Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1267 | 1268 | (Page 1269) | 1270 | 1271 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0


  Mratibu wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) Dkt. Jon Rees akizungumza na waandishi wa habari kuhusu dhamira ya mbio hizo Zanzibar ikiwa ni mara yake ya tatu.
  MBI2
  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Abdalla Mohd akizungumza na washiriki wa resi za baskeli kabla ya kuanza rasmi  zikiwa na lengo la kuimarisha huduma za afya Hospitali ya Kivunge na Makunduchi.
  MBI3
  Picha ya pamoja ya washiriki wa Bike Ride 2017 wakifurahia mbio hizo kabla ya kuanza rasmi.
  MBI4
  Washiriki wa Bike Ride 2017  wakijaanda na safari ya kilomita 300 itakayowachukua muda wa siku sita kuzunguka kisiwa cha Unguja.
  MBI5
  Washiriki wa resi za baskeli (Bike Ride 2017) wakikata maeneo ya  viwanja vya Maisra kuendelea na safari yao itakayochukua sita sita.
  Picha na Makame Mshenga.
  …………………………………………………………………………….
  Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar
  Mradi wa Kuimarisha huduma za Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi ya dola za Marekani 25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika Hospitali ya Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
  Fedha hizo zitapatikana kufuatia kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300 (Bike Ride 2017) katika mikoa mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.
  Akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon Rees kutoka Uingereza  amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya na Zanzibar wanashiriki.
  Amesema fedha hizo zitachangwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi  na zitatumika kuimarisha huduma za afya hasa  afya ya mama na mtoto katika Hospitali za Kivunge na Makunduchi.
  Amesema Resi hizo ambazo ni mara ya tatu kufanya  Zanzibar zilianzia Mji Mkongwe kuzunguka maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na zitrejea Mji Mkongwe.
  Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.
  Akizindua resi hizo, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd amesema Mradi wa HIPZ  umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa kutafuta fedha kwa ajili ya  huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.
  Amesema pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya huduma za afya pia mbio hizo ni sehemu ya kuwashawishi vijana kufanya mazoezi ambayo ni moja ya njia ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.
  Dkt. Fadhil amesema wakati serikali ipo katika mpango wa kuzipandisha daraja Hospitali ya Makunduchi na Kivunge kuwa za Mkoa, fedha hizo zitatumika kuanzisha majengo mapya na kuimarisha huduma za afya.

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimkabidhi mipira ya maji Mmoja wa Wazee wa Kijiji cha Mwera Kiongoni kwa ajili ya kuunganisha maji kupata huduma hiyo katika kijiji chao. Mipira hiyo jumla ya roli sita zimetolewa na Mbunge na Mwakilishi wa jimbo hilo la Tunguu Zanzibar.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akiwa na wananchi wa Kijiji cha Mwera Kiongoni sehemu ya Jimbo lake wakiitikia dua baada ya kukabidhi mipira ya maji kwa ajili ya kijiji hicho kuweza kupata huduma hiyo. kwa wakazi wake.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mhe. Simai Mohammed Said akisikiliza matatizo ya Wananchi wa Jimbo lake katika Kijiji cha Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati Unguja akiwa na wananchi hao akipata changamoto zinazowakabili. baada ya kukabidhi mipira ya maji iliotolewa na Mwakilishi na Mbunge kwa Wananchi wa kijiji hicho kuunga maji.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akizungumza na Wananchi wa jimbo lake katika Kijiji cha Mwera Kiongoni Wilaya ya Kati Unguja alipofika kukabidhi mipira ya maji roli sita ili kuweza kupata huduma ya maji safi na salama.
  Mwenyekiti wa Tawi la CCM Mwera Kiongoni akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhiwa mipira ya maji kwa ajili yao kupata huduma hiyo.
  Diwani wa Wadi ya Ubago akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimsikiliza Diwani wa Wadi ya Ubago akitowa maelezo ya upatikanaji wa maji hayo kwa wananchi wa kijiji cha mwera kiongoni. wanancc chi wa kijiji hicho walikuwa wakipata shida ya huduma hiyo muhimu kwa jamii.
  Imetayarishwa na OthmanMapara.Blog.
  Zanzinews.com.

  0 0

   Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika leo mjini Dodoma . TSNwalikuwa mmoja wa wadhamini. Dk Yonazi alisema kuwa ili kuwaezesha wananchi kiuchumi ni lazima jamii ihabarishwe juu ya fursa mbalimbali zilizopo, lakini pia muhimu wa sekta binafsi kuwa na ubunifu na mifumo ya kujitengenezea utajiri.Picha zote na Mroki Mroki-dailynewstzonline.blog

  Afisa Mtendaji Mkuu wa MM Maxcom , Juma Rajab akielezea uzoefu wake na kusema kuwa inahitajika kuwawezesha wajasiriamali wote, wadogo, wa kati na wakubwa ili kufanikisha wananchi kuweza kuingia katika uchumi wa viwanda.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akitoa mada juu ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo alisema ni vyema viongozi na jamii ikawana nautaratibu wa kuchapa kazi ili iweze kufanikiwa katika suala la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

   Wakuu wa Mikoa waliohudhuria Kongamano hilo.
   Wadau wa Kongamano hilo kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) nao walikuwepo. TSN ilikuwa moja ya wadhamini.
   washiriki wa Kongamano
   Wakuu wa Mikoa Mbeya, Amos Makala (kulia) na John Mongela wakifuatilia kongamano hilo.
   Dk. John Kyaruzi kutoka SAGGOT CTF akitoa mada na kuwelka wazi kuwa taasisi hiyo iko vizuri kuwawezesha wananchi. Aidha alisema ni vyema sasa wananchi wakalazimishwa kulima kibiashara tofauti na ilivyo sasa.
  Mkurugenzi wa Uhamasishaji Sera na Utafiti wa TPSF,Gili Teri akizungumza katika kongamano hilo na kuitaka Serikali iweke mazingira wezeshi ya uhakika na halisi kwa sekta binafsi ili ishiriki katika kukuza uchumi.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (Biashara na Uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika kongamano hilo.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa akizungumza na kuelezea Malego ya Kongamano hilo.
   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala akisalimiana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira walipokutana katika Kongamano la pili la  Uwezeshaji wananchi Kiuchumi mjini Dodoma.
   Dk. John Kyaruzi kutoka SAGGOT CTF akitoa mada na kuwelka wazi kuwa taasisi hiyo iko vizuri kuwawezesha wananchi. Aidha alisema ni vyema sasa wananchi wakalazimishwa kulima kibiashara tofauti na ilivyo sasa.
   Msimamizi wa Mijadala katika Kongamano hilo, Profesa Honest Ngowi akiongoza wawezeshaji.
   Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng'i Issa akifuatilia mijadala.
   Washiriki wakifuatilia mada kwa umakini kutoka kwa wawezeshaji wabobevu.
   Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (MB), akichangia mada wakati wa Kongamano la Pili la Uwezeshaji wananchi kiuchumi lililofanyika jana mjini Dodoma chini ya uandaa wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa mmoja wa wadhamini.
  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula akichangia mada wakati wa Kongamano la Pili la Uwezeshaji wananchi kiuchumi lililofanyika jana mjini Dodoma chini ya uandaa wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa mmoja wa wadhamini.
   Wawezeshaji wakifuatilia mada
   Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi akizungumza katika kongamano hilo.
   Mmoja wa washiriki akiuliza swali juu ya namna vijana wanavyowezeshwa kushiriki katika Uchumi wa viwanda hasa katika sekta ya Kilimo.
   Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADP), Francis Assenga akizungumza na kuweka wazi namna TADP inavyoweza kusaidia miradi mbalimbali hasa katika kilimo.
  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akijibu hoja mbalimbali ambazo ziliibuliwa katika kongamano la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililofanyika jana mjini Dodoma wengine meza kuu ni wawezeshaji katika kongamano hilo. TSNwalikuwa mmoja wa wadhamini.
   Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kongamano hilo.
   Jopo zima la wawezeshaji likiongozwa na Profesa Honest Ngowi (wanne kulia) likiwa meza kuu.
   Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wakiwa katika Kongamano hilo.
  Washiriki kutoka kada mbalimbali.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mlezi wa Taasisi ya Al- Hikma Foundation, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 18 ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally (kulia) na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikima Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo , katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikma Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo, katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  …………………………………………………………

  *Waziri Mkuu amuagiza Meya wa Temeke kesho atoe maamuzi ya kiwanja

  MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.

  Mohammed ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumapili, Juni 11, 2017), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo ni Taasisi ya Al-Hikma waangalie uwezekano wa kuboresha zawadi kwa kutoa scholarships (udhamini) kwa washindi au washiriki, hususan kwa washiriki wa Tanzania.

  “Ongeeni na nchi marafiki kama Saudi Arabia, waone uwezekano wa kutoa zawadi za ufadhili kwenye masomo ya sekta za kimkakati kama vile mafuta na gesi, ili kuongeza hamasa na chachu ya vijana walioko kwenye sekondari zetu nao waone fursa hii na kuichangamkia, badala ya mashindano kujikita kwenye madrasa peke yake,” amesema.

  Waziri Mkuu amewataka wazazi wafuatilie nyendo za vijana wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao na ustawi wa nchi yetu lakini akasisitiza pia waisaidie Serikali katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi.

  “Endeleeni kushirikiana na Serikali katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi na kuwafichua wakwepa kodi. Kila mmoja wetu ahakikishe analipa kodi stahiki kwa mujibu wa sheria. Hii itasaidia Serikali kuboresha huduma kwa wananchi ili waweze kufanya ibada zao vizuri zaidi,” amesema.

  Washindi wengine kwenye kundi hilo na umri wao kwenye mabano ni Abdulkarim Ahmed Farhina (22) wa Sudan ambaye ameshinda dola za Marekani 5,000, cheti, IPAD, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

  Wa tatu ni Mahamoud Ali Chamfi wa Comoro (18) na Seif Ramadhani Zombe (18) kutoka Taasisi za Tanzania ambao wote wamepata dola za marekani 3,000, cheti, IPAD, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

  Wa nne ni Khalil Mussa Hussein (17) kutoka Tanzania Bara ambaye amepata dola za marekani 1,500, cheti, IPAD, na ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Wa tano ni Ismail Issa Qasim (17) kutoka Tanzania Visiwani ambaye dola za marekani 1,000, cheti, IPAD, na ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,

  Washiriki wengine kwenye kundi la juzuu 30 walitoka nchi za Nigeria, Kenya, Uganda, Djibouti, Afrika Kusini, Rwanda, Ghana, Ethiopia, Congo DRC, Burundi na Msumbiji. Umro wao ulikuwa ni kati ya miaka 12 na 26.

  Washiriki wengine waliopewa zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi watano), Juzuu tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20 (washindi watatu).

  Viongozi wengine waliohudhuria kilele hicho ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Mohammed Gharib Billal, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Bin Mansour Al Malek. Wengine ni wawakilishi wanne wa Imam Mkuu wa Mskiti Mtakatifu wa Makkah, Sheikh Abdul Rahman Ibn Abdul Aziz as-Sudais; Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Meya wa Temeke, Bw. Abdallah Chaurembo kesho (Jumatatu, Juni 12, 2017) afuatane na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bw. Nassib Mmbaga hadi kwenye kiwanja kilichopo eneo la Matumbi na kukagua kama kuna uwezekano wa kuliongeza kwa taasisi ya Al-Hikma na wampe majibu Jumanne kwani limekaa wazi kwa muda mrefu licha ya kuwa walishaliomba na hawakupata majibu.

  “Mstahiki Meya wa Temeke na Mkurugenzi wako, kesho Jumatatu nendeni mkaangalie eneo husika kama linafaa kuongezwa na mfanye maamuzi. Eneo hilo limekaa wazi kwa muda mrefu, na hawa wanataka wanataka kujenga zahanati. Jumanne asubuhi nipate taarifa ya maamuzi yenu,” alisema Waziri Mkuu na kushangiliwa na maelfu ya waumini waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu (katikati) na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,  Bi. Beng Issa kulia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akikata utepe(ribbon) kuashiria kuzindua wa taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 wakati wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia ni  Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.  
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akionyesha kitabu cha taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 mara baada ya kuzindua taarifa hiyo wakati wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,(katikati) Mwenyekiti wa Bodi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Dk. John Jingu na kulia ni  Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Bi. Beng’i Issa.  
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama kushoto  akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Bw. Joel Bendera  taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya Julai 2015 mpaka April 2017 mara baada ya kuzindua taarifa hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng Issa.

  Watanzania wametakiwa kubadili fikra za kimtanzamo na kila mtu kutimiza wajibu wake kwa lengo la kuunga mkono dhamira ya serikali ya  awamu ya tano ili kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha ustawi wa jamii.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama alisema hayo wakati alipokuwa akifungua Kongamano la Pili la  Uwezeshaji Watanzania Kiuchumi, kuwa watanzania wanatakiwa kubadili fikra za kimtanzamo ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda, na kuboresha ustawi wa jamii.

  “ Nchi yetu imeamua kubadilisha mwelekeo wa uchumi wa nchi yetu na sisi tunawajibu wa kubadili fikra za kimtanzano ili kufikia uchumi wa viwanda,” aliongeza kusema Bi. Mhagama, ambaye alifungua kongamano hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

  Pia aliwataka washiriki wa kongamano kwenda kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha suala la uchumi wa wananchi unakuzwa. Na aliwasisitiza watumishi wa umma kuwa mfano katika kuchochea dhamira hiyo kwa kufanya kazi kwa vitendo.

  Alisema serikali imeweka mikakati kabambe ya kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi  inayoendana na soko la ajira kupitia program mbalimbali ikiwemo ya kuwafundisha vijana ujuzi waweze kutumika katika nguvu kazi. Na aliwataka wakuu wa mikoa yote kuainisha fursa za kiuchumi na kumpatia waziri mkuu ili zifanyiwe kazi.

  Halikadhalika aliitaka mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kuhakikisha fedha zilizopo katika mifuko yao inawafikia watanzania waweze kukopa na kuwekeza katika shughuli za uzalishaji na biashara. Kauli Mbiu ya Kongamano hilo ni Wezesha Watanzania Kushiriki Uchumi wa viwanda.

  Waziri huyo pia alizidua taarifa ya utekelezaji wa sera ya taifa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya julai  2015 mpaka April 2017. Pia alitoa vyeti na vikombe kwa sekta umma na binafsi waliofanya vizuri katika kutekeleza uwezeshaji wananchi kiuchumi. 
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la  Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi  (NEEC),Bi. Beng’I Issa alisema kongamano hilo lilikuwa la mafanikio kwa kuwa lilishirkisha wadau wote na kwa sasa wanalenga kwenda kutekeleza kwa vitendo majukumu yao. 

  “Kongamano hili tumepatiwa agizo la kila Wilaya kuwa na kiwanda kimoja na sisi tumejipanga kusimamia kwa vitendo,” na kuongea  kusema viwanda huwezesha mali ghafi kuongezwa thamani na kutoa ajira.

  Sambamba na hilo huongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo na kuwa chachu ya uchumi wa nchi kwa kuwa kilimo kina nafasi ya kuajiri watu wengi zaidi na kuongeza vipato vya wananchi.

  Pia kila halmashauri imepwa jukumu la kuainisha maeneo ya kufanyia biashara zikiwa na miundombinu yote na kumpatia waziri mkuu hadi ifikapo Agosti 2017 ili yaweze kufanyiwa kazi.Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJKNUAT), Profesa Dominic Kambarage alisema baraza linafanya kazi kubwa na nzuri na inatekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.

  ”Kutokana na kazi hii nzuri tuongeze nguvu ngazi ya mikoa na wilaya za kufanya kazi kwa vitendo na maeneo ya biashara yatengwe wananchi wawe na fursa za maeneo ya kufanyia biashara,”. Na taasisi za elimu ya juu na kati ziboreshe mitaala yao kwa ajili ya vijana kuondoa tatizo la ajira.

  0 0

   
  Mbunge wa Viti Maalumu Bi Amina Mollel, akiwakabidhi msaada wa vitu Mbalimbali Wanafunzi wenye mahitaji Maalumu wa Shule ya Msingi Buhangija iliyopo mkoani Shinyanga, Sambamba na Msaada huo aliweza Kukabidhi Kadi za Bima ya Afya Kwa ajili ya Matibabu. 
  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Buhangija Wakiwa wameketi, Wakati Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel alipofika Kwenye Kituo hicho Kukabidhi Misaada ya Vitu Mbalimbali Ikiwemo Chakula na Kadi ya Bima ya Afya Kwa ajili ya Matibabu Kwa Watoto hao. 
  Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel akipata Maelezo Mbalimbali Kutoka Mmoja wa Viongozi wa Kituo cha Buhangija Kinachohudumia Watoto wenye Mahitaji Maalum.

   
  Watoto wenye Albnism Wanaosoma Shule ya Msingi Buhangija iliyopo Mkoani Shinyanga Wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel, aliyefika Kwenye Kituo Hicho Kuwapatia Msaada wa Vitu Mbalimbali ikiwemo Kadi za Bima ya Afya Katika Mwezi Huu Mtukufu wa Ramadhani.

   
  Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel akizungumza na Baadhi ya Viongozi pamoja na Walimu Katika Shule ya Msingi ya Buhangija iliyopo Mkoani Shinyanga, Baada ya Kukabidhi Msaada wa Vitu Mbalimbali pamoja na Kadi za Bima ya Afya Kwa ajili ya Matibabu Kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum. 
  Walimu wa Shule ya Msingi ya Buhangija Wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Mbunge wa Viti Maalum Bi Amina Mollel ambae alifika Kwenye Shule hiyo Kwa ajili ya Kutoa Msaada Kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum.

  Picha kwa Hisani ya www.habari360.co.tz

  0 0


  DROO ya 13 ya Biko waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha Tanzania maarufu kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’, imefanyika leo asubuhi, huku mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaa, Amani Kabuku, mwenye miaka 23, akifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh milioni 20.

  Mshindi huyo ameibuka katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, kwa kushirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

  Akizungumza katika droo hiyo leo asubuhi, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema ni wakati wa kutajirika kwa kupitia mchezo wao wa Biko uliozidi kujizolea umaarufu katika kipindi kifupi tangu kuanzishwa kwake nchini Tanzania.

  Alisema anaamini washindi wao wanaoendelea kujipatia fedha mbalimbali kupitia mchezo wao, huku akiwataka Watanzania waendelee kucheza kwa kufanya miamala ya fedha kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000, ambapo namna ya kucheza ni kuweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.

  “Wanachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri yaushindi wa zawadi mbalimbali kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zikilipwa moja kwa moja kupitia simu zao za mikononi walizotumia kuchezea Biko,” Alisema Grace.

  Naye Balozi wa Biko Kajala Masanja aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kucheza Biko ili wajipatie chanzo kipya cha uchumi ili wajiendeshe kiuchumi.

  “Huu si muda wa kuachia wengine wajipatie fedha huku wengine tukikaa tu, badala yake wote tuamke ili kuchangamkia fursa ya kiuchumi kwa ajili ya kupata mtaji kwa ajili ya kujiendesha kimaisha kwa namna moja ama nyingine,” Alisema.

  Akizungumzia ushindi wake, mshindi huyo kutoka Mbezi, Amani aliwashukuru Biko kwa kumtangaza mshindi utakaompatia jumla ya Sh Milioni 20 ambazo zitamsaidia kwa kiasi kikubwa katika vitu vitakavyomuwezesha kiuchumi.

  “Nashukuru kwa kutangazwa mshindi wa Biko wa droo ya 13 ambayo kama nikipata fedha hizo Sh Milioni 20 hakika nitazitumia vizuri katika kuinua kipato change, ukizingatia kuwa nilicheza Biko kwa malengo ya kushinda kwa kumuomba Mungu,” Alisema Amani.

  Kwa kutangazwa mshindi huyo, Biko wanatarajia kumpatia zawadi yake mapema wiki hii kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anaziweka katika matumizi yake ya kuinua uchumi wake, huku mamilioni mengine yakiendelea kutoka kwa ushindi wa papo kwa hapo pamoja na Sh Milioni 20 kwa droo ya Jumatano hii.


  Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kulia akiwa kwenye majukumu ya kumtafuta mshindi wa droo ya 13 ya Biko ambapo kijana mwenye miaka 23 mkazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam, Amani Kabuku, alifanikiwa kuibuka na zawadi nono ya Sh Milioni 20. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

  Kajala Masanja kulia akizungumza huku akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam baada ya kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, huku akishuhudiwa na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.


  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akishuhudia jamii ya Wahadzabe wakitengeneza chakula cha mchana ambao ni unga utokanao na ubuyu. Kabila la Wahadzabe ni moja ya jamii za wawindaji na wakusanyaji wanaopatikana Tanzania ambao chakula chao kikuu ni nyama, matunda, mizizi na asali
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akionja unga wa ubuyu ambao ndiyo chakula maarufu cha jamii ya Wahadzabe.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akipewa maelezo kuhusu nyumba maarufu za jamii ya Wahadzabe
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akipewa maelezo ya matumizi ya mshale katika jamii ya Wahadzabe
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akichezewa ngoma maarufu ya jamii ya Wahadzabe ambayo huchezwa wakati wakimpokea Mgeni mwenye hadhi katika jamii.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jummane Maghembe akisaini kitabu cha Wageni mara alipowasilia katika kijiji cha Yaeda chini wilayani Mbulu mkoani Manyara.
  Mkurugenzi wa Rasilimali Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Bw. Zawadi Mbwambo (katikati) akisikiliza kwa makini risala iliyosomwa na Wawakilishi wa Jamii ya Wahadzabe kwa Mgeni rasmi

  0 0

  Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akifungua mafunzo ya siku tatu na kuelezea juu ya uhusiano wa ukusanyaji kodi na maendeleo katika sekta ya elimu nchini ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
   Afisa kutoka ActionAid Tanzania, Joyce John akitoa mada kuhusu utetezi wa haki za watoto maashuleni kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
   Mwalimu Khamis Kikwajuni akichangia mada kuhusu haki za watoto mashuleni pamoja na Umuhimu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kuwekeza katika sekta ya elimu kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
  Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Nduguru akitoa mada ya uhusiano wa Makusanyo ya Kodi Na Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa baadhi ya wadau na mbalimbali wa elimu kwenye mkutano ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania uliofanyika katika wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
   Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwasilisha kazi zilizofanyika makundi mbalimbali yaliyokuwa yanajadili haki za watoto mashulen, haki za binadamu, ukwepaji na upotevu wa kodi nchini.
    Meneja wa Mradi wa TENMET,  Nicodemus Eatlawe akichangia mada kuhusu mtazamo wa upatikanaji wa elimu, sera na sheria za elimu hapa nchini Tanzania wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana wilayani Kilwa.
  Mwenyekiti wa Chama cha walimu Mkoa wa Lindi, Bw. Bw.  Mlami Seba akifunga mafunzo kwa wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu yaliyoandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
   Baadhi ya wadau wa elimu wakionesha ujumbe
   Picha ya pamoja ya viongozi waliochaguliwa na washiriki wa mafunzo kuongoza Jukwaa La Elimu Kilwa (JEK). 

  Katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini leo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishirikiana na ActionAid Tanzania wameandaa mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Lindi wilaya ya Kilwa kwa siku tatu ili kupanga mpango kazi wa utetezi na ushawishi wa masuala ya elimu yatakayoleta matokeo chanya kwenye masuala ya elimu hapa nchini.
  Mkutano huu ulikuwa ulingazia changamoto zinazoikabili elimu ya msingi hapa nchini ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa ofisi za walimu, upungufu wa vyoo vya wanafunzi, uwiano usiokubalika kitaratibu wa mwalimu na wanafunzi, shule nyingine kukosa kabisa mwalimu wa kike, upungufu wa nyumba za walimu, kutokutosha kwa fedha za ruzuku, utegemezi wa bajeti ya nchi unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu.

  Mgawanyo wa ruzuku usiozingatia mahitaji ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe. Kuwa na mipango ya kibaguzi kwa shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa fedha (payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule. Kukosekana kwa mafunzo kazini kwa walimu, kutopandishwa madaraja walimu na utolipwa kwa wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.

  Katika majadiliano washiriki walichangia juu Upotevu wa kodi nchini hususani katika sekta ya madini na viwanda ndio chanzo cha kukosa fedha za kutosha kugharimia sekta ya elimu nchini.
  Akizungumza leo Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha alisisitiza serikali kuimarisha vyanzo vya mapato yetu kama nchi hasa kwa kukusanya kodi stahiki kwa kila mtu anayepaswa kulipa kodi. Ili tuondokane na utegemezi toka kwa wahisani. Kwa bajeti ya elimu 2016/17 takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. Hata hivyo hadi kufikia mwezi Machi 2017 wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu, sawa na asilimia 47.6%. 

  Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Ndunguru akielezea kuhusu ripoti ya utafiti ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi Mei mwaka 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na Fedha inaliyoonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi.

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Lindi, Bw.  Mlami Seba aliwasisitiza wadau wa elimu kutokata tamaa kufanya ushawishi na utetezi wa upatikanaji wa elimu bora nchini na maslahi ya walimu; Wadau wa elimu wanalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake. Pia alichanghia Kila mtu akilipa kodi stahiki kadri ya kile anachozalisha na pia serikali iwekeze kuboresha huduma za jamii na hususani sekta ya elimu. 

  Washiriki wa mafunzo hayo waliazimia kuanzisha jukwaa la wadau wa elimu wilayani Kilwa kama njia ya kuendeleza kazi ya ushawishi wa haki ya elimu nchini na wilayani kilwa na kama jukwaa la kuongeza ushirikiano. Washiriki walichagua uongozi na kuazimia utakua chini ya uratibu wa Chama cha walimu wilaya ya Kilwa.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.  Alimueleza balozi huyo kuwa Serikali imebaini na itakomesha ujanja unaofanywa na wafanyabiashara haramu wa kutakatisha fedha kwa kununua makundi makubwa ya mifugo na kuyachunga kwenye maeneo ya hifadhi nchini na baadae kuyauza kwa faida kwenye minada.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimkabidhi Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke majarida mbalimbali enye taarifa za vivutio vya Tanzania ofisini kwake mjini Dodoma. (Picha na Hamza Temba - WMU)


  0 0

  WATU tisa wamejeruhiwa na majambazi baada ya kuvamia machimbo mapya ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Nyakivangala, Isimani wilayani Iringa mkoani Iringa na kupora zaidi ya Sh Milioni 81, dhahabu zaidi ya gramu 400, na baadhi ya mali za wafanyabiashara katika eneo. Akizungumza na wanahabari, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela anasema tukio hilo lililitokea majira ya saa nne usiku juzi.

  0 0


  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akizungumza wakati wa halfa ya shirika la BRAC kuwakabidhi vifaa vyenye thamani ya milioni 153 wasichana wajasiriamali kutoka Mkoani Tanga kulia ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shabani kushoto ni Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee

  Diwani wa Kata ya Makorora Omari Mzee akizungumza katika Halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi

  Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shabani akizungumza katika halfa hiyo
  Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali katika halfa hiyo

  Mmoja kati ya wasichana wanaoishi kwenye mazingira magumu ambao wamejengewa uwezo na kupata fursa ya kujiendelea kukuza na kujiendeleza kiuchumi Aisha Mohamed akiishuru Brac kwa kuwawezesha ili waweze kukabiliana na maisha bnaada ya kupatiwa mafunzo
  Baadhi ya wananchi na wazazi wa wasichana wakifuatilia matukio mbalimbali ya makabidhiano vifaa vyenye thamani ya sh.,milioni 153 wasichana wajasiriamali 700 kutoka mkoani Tanga ili waweze kujikwamua kiuchumi
  Baadhi ya wananchi na wazazi wa wasichana wakifuatilia matukio mbalimbali ya makabidhiano vifaa vyenye thamani ya sh.,milioni 153 wasichana wajasiriamali 700 kutoka mkoani Tanga ili waweze kujikwamua kiuchumi
  Walimu ambao walikuwa wakiwafundisha wasichana hao masuala mbalimbali ya ujasiriamali wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa halfa hiyo

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wajasiriamali 700 mkoani hapa ambao walikabidhiwa vifaa vyenye thamani ya milioni 153 ambavyo ni vyerahani 90,mashine za kukaushia nywele 90,vifaa vya ufugaji wa kuku,vifaa vya kilimo,vifaa vya upishi,vifaa vya kwa ajili ya utengenezaji wa batiki na mabegi ya kike
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wajasiriamali 700 mkoani hapa ambao walikabidhiwa vifaa vyenye thamani ya milioni 153 ambavyo ni vyerahani 90,mashine za kukaushia nywele 90,vifaa vya ufugaji wa kuku,vifaa vya kilimo,vifaa vya upishi,vifaa vya kwa ajili ya utengenezaji wa batiki na mabegi ya kike
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wasichana wajasiriamali 700 mkoani hapa ambao walikabidhiwa vifaa vyenye thamani ya milioni 153 ambavyo ni vyerahani 90,mashine za kukaushia nywele 90,vifaa vya ufugaji wa kuku,vifaa vya kilimo,vifaa vya upishi,vifaa vya kwa ajili ya utengenezaji wa batiki na mabegi ya kike
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akimkabidhi cherehani cha kusonea nguo Aisha Mohamed wakati alipokwenda kuwakabidhi vifaa vyenye thamani ya sh.milioni 153 wasichana wajasiriamali 700 vilivyotolewa na Shirika la BRAC kwa wasichana waliopata mafunzo ya ujasiriamali na shirika hilo
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto akimkabidhi mashine ya kukaushia nywele mwanafunzi Thabituwa Shabani wakati wa halfa hiyo kulia ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shaban
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi katikati akikabidhi mabegi ya kike kwa wasichana 700 wa mkoa wa Tanga kushoto ni Meneja Mipango wa Elimu kutoka BRAC Tanzania Amina Shabani

  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


   Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba akizungumza na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wilaya Muheza wakati wa  ufunguzi wa mpango wa kutoa elimu waendesha bodaboda mkoani hapa ambao ulihudhurwa na wadau mbalimbali ikiwemo madereva wa bodaboda kulia ni Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Tanga (RTO) Nassoro Sisiwayah kushoto ni Kaimu Mkuu wa Polisi wilaya ya Muheza (OCD) ambapo aliwataka madereva wa bodaboda kuacha kutumika kuwabeba wahamiaji haramu na dawa za kulevya kwani watakaokamatwa hawatapona
   Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Tanga (RTO) Nassoro Sisiwayah akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba na kulia ni Katibu wa Bodaboda wilayani Muheza,Fransic Gerald
   Kaimu Mkuu wa Polisi wilaya ya Muheza,(OCD) akizungumza katika kikao hicho kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa APEC Bahati Alex
   Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa APEC Bahati Alex akizungumza katika kikao hicho wa pili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba kushoto mwenye miwani ni Kaimu Meneja wa Mfuko wa Mafao ya Wastaafu (GEPF) Erick Haule
   Katibu wa Bodaboda wilayani Muheza,Fransic Gerald akizungumza katika kikao hicho
   Kaimu Meneja wa Mfuko wa Mafao ya Wastaafu (GEPF) Erick Haule aliwataka madereva wa bodaboda kujiunga na mfuko huo
  kupitia mpango wa bodaboda Scheme ili waweze kunufaika.
    Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba katikati akifuatilia maswali mbalimbali kulia ni Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani Mkoani Tanga (RTO) Nassoro Sisiwayah
    Waendesha pikipiki wilayani Muheza maarufu kama bodaboda wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba wakati wa kikao hicho
   Waendesha pikipiki wilayani Muheza maarufu kama bodaboda wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba wakati wa kikao hicho
   Waendesha pikipiki wilayani Muheza maarufu kama bodaboda wakimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba wakati wa kikao hicho 
  Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

   
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni(wa pili toka kulia) akiwaongoza kuimba wimbo wa Taifa la Tanzania Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee(hawapo pichani). Wa pili kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, (wa kwanza kutoka kushoto) ni Mjumbe wa Sekretarieti ya SADC, Bw. Maemo Machete. Mkutano huo unafanyika kwa siku moja leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni kufungua rasmi mkutano huo wa siku moja.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akitoa hotuba ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee uliofanyika leo Juni 11, 2017 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga.
  Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC – Corrections/Prisons Sub Committee ambaye ni Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao hicho kama inavyoonekana katika picha.
  Wajumbe wa Mkutano huo toka nchi za SADC wakifuatilia majadiliano kama wanavyoonekana katika picha(katikati) ni Mkuu wa Magereza nchini Botswana, Silas Motlalekgosi.
  . Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa(kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo akiteta jambo na Mjumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC, Bw. Maemo Machete.
  Wajumbe wa kutoka Jeshi la Magereza Tanzania wakipitia baadhi ya nyaraka mbalimbali za Mkutano huo(kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani, SACP. Boyd Mwambigu(katikati) ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, SACP. Mzee Ramadhan Nyamka(kushoto) ni SACP. Justine Kaziulaya.
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Magereza toka nchi za SADC. Wa tatu toka kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Kitengo cha Habari na Mawasiliano – Jeshi la Magereza).
  Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Magereza/Taasisi za Urekebishaji za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Magereza toka nchi za SADC. Wa tatu toka kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

  0 0

   Waumin wa dini ya Kiislam wakisalia mwili wa Marehemu Sheikh Taufiq Malilo aliyekuwa Sheikh wa mkoa Kigoma kabla ya mwili huo kupelekwa makaburi ya Kazaroho kwa mazishi.
   Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa
   Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa


  Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kigoma.

  HATIMAYE aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma kwa zaidi ya miaka 30 Taufiq Malilo amezikwa huku sehemu kubwa ya wananchi wa mkoa Kigoma wakijitokeza kuhudhuria mazishi hayo.


  Shekhe Malilo ambaye alifariki Ijumaa jioni ya wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kisukari na moyo amezikwa juzi jioni katika makaburi ya Kazaroho Ujiji mjini Kigoma.

  Katika mazishi hayo yaliyofanyika majira ya saa 11 jioni yaliacha vilio na simanzi kwa mamia ya waislam waliohudhuria msiba huo wengi wakikumbana mafundisho ya dini ya kislam katka kuishi maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu.

  Wakati Mwili wa Shekhe Malilo ukipelekwa kaburini kwa ajili ya safari yake ya mwisho hapa duniani ili baadhi ya barabara kufungwa kwa muda ikiwemo sehemu ya barabara ya Lumumba ili kupisha umati mkubwa wa watu kutumia barabara hiyo kwa muda wakati wa kuelekea makaburini.

  Akisoma Wasifu wa marehemu Katibu wa BAKWATA wilaya ya Kigoma vijijini ,Sheikh Yassin Kabunguru alisema kuwa Alhaji Malilo alichaguliwa kuwa Sheikh wa mkoa Kigoma mwaka 1979 hadi mauti yalipomfika akiwa pia Ulamaa wa Taifa.

  Sheikh Kabunguru alisema kuwa katika uhai wake Alhaji Malilo alifundisha dini na kutembelea misikiti zaidi ya 600 mkoani Kigoma akiweka kambi kwa ajili ya kufundisha dini na kufungua shule mbalimbali za kiislam mkoani Kigoma kwa juhudi kubwa ambayo aliifanya binafsi.

  Akitoa mawaidha kabla ya kuelekea makaburi Sheikh Uwesu Mohamed alisema kuwa Alhaji Malilo aliishi katika misingi sita ya kiislam ambayo ilimfanya kuwa mcha Mungu,mnyenyekevu anayewapenda wengine,asiye na tamaa wala kujilimbikizia mali na kwamba Marehemu amekufa akiwa hana hata gari kutokana na sehemu kubwa ya kipato chake kutumia kuendeleza masuala ya dini.

  0 0
  Na Bashir Nkoromo

  Hatimaye Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi na Mbunge wa Kuteulia na Rais Alhaj Abdallah Bulembo, amemaliza ziara yake ya Kichama akiwa amefanikiwa kutembelea mikoa saba na jumla ya Wilaya 47 za mikoa hiyo.

  Katika ziara hiyo ambayo alianza May 26, 2017, aliihitimisha jana, Juni 10, 2017 katika mkoa wa Geita, ziara ikiwa imechukua zaidi ya wiki mbili, ambapo mkoa wa kwanza kufanya ziara hizo uliuwa Dar es Salam na badaye kuendelea katika mikoa ya Dodoma, Manyara, Tabora, Kigoma, Kagera na Geita ambao ndio mkoa aliomalizia.

  Alhaj Bulembo katika ziara hiyo ambayo haikuhusu Jumuia yake ya Wazazi Tanzania, bali ya Kichama zaidi ilikuwa mahsusi kwa kuagizwa na Bosi wake, Mwenyekiti wa CCM Rais John Magufuli, kwa lengo la kutoa shukrani kwa wana CCM kufuatia kura nyingi walizompa hadi kukipatia Chama Cha Mapinduzi kura nyingi wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2015.

  Hata hivyo Bulembo anasema, Shukrani hizo, ni za awali kwa kuwa Mwenyekiti Mwenyewe Rais Dk. John Magufuli atafanya ziara rasmi kutoa shukrani.

  Katika ziara hiyo, Alhaj Bulembo pia pamoja na mambo mengine ya kuhimiza ujenzi na uimarishaji Chama na Jumuia zake, alikuwa na ajenda za kufafanua kuhusu mabadiliko yaliyowaacha nje badhi ya waliokuwa Mabalozi na pia kufafanua kwa kina umuhimu wa Mabalozi wapya waliopatikana sasa na wale waliobaki kutokana na mabadiliko hayo ndani ya Chama.

  Alhaj Bulembo kwenye vikao vya ndani kwenye ziara hiyo alipata fursa za kuwapiga msasa, kwa kuwapa darasa zito Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM katika Wilaya husika, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia zote za Chama, Mabalozi na Watendaji wote wa serikali.

  Mara kadhaa alisisitiza umuhimu wa madiwani kuwa karibu na viongozi wa Chama hasa mabalozi, ikiwa ni pamoja na kuwatambua kwa karibu hadi kwa majina na kujenga mahusiano ya kawaida kwa lengo la kukuza ukaribu baina yao na viongozi hao, siyo tu wa kichama bali hadi wa kifamilia.

  Katika hali ambayo haikuwa ikitarajiwa, katika wilaya karibu zote alizofika, ilionekana dhahiri kwamba madiwani karibu wote walikuwa hawana mahusiano ya kawaida na mabalozi, hali hii ilijidhihirisha pale Alhaj Bulembo alipokuwa akiwasimamisha madiwani na kumuuliza kila mmoja alivyoshiriki kwenye uchaguzi wa mabalozi, idadi ya mashina na majina ya mabalozi katika kata zao.

  Madiwani wengi walijikuta wengine hawajui hata idadiya mashina katika kata zao, na pia walishindwa kutaja idadi ya mabalozi kwenye eneo lao, na kutaja majina ya mabalozi ndiyo ilikuwa kazi kubwa. Diwani alijikuta akitaja balozi mmoja au wawili tu, kata nzima.

  "Mnajua lengo la mahusiano haya, ni kukirahisisha Chama kupata kura kwa urahisi wakati wa uchaguzi, kwa sababu ninyi madiwani mkiwa mmeshajenga mahusiano na Wenyeviti wenu wa mitaa na mabalozi hakutakuwa na kazi ngumu ya kutafuta kura, na lazima mtambue kuwa Mabalozi ndiyo siri kubwa ambayo hufanikisha ushindi wa CCM katika chaguzi", anasema Bulembo kwa nyakati tofauti.

  Mbali na darasa alilokuwa akitoa kwenye vikao hivyo, katika ziara hiyo amewesha CCM kujizolea wanachama wapya 376 ambao walikihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM, wakiwemo waliokuwa viongozi wa Chadema katika vitongoji na Vijiji na aliyekuwa Katibu wa Chadema Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

  Baada ya Makala hiyo fupi yafuatayo ni matukio katika picha katika ziara ya mwisho wa ziara hiyo ambayo Bulembo aliifanya jana katika Wilaya za Mbogwe na Geita mkoani Geita.

  Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisiriki kuapa wakati wanachama wapya waliohamia CCM kutoka Chadema walipokuwa wakiapa na kuungwa mkono na wanachama wote katika kiapo hicho
  Wanachama wapya wa CCM wakiapa
  Wanachama wa CCM wapya wakiapa huku wakiungwa mkono na wanachama wote waliokuwa ukumbini, kula kiapo hicho
  Alhaj Bulembo akimvalisha kofia mmoja wa wanachama hao wapya
  Alhaj Bulembo akiwahoji baadhi ya madiwani kuhusu mahusiano yao ya karibu na mabalozi yalivyo
  Alhaj Abdallah Bulembo akiwa tayari kikabidhi kwa diwani fedha zilizochangwa kwa ajili ya kumsaidia mlemavu mmoja aliyeomba msada wakati wa kikao hicho
  Alhaj Bulembo akikabidhiwa zawadi mwishoni mwa kikao hicho
  Alhaj Bulembo akiagana na baadhi ya wanachama wakati akitoka ukumbini baada ya kikao hicho mjini Geita.
  Alhaj Bulembo akiwa katika Kivuko cha mv Sabasaba tayari kwa safari ya kwenda Mwanza jioni.
  Baadhi ya wandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wa Alhaj Bulembo wakiwa ndani ya Kivuko hicho
  Alhaj Bulembo akiwa ameketi na kiongozi mmoja wa CCM katika kivuko hicho

  Alhaj Bulembo akizungumza jambo na Doto wakiwa kwenye Kivuko hicho

  Alhaj Bulembo akitoka kwenye Kivuko hicho mwishoni mwa safari. PICHA: BASHIR NKOROMO
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdalah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mbogwemkoani Geita, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM, Mbalozi na Watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo, jana, Juni 10, 2017.
  Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea kadi kutoka kwa mmoja wa wanachama sita wa Chadema, waliotangaza kutahmia CCM wakati wa kikao hicho.
  Stephen Thobias akizungumza baada ya kutangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM wakati wa kikao hicho
  Nyambina Chacha akizungumza baada ya kutangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa kikao hicho
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akionyesha kadi za Chadema baada ya waliokuwa wanachama wa chama hicho kumkabidhi na kuhamia CCM wakati wa kikao hicho. Waliosimama mbele ni wanachama hao baada ya kukabidhiwa kadi za CCM
  GEITA🔽
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Alhaj Abdallah Bulembo akivishwa skavu baada ya kuwasili ofisi ya CCM wilaya ya Geita mkoani Geita, jana.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akienda ukumbini baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Geita mkoani Geita, jana
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiingia ukumbini huku akishangiliwa kwa nderemo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili meza kuu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzani, mkoa wa Geita, Mbunge wa Bukombe Doto Biteko na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Wilaya ya Geita Ahmed Mbaraka na Katibu wa CCM Wilaya ya Geita Muhoja mapande
  Alhaj Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuketi ukumbini
  Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Geita AllyRajabu kihamasisha wakati akisaliia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho
  Baadhi ya wajumbe wakiwa ukumbini

  0 0


  0 0


  Kaimu Katibu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Ndg Daniel Zenda aliesimama kushoto akizungumza na Wanachama na Viongozi Makada wa CCM Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Uvccm Mkoa wa Dar es Salaam.

  Kaimu Katibu Idara ya Organaizesheni na Uhusiano wa Kimataifa UVCCM Ndg Mohamed Suleiman akizungumza na Viongozi Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Uvccm Mkoa wa Dar es Salaam .

  Viongozi vyuo na vyuo vikuu wa mkoa wa dar es salaam wakimsikiliza Kaimu katibu Mkuu uvccm Shaka Hamdu Shaka

  Kiongozi wa idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Tawi la Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM ) ndg:Daud Ngasa akizungumzia mambo mbali mbali yahusuyo tawi lake kwa ndg Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka leo alipo kutana naviogozi na wa nachama Mkoa wa Dar es Saaalam

  Meza kuu ikisikiliza


  Kaimu katibu Mkuu uvccm Shaka Hamdu Shaka aliyesimama kulia akizungumza na Viongozi vyuo na vyuo vikuu wa Mkoa wa Dar es salaam jana katika ukumbi wa Uvccm Makao Makuu Upanga Dar es salaam.


  Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka akiagana na Viongozi wa Uvccm Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam.

  PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI

  0 0


  Mchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania na Nahodha wa Taifa stars Mbwana Sammata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema m mwishoni wa wiki iliyopita kuhusu maandalizi yao ya kucheza na Lesotho katika mkutano na waandishi uliofanyika katika makao makuu ya TFF .

  Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema mwishoni mwa wiki iliyopita.


  Mchezaji soka wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Sammata ameihakikishia kampuni ya Bia ya Serengeti ambayo ni wadhamini wa timu ya taifa Taifa Stars kwamba wachezaji wa timu hiyo watajituma ili kuhakikisha kuwa wanashinda mechi zote walizopangiwa kwenye ratiba.

  Samatta ambaye ni nahodha wa timu hiyo ya taifa alitoa hakikisho hilo jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) na kuhudhuriwa na Meneja Masoko wa SBL, Nicholus Machugu. Mkutano huo ulijadili mechi kati ya Taifa Stars na Lesotho timu ambayo Stars inatarajiwa kucheza nayo katika mashindano yajayo.Alithibitisha kuwa timu hiyo haitaiangusha SBL katika mechi zake kwa kuwa kampuni hiyo imeonesha kuithamini kutokana na udhamini wake kwa timu hiyo.

  Aidha alitoa wito kwa wachezaji wenzake kuhakikisha kuwa wanajiweka vizuri kkwa ajili ya mechi hizo ili waweze kuingia na kutambuliwa katika ramani ya soka barani Afrika.

  Samatta ambaye hivi sasa anafanya shughuli zake kama mchezji wa kulipwa nchini Ubeljiji aliinga jijini Dar es Salaam Jumatano ya wiki hii ili kuungana na wachezaji wenzake wa timu ya taifa kwa ajili ya mechi ya duru ya kwanza ya kufuzu mashindano Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Duru ya pili ya mashindano hayo itafanyika Januari 2018 na mechi ya fainali inatarajiwa kufanyika kufanyika Cameroon mwka 2019.

  Kwa upande wake Kocha wa Timu hiyo Salum Mayanga alisema kwamba timu yake imejitayarisha sawasawa kwa ajili ya mechi zote na kuongeza kuwa mazoezi ya timu hiyo iliyoyafanya walipokuwa Alexandria, Misri walikokuwa hivi karibuni hivi karibuni yaliwapa mwanga na ana matarajio makubw kwamba timu hiyo itashinda mechi zote.

  Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ni mashindano ni mashindano makubwa ya kimatiafa barani Afrika. Mashindano hayo yalianzishwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1957.

  Kuanzia mwaka 1967, yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili. Wanachama wa Mashirikisho ya Soka ya FIFA ndio walio na sifa za kushiriki mashindano hayo.

older | 1 | .... | 1267 | 1268 | (Page 1269) | 1270 | 1271 | .... | 1898 | newer