Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

DC MUHEZA AFUTURISHA WAKAZI WA WILAYA HIYO.

$
0
0

 Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 
  Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 
  Wageni wilayani Muheza Mkoani Tanga wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo 
 MKUU wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Saidi katikati anayefuatia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (DAS) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa wakipata futari iliyoandaliwa na mkuu huyo wa wilaya nyumbani kwake.
 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu huyo wa wilaya.
 Baadhi ya waalikwa wakipata futari hiyo
 Baadhi ya wageni waalikwa wakipata futari iliyoandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Wageni waalikwa wakipata futari nyumbani kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza.
 Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Muheza,Makame Seif katikati akiwahudumia wageni waalikuwa kwenye futari hiyo anayepokea chai ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew Mganga
 Waalikwa wakipata futari hiyo wa pili kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,MathewMganga
Wageni waalikuwa kwenye futari hiyo katikati ni Amina Omari Mwandishi wa gazeti la Mtanzania Mkoa wa Tanga na kulia ni Mariam Shedafa kutoka Azam TV Tanga
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiwa na wageni wengine wakishiriki kwenye futari hiyo ambayo iliandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo 
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa shukrani kwa kuitikia mwitikio wa futari hiyo
Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akiagana na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika futari hiyo.

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

SPIKA NDUGAI ATEMBELEWA NA BALOZI MDOGO WA MAREKANI NCHINI TANZANIA LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Inmi Patterson, pale alipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Balozi mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Inmi Patterson, pale alipomtembelea  leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale alipotembelewa na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania, wakiongozwa na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa Sarah Cooke(kulia kwake) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati)akimsikiliza Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Sarah Cooke (wa pili kushoto) pale Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akizungumza na Balozi kutoka Norway, Mheshimiwa Hanne Kaarstad (katikati) na Balozi kutoka Finland Mheshimiwa, Pekka Hukka (kulia) katika kikao kilichofanyika leo ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Hawa Ghasia (wa pili kulia) akiongoza kikao cha pamoja cha mashauriano kati ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja na Wadau wa Mashirika ya Maendeleo Duniani, kutoka Benki ya Dunia (World Bank) na Shirika la fedha la kimataifa (IMF) kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti na Wadau kutoka Mashirika ya Maendeleo Duniani wakiwa katika kikao cha Mashauriano ya pamoja kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Balozi wa China Dkt. Lu Youqing ampongeza Rais Magufuli na Serikali yake kwa bajeti nzuri

MSANII IRENE VEDA AULA UBALOZI WA UTALII KUPITIA BODI YA TAIFA YA UTALII TANZANIA (TTB)

$
0
0
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) Akimkabidhi mkataba Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda mara baada ya kusaini.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) akimwelekeza Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda sehemu za kusaini mkataba wake wa miaka miwili.
Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda(kushoto) akiendelea kusaini mkataba wake .
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) akimalizia kumwelezea Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda sehemu za mwisho za kusaini katika Mkataba huo.
Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda akimalizia kusaini Mkataba wake ili kuanza rasmi kazi za kupeperusha Bendera ya kutangaza Utalii nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) pamoja na Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda wakionesha Mikataba yao baada ya kumaliza kusaini.
Kuona kazi ambazo ameanza kuzifanya bofya

Instagram: www.instagram.com/twendetukataliitz

 Twitter: www.twitter.com/TukataliiTz 

Facebook: www.facebook.com/TwendeTukataliiTz



WANANCHI WA IRINGA WAHAMASIKA KUSAJILIWA VITAMBULISHO VYA TAIFA - USAJILI WAANZA RASMI MANISPAA HIYO

$
0
0
Wananchi wa Manispaa ya Iringa, Mkoani Iringa wamejitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa, baada ya zoezi hilo kumalizika katika Wilaya ya Mufindi iliyokuwa na Kata 36 na kuanza rasmi Manispaa ya Iringa. 

Katibu Tawala wa Manispaa ya Iringa ndugu Joseph Chitinka amefanya ziara kukagua maendeleo ya zoezi hilo na kushuhudia mamia ya wananchi waliofurika katika vituo vya Usajili wakijaza fomu za maombi ya Usajili pamoja na kuchukuliwa Picha, alama za vidole na saini ya Kielektroniki. 

Amesema kama viongozi wamefarijika sana kwa namna wananchi walivyojitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo. 

“ Sisi kama Manispaa tumefarijika sana kwa namna wananchi walivyotuunga mkono kwenye zoezi hili kwa kujitokeza kwa wingi na kuacha shughuli zao kuja kusajiliwa. Hii inaonyesha ni kwa namna gani wananchi wanatambua umuhimu mkubwa wa zoezi hili” alisisitiza. 

Zoezi la Usajili na Utambuzi katika Manispaa ya Iringa limeanza rasmi tangu tarehe 08 Juni 2017 kwa wananchi wa Kata za Kitwiru, Ruaha , Igumbilo, Mshindo, Kitanzini, Mivinjeni na Mlandege. Zoezi la Usajili katika Manispaa ya Iringa limepangwa kumalizika tarehe 30 Juni 2017 kabla ya kuanza Usajili katika Halmashauri ya Iringa. 

Mpango wa usajili katika Manispaa hiyo umepangwa kwa Kata ambapo kila Kata imepangiwa kati ya siku tatu hadi tano za Usajili kutegemeana na idadi ya Watu. 
 Wananchi wa Mtaa wa Kibwabwa A na B Manispaa ya Iringa wakiendelea na hatua za kujaza fomu za Maombi ya Vitambulisho vya Taifa, wakati Usajili wa Vitambulisho cha Taifa ukiendelea katika Manispaa hiyo. Wananchi mbali na kujaza fomu za maombi papo hapo wanapigwa picha, kuchukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki ili kukamilisha Usajili wao.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kitwilu wakiwa katika kituo cha Usajili wakisubiri kusajiliwa wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
 Mtendeji wa Kata ya Kitwilu Ndg. Simba Mansul Nyunza akitoa maelezo ya namna zoezi la Usajili linavyoendeshwa katika Kata yake wakati wa ziara ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndg. Joseph Chitinka.
 Watumishi wa NIDA wakiendelea na zoezi
 Mtendeji wa Kata ya Kitwilu Ndg. Simba Mansul Nyunza akitoa maelezo ya namna zoezi la Usajili linavyoendeshwa katika Kata yake wakati wa ziara ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndg. Joseph Chitinka. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

DKT.KIKWETE -VIWANDA VYA KUSINDIKA MATUNDA VISIWAKANDAMIZE WAKULIMA

$
0
0
Rais mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete akishika Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago -Kiwangwa Bagamoyo .(Picha na Mwamvua Mwiny.
Rais mstaafu wa awamu ya nne dk .Jakaya Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakikimbiza Mwenge wa Uhuru uliopita kutembelea shamba lake la mananasi lililopo Bago -Kiwangwa Bagamoyo .
Kongozi wa mbio za mwenge kitaifa Amor Hamad ,akizungumza baada ya kupata taarifa ya ujenzi ,wa kiwanda cha kusindika matunda cha sayona kilichopo Mboga – Msoga Chalinze ,kutoka kwa afisa uhusiano wa kampuni mama ya MMI ,Abubakar Mlawa
………………………….


Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo 

RAIS mstaafu wa awamu ya Nne ambae pia ni mkulima wa tunda la mnanasi ,dk.Jakaya Kikwete,amewataka wamiliki wa viwanda vya matunda kuacha kuwakandamiza wakulima kwa kununua matunda kwa gharama ya chini .

Amesema viwanda hivyo vinasaidia kupatikana kwa masoko ya ndani lakini vimekuwa havina uwiano wa gharama zinazolingana na maumivu anayoyapata mkulima.Aidha dk. Kikwete ameeleza kumekuwa na changamoto ya kushuka kwa soko kwa wakati mwingine hali inayokuwa ikisababisha wakulima kupata hasara kwa matunda kuoza yakiwa mashambani .

Akitoa taarifa ya shamba lake la mananasi lililipo Bago-Kiwangwa wilayani Bagamoyo ,wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda kutembelea shamba hilo ,alisema kilimo cha matunda kina tija endapo utalima kisasa na kuwa na soko la uhakika .

Kikwete alieleza ,viwanda vya usindikaji matunda mbalimbali ,vinapaswa kumjali mkulima ambae amekuwa akipata shida na kutumia gharama kubwa kuandaa shamba .“Wakati utafika watakosa matunda ,kutokana na gharama yao hailipi ,wakulima wa matunda tushindwa kukubali kuuza kwa bei ya chini ambayo hailipi ” alifafanua .

Rais huyo mstaafu ,alimwambia kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2017 ,Amor Hamad Amor ,kuwa mananasi huvunwa baada ya miezi 18 tangu kupandwa .“Bei ya mauzo hutegemea wanunuzi na wachuuzi wadogowadogo ambao hununua kwa ukubwa wa nanasi sh 400 hadi 800 inapovunwa kutoka shambani .

Dk.Kikwete alisema ,shamba lake lina ukubwa wa hekari 200 ambapo hekar 64 ndizo zimelimwa na zipo kwenye hatua ya palizi .Alisema pia wana chama chao cha wakulima wa matunda Kiwangwa wana ambapo wanamatayarisho ya miche mipya ya kuweza kuuzika nje za nchi.

“Mwenge kwa kuangaza shambani kwangu ni ishara ya nuru ,basi nitapata neema baadae,nashukuru kwa kuja kutembelea shamba langu kujionea shughuli nazofanya baada ya kustaafu” alisema .Kiongozi huyo pia alipita kujionea shughuli za ujenzi wa kiwanda cha Sayona kinachomilikiwa na kampuni MAMA ya MMI steel,kilichopo kata ya Mboga.

Afisa uhusiano wa kampuni za MMI steel ikiwemo Sayona,Abubakar Mlawa ,alimwambia kwamba ,kiwanda cha Sayona kimefikia asilimia 70 ya ujenzi na mwezi novemba mwaka huu kinatarajia kuanza kazi.Alieleza kiwanda hicho,kwasasa kimeajiri watu 100 wakiwemo mafundi ujenzi na kitakapoanza kazi kitaajiri watu 800.

Mlawa alisema,mahitaji makubwa ni matunda zaidi ya tani tisa kwa siku, hasa maembe,nyanya na matunda mengine hivyo wakulima wa matunda wachangamkie fursa hiyo.Alisema kiwanda cha Sayona ni moja ya uwekezaji mkubwa mkoani Pwani,na kinalenga kugharimu dollar mil.55 sawa na sh.bil.120 katika ujenzi wake.

Nae kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Amor Hamad ,alipongeza serikali kwa kuondoa ushuru wa mazao ya matunda na kuongeza kodi kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi hali inayoonyesha taifa kutaka kukuza soko la ndani.Alimpongeza rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Kikwete na kuwataka wakulima wa zao hilo kuiga mfano wake wa kulima kwa tija .

Amor aliwataka wananchi kujishughulisha kwa kufuata nyayo za waasisi wetu akiwemo Kikwete na waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda .“Niipongeze serikali kwa jitihada hizo kwani inaonyesha serikali inataka kukuza soko la ndani la nchi na wakulima kuthaminika  ili kujiletea maendeleo.

Mwenge wa Uhuru june 10,unatarajia kukabidhiwa mkoani Morogoro ,ukiwa Chalinze na Bagamoyo umepitia miradi iliyogharimu bil.128

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha Tano Mwaka 2017 hawa hapa.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNE 10,2017


MANISPAA YA UBUNGO YAINGIA MIKATABA KAZI YA BILIONI NNE

$
0
0

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) akikabidhi mikataba ya Wazabuni, Mwingine ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob (Katikati)
Zoezi la utiliaji saini Mikataba kazi za Manispaa ya Ubungo likiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob (Katikati)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (mwenye maiki?) Akizungumza wakati wa kusaini mikataba kazi, Mwingine ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob na Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Ramadhan Kwangaya

Zoezi la utiliaji saini Mikataba kazi za Manispaa ya Ubungo likiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob (Katikati)

Jana June 10, 2017 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amesaini mikataba ya kazi mbali mbali na makampuni ya Ujenzi, Barabara na Wazabuni 29.

Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya waandishi wa habari katika dhifa iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo Mtaa wa Kibamba CCM, Jijini Dar es salaam.

Katika dhifa hiyo iliyohudhuriwa pia na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob jumla ya mikataba 29 ilisainiwa na wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ambapo kati ya makampuni hayo, Makampuni 14 yamepewa kazi za Billioni 3.2 kwa kazi ya kusafisha barabara na mazingira yote ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuifanya Halmashauri ya Ubungo kuwa katika Hali ya usafi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tukio hilo la kusaini mikataba Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa mikataba kazi hiyo ipo katika makundi matatu ambayo ni miradi ya Maji, Barabara na usafi.

‘’Nawasihi wazabuni wote ambao mtasaini mikataba kazi hapa leo mkatekeleze yale yaliyo katika mikataba yenu ya kazi mimi kama Mkurugenzi sitasita kufuata kanuni na taratibu za kisheria na kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kufuata yale ambayo yako katika mikataba yenu’’ . Alisema Kayombo

MD Kayombo alisema kuwa katika nakubaliano hayo jumla ya Shillingi Millioni 400 zimesainiwa kwa ajili ya uchongaji wa barabara za Mitaa mbalimbali ya Halmashauri na Shilingi Millioni 200 Ni kwa ajili ya Miradi ya upelekaji wa maji katika kata za Mbezi na Mabibo.

Alieleza kuwa Kiasi kingine cha shillingi Millioni 200 ni kwa ajili ya Ukarabati mfumo wa maji Hospitali ya Sinza na ujenzi wa madarasa ya shule ya Sekondari ya Matosa sambamba na Nyumba sita za walimu zilizopo Kata ya GOBA.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob alisema kuwa Manispaa ya Ubungo imeingia katika historia kwa kusaini mikataba kazi hiyo na historia hiyo inatokana na umahiri wa Watumishi wa Manispaa hiyo katika Kusimamia Ukusanyaji wa Mapato na kubana Matumizi ya ruzuku zinazotoka Serikali kuu.

“Manispaa yetu ina miezi nane tu na tayari leo tunasaini mikataba kazi ambayo italipwa kwa fedha zetu za ndani hili ni jambo la kujivunia sana ‘na baada ya miezi michache tutasaini tena mikataba kazi mingine na kwa hii mikataba tunayosaini hapa leo tayari fedha zake zipo kwenye akaunti kwa hiyo ni suala la utekelezaji tu Alisema Jacob.

Alisema kuwa anaamini wote wanaosaini Mikataba hiyo hakuna hata mmoja aliyepenyeza Rushwa au Hongo yoyote na ndio maana mikataba hiyo imesainiwa kwa Uwazi na Ukweli na hakuna hata siku moja Manispaa ya Ubungo itasaini Mikataba kwa kujificga au kwenye giza alisisitiza Mstahiki Boniface Jacob.

Miongoni mwa mikataba kazi ambayo imesainiwa ni Ukarabati wa Mradi wa Maji Goba, Ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa na vyoo shule ya Sekondari Luguluni katika kata ya Kwembe, Ukamilishaji wa Ujenzi wa Madarasa ya shule ya Sekondari Matosa.

Pia ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba za walimu (6 in 1) katika Sekondari ya Matosa, Matengenezo ya Barabara ya Watani Makaburini (Makurumla), ujenzi na ukarabati wa mfumo wa maji katika hospitali ya Sinza, Ujenzi wa kivuko cha Mabibo katika Manispaa ya Ubungo, kutoboa na kuweka maji katika Barabara ya Sam Mujoma na Mandela Manispaa ya Ubungo, Mradi wa maji Mbezi Luiz na Ukarabati wa mradi wa Maji Mabibo Jeshini, Mabibo na Kawawa.

Akizungumza kwa niaba ya wazabuni wenzake, mzabuni wa Kampuni ya Singaruki Investment Ltd alisema kuwa kampuni zote zilizopata kazi katika Manispaa ya Ubungo ni dhahiri kuwa zilistahili kutokana na ufanisi katika utendaji kazi.

Alisema tayari wameshasaini mkataba kazi hivyo jambo la msingi ni kutekeleza yale yote yaliyopo katika mikataba kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za kisheria ambazo zimeainishwa kwenye Mikataba.

Aidha Mkurugenzi Kayombo ametoa siku 14 kwa wakandarasi wote kuhakikisha wanarudisha mikataba ya makubaliano mara baada ya kuisoma na kuielewa sambamba na kujaza mikataba hiyo.


IMETOLEWA NA:

KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

'KITIMOTO' MARUFUKU MAKAO MAKUU YA NCHI DODOMA

RC TABORA ASEMA KUWEKA MAKUNDI KATIKA MABARAZA YANARUDISHA NYUMA MAENDELEO YA WANANCHI

$
0
0
Na Tiganya Vincent, NZEGA

Madiwani katika Halmashauri za  Mkoa wa Tabora  wametakiwa kuepuka kujenga makundi miongoni mwao ambayo yamekuwa yakisababisha wananchi waliowachagua kuchelewa kupata maendeleo kwa sababu ya muda mwingi kushughulikia migogoro badala ya kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya Madiwani na Watendaji wa Manispaa ya Tabora yaliyofanyika wilayani Nzega  kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi jamii ya fursa na vikwazo kwa maendeleo (O&OD) iliyoboreshwa na usimamizi wa fedha za miradi ya maendeleo (LGDG)

Alisema makundi yatawafanya washindwe kuwajibika vizuri na kujikuta miaka mitano ya uongozi wao inakwisha bila kuwafanyia chochote wananachi zaidi ya kupigania kuondoana katika uongozi badala kukazania maslahi ya wananchi.

“Nyie ndio mliko zamu sasa mkiendekeza makundi na migogoro isiyokwisha, mtajikuta zamu zenu zinamalizika hamjawafanyia chochote wananchi waliowachagua badala yake kupambana kila mnapokutana katika vikao vyenu ….kila kikao itakuwa sisi hatumutaki fulani atuongoze au fulani fulani hatufai” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Bw. Mwanri aliongeza kuwa wakimruhusu Shetani wa namna hiyo apite kati yao hakuna tena kazi wala maendeleo kwa wananchi wao waliowachagua.

MAKALA FUPI YA KATIBU MKUU BI SIHABA NKINGA KATIKA MAKAZI YA WAZEE YA NJORO MOSHI NA MAGUGU BABATI

Kamati ya Pili ya Mchanga wa Madini kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Magufuli Jumatatu 12 Juni, 2017

BULEMBO ATINGISHA CHATO, MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA CHADEMA AHAMIA CCM

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alahj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Chato, Wajumbe wa Mabaraza ya Juuia za CCM, Madiwani, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, katika Ofisi ya CCM ya Wilaya hiyo mkoani Geita, leo Juni 9, 2017.
Wajumbe wakishangilia Ukumbini wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Bulembo alipowasulu ukumbini kwenye kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Bulembo akiingia ukumbini kuemdesha kikao hicho, leo
Wasanii wa Kikundi cha CCM, wakitumbuiza kuchangamsha kabla ya kuanza kikao hicho, leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Kasheku Msukuma na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chato Ibrahim Bagula
Ofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania Omari Kalolo akiimba nyimbo za hamasa wakati ajikitambulisha kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chato Ibrahimu Bagula akifungua kikao hicho.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Geita, Mbunge wa Bukombe Doto Biteko akisalimia baada yakutambuishwa kwenye kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Kasheku Msukuma, akimkaribisha Alhaj Bulembo kuzungumza kwenye kikao hicho
Mkuu wa Wilaya ya Chato Shabani akimkabidhi taarifa ya Wilaya hiyo.
Wajumbe ukumbini
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alahj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbewa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Chato, Wajumbe wa Mabaraza ya Juuia za CCM, Madiwani, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, katika Ofisi ya CCM ya Wilaya hiyo mkoani Geita, leo Juni 9, 2017.
Kada wa CCM Paschal Kitandula, akiahidi kumpatia Kiwanja, Chato, Alhaj Bulembo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa kuwa Meneja wa Kampeni ya Rais Dk. Magufuli wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimkabidhi ya Jumuia ya Wazazi mmoja wa wanachama wapya 130 waliojiunga na Jumuia hiyo wakati wa kikao hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Joseph Chacha ambaye alitangaza kuhamia CCM wakati wa kikao hicho. Chacha alikuwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema katika Wilaya za Geita na Chato.
Joseph Chacha akizungumza baada ya kupokewa rasmi ndani ya CCM wakati wa kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alahj Abdallah Bulembo akiagana na badhi ya Wana-CCM baada ya kikao chake na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Chato, Wajumbe wa Mabaraza ya Juuia za CCM, Madiwani, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, katika Ofisi ya CCM ya Wilaya hiyo mkoani Geita, leo Juni 9, 2017. PICHA: BASHIR NKOROMO

TPA WASAINI MKATABA WA UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

$
0
0
Benjamin Sawe-Maelezo

Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imesaini mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha bandari utakaowezesha bandari ya Dar es Salaam kupokea meli kubwa za mizigo na kushindana na bandari nyingine katika pwani ya bahari ya hindi.

Upanuzi huo utakaofanywa na kampuni ya China Harbor Construction ya China utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 336 na utadumu kwa miezi 36, ambapo utahusisha uongezaji wa kina cha lango la bandari na uongezaji wa kina cha maji kati ya gati namba 0, 1 hadi 7.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hatua hiyo inalenga kuifufua upya bandari ya Dar es Salaam ili ifanye kazi kwa ushindani na kuhudumia wateja wengi kuliko ilivyo sasa. 

“ Kukamilika kwa upanuzi na uongezaji wa kina cha maji katika gati namba 1 hadi 7 kutoka mita 8 hadi 15 kutawezesha meli kubwa na za kisasa zenye uwezo wa kubeba hadi makontena elfu kumi na tisa kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam na kuongeza ufanisi na kukuza uchumi wa Tanzania”, amesema Prof. Mbarawa.

Aidha Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu wezeshi ya reli na barabara ili kuhakikisha mizigo haikai muda mrefu bandarini.

“Ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge toka Dare s Salaam hadi Kanda ya Ziwa na Kigoma na ufufuaji wa reli ya Tazara kutawezesha bandari ya Dar e s Salaam kufanya kazi kwa ufanisi na kuvutia wafanyabiashara wengi hivyo nawataka wafanyakazi wote wa bandari kufanyakazi kwa bidii na uadilifu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko amesema kiasi cha dola za Marekani milioni 421, kitapatikana kwaajili ya ujenzi huo ambapo kati ya fedha hizo Benki ya Dunia itatoa mkopo wa masharti nafuu wa dola milioni 345.

Kukamilika kwa ujenzi huo kutaondoa adha ya baadhi ya meli kusubiri kwa muda mrefu kupata nafasi ya kutia nanga na kutaongeza hadhi ya bandari ya Dar es salaam na kuvutia wasafirishaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa (katikati) akishuhudia makabidhiano ya mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mtedaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. XU XINPEI. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA). Mhandisi Deusdedit Kakoko kulia na Mtedaji Mkuu wa Kampuni ya China Harbour Engineering Bw. XU XINPEI wakionyesha mkataba wa makubaliano ya upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kwa wadau wa sekta ya usafirishaji baada zoezi la utiaji saini wa mkataba huo kukamilika. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo). 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Prof: Makame Mbarawa akiongea na wadau wa sekta ya usafirishaji kabla ya zoezi la utiaji saini wa mkataba wa upanuzi na uongezaji wa kina cha Bandari kati ya Serikali na Kampuni ya China Harbour Engineering. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania (TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko na kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Bw. Mkinga Mkinga. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo). 

AFC LEOPARDS USO KWA USO NA GOR MAHIA KWENYE MECHI YA FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP- USHEMEJI POPOTE

$
0
0
Washindi wa nusu fainali za SportPesa Super Cup zilizofanyika Juni 08, 2017 Jijini Dar es Salaam, wanatarajiwa kukutana uso kwa uso kwenye mechi ya fainali ya kuwania kombe la michuano ya SportPesa Super Cup siku ya Jumapili ya tarehe 11, Juni 2017 itakayochezwa kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mechi za nusu fainali, AFC Leopards walipambana na mabingwa wa Ligi kuu Tanzania bara, Klabu ya Yanga na kuwang’oa kwa mikwaju ya penati 4-2 huku Gor Mahia kwa upande wao wakiifungasha virago timu ya Nakuru All Stars FC kufuatia ushindi wa magoli 2-0 ambayo yalitiwa kimiani na mshambuliaji Medie Kagere na George Odhiambo.     

Timu za Yanga na Nakuru All Stars FC ambazo ziling’olewa kwenye hatua ya nusu fainali, zilikabidhiwa medali za shaba na kiasi cha dola za kimarekani 5000 wakati wenzao (Gor Mahia na AFC Leopards) ambao wamefuzu kucheza fainali wakiwania kiasi cha dola za kimarekani 30,000.

Akizungumzia mshindano ya SportPesa Super Cup kwa ujumla, Mkurungezi wa Utawala na Utekelezaji SportPesa Tanzania Ndugu Abbas Tarimba alisema; “Michuano ilikuwa migumu ingawa timu zetu za Tanzania zimeaga katika hatua za awali lakini ni nafasi nzuri kwetu kama Tanzania kujipanga vizuri zaidi ili kuboresha sekta ya michezo na kufanya timu zetu kushika nafasi za juu maana kwa sasa tumeweza kutambua changamoto mbalimbali na jinsi ya kuzikabili.

SportPesa ni kampuni nguli ya michezo ya kubashiri inayojulikana kimataifa yenye makao yake makuu nchini Kenya ambayo imeanza rasmi shughuli zake nchini Tanzania Mei 9 mwaka huu na mpaka sasa imeshaingia makubaliano rasmi ya udhamini na vilabu vya Simba, Yanga na Singida United ikiwa imejidhatiti katika kuinua ba kuendeleza sekta ya michezo nchini.

Wafamasia Watakiwa kuzingatia Maadili

$
0
0
Msajili wa Baraza la Famasi Tanzania Bi. Elizabeth Shekalaghe akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wafamasia wanaotarajiwa kuanza kutoa huduma mara baada ya kuhitimu masomo yao na kula kiapo cha kuzingatia maadili ya taaluma hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Msajili wa Baraza hilo Bi. Zainabu Nyamungumi akiwasilisha mada katika mafunzo ya siku moja kwa wafamasia wanaotarajiwa kuanza kutoa huduma baada ya kuhitimu masomo yao na kula kiapo,Leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Usajili wa Baraza hilo Bw.Rashid Kiria akitoa ufafanuzi kuhusu mafunzo hayo.
Mmoja wa wafamasia hao akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam.

…………………………………………………………………………..

Frank Mvungi-Maelezo

Wafamasia nchini wametakiwa kuzingatia maadili na weledi katika kutekeleza majukumu yao ili kuchochea azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kutoa huduma bora za afya kote nchini hali itakayochea maendeleo na ukuaji wa sekta hiyo.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Msajili wa Baraza la Famasi nchini Bi. Elizabeth Shekalaghe wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa wafamasia waliohitimu masomo yao hivi karibuni katika vyuo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi na kula kiapo cha kuzingatia maadili ya taaluma hiyo adhimu kwa mustakabali wa ukuaji wa sekta ya afya hapa nchini.

“Mafunzo haya yamehusisha takribani wafamasia 160 na yanalenga kuwakumbusha wajibu wao na umuhimu wa kuzingatia maadili na kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza wakati watakapokuwa wanatekeza majukumu yao kwa kuwa wapo watakafanya kazi katika Mikoa, Halmashauri na Hospitali katika maeneo mbalimbali “ alisisitiza Shekalaghe.

Akifafanua amesema kuwa mafunzo hayo yameshafanyika katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Kaskazini,Mashariki na Kanda ya Ziwa dhamira ikiwa kuwajengea uwezo wafamasia wanaohitimu kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao mara baada ya kula kiapo.

Aliongeza kuwa jukumu la Baraza hilo ni kufuatilia mwenendo wa wafamasia ili kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili ya taaluma hiyo na wamiliki wa maduka ya dawa kuhakikisha kuwa wanaajiri wafamasia wenye sifa na waliosajiliwa ili watoe huduma bora kwa mujibu wa sheria na kanuni.

Kwa upande wake Naibu Msajili wa Baraza hilo Bi. Zainabu Nyamungumi akiwasilisha mada katika mafunzo hayo amesisitiza umuhimu wa wafamasia kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu zinazosimamia taaluma hiyo katika maeneo watakayokuwa wanafanya kazi.

Pia aliwataka kutekeleza kwa vitendo yale waliyofundishwa katika mafunzo hayo ili kuchochea ukuaji wa taaluma hiyo.

Naye mdau wa Taaluma hiyo ambaye pia ni mwanataaluma Bw. Manase Kejo iliwataka wafamasia hao kujiamini na kujiajiri kwa kuwa taaluma waliyo nayo ni fursa inayoweza kuzalisha ajira.

“Ni muhimu mkatambua kuwa taaluma hii ni muhimu na jambo kubwa ni kutambua kuwa mnaweza kujiajiri,” Alisisitiza Kejo.

Mwaka 2013 Tanzania ilikuwa na wafamasia takribani 450 na kufikia mwaka 2017 wamefikia 1600 hali inayoonyesha kuwa taaluma hiyo inaendelea kukua kwa kasi suala linalochagizwa na ongezeko la vyuo vinavyotoa taaluma hiyo kikiwemo Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma, Bugando na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili.

WATANZANIA WASHAURIWA KUBADILI MTAZAMO KUHUSU UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0
Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Prof. Honest Ngowi (aliyesimama) akizungumza katika Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji. Wengine picha ni watoa mada mbalimbali walioshiriki katika Kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (aliyesimama) akichangia nafasi ya Benki yake katika kuchagiza uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt. Jim Yonazi akizungumzia nafasi ya TSN katika kuwezesha juhudi za Serikali katika kuwawezesha wananchi kiuchumi ambapo alisema kuwa Shirika lake lina uwezo na teknolojia ya hali ya juu katika kuwafikia sehemu kubwa ya watanzania. Alitoa wito kwa taasisi za umma na binafsi kutumia nafasi hiyo kuwafikia walengwa wa huduma zao
Baadhi ya Manaibu Mawaziri wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
Baadhi ya wadau wa taasisi za uwezeshaji wananchi kiuchumi wakifuatilia kwa makini Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.
Baadhi ya wadau wa taasisi za uwezeshaji wananchi kiuchumi wakifuatilia kwa makini Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji.

……………………………………………………………………………

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Wito umetolewa kwa Watanzania hasa kwa wadau wanaojihusisha na uwezeshaji wananchi kiuchumi kubadili mitazamo juu ya namna sahihi ya kuwawezesha wananchi hao katika kutimiza lengo la serikali la kuwainua wananchi kiuchumi ili kuimarisha kipato na kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Wakizungumza katika Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji linalofanyika mkoani Dodoma wadau hao wamesema kuwa kuna ulazima wa wadau hao kujua mahitaji sahihi ya wananchi wanaohitaji huduma za uwezeshaji wa kiuchumi kwa kuwa kila kundi lina mahitaji yake.

Mwezeshaji wa Kongamano hilo, Prof. Honest Ngowi amesema kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi yoyote unazingatia mahitaji maalumu ya kila sekta ya kiuchumi na kutolea mfano kuwa wakulima nchini hawahitaji rasilimali fedha pekee ili kuongeza tija katika kilimo chao bali wanahitaji masoko ya uhakika ya mazao yao.

“Uzoefu kutoka kwa watekelezaji wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi unaonesha kuwa rasilimali fedha si kila kitu pekee katika kuwawezesha wananchi kiuchumi bali kila kundi linahitaji mahitaji yake, mfano mkulima anahitaji soko la mazao yake ili aweze kuongeza tija kwenye kilimo chake,” alisema Prof. Ngowi.

Akichangia mjadala huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki yake ina Dira ya kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kwa kuwawezesha wananchi kwa kuzingatia mahitaji maalumu kuendana changamoto za kimaeneo hili kuwezesha wananchi kiuchumi nchini ili kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali kuwafikisha wananchi wake kufikia hadhi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

“Muundo wa TADB ni tija katika kuchagiza uwezeshaji wananchi kiuchumi hasa wakulima wadogo nchini kwani Benki inafanyia kazi mnyororo mzima wa ongezeko la thamani katika kilimo kwa kutatua changamoto mbali mbali kama vile kiwango kidogo cha uzalishaji; ukosefu wa mbinu na teknologia za kisasa; matumizi madogo ya umwagiliaji,” alisema

Aliongeza: “Changamoto nyingine ni ukosefu wa mtaji na upatikanaji wa mikopo kwa wakulima; ukosefu wa masoko ya mazao; ufinyu wa bei za mazao; miundo mbinu mibovu ya usafirishaji; maghala ya kuhifadhi mazao; nishati ya umeme na miundombinu hafifu vijijini; ufinyu au kutokuwepo kwa ongezeko la thamani kwa mazao ya kilimo; mabadiliko ya hali ya hewa; na mmomonyoko wa udongo, pamoja na changamoto zinginezo,” aliongeza.

Kuanza kufanya kazi kwa Benki ya Kilimo kunaleta suluhisho la changamoto nyingi zilizokuwa zinaikabili sekta kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kama inavyowekwa bayana na dhima ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambayo inalenga kuwaongoza watanzania katika kujenga uchumi wenye nguvu kwa kuboresha mazingira ya kibiashara na kutoa fursa sawa za kiuchumi.

Kongamano la Mwaka la Uwezeshaji linafanyika katika kutekeleza Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi iliyoundwa mwaka 2004 na Sheria ya Uwezeshaji namba.16 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Awajulia Hali Watoto Wanawaosubiri kufanyiwa Upasuaji Wa Moyo Katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpokea Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza jinsi wanavyotoa huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto Doreen Sostenes (3) ambaye Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto Doreen Sostenes (3) ambaye Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimtazama mtoto Johnson Raphael (6) akichora picha ya mtu wakati alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo ili kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto Zuwena Said (4) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto Abdukarim Mahilo (2) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo huku Mama wa mtoto Fatuma Bakari akiangalia.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea na Maria Gervas ambaye ni mama wa Doreen Sostenes (3) anayelipiwa gharama za upasuaji wa Moyo na Tulia Trust Fund. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja akimuelezea Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson magonjwa mbalimbali ya moyo yanayowasumbua watoto. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimbembeleza mtoto Venance Christopher (14) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea jambo wakati akimjulia hali mtoto Rashid Kombo aliyelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Sulende Kubhoja.
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto Godwin Sharau alipotembelea leo chumba cha upasuaji wa Moyo kilichopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI).

Picha na JKCI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu EWURA

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images