Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1254 | 1255 | (Page 1256) | 1257 | 1258 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0

  NA IS-HAKA OMAR,  ZANZIBAR.

  MAMIA ya Wananchi wameudhuria mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar.Vuai Ali Vuai, Marehemu Bi.Mwanaisha Hassan Vuai huko Kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.

  Mazishi hayo yameongozwa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, aliyeambatana na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  pamoja na  jamhuri ya muungano Tanzania.

  Bi. Mwanaisha amefariki jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tasakhtaa  iliyopo  Vuga  Mjini  Zanzibar.

  Akizungumza mara baada ya mazishi hayo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Zanzibar, Nd. Vuai Ali Vuai alisema kifo cha Mama yake mzazi kimeacha pengo kubwa katika  familia hiyo  kwani marehemu huyo alikuwa akitegemewa na jamii kutokana na busara zake.

  Aidha  Vuai amewashukru wananchi mbali mbali waliojitokeza kumuunga mkono katika mazishi hayo na kuwasihi waendelee kuwa na umoja wa kushirikiana katika mambo mbali mbali ya kijamii.

  “  Mama yetu tulimpenda sana lakini ndio hivcyo amefariki sasa kilichobaki kwetu sisi tuliobaki ni kumuombea dua yeye pamoja na wazee wetu wengine waliofariki kabla yake.”, alisema  Naibu Katibu Mkuu huyo. 

  Mbali na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Idd pia  Mazishi hayo yameudhuriwa na Viongozi  mbali mbali  wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM   Abdulrahman Omar Kinana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar   Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi”,Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Shaka Hamdu Shaka,  Mkuu wa Mkoa kusini Unguja    Dk.Idrissa  Muslim Hija, Katibu  wa Kamati Maalum  ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari  Jabu.

  Viongozi wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Idrissa  Kitwana  Mustafa, Mnadhimu wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  wa CCM, Ali Salum Haji pamoja na baadhi ya Mawaziri, Manaibu Mawaziri  na Makatibu wakuu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

   Bi.Mwanaisha Hassan Vuai amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 ameacha watoto tisa (9) pamoja na wajukuu kadhaa.

  Mungu ailaze roho ya marehemu pahali pema peponi-Amin.
   Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balosi Seif  Ali Idd akipokelewa na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali mara baada ya kuwasili katika mazishi ya Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai, huko kijijini kwao Bwejuu.
   Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea Dua  Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
   Viongozi  mbali mbali wa Chama na serikali pamoja na wananchi wakiiombea wakiwa msikitini kabla ya kuanza kuiswalia Maiti ya Bi. Mwanaisha Hassan.
   Baadhi ya Viongozi na wananchi kwa upande wa wanawake wakiomba dua katika mazishi ya Marehemu Bi. Mwanaisha Hassan Vuai ambaye ni Mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Msitaafu wa CCM Zanzibar  Vuai Ali Vuai katika msikiti wa kijiji cha Bwejuu.
   Matukio tofauti ya kubebwa kwa maiti inapotolewa msikiti hadi sehemu ya kaburi ilipofanyiwa mazishi.
  Viongozi mbali mbali wa Chama na serikali wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Nd. Abdulrahman Omar Kinana wakimfariji Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM  Zanzibar  katika mazishi ya Mama yake mzazi yaliyofanyika huko kijijini kwao Bwejuu, Mkoa wa Kusini Unguja.( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR).

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza na balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing ofisini kwake leo mjini Dodoma ambapo wamejadili na kukubaliana mambo mbali mbali ya kuimarisha uhusiano wa China na Tanzania katika sekta ya maliasili na utalii. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuwakaribisha wawekezaji katika sekta ya viwanda vya uchakataji wa mazao ya misitu na ujenzi wa hoteli katika fukwe za Tanzania na Hifadhi za Taifa.
   Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing akimueleza jambo Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma leo. Balozi huyo amekubali ombi la Waziri Maghembe kuwaleta wadau wa mashirika ya utalii kutoka nchini China kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania na kuvitangaza nchi kwao.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akimfafanulia jambo balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing alipomtembelea ofisi kwake leo mjini Dodoma. Waziri Maghembe kupitia balozi huyo ameipongeza Serikali ya China na Wananchi wake kwa uamuzi wake wa hivi karibuni wa kufungia biashara haramu ya meno ya tembo nchini humo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiagana na Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing baada ya mazungumzo marefu ofisini kwake leo mjini Dodoma.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Dkt. LU Youqing (kushoto), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili, Dkt. Aloyce Nzuki (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Justa Nyange wakijadili jambo muda mfupi baada ya mazungumzo hayo. (PICHA ZOTE NA HAMZA TEMBA - WMU)

  0 0

  Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida zimeagizwa kutenga maeneo yenye hadhi ya kuwa viwanja vya michezo pamoja na kuhakikisha zinakuwa na benki ya wanamichezo katika halmashauri zao.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi ametoa maagizo hayo leo asubuhi kabla ya kuzindua mashindano ya michezo kwa shule za Sekondari (UMISSETA) kwa ngazi ya mkoa ambapo wanamichezo hao wataunda timu za Mkoa kwa ajili ya mashindano ya kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza mwezi ujao.

  Dkt. Nchimbi amesema halmashauri zimekuwa zikiwatelekeza wanamichezo mahiri hivyo wakianzisha benki ya wanamichezo kwa maana ya kuhifadhi kumbukumbu za wana michezo mahiri pamoja na kuwaendeleza hawatapata shida kipindi cha mashindano yoyote. 

  Ameongeza kuwa halmashauri zimekuwa zikijisahau katika kuandaa maeneno ya michezo hadi inapofika kipindi cha UMISETA hali inayopelekea kukosekana kwa viwanja vya kufanyia mazoezi ili kuwa na timu bora.

  Dkt. Nchimbi amewaasa wana michezo kuwa na nidhamu, utii, bidii na kuitumia michezo kuutangaza Mkoa wa Singida wenye fursa nyingi za uwekezaji pamoja na kujitangaza uwezo wao ili waweze kupata nafasi katika timu mbalimbali za kitaifa.

  Aidha amewasisitiza waamuzi wa michezo kutenda haki kwakuwa matendo yao ni darasa la nidhamu na maadili kwa wanafunzi wao na kuwatahadharisha wanafunzi wasio tii kuwa hawatapata nafasi katika timu ya Mkoa.

  Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Mageni Lutambi amewapongeza wakurugenzi wa halmashauri kwa kufanikisha upatikanaji na ushiriki wa timu za michezo za kila halmashauri.

  Dkt. Lutambi ameishukuru pia kampuni ya Coca cola kwa udhamini wa UMISSETA kwa kutoa vifaa kwa shule 118 ambavyo ni tisheti 3,776, mipira ya miguu 118 na mipira ya basketball 118 pamoja na ahadi ya kuendelea kugawa vifaa katika shule 45 zilizobaki.

  Ameongeza kwa kuwasihi wana michezo wote kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa kuzingatia sheria na kanuni za michezo ili kutengeneza timu ya ushindi ya mkoa.

  Akisoma taarifa ya Michezo ya Umiseta Afisa Michezo wa Mkoa Henry Kapella amesema jumla ya wana michezo 576 wameshiriki katika michezo hiyo ambapo wataunda timu ya mkoa ya michezo ya bao, riadha, mpira wa miguu na mpira wa pete. 

  Kapella ameongeza kuwa kauli mbiu ya michezo ya Umisseta kwa mwaka 2017 ni ‘Wekeza katika michezo kwa ustawi wa elimu na Viwanda’. 

  Kwa upande wao wanafunzi walioshiriki mashindano ya umisseta wamesema michezo inawajenga kiafya na kiakili kwa kuwa wanafunzi wanaoshiriki katika michezo huwa na ufaulu mzuri wa masomo yao.

  Wameongeza kuwa michezo inawaongezea nidhamu na kuwajenga kimaadili hivyo kufaulu inakuwa ni rahisi, aidha wamesema michezo ina faida nyingi ikiwemo kuwatengenezea ajira mara baada ya kumaliza masomo yao.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (aliyenyanua ubao) akipiga ubao wa kuashiria uzinduzi wa michezo ya UMISSETA mkoa wa Singida, mbele yake ni wanariadha wakianza mashindano.
   Wanamichezo kutoka Shule za Sekondari za Halmashauri ya wilaya ya Itigi wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (katikati) akiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa, kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi na Kulia Kwake ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida Florian Kimolo.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia kabla ya kuzindua mashindano ya UMISSETA ngazi ya Mkoa wa Singida.
   Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Angelina Mageni Lutambi akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA Mkoa wa Singida.
  Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida Henry Kapella akisoma taarifa ya michezo ya Umisseta wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ngazi ya Mkoa.

  0 0


  0 0


  0 0


  Meneja Masoko wa Bia laini Afrika Mashariki, Amou Majok (wa pili kushoto) akiwa pamoja na wasanii wa kundi la Navy Kenzo juzi jijini Dar, wakati Meneja huyo akitangaza kuhusu wasanii wa kundi hilo kushiriki katika tamasha la Castle Lite Unlocks litakalofanyika mwezi Julai. Wa kwanza kulia ni Meneja Msaidizi wa Chapa ya Bia laini, Isaria Kilewo.
  Wadau mbalimbali waliojitokeza wakiwa katika picha ya pamoja

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Wizara yake ambapo Bunge limepitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na Naibu wake Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali za Wabunge wakati wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma, ambapo Bunge hilo limepitisha Bajeti ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimpongeza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya jumla ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
   Mkurugenzi wa Idara ya Mipango-Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (kulia), akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa, Bw. Samwel Kamanga kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya wizara hiyo.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mbunge wa Babati Vijijini Mhe. Jitu Soni nje ya Ukumi wa Bunge mara baada ya Wabunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
   Gavana wa Benki Kuu (BOT), Prof. Beno Ndullu (kushoto), akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), baada ya Bunge kupitisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mjini Dodoma
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) akipeana mkono na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw. Mohamed Mtonga, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoro) akimshukuru na kumpongeza Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa kazi kubwa aliyoifanya katika kusimamia na kuhakikisha kuwa Bajeti ya Wizara hiyo inaandaliwa kwa viwango vya juu na hatimaye kupitishwa na Bunge Mjini Dodoma ambapo Wizara hiyo imeidhinishiwa kukusanya nakutumia shilingi trilioni 11.752 kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa saba kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Wizara na Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya kuhitimishwa kwa mjadala wa bajeti wa Wizara hiyo.

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo
  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali wakiwa kwenye kikao hicho,

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akihitimisha  mazungumzo yake  na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, Mabalozi, watendaji wa CCM na wa Serikali, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo, Wilaya hiyo ya Kaliua ndiyo imehitimisha ziara yake katika mkoa wa Tabora. PICHA; BASHIR NKOROMO

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumza na Walimu wa Msingi Ushokora inayomilikiwa na Jumuia hiyo, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo. Pamoja na mambo mengine, Bulembo alitaka kujua kwa nini walimu kwenye shule hiyo kongwe wanafanyia kazi yao chini ya miti kama alivyowakuta. Wapili kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyoAsher Msemwa na Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Abeid Busalama ambaye Bulembo alimpa jukumu la kufuatilia tatizo hilo la walimu kufanyika azi chini ya miti.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akipanda mti wa kumbukumbu katika Shule ya Msingi Ushokora mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ushokora mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akimpa chemshabongo Jacqueline Philber alipotembelea Shule ya Msingi Ushokora inayomilikiwa na Jumuia hiyo, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akiwapa maswali ya chemshabongo wanafunzi, alipotembelea Shule ya Msingi Ushokora inayomilikiwa na Jumuia hiyo, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akimpa swali la chemshabongo Mwanafunzi wa darasa la tano, Ibrahimu Kapewa, alipotembelea Shule ya Msingi Ushokora inayomilikiwa na Jumuia hiyo, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akimpa zawadi ya sh elfu kumi Mwanafunzi wa darasa la tano, Ibrahimu Kapewa, baada ya kufanikiwa kujibu vema swali la chemshabongo alilompa, alipotembelea Shule ya Msingi Ushokora inayomilikiwa na Jumuia hiyo, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuondoka kwenye Shule ya Msingi Ushokora inayomilikiwa na Jumuia hiyo, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Bisalama na Kulia i Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Aser Msemwa.
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Alhajj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM ya Wilaya ya Kaliua, mwanzoni mwa ziara yake katika Wilaya hiyo mkoani Tabora, leo. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Elias Kaseko na kulia ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo Shabani Mrisho
   

  0 0

  Na Jumia Travel Tanzania

  Siku ya Jumatatu ya Juni 5 itakuwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Mazingira Duniani’ ambayo huadhimishwa na mataifa tofauti duniani ikiwa imebeba kauli mbiu ya ‘Kuwaunganisha Watu na Mazingira Asilia.’ 

  Mapema wiki hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba  alitoa taarifa kwa umma kuwa kwa hapa nchini maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yatafanyika kijijini Butiama mkoani Mara, mahali alipozaliwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere, ikiwa ni kuenzi jitihada zake za kulinda na kuhifadhi mazingira.

  Katika kunogesha sherehe hizo Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa ofa kwa wananchi kutembelea hifadhi yoyote ya mbuga ya wanyama bila ya kiingilio chochote kwa siku tatu, kuanzia Ijumaa ya Juni 2 mpaka Jumapili ya Juni 4. Alisema kuwa lengo kubwa ni kuona uwepo wa wanyama na kujifunza kuwa mazingira yanahitaji kulindwa zaidi na zaidi.
  Kauli hiyo ya Waziri imekuja siku chache baada ya kampuni inayojihusisha na masuala ya huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika, Jumia Travel kuzindua kampeni ya ‘DemocratizeTravel’ inayolenga kuwakomboa waafrika na watanzania kiujumla katika kusafiri na kutalii vivutio mbalimbali nchini huku wao wakirahisisha huduma za malazi na hoteli.

  Kampuni hiyo inalenga kuhamasisha na kutoa elimu juu ya dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa wananchi ya kwamba mchakato mzima unaohusisha utalii ni gharama. Katika kulifanikisha hilo kampuni hiyo imedhamiria kuelimisha juu ya vivutio vilivyopo nchini, masuala ya msingi ya kuzingatia wakati wa kusafiri pamoja na kurahisisha gharama za malazi kupitia hoteli za kila hadhi zilizopo kwenye mtandao wao wa travel.jumia.com.   
  Baadhi ya changamoto zilizopo ni pamoja na mwamko mdogo wa watanzania kutembelea vivutio vya kitalii vilivyopo karibu na wanayoishi. Wapo baadhi yao hawafahamu kuwa wanaishi na vivutio hivyo na wengine huchukulia mchakato mzima unahusisha gharama kubwa.
  Vifuatavyo ni baadhi ya vivutio vya kitalii ambavyo watanzania mahali popote walipo wanaweza kwenda kuvitembelea wikendi hii bure kabisa kwa mujibu wa kauli ya serikali katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.

  Kanda ya Kaskazini. Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Mara kwa kiasi kikubwa imebarikiwa kuwa na hali ya hewa nzuri inayowavutia watalii, hifadhi za mbuga za wanyama, maeneo yenye masalia ya kale pamoja na milima ya kuvutia. Vivutio vinavyopatikana huko ni kama vile; Hifadhi za Taifa za Arusha, Mkomazi, Ziwa Manyara, Mlima Kilimanjaro, Serengeti na Ngorongoro. 

  Kanda ya Magharibi. Eneo hili inapatikana mikoa kama vile ya Kigoma na Rukwa ambayo nayo haijaachwa nyuma kwa upande wa vivutio vya kitalii. Wananchi wanaoishi katika au karibu na mikoa hii wanaweza kutembelea Hifadhi za Mbuga za Wanyama kama vile; Gombe, Katavi, Mahale, Rubondo na Saanane na kujionea wanyama wengi hususani sokwe wa kipekee. 

  Kanda ya Kusini. Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma ni baadhi ya mikoa inayoweza kupatikana katika ukanda huu ambapo kuna hifadhi za kitaifa kama vile; Kitulo, Mikumi, Ruaha na Udzungwa. Mbuga kama vile Mikumi inajulikana kuwa na idadi kubwa ya wanyama kama vile pundamilia, nyati na tembo.   
  Kanda ya Mashariki. Ukanda huu kwa kiasi kikubwa umepakana na fukwe ya bahari ya Hindi ambayo inapatikana kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara. Mbali na kuwa na hoteli nyingi zilizojengwa pembezoni mwa fukwe ya bahari hiyo lakini pia mikoa hiyo inavyovivutio vingine lukuki kama vile; Hifadhi ya Taifa ya Saadani, Mji wa Bagamoyo, Kisiwa cha Kilwa, Mapango ya Amboni na Mikindani. 

  Visiwa vya Zanzibar. Hakuna anayeweza kubisha kuwa vivutio mbalimbali vilivyomo visiwani humo hususani fukwe nyingi safi na za kuvutia pamoja na hoteli za kifahari ndivyo huwatoa watu kutoka mataifa mbalimbali duniani kwenda kuzuru. Mbali na visiwa hivi kusifika kuwa na sehemu nzuri za kupumzika bali pia vina utajiri mkubwa wa tamaduni za watu wa mataifa mbalimbali waliopata kuishi humo kama vile Waarabu, Waingereza pamoja na waafrika kwa ujumla. Lakini pia kuna majengo ya kale yaliyojengwa karne nyingi zilizopita ambayo mpaka leo hii bado yapo na vinginevyo vingi. 
  Uzuri wa nchi ya Tanzania umebarikiwa kuwa na vivutio vya kila namna karibuni kila mkoa. Hivyo kisingizio cha kutotembelea sehemu fulani kwa sababu ipo mbali kinakuwa hakina mantiki, Jumia Travel inakushauri anza kwanza na vilivyo karibu nawe na fursa hii iliyotolewa na serikali inaweza kuwa ni mwanzo mzuri kwako.


  0 0

  Grace Kisetu, Mkuu wa Idara ya Ijenzi wa Nguvu Pamoja wa TGNP Mtandao, akizungumza na washiriki katika warsha ya Uongozi wa Kijinsia kwa Madiwani wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  Husna Masoud, Diwani wa Viti Maalum, Kata ya Buguruni.
  Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mtoni wilayani Temeke, Kubra Abdallah.
  Baadhi ya Madiwani wanaoshiriki warsha hiyo ya siku tatu.


  Na Daniel Mbega


  MADIWANI wanawake wa vyama mbalimbali vya siasa katika Mkoa wa Dar es Salaam wamesema suala la kubadili mtazamo katika ushirikishwaji wa wanawake kwenye maendeleo ni la msingi na linapaswa kutekelezwa kuanzia ngazi za chini.


  Wakizungumza katika warsha ya siku tatu ya Uongozi wa Kijinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP Mtandao), madiwani hao wamesema haki za wanawake bado zinakandamizwa katika jamii huku vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vikishika kasi.


  Husna Masoud, Diwani wa Viti Maalum, Kata ya Buguruni (Chadema), amesema katika kata yake hakuna usawa hata wa uongozi na kwamba bado vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vinaendelea.


  “Suala la unyanyasaji wa kijinsia bado limetamalaki katika jamii na lazima tulizungumzie kwa mapana ili kukomesha vitendo hivyo,” alisema Husna.


  Kwa upande wake, Honorata Mashoto Mrisho, Diwani wa Viti Maalum Kata ya Ubungo (Chadema), amesema maamuzi mengi kuanzia ngazi ya kijiji hadi kata yamekuwa yakiwaacha nyuma wanawake, jambo ambalo linawanyima fursa za maendeleo.


  Amesema kama wawakilishi wa jamii kwenye vikao mbalimbali vya Kata, watajitahidi kupigia kelele masuala yote ya jinsia ili kuweka usawa pamoja na kuchochea maendeleo.


  Salma Said El Maamry, Diwani wa Viti Maalum, Kata ya Mburahati, Ubungo, amesema haki za mtoto wa kike bado zinakandamizwa na jamii, hivyo ni lazima kupambana kuhakikisha wanapata mahitaji yao yanayostahili.


  Amesema watoto wengi wa kike wanalazimishwa kuolewa kabla ya umri na jamii inafumbia macho, jambo ambalo linawanyika haki ya kutimiza ndoto zao katika maisha, hasa suala la elimu.


  Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mtoni wilayani Temeke, Kubra Abdallah, amesema watoto wa kike wanakosa vipindi vya masomo kutokana na ukosefu wa elimu ya kujihifadhi hasa wanapokuwa katika hedhi.


  “Elimu ya hedhi bado duni sana, hasa vijijini, kwa sababu watoto wengi wa kike wanapokuwa katika hedhi huhisi kwamba ni wagonjwa, hivyo hushindwa kuhudhuria vipindi ipasavyo… lazima elimu hii itolewe kwa jamii ili kuwawezesha watoto hawa wapate elimu kama ilivyo kwa wale wa kiume,” alisema Kubra.

  Awali, mmoja wa wawezeshaji kutoka TGNP Mtandao, Anna Kikwa, amesema warsha hiyo imelenga masuala mbalimbali kwa madiwani hao ikiwa ni pamoja na kubadilisha mawazo na uzoefu wa namna ya kufuatilia bajeti zinazohusu jinsia.

  “Malengo ya warsha hii ni kuongeza uelewa katika masuala ya uongozi na jinsia pamoja na bajeti kwa mlengo wa kijinsia,” alisema Anna Kikwa.


  Aidha, alisema malengo mengine ni kushirikishana uzoefu, changamoto, mbinu na mikakati ya uongozi kwa wanawake ili kukuza uwezo wao kama viongozi bora na kuboresha utendaji wao.


  Aliongeza pia kwamba, warsha hiyo imelenga kushirikishana masuala yaliyoibuka kwenye uraghibishi na tafiti mbalimbali zilizofanywa na TGNP Mtandao pamoja na taasisi nyingine.


  “Pia tunatakiwa kuweka mikakati ya pamoja ya kuongeza nafasi ya mwanamke katika kuchangia, kushawishi na kufanya maamuzi katika ngazi mbalimbali ikiwemo kuanzisha umoja wa madiwani wanawake nchini.


  Naye Grace Kisetu, Mkuu wa Idara ya Ijenzi wa Nguvu Pamoja wa TGNP Mtandao, amesema suala la haki ya mwanamke katika uongozi ndilo la msingi na kwamba taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele kulitetea.


  “TGNP imekuwa ikijihusisha katika utetezi wa haki za jamii kuanzia wanawake, watu wenye ulemavu, wanaume walio katika umaskini na kadhalika, lakini pia tunatetea makundi mbalimbali ya wanawake katika uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo katika shughuli mbalimbali ikiwemo kwenye uchimbaji wa madini,” alisema.
  0 0  The member of Workers Compensation Fund (WCF) Board of Trustees, Felix Kagisa (Center) officiating at the Sensitisation Seminar for Employers on the Rights and Obligations of employers and employees, held today (yesterday) in Dar es Salaam, On the Right side is The Director of Operation of WCF Ansilim Peter and on the left side is the member of Workers Compensation Fund (WCF) Board of Trustees Jaicy Kayera. 
  1
  The Director of Operation from Workers Compensation Fund (WCF) Ansilim Peter presenting a Paper during the Sensitisation Seminar for Employers on the Right and Obligations of employers and employee, held today (yesterday) in Dar es Salaam
  2
   The member of Workers Compensation Fund (WCF) Board of Trustees) Jaicy Kayera stressing a point during the Sensitisation Seminar for Employers on the Right and Responsibility of employers and employee, held today (yesterday) in Dar es Salaam
  3
  Senior Labour Officer of Temeke Municipality, Zevyanji Silungwe presenting Paper during the Sensitisation Seminar for Employers on the Right and Obligations of employers and employee, held today (yesterday) in Dar es Salaam
  4
  A cross section of Participants following the Seminar’s presentations during the Sensitisation Seminar for Employers on the Right and Obligations of employers and employee, held today (yesterday) in Dar es Salaam.
  …………………….


  By Benjamin Sawe.

  Tanzania Information Services
                                                                                   
  Dar es Salaam.
  Employers have been argued to promptly pay, to Workers Compensation Fund (WCF), contributions of their workers to enable the Fund to adequately and timely provide compensation benefits to effected workers.

  Speaking at the opening of a one-day sensitisation seminar to employers, Mr. Felix Kagisa, Board Member of the Fund, reminded employers that, according to the law establishing the fund, it was their responsibility to contribute to the fund for their employees.

  Workers Compensation Fund (WCF) was established under article 5 of Workers Compensation Act No. 20 of 2008 charged with the responsibility to provide compensation to workers who suffer occupational injuries, deaths or contract occupational diseases arising out of and in the course of their employment. It also deals with improving working environment to prevent occupational hazards.

  Mr. Kagisa told seminar participants that, with the country’s new drive for industrialisation, the establishment of the fund was timely as it will see more workers join the sector.

  “With more workers expected to join the industrial sector, the fund is very crucial for their survival” Mr. Kagisa said.He note that the establishment of the fund which started its operation in 1st of July, 2015, was aimed at addressing challenges faced by previous workers compensation system.

  He cited compensation of not more than 180,000/=and 83,000/= to workers with permanent disabilities and to dependents in the incident of death of employee as among those challenges.According to article 2 of Workers Compensation Act of 2008, Mr. Kagisa said all employers and workers in public and private sector in mainland Tanzania is eligible.  

  The Director of Operations of the Fund, Mr Anselim Peter, told participants that the fund has decided to arrange that sensitisation seminar to employers, as main stakeholders, to educate them on their role and obligations in regular monthly payments of subscription of their employees.On his part, Mr Jaicy Kayera (Trustee) emphasised that the fund was legally established to offer compensation to workers suffered from injuries, diseases and death while at work.

  Workers Compensation Fund is a government institution under the Prime Minister Office and established under article 5 of Workers Compensation Act, Cap 263 as amended December, 2015.

  0 0

  Tafadhali pokea CODES hapa chini Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imetoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati ambayo itatumika katika halmashauri za mikoa hiyo. 

  Akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi hao kwani yatawasaidia kupata mbinu mpya ambazo watazitumia wakati wa kutengeneza mipango mikakati katika maeneo yao. Alisema kwa dhamana waliyonayo watumishi hao ni vyema kutumia mafunzo hayo ya siku mbili vizuri ili baada ya mafunzo waweze kupata njia mbadala katika uandaaji wa mipango mikakati ambayo itasaidia kuleta maendeleo.
   Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati 

   “Hampo hapa kwa ajali, mpo kwasababu dhamana zenu ni kubwa, kwa kupitia mafunzo haya mtapata nyezo za kupangia mikakati ya kweli na mimi nataraji mtatoka hapa vizuri, haya ni mafunzo muhimu sana, “Tusiishie kwenye mikakati, tatizo ni jinsi gani ya kuanzisha miradi, tumekuwa na mawazo mengi sana lakini tuna changamoto ya kuyaweka kwenye miradi, tutoke kwenye kuwa na mawazo na sasa tuanze kuyafanyia kazi,” alisema Mongela. Pia Mongela aliwashukuru ESRF kwa kuandaa mafunzo hayo na kuwataka washiriki kufanya kazi kwa ushirikiano na ESRF kwani tayari wameonyesha nia ya kushirikiana nao ili kuhakikisha mipango ambayo wanaipanga inafanyiwa kazi. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwenye mafunzo kwa watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu kuhusu uandaaji wa mipango mikakati. 

   “Tuone jinsi gani tunatumia fursa hii vizuri, tunatakiwa tukitoka hapa tukatekeleze mipango hii na ESRF wapo tayari kushikana mikono na sisi hadi waoane mafanikio na mimi niwahakikishie sisi tupo tayari … nategemea mambo makubwa baada ya kuanzisha ushirikiano huu,” alisema Mheshimiwa Mongela. Nae Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida alisema kwa kipindi kirefu wamekuwa mstali wa mbele kusukuma mbele Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa kufanya shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa muhimu kwa maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. “Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, wa nje na ndani ya nchi, ESRF imekuwa ikisimamia na kuhimiza ufikiwaji wa malengo hayo sio tu katika ngazi ya Taifa bali pia katika ngazi ya wilaya na hata Kata,” alisema Dk. KidaMkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela (katikati) akizindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya. 

  Dk. Kida aliendelea kusema kuwa mafunzo hayo kutakuwa na mada zinazoelezea maelezo ya Jumla kuhusu mpango mkakati, upangaji wa bajeti, ufuatiliaji na namna ya kutoa taarifa, mikakati ya maendeleo ya kitaifa na kimataifa SDGs, FYDP II, Africa Agenda 2063, Vision 2025, mchakato wa kuandaa mpango mkakati na ufuatiliaji, upimaji, na utoaji wa taarifa (reporting, monitoring and evaluation) Aidha ESRF imezindua mwongozo wa kuandaa mipango mkakati ya wilaya, mwongozo ambao umetokana na andiko kubwa lililoandaliwa na serikali siku za nyuma kuhusu uandaaji wa mipango mkakati ya muda wa kati pamoja na bajeti (Government’s Medium Term Strategic Planning and Budgeting Manual). 
  Meza kuu ikionyesha mwongozo huo baada ya kuzinduliwa rasmi.Bwana Apolinary Tamayamali kutoka Ofisi ya Rais-IKULU akitoa neno kwa washiriki kuhusu mipango na mchakato wa uandaaji bajeti.Picha juu na chini ni Mkurugenzi Mtendaji wa Self Microfinance Fund, Mudith Cheyo akitoa mada kwa washiriki kuhusu uandaaji wa mipango mikakati.[/caption] Picha juu na chini ni Washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa mipango mikakati ambayo yamehusisha watumishi wa Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Maofisa Mipango wa Halmashauri za Wilaya wa Mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu.Picha juu na chini ni Washiriki wa mafunzo kuhusu uandaaji wa mipango mikakati wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa, John Mongela.

  0 0

  DROO ya kwanza ya Sh Milioni 20 na ya kumi kufanywa na waendeshaji wa bahati Nasibu ya Biko hatimae imepata mwenyewe baada ya kutangazwa mshindi wake ambaye ni Huruma Mkongwa wa jijini Arusha, akiibuka kidedea katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.

  Droo hiyo ni ongezeko la Sh Milioni 10 ambapo hapo awali droo zote zilikuwa zikihusisha kiasi hicho cha pesa kabla ya kuongezwa katika droo ya Jumatano ambapo waliongeza Milioni 10 nyingine hivyo kufikia Sh Milioni 20 na hivyo kutua kwa Mkongwa.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa kuchezesha droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Jumatano ya Sh Milioni 20 imekuwa tamu baada ya fedha hizo za zawadi ya juu kabisa kutoka kwenda kwa Mkongwa ambapo anakuwa mshindi wa kwanza kuzoa kiasi hicho cha pesa kutoka kwenye bahati nasibu yao inayotikisa nchini.
  Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akisalimiana na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid kabla ya kuanza kuchezesha droo ya 10 ya Jumatano ya Sh Milioni 20 ambapo mkazi mwingine wa Arusha, Huruma Mkongwa aliibuka kidedea.
  Balozi wa Biko Kajala Masanja akimtangaza mshindi wa Sh Milioni 20 Huruma Mkongwa kutoka mkoani Arusha baada ya kumaliza kuchezeshwa droo hiyo ya 10 ya Biko. Kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bakari Maggid.
  Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akifurahia jambo baada ya kupatikana mshindi wa Sh Milioni 20 katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam.

  Alisema ni imani yao ni kwamba kutoka kwa fedha hizo kutazidi kuibua fursa sahihi kwa washindi wao katika kuhakikisha wanatumia vema fedha hizo ili wanufaike kiuchumi kwa kutumia rasilimali fedha wanazopata kutoka Biko.

  “Jumatano ya leo imekuwa Jumatamu kwa mshindi wetu Huruma Mkongwa wa Arusha kupata mkwanja kutoka kwetu, huku Biko tukiwa na lengo kubwa la kukuza uchumi wa wananchi wote hususan wale wanaoamua kutuunga mkono kwa kucheza Biko mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo watakapoingia kwenye lipa bili au lipa kwa Mpesa wataweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456.

  “Huu ni wakati wa kupata zawadi mbalimbali kutoka Biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja ambapo hulipwa papo hapo kwa kupitia simu zao walizocheza muda mchache baada ya kushinda, hivyo ili washinde lazima wacheze mara nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya ushindi,” Alisema Heaven.

  Akizungumza kwa simu wakati anafanya mahojiano na Balozi wa Biko Kajala Masanja, Mkongwa alisema haamini kama ameshinda donge nono hilo kutoka Biko ingawa alikiri kucheza Biko akiomba Mungu ashinde ili atimize malengo yake,

  “Nashukuru dada Kajala kama mimi ndio mshindi hakika nimefurahi kwa kunitangaza mimi, maana nina uhitaji wa fedha ukizingatia kwamba shughuli zangu kwa sasa nashughulika na mambo ya magari yanayokwenda Namanga,” Alisema Mkongwa.

  Naye Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, alisema wanafurahishwa na utaratibu mzima unaofanywa na Biko katika kuwapata washindi wa papo kwa hapo na wale wa droo kubwa ya Sh Milioni 10 na hii ya Milioni 20 iliyofanyika Jumatano na kupatikana Mkongwa kutoka mkoani Arusha.

  “Ni wakati wa Watanzania kujitokeza kwa wingi kucheza Biko kwasababu fedha zipo nje nje na kila mtu anaweza kushinda, ukizingatia kuwa Biko wanakidhi vigezo vyote na mchezo wao ni mzuri unaoweza kutoa fedha kwa kila Mtanzania,” Alisema.

  Mkongwa anakuwa mtu wa kwanza kushinda donge nono la Sh Milioni 20 lililowekwa katika droo ya Jumatano, huku akiwa mtu wa pili kushinda dau kubwa likiwapo la Sh Milioni 10 ambapo zimetolewa kwa washindi tisa, huku yeye pekee akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake Sh Milioni 20 mapema iwezekanavyo kama atakavyopewa utaratibu na Biko.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
  ******

  Azimio la Arusha ni tamko rasmi la kisiasa lililokusiwa kuongoza Tanzania  Kijamaa kadiri ya kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Neno Azimio linatokana na Mji wa Arusha na lilipitishwa tarehe 26-29 January 1967.

  Tamko la Arusha lina sehemu tano, Yaani Itikadi ya Chama cha TANU, Siasa ya ujamaa, Siasa ya kujitegeea, Uanachama wa TANU na Azimio la Arusha.

  Kiini chake ni hiki, Tumeonewa kiasi chakutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na unyonge wetu ndio umetufanya tuonewe.

  Lengo kuu la Azimio la Arusha ni kupinga unyonyaji, ubaguzi ili kuleta usawa ndani ya jamii.

  Hili lilikuwa ni AZIMIO lenye misingi ya utu, na lengo kubwa la AZIMIO la ARUSHA ni kujitegemea, kiuchumi na si kisiasa peke yake na hasa kuwaondoa Waafrika katika mawazo ya kitumwa, kama Bob Marley alivyoimba, Emancipate yourself from mental slavery.

  Kitendo cha JPM kufuta posho, safari za nje, wakubwa kupunguzwa nguvu ya ubabe, Mali za watumishi wa umma kuhakikiwa, kuzuia kusafirishwa kwa wanyama hai na madini nje ya nchi, kuchunguzwa kwa mchanga wa madini, kutoa elimu bure yote haya ni matendo yanayoendana na misingi ya Azimio lililotaka kuondoa ubaguzi, kuondoa matabaka ndani ya jamii, kudumisha utu, kuondoa unyonyaji ili tuweze kujitegemea kiuchumi.

  Tumeanza kuheshimiana sasa. Ule msemo wa laki si pesa umekufa kabisa, zile kauli za unanijua Mimi nani hakuna tena. Haki ipo kwa wote ndani ya jamii.

  Hauwezi kuyafanya hayo bila ya kuwa na uzalendo kama alionao Rais Magufuli. Naona kila dalili Rais Magufuli akiturudisha kulienzi na kulidumisha Azimio la Arusha lililoasisiwa na Mwalimu Nyerere

  Na Emmanuel J. Shilatu
  01/06/2017
  0767488622

  0 0

  Mwenyekiti wa Baraza la wazee mkoa wa Arusha Mathius Kichao aliyeshika karatasi mkononi,akiwa anazungumza na waandishi wa habari hivi katibuni Jijini hapo.Picha na Vero Ignatus Blog.
  Katibu wa wazee wa Baraza la wazee Jijini Arusha Kassim Seremuka  akizungumza jinsi ambavyo wazee hao wamenifaika na vitambulisho vya bima ya afya .Picha na Vero Ignatus Blog.
  Baadhi ya viongozi na wajumbe wa Baraza la wazee katika mkoa wa Arusha wakiwa katika picha ya pamoja .Picha na Vero Ignatus Blog.
  Katibu wa Baraza la wazee Kassim Seremuka Jiji la Arusha akionyesha Kadi ya matibabu wanazotumia wazee wakienda kutibi wa Hospitalini.

  Na.Vero Ignatus, Arusha.

   Baraza la Wazee Jijini Arusha wamemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwaangalia wazee ambao walikuwa  Jumuiya ya Afrika Mashariki awalipe  stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii mambo mazuri bali manufaa wameyakosa baada ya kuvunjika Jumuiya hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari  kwa niaba ya wazee hao mwenyekiti wa Baraza hilo  Mathius Kichao amesema  kuwa hadi sasa kuna wazee ambao hawajalipwa stahiki zao jambo ambalo siyo zuri hata kidogo kwani wazee hao wananung'unika

    "Kuna muda wazee hawa waliandamana wakenda Dar es salaam ,wakalala barabarani,lakini viongozi wawakati ule hawakuona umuhimu kuwa kilio cha wazee ni hatari sana wakawafukuzwa,nitamke kuwa hadi sasa kuna wazee wa jumuiya ya Afrika Mashariki hawajalipwa chochote kile, niikumbushe Serikali wale wazee wanalaani ,naomba hii laana isitokee,Mhe,Magufuli awalipe stahiki zao kwani wameifanyia nchi hii vizuri zaidi  "alisema Mwenyekiti huyo

   Aidha wazee hao  katika jiji la Arusha wameiomba serikali ya awamu ya tano ipeleke  mswada wa wazee katika Bunge la Jamhuri ya Muungano  na upitishwe  ili  Wazee nchini Tanzania  waweze kunufaika na matunda ya nchi yao kwani  wao ni chombo cha harakati hivyo Taifa likiwasahau wazee hakuna maendeleo kwasababu  wazee  huwa  wanafahamu mambo mengi ya kihistotia ya Nchi pamoja na mila nzuri na desturi.

  "Tunawaomba viongozi mbalimbali wa Taifa hili wanapotembelea mkoa wa Arusha watenge muda wao ili waweze kuonana na wazee tutawashauri kwa yale tunayoyafahamu kwaajili ya manufaa ya nchi yetu na watoto pamoja na wajukuu zetu.

  Katibu wa wawazee katika Jiji la Arusha Kassim Seremuka amesema kuwa  baada  ya Taifa kupata uhuru 1961 serikali ilianza kuweka katika ajenda zake maswala yanayohusu wazee,ambapo mwaka 2002 umoja wa Mataifa wakapitisha maazimiao yake ambapo Tanzania kama nchi iliyasaini  kuhusiana na haki za wazee ndipo kuanzia hapo ndipo serikali  ikaandika Sera ya Taifa ya Wazee.

  Amesema kuwa katika  Sera hiyo iliainisha mambo mengi ikiwemo haki ya msingi ya kikatiba,za kisheria haki za msingi za kibinadamu,ambapo serikali iliweka matamko kuwa  katika ibara ya2( 2,1) inasema sera hiyo inawahusu wazee waliopo vijijini na mjini ,pamoja na makundi maalumu ya wazee wakiwemo wastaafu,wakulima ,wafugaji,na wavuvi ,amesema sera hiyo inawahusu vijana wanaofanya maandalizi ya uzee mwema .

  Amesema kuwa wao kama baraza la wazee jiji la Arusha limesaidia wazee kutambulika ndani ya miezi 7 kuanzia mwezi wa 10 2016 wameweza kuwaratibu na kuwaandikisha kwaajili ya vitambullisho vya bima ya afya tayari wazee zaidi ya 6000 wameshapata vitambulisho hivyo kwa kusaidiwa na halmashauri ya jiji imetoa sh milioni kumi na mbili kwaajili ya mpango wa Tiba kwa kadi (TIKA)

  Katibu huyo amesema kuwa fedha hizo imegawanywa kwenye vituo vya afya,vya kata na halmashauri,amesema wazee wakienda hospitali wanakwenda na kadi zao na wanatibiwa hadi kwenye hospitali ya rufaa ya mount Meru bila kipingamizi chochote .

  0 0  0 0  0 0

  Jumla ya taasisi kumi za vijana zimeungana ili kuzidisha nguvu ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana wenzao nchini Tanzania na zaidi ikilenga matumizi ya mpango wa uzazi. Vijana hao wamejizatiti kuhahakisha kuwa kuna uwekezaji wa kutosha kwenye elimu juu ya uzazi wa mpango na pia vijana kuhusisha kwenye maamuzi yanayohusu vijana na afya ya uzazi.

  Taasisi hizo zimetiliana saini makubaliano na kuwa taasisi moja ikayoitwa Tanzania Adolescent and Youth Reproductive Health (TAYAHR) jana jijini Dar es Salaam ambapo taasisi hiyo itajikita zaidi kwenye kutoa elimu, kuhusisha vijana na kuhakikisha huduma inafika kwenye maeneo sahihi kwa muda sahihi.

  Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mwenyekiti wa TAYAHR William Otuck alisema Tanzania ina changamoto kuona ya kwamba asilimia 27 ya vijana wenye miaka 15-19 wana mtoto au ni wajawazito huku utumiaji wa uzazi wa mpango na hasa vidonge vya uzazi kati yao ikiwa ni chini sana – yaani asilimia 13 peke yake huku pia wakiwa hawana elimu yeyote kuhusu afya ya uzazi na hivyo kukosa uamuzi sahihi kwenye masuala ya kujamiiana.

  ‘Robo ya wasichana wenye umri kati ya 15 na 19 Tanzania wana watoto au ni wajawazito na hali ni mbaya kwenye mkoa wa Katavi yenye asilimia 45 na Tabora asilimia 42 kwa wasichana wenye umri huo. Hii inamaanisha kuna idadi kubwa ya wasichana ambao wanakatisha masomo na kuingia kwenye hali ya kuwa mzazi wangali wana umri mdogo na hii kwa kiasi kikubwa uchangia kuongeza hali ya umasiki kwenye jamii’, alisema Otuck huku akiongeza kuwa idadi kubwa ya wasichana wadogo wakipata mimba pia kunachangia kuongezeka vifo vitokanavyo na uzazi.

  Akizungumzia kuhusu elimu na hali ya kupata mimba za utotoni, Otuck alisema tafiti zinaonyesha kuwa ni asilimia 10 wa wasichana ambao wana elimu mpaka ya sekondari ambao hupata mimba wakiwa na umri mdogo kulinganisha na wale wana elimu ya msingi ambao ni asilimia 34 na wale ambao hawana elimu kabisa ni asilimia 52.

  Taasisi hiyo chini ya uongozi wa vijana pia imelenga kuhamasisha wenye kutoa maamuzi (policy makers) kuwekeza kwenye kupanua wingo la matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango ili kufikia walengwa ambao bado hawajafikia, ambapo kwa sasa inaonyesha asilimia 23 ya wanawake vijana wanatamani kutumia uzazi wa mpango lakini bado huduma hiyo haiwajafikia na pia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango kwa vijana angalau kufikia asilimia 80 ifikapo 2010 na pia kuendeleza elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.

  Taasisi hizi kabla ya kufikia makubaliano yao zilianza mazungumzo mwezi Oktoba na Novemba mwaka jana chini ya FP2020 Secretariat, mradi wa Advance Family Planning (AFP) Tanzania pamoja na taasisi ya Torchlight Collectives. TAYAHR inaundwa na taasisi za Hope Centre for Children, Girls and Women in Tanzania, YAM-UMATI, AfriYAN, TYVA, SAYI, Restless Development, Zanzibar Youth Forum (ZAFAYCO), IYAFP/Young and Alive Initiative (YAAI), SHDEPHA+ na YUNA.

  0 0


   Baadhi ya Waombolezaji wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakia nyumbani kwa Mzee Ndesamburo. 
   Nyumbani kwa Marehemu Mzee Philemoni Ndesamburo aliyefariki dunia jana katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi. 
   Baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu wakijiandaa kwenda kutizama mwili wa Mzee Ndesamburo katika HospItali ya Rufaa ya KCMC.

   Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini ,Godbless Lema pamoja na mkewe Neema Lema wakiwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo.
   Mbunge wa jimbo la Arusha mjini ,Godbless Lema akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini mara baada ya kukutana nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo . 
   Mtoto wa Marehemu Ndesamburo ,Ndohorio Ndesamburo akiwaeleza jambo waombolezaji waliofika nyumbani kutoa pole kwa familia. 
   Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Kaskazini,Aman Golugwa akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo. 
   Baadhi ya viongozi wa Chadema wakiwa katika kikao kifupi nyumbani kwa mareheu Ndesamburo. 
   Familia ya marehemu Ndesamburo wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya kutizama mwili wa mpendwa wao. 
   Mkurugenzi wa kampuni ya World Frontier,John Hudson akimfariji ,mtoto wa marehemu Ndesamburo,Lucy Owenya nyumbani kwao eneo la Mbokomu mjini Moshi. 
   Baadhi ya waombolezaji wakiwafariji wafiwa.


  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

older | 1 | .... | 1254 | 1255 | (Page 1256) | 1257 | 1258 | .... | 1897 | newer