Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Wasindikaji Wadogo 1287 Wanufaika na TFDA

0
0
Na Frank Mvungi-Maelezo

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imetoa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula 1287 tangu mwaka 2013 ili waweze kusindika vyaklula vyenye ubora kwa mujibu wa sheria na kanuni za uzalishaji na kuhimili ushindani wa soko.

Akifungua mafunzo ya wasindikaji wadogo wapatao 60 wa vyakula yaliyoratibiwa na Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Bw. Raymond Wigenge, amesema dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini.

“Kukua kwa viwanda hivi kutakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ajira na kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha mazao ya chakula kutokana na kuwepo kwa soko la mazao ya vyakula”. Alisisitiza Wigenge.

Akifafanua Wigenge amesema Serikali inatambua kuwa viwanda vidogo vina nafasi kubwa ya kuchangia pato la Taifa hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inasisitiza ujenzi wa uchumi wa Viwanda.

Alieleza kuwa Mamlaka hiyo imeingia mkataba wa maridhiano (MOU) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambapo mchango wa taasisi hizo mbili utatambuliwa katika tasnia ya ujasiriamali wa bidhaa zinazodhibitiwa na Mamlaka.

“Katika makubaliano tuliyofikia kati ya TFDA na TBS ambapo kuanzia sasa mamlaka yetu itatumia matokeo ya vipimo vya maabara za TBS kusajili bidhaa husika na TBS itazingatia usajili wa TFDA wa jengo la bidhaa wakati wa kutoa alama ya ubora”. Alisisitiza Wigenge.

Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Chama Kuweka na Kukopa cha Wajasiliamali Wadogo Wanawake Tanzania (TASWE) na mwakilishi wa wanawake wajasiriamali Bi. Anna Matinde amesema kuwa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo yana umuhimu katika kuchochea maendeleo ya Viwanda hapa nchini.

“Sasa tumeona juhudi za Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini na tunapongeza hatua hizi ikiwemo kuandaa mafunzo haya na tumeona kweli kuna mabadiliko makubwa katika kuwawezesha wajasiriamali”. Alisisitiza Matinde.

Alieleza kuwa kwa ni vyema wajasiriamali wakaunga mkono juhudi hizo ili waweze kunufaika na uwezeshwaji unaofanywa na Serikali kwa wajasiriamali wote bila kujali ni wadogo au wa kati na hata wakubwa.Mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo ya siku moja ni pamoja na taratibu za usajili wa majengo ya vyakula, usajili wa vyakula, utaratibu wa utoaji wa alama ya ubora na teknolojia ya usindikaji wa vyakula.

Mafunzo hayo yamefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma, Rukwa, Manyara, Lindi,Mtwara,Tanga, Singida, Iringa, Kigoma, Kilimanjaro, na Morogoro.
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond Wigenge akifungua mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula (hawapo pichani) ambayo yaliatibiwa na Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Justin Makisi akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa mafunzo kwa wasindikaji wadogo wa vyakula.
Mwenyekiti wa Chama cha Kuweka na Kukopa Wajasiriamali Wadogo Tanzania (TASWE) na muwakilishi wa wanawake wajasiriamali Bi. Anna Matinde akipongeza juhudi za Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka hiyo Bw. Raymond Wigenge na kushoto ni Afisa Udhibiti Ubora Bi. Prisca Kuela
Baadhi ya wajasiriamali wakifuatilia mafunzo yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kwa wasindikaji wadogo wa vyakula .
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond Wigenge akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo wakati wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula.(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)

RC ANNA MNGWIRA ATEMBELEA FAMILIA YA DKT NDESAMBURO,AZUNGUMZA NA WANACCM KILIMANJARO.

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi alipotembelea ofisi za chama hicho kujitamburisha .kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Idd Juma ,na anayefuatia ni Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi,Aisha Amour.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Moshi,Elizabeth Minde (katikati) akifurahia jambo wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira (hayupo pichani) alipokutana na uongozi wa chama hicho katika ofisi za CCM-Mkoa wa Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro ,Idd Juma akitoa neon la shukrani mara baada ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mngwira kutembelea ofisi za chama hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira akitoka ofisi za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuonana na viongozi wa chama hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna mngwira akisalimaiana na Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro alipofika nyumbani kwa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo kutoa pole kwa familia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mngwira akisalimiana na mtoto wa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo ,Sindato Ndesamburo alipotembelea nyumbani kwa marehemu kutoa pole kwa familia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akitia saini katika kitabu cha waombolezaji mara baada ya kufika nyumbani kwa Marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole kwa familia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna mngwira akizungumza jambo na mjane wa Marehemu Dkt Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo alipofika nyumbani kutoa salamu za pole kwa familia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,akitembelea kaburi ulipolazwa mwili wa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo alipofika nyumbani kutoa salamu za pole kwa familia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akiongoza sala katika kaburi la marehemu Dkt Philemon Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mngwira akimpa mkono wa pole Mbunge wa viti maalumu na mtoto wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Lucy Owenya alipofika kutoa salamu za pole kwa familia y marehemu.
Mbunge wa Viti Maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akizungumza jambo na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira alipofika kutoa salamu za pole kwa familia.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akisalimiana na wananchi katika neo la Kwa Alphonce wakati akiwa njiani akitoka kutoa salamu za pole kwa familia ya Dkt Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mngwira akiwa katika picha ya pamoja na wananchi alipowasalimia katika eneo la Kwa Alphonce mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akizungumza na mmoja wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro aliposhuka kwenye gari kuwasalimia.
Na Dixon Busagaga wa Busagaga's Orijino Blog.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JUNE 9, 2017

0
0

BULEMBO AMALIZA ZIARA MKOANI KAGERA KWA KUUNGURUMA NA WAJUMBE WA BUKOBA VIJIJINI NA MULEBA, LEO

0
0
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akivalishwa Skavu alipokuwa kwenye mpaka wa Wilaya ya Bukoba Mjini na Wilaya ya Muleba, leo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akitangulia kwenda kupanda gari baada ya kuvishwa skafu
Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo kwenda Mjini Muleba ukitokea Bukoba mjini, leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba Muhaji Bushako aliyekuwa akimweleza jambo, wakati wa kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Muleba, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM na Watendaji wa Serikali, mjini Muleba, leo
Afisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania  Fadhili Mlami akisalimia wajumbe baada ya kutambulishwa kweye kikao hicho. Kulia ni Katibu wa Siasa na Oganaizesheni Makao Makuu ya Jumuia hiyo Daniel Mgaya
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Muleba mkoani Kagera, Bakari Juma, akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezwaji wa miradi mbalimbali katika Manispaa hiyo, alipoalikwa kutoa maelezo kwenye kikao hicho, leo 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimvisha shati la CCM Njami Mabula, ambaye yeye na wenzake saba walipokewa na Alhaj Bulembo baada ya kutangaza kuihama Chadema na  kujiunga na CCM, kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimvisha pama ya CCM Bushako Njami, ambaye yeye na wenzake saba walipokewa na Alhaj Bulembo baada ya kutangaza kuihama Chadema na  kujiunga na CCM, kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wapya aliowapokea baada ya kutangaza kuihama Chadema na  kujiunga na CCM, kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimpongeza Diwani wa Kata ya Karamba  Felix France, kwa kufanikisha wanachama hao wa Chadema kuhamia CCM kwenye kikao hicho mjini Muleba mkoani Kagera, leo
Katibu wa CCM mkoa wa Kagera  Rahel Ndegereka akifanya utambulisho wakati wa kikao hicho.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Constasia Buhiye akifua rasmi kikao hicho
katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania mkoa wa Kagera akimkabidhi kitenge Kwa Mama Buhiye ili akikabidhi kwa Alhaj Bulembo ikiwa ni zawadi kutoka kwa Nina Mama wa UWT wa mkoa huo.
Alhaj Bulembo akikifurahia kitenge hicho baada ya kukabidhiwa
Alhaj Bulembo akikabidhiwa pia kitambaa kwa ajili ya kushonea suti

Alhaj Bulembo akifurahia zawadi ya Kahawa aliyozawadiwa
Ukumbi ukilipuka kwa nderemo na vifijo baada ya zawadi hizo kukabidhiwa
Meza Kuu nao wakisimama kuunga mkono nderemo hizo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe katika kikao hicho, mjini Muleba mkoani Kagera, leo
KIKAO CHA BUKOBA VIJIJINI🔽
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini Novatus Mkwama, akizungumza wakati wa kufungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya hiyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, kikao kilichofanyika Bukoba mjini leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo na kulia ni Katibu wa CCM Mstaafu mkoa wa Kagera Faustine Kamaleki na Katibu wa CCM mkoa huo Rahel Ndegereka.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini Novatus Mkwama, akizungumza wakati wa kufungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya hiyo, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za CCM, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, kikao kilichofanyika Bukoba mjini leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo na kulia ni Katibu wa CCM mkoa huo Rahel Ndegereka.
Kikosi kazi cha mambo ya habari kikiwa kazini nje ya ukumbi wakati wa mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza wakati wa kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Costansia Bihiye na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Vijijini Novatus Mkwama.
Sekretarieti ya CCM Bukoba Vijijini ikiwa kazini wakati wa kikao hicho
Wajumbe wakimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo wakati akizungumza nao kwenye kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza wakati wa kikao hicho
Wajumbe wakimsikliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo alipokuwa akizungumza wakati wa kikao hicho
Maofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Tanzania, wakiwa kwenye kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati akizungumza wakati wa kikao hicho. PICHA: BASHIR NKOROMO

Waratibu Elimu Kata, Waganga wa Vituo vya Afya Wapewa Elimu ya Uhasibu

0
0
Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa akizungumza na waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC (hawapo pichani) kuhusu malengo ya kuanzishwa kwa mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).
Baadhi ya Waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje (hayupo pichani) wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).
Baadhi ya Waratibu wa Elimu Kata kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje (hayupo pichani) wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).
Sehemu ya Waratibu wa Elimu Kata na Waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na Mtwara DC wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje (hayupo pichani) wakati alipofungua mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mhandisi Sambwe Sijabaje (aliyeketi katikati) akiwa pamoja na baadhi ya waratibu wa elimu kata kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kuhusu namna ya kuutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS). Aliyeketi kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa


Na Mathew Kwembe, Mtwara

Waganga wafawidhi wa vituo vya afya, na Waratibu elimu kata kutoka Halmashauri 93 zilizo katika mikoa 13 nchini inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) nchini wameanza mafunzo ya siku mbili juu ya namna ya kutumia mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS).

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Tehama na Mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa, mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma na kusaidia upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi ya halmashauri.

Bwana Wengaa alisema kuwa kuunda kwa mfumo huo kutasaidia kuhakikisha fedha za ruzuku zinasimamiwa vizuri na taarifa za matumizi yake zinatolewa kwa usahihi tofauti na ilivyokuwa mwanzo.Alisema kuwa FFARS itawapatia watoa huduma mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawawezesha kutunza taarifa za fedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vyao. 

Bwana Wengaa aliongeza kuwa FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na sheria za manunuzi na utoaji taarifa. “Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, na hivyo watoa huduma wa afya kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia,” alisema.

Alisema kuwa mafunzo hayo yanafanyika katika Mikoa 13 ya Tanzania Bara inayotekeleza Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) ambapo waratibu elimu kata na waganga wafawidhi wa vituo vya afya wanashiriki.Aliitaja mikoa hiyo 13 kuwa ni pamoja na Mtwara, Lindi, Dodoma, Iringa, Mbeya, Njombe na Morogoro. Mikoa mingine ni Mara, Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Kigoma, na Kagera.

Mafunzo hayo yanafanyika katika ngazi ya halmashauri, ambapo mjini Mtwara mafunzo hayo yaliwahusisha waganga wafawidhi wa vituo vya afya, na Waratibu elimu kata kutoka Halmashauri za Manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bibi Beatrice Dominick, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mhandisi Sambwe Sijabaje alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia watoa huduma wa vituo vya halmashauri hizo mbili kuwa na mfumo maalum wa kuandaa taarifa za mapato na matumizi, na hivyo kuchangia uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa mfumo wa kielektroniki ili kuendana na wakati na mabadiliko ya teknolojia na mfumo wwa kujaza vitabu ulioboreshwa ili kukidhi changamoto mbalimbali za miundombinu ikiwemo umeme na kukosekana kwa huduma ya mtandao wa intaneti kwa baadhi ya vituo vya kutolea huduma.

Hata hivyo baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka Halmashauri za Manispaa ya Mtwara Mikindani na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wameiomba Serikali kuwapatia vitendea kazi kama vile Laptop ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi uliokusudiwa.

Mfumo huo wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwanufaisha Waganga wafawidhi wa vituo vya afya, na Waratibu elimu kata kutoka zaidi ya Vituo vya Afya 550, Zahanati 6800, Hospitali za Wilaya 135, na takribani Shule za Msingi na Sekondari 20,000 katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MASHINDANO YA UMISSETA NA UMITASHUMTA NGAZI YA TAIFA

0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya mpira kutoka kwa Afisa Masoko Msaidizi wa kampuni ya soda ya Coca Cola Bi. Pamela Lugenge kama ishara ya kuendeleza michezo nchini na pia kwa ajili ya kumsaidia kuendeleza mazoezi yake binafsi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassanakirusha mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Vijana wakionesha utayari wao wa kushiriki michezo wakati wa mashindano ya 38 ya UMISSETA na ya 22 ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

DIRECT PAY ONLINE GROUP [DPO] MDHAMINI WA KILIFAIR 2017 DARAJA LA PLATINAMU

0
0







Waziri wa Maliasili na Utalii,Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na maafisa wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) ambaye ni Mkuu wa Masoko na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Eran Feinsten (wa pili kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaloyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia taerehe 2 Juni, wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Direct Pay Online, Kate Gathii (kushoto) alipotembelea banda la kampuni hiyo ambao ni platnimu sponsor wa maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi kuanzia tarehe 2 June. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo,Eran Feinsten,wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii (TTB) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na Mkuu wa wilaya ya Moshi. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Direct Pay Online Group, Eran Feinsten (kushoto) jinsi wanavyotumia mfumo wa mawasiliano kutuma na kupokea fedha katika banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Utalii na Viwanda ya Kili Fair yaliyofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi katikati ni Mkuu wa wilaya ya Moshi, Kippi Warioba.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUTURISHA KWENYE VIWANJA VYA BUNGE

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Balozi wa Morocco nchini, Mheshimiwa Abdelilah Benrwayane katika futari aliyoiandaa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Juni 8, 2017.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge, Azan Mussa Zungu (kulia kwake), Mbunge wa Mbarali, Haroon Mulla Pirmohamed (wapili kushoto) na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa, Valentino Mlowola katika futari iliyoandaliwa wa Waziri Mkuul Kassim Majaliwa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mbunge wa Nsimbo, Mhandisi Richard Mbogo baada kufuturisha kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) IMETOA GAWIWO LA SHILINGI BILIONI 1.7 KWA SERIKALI

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Tifa (NIC) Bw. Sam Kamanga, akizungumza jambo wakati wa tukio la Shirika hilo kukabidhi gawiwo kwa Serikali, kiasi cha Sh. Bil. 1.7, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha, mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (MB) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, katika hafla ya makabidhiano ya gawiwo la Sh. Bil.1.7 liyofanyika mjini Dodoma.
Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakishiriki tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kufanya vizuri kibiashara katika Mwaka wa Fedha 2016/2017, tukio lililofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, mjini Dodom
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Doroth Mwanyika, akifurahia jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuikabidhi Serikali gawiwo la Sh. Bil. 1.7 baada ya Shirika hilo kupata faida katika mwaka wa fedha 2016/2017
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akisisitiza jambo wakati wa tukio la Shirika la Bima la Taifa (NIC) kukabidhi Serikalini gawiwo la Sh. bil. 1.7, baada ya Shirika hilo kupata faida kibiashara katika mwaka wa Fedha 2016/2017, Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akitoa neno la Shukrani kwa uongozi Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa ubunifu na uwajibikaji wao ulioliwezesha Shirika hilo kupata faida na kutoa gawiwo kwa Serikali, Mjini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

……………………….

Na Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma

SERIKALI imeendelea kupata neema kutokana na uwekezaji wake kwenye mashirika na taasisi mbalimbali yanayojiendesha kibiashara nchini ambapo leo Shirika la Bima la Taifa (NIC) limetoa gawiwo la Shilingi bilioni 1.707 baada ya kupata faida kiabishara mwaka 2016/2017.

Kwa nyakati tofauti mwaka huu, Serikali ilipokea kiasi cha Shilingi bilioni 1.7 kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kufuatiwa na NMB Bank Plc, iliyotoa kiasi cha Shilingi bilioni 16.5 hivi karibuni.

Akipokea Hundi kifani ya kiasi hicho cha Shilingi 1.707 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa, Bw. Sam Kamanga, Waziri wa Fedha na Mipango, amelipongeza shirika hilo kwa kuonesha maendeleo makubwa katika kipindi kifupi tangu azindue Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo mwishoni mwa mwaka uliopita.

“Nilipozindua Bodi yenu ya Wakurugenzi uliniahidi Mkurugenzi Mtendaji kuwa mtafanyakazi kwa bidii na kuanza kutoa gawiwo Serikalini, ninajisikia furaha sana kwa niaba ya watanzania kuona kuwa mnatimiza ahadi hiyo kwa kutoa asilimia 15 ya pato ghafi la mapato yenu. Nawapongezeni sana” alisisitiza Dkt. Mpango.

Alizitaka taasisi nyingine za umma zilizochini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina zinazofikia 260 kuanza kutumia huduma za bima kupitia Shirika la Bima la Taifa.

Alisema anafahamu kwamba kuna taasisi nyingine zina mikataba na mashirika mengine ya bima lakini akatoa wito kwa taasisi hizo kwamba baada ya kumaliza mikataba yao, waanze kupata huduma kupitia NIC ambalo manufaa yake yameanza kuonekana baada ya kuanza kurejesha sehemu ya faida yake kwa Serikali.

Hata hivyo Dkt. Mpango aliitaka NIC lisibweteke badala yake liboreshe huduma zake ili kuweza kujiongezea soko kwani mashirika ya bima yamekuwa na ushindani mkubwa.

Alilitaka Shirika hilo kutoa elimu kwa Umma wakiwemo wakulima, wafugaji na wananchi wengine kuhusu umuhimu wa kukatia bima mifugo, mazao, nyumba na vyombo vya moto ili kujiepusha na hasara zinazoweza kutokea wakati wa majanga.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alisema kuwa tukio hilo ni la kihistoria kwa Shirika hilo kutoa gawiwo kwa Serikali tangu lianzishwe miaka 54 iliyopita na kuzitaka Taasisi zote zilizo chini ya Wizara kuiga mfano wa NIC.

“Naamini leo ndiyo mmezaliwa na mna miaka mingine 100 mbele ya kutenda kwa ajili ya watanzania” Alisisitiza Dkt. KIjaji

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James alilipongeza Shirika hilo na kusisitiza kuwa Wizara ipo bega kwa bega kushirikiana nao ili kuhakikisha Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi kifani, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Bw. Sam Kamanga, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuzihamasisha Taasisi za Umma kukata bima NIC, na kwamba hatua hiyo ndiyo imeliwezesha shirika kutengeneza faida na kutoa gawiwo kwa Serikali.

Hata hivyo ameiomba Serikali kuyahamasisha mashirika zaidi ya 200 yaliyochini ya Msajili wa Hazina kutumia huduma za Taasisi yake ili kuongeza wigo wa mapato na kuleta faida zaidi kwa wabia wa Shirika hilo

“Ni Taasisi 15 tu ndizo zilizoitikia wito wa Serikali wa kutumia huduma za bima kupitia NIC lakini mashirika na taasisi nyingine bado hivyo ninaiomba Serikali itusaidie kufanikisha jambo hili” Alisistiza Bw. Kamanga.

Aliiahidi Serikali kwamba Shirika lake linatarajia kuongeza gawiwo zaidi za kiasi hicho kilichotolewa kutokana na mikakati kabambe ya kiabiashara waliyojiwekea.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WAPUNGUA HADI ASILIMIA 6.1

0
0
Na Benjamin Sawe

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2017 umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2017. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Aprili, 2017.

“Mfumuko wa Bei wa Taifa umepungua kutoka asilimia 6.4 kwa mwezi Aprili, 2017 hadi kufikia asilimia 6.1 kwa mwezi Mei , 2017 kutokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Mei, 2017,” amesema Kwesigabo. Kwesigabo amesema Mfumuko wa Bei wa mwezi Mei, 2017 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.2 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.5 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2017.

Amesema Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 109.26 kwa mwezi Mei, 2017 kutoka 109.04 mwezi Aprili, 2017 kutokana na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Kwesigabo ametaja bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi kuwa ni pamoja na mahindi yaliyoongezeka kwa asilimia 4.2, maharage mabichi kwa asilimia 2.9, maharage ya soya kwa asilimia 2.2, unga wa mtama kwa asilimia 1.5, viazi mviringo kwa asilimia 2.0, mihogo mikavu kwa asilimia 2.3, na magimbi kwa asilimia 2.5.

Aidha bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na mkaa ulioongezeka kwa asilimia 2.5. Ameongeza kuwa Mfumuko wa Bei kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Mei, 2017 umepungua hadi asilimia 11.8 kutoka asilimia 12.0 mwezi Aprili, 2017. Aidha, badiliko la Fahirisi za Bei kwa bidhaa zisizo za vyakula umepungua hadi asilimia 3.0 mwezi Mei, 2017 kutoka asilimia 3.4 mwezi Aprili, 2017.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo akiongea na wanahabari kuhusu Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Mei 2017 jijini Dar es Salaam leo.

WAZIRI MKUU AFUNGUA SEMINA YA MTANDAO WA WABUNGE AFRIKA TAWI LA TANZANIA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Semina ya Mtandao wa Wabunge Afrika Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC). Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Akson na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, Kulia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC) Kepteni Mstaafu (MB) John Mkuchika, na Mbunge wa wa Manyoni Mashariki Daniel Mtuka Nyuma walio simama ni waBunge wanao shiriki Semina hiyo ya siku Mbili ambayo inaendeshwa na UNDP. PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimina na Mshauri wa Maswala ya Bunge kutoka ofisi ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania ,Bibi Anna Hovhannesyan , baada ya kufungua Semina ya Mtandao wa Wabunge Africa Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC) Semina hiyo ya siku mbili inafanyika Mkoani Dododma katika ukumbi wa Hoteli ya African Dreams . June 9, 2017 na June10,2017 nakuendeshwa na UNDP.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki ,baada ya kufungua Semina ya Mtandao wa Wabunge wa Africa Tawi la Tanzania walio katika Mapambano Dhidi ya Rushwa (APNAC) katikati ni Naibu Spika Dr Tulia Akson, Semina hiyo ya siku mbili inafanyika Mkoani Dododma katika ukumbi wa Hoteli ya African Dreams . June 9, 2017 na June10,2017 nakuendeshwa na UNDP.

BULEMBO AANZA ZIARA MKOANI GEITA, LEO APIGA MIKUTANO WILAYANI BUKOMBE

0
0
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo na msafara wake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM na Jumuia zake mkoa wa Kagera, wakati wakiagana tayari kuingia katika mkoa wa Geita leo asubuhi.
 Alhaj Abdallah  Bulembo akiagana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera
 Mwandishi wa Star Tv Abdallah Tilata aliyeko kwenye msafara wa Alhaj Abulembo akiagana na Katibu Tawala wa Halmashari ya Wilaya ya Muleba Benjamin Mwikasyele kabla ya mafara kwenda mkoani Geita
 Mwandishi wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo Happines Mtweve akiagana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera
 Ben Mugisha ambaye ni Dereva wa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Bulembo, akiagana na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Rahel Ndengeleka.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari walioko kwenye msafara wa Alhaj Bulembo wakiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa Chama na Jumuia mkoa wa Kagera
RASMI MKOANI GEITA🔽
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM na Jumuia zake waliompokea katika eneo la Nampalahala baada ya kuingia katika mkoa huo kuendelea na ziara yake ya Kichama, leo.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipeana mkono wa furaha na Katibu wa CCM mkoa wa GeitaAdam Ngalawa wakati wa mapokezi hayo
 Baadhi ya waliopo katika msafara wa Alhaj Bulembo wakipata kifungua kinywa katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, kabla ya kikao kuanza leo. Kushoto ni Victoria Patrick na Happines Mtweve na kulia ni Ben Mugisha.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akivishwa vazi la heshima la Kabila la Wasukuma alipowasili wilayani Bukombe, leo. Anayemvisha ni Mzee wa Bukombe, Hakim Mstaafu Joseph Bulugu
 Alhaj Abdallah Bulembo akishukuru baada ya kupewa heshima hiyo.
 Alhaj Bulembo akiwasili ukubini kuongoza kikao cha wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bukombe, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za Chama, Mabalozi na watendaji wa Serikali
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akijadili jambo na Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Geita Doto Biteko wakati wa kikao hicho
 Ofisa wa Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Omari Kalolo akisalimia wakati wa kikao hicho
 Ofisa kutoka Makao Makuu ya Jumuia ya Wazazi Fadhili Mlami akisalimia wakati wa kikao hicho
 Katibu wa Siasa na Oganaizesheni Daniel Mgaya akisalimia wakati wa kikao hicho
 Wajumbe ukumbini wakati wa kikao hicho.
 Katibu wa CCM mkoa wa Geita Adam Ngalawa akizungumza wakati wa kikao hicho.
 Wajumbe ukumbini
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Bukombe Jacob Butachange, akisalimia baada ya kutambulishwa katika kikao hicho.
Mbunge wa Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Geita Doto Biteko akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Alhaj Bulembo na Kulia ni Butachage.
Mjumbe w Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Bukombe, Wajumbe wa Mabaraza ya Jumuia za Chama, Mabalozi na Watendaji wa Serikali, leo. PICHA BASHIR NKOROMO



TEHAMA YAKUZA UFANISI MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)

0
0
Serikali Mtandao inarahisisha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa umma. Usikose kuangalia kipindi hiki cha Seikali Mtandao katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) uone jinsi wanavyotumia mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika kazi zao za kila siku.

TEWW yatakiwa Kupunguza Idadi ya Wasiojua Kusoma na Kuandika

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa nane wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Fidelis Mafumiko na Afisa Utumishi Bi. Mayasa Omary na kushoto ni viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Fidelis Mafumiko akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi hiyo katika mkutano uliofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Kassim Nihuka na kulia ni watumishi wa taasisi hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima baada ya kufungua mkutano wa Baraza hilo jana Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Fatma Salum (MAELEZO).

Serikali imetoa rai kwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima nchini (TEWW) kuandaa mkakati wa kusaidia kupunguza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika. 

Rai hiyo imetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wakati akifungua mkutano wa nane wa Baraza la Wafanyakazi la Taasisi hiyo.

Akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo, Dkt. Akwilapo aliitaka TEWW kuandaa utaratibu mzuri wa kuwafikia wananchi wengi ambao hawajui kusoma na kuandika ili waweze kupata elimu kupitia taasisi hiyo.

“Ongezeko la wasiojua kusoma na kuandika linaelekea kuwa tatizo kubwa hapa nchini, hivyo natoa rai kwa taasisi hii kujadili namna ya kuendeleza kampeni za kisomo na kutoa mafunzo kwa wawezeshaji wa programu za kisomo ili kukabiliana na tatizo hilo.” Alisema Akwilapo.

Sambamba na hilo Dkt. Akwilapo aliwasisitiza watumishi wa taasisi hiyo kufuata sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli zake ili kufikia malengo waliyojiwekea na kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya elimu nchini.

Aidha Katibu Mkuu huyo aliIshauri TEWW kuandaa utaratibu mzuri wa kuwasaidia kielimu wanafunzi wa kike walioshindwa kuendelea na masomo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kulazimishwa kuolewa au kupata ujauzito.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Fidelis Mafumiko alisema kuwa taasisi hiyo inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuendesha programu za elimu kwa vijana na watu wazima walikosa elimu kupitia mfumo rasmi.

Alieleza kuwa program hizo ni pamoja na programu ya kuzuia ndoa za kulazimishwa za utotoni (Child Early and Forced Marriages) inayoendeshwa kwa kushirikiana na Taasisi ya Commonwealth of Learning ambayo imepanga kuwafikia walengwa 3000 katika mikoa ya Lindi, Rukwa na Dodoma.

Pia Dkt. Mafumiko alisema kuwa TEWW kwa kushirikiana na UNICEF wanaandaa programu kwa ajili ya vijana walio nje ya mfumo rasmi wa shule ikilenga kuwafikia vijana wapatao laki tano ndani ya miaka mitatu katika mikoa ya Tabora, Katavi, Geita, Rukwa, Dodoma, Simiyu, Shinyanga, Singida, Lindi na Manyara. 

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ilianza mwaka 1975 na ipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na ina jukumu la kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Elimu ya Watu Wazima na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya watu katika jamii wakiwemo waliokosa fursa ya kupata elimu katika mfumo rasmi.

Mshindi wa Milioni 20 Arusha akabidhiwa mzigo wake

0
0
WAENDESHAJI wa Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku, jana wamemkabidhi zawadi yake jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa Arusha, Oscar Haule, huku wakijigamba kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwakwamua washiriki wao kwa kuwapa fedha zao haraka ili waziingize katika majukumu yao ya kiuchumi.Mbali na kumpa zawadi hiyo ya fedha taslimu mshindi huyo, Biko pia wametangaza kutoa jumla ya Sh Milioni 500 kwa washindi wao waliocheza Biko mwezi Mei.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema wanaamini kuwa kiasi cha pesa walichompa mshindi wao atazitumia vizuri katika kujiletea maendeleo kama ilivyokuwa dhamira ya kucheza Biko na kufikia kutoa Sh Milioni 500 kwa washindi wa mwezi Mei.

Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko Oscar Haule mwenye fulana nyekundu akipokea hundi yake ya ushindi kutoka kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania, Charles Mgeta kulia akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa Milioni 20 wa Biko droo ya Jumatano Oscar Haule wa jijini Arusha mwenye fulana nyekundu.

“Tunampongeza Haule kwa kushinda donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Biko katika droo iliyochezeshwa juzi Jumatano, sambamba na kuwapongeza wote wanaocheza mchezo huu kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456,” Alisema Mgeta.

Naye Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema mchezo wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na kushinda, hivyo kila Mtanzania anapaswa kuanza kucheza ili aweze kuibuka na ushindi wa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku zawadi nono ya droo kubwa ya Jumapili hii ikiwa ni Sh Milioni 20 kama ilivyokuwa Jumatano iliyopita.

“Huu ni wakati wakutajirika kwa kupitia Biko Tanzania ambapo hakuna bahati nasibu inayolipa haraka kama Biko, hivyo Watanzania wanapaswa kutumia vyema fursa za uwapo wa bahati nasibu hii iliyojizolea umaarufu nchini,” Alisema Kajala.

Naye Mshindi huyo wa Arusha, Oscar Haule, aliwashukuru Biko kwa kumkabidhi fedha zake haraka, huku akisema kuwa ni wazi ujio wa bahati nasibu ya Biko umekuja kwa ajili ya kumuondolea ugumu wa maisha yake.

“Nashukuru Mungu kwa kunipa bahati ya ushindi wa Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wote nao kucheza Biko ili washinde kama nilivyokuwa mimi kwa sababu ndani ya mchezo huu hakuna kujuana bali bahati kwa wale waliocheza,” Alisema.

Hadi sasa Biko wameshatoa zawadi kwa washindi wa Mwezi Mei jumla ya Sh Milioni 500, huku mshindi wa Jumapili hii kwenye droo kubwa akitarajiwa kuibuka na Sh Milioni 20 sanjari na zawadi za papo kwa hapo zinazotolewa kwa kupitia simu za mikononi zilizotumika kuchezea mchezo wa Biko.

Mvua haijazuia kompyuta za Bayport kusambazwa mikoani

0
0

Mratibu wa Masoko wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa akimkabidhi kompyuta mbili Kaimu Mkurugenzi wa Mbulu, mkoani Manyara, Deogratias Kashasha.

Na Mwandishi Wetu, Mbulu
KWA miezi kadhaa sasa mvua imeendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, hali inayoonyesha kukidhi kiu ya watu wengi waliokuwa wakiiomba inyeshe katika maeneo yao.

Hata hivyo, licha ya mvua hiyo kunyesha, lakini baadhi ya maeneo imekuwa na matokeo mabaya kutokana na kuezua nyumba, kuharibu miundo mbinu muhimu ikiwamo ya barabara.

Matokeo hayo yameibua changamoto mpya hususan za kufikika kwa urahisi katika maeneo hayo yanayoendelea kukumbwa na mvua kubwa. Mbali na mvua hiyo kunyesha, hata hivyo uwajibikaji unaendelea kufanyika kwa sekta na watu mbalimbali kuendelea na maisha yao ya kila siku ili wakuze uchumi.

Zoezi la kutoa msaada wa kompyuta lilivyokuwa linaendelea katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Licha ya maeneo mengi kukumbwa na mvua, lakini Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services imeendelea na usambazaji wa kompyuta katika ofisi za serikali mikoani kama ilivyozindua utaratibu huo mwishoni mwa mwaka jana.

Bayport ambayo ni Taasisi ya Kifedha inayojihusisha na mikopo ya fedha, mwaka jana ilianzisha mpango wa kusambaza kompyuta kwenye ofisi za serikali ambapo tukio la uzinduzi lilihudhuliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki. Jumla ya kompyuta ambazo Bayport iliamua kuzisambaza kwa serikali ni 205, ambapo tayari maeneo mbalimbali wamefikiwa na kompyuta hizo kwa ajili ya kupunguza changamoto ya vifaa vya ofisi.

Akizungumza katika usambazaji wa kompyuta kwenye mikoa ya Singida, Manyara, Iringa, Songwe na Ruvuma, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, anasema licha ya mvua kubwa kupiga, lakini wameendelea na zoezi lao la kuhakikisha wanafikisha msaada wa kompyuta.
Anasema kufikisha kompyuta hizo ni sehemu ya kushirikiana vizuri na ofisi za umma katika mikoa ya Tanzania ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi, ukizingatia kuwa baadhi ya ofisi zimekuwa na tatizo la kukosa huduma muhimu za kompyuta.
“Hatujaangalia mvua kubwa inayonyesha katika nchi yetu kwa muda mrefu sasa, badala yake tuliendelea na zoezi letu zuri la kufikisha kompyuta katika ofisi za umma kama tulivyopewa mpangilio mzuri na Wizara ya Utumishi mwaka jana.

“Ukiacha maeneo tuliyosambaza kompyuta kwa hatua ya awali, msimu huu wa mvua pekee tumefikisha vifaa hivi katika maeneo ya Mbulu (Manyara), Kilolo (Iringa), Kondoa, Mbinga (Ruvuma), Songwe na Busokelo mkoani Mbeya ambapo kila ofisi ya Umma iliyopangwa kupokea msaada huo ilipokea kompyuta mbili,” Alisema Mercy.

Mratibu huyo wa Masoko wa Bayport anasema kwamba ulimwengu umebadilika kutokana na mahitaji makubwa ya sayansi na teknolojia, hivyo wazo la kutoa msaada wa kompyuta limekuja wakati muafaka, akiamini kuwa litapunguza changamoto ya utendaji hafifu wa watumishi wa umma waliokuwa wanakabiliwa na uhaba wa kompyuta.

Anayataja maeneo mengine ya nchi ambayo yamepokea kompyuta zao ni pamoja na Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Bukoba, huku wakijipanga kwa maeneo mengine yaliyopangwa wafikishiwe msaada huo haraka ambapo ukiacha kompyuta 125 zilizobakia Utumishi, nyingine 80 zinaendelea kusambazwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania.

“Ni matumaini yetu kuwa watumishi wa umma watatoa huduma bora kwa wananchi wao kwa kupitia msaada wa kompyuta tunaotoa kwa ofisi serikali kama tulivyoelekezwa na serikali tulivyopeleka wazo la kutoa msaada wa kompyuta 205 zenye thamani ya Sh Milioni 500,” Alisema Mercy.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu, mkoani Manyara, Deogratias Kashasha, anasema msaada wa kompyuta mbili waliyopokea kutoka Bayport umekuja wakati muafaka, hivyo ni wajibu wao kufanya kazi kwa bidii kwa kuzitumia vyema mashine hizo.

“Wenzetu wa Bayport wamefanya jambo sahihi kwa sababu wametuletea msaada wa kompyuta ambazo kwa hakika zitatusaidia kwa namna moja ama nyingine kutoa huduma bora kwa Watanzania kwa kupitia ofisi zetu.

“Dunia ya leo inahitaji matumizi makubwa ya kompyuta kwa mambo mengi, hivyo wakati tunashukuru kwa msaada huu, niwahakikishie kwamba zitarahisisha utendaji kazi kwa watumishi wetu kulingana na matumizi tutakayojipangia,” Alisema Kaimu huyo Mkurugenzi wakati anapokea kompyuta hizo hivi karibuni ofisini kwake.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida, Rashid M.Mandoa Anasema kwamba ni jambo la kutia moyo kuona taasisi ya Bayport imeamua kujitoa vyema kusaidia wadau wao kuwasaidia vifaa vya kiutendaji vya kompyuta ambazo ni muhimu.

Anasema hakuna asiyejua umuhimu wa kompyuta kwa mambo mengi kama vile kuweka rekodi mbalimbali za kiofisi, kuunganisha mawasiliano ya kiofisi au hata kuweka urahisi wa kumbukumbu katika maeneo mengi hali inayoweza kurahisisha.

“Tumepokea msaada huu wa kompyuta mbili kutoka kwa Bayport likiwa ni wazo zuri lililoanzishwa mwaka jana tulipoona linazinduliwa pia na ofisi ya Utumishi wa Umma kwa minajiri ya kuorodesha maeneo yatakayofikiwa, huku wilaya yetu ikiwa miongoni mwao.

“Hakika tunashukuru kwa msaada huu na kwa kiasi kikubwa utatusaidia kuwahudumia wana Singida ambao kwa namna moja ama nyingine wana uhitaji mkubwa wa huduma bora kutoka kwenye serikali yao ya Hapa Kazi tu,” Alisema huku akishuhudiwa na Meneja wa Bayport mkoani Singida Awali Chaula.

Halmashauri ya Kilolo mkoani Iringa, Mkurugenzi wake Violet Issacka Hakuwa nyuma kuwapongeza Bayport akiwataka waendelee kushirikiana naye katika kuwakomboa na kuwahudumia wananchi kwa kupitia sekta mbalimbali za kimaendeleo.

“Ni bahati kubwa kufikiwa na msaada huu kwa sababu tunaamini si kila Halmashauri ya Tanzania inaweza kupata msaada wa kompyuta kutoka kwenye taasisi ya Bayport Financial Services.

“Tufanya kazi kwa bidii na tunaomba Bayport muendelee kushirikiana na sisi kwa mambo mengine ya kimaendeleo, tukiamini kuwa uwezo huo mnao kutokana na kuguswa kwenu kwa mambo mengi ya kijamii mnayoendelea kuyafanya kila siku,” Alisema.

Bayport ni miongoni mwa taasisi zinazojitolea kwenye jamii kwa mambo mengi, huku mwaka jana wakifanya sherehe kubwa za kutimiza miaka 10 ya huduma zao za mikopo sanjari na kujitolea kwenye jamii kwa mambo mengi.



NAIBU WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO AKUTANA NA VIONGOZI WA TANZANIA MEDIA FUND (TMF) OFISINI KWAKE MJINI DODOMA

0
0
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akizungumza na viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.
Meneja Huduma kutoka Tanzania Media Fund (TMF) Bw. Alex Kanyambo akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) wakati viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Tanzania Media Fund (TMF) Bw. Alex Kanyambo(kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) wakati viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo.
Mtendaji Mkuu wa Tanzania Media Fund (TMF) Bw. Alex Kanyambo(kushoto) akijadilana jambo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(katikati) pamoja na Mkurugenzi Idara ya Hbabari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (kushoto) wakati viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma kuzungumza masuala mbalimbali yahusuyo Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma wa pili kulia ni Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi.

Picha zote na Octavian Kimario MAELEZO DODOMA

VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA BINAFSI WAMETAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA – PROF. MOHAMED JANABI

0
0
Na Mwandishi wetu – JKCI
Viongozi wa mashirika ya Umma na Binafsi  wametakiwa kujenga mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara ili kufahamu  kama wana magonjwa yanayowasumbua au la na kwa kufanya hivyo wataweza  kupata matibabu kwa wakati.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya upimaji wa Afya zao.
 Prof. Janabi alisema baadhi ya viongozi  hawana mazoea ya kupima afya zao japo mara moja kwa mwaka na inapotokea wamegundulika  kuwa na tatizo  la ugonjwa huwa ni  kubwa na limeshaleta madhara mwilini,   na wakati  mwingine huwa  ni vigumu kutibika lakini  tatizo kama hilo likigundulika  mapema katika hatua ya awali  huwa ni  rahisi kutibika.
 Akizungumzia kuhusu magonjwa ya Moyo Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema ni muhimu mgonjwa afuate maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa aliyopewa na daktari wake kwani kuna baadhi ya wagonjwa wamekuwa na tabia ya kuacha kutumia dawa pindi wanapojiona wamepata naafuu jambo ambalo siyo sahihi.
 Akielezea  jinsi ya kujikinga na magonjwa ya Moyo kwa upande wa chakula Afisa Lishe kutoka JKCI Louisa Shem  alisema ni muhimu kupunguza utumiaji wa vyakula vya mafuta kupita kiasi hasa mafuta yatokananyo na wanyama, kutumia vyakula vya nafaka zisizokobolewa.
 Kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji wa bidhaa zitokanazo na tumbaku ikiwemo sigara, kufanya mazoezi ya mwili angalau nusu saa kwa siku na kupunguza matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama Kazini kutoka  NHC Dkt. Yothan Mackenzie  alisema hivi karibuni walikuwa na mkutano wa Baraza la Wafanyakazi katika mkutano huo kulikuwa na mada ya ulaji na afya wakaona ni vyema mada hiyo iende sambamba na upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Moyo.
 Dr. Mackenzie alisema wanawapima viongozi hao kwa awamu hadi sasa jumla ya wakurugenzi na wakuu wa vitengo 14 wamepima na kujuwa afya zao na viongozi wengine wataendelea kupima kwani Shirika lao linaamini kuwa  mfanyakazi akiwa na afya njema ataweza kufanya kazi zake vizuri.
 Baadhi ya magonjwa waliyopima viongozi hao ni pamoja na  Moyo, tezi dume, figo na sukari.

ORIFLAME YASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UTOAJI HUDUMA NA UUZAJI BIDHAA ZAKE ZA VIPODOZI DUNIANI

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kusheherekea miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili kushoto ni Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt, Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu.

 Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina Rangnitt (wapili kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra,Mtaalamu wa masuala ya siasa na biashara kutoka ubalozini, Ludvig Bontell na Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu. 

 Meneja Masoko wa Oriflame Afrika Mashariki, Mary Riungu jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kutimiza miaka 50 ya kampuni hiyo katika utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani. Wapili Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oriflame Afrika Mashariki, Piyush Chandra, Balozi wa Uswisi nchini Tanzania, Katarina. 
 Balozi wa bidhaa za Oriflame Tanzania, Missie Popular akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kutambulishwa na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo katika nchi za Afrika Mashariki, Mary Riungu wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za vipodozi Duniani.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya utoaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa za Oriflame, wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi wakuu wa Kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA VENANCE NESTORY)

JAFO AKUNWA NA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA SERIKALI NYAMAGANA

0
0
Wananchi wakiwa katika dirisha la malipo katika Kituo cha Afya cha Nyamagana.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua utekelezaji wa maagizo katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika dirisha la malipo kukagua matumizi ya mfumo wa kielektroniki kama umefungwa katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua utekelezaji wa maagizo katika Kituo cha Afya Nyamagana Jijini Mwanza
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya Umiseta yaliyozinduliwa na Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu jana Jijini Mwanza.

……………………


NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amempongeza Mbunge wa Nyamagana na Viongozi wote wa Wilaya ya Nyamagana kwa kutekeleza maagizo ya serikali kwa maslahi mapana ya wananchi.

Mnamo mwezi Februari, mwaka huu Jafo alitembelea wilaya ya Nyamagana ambapo licha ya kuongea na watumishi alitembelea pia miradi ya maendeleo na kutoa maagizo mbalimbali.

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi wa barabara za lami zinazojengwa chini ya ufadhili wa Benki ya dunia pamoja na kukagua miundombinu na utoaji wa huduma katika kituo cha afya cha Nyamagana.

Katika ziara yake, alitoa maagizo mbalimbali ambayo alitaka yatekelezwe Kabla ya mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Hata hivyo, jana baada ya kufanikisha zoezi la ufunguzi wa mashindano ya UMISETA yaliyozinduliwa rasmi na Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan, Jafo amefuatilia utekelezaji wa maagizo hayo na kukuta viongozi na watendaji wa jiji la Mwanza wametekeleza kwa kiwango cha kuridhisha.

Katika ujenzi wa barabara ijulikanayo kwa jina la Tilapia road, Jafo amekuta barabara ya lami imekamilika na kubakia maeneo madogo sana ya kuweka taa za barabarani.

Katika Kituo cha Afya cha Nyamagana, Naibu Waziri Jafo amekuta agizo la kuwekwa kwa mifumo ya kukusanya mapato kwa njia ya kielektroniki ukiwa umekamilika na mapato yameanza kuongezeka kutoka sh. milion 4 hadi Sh.milioni 10 kwa mwezi.

Mbali na hilo, pia amekuta wamekamilisha kutenga eneo Maalum kwa wagonjwa wa bima ambapo katika eneo hilo la bima mapato yameongezeka kutoka wastani wa Sh.milioni 6 hadi zaidi ya Sh.milioni 10 kwa mwezi.

Kufuatia utekelezaji huo, Jafo amewapongeza viongozi wote wa Nyamagana akiwemo Mkuu wa wilaya, Mbunge, madiwani pamoja na timu ya watendaji wa jiji la Mwanza huku akiwataka

watendaji hao kuchapa kazi ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live


Latest Images