Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1269 | 1270 | (Page 1271) | 1272 | 1273 | .... | 1898 | newer

  0 0  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka Wakuu wa wilaya kuacha historia katika utendaji wao (legacy) kwenye maeneo wanayoongoza.

  Naibu Waziri Jafo aliyasema hayo mjini Morogoro alipokuwa akifungua semina kwa Wakuu wa wilaya ya kuwajengea uwezo katika usimamizi wa Miradi ya Maendeleo katika sekta ya Kilimo awamu ya pili(ASDPII) itakayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.

  Akifungua semina hiyo, Jafo amewataka wakuu hao washindane katika kufanikisha Mipango ya maendeleo ya serikali ili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Kadhalika, amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kuwapa taarifa za fedha za maendeleo ya miradi hiyo wakati wa utekelezaji ili wakuu hao wa wilaya waweze kufuatilia mwenendo wa utekelezaji wa Miradi hiyo.

  Jafo amesisitiza kwamba katika kipindi cha hichi ambacho kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini sekta ya kilimo ndio inategemewa kuzalisha malighafi za viwandani. Aidha amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia vyema sekta ya Kilimo ili Tanzania licha ya kutegemea mazao ya biashara kwa fedha za kigeni sasa Tanzania ijielekeze pia kuzalisha mazao mengi ya chakula.

  Amesema ukifanyika uzalishaji wa mazao ya chakula na ziada ya mazao hayo kuyauza nje ya nchi yataongeza fedha za kigeni nchini. “Tuna uwezo wa kufanya hivyo kutokana na uwepo wa ardhi ya kutosha yenye rutuba na vyanzo vingi vya Maji,”amesema Jafo

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya.

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa maendeleo pamoja waratibu wa ASDP II wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na Ofisi ya Kilimo.

  0 0


  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi akimkabidhi vitanda 35 Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga ndg Charles Makoga kwa ajili ya kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi wa shule ya Isalavanu iliyopo katika Wilaya ya Mufindi
  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa sambamba n wanafunzi wa shule ya sekondari y Isalavanu pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga
  Na Fredy Mgunda, Mufindi.

  Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi amefanikiwa kutatua tatizo la vitanda katika shule ya sekondari Isalavanu iliyopo Kata ya Isalavanavu kwa kutoa vitanda 35 ikiwa lengo la kuendelea kuboresha na kuinua elimu ya shule hiyo.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi vitanda hivyo alisema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na ziara yake akiyofanya wiki kadhaa zilizopita wakati alipozitembelea shule mbalimbali za jimbo la Mafinga Mjini kujua changamoto na kuanza kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.

  "Niligombea ubunge wa jimbo la Mafinga kwa lengo la kuleta maendeleo ndio maana Leo nipo hapa katika shule ya sekondari ya Isalavanu kuanza kuinua elimu ya shule hii kwa kuboresha miundombinu ya shule na baadae nitatu changamoto nyingine"alisema Chumi

  Chumi aliwataka wanafunzi wa shule ya Isalavanu kusoma kwa bidii ili kuleta matokeo chanya katika jimbo la Mafinga Mjini kwa lengo la kumuongezea kasi ya kutafuta wafadhili wa kusaidia kuleta maendeleo katika jimbo la Mafinga.

  " Kwa kweli najitahidi kutafuta wafadhili wa kusaidia kutatua changamoto za jimbo la Mafinga Mjini lakini wananchi wangu na ninyi wanafunzi mnatakiwa kunipa matokeo chanya na kufanya maendeleo yenu ya mtu moja moja na vikundi pia natamani siku moja kila sekta niwakute watu kutoka jimbo la mafinga Mjini" alisema Chumi

  Aidha Chumi aliwaomba wanafunzi na waalimu kufanya jitihada kuhakikisha wanapata matokeo chanya ili kuitambulisha shule na jimbo la Mafinga Mjini kwa lengo la kuwafanya wananchi na viongozi wa serikali kuangalia shule hiyo kwa jicho la tatu.

  "Mkifanya vizuri kwa kufaulu mitihani ya taifa mtasaidia kuitangaza shule hii na kunifanya Mimi iwe rahisi kutafuta wafadhili kwa kuwa mmefanya vizuri kwenye matokeo ndio maana naomba sana na kusisitiza kuwa naomba mfanye vizuri kwenye matokeo tu kila kitu kita kaa vizuri "alisema Chumi

  Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga aliiomba serikali kuingalia shule hiyo ili kuifanya kuwa moja kati ya shule bora hapa nchini kwa kuboresha miunombinu ya shule ili wanafunzi kusoma bila woga wala hofu pamoja waalimu kufundisha bila kuwa na woga wowote.

  "Jamani mimi naomba kuwa muwazi kwa ukweli mbunge wetu Cosato Chumi anafanya kazi sana kwa kulitetea jimbo hilo hasa ukiangazia jinsi gani anazungumzia sana maendeleo ya wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa kwa ujumla" alisema Makoga

  "Makoga aliwataka wananchi na wanafunzi kudhamini mchango wa mbunge huyo kwa mchango wake katika kuleta matokeo chanya ya jimbo na mkoa wa Iringa kwa ujumla hivyo anapaswa kupewa heshima kwa kazi anayofanya katika maendeleo ya yanayoonekana" alisema makoga

  Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo walimshukuru mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini mh Cosato Chumi kwa kutimiza ahadi yake ya kuwatatulia changamoto ya vitanda katika shule yao.

  0 0

  Napenda kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri Muungano Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kutokana na uzalendo, uthubutu na ujasiri aliouonyesha katika katika kulinda rasilimali zetu zimnufaishe Mtanzania.

  Watanzania tulio wengi tunashindwa mambo kuyafanya kutokana na kukosa ushupavu wa uthubutu katika kuamua kuyafanya mambo. Hakuna jambo lililowahi kufanikiwa bila ya kuwepo kitu uthubutu. Uthubutu ndio mwanzo wa mafanikio ya jambo lolote lile.

  Mwalimu Nyerere alijizatiti akiwa na malengo ya kupigania Uhuru wa Tanganyika wakati akijua fika kuna mkoloni Mwingereza aliyekuwa akitawala lakini alitanguliza mbele uthubutu wa kuweza jambo na hatimaye mnamo Disemba 9, 1961 malengo yake yalitimia.

  Miaka ya 1980's kuliibuka genge kubwa la wahujumu uchumi nchini ambao walificha bidhaa ili waje wazilangue. Kuliibuka mafisadi wa kiuchumi ambao walikuwa na nguvu iliyopitiliza ya kuogopwa lakini akaibuka Ndugu Edward Moringe Sokoine kupambana nao vikali kwa kutanguliza uthubutu kwanza na hatimaye wahujumu uchumi wenyewe wakaanza kutoa mafichoni Mali na bidhaa walizozificha kutokana na kuibuka kiongozi shupavu na jasiri aliyekuwa na uthubutu wa kukabiliana nao.  Hatimaye Sokoine alifanikiwa kushinda vita dhidi yake na wahujumu uchumi.

  Hayo yote ni matokeo ya uthubutu. Leo hii ameibuka kiongozi mwingine Rais Dk. John Pombe Magufuli ambaye ni mfano bora wa kuigwa kutokana na kutanguliza mbele uzalendo na uthubutu wa kupambana na wahujumu rasilimali zetu na yupo tayari kuzilinda.

  Uzalendo wa Rais Magufuli ulianza kwa kuzuia makontena 277 yenye mchanga wa madini yasisafirishwe kwenda nje na kuunda tume mbili ambazo zimetufunua macho juu ya matrilioni ya pesa tuliyokuwa tunaibiwa.

  Watanzania hatukupaswa kabisa kuwa maskini, kukosa madawa hospitalini, kukosa miundombinu bora, kuwa na Kilimo duni huku tukikosa pembejeo, kula mmoja. Watanzania hatukustahili maisha ama maumivu haya.

  Waliotufikisha hapa Rais Magufuli amewafuta kazi, ameagiza walio nje ya madaraka waanze kuhojiwa Mara moja. Na kauli ya Rais inakwenda mbali zaidi ya hapo kwamba hawataishia kuhojiwa tu bali watapandishwa mahakamani.

  Kwa muda mrefu tumekuwa tukilalamika tukiibiwa madini, tumekuwa tukilalamika rasilimali zetu hazitunufaishi Watanzania. Tulikosa kabisa jasiri Mzalendo wa kuanzisha vita hii ya ukombozi wa kiuchumi.

  Naupongeza uzalendo na uthubutu aliouonyesha Rais Magufuli. Sasa ni wajibu wetu kama Taifa kuungana kwa pamoja ili kuziokoa rasilimali zetu zitunufaishe sote na vizazi vyetu.

  Emmanuel John Shilatu
  12/06/2017
  0767488622

  0 0

  Mkuu wa Mifumo ya Mawasiliano PS3 bwana Desderi Wengaa akizungumza mafanikio yaliyopatikana kwa watumishi 10931 wa Halmashauri 93 ambazo zinatekeleza Mradi wa PS3 nchini
  Baadhi ya waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi.
  Baadhi ya waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi
  Baadhi ya watoa mada ambao ni wahasibu kutoka Manispaa ya Lindi na halmashauri ya wilaya ya Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati alipoyafungua mafunzo hayo katika mkoa wa Lindi.
  Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Lucas Mrema akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mjini Lindi.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura wakati akifungua mafunzo ya waratibu elimu kata na waganga wafawidhi kutoka Manispaa na halmashauri ya wilaya ya Lindi.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura akiwa katika picha ya pamoja na waratibu elimu kata na waganga wafawidhi kutoka Manispaa ya wilaya ya Lindi.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura akiwa katika picha ya pamoja na waratibu elimu kata na waganga wafawidhi kutoka halmashauri ya wilaya ya Lindi.

  Mtoa mada wa mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki bwana Hamis Zikatimu akiwaelekeza waratibu elimu kata na waganga wafawidhi kutoka halmashauri za wilaya ya Lindi na Manispaa namna ya kuutumia mfumo huo.

  ……………………………..

  Na Mathew Kwembe, Lindi

  Jumla ya watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa 10,931 kutoka Halmashauri 93 za Mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) wamepewa mafunzo ya uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha katika awamu ya kwanza na ya pili ya mafunzo hayo yaliyofanyika katika mikoa hiyo.

  Mkuu wa Mifumo ya Mawasiliano PS3 bwana Desderi Wengaa ameyasema hayo jana mjini Lindi kabla ya kumalizika kwa awamu ya pili ya mafunzo hayo ambayo yaliwahusisha waratibu wa elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka mikoa 13 iliyo chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

  Bwana Wengaa amefafanua kuwa katika awamu ya kwanza ya mafunzo ambayo yalitolewa kwa wakufunzi waliowafundisha watumishi kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa, jumla ya wakufunzi 2883 walipewa mafunzo hayo kwenye mikoa hiyo.

  Akizungumza kabla ya kuhitimishwa kwa awamu ya pili ya mafunzo hayo yanayoendelea katika mkoa wa Lindi bwana Wengaa amesema kuwa katika awamu ya pili ya mafunzo jumla ya watumishi Mamlaka za Serikali za Mitaa 10,048 kutoka Mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) walifaidika na mafunzo ya uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha.

  Ameongeza kuwa mara baada ya Waratibu wa Elimu kata na Waganga wafawidhi wa vituo vya afya kupewa mafunzo ya aina hiyo, watumishi hao watapaswa kwenda kuwapa mafunzo kama hayo kwa wahasibu katika ngazi ya shule na Zahanati.

  “Lengo ni kuufanya mfumo wetu unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS) uanze kutumika ifikapo julai mosi, 2017 kama Serikali ilivyokusudia,” alisema.

  Alisema kuwa mfumo huo umeundwa kuweza kukidhi changamoto mbalimbali za miundombinu, ikiwemo umeme, na kutokuwa na upatikanaji wa mtandao kwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma katika halmashauri mbalimbali na hivyo mfumo huo hautakuwa tu katika muundo wa kielektroniki, lakini pia kutakuwa na muundo wa kujaza kwenye vitabu.

  “Mfumo wa kujaza katika vitabu na wenyewe umeboreshwa na kuwa rahisi kwa mtumiaji kujaza taarifa sahihi, na huu utatumika kwa vile vituo ambavyo changamoto ya upatikanaji wa miundombinu wezeshi katika matumizi ya kielektroniki,” alisema na kuongeza kuwa mara baada ya kujaza katika vitabu, takwimu hizo zitaingizwa katika mfumo kwenye ngazi ya halmashauri na vituo kupatiwa taarifa ya vituo vyao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi bwana Jomaary Satura aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuhakikisha kuwa wanatumia fursa hiyo kujipatia ujuzi ambao watakwenda kuutumia ili kuwezesha malengo ya serikali kufikiwa.

  Bwana Satura aliongeza kuwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa hawana budi kujifunza kwa bidii mafunzo hayo ili waweze kuandaa taarifa sahihi na kufunga mahesabu yao vizuri.

  “Bila kufanya hivyo halmashauri zitaendelea kupata hati chafu na huku watendaji ake wakiitwa mchwa,” alisema.

  Mfumo huo wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID.

  Mikoa 13 inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ni Mtwara, Lindi, Dodoma, Iringa, Mbeya, Njombe na Morogoro. Mikoa mingine ni Mara, Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Kigoma, na Kagera.

  0 0

  Je unajua jinsi TEHAMA inavyoboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma katika Mkoa wa Iringa hasa Wilaya ya Kilolo na Mufindi. Usikose kuangalia kipindi hiki.

  0 0

  MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata amesema ili kukabiliana na utoro mashuleni pamoja na kusuasua kwa elimu,walimu hawana budi kutafuta namna ya kuwavutia watoto kupenda shule kupitia njia ya michezo.

  Mbunge Mlata alitoa ushawishi huo alipokuwa akiongea na wanafunzi,wazazi na walezi wa watoto wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Vincent iliyopo katika Mji mdogo wa Mitundu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida.

   “Ni lazima walimu mtafute namna ya kuwavutia watoto kupenda shule,kwa mfano michezo mtu mwingine anaweza akaenda shule kwa ajili ya michezo tu anasema shuleni huwa kuna mpira,huwa wanacheza ngoja niende”alifafanua Mlata ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida.

  Kwa mujibu wa Mlata mwanafunzi pindi anapokwenda shuleni kwa lengo la kushiriki katika michezo,inakuwa ni rahisi pia kumpata kwenye masomo darasani.

  Aidha Mbunge huyo aliweka bayana kwamba ili kuhakikisha michezo mashuleni inawezekana kuwepo kwa kipindi chote,alitumia hafla hiyo kukabidhi mipira kumi na jezi pea kumi kwa ajili ya kugawa katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu.

  “Mimi sikuwa najua kwamba mmeongoza mmewafunga wanyiramba sisi wakimbu tumewafunga wale wanyiramba goli 3- 0 kwa hiyo nakuja kuhimiza michezo mashuleni”alibainisha Mbunge huyo mpenda michezo.

  Hata hivyo aliweka bayana kwamba ndiyo maana utoro mashuleni na kusuasua kwa elimu kunakochangiwa na wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo alilazimika kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi kuhakikisha anazisajili shule ambazo bado hazijasajiliwa ili kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali huo mrefu.

  Ni Baadhi ya vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata kwa ajili ya kuhamasisha michezo katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakati wa sherehe za Juma laa Taaluma lililoandaliwa na kata hiyo.(Picha Na Jumbe Ismailly)

  0 0

  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 13, 2016 amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba Jijini Dar es salaam kujionea hali ya Miundombinu ikiwemo majengo ya shule na ufanisi wa utoaji elimu katika Shule hiyo.

  Mara baada ya kuzuru katika Shule hiyo Mkurugenzi Kayombo amebaini kuwapo na ubovu wa madarasa hivyo kuamua kujenga madarasa mengine mapya matano kwa ajili ya wanafunzi kujisomea kwa uhuru na amani shuleni hapo.

  Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba vitano vya madarasa utaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili ya wanafunzi na walimu.

  MD Kayombo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa madarasa hayo yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amesema ujenzi wa madarasa hayo utakuwa wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya ubora wa majengo ya serikali.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza jambo mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (kushoto) na Afisa Uchumi Mkuu Ndg Yamo Wambura wakikagua majengo ya shule ya msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba wakati wa ziara ya kikazi
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua maendeleo ya wanafunzi wa darasa la nne mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayomboakimsikiliza kwa makini Mwalimu Magreth Kapinga mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
  Madarasa manne yaliyoamuliwa kuvunjwa na kujengwa upya madarasa mengine matano katika Shule ya Msingi Hondogo Jijini Dar es salaam
  Mwalimu Happness Mashimba akiwa darasani akifundisha somo la Kiswahili darasa la nne kwa kujitolea kipindi hiki cha likizo kama alivyokutwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifurahia jambo na wanafunzi mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa maelekezo ya kazi mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba

  0 0

  Dar es Salaam, Wateja wa Vodacom Tanzania PLC  ambao ni watumiaji wa huduma ya kifedha ya M-Pesa wameanza kunufaika na gawio la shilingi bilioni 7.9.Gawio hilo limeanza kuwanufaisha jumla ya watumiaji milioni saba wa huduma ya M-Pesa nchi nzima.
  Utoaji wa gawio unaendana na matakwa ya Benki kuu ya Tanzania. Hadi sasa Vodacom tayari imeshatoa jumla ya shilingi bilioni 80 kama gawio ambalo huhifadhiwa kwenye akaunti maalum ya M-Pesa Trust iliyopo kwenye benki za biashara hapa nchini.
  Kabla ya gawio la sasa, jumla ya Tsh  bilioni 72 zilishagawiwa katika awamu tofauti tangu kampuni hii ianze utaratibu wa kutoa gawio Mwezi Disemba 2016. Utoaji wa gawio hufanyika kila baada ya miezi mitatu na gawio la sasa ni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka 2017.
  Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa biashara ya mtandao wa kampuni hiyo,Sitoyo Lopokoiyit alisema “M-Pesa  inamwezesha kila mteja kupata huduma ya kifedha. Tunapojitahidi kumfikia kila Mtanzania, tunaendelea kutoa huduma bora na za kisasa zinazoziwezesha Serikali na biashara kufanya kazi pamoja na huku tukitoa faida nono kwa mawakala na wabia wetu,” alisema
  Mkurugenzi huyo aliwaasa wateja ambao tayari wameanza kunufaika na  gawio hili kutumia fedha hizo kununua Ukarimu bando ili waweze kunufaika zaidi kimawasiliano kwa wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na kufanya malipo ya moja kwa moja kutoka kwenye simu zao wanaponunua bidhaa na huduma mbali mbali na kusititiza kwamba kwa sasa kuna mamia ya wakala wanaopokea malipo kwa njia ya M-Pesa na APP mpya ya M-Pesa imefanya malipo kuwa rahisi zaidi.
  Lopokoiyit alifafanua kuwa, kiasi ambacho mteja anapokea kama gawio hutegemeana na matumizi yake kupitia huduma ya M-Pesa kama kutuma pesa, kununua muda wa maongezi, kulipa huduma na bidhaa pamoja na nyingine. Alisema Vodacom itaendelea na jitihada za kuboresha maisha ya wateja wake kupitia huduma mbali mbali mbali na kuwataka wateja wa Vodacom kuendelea kutumia huduma ya M-Pesa ili waweze kunufaika na mambo mbali mbali ikiwamo gawio.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikutana na wakuu wa mikoa wote katika kikao kilichohudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, baadhi ya mawaziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 13, 2017  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akikaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi wetu uliopo jijini Paris. Mhe Gambo yupo katika ziara ya mafunzo nchini Ufaransa, ambapo pamoja na mafunzo hayo amekua akiutangaza mkoa wa Arusha kama kitovu cha utalii nchini Tanzania. 

  Mhe Gambo, akiwa huko mefanya mazungumzo na Balozi Shelukindo, na kubadilishana mawazo ya namna ya kuvutia wananchi wa nchi hiyo kutembelea Tanzania. 

  Ufaransa ni moja ya zinazoleta watalii wengi nchini Tanzania. Pamoja na mambo mengine  Mhe RC na Balozi wamejadiliana mambo ya Msingi ya kufanya ili kuongeza watalii kutoka Ufaransa kuja Arusha, kupata wawekezaji kutoka Ufaransa kuja Arusha pamoja na namna ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani humo, pamoja na kuanzisha tukio la kimataifa la kutangaza utalii mkoani Arusha kila mwaka.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kukaribishwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo katika ubalozi wetu uliopo jijini Paris.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimvalisha cheo cha Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Nd,Ali Abdalla Ali katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Ali Abdalla Ali kuwa  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kabla alikuwa  Naibu Kamishana.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad  kuwa   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU )  katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeir Ali Maulid ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
  Baadhi ya Makamanda wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU na Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakiwa katika hafla ya kuwapishwa wakuu wao Wapya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika Ukumbi wa wa Ikulu Mjini Unguja leo.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu (kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Said na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri (kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, ni miongoni mwa Viongozi waliohudhurika katika hafla ya kuwapishwa Mkuu wa JKU na Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali  baada ya kuwaapisha rasmi  Kamishana Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Ali Abdalla Ali kuwa (wa nne kushoto) na Kanal Ali Mtumweni Hamad   Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar  JKU  (wa nne kulia)  hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. (Picha na Ikulu)


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Viongozi wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), aliowateua hivi karibuni kuwa Wakuu katika Vikosi hivyo. 

  Katika hafla hiyo, Dk. Shein kabla ya kumuapisha Naibu Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Ali Abdalla Ali, alimfisha cheo cha Ukamishna na baadae kumuapisha kuwa Kamishna wa Chuo cha Mafunzo, Zanzibar.

  Wakati huo huo, Dk. Shein, amemuapisha Kanal Ali Mtumweni Hamad kuwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga Uchumi, Zanzibar (JKU).

  Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za (SMZ), Haji Omar Kheir, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

  Wengine ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud,  Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angeline Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
   Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe.Dk Khamis Kigwangalla  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
   Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akifuatilia jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Suzan Kolimba  hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana  Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Mbunge wa Mtama Mhe.Nape Nnauye  katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
   Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mhe.Fatma Toufiq akiuliza swali katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
  Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mhe.Ritta Kabati akiuliza swali katika kikao cha 46 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 13, 2017.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wanakwaya wa Furahini K.K.K.T Ilongero-Mijuhu Singida  Bungeni Mjini Dodoma.
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kwaya ya Furahini K.K.K.T Ilongero-Mujuhu Singida walipokuja kumtembelea Bungeni mjini Dodoma.

  Picha zote na Daudi Manongi, MAELEZO, DODOMA.

  0 0

   Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo akipokea msaada wa vitanda vya wagonjwa wa kipindupindu kwa Afisa Mkaguzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF) Bi. Francesca Morandini katika kambi ya kipindupindu Chumbuni.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alipotembele kambi ya kipindupindu Chumbuni.

  Picha na Makame Mshenga.

  0 0


  Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imezindua kampeni mpya ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo sambamba na kuzindua utaratibu wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea wateja wa Mtandao huo katika maeneo yote nchi nzima mjini na vijijini.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika soko la Makumbusho lililoko Kinondoni Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mr Nguyen Van Son, amesema tangu kuzinduliwa kwa huduma za kampuni hiyo, wamepata mapokezi mazuri kutoka kwa watanzania ambao hadi sasa zaidi ya wateja milioni tatu na laki tano, tayari wamejiunga na mtandao huo na wanafurahia huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu.

  “Tunafarijika sana kwa namna ambavyo Watanzania wameendelea kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa jamii hii, ni faraja kubwa kwetu kwamba katika kipindi hiki kifupi tumepata mafanikio makubwa na bado tunaendelea kupata wateja wanaojiunga na mtandao wetu siku hadi siku,” Jambo hili linatufanya tusilale tufikilie ni namna gani tunapaswa kuendelea kukizi mahitaji yao.

  “Kuzinduliwa kwa kampeni hii itakuwa ni sehemu ya sisi kusogea karibu na wateja wetu, kuwahudumia pamoja na kuwasikiliza ni nini wanahitaji kutoka kwetu,” Tunaamini kabisa kwamba kuwa karibu na wateja wetu tutajenga mtandao bora kabisa utakao kuwa na huduma zinazolenga maisha halisi ya Watanzania.

  Aidha Naibu Mkurugenzi huyo alitaarifu kuwa, Kampuni hiyo imeanza utaratibu wa kuwa na vifurushi Maalumu kulingana na maeneo na mahitaji ya wateja husika, Huku akitolea mfano wa kuwa na vifurushi maalumu kwa wateja wa Mtandao huo wa Zanzibar ambao wameanzishiwa kifurushi maalumu cha ZANZIBAR YETU, ambacho kwa watumiaji wa Halotel wataweza kuongea bure siku za mwisho wa wiki kwa shilingi 1000 pamoja na vifurushi vingine, Kwa wateja wapya wa mikoa ya Mbeya, Manyara, Pwani, Arusha, Kilimanjaro na Mara, Mkoa huo wanaweza kupata dakika 60 za kupiga simu bure ndani ya mtandao kila wanapoweka muda wa maongezi kwa siku 30 baada ya kusajili . 
   
  Pamoja na Ofa ya Kiboko yao ambayo inapatika katika baadhi ya minara ya 3G ya mtandao huo.Naibu Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa, licha ya kuboresha na kutoa huduma zinazowalenga Watanzania, kampuni hiyo pia imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha Mawasiliano na ubora wa Mtandao huo ambapo hivi karibuni mtandao huo ulitangaza uwekezaji wa zaidi ya bilioni 200 kwa ajiri ya kuboresha ubora wa sauti na kasi ya intaneti, huku wakitarajia kuwekeza zaidi katika mwaka ujao wa fedha. 

  Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka Laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa Mtandao huo, Salim Selemani, ambae amejiunga na Mtandao huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao. Pamoja nae katika picha ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo Frank Mwakyoma na waendesha pikipiki wa kituo cha makumbusho.
  Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka Laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa Mtandao huo, Simon Mkumbo, ambae amejiunga na Mtandao huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao.
  Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son, akitoa maelekezo namna ya kupata huduma za mtandao huo kwa baadhi wa wafanyabiashara wa nguo katika stendi ya Makumbusho mara baada ya kujiunga na mtandao huo, Kampuni hiyo imezindua huduma ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na mtandao huo pamoja na wafanyakazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja wa mtandao huo.
  Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala, kwa pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Nguyen Van Son, wakitoa maelezo juu ya huduma za mtandao huo kwa wafanya biashara wa Matunda wa soko la Makumbuso, Wakati wa uzinduzi wa huduma ya” Switch to Halotel” yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Pamoja na wafanya kazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja. Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Tawi la Dar es Salaam Vu Huy Thiem.
  Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala, kwa pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Nguyen Van Son, wakitoa maelezo juu ya huduma za mtandao huo kwa wafanya biashara wa Matunda wa soko la Makumbuso, Wakati wa uzinduzi wa huduma ya” Switch to Halotel” yenye lengo la kuhamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo, Pamoja na wafanya kazi wa Mtandao huo kutembelea maeneo mbalimbali kutoa huduma kwa wateja. Pamoja nao katika picha ni Mkurugenzi wa Tawi la Dar es Salaam Vu Huy Thiem.
   

  0 0

  Kufuatia michuano ya mpira wa kikapu iliyozinduliwa na makamu wa raisi Mhe. Samia Suluhu Hassan wiki zilizopita, ameonyesha kuunga mkono zoezi hilo la kuwasaka wawakilishi lililofanyika katika mikoa mbalimbali. Sprite inaendelea kuibua hisia zaidi ikizileta pamoja zile timu zilizofuzu katika ngazi ya kimkoa kwenye fainali. 

  Michuano ya kinyang'anyiro hiko yalishaanza toka 12 na tayari baadhi ya timu zilishaanza kuchuana huku kila timu ikiwa na matumaini makubwa ya kuibuka bingwa wa kudunda kikapu kitaifa mwaka 2017.
  Finali hizi zitaendelea kupigwa mkoani Mwanza ndani ya viwanja vya chuo cha Butimba hadi tarehe 14 huku timu zikicheza mfululizo kwa mtoano ambapo bingwa atapatikana. Maandalizi yakiwa yamepamba moto, timu nazo zinaendelea kujinoa huku wachezaji wakijigamba kuwa mafahali katika finali hizo. 

  Mshikemshike huu umewazoa mashabiki mbalimbali wa mpira wa kikapu kutoka Mwanza na wengine kutoka mikoa ya jirani kuja kushuhudia. Finali hizi pia zinasindikizwa na burudani za kukata na shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki ambapo msanii Dogo Janja alitokelezea kuchangamsha mshabiki na pafomansi la kibabe.

  Washiriki wengine wakiwemo wadau wakubwa wa mpira wa kikapu nchini, pia wamejitokeza kushuhudia nani ataibuka kinara.
  Lengo kubwa hasa la mashindano haya ni kuibua vipaji vya vijana katika michezo hususani mpira wa kikapu hapa nchini kuanzaia ngazi za chini hadi kitaifa. Na itakuwa ni fursa nzuri kwa vijana kujumuika pamoja na kuleta hamasa kwa vijana wengine kushiriki katika mchezo huu na hatimaye kuibua wachezaji mabingwa kitaifa hata kimataifa.

  0 0

  Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano (kushoto)akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi mpya ya Benki ya TPB,kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu TPB,Sabasaba Moshingi ,ambapo ofisi hiyo mpya ipo katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya. 
  Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akizindua jiwe la msingi katika benki ya TPB iliyopo eneo la Mwanjelwa. 
  Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindanoakizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la ofisi ya benki ya TPB Mwanjelwa. 
  Afisa Mtendaji Mkuu TPB SabaSaba Moshingi ,kushoto akimkabidhi ripoti ya Mwaka Msajili wa Hazina Dkt Osward Mashindano katika hafla ya uzinduzi wa ofisi mpya ya jengo la Tpb Mwanjelwa jijini Mbeya. 
  Msajili wa Hazina Nchini Dkt ,Osward Mashindano akionesha kadi maalum aliyokabidhiwa na benki ya TPB mara baada ya kuzindua jengo hilo la ofisi eneo la mwanjelwa jijini Mbeya. 
  Meza kuu katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa TPB.   TAASISI za kifedha nchini, zimetakiwa kuboresha mifumo ya utendaji kazi, ili kwenda sambamba na mabadiliko ya ukuaji wa uchumi.

  Kauli hiyo, imetolewa leo na Msajili wa Hazina Dkt .Osward Mashindano, wakati akizindua Ofisi kuu ya Benki ya TPB iliyoko katika eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya.Amesema, wakati uchumi wa dunia unakua ni vema taasisi hizo zikajiimarisha kiutendaji ili kukidhi vigezo vya ushindani wa kibiashara ndani na nje ya nchi.

  “Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta za kifedha nchini zinatoa msukumo unaotakiwa kwenye shughuli za kiuchumi, hivyo ni wakati wenu nanyi kubadili mifumo ya utendaji kazi ili kwenda sambamba na ukuaji huo wa uchumi“,alisema.

  Aidha ametoa wito kwa taasisi za kifedha nchini kuhakikisha inaweka mazingira rafiki kwa wananchi wa kipato cha chini kwa kuweka gharama nafuu za huduma zao ili waweze kuzimudu.Pia, Mashindano ameipongeza benki ya TPB kutokana na na jitihada zake za kupeleka huduma karibu na wananchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mawakala.

  Hata hivyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi, alisema benki hiyo imetoa gawio kwa serikali kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 ambapo hundi hiyo inatarajiwa kukabidhiwa mjini Dodoma.

  0 0

    
   Na Eliphace Marwa – Maelezo.

   Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Jijini Dar es Salaam limetahadharisha, madereva kuwa makini wakati wakiendesha vyombo vya moto ili kuepuka ajali zinazosababishwa na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.

  Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani SACP Fortunatus  Muslimu wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama barabarani katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari mpaka Mei mwaka huu ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka jana.

  Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda Muslimu amesema kuwa ajali za barabarani zimepungua ukilinganisha na mwaka jana kwani katika kipindi cha mwezi Januari mpaka Mei jumla ya ajali za magari zilikuwa 4,177, vifo 1,286 na majeruhi 3,882 ukilinganisha na ajali 2,411, vifo 1,034 na majeruhi 2,291 katika kipindi kama hicho mwaka huu.

  Aidha kwa upande wa ajali za pikipiki Kamanda Muslimu amesema kuwa katika kipindi cha Januari mpaka Mei mwaka jana jumla ya ajali za pikipiki zilikuwa 1,110, vifo 347 na majeruhi 950 ukilinganisha na ajali 607, vifo 302 na majeruhi 455 katika kipindi kama hicho mwaka huu.

  Pamoja na kupungua kwa ajali nchini Kamanda Muslimu amesema kuwa ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na makosa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja mwendokasi wa madereva, kupita magari bila ya tahadhari, ulevi pamoja na kubeba abiria kupita kiasi kwa njia zilizo hatarishi.

  Kamanda Muslimu aliongeza kuwa kwa sasa ukamataji wa makosa ya barabarani yatakuwa kipaumbele, hivyo dereva atakeyekiuka sheria atachukuliwa hatua palepale ili kujenga utii wa sheria bila ya shuruti.

  “Ukamataji wa makosa utakuwa ni moja ya kipimo cha utendaji wa askari barabarani  ili waweze kukamata makosa mengi mpaka pale madereva watakapoacha kukiuka sheria”, alisema Kamanda Muslimu.

  Aidha Kamanda Muslimu amesema kuwa jeshi hilo halitomuonea mtu wala kumbambikia mtu makosa kwani ukamataji huo wa makosa ya barabarani unalenga kuzuia ajali na sio kukusanya mapato na hivyo kuwataka askari kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wafanye kazi kwa nidhamu na maadili ya jeshi hilo.

  Kamanda Muslimu amewataka watumiaji wa barabara kutii sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima ambazo husababisha vifo na majeruhi na kupelekea kuathiri uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla kutokana na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
   Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani SACP Fortunatus  Muslimu 


  0 0

  Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.

  Mkuu wa Kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Bi. Asha Hassan amesema Zanzibar bado ipo nyuma katika kiwango cha Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) cha kuwapatia matone ya Vitamn A watoto wenye umri kuanzia miaka miwili hadi miaka mitano.

  Bi. Asha alieleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kuwapatia matone ya Vitamen A watoto wenye umri huo lililoanza tarehe 1 Juni ambalo linategemea kumalizika mwishoni mwa mwezi huu kwa awamu ya kwanza mwaka huu na awamu ya pili itafanyika mwezi Disemba.

  Alisema Zanzibar hadi hivi sasa imefikia asilimia 82 katika  mpango huo wakati kiwango kilichowekwa na Shirika la Afya  Ulimwenguni ni asilimia 95.Alizitaja Wilaya tatu za Mkoa Mjini Magharibi ndizo zenye asilimia ndogo zaidi chini ya asilimia 70 wakati Wilaya ya Kati inaongoza kwa kuwa na zaidi ya asilimia 95.

  Alisema Kitengo kimeanzisha utaratibu wa kuwafuata wazazi wanaoishi mbali na vituo vya afya ili kuwapatia watoto  matone ya Vitamin A lakini baadhi ya wazazi wamekuwa hawatoi mashirikiano.

  Aliwasisitiza wazazi kufanya juhudi kuhakikisha watoto wao wanapata matone hayo kwa vile ni muhimu katika kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maambukizo ya maradhi ikiwemo kuharisha na kutoona vizuri.Afisa Kitengo cha Lishe Wilaya ya Mjini Fatma Ali Saidi alisema kumekuwa na dhana potofu  kwa wananchi hasa wanaoishi mjini kwamba watoto wao hawahitaji matone ya Vitamin A kwa vile wanakula vizuri lakini dhana hiyo sio sahihi.

  Alisema utafiti uliofanywa na Kitengo hicho unaonyesha kwamba watoto  wenye hali nzuri ya Vitamin A  Zanzibar ni asilimia 12 na asilimia 88 iliyobaki wanaupungufu.Aliwatoa wasi wasi wazazi kuwa hata wale wachache wenye Vitamin A vya kutosha mwilini wanapopewa matone hayo hayana madhara yoyote na wanaweza kutumia. 

  Washiriki wa mkutano huo walikishauri Kitengo cha Lishe kuongeza kutoa elimu kwa wazazi kwani baadhi yao bado hawajaelewa umuhimu wa matone ya Vitamin A na wengine wanadhani kuwa matone hayo ni sawa na chanjo jambo ambalo sio sahihi.                            
   Mkuu wa Kitengo cha Lishe kutoka Wizara ya Afya Asha Hassan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la kuwapatia matone ya Vitamin A watoto wenye umri wa miaka miwili hadi mitano katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
   Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika kazi za vikundi kupanga mikakati ya kuihamasisha jamii kuitikia kampeni ya kuwapatia watoto matone ya Vitamin A katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
   Mwandishi wa habari wa Gazeti la Zanzibar Leo Nasra Manzi akiwasilisha kazi ya kukundi chake katika mkutano wa kuwaelimisha waandishi kuhusu matone ya Vitamin A katika ukumbi wa Malaria Mwanakwerekwe.
  Picha na Makame Mshenga.

  0 0

  MSHINDI wa Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ wa droo ya 13, Amani Kabuku, jana amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa zawadi hiyo ya donge nono itamkomboa kiuchumi, licha ya umri mdogo aliokuwa nao, akiwa na miaka 23 tu.

  Makabidhiano hayo ya Biko na Kabuku ambaye pia anatokea katika familia ya mwanahabari nguri nchini Tanzania, Generali Ulimwengu, yalifanyika katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam, sambamba na kumpatia elimu ya kifedha saa chache kabla ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiza fedha zake alizoshinda katika droo hiyo ya aina yake.

  Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, akiwa katika furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana. 


  Mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 13 ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, katikati akiwa amepakatia fedha zake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyekamilisha mchakato wa kufungua akaunti ya mshindi huyo na kuingiza pesa zake. 

  Akizungumza kwa furaha kubwa, mshindi huyo alisema ndio kwanza amemaliza kidato cha sita na kuibukia kwenye fedha hizo za Biko, hivyo anaamini zitamkomboa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maisha yake yanakuwa mazuri.

  Mshindi wa Sh Milioni 20 katikati Amani Kabuku, akisaidiwa kushika 'maburungutu' yake ya fedha baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.  Alisema amecheza mara nne tu kabla ya kutangazwa mshindi katika droo ya 13 iliyofanyika Jumapili iliyopita, ambapo hata hivyo hakuamini haraka hadi alipowaona baadhi ya wafanyakazi wa Biko walipomfuata nyumbani kwao kwa ajili ya kumhakikishia juu ya ushindi huo.

  “Ni furaha kubwa niliyokuwa nayo kwa sababu naamini huu ni wakati wa kuaga umasikini maana wengi wanatafuta nafasi kama hii ambayo leo Mungu ameniletea mimi ili niweze kutimiza ndoto zangu katika umri niliokuwa nao, hivyo nawashukuru Biko, huku nikiwataka Watanzania wacheze kwa wingi ili nao washinde kama ilivyokuwa mimi,”

  Alisema Kabuku. Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kutumia fursa ya uwapo wa mchezo wa bahati nasibu ya Biko ili washinde zawadi nono kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazotoka kwa ushindi wa papo kwa hapo, ambapo bahati nasibu yao ikichezeshwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.

  “Baada ya kuingiza namba ya kampuni kinachofuata ni kuweka kiasi cha kununua tiketi kuanzia Sh 1000 au zaidi, huku wale wanaocheza mara nyingi wakiwa na nafasi kubwa ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili, ambapo Jumapili hii mshindi mwingine wa Sh Milioni 20 akitarajiwa kupatikana katika droo kubwa,” Alisema Heaven.

  Kwa mwezi Mei pekee, bahati nasibu ya Biko imeweza kutoa jumla ya Sh Milioni 500 kwa washindi wake wa papo kwa hapo pamoja na wale walioibuka na droo kubwa zinazofanyika Jumatano na Jumapili, huku wakiamini kuwa uwapo wa mchezo wao wa kubahatisha ukiwa ni njia ya kukuza uchumi kwa washiriki wao na Watanzania kwa ujumla, huku pia ukiwa ni mchezo rahisi kuliko michezo mingine yoyote inayofanyika nchini Tanzania.

  0 0


older | 1 | .... | 1269 | 1270 | (Page 1271) | 1272 | 1273 | .... | 1898 | newer