Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNE 12,2017

0
0


WANAHARAKATI 42 KATI YA 50 WAFIKA KILELE CHA UHURU,MLIMA KILIMANJARO KWA LENGO LA KUCHANGISHA FEDHA ZA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

0
0
Wanaharakati walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro wakiimba na kucheza wakati wakishuka kutoka Mlima Kilimanjaro.
Timu ya Wanaharakati 86 kutoka taasisi na kampuni mbalimbali walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia mapambano dhidi ya Ukimwi wakishuka kutoka katika kilele cha Uhuru. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akijiandaa Timu ya Wanaharakati wakati wakishuka kutoka kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zara ,Zainabu Ansel (katikati) akiowangoza wanaharakati hao wakati wakishuka katika lango la Mwika. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Herman Kapufi aliyeshiriki Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi.Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira (kulia ) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Rombo ambaye ni kaimu Mkuu wa wilaya ya Moshi,Agnes Hokororo (katikati) na kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi ,Aisha Amour .Baadhi ya Wanaharakati walioshiriki changamoto hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi ,TACAIDS ,Dkt Leonard Maboko akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea wanaharakati hao. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitoa hotuba yake ya kwanza wakati w hafla fupi ya kuwapokea wanaharakati hao. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akipeana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita,Richard Jordnson mara baada ya kutoa hotuba yake. Wawakilishi wa Benki ya NMB,wakiongozwa na Meneja wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi ,Emanuel Kishosha wakifuatilia hafla hiyo ,NMB ni moja kati ya taasisi zilizochangia katika kufanikisha wanaharakati kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya Ukimwi.



Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitoa vyeti kwa wanaharakati 42 kati ya 50 waliopanda na kufanikiwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu ,Richard Jordnson akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo. Mkuu wa wilaya ya Rombo,Agnes Hokororo ambaye pia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Moshi akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya wanaharakati walioshiriki zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi. Kaimu mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Charles Ngendo akizungumza katika hafla hiyo.
Wanaharakati katika changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano ya Ukimwi kupitia kampeni ya Kili Challange inayoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

ARUMERU YANUFAIKA NA MITAMBO YA KISASA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA TAHADHARI

0
0
Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei akizungumza na baadhi ya wanufaika wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari (hawapo pichani) walipotembelea kufanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo Wilayani Arumeru Juni 09, 2017.
Baadhi ya wakazi wa Vijiji vya Mbuguni Wilayani Arumeru wakimsikiliza Mratibu Taifa wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bw.Daniel Alfei (hayupo pichani) wakati wa tathimini ya utekelezaji wa mradi huo iliyofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu 09Juni, 2017.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Mosha akizungumza na wakazi wa Mbuguni Arumeru wakati wa Tathimini ya Utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari iliyofanywa na ofisi yake June, 2017.
Mmoja wa wanufaika wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari Bi. Mariam Daudi (Mkulima) kutoka Kijiji cha Makiba Wilaya ya Arumeru akionesha simu aliyopewa na mradi huo inayosaidia kupokea taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa wakati wa mkutano wa tathimini ya utekelezaji wa mradi eneo la Mbuguni Meru.
Bi. Elizabeth Laiza kutoka Kijiji cha Shambarai Arumeru akieleza faida za mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kwa timu ya tathimini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (haipo pichani).
Fundi Sanifu Mkuu Bonde la Pangani Bw. Vendelin Basso akionesha namna ya kusoma vifaa vya kupima kina cha maji kwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Mosha
Muonekano wa Vifaa vya kisasa vya kupima kina cha maji vilivyofungwa na mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika mto Kikuletwa Kijiji cha Kikwe Meru ambavyo husaidia katika taarifa za utabiri wa hali ya hewa na kuchukua tahadhari ya mafuriko.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru Bw. Christopher Kazeri akizungumza jambo wakati wa mkutano na Timu ya Ukaguzi wa Utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Juni 2017.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

SERENGETI, NGORONGORO NA KILIMANJARO SI VIVUTIO PEKEE VINAVYOPATIKANA TANZANIA

0
0
Na Ripota wetu
Watalii wanaokuja Tanzania na kuelekea moja kwa moja kwenye hifadhi za taifa za Serengeti, Kilimanjaro au Ngorongoro inamaanisha nini? Ni kwamba wanakuwa wamekwishaambiwa kuwa ukifika Tanzania sehemu pekee za kutembelea ni hizo tu? Je tunawezaje kukabiliana na hali hii ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kufifisha vivutio vilivyopo maeneo mengine nchini kutotembelewa?
Hakuna anayeweza kubisha kwamba sehemu ya Kaskazini mwa Tanzania imebarikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na vivutio visivyopatikana duniani kote. Vivutio kama hifadhi za kitaifa za Serengeti, bonge la Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro na hivi karibuni mti mrefu zaidi barani Afrika uligunduliwa.

Tunapenda kukufahamisha kwamba tangu mwaka huu wa 2017 uanze nchi yetu imeshuhudia watu mbalimbali maarufu duniani wakifurika nyanda za Kaskazini wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu wa Israel, Bw. Ehud Barak, muigizaji wa filamu kutokea Hollywood nchini Marekani, Will Smith na familia yake.

Kama hiyo haitoshi hazijapita hata wiki mbili tangu aliyekuwa nguli wa kusakata kabumbu nchini Uigereza, David Beckham ambaye aliwahi kuvichezea vilabu vya Manchester United, Real Madrid, LA Galaxy na PSG naye kutembelea hifadhi ya mbuga ya Serengeti akiwa na familia yake.

Huyo hakuwa mchezeji pekee kutokea bara la Ulaya kufanya hivyo kwani nyota anayechezea kwa mkopo katika klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza akitokea Liverpool, Mamadou Sakho naye pamoja na mkewe na watoto wake wa kike wawili wameonekana wakifurahi mapumziko yao katika hifadhi ya mbuga ya wanyama ya Serengeti.
Jambo la msingi la kujiuliza hapa ni kwanini watu hao wote mashuhuri pindi tu watuapo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Nyerere hubadilisha ndege na kuelekea moja kwa moja uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ambapo kutokea pale ni rahisi kwenda hifadhi za kitaifa za Serengeti, Ngorongoro na Mlima Kilimanjaro?

Tunafahamu kwamba suala la watalii kutembelea sehemu wanazozitaka wanapofika nchini Tanzania ni maamuzi yao na pia huchangiwa na sababu kadhaa kama vile vivutio miundombinu kama vile usafiri, hoteli zenye hadhi na kuvutia lakini pia na hali ya hewa kinaweza kuwa kigezo kingine.

Kwa kuzingatia sababu za miundombinu na huduma bora za malazi na zenye viwango vya kimataifa, hakuna ubishi kwamba nyanda za Kaskazini zimejitahidi kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watalii. Lakini linapokuja suala la vivutio vya kitalii na hali ya hewa bado Tanzania tumejaaliwa vivutio vya kila aina na hali ya hewa nzuri karibuni kila mikoa ya nchi hii.

Kwa mfano, ukitembelea mikoa ya Magharibi utakutana hifadhi za Gombe, Katavi, Mahale, Rubondo na Saanane. Kwa ukanda wa Mashariki kuna fukwe safi za bahari ya Hindi, visiwa vya Zanzibara, hifadhi ya Saadani, kisiwa cha Kilwa, mapango ya Amboni (Tanga) na Mikindani (Mtwara). Wakati ukienda Kusini mwa Tanzania yapo mengi ya kufurahi na kuyaona katika hifadhi za Kitulo, Mikumi, Ruaha na Udzungwa.
Utajiri wa maliasili unaopatikana katika hifadhi hizo hapo juu ni Dhahiri kwamba nchi ya Tanzania haijabarikiwa sehemu chache pekee. Bali tu ni namna tunavyovitangaza, kuvitolea elimu ya kutosha na kuvipa kipaumbele kwa wageni na watalii kuvitembelea.

Yapo mambo kadhaa ya kujifunza kutokana na ugeni wa watu hao mashuhuri kupendelea kuzuru baadhi ya sehemu tu nchini.

Kwanza kabisa, kuwa na vivutio pekee haitoshi kuwashawishi watalii kuja nchini kuvitembelea bila ya kuvitangaza. Dunia kwa sasa ina takribani zaidi ya nchi 190 na zote hizo zikiwa na vivutio vya kila namna. Watalii hawawezi kutembelea sehemu kama hawajafahamishwa ina mambo gani yatakayowavutia na kushawishika kutoka huko walipo. Hivyo basi badala ya kutegemea watalii na watu mbalimbali kusikia sifa za vivutio tulivyonavyo Tanzania kutoka kwa watu wao wa karibu, serikali na wananchi tunaowajibu wa kuvitangaza vivutio vyetu.
Lakini pia, sekta ya utalii kwa kiasi kikubwa huendena na uwepo wa miundombinu ya kisasa na ya kuvutia itakayowawezesha watalii kuvifikia vivutio na kufarahia muda wao pindi wanapokuwepo huko. Hapa tunazungumzia miundombinu kama vile usafiri na huduma za malazi kitu ambacho mikoa ya Kaskazini imejitahidi kuwekeza kwa kiasi kikubwa. Uwepo wa uwanja wa ndege kimataifa wa Kilimanjaro, barabara na hoteli kadhaa zenye hadhi na viwango vya kimataifa ni vichocheo vikubwa kwa watalii kupenda kutembelea vivutio vya huko.

Hivyo basi kwa kumalizia, bado serikali na wananchi kwa ujumla tunalo jukumu la kuvitangaza na kuvilinda vivutio tulivyonavyo. Kwa kuvitangaza tunaweza kulifanikisha hilo kwa kuvitembelea na kuwajulisha watu wetu wa karibu juu ya mambo yanayopatikana huko. Pongezi kwa serikali kwani siku chache zilizopita katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani ilitoa ofa kwa watanzania wote kutembelea hifadhi za mbuga za wanyama bila ya kiingilio chochote kwa siku tatu mfululizo ili kujionea mazingira na maliasili tulizojaaliwa.

Mbio za mwenge wa uhuru zazindua ujenzi wa kiwanja cha Philip Morris Tanzania mjini Morogoro.

0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania Ltd Dagmara Piasecka akipokea mbio za mwenge wa Uhuru baada ya kuzindua ujenzi wa kiwanda mjini Morogoro Jumamosi .
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro. Ujenzi wa kiwanda hicho ambao utagharimu zaidi ya 60bn/- utawaongezea faida wakulima wa zao la tumbaku hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka.


Philip Morris Tanzania yazindua ujenzi wa kiwanda Morogoro

Morogoro Jumamosi 10 Juni 2017…..Wakulima wa zao la tumbaku nchini wanatarajia kufaika na ulimaji wa zao hilo baada ya kampuni yaPhilp Morris Tanzania Limited kuwekeza zaid ya Sh. Bilioni 60 kwenye ujenzi wa kiwanda kipya, eneo la Kingolwira katika Halmashauri ya Morogoro mjini.

Kampuni ya Philip Morris ambayo imekuwa ni mnunuzi mkubwa zaid wa tumbaku inayolimwa zaidi hapa nchini ikiwa inanunua zaidi ya asilimia 40, inatarajiwa kuongeza ununuzi wake baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda.

Akiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho, kiongozi wa kitaifa wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema amefurahisha na uamuzi wa kampuni ya Philip Morris Tanzania kuamua kujenge kiwanda hapa nchini kwani mbali na kuongeza ununuzi wa zao la tumbaku na kuongeza kipato kwa wakulima wetu, lakini pia kitatoa ajira kwa watanzania na pia kuongeza na kukuza uchumi wa taifa.

‘Nimepata taarifa kuwa kampuni hii imekuwa ndio inaongoza kwa kununua tumbaku ya Tanzania na sasa mmeamua kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Nawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambapo kauli mbiu yake ni Tanzania ya viwanda. 
Lakini pia serikali imekuwa kwa muda mrefu ikitaka makampuni kuwekeza kwenye viwada na hasa vya mazao ya kilimo kwa kunaongeza thamani ya mazao yetu na kuongeza kipato kwa wakulima wetu,’ alisema Amour huku akiongeza kuwa makampuni mingine yanayonunua bidhaa za mkulima ni muhimu wakawekeza kwenye viwanda ili kupata bidhaa za mwisho zinazotengenezwa hapa nchi.

Serikali imekuwa msitari wa mbele kuunga juhudi zozote za kuinua kipato cha wakulima wetu. Hii imejidhiirisha baada ya budget ya mwaka kufuta baadhi ya kodi ambazo zimekuwa ni changamoto kwa wakulima. Hii yote inaonyesha ni jinsi ngani tumekuwa msitari wa mbele kukuza sekta hii kwa vyovyote mwekezaji yeyote inakuja na kuwekeza kwenye kilimo ni wa kupongezwa, aliongeza Amour.

Nawapa changamoto wakulima wetu wa tumbaku kuongeza bidii ya kulima zao hilo kwani mnunuzi mkubwa wa zao lao kwa sasa ameamua kuja na kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Hii ni faida kwa upande wao. 
Aliongeza Amour huku akitoa rai kwa wafanyikazi ambao watapata ajira kwenye kiwanda hicho cha Philip Morris Tanzania kufanya kazi kwa bidii kwani kutakuwa ni chachu ya kuvuta wawekezaji zaidi.’Uwekezaji kama huu ni taji kwa wasomi wetu kwani kunapanua ajira hapa nchini lakini nawaomba Watanzania ambao watapata hiyo fursa kuheshimu kanuni za ajira na kuwa na uhusiano mwema na wawekezaji kwani kiwanda kikifanya kazi zake kwa faida wafanyakazi pia nao watanufaika, alisema Amour.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano Philip Morris Tanzania Evans Mlelwa amesema uamuzi wa kampuni yake kuamua kujenga kiwanda hapa nchini kunatokana na mazingira mazuri ya biashara, amani na utulivu, kiwango cha ukuaji wa uchumi pamoja na sera nzuri ya viwanda hapa nchini Tanzania.

‘Manufaa ya kiwanda hiki ni katika kuongeza mapato yatokanayo na na kodi kwa serikali, kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na pia kuongeza kwa ulimaji wa zao la tumbaku na kutoa ajira katika nyanja mbali mbali kama uzalishaji na usambazaji, alisema Mlelwa huku akiongeza kuwa kampuni yake itajikita zaidi kwenye huduma za jamii kama elimu na kuhahakisha Wananchi wanaozunguka kiwanda wanapata maji salama kwa matumizi ya nyumbani.

‘Wanawake wamekuwa wakisahaulika sana. Sisi tuna mpango mzuri wa kuwawezesha na kuwainua kichumi na ndio maana nasema kiwanda kiwanda hiki kitakapokamililika kitakuwa na manufaa mengi kwa Wananchi wetu, alisema Mlelwa.

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 45, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 12, 2017

0
0
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Joyce Ndalichako akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe. Eng Stella Manyanya akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Mbunge wa Mbinga Mjini(CCM) Mhe. Sixtus Mapunda akiuliza swali katika kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dk Susan Kolimba  katika kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Mbunge wa Kalenga (CCM) Mhe. Godfrey Mgimwa  akiuliza swali katika kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Mbunge wa Mwibara (CCM) Mhe. Kangi Lugola akiuliza swali katika kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mhe. Asha Juma akiuliza swali katika kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Makazi katika kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Holy Trinity English Medium kutoka Mkoani Dodoma wakiwa Bungeni kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali katika kikao cha 45 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 12, 2017.

Picha zote na Daudi Manongi, MAELEZO, DODOMA.

ISOME TAARIFA YA KAMATI YA PILI YA MAKINIKIA 12 Juni, 2017

0
0

Barclays Bank Tanzania hosts an Iftar dinner for its customers in Dar

0
0
 Barclays Bank Tanzania Acting Board Chairman, Simon Mponji (right), with some invited guests during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam at the weekend.
 Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left) talking to former Barclays MD, Rished Bade (centre) during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam at the weekend. Looking on is BBT Acting Board Chairman, Simon Mponji.
 Barclays Bank Marketing and Communications Manager, Joe Bendera (left), welcomes Sheikh Said Mpeta from the National Muslim Council of Tanzania (BAKWATA) at an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam. BBT Citizenship Manager, Hellen Siria looks on.
  Some invited guests breaking the fast at an occasion hosted by Barclays Bank Tanzania in Dar es Salaam.
 Barclays Bank Tanzania Retail and Business Banking Director,  Kumaran Pather (second right), exchanging views with some guests during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam recently.
Barclays Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed (left), with some invited guests during an iftar hosted by the bank to its customers in Dar es Salaam. On his left are; former MD, Rished Bade, Acting Board Chairman, Simon Mponji, Retail and Business Banking Director, Kumaran Pather and CEO’s Roundtable Chairman, Ali Mufuruki.

UNESCO organize 3 day symposium to address gender gap in STEM subjects

0
0
Girls and women face multiple challenges that compromise their education opportunities. One area of longstanding concern is the low rate of female participation in science, technology, engineering and mathematics (STEM) education and consequently STEM careers. This is a major concern, as STEM careers are often called ‘jobs of the future,’ driving social and personal well-being, inclusive growth and sustainable development, through innovation and creativity.

Why does this gender gap exist and how can it be addressed? The UNESCO International Symposium and Policy Forum will be organized over three days, serving as a platform for debate and hands-on learning, seeking to: 

Present latest findings from research and practice 
Facilitate policy dialogue, experience-sharing and networking
Make the case for strengthening girls’ education in STEM subjects

The programme will be based on the overarching theme of girls’ education in STEM, with four sub-themes/tracks:

 Building the foundations: Gender-responsive quality STEM education
Changing the equation: Addressing stereotypes and bias hindering girls’ participation
Gravitating into the field: Reaching out, engaging and empowering girls and women
Wiring the network: Partnerships, cross-sector learning and cooperation

This event will bring together over 200 delegates including: the Ministry of education and other officials; education practitioners and educators; researchers and experts; representatives of intergovernmental and non-governmental organizations; development partners; civil society representatives; private sector stakeholders and others.

INTERESTED IN JOINING?
Participation will be by invitation only. Interested participants can register, submit a proposal for a presentation or a workshop, or reserve an exhibition booth online before 19 June 2017. To ensure a balanced audience, all requests will be evaluated based on profile, gender and geographical representation. 
Submit a request to reserve an exhibition booth (link is external)

30 Kufanyiwa Upasuaji wa Mtoto wa Jicho Muhimbili

0
0
Timu ya  Madaktari kutoka nchini Japan kwa kushirikiana na watalaam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na MUHAS wanatarajia kuwafanyia upasuaji wagojwa 30 wenye matatizo ya mtoto wa jicho.

Akipokea msaada wa kifaa cha utakasaji (Sterilizing instruments ) pamoja na vifaa mbalimbali vitakavyotumika wakati wa upasuaji huo (Consumables) kutoka kwa timu ya wataalam wa afya wa nchini Japan, Mkuruenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru amesema zoezi hilo la upasuaji litafanyika kesho na keshokutwa .

‘’Tumekua na ushirikiano mzuri na wataalam hawa  kwa muda wa miaka 12 sasa na niamini ushirikiano huu utaendelea, lakini pia  uwepo wa Madaktari  hawa utusaidia kuwajengea uwezo watalaam wetu hapa Muhimbili,” . Amesema Profesa Museru.

Profesa Museru amesema msaada huo umekuja wakati muafaka ambapo MNH ina mahitaji ya vifaa mbalimbali  vya  vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia  wagonjwa .

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na MNH katika kuboresha huduma za afya na kudumisha ushirikinao huo wa kihistoria.
 Mkurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (wa tatu kutoka kushoto) akipokea kifaa cha sterilizing kutoka kwa Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida (kulia).  Kutoka Kushosho ni Mkuu wa Idara ya Macho Muhimbili, Dk Mtemi Baruani na Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Muhimbili, Dk Julieth Magandi. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Yamasaki Eye, Dk Takashi Yamasaki na Kenji Takeuchi wa Take Opht Medical Corporatio. Kifaa hicho kitatumika wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya macho.
 Mkurungezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akimshukuru Balozi wa Japan, Masaharu Yoshida baada ya kuupokea Leo.
 Mmoja wa wataalamu wa Afya kutoka Japan, Chika Yoshinda akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kifaa hicho, jinsi ya kikutumia na kukitunza.
 Baadhi ya wataalamu wa afya kutoka Muhimbili na Serikali ya Japan wakimsikiliza, Chika Yoshinda.

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA PILI YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA MADINI YALIYO KWENYE MAKONTENA YENYE MCHANGA UNAOSAFIRISHWA NJE YA NCHI

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini wakati ikifunguliwa kwenye kabrasha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli  mara baada ya kumkabidhi Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hiyo ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai, Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma wakati wa Wimbo wa Taifa ukipigwa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai, Kaimu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi, Mwenyekiti wa kamati ya pili ya Madini Propfesa Nehemiah Osoro pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo waliojumuika na viongozi wa Dini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifatilia kwa makini Ripoti ya pili ya Kamati ya Madini Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Castle Lite Unlocks Vanessa Mdee atapanda jukwaa moja na Cassper Nyovest, Diamond na Future trh 22/Julai/2017

0
0
Meneja Masoko wa Bia laini Afrika Mashariki, Amou Majok (kushoto) akiwa pamoja naVanessa Mdee juzi jijini Dar, wakati Meneja huyo akitangaza kuhusu msanii huyo kushiriki katika tamasha la Castle Lite Unlocks litakalofanyika mwezi Julai. Kulia ni Meneja Msaidizi wa Chapa ya Bia laini, Isaria Kilewo.

Vanessa Mdee  akizungumza jambo  Meneja Msaidizi wa Chapa ya Bia laini, Isaria Kilewo mapemamwishoni wa wiki iliyopita jijini Dar wa kutangaza kuhusu msanii huyo kushiriki katika tamasha la Castle Lite Unlocks litakalofanyika mwezi Julai.
Vanesa Mdee  akikata keki 


Vanessa Mdee akifurahi jambo wakati wa kutangazwa kuungana na wasanii wengine katika tamasha la Castle Lite Unlocks litakalofanyika mwezi Julai.

WAKAZI WA MANISPAA YA UBUNGO WAMPONGEZA JPM KWA MAAMUZI MAGUMU KWA MANUFAA YA WATANZANIA

0
0
Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli

Wakazi wa Mitaa tofauti tofauti katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam ukiwemo Mtaa wa kimara, Ubungo, Sinza, Mabibo, Mwembechai na Magomeni wamempongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli kwa kuunga mkono maoni/Mapendekezo ya Ripoti ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena zaidi 250 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli ameunga mkono ripoti hiyo kutokana na ukiukwaji wa sheria za nchi na upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali kupitia biashara ya Makinikia na madini yanayosafirishwa nje ya nchi.

Wananchi hao wamesifu uwepo wa Rais Magufuli huku wakieleza kuwa Tanzania imefanikiwa kupata kiongozi imara na madhubuti atakayeweza kuifanya Tanzania kuwa ya neema na mafanuikio makubwa.

Mapendekezo hayo ya kamati maalumu yaliyoungwa mkono na Rais Magufuli ni ishirini na moja kama ifuatavyo

1. Serikali, kupitia Msajili wa Makampuni ichukue hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Acacia Mining Plc ambayo imekuwa inaendesha shughuli zake nchini kinyume na matakwa ya Sheria.
2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni yote ya madini ambayo yamekwepa kulipa kodi na mrahaba stahiki kwa mujibu wa sheria.

3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi mpaka hapo makampuni ya madini yanayodaiwa yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki kwa mujibu wa sheria.
4. Serikali ianzishe utaratibu utakowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia (smelter) ili kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira kwa watanzania.

5. Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini na kuongeza muda wa leseni, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini, makampuni yaliyohusika kuandaa nyaraka za usafirishaji wa makinikia(Freight Forwarders(T)Ltd na makampuni ya upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchina upotoshaji.

6. Serikali ifute utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba ya asilimia 90 na kusubiri malipo ya asilimia 10 kulipwa baadaye wakati makampuni hayo ya madini huyauza madini hayo na kupewa fedha taslimu kwa mkupuo.

7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa Watumishi wa idara ya walipakodi wakubwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kushughulikia madai ya kodi ambayo Mabaraza ya Rufaani ya Kodi na Mahakama zimekwisha yatolea uamuzi na vilevile ichunguze mienendo ya watumishi wa mabaraza ya Kodi kwa kutotolea maamuzi ya kesi za kodi kwa muda mrefu kuhusu mashauri yaliyochukua muda mrefu kukamilika katika vyombo hivyo.

8. Benki Kuu ya Tanzania ifuatilie malipo ya fedha za kigeni yanayotokana na mrahaba kwa mauzo ya madini.

9. Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya migodi na viwanja ndege vilivyopo vigodini ili kudhibiti vitendo vya hujuma vinavyoweza kuwa vinafanywa na makampuni ya migodi ikiwemo utoroshaji wa madini.

10. Sheria iongeze kiwango cha adhabu zilizoainishwa kwa makosa ya ukiukwaji wa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi.

11. Serikali kupitia wataalum wabobezi katika majadiliano na mikataba (expert in negotiation and contract) wapitie mikataba yote mikubwa ya uchimbaji madini ipitiwe (review) na kufanya majadiliano na makampuni ya madini ili kuondoa misamaha yote ya kodi isiyokuwa na tija kwa taifa na badala yake kuweka masharti yenye tija kwa pande zote mbili kwa kuzingatia maslahi ya nchi;

12. Sheria iweke kiwango maalum cha asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na Serikali katika makampuni yote ya madini nchini. Aidha, Sheria ielekeze Serikali kufanya majadilaino ili kuwezesha Serikali kununua hisa katika makampuni ya uchimbaji madini ili kuiwezesha kupata mapato zaidi na ushiriki katika maamuzi muhimu katika biashara ya madini.

13. Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara ya usafirishajibidhaa nje ya nchi kupitia bandari kama ilivyokuwa kama lilivyokuwa shirika la NASACO ili kudhibiti biashara haramu na kuondoa mianya ya ukwepaji kodi.

14. Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali asili ya watanzania na iwekwe chini ya udhamini na uangalizi wa Rais kwa manufaa ya watanzania.

15. Sheria itamke bayana kuwa mikataba yoyote ya uchimbaji mkubwa wa madini (Mining Development Agreement) isiwe ya siri na lazima yaridhiwe na Bunge kabla ya kuanza kutekelezwa.

16. Sheria itoe masharti ya wazi ya kuzingatiwana iondoe uhuru wa mamlaka ya (discretionary powers) za Waziri wa Nishati na Madini, kamishna wa madini na maafisa madini wakanda katika utoaji wa leseni za uchimbaji madini.

17. Sheria ya madini iweka masharti kwamba mwombaji wa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini lazima yaoneshe mchanganuo wa kina kuhusu namna mafunzo kwawazawa yatakavyotolewa kwa lengo la ajiri kama wataalam na kuchukua nafasi za uendeshaji wa migodi husika na kupunguza au kuondoa kabisa wataalam kutoka nje ya nchi.

18. Sheria ielekeze makampuni ya madini kuweka fedha zinazotokana na mauzo ya madini katika benki zilizopo nchini ili kuimarisha uchumi wa nchi na kuondoa mianya ya ukwepaji wa kodi na tozo mbalimbali.

19. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au kufuta na kubadili kabisa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi ili kuondoapamoja mambo mengine masharti yote yasikuwa na manufaa kwa taifa ikiwa ni pamoja na masharti yaliyomo kwenye kifungu thabiti (stability provision).

20. Serikali igharimie nakutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali ili kuwapatia uelewa na weledi katika nyanja ya majadiliano na uendeshaji wa mashauri yatokanayo na mikataba ikiwemo ya mikataba ya madini (skills in negotiation and arbitration).

21. Serikali kupitia Kamishna wa Madini iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kaw makampuni ya madini ili kujihakikishia uzingatia au ukiukwaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji na kuchukua hatua ipasavyo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

SPIKA WA BUNGE AFIKA UBALOZI WA IRAN KUTOA POLE KUFUATIA SHAMBULIO LA KIGAIDI KATIKA BUNGE LA NCHI HIYO.

0
0
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang alipokwenda kumpa pole kufuatia shambuliyo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Iran kufuatia shambulizo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6. Kushoto ni Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akizungumza na Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang alipokwenda kumpa pole kufuatia shambulizo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Mhe. Dotto Biteko ambaye aliambatana na Mhe Spika na kushoto ni Mkalimani wa Balozi huyo.
Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akiagana na Balozi wa Iran hapa nchini Mousa Farhang mara baada ya kumpa pole kufuatia shambulizo la Kigaidi katika Bunge la nchi hiyo ambapo watu 12 waliuwawa wakimeo Wabunge 6.



(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI BAADA YA KUPOKEA RIPOTI YA KAMATI YA PILI YA MADINI JUNE 12, 2017

0
0

WAZIRI UMMY MWALIMU AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI TANZANIA

0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akutana na balozi mdogo wa marekani Inmi Patterson (Wa pili kutoka Kushoto) katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam mapema asubuhi. Barozi Inmi Patterson ameahidi kuendelea kuisaidia Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto kwa kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Bima ya Afya kwa watu wote bila kusahau masuala ya uzazi wa mpango.

Pia Mheshimiwa Ummy Mwalimu hakusita kuonesha jitihada za Serikali katika kuhudumia wananchi wake ikiwemo kuongeza ajira mpya kwa watumishi wa Afya ili kuimarisha shughuli za utoaji huduma, Kuendelea kuboresha Miundombinu hususani katika vituo vya Afya ili kuboresha utoaji wa huduma za Upasuaji na Dharura ili kuokoa maisha ya mama na mtoto. Pia kikao hicho kilihudhuriwa na Brian Rettman kutoka PEPFAR (Wapili Kulia kutoka kwa Waziri), Sharon Cromer kutoka USAID Mission (Wa pili kushoto kutoka kwa Mh. Waziri) na Maestro Evans Mkurugenzi mkazi wa CDC (Wa kwanza Kushoto Kutoka kwa Mh. Waziri).

Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu

0
0

 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakishiriki zoezi la uchangiaji damu.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusiana na zoezi la uchangiaji damu salama na kuipongeza Benki ya KCB kwa kushiriki katika zoezi hilo lililofanyika Makao Makuu ya benki hyo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akimpongeza mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya KCB Bi. Francisca Alphonce kwa kuwa mmoja wa watanzania waliojitokeza kuchangia damu salama
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) kwenye picha ya pamoja na sehemu ya timu ya menejimenti ya Benki ya KCB Tanzania na baadhi ya wakilishi kutoka wizarani. Timu ya menejimenti ya Benki ya KCB, Wapili kulia ni Bw. Cosmass Kimario, wakwanza kulia ni Bw. Masika Mukule, wakwanza kushoto ni Bi. Christine Manyenye, wakwanza kushoto juu ni Bi. Joyce Wiki Mwashigadina watatu kulia juu ni Bw. Rojas Mdoe.
 
Dar es Salaam, 12 Juni 2017 – Wafanyakazi wa Benki ya KCB Bank Tanzania leo wamechangia damu. Hii ni katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uchangiaji damu (world blood donor day) ambayo itaadhimishwa dunia nzima jumatano wiki hii, tarehe 14 Juni.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo  ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Cosmas Kimario alisema  kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji  jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.

“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu” alisema Kimario.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa swala la kuchangia damu ni la muhimu sana kwani kuna wagonjywa wengi wenye hitaji la damu hivyo elimu juu ya uchangiaji damu salama ni muhimu kutolewa kwa jamii ili kuifanya jamii kuwa na uelewa mpana juu ya zoezi hilo. 

“Tumeamua kuandaa uchangiaji wa damu ili kuisaidia serikali katika sekta ya Afya hususani katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu” aliongeza Kimario.

Akizungumza katika zoezi hilo Waziri Ummy Mwalimu aliipongeza Benki ya KCB Tanzania kwa mchango wake huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa ukarimu wa Benki hiyo, akibainisha kwamba serikali inahitaji kubwa la damu hivyo inawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wengi zaidi kujitokeza kuchangia damu na kuokoa maisha kwa kuwa serikali haiwezi kufanikisha malengo peke yake.

“Nawapongeza sana Benki ya KCB kuwa wakwanza kuanzisha zoezi hili mwaka huu. Nawahimiza na wengine wajitokeze na waige mfano huu” alisema Waziri.

Zoezi hilo lilifanyika makao makuu ya ya Benki ya KCB, Oysterbay jijini Dar es Salaam. Wakizungumza mara baada ya kuchangia damu kwa hiari baadhi ya wafanyakazi wa benki ya KCB wamesema kuwa zoezi hilo limeenda vizuri na kuwa suala la kuchangia damu ni lamsingi sana kwani wapo watu waliopungukiwa damu, wagonjwa na wanaopata ajali na kuhitaji damu.

Kwako wewe mtanzania jiulize kwanini usichangie damu kuokoa maisha ya watanzania wengine.


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAVALISHA VYEO MAAFISA WA MAGEREZA KWA NIABA YA RAIS,AHIMIZA HAKI NA USAWA MAGEREZA

0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride katika hafla fupi ya kuwavalisha Vyeo Maafisa Magereza kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa mahaliwa alimwakisha Rais John Pombe Mgufuli katika hafla hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha Jeremiah Nkondo kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017.  Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla  hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo Tusekile Mwaisabila kuwa Naibu Kamishina wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika  hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimvalisha cheo, Afwililwe Mwakijungu kuwa Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo . (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 
Manaibu Kamishina wa Magereza wakisoma Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma baada ya kuvalishwa vyeo na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa aktika hafla fupi iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika hafla fupi ya kuvalisha vyeo Maafisa magereza iliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni 12, 2017. Mheshimiwa majaliwa alimwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa magereza aliowavalisha Vyeo kwa Niaba ya Rais John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam Juni, 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) 

           
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka maaafisa na makamanda wa Jeshi la Magereza nchini waendelee kusimamia haki na usawa wanapotimiza wajibu wao.

Ametoa wito huo leo jioni (Jumatatu, Juni 12, 2017) wakati akizungumza na maafisa na makamanda wa jeshi hilo katika hafla ya kuwavisha vyeo maafisa 29 iliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye amefanya kazi hiyo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewavisha vyeo maafisa watano kuwa Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) na maafisa 24 kuwa Kamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP). Maaafisa hao walipandishwa vyeo Mei 25, mwaka huu.

“Ninyi ni viongozi wakuu katika mikoa mnayotoka. Huko kuna makamanda walio chini yenu na jamii inayowazunguka. Endeleeni kuwahudumiana na kulitumikia Taifa hili kwa weledi mkubwa. Endeleeni kusimamia usawa na haki katika kazi zenu za kila siku,” amesema.

Waziri Mkuu amesema hana shaka na utendaji kazi wa jeshi la Magereza kwani watumishi wake ni waadilifu. “Jeshi hili linayo nidhamu ya hali ya juu, mbali ya jukumu lenu la ulinzi, mnafanya kazi nidhamu, weledi na uadilifu mkubwa,” amesema.

Amesema Serikali inatambua changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kila siku na kwamba inajitahidi kuzishughulikia hasa baada ya kukamilisha zoezi la kuondoa watumishi hewa.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuhutubia maafisa hao, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Yusuph Masauni amewataka maafisa waliovishwa vyeo wazingatie maadili ya kazi zao na uzalendo kama ambavyo wameapa kwenye kiapo cha maadili.

Maafisa watano waliovalishwa vyeo kuwa Naibu Kamishna wa Magereza ni SACP Uwesu Ngarama; SACP Gideon Mkana (Mkuu wa Chuo cha TCTA); SACP Jeremiah Nkondo (RPO-Kagera); SACP Tusekile Mwaisabila (RPO-Lindi) na SACP Augustine Mboje (RPO-DSM).

Maafisa 24 waliovalishwa vyeo kuwa Makamishna Waandamizi Wasaidizi wa Magereza (SACP) ni ACP Mbaraka Semwanza; ACP George Mwambashi; ACP Charles Novati; ACP Faustine M. Kasike; ACP Joel Bukuku; ACP Deogratius Lwanga; ACP Boyd P. Mwambingu (RPO Pwani); ACP Athumani Kitiku (RPO Mwanza) na ACP Hassan Mkwiche (RPO Kilimanjaro).

Wengine ni ACP Luhende D. Makwaia; ACP Hamza R. Hamza; ACP Jeremiah Y. Katengu; ACP Mzee R. Nyamka (Kaimu RPO Morogoro); ACP Afwilile Mwakijungu (Mkuu wa gereza la Isupilo, Iringa); ACP Ali Kaherewa (Kaimu RPO Singida); ACP Ismail Mlawa (RPO Mtwara); ACP Chacha B. Jackson; ACP Rajab N. Bakari; ACP Kijida P. Mwankingi; ACP Julius C. Ntambala; ACP Mussa M. Kiswaka; ACP Justin Kaziulaya na ACP Bertha J. Minde.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JUNI 12, 2017.

ARUMERU YANUFAIKA NA MITAMBO YA KISASA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA HALI YA HEWA NA TAHADHARI

0
0

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu (bajeti) Bi. Grace Mosha akizungummza jambo wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru Bw. Christopher Kazeri walipotembelea Wilaya ya Arumeru Arusha.
ARE2
Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Arusha Bi.Maria Saidia akizungumza na Ti,mu ya ukaguzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotembelea kuona Utekelezaji wa Mradi wa wakati wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari uliofunga mitambo ya kisasa ya taarifa za hali ya hewa Wilayani Arumeru mkoani Arusha.
ARE3
Muonekano wa Mitambo ya kisasa ya utoaji wa taarifa za hali ya hewa uliofungwa katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mifumo ya Tahadhari unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ufadhiri wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme).
 (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Wananchi wa Arumeru wameanza kunufaika na mradi wa Kuimarisha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa na Mfumo wa Tahadhari unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kufungiwa mitambo ya kisasa ya kutoa taarifa za hali ya hewa na tahadhari.

Zaidi ya mitambo 40 imefungwa  nchi nzima ikiwa  Arumeru na Liwale ni moja ya wilaya za mfano ambazo mitambo hiyo imekuwa  ikisaidia Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kutoa taarifa za  utabili wa hali ya hewa  zenye uhakika na uharaka.

Mradi huo mpaka sasa umefanikiwa kufunga Mitambo katika maeneo ya Mbuguni, Hifadhi ya Taifa Arusha, Lyamungo, Manyara, Babati Longido, maeneo ya Bonde la Mto Pangani,Lushoto pamoja na Mombo
Wakizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waliofanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo,wakazi wa Arumeru wamesema tangu mitambo hiyo  ilipofungwa wamekuwa wanufaika wakubwa. 

“Sisi wakulima na wafugaji wa Mbuguni tumefaidika sana na uwepo wa mitambo ya kisasa ya utoaji wa taarifa za hali ya hewa katika maeneo yetu kwani kumesaidia wakulima kulima mazao yanayoendana na hali ya hewa na kuondokana na athari za mafuriko kwa kuzingatia taarifa za utabiri zinazotokana na mitambo iliyofungwa” alibaini Bi.Pepetua Mafia
Pamoja na hilo walikiri ongezeko la tahadhari kwa kuwa Mamlaka ya Hali ya Hewa imekuwa ikituma jumbe fupi za taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa maeneo yao katika simu za mkononi walizopewa na mradi huo.

“Tunafarijika na tunaona umuhimu wa taarifa za utabiri zinazotumwa katika simu hizi tulizopewa na mradi huu kwani imekuwa rahisi kujua vipindi mbalimbali vya hali ya hewa na kutusaidia kuweza kupanga shughuli za uzalishaji ikiwemo kilimo na ufugaji wenye tija ambapo kila baada ya siku kumi tunapokea jumbe kutoka Mamlaka ya hali ya hewa”alisisitiza mkazi wa Shambarai Bi.Elizabeth Laiza

Aidha pamoja na mafanikio hayo wakazi wa Arumeru waliomba Serikali kuongeza vituo na kujengewa uwezo zaidi ili kuepuka changamoto za uelewa mdogo wa taarifa za hali ya hewa.

“Tunaiomba Serikali itujengee uwezo zaidi juu ya umuhimu wa taarifa za hali ya hewa na tahadhari ili kutatua changamoto za kutojali taarifa hizo na kusaidia kuyakabili majanga ya mafuriko na ukame yanapotokea.” alisema Bw. Elibokea Lukio mkazi wa Maloloni.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi masuala ya Bajeti Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Grace Mosha alipongeza jitihada zilizopo za waratibu wa  Ofisi yake kwa kushirikiana na wadau ikiwemo Wizara na Maji na Umwagiliaji Bodi ya Bonde la Mto Pangani, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini na kuwaomba kuendelea kutekeleza mradi huu ikiwezekana kuongeza mitambo hiyo kulingana na uhitaji.

“Niwapongeze wadau wote wa mradi kwani mradi umekuwa na matokeo chanya kwakuwa wananchi wamekiri na kuomba Serikali ifunge mitambo mingi zaidi ili kuifikia nchi nzima badala ya mitambo iliyopo sasa”.Alisisitiza Bi.Mosha

AWALI:Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Hali ya Hewa na Mfumo wa Tahadhari ni mradi wa mfano na utekelezaji wake ni katika Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi na Arumeru mkoani Arusha ambapo umelenga kuwajengea uwezo wananchi katika kupata taarifa za tahadhari zitazosaidia kujiandaa, kukabili hali pindi unapotokea  Ukame na Mafuriko ikiwa ni maeneo yanayoathiriwa zaidi.Mradi huu ulianza kutekelezwa rasmi mwaka 2015 Ukiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ufadhiri wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme)

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNE 13,2017

0
0
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images