Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1264 | 1265 | (Page 1266) | 1267 | 1268 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akisaini kitabu cha Wageni na baadaye kutoa pole kwa familia ya Marehemu Philemon Ndesamburo nyumbani kwake Kiboroloni, Moshi Mjini .
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira ameshawasili mkoani kwake tayari kwa kuanza kazi rasmi,ambapo leo ameanza  majukumu yake kwa kukutana na kamati ya siasa  ya Mkoa huo .
   RC Mghwira akisaini kitabu cha Wageni kabla ya kuanza kuzungumza na kamati ya siasa ya mkoa wa Kilimanjaro mapema leo.
   Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,RC Anna Mghwira akisalimiana na viongozi mbalimbali wa kamati ya Siasa ya Mkoa,mapema leo
  RC Mghwira akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi mara baada ya kuwasili nje ya ofisi yake,tayari kwa kuanza kazi kama Mkuu wa Mkoa mpya mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

  Pamoja na malalamiko na manung’uniko ya hali ngumu ya maisha kwa watanzania wengi, Tanzania ndio yenye kiwango cha chini cha mfumuko wa bei wa wastani wa asilimia 6.1 kwa mwezi Mei 2017 kwa nchi za Afrika Mashariki.

  Hayo yamebainishwa leo bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2017/18.

  Mhe. Dkt. Mpango amesema mfumuko wa bei katika nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka 2016 uliendelea kuwa wa kiwango cha tarakimu moja, ambapo Rwanda ilikuwa na asilimia 7.1, Uganda asilimia 5.4, Tanzania asilimia 5.2, Kenya asilimia 6.3 na Burundi asilimia 5.6.

  Alisema kufikia mwezi Aprili 2017, mfumuko wa bei kwa nchi hizi ulipanda, ambapo kwa Burundi ulifikia asilimia 21.10, Rwanda asilimia 13.0; Kenya asilimia 10.28; Uganda asilimia 6.4 na Tanzania asilimia 6.4. 

  “Hata hivyo, kwa upande wa Tanzania mfumuko wa bei umeendelea kushuka mpaka asilimia 6.1 kwa mwei Mei 2017” amesema Dkt. Mpango

  Mhe. Dkt Mpango amesema kwa miaka minne mfululizo, wastani wa mfumuko wa bei kwa Tanzania umeendelea kupungua, ukibaki katika kiwango cha tarakimu moja.

  Amesema kwa mwaka 2016, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.6 mwaka 2015. Kupungua kwa wastani wa mfumuko wa bei nchini kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na: mwenendo wa kushuka kwa bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia na nchini; kuimarika kwa upatikanaji wa vyakula nchini na hivyo kuimarisha wastani wa bei; na kuwepo kwa sera madhubuti za usimamizi wa bajeti na fedha.

  Mhe. Dkt. Mpango amesema mfumuko wa bei uliongezeka kidogo, ambapo ulifikia asilimia 6.4 mwezi Aprili 2017 lakini ukiwa ndani ya maoteo ya wastani wa tarakimu moja (asilimia 5 – 8) kwa mwaka 2017.

  Hali ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei nchini ilichangiwa na hofu iliyotokana na kuchelewa kwa msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini na hivyo kuwepo kwa taharuki ya kutokea upungufu wa chakula. Hata hivyo, maeneo mengi yamepata mvua ya kutosha na hivyo bei ya chakula nchini inatarajiwa kupungua.

  Mhe. Dkt. Mpango amesema kasi ya ukuaji wa uchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ilishuka kutoka wastani wa asilimia 6.5 mwaka 2015 hadi asilimia 5.3 mwaka 2016 ijapokuwa Jumuiya hii iliendelea kuongoza kwa ukuaji miongoni mwa Jumuiya mbalimbali za Afrika.

  Amesema kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi katika Jumuiya hii ilichangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka kwa bei za bidhaa na kudorora kwa uchumi wa dunia. Maoteo ya mwenendo wa uchumi katika ukanda huu yanaonesha utakua kwa wastani wa asilimia 5.7 mwaka 2017 na asilimia 6.0 mwaka 2018.

  “Matarajio haya yanazingatia hatua zinazochukuliwa na nchi za ukanda huu katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na uendeshaji biashara kama vile kuwa na maeneo tengefu ya ujenzi wa viwanda (industrial parks), hususan, vya nguo, bidhaa za ngozi, kilimo, madawa na vifaa tiba” ameongeza Dkt. Dkt. Mpango

  Amesema kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), kasi ya ukuaji wa uchumi ilishuka kutoka wastani wa asilimia 1.9 mwaka 2015 hadi asilimia 1.1 mwaka 2016.

  Mhe. Dkt. Mpango amesema kasi ndogo ya ukuaji wa uchumi katika Jumuiya hii ilichangiwa na uhaba wa nishati ya umeme pamoja na ukame uliochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa ya La Nina.

  Amesema licha ya kasi ndogo ya ukuaji, Jumuiya hii iliendelea kuwa ya tatu kwa ukuaji miongoni mwa Jumuiya za barani Afrika na unatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 1.4 mwaka 2017.

  Waziri wa Fedha amesema mfumuko wa bei ulifikia asilimia 10.5 mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 5.7 mwaka 2015, ukichangiwa na ukame na kuyumba kwa utekelezaji wa sera za mapato na matumizi kwa baadhi ya nchi wanachama.

  Ameeleza kuwa matarajio katika nchi hizo ni kuwa kwa mwaka 2017 mfumuko wa bei utapungua hadi kufikia asilimia 8.7 kutokana na kushuka kwa gharama za bidhaa, kuimarika kwa upatikanaji wa nishati ya umeme, na uthabiti wa bei ya mafuta; na kuimarika kwa hali ya hewa.

  0 0

  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Finland nchini, Pekka Hukka ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamejadili namna ya kuimarisha sekta ya misitu nchini ikiwemo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuwekeza katika viwanda vya kuchakata mazao ya misitu pamoja na uzalishaji wa nishati mbadala.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimsikiliza Balozi wa Finland nchini, Pekka Hukka (kulia) ofisini kwake leo mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi. 
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson ofisini kwake mjini Dodoma leo ambapo wamezungumza kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili katika kuendeleza sekta ya Maliasili hususan vita dhidi ujangili, kuongeza idadi ya watalii pamoja na mapato yatokanayo na utalii.
   Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson (katikati) akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akimkabidhi Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson majarida mbalimbali yanayozungumzia vivutio vya utalii vya Tanzania ofisini kwake mjini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi (kushoto) akizungumza katika kikao hicho cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) na Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani nchini, Inmi Patterson leo mjini Dodoma. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki kuchoma nyavu za uvuvi haramu kwenye dampo la Buhongwa, wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza vyombo vya dola nchini kuwakamata bila kuwaonea huruma viongozi watakaobainika kujihusisha au kuhujumu kazi ya kupambana na uvuvi haramu nchini. 

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo wakati akishiriki katika zoezi la uchomaji wa zana haramu za uvuvi 5,662 kwenye eneo la Buhongwa wilayani Nyamagana mkoani Mwanza zilizokamatwa katika Ziwa Victoria. 

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi kushiriki katika shughuli za uvuvi haramu hivyo inabidi wachukuliwe hatua ili kukomesha kabisa tatizo la uvuvi haramu katika Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini. 

  Ameeleza kuwa uvuvi haramu katika Ziwa Victoria umekuwa ni tatizo sugu na hali ambayo imesababisha kupungua kwa samaki na mapato kwa Serikali ambayo ni muhimu kwa ajili ya shughuli maendeleo. 

  Amesema licha ya uvuvi haramu kupunguza mapato ya Serikali kutoka kwenye viwanda hali ya ajira nayo sio nzuri zilizokuwa zinatoka kwenye viwanda ambazo zimepungua kwa asilimi 49. 

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepongeza kazi kubwa iliyofanyika ya ukamataji wa zana haramu za uvuvi katika Ziwa Victoria na amewahakikishia viongozi wa mkoa wa Mwanza kuwa Serikali ipo pamoja nao katika kazi hiyo. 

  “Serikali yenu itaendelea kushirikiana nayi katika kuhakikisha kuwa rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria zinaendelea kuwepo kwa kuendelea kutoa fedha na vitendea kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi kwa lengo la kuhifadhi ziwa Victoria” Amesisitiza Makamu wa Rais. 

  Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema oparesheni za uvuvi haramu katika Ziwa Victoria zitaendelea kuimarishwa ipasavyo mkoani Mwanza mpaka vitendo hivyo vikomeshwa. 

  Amesema mkoa wa Mwanza ulikuwa na viwanda Sita vya kuchakata samaki lakini kutokana na kupungua kwa samaki katika Ziwa Victoria ni viwanda Vinne tu mpaka sasa ndio vinafanya kazi hali ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa mapato kwa Serikali na ajira kwa vijana mkoani huo. 

  Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza John Mongela ameeleza kuwa kutokana na viwanda hivyo kusitisha shughuli za uzalishaji zaidi ya watu mamia ya watu wamekosa ajira.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye shughuli za mazingira ambapo nyavu zilizotumika kwenye uvuvi haramu zimeteketezwa katika dampo la Buhongwa, wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini, Mheshimiwa, Sarah Cooke kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini, Mheshimiwa Inmi Patterson kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 8, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 08/06/2017.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar walipokuwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipozungumza nao leo walipofika Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 08/06/2017.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar pamoja na Viongozi wengine baada ya mazungumzo yalitofanyika katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na Ikulu.] 08/06/2017.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba amezindua albamu ya kwaya ya Cecilia uliofanyika katika Kanisa la Katoliki Mjini Mafinga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali mkoani humo.

  Katika uzinduzi wa albamu hiyo, Mwigulu alifanikwa kuchangisha harambee ya uzinduzi na kufanikiwa kupata milioni 25 na kuzidi kufanikisha mafanikio ya kwaya hiyo.

  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve amesema kuwa anamshukuru sana Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba kwa kuweza kuwatembelea na kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kufanikisha zoezi zima la uzinduzi wa kwaya ya Cecilia.

  "Namshukuru sana Waziri  Mwigulu kwa kuweza kukubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kwaya ya Cecilia na kufanikisha zoezi zima ikiwemo kupatikana kwa milioni 25 ikiwa ni harambee ya uzinduzi,"amesema Rose.

  Katika uzinduzi wa albamu hiyo baadhi ya viongozi mbalimbali waliweza kuwepo ikiwemo Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi na Mkuu wa Wilaya Mafinga Jamhuri William.
  Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja  Mchungaji wa Kanisa Katoliki la Mjini Iringa Leornad Muli na viongozi mbalimbali wa jimbo la Iringa Mjini akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mafinga Cosato Chumi (wa nne kulia), Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve
   Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akizindua albamu ya kwaya ya Cecilia katika kanisa la Katoliki la Mjini Mafinga akiwa ameambatana na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve
    Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve (kulia) wakati wanawasili katika kanisa la Katoliki la Mjini Mafinga.. 
   Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve wakiwa wanatoa sadaka  katika  Kanisa Katoliki la Mjini Mafingawakati wa uzinduzi wa Albamu ya kwaya ya Cecilia iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve akiwa anawasalimia waumini wa  Kanisa Katoliki la Mjini Mafinga akiwa amembatana na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakati wa uzinduzi wa Albamu ya kwaya ya Cecilia iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba.
  Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Iramba Magaharibi Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa (CCM) Rose Tweve (kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakifuatilia misa katika  Kanisa Katoliki la Mjini Mafinga wakati wa uzinduzi wa Albamu ya kwaya ya Cecilia iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki iliyopita.


     

  0 0

  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof. Ibrahim Juma akiwa ofisini kwake na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga pamoja na ujumbe alioongozana nao. Ujumbe huo kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ulifika Ofisini kwa Kaimu Jaji Mkuu kwa ajili ya kujitambulisha kwake, kumpongeza kwa kuteuliwa pamoja na kuzungumzia masuala ya Ushirikiano baina ya Tume hiyo na Mahakama ya Tanzania.
  JAJI2 JAJI3

  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 08, 2017.
  NGA2
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –(TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA3
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk Philip Mpango akisoma  Taarifa ya hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA4
  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA5
  Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mbunge wa Ndanda (CHADEMA) Mhe.Cecil Mwambe  katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA6
  Naibu Waziri Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA7
  Mbunge wa Viti maalum (CCM) Mhe.Maida Abdallah akiuliza swali katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA8
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge,Kazi ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba  katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA9
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Prof Jumanne Maghembe akiteta  jambo na Mbunge wa Hanang’  katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 8, 2017.
  NGA10
  Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Rhoda Kunchela akiuliza swali  katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma June 8, 2017.

  Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.

  0 0


  Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khatib Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mifuko ya Saruji kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana mkoani humo ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.
  Mkuu wa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah mabati kwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi la makabidhiano ya msaada huo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo Zantel walitoa jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350, vyote vikigharimu Sh. 13 milioni.  Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah akiwakabidhi wakuu wa wilaya za mkoa huo mabati yalitolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni katika mkoa huo. Zoezi hilo lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar ambapo jumla ya mabati 350 na Saruji mifuko 350 kwa pamoja vilikabidhiwa na Kampuni ya Zantel. (Katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mhe. Salama Mbarouk Khatib na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkoani Mhe. Hemed Suleiman Abdallah.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Kusini Pemba, Ndg. Yussuf Mohammed Ali (kushoto) akimtambulisha Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Khamis Baucha (wa pili kushoto) kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mwanajuma Majid Abdallah (hayupo pichani) kabla ya Mkuu huyo wa Zantel kukabidhi msaada wa Saruji na Mabati kwa ajili ya waathirika wa mafuriko mkoani humo. Msaada huo una gharama ya Sh 13 milioni na lilifanyika jana kisiwani Pemba-Zanzibar. Wa tatu Kulia ni Ofisa wa fedha na Utawala wa Tawi la Zantel–Pemba, Yakoub Fadhil Juma.

  0 0


  Beki wa Yanga, Juma Abdul, (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa AFC Leopards Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Katika mchezo huo AFC Leopards wameibuka na uwashinda wa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya 0-0.
  Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akiwania mpira na Kiungo wa AFC Leopards, Alan Katerega, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

   Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
  MABINGWA Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom (VPL) Yanga leo wameaga amashindano ya SportPesa Super Cup kwa mikwaju ya penati 4-2 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

  Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Uhuru ulianza majira ya saa 8 kamili kwa kuzikutanisha timu ya Yanga dhidi ya AFC Leopard ya nchini Kenya.Mpaka dakika 90 za mpira zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu na kuelekea kwenye mikwaju ya penati.

  Timu zote zilionekana kushambulia kwa kupokezana lakini safu za ushambiaji hazikuwa makini na kupoteza nafasi walizozipata mara kadhaa.

  Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Emanuel Martin na kuingia Said Musa, akatoka Maka Edward na kuingia Said Makapu, Yusuph Mhilu alitoka na kuingia Samwel Greyson na Pato Ngonyani alitoka na kuingia Babu Ally.
  AFC Leopard wakafanya mabadiliko kwa kumtoa Abwao Marcus na kuingia Ingotsi Marselas.

  Wachezaji waliopiga penati kwa upande wa Yanga ni Nadir Haroub, Obrey Chirwa ambao walipata na Said Makapu na Said Musa kukosa kwa upande wa Yanga.Kwa upande wa AFC Leopard ni golikipa Jan Otieno, Otieno Duncan, Bernad Mango na Katerega Allan ambao walipata na Ingotsi Marselas alikosa
  Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 
  Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mabeki wa AFC Leopards, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji wa Yanga Yusuph Mhilu (kushoto) akimtoka beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
  Winga wa Yanga, Yusuph Mhilu (kushoto) akimfinya beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
  Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
  Mhilu akimkalisha beki wa AFC Leopards


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege ameupongeza mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS na kueleza kuwa mfumo huo ni suluhusisho la hati zenye mashaka katika halmashauri mbalimbali nchini.

  Mfumo wa FFARS unatekelezwa katika mikoa 13 kwenye halmashauri 93 kwa ushirikiano wa serikali na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) pamoja na Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS) unaofadhiliwa na watu wa Uswizi (Swiss Tropical and Public Health Institute). 

  Akifungua mafunzo kuhusu mfumo huo kwa maafisa elimu kata na Waganga Wafawidhi katika vituo vya afya kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala,yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama,Berege alisema mfumo wa FFARS ni mwarobaini wa tatizo la halmashauri kupewa hati zenye mashaka. 

  Alisema mfumo huo utawezesha takwimu nyingi za halmashauri za wilaya kukusanywa kwa usahihi zaidi kutoka vituo vya kutolea huduma ambavyo vitakusanya na kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo huo. 

  “Takwimu ni tatizo la kitaifa,hivyo mfumo huu utasaidia kuondoa tatizo hili kwa kuongeza uwazi na umakini katika masuala ya uhasibu na utoaji taarifa za fedha”,alieleza Berege. “Halmashauri zimekuwa zikipata hati zenye mashaka kwa sababu uwekaji takwimu haupo vizuri,FFARS ni tiba ya hati zenye mashaka,pamoja na kuendelea kutumia njia za vitabu/makaratasi,ni vyema halmashauri zikawa tayari kutumia njia za ki- elektroniki katika utunzaji takwimu”,aliongeza Berege. 

  Aidha alilishukuru Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kufadhili mradi huo na kuwataka watanzania kuutumia vizuri ili kuleta maendeleo katika halmashauri. 

  Naye Mshauri wa Kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno alisema mafunzo ya FFARS kwa Maafisa elimu kata na Waganga Wafawidhi katika vituo vya afya yanatolewa na wahasibu wa halmashauri za wilaya waliopatiwa mafunzo hivi karibuni na maafisa kutoka PS3, HPSS na maafisa kutoka TAMISEMI ili nao wawafundishe watoa huduma wengine katika vituo vya kutolea huduma. 

  “PS3,HPSS,TAMISEMI na wadau wengine tumeamua kutoa mafunzo kuhusu mfumo wa FFARS ambao utaanza kutekelezwa Julai 1,2017 ili kuwawezesha watumishi katika vituo vya sekta ya afya na elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo huu katika shule,zahanati,vituo vya afya na hospitali za wilaya”,alisema Otieno. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege akifungua kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya kutoka halmashauri hiyo leo Alhamis June 8,2017 katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akifungua mafunzo hayo.Kushoto ni Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno,kulia ni Mratibu wa PS3 Halmashauri ya Msalala,Elikana Zabron 
  Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno akielezea malengo ya mafunzo ya mfumo wa FFARS 
  Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno akizungumza ambapo alisema mwongozo wa FFARS upo katika mfumo wa kielektroniki na mfumo wa zamani ulioboreshwa wa kujaza katika vitabu kulingana na miundombinu iliyopo katika vituo vya kutolea huduma nchini Tanzania 
  Mratibu wa PS3 Halmashauri ya Msalala,Elikana Zabron akizungumza ukumbini 
  Mratibu wa HPSS halmashauri ya Msalala,Happiness Josephat akiwa ukumbini wakati wa mafunzo kuhusu FFARS 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini 
  Mhasibu wa Afya wa Halmashauri ya Msalala, Peter Mathew Swai akiwasilisha mada kuhusu FFARS 
  Washiriki wakifuatilia mada 
  Mafunzo yanaendelea 
  Mshiriki akisikiliza mada na kuandika dondoo muhimu 
  Mafunzo yanaendelea 
  Washiriki wa mafunzo hayo wakifanya kazi za vikundi kuhusu namna ya kuandaa taarifa mbalimbali za miamala ya fedha 
  Kazi za vikundi zikiendelea 
  Washiriki wakiandika kazi ya kikundi 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka PS3, HPSS na washiriki wa mafunzo ya FFARS 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka PS3, HPSS na maafisa elimu kata kutoka halmashauri ya Msalala 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka PS3, HPSS,wakufunzi na waganga wafawidhi wa vituo vya afya kutoka halmashauri ya Msalala. 


  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0

  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kushoto) pale alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza jambo pale alipopata ugeni wa Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisisitiza jambo pale alipopata ugeni wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Ndg. Abdulrahman kinana (kulia) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Ndg. Abdulrahman kinana (kulia) pale alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akipiga picha ya pamoja na katibu Mkuu wa CCM Taifa, Ndg. Abdulrahman kinana (kulia) pale alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah.

  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0


  0 0  0 0

  Balozi Mwinyi akipokea kitabu chenye mwongozo wa namna ya kushiriki mashindano hayo. 
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika MasharikI, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimsikiliza Afisa Mkuu wa Uhusiano wa Sekrearieti ya Jumuiya ya Afrika Mshariki, Bw. Otrhieno Richard Owora (kushoto). Katika mazungumzo hayo, wawili hao walizungumzia maandalizi ya uzinduzi wa mashindano ya kubuni nembo mpya ya EAC yatakayowahusisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo kwenye nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Uzinduzi huo utafanyika kwenye Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tarehe 09 Juni 2017. 
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kushoto), pamoja na Maafisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, wa kwanza kulia ni Bw. Ally Kondo pamoja na Robi Bwiru wakinukuu mambo yaliyokuwa yakizungumzwa na Balozi Mwinyi pamoja na Bw. Owora. 
  Mazungumzo yakiendelea.
   
  Picha ya pamoja. 


  0 0

   Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Mheshimiwa Rajabu Hassan Gamaha anayeangalia camera akizungumza na baadhi ya wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa 8 wa Afrika Mashariki wa Sekta ya Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao walifika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini Bujumbura, Burundi leo kwa mazungumzo yaliyolenga kuimarisha uhusiano mwema ulipo baina ya Burundi na Tanzania. Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana L. Pallangyo aliyevaa suti nyeupe.

  Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bwana Felix Ngamlagosi akisisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi Rajabu juu ya uhusiano wa Taasisi ya EWURA na Taasisi mpya iliyoanzishwa Nchini Burundi  yenye jukumu la Kudhibiti Nishati ya Mafuta na Maji, pembeni yake ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhandisi Abdillah Mataka.
  Balozi Rajabu na Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Mazungumzo hayo.

  0 0

  Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour (aliesimama) akizungumza na katika kituo cha Sober House wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga (aliesimama) akizungumza wakati wa Mwenge wa Uhuru ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House , Al –Karim Bhanji (katikati)akizungumza jinsi wanavyoendesha kituo hicho wakati mwenge huo ulivyopita katika kituo hicho leo Bagamoyo mkoani Pwani.kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwasili katika Kituo cha Sober House
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya pamoja na Watendaji wa Kituo hicho.
  Mkurugenzi wa kituo hicho,Al –Karim Bhanji (katikati) akiwa ameshika Mwenge wa Uhuru
  Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017, Amour Hamd Amour akiwaaga viongozi na Watendaji wa Kituo hicho.
  Mwenge wa Uhuru
   
  Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru , Amour Hamad Amour amewaasa watendaji mbalimbali nchini kuwajali vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali pale inapotokea.

  Kiongozi huyo ameyasema leo wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipopita katika mradi wa kituo cha watu walioathirika na Dawa za Kulevya Sober House Kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani,

  Amesema kuwa vijana ndio wamekuwa waathirika wakubwa katika matumizi ya dawa za kulevya ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

  Nae Mkurugenzi Kituo hicho, Al –Karim Bhanji amesema vijana walioathirika na dawa za kulevya wanatakiwa kupewa upendo,kuwaacha kunaweza kukasababisha kurudi katika matumizi ya dawa za kulevya.

  Bhanji amesema malengo ya kituo hicho ni kuwa na walimu ambao watakuwa wanawafundisha waathirika hao ili kurudi kuendesha biashara zao kutokana na elimu itakayotolewa na kituo hicho.

  Amesema kuwa kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia kituo kituo kitaanzisha darasa la kompyuta, ambapo waathirika watajifunza na wengine wanaweza kuwa na ujuzi tofauti.

  Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj Madjid Mwanga amesema kuwa Mwenge umetoa hamasa kubwa na kupelekea kufungua miradi mbalimbali ,ambapo Sober House ni mradi ambao umeokoa vijana wengi waliotumbukia kwenye matumizi ya dawa za Kulevya.

  0 0

  Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa,(wapili kulia), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali za wanavyuo wa elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam, wakionyesha vipeperushi vyenye melezo ya Mfuko huo, baada ya semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kuelimisha wanafunzi shughuli mbalimbali za Mfuko na fursa zilizopo. Semina hiyo imefanyika leo Juni 8, 2017.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi. Costantina Martn, akifungua semina hiyo leo Juni 8, 2017

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  ZAIDI ya wawakilishi 250 wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kutoka jijini Dar es Salaam wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari (PSS), baada ya kushiriki semina ya siku moja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Juni 8, 2017.

  Wanafunzi hao kutoka taasisi 20 za elimu ya juu, wamehudhuria semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kwa uratibu wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO), ili kuwapatia elimu wanafunzi hao kuhusu shughuli za Mfuo na faida azipatazo mwanachama ikiwemo mafao mbalimbali.

  Kabla ya zoezi hilo la kujiunga na Mfuko, awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi. Costantina Martin, aliwaasa wanafunzi hao kujijengea utamaduni wa kuweka akiba kwani manufaa yake huonekana katika kipindi kifupi.

  “Mimi nina mototo yuko chuo kikuu huwa ninampatia fedha kidogo za kujikimu lakini namueleza aweke akiba, ningependa kuwahamasisha vijana mjenge utamaduni wa kujiwekea akiba kidogo kidogo,zile posho mnazopata, na fedha kutoka kwa wazazi wenu, mnaweza kutenga sehemu ya fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ili kujiwekea akiba.” Alsoema Bi. Costantina Martin, wakati akifungua semina hiyo.

  Alisema, PSPF, kama Mfuko wa hifadhi ya jamii, moja ya malengo yake ni kuandikisha wanachama wapya , kukusanya michango, kuwekeza na kuwalipa mafao na pensheni wastaafu na wategemezi iliw aweze kupata fedha kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku.

  Aliwashauri wanafunzi hao kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, ili hatimaye waanze kufaidi mafao mbalimbali ikiwemo faola matibabu ambapo mwanachama anapatiwa bima ya afya itakayomuwezesha kutibiwa yeye mwanachama na wategemezi wake.

  Ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama, PSPF inaendesha mipango ya aina mbalimbali ya uchangiaji, mpango wa lazima na mpango wa hiari ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama katika Hifadhi ya PSPF.

  “Najua wataalamu wetu watawapa elimu ya kutosha kuhusu aina za wanachama kwani hata ninyi mnaweza kuwa wanachama wetu kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari PSS, ambapo mnaweza kujiunga na kupatiwa kadi zenu leo hii baada ya semina.” Alsiema.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO), Bw.Stanslaus Peter Kadugalize, ameishukuru PSPF kwa kuwa mshirika mzuri na kukubali ombi la wanafunzi hao kupatiwa elimu juu ya hifadhi wa jamii.

  “ Ninachoomba, PSPF inaweza kuangalia namna gani inaweza kusaidia wanafunzi katika ushiriki wao kwenye elimu, kwa mfano mnaweza kutusaidia hata kutujengea vimbweta kwenye vyuo vyetu, lakini pia mnaweza,uwekeza kwenye ujenzi wa hosteli ambazo sisi wanafunzi tutalipa kodi.” Alsiema.

  Maafisa wa PSPF, walitoa mada mbalimbali ambazo miongoni mwake ni pamoja na jenga career na PSPF, ambao ni mkopo wa elimu, Jipange kimaisha na PSPF, ambapo PSPF hutoa mikopo kwa mwajiriwa mpya,

  Hata hivyo wanafunzi hao waliiomba PSPF kutengeneza mfumo ambao unaweza kuwasaidia wanafunzi kuwawezesha nkushiriki kwenye elimu bila matatizo. “Wanafunzi hawahitaji fedha nyingi, mnaweza kuweka mfumo utakaowawezesha wanafunzi kupata mikopo midogo ya fedha ili kuwawezesha kujikimu wawapo vyuoni na hatimaye wanafunzi hao wanaweza kurejesha fedha hizo kwa utaratibu utakaokubaliwa na pande mbili.
  Mwenyekiti wa TAHILISO, Bw.Stanslaus Peter Kadugalize,(aliyesimama), akifafanua baadhi ya mambo mwishoni mwa semina hiyo. Wengine kutoka kushoto, ni Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi. Zuhura A. Rashid, Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
  Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi.Zuhura A.Rashid, (kushoto), akijaza fomu ya kujiunga na PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS)
  Viongozi wa wanafunzi wakijaza fomu za kujiunga na PSPF
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi.Costantina Martin,akifungua semina hiyo
  Kely Malinga, wa call centre ya PSPF akiwa kazini
  Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, akizungumza kwenye senima hiyo
  Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, akizungumza kwenye senima hiyo
  Afisa Matekelezo wa PSPF, Bw. David Mutabazi, akitoa mada yake jinsi masuala ya hesabu za kulipa mafao zinavyofanyika
  Bi. Neema na Bw. Njaidi wakiwaongoza washiriki wa semina hiyo, kutembelea pfisi za PSPF ili kujionea utendaji kazi wa ofisi hizo kabla ya kuanza semina
  Washiriki wakijisajili
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akizunguzma na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa elimu ya juu, walipotembelea kuona jinsi utunzaji taarifa za wanachama wa Mfuko zinavyohifadhiwa. Hii ilikuwa ni sehemu ya semina waliyopewa viongozi hao na maafsia wa PSPF jijini Juni 8, 2017
  Washiriki wakionyeshana fomu za PSS, za wanachama wa mpango wa uchangiaji wa hiari
   Afisa wa PSPF anayeshughulikia masoko, Bw. Magira Werema akizungumza wakati wa kutoa elimu viongozi hao wa wanafunzi

  Mshiriki akijaza fomu za kujiunga na PSS
  Washiriki wakiwa kwenye foleni ya kupiga picha za vitambulisho vya kadi za uanachama wa PSPF kupitia mpango wa PSS
  Afisa mwandamzi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Delphis Richard, (kushoto), akitoa mada iliyoelezea faida mbalimbali azipatazo mwanachama wa Mfuko huo kwa washiriki
  Washiriki wakijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
  Bi. Neema(kushoto), akimuelekeza jambo mshiriki huyu wa semina
  Mkuu wa idara ya call centre, Bi Queen, (katikati), akitoa maelezo kwa washiriki walipotembelea ofisi za huduma kwa wateja, za PSPF makao makuu 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Costantina Martin, (katikati), akiongozana na Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Mkoa wa Dar es Salaam, Neema Lowassa, (kulia) na Afisa Mwandamizi wa Utafiti, Mapesi Maagi. Kuelekea kwenye ukumbi wa mkutano ambako kulifanyika semina ya siki moja ya viongozi wa serikali za wanafunzi wa elimu ya juu jijini Dar es Salaam jana Juni 8, 2017.
  Afisa mwandamizi wa kitengo cha utunzaji kumbukumbu (record keeping), Bw. Gwamaka A. Ngomale, (mwenye kofia), akiwaeleza washiriki hao namna PSPF inavyotunza kumbukumbu kwenye mfumo wa kielektroniki wa makabati (electronic shelves)
  Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi.Zuhura A. Rashid, akitoa neno la shukurani baada ya semina kumalizika

  0 0


  · Waunga mkono kampeini ya kitaifa ya usafi wa mazingira

  Mashirika ya kimataifa yanayounga mkono juhudi za serikali kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama leo kwa pamoja yameunga mkono kampeni ya kitaifa ya usafi ijulikanayo kama Niko Tayari inayoendeshwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

  Mashirika hayo ni UNICEF (Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto), Benki ya Dunia, Shirika la misaada la Uingereza (DFID), Shirika la Miradi la Ujerumani (GIZ) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA). Wawakilishi wa mashirika hayo walikutana kwenye ukumbi wa mikutano, Ubungo Maji, jijini Dar es salaam leo.

  Mashirika hayo ya maendeleo yamekubali kuunga mkono kampeini hiyo ilizinduliwa mwezi uliopita mjini Dodoma ikiwa na lengo la kuhamisha usafi wa mazingira kwa kila Mtanzania hasa kuwa na choo katika kila familia na kujenga utamaduni wa kunawa mikono baada ya matumizi yake. Kwa kufanya hivyo kutasaidia kupunguza vifo hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi nchini.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mratibu wa kampeini ya Nipo Tayari Anyitike Mwakitalima kutoka Wizara ya Afya alisema ili kuwa na huduma bora ya maji, usafi wa mazingira ni muhimu kuzingatiwa. ‘Kwa kujitokeza wadau wetu wa Maendeleo na kuunga mkono kampeini yetu ni kitu cha kupogezwa sana na pia niishara kwamba malengo yetu ya kuwa na mazingira salama yatafanikwa’, alisema Mwakitalima. 

  Zaidi ya mashirika 10 ya maendeleo ya kimataifa yamejitokeza kuunga mkono kampeini hiyo inayojumuisha mikoa yote Tanzania Bara.

  Kampeini hiyo ya usafi wa mazingira na matumizi bora ya choo (NikoTayari) inatarajiwa kuwa chachu ya upatikanaji wa maji safi na salama na kuboresha afya za Watanzania wote, mijini na vijijini.   Afisa Afya Mkoa wa Pwani Emmanuel Mwandepa akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.


  Mwakilishi wa TAMISEMI, Idara ya Afya, Mwajina Lipina akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeini ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora. 
  Mratibu wa huduma ya maji na usafi wa mazingira shule kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Technolojia Theresia Kuiwipe akitoa ishara ya Nipo Tayari kuunga mkono kampeni ya Taifa ya usafi wa mazingira wakati wa mkutano wa wadau wa maji uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iko chini ya Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii ikiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira na matumizi ya choo bora.

older | 1 | .... | 1264 | 1265 | (Page 1266) | 1267 | 1268 | .... | 1897 | newer