Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1249 | 1250 | (Page 1251) | 1252 | 1253 | .... | 1896 | newer

  0 0


  BAHATI Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku, sasa imezidi kuchanja mbuga baada ya kuongeza donge nono la washindi wa droo zao kubwa, ambapo sasa mshindi wa droo ya Jumatano hii anatarajiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20.

  Mbali na kutoa kiasi hicho cha pesa, tayari imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili ambaye ni Leopard Mpande wa jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia Biko ikiwa imeshapata washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo. 


  Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya tisa ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea kwa kutangazwa mshindi hivyo atajinyakulia Sh Milioni 10 kutoka Biko. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.

  Kajala Masanja akizungumza na Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo.
  Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akiandika dondoo za mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko aliyetangazwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea katika droo hiyo.

  Akizungumza leo katika droo iliyompata Mpande, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba wameamua kuongeza zawadi ya droo kubwa ya jumatano hii kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 ili kuwawesha washiriki nafasi ya kujikwamua kimaisha kwa zawadi za BIKO, "Changamkieni fursa hii" alisema.

  Alisema droo ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 itafanyika Jumatano, huku akiwataka watu wacheze mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za MPESA, TIGOPESA na AIRTEL Money kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili au lipa kwa MPESA ambapo watatakiwa waingize namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kuweka pia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.

  “Ukifanya hivyo utaweka kiasi cha kununua tiketi kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo Sh 1000 itakuwa na nafasi mbili za ushindi kwenye droo kubwa ya Jumatano pamoja na kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na sh 1,000,000, huku donge kubwa likipanda kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 Jumatano hii.

  “Biko ni kutoa pesa kwa washindi wetu ili wafanikiwe katika maisha yao, hivyo wanachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi, huku pia nikimpongeza mkazi wa Arusha, ndugu Mpande kufanikiwa kuibuka na Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa Jumapili,” Alisema.

  Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo, aliwapongeza Biko kwa kufikia hatua ya kutoa Sh Milioni 20 kwa washindi wa droo kubwa ya Jumatano akisema ni hatua nzuri, hivyo Watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo ili waibuke na mamilioni ya Biko.

  “Sisi tunafuatilia kwa karibu mchezo wa Biko na tunaridhishwa na utaratibu wao wa upatikanaji wa washindi wa droo zao kubwa na ni mchezo wenye uaminifu mkubwa hapa nchini ambapo wanatarajia droo ya Jumatano hii kutoa Sh Milioni 20, jambo ambalo ni zuri kwa mustakabali wa kukuza uchumi kwa washiriki wote wa bahati nasibu ya Biko,” Alisema Ngolo na kumpongeza pia mshindi wa Arusha aliyeibuka na jumla ya Sh Milioni 10,” Alisema.

  Kwa mujibu wa Biko, droo ya Jumatano hii itatoa Sh Milioni 20, huku mshindi wao wa Arusha wa Sh Milioni 10 akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo kama walivyopewa washindi wengine walioshinda katika droo nane za Jumatano na Jumapili zilizopita.

  0 0

  Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akikaribishwa katika Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) mara baada ya kufungua Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera kuanzia tarehe 28 Mei had Juni 01.

  Wito umetolewa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwafikia wakulima, wafugaji na wavuvi wadogo nchi nzima ili kuweza kuwakwamua katika changamoto zinazorudisha nyuma juhudi zao za kujiongezea kipato kwa kukosa mitaji ya uhakika katika kuongeza tija ya kilimo nchini.

  Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Kampeni ya Wiki ya Maziwa inayofanyika Kitaifa mjini Bukoba, mkoani Kagera.

  Mhe. Ole Nasha amesema kuwa dhima ya kuanzishwa kwa TADB ni kutoa suluhisho la ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha na mikopo kwa wakulima wadogo nchini ili kuchagiza maendeleo ya kilimo nchini hivyo Benki ina wajibu wa kuwafikia wakulima wote wadogo wenye uhitaji wa mikopo.

  “Nawaomba mujielekeze kutoka mikopo yenu ya gharama nafuu kwa wakulima wadogo ambao hawawezi kupata mikopo kwenye benki za biashara ili kutekeleza lengo la Serikali la kuwainua wakulima kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” Mhe. Ole Nasha alisema.

  Aliongeza kuwa anafahamu kuwa Serikali ikishirikiana na TADB ilifanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kupelekea Bodi ya Benki ya Maendeleo Afrika kutoa kibali cha kuipatia TADB fedha za kukopesha kwenye sekta ya kilimo, na kuitaka Benki hiyo kutumia fedha hizo kwa kuwapatia wakulima wadogo ambao ni wahitaji zaidi wa miko hiyo.

  “Naomba muwakopeshe wakulima hizo fedha ya zaidi  Bilioni 200 ili kuwaongezea tija katika shughuli zao,” aliongeza.

  Kwa mujibu wa mpango kazi wa TADB hadi kufikia miaka mitano ijayo itakuwa imefungua ofisi sita za kikanda zenye lengo la kuwahudumia wakulima wote nchini. Ambapo katika hatua za awali Benki hiyo inaendelea kuwajengea uwezo wakulima wa nchi nzima ili kuwaandaa kupata mikopo kutoka Benki hiyo.

  Mpango kazi huo unaweka bayana malengo mengine yanayojumuisha utafutaji wa fedha toka vyanzo mbalimbali zenye gharama nafuu kwa minajili ya kuwakopesha Wakulima katika hatua zote za mnyororo wa ongezeko la thamani kwenye mazao ya Kilimo na kupanua wigo wa utaoji mikopo toka Minyororo Kumi na Minne (14) ya mwanzo na kuhusisha pia mazao mengine ya Kilimo na pia kuwaunganisha wakulima na masoko ya ndani na nje ya nchi.

  TADB ni taasisi ya serikali ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo  na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
  Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (kushoto) akizungumza wakati Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) alipotembelea Banda la TADB.
  Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) akizungumza na maafisa wa TADB (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa Benki hiyo kuwafikia wakulima wote nchini.
  Afisa Tathmini wa Mikopo Mwandamizi wa TADB, Bw. Mubezi Buberwa (kulia) na Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (wapili kulia) wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) wakati alipotembelea Banda la TADB.
  Afisa Tathmini wa Mikopo Mwandamizi wa TADB, Bw. Mubezi Buberwa (kulia) akifafanua hoja mbali mbali kuhusiana na mikopo inayotolewa na Benki hiyo.
  Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa TADB, Bw. Saidi Mkabakuli (kulia) akimuelezea Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa William Tate Ole Nasha (MB) (mwenye tai) mpango wa TADB kuwafikia wakulima nchi nzima.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba, akiwa katika mkutano na waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Jijini Dar Es Salaam leo, akizungumza kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Tarehe 5 Juni, ambapo Kitaifa mwaka huu yatafanyika Mkoani Mara kijijini Butiama kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambapo Pamoja na Mambo Mengine pia alikuwa Mwanahakati wa Mazingira. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Mkamu wa Rais Mwandisi Ngosi Mwihava.

  0 0


  Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, William Malonza, akimuonyesha moja ya bidhaa zizalishwazo na kiwanda hicho, Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, wakati wa maonyesho ya tano ya Kimataifa ya biashara yanayofanyika katika viwanja vya Mwahako Tanga.

  Mwijage ameyafungua maonyesho hayo leo katika viwanja ya maonyesho Mwahako ambayo yamezishirikisha mataifa mbalimbali ya Barani Afrika na Asia.

  Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akisalimiana na Afisa Masoko kiwanda cha saruji cha Rhino Tanga, Carolina Hillary wakati alipotembelea banda la maonyesho ya tano ya Kimataifa yalifunguliwa jana Tanga katika viwanja vya maonyesho Mwahako.

  Waziri wa viwanda na Biashara, Chales Mwijage, akibadilishana mawazo na Meneja Mkuu Idara ya Masoko kiwanda cha Saruji cha Rhino Tanga, William Malonza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Tanga.
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Chales Mwijaga akipata maelekezo ya namna mkonge unavyoweza kutengeneza dawa pamoja na mafuta aina mbalimbali.

  Simba ni moja katika wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya maonyesho Tanga  Wakazi wa Tanga wakiangalia Kobe ambaye ni moja ya vivutio katika maonyesho ya tano ya Kimataifa yanayofanyika Tanga. blog ya kijamii ya tangakumekuchablog 0655 902929

  0 0

  Inspekta Jenerali wa Polisi (Mteule) Simon Sirro


  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akijibu hoja mbalimbali wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 bungeni mjini Dodoma.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo makani akijibu hoja mbalimbali wakati wa kuhitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 bungeni mjini Dodoma.
  Picha ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, Viongozi wakuu na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo wakiwa nje ya lango la Bunge mara baada ya kikao cha Bunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo.

  Na Hamza Temba - WMU 
  ---------------------------------------------------------------------
  Serikali inafikiria kuunganisha taasisi zote zinazohusika na sekta ya uhifadhi wa wanyamapori nchini kuwa chombo kimoja chenye nguvu  kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa taasisi hizo pamoja na kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika sekta hiyo muhimu hapa nchini.


  Akizungumza mwishoni mwa wiki bungeni mjini Dodoma wakati akihitimisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe alisema anaunga mkono ushauri uliotolewa na wabunge mbalimbali ukiwemo wa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye juu ya umuhimu wa kuunganisha taasisi hizo za uhifadhi.


  "Wakati umefika sasa, tusiwe na makampuni (taasisi) zaidi ya manne ndani ya sekta hii ya wanyamapori, tuwe na kampuni (taasisi) moja tu ambayo itapunguza gharama katika uendeshaji, tutaunganisha jeshi la wahifadhi na jeshi hilo tutakalolitengeneza ni jeshi moja tu ambalo litakua na malezi chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania, ili kujenga nidhamu, kuheshimu haki za binadamu na kufanya kazi kwa mujibu wa maslahi ya taifa,". alisema Maghembe. 


  Aliongeza kusema "Jeshi hilo ambalo tunaliandaa kisasa, jeshi usu litakua na "chain ya comand" moja na litawajibika kijeshi kwa makosa ya haki za kibinadamu na usaliti wa taifa au usaliti wa uchumi wa nchi yetu".


  Awali akiwasilisha bungeni hapo hotuba ya makadidirio ya mapato na matumizi ya Wizara yake, Prof. Maghembe alizitaja taasisi hizo kuwa ni Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) na  Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).  


  Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) lilianzishwa mwaka 1959 kwa Sheria ya Hifadhi za Taifa Sura 282 na kupewa dhamana ya kusimamia na kuendeleza maeneo yaliyoanzishwa kisheria kuwa Hifadhi za Taifa. Hifadhi hizo ambazo zipo 16 zina jumla ya kilometa za mraba 57,365.80. 


  Kwa upande wake, Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) ilianzishwa kwa Sheria Sura 284 na kupewa jukumu la kusimamia eneo la kilometa za mraba 8,292 kwa ajili ya kuhifadhi, kuendeleza utalii na wafugaji wenyeji wa eneo hilo ambapo wakati mamlaka ikianzishwa walikua takriban 8,000 mwaka 1959 na idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia zaidi ya wakazi 90,000 mwaka uliopita, 2016. 


  Nayo, Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) ilianzishwa kwa Tangazo la Serikali Na.135 la tarehe 9 Mei, 2014 chini ya Kifungu cha 8 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Sura 283 ikisomwa pamoja na marekebisho yake yaliyotolewa katika Tangazo la Serikali Na.20 la tarehe 23 Januari 2015. Mamlaka hiyo ilianza kazi rasmi tarehe 1 Julai, 2016. 


  Mamlaka hiyo ina jukumu la kusimamia uhifadhi wa wanyamapori kwenye Mapori ya Akiba 28, Mapori Tengefu 42  na maeneo ya wazi yenye mazalia ya wanyamapori, mtawanyiko na shoroba. Aidha, Mamlaka inashirikiana na jamii katika kusimamia maeneo 22 ya jumuiya za hifadhi za wanyamapori na maeneo manne ya ardhioevu yenye umuhimu wa kimataifa (Ramsar Sites).


  Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ilianzishwa kwa Sheria Sura 260 kwa lengo la kusimamia, kufanya na kuratibu utafiti wa wanyamapori nchini. Taasisi hiyo ina wajibu wa kutoa ushauri kuhusu uhifadhi endelevu wa wanyamapori kwa kutumia matokeo ya utafiti wa kisayansi. Aidha, TAWIRI inawajibu wa kufanya Sensa ya makundi mbalimbali ya Wanyamapori ili kushauri Wahifadhi na Serikali.


  Akizungumzia umuhimu wa uhifadhi wa Wanyamapori, Prof. Maghembe alisema sekta ya maliasili kwa ujumla inachangia asilimia 21.4 ya pato lote la taifa, ambapo mchango wa wanyamapori kupitia utalii ni asilimia 17.5 na misitu asilimia 3.9. Aliongeza kuwa wanyamapori pia husaidia katika tafiti mbalimbali duniani kwa ajili ya utafutaji wa dawa za kutibu maradhi ya binadamu.


  Katika mwaka huu wa fedha 2017/2018, Bunge limeidhinisha Sh. bilioni 148.597 kwa ajili ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii, ambapo Sh. bilioni 96.794 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh. bilioni 51.803 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 

  0 0


  Tabora, Tanzania

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Alhaj Abdallah Bulembo, ameendelea na ziara yake ya Kichana katika mikoa mitano ambapo leo ziara hiyo imemfikisha katika Wilaya za Igunga na Nzega mkoani Tabora, ambako amefazungumza katika vikao vya ndani na Wajumbe wa Halmashauri Kuu za CCM za wilaya hizo, Mabalozi na watendani wa CCM na Serikali.

  Pamoja a kuzungumzia uchaguzi wa ndani ya Chama unaoendelea ngazi za mashina, pia amesisitiza haja na umuhimu wa madiwani kufanya kazi kwa Karibu na Mabalozi. Zifuatazo ni mfululizo wa matukio katika picha kuhusu ziara hiyo, tafadhali endelea kutazama.

  0 0

   Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kulia akiteta jambo na  Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kulia wakati alpolitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye  viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
   Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kushoto akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kunufaika na huduma zinazo tolewa nao kwa wananchi walilitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
   Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Bima ya Taifa Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo kushoto akitoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuweza kunufaika na huduma zinazo tolewa nao kwa wananchi walilitembelea banda lao  wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga
   Wananchi wakipima presha kwenye banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo

  Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia kushoto akisubiri kujeza fomu za wananchi ambao wanakwenda kupima uzito na afya kwenye Banda lao ambapo wanatoa elimu namna ya kujiunga na mfuko huo,kupima afya.habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

   Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma (Hawapo Pichani) wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith Mahenge ofisini kwake akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na Kusisitiza Utekelezaji wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Songea. 
   Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith Mahenge akizungumza
   Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (Hawapo Pichani) akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na Kusisitiza Utekelezaji wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Songea. 
  Mtendaji wa Mahakama, Samson Mashalla akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu Utumishi kwa Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Jaji Kiongozi kwenye kanda hiyo. 


  Na Lydia Churi, Songea

  Katika ziara hiyo Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali amesema Mahakama itashirikiana na wadau wake ili kuhakikisha kesi zinamalizika kwa haraka kwenye mahakama mbalimbali nchini. 

  Amesema kupitia nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa mahakama ya Tanzania ambayo inasisitiza kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama, Mahakama itatoa elimu kwa wananchi pamoja na viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya juu ya masuala mbalimbali yanayohusu utoaji wa haki kwa wananchi. 

   Jaji Kiongozi amesema Mahakama imejiwekea mikakati ya kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati na kwa haraka ukiwemo mkakati wa kesi kutokukaa kwa zaidi ya miaka 2 kwenye Mahakama Kuu, miezi 12 Mahakama za mikoa na Wilaya pamoja na miezi sita kwenye Mahakam za Mwanzo. Mikakati mingine ni ile ya kesi kusikilizwa kwa mfululizo na kuwekwa kwa maahirisho mafupi mafupi ya kesi kwenye Mahakama mbalimbali nchini na Majaji na Mahakimu kupangiwa idadi ya kesi watazosikiliza katika kipindi cha mwaka moja. 

  Aidha, kila Jaji amepangiwa kusikiliza na kumaliza kesi 220 kwa mwaka ambapo Mahakimu wamepangiwa kumaliza kesi 250 kwa mwaka. 
  Akizungumzia Maadili kwa watumishi wa Mahakama, Jaji Wambali amewataka watumishi hao kuwahudumia wananchi wanaofika mahakamani kwa bidii, uaminifu, na uadilifu ili kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama. 

  Amesema watumishi wa Mahakama hawana budi kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano kwa kuwa kazi za mahakama zinategemeana ambapo kila kada ina umuhimu wake katika wananchi kufikia haki zao za msingi.
   Jaji Kiongozi yuko kwenye ziara katika kanda za Songea na Mtwara kwa ajili ya kukagua shughuli za kimahakama pamoja na kusisistiza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania. Tayari ametembelea mahakama zilizoko Songea mjini na zile za wilaya za Mbinga, Nyasa, Namtumbo, na Tunduru.

  0 0


  0 0

  · Wateja wa mtandao wa simu Zantel sasa kufurahia mawasiliano na ndugu jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu kwa kutumia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni.

  Kampuni ya simu ya Zantel inaendelea kutimiza ahadi yake ya kuongeza thamani katika maisha ya wateja wao na sasa kutangaza ofa maalum inayowalenga waumini wa dini ya Kiislamu nchini ili kuadhimisha mwezi mtukufu wa mfungo wa Ramadhani duniani kote.

  Akitangaza habari hii makao makuu ya kampuni ya Zantel yaliyopo Msasani jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa Zantel Bw. Benoit Janin amesema “Ramadhani ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki na ofa hii ni ishara ya Zantel kuwasaidia wateja wake kuweza kuungana na kuwasiliana kwa urahisi zaidi na wapendwa wao”.

  Aliongeza kwa kusema mtandao wa Zantel utaendelea kutoa huduma kwa mamilioni ya Watanzania kuwasaidia kutimiza malengo na ndoto zao kupitia vipengele mbali mbali vya huduma za kampuni hiyo ikiwa ni pamoja bidhaa na huduma za upigaji simu, vifurushi vya internet na mtandao.

  Alisema kampuni itahakikisha vyote hivi kwa kutoa huduma na bidhaa bora za upigaji simu na vifurushi vya intaneti huku tukihakikisha tunawekeza faida endelevu. Kwa mwaka 2016 kulikua na matatizo mbali mbali ila kwa sasa mkakati wetu ni kuhakikisha tunatoa vipao mbele kwa vitu vyenye umuhimu mkubwa kwa wateja ikiwemo kuwa mtandao bora unaotoa intaneti ya kasi zaidi wa 4G, kupenya na kuwafikia watumiaji wengi zaidi,na kujiandaa kwa siku zijazo kuwa kampuni ya bidhaa inayopendwa zaidi.

  “Tunahitaji kuwa tayari kwa siku zijazo kwa njia mbali mbali za kuongeza mapato pamoja na huduma zinazoongeza thamani ya mtandao wa zantel ikiwemo uboreshaji wa vifurushi vya intaneti, tayari tunaona mabadiliko makubwa katika mtandao wetu” aliongezea kwa kusema “Kutakua na bidhaa mbali mbali tutakazozitoa kipindi hiki zitakazofurahiwa na wateja wetu kukiwa na mpangilio wa ofa zilizoanza tarehe 24/05/2017” Aliongezea.

  Akielezea zaidi kuhusu ofa hii, Mkurugenzi wa masoko wa Zantel Bw. Gasper Mbowa amesema”Ofa hii ya Ramadhani imelenga kuwazawadia wateja wetu wa malipo ya kabla watakaojiunga na vifurushi vyetu kwa kiasi chochote au kwa kuongeza muda wa maongezi kwenye kipindi cha mfungo wa Ramadhani. Mteja yoyote atakayeongeza mda wa maongezi atapata asilimia 50 ya muda wa maongezi moja kwa moja utakaomuwezesha kupiga simu Zantel kwenda Zantel, ofa hii itakua inatumika kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi.

  Vivyo hivyo wateja wataweza kutumia huduma zetu zilizozinduliwa hivi karibuni kama ‘Zantel madrassa itakayowawezesha kujifunza dini ya kiislamu kwa kupokea mafunzo ya Quran, hadith, dua, habari za BAKWATA na huduma nyingine nyingi kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia ujumbe mfupi wa maneno au kwa kupiga simu.

  Mbowa aliongezea kuwa wateja wa Zantel wanaweza kuwapigia simu ndugu, jamaa na marafiki waliopo mashariki ya kati kwa bei nafuu zaidi kupitia kifurushi cha kimataifa cha uarabuni. “Kwa shilingi za kitanzania 2,000 wateja watapata dakika 4 za kupiga simu Qatar, Oman, UAE, Lebanon, Pakistan, Yemen & Saudi Arabia, na kwa shilingi 5,000 watapata dakika 7 kupiga simu kwenda kwenye nchi tajwa, na fedha hizo zitakatwa moja kwa moja kwenye akaunti zao”

  Vifurushi vyote hivi vitapatikana kwa kujiunga kwa kupiga *149*15# na kwa vifurushi vya ‘Bonga Mpakabasi’, ‘Zantel Madrassa’ wateja wataweza kujiunga kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa kutumia neno SUB na kutuma kwenda namba 15586 au kwa kupiga namba 15586

  0 0

  Semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu VVU na Ukwimu iliyoandaliwa na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,mjini Dodoma.

  Miongoni mwa masuala yaliyozungumzwa katika semina hiyo ni changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania katika mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi.

  Changamoto hizo ni pamoja na Sheria ya Magereza, adhabu ndogo kwa wanaoambukiza watu wengine VVU kwa makusudi zilizoanishwa katika Sheria ya Ukimwi, mila na desturi zilizopitwa na wakati (ukiwamo ukeketaji) na unyanyasaji wa kijinsia.

  Mzungumzaji mkuu katika semina alikuwa ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Elizabeth Kaganda. 
   Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS,  Elizabeth Kaganda akitoa elimu ya sheria ya maambukizi ya ukimwi wakati wa semina ya wahariri wa vyombo  vya habari na waandishi wa habari kuhusu VVU na Ukwimu iliyoandaliwa na Tacaids mjini Dodoma.
    Mkutumbi (LIBRARIAN) Bwana Elisha Mngale kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS, akifafanua tafiti za maambukizi ya Ukimwi zinazofanywa na Tume hiyo.
   Waandishi wakitoa taarifa mbalimbali na changamoto zinazohusiana na maambukizi ya ukimwi wakati wa semina ya wahariri wa vyombo  vya habari na waandishi wa habari kuhusu VVU na Ukwimu iliyoandaliwa na Tacaids iliyofanyika mjini Dodoma.
  Waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali wakifuatilia mada katika semina hiyo.

  Picha zote na Philemon Solomon.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka Mara baada ya kuwasili katika Mahafali ya Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam jana katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni.

  Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo akisalimiana na Kaimu Mwenyekiti Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Asha Ferouz Mara baada ya kuwasili katika Mahafali ya Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar Es Salaam Leo katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni.

  Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo pamoja na Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakiwasili Ukumbini.

  Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo pamoja na Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakiteta jambo.

  Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo pamoja na Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wakifurahia jambo.

  Meza Kuu wakiburudika na nyimbo ya CCM uku wa kionesha Ishara Mshikamano na Umoja


  Wahitimu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Wakicheza uku wa kishikana Mikono ishara ya Umoja

  Wanafunzi wakishangilia

  Kaimu Mwenyekiti wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Asha Ferous akisoma Taarifa kwa Mgeni Rasmi Katika Sherehe za Mahafali ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam jana

  Wana Vyuo na Vyuo Vikuu Wakiwa Ukumbini


  Kaimu Katibu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Ndg Daniel Zenda akizungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon jana

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na
  Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana

  Baadhi ya Wahitimu wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka  Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg:Rodrick Mpogolo akipeana Mkono na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM mara ya Baada ya kumaliza kuzungumza katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na
  Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana

  Wanavyunzi wahitimu Wakiimba Shairi katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana

  Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Cha Kidemokrasia wa kwanza kulia Ndg:Aloyce Mukami akiwa katika mahafali hayo

  Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Cha Madaktari MUHIMBILI akishangilia jambo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana

  Naibu Katibu Mkuu CCM Bara ndg:Rodrick Mpogolo akitoa Vyeti kwa Wahitimu Makada wa CCM Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana.

   Kada Aldelatus Mushumbusi toka Tawi Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM Mabibo Hostel akikabidhiwa Cheti na Mgeni Rasmi Ndg :Rodrick Mpogolo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana

  Kada Aldelatus Mushumbusi toka Tawi Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM
  Mabibo Hostel akipewa Mkono wa Pongezi na Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana

  Kaimu Mwenyekiti wa Idara ya Vyuo na Vyuo vikuu UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam Asha Ferouz akikabidhiwa Cheti cha pongezi na Mgeni Rasmi ndg:Rodrick Mpogolo katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana.

  “Ujana ni rika, ujana ni wakati na wakati haurudi nyuma” haya yalizungumzwa na mgeni rasmi Ndg. Rodrick Mpogoro Naibu
  katibu Mkuu CCM Bara kwenye mahafali ya Vijana Chama Cha mapinduzi
  kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo
  28/05/2017 katika ukumbi wa King Solomoni Kinondoni.

  Ndg. Rodrick Mpogoro alisema, Siri pekee ya kufanikiwa kwa mtu yeyote
  inategemea namna anavyotazama na kutathmini mambo. Ni mtazamo chanya pekee ndiyo humvusha mtu kwenye mafanikio, hivyo ipo haja kwenu vijana kujikita kutazama fursa zinazowazunguka na kuwa wabunifu ili
  kujitengenezea vipato vyenu wenyewe kuliko kusubiria ajira, alisema.

  “Sura ya Chama Cha Mapinduzi inajengwa na wanachama wenyewe kwa vitendo,jengeni uadilifu, zungumzeni habari ya uzalendo wa nchi yenu, jengeni maslahi kwa wanyonge, jifunzeni historia ya Chama, someni katiba na kanuni zake, fanyeni kazi kwa bidii na jengeni moyo wa kujitolea
  mkifanya hayo mtafanikiwa*. Alisema.

  Alifahamisha kuwa ni vyema kwa wanachama, wananchi na kila mpenda amani, umoja na maendeleo ya Taifa kuendelea kumuunga mkono Rais wetu Mhe Dr. John Pombe Magufuli katika juhudi anazozifanya za kupambana na ubadhilifu wa mali za umma kwani anaiishi misingi ya Chama Cha mapinduzi kama ilivyoainishwa kwenye madhumuni yake kupitia katiba Ibara ya 5. 

  *”Simameni imara katika kumuunga mkono Rais wetu kwani anaiishi misingi ya Chama Cha Mapinduzi katika kujenga uzalendo wa nchi”.
  Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Ndg Rodrick Mpogolo akizungumza na Wahitimu Makada wa CCM Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM katika Sherehe za Mahafali ya kuwaaga Makada wa CCM idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu uvccm Mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa King Solomon Kinondoni jana.

  Maonyesho ya karatee

  PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI UVCCM

  0 0  Na  Bashir   Yakub  

  Mikataba yote ya kimataifa huongozwa na wajibu wa aina mbili. Wajibu ulioandikwa(express obligation) na wajibu ambao haukuandikwa(implied obligation). 

  Wajibu ulioandikwa ni masharti yote ya mkataba yaliyo katika maandishi  ambayo wahusika husoma na kuridhia, wakati wajibu usioandikwa ni masharti ya mkataba ambayo hayakuandikwa katika mkataba lakini  yapo kwa asili au yapo kwa kuwa tayari yalishasemwa na sheria na hivyo si lazima kuyaandika katika mkataba. 

  Mathalan, mfanyakazi  wako wa duka hawezi kukuibia halafu akasema kwenye mkataba wangu wa ajira hakuna sharti la uaminifu. Laa hasha  uaminifu  ni sharti la asili "implied obligation" kwa hiyo liandikwe au lisiandikwe  bado lipo tu.Kwenye mikataba ya kimataifa kama ile ya kwetu na makampuni  ya madini masharti yafuatayo ni ya  asili na hayahitaji kuwa yameandikwa ili kuyatekeleza :

  1. Wajibu wa kuanika taarifa zote muhimu kuhusu  shughuli inayotekelezwa katika mkataba( Implied covenant to disclose all necessary information over the subject matter). 
  2. Wajibu wa kutekeleza na kutenda  kwa nia njema(Implied covenant to act in good faith and fair dealing). 

  3. Wajibu wa kila mhusika katika mkataba kuwa  mkweli . Hili huwa ni katazo la udanganyifu(Fraud). 
  Haya yawe yameandikwa kwenye mkataba au hayakuandikwa yakikiukwa tafsiri  yake ni kukiuka masharti ya mkataba.

  Matendo kama kulaghai kuhusu uzito wa madini yanayochukuliwa, kulaghai kuwa unachukua dhahabu huku ukijua unachukua zaidi ya dhahabu, kulaghai kuhusu bei , kutotoa taarifa sahihi za kipi unapata na kipi hupati,nk ni kukiuka wajibu  na masharti ya mkataba jambo ambalo  ni kinyume cha sheria. Na ikiwa wamekiuka mkataba kwa misingi hiyo  basi Tanzania inaweza kufanya yafuatayo. 


  0 0


  Na Sixmund J. Begashe 

  Serikali ya Uswisi imeamua kuinga mkoni Serikali ya Jamhuuri ya Muungano wa Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa kuziwezesha program tano kiasi cha Dola za kimarekani 100,000 ambazo ni takribani Shilingi milioni 220/= ili ziweze kutoa elimu kwa njia za burudani ya mapambano dhidi rushwa nchini.

  Akizungumza kabla ya kusaini mikataba ya program hizo, Balozi wa Uswisi hapa nchini Mh ARTHUR MATTLI amesema kuwa Tanzania kwa sasa inafanya vizuri zaidi katika mapambano dhidi ya rushwa ukilinganisha na nchi nyingi barani Afrika hivyo wameona ni vyema ikaungwa mkono katika mapambano haya.

  Balozi Mattli ameongeza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha kuwa katika nchi za Afrika mashariki Tanzania inaongoza katika mafanikio yanayotokana na mapambano dhiri ya rushwa hivyo serikali yake imeona nivyema ikaunga mkono jitihada hizi kwa kuziwezeshwa program zitakazo toa elimu juu ya madhara ya rushwa kwa kupitia sanaa ili watanzania waweze kuipokea nakuielewa elimu hiyo kwa urahisi zaidi.

  Akizungumza baada ya kusaini makubaliano ya kupokea fedha za kuendesha programa ya Museum Art Explosion, kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti pamoja na kuishukuru Serikali ya Uswizi kwa kutambua jitihada za Makumbusho ya Taifa katika kuelimisha jamii juu ya mambo yanayo wahusu, amemwakikishia Balozi huyo kuwa fedha walizo pata zitatumika kama zilivyo kusudiwa na si vinginevyo.

  Nae Mkurugenzi wa Elimu kwa Jamii wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Bw EKWABI MUJUNGU ameishukuru Serikali ya Uswizi kwa kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Rushwa na kuahidi kufanya kazi kwa karibu na Taasisi zilizo wezeshwa na Ubalozi huo ili kuhakikisha malengo yaliyokusudia ya kupambana na rushwa yanafanikiwa.

  Taasisi zilizo wezeshwa ni pamoja Makumbusho ya Taifa kupitia Program ya MUSEUM ART EXPLOSION AGAINST CORRUPTION, Tanzania House of Talent (THT), Kijiji Studii Tanzania, Goba Africa LTD na Art in Tanzania.
   Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
   Balozi wa Uswisi nchini mh ARTHUR MATTLI akizungumza na viongozi wa program zilizowezeshwa na Ubalozi huo katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
   Katikati ni Balozi wa Uswisi nchini Mh ARTHUR MATTLI  na kulia ni Mkurugenzi wa Mkumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure wakishuhudia Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Bw Saimon Maliti akitia sahii makubaliano ya fedha za kuendeshea program ya Museum Art Explosion kwa mapambano dhidi ya rushwa 
  Kulia ni Mkurugenzi wa Elimuli kwa Jamii wa TAKUKURU Bw Ekwabi Mujungu na Muanzilishi wa THT Bw Ruge Mutahaba wakimsikiliza kwa Makini Balozi wa Uswisi nchini Mh  ARTHUR MATTLI(ayupo pichani)  .

  0 0


  Usikose kutazama matangazo ya moja kwa moja ya kuapishwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Simon Sirro kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam. Matangazo haya yatarushwa hewani kuanzia saa 3:30 asubuhu hii kupitia TBC, AZAM TV na ITV. Pia yatapatikana kupitia tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz (tembelea tovuti hiyo kupitia simu ya mkononi, computer, tablet ama kifaa chochote cha mtandao)

  0 0

  Mtaalam wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. David Plotner (kushoto) kutoka shirika la CDC Marekani akijadiliana na maafisa wa TEHAMA wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee (katikati) na Abdullah Othman (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee akitoa mafunzo ya kutumia Dodoso kwa njia ya tablet kwa washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Mratibu wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bi. Hellen Hillary (kushoto) kwa upande wa Tanzania Bara akijadiliana na mratibu wa utafiti huo kwa upande wa Tanzania Zanziar Bi. Nuru Masoud (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Meneja wa Takwimu za Jamii Bi. Sylvia Meku (katikati) akiwaelekeza washiriki wa mafunzo ya awali ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. Frank Mapendo (kushoto) na Jocelyne Rwehumbiza (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam akijibu maswali kutoka kwa Mtakwimu Bw. Stephen G. Cosmas wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
  Mtakwimu Bi. Hellen Mtove wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akimhoji mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati wa majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

  0 0

   Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili wa kikundi cha Thimba wakifanya onyesho lake kwenye tamasha la Gulio lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM kwenye mnada wa National, Nyakato mkoani Mwanza.
   Msanii nyota wa muziki wa hip hop wa Mwanza, Kembo akifanya onyesho kwenye tamasha la Gulio lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM kwenye mnada wa National, Nyakato mkoani Mwanza.

   Umati wa watu uliofika katika uzinduzi wa tamasha la Gulio la Mtaa lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM ambalo lilifana sana.
   Mkurugenzi Mkuu wa 102.5 Lake FM, Doreen Noni akiwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza katika kampeni hiyo na kuwaomba kuitumia kituo chao kupaza sauti.
   Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mama Ntilie waliopewa mafunzo ya upishi wenye usafi wa hali ya juu na kuzawadiwa zawadi mbalimbali wakati wa tamasha la Gulio la Mtaa.
  Mwakilishi wa kampuni ya Tigo, Baraka Siwa akizungumza katika tamasha hilo.

   Msanii ajulikanaye kwa jina la Manota  kutoka kikundi cha Tanzania Youth Talent (TYT) akionyesha manjonjo katika uzinduzi wa tamasha la Gulio la Mtaa lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM ya Mwanza.
   Msanii wa hip hop, Abuu Mkali akifanya onyesho atika tamasha la Gulio la Mtaa lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM kwenye mnada wa National, Nyakato mkoani Mwanza.

  Zaidi ya wasanii 20 wa muziki wa hip hop, bongo fleva, zouk, taarabu na ngoma za asili wa Kanda ya Ziwa walinogesha uzinduzi wa kampeni ya Gulio la Mtaa iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM katika mnada wa wafanya biashara wa National, Nyakato wilaya ya Ilemela mjini Mwanza.

  Wasanii hao ni Dogo D, Ngeta, H Mkali, G Stanza, Goliath, D Chance ambao ni wa hip hop wakati wa bongo fleva ni Abuu Mkali, King Suva, l Mavoko, Sania, na Lakezonia wakati wa zouk ni Sanja, Man Je Paul na Pradetha.

  Mbali ya wasanii hao, pia kulikuwa na msanii wa taarabu, Fatina huku kwa upande wa ngoma za asili kulikuwa na Kanyau, Shimba na KG wakati kwa upande wa muziki wa Raga alikuwa myota wa miondoka hiyo Volcano.

  Tamasha hilo pia hakikuwa sahau wasanii wa vichekesho kama Mama Manungwa, Malale na Mayala huku kikundi cha Tanzania Youths Talent (THT) kikionyesha staili mbalimbali za muziki na msanii wa wa wafanyabiashara wa Mnadani, Kembo akionyesha ujuzi wake katika miondoko ya hip hop.

  Mbali ya kupata uelewa wa masuala ya biashara, wafanyabiashara hao walipata burudani kutoka wasanii hao nyota kutoka kanda ya ziwa chini ya udhamini wa kampuni ya Tigo, Pepsi, Genic Studios, Lake Zone tents, Busybees Enterprises, Mama Sarakikya decoration na Mamba Entertainment.

  Tamasha hilo pia lilishuhudia redio hiyo kwa kushirikiana na wadhamini waliwazawadia Mariam Magembe kuwa mama lishe bora huku Khatibu Ramadhani alishinda taji la mwanazengo hodari.

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya biashara ndogondogo, minada na masoko, Justine Sagala, amekipongeza kituo cha 102.5 Lake FM kwa ujio huo kwani amesema ni wazo lenye tija baina ya radio nawananchi.

  Mkurugenzi Mkuu wa 102.5 Lake FM, Doreen Noni aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza katika kampeni hiyo na kuwaomba kuitumia kituo chao kupaza sauti zao.

  “Nimefuraishwa na mwitikio wenu katika uzinduzi huu na hii ni fursa kwenu kujua nini tunachokifanya kwa ajili ya ustawi wa jiji na wananzego kwa ujumla,” alisema Doreen.

  Mkuu wa Maudhui na vipindi wa redio hiyo, Yusuph Magupa aliwashukuru mashabiki wote waliofika katika uzinduzi huo na kuwaomba kushirikiana nao.

  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry kutumia fursa ya uwepo wa Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora, BTI mkoani humo kwa kuandaa utaratibu maalum utakaowawezesha wananchi hususan wafugaji wa nyuki kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi ya ufugaji wa nyuki chuoni hapo kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa bidhaa hiyo na kuwaongezea kipato.

  Waziri Maghembe ametoa kauli hiyo leo alipotembelea chuoni hapo wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tabora kwa ajili kujionea changamoto mbalimbali za uhifadhi na kuona namna kukabiliana nazo ikiwa ni ahadi aliyoitoa bungeni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018.

  “Mkuu wa Mkoa, tafadhali andaa utaratibu maalum kwa wananchi wako, wale wafugaji wa nyuki wanaweza kuja kwenye chuo chetu hapa hata siku tatu, hata siku mbili, wafundishwe namna bora ya kufuga nyuki, yani watoke kabisa huko Skonge, waletwe hapa, walale hapa sku moja au mbili wafundishwe baadae warudi makwao wajue namna bora ya kufuga na kuvuna asali,” alisema Maghembe.

  Kwa upande wake Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema maelekezo hayo kwao ni faraja kwakuwa tayari kuna maelekezo ya kiserikali kusaidia makundi ya kinamama na vijana ikiwemo utoaji wa mikopo kwa vikundi vyao vya ujasiriamali.

   “Katika Mkoa wangu tuna makundi haya ya kinamama na vijana ambao tumetakiwa kuwasaidia kwa maana ya kutenga “percent” (asilimia) fulani katika “own source” (vyanzo vya ndani vya mapato), kwahiyo kwa maelekezo hayo hayo nitakachofanya mimi ni kuhakikisha kwamba tunaenda kuwaeleza katika hali ya kawaida kwamba tungeweza kuwapa mikopo lakini tungependa tuwape mikopo baada ya kupata taaluma na waweze kujua vizuri namna bora ya kufuga nyuki na kurina asali”, alisema Mwanri.

  Mkuu wa Chuo hicho, Semu Daudi alisema chuo hicho kina jumla ya wanafunzi 155 na kinatoa mafunzo ya Cheti na Diploma ya Ufugaji wa Nyuki. 

  Naye Mkuu wa Kituo kidogo cha Utafiti wa Ufugaji Nyuki chuoni hapo, Humphrey Natali alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi ikiwemo usafiria ambapo gari lililokuwepo limepelekwa matengenezo na kompyuta zilizopo nazo ni za muda mrefu.

  Waziri Maghembe ameahidi kukipatia kituo hicho gari moja huku akimuagiza, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuona uwezekano wa kumaliza changamoto mbalimbali chuoni hapo.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na uongozi wa chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora BTI alipotembelea chuoni hapo leo. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho Semu Daudi na Mratibu Mkuu wa Mafunzo, Igunda John.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakati akitoa maelekezo mbalimbali chuoni hapo.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry baada ya kutembelea Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora, BTI leo.

  0 0

  Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kuzifuata fursa zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini ili kuiunga mkono Serikali katika jitihada zake za kukuza uchumi wa viwanda.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati akizungumza wakati akitoa taarifa ya mbio za Mwenge unaotaraji kuzuru katika Manispaa ya Ubungo Tarehe 31, Mei 2017.

  Alisema kuwa katika mikoa mbalimbali Mwenge wa Uhuru ulipopita umekutana na fursa ambazo Watanzania wakizitafuta na kuzifanyia kazi wataondokana na uvivu, kukaa bila kufanya kazi na umasikini kwa kuwa sasa Serikali iliyopo madarakani ni ya kazi.

  Aliongeza kuwa, nchi nyingi zimekuwa kiuchumi kupitia viwanda na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kukuza uchumi wa viwanda, wananchi wanapaswa kuzichangamkia fursa mbalimbali ili kufanikisha dhamira ya Serikali kufikia uchumi wa viwanda.

  MD amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Ubungo utapita katika Miradi mitano ya Maendeleo ambapo Miradi minne kati ya hiyo itazinduliwa na Mradi mmoja wa Ujenzo wa Kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la Msingi.

  Alisema kuwa Miradi yote hiyo itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 itagharibu jumla ya shilingi Bilioni 2,854,647,991.89

  Imetolewa Na;
  Kitengo cha Habari na Uhusiano
  Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
  Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.

older | 1 | .... | 1249 | 1250 | (Page 1251) | 1252 | 1253 | .... | 1896 | newer