Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46318 articles
Browse latest View live

Chadema watangaza rasmi kumuunga Mkono Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na kuachana na Mgombea wa NASA


CHAMA CHA WALIMU NA ASASI ZA KIRAIA ZA ELIMU SINGIDA WAUNGANA KUHAMASISHA UTOAJI WA ELIMU BORA KUPITIA RASILIMALI ZA NDANI

$
0
0
 Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Ndunguru akielezea kuhusu ripoti ya utafiti ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi Mei mwaka 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na Fedha inaliyoonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi.

  Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa upatikanaji wa elimu nchini Tanzania wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana mkoani Singida yaliyofanyika kwa siku tatu.
 Mdau wa Elimu kutoka asasi za kiraia, Lucy Mkosamali akichangia mada ya umuhimu wa uwekezaji katika maendeleo ya sekta ya elimu kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
 Mwenyekiti wa Chama wa walimu Wilaya ya Singida, Bw. Hamisi Mtundua akichangia mada kwa kutoa uzoefu wake kuhusu maslahi ya walimu na miundombinu ya shule za vijijini kwenye mafunzo yaliyofanyika mkoani humo.
 Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akichangia mada kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
 Washiriki wa mafunzo wakifanya kazi za makundi kuhusu haki ya kupata elimu bora kwenye mafunzo yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania. 
Mwakilishi wa Walimu Wanawake Chama cha walimu Manispaa ya Singida, Bi. Innosanta Shayo  akiwasilisha kazi ya kikundi cha Tano waliyokuwa wakijadili jinsi ya mtoto kupata haki katika elimu.

Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu mkoani Singida wakifuatilia mafunzo
 Mratibu wa Elimu kata ya Mtinko akichangia mada ya haki za watoto mashuleni pamoja na Umuhimu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani kuwekeza katika sekta ya elimu kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akiwaelekeza washiriki wa mafunzo namna ya kuhamasisha haki za watoto mashuleni kwa vitendo kwenye mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akitoa uzoefu wake kuhusu kuhamasisha haki za watoto mashuleni wakati wa elimu ya vitendo kwenye mafunzo ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini mkutano huu uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida yalioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
Washiriki wa mafuzo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo yaliyofanyika kwa takribani siku tatu mkoani Singida

Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) kwa kushirikiana na ActionAid Tanzania waliandaa mafunzo ya siku tatu kwa wanachama wa chama cha walimu na asasi za kiraia za elimu mkoa wa Singida kuhamasisha upatikanaji wa haki za mtoto shuleni na maendeleo ya sekta ya elimu kwa kushawishi serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kutumia rasilimali za ndani. 

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja Mradi kutoka ActionAid Tanzania Karoli Kadeghe alielezea katika bajeti ya elimu 2016/17, takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. 

Hata hivyo, hadi kufikia mwezi Machi 2017, wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu sawa na asilimia 47.6%. Alisisitiza kuwa ni vyema serikali iimarishe  vyanzo vyake vya mapato vya ndani ili kuepuka aibu hii na sisi wadau wa elimu tunalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake. 

Kila mtu akilipa kodi stahiki kadiri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.

Mkufunzi wa Mafunzo hayo Wakili Dominic Nduguru akiwasilisha mada juu ya ulipaji wa kodi na Uwekezaji katika Elimu alitumia ripoti ya utafiti ya shirikisho la dini (Interfaith standing committee) iliyozinduliwa Mwezi Mei, 2017 kwa kuwashirikisha kamati ya kudumu ya Bunge ya Uchumi na Fedha inaonyesha kuwa Tanzania kwa sasa inapoteza takribani dola bilioni 1.83 sawa na Tsh trilioni 4.09 kwa mwaka kupitia misamaha ya kodi, uhamishaji wa fedha nje ya nchi bila kufuata utaratibu, kushindwa kutoza kodi sekta isiyo rasmi na aina nyingine za ukwepaji kodi. Pia alidokeza ripoti kadhaa zinazoonesha upotevu au ukwepaji wa kodi unaofanywa na makampuni ya kigeni na wawekezaji wakubwa ambao unaathiri uwekezaji katika uboreshaji wa huduma za jamii hususani sekta ya elimu.

Washiriki wa mafunzo hayo kutoka chama cha walimu na asasi za kiraia za elimu mkoa wa Singida wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Nguvu ya kodi, haki za binadamu, haki ya watoto mashuleni, ushawishi na utetezi wa maslahi ya walimu na haki za watoto, umuhimu wa ukusanyaji wa kodi na rasilimali za ndani ili kuboresha miundombinu ya elimu na ubora wa elimu.

Viongozi na wanachama wa chama cha walimu pamoja na asasi za kiraia za elimu mkoani Singida wameazimia kuyafanyia kazi mafunzo hayo na kuungana kwa pamoja kwa kutengeza Mtandano wa Elimu Singida ili kushawishi mamlaka na serikali kusimamia ukusanywaji wa mapato ya ndani ili kuboresha sekta ya elimu. Washiriki walichagua uongozi wa mpito wa Mtandao wa Elimu Singida na kuchagua taasisi ya Youth Movement for Change kama sekretarieti ya muda.

WAZIRI MWIJAGE MGENI RASMI UFUNGUZI WA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA JIJINI TANGA KESHO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage kuwa mgeni kwenye maonyesho ya kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa kwenye na Waziri Mwijage
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisalimiana na wanawake wajasiriamali wakati akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa kwenye na Waziri Mwijage
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akisalimia na baadhi ya wajasiriamali wakati apokuwa akikagua mabanda mbalimbali kuelekea uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa yatakayofunguliwa na Waziri Mwijage
Baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) wakiendelea na matayarisho ya Banda lao ambalo lipo kwenye viwanja Mwahako Jijini Tanga 
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Salehe Masoud kushoto akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakati alipokwenda kukagua na kutembelea kuona maendeleo ya mabanda hii leo 
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa kulia akisisitiza jambo kwa mjumbe wa kamati ya maandalizi ya maonyesho hayo,Salehe Masoud wakati alipotembelea kukagua mabanda leo
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yatakayoanza kesho kwenye viwanja vya Mwahako Salehe Masoud kushoto akimuonyesha kitu Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa wakati alipokwenda kukagua na kutembelea kuona maendeleo ya mabanda hii leo habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE (TAWLA) CHAFANYA MKUTANO WAKE WA MWAKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka akfungua mkutano wa mwaka wa Chama hicho ulioshirikisha wanachama wake ambao ni wanasheria wanawake, Mkutano huo umefanyika leo kwenye Hoteli ya New Afrika jijini Dar es salaam na kujadili mambo kadhaa yakiwemo mafanikio na changamoto zinazokabili chama chao pamoja na jamii kwa ujumla wake.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
 
Kutoka kulia ni Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania ( TAWLA), Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka, Tike Mwambipile Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWLA) na Lulu Ngwanakilala Mtoa mada katika mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyojadiliwa na washiriki wa mkutano huo.
Mtoa mada Shamshard Remhamtulla akizungumza katika mmkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Kutoka kulia ni Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania ( TAWLA), Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania (TAWLA) Bi. Athanasia Soka, Tike Mwambipile Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWLA_
Lulu Ngwanakilala Mtoa mada akizungumza jambo na washiriki wa mkutano wa Chama cha Wanasheria wanawake wa mwaka uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mtoa Mada Madeline Kimei kulia akijiandaa kutoa mada katika mkutano huo.
Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania ( TAWLA) akielezea baadhi ya taratibu katika mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo Wanasheria wanawake wakifuatilia mada.
  
Kutoka kulia ni Mary RichardLatifa Mwabondo na Khadija Ngasongwa wanachama wa (TAWLA) wakiwa katika mkutano huo.
 
Madeline Kimei Mtoa mada wa mkutano huo pamoja na washiriki wengine wakiwa katika mkutano huo.
Jaji wa Mahakama Kuu Jaji Leila Ngonya pamoja na washiki wengine wanachama wa (TAWLA) wakiwa katika mkutano huo.
Josephine Arnold kutoka (TAWLA) akimsajili mshiriki wa mkutano huo na mwanachama wa (TAWLA) Bi. Mariam Mungula
Washiriki mbalimbali wakijisajili kwa ajili ya kushiriki mkutano huo.
Mmoja wa watoa mada Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kushoto akifuatilia jambo katika mkutano huo kulia ni Mariam Mungula na baadhi ya washiriki.

RC MAKONDA AKABIDHIWA MWENGE WA UHURU UKITOKEA MKOANI LINDI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi wakijadili jambo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kulia) wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.Muonekano wa Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam ukitokea Mkoani Lindi.


Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Me 27, 2017 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kumulika miradi ya Maendeleo.

Mara baada ya kukagua Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utazuru katika Wilaya ya Kigamboni Tarehe 28/05/2017, Siku ya Tarehe 29/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala, Tarehe 30/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni na Tarehe 31/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Mwenge wa uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika hivyo kuzuru katika Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu.

Mhe Makonda alisema kuwa Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali kutokana na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Mhe Makonda alisema kuwa jitihada ya kudhibiti kusambazwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya ni kuifanya kuwa ajenda muhimu kiutekelezeji kwa mustakabali wa maisha ya watanzania kwa kuwa Jambo hilo linagusa nguvu kazi ya Taifa.

Rc Makonda amebainisha kuwa jumla ya Miradi 40 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa na thamani ya Shilingi Bilioni 244,392,530,334 ambapo Miradi 12 itazinduliwa, Miradi 15 itawekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili itafunguliwa na Miradi 11 itatembelewa.

Mhe Makonda amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili huku akitoa wito kwa Wakazi wa Manispaa ya Temeke, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote utakapozuru kwani pamoja na mambo yote Mwenge wa Uhuru ni urithi na nembo ya umoja katika maendeleo yetu.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa weledi wake katika utendaji hususani katika kudumisha amani na kuchagiza ukuzaji wa uchumi wa nchi kwa kutilia msisitizo uwajibikaji serikalini, Kukemea wizi na Ubadhilifu wa Mali za umma sambamba na Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.

Mhe Zambi alisema kuwa Wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli katika mapambano dhidi ya wizi wa Mali za Watanzania hususani Vita ya kiuchumi aliyoianza hivi karibuni kwa kuzuia Mchanga wa dhahabu kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Mhe Zambi ametoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza Hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.

Mwenge wa Uhuru utamaliza mbio zake mkoani Dar es salaam siku ya tarehe 31/05/2017 na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani siku ya tarehe 01/06/2017 katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kuelekea Mafia Mkoani Pwani.

NAIBU WAZIRI NGONYANI AKAGUA UJENZI DARAJA LA KELEMA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akikagua hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu hatua za ujenzi zilizofikiwa za Daraja la Kelema Mita 220 linalounganisha wilaya ya Chemba na kondoa mkoani Dodoma, leo.

 Mkandarasi wa Kampuni ya Chicco, Li Jianzheng, akimounesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), namna ya usukwaji nondo katika Daraja la Kelema lenye urefu wa mita 220 wakati alipokagua daraja hilo mkoani Dodoma leo.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mayamaya-Mela Km 99.35 Eng. Leornado Licari akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, kuhusu ujenzi wa Daraja la Msui lenye urefu wa mita 45 lililopo katika barabara hiyo, mkoani Dodoma, leo.
 Mhandisi Mshauri wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Mela – Bonga Km 88.8 Eng. Kini Kuyonza akimuonesha taarifa ya mradi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Manyara, leo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akikagua zege lililowekwa katika barabara ya Mela-Bonga KM 88.8 eneo la Mlima Kolo uliopo wilaya ya Kondoa, wakati alipokagua ujenzi wake, leo. Kulia ni Mhandisi Mshauri wa mradi huo Eng. Kini Kuyonza

WANAFUNZI WANOKWENDA VYUO VIKUU VYA NJE VIGEZO LAZIMA VIZINGATIWE– TCU

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

WANAFUNZI wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa kupita katika Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kwa ajili ya kuangalia vigezo ambavyo vinahitajika.

Hayo yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk. Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Dk. Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda kusoma vyuo vya nje anatakiwa kuwa na ufaulu wa D mbili ambazo ni viwango vilivyowekwa.

Amesema kuwa mwanafunzi anayekwenda kusoma nje bila kupita katika tume hiyo ilivyowekwa kwa ajili ya kuratibu,  akirudi anakuwa anakosa sifa katika mfumo wa elimu nchini.

Kwa upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya amesema kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali. Amesema India imekuwa ikitoa elimu bora na kwamba Tanzania ni nchi ambayo inanufaika kwa kupata ufadhili wa watu 25 kila mwaka.
Naye, Mkurugenzi wa Global Education Link  (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa nchi ya India  iangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya ufadhili hadi kufikia 100 kutokana na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa GEL imekuwa katika msisitizo wa mara zote katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapita TCU  kwa ajili ya kuhakikiwa..
Maonesho vya vyuo vikuu vya nchini India yamefadhiliwa a kampuni ya Global Education Link (GEL).
 Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Dk.Fabian Mahundu akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa India Nchini Tanzania, Sandeep Arya  akizungumza akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Nassor akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda  katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk.Fabian Mahundu akiwa na Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel wakitembelea  mabanda katika  maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India.leo jijini Dar es Salaam. 
 Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya akiwa katika picha ya  watanzania  25 waliopata ufadhili wa Serikali ya India wa kusoma katika vyuo vikuu vya nchi hiyo leo jijini Dar es  Salaam.

BULEMBO AENDELEA NA ZIARA YAKE MERERANI LEO

$
0
0
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Abdallah Bulembo akipewa na Wazee, heshima ya Kiongozi Mkuu wa Kabila la Wamasai la Ulaigwanani, alipowasili ukumbini kuzungumza na Watendaji na viongozi na wanachama wa CCM wakiwemo mabalozi, katika mji mdogo wa Mererani mkoani Manyara, leo, May 27, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo).
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Abdallah Bulembo akizungumza ukumbini na Watendaji wa serikali, viongozi na wanachama wa CCM wakiwemo wajumbe wa nyumba kumi, katika mji mdogo wa Mererani mkoani Manyara, leo May 27, 2017.
 Viongozi na wanachama wa CCM wakiwemo wajumbe wa nyumba kumi wakishangilia wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa CCM, Abdallah Bulembo alipozunumza nao ukumbini katika mji mdogo wa Mererarini mkoani

MAREKANI YAAHIDI KUWAJENGEA UWEZO WANAWAKE NA VIJANA WA ZANZIBAR.

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala ” Mabodi” akizungumza na Mkurugenzi wa taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia duniani (NDI), Dkt. Keith Jenningspamoja na ujumbe wake



NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Sadala amefanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia Duniani (NDI), kanda ya mashariki na kusini mwa afrika, Dkt. Keith Jennings, huko Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo Naibu Katibu Mkuu huyo alieleza kwamba CCM imekuwa mdau mkubwa wa kutekeleza dhana ya demokrasia kwa vitendo, sambamba na kutoa fursa za uongozi kwa makundi yote ya kijamii.

Alisema ujio wa taasisi hiyo Zanzibar utafungua fursa mbali mbali kwa vijana na wanawake kupata ujuzi wa kukabiliana na changamoto za kisiasa na kiuchumi.

Pia Dkt. Mabodi aliishauri Taasisi hiyo kufungua Ofisi hapa nchini kwa lengo la kuratibu masuala mbali mbali yakiwemo kuwapatia Vijana fursa za kimasomo nchini marekani ili waweze kujifunza na kupata ujuzi wa fani zinazokubalika katika soko la ajira hapa nchini.

“Vijana na Wanawake wa Zanzibar wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa ajira, hivyo taasisi yenu ikitoa fursa za mafunzo ya ujasiria mali itasaidia kukabili tatizo hilo.”, alisema Dkt. Mabodi.

Naye Mkurugenzi wa taasisi ya kimarekani inayoshughulikia masuala ya Demokrasia duniani (NDI), kanda ya mashariki na kusini mwa afrika, Dkt. Keith Jennings alieleza kuwa taasisi hiyo inajishughulisha na masuala ya Demokrasia na kutoa mafunzo ya ujasiria mali kwa vijana na wanawake duniani.

Dkt. Keith alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni taasisi hiyo kujitambulisha kwa CCM Zanzibar na kubadilishana mawazo yatakayosaidia kufanya kazi za kisiasa kwa pamoja.

” Taasisi yetu imekuwa ikitoa mafunzo ya ujasiriamali pamoja na mbinu za kutumia fursa zinazopatikana katika mifumo ya Kidemokrasia kwa vijana na wanawake, hivyo tunatarajia hata kwa Zanzibar makundi hayo yatanufaika na mpango huo.”, alieleza Dkt. Keith.

Dkt. Keith alisema Zanzibar ina historia kubwa ya kisiasa hivyo taasisi hiyo ina dhamira ya kuwajengea uwezo vijana mbali mbali hapa nchini ili waweze kutumia vizuri fursa zilizopo katika michakato ya kidemokrasia.

JUMUIYA YA MADOLA YA WAPIGA MSASA WABUNGE KUTOKA NCHI 16

$
0
0
Wajumbe wa Bunge la Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa Mafunzo ya wiki moja yalioandaliwa na Bunge hilo, katika mafunzo hayo Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania limewakilishwa na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson na Baraza la Wawakilishi Zanzibar limewakilishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said.
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson pamoja na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said wakishiriki katika masomo ya wiki pamoja huko Afrika Kusini University of Wits ambapo jumla ya Wabunge kutoka nchi 16 kutoka Jumuiya za Madola wameshiriki masomo hayo. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwasilisha kazi ya kikundi wakati wa mafunzo hayo ya wiki moja yanayofanyika Nchini Afrika Kusini yalioandaliwa na Umoja wa Bunge la Jumuiya ya Madola, akieleza kuhusiana na umuhimu wa kamati za kudumu za mabunge ya Jumuiya Madola kuelekea karne 21. 

Kutoka kushoto ni Mbunge kutoka India Ajay Misra, Naibu Spika Tanzania Dr Tulia Ackson, Seneta kutoka Jamaica Charles Pearnel na Mussa Dlamini Swaziland. Masomo hayo yanafanyika Johanessberg University of Witwatersrand kwa wiki moja na kudhaminiwa na Commonwealth Wealth. 
Wawakilishi kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Naibu Spika Dr.Tulia Ackson pamoja Simai Mohammed Said kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa masomomi South Africa University of Witwatersrand wakibadilishana mawazo na Mbunge wa Swaziland Mhe Mussa Dlamini
Naibu wa Spika wa Jamhuri ya Muungano Dr Tulia Ackson akisikilizwa kwa umakini na washiriki wenzake. Kutoka kushoto Mhe.Simai Mohammed Said ( Zanzibar ) Pearnel Charles Junior ( Jamaica) Mussa Dlamini ( Swaziland ) na Ajay Misra ( India).
Waheshimiwa Wabunge wa Nchi za Jumuiya ya Madola wakiwa katika mafunzo Nchini South Africa. wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini. 
Wajumbe kutoka Mabunge ya nchi za Jumuiya ya Madola ( Commonwealth Countries) wakitembelea Mahakama ya Katiba ( Constitutional Court ) katika mji wa Johannesburg.
Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo hayo kutoka kushoto Mbunge wa Jamaica.Mhe.Heroy Clarke ( MP), Charles Pearnel Seneta pia akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Jamaica, Stewart Michael ( MP) na Victor Wright ( MP ). 
Mjumbe kutoka Jumuiya ya Madola pia akiwa Mwakilishi kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akibadilishana mawazo na Profesa David Everatt ambaye ni Kiongozi wa Skuli ya Utawala katika University of Wits, South Afrika. 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Tulia Ackson akitoa nasaha zake za shukrani kwa niaba ya Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola walioshiriki mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa University of Witwaterstrand, Johannesburg South Africa.

BILLNAS JIWE LA MWEZI XXL YA CLOUDS FM NA MAKAMUZI YA SHOO YA NGUVU NA MZEE WA MBEYA LEO.

Menejimenti Ya DCC Yapongezwa kwa Kurejesha Uhai wa Shirika.

$
0
0


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na wafanyakazi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Sipora Liana na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Isaya Mwita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na menejimenti za Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara yake katika ofisi za mashirika hayo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akisisitiza jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo akielezea jambo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo. Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam(DDC) wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi katika Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maenedeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC).
Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko la Kariakoo Hetson Msalale Kipsi akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (hayupo pichani) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC), Rwandiko Manumbu akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika hilo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya yake kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akipokelewa na baadhii ya wajumbe wa Bodi za Mashirika ya Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) NA Shirika la Masoko Kariako alipowasili katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akisalimiana na mmoja wa wafanyabiashara katika Soko la Kariakoo Shimoni wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita (kushoto) akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(mwenye suti nyeusi) kuelekea katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Machinga wanaopanga bidhaa zao mbele ya Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam.

Picha zote: Frank Shija – MAELEZO

………………….

Nuru Juma – MAELEZO.

Serikali imeipongeza Bodi na Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) kwa juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo richa ya changamoto wanazo kumbana nazo.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo alipokutana na menejinti ya mashirika hayo leo.

Waziri Simbachawene alisema kuwa amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika nayo hivyo hana budi kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda mfupi imeweza kufanya mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo.

“Pamoja na kuipongeza bodi hii lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kama kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani hilo ndilo lilikuwa lengo la kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na kuweka mahali ambapo watoto wataweza kucheza ili kuhakikisha shirika linajiongezea kipato na kuiongezea Serikali kipato pia,” alisema Waziri Simbachawene.

Simbachawene alitumia nafasi hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa taarifa nyingine itakayohusisha mali zote za mashirika hayo.

Aidha ameutaka uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo kuwa wabunifu kwa kuanzisha masoko sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi na njia ya kuongeza ajira kwa vijana.

Alilitaka Shirika hilo kuachana na mawazo ya kizamani na badala yake wajipange kimkakati ili kuendana na wakati ikiwemo kufikiria namna ya kuwaza kushusha mizigo katika soko hilo kwani serikali haitaweza kuruhusu maroli ya mizigo kufika katika soko hilo ili kupunguza ya kuepuka msongamano katikati ya jiji.

Aliushauri uongozi huo uandae mikakati ya kuwezesha soko hilo kuwa la kiwango cha juu (Super Market) na kuwalipisha wafanyabiashara kiwango kinachoendana na bei halisi ya soko kama ambavyo wapangishaji wengine wamekuwa wakitoza ili kukuza kipato kwa Taifa.

Waziri Simbachawene ameahidi kushirikiana na mashirika hayo katika kutatua changamoto ambazo zinahitaji msaada wa uongozi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii kwani Serikali ya Awamu ya Tano inahitaji watu wanaojituma na kuchapa kazi.

Awali akiwasilisha taarifa fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Shirika hilo Rwandiko Manumbu alisema kuwa pamoja na changamoto wanazokumbana nazo Shirika limefanikiwa kutoa shilingi milioni 140/- kama gawio kwa mwanahisa wake ambaye ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

“Mhe. Waziri, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Shirika hili tumeweza kutoa gawio la kiasi cha shilingi milioni 140/- kwa Halmashauri ya Jiji na haya ni mafanikio makubwa kwetu,” alisema Manumbu.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amempongeza Waziri Simbachawene kwa utayari wake wa kushughulikia changamoto zinazo yakabli mashirika hayo ikiwa ni pamoja na kutenga muda wake kuja kusikiliza matatizo yao.

Pamoja na pongezi hizo Mwita alishauri Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam (DDC) kuangalia uwezekano wa kurejesha bendi za muziki kama ambavyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alivyokuwa amedhamiria wakati wa uanzishwaji wa Shirika hili.

Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo ni mashirika ya Umma yanayoongozwa na Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam chini ya Sheria za Makampuni namba 2012 ya mwaka 1971 na Sheria ya Bunge namba 36 ya mwaka 1974, “The Kariakoo Market Corporation Act, 1974

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY 28,2017

TRA Watoa Somo la Ulipaji Kodi kwa Wafanyabiashara wa Kichina

$
0
0


Meneja wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu semina juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria kwa wafanyabiashara kutoka China iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
2
Mrakibu wa uhamiaji na Afisa Vibali vya Ukazi, Eliud Ikomba akitoa semina kwa wafanyabiashara kutoka China (hawapo pichani) juu ya sheria za uhamiaji katika semina iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
3
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka China wanaofanya biashara zao nchini wakisikiliza mafunzo mbalimbali juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria katika semina iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.    
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa somo la masuala ya kodi kwa wafanyabiashara kutoka China wanaoishi nchini kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya sheria na taratibu za ulipaji kodi katika semina kuhusu mafunzo hayo leo Jijini Dar es Salaam.

Akiwasilisha mada wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Gabriel Mwangosi amesema kuwa Tanzania ya sasa ina fursa nyingi za uwekezaji hivyo wafanyabiashara hao watakapokuja kuwekeza lazima wafahamu kanuni na taratibu za ulipaji kodi nchini ili waweze kuendana na sheria zilizopangwa na nchini.

“Semina hii mahususi imeandaliwa kwa ajili ya wafanyabiashara wa kichina wanaoishi nchini kupata mafunzo ya kodi zikiwemo za zuio, majengo pamoja na ushuru na forodha ambazo ni lazima wazifahamu kwa manufaa ya Taifa letu na wao pia,”alisema Mwangosi.

Mwangosi ameongeza kuwa hii ni mara ya 6 kufanyika kwa semina hizo kwa wafanyabiashara hao ambapo tangu zianze kufanyika zimewasaidia kutokwenda kinyume na taratibu zilizowekwa nchini.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dotto Stanley amesema kuelimisha umma hasa kwa wageni kutoka nje ya nchi ni jambo la msingi litakalowarahisishia kufahamu sheria za nchi ambapo kwa namna nyingine itachochea uwekezaji.

“Kwa kawaida wafanyabiashara wakubwa huwa wanahitaji kufahamu sheria na taratibu za nchi husika kabla hawajaamua kuwekeza mahali hivyo mafunzo hayo yatachochea uwekezaji nchini kwa sababu watakuwa na uelewa wa mchakato mzima juu ya sheria za uwekezaji na kodi.”alisema Stanley.

Naye Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd, Anne Werema Maneno amesema kuwa changamoto kubwa inayowapata wafanyabiashara wa kichina ni kukosa uelewa juu ya jinsi ya kuwekeza nchini hasa katika suala la ulipaji kodi.

“Changamoto hiyo inawapelekea wafanyabiashara kukosa muelekeo wa biashara waliyopanga kufanya kwani wengi wao wakifika Tanzania hubadilisha biashara baada ya kufahamishwa sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu biashara hivyo semina hiyo itawapa uelewa utakaowawezesha kuchagua biashara watakayoweza kuifanya kulingana na mtaji wa mfanyabiashara husika,”alisema Bi. Anne.

Aidha, katika semina hiyo ya siku moja imeambatana na fursa ya kupata mafunzo kutoka kwa taasisi zingine zinazofanya kazi moja kwa moja katika shughuli ya uwekezaji ambazo ni pamoja na TRA, TIC, Idara ya Uhamiaji, Idara ya Kazi pamoja na Taasisi za Kibenki.

Mafunzo hayo juu ya Kodi, Utaratibu na Sheria kwa wafanyabiashara hao yameandaliwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Kampuni ya Jiteng Consultancy Ltd na kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa ikiwa ni utaratibu wa kawaida wakukutana na wadau mbalimbali wa Kodi.

CHAMA CHA WAONGOZA WATALII TANZANIA (TTGA) WALIA NA MIUNDO MBINU MIBAYA YA BARABARA NDANI YA HIFADHI ,WASEMA HADI SASA MIKATABA IMEKUWA DONDA NDUGU KWAO!

$
0
0

Wakwanza kulia ni Mwenyekiti wa chama cha waongoza Watalii Halifa Msangi,Wakwanza kushoto ni Katibu wa umoja huo Emanuel Mollel,Haji Mbuguni Mjumbe wa (TTGA)Omari Rajabu mjumbe,Apolinary Kiwhili M/Msaidizi wakiwa katika maonyesho ya utalii ya 18 ya Karibu Fair 2017Picha na Vero Ignatus Blog.

Wa pili kulia ni mwenyekiti wa Chama cha waongoza Utalii Nchinni Tanzania Halifa Msangi,Wa kwanza kushoto Katibu wa chma hicho Emanuel Mollel,wakiwa na wajumbe wa chama hicho ,pamoja na Hosiana F. Siao.Picha na Vero Ignatus Blog.
Wakizungumza na wageni mbalimbali Ambao walitembelea banda lao katika maonyesho ya Utalii yaliyo shirikisha zaidi ya makampuni 300 ya utalii,amabapo washiriki wa ndani yanchi ni 60% na yale ya nje ni 40% ambapo huwa wanafanyika lila mwishoni mwa mwezi mei .Picha na Vero Ignatus Blog.Chama cha waongoza Watalii wakiwa kwenye banda lao ndani ya viwanja vya magereza katika maonyesho ya Karibu Fair yaliyo beba kauli mbiu isemayao Utalii endelevu kwa Maendeleo.Picha na Vero Iganatus Blog.
Maongezi yakiendelea na wageni waliotembelea banda lao.Picha na Vero Ignatus Blog.




Na.Vero Ignatus ,Arusha

Chama cha waongoza Watalii nchini Tanzania (TTGA) wameiomba Serikali iwapatie eneo huru kati ya Hifadhi ya Ngorongoro na ile ya Serengeti ,kwani katika eneo hilo la Ndutu katika upande wa Serengeti hakuna barabara za kufanyia mizunguko za kwenda kuangalia wanyama .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama hicho ndugu Halifa Msangi kwamba changamoto kubwa wanayoipata kama waongoza watalii ,ni kipindi ambacho wanyama pundamilia na Nyumbu wanapohama kuelekea upande mwingine hawawezi kuwapeleka wageni kwenda kuwaona wanyama hao upande wa pili

"Katika eneo la Ndutu wananyama pundamilia na nyumbu huwa wanatabia ya kuhama na kuelemea upande mwingine,sasa unakuta wewe muongozaji ukiwa na kibali cha upande mmoja tu huwezi kuwapeleke wageni mahali wanyama walipo kwani hakuna barabara ya kufanyia mizunguko kwenda kuwaona wanyama jambo ambalo tumekuwa tukipata changamoto kubwa na maswali mengi kutoka kwa wageni tumeizungumzia changamoto hii kwa muda mrefu sasa."alisema Halifa.

Kwa upande wake Katibu wa chama hicho cha waongoza watalii Emanuel Alfayo Mollel amesema kuwa changamoto nyingine kubwa ni barabara zilizopo ndani ya Hifadhi haswa kutoka Ngorongoro kuelekea Serengeti ,barabara hizo zimejazwa vifusi kwa ya km 10 ambavyo havijasambazwa jambo ambalo wakati mwingine vinaweza vikapelekea hata kusababisha ajali pale ambapo dereva anahangaika kuvikwepa.

''jamani miundo mbinu ndani ya hifadhi haswa Tarangire na Manyara ni changamoto kubwa wakati wa mvua hakupitiki, "alisema Emanuel.

Amesema kuwa asilimia 90 ya waongoza Watalii ni waajiriwa kwenye makampuni ya Utalii ,hadi sasa mikataba yao imekuwa ni donda ndugu kwani mikataba hiyi ipo tayari lakini hakuna wakuisimamia ili ifanye kazi kama inavyohitajika.

Amesema Waongoza watalii nchini Tanzania kilianzishwa mwaka 1999,kina jumla ya wanachama zaidi ya 3000 ,Wanachama ni 1130 ,wanachama hai waliolipa ada zao kwa mwaka 2017 ni 567 tu,amewataka waongozaji watalii hao ambao sio wanachama waamue kuiunga kwani hakuna njia nyingine ya kutatua changamoto waliyonayo zaidi ya kuwa wamoja.

Rais Magufuli awatembelea wagonjwa Hospitali ya Taifa Muhimbili

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu. Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha) aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya Matibabu 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari, Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimtakia heri mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na Mama yake Mwanahabibi Mohamed Mtei. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini

WANANCHI WA KITETO WAENDELEA KUJIUNGA NA MFUKO WA PPF

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera (wa pili kulia) akikabidhiwa vifaa tiba na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele (wa pili kushoto) kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Kiteto katika hafla iliyofanyika mwishoni wa wiki iliyopita. PICHA NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG- KITETO. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera akitoa maelezo mafupi kuhusu faida za kujiunga na Mfuko wa PPF katika hafla ya kukabidhiwa vifaa tiba toka Mfuko wa PPF kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Manyara. Mkuu wa wilaya Kiteto, Manyara, Bw. Tumaini Magesa akitoa shukrani zake za pekee kwa Mfuko wa PPF jinsi ilivyoweza kuwakomboa wananchi wa wilaya yake kwa kuwapatia vifaa tiba. Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini, Bw. Jacob Sulle akiendelea kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya ya Kiteto, Manyara ili waendelee kujiunga na Mfuko wa PPF. Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele akitoa maelezo mafupi wakati wa ugawaji wa vifaa tiba vilivyotolewa na PPF katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.  Makamu Mwenyekiti wa Wilaya ya Kiteto, Bw. Paul Tunyoni akitoa shukrani zake za pekee kwa Mfuko wa PPF kwa kuweza kuwafikia wananchi wengi na kuwapa elimu juu ya kujiwekea mafao kwa mfumo wa 'WOTE SCHEME'.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya Kiteto walioweza kuhudhuria halfa ya ugawaji wa vifaa Tiba.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera akimkabidhi kitambulisho cha uanachama wa Mfuko wa PPF kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari 'WOTE SCHEME' kwa Mfugaji Ngaisi Laizer.  
 Mfugaji Ngaisi Laizer akionesha kitambulisho chake cha uanachama wa mfuko wa PPF.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PPF na viongozi wa wilaya ya Kiteto.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Janet Ezekiel akiwaandikisha wanachama wapya wa Wilaya ya Kiteto, Manyara. Meneja wa PPF Kanda ya Kaskazini, Bw. Jacob Sulle (wa kwanza kulia) akiwaandikisha wanachama wapya wa Wilaya ya Kiteto, Manyara.  Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Kiteto wakijiunga na Mfuko wa PPF baada ya kupata elimu.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa PPF, Bi. Lulu Mengele akitoa elimu kwa wananchi.

MKUU WA WILAYA YA MBOGWE AONGOZA ZOEZI LA USAFI WA MAZINGIRA.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Mh Martha Mkupasi ameongoza wakazi wa Mbogwe kwenye Zoezi la Usafi wa Mazingira kwa kufanya usafi eneo la Kituo cha Afya Masumbwe na maeneo yanayozunguka kituo hicho.

Akiongea na wananchi baada ya zoezi la usafi, mh Mkupasi amewataka wananchi kujijengea tabia ya kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguka kila siku na wasisubiri mwisho wa mwezi kwani kwa kupenda usafi itawasaidia kujiepusha na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu. Pia amewasisitiza wananchi kutunza mazingira na kuepuka kukata miti ovyo badala yake wapande miti ya kutosha .

Pamoja na hayo mh Mkupasi aliongea na Vijana wa Kikundi cha Scout walioungana na wananchi kwenye zoezi la usafi , nakuwahimiza kupenda masomo yao ya kila siku na kuweka bidii kwani bila elimu hawezi kutimiza ndoto zao .

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, Afisa Mazingira wa Wilaya Charles Karibu Tuyi aliwashukuru wananchi na kikundi cha scouti kwa kujitolea kuja kufanya usafi wa mazingira kwenye kituo cha afya Masumbwe na kuwahimiza kuendelea kusafisha mazingira wanayoishi na kuwataka waepuke kutupa uchafu kwenye mitaro kwani utupaji wa taka ngumu unaweza kuziba mitaro na kusababisha mafuriko .

TIMU YA WATAALAM YAAGIZA KUANDA RIPOTI YA KUMALIZA MGOGORO WA BWAWA LA ULUWA WILAYANI SIKONGE.

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe
 
Na Tiganya Vincent, Sikonge 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameteua timu ya Maafisa watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa ajili ya kuandaa taarifa(ripoti) itakayowasilishwa kwake Jumatano(wiki inayoanza kesho) ili imwezeshe kutoa maamuzi yatakaondoa kuondoa mgogoro uliosababisha ujenzi Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Uluwa ushindwe kuendelea kwa sababu ya maji yake kuelekezwa katika Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi. 

Hatua hiyo itasaidia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 313 ambazo hadi hivi sasa zimeshatumika katika ujenzi wa mradi huo ambao ni kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji wa mpunga katika vijiji viwili vya Mtakuja na Kiloleni kama mradi utaendelea. Profesa Maghembe alichukua uamuzi huyo jana wilayani Sikonge baada ya kutembelea Mradi huo huku akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri ili kujionea hatua ulipokuwa umefikia na hiyo mifereji ilijengwa kuelekea katika Msitu wa Hifadhi. 

Alistaja wataalam hao kuwa ni Ofisa wa Maliasili, Misitu, Kilimo na Mhandisi wa Maji, Mhandishi wa Ujenzi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mteandaji wa Halmashauri ya Sikonge ambao aliwapa jukumu la kuandaa taarifa itakayoonyesha mambo mbalimbali ikiwemo kupima na kuonyesha kiasi cha eneo ambalo wananchi wanalohitaji kwa ajili ya kilimo hicho na eneo lilobaki katika Msitu huo wa Hifadhi. 

Profesa Maghembe aliwaambia kuwa uharaka na ubora wa ripoti ya Halmashauri ndio utakaoisaidi Wizara ya Maliasili na Utalii kufikia maamuzi haraka ambayo baada ya wataalam wake kuipitia atawalisha mapendekezo na hatua waliofikia kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya hatua zaidi. 

Aliongeza kuwa wakati hatua za kupata eneo hilo zikiendelea ni vema uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ukaanza kujipanga kwa kuandika andiko la mradi wa kuomba fedha kutoka Wizara ya Maji ili kazi ya ujenzi huo ikamilike na ianze kuwanufaisha wananchi. 

Aidha , Waziri huyo wa Maliasili na Utalii alitoa wito kwa wananchi wote watakaopata maeneo karibu na Hifadhi mbalimbali kuwa walinzi wa kwanza wa rasilimali hizo na kuwakemea wale wote watakaonekana kutaka kuzihujumu kwa faida binafsi. Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri alisema kuwa sehemu kubwa ya ardhi ya Halmashauri ya Sikonge ni mistu ya hifadhi ambayo inafikia asilimia 95 na asilimia tano tu ndio inatumika kwa matumizi mengine ya binadamu ikiwemo kilimo. 

Kufuatia hali hiyo aliwaasa viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa makini wakati wanaendesha zoezi hilo la kuomba eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 500 kwa kuangalia mahitaji yao halisi ili isije ikatokea wameshapewa wanaanza tena kuomba nyongeza. 
 
Aidha , Mkuu huyo wa Mkoa alimweleza Waziri Maghembe, Ofisi yake itatuma Wataalam wiwili waungane na wa Halmashauri kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haraka na umakini ili wananchi waanze kufanikisha mradi huo. 

Akisoma taarifa ya mradi huo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Abel Busalama alisema kuwa mradi huo uliogharimu hadi sasa milioni 313 .8 ambao ungevinufaisha vijiji vya Mtakuja na Kiloleni ulishindwa kuendelea baada mjenzi kujenga mifereji ya umwagiliaji akielekeza katika Msitu wa Hifadhi wa Ipembampazi jambo lililopelekea wananchi wa vijiji hivyo kuvamia msitu na kuanzisha mashamba ya mpunga na wengine kuingiza mifugo kwa ajili ya malisho. 

Hivyo alimwomba Waziri huyo mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii kutoa ruhusa ya eneo la hekta 500 katika Msitu wa Hifadhi ya Ipembampazi liweze kupima na kutumika kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji . 

Ujenzi wa mradi huo ulifika hatua ya pili ambapo ilibaki hatua ya tatu ili uanze kutumika na ndipo ulisimamishwa.

Tanzania yatumia Siku ya Afrika Saudi Arabia kutangaza utamaduni wake

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akifurahia chakula cha asili ya Tanzania na mabalozi wa nchini nyingine katika maadhimisho ya Siku ya Afrika nchini hapa yaliyofanyika hivi karibuni.


Na Mwandishi Wetu, Riyadh

Balozi wa Tanzania UBALOZI wa Tanzania nchini Saudi Arabia, uliungana na ofisi nyingine za balozi za nchi mbalimbali kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Afrika yaliyofanyika hivi karibuni nchini Saudi Arabia.

Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na kutangaza utamaduni, ambapo kwa Tanzania, shamra shamra hizo zilikonga nyoyo za wahudhuriaji wengi, ambapo wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini hapa waliimba nyimbo za kuisifu na kuipamba Tanzania.
Wanafunzi wa kitanzania baada ya kutumbuiza nyimbo za kuisifu Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliuambia Mtandao huu kuwa kusudio la kuungana na mabalozi wengine lilifanikiwa kwa sababu lengo halisi ni kuitangaza Afrika na nchi zao, ambapo anaamini kwa maadhimisho hayo nchi yake imepiga hatua kujitangaza kwa kuonyesha utamaduni wao kwa kupitia, ngoma, nyimbo, ngojera, maonesho ya mavazi na maonesho ya vyakula vya asili vya nchi zilizoshiriki,
Wakati wa Maakuli. Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akiwa ameshika sahani ya chakula katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ambapo vyakula vya asili, ngoma na utamaduni wa Tanzania ulionyeshwa katika tukio hilo.
Viewing all 46318 articles
Browse latest View live




Latest Images