Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Wasanii wa Maigizo, Filamu, Muziki, Uchoraji na Ngoma za Asili Dar 'Wanolewa'...!

$
0
0
Baadhi ya wasanii wakiwa kwenye kazi za vikundi kwa majadiliano zaidi juu ya semina semina ya wasanii wa sanaa za maigizo, filamu, muziki, uchoraji na ngoma za asili jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa wasanii juu ya umuhimu wa wao kushiriki katika mchakato wa uundaji Katiba Mpya na kutumia kazi zao katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mmoja wa wasanii hao akiwasilisha mada ya kundi lao katika semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa wasanii juu ya umuhimu wa wao kushiriki katika mchakato wa uundaji Katiba Mpya na kutumia kazi zao katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia
Picha mbalimbali juu ni baadhi ya wasanii wanaoshiriki Semina ya wasanii wa sanaa za maigizo, filamu, muziki, uchoraji na ngoma za asili jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye kazi za makundi za majadiliano. Semina hiyo imeandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa wasanii juu ya umuhimu wa wao kushiriki katika mchakato wa uundaji Katiba Mpya na kutumia kazi zao katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya wasanii wa sanaa za maigizo, filamu, muziki, uchoraji na ngoma za asili jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye semina
 
Baadhi ya wasanii wa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa kwenye semina hiyo.
Baadhi ya wasanii wa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa kwenye semina hiyo.[/caption] [caption id="attachment_35675" align="aligncenter" width="640"] Baadhi ya wasanii wa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa kwenye semina hiyo iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).[/caption] [caption id="attachment_35682" align="aligncenter" width="568"] Baadhi ya watoa mada kwenye semina hiyo wakijadiliana jambo.[/caption] [caption id="attachment_35677" align="aligncenter" width="640"] Mmoja wa watoa mada katika semina hiyo, Kenny Ngomuo (kulia mbele) kutoka TGNP akizungumza katika semina hiyo.[/caption] [caption id="attachment_35673" align="aligncenter" width="640"] Kutoka kulia ni baadhi ya waratibu wa semina hiyo kutoka TGNP wakiwa na wasanii wa jijini Dar es Salaam wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa kwenye semina hiyo iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Mkuu wa kitengo cha habari na uhusiano wa TGNP, akizungumza katika semina hiyo iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo Dar es Salaam. Picha ya pamoja ya washiriki wa semina ya wasanii wa sanaa za maigizo, filamu, muziki, uchoraji na ngoma za asili jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa wasanii juu ya umuhimu wa wao kushiriki katika mchakato wa uundaji Katiba Mpya na kutumia kazi zao katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

RAIS KIKWETE AITAKIA KILA LAKHERI TAIFA STARS KWENYE MECHI YAO YA MARUDIANO MASHINDANO YA CHAN

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wachezaji wa Taifa Stars aliokutana nao Uwanja wa ndege wa Mwanza leo Julai 24, 2013 wakati yeye akielekea Bukoba na Taifa Stars wakiwa wamemaliza kambi na sasa wanaelekea Uganda kupambana na The Cranes katika mechi ya marudiano ya CHAN.

Exim Bank receives certificate of appreciation from African diplomatic corps

$
0
0
 
 The Dean of the African Ambassadors in Tanzania and Angola Ambassador Prof.Ambrosio Lukoko (right) hands over a certificate of appreciation to the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (left) in appreciation for the bank’s support to the Africa Day Golden Jubilee Celebrations held in Dar es Salaam in May this year.
 The Dean of the African Ambassadors in Tanzania and Angola Ambassador Prof.Ambrosio Lukoko (fourth right) hands over a certificate of appreciation to the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (fourth left) in appreciation for the bank’s support to the Africa Day Golden Jubilee Celebrations held in Dar es Salaam in May this year. Looking on third from the left is the Zimbabwean Ambassador Edzai Chimonyo.
 The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (centre) shares a light moment with the Zimbabwean Ambassador Edzai Chimonyo (second left) during a certificate handover event held in Dar es Salaam yesterday in appreciation for the bank’s support to the Africa Day Golden Jubilee Celebrations held in Dar es Salaam in May this year. Right is the Sudanese Ambassador Elwalud Abdlla.
 The Zimbabwean Ambassador Edzai Chimonyo (left) discusses a point with the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (second left) during a delegation visit by African Ambassadors at the bank’s headquarters in Dar es Salaam yesterday. Looking on at the right is the Dean of the African Ambassadors in Tanzania and Angola Ambassador Prof.Ambrosio Lukoko
 The Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant (right) shares a light moment a delegation of African Ambassadors during a courtesy visit at the bank’s headquarters in Dar es Salaam yesterday in appreciation for the bank’s support to the Africa Day Golden Jubilee Celebrations held in Dar es Salaam in May this year. Left is the Sudanese Ambassador Elwalud Abdlla
=========  =========  ========

Exim Bank receives certificate of appreciation from African diplomatic corps

EXIM Bank Tanzania has received a certificate of appreciation from the African Diplomatic Corps in recognition for the bank’s support for African Day Golden Jubilee Celebrations held in Dar es Salaam in May.

This was during a visit lead by the Dean of the African Ambassadors in Tanzania and Angola Ambassador Prof.Ambrosio Lukoko who was accompanied by the Zimbabwean Ambassador Edzai Chimonyo, Sudanese Ambassador Elwalud Abdlla and the Mozambique High Commissioner H.E Vicente Veloso.

Speaking during the event, the Exim Bank Tanzania Managing Director Anthony Grant pledged his bank’s commitment to continue supporting the group. “We are so grateful for this certificate of appreciation in recognition to our support to African Day Golden Jubilee Celebration held in Dar es Salaam in May. We will continue supporting various diplomatic endeavors,” Grant said.

Grant during the meeting noted that his bank is committed to supporting various economic development activities in the country. “We are committed to continue supporting Small and Medium Enterprises (SMEs) and women because they play a significant role in the micro and small enterprises sub-sector,” Grant said.

Grant said the bank has recorded major achievements this year among which include short listing for this year’s African Bankers Awards held in marrakech, morocco and emerging winner for the Customer Care sub-category in Tanzania’s banking industry according to a report by international Audit Firm KPMG released recently.

The Dean of the African Ambassadors in Tanzania Prof.Ambrosio Lukoko thanked the bank for its support to the group and called for continued support in the future

RAIS KIKWETE AWASILI BUKOBA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU SITA

$
0
0
 Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya kuweka  jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe Peter Serukamba wakishangilia wakati Rais Kikwete akiweka jiwe la msingi
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Rais Kikwete akisalimiana na Mhashamu Methodius Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba
 Sehemu ya uwanja wa ndege wa Bukoba unaokarabatiwa na kupanuliwa
 Rais Kikwete akiwasili Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Rais Kikwete akisalimiana na wanachama wa KCU alipowasili Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Rais Kikwete akisalimiana na wananchi waliofurika kushuhudia ufunguzi wa  jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Rais Kikwete akiendelea kusalimia wananchi.
 
Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD John Binushu  akimkaribisha Rais Kikwete Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Sehemu ya umati wa wananchi kwenye ufunguzi wa jengo hilo
 Jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Rais Kikwete akipokea risala toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD John Binushu 
 Rais Kikwete akipokea zawadi ya kahawa toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KCU (1990)LTD John Binushu 
 Rais Kikwete akifunua kitambaa kama ishara ya Kufungua rasmi jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Rais Kikwete akikata utepe Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Rais Kikwete akihutubia wananchi baada ya Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Wananchi wakimsikiliza Rais Kikwete
 Rais Kikwete akihutubia
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa KCU baada ya kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe. Fabia Massawe baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba leo tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku sita mkoani humo
 Rais Kikwete akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman ambaye pia yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi
 Rais Kikwete akisalimiana na Mstahiki Meya wa Bukoba Mhe Anatory Amani
 Vijana wa Skauti wa Bukoba wakimlaki Rais Kikwete uwanjani hapo
 Wanahabari toka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini
 Kijana wa Skauti akipiga saluti kuomba kumvisha skafu Rais Kikwete
 Rais Kikwete akivishwa skafu
 Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli. Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe
 Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
 Rais Kikwete akisalimiana na viongozi na wananchi waliofika uwanjani kumlaki
 Rais Kikwete akisalimiana na Mkuu wa JKT
 Rais Kikwete akisalimiana na viongozi wa dini mbalimbali waliokuwepo uwanjani
 Rais Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni
 Ngoma ya Kihaya ikimlaki Rais Kikwete Bukoba
 Karibu Bukoba mheshimiwa Rais....
 Sehemu ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba
 Viongozi wa dini wakiwa bega kwa bega kwenye sherehe hizo
 Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe akimkaribisha Rais Kikwete kuongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba
 Rais Kikwete akiongea na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Rais Kikwete akipata maelezo kabla ya kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
---------------------------------------------------------------
Ndugu Wananchi, kama ambavyo nimewahi kuwajulisha mara nyingi kupitia vyombo vyetu vya habari juu ya Mkoa wetu wa Kagera kupewa heshima kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kitaifa mwaka 2013, leo napenda kuwajulisha juu ya maandalizi ya maadhimisho hayo ambayo yataadhimishwa tarehe 25/07/2013 hapa mkoani kwetu katika Wilaya ya Muleba katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Kaboya. Pia nawajulisha kuwa maadhimisho hayo yataambatana na ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkoa wa Kagera.

MAADHIMISHO YA MASHUJAA MWAKA 2013
Ndugu Wananchi, Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Kumbumbu ya Mashujaa mkoani Kagera yanaendelea vizuri kamati mbalimbali za maandalizi zinatekeleza majukumu yake ya mwisho ili kufanikisha maadhimisho siku ya Alhamisi ya wiki hii tarehe 25 Julai, 2013. Kamati zinazoandaa maadhimisho hayo ni Kamati ya Mapokezi, Usafiri na Malazi; Kamati ya Ujenzi Uwanja na Mapambo; Kamati ya Chakula na Afya; Kamati ya Ulinzi na Usalama; na Kamati ya Burudani, Habari na Uhamasishaji.

Ndugu wananchi, Kwa kiwango kikubwa maandalizi yote yamekamilika na tunatarajia kuanzia leo kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya mkoa, pia nje ya nchi watakaohudhuria maadhimisho hayo.
Mkoa wetu umejipanga vizuri kuwapokea wageni wote watakofika mkoani hapa kwa ukarimu na bashasha kubwa.

Wajibu wa Wananchi
Ndugu wananchi, Napenda kutumia fursa hii kuwaomba kuwa wakarimu kwa wageni wetu wote tunaowatarajia kuanzia leo kwa kutekeleza majukumu yenu kama Wanakagera kama ifuatavyo;
Ø Kila mwananchi kuhakikisha maeneo yake na mazingira yanayomzunguka yanaendelea kuwa katika hali ya usafi kama utamaduni wetu. Pia kumwajibisha mtu yeyote atakaeonekana anachafua mazingira yetu. Hili ni jukumu la kila mwananchi.
Ø Kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha Siku yenyewe ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2013 huko Kaboya Wilayani Muleba. Kwani hatuna budi kuwakumbuka Mashujaa wetu kwa sababu ya historia ya mkoa wetu kushiriki katika vita ya kumwondoa adui aliyekuwa amevamia nchi yetu kupitia ardhi ya mkoa huu mwaka 1978 hadi 1979.
Ø Kila mwananchi kuhakikisha anaitunza amani na utulivu kama destuli ya mkoa wetu kwa wakati wote wageni wetu watakapokuwepo hapa mkoani na baada ya maadhimisho ya Mashujaa. Aidha, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imejipanga vizuri kuhakikisha amani na utulivu vinatawala wakati wote. Kwa mwananchi yeyote atakayeona viashiria vya uvunjifu wa amani atoe taarifa mara moja ili taarifa hizo zifanyiwe kazi mara moja.

Wajibu wa Vyombo vya Habari
Ndugu Wananchi, Vyombo vyetu vya habari vina wajibu wa kuhakikisha vinaendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu Maadhimisho ya Mashujaa kama ambavyo vimekuwa vikifanya kuanzia mwezi Mei, 2013.

Aidha, nawaombeni Waandishi, Wahariri na Wamiliki wa vyombo vya habari kutumia fursa hii kuutangaza mkoa wetu wa Kagera katika sekta mbalimbali za uwekezaji na fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wetu.
Vilevile nawaombeni Wamiliki wa vyombo vya habari hasa redio zetu za jamii kutoa muda wa kutosha katika vituo vyenu vya redio kurusha habari na matukio ya Kumbukumbu za Mashujaa papo kwa papo (live coverage) siku ya maadhimisho ili wananchi ambao hawatapata muda wa kufika Kaboya wazipate habari hizo kupitia redio zetu za Jamii.

ZIARA YA MHE. RAIS MKOANI KAGERA
Ndugu Wananchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye atakayekuwa mgeni Rasmi Katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2013. Pia Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mkoa wetu wa Kagera.
Ndugu Wananchi, Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais Kikwete anatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wetu kama ifuatavyo:
§ Kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
§ Kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma - Rusahunga
§ Kuweka jiwe la msingi barabara ya kiwango cha lami Kyaka hadi Bugene
§ Kufungua Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
§ Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
§ Kuzindua mradi wa maji Muleba
§ Kuzindua kivuko kipya Rusumo (Ngara)
§ Kuzindua mradi wa usambazaji umeme vijijini Nyaishozi (Karagwe)
§ Kuzindua Wilaya Mpya ya KyerwaNdugu Wananchi, Vilevile Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataongea na wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara katika Wilaya zetu ndani ya mkoa.

Ndugu Wananchi, nawaombeni kujitokeza kuanzia tarehe 24/07/2013 uwanja wa ndege wa Bukoba ili kumpokea Mheshimiwa Rais, pia atakapokuwa anafanya ziara katika Wilaya zetu tujitokeze kwa wingi kumsikiliza. 
 
Mwisho; Nawatakia ushiriki mzuri katika kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa na mapokezi mazuri ya wageni wetu hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kagera: Amani na Maendeleo. 
Amani na Maendeleo; Kagera.

Imetolewa na: Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe
Mkuu wa Mkoa
KAGERA

BONDIA MTANZANIA OMARI KIMWERI 'LION BOY' KUPAMBANA TENA AUSTRALIA

$
0
0

Omari Kimweri
BONDIA Mtanzania OmariKimweri  'Lion Boy' anaefanya shughuli zake nchini  Australia,anatarajia kupanda ulingoni mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya mpambano wake mwingine baada ya kuwatwanga mabondia kadhaa nchini humo.
 
Bondia huyo anaechezea uzito wa light flyweight amesema kuwa ataendeleza wimbi la ushindi kwa kutoa vipigo kama alivyotoa kwa bondia   Yodpichai Sithsaithong pamoja na  Lookrak Kiatmungmee ambazo ndio mechi zake za mwisho kucheza kabla ya hii inayomkabili punde

Aliongeza kwa kusema kuwa unajua mimi ni Bingwa hivyo sito kubali kupoteza mpambano huo utakaofanyika katika ukumbi wa  The Melbourne Pavilion nchini  Australia mpambano huo utakaosimamiwa na kamisheni ya nchi hiyo umekuwa gumzo kila kona kwa kuwa bondia Mtanzania  Kimweri amejizolea umaarufu mkubwa nchini humo
Bondia huyo aliyeanza kujishulisha na mchezo wa ngumi za kulipwa nchini    Australia mwaka 
2007  

Mpaka sasa akiendelea na shughuli zake hizo amesema lengo lake kubwa ni kuchukuwa mikanda inayotambulika kimataifa, ingwa yeye kwa sasa ni bingwa wa WBO ambapo aliupata kwa kumtwanga bondia  Panmongkol Ekarin  wa Thailand.
 
Bondia huyo amewaomba watanzania kumuombea duwa kwani ana kibarua kizito cha kuitanganza nchi yake kimataifa, bondia huyo mwenye uraia wa nchi mbili Tanzania na Austalia amesema ana mpango wa kuja Tanzania na kudhamini mchezo huo kama mfadhili endapo marengo yake yatatimia, alisema 'mimi nataka nije kupigana Tanzania nikiwa mchezaji na promota vile vile hivyo nafanya mpango huo mambo yakiwa mazuri nitakuja bongo ili nifanye uwekezaji katika Boxing '

Bondia huyo mpaka sasa amekwisha cheza mapambano   15 akishinda 12  na kupoteza mapambano matatu bondia huyo anayefananishwa na Simba muwindaji amekuwa tishio kwa mabondia wenye uzito wake kwa niaba ya watanzania wote tunaungana kumsapoti bondia Omari Kimweri anayefanya kazi zake nchini Austalia aweze kushinda mpambano waku huo Mungu Ibariki Africa,Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri, AMIN
Bondia Mtanzania Omari Kimweri akinyooshwa mkono juu kuashiria ushindi wake

Mapigano makali yazuka tena Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

$
0
0
Mapigano makali yamezuka tena Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kati ya M23 na  Jesshi la Congo FRDC lakini pia wananchi waishio maeneo ya mashariki wapiganaji wa kundi la Mai mai wameamua kujitoa muhanga kupambana na M23 .Kuangalia uwanja wa vita na jinsi hali ilivyo bofya hapa kupata ripoti maalum ya VOA.

Benki ya Dunia yaipa changamoto Afrika kuboresha matumizi ya ardhi kuondoa umasikini

$
0
0
WASHINGTON, DC, Julai 22, 2013 – Benki ya  Dunia imetoa changamoto kwa nchi za Afrika  kuhimiza maendeleo endelevu ya  ardhi  ili kupunguza umaskini na kujiletea maendeleo.

Ripoti ya Benki hiyo iliyotolewa Julai 22, 2013  imeeleza kuwa ingawa nchi za Afrika ina karibu nusu ya eneo la ardhi nzuri  ambayo haijaendelezwa kwa kilimo, bara hilo limeshindwa  kuiendeleza ardhi hiyoinayokadiriwa kuwa hekta milioni  202 kujikwamua katika umaskini, kuleta maendeleo ya uchumi,kuongeza nafasi za kazi na kulleta mafanikio kwa jumla.

Ripoti hiyo inayoitwa  “Kutumia ardhi ya Afrika kwa mafanikio ya pamoja,”  inaeleza kuwa  nchi za Afrika najamii zake zinaweza kabisa kuondoa tatizo la uporaji wa ardhi, kuzalisha mazao ya chakula na kubadilisha  taratibu za usimamizi na umiliki  wa ardhi katika mwongo ujao.Afrika, Ripoti  hiyo imeeleza, ina kiwango kikukbwa cha umaskini ambapo asilimia  47.5 ya watu wake wana kipato chini ya  dola za Marekani $1.25 kwa siku..

“Licha ya kuwa na ardhi kubwa na utajiri wa madini, Afrika bado ni maskini ,”  anasema  Makhtar Diop, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Afrika. “Kuboresha usimamiaji wa ardhi ni muhimu kwa maendeleo ya haraka na kutoa nafasi  zaidi kwa waafrika , wakiwemo wanawake ambao ni asilimia 70 ya wakulima wa Afrika ambao wanakwazwa  kumiliki ardhi na sheria za kimila..Hali hii haikubaliki na lazima ibadilike ili waafrika waweze kunufaika na ardhi yao.”

Ripoti hiyo imeeleza kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ardhi ya ardhi haijarasimishwa, hivyo kuwa na hatari kubwa ya uporaji na kuchukuliwa kwa malipo ya chini ya fidia. Hata hivyo kumekuwa na matumaini ya maboresho  chini ya mipango inayoendelezwa katika nchi za   Ghana, Malawi, Msumbiji,, Tanzania, na Uganda ambapo  mpango wa kutumia  ardhi kwa mafanikio ya pamoja  unaweza kuleta mapinduzi  ya  uzalishaji wa kilimo na uporaji wa ardhi na  kuondoa umaskini wa kutupea Afrika..

Mpango wa kuleta mabadiliko

Ripoti hiyo inapendekeza kuwa Afrika inaweza kufanikiwa kuendeleza ardhi yake  katika kipindi cha muongo ujao kwa::

· Kuwa na mabadiliko  na uwekezaji kurasimisha ardhi  na  maeneo muhimu yanayomilikiwa na watu binafsi.
· Kusimamia taratibu za umiliki za maeneo yaliyovamiwa  na kujengwa  bila mpangilio mijini ambapo wanaishi zaidi ya  watu asilimila 60 barani Afrika.  .
· Kukabiliana na udhaifu wa utawala na rushwa katika mfumo wa  usimamizi wa ardhi katika nchi za Afrika ambao  kwa kawaida unapendelea wakubwa na kuathiri maslahi ya wananchi walio maskini.
· Serikali za Afrika kuwa na dhamira  ya kisiasa  kuhimiza  mabadiliko haya ya ardhi kuvutia raslimali na uwezekezaji wa jamii ya kimataifa. .

Ripoti  hiyo inasema kuwa mpango huo utagharimu  nchi za Afrika  na  washirika wa maendeleo , ikiwemo sekta bianfsi kiasi cha  dola za Marekani bilioni 4.5  katika kipindi cha miaka 10 kuleta mabadiliko ya sera na uwekezaji

USAFI WA JIJI LA DAR ES SALAAM NI ZOEZI ENDELEVU-MKUU WA MKOA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusu Usafi wa Jijinla Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Saidi Meck Sadiki Ofisini kwake leo katika mkutano wake na waandishi wa habari. Amesema katika taarifa yake aliyoisoma kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal katika ziara yake ya siku moja katika Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 21/07/2013 katika ukumbi wa Karimjee alisisitiza kuwa zoezi la usafi wa Jiji la Dar es Salaam ni endelevu mpaka tutakapofika wakati wa kuridhisha kuwa JIJI LETU SASA NI SAFI.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesisitiza kuwa jukumu hili la usafi katika Jiji letu hili litafanikiwa ikiwa mambo makubwa matatu yatazingatiwa:

1.Ushiriki wa Wakazi wa Dar es Salaam (Wana Dar es Salaam) kikamilifu katika kufanikisha zoezi hili.Hii inaonekana kuwa kama wakazi wa Dar es Salaam tutakuwa na utamaduni wa kupenda usafi na kuchukia uchafu basi tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani sisi tutakuwa askari wa sisi kwa sisi. Hata hivyo ikitokea umemuona mwenzako amepanga biashara sehemu isiyotakiwa au ametupa takataka ovyo tutakuwa wa kwanza kukemeana sisi kwa sisi na kuacha kufanya hivyo sambamba na kuacha kununua bidhaa hizo katika maeneo yasiyofaa.

2.Viongozi/Wanasiasa kukemea suala hili la uchafu katika Jiji la Dar es Salaam: Hii imeonekana kuwa Jitihada, Juhudi na Nguvu nyingi zimekua zikifanywa na Serikali yetu ili kuhakikisha Jiji letu linakua safi,lakini kwa bahati mbaya imeripotiwa/imeonekana kuwa kuna viongozi/Wanasiasa wengine wametumika katika kuwapa viburi baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufanya biashara katika maeneo yasiyotakiwa hivyo kusababisha hasara ya kutupa takataka ovyo na kukwepa kulipa ushuru wa bidhaa wanazoziuza ili hali wamepangiwa maeneo yao husika kwa ajili ya kufanya shughuli zao.

3.Wanahabari/Waandishi wa Habari: Jukumu la waandishi wa habari ni kubwa sana katika kufanikisha kampeni hii kwani wao ndio wamekuwa wakitupatia habari mbalimbali za kuhusu uchafu wa Jiji la Dar es Salaam hivyo ninawaomba kuendelea kushirikiana katika kuibua sehemu ambazo zimekaidi katika kufanikisha zoezi hili na kuziripoti/kukemea na kuelimisha  moja kwa moja kwa kutumia  vyombo mbalimbali vya habari  ili Jamii kwa ujumla ipate kujua hali ilivyo na kuacha tabia hiyo.

WITO
Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa wito kuwa Wana Dar es Salaam tujenge utamaduni wa kuchukia uchafu na kulitunza na kulilinda Jiji letu la Dar es Salaam,aidha wamachinga wafanye biashara zao katika maeneo yao waliyotengewa ili kuepusha uchafuzi wa mazingira pamoja na usumbufu wa hapa na pale na sheria na taratibu zitachukuliwa kwa yeyote atakaesababisha uchafu katika Jiji letu la Dar es Salaam.

TUKIAMUA TUNAWEZA KWA PAMOJA TUSHIRIKIANE KATIKA KUWEKA MAZINGIRA YA JIJI LA DAR ES SALAAM  KUWA SAFI.

                                                                                   Imetayarishwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.



mkoa wa iringa waadhimisha siku ya mashujaa nchini,kitaifa yafanyika mkoani kagera

$
0
0


 Leo ni siku ya maadhimisho ya mashujaa  nchini Tanzania na kitaifa yamefanyika katika mkoa wa kagera,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mh. RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JAKAYA KIKWETE.

Katika mkoa wa Iringa maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya bustani ya manispaa ya iringa na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa mkuu wa wilaya ya kilolo GERALD GUNINITA badala ya mkuu wa mkoa wa Iringa CHRISTINE ISHENGOMA.

Akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa wanaadhimisha siku hii ya leo kwa sababu ya kuwakumbuka mashujaa ambao walipigana uhuru wa taifa letu.

Guninita amesema pia dhumuni la kuwa kumbuka mashujaa hao ni kwa sababu walikuwa wakipambana dhidi ya Nduli Idiamini, ambaye alichokoza Taifa letu mwaka 1978.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa wakazi wa iringa na watanzania kwa ujumla wanapaswa kukumbuka kuwa mashujaa hao walikufa wakati wakipigania amani na uhuru wa taifa letu hivyo ni muhimu kuwaenzi ili kudumisha amani yetu kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadaye.

Ngoma Africa band kutumbuiza Jambo seeheim Festival ,28.07.2013,

$
0
0
 Ngoma Africa band kutumbuiza Jambo seeheim Festival , Jumapili 28.07.2013,

  Mjini Seeheim-Jugenheim,Ujerumani

Kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kinatarajiwa kutingisha jukwaa la Jambo Seeheim  usiku wa jumapili 28.Julai 2013 kuanzia saa 2.00 usikukatika ukumbi wa Sport & Kulturhalle uliopo Berg Strasse,mjini Seeheim-Jugenheim,huko Ujerumani.
 
Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya itavaana tena jino kwa jinona washabiki wa muziki katika International African Festival tubingen 2013 siku yaijumaa ya 9 na 10 .08.2013 mjini Tubingen,South Germany.Wadau kaeni tayari tayari kwa gwaride la FFU wa Ngoma Africa band.msikose kuwasikiliza at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

UNIC YAHAMASISHA VIJANA WILAYANI KARAGWE KUJIUNGA KATIKA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA.

$
0
0
IMG_0620
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya Wilayani Karagwe Mwl. Emmanuel Muganyizi kuhusiana na umuhimu wa wanfunzi wa shule yake kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa na faida zake.
IMG_0638
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ndama na kuwapa hamasa ya kuwa walezi wazuri wa vilabu hivyo vitavyoanzishwa shuleni hapo ikiwa ni kama somo la ziada kwa wanafunzi wao ili wasipate muda wa kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
IMG_0644
Usia Nkhoma Ledama akiongozwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya wilayani Karagwe kuelekea madarasani kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
IMG_0672
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na vijana wa shule za sekondari Ndama wilayani Karagwe mkoani Kagera, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa (UN Club) vinavyoanzishwa mashuleni kwa kuwa kwanza vitawasaidia kujitambua.

Amewaambia kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu hivyo mashuleni kujiunga kwa wingi zaidi na kutawawezesha kujifunza shughuli za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.

Bi. Usia pia amewafafanulia vijana kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya kazi za kujitolea.
IMG_0666
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndama wakimsikiliza kwa makini Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
IMG_0677
Usia Nkhoma Ledama katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndama pamoja na Mkurugenzi wa Radio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe Bw, Joseph Sekiku (kushoto).
IMG_0567
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akijitambulisha kwa baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Kushoto mwenye suti ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Johnbosco Paul.
IMG_0580
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akikagua Maktaba ya Shule ya Sekondari Kayanga. Kulia ni Mwl. Mkuu wa Shule ya Kayanga Johnbosco Paul.
IMG_0704
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya sekondari ya Kayanga amewaelezea kuwa pindi watoto wao wanapojiunga na klabu za Umoja wa mataifa zilizopo mashuleni watapata elimu na uzoefu utakaotengeza thamani ya CV zao na kuzipa uzito zaidi na pia watapata ufahamu wa mambo mengi utakao wasaidia wasijiunge na vikundi visivyofaa wala kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.

Amewaambia wazazi hao ndani ya klabu hizo hutokea kupata tarajali, uzoefu wa kazi, na kwamba kwa kupitia klabu hizo vijana wote shule zilizopo mikoa yote ya Tanzania watakuwa na nafasi ya kuwa karibu na taratibu na kanuni za Umoja wa Mataifa.
IMG_0603
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakiwa mapumzikoni kuelekea kupata uji.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURU NA WAKAZI WA KAGERA WILAYA YA MISENYI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera, baada ya kufuturu nao futari ya pamoja aliyoiandaa katika Kiwanda cha Kagera Sugar, jana Julai 24, 2013. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali Mstaafu, Issa Njiku (kushoto) ni Mmiliki wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Nassor Seif.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Hashim Ranner, baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari ya pamoja na wananchi wa Mkoa wa kagera iliyofanyika katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya ya Misenyi jana Julai, 24, 2013. Katikati ni Mmiliki wa Kiwanda hicho, Nassor Seif.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi alioshiriki nao Futari ya pamoja katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya ya Misenyi Mkoa wa Kagera, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo jana Julai 24, 2013

 Baadhi ya wananchi waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria hafla ya futari ya pamoja, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akizungumza nao jana Julai, 24, 2013. Picha na OMR

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA LEO KAMBI YA KABOYA, BUKOBA, MKOANI KAGERA

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka ngao/sime katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera leo Julai 25, 2013.

Katika maadhimisho haya alikuwepo pia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu

PICHA NA IKULU.
 Viongozi wa dini wakisoma dua kwenye maadhimisho hayo. Pembeni ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu.
 Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Wazee ambao ni sehemu ya mashujaa wetu walio hai waliohudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera leo Julai 25, 2013.

Sikiliza na angalia kwa makini Video Dada D Show ndani ya Jiji la Kansas City U.S.A

$
0
0
Dada D Show ni kipindi cha saa nzima kinachohusu MAHUSIANO kinachorushwa na Radio mpya ya mtandaoni ya GENN (Global Entertainment and News Network) yenye maskani yake jijini Kansas, jimbo la Kansas nchini Marekani.

Kipindi hiki kinaongozwa na "Dada D wa KC" na husikika kila Jumamosi kuanzia saa moja usiku kwa saa za Marekani ya kati (&:00 PM Central Time)

Karibu kuangalia

Rais Kikwete azindua Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi jengo la Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Bukoba mapema leo asubuhi.Kushoto ni Jaji Mkuu,Mhe. Mohamed Chande Othman.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akikata utepe akisaidiwa na  Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakifungua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya ukaguzi wa Jengo hilo mara baada ya kulizindua rasmi leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Kikwete (katikati) , Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman wa pili kushoto, Jaji Mkuu wa Zanzibar,Mhe. Othman Makungu (wa Tatu ), Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Fakih Jundu (wa pili kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Mhe. Gad Mjemmas,kulia,Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Mathias Chikawe (wa pili kushoto)na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Ltn Mstaafu, Fabian Massawe wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama Bukoba Mara baada ya uzinduzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. (Picha na Mary Gwera,Mahakama ya Tanzania)
Muonekano wa jengo la Mahakama Kuu Bukoba lililozinduliwa na rais.

AGNES MASOGANGE NA MELISA EDWARD KUPANDISHWA KIZIMBANI TENA TAREHE 13 AGOSTI 2013

$
0
0

Hatima ya msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya kesi yao inatarajiwa kusomwa tena tarehe 13 Agosti mwaka huu nchini humo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili tayari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.

Alisema kuwa kutokana na ushahidi kutokukamilika ndiyo sababu ya akinadada hao kusubiri kupanda kizimbani tena tarehe 13 ya mwezi ujao.

Kamanda Nzowa aliweka wazi kuwa nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo hilo: "Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi," alisema Nzowa.

Wadada hao ambao walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakitokea Tanzania, walikutwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazina matumizi nchini, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita.
CHANZO JESTINA GEORGE BLOG

SWAHILI TV MTAANI KUNANI

$
0
0

Na Alex Kassuwi
Kwa wanakijiji wenzangu, miaka 30 iliyopita nisingeliweza kuamini ninayo yaona na kuishi hivi sasa. Kwa kifupi tuliona waakija kijijini kama mapadri, wataalamu waa mashirika toka nje ama walimu. Nilijemga imani kila  mzungu ni msomi na tajiri. Nilipohamia ughaibuni nimekuta ni tofauti sana, wapo wazungu wengi mbumbumbu na wanabangaiza tu. Ushauri kwa dada zangu wanaowinda kuolewa na wazungu "kila king'aacho sio dhahabu"
   Kwa matukio ya Swahili TV mtaani kunani tembelea www.swahilitv.blogspot.com

MMILIKI WA HOME SHOPPING CETRE AKIWA HOSPITALINI SOUTH AFRICA BAADA YA KUMWAGIWA TINDIKALI

$
0
0


MFANYABIASHARA maarufu na Mmiliki wa maduka ya Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad, ambaye wiki iliyopita alimwagiwa tindikali maeneo ya Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, sasa yuko Afrika Kusini kwa matibabu zaidi .

Wiki iliyopita majira ya saa moja jioni, mfanyabiashara huyo alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara baada ya kutenda tukio hilo, mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo akijaribu kumkimbiza pasipo mafanikio baada ya kuteleza na kuanguka.

Hatua hiyo ilitoa mwanya kwa mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia usafiri aina ya pikipiki.

Hapo awali ilidaiwa kuwa Saad alikuwa anaweza kuzungumza japo amefungwa mashine sehemu ya pua kwa ajili ya kumsaidia kupumua.  Matukio ya watu kumwagiwa tindikali yameonekana kushamiri nchini katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kumwagiwa tindikali mmiliki huyo wa Home Shopping Centre, limekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa maji maji yanayosadikiwa kuwa ni tindikali majira ya usiku akiwa nyumbani kwake.SOURCE BOFYA HAPA

MZEE SMALL ANAENDELEA VIZURI KIASI,LAKINI BADO ANAHITAJI MSAADA WENU WADAU

$
0
0
Taarifa / Mrejesho : Hali ya Msanii nguli wa maigizo hapa nchini Tanzania, Ndg Said Bin Wangamba almaarufu kama Mzee Small inaendelea vizuri, na ANASHUKURU sana kwa wale wote wanaomkumbuka katika kipindi hiki kigumu cha maradhi. Kwa sasa anaweza kujikongoja taratibu mwenyewe.,

Anaendelea na mazoezi ya kila siku, na kubwa ni dozi ya dawa kwa ajili ya kumsaidia kuondoa uvimbe uliogundulika miezi kadhaa iliyopita, kichwani mwake ambapo dozi moja tu inagharimu takribani 30,000TZS pamoja na mahitaji mengine ya lazima ya kila siku,
 Kwa yeyote atakaeguswa tafadhali unaweza kuwasiliana na Mzee wetu kupitia, M-PESA kwa kutumia namba ya Said Ngamba (Mzee Small) 0754647265 na TIGO PESA kwa kutumia namba ya mkewe 0658111311,

Changamoto: Ni Wakati MUAFAKA Sanaa kuwa Ajira Rasmi na yenye MAPATO STAHIKI,

Alituchekesha na kutuondolea uchovu kwa kipaji chake, nasi tumkumbuke na kumuenzi,
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma

Nafasi ya kazi (for Web Designers).!

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images