WASAINI MKATABA WA MASHIRIKIANO(MoU)

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(wa tatu kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(wa pili kulia) wakisaini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili. MoU imejikita kwenye ushirikiano wa Utafiti, Taaluma, kubadilishana wataalamu, ziara za kitaaluma kwa wanafunzi.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) wakisaini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha. 
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) wakibadilishana mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha. 
Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(kulia) akizungumza jambo baada ya taasisi hiyo na Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)kuweka saini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha,kushoto ni Dk Richard Massika.

Balozi wa Sweden atembelea Wizara ya Mambo ya Nje

$
0
0
Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga (Kulia)akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Sweden Nchini Mhe. Katarina Rangnitt katika ukumbi wa Wizara Juni 14,2017. Katika mkutano huo walijadiliana masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Sweden pamoja na hali ya usalama nchini Burundi.
Mheshimiwa Waziri Mahiga, Balozi wa Sweden nchini pamoja na Wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika mkutano huo,

NINI UFANYE IKIWA MTU AMEJENGA NA KUZUIA NJIA.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.           

Jirani  yako  au  mtu  mwingine  yeyote  amejenga   na  kuziba  njia. Njia  yoyote iwe  kubwa  kama  barabara  ama  ndogo  ambayo  hata  gari  haiwezi  kupita. Iwe  tu kama  ya   pikipiki  au  baiskeli au hata  ya  miguu  tu.  Yote  haya  hayajalishi  na hizi  zote  ni  njia kwa  mujibu  wa  sheria.

1.HAKI  YA  NJIA  KISHERIA .
Kifungu  cha  151  cha  sheria  namba   sheria  ya  ardhi  ya  mwaka  1999 kinaeleza  haki  hii. Kinaitambua  haki  hii  kwa  kusema  kuwa  haki  ya  njia  ipo  kwa  njia  zile  ambazo  ni  kwa ajili  ya  matumizi  ya  umma.  Umma  hapa  humaanisha  watu  wote  lakini  pia  wakazi  wa  eneo  fulani  wanaotumia  njia  hiyo  kwa  ajili  ya  shughuli  zao  mbalimbali.
Kifungu  kimepanua matumizi  ya  njia  ya  umma  kwa   kumaanisha  hata  njia  zilizotengwa  kwa ajili  ya  makampuni  binafsi. 

Kwa  mfano  kuna  sehemu  ukipita  utaona njia  au  sehemu  ya  lami  ya  barabara imekatwa  maalum  kwa  ajli  ya  kuruhusu watu  au magari  ya  kampuni  fulani  kupata  sehemu  ya  kuingilia.

Lakini  pia  zipo  njia  zimetengwa  kwa  ajili  ya  shughuli  za serikali. Haraka  utaona  kuwa haki  ya njia  haijagusa tu  kule  mitaani  wanakoishi  watu  tu  bali  hata  sehemu  za  makampuni  binafsi  nk.

2.   KUZIBA  NJIA  YA  UMMA.

Kuziba  njia  ya  umma  ni  kosa  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  177( 4 )  cha  sheria  ya  ardhi. Wako  watu  wakorofi  huko  mitaani  huziba  njia  kwa  makusudi.  Yawezekana kabisa  mtu  akiwa  anajua kabisa eneo  fulani  ni  njia  na  watu  hupita  hapo  lakini  kwa makusudi  au bila  kujali  akajenga  ukuta au akaweka uzio  wa  sinyenge  au  akapanda  mti  pale  au  akaweka  kifusi au  kwa  namna  nyingine  yoyote. 

Na  wengine  huambiwa  na  watu  lakini  wasisikie   kwasababu  ya  pesa,  au  urafiki  na  viongozi  wa  serikali  au  cheo  au  rushwa  au  vinginevyo.  Basi  yatupasa  kujua kuwa  watu  hawa  huwa  wakitenda  makosa  na si  wakunyamazia.

Njia  kuzibwa si  lazima  iwe  imezibwa yote.  Hata kuibana na kuitoa  katika  uhalisia  wake  katika  kiwango  chochote  nako  ni  kuziba  njia.  Njia  yafaa  iachwe  vilevile  ilivyo.
          
  KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

WAZIRI MAHIGA APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KWA MWAKILISHI MKAZI WA UNIDO

$
0
0
Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO nchini, Bw.Stephen Bainous Kargbo, Juni 14,2017, katika ukumbi wa Mikutano Wizarani. 
Mhe. Waziri Balozi Augustine Mahiga (Katikati), Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO, Bw. Stephen(Kushoto) Bainous Kargbo na kulia ni Balozi Grace Martin, Mkurugenzi Idara ya Itifaki wakiwa katika mazungumzo.
Mhe. Waziri Balozi Mahiga, Mwakilishi Mkaazi wa UNIDO na Wataalam kutoka Wizarani na Ofisi za UNIDO wakiwa katika picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho..

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akijibu Maswali Bungeni mjini Dodoma Juni 15, 2017. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenya Ulemavu, Jenista Mhagama bungeni mjini Dodoma, Juni 15, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu wa Bunge, Dkt, Thomas Kashililah, Mbunge wa Igunga, Dkt.  Dalaly Kafumu na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja wa Bunge mjini Dodoma Juni 15, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitea na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 15, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mbunge wa Rombo, Joseph Selasini kwenye jengo la Utawala la Bunge Juni 15, 2017.

MADAKTARI WA KICHINA WAJITAMBULISHA NA KUAGA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Kichina wanaotoa huduma katika Hospitali mbali mbali za Unguja na Pemba wakiongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa tatu kulia) katika mazungumzo yao aliwakaribisha Madakatari 21 wapya na kuwaaga 21 waliomaliza muda kutoka  Jamhuri ya Watu wa China katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Ujumbe wa Madaktari wa Kichina unaoongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa pili kushoto) katika mazungumzo yao Rais aliwakaribisha Madakatari 21 wapya na kuwaaga 21 waliomaliza muda kutoka  Jamhuri ya Watu wa China (hawapo pichani) katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo,(kushoto) Kiongozi wa Madakatari waliomaliza muda Xu Zhuoqun.
 Baadhi ya Madakatari wa Kichina waliofika Ikulu Mjini Unguja kuoanana na Rais leo ambapo jumla yao ni  Aroubaini na mbili wakiwemo wapya Ishirini na moja wanaomaliza muda wao wa kazi waliofika kumuaga Rais na Ishirini na Moja walikaribishwa na Rais katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  Ujumbe wa Madaktari wa Kichina unaoongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (wa nne kushoto) baada ya mazungumzo na kuwaaga Madaktari hao waliomaliza muda wao wa kazi hapa Nchini, leo walipofika Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimkaribisha Kiongozi wa Madaktari wapya Ishirini na moja kutoka Jamhuri ya Watu wa China Wang QI baada ya mazunguzo na Madaktari hao waliofika Ikulu Mjini Unguja leo wakiongozwa na Balozi Mdogo wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe.Xie Xiaowu (katikati) Kiongozi wa Madaktari waliomaliza muda Xu Zhuoqun.

WADAU WA JOTOARDHI WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo akifungua warsha ya siku moja ya wadau wa Jotoardhi uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo Juni 15 2017. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogspot) 
Ofisa misitu Mkuu Kitengo cha Nishati Mbadala, Paul Kiwele akiongea wakati wa Warsha ya wadau wa Jotoardhi iliyofanyika Dar es Salaam leo. 
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Kato Kabaka akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya wadau wa Jotoardhi iliyofanyika Dar es Salaam leo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (katikati) akibadilishana mawazo na Meneja Maendeleo wa Biashara pia Mwanajeolojia Mwandamizi wa Kampuni ya GeothermEx, Ann Robertson-Tait baada ya kufungua warsha ya siku moja ya wadau wa Jotoardhi uliofanyika katika Kituo cha mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Kato Kabaka. 
Meneja Maendeleo wa Biashara pia Mwanajeolojia Mwandamizi wa Kampuni ya GeothermEx, Ann Robertson-Tait akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Carbon Counts, Mshauri wa Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi Paul Zakkour (kushoto) na Mshirika wa Kampuni ya Norton Rose Fulbright, Richard Metcalf walipohudhuria warsha hiyo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo akiagana na Mshirika wa Kampuni ya Norton Rose Fulbright, Richard Metcalf. Kutokea (kushoto) ni Kaimu Kamishna wa Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Juma Mkobya. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Olsuswa Energy, Michael Kimei (kushoto) na Mkurugenzi Biashara wa Kampuni hiyo, Raul Bayona (kulia) wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Carbon Counts, Mshauri wa Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi Paul Zakkour walipohudhuria warsha hiyo. 
Mshirika wa Kampuni ya Norton Rose Fulbright, Richard Metcalf akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau wa Jotoardhi huku mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo akimsikiliza kwa makini jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Kato Kabaka 
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali. 
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali. 

Mamlaka ya Mapato ya Tanzania yatumia Tehama kuboresha utoaji wa huduma zake kwa umma

$
0
0
Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku.

CCM YAWATAKA VIONGOZI WALIOTAJWA KATIKA TAARIFA MBILI ZA UCHUNGUZI WA MCHANGA KUTOA USHIRIKIANO KWA VYOMBO VYA DOLA

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi kimewataka viongozi waliotajwa katika taarifa mbili za uchunguzi wa Mchanga wa Madini kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kwa kuwa wamelisababishia Taifa hasara kubwa ya Matrilioni ya Fedha, kutokana na Mchanga wa Madini kwenda nje ya nchi.

Mbali na hilo Chama kimesisitiza kuwa hakitasita kuchukua hatua kwa wanachama wake iwapo watabainika kuliingizia Taifa hasara kupitia Mchanga wa Madini, ila kwa sasa kinaviachia kwanza vyombo vya dola vifanye kazi yake ya kuwahoji waliotajwa kwenye ripoti hizo mbili.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi HAMPHREY POLEPOLE, amesema CCM imetoa pongezi za dhati kwa Rais MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM kwa hatua yake ya uthubutu wa kusimamia raslimali za Taifa.

POLEPOLE amesema katika Histori ya nchi hatua zilizochukuliwa na Rais MAGUFULI hazijawahi kuonekana popote, hivyo inashangaza kuona baadhi ya Wanasiasa wanakejeli hatua hizo za kishujaa zilizochukuliwa na Kiongozi wa nchi.

Pamoja na mambo mengine, POLEPOLE, amesema kilichofanywa na Rais MAGUFULI ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo imeelekeza kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya Wawekezaji katika Migodi ya Madini hapa nchini.

Hata hivyo, CCM kimepongeza hatua za awali zilizooneshwa na Mmliki wa Kampuni ya Acacia kwa kukiri kukosea na kuahaidi kufanya mazungumzo na serikali ili kulipa kiasi cha pesa kinachodaiwa na Tanzania.

TURKISH AIRLINES YAANDAA IFTAR KWA WATEJA WAKE DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Turkish Airlines nchini Tanzania, Ahmet Sahin, akiwakaribisha wageni waliohudhuria Iftar iliyoandaliwa kwa ajili ya wageni na wadau mbalimbali iliyofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakipakua na kupata chakula cha futari iliyoandaliwa na shirika la ndege la Turkish Airlines. Wageni na wadau mbali mbali wakipata Iftar iliyoandaliwa na Shirika la ndege la Turkish Airlines nchini Tanzania iliyofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Wageni waalikwa wakibadirishana mawazo katika hafla hiyo.  Baadhi ya wageni waalikwa wakiongea na Mkurugenzi wa Shirika la ndege la Turkish Airlines Tanzania, Ahmet Sahin.

DC SHINYANGA AFANYA ZIARA KATA YA DIDIA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Alhamis June 15,2017 amefanya ziara katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini na kukagua miradi ya maendeleo. 

Mbali na kutembelea miradi hiyo ambayo mradi wa maji wa visima virefu,zahanati ya Didia na Kituo cha Polisi Didia pia amezungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli kilichopo katika kata ya Didia. 

Matiro alikuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga lakini pia watalaam mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Bakari Kasinyo. 

Tazama picha za matukio yaliyojiri wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa ziara yake leo Alhamis June 15,2017 katika kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya jengo la Kituo cha Polisi Didia ambacho kipo mbioni kukamilika ujenzi wake 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisilikiza maelezo kutoka kwa diwani wa kata ya Didia Luhende Masele ambaye alisema ujenzi wa kituo hicho unalenga kuwasogezea karibu wananchi huduma za kipolisi ili kukabiliana na vitendo vya kihalifu katika mji wa Didia ambao una wafanya biashara wengi 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama akiondoka na msafara wake katika kituo cha polisi Didia kuangalia jinsi ujenzi unavyoendelea 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiwa katika zahanati ya kijiji cha Didia ambayo inaendelea kujengwa 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo (kulia) akielezea jinsi ujenzi wa zahanati ya Didia ulivyokwama kumalizika kutokana na kukosekana kwa pesa 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na msafara wake wakiondoka katika zahanati ya kijiji cha Didia 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia bomba la maji ya kisima kirefu katika kijiji cha Chembeli.Mradi upo katika kijiji cha Didia na Bukumbi lakini kijiji cha Chembeli kimesaidiwa mabomba mawili kwa ajili ya wananchi hata hivyo changamoto ni kwamba bomba linaloleta maji limekuwa likipasuka mara kwa mara hivyo kusababisha kero kwa wananchi 
Hapa ni katika moja ya eneo ambapo bomba la maji limekuwa likipasuka na wananchi kulazimika kulifunga kwa mapira/kamba za kuvutika.Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisikiliza maelezo kwa Mhandisi wa maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba (wa tano kulia) 
Bomba likiwa limefungwa kwa mapira/kamba za kuvutika baada ya kupasuka hivi karibuni 
Mhandisi wa maji wa halmashauri ya Shinyanga Vijijini Sylivester Mpemba akielezea namna inavyotokea bomba la maji lipasuke.Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alimuagiza kufuatilia na kuchukua hatua madhubuti kuhusu tatizo la bomba la maji kupasuka mara kwa mara katika kijiji cha Chembeli 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chembeli ambapo aliwataka kutunza mradi wa maji uliopo katika kijiji hicho sambamba na kuwahamasisha kulima mazao yanayostahili ukame kama vile mtama,uwele badala ya kutegemea mahindi pekee ili kukabilina na njaa 
Wakazi wa kijiji cha Chembeli wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro 
Mkazi wa kijiji cha Chembeli akielezea kero zilizopo katika kijiji hicho 
Mkazi wa kijiji cha Chembeli Maria Tungu akielezea kero ya maji katika kijiji hicho ambapo wanawake wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya maji katika visima na mto unaounganisha kijiji hicho na kijiji jirani cha Buyubi 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Chembeli wakati akielezea kero yake 
Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akizungumza katika kijiji cha Chembeli 
Katibu tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akizungumza katika kijiji cha Chembeli 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasili katika kitongoji cha Danduhu kijiji cha Didia ambapo mkazi wa eneo hilo Mashaka Mayala Komanya amejenga nyumba juu ya mradi wa maji 
Nyumba iliyojengwa juu ya mradi wa maji 


Diwani wa kata ya Didia Luhende Masele akimweleza mkuu wa wilaya hatua walizozichukua kutokana na mwananchi huyo kujenga nyumba juu ya mradi wa maji ya visima virefu uliopo katika kata hiyo ikiwa ni kukubaliana bomba linalopita katika nyumba hiyo lihamishiwe karibu na barabara kwani halipitishi maji kwa sasa.Masele alisema mwenye nyumba hiyo anadai mradi huo ulipitishwa hapo bila yeye kushirikishwa 


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini kuhakikisha taratibu za vikao zinafuatwa kwa kuandika muhtasari wa makubaliano watakayoyafikia ili kupata muafaka kuhusu jengo hilo kujengwa juu ya mradi wa maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji .
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Vijijini Bakari Kasinyo akimpa maelekezo afisa mtendaji wa kijiji cha Didia Shimba Waziri(wa pili kulia) kuhusu nyumba hiyo kujengwa juu ya mradi wa maji. 

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA MAAFISA MIFUGO WA WILAYA NA MIKOA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Maafisa Mifugo wa Mikoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma Juni 15, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aki kukizindua kitabu  cha "Mwongozi wa kitaifa wa Usimamizi wa Huduma za Mifugo" kwenye Mkutano wa Maafisa Mifugo wa Wilaya na Mikoa kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma, Juni15, 2017.(picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi  Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba kitabu  cha "Mwongozi wa kitaifa wa Usimamizi wa Huduma za Mifugo" baada ya kukizindua kwenye Mkutano wa Maafisa Mifugo wa Wilaya na Mikoa kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma, Juni15, 2017.(picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba baada ya kufungua Mkutano wa Maafisa Kilimo wa Wilaya na Mikoa kwenye ukumbi wa Chuo cha mipango  mjini Dodoma Juni 15, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene na Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Tate Ole- Nasha.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Grace Matemu ambaye ni Meneja wa tawi la Benki ya NMB la Bunge wakati alipokwenda katika tawi hilo mjini Dodoma  kupata huduma za kibenki Juni 15, 2017.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA SPORTPESA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ubashiri wa michezo ya SportPesa Bw. Pavel Slavkov (kushoto), katikati ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Bw. Abbas Tarimba.Viongozi hao wa SportPesa walimtembelea Makamu wa Rais Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa SportPesa waliofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa lengo la kujitambulisha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa SportPesa Tanzania. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la kuwa mgeni rasmi katika mchezo kirafiki kati ya Timu ya Everton ya nchini Uingereza na timu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo ilitwaa kombe la michuano ya Sportpesa iliyofayika hapa nchini hivi karibuni.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amekubali ombi hilo baada ya Kukutana na kufanya mazungumzo na Watendaji wa Kampuni inayojishughulisha na ubashiri wa michezo ya Sports Betting nchini ambao waliongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji Tarimba Abbas Ikulu- Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepongeza mipango na mikakati mizuri ya kampuni hiyo ya kutaka kukuza vipaji vya wanamichezo hasa kwa mpira wa miguu kwa Tanzania Bara na Zanzibar na kusema kama malengo hayo yatafikiwa Tanzania itakuwa bora katika mchezo wa mpira wa katika bara la Afrika na Dunia kwa ujumla.

Makamu wa Rais pia amewahakikishia watendaji wa kampuni hiyo kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi na pindi wakiwama katika jambo lolote wawasiliane na ofisi yake ili tatizo linalowakabili liweze kutafutiwa ufumbuzi ili lisikwamishe shughuli za kampuni hiyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sports Betting nchini Tarimba Abbas amemweleza Makamu wa Rais kuwa kampuni hiyo ina malengo makubwa ya kufanya biashara hapa nchini kwa kuzingatia sheria na kanuni za nchini.

Mkurugenzi huyo Tarimba Abbas amesema katika mipango yao wanataka katika kipindi cha miaka Mitatu ijayo kampuni yao iwe ni moja ya kampuni bora nchini katika ulipaji wa kodi kwa Serikali kama wanavyofanya kwa sasa katika Serikali ya Kenya.

Amesema mipango na mikakati waliyonayo kwa sasa ni kuhakikisha wanainua vipaji vya wanamichezo nchini kwa sababu Tanzania Bara na Zanzibar kuna vipaji vingi vya wachezaji wa mpira wa miguu ambavyo haviendelezwi ipasavyo.

Watendaji wa Kampuni hiyo pia wamemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kukubali ombi lao na kuwa Mgeni rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya Timu ya Everton ya nchini Uingereza na timu ya Gor Mahia ya Kenya mchezo ambao unatarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya Sports Betting nchini Tarimba Abbas amesema moja ya lengo la kuileta Timu ya Everton nchini ni pamoja na mambo mengine ni kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii nchini kupitia mchezo huo ambao unatarajiwa kuangaliwa na maelfu ya watazamaji Duniani kote.

Mkurugenzi huyo pia amemweleza Makamu wa Rais kuwa tayari wameshawasiliana na mamlaka inayohusika na masuala ya utalii nchini ili iweze kutumia fursa hiyo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini kama hatua ya kuongeza idadi ya watalii watakaokuja kutembelea vivutio nchini na kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta hiyo.

NAIBU WAZIRI WA AFYA MHE.KIGWANGALLA AZINDUA RIPOTI YA WATOTO LEO MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla akionyesha Ripoti ya Watoto baada ya kuizindua leo Mjini Dodoma.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba Nkinga na Kushoto kwake ni Mwenyekiti Baraza la Watoto Joel Kiyungu.
Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla, Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba Nkinga na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Joel Kiyunga wakionyesha Ripoti ya Watoto baada ya kuzinduliwa leo Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba Nkinga akisoma kipeperushi katika banda la UNICEF  katika kongamano la Watoto,Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla akipata maelezo baada ya kutembelea banda la Plan Internaltional katika kongamano la Watoto,Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto(Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi Sihaba,Mwakilishi mkazi  wa UNICEF Nchini Bi Maniza Zaman na Mkurugenzi  wa Watoto Bi Margareth Mussai katika kongamano la Watoto,Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.
Mkurugenzi  wa Watoto Bi Margareth Mussai akiwa na wabunge wa Viti Maalum Bi Fatma Taufiq, Kiteto Koshuma na Bi.Suzan Lyimo katika kongamano la Watoto,Wazazi/Walezi na Wadau katika kuadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Mkoani Dodoma.
Picha Zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MAWIO

DMF, CBA BANK WASHIKIANA NA MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU, MBAGALA JIJINI DAR

$
0
0
Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Cesilia Meela akiwatoa damu baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbagala, Jijini Dar es salaam wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya Units 106 zilipatikana.
Sehemu ya Wakazi wa eneo la Mbagala Rangi Tatu wakishiriki zoezi la uchangiji damu, llililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana.
Mdau Pina Mshana alikuwa ni mmoja wa waliochangia damu katika zoezi hilo, ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Damu Duniani.

Mmoja wa wachangia Damu akiingalia damu yake wakati akichangia.
Wachangia damu wakiwa kwenye foleni.
Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel akijadiliana jambo na mmoja wa waauguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, wakati wa zoezi la uchangiaji Damu, Mbala Rangi Tatu.


MANISPAA YA KINONDONI YATAKA BILIONI 4 ZILIZOPO KWENYE AKUNTI ZA KATA ZITUMIKE KWENYE MIRADI ILIYOKUSUDIWA

$
0
0

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akizungumza wakati wa kikao cha baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispa hiyo Magomeni jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli aakizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.

Diwani wa Kata ya Magomeni ,Julian Bujugo akichangaia katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kinondoni



Afisa Utumishi wa Manispaa ya Kinondoni, Anna Mwakasyesye akijibu hoja za Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika kikao cha baraza


Sehemu ya Madiwani walioshiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya KINONDONI



Diwani wa Kata ya Kunduchi kwa tiketi ya Chma cha Mapinduzi ,Michael Urio akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo Magomeni jijini Dar es Salaam



Diwani wa kata ya Mwananyamala , Songoro Mnyonge akichangia mada katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo Magomeni jijini Dar es Salaam


Mchumi wa Manispaa ya Kinondoni Eugene Haruna akijibu hoja za madiwani katika kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya KINONDONI


Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi(PMU manispaa ya Kinondoni akijibu hoja za Madiwani wa Manispaa hiyo
Diwani wa kata ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni ,Thadey Massawe akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akijadili jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli katika kikao cha Baraza la Madiwan

Diwani wa Viti Maalum CHADEMA ,Caroline Kazinza akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limeagiza kuhakikisha fedha zote zilizopo katika akaunti za kata zaidi ya Bilioni 4.9 zifanyiwe utaratibu wa manunuzi hili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika kata hizo.

Maazimio hayo yamefikiwa katika baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo lililongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo ,Benjamini Sitta na kumuagiza .

Aidha baraza hilo pia limeridhia maombi ya kamati ya Fedha kwa kutaka kubuni vyanzo vipya fedha vitakavyosaidia Halmashauri hiyo kupta fedha zaidi licha ya baadhi ya vyanzo kuahamia serikali kuu.

pia kikao hicho kilipitisha azimio la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kitendo chake cha kizalendo cha kuhakikisha kuwa fedha za watanzania zilikuwa zinapotea kutokana na mchanga wa Madini uliokuwa ukisafirishwa nje kiholela unapangiwa utaratibu wa kunufaisha Serikali.

RC MASENZA AFUTULISHA ZAIDI YA WATU MIA MBILI (200)

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Iringa bi Amina Masenza akiwa sambamba na katibu tawala wa mkoa wa Iringa bi wamoja Ayoub wakiwa katika viwanja vya Ikulu ndogo wakifurahia jambo baada ya futari ya pamoja wa watu zaidi ya miambili

Baadhi ya watu waliojitokeza kushiriki futari pamoja na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza.


Na Fredy Mgunda, Iringa


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina masenza amefutulisha futari watu zaidi ya mia mbili katika eneo la Ikulu iliyopo kata ya gangilongo kwa lengo kudumisha amani na upendo.

Akizungumza baada ya futari Mkuu wa mkoa masenza aliwataka waumini wote wa dini ya kiislamu na wakristo kuwa makini katika maeneo ya ibada ili kuepukana na kutoka kwa shambilio lolote lile ambalo litasababisha maafa.

"Tumeona nchi nyingine kipindi hiki cha ramadhan kukitokea milipiko mingi ya kujitoa mhanga kwa baadhi ya watu wenye itikadi kali hivyo tunapaswa kuwa makini mno mwezi huu hata miezi mengine yote kwa kudumisha amani yetu"alisema Masenza

Masenza aliwaomba wananchi wote wa mkoa wa Iringa kuwafichua waalifu wanaofanya shughuli hiyo kwa njia yoyote ile ili kuendelea kudumisha tunu tuliyokuwa nayo toka wakati tunapata Uhuru hadi hii Leo.

Aidha Masenza aliwaomba watanzania kuendelea kumuunga mkono na kuombea Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli katika vita hii ya kukuza uchumi kutoka hapa tulipo hadi uchumi wa kati kwa kuwa vita hii sio lelemama.

"Ni kitu kigumu sana unapogusa maslai ya mtu binafsi kwa maslai ya wanyonge huwa inakuwa vita kubwa kupambana nayo lakini Rais wetu mpendwa anafanikiwa hilo hivyo lazima tuwe tunamuombe na kumuunga mkono ili tuendelee kumpa moyo kwenye vita hii" alisema Masenza

Niwaombe wananchi wa mkoa wa Iringa kuwapuuza viongozi wanaopotosha ukweli wa mambo ambayo serikali inayafanya kwa manufaa ya wananchi wa kipato cha chini,kati na wale wenye kipato kikubwa pasipo kumnyang'a au kumdhulumu mtu haki yake.

Katika futari hiyo kulihudhuriwa na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Iringa kama Kilolo iliwakilishwa na mh Asia Abdalah,Mufindi Jamhuri William na wilaya ya Iringa Richard Kasesela.

Lakini mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah aliwataka wananchi na viongozi kutunza amani na kuacha kufanya uharifu kipindi hiki cha ramdhan hata baada ya kuisha ramadhan ili kuendelea kuweka nchi kwenye utulivu uliopo sasa.

"Unakutana na mtu kipindi hiki anajifanya kafunga lakini matendo yake hayaendani ya wakati uliopo lakini kuna wengine saizi wametulia ila ramadhan ikiisha tu anaanza matendo ya uvunjifu wa amani hivyo niwaombe tena na tena wananchi kutunza amani iliyopo "alisema Abdalah

Abdalah alimshukuru mkuu wa mkoa wa Iringa bi Amina masenza kwa futari ambayo imewakutanisha watu mbalimbali kukaa pamoja na kubadilisha mawazo japo kwa muda mchache hivyo kuwaomba wakuu wenzake wa wilaya zote za mkoa wa Iringa kuiga mfano wa mkuu wa mkoa.

Nao baadhi ya viongozi wa dini waliofika eneo la futari walimpongeza mkuu wa mkoa kwa kufutulisha watu mbalimbali ambao imekuwa fursa ya kufanya wabadilishane mawazo ya kujenga tofauti na kila mmoja angefuturu kwake.

"Hili ni jambo jema sana kwa kiongozi wetu wa mkoa maana leo tumekutana na viongozi kutoka dini mbalimbali hata wengine sio viongozi lakini tumebadishana mawazo na hili ni jambo jema kwetu sisi kwa ukweli tumejifunza mambo mengi leo mungu ambariki mheshimiwa mkuu wa mkoa" walisema viongozi wa dini
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images