Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

MWENGE WA UHURU WAMALIZA ZIARA YAKE MKOANI RUKWA LEO, WAPAA ANGANI KWA NDEGE KUENDELEZA MBIO ZAKE MKOANI TABORA

$
0
0
Mwenge huo wa Uhuru umetembelea miradi 23 ya maendeleo na miradi 28 ya vikundi Mkoani Rukwa vyenye thamani ya fedha za kitanzania zaidi ya shilingi bilioni 3.4 ikiwa ni mchango wa Serikali kuu, Halmashauri, Wananchi na Wadau wengine wa maendeleo.
Ndege ndogo ya Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipaa angani katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga leo tarehe 23 Julai 2013 ikiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa sita pamoja na Mwenge wa Uhuru utakaoenda kukabidhiwa Mkoani Tabora na Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa. Wakimbiza mwenge hao ni Ndugu Juma Ali Simai (Kiongozi), Zamda A. John, Christopher Emmanuel, Seperatus Lubinga, Zuwena Abdallah na Mgeni S. Mgeni.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya Mwenge wa Uhuru mara baada ya kukamilisha ratiba yake katika Wilaya hiyo na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla. Mkuu huyo wa Mkoa atasafiri kwa ndege kuukabidhi Mwenge huo Mkoani Tabora.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa hotuba ya kuwaaga wakimbiza mwenge kitaifa na Mwenge wa Uhuru muda mfupi kabla ya kusafiri na Mwenge huo kwa ajili ya kuukabidhi Mkoani Tabora mapema leo tarehe 23 Julai 2013. Katika hotuba yake hiyo aliwapongeza wakimbiza Mwenge wote na wananchi Mkoani Rukwa kwa kufanikisha zoezi hilo kikamilifu na kuwapa vyeti vya pongezi wakimbiza Mwenge hao wa kitaifa.
 Picha ya pamoja kati ya kikundi cha matarumbeta kilichokuwa mstari wa mbele katika kutumbuiza kwenye ziara ya Mwenge Mkoani Rukwa na baadhi ya wakimbiza Mwenge kitaifa na mratibu wa Mwenge Mkoa wa Rukwa Ndugu Abubakari Serungwe wa kwanza kulia (mbele). 

 
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Juma Ali Simai akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga katika Stendi kuu ya mabasi Mjini Sumbawanga tarehe 22 Julai 2013. Kulia ni Diwani wa kata ya katandala Ndugu Kisabwite na Mbunge Jimbo la Sumbawanga Mjini Aeshi Hillal.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kmanta akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani humo tarehe 20 Julai 2013.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo machachari katika mbio za mwenge wa Uhuru Moshi Chang'a akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka Mwenge wa Uhuru mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Kalambo tarehe 21 Julai 2013.
 Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Methwew Sedoyyeka akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a tarehe 21 Julai 2013 na kuahidi kuukimbiza katika wilaya yake kwa amani, nguvu na uadilifu mkubwa.
 Baadhi ya raia wa kigeni nao waliomba kupiga picha na Mwenge wetu wa Uhuru.
Wananchi na wanafunzi walihamasika vya kutosha na Mwenge wa Uhuru kiasi cha wengine kupanda juu ya miti ili waweze kupata taswira yake mwanana.
 Wanafunzi na wananchi wakiwa juu ya miti kushuhudia Mwenge wa Uhuru na ujumbe wake.
  Kwa wengine kuuona Mwenge wa Uhuru vizuri haikuwa kazi rahisi walilazimika hata kuhatarisha maisha yao.
 Picha ya pamoja kati ya mratibu wa Mwenge Mkoani Rukwa ndugu Abubakar Serungwe na baadhi ya wakimbiza mwenge kitaifa pamoja na katibu wa CCM Sumbawanga Mjini Mama Silaf Maufi. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa "rukwareview.blogspot.com)

wananchi na wadau kushiriki kutoa maoni kwa ajili ya Sera Mpya ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Maendeleo,

$
0
0
Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prisca Ulomi (kushoto) akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu ushiriki wa wananchi na wadau mbalimbali katika utoaji wa maoni kwa ajili ya kuandaa Sera Mpya ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Maendeleo, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa. PICHA ZOTE NA ELIPHACE MARWA-MAELEZO



  • Mkurugenzi, Idara ya Habari MAELEZO, Bw. Asah Mwambene;

  • Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Bi. Zamaradi Kawawa;

  • Ndugu Wanahabari;

  • Ndugu Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,


Habari za asubuhi.


  1. Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wote mliofika katika mkutano huu muhimu wenye lengo la kuwaalika wananchi na wadau wa Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)  kutoa maoni yao kwa ajili ya kuandaa Sera mpya ta TEHAMA kwa Maendeleo.  Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tayari imeanza kuhuisha Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2003 pamoja na kuandaa mpango wake wa utekelezaji. Mahuisho haya ya Sera ya TEHAMA yanalenga kuiwezesha nchi na Taifa letu kwenda sambamba na ukuaji wa kasi wa Teknolojia  ya Habari na Mawasiliano duniani na matumizi yake kwa wananchi. Pia ukuaji na mabadiliko ya kasi yanayotokea kwenye sekta hii yanahitaji uwekezaji mkubwa na wenye kushirikisha sekta na wadau mbalimbali na hivyo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia  imeona ni wakati muafaka Sera iliyopo ihuishwe ili Sekta iweze kuendeshwa kwa ufanisi zaidi na hatimaye kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya nchi.






  1. Zoezi hili la uhuishaji wa Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003 ni sehemu ya utekelezaji wa  program ya kujenga Jamii Habari na Kuendeleza Sekta ya TEHAMA (TANZICT) inayofadhiliwa kwa pamoja baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Finland katika jitihada za kuendeleza Sayansi, Teknolojia, ubunifu na TEHAMA hapa nchini ili Sekta iweze kuchangia ipasavyo katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya hapa nchini. Kwa kuwa masuala ya utumiaji wa huduma za TEHAMA na manufaa yake kwa wananchi ni suala mtambuka, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inashirikisha wadau kutoka katika sekta mbalimbali ili waweze kufahamu na kujenga uelewa wa pamoja mapema na hatimaye kuwa na Sera mpya ya TEHAMA kwa Maendeleo inayotekelezeka na yenye kujibu changamoto zinazowakabili wananchi na kuleta maendeleo ya Taifa letu.



Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,


  1. Ni dhahiri kuwa sekta ya Mawasiliano inakuwa kwa kasi kubwa sana duniani kote na hapa nchini kwetu pia. Lengo la kuhuisha Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2003 ni kutengeneza Sera itakayochochea maendeleo endelevu ya Kijamii na Kiuchumi hapa nchini; ikiwa ni kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta, kujumuisha masuala ambayo hayakuwepo katika Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003 na kujumuisha maendeleo makubwa ya kiteknolojia yaliyotokea katika Sekta ya TEHAMA kwa kipindi cha miaka kumi (10) tangu Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003 iliporidhiwa na kuanza kutekelezwa na Serikali.




  1. Dhumuni la zoezi hili ni kupata Sera ya Taifa ya TEHAMA endelevu na kamilifu itakayokidhi mahitaji ya huduma za TEHAMA na inayojibu hoja zinazotokana na mabadiliko ya kasi ya kiteknolojia yanayotokea Duniani kote; Sera itakayotekelezeka katika nyanja za kiuchumi na kijamii kwa kuwa TEHAMA ni suala mtambuka; na kuhakikisha inatoa mchango wake ipasavyo kama kichochezi kikuu cha maendeleo katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa kila siku katika sekta mbalimbali na kurahisisha maisha ya wananchi. Zoezi hili la uhuishaji wa Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2003 linawahusisha wadau na wananchi wote kwa ujumla ili kufanikisha upatikanaji wa Sera shirikishi; jumuishi na itakayomilikiwa na wadau wote kwa ajili ya kuleta ufanisi katika utekelezaji wake.



Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,


  1. Sera hii mpya inatarajiwa kujikita katika Nguzo kuu Nane tofauti na Sera ya mwaka 2003 ambayo ilikuwa na jumla ya nguzo kumi. Nguzo ya Kwanza inahusu maendeleo ya rasilimali watu na uongozi katika TEHAMA (ICT Leadership and Human Capital Development) na inalenga Kuwa na Jamii Habari inayoendeshwa na viongozi mahiri wenye ujuzi na uwezo wa hali ya juu katika TEHAMA ili kwenda sambamba na viwango vya Kimataifa katika kufikia malengo ya maendeleo ya Tanzania. Nguzo ya pili inazungumzia upatikanaji wa huduma za mawasiliano na miundombinu ya TEHAMA (ICT Access and Infrastructure) yenye lengo la Kuwa na Jamii Habari inayoendeshwa kupitia upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wote na miundombinu ya TEHAMA yenye uwezo mkubwa. Ya tatu ni maendeleo ya sekta ya TEHAMA (ICT Sector development). Nguzo hii inasisitiza Tanzania kuwa na Sekta mahiri ya TEHAMA katika uzalishaji na uendelezaji wa huduma za kisasa za TEHAMA kuanzia ngazi ya viwanda vidogo vidogo hadi vikubwa.


  1. Nguzo ya nne ni huduma mtandao na uendelezaji wa maudhui ya kitaifa/nyumbani (E-services and local content development) Nguzo hii imejikita katika utoaji huduma za kielektroniki za nyongeza zinazozingatia mahitaji na mazingira ya mtumiaji na zenye ubora wa hali ya juu ambazo zitawezesha maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini. Ya tano ni Ulinzi, Usalama na Viwango katika TEHAMA (ICT Safety, Security and Standardization). Nguzo hii inaitaka nchi yetu ya Tanzania kuwa nchi salama kielektroniki; na yenye mifumo na huduma za TEHAMA zinazotegemewa na kuaminiwa ambazo zitawezesha uchumi endelevu. Nguzo ya sita inahusu masuala ya kisheria, udhibiti na mfumo wa uendeshaji TEHAMA  nchini (Legal, regulatory and Institutional framework). Nguzo hii inatoa mwelekeo wa Tanzania kuwa nchi yenye mfumo madhubuti wa kisheria na kiudhibiti katika TEHAMA unaohusisha matumizi bora ya vyombo vya kisheria yanayozingatia utendaji bora Kikanda na Kimataifa katika kuendeleza na kulinda huduma za kielektroniki. Ya saba ni Ushirikiano wa Kitaifa, Kikanda na Kimataifa katika nyanja ya TEHAMA (Local, Regional and International Cooperation). Nguzo hii inaitaka Tanzania kuwa Taifa linaloongoza katika kutambua na kutumia ushirikiano wa kimkakati katika TEHAMA Kitaifa, Kikanda na kimataifa katika kujenga Jamii Habari. Na nguzo ya nane inahusu Sekta za uzalishaji (Productive sectors). Nguzo hii ina lengo la kuifanya Tanzania kuwa na Sekta za uzalishaji madhubuti, zenye ufanisi na ambazo zinashirikiana  ili kuwa na matokeo ya matumizi ya TEHAMA katika utendaji kazi katika sekta hizo kama vile ya madini, nishati, mafuta na gesi, utalii, kilimo, viwanda na biashara, ujasiriamali, na huduma za kifedha.





Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,


  1. Kwa kutambua mchango wa wadau na wanachi kwa ujumla katika kufanikisha ukuaji wa Sekta ya TEHAMA; matumizi yake kwa wanachi katika kutatua changamoto zinazowakabili katika maisha ya kila siku; na mchango wa Sekta ya TEHAMA katika kuleta maendeleo ya Taifa letu, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia inatoa fursa kwa wadau na wananchi wote kwa ujumla kushirikiana na Wizara kutoa maoni yatakayofanikisha uaandaji wa Sera mpya ya TEHAMA kwa Maendeleo. Wadau na wananchi wote mnaalikwa kutoa maoni yenu kwa kutumia barua pepe ya Wizara ambayo ni mst@mst.go.tz, kutembelea tovuti ya Wizara www.mst.go.tz na kuwasilisha kwa maandishi Wizarani kwa Katibu Mkuu kwa barua kupitia sanduku la Posta 2645, Dar es Salaam. Wizara itapokea maoni hayo kuanzia tarehe 24 Julai, 2013 hadi tarehe 15 Agosti, 2013. Maoni yenu ndugu wananchi na wadau wa Sekta ya TEHAMA yatapokelewa; kuchambuliwa; na kujumuishwa kwenye Sera mpya ya TEHAMA kwa maendeleo (ICT4D).


Ndugu Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana,

  1. Kabla sijamaliza, kwa niaba ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau na wananchi wote wanaoshiriki kwa njia moja au nyingine katika kuandaa Sera hii mpya ya TEHAMA kwa Maendeleo. Natoa wito kwa watanzania na wadau wote kutoa maoni kuhusu Sera hii kuanzia tarehe 24 Julai, 2013 hadi tarehe 15 Agosti, 2013 ili kufanikisha uaandaji wa Sera kwa wakati.

Asanteni kwa kunisikiliza.


Imetolewa na;

Prisca J. Ulomi

Afisa Habari Mwandamizi,


Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Shiwata watakiwa kuchangia ujenzi wa nyumba zao Mkuranga.

$
0
0
 MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umewataka wanachama wake kuchangia ujenzi wa nyumba zao katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga ili kukamilisha mradi huo.
 
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caasim Taalib alisema jana Dar es Salaam katika mkutano wa wanachama wanaochangia ujenzi ambapo mpaka sasa nyumba 29 zimekamilika na wanachama 220 wamechangia ujenzi na jumla zilizokusanywa ni mil. 82.5.

Alisema SHIWATA haina fedha za kujenga nyumba za wanachama wake wala haina chanzo cha mapato kama si kwa njia ya kuchangishana na baada ya hapo kuwakabidhi wale waliokamilisha uchangiaji wa ujenzi wa nyumba hizo.

‘Ujenzi wa nyumba za wasanii utafanikiwa kwa kila mwanachama kuchangia nyumba yake kwa kujiaminisha kuwa hakuna utapeli wala biashara katika gharama za ujenzi wa nyumba hizo’alisema Taalib.

SHIWATA ambayo inaundwa na wasanii, wanamichezo, wanahabari na vijana wapatao 7,000 ilikuwa ikabidhi nyumba Agosti mwaka huu kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.

Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni mwanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).  

 Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 29 kwa ajili ya wasanii katika eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili kujikwamua kimaisha.

RAIS DKT SHEIN AONZGOZA MAZISHI YA WANAJESHI WALIOUWAWA DARFUR

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akijumuika na Vingozi na
Waislamu wengine katika Hitma ya wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa
risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni,Merehemu  Sgt Shaibu
Shehe Othman, na  Cpl Mohammed Juma Ally  iliyosomwa katika msikiti
Masjid Nuru Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na
Waislamu wengine katika kuwaswalia  Merehemu Sgt Shaibu Shehe
Othman,na Cpl Mohammed Juma Ally ,mbele katika msikiti  Masjid Nuru
Muhammad,Mombasa Mjini Unguja leo,wanajeshi waliouwawa kwa kupigwa
risasi Jimbo la Daafur nchini Sudan hivi karibuni.


Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
wakibeba Jeneza la mwili wa Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,baada ya
kuwasilim katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa
ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la
Daafur nchini Sudan hivi karibuni.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) na viongozi wengine
walihudhuria katika mazishi ya Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman,
katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar jana,akiwa ni miongoni
mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Daafur nchini
Sudan hivi karibuni.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia udungo katika Kaburi la Marehemu Sgt
Shaibu Shehe Othman,aliyezikwa leo Mwanakwerekwe Mjini Unguja, akiwa
ni miongoni mwa wanajeshi wa jeshi la Ulinzi la Tanzania 7 waliouwawa
hivi karibuni  Nchini Sudan Jimbo la Daafur.


Baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na
Ndugu na Jamaa wa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na  Cpl Mohammed Juma Ally ,waliofurika katika viwanja vya makaburi ya
Mwanakwerekwe,ambapo ndipo walipozikwa leo,mchana.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati)  na Vingozi na
Waislamu,wakiangalia  Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la
Tanzania,walipokuwa wakitoa hesha ya mwisho kwa marehemu Sgt Shaibu
Shehe Othman,wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Mwanakwerekwe leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.


==========     ===========
Na Ali Issa,Maelezo Zanzibar.              
                                                  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi  Ali Mohamed Shein leo alikuwa miongoni mwa wananchi wa Zanzibar walio hudhuria Mazishi ya walio kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa  Tanzania JWTZ Sajenti Shaibu Shekhe Othuman na Koplo Mohamed Juma Ali Wenye asili ya Zanzibar walio fariki dunia kwa shabulizi la kushutukiza na waasi wakati wakilinda Amani Nchini Darfur.


Dkt Shein akiambatana Wananchi  na viongozi mbali mbali wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania  wakiwemo Makamo wa Pili Rais  Balozi Seif Ali Iddi ,Wazi wa Ulizi Tanzania Shamsi Vuai Nahodha ,Waziri wanchi Afisi ya Rais Ikulu mwinyihaji Makame Mwadini, Mkuu wa Mkoa Mjini magharibi Abdalla Mwinyi Khamis Bregedia Jeneral  Kamanda wa Bregedi ya Nyuki Sharif Sheikhe Othuman  na wakuu wa Vikosi  vyote vya  Ulizi na Usalama hapa Zanzibar.


Mazishi hayo yakiambatana na sala ya Maiti iliosaliwa katika Msikiti  Mkuu wa Ijumaa wa Noor Muhamad S.A.W ulioko  Mombasa Mjini Unguja, yalielekea Mwanakwerekwe kwa Mzishi  yakiongozwa kwa Gwaride la Jeshi kwa mwendo wa pole na kutoa  salamu zao za Mwisho.


Wakitoa salamu za  Rambi rambi ASP Luten Sabato Devid okoku na FA Kepten Franki Adam Mtwazi   kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya  Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kua, amestushwa na kuhuzunishwa kwa tukio la Jumamosi Julai 13 wiki iliopita ambalo lilifanywa na waasi na hatimae kupoteza maisha kwa askari wao Saba kitu ambacho si kimetia huzuni kwa familia bali hata kwa Taita la Tanzania, hivyo wako pamoja kwa kuomboleza katika kipindi hiki kigumu.


Wamesema  Sajent Shaibu na Koplo Mohamed watakumbukwa daima  kutokana na mchango wao walio utoa katika uhai wao wakiwa watumishi wa taifa hili na Mataifa Mengine ya Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla.


Wakitoa wasfu wa MP 72 Shaibu Sheikhe alizaliwa mwaka 1972 katika kijiji kiitwacho Urusi kiliopo mkoa wa Mjini Magharibi na alipata Elimu yake ya Msingingi kijijini hapo na kumaslizia  elimu yake ya sekondri katika skuli ya  Bembela mwa 1991na alijiunga na jeshi hilo mwaka 1992 .Sajenti Shaibu ameowa na ameacha mke na watoto wanne .


Koplo Mohamed alizaiwa 1981 huko pemba katika kijiji kiitwacho Konde na alipata Elimu yake ya msingi na sekondari katika skuli ya Miti ulaya mwaka 1989 -2002 na  alijiunga na jeshi la wana nchi Tanzania akiwa ametumikia kwamuda wa miaka 11na siku kuminambili hadi kufa kwake, ameacha mke na mtoto mmoja.Muungu aziweke Roho za Marehemu Peponi Amini.


Katika hali isiyotarajiwa miongoni mwa gari zilizokuwa zikienda mazishini gari moja aina ya Rova namba JW 2955 kutoka kikosi cha 101 ilipata ajali katika maeneo ya Mwanakwerekwe na kujeruhi watu 19 wakiwemo askari watatu wa JWTZ.


Ajali hiyo ilisababishwa na msongamano wa magari ambapo iliacha barabara na kuanguka baada ya dereva aliyejulikana kwa Salim Mansur MT 98501 kushindwa kuidhibiti gari hiyo.


Baada ya Ajali hiyo majeruhi hao walipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mnazi Mmoja kwa ajili ya matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.


iliyokuwa imebeba wanajeshi na Raia kwa ajili ya mazishi na kujeruhi imeelezwa kuwa wakati marehemu hao wakipelekwa mazishini Gari ya Askari hao aina Rova ikiwa imebeba askari na wana nchi waendao mazikoni ilianguka mwana kwerekwe ikidaiwa gari hiyo kupakia watu wengi iliopelekea kuzidi mzigo na kupinda krosi karibu na eneo la mazishi Gari hiyo ilianguka na watu kuumia vibaya badhi yao.


SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar YALIVUNJILIA MBALI SHIRIKA LA UTALII ZANZIBAR

$
0
0
NA MIZA KONA / HABARI MAELEZO ZANZIBAR

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kulivunja Shirika la Utalii Zanzibar kutokana na changamoto zinazolikabili Shirika hilo hivi sasa.

Akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2013/2014 huko katika Baraza la Wawakilishi Chukwani,Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema sababu kubwa ya kuvunjwa shirika hilo ni kushindwa kuhimili ushindani uliopo wa biashara ya sekta hiyo.

Amesema kuwa taratibu za kulivunja rasmi Shirika la Utalii la Zanzibar zinatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao kuanzia sasa.

Akizungumzia Shirika la Utangazaji Zanzibar(ZBC) amesema linatarajia kuweka vifaa vipya vya Studio pamoja na kununua gari moja ya kurushia matangazo ya moja kwa moja kutoka nje ya studio hasa katika sherehe na maadhimisho ya Kitaifa.

Waziri Said Ali Mbarouk amesema lengo la Wizara ni kusimamia mazingira bora ya kazi ili kuliwezesha Shirika la ZBC kutoa huduma bora na zenye ufanisi.

Akitoa maoni ya Kamati ya Mifugo, Utalii, Uwezeshaji na Habari Mwenyekiti wa kamati hiyo Mlinde Mbarouk Juma wameshauri watendaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar kubadilika kiutendaji. kufanyakazi kwa umakini zaidi na kuacha kufanyakazi kwa mazoea .

“Kwa kuwa uendeshaji wa Mfumo wa Digital unahitaji umakini wa hali ya juu kwa kutokuwa makini tutakuja kulaumiana na kuona ni bora tungelibaki katika mfumo wa analogia”, alisema Mwenyekiti Mlinde.

Aidha ameeleza kuwa Utalii ni chachu ya maendeleo katika nchi jirani, lakini bado Zanzibar haujapewa kipaumbele na kuwekewa mikakati na kuwanufaisha wananchi wengi.

“Kamati inatoa rai kwamba dhana ya Utalii kwa wote itekelezwe kwa vitendo na wala sio maneno pamoja na kuwekwa sera na sheria ambazo zitapunguza gharama kwa wazawa.” Alisisitiza Mlinde.

Wameishauri Wizara kujidhatiti katika kuutangaza Utalii wa Zanzibar kwani kufanya hivyo utaweza kuongeza soko katika mataifa mbali mbali na kuitangaza katika nchi za jirani.

Katika kutekeleza majukumu yake Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo imeomba iidhinishiwe jumla ya shilingi 9,985,000,000 kwa kazi za kawaida na shilingi 510,000,000 kwa kazi za maendeleo.

MBUNGE MSIGWA AWATAKA WANANCHI WA IRINGA KUJIKITA KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO NA KUACHANA NA SIASA ZA CHUKI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Iringa  mjini mchungaji PETER   MSIGWA  amewataka wananchi wa manispaa ya Iringa kujikita katika shughuli za maendeleo na kutowajali viongozi wa siasa wanaonadi siasa  za chuki.
 
Ameyasema hao wakati wa mkutano na wananchi katika kata ya Mlandege na kuwataka wananchi hao kupokea misaada  watakayopewa na kiongozi yoyote wa siasa.Mbunge  MSIGWA  ameongeza kuwa kutokana na  kuendeleza  shughuli za maendeleo kwa wananchi wake amewahakikishia wapinzani wake kuwa kamwe hawataweza kulikomboa jimbo hili la iringa mjini.
 
Kwa upande mwingine Mbunge huyo amesema hatobadili msimamo wake wa kuwarudisha wafanyabiashara wadogowadogo maeneo ya mjini kwa ajiri ya kufanyia biashara hata kama si maeneo ya mashine tatu ambapo manispaa inawazuia.Amesema kuwa yeye kama mbunge amewekwa kama msemaji wa wananchi kwa hiyo ni lazima atimize wajibu wake.
 
Msingwa amesema kuwa hayuko tayari kuona wananchi wake wakihangaika hasa wafanyabiashara wadogo wadogo katika jimbo lake wakati walimchagua yeye kama mwakilishi wao katika kero zao.
 
Aidha ameongeza kuwa hatounga mkono suala la kuwekwa standi ya haice katika maeneo ya mashine tatu wakati tayari manispaa imekataa hilo si eneo la kufanyia biashara.

NAIBU MEYA WA MKOA WA IRINGA APATIKANA

$
0
0
 Leo umefanyika uchaguzi wa Naibu Meya katika manispaa ya Iringaambapo ushindi katika uchaguzi huu amekuwa ni GEREVAS NDAKI ambaye alikuwa akishikilia nafasi hiyo toka awali.
 
Uchaguzi huo umefanyika katika kikao cha baraza la madiwani wa manispaa ya iringa  ambapo umeambatana na kamati mbalimbali za baraza hilo ikiwemo kamati ya afya, mazingira fedha na nidhamu.
 
Katika uchaguzi huo ni mugombea mmoja tu ambaye aliwania nafasi hiyo kupitia chama cha mapinduzi ccm na wajume 23 ndio walishiriki katika uchaguzi huo na kura moja iliharibika.
 
Kwa upande wake naibu meya aliyechaguliwa amewashukuru wote waliomchagua na kusema kwa hata hiyo kura moja ambayo haijamchagua anaishukuru pia kwani inatokana na na mhusika kutoridhika na kazi ya ke hivyo bado anaowajibu wa kujipanga upya ili aweze kumfanya mtu huyo akubaliana na uwajibikaji wake.

Uzazi pasipo mipango unavyowatesa wanawake Kishapu

$
0
0
 Bi. Rejina Moshwa (37) mkazi wa Kijiji cha Isoso akizungumza na mwandishi wa habari kutoka Clouds FM Aziz Kindamba
=======  ========  =======
Uzazi pasipo mipango unavyowatesa wanawake Kishapu

Na Thehabari.com, Kishapu

WASUKUMA ni moja ya makabila nchini Tanzania ambayo awali yalishikilia desturi ya familia kuwa na idadi kubwa ya watoto. Familia moja yaani baba na mama waliendelea kuzaa kadri walivyo jaaliwa kupata watoto bila kujali ukubwa wa familia. Mume pia hakuwa na kizuizi katika familia cha kuongeza mke mwingine endapo atakuwa na ardhi (mashamba) na mifugo (hasa ng'ombe) ya kutosha kuweza kuihudumia familia aliyonayo.

Wapo walioamini kwamba kuwa na ukubwa wa familia ni kuongeza nguvu kazi katika uzalishaji kwa kutumia ukubwa wa familia. Hata hivyo pia wapo walioamini uzazi ni mpangilio wa Mungu hivyo haupaswi kupangiliwa na wazazi bali mola mwenyewe. Hivyo basi familia za imani hii ziliendelea kuza hadi pale uwezo wa kupata watoto ulipopotea wenyewe au vizuizi vingine.

Hata hivyo sasa hivi mambo yamebadilika kiuchumi, hali ni ngumu hivyo familia nyingi zinapangia idadi ya watoto. Waliojisahau na kuendelea kuzaa idadi kubwa ya watoto pasipo na uwezo kuwamudu wanajuta na kutamani wangelipata uelewa wa elimu hiyo awali.

Hali hii ya majuto ndiyo inayozikuta baadhi ya familia katika vijiji anuai Kata ya Kishapu, mkoani Shinyanga, baada ya kuzungumza na mwandishi wa makala haya. Familia hizi zimejikuta na idadi kubwa ya watoto kiasi cha baba na mama kushindwa kuwapatia mahitaji ya msingi watoto wao hivyo familia kuendelea kuwa na maisha duni kiuchumi.

Bi. Rejina Moshwa (37) mkazi wa Kijiji cha Isoso ni miongoni mwa familia zinazojutia uamuzi wa kuwa na idadi kubwa ya watoto. Anasema familia yao ilikuwa na jumla ya watoto 10, lakini bahati mbaya wawili walifariki dunia hivyo kubakia na watoto nane ambao ni mzigo mkubwa hivi sasa.

"...Hatukuwa na elimu ya kupangilia watoto tulizaa mfululizo kadri ya tulivyo jaaliwa, lakini watoto hawa sasa ni mzigo kwetu, tunajuta. Tumeshindwa kuwasomesha na wamekosa muelekeo...na hata upatikanaji wa chakula cha familia nzima ni tatizo...hasa ukichangia na hivi karibuni ukame uliibuka eneo hili mambo yamezidi kuwa mabaya," anasema Bi. Moshwa.

Paschal Kulwa Manyinzi (42) ni mume wa Bi. Rejina Moshwa, anasema licha ya kuwa na mifugo kidogo yeye ni mkulima wa mazao mchanganyiko yaani Pamba, mtama, karanga na viazi. Anakiri watoto wake mwenyewe kuwa mzigo mkubwa kimalezi kwa sasa. "Wakati tunaanza kuzaa nilifuata mila na desturi za zamani, unajua zamani suala la kuzaa halikuwa la kupangilia, mtu ulikuwa unazaa tuu...suala la kupangilia limeanza juzi.

"Zamani (enzi za wazazi wetu) idadi kubwa ya watoto katika familia ilikuwa ni nguvu kazi...lilikuwa likizaidia katika kilimo...kama mtu ulikuwa hauna familia kubwa ulitapata shida kwenye kilimo. Lakini dunia ya sasa huwezi kuzaa kama mimi ni mzigo," anasema Manyinzi.

Hata hivyo licha ya ukubwa wa familia hii haina ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo kwani heka tano ambazo inadai ilipewa kwa urithi toka kwa wazazi wa Manyinzi imetwaliwa na Serikali kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kubaki heka moja. Familia hii inalazimika kukodi ardhi kwa ajili ya kilimo kila msimu wa kilimo.

Modesta Machia (43) ni Mkazi wa Kijiji cha Kishapu, Kata ya Kishapu Wilaya ya Kishapu. Anasema yeye na mumewe wana jumla ya watoto nane walio hai kati ya 10 ambao walibahatika kuwazaa. Anasema watoto wawili walitangulia mbele za haki. Anasema watoto walionao kwa sasa ni mzigo katika malezi.

"...Mwanzoni tulikuwa tunazaa haraka haraka kwa kuwa hatukuwa na uelewa juu ya uzazi wa mpango...lakini laiti ningejua nisingelikubali kupata idadi kubwa ya watoto kama ilivyo sasa...lakini nimepata uelewa nikiwa nimechelewa na nimefunga kizazi kabisa," anasema Bi. Machia. Anasema mume wake kwa sasa ni muhudumu wa usafi katika zahanati ya kijiji chao.

Mwanamama huyu anashauri familia nyingine kuzaa kwa mpangilio na kuzingatia kipato cha familia ili kupunguza umaskini wa kiuchumi katika familia. Anasema mwanamke kuzaa mfululizo hushindwa kuchangia shughuli za kujiongezea kipato katika familia na hata kuchoka mapema kwenye shughuli za uzalishaji mali.

Hata hivyo changamoto nyingine kwa uzazi wa idadi kubwa ya watoto ipo kwa akinamama pekee, kwani inapotokea mke na mume wakatofautiana na kufikia kuachana, idadi kubwa ya kinababa humuachia mke watoto waliozaa na yeye kwenda kuoa sehemu nyingine. 

Bi. Paskazia John mama mwenye watoto nane amekubwa na hali kama hiyo, kwani baada ya kuzaa na mumewe watoto nane walikorofishana na kutengana hivyo mwanaume kumuachia watoto wote nane ambao kwake ni mzigo mara dufu. Anasema unapoolewa katika familia ya kisukuma hasa maeneo ya vijijini kuzaa idadi kubwa ya watoto ni kitu cha kawaida. Anaongeza kuwa na endapo utaonekana mvivu wa kuzaa mwanaume anaweza kukuongezea mke mwenzako ili akusaidie.

Anabainisha kuwa baadhi ya wanaume wa kisukuma wanaamini kwamba kuwa na idadi kubwa ya watoto ni sawa na kuwa na uwezo kiuzalishaji, yaani watoto watatumika kama nguvu kazi shambani. Lakini kwa kuwa kaya nyingi za maeneo ya wasukuma mama (mke) pamoja na watoto huwa ndiyo watendakazi wakubwa mashambani huku baba akibaki kuwa msimamizi na kiongozi wa familia wanawake ndiyo wenyemzigo mkubwa katika familia nyingi za kuangaika na watoto.

Hata hivyo si familia zote zenye mzigo mkubwa wa watoto wanashindwa kuzimudu. Ally Sosoma (60) ni mkulima na mkazi wa Kijiji cha Isoso, katika familia yake ana jumla ya watoto 20 ambao wamepatikana ndani ya wake watatu. Anasema familia yake imeanza kuwa mzigo mkubwa kwake baada ya kuanza ukame mfululizo yaani mwaka 2011 hadi sasa. Anaongeza kuwa hapo nyuma haikuwa mzigo kwa kuwa alikuwa anajituma na ardhi ya kutosha hivyo alizalisha chakula na ziada ya kutosha jambo ambalo haikuwa tabu kuendesha familia yake.

Anasema mila na desturi ya kuwa na idadi kubwa ya watoto ameirithi kutoka kwa baba yake ambaye alikuwa na wake watatu. "...Pamoja kwamba baba alikuwa na wake watatu lakini baba yangu mkubwa alikuwa na wake saba hivyo alikuwa na watoto wengi sana, hivi ndio chanzo cha kuwa na idadi kubwa ya watoto...mimi nilipenda na ndiyo maana nimezaa wengi. Lakini si kweli kwamba watu wanasema ukioa mwanamke wa kisukuma na kutozwa ng'ombe nyingi lazima akuzalie watoto wengi," anasema Sosoma.

Kwa upande wake, Yamesa Sheka mkulima mkazi wa Kishapu; anasema mila na desturi za kuwa na idadi kubwa ya watoto kwa sasa zimepitwa na wakati kutokana na kupanda kwa gharama za maisha. Idadi kubwa ya watoto inachangia umaskini katika familia nyingi kwa kile wazazi kushindwa kuwahudumia watoto. Kijana huyu anawatoto saba kwa sasa lakini anajuta kuwapata kwani ni mzigo kuwalea. "...Ningelipata elimu ya uzazi mapema ningelikomea watoto wanne tu, lakini haikuwa hivyo," anasema Sheka.

Maxmilian Lugembe ni Ofisa Mtendaji Kata ya Kishapu, akizungumzia utaratibu wa familia kuzaa idadi kubwa ya watoto anasema inachangiwa na mfumo dume ambao wameuendekeza familia nyingi za kisukuma. Anasema katika mfumo huo baba ndiye mwenye maamuzi ya kuongeza watoto bila kushauriana na mwenza wake. 

"...Maeneo haya familia kuwa na watoto 10 au 8 ni kitu cha kawaida. Elimu inatolewa ya uzazi wa mpango ambayo anaipata mama pekee lakini kutokana na mfumo dume mama hana uamuzi katika familia hivyo unakuta aisaidii...kwanza wanaume hawataki wake zao kujiusisha na uzazi wa mpango (kutumia dawa kupanga uzazi) na wengine wakifanya kwa siri na kugundulika unakuwa ugomvi mkubwa," anasema Lugembe. 

"Inafikia wakati hata wanawake wanaoonekana kupanga uzazi katika ndoa zao wanaaminika kuwa ni wahunu, yaani wanataka kupumzika kuzaa ili wapate nafasi ya kufanya maovu (uhuni) nje ya ndoa. Wapo wanaoamini kuwa ishara ya kumpenda mwanaume ni kumzalia watoto...unazaa uwezavyo hadi uchoke," anasema.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MAKAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi na Bw. Manoj Kohli wa Airtel ambaye pia ni Mkurugenzi wa Pamoja wa chama hicho alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Beatrice Singano, mmoja wa wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na maofisa waandamizi wa Wizara ya pamoja na  wajumbe wa Chama cha  Makampuni ya Simu za mkononi alipokutana nao kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.PICHA NA IKULU

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA UINGEREZA TONY BLAIR, RAIS RAJOELINA WA MADAGASCAR IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar Mhe Andy Rajoelina Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza  Rais wa serikali ya mpito ya Madagascar Mhe Andy Rajoelina baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwonesha mandhari mbalimbali Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe. Tony Blair na mkewe Cherie Blair Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013.PICHA NA IKULU.

STARS YAMALIZA KAMBI YAKE JIJINI MWANZA KUONDOKA KESHO KUELEKEA UGANDA, KIM POULSEN ASEMA "NG'O SING'ATUKI" - KASEJA BADO CHAGUO BORA.

$
0
0
Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen (kulia) akizungumza  na wandishi wa habari (hawako pichani) ikiwa ni siku moja kabla ya kuondoka jijini Mwanza mara baada ya kumaliza kambi, kushoto ni Afisa habari wa TFF Michael Wambura. 
NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
Ni takribani majuma mawili sasa Taifa Stars imekuwa jijini Mwanza ikiweka Kambi kuelekea kipute cha marudiano na 'The Cranes', katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa jumamosi hii ya tarehe 27 mwezi wa 7mwaka 2013 mjini Kampala.

Sasa kambi imefikia tamati, yamesalia masaa kadhaa ambapo kesho mchana majira ya saa 7 na dakika 25, wawakilishi hao wa taifa la Tanzania, Taifa Stars wataondoka kwa ndege ya Shirika la Precission Air kuelekea nchini Uganda kuisaka tiketi ya CHAN. 


MSIKILIZE KIM POULSEN KWA KUBOFYA PLAY..

KWA UFUPI: Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen amezungumzia mapengo yaliyopo kwenye kikosi chake kuanzia kutokuwepo kwa Kapombe kwenye idara ya ulinzi na sasa Mwinyi Kazimoto katika idara ya kiungo, bila shaka kikosi kitakuwa na utofauti ambao anaona ni sehemu ya marekebisho na anamaboresho.

Lakini pia hakufurahishwa na namna alivyoondoka Mwinyi Kazimoto akitegemea Shirikisho la Soka nchini TFF litatumia busara zake kumwajibisha mchezaji huyo kukosa uzalendo.

Amezungumzia pia baadhi ya maoni ya wadau wa soka mfano suala la Juma Kaseja kutajwa na baadhi yao kuwa amezeeka, kiwango kimeshuka hivyo hastahili kuchezea Taifa stars. Amehoji
-Hivi factor ya msingi unayotizama kwa mchezaji ni umri wake au kiwango chake uwanjani? Kwa idara ya goalkeeping kwa uri wa Kaseja miaka 29 ni umri mzuri sana kwa golikipa, lakini pamoja na hayo yote ana kiwango kikubwa mno.

Amejaribu pia kuizungumzia idara ya difensi' kwa tathimini ya baadhi ya mechi kubwa ambazo timu ya taifa imecheza siku zilizopita akisema kuwa kwa wale wanaofikiri kuna mapungufu makubwa kwenye safu ya ulinzi, mechi ngumu dhidi ya Zambia, dhidi ya Cameroon, akiuliza magoli mangapi yalifungwa goli la Stars kwenye mechi hizo?... jibu ni goli moja huku Stars ikiibuka na ushindi.

Hivyo haoni kama kuna tatizo kubwa kama linavyozungumzwa bali kilichokosekana kwa wachezaji wake hususani kwa mechi dhidi ya Uganda ni kukosa umakini.
Afisa habari wa TFF Michael Wambura ameshukuru umma wa wapenzi wa soka wa jiji la Mwanza kwa kutimiza wajibu wao kuonyesha uzalendo siku zote za kambi akiamini kuwa kuna wadau wengi wataondoka na timu wakiungana na mashabiki wa Kagera kwenda kuipa sapoti National Teem.

Afisa habari wa TFF Michael Wambura na Kim Poulsen wakiwa mbele ya wandishi wa habari katika ukumbi wa Nyerere hotel Lakairo jijini Mwanza Tanzania

Mahojiano na wadau wa GENN Radio (Kansas U.S.A)

$
0
0

Bwn. Robert Otto ambae ni Mkurugenzi wa kituo cha Global Entertainment and News Network (GENN) kiliyopo Kansas City nchini Marekani. Picha zote na (swahilivilla.blogspot.com)
Dada D ni mtangazaji wa kituo cha Global Entertainment and News Network (GENN) kiliyopo Kansas City nchini Marekani.

Vile vile Dada D Show ni kipindi kinachokwenda hewani kila Jumamosi Mida ya Saa 8:00 PM Est Time kwenye vionjo na vibwagizo Mchanganyiko wa mahusiano ya Mapenzi ndani ndoa, Mahaba, maelewano na malezi ya watoto kwa familia na kufunzani zaidi ndani ya Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Jijini Kansas City.

Mtangaziji AJ wa kipindi cha kuamshana na asubuhi njeema ndani ya  Global Entertainment and News Network (GENN) kiliyopo Kansas City nchini Marekani.

Katika beti hii tunawakaribisha sana katika Mahojiano haya baina ya Jamii Production na wadau wakuu wa Global Entertainment and News Network (GENN) iliyopo Kansas City nchini Marekani.

Katika mahojiano haya, utasikia Mkurugenzi wa kituo Bwn. Robert Otto na watangazaji AJ na Dada D wakizungumzia harakati zao kwenye kituo hiki kipya cha Radi

Taasisi ya Aisha Sururu yamsaidia mlemavu

$
0
0
TAASISI ya Aisha Sururu, imetoa msaada wa baiskeli maalum kwa mtoto mlemavu, Saada Hamis Hamad (14), ambaye ni mshindi wa kwanza, kundi maalum, katika mashindano ya kuhifadhi Quran Tukufu, kitaifa.

Saada ambaye mikono na miguu yake imelemaa, alikabidhiwa baiskeli hiyo juzi jioni, na mwenyekiti wa taasisi hiyo, Aisha Sururu, ambapo alisema ina mahitaji muhimu kwa mtu mwenye ulemavu, ikiwemo sehemu ya kujisaidia.

Akizungumza mara baada ya kupokea baiskeli hiyo, aliishukuru taasisi kwa kumsaidia kwa mambo mengi, ikiwemo kuibua kipaji chake cha kuhifadhi Quran na kumsafirisha kwa mara ya kwanza.

Alisema tangu apate akili, amekuwa akijisaidia kwa tabu bila staha na kwamba kupitia baiskeli hiyo, itamsaidia mambo mengi ikiwemo kuzunguka maeneo mbalimbali, ambapo hapo awali alishindwa kwani ili kutoka sehemu moja kwenda nyingine ilikuwa lazima abebwe.

"Kabla ya hapo nilikuwa nipo tu nyumbani, sikuwahi kupelekwa shule wala kutoka nje ya mji wangu, lakini nashukuru nimejifunza mengi na nimepata msaada huu,"aliongeza Saada.

Mtoto huyo, ambaye ni mkazi wa Mamoja, Pemba, alisema kuwa, ana ndugu zake wanne, ambao wawili kati yao ni walemavu kama yeye isipokuwa kaka yake wa kwanza ambaye alizaliwa akiwa mzima wa viungo.

Aisha, ambaye pia ni diwani wa viti maalum Ilala, aliwataka wahisani wengine kujitokeza na kununua baiskeli mbili kwa ajili ya ndugu zake Saada hasa mdogo wake ambaye anasoma chekechekea.

"Mdogo wake amekuwa akibebwa kwa ajili ya kupelekwa shule na kuridishwa nyumbani, hivyo baiskeli hiyo itapunguza adha na kumsaidia kuhudhuria masomo bila wasiwasi,"aliongeza.

Washindi watano waibuka na Milioni 10 kwenye Promosheni ya 'Cheka Plus' ya Vodacom

$
0
0
Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi watano wa Sh Milioni Mbili wa promosheni ya Cheka Plus kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.Promosheni hiyo inaendeshwa kila mwezi na Vodacom.
Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humud Abdulhussein(kulia)akimshuhudia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akiongea na mmoja wa washindi wa Promosheni ya Cheka Plus ambapo washindi watano walijishindia shilingi milioni mbilimbili kila mmoja kupitia Promosheni hiyo kubwa ya mwezi.

Kampuni ya Vodacom Tanzania imeendelea kuboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha kujishindia kitita cha Shilingi Milioni 10 kupitia promosheni ya 'Cheka Plus.'

Kitita hicho cha Shilingi Milioni 10 kimenyakuliwa na washindi watano (5) ambapo kila mmoja amejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 2 kila mmoja kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus' iliyofanyika tarehe 20 mwezi huu. 

Washindi hao ni pamoja na; Musa Hussein Ellmy ambaye ni mkazi wa (Karatu - Arusha), Vumi Joshua Mteru (Kilimanjaro), Joseph Godfrey Kyando (Tunduma, Mbeya), Anatori Emmanuel Chogolo (Dar es Salaam), na Amina Joseph Mmbaga (Arusha).

Meneja Uhusiano wa Umma wa Kampuni hiyo Bw. Matina Nkurlu, alisema kuwa zaidi ya wateja 6,000 wamefaidika na ofa hiyo kabambe inayoendelea hivi sasa nchi nzima ambapo zaidi ya Shilingi Milioni 100 zilikabidhiwa kwa wateja mbalimbali walioshinda kupitia Promosheni ya 'Cheka Plus.'

Nkurlu alisema kuwa hadi hivi sasa, tayari wateja mbalimbali nchini wameweza kujishindia kiasi kinachofikia zaidi ya Shilingi milioni 100 "Tumekuwa tukipata washindi 100 kila siku ambapo wamekuwa wakijishindia shilingi 10,000 kila mmoja na washindi wengine 10 wakijinyakulia shilingi 50,000 kila siku, sambamba na droo kubwa ya mwezi ambapo katika washindi watano(5) kila mmoja wao amekuwa akijinyakulia kitita cha shilingi milioni mbili.

Hivyo toka uzinduzi wa promosheni hii ya 'Cheka Plus,' wateja takribani 10 wameweza kujishindia kiasi cha shilingi milioni mbili mbili kila mwezi," alisema Nkurlu nakuongeza kuwa "promosheni hiyo bado inaendelea hivyo ninapenda kuwasihi wateja wa mtandao wa Vodacom kuendelea kufaidika na huduma zetu ikiwemo promosheni ya "Cheka Plus" na kuweza kujishindia zawadi kemkem sambamba na kuendelea kuwasiliana na wapendwa wao."

Kampuni hiyo kupitia mpango wake wa Promosheni ya 'Cheka Plus,' umewezesha wateja kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS), na kuperuzi kwenye mtandao wa intaneti bila hofu.

Ili kuweza kujiunga na huduma ya Cheka Plus, wateja wanashauriwa kupiga *149*01 # na kuchagua kifurushi wanachokitaka. Promosheni ya Cheka Plus inawezesha wateja kutuma SMS na kupiga simu katika kiwango cha bei nafuu kabisa.

msajili wa vyama vya siasa aionya CHADEMA

$
0
0
Na Jennifer Chamila,MAELEZO.
 
Msajili wa vyama vya Siasa nchini amewaasa wanachama na viongozi wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi badala ya kutumia uwezo na muda wao kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani ya nchi.

Pia amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa  leo jijini Dar es Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili wa vyama vya siasa Sisty Nyahoza alisema  kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA au chama chochote cha siasa kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya kutumia nguvu  ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote yule.

Anaongeza kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya kujilinda lakini hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya kujilinda kama walivyo tangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume na Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.

Nyahozo ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama vilivyopo katika Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi kufanya mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yao.Bali wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale wanapo sikia au kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au watu wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA  la tarehe 9 mwezi huu linavyo sema.

“Hakuna maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA yanayoruhusu kutumia nguvu kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa Chama.Ni vyema wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti maalumu kwa Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha aman utulivu na umoja wa Kitaifa”, alisema Nyahoza.

Alisema kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa “Bila kujali masharti ya ibara ya (1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa kuandikishwa ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa.

Nyahoza alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza mpango walio tangaza wa kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa vijana wao nchi nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo  watashindwa kutii agizo hilo  hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

SIKILIZA SINGO MPYA YA MWANADADA NEY LEE IITWAYO NIPE MUDA

$
0
0

Habari zenu kaka/dada/wadau wa muziki wa bongoflava. Napenda mimi Ney Lee baada ya kutoa wimbo na video yangu ya Umekwenda, hii leo pia napenda kuwajulisha nimetoa wimbo wangu mpya unaitwa "Nipe muda" produced by Mswaki, imeandikwa na kuibwa na mimi mwenyewe. Kwenye email hii nimetuma na attachment ya wimbo wenyewe na cover art yake. Asante kwa kusoma na kusikiliza. kkkkkkkkkkkkkkkk

PERMITS FOR CONDUCTING NON-CONSUMPTIVE WILDLIFE UTILIZATION OUTSIDE THE NATIONAL PARKS AND NGORONGORO CONSERVATION AREA

$
0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF NATURAL RESOURCES AND TOURISM




REF: PERMITS FOR CONDUCTING NON-CONSUMPTIVE WILDLIFE UTILIZATION OUTSIDE THE NATIONAL PARKS AND NGORONGORO CONSERVATION AREA

The Ministry of Natural Resources and Tourism is hereby reminding all Tour Operators and owners of Tourist Lodges and Campsites operating in wildlife areas that Regulation 4 of The Wildlife Conservation (Non-Consumptive Wildlife Utilization) Regulations, 2008requires ALL owners of Tourist Lodges and Campsites operating in wildlife areas to obtain a permit from the Director of Wildlife before conducting any tourism activities outside the National Parks and Ngorongoro Conservation Areas.

Following adoption of the electronic permitting system, application for permits can  done online. A customer can fill the form on his/her own or through assistance by our officers at the Tourist Hunting, CITES and Photographic Tourism Office (Arusha), Selous Game Reserve (Matambwe and Mtemere entry gates) and/or Wildlife Division – Headquarters office (Dar es Salaam).

The Online system can be accessed through http://196.41.43.158:8092/default.aspx. To register please fill in the attached registration form, scan and send to support@mnrt.go.tz. Username and initial passwords will be sent through your users email. With this letter, you are officially reminded to comply with the provisions of these regulations

Sincerely Yours


Tarishi, M.K
PERMANENT SECRETARY
Ministry of Natural Resources and Tourism

WAZIRI SAMUEL SITTA UFUNGUA RASMI BARAZA LA VIJANA LA TAIFA LA KATIBA.

$
0
0
Picha ya pamoja katikati ni Waziri wa Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta, kushoto kwake ni Bwana Julius Toneshe na Meneja Mipango wa TYC Bi. Rahma Bajun. Wa kwanza kutoka kulia kwake ni   Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Lenin Kazoba na Meneja wa Restless Development.
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Urambo Mashariki, Mhe. Samuel Sitta akiwahutubia vijana (hawapo pichani) waliohudhuria wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba lililofanyika leo 24/07/2013 jijini Dar es Salaam.
 Bwana Julius Toneshe aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo akiongea wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Lenin Kazoba (kushoto) akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta aliyekaa kulia wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mipango wa Taasisi ya Vijana ya Youth Coalition (TYC) Bi. Rahma Bajun akiongea baada ya kumkaribisha mgeni rasmi Mhe. Samuel Sitta kwa ajili ya kutoa hotuba yake na kufanya ufunguzi rasmi wa Baraza la vijana la Taifa la Katiba leo 24/07/2013 jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Taasisi ya Vijana ya Tanzania Youth Coalition Rebecca Gyum akiongea wakati wa ufunguzi wa Baraza la Vijana la Taifa la Katiba lililofunguliwa rasmi na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Samuel Sitta.
  Baadhi ya washiriki ambao ni vijana mbalimbali kutoka Wilaya 50 za mikoa yote Tanzania wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Mhe. Samuel Sitta (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba kwa vijana ha oleo jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

MASELE AWAPA RUNGU TMAA, AWAAGIZA KUWAKAMATA WANAOTOROSHA MADINI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza katika Baraza la Wafanyakazi wa TMAA leo jijini Dar es Salaam.
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Madini Tanzania (TMAA), Mhandisi Paulo Masanja akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala huo, lililoketi jijini Dar es Salaam, jana. Anayefuata ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele.
WAJUMBE wa Baraza la wafanyakazi la WAkala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika jana Dr es Salaam.
WAJUMBE wa Baraza la wafanyakazi la WAkala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika jana Dr es Salaam.
MJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Madini Tanzania (TMAA), akitoa mada kwenye mkutano wa baraza hilo uliofanyika jana mjini Dar es Salaam
  WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Masele baada ya kufungua kikao cha Baraza
 WAJUMBE wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa Madini Tanzania (TMAA) wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Masele baada ya kufungua kikao cha Baraza. Imetayarishwa na theNkoromo Blog
 

=========   ===========   ==============

NA MWANDIHI WETU
SERIKALI imeiagiza Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), kuwakamata wanaotorosha madini.

Pia, imeiagiza TMAA kuhakikisha inaokoa rasilimali za nchi ili ziweze kulinufaisha taifa na wananchi wake na umeutaka wakala huo, kuwabana wachimbaji wadogo ili walipe kodi stahiki za serikali.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifungua mkutano wa tatu wa baraza la wafanyakazi la TMAA.
Alisema Wakala huo, uhakikishe kuwa serikali inapata mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara za madini.

Masele alisema katika kufanikisha hilo, TMAA isiache kuwakamata wale watakaobainika wanatorosha madini nje ya nchi.

"Naomba muwakamate watakaobainika wanatorosha madini yetu, mukifanya hivyo mutakuwa mumetekeleza wajibu wenu," alisema.

Alisema jukumu lingine ambalo TMAA inapaswa kulipa kipaumbe ni kuhakikisha inaokoa rasilimali za nchi.

Masele alisema miongoni mwa rasilimali za nchi ni pamoja na madini hivyo amewataka wakala huo kuhakikisha inaisimamia vya kutosha rasilimali hiyo.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, TMAA iongeze juhudi za kukusanya mapato ikiwa ni pamoja  na kuwabana wachimbaji wadogo ili walipe kodi.

Alisema kiasi kikubwa cha fedha kinapotea kutokana na wachimbaji wadogo kukwepa kulipa kodi.  Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa TMAA, Mhandisi Paulo Masanja, alisema wakala huo umepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake.

Alisema moja ya mafanikio hayo ni kwamba baadhi ya wamiliki wa migodi mikubwa nchini kuanza kulipa kodi ya mapato ambapo, kuanzia 2009 hadi sasa wamekusanya sh. bilioni 473.9.

Mhandisi Masanja alisema kutokana na ukaguzi wa kimkakati uliofanywa na wakala huo , sh. bilioni 1.8 na wachimbaji madini ya ujenzi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kama mrahaba.Alisema baraza la wafanyakazi la wakala huo, liliundwa kwa mujibu wa sheria na lilianzishwa MEi 5, 2011.
 

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwahamasisha wakulima wa mwani na wafugaji kukopa ili kukipatia mitaji

$
0
0
 Na Maelezo Zanzibar   24/07/2013

Wizara ya Mifugo na Uvuvi inakusudia kuwahamasisha wakulima wa mwani na wafugaji wa mazao ya baharini ,kujiunga na vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa ili kujipatia mitaji ambayo itakayowawezesha kuanzisha vyanzo vya ziada kwa ajili ya kujiongezea kipato.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2013/2014 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilah Jihad Hassan amesema wataendelea kutoa elimu kwa wakulima wa mwani juu ya ukulima bora kwa uhifadhi pamoja na kuhamasisha matumizi ya bidhaa zinazotokana na zao hilo kwa maslahi ya akina mama na vikundi vinavyozalisha mwani

Aidha ameeleza kuwa wizara yake itaimarisha ufugaji wa samaki, kaa, chaza pamoja na mazao mengine ya baharini.  “Wizara yangu itaendelea kuimarisha uvuvi wa kienyeji kwa kuongeza uelewa wa jamii juu ya uvuvi endelevu pamoja na kufanya doria 310 kutoka maeneo ya hifadhi na maeneo ya maji ya kina kirefu”, alifahamisha Waziri Jihad.

Aidha amesema kuwa Wizara inakusudia kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao yake kwa kuimarisha huduma za elimu kwa wafugaji kwa kuvijengea uwezo vituo vya utafiti wa mifugo pamoja na kuongeza thamani na ubora wa mazao na bidhaa za mifugo.  Hata hivyo amesema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wafugaji juu ya kuwakinga wanyama na maradhi ya kuambukiza, maradhi ya kupe pamoja na kuwahamasisha wananchi juu ya kuzuia ukatili kwa wanyama.

Hata hivyo ameeleza kuwa kupitia Idara ya Uzalishaji Mifugo Wizara yake imeweza  kukamilisha ujenzi wa uzio kituo cha kupandishia ng’ombe kwa sindano ambapo jumla ya ng’ombe 2,540  wamepandishiwa kwa shindano Unguja na Pemba.

Katikia kutekeleza malengo yake  waziri huyo ameliomba baraza limuidhinishie jumla y ash 4,905,000,000 kwa ajili ya matumizi. 

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO 
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images